SWALI: Kwanini Bwana Yesu alipowatuma wanafunzi wake kuhubiri aliwaambia wasihame- hame nyumba watakazo Karibishwa?
Luka 10:7
[7]Basi, kaeni katika nyumba iyo hiyo, mkila na kunywa vya kwao; maana, mtenda kazi amestahili kupewa ujira wake. Msihame-hame kutoka nyumba hii kwenda nyumba hii.
JIBU: Luka 10, Mathayo 10, Na Marko 6, Kristo inawafundisha mitume wakee nidhamu ya kimisheni. Pale ambapo watu wa Mungu watatoka na kwenda kuhubiri injili kwenye miji, mataifa au nyumba za Watu.
Ukisoma pale utaona Kristo anawapa maagizo kadha wa kadha mfano amri ya kutoa huduma zao bure, anawaagiza wawe wapole kama Hua, na wenye busara kama nyoka, vilevile nyumba watakazokaribishwa kisha chakula kikawekwa mbele yao wale bila kuuliza- uliza…
Lakini agizo lingine lilikuwa ni kutohama-hama nyumba moja kwenda nyingine. Kwamfano wameingia mji fulani halafu ikatokea familia moja ikawaalika kukaa kwao kwa kipindi chote cha huduma, hawapaswi kuhama- hama bali wakae pale mpaka watakapotoka na kwenda mji mwingine ikiwa yule mfadhili hana neno nao. Hata kama wakialikwa nyumba nyingine hawapaswi kuhama- hama..
Swali linakuja kwanini iwe hivyo?
Bwana Yesu alijua kuwa katika ziara mialiko kwa watumishi wa Mungu, huwa ni mingi. Na hivyo ili kuzuia dhamiri mbaya na wengine kuvunjika mioyo, akatoa agizo hilo Kwasababu mfano imetokea mtumishi amealikwa kisha kesho yake akahamia nyumba nyumba nyingine, Yule wa kwanza atajisikiaje? Pengine picha itakayoonekana hapo ni kuwa wanatafuta maisha mazuri, au matajiri wenye hadhi ya kuwatunza..
Lakini wakitulia sehemu moja huleta adabu na kuonyesha tabia ya kuridhika.
Lakini pia Kristo alitaka akili zao zijikite zaidi kwenye huduma.. Kwani kitendo cha kila siku kuhama hapa kwenda kule, hupoteza umakini kihuduma, ni sawasawa na mtu ambaye kila siku anahama nyumba moja ya kupanga kwenda nyingine…unaelewa ni usumbufu gani anaokutana nao.. kuanza tena kuyazoelewa mazingira mapya ni gharama.
Hasa sasa kama watumishi wa Mungu…tunafundishwa utulivu tuwapo ziarani…Mara nyingi ule mlango wa fadhili ambao unafunguliwa wa kwanza, huwa ni wa Mungu…tulia katika huo huo…nyumba ile ya wageni unayoingia ya kwanza…ikiwa amani ya Kristo imekaa ndani yako…tulia hiyo hiyo mpaka utakapomaliza ziara zako…usiwe mtu wa kutafuta makao mazuri, Kwasababu kumbuka upo ziarani… mahali pa muda tu.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >>
https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Print this post