Shalom, karibu tujifunze Neno la Mungu, ambalo ndio cha kweli cha roho zetu.
Kawaida ya Mungu ni huwa hatoi agizo juu ya agizo. Yaani kwa mfano leo akikupa agizo fulani ulitelekeze, haundi agizo lingine juu yake kulibatilisha hilo la kwanza, Atafanya hivyo endapo tu lile la kwanza litakuwa limeisha muda wake.
Mara nyingi tunakuwa tukiacha yale maagizo ya kwanza ya Mungu, na hiyo inatupelekea aidha kukutana na hukumu yake, au kushindwa kutekeleza mipango yetu kwa wakati.
Kwamfano utakutana na nabii mmoja katika biblia enzi za wafalme, ambaye alipewa maagizo na Mungu ya kwenda kumtolea unabii Mfalme mwasi Yeroboamu, akaambiwa akishamaliza kazi yake asile wala asinywe chochote katika mji huo, wala asilale au kupumzika na njia atakayoipita asiirudie tena hiyo hiyo. Lakini huyu nabii alipomaliza kweli kazi ya huduma alianza safari ya kuondoka. Lakini akiwa njiani alikutana na nabii mwingine mzee, akamshurutisha, aende kulala nyumbani kwake. Lakini yeye akamwambia Bwana amenionya nisikae mahali popote kwenye mji huu.
Sasa yule nabii mzee alipoona kuwa kijana huyu hataki, akamtungia habari za uongo na kumwambia, Bwana ameniambia ameghahiri, mpango wake, hivyo anataka uje ule upumzike nyumbani kwangu. Na yule kijana pasipo kufikiria ni kwanini Mungu awe kigeugeu, saa hiyo hiyo akamwamini, kwasababu tu ni nabii mwenzake tena mzee, anauzoefu wa mambo ya kinabii, akaenda kukaa kwake. Kitu kilichomtokea hatuna haja ya kueleza, sote tunajua alikuja kuliwa na simba, kwa kuyaasi maagizo ya Mungu (Soma 1Wafalme 13)
Tunamwona Mtu mwingine anaitwa, Balaamu, naye pia mwanzoni Mungu alimuonya asiende kuwalaani Israeli, lakini baadaye akawa analazimisha mawazo yake kwa Mungu, kilichofuata ilikuwa ni Mungu kumwambia haya nenda nitakuwa pamoja nawe..kumbe hakujua tayari njia Mungu alikuwa ameshamuandalia malaika wake amuue, na kama sio yule punda kumsaidia habari yake tusingeisoma leo hii kwenye biblia (Soma Hesabu 22).
Hiyo yote ni kutozingatia agizo la kwanza Mungu alilokupa, Siku zote agizo linalokuja juu ya agizo lile la mwanzo huwa halitokani na Mungu.
Tukisoma tena habari nyingine maarufu katika biblia ile ya Wana wa Israeli walipokuwa wanatoka Babeli utumwani, baada ya kukaa kule miaka 70. Biblia inatuambia Mungu alimuamsha moyo mfalme Koreshi wa uajemi, ili atoe amri kuwa watu wote waondoke kwenye makoloni yake, waende Yerusalemu kumjengea Mungu nyumba, kufuatana na unabii uliotolewa na Yeremia zamani.
Tunaona baada ya hapo Mfalme aliwapa zawadi nyingi sana, Hivyo waliondoka kwa moyo mkunjufu wakijua kabisa Mungu kaitimiza ahadi yake ya kwenda kumjengea nyumba Yerusalemu. Lakini walipofika kule na kuanza kutia msingi wa nyumba ya Mungu, maadui zao wakaanza kunyanyuka hilo likawadhoofisha, na kama hiyo haitoshi wakaandika waraka wa uchongezi wakampelekea mfalme mwingine wa uajemi ambaye alikuja kutawala baada ya Koreshi, aliyeitwa Dario, mfalme alipousoma, akatoa amri nyingine, kuwa usiendelee ujenzi wowote Yerusalemu, wa nyumba ya Bwana. Na mtu yeyote atakayefanya vile ilikuwa ni kifo.
Wayahudi waliposikia, juu waraka huo mpya, wote wakavunjika moyo, wakaacha kuijenga nyumba ya Mungu ambayo ilikuwa tayari katika hatua nzuri, Hivyo ikapelekea nyumba hiyo kubakia hivyo hivyo kwa muda wa miaka mingi sana..Kila mtu akarudi kuendelea na shughuli zake kila siku.
Wakasau kuwa ni Mungu ndiye aliyewapa maagizo kuwa wakamjengee nyumba yeye, hawakujiuliza sasa haya maagizo mengine yanatoka wapi?
Mpaka baadaye sana, tunaona manabii wawili yaani Hagai na Zekaria wanatokea, wanawatabiria na kuwauliza kwanini mnaacha kujenga nyumba ya Mungu, wakidai kuwa huu sio wakati wa kumjengea Mungu? Kwa muda wako soma kitabu chote cha Hagai utaona mambo hayo.
Unaona, walisikiliza sauti ya pili, wakaicha ile ya kwanza, na hiyo ikawapelekea kucheleweshwa kwa huduma yao waliyokuwa wameshaianza,.. Siku zote sauti ya pili ni ya shetani, na sio ya Mungu.
Vilevile katika agano jipya kuna agizo ambalo tayari Mungu alishatupa.
Marko 16:15-16 Inasema..
“Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe.
Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa”.
Hili ni agizo ambalo Kristo alishatoa kibali, kufanya.. Lakini dunia ya sasa shetani ameshaiingilia, kiasi kwamba, sehemu nyingine watu hawaruhusiwi kuhubiri kabisa, sheria za nchi zao zimekataza..Sasa wewe kama mkristo ukiogopa sheria ya wanadamu, ukasema pengine huu sio wakati wa kufanya hivyo, ujue kuwa utafanana na wana wa Israeli walipokuwa wanalijenga hekalu la pili, utasubiria wee, na kamwe hiyo siku ambayo unayoina itafaa haitafika, Mungu atakachofanya ni kukumbusha tu, uliacha agizo la kwanza.
Sio hilo tu yapo maagizo mengine madogo madogo, yanakubana kiasi kwamba yanakufanya ushindwe hata kuiendeleza kazi ya Mungu, mpaka uwe na hiki au kile, au ukamilishe hiki au kile..Hayo yote hatupaswi kuyazingatia sana, mengine yana agenda ya shetani nyuma yake kukumwisha tu, bali tuzingatie lile agizo kuu la mwanzo ambalo Kristo ametupa enendeni ulimwenguni kote.
Mwingine atasema familia yangu iko hvi au vile..hupaswi kuangalia hayo yote
Safari ya imani, si mteremko muda wote, kuna wakati itasumbuliwa na mambo mengi, lakini hatupaswi kuyaogopa kwasababu Mungu ameshaahidi atakuwa na sisi katika hayo yote. Kama tu vile alivyokuwa kwa mababa zetu katika mapito yao.
Shalom.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
MAAGIZO YA BWANA YESU NI BORA KULIKO MAAGIZO YA DAKTARI:
Nini maana ya “mkilichukia hata vazi lililotiwa uchafu na mwili”?
BWANA AYAGANGE NA MACHO YETU PIA.
Mungu anaposema “nitaliweka jina langu” ana maana gani?
KIFO CHA MTAKATIFU PERPETUA NA FELISTA.
Rudi nyumbani
Print this post
Shalom, karibu tujifunze maneno ya uzima.. Lipo swali ambalo linaulizwa na watu wengi, kwamba kama Mungu anajua kuna jambo litakwenda kutokea mbeleni ambalo litanisababishia mauti, kwanini basi asinizuie kwenda kulifanya badala yake ananiacha mpaka naingia, na mwisho wa siku napotea na kwenda kuzimu? Mbona kama vile atakuwa sio Mungu wa upendo?
Kama na wewe swali hili lipo ndani yako basi tuzidi kutafakari pamoja somo letu la leo,
Kitabu cha Mithali kinasema..
“Kwa kuwa mtego hutegwa BURE, Mbele ya macho ya ndege ye yote”.( Mithali 1:17).
Embu jiulize, mtu anayetega mtego wa kumshika ndege kwa ajili ya kitoweo chake, Je! Unadhani Mungu hampendi ndege yule? Au unadhani Mungu hajampa uwezo wa kuwakimbia maadui zake kiwepesi?
Au mtu anayetega mtego wa kunasa panya, unadhani Mungu anawachukia panya, na hivyo kawaondolea uwezo wa kuwakimbia adui zao?
Au mtu anayetega ndoano kuvua samaki, unadhani Mungu hawapendi samaki wake,?
Sikuzote mpaka umeona kitu fulani kinaundiwa mitego, basi ujue kuwa kitu hicho kilishashindikana kukamatika kwa njia rahisi, au ya kawaida, hivyo kimetafutiwa njia mbadala, kwamfano leo hii unaweza kumuona ndege katua hapo pembeni yako, hatua kadhaa tu pembeni, lakini embu kajaribu kwenda kumkamata kwa mikono yako kama utaweza,? Au umwone panya anakatiza kwenye kona ya nyumba, au store, halafu fanya mazoezi ya kwenda kumkata kwa mikono kama vile unavyokamata chura uone kama itakuwa ni kazi rahisi kwako.
Au umwone samaki anaelea juu ya maji, hivyo unatakwenda kwenda kumchota haraka kwa mikono yako, jaribu zoezi hilo kama litakuwa rahisi. Huwezi kuwapata kwasababu Mungu tayari kashawekea uwezo ndani yao wa kujiangua kutoka kwa maadui zao kivyepesi sana.. na wenyewe wanajua kabisa maadui zetu ni ngumu kutushika kwasababu hawana wepesi tulionao sisi, au hawana uhodari tulionao sisi wenyewe.. Na sisi tunaowawinda tunajua kuwa ili waendelee kuwa salama ni wajibu wao, kutotuamini sisi kwa kitu chochote siku zote za maisha yao hapa duniani, haijalishi tutawavutia kwa vitu vingi kiasi gani wanavyovipenda.
Vivyo hivyo na sisi wanadamu, Mungu ameshatupa uwezo mkubwa sana ndani yetu wa kumshinda adui yetu shetani, na yeye analijua hilo, hawezi kuja na kukukamata hivi hivi kama anavyotaka, hana uwezo huo, anajua kabisa hawezi kukupata, lakini anachokifanya ni kijiundia mitego yake mbalimbali, ambayo hiyo ikishakunasa, basi hapo ndipo anakuwa na uwezo wa kukufanya chochote anachotaka ikiwemo hata kukuua.
Kwamfano mtego mmojawapo maarufu , ni uasherati, shetani anaweza kukuletea kahaba, ili mkazini, lengo lake sio ukutane na kahaba au uzini tu halafu basi, hapana, bali ni ukosane na Mungu wako kwa kitendo hicho, ili apate nafasi ya kuyaachilia mapepo yake yaingie katika maisha yako kukuharibu kirahisi katika kila nyanja, ikiwemo upate na magonjwa ya zinaa kama vile ukimwi ili ufe kabla ya wakati wako.
Lakini hayo anajua hayawezi kuja hivi hivi, ni mpaka akuwekee mtego, ndipo hapo anakuletea kahaba mzuri, au mwanaume mwenye pesa, anakulaghai na wewe bila kufikiri kuwa ule ni mtego umewekwa mbele yako unakwenda kuuva, ukidhani kuwa Mungu atakuepusha nao.. Hilo Mungu hawezi kulifanya ndugu yangu.
Kwa nafasi yako soma kitabu cha Mithali sura ya 7 yote, uone jinsi, kijana mpumbavu aliyetegwa na mwanamke mzinzi, na hatma yake inavyokuwa; hatuwezi kusoma vyote lakini vile vifungu vya mwisho mwisho vinasema..
Mithali 7:21 “Kwa maneno yake mengi na ulaini akamshawishi, Kwa ubembelezi wa midomo yake akamshinda. 22 Huyo akafuatana naye mara hiyo, KAMA VILE NG’OMBE AENDAVYO MACHINJONI; Au mpumbavu kuadhibiwa katika pingu; 23 Hata mshale umchome maini; KAMA NDEGE AENDAYE HARAKA MTEGONI; Wala hajui ya kuwa ni hasara ya nafsi yake. 24 Basi, wanangu, nisikilizeni sasa, Mkayaangalie maneno ya kinywa changu. 25 Moyo wako usizielekee njia zake, Wala usipotee katika mapito yake. 26 Maana amewaangusha wengi waliojeruhi, Naam, JUMLA YA WALIOUAWA NAYE NI JESHI KUBWA. 27 Nyumba yake ni njia ya kwenda kuzimu, Hushuka mpaka vyumba vya mauti.
Mithali 7:21 “Kwa maneno yake mengi na ulaini akamshawishi, Kwa ubembelezi wa midomo yake akamshinda.
22 Huyo akafuatana naye mara hiyo, KAMA VILE NG’OMBE AENDAVYO MACHINJONI; Au mpumbavu kuadhibiwa katika pingu;
23 Hata mshale umchome maini; KAMA NDEGE AENDAYE HARAKA MTEGONI; Wala hajui ya kuwa ni hasara ya nafsi yake.
24 Basi, wanangu, nisikilizeni sasa, Mkayaangalie maneno ya kinywa changu.
25 Moyo wako usizielekee njia zake, Wala usipotee katika mapito yake.
26 Maana amewaangusha wengi waliojeruhi, Naam, JUMLA YA WALIOUAWA NAYE NI JESHI KUBWA.
27 Nyumba yake ni njia ya kwenda kuzimu, Hushuka mpaka vyumba vya mauti.
Ndege anayenaswa kwenye mtego ni kajitakia mwenyewe na sio kwamba alikuwa ni dhaifu, tamaa zake ndizo zilizompeleka pale,. Leo hii, unapojikuta kwenye matatizo mazito, ambayo unajua kabisa ni kwasababu ya dhambi Fulani uliyoifanya ndio yakakukuta, usianze kumlaumu Mungu ni kwanini hakukuepusha nayo hapo kabla. Mungu alishakupa uwezo huo tangu zamani, Na Mungu naye hawezi kumlaumu shetani, kwasababu shetani naye analo la kujitetea, anasema mimi sikumuita mtu aje kwenye mtego wangu, wala sikumlazimisha mtu, kufuata kile nilichokiweka kwenye mtego, ni yeye mwenyewe alinifuata, ni ndio hapo akanasikia akaangamia, ilikuwa ni wajibu wake kuchukua tahadhari anapoishi duniani.
Na ndio maana biblia inasema..
Hosea 4: 6 “Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa;..”
Tukikosa maarifa ya kuzijua njama za shetani, au kuyajua mafumbo ya shetani, tutajikuta tunaingia katika matatizo ambayo tutajiuliza ilikuwaje kuwaje tumejikuta hapa,
Ufunuo 2:24 “Lakini nawaambia ninyi wengine mlioko Thiatira, wo wote wasio na mafundisho hayo, WASIOZIJUA FUMBO ZA SHETANI, kama vile wasemavyo, Sitaweka juu yenu mzigo mwingine. 25 Ila mlicho nacho kishikeni sana, hata nitakapokuja”.
Ufunuo 2:24 “Lakini nawaambia ninyi wengine mlioko Thiatira, wo wote wasio na mafundisho hayo, WASIOZIJUA FUMBO ZA SHETANI, kama vile wasemavyo, Sitaweka juu yenu mzigo mwingine.
25 Ila mlicho nacho kishikeni sana, hata nitakapokuja”.
Hivyo kila mmoja anao wajibu wa kupata maarifa sahihi ya kuitambua mitego ya adui. Na maarifa hayo utayapata kutoka katika Neno la Mungu tu basi, biblia imejaa siri za kuepukana na hila za adui. Na ndio maana shetani hapendi watu waisome.
Kuwa msomaji wa biblia kila siku, tafakari , usiisome kama gazeti, hiyo tu ndio itakayokuwa nuru yako katika zama hizi za kumalizia, kumbuka mitego ni mingi, vishawishi ni vingi, na ipo ya aina tofauti toauti, uwezo umepewa, pengine umepungukiwa tu na maarifa. Hivyo ni wajibu wako kuyatafuta maarifa hayo, ambayo utayapata katika Neno la Mungu. Yaani BIBLIA.
Hakuna jaribu lolote linalotendeka leo hii, ambalo halijawahi kuandikwa katika biblia na njia ya kuepukana nalo., Hivyo jijengee desturi ya kusoma Neno la Mungu. Ili usiwe wa kumlaumu Mungu, kwanini hiki, kwanini kile, wakati ni wewe mwenyewe uliyakataa maarifa, hivyo ukanasika kirahisi.
Bwana akubariki.
UFUNUO NI NINI, NA NITAPOKEAJE UFUNUO KUTOKA KWA MUNGU?
ZIFAHAMU HUDUMA KUU (10) ZA SHETANI DUNIANI.
Uga ni nini? Na kazi yake ni ipi kibiblia?
TAZAMA, NASIMAMA MLANGONI.
Kwanini Mungu awachome watu kwenye ziwa la moto na hali yeye ndiye aliyewaumba?
JINA LAKE KWA KIEBRANIA NI ABADONI, NA KWA KIYUNANI NI APOLIONI.
Mlima wa Mizeituni ni moja ya milima saba ambayo inauzunguka mji wa Yerusalemu kule Israeli . Mlima huu upo upande wa Mshariki mwa mji huo, umbali usiozidi kilometa moja, mpaka kuuingia mjini Yerusalemu. Hivyo haupo mbali sana.
Umeitwa mlima wa Mizeituni, kutokana na kuwa na sifa ya kuzungukwa na miti mingi ya mizeituni pembezoni mwa mlima huo.
Mlima huu umetajwa mara mbili katika agano la kale, mara ya kwanza ni siku ile Daudi alipokuwa anafukuzwa na mwanawe Absalomu, biblia inatuambia aliupanda mlima huu akiwa analia peku, akiambatana na wale watu aliokuwa nao kwenye ufalme.(2Samweli 15:30).
Sehemu nyingine ni katika kitabu cha Zekaria ambacho kinaeleza unabii wa masihi siku atakaposhuka mara ya pili hapa duniani, kwamba atashukia kwanza juu ya mlima huu;
Zekaria 14:3 “Hapo ndipo atakapotokea Bwana, naye atapigana na mataifa hayo, kama vile alipopigana zamani siku ya vita. 4 Na siku hiyo miguu yake itasimama juu ya mlima wa Mizeituni, unaoelekea Yerusalemu upande wa mashariki, nao mlima wa Mizeituni utapasuka katikati yake, upande wa mashariki na upande wa magharibi; litakuwako huko bonde kubwa sana; na nusu ya mlima ule utaondoka kwenda upande wa kaskazini, na nusu yake itaondoka kwenda upande wa kusini”.
Zekaria 14:3 “Hapo ndipo atakapotokea Bwana, naye atapigana na mataifa hayo, kama vile alipopigana zamani siku ya vita.
4 Na siku hiyo miguu yake itasimama juu ya mlima wa Mizeituni, unaoelekea Yerusalemu upande wa mashariki, nao mlima wa Mizeituni utapasuka katikati yake, upande wa mashariki na upande wa magharibi; litakuwako huko bonde kubwa sana; na nusu ya mlima ule utaondoka kwenda upande wa kaskazini, na nusu yake itaondoka kwenda upande wa kusini”.
Lakini katika agano jipya mlima huu umetajwa mara nyingi kidogo;
Lakini cha kufahamu zaidi ni kuwa habari zote ambazo Yesu Kristo alizitaja kuhusiana na siku za mwisho na kurudi kwake mara ya pili duniani, alizizungumzia juu ya mlima huu wa mizeituni. Utasoma hayo katika (Mathayo 24, Marko 13, Luka 21)
Hata siku ile Yesu alipoulilia mji wa Yerusalemu, juu ya maangamizi yake yaliyo mbeleni, alikuwa amesimama juu ya mlima huu.(Luka 19:37-44)
Na juu ya mlima huu, ndio aliopaa kutoka ulimwenguni, mara ya mwisho alipokutana na wanafunzi wake baada ya siku zile 40 na kuwapa maagizo ya kuhubiri injili, na kuingojea ahadi ya Roho Mtakatifu..
Matendo 1:9 “Akiisha kusema hayo, walipokuwa wakitazama, akainuliwa, wingu likampokea kutoka machoni pao. 10 Walipokuwa wakikaza macho mbinguni, yeye alipokuwa akienda zake, tazama, watu wawili wakasimama karibu nao, wenye nguo nyeupe, 11 wakasema, Enyi watu wa Galilaya, mbona mmesimama mkitazama mbinguni? Huyu Yesu aliyechukuliwa kutoka kwenu kwenda juu mbinguni, atakuja jinsi iyo hiyo mlivyomwona akienda zake mbinguni”.
Matendo 1:9 “Akiisha kusema hayo, walipokuwa wakitazama, akainuliwa, wingu likampokea kutoka machoni pao.
10 Walipokuwa wakikaza macho mbinguni, yeye alipokuwa akienda zake, tazama, watu wawili wakasimama karibu nao, wenye nguo nyeupe,
11 wakasema, Enyi watu wa Galilaya, mbona mmesimama mkitazama mbinguni? Huyu Yesu aliyechukuliwa kutoka kwenu kwenda juu mbinguni, atakuja jinsi iyo hiyo mlivyomwona akienda zake mbinguni”.
JE! MLIMA HUU UNAO UMUHIMU WOWOTE KWETU? NA JE! NI SAHIHI KWENDA KUOMBA JUU YA MLIMA HUU?.
Ni wajibu wetu kujua kuwa huu ndio mlima ambao Kristo atashukia siku ile atakaporudi mara ya pili kuuhukumu ulimwengu na kutawala kama mfalme. Na kama tulivyosoma katika unabii wa Zekaria ni kwamba siku hiyo atakapokuja, mlima huu utagawanyika katikati, upande wa Mashariki, na Upande wa Magharibi, na hapo katikati kutakuwa na bonde kubwa sana. Siku hiyo atauwa waovu wote watakaokuwepo duniani kwa wakati huo.. Kipindi hichi ndio kile biblia inasema kila jicho litamwona, na mataifa yote watamwombolezea, watu watatamani milima iwaungukie kwasababu watauliwa na Kristo mwenyewe. (Mambo hayo watakutana nao wale watakaoukosa unyakuo)
Kwa urefu wa somo hilo fungua hapa >>WATAMTAZAMA YEYE AMBAYE WALIMCHOMA;
Na baadaye akishawamaliza waovu wote ataingia mji wa Yerusalemu, na kisha atatawala kama Mfalme wa Wafalme na Bwana wa Mabwana, juu ya dunia nzima kwa muda wa miaka 1000,
Ataitengeneza upya hii dunia, kutakuwa na amani ya milele isiyoelezeka. Dunia itakuwa kama paradiso. Na wakati huo upo karibuni sana. Hivyo ni wajibu wetu sisi sote kujua mambo yatakayoendelea Israeli katika siku za mwisho, ikiwemo juu ya mlima huu wa mizeituni, ili tujue leo hii tunasimama wapi. Tusiishi tu kama watu wengine wa ulimwengu, wasioona mambo ya mbeleni.
Lakini sasa tukirudi kwenye sehemu ya pili ya swali letu je! Ni Sahihi kwenda kuomba juu ya mlima huu?
Watu wengi wamekuwa wakienda Yerusalemu, kupeleka maombi yao, wakidhania kuwa mahali pale ndipo Mungu atawasikia vizuri zaidi kuliko huku walipo, wengine wamekuwa wakikesha kwenye ule ukuta wa maombolezo, wengine juu ya mlima huu wa Mizetuni, wengine kwenye mto Yordani n.k..
Lakini ukweli ni kwamba kufanya hivyo ni kukosa maarifa ya kutosha juu ya agano tulilo nalo leo hii. Bwana Yesu alimwambia Yule mwanamke;..
Yohana 4:21 “Yesu akamwambia, Mama, unisadiki, saa inakuja ambayo hamtamwabudu Baba katika mlima huu, wala kule Yerusalemu…. 4.23 Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu.
Yohana 4:21 “Yesu akamwambia, Mama, unisadiki, saa inakuja ambayo hamtamwabudu Baba katika mlima huu, wala kule Yerusalemu….
4.23 Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu.
Agano la Damu ya Yesu, ni agano la kimbinguni, kiasi kwamba mtu yeyote mahali popote atasikiwa na Mungu ikiwa tu ataingizwa katika agano hilo lililo bora. Na Mtu ataingia ndani ya agano hilo, kwanza kwa kumwamini Yesu Kristo, kisha kutubu dhambi zake, na baada ya hapo kuwa tayari kubatizwa na kupokea Roho Mtakatifu. Akikamilisha hatua hizo anakuwa ameshaokoka.
Na mtu kama huyo maombi yake yanasikiwa, ziadi hata mtu aliyekwenda kuomba juu ya mlima huu.
Je! Wewe umeingizwa kwenye agano hili?. Je! Una habari kuwa Yesu Kristo yupo mlangoni kurudi? Na unabii huo upo mlangoni kutimia? Unasubiri nini usimkaribishe Kristo moyoni mwako. Bado unatangatanga na ulimwengu ili siku ile ikujie ghafla?. Mambo yatakayoendelea huku duniani kwa watakaoukosa unyakuo hayaelezeki ndugu yangu, Ni heri leo ukayakabidhi maisha yako kwa Yesu. Kama moyo wako leo hii upo tayari kufanya hivyo. Basi uamuzi huo ni wa busara sana. Hivyo fungua hapa kwa ajili ya kupata maelekezo ya sala ya Toba. >>> SALA YA TOBA
Na Bwana akubariki sana.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312
MAPIGO YA VITASA SABA, NA SIKU YA BWANA.
CHUKIZO LA UHARIBIFU
UFUNUO: Mlango wa 20
Amin, nawaambia, Kizazi hiki hakitapita..
UTAWALA WA MIAKA 1000.
Rudi Nyumbani:
Biblia inaziorodhesha bahari kuu nne, tuzisome;
1 ) Bahari ya shamu: Kwa sasa inajulikana kama bahari nyekundu, (Kwa kiingereza red sea). Hii ni ile bahari ambayo wana wa Israeli waliivuka baada ya Mungu kuipasua pale walipokuwa wanafuatiliwa na maadui zao, ambapo tunaona baadaye walikuja kumezwa na bahari ile.
Kutoka 15:22 “Musa akawaongoza Israeli waende mbele kutoka Bahari ya Shamu, nao wakatokea kwa jangwa la Shuri; wakaenda safari ya siku tatu jangwani wasione maji”.
2) Bahari kubwa , au bahari ya Wafilisti, (Kutoka 23:31): Kwasasa inajulikana kama habari ya Mediteranea. Ipo upande wa Magharibi wa taifa la Israeli. Hii ndio bahari kubwa kuliko zote zinazoorodheshwa kwenye biblia.
Hesabu 34:6 “Kisha mpaka wenu wa upande wa magharibi mtakuwa na bahari kubwa na mpaka wake; hii ndiyo mpaka wenu upande wa magharibi”.
Soma pia Yoshua 9:1, 15:47, 23:4, Ezekieli 47:19
3) Bahari ya Galilaya; Au kwa jina lingine Bahari ya Tiberia, au ziwa la Genesareti au Bahari ya Kinerethi Yoshua 12:3, 13:27, 34:11. Hii ndio ile bahari ambayo Bwana Yesu alitembea juu ya maji.
Luka 5:1 “Ikawa makutano walipomsonga wakilisikiliza neno la Mungu, yeye alikuwa amesimama kando ya ziwa la Genesareti,”
Mathayo 4:18 “Naye alipokuwa akitembea kando ya bahari ya Galilaya, aliona ndugu wawili, Simoni aitwaye Petro, na Andrea nduguye, wakitupa jarife baharini; kwa maana walikuwa wavuvi”.
4) Bahari ya chumvi: Hii ni habari ndogo sana, ambapo ipo chini ya mto Yordani, maji yake ni ya chumvi nyingi sana, jambo ambalo linaifanya bahari hiyo isiwe na kiumbe wa kuishi ndani yake kama samaki, sehemu nyingine wanaiita ‘bahari mfu’(Dead Sea)
Hesabu 34:3 “ndipo upande wenu wa kusini utakuwa tangu bara ya Sini kupita kando ya Edomu, na mpaka wenu wa kusini utakuwa tangu mwisho wa Bahari ya Chumvi kuelekea mashariki”;
Kumbukumbu 3:17, Yoshua 15:2.
Shalom, tazama maeneo mengine mbalimbali ya biblia chini.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312 / 0693036618.
Jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mto Frati upo nchi gani, Umuhimu wake katika biblia ni upi?
MTO YORDANI UKO NCHI GANI KWA SASA?
Sharoni ni nini au ni wapi kibiblia?(1Nyakati 5:16)
JIEPUSHE NA MANENO YA MANABII WA UONGO.
Kikoto ni nini?
Kikoto ni aina ya kiboko mfano wa mjeledi. Tazama picha juu.
Tunaweza kuona wakati ule Yesu alipokwenda Hekaluni na kukuta watu wameigeuza nyumba yake kuwa pango la wanyang’anyi, tendo alilolifanya ni kuunda aina hii ya mjeledi, kwa kuusokota kwa kamba mbeleni. Ili awaadhibu vizuri wale watu waliokuwa wanasitiri maovu yao kule, waliokuwa wanafanya biashara zao mule ndani , pamoja na mifugo yao.
Yohana 2:13 “Na Pasaka ya Wayahudi ilikuwa karibu; naye Yesu akakwea mpaka Yerusalemu. 14 Akaona pale hekaluni watu waliokuwa wakiuza ng’ombe na kondoo na njiwa, na wenye kuvunja fedha wameketi. 15 Akafanya kikoto cha kambaa, akawatoa wote katika hekalu, na kondoo na ng’ombe; akamwaga fedha za wenye kuvunja fedha, akazipindua meza zao; 16 akawaambia wale waliokuwa wakiuza njiwa, Yaondoeni haya; msiifanye nyumba ya Baba yangu kuwa nyumba ya biashara”.
Yohana 2:13 “Na Pasaka ya Wayahudi ilikuwa karibu; naye Yesu akakwea mpaka Yerusalemu.
14 Akaona pale hekaluni watu waliokuwa wakiuza ng’ombe na kondoo na njiwa, na wenye kuvunja fedha wameketi.
15 Akafanya kikoto cha kambaa, akawatoa wote katika hekalu, na kondoo na ng’ombe; akamwaga fedha za wenye kuvunja fedha, akazipindua meza zao;
16 akawaambia wale waliokuwa wakiuza njiwa, Yaondoeni haya; msiifanye nyumba ya Baba yangu kuwa nyumba ya biashara”.
Ili kujua Bwana Yesu alimaanisha nini kusema msiigeuze nyumba ya Baba yangu kuwa pango la wanyang’anyi fungua hapa>> USIIGEUZE NYUMBA YA MUNGU KUWA PANGO LA WANYANG’ANYI.
Hiyo ni kutuonyesha kuwa wivu wa Mungu sikuzote unaleta adhabu.
Na adhabu hii ipo kwenye makundi mawili;
Kundi la kwanza: Ni kwa wale watu wanaolinajisi hekalu lake leo hii (yaani Kanisa), kwa kufanya mambo ambayo hayana misingi ya kiimani. Mfano kuigeuza kazi ya Mungu kama biashara, kuabudu masanamu, kwenda nusu uchi kanisani, n.k.
Na kundi la pili: Ni lile la watu wanaolinajisi hekalu lake (yaani Miili yao) kwa kufanya mambo ambayo hayampendezi. Kama vile uzinzi, uuaji, ulevi, n.k. Kwani biblia inasema;
1Wakorintho 6:18 “Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe. 19 Au hamjui ya kuwa MWILI WENU NI HEKALU LA ROHO MTAKATIFU aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe; 20 maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu”.
1Wakorintho 6:18 “Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe.
19 Au hamjui ya kuwa MWILI WENU NI HEKALU LA ROHO MTAKATIFU aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe;
20 maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu”.
Na inasema tena;
1Wakorintho 3:16 “Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu? 17 Kama mtu akiliharibu hekalu la Mungu, Mungu atamharibu mtu huyo. Kwa maana hekalu la Mungu ni takatifu, ambalo ndilo ninyi”.
1Wakorintho 3:16 “Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu?
17 Kama mtu akiliharibu hekalu la Mungu, Mungu atamharibu mtu huyo. Kwa maana hekalu la Mungu ni takatifu, ambalo ndilo ninyi”.
Unaona? Na kikoto hichi tayari kipo mkononi mwa Bwana. Hivyo tujichunguze na sisi tumelitunzaje hekalu lake? Kama tumekuwa tukiliharibu, ni heri tumgeukie kwa Bwana sasa, kabla ya wakati wa kuharibiwa haujafika. Kwasababu ukishafika na tukakutwa katika hali kama hizo, tujue kuwa hakuna neema tena.
Nini maana ya uvuvio?.
Nini maana ya kuabudu?
MOJA YA HIZI SIKU TUTAONA MABADILIKO MAKUBWA SANA.
FANYIKA SIPORA WA KRISTO, UNYAKUO UPO KARIBU.
MADHARA YA KUPUUZIA MAAGIZO YA MSINGI MUNGU ANAYOKUPA.
Mataifa ni nini katika Biblia?
Neno hilo italisoma katika ile habari ya Stefano alipokuwa anatumiwa na Mungu kufanya ishara na maajabu yasiyokuwa ya kawaida katika kanisa lake.
Lakini baadhi ya wayahudi wa masinagogi mbali mbali walipoliona hilo wakamchukua kuja kujadiliana naye, na baada ya kuona kuwa wameshindwa waliingiwa wivu na kufanya mambo ambayo huwezi kudhani dhehebu la dini linaweza kufanya. Sasa moja ya sinagogi hilo lilikuwa ndio hilo lililoitwa Sinagogi la Mahuru; kulikuwa na mengine pia tusome.
Matendo 6:8 Na Stefano, akijaa neema na uwezo, alikuwa akifanya maajabu na ishara kubwa katika watu. 9 Lakini baadhi ya watu wa sinagogi lililoitwa sinagogi la Mahuru, na la Wakirene, na la Waiskanderia, na la wale wa Kilikia na Asia, wakaondoka na kujadiliana na Stefano; 10 lakini hawakuweza kushindana na hiyo hekima na huyo Roho aliyesema naye. 11 Hata wakashawishi watu waliosema, Tumemsikia mtu huyu akinena maneno ya kumtukana Musa na Mungu. 12 Wakawataharakisha watu na wazee na waandishi, wakamwendea, wakamkamata, wakampeleka mbele ya baraza. 13 Wakasimamisha mashahidi wa uongo waliosema, Mtu huyu haachi kusema maneno ya kufuru juu ya mahali hapa patakatifu na juu ya torati;
Matendo 6:8 Na Stefano, akijaa neema na uwezo, alikuwa akifanya maajabu na ishara kubwa katika watu.
9 Lakini baadhi ya watu wa sinagogi lililoitwa sinagogi la Mahuru, na la Wakirene, na la Waiskanderia, na la wale wa Kilikia na Asia, wakaondoka na kujadiliana na Stefano;
10 lakini hawakuweza kushindana na hiyo hekima na huyo Roho aliyesema naye.
11 Hata wakashawishi watu waliosema, Tumemsikia mtu huyu akinena maneno ya kumtukana Musa na Mungu.
12 Wakawataharakisha watu na wazee na waandishi, wakamwendea, wakamkamata, wakampeleka mbele ya baraza.
13 Wakasimamisha mashahidi wa uongo waliosema, Mtu huyu haachi kusema maneno ya kufuru juu ya mahali hapa patakatifu na juu ya torati;
Sasa ni kwanini liitwe kwa jina hilo?
Biblia haijaeleza chochote kuhusu chimbuko la sinagogi hilo mpaka wakajiita hivyo, lakini inaaminiwa na baadhi ya wanazuoni kuwa kulikuwa na kundi la wayahudi ambao walikuwa ni watumwa wa dola ya Ki-Rumi, Na baadaye wakafanywa kuwa huru, na ndipo hapo wakawa na sinagogi lao, wakaliita Sinagogi la mahuru. Yaani sinagogi la watu waliofanywa kuwa huru.
Hivyo hata kama chimbuko la jina hilo lingekuwa ni tofauti na hiyo, lakini bado jina lake ni nzuri, “Mahuru”. Lakini shida inakuja ni pale ambapo mioyo yao haiakisi jina hilo. Ni wazi kuwa watu hawa hawakuwekwa huru moyoni, kwasababu kama wangewekwa huru wasingekuwa na wivu, na wasingemzushia Stefano habari za uongo. Hiyo ni kuonyesha kuwa walikuwa ni watu walio mbali na wokovu kuliko hata watu wasiomjua Mungu kabisa.
Tunajifunza nini?
Hatushangai hata sasa kuona yapo makanisa mengi, na mikusanyiko mingi, yenye majina mazuri ya rohoni, yenye misalaba mingi, yenye kila aina ya mapambo mazuri ya rohoni. Lakini ndani yake wanazipinga nguvu za Roho Mtakatifu kama walivyompinga Stefano.
Biblia ilishatabiri katika kitabu cha 1Timotheo 3 kuwa katika nyakati za mwisho watatokea watu wengi wa namna hiyo
2Timotheo 3:1 “Lakini ufahamu neno hili, ya kuwa siku za mwisho kutakuwako nyakati za hatari.
2 Maana watu watakuwa……….
5 wenye mfano wa utauwa, lakini wakikana nguvu zake; hao nao ujiepushe nao”.
Unaona watakuwa wenye mfano wa utauwa lakini wanazikana Mungu za Mungu.
Huu si wakati wa kujivunia dhehebu au dini ndugu, ni wakati wa kujivunia Kristo ndani yako. Unaweza ukawa na dhehebu zuri kweli, kubwa kweli, lakini Mungu amelikataa, wewe litakufaidia nini? Tunapaswa tuutafute utakatifu kwa bidii kwasababu hatuwezi kumwona Mungu tusipokuwa nao(Waebr 12:14).
Tunapaswa tujichunge tusifanane na hawa wa sinagogi la mahuru ambao wana jina zuri lakini ni wapinga-Kristo ndani yao.
Bwana atusaidie.
Mpumbavu ni nani katika biblia? (Zaburi 14:1, Mithali 10:14)
Nini Maana ya Hosana?
UFUNUO: Mlango wa 18
Introduction
In the heart of ancient Israel’s journey into the Promised Land lie two significant mountains: Mount Gerizim and Mount Ebal. Located in Samaria and facing each other directly, these two mountains were not just geographical landmarks but served as vivid illustrations of the covenant between God and His people. Through them, God presented the Israelites with a life-altering choice—blessing for obedience and curse for disobedience.
This symbolic moment reveals a deep theological truth: God’s covenant demands a response, and the results of that response echo through our lives, both physically and spiritually.
While still in the wilderness, Moses gave Israel a prophetic instruction from God. After crossing the Jordan River into Canaan, the Israelites were to hold a covenant-renewal ceremony at Mount Gerizim and Mount Ebal.
“And when the Lord your God brings you into the land that you are entering to take possession of it, you shall set the blessing on Mount Gerizim and the curse on Mount Ebal.”— Deuteronomy 11:29,
They were to build an altar (on Ebal), write the entire Law on large stones, and divide the tribes into two groups. Half of the tribes would stand on Mount Gerizim to pronounce blessings, while the other half would stand on Mount Ebal to declare curses. In the valley between stood the Levitical priests with the Ark of the Covenant, representing God’s presence and authority.
“And half of them shall stand on Mount Gerizim to bless the people, and half of them on Mount Ebal for the curse…”— Deuteronomy 27:12–13
Later, Joshua fulfilled this exact command after leading the Israelites across the Jordan:
“And all Israel, sojourner as well as native born, with their elders and officers and their judges, stood on opposite sides of the ark before the Levitical priests… Half of them in front of Mount Gerizim and half of them in front of Mount Ebal…”— Joshua 8:33
This dramatic gathering was a powerful reminder: God’s covenant involves both promise and responsibility.
“I call heaven and earth to witness against you today, that I have set before you life and death, blessing and curse. Therefore choose life…”— Deuteronomy 30:19
“For the law was given through Moses; grace and truth came through Jesus Christ.”— John 1:17
“Our fathers worshiped on this mountain, but you say that in Jerusalem is the place where people ought to worship.”— John 4:20
The Samaritans still honored Mount Gerizim as sacred. But Jesus responded with a revelation of New Covenant worship:
“The hour is coming when neither on this mountain nor in Jerusalem will you worship the Father… true worshipers will worship the Father in spirit and truth.”— John 4:21, 23
In Christ, physical locations give way to spiritual realities. True blessing is not tied to geography but to relationship with God through Jesus.
Even today, Mount Gerizim and Mount Ebal stand as spiritual metaphors. Every believer faces a similar choice: to walk in obedience and receive God’s blessings (Gerizim), or to reject His Word and suffer the spiritual consequences (Ebal).
God’s Word is clear—those who walk in His ways will experience the fruit of obedience:
“Blessed is the man who walks not in the counsel of the wicked… but his delight is in the law of the Lord.”— Psalm 1:1–2
But those who reject His truth will find themselves cut off from His blessing:
“But they refused to pay attention… therefore great wrath came from the Lord of hosts.”— Zechariah 7:11–12
Mount Gerizim and Mount Ebal are more than historical sites—they are enduring symbols of the choices we make daily in our walk with God. The Law, blessings, curses, sacrifice, and grace all intersect on those slopes. Through Christ, the curse is broken, and the blessing is fulfilled in those who believe and obey.
We now live not under the shadow of the Law, but in the reality of grace. Yet the principle remains: our lives are shaped by our response to God’s Word.
Will you choose the path of Gerizim or Ebal? The mountain of blessing or the mountain of judgment?
Adui yetu shetani, usiku na mchana anatafuta kutumeza, kama biblia inavyosema katika..1Petro 5:8 “ Mwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, kama simba angurumaye, huzungukazunguka, AKITAFUTA MTU AMMEZE”.
Hivyo anazo njia nyingi za kummeza mtu, na kila siku anabuni njia mpya…Lakini anayo moja maarufu anayoitumia ambayo ni ya MAWAZO. Anachofanya ni kupanda mbegu Fulani mbaya ndani ya mtu, ambayo hiyo mbegu inavyozidi kukuwa ndani yake inamletea kukata tamaa na mwisho kuanguka kabisa. Sasa yafuatayo ni baadhi ya Mawazo ambayo, ukiona yanakuja ndani yako, fahamu kuwa ni mawazo ambayo yamebuniwa na ibilisi, hivyo Yakatae na kuyapuuza.
Hii ni silaha moja maarufu ya adui shetani kwa watu wa Mungu. Anayatengeneza mawazo haya ndani ya mtu, na kumfanya aishiwe nguvu ya kuendelea kumtafuta Mungu na kuwa na amani.
Hivyo wazo lolote linalokuja ndani yako kwamba tayari umemkufuru Roho Mtakatifu, kwasababu pengine ulishawahi kusema maneno Fulani wakati Fulani, kuikejeli injili. Au ulifanya dhambi Fulani kubwa sana, ambayo haielezeki, au ulirudi nyuma baada ya wokovu wako, na sasa unataka kutubu uanze upya, Ukiona hilo wazo linakuja ndani yako, kukuambia kuwa ulishamkufuru Roho Mtakatifu, Fahamu kuwa hilo ni wazo la ibilisi asilimia 100, hivyo lipuuzie usilipe nafasi hata kidogo. Hakuna mwanadamu aliyemkufuru Roho Mtakatifu na bado ana hofu ya Mungu..Lakini usipolipuuzia hili wazo na kuendelea kukaa nalo moyoni, litazidi kukua na mwishowe litakufanya usiendelee kumtafuta Mungu, na litakufanya uwe unakosa amani na furaha kila wakati.
Hii ni silaha nyingine ya shetani, kuharibu watu wa Mungu..Ukiona upo kwenye hili tatizo kwamba unaona kama Mungu anakuchukia, hakupendi anawapenda tu baadhi ya watu Fulani, au watumishi wake..Jua tayari upo katika shambulizi la adui yako shetani, tayari upo katika anga zake anakuharibu kidogo kidogo.
Fahamu kuwa Mungu hamchukii mtu yeyote yule hata yule mwovu kuliko wote, ingekuwa anakuchukia sidhani kama angekuumba uishi katika hii dunia, mpaka umejiona umetokea kwenye hii dunia, jua ni kwaajili ya upendo wake kwako. Hivyo hilo wazo la kujiona hupendwi ni kutoka kwa adui.
Mungu anasikia maombi ya kila mwanadamu..kama kilio cha dhambi tu kinamfikia mbinguni, kwanini maombi yasimfikie?. Yanamfikia isipokuwa majibu ya maombi yanatofautiana mtu na mtu. Wapo ambao watapeleka maombi yao watajibiwa kama walivyoomba na wapo ambao hawatajibiwa, sasa wale ambao hawatajibiwa maombi yao, ipo sababu, na Mungu wa upendo atahakikisha wanaijua hiyo sababu kwa njia yeyote ile, ili warekebishe wapokee majibu ya maombi yao.. Kamwe hawezi kumwacha mtu yeyote hewani tu!, bila kumpa sababu ya kwanini hajapokea majibu ya maombi yake..Kinachowakwamisha wengi ni kukata tamaa kirahisi… Unapokata tamaa tayari umekatisha safari yako ya kupokea baraka zako ukiwa katikati.
Kwa mfano, mtu anaweza kwenda kumwomba Mungu naomba unipe mume bora, au mke bora..lakini ukimwangalia ni kahaba, hivyo Mungu mwema hawezi kumpa kitu kizuri kabla hajamtengeneza kwanza…Kwahiyo wakati anasubiria majibu ya maombi yake, Mungu anamletea mhubiri, ambaye atamhubiria wokovu, na njia bora ya kuishi Maisha ya kumpendeza Mungu, anapotii na kukubali kubadilika na kuacha njia zake mbaya..Mungu ndipo anamletea jibu la
maombi yake aliyomwomba, analetewa mwenzi mwema wa Maisha, ambaye hatamsumbua na aliye mcha Mungu kama yeye. Lakini kama hatatii bado anataka kuendelea kukaa na ukahaba wake ndio atakaa hivyo hivyo kwa muda mrefu mpaka siku atakapofunguka akili, atarudia kuomba yale yale maneno lakini hataona majibu…
Hizo tu ndizo sababu za Mungu kuchelewesha majibu, lakini si kwamba Mungu hasikii maombi… Anayasikia, isipokuwa katika ujibuji wake ndio suala lingine.
Hivyo ukikosa kujiamini na kufikiri Mungu hajawahi kusikia maombi unayoomba chumbani kwako, au barabarani unapotembea, au kazini unapofanyia kazi…basi jua umeshambuliwa rohoni na adui shetani. Kazana kujua kwanini hujapata majibu lakini usifikiri kwamba hujasikiwa kabisa. Tayari umeshasikiwa, na uliloliomba limeshafanyiwa kazi, wewe fuatilia ombi lako lipo katika hatua gani sasa.
Marko 11:24 “Kwa sababu hiyo nawaambia, Yo yote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu”.
Ndugu ukifikiri kwamba unaweza kufikia kiwango cha utakatifu kiasi kwamba huna kosa kabisa..basi fahamu kuwa hutaweza kamwe kumtumikia Mungu, kumbuka bado tunaishi duniani,
na lazima tutakuwa na kasoro nyingi, ambazo nyingi hatuzijui kama tunakosea…Sasa kama Mungu angezihesabu hizo biblia inasema hakuna mtu angesimama. Baada ya kuokoka ukiamka asubuhi usianze kukaa kuhesabu makosa yako, ukifanya hivyo kamwe hutaweza kumtumikia Mungu, na shetani atakusumbua sana na kila dakika atakuletea mawazo wewe ni mbaya, wewe hustahili, wewe hufai, wewe umeshamkosea Mungu, hufai, hufai n.k
Ukiamka asubuhi anza kuhesabu ni mazuri mangapi umemfanyia Mungu wako, na kama hujafanya kabisa ndipo uhuzunike, na tafuta kufanya, na jioni ukirudi..Mwambie Bwana asante kwa hichi kizuri ulichoniwezesha kukufanyia siku ya leo, na pia naomba nisamehe makosa yangu
yote niliyokukosea wewe pasipo kujua siku ya leo. Na kama unayakumbuka baadhi uliyoyafanya hakikisha kesho unayarekebisha, na ukishatubu tu usianze kujilaumu laumu!..Ukifanya hivyo utaruhusu mashambulizi ya shetani kukuvamia na kukuletea mawazo yale yale kwamba Mungu
alichukizwa na wewe jana, hivyo hawezi kuendelea kutembea na wewe leo…Kwahiyo siku zote Vaa ngao ya Imani, ili uweze kuizima hiyo mishale ya adui. Mungu wetu wa upendo hakai huko mbinguni na karatasi na kalamu akitiki mabaya tunayoyafanya baada ya sisi kuokoka…hafanyi hivyo, yeye yupo kutazama mema yetu, maadamu tumeshaokoka na
kumwamini na tumeweka mbali Maisha ya dhambi. Basi tunakuwa tunahesabiwa haki kwa Neema na si kwa matendo. Na hivyo kidogo kidogo anatutakasa mpaka unafika wakati tunakuwa wakamilifu kabisa kwake.
Hivyo hizo ni silaha 4 za adui yetu shetani. Sasa kama hizi Habari ni mpya kwako, na kama zimekufungua macho, basi ni dalili ya kwamba ulikuwa huna Ngao mkononi mwako, hivyo
ulimfungulia shetani nafasi ya kukushambulia ndio maana husongi mbele kiimani, na hiyo ni kutokana na kwamba pengine nafasi ya kutafuta kumjua Mungu Zaidi katika Maisha yako ni ndogo, au ulikuwa umesongwa na hivyo kulifahamu Neno imekuwa ngumu kwako, kwahiyo nakushauri mtu wa Mungu usiruhusu tena kusongwa..Neno hili wakristo wote waliofanikiwa ambao umeona wamesimama na hawapelekwi ni kwasababu, wana ngao za Imani mikononi
mwao, ni kwasababu Hivyo vipengele 4 hapo juu wamevishinda tangu zamani. Hivyo ni wewe peke yako umebaki.
Anza kumtafuta Mungu kwa bidii, anza kusoma Neno kwa bidii, usipitishe siku bila kushika biblia, na usomapo usisome kwa kutimiza wajibu, Ukilisoma Neno la Mungu na kulielewa ndivyo linavyokaa ndani yako, na linakupa Imani na maarifa, na ndivyo linavyokuweka huru, Ukilikosa hilo kamwe usitegemee kumshinda shetani, na wala kamwe usitegemee kama utaweza kumtumikia Mungu. Kwasababu shetani hawezi kuruhusu umtafute Mungu kirahisi rahisi hivyo, ni lazima akuletee hivyo vita vya kimawazo, akishinda hivyo atakuletea na vya nje, sasa ni wajibu wetu kufahamu kuwa tupo vitani. Ni lazima upambane kumjua Mungu.
Mathayo 11:12 “Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka”
jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312 / 0693036618
ESTA: Mlango wa 8, 9 & 10. (SIKU KUU YA PURIMU)
KWANINI LEO HII KUNA KUNDI KUBWA LA WAKRISTO WALIORUDI NYUMA?
NIMEOKOKA, ILA MUNGU NDIYE ANAYEJUA NITAKWENDA WAPI.
FAHAMU JINSI KRISTO ANAVYOPONYA WATU ROHO.
JE NI DHAMBI KUWA NA MAHUSIANO KABLA YA NDOA?
WhatsApp
Kabari ni nini?
Kabari ni ni kipande kikubwa cha kitu Fulani aidha mbao, chuma, dhahabu, shaba n.k.. (donge)
Katika biblia tunaona wana wa Israeli walipoingia nchi ya ahadi na kuwepo maagizo kuwa vitu vyote vya thamani watakavyovikuta kule vitatolewa wakfu kwa Bwana(Yoshua 6:19), lakini tunaona walipofika kulikuwa na mtu mmoja aliyeitwa Akani, mwana wa Karmi, huyu alipofika tu aliyeingiwa na tamaa, pale alipoona vitu vya thamani, ikiwemo hizi kabari (vipande) vya dhahabu, hakuvithaminisha kwa Bwana, bali alikwenda kuvificha(Yoshua 7:11).
Akasababisha mpaka taifa zima la Israeli kupigwa na kufadhaishwa mbele ya maadui zao. Hiyo ikawafanya wapepeleze tatizo ni nini, ndipo walipogundua kuwa ni huyu Akani ameficha baadhi ya vitu vya thamani walivyovikuta kule, hivyo wakamkamata na kumuua.
Yoshua 7:21 “Nilipoona katika nyara joho nzuri ya Babeli, na shekeli mia mbili za fedha, na kabari YA DHAHABU, uzani wake shekeli hamsini, basi nalivitamani nikavitwaa; tazama, vimefichwa mchangani katikati ya hema yangu, na ile fedha chini yake….. 24 Kisha Yoshua, na Israeli wote pamoja naye, wakamtwaa Akani, mwana wa Zera, na ile fedha, na Lile joho, na ile KABARI YA DHAHABU, na wanawe, na binti zake, na ng’ombe zake, na punda zake, na kondoo zake, na hema yake, na vitu vyote alivyokuwa navyo, wakavileta juu hata bonde la Akori”.
Yoshua 7:21 “Nilipoona katika nyara joho nzuri ya Babeli, na shekeli mia mbili za fedha, na kabari YA DHAHABU, uzani wake shekeli hamsini, basi nalivitamani nikavitwaa; tazama, vimefichwa mchangani katikati ya hema yangu, na ile fedha chini yake…..
24 Kisha Yoshua, na Israeli wote pamoja naye, wakamtwaa Akani, mwana wa Zera, na ile fedha, na Lile joho, na ile KABARI YA DHAHABU, na wanawe, na binti zake, na ng’ombe zake, na punda zake, na kondoo zake, na hema yake, na vitu vyote alivyokuwa navyo, wakavileta juu hata bonde la Akori”.
Hiyo inatufundisha nini? Inatufundisha kuwa tusiwe na tamaa ya mali ikiwa sisi ni watoto wa Mungu, kwani haitatugharimu maisha yetu tu, bali itagharimu kama sio kuathiri na maisha ya wengine pia. Na ndio maana biblia inasema,
1Timotheo 6:10 “Maana shina moja la mabaya ya kila namna ni kupenda fedha; ambayo wengine hali wakiitamani hiyo wamefarakana na Imani, na kujichoma kwa maumivu mengi”.
Bwana atusaidie, tupende kujikusanyia zaidi kabari za ufalme wa mbinguni kuliko hizi za hapa duniani..Kwani za hapa duniani ni za kitambo tu, lakini zile zinadumu milele.
Tazama tafsiri ya maneno mengine chini.
Mkatale ni nini katika biblia? (Matendo 16:24)
Daawa ni nini kama tunavyosoma katika biblia?
Kwanini Yesu Kristo ni mwana wa Adamu?
JIEPUSHE NA UNAJISI.
Kuna tofauti ya kumpa Mungu utukufu na kumshukuru Mungu. Mungu anapokufanyia jambo zuri, lakukupa faraja na furaha, na moyoni ukafurahi, ni kawaida ya kila mwanadamu mwenye moyo wa shukrani, huwa anakwenda kupiga magoti na kumshukuru Mungu wake kwa alilomtendea aualiyomtendea, na zaidi sana huwa anaambatanisha hata na sadaka yake ya shukrani.
Sasa hilo ni jambo moja ambalo linampendeza sana Mungu wetu, pale tunapomshukuru, lakini lipo lingine linalompendeza pia ambalo litatufungulia milango ya baraka mara mbili. Na jambo hilo si lingine zaidi ya KURUDI KUMPA MUNGU UTUKUFU.
Kurudi kumpa Mungu utukufu, ni kitendo cha kurudi na kutangaza kwa wazi, yale yote Mungu aliyokufanyia.. Hivyo Mungu wako anakuwa anatukuzwa katikati ya watu.
Ni jambo linalodharaulika na wengi lakini ni la umuhimu sana. Kurudi kumpa Mungu utukufu…Je umeshawahi kurudi kumpa Mungu utukufu kwa jambo lolote jema alilokufanyia?
Hebu tusome hichi kisa maarufu kwenye biblia..
Luka 17:11 “Ikawa walipokuwa njiani kwenda Yerusalemu, alikuwa akipita katikati ya Samaria naGalilaya. 12 Na alipoingia katika kijiji kimoja, alikutana na watu kumi wenye ukoma; wakasimama mbali, 13 wakapaza sauti wakisema, Ee Yesu, Bwana mkubwa, uturehemu! 14 Alipowaona aliwaambia, Enendeni, mkajionyeshe kwa makuhani. Ikawa walipokuwa wakiendawalitakasika. 15 Na mmoja wao alipoona kwamba amepona, alirudi, HUKU AKİMTUKUZA MUNGU KWA SAUTİ KUU; 16 akaanguka kifudifudi miguuni pake, akamshukuru; naye alikuwa Msamaria. 17 Yesu akajibu, akanena, Hawakutakaswa wote kumi? Wale kenda wa wapi? 18 JE! HAWAKUONEKANA WALİORUDİ KUMPA MUNGU UTUKUFU İLA MGENİ HUYU? 19 Akamwambia, Inuka, enenda zako, imani yako imekuokoa”
Luka 17:11 “Ikawa walipokuwa njiani kwenda Yerusalemu, alikuwa akipita katikati ya Samaria naGalilaya.
12 Na alipoingia katika kijiji kimoja, alikutana na watu kumi wenye ukoma; wakasimama mbali,
13 wakapaza sauti wakisema, Ee Yesu, Bwana mkubwa, uturehemu!
14 Alipowaona aliwaambia, Enendeni, mkajionyeshe kwa makuhani. Ikawa walipokuwa wakiendawalitakasika.
15 Na mmoja wao alipoona kwamba amepona, alirudi, HUKU AKİMTUKUZA MUNGU KWA SAUTİ KUU;
16 akaanguka kifudifudi miguuni pake, akamshukuru; naye alikuwa Msamaria.
17 Yesu akajibu, akanena, Hawakutakaswa wote kumi? Wale kenda wa wapi?
18 JE! HAWAKUONEKANA WALİORUDİ KUMPA MUNGU UTUKUFU İLA MGENİ HUYU?
19 Akamwambia, Inuka, enenda zako, imani yako imekuokoa”
Waliponywa wote kumi lakini ni huyu mmoja tu ndiye Aliyepaza sauti yake, kwa sauti kuu, akitangaza jinsi alivyoponywa njia nzima, mpaka alipofika kwa Bwana Yesu..Pengine wale 9 walikwenda kutoa sadaka zao za shukrani tu!..Lakini hawakumtukuza Mungu, walakutangaza waliyofanyiwa kwa wazi, kwasababu zao wenyewe, labda waliona aibu, au waliogopa kutengwa, au kuonekana wa kikale…Lakini huyu hakujali hayo, alitangaza kwa watu lililomtokea kuanzia mwanzo hadi mwisho..
Na hivyo likawa ni jambo jema mbele za Mungu..
Je na wewe ulishawahi kurudi kumpa Mungu utukufu?… Bwana alipokuponya ugonjwa ambao ilikuwa ni ngumu kupona, je! Ulishawahi kusimama na kutangazia watu wawili au watatu mambo makuu Mungu aliyokufanyia?..au uliishia kuwatukuza madaktari tu! Kwamba walikupambania lakini hukuwahi kumtaja Mungu maneno yasiyozidi mawili?..Kama ndivyo basi badilika leo.
Je ulishawahi kumpa Mungu utukufu kwa huyo mtoto uliyempata ambaye ulihangaika miaka mingi bila kupata mtoto?..Ni kweli pengine ulitoa sadaka ya shukrani, hiyo ni vizuri…lakini bado haitoshi…Mungu wako anapaswa atukuzwe mbele za watu kwa hicho alichokufanyia.. Inapaswa watu wamwonapo mwanao aliyekupa Mungu, wamfikirie Mungu wako na si daktari wako wala jitihada zako.
Nyumba Mungu aliyokupa, mali alizokupa, afya aliyokupa, uzima anaokupa, cheo alichokupa, elimu aliyokujalia, nguvu alizokupa n.k…Je Mungu wako anatukuzwa katika huo? Au jitihada zako?..Watu wanapaswa wakitazama cheo chako wanakumbuka ushuhuda uliowasimulia wa jinsi Mungu alivyokuweka pale kimiujiza, na sio wanakumbuka jinsi ulivyopambana…Watu wanapokuona leo umesimama ni mzima, wanapaswa wakumbuke ushuhuda uliowaambia jinsi ulivyokuwa hatiani kupona na ukamwomba Mungu na Mungu akakufungulia mlango wa uponyaji… ili Mungu wako atukuzwe kwao.
Watu wanapokuona una hiki au kile..wanapaswa wautafakari uzuri wa Mungu wako, na utukufu wake, kwa utukufu uliomrudishia wakati unavipata hivyo…kila kitu wajue ni Mungu kakusaidia na si nguvu zako.
Na hatumpi Mungu wetu utukufu kwa yale aliyotutendea kwa kuwawekea watesi wetu CD za mipasho!.. Kwasababu siku hizi zipo nyimbo za dini ambazo hazina tofauti na nyimbo za kidunia (Taarabu)..zimejaa maneno ya kiburi na ushindani. Kwamba Mungu kanitendea hichi ili maadui
zangu waone waumie moyo…Hapana! mpango wa Mungu sio maadui zetu waumie moyo na waone Mungu alichotufanyia halafu basi!. Mungu hatupiganii ili awachome watu mioyo, bali ili awageuze nia zao wamgeukie yeye.
Hivyo ukimpa Mungu utukufu mbele za watu, jinsi inavyopaswa, kwa kutangaza kwa kina ulipotoka na ulipo sasa, na jinsi gani Mungu alivyokuokoa, kwa neema…Wale wanaokusikiliza akili zao zitahama kutoka kushindana na wewe, na kuhamia kumtafakari Mungu wako, na hivyo nao pia wamtamtamani Mungu wako aliyekutendea mambo makuu namna hiyo. Na watakuuliza “nami nifanyaje Mungu anitendee kama alivyokutendea wewe”
Lakini ukianza kuwawekea mipasho, watakuchukia na hawatavutiwa na unachokiamini, hivyo utakuwa nawe pia unaifanya kazi ya ibilisi ya kuwapeleka watu mbali na Mungu, na moyoni ukidhani umemtukuza Mungu kwa nyimbo zako hizo za kiburi na majivuno kumbe ndio unaenda kinyume na mapenzi ya Mungu.
Hivyo Usiache kamwe kurudi kumpa Mungu utukufu kwa jambo lolote lile analokutendea, hata liwe dogo kiasi gani…Nenda kalitangaze kanisani, kalitangaze kwa rafiki zako, kalisimulie kwa ndugu, kalisimulie kwa yoyote yule ambaye utapata nafasi ya kumsimulia..hakikisha tu lengo lako ni Mungu atukuzwe na si wewe utukuzwe, au kujisifu.
JE KUNA UISLAMU KATIKA BIBLIA?
Mavu ni nini katika biblia?(Kutoka 23:28, Kumb 7:20)
CHAPA YA MNYAMA
WINGU KUBWA LA MASHAHIDI.
BABA YANGU ANATENDA KAZI HATA SASA!.