Isaya 30:21
[21]na masikio yako yatasikia neno nyuma yako, likisema, Njia ni hii, ifuateni; mgeukapo kwenda mkono wa kulia, na mgeukapo kwenda mkono wa kushoto.
Sisi kama watoto wa Mungu tunaweza kufanya Maamuzi Sahihi katika maisha yetu lakini pia tunaweza kufanya maamuzi yasiyo sahihi katika maisha…tunaweza pita mkono wa kulia lakini pia tukakosea na kupita mkono wa kushoto..
Lakini wengi wetu tunadhani yale maamuzi sahihi tuliyoyafanya ndio kwamba njia tumeiona na yale yasiyo sahihi tumepotea…lakini ukweli ni kuwa kwa Mungu bado tunahitaji maongozo yake sahihi sio tu katika yale mabaya tuliyokosea, lakini pia katika maamuzi mazuri yote tuliyoyachukua bado tunamwita Yeye sana atuonyeshe njia.
Kwasababu kwa Mungu maamuzi sahihi sio kuona mafanikio ya kweli, unaweza kufikia yaliyo sahihi lakini mwisho wake ukapotea.
Mstari huo unasema…
“mgeukapo kwenda mkono wa kulia, na mgeukapo kwenda mkono wa kushoto.
Mtaisikia sauti yangu ikisema njia ni hii..”
Ni ajabu kuona watu wanamlilia Mungu awaonyeshe njia kwenye nyakati za mambo mabaya tu zile za shida, nyakati za majuto, Nyakati za kupata hasara, nyakati za magonjwa, nyakati za kutafuta mwezi wa maisha, nyakati za kunyauka…nyakati za mkono wa kushoto.
Lakini hawana muda wa kumlilia Mungu awaonyeshe njia yake nyakati za mkono wa kuume..yaani za kufanikiwa, za kustawi, za kuinuka, za afya, za amani, za kupandishwa cheo, za kutajirika, nyakati ambazo chakula kipo, makazi yako, elimu ipo, Fedha ipo,
Wakiona mambo yote yapo sawa, wanadhani njia ndio wameshaiona..ndugu yangu humu duniani wapo watu wamefanikiwa sana, wapo watu imara na makini, wana bidii na ufanisi mzuri, ndoa zao zipo thabiti, watu wema, na kwasababu wamechagua njia hiyo basi juhudi zao zimewapa mafanikio sahihi ya ki- Mungu, wanatenda sawasawa wala hawana shida..si watu wajinga..pande zote wapo imara, hata wao wenyewe wanajiona hawakufanya maamuzi mabaya, lakini baadaye wanaishia katika majuto aidha ya kunaswa na mitego mibaya ya ibilisi au majuto baada ya kufa kukosa uzima wa milele..
Kwasababu maamuzi sahihi sio kuona njia sahihi…
Biblia inasema..
Mithali 16:25
[25]Iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu; Lakini mwisho wake ni njia za mauti.
Tunamwitaji Mungu ndugu..
Bwana Yesu alitoa mfano huu..
Luka 12:16-21
[16]Akawaambia mithali, akisema, Shamba la mtu mmoja tajiri lilikuwa limezaa sana; [17]akaanza kuwaza moyoni mwake, akisema, Nifanyeje? Maana sina pa kuyaweka akiba mavuno yangu. [18]Akasema, Nitafanya hivi; nitazivunja ghala zangu, nijenge nyingine kubwa zaidi, na humo nitaweka nafaka yangu yote na vitu vyangu. [19]Kisha, nitajiambia, Ee nafsi yangu, una vitu vyema vingi ulivyojiwekea akiba kwa miaka mingi; pumzika basi, ule, unywe, ufurahi. [20]Lakini Mungu akamwambia, Mpumbavu wewe, usiku huu wa leo wanataka roho yako! Na vitu ulivyojiwekea tayari vitakuwa vya nani? [21]Ndivyo alivyo mtu ajiwekeaye nafsi yake akiba, asijitajirishe kwa Mungu.
[16]Akawaambia mithali, akisema, Shamba la mtu mmoja tajiri lilikuwa limezaa sana;
[17]akaanza kuwaza moyoni mwake, akisema, Nifanyeje? Maana sina pa kuyaweka akiba mavuno yangu.
[18]Akasema, Nitafanya hivi; nitazivunja ghala zangu, nijenge nyingine kubwa zaidi, na humo nitaweka nafaka yangu yote na vitu vyangu.
[19]Kisha, nitajiambia, Ee nafsi yangu, una vitu vyema vingi ulivyojiwekea akiba kwa miaka mingi; pumzika basi, ule, unywe, ufurahi.
[20]Lakini Mungu akamwambia, Mpumbavu wewe, usiku huu wa leo wanataka roho yako! Na vitu ulivyojiwekea tayari vitakuwa vya nani?
[21]Ndivyo alivyo mtu ajiwekeaye nafsi yake akiba, asijitajirishe kwa Mungu.
Ndugu kila siku uamkapo asubuhi anza na siku ya na Bwana, ibilisi ni kama simba angurumaye kutafuta mtu kama wewe akumeze…acha kiburi cha uzima..katika nyendo zako zote mwombe Mungu akuonyeshe njia, na hiyo huja kwa kuwa mwombaji, na kujinyenyekeza sana mbele za Mungu..haijalishi wewe ni mchungaji, nabii, raisi, bilionea au nani…jinyenyekeze Kwa Bwana…kuwa mwombaji uisikie sauti ya Bwana..
Na hakika atakujibu..na kukupa mwongozo wake mwema..
Mungu atakujibu daima aidha Kwa Sauti ya Roho wake Mtakatifu ndani yako, au kupitia Neno lake, au kupitia amani moyoni mwako, katika kila hatua. Kwasababu yupo sikuzote kutusaidia tusipotee.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Mafundisho mengine:
Nzi wa Misri, na Nyuki wa Ashuru vilimaanisha nini? (Isaya 7:18-20).
Isaya 40:12 ‘maji kwa konzi ya mkono, na mbingu kwa shubiri’
Huyu Imanueli tunayemsoma katika Isaya ni nani?.
Print this post