Watu wengi wanasoma biblia lakini si wote wanayafikia maneno SAFI YA MUNGU. Jambo ambalo watu wengi hatujui ni kuwa tunadhani, tunapoisoma biblia kwa mara moja, tayari tumeshayafikia “maneno safi ya Mungu”, yale yenye uwezo wa kubadilisha Maisha yetu katika ubora wote.
Ni vizuri ukafahamu hii biblia tunayoisoma, haipo wazi kama unavyodhani, ni kitabu kilichoficha maneno SAFI YA MUNGU (Pure word of God), Ambayo hayapatikani hivi hivi tu, kwa usomaji wa kawaida tuliouzoea sikuzote. Watu ambao wanauwezo wa kufikia hapa, basi Maisha yao ya kiroho yanakuwa na mageuzi makubwa sana, kutokana na nguvu ya Neno hilo.
Leo kwa neema za Bwana tutaona mtu anawezaje kuyafikia maneno haya;
Biblia imefananisha Neno la Mungu na madini ya fedha (Silver), sehemu nyingine na Dhahabu.
Sasa ukisoma, Zaburi 12:6 inasema..
Zaburi 12:6 “Maneno ya Bwana ni maneno safi, Ni fedha iliyojaribiwa kalibuni juu ya nchi; Iliyosafishwa mara saba”.
Maana yake ni kuwa, ili uweze kufahamu haya “Maneno safi ya Mungu” yanapatikanaje, unapaswa utazame jinsi Fedha/dhahabu safi, inavyopatikana na kusafishwa.
Kwa kawaida, madini haya yanapochimbwa, huwa hayang’ai kama unavyoona katika maduka ya VITO vya thamani. Bali yanakuwa kama miamba tu, au maudongo udongo, yaani dhahabu halisi inakuwa imechanganyikana sana na uchafu wa aina mbali mbali.
Hivyo wanachokifanya ili kuitoa takataka hizo katikati ya madini, ni kwenda kuiyeyusha katika joto kali sana. Hiyo inapelekea, uchafu kujitenga na fedha, kwani zile takataka zote zinapanda juu, na ile fedha/dhahabu, inabaki chini, kisha wanauzoa ule uchafu wote uliokuja juu, baadaye wanaicha igande tena kisha inatokea dhahabu yenyewe.
Sasa kwa kawaida,wafua fedha/dhahabu, wengine wanairudia hiyo hatua mara mbili au tatu, na kwa jinsi wanavyoirudia mara nyingi na kuondoa hata zile takataka ndogo sana, ndivyo, dhahabu hiyo inavyozidi kuleta mng’ao mzuri sana na wakuvutia sana.
Hivyo Mungu alitumia mfano huo kuonyesha pia jinsi NENO LAKE SAFI, linavyopatikana. Ni kama fedha iliyosafishwa MARA SABA katika moto,. Ikiwa na maana kuwa, zipo hatua saba, za kulifikia NENO safi la Mungu, alilokusudia limletee matokea makubwa katika Maisha yake..
Sasa hii mara saba, mtu anaifikiaje?
Ukiwa ni mtu wa kusoma biblia mara moja tu, na kujiona kuwa tayari umeshajua kila kitu, ufahamu kubwa hapo bado hujalifikia hili Neno safi la Mungu. Kulifikia kunahitaji utulivu, na pia kulitafakari tena na tena, na tena, na tena, kila siku, na sio kusoma tu kama gazeti.
Kwamfano leo unaweza kusoma habari za wana wa Israeli jinsi Mungu alivyowatoa katika nchi ya Misri, kwa mara ya kwanza ukaielewa kama stori tu, lakini ukigotea hapo, ukasema tayari nimeshaelewa hapo, sina haja ya kurudia tena siku nyingine.. Nakuambia biblia kwako itakuwa haina tofauti na vitabu kingine cha kihistoria ulichowahi kusoma huko nyuma.
Lakini ukasema siku nyingine nitatafakari, kisha ukamwomba Mungu, na kukaa katika utulivu ukairudia habari ile, utaona jambo jipya, limefunuliwa ndani yako, ambalo hukuwahi kulijua hapo mwanzo..
Wakati mwingine tena ukamwomba Roho Mtakatifu akusaidie, kisha ukarudia tena kusoma habari ile ile, utashangaa jambo lingine jipya unalipata ambalo siku za nyuma hukulipata..
Hivyo hivyo unavyozidi kuendelea, kurudia na kurudia ndivyo unavyolisafisha Neno la Mungu ndani yako,, Na matokeo yake ni kuwa, nguvu za Neno lake zinapenya katika roho yako, na kuleta mabadiliko makubwa sana, maishani mwako.
Shida inakuja pale, tunapodhani tumeimaliza biblia yote, pale tunaposoma habari Fulani na kujisemea moyoni, Aaah, tayari, yule kipofu Yesu aliishia kumpaka mate machoni akapona.. hivyo tunapita juu juu tu, kama sio kuiruka habari yote.
Wakati mwingine kanisani, unafundishwa, somo ambalo pengine ulishawahi kulisikia huko nyuma, na wewe badala ya kuwa mtulivu rohoni kusikiliza kwa makini, unasema, tayari hili nalifahamu..
Kumbuka, maneno safi ya Mungu, yanapatikana katika matanuru saba.
Hivyo natumai, kuanzia sasa sote, tutaacha kuwa wavivu wa kuyatafakari maandiko. Kwasababu lengo letu ni kuona nguvu za Neno la Mungu kweli zikifanya katika Maisha yetu ya wokovu. Tujitahidi sana kujifunza biblia.
Bwana akubariki sana.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali. Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
Mada Nyinginezo:
JINSI ROHO MTAKATIFU ANAVYOWAFUNULIA WATU MAANDIKO.
EPUKA KUPELELEZA KILA KITU MUNGU ANACHOKUAHIDIA.
Biblia inamaana gani kusema “vipo sita, naam saba”?
IEPUKE GHADHABU YA MUNGU.
DHIKI KUU INAKUJA NA UNYAKUO UPO KARIBU.
Rudi nyumbani
Print this post
SWALI: Ni mema gani na mabaya gani, Adamu na Hawa waliambiwa watayajua?, Kwasababu Kama ni mema siwalikuwa wanayafanya hapo kabla?
JIBU: Ili tuweze kuelewa vizuri, tujifunze katika mifano ya kawaida ya maisha.
Haiwezekani mtu kujijua kwamba yeye ni mrefu kama hajakutana na mtu mfupi katika maisha yake..
Yeye siku zote atajiona yupo kawaida tu..lakini siku atakapokutana na aliowazidi kimo ndipo atakapojijua kumbe yeye ni mrefu.
Kadhalika haiwezekani kujijua kama kwasasa una afya kama hujawahi kupitiaga kuumwa…zaidi ya yote hutajua hata maana ya kuwa na afya ni nini.
Lakini siku ile utakapougua na hamu yote ya kula kupotea, ndipo utakapojijua kuwa kumbe siku kadhaa nyuma ulikuwa ni mwenye afya sana.
Vile vile haiwezekani kujijua kuwa unatenda wema kama hujawahi kuujua ubaya…
Wewe utakuwa unaufanya tu! Na kuona kawaaida, Lakini hutajua kama unachofanya ni kitu chema…siku utakapokuja kuuona ubaya, ukifanywa na mwingine..ndipo utakapojua kuwa kumbe wewe ulikuwa mwema. N.k
Sasa hiyo ni mifano tu ya kimaisha,Sasa tukirudi pale Edeni,jambo ni lile lile, Adamu na Hawa walikuwa wanatenda mema lakini walikuwa hawajijui kama wanatenda mema, mpaka siku walipofanya ubaya na kuona madhara yake.
Ndio maana Mungu aliwakataza Adamu na Hawa wasile yale matunda, maana yake wasiujaribu ubaya…kwasababu siku watakapoujaribu ndipo watakapojijua kuwa kumbe siku kadhaa nyuma walikuwa katika mema.
Maana yake watajujua kumbe walikuwa katika utakatifu..
Hiyo ndio maana ule mti ukajulikana kama ni mti wa UJUZI WA MEMA NA MABAYA …Na si mti tu wa UJUZI WA MABAYA..hapana! bali mema na mabaya.. kwasababu mambo hayo mawili yanakwenda pamoja…hayaachani…
Kadhalika na sisi tunapokuwa dhambini tunakuwa tunajiona tupo sawa na njia zetu hizo, Hatujioni kama tupo hatarini, wala matatizoni, tunaona ni kawaida maisha ndivyo yalivyo..
Lakini siku tunapompokea Yesu, na kuonja Mema.. ndipo macho yetu yanafumbuliwa na kuelewa kwamba kumbe maisha tuliyokuwa tunaishi yalikuwa ni maisha mabaya, yalikuwa yana kasoro nyingi, yalikuwa ni ya mateso, yalikuwa ya tabu na hatari…lakini tulipokuwa huko dhambini tulikuwa hatulioni hilo..
Na YESU KRISTO, Ndiye ule MTI WA UZIMA. Kwamba kila atakayeonja matunda ya mti ule hatatamani tena mabaya..na macho yake yatafumbuliwa, na kujitambua na hivyo kujitenga mbali na dhambi..
Adamu na Hawa walipokula na kujijua kuwa wapo dhambini walitamani kurudi, lakini walishindwa kwasababu njia ilifungwa.
Lakini sasa njia imefunguliwa, ipo wazi na njia hiyo si nyingine zaidi ya YESU KRISTO. Ni kwasababu gani leo unaona ulevi unaoufanya ni kawaida?..ni kwasababu bado hujampokea Yesu na macho yako kufumbuliwa..siku utakapoocha kipawa cha Roho Mtakatifu ndipo utajiona kuwa hizo pombe zilikuwa ni sumu, huo uasherati ulikuwa ni kitanzi na wala hauna raha yoyote zaidi ni mateso..
Ndipo utakapojua kuwa kumbe maisha ya chuki, vinyongo na visasi yalikuwa ni maisha ya shida.
Bwana leo anatuita wote..na anasema tuonje!..Maana yake tujaribu kula matunda hayo ya mti wa uzima, tuone kama tutatamani kubaki dhambini.
Zaburi 34:8 “Onjeni mwone ya kuwa BWANA yu mwema; Heri mtu yule anayemtumaini”.
Je! Umempokea Kristo?
Kama bado mlango wa kutubu upo wazi sasa, lakini hautakuwa hivyo siku zote. Mpokee Yesu leo akutue mizigo na utapata raha ambayo hujawahi kuipata.
Mathayo 11:28 “Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha 29 Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu”
Mathayo 11:28 “Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha
29 Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu”
Maran atha!
JINSI EDENI ILIVYOKUWA.
Biblia imemaanisha nini iliposema “hawezi mtu kusema, Yesu ni Bwana, isipokuwa katika Roho Mtakatifu”
JIFUNZE KUELEWA MAANA YA KUOA/KUOLEWA KABLA YA KUINGIA HUKO.
MTI WA UZIMA NA MTI WA MAARIFA.
Kama wakitenda mambo haya katika mti mbichi, itakuwaje katika mkavu?
Bwana alisema…
Zaburi 34:8
[8]Onjeni mwone ya kuwa BWANA yu mwema; Heri mtu yule anayemtumaini.
[8]Onjeni mwone ya kuwa BWANA yu mwema;
Heri mtu yule anayemtumaini.
Maana yake ni kuwa Mungu ametoa nafasi kwa kila mtu ambaye yupo mbali na neema kuonja au kujaribu kwanza uzuri ulioko ndani yake kabla hajauingia moja kwa moja..kwamfano kujaribu kungalia kama ndani ya Kristo kuna furaha, au amani, au upendo n.k.
Na pale mtu anapoona kuwa ipo basi anawajibika kumuishia Mungu maisha yake yote, lakini kama hajaiona basi anaruhusiwa kughahiri uamuzi wake..Na Ukweli ni kwamba hakuna aliyemjaribu Kristo akatamani kutoka baada ya hapo.
Lakini sio sisi tu tunaonja vya Mungu.. Mungu naye pia anayotabia ya kutuonja sisi auminifu wetu na uelekevu wetu kwake kama tunakidhi kweli vigezo vya yeye kutupa moja kwa moja kile tulichomuomba…au kutukaribia moja kwa moja milele.
Sasa hatua kama hii ukishafikia tambua kuwa unapaswa ung’ang’ane kweli kweli kwasababu huwa hakiwi kipindi cha raha sana.
Tukirudi kwenye biblia…tunaona wana wa Israeli walipotoka Misri, Mungu alikuwa nao karibu katika kiila hatua waliyopiga, walichokitaka walikipata wala hawakuachwa bila majibu..mpaka wanavuka bahari ya shamu wote wakawa wanamwimbia Mungu na kumchezea kwa shangwe kwa jinsi alivyowatendea miujiza mikubwa..Hivyo hilo likamvutia Mungu sana..Mungu akashawishika kushuka atembee nao milele katika furaha na raha..
Lakini kabla ya yeye kufanya vile ilimpasa kwanza AWAONJE..aone kama ni kweli wamekidhi vigezo vya yeye kuwa Mungu wao au la.
Hivyo alichofanya ni kuwaacha siku tatu kwa Kiu kule janwani pindi tu walipovuka bahari ya shamu, jambo ambalo hawajawahi kulipitia kabisa maisha yao yote tangu walipoanza kutembea na Mungu..
Tusome…
Kutoka 15:22-25
[22]Musa akawaongoza Israeli waende mbele kutoka Bahari ya Shamu, nao wakatokea kwa jangwa la Shuri; wakaenda safari ya siku tatu jangwani wasione maji. [23]Walipofika mahali palipoitwa Mara hawakupata kuyanywa yale maji ya Mara, kwa kuwa yalikuwa machungu; kwa ajili ya hayo jina lake likaitwa Mara. [24]Ndipo watu wakamnung’unikia Musa, wakisema, Tunywe nini? [25]Naye akamlilia BWANA; BWANA akamwonyesha mti, naye akautia katika hayo maji, maji yakawa matamu. Basi akawawekea amri na hukumu huko, AKAWAONJA HUKO.
[22]Musa akawaongoza Israeli waende mbele kutoka Bahari ya Shamu, nao wakatokea kwa jangwa la Shuri; wakaenda safari ya siku tatu jangwani wasione maji.
[23]Walipofika mahali palipoitwa Mara hawakupata kuyanywa yale maji ya Mara, kwa kuwa yalikuwa machungu; kwa ajili ya hayo jina lake likaitwa Mara.
[24]Ndipo watu wakamnung’unikia Musa, wakisema, Tunywe nini?
[25]Naye akamlilia BWANA; BWANA akamwonyesha mti, naye akautia katika hayo maji, maji yakawa matamu. Basi akawawekea amri na hukumu huko, AKAWAONJA HUKO.
Unaona mstari wa 25 inasema Mungu akawaonja huko.kama kweli walimpenda kutoka moyoni au ni kwa miujiza tu..au kwa mikate tu..au kwa mafanikio tu..
Lakini tunaona wana wa Israeli walinung’unika badala ya kujinyenyekeza..Hivyo Mungu hakuona ukamilifu ndani yao.akajua kumbe walimpendea kwasababu walipata raha tu lakini sio kwasababu ni Mungu wao..Laiti wangejinyenyeza ni wazi kuwa tangu ule wakati na kuendelea wasingekaa kusikia kitu kinachoitwa shida au taabu au masumbufu…
Ndugu yangu..Mungu akidhamiria kushuka kwako moja kwa moja kukaa na wewe au kukupa kitu fulani ulichomuomba ni sharti kwanza AKUONJE..uaminifu wako kama alivyofanya kwa Ibrahimu kumtoa mwanae Isaka..Hiyo ndio kanuni yake ambayo wana wa Israeli walishindwa kuielewa..
Soma pia Kumbukumbu 8:1-3 utaona Bwana akilisisitiza neno hilo hilo..
Hivyo ndugu uliyeokoka..lijue jambo hilo, liweke akiba moyoni mwako. Kabla hujawa rafiki wa Mungu wa milele ni sharti kwanza akuonje..ukikidhi vigezo basi ndio kimekuwa chako milele.
Shalom.
BIRIKA LA SILOAMU.
USIPOTEZWE NA MANENO YA MANABII WA UONGO.
UFUNUO: Mlango wa 14
KUOTA MAFURIKO,KUOTA MAJI MENGI,KUOTA MAWIMBI.
Je! ni risasi hizi tunazozijua za bunduki, au ni risasi ya namna gani?.
Jibu: Katika biblia kuna maneno yaliyotumika ambayo yakiletwa katika nyakati zetu, yanabadilika maana kabisa.. kwamfano utaona Neno “fisadi” likitajwa katika biblia.. Maana halisi ya neno hilo sio “mtu anayedhulumu fedha za umma”.. Bali maana halisi ya neno hilo ni “mtu anayefanya uasherati uliovuka mipaka”.
Hali kadhalika kuna neno kama “Fedha”.. Neno hili kama lilivyotumika nyakati za kale ni tofauti na linavyotumika leo, Leo hii ukizungumzia Fedha, moja kwa moja akili zinakwenda katika “Hela” iwe ya noti au sarafu. . Lakini kiuhalisia maana halisi ya neno Fedha sio “Hela”.. Bali ni madini aina ya “Fedha” kama vile yalivyo madini aina ya dhahabu.. Hata pale katika maandiko Bwana aliposema Fedha na dhahabu ni mali yangu,(Hagai 2:8) hakumaanisha “Hela na dhahabu”… bali alimaanisha madini aina ya fedha, na madini aina ya dhahabu, ndio mali za Bwana. ..
Sasa kwanini madini haya ya fedha leo ndio yamegeuzwa maana na kuwa Hela/pesa?..kiasi kwamba hela yoyote leo inaitwa fedha.
Ni kwasababu tangu zamani hata sasa malighafi inayotumika kutengenezea sarafu nyingi, ni madini hayo ya fedha.. utaona sarafu nyingi, kama zile za sh.10, au 20 au 500 hazijatengenezwa kwa chuma, wala dhahabu bali zimetengenezwa kwa madini ya fedha,..hivyo hiyo ikafanya Hela zote zijulikane kama fedha..siku hizi hata Noti zote zinajulikana kama ni fedha, jambo ambalo kiuhalisia sio sawa.
Na madini ya fedha yanaweza kutumika kwa matumizi mbalimbali sio tu kutengenezea sarafu, bali pia vyombo vya chakula, urembo n.k..isipokuwa tumizi lililo maarufu ni hilo la kutengenezea Sarafu.
Kwa mantiki hiyo hiyo pia kwa Neno “Risasi”. Leo hii ukitaja neno risasi moja kwa moja akili za wengi zinakwenda kwenye kile kipande kidogo cha chuma kinachotoka ndani ya bunduki.
Lakini kiuhalisia hiyo sio maana ya Risasi.. Risasi ni aina nyingine ya madini, ijulikanayo kwa jina hilo.. kama vile ilivyo fedha, dhahabu, almasi, chuma, shaba n.k.. Vivyo hivyo kuna madini aina ya Risasi ambayo kwa lugha ya kiingereza yanaitwa “Lead”.
Na madini haya yajulikanayo kama Risasi yanamatumizi mengi mbali mbali kama vile Fedha ilivyokuwa na matumizi mbali mbali sio tu kutengeneza sarafu, bali pia vitu vingine.. Kadhalika madini haya ya Risasi matumizi yake ambayo ni maarufu leo hii ni kutengenezea hicho kisilaha kidogo kijulikanacho kama risasi leo… lakini hayo sio matumizi pekee ya madini hayo, bali ina matumizi mengine mengi ambayo ndio hasaa yaliyokuwa yanatumika enzi za zamani.
Nyakati za biblia madini hayo ya Risasi, yalikuwa yanatumika sana sana katika kutengenezea vyombo vya kupikia, na kuhifadhia vitu vya moto sana, kwasababu yalikuwa ni magumu kuyeyuka hata kwa moto mkubwa, madini ya chuma yanawahi kuyeyuka kabla ya Risasi, kadhalika madini haya yalitumika kwaajili ya maandishi, yalikuwa ni bora kwa kuhifadhi maandishi kwa muda mrefu, tofauti na mengine yote. (Ayubu 19:24).
Hivyo yalikuwa ni madini ya kibiashara sana enzi za zamani na hata sasa.. Nyakati hizi yamezidi matumizi mpaka kufikia kutengeneza vifaa vya kisilaha kama hizi risasi zinazotumika katika bunduki.
Katika biblia madini hayo yameonekana yakitajwa katika sehemu kadhaa..
Ezekieli 27:12 “Tarshishi alikuwa mfanya biashara kwako, kwa sababu ya wingi wa utajiri wa kila aina; kwa fedha, na chuma, na bati, na risasi, walifanya biashara, wapate vitu vyako vilivyouzwa”.
Unaweza kuyapata pia katika vitabu vifuatavyo… Hesabu 31:22, Yeremia 6:29 na Zekaria 5:7
Lakini katika roho sisi watu wa Mungu tunafananishwa na vitu hivyo vya thamani.. kama fedha, dhahabu, almasi n.k
Kama vile chuma na dhahabu ili viwe imara na ili ving’ae ni lazima vipitishwe kwenye moto, na watu wa Mungu waliookoka ili wawe wa thamani mbele za Mungu ni lazima wapitishwe kwenye moto (yaani majaribu mbali mbali).
Kadhalika ili risasi iwe bora ni lazima ipitishwe nayo kwenye moto.. Na sisi tunafananishwa na risasi za Bwana.. na matumizi makubwa ya risasi katika zama zetu hizi ni SILAHA, Kadhalika na sisi ni silaha za Bwana, dhidi ya majeshi yote ya adui..Ili tuwe imara hatuna budi kupitishwa katika moto.. Ndivyo maandiko yanavyosema…
Ezekieli 22:18 “Mwanadamu, nyumba ya Israeli imekuwa taka za fedha kwangu; wote wamekuwa shaba, na bati, na chuma, NA RISASI, kati ya tanuu; wamekuwa taka za fedha. 19 Basi Bwana MUNGU asema hivi; Kwa sababu ninyi nyote mmekuwa taka za fedha, tazama, nitawakusanya kati ya Yerusalemu. 20 Kama vile watu wakusanyavyo FEDHA, NA SHABA, NA CHUMA, NA RISASI, NA BATI, KATI YA TANUU, ILI KUVIFUKUTIA MOTO NA KUVIYEYUSHA; ndivyo nitakavyowakusanya ninyi katika hasira yangu, na ghadhabu yangu, nami nitawalaza huko, na kuwayeyusha. 21 Naam, nitawakusanya, na kuwafukutia moto wa ghadhabu yangu, nanyi mtayeyushwa kati yake”.
Ezekieli 22:18 “Mwanadamu, nyumba ya Israeli imekuwa taka za fedha kwangu; wote wamekuwa shaba, na bati, na chuma, NA RISASI, kati ya tanuu; wamekuwa taka za fedha.
19 Basi Bwana MUNGU asema hivi; Kwa sababu ninyi nyote mmekuwa taka za fedha, tazama, nitawakusanya kati ya Yerusalemu.
20 Kama vile watu wakusanyavyo FEDHA, NA SHABA, NA CHUMA, NA RISASI, NA BATI, KATI YA TANUU, ILI KUVIFUKUTIA MOTO NA KUVIYEYUSHA; ndivyo nitakavyowakusanya ninyi katika hasira yangu, na ghadhabu yangu, nami nitawalaza huko, na kuwayeyusha.
21 Naam, nitawakusanya, na kuwafukutia moto wa ghadhabu yangu, nanyi mtayeyushwa kati yake”.
Je umempokea Yesu?.. je wewe ni dhahabu safi?, ni fedha safi?, ni Risasi safi kwa Bwana?.. kama bado unasubiri nini?..Unawezaje kuishi maisha ya namna hayo yasiyo na thamani yoyote mbele za Mungu..Mpokee Kristo leo, na ukabatizwe katika ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa jina la Yesu Kristo, upate ondoleo la dhambi, na Bwana atakupa kipawa cha Roho wake Mtakatifu, atakayekuongoza katika kweli yote.
Bwana akubariki.
Ni kwa namna gani malaika wa mbinguni wanaweza kutuhubiria sisi injili?
APENDAYE FEDHA HASHIBI FEDHA.
Fuawe ni nini? Kama tunavyosoma katika Isaya 41:7
KUNA UMUHIMU WA KUWA MTU WA KURIDHIKA.
ONDOA TAKATAKA KATIKA FEDHA, NA CHOMBO KITATOKEA KWA MTAKASAJI.
Ufisadi una maanisha nini katika biblia?
JIBU: Saumu ni neno lenye asili ya lugha ya “kiaramu” lenye maana ya “kujizua kufanya jambo/kitu fulani kwa ajili ya ibada”.
Hivyo pale mtu anapoacha kula kwa kipindi fulani, kwa ajili ya sala..Mtu huyo yupo katika saumu.au kwa jina tulilolizoea tunasema yupo katika mfungo.
Neno hilo utalipata katika vifungu hivi kwenye biblia..
Zekaria 8:19
[19]BWANA wa majeshi asema hivi, Saumu ya mwezi wa nne, na saumu ya mwezi wa tano, na saumu ya mwezi wa saba, na saumu ya mwezi wa kumi, zitakuwa furaha na shangwe, na sikukuu za kuchangamkia, kwa nyumba ya Yuda; basi zipendeni kweli na amani.
Yoeli 1:14
[14]Takaseni saumu, iteni kusanyiko la dini,
Wazee na wakusanye wenyeji wote wa nchi; Waende nyumbani kwa BWANA, Mungu wenu, Na kumlilia BWANA,
Soma pia Yoeli 2:15.utaliona neno hilo.
Saumu ya kweli ni ipi?
Lakini pia tofauti na wengi tunavyodhani..kwamba saumu inayompendeza Mungu ni ile ya chakula tu..ni kweli hiyo anaitazama lakini sio kiini cha saumu anayotaka kuiona ndani ya mtu.. Saumu anayoipokea ni ile ya kufunga vifungo vya uovu na dhambi.
Isaya 58:3-8
[3]Husema, Mbona tumefunga, lakini huoni? Mbona tumejitaabisha nafsi zetu, lakini huangalii? Fahamuni, siku ya kufunga kwenu mnatafuta anasa zenu wenyewe, na kuwalemea wote watendao kazi kwenu. [4]Tazama, ninyi mwafunga mpate kushindana na kugombana, na kupiga kwa ngumi ya uovu. Hamfungi siku hii ya leo hata kuisikizisha sauti yenu juu. [5]Je! Kufunga namna hii ni SAUMU niliyoichagua mimi? Je! Ni siku ya mtu kujitaabisha nafsi yake? Ni kuinama kichwa kama unyasi, na kutanda nguo za magunia na majivu chini yake? Je! Utasema ni siku ya kufunga, na ya kukubaliwa na BWANA? [6]Je! Saumu niliyoichagua, siyo ya namna hii? Kufungua vifungo vya uovu, kuzilegeza kamba za nira, kuwaacha huru walioonewa, na kwamba mvunje kila nira? [7]Je! Siyo kuwagawia wenye njaa chakula chako, na kuwaleta maskini waliotupwa nje nyumbani kwako? Umwonapo mtu aliye uchi, umvike nguo; wala usijifiche na mtu mwenye damu moja nawe? [8]Ndipo nuru yako itakapopambazuka kama asubuhi, na afya yako itatokea mara; na haki yako itakutangulia; utukufu wa BWANA utakufuata nyuma ukulinde.
[3]Husema, Mbona tumefunga, lakini huoni? Mbona tumejitaabisha nafsi zetu, lakini huangalii? Fahamuni, siku ya kufunga kwenu mnatafuta anasa zenu wenyewe, na kuwalemea wote watendao kazi kwenu.
[4]Tazama, ninyi mwafunga mpate kushindana na kugombana, na kupiga kwa ngumi ya uovu. Hamfungi siku hii ya leo hata kuisikizisha sauti yenu juu.
[5]Je! Kufunga namna hii ni SAUMU niliyoichagua mimi? Je! Ni siku ya mtu kujitaabisha nafsi yake? Ni kuinama kichwa kama unyasi, na kutanda nguo za magunia na majivu chini yake? Je! Utasema ni siku ya kufunga, na ya kukubaliwa na BWANA?
[6]Je! Saumu niliyoichagua, siyo ya namna hii? Kufungua vifungo vya uovu, kuzilegeza kamba za nira, kuwaacha huru walioonewa, na kwamba mvunje kila nira?
[7]Je! Siyo kuwagawia wenye njaa chakula chako, na kuwaleta maskini waliotupwa nje nyumbani kwako? Umwonapo mtu aliye uchi, umvike nguo; wala usijifiche na mtu mwenye damu moja nawe?
[8]Ndipo nuru yako itakapopambazuka kama asubuhi, na afya yako itatokea mara; na haki yako itakutangulia; utukufu wa BWANA utakufuata nyuma ukulinde.
Umeona? Hivyo na wewe ufungapo basi fahamu kuwa Mungu anatazamia kuona mageuzi makubwa ya maisha yako dhidi ya dhambi na kutenda haki. Usifunge tu kidini ili kutumiza sheria.Funga kwa lengo la kuwa mkamilifu mbele zake.
Vinginevyo unaweza ukafunga hata siku 40 usiku na mchana bila kula, kama Musa na Mungu bado akaona unafanya kazi bure.
NJIA SAHIHI YA KUFUNGA.
KWARESMA IPO KIMAANDIKO?
Maana Ya Maneno Katika Biblia.
Mafundisho
Si kila tunayemuhubiria, ni lazima tuone matokeo ya papo kwa papo ya badiliko.. Ni kweli tunatamani iwe hivyo kwa watu wote , na wakati mwingine ukiwa kama muhubiri unaweza kuvunjika moyo, pale ambapo unazunguka kila mahali, mwezi mzima, au mwaka mzima, kuhubiri, halafu hufanikiwi kupata tunda lolote la kudumu, au hata ukiyapata basi ni machache sana, ukilinganisha na nguvu ulizowekeza hapo.
Lakini ukiwa katika hali kama hiyo, jambo ambalo unapaswa usilitoe katika akili yako ni kuwa, mwisho wa mavuno sio siku hiyo unayohubiri, mwisho wa mavuno sio leo uliyopo mkononi mwako. Mwisho wa mavuno utakuwa ni siku ile ya mwisho, Mungu atakapotuma malaika zake, kuyatenganisha magugu na ngano. Na ngano kuziweka ghalani, sio sasa.
Mathayo 13:39b … mavuno ni mwisho wa dunia; na wale wavunao ni malaika…. 49 Ndivyo itakavyokuwa katika mwisho wa dunia; malaika watatokea, watawatenga waovu mbali na wenye haki,
Mathayo 13:39b … mavuno ni mwisho wa dunia; na wale wavunao ni malaika….
49 Ndivyo itakavyokuwa katika mwisho wa dunia; malaika watatokea, watawatenga waovu mbali na wenye haki,
Kwahiyo ndugu, huyo mtu unayemshuhudia/ unaowashuhudia, ikiwa hawaonyeshi badiliko leo, bado wewe endelea kuhubiri, kwasababu wakati wa kuhitimisha kila kitu bado. Pengine leo unapanda mbegu, mwingine kesho atatia maji, au wewe unatia maji leo, mwingine atapalilia, au wewe utapalilia mwingine atamalizia kuvuna,.kabla ya mwisho wa mavuno kufika.
Kwahiyo, usivunjwe moyo sana, mwisho wa dunia bado, japo upo karibu sana, hivyo wewe endelea kuingaza nuru ya Kristo katika hichi kipindi kifupi tulichobakiwa nacho, hata kama matunda hutayaona sasa. Mwachie Mungu amalize kazi zake. Kwasababu Biblia inasema..
Mhubiri 11: 4 Mwenye kuuangalia upepo hatapanda; Naye ayatazamaye mawingu hatavuna.
Songa mbele. Tangaza habari za Kristo.
Nini maana ya mhubiri 9:11? si wenye mbio washindao katika michezo?
AHADI YA ROHO ILIYOSALIA SASA KWA KIPINDI CHETU.
Ahera ni wapi? Kama tunavyosoma katika biblia.
UPO UMUHIMU MKUBWA WA KUMTOLEA BWANA!
Jina la Mwokozi wetu, Yesu libarikiwe.. Karibu tujifunze biblia, leo tutajifunza jambo dogo, linalohusiana na faida za kumtolea Bwana.
Moja ya mambo ambayo shetani kayakoroga sana katika Ukristo na nje ya ukristo, ni suala la utoaji.
Shetani hataki watu wanaomjua Mungu wawe watoaji na hata wale wasiomjua Mungu wawe watoaji.
Kwasababu anajua hata mtu asiyemjua Kristo akiwa mtoaji, basi atapata thawabu kwa hicho…kwahiyo atajitahidi kumpandikizia mtu roho ya kutokutoa kwa gharama zozote, hata akisikia jambo lolote linalohusiana na kutoa asisikilize, na hata achukie kabisa.
Lakini nataka nikuambie.. Chochote unachokitoa aidha kwa Bwana au kwa mtu , kina thamani kubwa sana kwake yule unayekipokea…Kama ni Kristo au kama ni mwanadamu mwenzako.
Sijui kama umewahi kupitia mazingira fulani ambayo upo katika hali ya kuhitaji sana, halafu anatokea mtu anakusaidia, au anakukopesha…kuna furaha fulani unaipata isiyokuwa ya kawaida.
Sasa wengi wetu tunafikiri ni sisi tu waanadamu ndio tunapitia hayo mazingira ya kupungukiwa na kuhitaji msaada..Lakini leo nataka nikuambie ya kwamba futa hayo mawazo… Hata Kristo naye ambaye ni Mungu, anapitia hayo mazingira kila siku, na anatafuta watu wa kumsaidia, Ingawa yeye ana kila kitu..
Kikawaida ukiwa na mtoto au watoto wanaokupenda na wewe unawapenda, halafu uwaone wanapitia shida..ni wazi kuwa wewe ndio utateseka zaidi na kupitia shida zaidi..kwasababu kwanza ni damu yako, na vile vile wapo moyoni mwako..
Na Kristo naye ni hivyo hivyo, wale wote ambao wapo katika agano la damu yake, na wapo moyoni mwake, na yeye yupo mioyoni mwao..wanapopitia matatizo ni yeye ndiye anayekuwa katika shida..zaidi hata ya yule anayepitia shida.
Kwahiyo hata Kristo naye anapitia shida hata sasa, ndivyo maandiko yanavyosema..
Mathayo 25:41 “Kisha atawaambia na wale walioko mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake; 42 kwa maana nalikuwa na njaa, msinipe chakula; nalikuwa na kiu, msininyweshe; 43 nalikuwa mgeni, msinikaribishe; nalikuwa uchi, msinivike; nalikuwa mgonjwa, na kifungoni, msije kunitazama. 44 Ndipo hao pia watajibu, wakisema, Bwana, ni lini tulipokuona wewe una njaa, au una kiu, au u mgeni, au u uchi, au u mgonjwa, au u kifungoni, tusikuhudumie? 45 Naye atawajibu, akisema, Amin, nawaambia, Kadiri msivyomtendea mmojawapo wa hao walio wadogo, hamkunitendea mimi. 46 Na hao watakwenda zao kuingia katika adhabu ya milele; bali wenye haki watakwenda katika uzima wa mmilele”.
Mathayo 25:41 “Kisha atawaambia na wale walioko mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake;
42 kwa maana nalikuwa na njaa, msinipe chakula; nalikuwa na kiu, msininyweshe;
43 nalikuwa mgeni, msinikaribishe; nalikuwa uchi, msinivike; nalikuwa mgonjwa, na kifungoni, msije kunitazama.
44 Ndipo hao pia watajibu, wakisema, Bwana, ni lini tulipokuona wewe una njaa, au una kiu, au u mgeni, au u uchi, au u mgonjwa, au u kifungoni, tusikuhudumie?
45 Naye atawajibu, akisema, Amin, nawaambia, Kadiri msivyomtendea mmojawapo wa hao walio wadogo, hamkunitendea mimi.
46 Na hao watakwenda zao kuingia katika adhabu ya milele; bali wenye haki watakwenda katika uzima wa mmilele”.
Umeona?
Na “Wadogo” wanaozungumziwa hapo sio wale watu wanaosimama njiani na kuomba, ambao wengi wao ni watu wakidunia na walevi, watukanaji, na hata wengine wanamtukana Kristo hadharani..
Bali “wadogo”, Kristo anawaozungumzia hapo ni wale ambao “Ndani yao yupo Kristo wa kweli”… Lakini wapo katika mahitaji pengine kutokana na kuishikilia imani yao, wapo vifungoni pengine kutokana na kuhubiri injili, hawana chakula, mavazi n.k kutokana na mambo ya kiimani wanayoyafanya. Hao ndio ambao ukiwasaidia unakuwa umemsaidia Kristo mwenyewe…Kwasababu Kristo yupo ndani yao.
Sasa kuna aina ya mahubiri, yameenea sana leo, kwamba watu wote waliompokea Kristo, hawapitii kabisa kipindi cha kuwa na mahitaji.. Nataka nikuambie hiyo injili si ya ukweli..watu waliookoka watapitia vipindi vyote, vya kupungukiwa na vya kuongezekewa, watapitia vipindi vya magonjwa, watapitia vipindi vya vifungo, na dhiki kwasababu bado wapo ulimwenguni..Lakini hiyo haimaanishi kuwa hawatapitia pia vipindi vya raha, watavipitia lakini pia vya dhiki watakutana navyo.
Sasa katika wakati kama huo, ambao unaona watu wa Mungu wapo katika hali ya kuhitaji, huo ndio wakati wa kujizombea baraka..kwasababu ukiwasaidia hao, umemsaidia Kristo mwenyewe..Mungu anaruhusu watu wake wawe hivyo, sio kwamba hawezi kuwatajirisha ghafla la!..bali anawafanya hivyo, ili watu wengine wapate nafasi ya kubarikiwa kwa kuwasaidia.
Kwahiyo ndugu usikwepe hata kidogo kumtolea Bwana kwasababu kuna thawabu kubwa, Bwana Yesu mwenyewe alisema maneno haya…
Marko 9:41 “Kwa kuwa ye yote atakayewanywesha ninyi kikombe cha maji, kwa kuwa ninyi ni watu wa Kristo, amin, nawaambia, hatakosa thawabu yake”.
Na hilo sio jukumu la kundi fulani tu la watu, kwamba ni watu fulani wenye uwezo ndio wanapaswa wamtolee Bwana..Au kwamba ni washirika na waumini tu, hapana!..bali ni la watu wote, walio wahudumu na wasio wahudumu…Watumishi na wasio watumishi. Wote hatuna budi kumtolea Bwana kwa namna hiyo, kama tunataka kubarikiwa.
DALILI ZIPI ZITAMTAMBULISHA MTU KUWA AMEFANYIKA KIUMBE KIPYA?
Zile Rangi saba za Upinde wa Mvua zinawakilisha nini?
Roho, Nafsi, na Mwili vina utofauti gani?
Katika (Mathayo 25:8 na Marko 16:8) Wale wanawake walitangaza kufufuka kwa Bwana au walikaa kimya?
MKARIBIE BWANA ZAIDI ILI UFANYIKE NGUZO.
HEKIMA YA KIMUNGU, INAINGIAJE MIOYONI MWETU?
SWALI: Kwanini katika Mwanzo 5:2 tunasoma Mungu aliwaita Adamu na Hawa jina moja la Adamu..na sio mawili tofauti.?
Mwanzo 5:2
[2]mwanamume na mwanamke aliwaumba, akawabariki akawaita jina lao Adamu, siku ile walipoumbwa.
JIBU: Kumbuka siku Mungu alipowaumba wanadamu(mwanamke na mwanamume)..hàkuwaumba wote kwa pamoja..Bali alimuumba ADAMU peke yake..kisha hawa baadaye..ambaye alikuja kuumbwa kutoka katika ubavu wa Adamu.
Hivyo wakati Mungu anatoa majina kwa viumbe vyake Hawa hakuwepo..Jina hilo alikuja kupewa na Adamu mwenyewe baadaye soma..
Mwanzo 3:20
[20]Adamu akamwita mkewe jina lake Hawa; kwa kuwa yeye ndiye aliye mama yao wote walio hai.
Kwahiyo kwanini Mungu aliwaita jina moja ni kwasababu alipomuona Hawa alimuona Adamu kwasababu ni zao lake..hivyo machoni pake hakuona mwanamke anastahili kuitwa kitu kingine tofauti na jina la Mume wake ..Ni sawa na wewe uone ‘sisimizi’ huwezi wala huioni sababu ya kumuita sisimizi wa kike jina tofauti na yule wa kiume..wote utawaita tu jina moja sisimizi..na ndivyo ilivyokuwa machoni pa Mungu kwa Adamu na Hawa.
Lakini Mungu alitaka kutufundisha nini kwa kuwaita vile?
Ikiwa wewe ni mwanamke fahamu kuwa ukishaolewa, Mungu hakuoni tena kama ni mtu tofauti na mumeo. Atakutambua kwa jina lake. Hivyo jifunze kumtii mumeo. Kwasababu yeye ndio kila kitu kwako kwa muda huo.
Vilevile wewe kama mume..mpende mke wako, kwasababu ule ni ubavu wako. Na ndio maana haitwi jina lingine zaidi ya hilo la kwako. Hata kama utajaribu kumuita kwa majina mengine lakini Mungu anamtambua kwa hilo jina lako. Hivyo jifunze kumpenda na kumuhudumia.
KWANINI YESU NI ADAMU WA PILI?
Je Mungu aliumba watu wengine kabla ya Adamu?
Ni kwanini Raheli afanye vile, ilihali Mungu alikataza ibada za sanamu?.
Jibu: Tusome,
Mwanzo 31:18 “Akachukua wanyama wake wote, na mali yake yote aliyokuwa ameyapata, na wanyama aliowapata katika Padan-aramu, ili afike kwa Isaka babaye katika nchi ya Kanaani. 19 Basi Labani alikuwa amekwenda kuwakata manyoya kondoo zake, na Raheli akaviiba vinyago vya babaye”.
Mwanzo 31:18 “Akachukua wanyama wake wote, na mali yake yote aliyokuwa ameyapata, na wanyama aliowapata katika Padan-aramu, ili afike kwa Isaka babaye katika nchi ya Kanaani.
19 Basi Labani alikuwa amekwenda kuwakata manyoya kondoo zake, na Raheli akaviiba vinyago vya babaye”.
Lengo la Raheli kuiba vinyago vya baba yake si kwasababu alikuwa anataka kwenda kuviabudu (yaani kuvifanya miungu yake) kama baba yake alivyofanya..
Hapana bali lengo la kufanya vile ni ili akaviharibu. Kwasababu hivyo ndio vimekuwa chanzo cha matatizo yote, (Kati ya Labani na Yakobo).
Ikumbukwe kuwa Raheli ndiye aliyekuwa mke wa ahadi wa Yakobo, na mara ya kwanza kabisa aliahidiwa kumchukua kutoka kwa Baba yake Labani, baada ya kutumika kwa miaka 7, lakini tunaona baada ya miaka hiyo ya utumishi kuisha…Yakobo hakupewa Raheli badala yake aliozwa Lea dada yake.
Mwanzo 29:25 “Ikawa, kulipokuwa asubuhi, kumbe! Ni Lea. Akamwambia Labani, Nini hii uliyonitenda? 26 Sikukutumikia kwa Raheli? Mbona umenidanganya? Labani akasema, Havitendeki hivi kwetu, kumtoa mdogo kabla ya mkubwa”
Mwanzo 29:25 “Ikawa, kulipokuwa asubuhi, kumbe! Ni Lea. Akamwambia Labani, Nini hii uliyonitenda?
26 Sikukutumikia kwa Raheli? Mbona umenidanganya? Labani akasema, Havitendeki hivi kwetu, kumtoa mdogo kabla ya mkubwa”
Ukiendelea kusoma mbeleni utazidi kuona visa Labani alivyokuwa anamfanyia Yakobo, mpaka Labani kufikia hatua ya kutaka kumfilisi Yakobo mali zake.
Mwanzo 31:36-4236 Yakobo akakasirika, akagombana na Labani. Yakobo akajibu, akamwambia Labani, N’nini hatia yangu? Nayo ni nini dhambi yangu, hata ukanifuatia namna hii? 37 Umepapasa-papasa vyombo vyangu vyote; ni kitu gani ulichokiona cha nyumbani mwako? Kiweke hapa mbele ya ndugu zangu, na ndugu zako, wakaamue kati yetu. 38 Miaka hii ishirini nimekaa kwako; kondoo zako wala mbuzi zako wake hawakuharibu mimba wala waume katika wanyama wako sikuwala. 39 Kilichoraruliwa na hayawani sikukuletea, mimi mwenyewe nimetwaa hasara yake, wewe umekidai katika mkono wangu, ikiwa kilichukuliwa mchana, au ikiwa kilichukuliwa usiku. 40 Hii ilikuwa hali yangu; mchana jua likanipata, na baridi usiku, usingizi ukanitoka machoni mwangu. 41 Miaka hii ishirini nimekaa nyumbani mwako; nilikutumikia miaka kumi na minne kwa binti zako wawili, na miaka sita kwa wanyama wako, nawe umebadili mshahara wangu mara kumi. 42 Kama Mungu wa baba yangu, Mungu wa Ibrahimu na Hofu ya Isaka, hangalikuwa pamoja nami, hakika sasa ungalinifukuza mikono mitupu. Mateso yangu na kazi za mikono yangu Mungu ameziona, akakukemea usiku huu”.
Mwanzo 31:36-4236 Yakobo akakasirika, akagombana na Labani. Yakobo akajibu, akamwambia Labani, N’nini hatia yangu? Nayo ni nini dhambi yangu, hata ukanifuatia namna hii?
37 Umepapasa-papasa vyombo vyangu vyote; ni kitu gani ulichokiona cha nyumbani mwako? Kiweke hapa mbele ya ndugu zangu, na ndugu zako, wakaamue kati yetu.
38 Miaka hii ishirini nimekaa kwako; kondoo zako wala mbuzi zako wake hawakuharibu mimba wala waume katika wanyama wako sikuwala.
39 Kilichoraruliwa na hayawani sikukuletea, mimi mwenyewe nimetwaa hasara yake, wewe umekidai katika mkono wangu, ikiwa kilichukuliwa mchana, au ikiwa kilichukuliwa usiku.
40 Hii ilikuwa hali yangu; mchana jua likanipata, na baridi usiku, usingizi ukanitoka machoni mwangu.
41 Miaka hii ishirini nimekaa nyumbani mwako; nilikutumikia miaka kumi na minne kwa binti zako wawili, na miaka sita kwa wanyama wako, nawe umebadili mshahara wangu mara kumi.
42 Kama Mungu wa baba yangu, Mungu wa Ibrahimu na Hofu ya Isaka, hangalikuwa pamoja nami, hakika sasa ungalinifukuza mikono mitupu. Mateso yangu na kazi za mikono yangu Mungu ameziona, akakukemea usiku huu”.
Sasa kwa mambo kama hayo na mengine mengi ni wazi kuwa Raheli aliamini miungu ya baba yake ndio chanzo cha matatizo yote (Au ndiyo inayompelekesha yeye kuwa hivyo alivyo, au kutoa maamuzi anatoyatoa, ya kusumbua Yakobo).
Hivyo siku anaondoka yeye na Yakobo, Raheli aliiba ili kwamba baba yake asiitumie hiyo ikamwaribu akili na kusababisha madhara zaidi kwa Yakobo na kwake yeye Raheli. Hivyo ikawa msaada kwa Labani baba yake na Yakobo.
Hiyo ndio sababu (Ni ili amponye baba yake)..Endapobaba yake angeendelea navyo mbali na kumharibu akili, vingemsababishia kuadhibiwa na Mungu.Kwasababu wote wanaoabudu miungu, hawafiki mbali.
Hivyo Raheli aliiba ili akaiharibu.Ndio maana hata baada ya kuiiba alienda kuikalia (Mwanzo 31:34-35). Sasa kwa mtu mwenye lengo la kwenda kuiabudu asingeikalia, hakuna mtu anayeweza kukalia mungu wake..(hata wote wanaoabudu sanamu, huwa wanaziheshimu hizo sanamu zao)..hawawezi kuzikalia kwa lengo lolote lile.
Na baada ya hapo hatuoni, Labani akimfuatilia wala kumsumbua tena Yakobo.Ikifundisha kuwa kuna mazingira tutawaokoa watu kwa kuwanyakua kutoka kwenye hatari..kama Raheli alivyofanya kwa Baba yake.
Yuda 1:2 “na wengine waokoeni kwa kuwanyakua katika moto; na wengine wahurumieni kwa hofu, mkilichukia hata vazi lililotiwa uchafu na mwili”.
Maran atha
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
MTI UANGUKAPO, PAPO HAPO UTALALA.
Nifanye nini ili niishi maisha ya ushindi siku zote?
MKUU WA UZIMA AKUWEKE HURU.
HAKUNA MTU ANIONDOLEAYE, BALI MIMI NAUTOA MWENYEWE
Waanaki ni jamii ya watu wakubwa na warefu waliotoka katika uzao wa mtu mmoja anayeitwa Anaki mtoto wa arba (Yoshua 15:13, 21:11)..Maana halisi ya jina hilo kulingana na lugha ya kuyahudi ni ‘MTU MREFU’ au ‘MWENYE SHINGO NDEFU’.
Watu hawa waliishi upande wa kusini mwa Israeli, walikuwa ni wakubwa sana na wenye nguvu kuliko watu wengine wa kawaida walioishi ulimwenguni wakati ule.. vilevile walikuwa na nguvu kubwa za kivita, hakuna taifa lililoweza kushindana nalo.
Habari zao utazisoma sehemu nyingi sana katika biblia..lakini hivi ni baadhi ya vifungu vinavyowaelezea.
Kumbukumbu la Torati 1:28
[28]Twakwea kwenda wapi? Ndugu zetu wameiyeyusha mioyo yetu, wakituambia, Wale watu ni wengi, ni warefu kuliko sisi; miji nayo ni mikubwa, imejengewa kuta hata mbinguni; na zaidi ya hayo huko tumewaona Waanaki.
Kumbukumbu la Torati 9:1-3
[1]Sikiza, Ee Israeli; hivi leo unataka kuvuka Yordani uingie kwa kuwamiliki mataifa yaliyo makubwa, na yenye nguvu kukupita wewe, miji mikubwa iliyojengewa kuta hata mbinguni, [2]watu wakubwa, warefu, wana wa Waanaki, uwajuao, uliokuwa ukisikia wakitajwa hivi, Ni nani awezaye kusimama mbele ya wana wa Anaki? [3]Basi jua siku hii ya leo kuwa BWANA, Mungu wako, ndiye atanguliaye kuvuka mbele yako kama moto uteketezao; atawaangamiza, tena atawaangusha mbele yako; ndivyo utakavyowafukuza na kuwapoteza upesi, kama alivyokuambia BWANA.
[1]Sikiza, Ee Israeli; hivi leo unataka kuvuka Yordani uingie kwa kuwamiliki mataifa yaliyo makubwa, na yenye nguvu kukupita wewe, miji mikubwa iliyojengewa kuta hata mbinguni,
[2]watu wakubwa, warefu, wana wa Waanaki, uwajuao, uliokuwa ukisikia wakitajwa hivi, Ni nani awezaye kusimama mbele ya wana wa Anaki?
[3]Basi jua siku hii ya leo kuwa BWANA, Mungu wako, ndiye atanguliaye kuvuka mbele yako kama moto uteketezao; atawaangamiza, tena atawaangusha mbele yako; ndivyo utakavyowafukuza na kuwapoteza upesi, kama alivyokuambia BWANA.
Soma pia Kumbukumbu 2:11, 21, Yoshua 11:21, 22, 14:12, 15….utaona habari zao.
Sasa wayahudi kulingana na desturi zao wanaamini watu hawa chimbuko lao lilikuwa ni kutoka katika ule uzao wa Wanefili (majitu) yaliyokuwepo kabla ya gharika kushushwa ulimwenguni (Mwanzo 6:4). Na ndio uzao ule ule uliokuja kuonekana hadi wakati wa mfalme Daudi (Yule Goliati)
Lakini kwanini Mungu aliruhusu watu hawa wawepo duniani?..kwanini asingeumba tu watu wote walingane?
Ni kuonyesha kuwa hata sasa rohoni wapo watu ambao ni majitu (wana wa anaki) karibu katika nyanja zote ya maisha..Na lengo lao ni kuweka vitisho tu na kuogopesha, lakini kama vile watu wa Mungu walivyoweza kuwashida kwa kumtegemea Bwana..vivyo hivyo na watakatifu wa sasa wanaweza kuwashinda kwa kumtegemea Bwana YESU katika mapito yao.
Unapoona mataifa makubwa yenye nguvu kubwa yanakuja kupigana na wewe uliye taifa dogo huna haja ya kuogopa maadamu Bwana yuko pamoja na wewe.
Ikiwa watu wenye nguvu wamekuzunguka kuupinga wokovu wako..wewe kama mkristo huna haja ya kutikisika maadamu Bwana yupo upande wako.
Kumbuka alichokifanya kwa Waanaki wa Yeriko ndicho atakachokufanyia na wewe ambaye uliyemwamini Yesu Kristo. Lakini kama upo nje ya wokovu fahamu huna tumaini, twewe utakuwa kama panzi kwa kila adui atakayetokea mbele yako, kukupinga. Na mwisho wa siku utakuwa ni mtu wa kuchukuliwa mateka tu daima..Lakini ya nini yote hayo yakukute katika ulimwengu huu wa dhambi, ni heri ukampa Kristo maisha yako leo akuweke salama. Hizi ni siku za mwisho Yesu yupo mlangoni kurudi. Tubu dhambi zako kwa mumaanisha kuziacha umgeukie Yesu akusemehe. Kwasababu hakuna tumaini lolote nje ya Kristo.
MUNGU HAONI SHIDA KUMUHAKIKISHIA MWOVU ULINZI.
INJILI YA MANENO LAINI ITAKUGHARIMU.
UZAO WA NYOKA.
WALA MSIUANGALIE MWILI, HATA KUWASHA TAMAA ZAKE.
WhatsApp