Hedaya ni nini?
Hedaya ni neno linalomaanisha zawadi. Ni zawadi inayotolewa kuonyesha shukrani, au kuridhishwa kwa wema Fulani uliofanyiwa au kwa uzuri wake.
Katika biblia Neno hilo tunaliona katika vifungu vifuatavyo;
Zaburi 68:28 “Ee Mungu, uziamuru nguvu zako; Ee Mungu, uwe hodari uliyetufanyia makuu. 29 Kwa ajili ya hekalu lako Yerusalemu Wafalme watakuletea hedaya”.
Zaburi 68:28 “Ee Mungu, uziamuru nguvu zako; Ee Mungu, uwe hodari uliyetufanyia makuu.
29 Kwa ajili ya hekalu lako Yerusalemu Wafalme watakuletea hedaya”.
Zaburi 76:11 “Wekeni nadhiri, mkaziondoe Kwa Bwana, Mungu wenu. Wote wanaomzunguka wamletee hedaya, Yeye astahiliye kuogopwa”.
Isaya 18:7 “Wakati huo Bwana wa majeshi ataletewa hedaya na watu warefu, laini; Watu watishao tangu mwanzo wao hata sasa; Taifa la wenye nguvu, wakanyagao watu, Ambao mito inakata nchi yao; mpaka mahali pa jina la Bwana wa majeshi,mlima Sayuni”.
Hata sisi leo hii kila mmojawetu analojukumu la kumpelekea Mungu wetu hedaya,
Na tunampelekea kwa njia mbili:
Njia ya kwanza: ni kwa sifa za midomo yetu: Yaani kumsifu na kumwabudu, na kumpa shukrani kwa vinywa vyetu kwa wema wake wote anaotutuendea, na kwa ukuu wake wote alionao ulimwenguni kote.
Njia ya pili: Ni kwa Kumtolea sadaka: Unapotoa sadaka( yaani fedha, mali n.k.), ni unaonyesha shukrani kwa Mungu, kwa kile alichokufanyia, unaonyesha shukrani kwa neema aliyokupa ya uhai, na kila kitu.
Hivyo huo ni wajibu wa kila mmojawetu. Na hiyo ndio tafsiri ya Hedaya kibiblia.
Shalom.
jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Tazama maana nyingine za maneno chini;
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312 / 0693036618.
Mada Nyinginezo:
Mkatale ni nini katika biblia? (Matendo 16:24)
Daawa ni nini kama tunavyosoma katika biblia?
UHARIBIFU HAUNA KIFUNIKO.
TAFUTA KUIFANYA KAZI YA MUNGU KWA HUDUMA MUNGU ALIYOIWEKA NDANI YAKO.
NA MTU MMOJA AKAVUTA UPINDE KWA KUBAHATISHA, AKAMPIGA MFALME
Amin, nawaambia, Kizazi hiki hakitapita..
CHUKIZO LA UHARIBIFU
Rudi Nyumbani:
Print this post
Yusufu alipochukuliwa Misri alikuja kuwa mtu mkuu, kama tunavyosoma katika biblia, lakini kilichomtofautisha yeye na ndugu zake mbele za Mungu, sio ule ukuu aliokuwa nao, wala sio kile cheo alichokipata, hapana, bali ni mahali ambapo moyo wake ulikuwepo pindi alipokuwa Misri, utaona japokuwa aliishi kule kwa miaka mingi sana, tangu akiwa kijana mdogo kabisa, lakini moyo wake wote ulikuwa katika nchi ya ahadi ya baba zake, na ndio maana utaona alipokaribia kufa aliwaambia wana wa Israeli, kuwa siku watakapopandishwa kutoka katika nchi ya Misri na Mungu, basi mifupa yake wasiiache kule, bali waibebe mpaka nchi ya kaanani.
Kutoka 13:19 “Musa akaichukua ile mifupa ya Yusufu pamoja naye; maana, alikuwa amewaapisha sana wana wa Israeli, akisema, Mungu hana budi atawajilia ninyi; nanyi mtaichukua mfupa yangu kutoka hapa pamoja nanyi’.
Tofauti na wale watoto wengine 11 wa Yakobo, japokuwa walikaribishwa tu Misri, hawakuwepo kule maisha yao yote, lakini walipofika, waliishi kama ndio nyumbani kwao, mawazo ya kurudi Kaanani hayakuwepo, na ndio maana hata waliposikia habari za Yusufu kuondolewa mifupa yake, hilo halikuwawazisha nao waseme hivyo, kwasababu uzuri wa Misri ulishawaridhisha mioyo yao.
Utaona hiyo tabia Yusufu aliyokuwa nayo aliirithi kutoka kwa baba yake Yakobo, kwani alipokuwa Misri kwa kipindi kifupi, aliwaambia, atakapokufa wahakiishe hawamziki katika nchi ile, bali katika nchi ya Baba zake walizozikiwa (yaani Kaanani).
Mwanzo 49:29 “Akawaamuru, akasema, Mimi ninakwenda kukusanywa pamoja na watu wangu; mnizike pamoja na baba zangu, katika pango iliyomo shambani mwa Efroni, Mhiti; 30 katika ile pango iliyomo shambani mwa Makpela, iliyo mbele ya Mamre katika nchi ya Kanaani, aliyoinunua Ibrahimu pamoja na shamba kwa Efroni Mhiti, pawe milki yake ya kuzikia. 31 Humo walimzika Ibrahimu, na Sara mkewe; humo wakamzika Isaka, na Rebeka mkewe; nami humo nikamzika Lea”;
Mwanzo 49:29 “Akawaamuru, akasema, Mimi ninakwenda kukusanywa pamoja na watu wangu; mnizike pamoja na baba zangu, katika pango iliyomo shambani mwa Efroni, Mhiti;
30 katika ile pango iliyomo shambani mwa Makpela, iliyo mbele ya Mamre katika nchi ya Kanaani, aliyoinunua Ibrahimu pamoja na shamba kwa Efroni Mhiti, pawe milki yake ya kuzikia.
31 Humo walimzika Ibrahimu, na Sara mkewe; humo wakamzika Isaka, na Rebeka mkewe; nami humo nikamzika Lea”;
Unaona, hicho pia ndicho kilichomtofautisha Yakobo kwa Esau.. sikuzote, wana wa urithi, hawatazami ya hapa, bali wanatazama ya mbele, wanaishi kama wapitaji, na mazingira huwa hayawakwamishi hata kidogo kutokuwaza makao yao ya milele, utajiri hauwakwamishi, vyeo vyao vya muda, haviwafanyi wasahau makao yao halisi, hata hali ngumu za kimaisha haziwakwamishi wasiwaze kurejea nchini mwao siku moja.
Na ndicho utakiona pia kwa Danieli, japokuwa alichukuliwa utumwani Babeli, hadi akawa mtu mkuu katika nchi ile ya kipagani, Lakini kila siku (mara tatu kwa siku) alikuwa haachi kuomba dua juu ya Yerusalemu, madirisha yake yalikuwa yamefunguliwa kuelekea Yerusalemu ilipo, mbali sana, maelfu kwa maelfu ya kilometa, lakini aliiwaza kila wakati na kuiombea kana kwamba alikuwa Israeli. Tofauti na wayahudi wote waliochukuliwa utumwani Babeli kwa wakati ule.(Danieli 6:10)
Utamwona Nehemia naye, japokuwa alikuwa ni mnyweshaji wa Mfalme wa Umedi na Uajemi, lakini akili yake yote, na mawazo yake yote, yalikuwa Yerusalemu, akawa anaulizia habari za mji na hekalu linaendeleaje kila wakati, hadi siku moja aliposikia hali ya mji sio nzuri, kuta zake zimeharibiwa, alilia na kufunga na kuomboleza kwa muda mrefu (Nehemia 1)
Watu kama hao wanaonyesha ni kama kwa bahati mbaya tu walikuwepo katika nchi ya ugenini, wengine walitumainia kabla hawajafa wataiona Yerusalemu, lakini mpaka wanakufa hawakuiona, lakini mioyo yao ilikuwa huko.
Waebrania 11:13 “Hawa wote wakafa katika imani, wasijazipokea zile ahadi, bali wakaziona tokea mbali na kuzishangilia, na kukiri kwamba walikuwa wageni, na wasafiri juu ya nchi. 14 Maana hao wasemao maneno kama hayo waonyesha wazi kwamba wanatafuta nchi yao wenyewe. 15 Na kama wangaliikumbuka nchi ile waliyotoka, wangalipata nafasi ya kurejea.”.
Waebrania 11:13 “Hawa wote wakafa katika imani, wasijazipokea zile ahadi, bali wakaziona tokea mbali na kuzishangilia, na kukiri kwamba walikuwa wageni, na wasafiri juu ya nchi.
14 Maana hao wasemao maneno kama hayo waonyesha wazi kwamba wanatafuta nchi yao wenyewe.
15 Na kama wangaliikumbuka nchi ile waliyotoka, wangalipata nafasi ya kurejea.”.
Swali Na sisi ambao tunasema ni wapitaji hapa duniani (Kizazi cha watakao nyakuliwa) Je siku zote tunaishi maisha ya kuutafakari urithi wetu wa kimbinguni tuliowekewa, Je tunaitafakari hiyo Yerusalemu mpya ya kimbinguni? Au tunaishi tu hapa duniani kama tumefika?
Shughuli za ulimwengu zinatuzidi mpaka hatuyawazi tena mambo ya mbinguni? hatuwezi kusema tupo busy, zaidi ya Yusufu ambaye dunia nzima alikuwa anaihudumia kwa chakula, na isitoshe alikuwa ni waziri mkuu wa taifa kubwa ulimwenguni, lakini aliiwaza Yerusalemu kiasi cha kukataa kuzikwa kwenye nchi isiyo yake..Sisi hatuwezi kuwa bize zaidi ya Danieli na Nehemia ambao wao walikuwa ni wakuu katika nchi ya Babeli na Umedi, lakini walilia usiku na mchana juu ya Yerusalemu mji wao..wengine mpaka wakaenda kuukarabati.
Lakini sisi tunao mji ulio mkuu kuliko yao. Tunapoishi hapa duniani tukumbuke kuwa, biblia inasema, kule hakitaingia kilicho kinyonge, maana yake ni kuwa hawataingia wasiokuwa na mpango nao, hawataingia ambao hawaulizii habari zake sasa, watakaoingia kule ni wale tu waliostahili kuingia humo, Si kila mtu atauingia huo mji wa kimbinguni, haijalishi utasema leo umeokoka,
Hivyo tuanze sasa kuishi maisha ya kama watu waonaomngojea Bwana wao (Luka 12:36), kwasababu muda tuliobakiwa nao ni mchache sana, Siku ya ukombozi wetu imekaribia, Parapanda wakati wowote italia, kisha tutakwenda mbinguni kwenye karamu ya mwana-kondoo, na baada ya hapo utafuata utawala wa miaka 1000, wakati huo wote tutakuwa tukijiandaa kwa ajili ya mbingu mpya na nchi mpya na hiyoYerusalemu mpya ishukayo kutoka mbinguni.
2Petro 3:13 “Lakini, kama ilivyo ahadi yake, mnatazamia mbingu mpya na nchi mpya, ambayo haki yakaa ndani yake”.
Ufunuo 21:1 Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya; kwa maana mbingu za kwanza na nchi ya kwanza zimekwisha kupita, wala hapana bahari tena. 2 Nami nikauona mji ule mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, umewekwa tayari, kama bibi-arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe. 3 Nikasikia sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha enzi ikisema, Tazama, maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu, naye atafanya maskani yake pamoja nao, nao watakuwa watu wake. Naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao.
Ufunuo 21:1 Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya; kwa maana mbingu za kwanza na nchi ya kwanza zimekwisha kupita, wala hapana bahari tena.
2 Nami nikauona mji ule mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, umewekwa tayari, kama bibi-arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe.
3 Nikasikia sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha enzi ikisema, Tazama, maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu, naye atafanya maskani yake pamoja nao, nao watakuwa watu wake. Naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao.
Tukose vyote, tupitwe na vyote, lakini tusikose mambo hayo ambayo biblia inasema jicho halijawahi kuona wala sikio kusikia.
Bwana akubariki.
MAMBO YA KUJIFUNZA KATIKA KITABU CHA RUTHU:
WAKATI WA KRISTO KUSIMAMA,UMEKARIBIA SANA.
MAMBO 5 AMBAYO KILA MKRISTO ANAPASWA KUFAHAMU.
VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 2
JE! KUNA UCHAWI KATIKA KUTENDA WEMA?
WhatsApp
JIBU: Roho Mtakatifu na Roho Takatifu ni kitu kimoja, inategemea neno hilo limetumika wapi
Roho wa Mungu anapozungumza ndani yetu, au kutuongoza, au kutufundisha..anakuwa kama ni mtu yupo ndani yetu akifanya hizo kazi..anakuwa kama ni mtu mwingine mpole ndani yetu anazungumza nasi, anatufundisha, anatushauri, anatufariji, anatutia moyo, anatuongoza n.k..Hivyo hiyo tabia ya kuwa kama mtu wa pili ndani yetu, ndiyo inayofanya biblia sehemu zote iitaje Roho ya Mungu, kwa cheo cha uutu. (yaani Roho M-takatifu).
Hali kadhalika, linapokuja suala la tabia ya Roho ya Mungu, ni sahihi kabisa kusema Roho ya Mungu ni Roho Takatifu, ni Roho Nyenyekevu, ni Roho Tulivu, Ni roho Njema (Danieli 5:12) n.k Hapo hatujaivisha uutu lakini tumeielezea sifa yake.
Yapo madhehebu yanayofanya mambo haya yawe magumu kwa maneno hayo mawili, na hata mengine yamebadilisha biblia zao, kila mahali palipoandikwa kwenye biblia neno Roho Mtakatifu, yamebadilisha na kuweka Roho Takatifu..Hivyo kwao ni kosa kutumia neno Roho Mtakatifu mahali popote. Vile vile yapo mengine ni kosa kutumia neno Roho Takatifu. Pasipo kujua kwamba maneno yote mawili ni sahihi, inategemea ni wapi yametumika.
Kumbuka pia ni wajibu wa kila mmoja aliyeokoka kuwa na Roho Mtakatifu.
Mungu atubariki.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312
JE WAJUA?
MAKEDONIA.
Roho, Nafsi, na Mwili vina utofauti gani?
Yuko azuiaye sasa hata atakapoondolewa! ni nani huyo?
JE VIBWENGO NI KWELI VIPO?
SWALI: Mungu anaposema yeye ndiye achunguzaye “viuno ya mioyo” anamaanisha nini, Je! hivyo viuno ni vipi? Kama tunavyovisoma katika vifungu vifuatavyo;
Yeremia 11:20 “Lakini, Ee Bwana wa majeshi, uhukumuye haki, ujaribuye viuno na moyo, nijalie kuona kisasi chako juu yao; kwa maana nimekufunulia wewe neno langu”. Yeremia 17: 10 “Mimi, Bwana, nauchunguza moyo, navijaribu viuno, hata kumpa kila mtu kiasi cha njia zake, kiasi cha matunda ya matendo yake”. Yeremia 20: 12 “Lakini, Ee Bwana wa majeshi, wewe wawajaribu wenye haki, waona viuno na mioyo, nijalie kuona kisasi chako juu yao; kwa maana nimekufunulia wewe neno langu”.
Yeremia 11:20 “Lakini, Ee Bwana wa majeshi, uhukumuye haki, ujaribuye viuno na moyo, nijalie kuona kisasi chako juu yao; kwa maana nimekufunulia wewe neno langu”.
Yeremia 17: 10 “Mimi, Bwana, nauchunguza moyo, navijaribu viuno, hata kumpa kila mtu kiasi cha njia zake, kiasi cha matunda ya matendo yake”.
Yeremia 20: 12 “Lakini, Ee Bwana wa majeshi, wewe wawajaribu wenye haki, waona viuno na mioyo, nijalie kuona kisasi chako juu yao; kwa maana nimekufunulia wewe neno langu”.
Zaburi 7: 9 “Ubaya wao wasio haki na ukome, Lakini umthibitishe mwenye haki. Kwa maana mjaribu mioyo na viuno Ndiye Mungu aliye mwenye haki”.
Ufunuo 2:22 “Tazama, nitamtupa juu ya kitanda, na hao wazinio pamoja naye, wapate dhiki kubwa wasipotubia matendo yake; 23 nami nitawaua watoto wake kwa mauti. Na makanisa yote watajua ya kuwa mimi ndiye achunguzaye viuno na mioyo. Nami nitampa kila mmoja wenu kwa kadiri ya matendo yake”.
Ufunuo 2:22 “Tazama, nitamtupa juu ya kitanda, na hao wazinio pamoja naye, wapate dhiki kubwa wasipotubia matendo yake;
23 nami nitawaua watoto wake kwa mauti. Na makanisa yote watajua ya kuwa mimi ndiye achunguzaye viuno na mioyo.
Nami nitampa kila mmoja wenu kwa kadiri ya matendo yake”.
Ukisoma pia Mithali 23:16 , na Ayubu 31:19 inazungumzia maneno hayo hayo;
JIBU: Mara nyingine biblia inapolitaja Neno viuno haimaanishi tu hivi viuno vya miili yetu tunavyovivalia mikanda, hapana, bali viuno sehemu nyingine linatumika kumaanisha NIA au WAZO, la mtu. Mungu kabla hajambariki mtu au kumuhukumu au kumsamehe huwa anatazama vitu hivyo viwili, cha kwanza ni Moyo na cha pili ni Nia.
Kwamfano, Mungu anaweza kumsamehe mtu dhambi zake bila hata ya kuzungumza maneno yoyote kwenye kinywa chake kuonyesha anaomba msamaha, Yaani ule moyo tu wa kujutia dhambi zake, moyo wa kuugua, moyo wa kusema kosa hili sitakaa nilirudie tena, siku baada ya siku anajutia makosa yake, na hataki kuyatazama wala kuyarudia tena, hiyo tayari ni toba inayozungumza sana mbele za Mungu kuliko sala za toba elfu mtu anazoongozwa kila siku na huku hana majuto na dhambi zake.
Jambo kama hilo utaliona kwa Yule mwanamke kahaba, aliyekwenda kumlilia Yesu, utaona hakuzunguza Neno lolote lakini Bwana Yesu alimwambia umesamehewa dhambi zako. (Luka 7:37-48)
Vilevile Mungu huwa anachunguza Nia, kwa mfano wengi wetu tunamuhukumu Yuda kama ndiye aliyempeleka Yesu msalabani, lakini ukisoma pale utaona Yuda hakuwa na Nia ya Bwana Yesu kufikishwa katika mateso na kusulibiwa na ndio maana akawaomba watakapomchukua wasimtendee dhara lolote (Marko 14:44), kwani yeye lengo lake lilikuwa ni kupata pesa tu..Lakini alipoona wale watu wamevuka mipaka, mpaka kwenda kumsulibisha alijuta kwa kulia sana, hadi ikamfanya aende kujinyonga, kwa madhara aliyosababisha, Hivyo Mungu anayechunguza Nia hatamuhukumu kwasababu alimpeleka Yesu msalabani bali atamuhukumu kwa kosa lingine la kutokuwa na moyo mkamilifu kwake kama ilivyokuwa kwa mitume wenzake.
Huo ni mfano tu,
Hivyo nasi tunapaswa tuwe makini sana, usiende kuzini ukamwambia Mungu nilipitiwa, yeye hashawishiwi kwa maneno , anachunguza moyo na Nia ya mwanadamu zaidi ya fikra zetu. Hivyo tusijidanganye tuna la kujitetea mbele zake, hata Siku ile ya Hukumu (Anachunguza viuno vyetu). Halikadhalika hata ukitenda tendo la haki, huna haja ya kumwambia Mungu, kumbuka hiki kumbuka kile, yeye anajua yote (Mhubiri 5:8).
Bwana atusaidie,
Malaika wa maji ni yupi na Je kuna aina ngapi za malaika?
JINSI MUNGU ANAVYOIPIGA NA KUIPONYA AFRIKA.
BWANA WA MAJESHI.
JINSI YA KUSOMA BIBLIA.
Nini maana ya Usiwe mwovu kupita kiasi? (Mhubiri 7:17)
SWALI: Huu mstari una maana gani? Amos 9:2 “Wajapochimba waingie katika kuzimu, mkono wangu utawatoa huko; nao wajapopanda hata mbinguni, nitawatelemsha toka huko”
JIBU: Jina la Bwana wetu Yesu Kristo libarikiwe, Ni muhimu kufahamu sio kila mahali panapozungumzia Neno mbinguni katika biblia panamaanisha “mbinguni kule Malaika watakatifu walipo” Hususani katika agano la kale. Neno mbinguni pia linaweza kutumika na wapagani kumaanisha mbingu yao, kadhalika mbinguni kunaweza kumaanisha “sehemu iliyo inuka sana”.
Mtu aliyejiinua sana moyo wake katika roho anaonekana amepanda mpaka mbinguni.
Hali kadhalika sio kila mahali panalipoandikwa neno “kuzimu” katika biblia hususani agano la kale, kuna maanisha kule kuzimu, roho za viumbe walioasi zilipo!..hapana! sehemu nyingine panapotajwa neno kuzimu panamaanisha mahali pa chini sana. Kwamfano mtu aliye katika vifungo vingi vilivyomfanya awe chini sana, katika roho ni kama yupo kuzimu. (Yona na Mariamu na Hana).
Kwamfano tunaweza kusoma mistari ifuatayo ili tupate kuelewa vizuri.
Yona 2:1 “Ndipo Yona akamwomba Bwana, Mungu wake, katika tumbo la yule samaki, 2 Akasema, Nalimlilia Bwana kwa sababu ya shida yangu, Naye akaniitikia; KATİKA TUMBO LA KUZİMU NALİOMBA, Nawe ukasikia sauti yangu. 3 Maana ulinitupa vilindini, Ndani ya moyo wa bahari; Gharika ya maji ikanizunguka pande zote; Mawimbi yako yote na gharika zako zote zimepita juu yangu”
Yona 2:1 “Ndipo Yona akamwomba Bwana, Mungu wake, katika tumbo la yule samaki,
2 Akasema, Nalimlilia Bwana kwa sababu ya shida yangu, Naye akaniitikia; KATİKA TUMBO LA KUZİMU NALİOMBA, Nawe ukasikia sauti yangu.
3 Maana ulinitupa vilindini, Ndani ya moyo wa bahari; Gharika ya maji ikanizunguka pande zote; Mawimbi yako yote na gharika zako zote zimepita juu yangu”
Sasa hapo Yona sio kwamba alishuka kuzimu, mahali pa wafu, hapana, bali katika mazingira ya lile tumbo la samaki alilokuwemo ndio akakufananisha na KUZIMU. Mahali pabaja mfano wa kuzimu. Na mtu anapokuwa katika mazingira hayo yanayofananishwa na kuzimu, anaweza kupandishwa juu na kutoka huko, kama Yona na Hana mama yake Samweli.
1Samweli 2:6 “Bwana huua, naye hufanya kuwa hai; Hushusha hata kuzimu, tena huleta juu. 7 Bwana hufukarisha mtu, naye hutajirisha; Hushusha chini, tena huinua juu”
1Samweli 2:6 “Bwana huua, naye hufanya kuwa hai; Hushusha hata kuzimu, tena huleta juu.
7 Bwana hufukarisha mtu, naye hutajirisha; Hushusha chini, tena huinua juu”
Na andiko lingine ndio hilo la kwenye Amosi 9:2 “Wajapochimba waingie katika kuzimu, mkono wangu utawatoa huko; nao wajapopanda hata mbinguni, nitawatelemsha toka huko”
Lakini mtu anayeshuka katika ile kuzimu halisi ya sehemu ya wafu walioasi, biblia inasema hawezi kurudi tena wala hawezi kutoka huko.
Ayubu 7:9 “Kama vile wingu likomavyo na kutoweka, Ni vivyo huyo ashukaye kuzimuni hatazuka tena kabisa. Hatarudi tena nyumbani kwake, Wala mahali pake hapatamjua tena”.
Kwahiyo unaweza ukawa unapitia hali fulani katika hii dunia, ambapo mahali ulipo ni kama kuzimu, kila kona unaona giza limekuzunguka na mashaka, huoni unafuu popote, nataka nikuambie lipo tumaini kwa Kristo, maadamu bado unaishi, Bwana anaweza kukunyanyua tena na kukutoa huko Kuzimu, ulipo na kukupandisha juu, Hivyo Mwamini, omba kwa bidii na mshukuru, siku isiyokuwa na jina utaona miujiza.
Vivyo hivyo unaweza kuwa katika mahali fulani, au ukawa katika nafasi fulani na moyo wako ukainuka sana, pengine ukajiona ni mungu-mtu, kila mtu anakuogopa, kila mtu anakuhofu au wewe ukajiona ni bora sana kuliko wengine wote wanaokuzunguka, nataka nikuambia mbele za Mungu, umejiinua na kufika mbinguni, na biblia inasema wote wajikwezao watashushwa (Luka 14:11).
Kwa maelezo marefu kuhusu mbungini fungua hapa >> mbinguni ni wapi?
Hivyo mstari huo katika Amosi hauzungumzii Mbingu halisi, Malaika watakatifu waliopo, bali wala hauzungumzii Kuzimu halisi, wafu waliokufa katika dhambi walipo… Bali inazungumzia hali fulani ya maisha ambayo mtu yupo chini sana mfano wa kuzimu, na hali fulani ya maisha ambayo mtu kajiinua sana juu mfano wa mbingu.
FUNGUO ZA UZIMA, MAUTI NA KUZIMU.
ALIKUWAKO NAYE HAYUKO, NAYE YU TAYARI KUPANDA KUTOKA KUZIMU.
CHAPA YA MNYAMA
UJIO WA BWANA YESU.
MAMBO MANNE,YANAYODHOOFISHA UOMBAJI WAKO.
Kuota unajifungua kuna maanisha nini?
Ndoto hii inaweza ikawa na maana mbili, maana ya kwanza ambayo ninaweza kusema inawapata wengi, ni ile inayotokana na shughuli nyingi au mambo tuliyowahi kuyapitia, au kuyawaza, au kuyatenda mara kwa mara huko nyuma.
Biblia inasema.
Mhubiri 5:3 “Kwa maana ndoto huja kwa sababu ya shughuli nyingi;…….”.
Hivyo sishangai kama ndoto hii atakuwa anaotwa na mwanamke, kwasababu yeye kwa sehemu kubwa katika maisha yake, amekuwa akiwaza pengine siku moja atajifungua, au hivi karibuni anakwenda kujifungua au mwengine tayari huko nyuma alishawahi kujifungua,..
Hivyo matukio kama hayo kujirudia rudia katika ndoto zake litakuwa ni jambo la kawaida sana. Kwahiyo kama wewe ni mmojawapo wa wanaoyapitia hayo, basi ipuuzie tu ndoto ya namna hiyo, kwasababu haina maana yoyote rohoni.
Lakini maana ya pili, ambayo ni ya rohoni, ni kwamba ikiwa ndoto hii umekujia kwa namna ambayo sio ya kawaida, yaani kwa uzito mkubwa sana, na unahisi kuna uzito Fulani ndani ya moyo wako, basi ujue ndoto hiyo imebeba ujumbe. Na tafsiri yake ni kuwa lipo jambo zuri au baya linakwenda kukujia, kulingana na ulichokuwa unakifanya katika maisha yako.
Tunajua sikuzote mpaka mtu anafikia hatua ya kuzaa ni wazi kuwa tayari huko nyuma alishabeba mimba kwa muda mrefu, hivyo angalia katika maisha yako ni nini umekuwa ukikibeba, na ukikisubiria, basi ujue hivi karibuni utakwenda kukiona kikijidhihirisha (kukuletea matokeo fulani). Kama umekuwa ukifanya jambo jema basi tazamia kuona matunda ya wema wako hivi karibuni.
Luka 1:30 “Malaika akamwambia, Usiogope, Mariamu, kwa maana umepata neema kwa Mungu.31 Tazama, utachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume; na jina lake utamwita Yesu.
Luka 1:30 “Malaika akamwambia, Usiogope, Mariamu, kwa maana umepata neema kwa Mungu.
31 Tazama, utachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume; na jina lake utamwita Yesu.
Lakini kama wewe ni mwenye dhambi (yaani haupo ndani ya Kristo) basi jiandae hivi karibuni kukutana na matunda ya mambo maovu uliyokuwa unayafanya katika maisha yako,
biblia inasema..
Ayubu 15:35 “Wao hutunga mimba ya madhara, na kuzaa uovu, Nalo tumbo lao hutengeza udanganyifu”.
Zaburi 8:14 “Tazama, huyu ana utungu wa uovu, Amechukua mimba ya madhara, amezaa uongo”
Yakobo 114 “Lakini kila mmoja hujaribiwa na tamaa yake mwenyewe huku akivutwa na kudanganywa.15 Halafu ile tamaa ikiisha kuchukua mimba huzaa dhambi, na ile dhambi ikiisha kukomaa huzaa mauti”.
Yakobo 114 “Lakini kila mmoja hujaribiwa na tamaa yake mwenyewe huku akivutwa na kudanganywa.
15 Halafu ile tamaa ikiisha kuchukua mimba huzaa dhambi, na ile dhambi ikiisha kukomaa huzaa mauti”.
Unaona wanachozaa sikuzote watu waovu ? Na ndio maana sehemu nyingine inasema..
Mathayo 3:10 “Na shoka limekwisha kuwekwa penye mashina ya miti; basi kila mti usiozaa matunda mazuri hukatwa na kutupwa motoni”.
Hivyo jiangalie wewe katika maisha yako yote, na mambo yako yote unayoyatenda Je, ni jambo gani unakwenda kulizaa hivi karibuni? Je! ni uzima, au mauti?
Lakini habari njema ni kuwa Yesu leo anaweza kukuokoa, na kukufanya umzalie matunda mazuri, na akabatilisha mabaya yote ambayo yamepangwa mbele yako, ikiwa tu utakubali kumruhusu ayageuze maisha yako, Yeye yupo tayari kukusamehe ikiwa utakuwa tayari kutubu kwa moyo wako wote, Hivyo ikiwa upo tayari kufanya hivyo leo, basi uamuzi huo ni wa busara sana. Unachotakiwa kufanya ni kufungua hapa kwa ajili ya kuongozwa sala ya Toba.>>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Na Mungu peke yake atakigeuza unachokizaa kiwe chema.
Bwana akubariki sana.
Au jiunge kwa kubofya link hii>>
Kwa mgawanyo bora wa masomo download App hapa>> App wingu la mashahidi
HERODE NA PILATO, MAADUI WAWILI WAPATANA.
Mwaloni ni nini? Na je unafunua nini rohoni?
Arabuni maana yake ni nini?
MOTO HUFA KWA KUKOSA KUNI.HATA UASHERATI NAO
UNYAKUO.
Mtu akikufanyia fadhila ya hali ya juu, ni wazi kuwa nafsi yako haitatulia mpaka na wewe utakapohakikisha umemrudishia naye pia fadhila..hiyo ni hali ya kawaida ya kibinadamu kabisa, hata kama hakitafikia kile alichokufanyia walau utaonyesha shukrani kwa kumwombea dua kwa Mungu.
Hata sisi tunapookoka, tunapogundua kuwa kumbe kuna mtu alitupenda upeo, kumbe kuna mtu alikufa kwa ajili ya dhambi zetu na kama asingekufa leo hii sisi tungekuwa ni wa kuzimu.
Ni dhahiri kuwa kama tumeithamini fadhila hiyo ya kipekee basi na sisi ni lazima tutaonyesha kurudisha kitu Fulani kwake, ni kweli hatuwezi kumrudishia fadhila za matendo yetu mema kama yeye aliyotufanyia, kwasababu mpaka hapa tulipo tulishamkosea Mungu mara nyingi sana. Lakini fadhili tunayoweza kumrudishia ni kuupeleka Upendo wake, uwafikie na wengine, ambao bado haujawafikia, ili nao pia waokolewe kama sisi. Na hiyo ndio inayotufanya tuwahubirie injili na wengine, na kuwaombea.
Mtume Paulo alisema maneno haya;
2Wakorintho 5:14 “MAANA, UPENDO WA KRISTO WATUBIDISHA; maana tumehukumu hivi, ya kwamba mmoja alikufa kwa ajili ya wote, basi walikufa wote”;
Unaona? Vivyo hivyo na sisi, huu upendo wa ajabu wa Yesu kutoa maisha yake kwa ajili yetu sisi bure, ugeuke na kuwa deni kwetu,..Huu ndio utupe sababu ya kuwapelekea watu wengine habari njema, tusiuchukulie bure tu..
2Wakorintho 6:1 “Nasi tukitenda kazi pamoja naye twawasihi msiipokee neema ya Mungu bure. 2 (Kwa maana asema, Wakati uliokubalika nalikusikia, Siku ya wokovu nalikusaidia;tazama,wakati uliokubalika ndiyo sasa; tazama siku ya wokovu ni sasa)”.
Kama wewe umeokolewa mshukuru Mungu sana kwa neema hiyo , lakini kumbuka wapo watu wengi wanaohitaji kuokolewa kama wewe, swali tujiulize tangu tumeokoka Je viungo vyetu vimeleta faida yoyote kwa Kristo? Je kilishamleta mmoja katika neema ya wokovu au la? Kama karama yako haijawahi kufanya hivyo, badala yake imetumika kuwaburudisha tu watu, basi ujue karama hiyo ni feki, haijatoka kwa Mungu.
Hivyo kwa pamoja sote, tuufanye upendo wa Kristo kama deni kwetu. Huo utubidiishe kumtumikia Mungu, kwa karama zetu na kwa tulivyonavyo, ili neema ya Mungu iwafikie na wengine kama sisi nao pia waufurahie wokovu wa Bwana wetu Yesu Kristo.
Kilichoawafanya mitume waupindue ulimwengu kwa wakati wao, ni kwasababu kwa pamoja waliutambua Upendo wa Kristo, hivyo ukageuka kuwa deni kwao, wakamtumikia Mungu kwa vyote walivyokuwanavyo, na ndio maana na hapo wanasema Upendo wa Kristo watubidiisha, vivyo hivyo na sisi, tuugeuze Upendo huu kuwa deni.
Na Bwana atatuonekania katika maisha yetu.
UWEZA WA MUNGU UNAONEKANA WAPI?
Mungu aliposema Yesu ni mwanawe pekee, alimaanisha hakuwa na wengine?
LAKINI USIKU WA MANANE, PAKAWA NA KELELE.
MISTARI YA BIBLIA KUHUSU UPENDO.
Ndoto ya Kuota unapigana na mtu kuna inamaanisha nini?
Ndoto hii inaweza ikawa na maana mbili, maana ya kwanza, ni kuwa upo katika mashindano, Na maana ya pili ni kuwa upo katika vita.
Tukianzana na maana ya kwanza ambayo ni mashindano.
Kwa namna ya kawaida, ikiwa kipo kitu Fulani ambacho kinathamani fulani, na wote mnakitamani au kukigombania ili mkipate, au mmoja anakizuia ili kisipatikane, ni rahisi kutokea kutokuelewa na mwisho wa siku mapigano, kwamfano wengine wanaishia kupigana kisa, fedha, wengine madini, wengine fursa, wengine wapenzi, na wengine thawabu n.k,
Na ndio maana utamwona mtu kama Yakobo katika biblia, alipiigania thawabu yake sana usiku kucha kwa kushindana mweleka na Yule malaika aliyemtembelea usiku..
Mwanzo 32:24 “Yakobo akakaa peke yake; na mtu mmoja akashindana naye mweleka hata alfajiri.25 Naye alipoona ya kuwa hamshindi, alimgusa panapo uvungu wa paja lake; ukateguka uvungu wa paja la Yakobo alipokuwa akishindana naye.26 Akasema, Niache, niende, maana kunapambazuka. Akasema, Sikuachi, usiponibariki.27 Akamwuliza, Jina lako n’nani? Akasema, Yakobo.28 Akamwambia, Jina lako hutaitwa tena Yakobo, ila Israeli, maana umeshindana na Mungu, na watu, nawe umeshinda”.
Mwanzo 32:24 “Yakobo akakaa peke yake; na mtu mmoja akashindana naye mweleka hata alfajiri.
25 Naye alipoona ya kuwa hamshindi, alimgusa panapo uvungu wa paja lake; ukateguka uvungu wa paja la Yakobo alipokuwa akishindana naye.
26 Akasema, Niache, niende, maana kunapambazuka. Akasema, Sikuachi, usiponibariki.
27 Akamwuliza, Jina lako n’nani? Akasema, Yakobo.
28 Akamwambia, Jina lako hutaitwa tena Yakobo, ila Israeli, maana umeshindana na Mungu, na watu, nawe umeshinda”.
Hivyo kama wewe umeokoka halafu ukaota, unapigana na mtu muda mrefu mpaka unachoka, ni mapambano tu, Hapo ni Mungu anakukumbusha habari ya Yakobo, kwamba unapaswa utafute thawabu zake kwa nguvu mpaka uzipate, kuliko kitu kingine chochote unachoweza kukitafuta katika hii dunia. Hiyo ndio tafsiri ya kwanza.
Tafsiri ya pili: Kuota unapigana ni ishara ya vita.
Wakati mwingine, watu wanaweza kupigana, si kwa ajili wanagombania kitu Fulani, hapana, bali ni kwa ajili ya chuki, wivu, fitna, kiburi, n.k..Lengo kuu ni kutaka kukuangamiza tu basi,
Hivyo kuota unapigana na mtu, pia inaweza ikawa ni ishara una vita vya kiroho, na vita hivyo vinatoka upande wa ibilisi, haijalishi ni kwa kupitia wachawi,au mapepo, au watu wa kawaida, au vyovyote vile, lakini upo katika vita, Hivyo kama wewe upo ndani ya Kristo, zidisha ukaribu wako na Mungu katika maombi, na kujifunza Neno,..Kwasababu Bwana anasema..
Waamuzi 8:33 “kisha itakuwa, asubuhi, mara litakapokucha jua, wewe utaamka asubuhi na mapema, na kuushambulia mji huo; tena, angalia, hapo yeye na wale watu walio pamoja naye WATAKAPOKUTOKEA NJE KUPIGANA NAWE, ndipo utapata kuwatenda kama utakavyopata nafasi”.
Lakini kama wewe hujaokoka, ni wazi kuwa upo hatarini, hivyo tahadhari hizi zichukue,
Mpe leo Yesu maisha yako ayaokoke, haijalishi wewe ni wa dini gani,au dhehebu gani, Yesu Kristo anawaokoa watu wote. Ikiwa leo utakubali kutubu dhambi zako zote kwa kumaanisha kabisa kuziacha, atakusamehe na kukukubadilisha na kukupa Roho wake, ambaye atakaa ndani yako milele..Na ndiye atakayekulinda na mipenyo yote ya ibilisi katika maisha yako, kwasababu tayari utakuwa ndani ya ulinzi wa ki-Mungu.
Hivyo kama leo upo tayari kufanya hivyo, basi fungua hapa kwa ajili ya kuongozwa sala ya Toba, na maombezi>>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Kumbuka hizi ni siku za mwisho, na shetani anawinda roho za watu, kwa bidii sana ili awaangamize, kwasababu anajua wakati aliobakiwa nao ni mchache, na ndio maana unaona mapambano tu, hivyo usipuuzie wokovu ndugu yangu.
Ukiwa umefungua hapo juu na kufuata maelekezo yote, Basi Bwana akubariki sana, na Hongera kwa kuokoka.
Pia tazama masomo mengine chini ya kukusaidia kukua kiroho.
JIEPUSHE NA UNAJISI.
NA ROHO NA BIBI-ARUSI WASEMA, NJOO!
Ibada ni nini,Na je ili ikamilike inapaswa iwe na nini na nini?
MKUMBUKE MKE WA LUTU.
HASIRA YA MUNGU KUKUWAKIA, KWA KUTOMZUNGUZIA TU MUNGU IPASAVYO.
Jina la Bwana wetu Yesu libarikiwe.
Karibu tujifunze Biblia,
Umewahi kujiuliza kwanini siku zote vita vya wanajeshi vinakuwaga ni vigumu? Haijalishi watakuwa wamevaa mavazi gani ya kujikinga na silaha na risasi, lakini bado vita huwa vinakuwa vigumu? Umewahi kujiuliza ni kwanini?
Ni kwasababu wale wanaokwenda kupambana nao wapo kama wao…Adui naye kashikilia silaha kama ya kwao, wamepitia mafunzo kama ya kwao, nao pia wamevaa mavazi ya kujikinga na risasi kama wao. Kwaufupi karibia kila kitu alilichonacho mwanajeshi adui yake naye anacho..Hapo ndipo unapokuja ugumu wa vita. Na sio tu katika vita, bali hata katika michezo wanaocheza watu wa kidunia..Michezo yao inakuwa ni migumu kwasababu wapinzani wao nao pia wamejiandaa kama wao, wana mbinu kama zao, na pia wana akili kama zao..
Na katika ulimwengu wa roho tunapaswa tulitambue hilo. Kwamba tupo vitani, na tunayepambana naye hayupo mikono mitupu, bali naye pia ni askari kama sisi.
Pale tunaposoma andiko la kwenye Waefeso 6:11 kwamba “Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani.” Maana yake ni kwamba shetani naye upande wa pili kashika silaha kama sisi. Angekuwa si askari kama sisi biblia isingetuambia tushike ngao, ngao ya nini kama unayepambana naye hana silaha kali? Unaona.
Kwaufupi katika ulimwengu wa roho, wote tunafanana kimwonekano…shetani na mapepo yake pamoja na sisi. Wote tumevaa silaha.
Ukizidi kusoma hiyo habari ya kwenye Waefeso utaona biblia inasema tukamate upanga wa roho ambao ni Neno la Mungu…sasa jambo la muhimu kufahamu ni kuwa upanga huo huo (yaani Neno la Mungu) shetani pia anao. Na upanga huo huo tunaotumia kumkata, ndio huo huo anaotumia na yeye kutukata sisi tusipokuwa watashi.
Utauliza ni wapi shetani amewahi kuwa na Neno la Mungu (na kulitumia hilo kumkata mtu wa Mungu)?
Kasome Luka 4:9-13, uone jinsi alivyolitumia kumshambulia Bwana kule jangwani.
Hivyo mwanajeshi wa kweli aliye vitani hafurahii tu kubeba bunduki au mkuki na kuvaa kijeshi, kwasababu anajua hata adui yake naye kashika bunduki kama yake, na anajua asipokuwa makini anaweza kufa na silaha zake mkononi, hivyo anachojiaminisha nacho ni UTASHI wa kutumia silaha yake, uwezo wa kukwepa, uwezo wa kukinga, na ushapu na ushupavu. Kwahivyo ndivyo atakavyomshinda adui yake, lakini akilala tu na kusema tayari ana bunduki mkononi, tayari amevaa nguo ya kuzuia risasi basi ni dhahiri huyo mwanajeshi anakwenda kufa huko.
Ndugu kama askari tusifurahie tu kulikariri Neno, bali tufurahie uwezo wa kulichambua vyema, kama aliokuwa nao Bwana Yesu…Kwasababu biblia inasema Neno la Mungu ni upanga ukatao kuwili, lina makali pande zote kama sime, maana yake pia adui yako akilishika anaweza kukudhuru nalo na ukakatikakatika kabisa.
Na kama tulivyotangulia kusema kuwa shetani na mapepo yake ni wanajeshi kama sisi, yamevaa makombati, na yanaouwezo mzuri wa kutumia silaha, hivyo ni ushapu wetu, na utashi wetu ndio utakaowashinda…Sasa utauliza ni wapi biblia inasema kwamba mapepo ni majeshi?
Waefeso 6:11 “Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani. 12 Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya MAJESHİ YA PEPO WABAYA katika ulimwengu wa roho”.
Waefeso 6:11 “Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani.
12 Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya MAJESHİ YA PEPO WABAYA katika ulimwengu wa roho”.
Hebu jiulize kwanini biblia haijatumia neno hapo “umati wa pepo wabaya” badala yake imetumia neno “jeshi”?.. maana yake ni kwamba haya maroho nayo yamevaa silaha na makombati, yapo vitani kupambana…hayapo hayapo tu!
Pia tunaweza kusoma andiko lingine linalozungumzia majeshi ya mapepo wabaya..katika Luka 8:30 “Yesu akamwuliza, Jina lako nani? Akasema, JİNA LANGU Nİ JESHİ; kwa sababu pepo wengi wamemwingia”
Kwanini yalipoulizwa majina yao, hayakusema “jina letu umati” badala yake yakasema “jeshi”?. Hiyo ni kuonyesha kuwa yapo vitani, yameshika silaha. Na sisi wakristo hatupaswi kulala, tunapaswa tusimame tushike silaha!. Na tuongeze utashi wa hali ya juu katika kutumia silaha (yaani Neno la Mungu).
Hivyo hatuna budi kuingia ndani sana katika kujifunza Neno la Mungu, na kuweza kulitumia. Bwana wetu Yesu alikuwa mfano mzuri…Shetani alikuja na Neno, lakini Bwana alikuwa na Neno zaidi ya lile..hivyo shetani alipomtupia ule upanga, Bwana aliukinga na kumkata kwa utashi aliokuwa nao wa kuweza kulitumia Neno.
Vivyo hivyo katika maisha na katika wokovu tuna vitu vingi sana, ambavyo shetani anatutesa navyo kwasababu tu hatujui jinsi ya kulitumia Neno vizuri(hatuna utashi, wala ushapu, wala uzoefu wa Neno). Neno tunalo, lakini jinsi ya kulitumia ndipo tunaposhindwa na hivyo adui shetani analitumia hilo hilo kutumaliza.
Sasa Ni kwa namna gani tutaweza kulitumia Neno vizuri ili kuzishinda hila za shetani? Ni kwa kujifunza kwa bidii Neno, na si kusoma tu!. Ipo tofauti kubwa sana ya kusoma na kujifunza Neno. Mtoto wa darasa la kwanza aliyejifunza kusoma leo…ukimpa kitabu cha biolojia cha kidato cha sita, anaweza kukisoma chote, na hata kukariri baadhi ya picha na vimaneno. Lakini hapo bado hajajifunza chochote…haijalishi kakariri mistari mingapi ya kitabu hicho.
Hivyo na sisi hatupaswi kuisoma biblia tu peke yake, bali tunapaswa tujifunze..Maana yake tunakaa chini tunasoma kitabu kimoja, na kukitafakari, na kwenda kutafuta zaidi huku na huko, maarifa juu ya hicho kitu, ili kukijazia nyama kile tulichokisoma. Na si kusoma mstari mmoja tu! Pasipo kuelewa kiini cha huo mstari toka juu, na kujisifu kwamba tunazo silaha.
Bwana atusaidie na kuzidi kutujaza Roho wake mtakatifu, ili tuweze kulitumia vyema neno lake.o
2Timotheo 2:15 “Jitahidi kujionyesha kuwa umekubaliwa na Mungu, mtenda kazi asiye na sababu ya kutahayari, UKİTUMİA KWA HALALİ NENO LA KWELİ”
Bwana atubariki.
Kama hujaokoka! Bwana Yesu yupo mlangoni kurudi.
Mbinguni ni sehemu gani?
ROHO YA MPINGA KRISTO IKITENDA KAZI SIKU HIZI ZA MWISHO
Je! Kusoma biblia kwenye simu ukiwa kanisani ni dhambi?
ZIKIMBIE TAMAA ZA UJANANI! NA MTU YEYOTE ASIUDHARAU UJANA WAKO.
Neno la Mungu ni upanga.
UPONYAJI WA ASILI
Jina la Bwana wetu na mwokozi wetu Yesu Kristo lihimidiwe daima.
Natumai u mzima, hivyo nakukaribisha tuyatafakari kwa pamoja maneno ya uzima ya Mungu wetu,.
Leo tutatazama tukio moja kati ya mengi yaliyokuwa yanaendelea kipindi kifupi kabla ya Kristo kuingia katika mateso makali ya kusulibiwa. Na tukio lenyewe ni lile na maadui wawili kukutana tena na kupatana…,Ambao ni Herode na Pilato.
Luka 23:11 “Basi Herode akamfanya duni, pamoja na askari zake, akamdhihaki, na kumvika mavazi mazuri; kisha akamrudisha kwa Pilato. 12 Basi siku ile ile Herode na Pilato walipatana kwa urafiki kwa maana hapo kwanza walikuwa na uadui wao kwa wao”.
Luka 23:11 “Basi Herode akamfanya duni, pamoja na askari zake, akamdhihaki, na kumvika mavazi mazuri; kisha akamrudisha kwa Pilato.
12 Basi siku ile ile Herode na Pilato walipatana kwa urafiki kwa maana hapo kwanza walikuwa na uadui wao kwa wao”.
Ulishawahi kujiuliza ni kwanini hawa watu wasipatanishwe na mambo mengine ya msingi mfano ya kidiplomasia, au ya kiuchumi, mpaka wapatanishwe na kukamatwa kwa mtu Fulani mwenye haki?. Utajiuliza Yesu alikuwa ana umuhimu gani kwao? Kwani ni yeye ndiye aliyewagombanisha? Kwanza wao walikuwa ni warumi Yesu ni myahudi, wao wapo Israeli kwa lengo la kutimiza mambo yao ya kiutawala na kuhakikisha nchi inastawi na kupeleka kodi nzuri kwa mkuu wao Kaisari aliyeko huko Rumi kwao, maelfu ya maili kutoka hapo walipo, Hivyo Yesu hakuwa na umuhimu wowote kwao, kwasababu yeye hakuwa mwanasiasa wala mfanyabiashara, au jasusi fulani..
Hivyo ukitazama kwa ukaribu utagundua kuwa muungano ule haukuwa wa kawaida, Bali ni muungano uliobuniwa na mamlaka tofauti na wanaoujua wao, na hiyo si nyingi zaidi ya ile ya mamlaka ya giza.
Na ndio maana kipindi kifupi kabla Bwana Yesu hajakamatwa kule Gethsemane, aliwaambia wale waliokuja kumkamata kuwa huu ndio WAKATI WA MAMLAKA YA GIZA kutenda kazi (soma Luka 22:52-53).
Mamlaka ya giza siku zote, ikitaka kuleta dhiki, huwa inafanya kazi ya kuwakutanisha na kuwapatanisha kwanza pamoja wakuu, hata wale maadui walioshindikana wa muda mrefu, inawapatanisha..Na inafanya hivyo ili kuongeza nguvu ya kutimiza azma yake ya maangamizi, na si kingine..
Na ndio maana, kipindi kile Kama Herode na Pilato wasingeungana, Bwana Yesu asingesulibiwa kwa namna yoyote ile, kwasababu amri ilipaswa iidhinishwe na pande zote mbili,. Na sio tu hao wafalme wawili waliungana, bali biblia inatuambia pia pamoja na mataifa, na watu wa Israeli ikiwemo waandishi na makuhani, waliungana pamoja ili kufanya shauri la kumwangamiza Kristo. Mpaka mafarisayo na Masadukayo ambao kutwa kuchwa walikuwa wakikinzana lakini waliungana kipindi hicho (Kasome Mathayo 22:34).
Matendo 4:25 “ nawe ulinena kwa Roho Mtakatifu kwa kinywa cha babaetu Daudi, mtumishi wako, Mbona mataifa wamefanya ghasia, Na makabila wametafakari ubatili? 26 WAFALME WA DUNIA WAMEJIPANGA, NA WAKUU WAMEFANYA SHAURI PAMOJA Juu ya Bwana na juu ya Kristo wake. 27 MAANA NI KWELI, HERODE NA PONTIO PILATO PAMOJA NA MATAIFA NA WATU WA ISRAELI, walikusanyika katika mji huu juu ya Mtumishi wako mtakatifu Yesu, uliyemtia mafuta”
Matendo 4:25 “ nawe ulinena kwa Roho Mtakatifu kwa kinywa cha babaetu Daudi, mtumishi wako, Mbona mataifa wamefanya ghasia, Na makabila wametafakari ubatili?
26 WAFALME WA DUNIA WAMEJIPANGA, NA WAKUU WAMEFANYA SHAURI PAMOJA Juu ya Bwana na juu ya Kristo wake.
27 MAANA NI KWELI, HERODE NA PONTIO PILATO PAMOJA NA MATAIFA NA WATU WA ISRAELI, walikusanyika katika mji huu juu ya Mtumishi wako mtakatifu Yesu, uliyemtia mafuta”
Umeona hapo, timu ya kumwangamiza Yesu ilikuwa ni kubwa sana kuliko unavyoweza kudhani na sehemu kubwa ya hiyo ilikuja kwa kupatana kwa maadui.
Ndivyo itakavyokuwa katika dhiki kuu ndugu yangu. Roho ya mpinga-Kristo, itayakutanisha mataifa takribani yote ulimwenguni, na kitakachowakutanisha sio mikataba ya amani unayoiona leo hii inayosainiwa kila siku, sio makubaliano ya kiuchumi, wala sio mazungumzo ya kidiplomasia, hayo hayawezi kuipatanisha dunia hata kidogo, yameshafanyika mara nyingi huko nyuma, mpaka leo hii hakuna hata moja lililowezekana..
Kitakachokuja kuipatanisha dunia na kuwa na serikali moja ya makubaliano ambayo bila hiyo mtu hataweza, kuuza wala kununua, wala kuajiriwa itakuwa ni ya mamlaka ya giza, juu ya UKRISTO halisi ulimwenguni. Utajiuliza ukristo una nguvu gani mpaka uyasababishe mataifa yaungane?,
jibu ndio kama lile la Bwana Yesu, kwani yeye alikuwa na ushawishi gani mpaka Herode na Pilato maadui wa muda mrefu waungane,. Utagundua kuwa shetani ni lazima afanye hivyo ili atimize agenda yake vizuri.
Hapo ndipo wale ambao watakaokuwa wameukosa unyakuo, watayashuhudia haya, ghafla tu kutatokea visa visivyokuwa na mashiko ambavyo vitawalenga wakristo wale walioachwa kwenye unyakuo, na hivyo vitasababisha dunia nzima uinganishwe chini ya mfumo mmoja wa mpinga-kristo, Hapo ndipo kutakuwa na dhiki ambayo haijawahi kutokea tangu dunia iumbwe, na hiyo itawalenga wale wanawali vuguvugu waliokukosa unyakuo, ambao hawatakuwepo kwenye huo mfumo wao.
Mambo hayo ndugu yangu, yapo mlangoni kutokea, na yatakuja kwa ghafla sana, dalili karibia zote za mwisho wa dunia zimeshatimia, siku yoyote unyakuo utapita, na ndio maana Bwana Yesu anataka kutuepusha na huo wakati mbaya sana, wa kuharibiwa kwa ulimwengu.
Anasema,
Ufunuo 3:10 “Kwa kuwa umelishika neno la subira yangu, mimi nami nitakulinda, utoke katika saa ya kuharibiwa iliyo tayari kuujilia ulimwengu wote, kuwajaribu wakaao juu ya nchi. 11 Naja upesi. Shika sana ulicho nacho, asije mtu akaitwaa taji yako.
Ufunuo 3:10 “Kwa kuwa umelishika neno la subira yangu, mimi nami nitakulinda, utoke katika saa ya kuharibiwa iliyo tayari kuujilia ulimwengu wote, kuwajaribu wakaao juu ya nchi.
11 Naja upesi. Shika sana ulicho nacho, asije mtu akaitwaa taji yako.
Je! tumejiwekaje tayari? Je na sisi tumelishika Neno la subira yake? Bwana Yesu akirudi usiku wa leo tunao uhakika wa kwenda naye mbinguni?. Kama hatuna uhakika huo, ni dhahiri kuwa tutababaki, hivyo ni heri tuyasalimishe maisha yetu kwa Bwana ayaokoe ndani ya hichi kipindi kifupi tulichobakiwa nacho. Na yeye mwenyewe atahakikisha anatufikisha ng’ambo salama.
Maran Atha.
JINSI DHAMBI INAVYOMGHARIMU MTU SANA.
Bilauri ni nini kibiblia?(Ufunuo 21:11,22:1)
MWACHE YESU, NDIO AWE WA KWANZA KUKUHURUMIA.
HERI YULE ATAKAYEKULA MKATE KATIKA UFALME WA MUNGU.
FAIDA ZA KUFUNGA NA KUOMBA.