Category Archive Uncategorized @sw-tz

WEWE NI BWANA UNIPONYAYE.

SALA FUPI YA UPONYAJI!

Zaburi 107:17 “Wapumbavu, kwa sababu ya ukosaji wao, Na kwa sababu ya maovu yao, hujitesa.
18 Nafsi zao zachukia kila namna ya chakula, Wameyakaribia malango ya mauti.
19 Wakamlilia Bwana katika dhiki zao, Akawaponya na shida zao.
20 Hulituma neno lake, huwaponya, Huwatoa katika maangamizo yao”.

(Uimbe wimbo huu uliotungwa na Don Moen, kufuatia Zaburi hiyo)

Mimi ni Mungu nikuponyaye,
Mimi ni Bwana mponyaji wako,
Hulituma Neno langu,
Na kukuponya magonjwa yako,
Mimi ni Bwana mponyaji wako.

Wewe ni Mungu,
Uniponyaye,
Wewe ni Bwana Mponyaji wangu,
Hulituma Neno lako,
Na kuniponya magonjwa yangu,
Wewe ni Bwana mponyaji wangu.

Urudie kwa kadri uwezavyo pale Upitiapo misiba, magonjwa na shida..mwambie “Mungu” wewe ni Bwana uniponyaye,.. wewe ni Bwana uniponyaye..wewe ni Bwana mponyaji. Na nguvu uponyaji utashuka juu yako, na kukuponya na magonjwa uliyonayo  au misiba unayopitia.

“Amen”


Mada Nyinginezo:

UPONYAJI WA YESU.

KWA KUPIGWA KWAKE SISI TUMEPONA.

NJIA SAHIHI YA KUMPATA MWENZA WA MAISHA KIBIBLIA.

UFALME WAKO UJE.

JIFUNZE KUJITOA KWA MUNGU NA KUWA MKARIBISHAJI.

Rudi Nyumbani:

Print this post

KITABU CHA UCHAWI.

Kabla ya kutafuta kitabu cha uchawi ni vizuri kufahamu kwanza Uchawi asili yake ni wapi.

Wapo watu wengi mitandaoni, wengine ni wachawi kweli, na wengine ni matapeli, wameandika vitabu wanakuambia ununue, na katika vitabu hivyo, wanaorodhesha njia mbalimbali za kutatua matatizo yako, au njia za kuwapiga maadui zao.. Lakini kabla hujafikiria kuungana nao ndugu yangu, ni vizuri kwanza ukafahamu uchawi asili yake ni wapi?

Uchawi ni kitendo cha kwenda kutafuta msaada kutoka katika mamlaka mengine tofuati na yale ya Mungu  ili kutimiziwa malengo Fulani, ya mwilini au rohoni. Na kama tunavyofahamu hakuna mamlaka mengine yaliyo tofauti na Mungu zaidi ya yale ya shetani.

Kwamfano, unapokuwa na uhitaji labda wa mke, na unaona kwa akili zako huwezi kumpata mwanamke umtakaye, hapo inakugharimu kutafuta msaada kutoka katika mamlaka nyingine..

Ndio hapo yanazuka mambo mawili, aidha uende kwa Mungu, au uende kwa shetani, ukienda kwa shetani utapata maagizo Fulani, yanatoka katika kitabu cha kichawi walichonacho, Vivyo hivyo ukienda kwa Mungu utapokea maagizo kutokana na kitabu kitakatifu cha Mungu kiitwacho BIBLIA.

Lakini jambo ambalo watu wengi hawajui ni kuwa, shetani hana lengo lolote zuri  na mwanadamu zaidi ya kumwangamiza, atakupa kwa lengo la kukuangamiza mwisho wa siku, na ukishakufa ni moja kwa moja unakwenda katika moto wa milele..

Zipo shuhuda nyingi za watu waliokwenda kwa waganga, kutafuta msaada wa shetani, lakini mwisho wake wameishia pabaya sana.. Na kibaya zaidi ulimwengu huu wa sasa, watu wengi wanakimbilia humo hawajui kuwa lile ni shimo kubwa sana la mauti..Ambalo ukiingia kutoka huko ni kugumu sana.

Usihatarishe maisha yako, kwa mambo ambayo hayakupeleki popote, Usije ukasema haujaambiwa, kukutana na ujumbe huu ni makusudi kabisa Mungu anakuonya, ikiwa wewe ni mmojawapo unayetafuta kujui kitabu cha uchawi, hizi ni siku za mwisho, biblia inasema hivi..

1Timotheo 4:1 “Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani;”

Unaona, biblia inasema wengi watajitenga na Imani na kusikiliza mafundisho ya mashetani,..Kumbuka Uchawi wa kwanza kabisa ulifanywa na Shetani pale Edeni, Ukitaka kujua uchawi wenyewe ni upi na madhara gani yalitokea baada ya pale..fungua hapa usome..>>>> JINSI WATU WANAVYOZAMA KATIKA USHIRIKINA NA UCHAWI.

Na ndio maana hata katika Israeli Mungu alipiga kabisa marufu watu wanaofanya uchawi, kwasababu alijua madhara yake kwao.

Kumbukumbu 18:9 “Utakapokwisha kuingia katika nchi akupayo Bwana, Mungu wako usijifunze kutenda kwa mfano wa machukizo ya mataifa yale.
10 Asionekane kwako mtu ampitishaye mwanawe au binti yake kati ya moto, wala asionekane mtu atazamaye bao, wala mtu atazamaye nyakati mbaya, wala mwenye kubashiri, wala msihiri,
11 wala mtu alogaye kwa kupiga mafundo, wala mtu apandishaye pepo, wala mchawi, wala mtu awaombaye wafu.
12 Kwa maana mtu atendaye hayo ni chukizo kwa Bwana; kisha ni kwa sababu ya hayo Bwana, Mungu wako, anawafukuza mbele yako.
13 Uwe mkamilifu kwa Bwana, Mungu wako”.

Hivyo ndugu, usifirie kutafuta eti hicho kinachoitwa kitabu cha uchawi, Ni heri utubu dhambi zako leo umgeukie YESU KRISTO, haijalishi wewe utakuwa ni muislamu, au mhindu, vyovyote vile, ukimpa Yesu maisha yako leo atakuokoa na kukupa uzima wa milele. Na atakupa pia vile vitu ambavyo ulikuwa na haja navyo kwa wakati wake.

Hivyo kama upo tayari leo kufanya hivyo, na unahitaji kuyakabidhi maisha yako kwake, basi fungua hapa kwa ajili ya sala ya Toba na Mungu akubariki..>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA

Pia unaweza pia kufungua na masomo mengine hapa chini ujifunze, naamini yatakutoa sehemu moja hadi nyingine kiroho.

Mada Nyinginezo:

 

Rudi Nyumbani:

Print this post

Neno la Mungu ni upanga.

Ni kwa namna gani Neno la Mungu ni upanga?


Biblia haisemi Neno la Mungu ni upanga tu, hapana bali inasema  ni zaidi ya upanga wowote mkali ukatao kuwili..

Waebrania 4:12 “Maana Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo.

13 Wala hakuna kiumbe kisichokuwa wazi mbele zake, lakini vitu vyote vi utupu na kufunuliwa machoni pake yeye aliye na mambo yetu.”.

Unaona? Ni zaidi ya upanga. Na kama tunavyojua upanga unaokata kuwili ni upanga ambao unatumika sana sana katika vita, yaani ukiupeleka upande wa kulia unakata na vilevile ukiurudisha upande wa kushoto bado unakata(Ufunuo 1:16, 2:12, 19:12).. Ni mfano wa msimeno unakata mbele na nyuma.

Sasa Mungu anakuambia Neno lake ni zaidi ya huo upanga. Akiwa na maana kuwa linakata pande zote, kwa wale wote watakaokwenda kinyume nalo, linakata matajiri, linakata maskini, linakata wenye vyeo linakata wasio na vyeo, linakata weupe, linakata weusi, linakata wenye dhambi vilevile linakata na waliookoka ikiwa hawatadumu katika maagizo yake.

Na kukata kwake sio butu, bali kwa ukali sana, likipita linatenganisha kabisa kabisa, yaani mfano Mungu akipitisha upanga katika taifa basi ujue taifa hilo ndio mwisho wake umefika, akipitisha upanga katika familia basi ujue ni upanga kweli kweli unaotenganisha, haijalishi  ndugu hao watakuwa wanapendana au wameshikamana kiasi gani.Soma.

Mathayo 10:34 “Msidhani ya kuwa nimekuja kuleta amani duniani; la! Sikuja kuleta amani, bali upanga.

35 Kwa maana nalikuja kumfitini mtu na babaye, na binti na mamaye, na mkwe na mkwe mtu;

36 na adui za mtu ni wale wa nyumbani mwake”.

Vilevile alisema, katika wakati wa Mwisho atayaangamiza mataifa kwa Neno lake, ambao ndio huo upanga utokao katika kinywa chake..

Ufunuo 19:14 “Na majeshi yaliyo mbinguni wakamfuata, wamepanda farasi weupe na kuvikwa kitani nzuri, nyeupe, safi.

15 Na upanga mkali hutoka kinywani mwake ili awapige mataifa kwa huo. Naye atawachunga kwa fimbo ya chuma, naye anakanyaga shinikizo la mvinyo ya ghadhabu ya hasira ya Mungu Mwenyezi.

16 Naye ana jina limeandikwa katika vazi lake na paja lake, MFALME WA WAFALME, NA Bwana WA MABwana”.

Hivyo, Mungu anatuasa tutubu, tumgeukie yeye, ili kusudi kwamba Neno lake, liwe chakula na uzima kweli badala ya upanga, Kwasababu kwa kupitia hilo hilo Mungu alifanya mbingu na nchi, kwa kupitia hilo hilo, alituumba sisi, kwa kupitia hilo hilo alinatuponya na kutuokoa, na kutubariki. Lakini kwa kupita hilo hilo atatuhukumu kama tusipotaka kuitii injili. Na ndio anatuhimiza mpaka sasa tutubu kwa kurudi kwake kumekaribia.

Ufunuo 2.16 Basi tubu; na usipotubu, naja kwako upesi, nami nitafanya vita juu yao kwa huo upanga wa kinywa changu.

Neno la Mungu ni upanga.

Shalom.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

USIPOLITENDEA KAZI NENO LA MUNGU.

UTASIMAMA PEKE YAKO SIKU ILE.

MAPAMBANO DHIDI YA SHETANI.

KWANINI TUNAPASWA TUJIZUIE?

MAPIGO YA VITASA SABA, NA SIKU YA BWANA.

UTAWALA WA MIAKA 1000.

ROHO ZILIZO CHINI YA MADHABAHU:

Rudi Nyumbani:

Print this post

Neno la Mungu la leo.

Neno la Mungu la leo ni lipi?


Kwanza nakupongeza kwa kupenda kutafuta kujua Neno la Mungu la leo..

Bwana Yesu alisema kila atafutaye huona (Mathayo 7:8), Hivyo kwa kuwa na wewe umetafuta kujua Neno la Mungu la leo kwako, basi ni hakika kuwa lipo jambo jipya Mungu atakufundisha.

Sio kwa bahati mbaya umefika mahali hapa.,

Paulo alimwambia Timotheo.

1Timotheo 4:13 “Hata nitakapokuja, ufanye bidii katika kusoma…..”

Unaona ni jukumu la kila mmoja wetu kuonyesha bidii katika kusoma(kujifunza) Neno la Mungu.

Wewe unaonyesha bidii hiyo  hivyo, usiache kupitia somo hili mpaka mwisho, lipo ambalo Mungu amekuandalia leo..

Lakini kabla hatujaendelea unaweza kufungua hapa  uingie katika horodha ya masomo ya kujifunza yaliyotangulia zaidi ya 1000, pamoja na maswali na majibu ..

>>> MAFUNDISHO MAPYA.


Leo tutajifunza nini maana ya Upendo na je! kuna aina ngapi za upendo?

Upendo ni kitendo cha kuonyesha hisia za tofauti za ndani kwa mtu mwingine, Ni hisia zinazoonyesha matokeo chanya, aidha umeridhishwa na mtu huyo, au umemkubali, au umemuhurumia, au unataka kumkaribia uwe karibu naye.

Kuna aina kuu tatu za upendo.

  1. Upendo unaotokana na Hisia, (Eros), Mfano wa upendo huu ni mke na mume. Sulemani aliutaja upendo huu sana katika kitabu cha Wimbo ulio bora (Wimbo 1:13-17)
  2. Upendo unatokana na  mahusiano mtu mmoja aliyo nayo kwa mwingine.(Phileo). Kwamfano unaweza ukawa unampenda mtu kutokana na kwamba ni mchezaji mwezako, au mfanyakazi mwenzako, au mkristo mwenzako, au mwanafunzi mwenzako n.k. mazingira yakishawatawanyisha, au itikidi zikitofautiana basi Upendo huu unakufa.
  3. Upendo wa ki-Mungu (Agape). Upendo huu ndio Upendo mkuu kuliko yote, Ni upendo usiokuwa na Masharti, Ni upendo ambao mtu anakupenda sio kwasababu ulimfanyia hiki au kile, au kwasababu unaendana naye kitu Fulani, hapana..Ni upendo usiohesabu mazuri wala mabaya kama kigezo cha kukupenda, ..

Upendo huu ndio ule ambao Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa mwanawe wa pekee ili kila mtu amwaminiye asipotee bali awe na uzima wa milele (Yohana 3:16).

 Na Upendo aliokuwa nao Yesu, ukamfanya mpaka auote uhai wake kwa ajili yetu sisi wenye dhambi. Upendo wa namna hii ukiwa nao basi ujue kuwa Upo karibu na Mungu sana kuliko mwanadamu mwingine yeyote duniani.

Na unamjua Mungu, zaidi mwanadamu mwingine yoyote duniani haijalishi atasema anaona maono, au ana mafunuo mengi kiasi gani..

1Yohana 4:7 “Wapenzi, na mpendane; kwa kuwa pendo latoka kwa Mungu, na kila apendaye amezaliwa na Mungu, naye anamjua Mungu.

8 Yeye asiyependa, hakumjua Mungu, kwa maana Mungu ni upendo”.

Tabia za upendo huu unaweza kuzisoma katika kitabu cha 1Wakorintho 13:4-8

Kwa urefu wa maelezo haya juu ya aina hizi za upendo fungua hapa usome..>> UPENDO

Hivyo hiyo yote ni kuonyesha jinsi gani Mungu anatupenda na kutujali, Hivyo kama wewe ni mwenye dhambi ujue kuwa Mungu anakupenda bado na hivyo hataki upotee, uende kuzimu, mgeukie leo akuoshe dhambi zako. Ili ukaurithi uzima wa milele aliotuandalia. Hilo ndilo Neno la Mungu la leo.

Shalom.

Tazama vichwa vingine vya masomo chini, kwa maarifa zaidi ya kiroho.

Mada Nyinginezo:

RABI, UNAKAA WAPI?

KWANINI YESU ALIMUITA BABA YAKE “ABA”?

MANENO ALIYOWEZA KUTAMKA YESU TU PEKE YAKE.

SAMEHE KUTOKA NDANI YA MOYO WAKO.

WAFALME WATOKAO MAWIO YA JUA.

UNYAKUO.

Rudi Nyumbani:

Print this post

NENO LA MUNGU NI NINI?.

Neno la Mungu ni nini?


Neno la Mungu ni ujumbe kutoka kwa Mungu, au mkusanyiko wa jumbe kutoka kwake. Ukisoma katika maandiko utaona mara nyingi manabii walikuwa wanasema maneno haya “Neno la Bwana linakanijia kusema”..Soma (Yeremia 1:11, Yeremia 13:3, 1Nyakati 22:8)

Wakiwa na maana ujumbe wa Mungu umenifikia kuwaambia. Hivyo biblia kwa ujumla inajulikana kama  Neno la Mungu.

Lakini pia Neno la Mungu ni jina la YESU KRISTO.

Ukisoma..

Yohana 1:1 “Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu.

2 Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu.

3 Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika.

4 Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu….

14 Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli”.

Neno la Mungu ni nini?

Kwanini YESU aitwe Neno?

Anaitwa Neno Kwasababu yeye ndiye kinywa chote cha Mungu,(Yohana 8:38), Yeye ndio wazo lote la Mungu, yeye ndiye utimilifu wote wa Mungu kwa jinsi ya mwili (Wakolosai 2:9)..Yeye ndiye aliyepewa hukumu yote na Mungu, na yeye ndiye aliyepewa milki ya vitu vyote..

Hivyo chochote afanyacho, chochote asemacho, ni sauti ya Mungu kweli, na ujumbe wa Mungu kweli kweli kwetu..

Na ndio maana utamsoma katika Ufunuo akijitambulisha kwa jina hilo.

Ufunuo 19:12 “Na macho yake yalikuwa kama mwali wa moto, na juu ya kichwa chake vilemba vingi; naye ana jina lililoandikwa, asilolijua mtu ila yeye mwenyewe.

13 Naye amevikwa vazi lililochovywa katika damu, na jina lake aitwa, Neno la Mungu.

14 Na majeshi yaliyo mbinguni wakamfuata, wamepanda farasi weupe na kuvikwa kitani nzuri, nyeupe, safi”.

Hivyo ukiyashika maneno ya Yesu, basi umelishika Neno la Mungu, ukiyashika maagizo ya Yesu basi umeyashika maagizo yake…Naamini umeshafahamu sasa Neno la Mungu ni nini!

Bwana akubariki.

Je! Unatambua kuwa tunaishi katika siku za mwisho? Je! Una habari kuwa hili ndio kanisa la mwisho lijulikanalo kama Laodikia, na kwamba hatutakuwa na kanisa lingine zaidi ya hili,.Pengine kizazi chetu zitashuhudia tukio la ujio wa pili wa Kristo? Dalili zote zinaonyesha, Kama ni hivyo Je! Umejiwekaje tayari?..Bado upo kwenye dhambi?

Ikiwa utahitaji kumpa Yesu maisha yako leo basi uamuzi utakaoufanya ni wa busara sana, hivyo fungua hapa kwa ajili ya sala ya toba..>>>

Maran Atha.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

KWANINI YESU KRISTO ALIKUJA DUNIANI?

JINA LA MUNGU NI LIPI?

NITAFUNGUAJE MILANGO ILIYOFUNGWA MBELE YANGU?

USITOKE NJE YA HIFADHI YA MUNGU.

HUYU SI YULE SEREMALA, MWANA WA MARIAMU?

DHIKI KUU INAKUJA NA UNYAKUO UPO KARIBU.

Rudi Nyumbani:

Print this post

YESU AKALIA KWA SAUTI KUU.

Yesu akalia kwa sauti kuu..


Wengi tunajiuliza ni maneno gani aliyatoa Bwana Yesu pale msalabani alipolia kwa sauti ya juu namna hiyo?

Embu tusome vifungu vyenyewe;

Marko 15:34 “Na saa tisa Yesu akapaza sauti yake kwa nguvu, Eloi, Eloi, lama sabakthani? Maana yake, Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?

35 Na baadhi yao waliosimama pale, walisema, Tazama, anamwita Eliya.

36 Na mmoja akaenda mbio, akajaza sifongo siki, akaitia juu ya mwanzi, akamnywesha, akisema, Acheni, na tuone kwamba Eliya anakuja kumtelemsha.

37 NAYE YESU AKATOA SAUTI KUU, AKAKATA ROHO.

38 Pazia la hekalu likapasuka vipande viwili toka juu hata chini.

39 Basi yule akida, aliyesimama hapo akimwelekea, alipoona ya kuwa alikata roho jinsi hii, akasema, Hakika mtu huyu alikuwa Mwana wa Mungu”.

Ili kujua ni  maneno gani aliyasema, ni vizuri tukaangalia katika vitabu vingine vya injili vinasema katika wakati huo huo alipokuwa anakaribia kukata roho Tusome..

Yohana 19:28 “Baada ya hayo Yesu, hali akijua ya kuwa yote yamekwisha kumalizika ili andiko litimizwe, akasema, Naona kiu.

29 Kulikuwako huko chombo kimejaa siki; basi wakatia sifongo iliyojaa siki juu ya ufito wa hisopo, wakampelekea kinywani.

30 Basi Yesu alipokwisha kuipokea ile siki, alisema, IMEKWISHA. Akainama kichwa, akaisalimu roho yake.”.

Unaona hapo mstari wa 30 unaonyesha dakika ile ya mwisho kabla ya kuikata roho yake alisema haya maneno “IMEKWISHA”..

Maneno haya hakuyasema kwa unyonge, au kwa utaratibu, au kwa sauti ya kawaida kama yale mengine..Hapana, bali alipofika hapo biblia inasema AKATOA SAUTI KUU.. IMEKWISHA.

Sauti ambayo kila mmoja aliyekuwa maeneo yale aliyasikia maneno haya..kiasi kwamba Yule akida wa askari alipoona jinsi alivyokata roho kwa Tamko zito kama lile..Akakiri kuwa Yule alikuwa kweli ni mwana wa Mungu.

Yesu akalia kwa sauti kuu,

Lakini kwanini Bwana Yesu aamue kufanya vile?,

Ilikuwa ni kutuambia mimi na wewe kuwa Ile hati ya mashitaka imekwisha. Na ndio maana saa ile ile pazia la hekalu likapasuka, na kiti cha rehema kikaonekana, ikiwa na maana kuwa tangu wakati wa Kristo kufa,  rehema inapatikana bure, na kwa uwazi, sio tena nyuma ya pazia ambapo ilihitaji kuwepo na mtu wa kuwapatanisha na Mungu(Kuhani mkuu)..Lakini sasa hilo halipo tena, kwasababu hati ya mashitaka imeondolewa.

Mtu yeyote anaweza kumkaribia Mungu na kusamehewa kupitia YESU KRISTO.

Hivyo hata na wewe leo, kama ni mwenye dhambi unaweza kuupokea msamaha kutoka kwake hapo hapo ulipo. Yesu anaweza kuja ndani ya moyo wako siku hii hii ya leo, bila hata ya kuhani kuwepo karibu yako, au mchungaji, au mtu yeyote..Ni wewe tu kufungua moyo wako, na kukubali kumpokea Yesu.

Ikidhamiria kufanya hivyo alisema mwenyewe..

Yohana 6:37 “Wote anipao Baba watakuja kwangu; wala ye yote ajaye kwangu sitamtupa nje kamwe.”

Hivyo leo hii ukimpa maisha yako utaanza kuona badiliko la ajabu sana ndani yako. Kama upo tayari sasa kutubu dhambi zako..Basi fungua hapa kwa ajili ya sala ya toba. >>> KUONGOZWA SALA YA TOBA

Mada Nyinginezo:

Kwanini Bwana Yesu alisema pale msalabani naona kiu?

USO WAKE ULIKUWA UMEHARIBIWA SANA ZAIDI YA MTU YE YOTE.

KWANINI YESU KRISTO NI WA MUHIMU KWETU SASA?

WINGU KUBWA LA MASHAHIDI.

MKUU WA UZIMA AKUWEKE HURU.

Rudi Nyumbani:

Print this post

Kuzimu kuna nini?

Kuzimu kuna nini?


Kuzimu sio mahali pa kupatamani hata kidogo, wala sio mahali ambapo utatamani hata adui yako aingie..

Na ndio maana Bwana Yesu alisema maneno haya..

Marko 9:43  “Na mkono wako ukikukosesha, ukate; ni afadhali kuingia katika uzima u kigutu, kuliko kuwa na mikono miwili, na kwenda zako jehanum, kwenye moto usiozimika;

44  ambamo humo funza wao hafi, wala moto hauzimiki.]

45  Na mguu wako ukikukosesha, ukate; ni afadhali kuingia katika uzima, u kiwete, kuliko kuwa na miguu miwili, na kutupwa katika jehanum;

[ 46  ambamo humo funza wao hafi, wala moto hauzimiki.]

47  Na jicho lako likikukosesha, ling’oe, ulitupe; ni afadhali kuingia katika ufalme wa Mungu, una chongo, kuliko kuwa na macho mawili, na kutupwa katika jehanum;

48  ambamo humo funza wao hafi, wala moto hauzimiki”.

Unaona, akiwa na maana kuwa kama itabidi kiungo chako kimoja tu cha thamani, kiondoke ni heri ukafanya hivyo kuliko uende kuishia huko milele.

Ikiwa unataka kujua kwa Urefu Jehanum ni nini? Unataka kujua hao funza wanamaanisha nini?, kuzimu kuna nini ,fungua hapa usome Habari yao.. >>>> Jehanamu ni nini?

Haya Maisha tuliyopewa ni ya kitambo kifupi sana, tunapaswa tujitathimini tukifa leo tutakwenda wapi ikiwa tupo nje ya Kristo? Biblia inatuambia Kuzimu haishibi watu, wala uharibifu hauna kifuniko, ikiwa na maana kuwa kila dakika, kila sekunde watu wanashuka huko wengi sana..

Lakini kwanini hayo yote yatukute angali bado tunao muda wa kutubu? Tutubu dhambi zetu, na kuyasalimisha Maisha yetu kwake, tuseme ulimwengu sasa basi, leo hii tunamgeukia Kristo.

Hivyo Ikiwa wewe ni mmojawapo ambaye unasema leo nipo tayari kumpa Yesu Maisha yangu, basi uamuzi unaoufanya ni wa busara sana.

Basi, hapo ulipo, chukua muda mchache ujitenge peke yako. Kisha piga magoti, kisha fuatisha sala hii kwa Imani, ukijua kuwa Mungu yupo hapo karibu na wewe pembeni yako kukusikia..Kisha ukiwa sasa katika utulivu Sema sala hii kwa sauti.

EE MUNGU BABA, NAJA MBELE ZAKO, NIKIWA NINAJITAMBUA KUWA MIMI NI MKOSAJI NA NIMEKUTENDA DHAMBI NYINGI, NA KWAMBA NIMESTAHILI HUKUMU. LAKINI WEWE MUNGU WANGU ULISEMA KATIKA NENO LAKO KUWA WEWE NI MUNGU WA REHEMA UNAYEWAREHEMU  MAELFU ELFU YA WATU WANAOKUPENDA WEWE. NA LEO HII NINAKUJA MBELE ZAKO NAHITAJI MSAMAHA WAKO NA MSAADA WAKO MUNGU WANGU, NINATUBU DHAMBI ZANGU ZOTE KWA KUMAANISHA NA KWA MOYO WANGU WOTE, NINAKIRI KUWA YESU KRISTO NI BWANA, NA YEYE NDIYE MWOKOZI WA HUU ULIMWENGUNI. HIVYO NAOMBA DAMU YA MWANAO TAKATIFU INISAFISHE UOVU WANGU WOTE SASA NIFANYIKE KUWA KIUMBE KIPYA KUANZIA LEO NA HATA MILELE.

ASANTE BWANA YESU KWA KUNIPOKEA NA KUNISAMEHE.

AMEN.

Sasa ikiwa umefuatisha sala hiyo kwa Imani ..Hatua iliyobakia kwako ni kuithitisha toba yako kwa Vitendo ikiwa ulikuwa unafanya mambo yote ambayo hayampendezi Mungu unayaacha na kujitenga nayo, Sasa Mungu akishaona umegeuka kwa vitendo basi toba yako anaipokea na atakuwa na uhalali kwa kuja ndani yako wakati huo huo na kufanya makao ya milele kwako.

Vile vile unahitaji, kutafuta kanisa la kiroho ambalo utajumuika na wakristo wengine katika kumwabudu Mungu, na kujifunza biblia ili uukulie wokovu. Na vilevile ili upate ubatizo sahihi wa kuzamishwa katika maji mengi na kwa jina la YESU KRISTO kwa ajili ya ondoleo la dhambi zako.

Hongera kwa kuokoka.

Pia nakualika kutembelea tovuti hii mara kwa mara, yapo mafundisho mengi zaidi ya 1000, na maswali mengi sana yaliyojibiwa ya kwenye biblia..

Au kama utakuwa unapenda utumiwe kwa njia ya whatsapp basi utatumia ujumbe katika namba hii +255789001312 .. Bwana akubariki sana.

Mada Nyinginezo:

MADHARA YA KUKOSA MAJI YA UZIMA BAADA YA KIFO.

DHIKI KUU INAKUJA NA UNYAKUO UPO KARIBU.

CHUKIZO LA UHARIBIFU

MAPIGO YA VITASA SABA, NA SIKU YA BWANA.

UTAWALA WA MIAKA 1000.

HAPO NDIPO WATU WALIPOANZA KULIITIA JINA LA BWANA.

Rudi Nyumbani

Print this post

Kuota upo na mtu maarufu/kuota unaongea na mtu maarufu.

Kuota upo mtu na maarufu/kuota unaongea na mtu maarufu kuna maana gani?

Ndoto zipo katika makundi makuu matatu, zipo ndoto zinazotokana na Mungu, pia zipo ndoto zinazotokana na shetani, halikadhalika zipo ndoto zinazotokana na mtu mwenyewe.

Ili kufahamu vizuri juu ya makundi haya. Bofya hapa usome. >>> Nitajuaje kama ndoto ni ya Mungu au ya Shetani?

Wengi wetu tunakosa shabaha pale tunapotaka kila ndoto ipatiwe tayari yake ya rohoni, lakini ukweli ni kwamba si kila ndoto inayotafsiri ya maana, husususani hizo zinazotokana na sisi wenyewe.

Sasa tukirudi kwenye swali Kuota upo na mtu maarufu/kuota unaongea na mtu maarufu kuna maana gani?

Jibu ni kwamba, ndoto nyingi za namna hii zinatokana na shughuli zetu za kila siku

Mhubiri 5:3 “Kwa maana ndoto huja kwa sababu ya shughuli nyingi; na sauti ya mpumbavu kwa njia ya wingi wa maneno”

Unaona Shughuli za kila siku ni Pamoja na yale mambo ambayo tunayoana mara kwa mara kila siku, au tunayasikia, kwamfano mtu kama raisi wa nchi, huyu ni mtu ambaye karibu kila siku tunamwona katika vyombo vya Habari, au tunamsikia katika radio, au tunamsoma katika magazeti, au tunamsikia akizungumziwa na watu wengine..

Ni mtu ambaye kila mmoja wetu amemkaa kichwani, kama vile tu ndugu zetu wa nyumbani. Hivyo mtu kuota raisi wa nchi, au kuota unaongea na raisi,au kuota uko na raisi si jambo la kushangaza.

Naamini ni maelfu ya watu kila siku yanamuota raisi wa nchi yao.

Na sio raisi tu, unaweza kumwota mtu mwingine yoyote maarufu, ambaye tayari anajulikana sana katika jamii, inaweza ikawa ni msanii, au mbunge, au mchungaji, au mchezaji n.k.

Hivyo ndoto ya namna hii, ikikujia usiitilie maanani sana.

Lakini ikija katika uzito wa hali ya juu, na ndoto yenyewe umeiota imeonekana kama ilikuwa ni kweli. Na ukaona kama ni bahati umekutana na mtu huyo,

Basi ujue ni Mungu anataka kukupa hisia  Fulani ya kipekee uionje pale unapokutana na mtu Fulani maarufu. Anataka uone, jinsi inavyokuwa,  ikiwa watu maarufu wa dunia hii ukikutana nao unajihisi wewe ni mtu Fulani spesheli uliyepata bahati, vipi kuhusu kukutana na yeye ambaye ni Maarufu na Mkuu kuliko watu wote na vitu vyote duniani siku ile? Utakuwa katika hali gani?

Anataka uone siku ile maelfu kwa maelfu wa watu watakapo kusanyika mbele zake , kupokea heshima zao kutoka kwake wewe utakuwa wapi?

Je! atakuita, uwe karibu naye, au atakukataa na kukufukuza?

Bwana Yesu mwenyewe alisema..

Luka 9:26  “Kwa sababu kila atakayenionea haya mimi na maneno yangu, Mwana wa Adamu atamwonea haya mtu huyo, atakapokuja katika utukufu wake na wa Baba na wa malaika watakatifu”.

Hivyo usimwonee haya Kristo mpe leo Maisha yako. Ili siku ile, atakapopokea heshima kutoka kwa watu wote na malaika zake, basi na wewe pia akuite.

Hiyo ndio maana ya Kuota upo na mtu maarufu/kuota unaongea na mtu maarufu.

Hivyo Kama upo tayari kumpa Yesu Maisha yako leo, utataka kuongozwa sala ya toba basi fungua hapa >>> KUONGOZWA SALA YA TOBA

Ubarikiwe sana..

Group la whatsapp Kwa mgawanyo bora wa masomo download App hapa>> App wingu la mashahidi

Mada Nyinginezo:

KARAMU YA MWANA-KONDOO.

BASI MUNGU ALIMWADHIMISHA MNO.

MFALME ANAKUJA.

KWANINI YESU KRISTO NI WA MUHIMU KWETU SASA?

MTINI, WENYE MAJANI.

Uasherati wa Kiroho maana yake nini?

Rudi Nyumbani:

Print this post

KUOTA UNAKOJOA KITANDANI.

Kuota unakojoa kitandani kuna maanisha nini?


Ndio ni kweli zipo ndoto zinazotokana na Mungu, na ni vizuri kuzifahamu hizo, na pia zipo ndoto zinazotokana na shetani pia hizo ni vizuri ukazifahamu.. Kama utahitaji kuzijua kwa undani bofya hapa >> Nitajuaje kama ndoto ni ya Mungu au ya Shetani?

Lakini kuna ndoto pia ambazo hazitokani na Mungu wala shetani bali zinatokana na sisi wenyewe.. Na hizo ndizo tunazoziota katika Maisha yetu kwa sehemu kubwa, naweza kusema hata Zaidi ya asilimia 90.

Tatizo linakuja ni pale watu  wanapotaka ndoto zinazotokana na sisi  wenyewe basi wapate tafsiri yake ya kiroho. Hilo ndio linalowafanya wengi waangukie katika tafsiri za uongo.

Lakini leo ni vizuri ukaujua ukweli juu ya ndoto za kuota unakojoa kitandani.

Biblia inasema.

Isaya 29:8 “Tena itakuwa kama mtu mwenye njaa aotapo, kumbe, anakula; lakini aamkapo, nafsi yake haina kitu; na kama mtu mwenye kiu aotapo, kumbe, anakunywa; lakini aamkapo, kumbe, anazimia, na nafsi yake inatamani; hivyo ndivyo utakavyokuwa huo wingi wa mataifa waletao vita juu ya mlima Sayuni”.

Umeuelewa mstari huo?

Ndoto kama hizi za ukota unakojoa kitandani ni ndoto zinazotokana na mwili wenyewe. Na hiyo inakuja pale kibofu chako kinapojaa sana mkojo, Na hapo ndipo ubongo wako unatengeneza matukio ambayo yatakufanya ujione kama unajiokojolea ili tu aumke, uende ukakoje.. Na kama mwili utakuwa umezidiwa sana, na ndio hapo unakuta mtu anajikojolea kweli, aidha sana au kidogo.

Mwingine utakuta anaota anakojoa mkojo ambao hauishi, au kila saa anakojoa kojoa, unaona yote hiyo mifumo tu ya mwili.

Kama vile unapolala na njaa, usiku utajiona unatafuta chakula, au unakula haushibi, huo ni mfumo wa ubongo, kukuarifu kuwa mwili unahitaji chakula.  Vivyo hivyo unapojikuta katika ndoto ya kuota unakojoa kitandani, hupaswi kuwa na hofu au wasiwasi.

Ipuuzie tu, na kama inakuja mara kwa mara, hakikisha ulalapo hunywi maji mengi, au vitu vyenye maji maji, na kwa kufanya hivyo hutakaa uone  tena ikikurudia.

Hivyo kuota unakojoa kitandani ni ndoto ya ubongo wetu wenyewe. Ipuuzie

Shalom.

Group la whatsapp  Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Mada Nyinginezo:

HAPO NDIPO WATU WALIPOANZA KULIITIA JINA LA BWANA.

KIFO CHA REINHARD BONKEY KINAACHA UJUMBE GANI KWETU?

JISHUSHE ILI MUNGU AKUHUDUMIE.

WACHUNGAJI WA BWANA MAKONDENI.

KILA MMOJA WENU AJUE KUUWEZA MWILI WAKE.

Kwanini Mungu anasema “Afanyaye malaika zake kuwa pepo”?

ZIKIMBIE TAMAA ZA UJANANI! NA MTU YEYOTE ASIUDHARAU UJANA WAKO.

Rudi Nyumbani:

Print this post

KUOTA UMEFUNGA NDOA.

Kuota umefunga ndoa  kuna maanisha nini?


Ndoto ya namna hii mara nyingi inaangukia katika kundi la ndoto zinazozotokana na shughuli nyingi..

Mhubiri 5:3 “Kwa maana ndoto huja kwa sababu ya shughuli nyingi; na sauti ya mpumbavu kwa njia ya wingi wa maneno”.

Na hii inatokana na kwamba pengine umekuwa ukiwaza kuoa au kuolewa hivi karibuni, au umekuwa ukitamani sana  kuoa au kuolewa kwa muda mrefu lakini bado malengo yako ya ndoa hujayafikia, au umehudhuria ndoa nyingi, au umezitazama, n.k. 

 Hivyo siku zote zile unachokifanya sana, au unachokiwaza sana, ni lazima kitajirudia tu katika ndoto zako, kama sio mara moja basi ni mara kwa mara, hilo ni jambo la kawaida.

Kwa mfano utakuta mwingine amekuwa akitafuta sana ajira kwa muda mrefu, au amekuwa akiwaza sana  ajira kwa muda mwingi, hivyo mtu kama huyu kuota yupo kwenye interview litakuwa ni jambo la kawaida kwake..

Na ndivyo vivyo hivyo katika kuota umefunga ndoa..mara nyingi ni ndoto itokanayo na shughuli za kila siku.


Lakini pia lipo jambo lingine la rohoni unapaswa ujue. Kumbuka kuwa Mungu huwa anazungumza pia na watu  katika ndoto kwa kupitia Maisha ya kawaida kabisa ya siku zote. Hivyo Ikiwa ndoto hii ya kuota umefunga ndoa imekujia kwa uzito wa kitofauti..

Na ukaifarahia hiyo ndoa na ukatamani ingekuwa hivyo kweli, Fahamu kuwa Mungu anakuonyesha kuwa ipo HARUSI ILIYO BORA NA KUU kuliko hiyo, inayokuja huko mbele. Na hiyo si nyingine Zaidi ya mwanakondoo (Yesu Kristo na kanisa lake)

Hilo usilisahau hata kidogo, katika Maisha yako. Kwasababu biblia inatuambia itakuwa ni Harusi ya pekee sana, ambayo karamu yake itafanyika mbinguni. Wakati huo wapo watu watatamani kuingia lakini waseweze, kitakachobakia kwao ni kilio na kusaga, kwa kuikosa tu.

Harusi hiyo ya Bwana Yesu na kanisa lake sio kama hii ya kimwilini, hapana, bali itakuwa ni ya rohoni, ambapo ndoa inaanzia hapa hapa duniani, na karamu itakuwa ni mbinguni.

Huko ndipo tutakapokutana na mambo ambayo jicho halijawahi kuona wala sikio kusikia..ili kufahamu vizuri jinsi karamu hiyo itakavyokuwa..Fungua hapa >>>>> KARAMU YA MWANAKONDOO

Fahmu kuwa Hizi ni nyakati za mwisho, Unyakuo upo karibu, Yesu yupo mlangoni kurudi, kulinyakua kanisa lake Je! Umeokoka? Umemkabidhi Maisha yako? Kama bado ni vizuri ukafanya uamuzi huo sasa, kukutana na ujumbe huu sio bure.Bali Mungu anayo malengo makubwa na wewe maishani mwako… Fanya hima nawe pia usionekane umeikosa siku ile ya Harusi kuu ya mwana-kondoo.

Ufunuo 19:7 “Na tufurahi, tukashangilie, tukampe utukufu wake; kwa kuwa arusi ya Mwana-Kondoo imekuja, na mkewe amejiweka tayari.

8 Naye amepewa kuvikwa kitani nzuri, ing’arayo, safi; kwa maana kitani nzuri hiyo ni matendo ya haki ya watakatifu.

9 Naye akaniambia, Andika, Heri walioalikwa karamu ya arusi ya Mwana-Kondoo. Akaniambia, Maneno haya ni maneno ya kweli ya Mungu”

Shalom.

Group la whatsapp Kwa mgawanyo bora wa masomo download App hapa>> App wingu la mashahidi

Mada Nyinginezo:

KUOTA UPO UCHI.

KUOTA UNAPAA.

KUOTA UNAOLEWA/UNAOA.

KUOTA UNATOKA DAMU YA HEDHI.

KUOTA UNAOLEWA/UNAOA.

Rudi Nyumbani:

Print this post