SAUTI YA BWANA I JUU YA MAJI MENGI.

SAUTI YA BWANA I JUU YA MAJI MENGI.

Zaburi 29:3

[3]Sauti ya BWANA i juu ya maji; Mungu wa utukufu alipiga radi; BWANA yu juu ya maji mengi.

Ulishawahi kujiuliza kwanini ulimwengu ufunikwe kwanza na maji kote, ndipo Mungu atue juu yake lakini pia aseme Neno?(Mwanzo 1:1-2)

Vipi kama maji yasingekuwepo je Mungu asingesema lolote?….ndio ni kweli Neno la Bwana linasimama mahali popote lakini amejiwekea utaratibu wake wa kuzungumza..si kila eneo sauti yake yenye mamlaka ataiachia..

Palipo na maji sauti yake hutokea…

Ndio maana baadaye mwandishi wa zaburi Kwa uvivio wa Roho anasema…

Zaburi 29:3

[3]Sauti ya BWANA i juu ya maji; Mungu wa utukufu alipiga radi; BWANA yu juu ya maji mengi.

Sasa ni lazima tufahamu kwamba Mungu hakai kwenye maziwa, au bahari au mito…hapana bali Mungu hukaa katika moyo wa Mtu..

Lakini moyo wenye maji mengi… na hapo ndipo Sauti yake yenye nguvu kama radi inaposikika…

Hata mawingi ili yatoe radi huhitaji yajawe kwanza na maji, bila hivyo kamwe huwezi sikia sauti yoyote nyuma yake

Biblia inasema…

Yohana 4:13-14

[13]Yesu akajibu, akamwambia, Kila anywaye maji haya ataona kiu tena;

[14]walakini ye yote atakayekunywa maji yale nitakayompa mimi hataona kiu milele; bali yale maji nitakayompa yatakuwa ndani yake chemchemi ya maji, yakibubujikia uzima wa milele.

Na mahali pengine anasema maji hayo ni Roho Mtakatifu. (Yohana 7:39)

Mtu yeyote anayempa nafasi Roho Mtakatifu, ndani yake, kwa kutii, kwa kuwa mwombaji, mwenye ibada nyingi kumtafuta Mungu, kujitenga na dhambi …Huyo Anaongeza wingi wa maji ndani yake na matokeo yake ni kuwa sauti ya Mungu inasikika, na sio tu kisikika lakini pia inakuwa na nguvu kama ngurumo.

Tukiwa wakame, au tuna maji machache, kinyume chake, ni kuwa hatuwezi kumwona Mungu, wala kuisikia sauti yake. Penda kumtii Roho Mtakatifu. Tafuta kwa bidii kumjua Mungu, ongeza maji yako, Bwana aseme.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Print this post

About the author

Nuru ya Upendo administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments