Zawadi kubwa Mungu aliyompa mwaminio ni UTAKATIFU.
Utakatifu ni ile hali ya kuwa mkamilifu kama Mungu, kutokuwa na dosari au kasoro yoyote, msafi asilimia mia moja, bila kosa lolote ndani yako.
Sasa heshima hii tumetunukiwa na Mungu, jambo ambalo hapo zamani halikwepo, ilihitaji matendo ya haki ya Mtu kuufikia, lakini hapakuwahi kutokea mwanadamu yoyote aliyeweza kufikia cheo hicho cha juu sana cha Mungu, yaani kutokuwa na dhambi kabisa.
Lakini pale tunapomwamini Bwana Yesu, siku hiyo hiyo, Mungu anatufanya Watakatifu kama yeye, haijalishi bado tutakuwa na asili ya dhambi nyingi kiasi gani. Hiyo ndio maana ya neema. Tunaitwa watakatifu bila ya kujisumbua kwa lolote.
Lakini sasa lengo la Mungu sio tuwe “watakatifu katika dhambi” Bali “tuwe watakatifu katika utakatifu”. Hivyo kuanzia huo wakati anaanza kumfundisha mtu kuusomea hadi kuuhitimu Utakatifu wake, aliopewa ili aendane na cheo alichotunukiwa tangu mwanzo.
Na hapo mtu akishindwa kupiga hatua, basi anaondolewa heshima hiyo kwake, na hivyo hawezi tena kuwa kama Mungu, na matokeo yake wokovu unampotea.
Mwaka Fulani hapa nchini kwetu kulikuwa na askari mmoja aliyeonyesha kitendo cha kishujaa kukataa rushwa ya milioni 10, ambapo alishawishiwa aipokee ili aifute kesi ya watuhumiwa wawili waliokuwa wanakabiliwa na mashtaka,. Lakini yeye hakukubali, na ilipokuja kubainika, mkuu wa jeshi la polisi (IGP) akafurahishwa naye, Akampandisha cheo (kwani alikuwa ni askari wa chini). Lakini cha kushangaza baada ya kama miaka miwili tukaja kusikia Yule askari aliyepandishwa cheo ameshushwa cheo kile. Kufuatilia ni kwanini imekuwa hivyo? Jeshi la polisi likatoa taarifa kuwa alionyesha utovu wa nidhani, wa kukataa kwenda kwenye mafunzo ya cheo chake kipya. Akidhani kwasababu IGP amempandisha basi inatosha hakuna haja ya mafunzo tena. Akasahau kuwa ufahamu wake wa kielimu ni lazima uendane na cheo chake, kwamba akiwa bado na cheo kikubwa, wakati huo huo anapaswa aendelee kusoma,na kujifunza kimatendo, ili aweze kutumika ipasavyo. Lakini akashushwa cheo na kuchukuliwa hatua za kinidhamu kwa kukataa kutii amri ya jeshi.
Ndivyo ilivyo katika UTAKATIFU tunaopewa na Mungu bure, ni lazima tuutendee kazi kwa kila siku kupiga hatua mpya ya mabadiliko. Huwezi kusema umeokoka (wewe ni mtakatifu), halafu maisha yako ya mwaka jana na mwaka huu ni yaleyale wewe sio mtakatifu. Kila siku lazima uwe na mabadiliko, ulikuwa unabeti, unaacha kubeti, ulikuwa unavaa mavazi ya uchi uchi, unayachoma moto, ulikuwa unajichubua, unaacha, ulikuwa unasengenya unakaa mbali na wasengenyaji, ulikuwa unakesha kwenye muvi usiku kucha unaacha hayo, unatumia muda wako mwingi kwenye kujisomea biblia, ulikuwa ni mtu wa rushwa unaanza kuondoa vitendo hivyo kwenye biashara yako. Ulikuwa huwezi kufunga na kuomba unaanza kujizoeza kuwa mtu wa rohoni, unafunga, unaomba, na kukesha, Huko ndiko Mungu anakokutaka. Anaona umekiheshimu cheo alichokupa.
Ukiwa ni mtu wa kupiga hatua kila siku, basi Mungu atazidi kukuona wewe ni MTAKATIFU na hivyo utakuwa karibu na yeye. Lakini ukiishi hoe hae, hutambuliki kama umeokoka, au vipi, tabia zilezile za zamani unaendelea nazo, wala hujihangaishi kuziondoa. Usijidanganye wewe umeokoka.
Bwana atusaidie..
Je! Upo ndani ya Kristo? Je unataarifa kuwa hizi ni siku za mwisho? Yesu amekaribia kurudi? Ni nini utamweleza Mungu siku ile endapo leo utaukataa wokovu unaoletwa kwako bure.. Tubu dhambi zako, mgeukie Bwana, akupe Roho Mtakatifu, akupe heshimu hiyo ya utakatifu. Hivyo Ikiwa upo tayari kufanya hivyo basi fungua hapa kwa ajili ya mwongozo wa sala ya toba >>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Bwana akubariki.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618 Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > WHATSAPP-Group
Mada Nyinginezo:
FUNDISHO KUU LA NEEMA YA MUNGU KWETU.
UTAKASO NI SEHEMU YA MAISHA YA MKRISTO YA KILA SIKU.
Kwanini hatuirithi neema kama tunavyoirithi dhambi?
HATARI YA KUHUBIRI INJILI TOFAUTI NA ILIYOANDIKWA KWENYE BIBLIA.
Jina Palestina limetoka na Neno la kiyunani Filistia, lenye maana ya ardhi ya wafilisti. Kwahiyo ile Filisti inayotajwa kwenye biblia ndio Palestina unayoisikia sasa.
Lakini Jambo ambalo wengi wanachanganya ni kudhani kuwa wafilisti walikuwa ni waarabu. Si kweli, kwani waarabu walikuwa ni watoto wa Ishmaeli kutoka kwa Ibrahimu, lakini wafilisti walikuwepo kabla hata ya Ibrahimu, na walitokea katika uzao wa Hamu.
Mwanzo10:14 na Wapathrusi, na Wakasluhi; huko ndiko walikotoka Wafilisti na Wakaftori.
Watu hawa walikuwa ni wapagani moja kwa moja, na waliabudu miungu yao mikuu mitatu iliyoitwa Ashtorethi, Baal-zebubu, na Dagoni.(Waamuzi 16:23, 2Wafalme 1:2, 1Samweli 31:10,)
Wafilisti walikwenda kuweka makazi yao, katika nchi ya Kaanani. Upande wa kusini, kutoka mto Yordani mpaka ule wa ile habari kubwa (Bahari ya Mediterenia). Na baadaye kipindi cha akina Samweli wakawa na miji yao mitano imara iliyoitwa Gaza, Ashdodi, Gathi, Ashkeloni, Ekroni (1Samweli 6:17, Yoshua 13:3)
Hivyo Ibrahimu alipoitwa na Mungu na kuambiwa aindee nchi ile aliwakuta tayari wapo, na wameshajiwekea ngome zao (Mwanzo 21:32, 34, 26:1).
Na wana wa Israeli walipokuwa wanavuka kuingia nchi yao ya ahadi Waliambiwa wawaangamize wakaanani wote, kwasababu wamepewa nchi yote. Lakini tunaona walipuuzia, na kule kukawia kawia kwao na kuridhika, Mungu akawaambia watu hawa watakuwa “mwiba” kwao .
Waamuzi 2:1 Kisha malaika wa Bwana alikwea juu kutoka Gilgali kwenda Bokimu. Akasema, Mimi nimewaleta ninyi mkwee juu kutoka nchi ya Misri, nami nimewaleta hata nchi niliyowaapia baba zenu; nami nilisema, Mimi milele sitalivunja hilo agano langu nililoagana nanyi; 2 nanyi msifanye agano lo lote na hawa wenyeji wa nchi hii; zipomosheni nchi madhabahu zao; lakini hamkuisikia sauti yangu; je! Mmefanya haya kwa sababu gani? 3 Basi kwa ajili ya hayo mimi nilisema zaidi, Mimi sitawafukuza watoke mbele zenu; lakini watakuwa kama miiba mbavuni mwenu, na miungu yao itakuwa ni tanzi kwenu.
Na ndivyo ilivyokuwa Yoshua hakuweza kuwatoa wenyeji wote wa Filisti(Yoshua 11:20-23). Na ndio hao wakaja kuwasumbua baadaye.
Ni wazi kuwa Israeli walipigana vita vingi, lakini moja wa maadui zao waliokuwa wanawasumbua sana basi ni hawa wafilisti, kwasababu walikuja kupata nguvu, sio tu ya wingi wa watu, bali pia ya kiteknolojia katika silaha, kiasi kwamba Israeli ilitegemea kunolewa silaha zao kutoka Filisti.(1Samweli 13:19-23). Na zaidi sana waliwazidi Israeli hata kimaendeleo, kwa kipindi kirefu hawakuweza kuwashinda
Na wana wa Israeli walipomkosea Mungu aliwaweka kwenye mikono yao, wakataabishwa kwa muda mrefu, kisha walipomlilia Bwana, walinyanyuliwa mkombozi. Ndio hapo tunawaona waamuzi kama wakina Samsoni, Shamgari, Samweli, Sauli, Daudi.Wakipigana vita vingi sana na watu hawa.Ambavyo tunavyosoma katika biblia (Waamuzi, Samweli 1&2, Wafalme 1&2,)
Lakini wakati Israeli inachukuliwa utumwani taifa hili nalo halikupona lilianguka, katika mkono wa mfalme Nebukreza wa Babeli, na kupotea kabisa. (Yeremia 47:47, Ezekieli 25:15-17, Sefania 2:4-7).
Tangu huo wakati hakukuwa na taifa rasmi la wafilisti, wala haikuwa rahisi kuwatambua kwa miaka zaidi ya 2500. Mpaka ilipofikia mwaka 1948, Taifa la Israeli kuundwa tena kwa mara ya kwanza, eneo hilo la wafilisti, kusini mwa Israeli, lilikuwa tayari linajulikana kama “Palestina”
Palestina ya leo ni mahali palipo na mchanganyiko wa jamii mbalimbali za watu, walio wa asili ya kifilisti wakiwa ni wachache sana, lakini wengi wao sasa ni waislamu waliohamishiwa hapo na waturuki, kutoka katika mataifa mbalimbali kati ya karne ya 16-19, pamoja waarabu katika karne ya 20 ambao nao waliletwa na waingereza.
Hivyo mpaka sasa tunavyoona, ni kwamba Palestina imemezwa zaidi na dini ya kiislamu na jamii kubwa ya waharabu. Na cha kushangaza ni kwamba ijapokuwa jamii ya sasa ni tofauti kabisa,na wafilisti wa zamani, bado migororo ile ile ya zamani inanyunyuka tena. Kuonyesha kuwa Neno la Mungu halipiti milele.
Ule mwiba bado utawasumbua wayahudi.
Lakini ipo sababu nyingine ya Rohoni. Kumbuka kuwa hatma ya huu ulimwengu, itakuwa ni Dunia nzima kusimama kinyume na taifa teule la Mungu Israeli. Ili Yesu Kristo atokee mawinguni na kuwapigania watu (Matendo 1:6, Ufunuo 19) . Na tayari Mungu alishaahidi kuwa atafanya mataifa yote kuwa kama kikombe cha kulemea,. Ili tu ayachonganishe, kisha mwisho wake uwe ni yeye kulitetea taifa lake, ndipo huo mwisho ufike.
Wewe huoni mvuragano huu, unayagusa mataifa yote duniani.
Zekaria 12:3 Tena itakuwa siku hiyo, nitafanya Yerusalemu kuwa jiwe la kuwalemea watu wa kabila zote; wote watakaojitwika jiwe hilo watapata jeraha nyingi; na mataifa yote ya dunia watakusanyika pamoja juu yake
Unaweza kuona ni jinsi gani tupo mwishoni kabisa mwa dunia. Hii neema tuliyonayo huku katika mataifa, ndio inafikia ukomo wake, na kurejea Israeli. Maana Mungu anasema atawarudia watu wake (Warumi 10&11), na kuwaokoa, wakati huo yatakapokuwa yanatendeka unyakuo utakuwa umeshapita huku kwetu.
Zekaria 12:9 Hata itakuwa siku hiyo, ya kwamba nitatafuta kuwaangamiza mataifa yote watakaokuja kupigana na Yerusalemu. 10 Nami nitawamwagia watu wa nyumba ya Daudi, na wenyeji wa Yerusalemu, roho ya neema na kuomba; nao watamtazama yeye ambaye walimchoma; nao watamwombolezea, kama vile mtu amwombolezeavyo mwanawe wa pekee; nao wataona uchungu kwa ajili yake, kama vile mtu aonavyo uchungu kwa ajili ya mzaliwa wake wa kwanza. 11 Siku hiyo kutakuwa na maombolezo makuu huko Yerusalemu, kama maombolezo ya Hadadrimoni katika bonde la Megido
Je! Unaishije sasa hivi, Umehubiriwa injili mara ngapi, bado unashupaza shingo yango? Huko uendako unatarajia ukawe mgeni wa nani. Na ukweli umeshaujua kuwa tunaishi katika siku za kumalizia, Unyukuo wa kanisa ni wakati wowote. Huu ni wakati sasa ya kuyathimini maisha yako ya rohoni, angalia dunia inapoelekea, kufumba na kufumbua mambo yanabadilika. Uamuzi ni wako. Lakini ikiwa utapenda Yesu akuokoe, akufanye kiumbe kipya basi fungua hapa upate mwongozo wa sala ya toba. >>>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Bwana akubariki.
Shalom.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mada Nyinginezo:
NIMEAZIMIA KUWAKUSANYA MATAIFA. NIPATE KUWAMWAGIA GHADHABU YANGU
KUNA NGUVU YA ZIADA KATIKA KULING’ANG’ANIA KUSUDI LA MUNGU.
Konzo la Ng’ombe ni nini? (Waamuzi 3:31).
Bahari mbalimbali zilizoorodheshwa kwenye biblia.
Mataifa ni nini katika Biblia?
Swali: Je katika Mwanzo 10:25 tunasoma kuwa nchi/dunia iligawanyika? Swali ni Je! Iliwaganyikaje? Na je ule ndio ulikuwa mwanzo wa mabara saba (7) tuliyonayo leo?.
Jibu: Tusome,
Mwanzo 10:25 “ Eberi akazaliwa wana wawili wa kiume; jina la wa kwanza ni Pelegi maana KATIKA SIKU ZAKE NCHI ILIGAWANYIKA; na jina la nduguye ni Yoktani”.
Kama ukiendelea mbele kidogo kusoma Mlango wa 11 wa kitabu hiko cha Mwanzo utaona kuna tukio lilitokea ambalo ndio lile la kujengwa kwa Mnara wa Babeli, ambapo watu wale walipokuwa katika hatua za awali za kuujenga Mungu alishuka na kuchafua lugha zao na Semi zao, ili wasisikilizane. Na hiyo ikawafanya waache kuujenga ule mnara na kila mmoja kutawanyika na njia yake.
Mwanzo 11:1 “Nchi yote ilikuwa na lugha moja na usemi mmoja.
2 Ikawa watu waliposafiri pande za mashariki waliona nchi tambarare katika nchi ya Shinari; wakakaa huko.
3 Wakaambiana, Haya, na tufanye matofali tukayachome moto. Walikuwa na matofali badala ya mawe, na lami badala ya chokaa.
4 Wakasema, Haya, na tujijengee mji, na mnara, na kilele chake kifike mbinguni, tujifanyie jina; ili tusipate kutawanyika usoni pa nchi yote.
5 Bwana akashuka ili auone mji na mnara waliokuwa wakiujenga wanadamu.
6 Bwana akasema, Tazama, watu hawa ni taifa moja, na lugha yao ni moja; na haya ndiyo wanayoanza kuyafanya, wala sasa hawatazuiliwa neno wanalokusudia kulifanya.
7 Haya, na tushuke huko, tuwachafulie usemi wao ili wasisikilizane maneno wao kwa wao.
8 BASI BWANA AKAWATAWANYA KUTOKA HUKO WAENDE USONI PA NCHI YOTE; wakaacha kuujenga ule mji.
9 Kwa sababu hiyo jina lake likaitwa Babeli; maana hapo ndipo Bwana alipoichafua lugha ya dunia yote; na kutoka huko Bwana akawatawanya waende usoni pa nchi yote”.
Hapo Mstari wa 8 unasema “BWANA AKAWATAWANYA KUTOKA HUKO WAENDE USONI PA NCHI YOTE”.
Sasa huo Mtawanyiko waliotawanywa wanadamu ndio “mgawanyiko wa nchi” unaozungumziwa katika Mwanzo 10:25 na unarudiwa tena katika 1Nyakati 1:19, Na ulitokea katika nyakati za mtu mashuhuri aliyeitwa “Pelegi” aliyekuwa mwana wa Eberi.
Hivyo mgawanyiko wa nchi haukuwa wa kiografia bali wa watu!.. na wala mabara 7 hayakuzaliwa hapo!, na Zaidi sana biblia haijataja mahali popote kuwa dunia iligawanyika na kuwa mabara 7, huenda yalikuwa hivi hivi saba tangu uumbaji, au huenda yalizalika kipindi Fulani baada ya uumbaji, tusichokijua sisi lakini si hiko kilichotajwa katika Mwanzo 10:25. Mgawanyiko huo wa Mwanzo 10:25 unahusu watu na si mabara.
Kujua ufunuo uliopo nyuma ya mnara wa Babeli basi fungua hapa >>TUUTAFUTE USEMI MMOJA. TUUJENGE MNARA WA MUNGU
Bwana akubariki.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mada Nyinginezo:
Kwanini hatupaswi kujilipiza kisasi?… Kwasababu maandiko yanatufundisha kuwa kisasi ni juu yake yeye atalipa.
Warumi 12:19 “Wapenzi, msijilipize kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu; maana imeandikwa, KISASI NI JUU YANGU MIMI; MIMI NITALIPA, ANENA BWANA.
20 Lakini, Adui yako akiwa na njaa, mlishe; akiwa na kiu, mnyweshe; maana ufanyapo hivyo, utampalia makaa ya moto kichwani pake”.
Tabia ya kujilipiza kisasa Bwana Mungu aliikataa tangu Mwanzo na Bwana Yesu akaja kuithibitisha tena katika Mathayo 5.
Tunaona baada ya Kaini kumwua ndugu yake Habili kwasababu ya wivu, Mungu alimlaani Kaini kwa kosa lile..
Lakini Mungu hakumwua Kaini bali alimlaani juu ya ardhi kwamba ataendelea kuishi lakini ardhi itamkataa… Kila kilimo atakachokifanya juu ya ardhi hakitafanikiwa, ndio maana baada ya pale hatuoni Kaini na uzao wake wakiendelea na kazi yake ya ukulima badala yake tunasoma wanaanza kutengeneza vyuma, na wapiga filimbi (Mwanzo 4:17-22).
Sasa baada ya Bwana Mungu kumlaani Kaini alijua kabisa kuna watu watakuja kusikia habari zake kwamba ni mwuaji, na pia kalaaniwa na Mungu, hivyo watataka wajichukulie hukumu aidha ya kumwua au kumnyanyasa…
Sasa Mungu kwa kulijua hilo, akamwekea Kaini alama, ili kila mtu atakayemwona asimguse…
Na alama hiyo ikaendelea kuwepo juu ya Kaini na uzao wake, iliyowatofautisha uzao wa Kaini na uzao mwingine.
Na Bwana akasema mtu atakayemwua Kaini, basi atalipwa kisasi mara 7,
Mwanzo 4:13 “Kaini akamwambia BWANA, Adhabu yangu imenikulia kubwa, haichukuliki.
14 Tazama, umenifukuza leo katika uso wa ardhi, nitasitirika mbali na uso wako, nami nitakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani; hata itakuwa kila anionaye ataniua.
15 BWANA akamwambia, Kwa sababu hiyo ye yote atakayemwua Kaini atalipizwa kisasi mara saba. BWANA akamtia Kaini alama, mtu amwonaye asije akampiga”
Hivyo watu walivyosikia hivyo wakaogopa kumnyooshea mikono yao Kaini, kwasababu walijua kuna adhabu kubwa sana katika kufanya hayo…
Umeona?..Kumbe kisasi na hasira ndani ya maisha ya mtu ni machukizo makubwa sana mbele za Mungu..
Ndivyo maandiko yanasema…
Mithali 24:17 “Usifurahi, adui yako aangukapo; Wala moyo wako usishangilie ajikwaapo;
18 BWANA asije akaliona hilo, likamkasirisha; Akageuzia mbali naye hasira yake”.
Ikiwa na maana kuwa kama adui yako amekutenda mabaya na wewe usimrudishie yale mabaya, mwombee Bwana ambadilishe, itakuwa heri kwako…na utasikia ule mzigo umeondoka ndani yako…
Lakini kama ukifikiri kwamba njia ya kuondoa mzigo (uchungu) ndani yako ni wewe kujilipiza kisasi, nataka nikuambie kuwa ndio utauongeza badala ya kuupunguza, kwasababu utakayemlipa kisasi utakuwa umeweka uadui naye hivyo shetani anaweza kumtumia tena kufanya jambo lingine kwa wakati mwingine kwa njia nyingine…lakini lililo baya zaidi ni kwamba utakuwa umekosana na Mungu pia.
Sasa nini kifanyike ili kuishinda nguvu ya kisasi ndani yako?
1. Wokovu.
Wokovu ndio mlango wa Imani. Ni lazima kumwamini Yesu na kumkiri.
2. Maombi (yanayoambatana na mifungo).
Baada ya kuokoka ni lazima uwe mtu wa maombi. Maombi yatakufanya uwe na nguvu za kiroho ambazo zitakusaidia wewe kushinda dhambi.
3 .Kusoma Neno.
Neno la Mungu (biblia) litakusaidia kukujenga utu wako wa ndani. Kwamfano Neno lifuatalo ukilijua litakusaidia wewe kutolipiza kisasi.
Mhubiri 7:21 “Tena, usitie moyoni mwako maneno yote yaliyosemwa; usije ukamsikia mtumwa wako mwenyewe ali anakutukana.
22 Kwa kuwa mara nyingi moyo wako pia unajua ya kwamba wewe mwenyewe umewatukana watu wengine”.
Mambo haya matatu ukiyazingatia sana basi Nguvu ya kisasi haiwezi kufanya kazi ndani yako, utakuwa mtu wa kusamehe na kuombea wanaokuudhi, na mengine kumwachia Bwana, na hivyo utu wako wa ndani utajengeka sana.
Maran atha!.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618 Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > WHATSAPP-Group
Mada Nyinginezo:
Biblia inaposema Kaini akatoka mbele za uso wa Bwana, Inamaana gani?
Mtu wa kwanza kufa alikuwa nani?
Rohoni vipo vikombe viwili ambavyo Mungu ameviandaa kwa wanadamu.
KIKOMBE CHA GHADHABU
Kama hufahamu, Mungu Huwa anajiwekea “akiba” ya hasira yake. Ikiwa na maana si mwepesi kutimiliza hasira yake Kwa haraka, Huwa anaikusanya na siku ikifika kipimo chake Kisha akaimimina hapo huwa hapana Rehema Tena. Ni kilio na kusaga meno!.
Soma
Nahumu 1:2-3
[2]BWANA ni Mungu mwenye wivu, naye hujilipiza kisasi; BWANA hujilipiza kisasi, naye ni mwingi wa hasira; BWANA hujilipiza kisasi juu ya adui zake, huwawekea adui zake akiba ya hasira.
[3]BWANA si mwepesi wa hasira, ana uweza mwingi, wala hatamhesabia mtu mwovu kuwa hana hatia kamwe; BWANA ana njia yake katika kisulisuli na tufani, na mawingu ni mavumbi ya miguu yake.
Mifano halisi ya hasira ya Mungu tunaiona kipindi Cha gharika, kipindi Cha sodoma na Gomora. Na ameahidi pia katika siku za mwisho ataleta hukumu hiyo Kwa ulimwengu mzima, na itatimilika yote katika lile ziwa la moto.(2Petro 3:7-5)
Utapata majibu Kwanini Leo, Mungu anaonekana kama vile yupo kimya Kwanini uovu unaendelea hachukui hatua stahiki duniani, fahamu ni kwamba anangoja kipimo chake kijae, kikombe kijae ili waovu wanywe ghadhabu yake yote. Ndivyo alivyowaambia Ibrahimu kuhusu kuangamia Kwa wakaanani, alikuwa anasubiria uovu wao utumie (Mwanzo 15:16), na siku ilipofika Yoshua aliwaangamiza wote.
Hivyo mtu unapokuwa mwovu unakijaza kikombe Cha ghadhabu ya Mungu, Na kama dhiki kuu itakupita basi utakatana na kikombe hicho siku Ile ya hukumu, utakinywa Kwa kutupwa kwenye lile ziwa la moto.
Ufunuo wa Yohana 14:10
[10]yeye naye atakunywa katika mvinyo ya ghadhabu ya Mungu iliyotengenezwa, pasipo kuchanganywa na maji, katika kikombe cha hasira yake; naye atateswa kwa moto na kiberiti mbele ya malaika watakatifu, na mbele za Mwana-Kondoo.
KIKOMBE CHA BARAKA.
Lakini pia watakatifu nao Bwana anawawekea akiba ya Baraka na mema. Kwa maisha ya haki wanayoishi sasa hapa duniani, usidhani kuwa hayo mema unayotendewa ndio malipo stahiki Kutoka Kwa Mungu wako,hapana..Bwana anakijaliza kikombe Cha watakatifu na siku Ile tutakinywea na Yesu Kristo kule mbinguni kwenye Karamu ya Mwana kondoo. Haleluya.
Mathayo 26:27-29
[27]Akakitwaa kikombe, akashukuru, akawapa, akisema, Nyweni nyote katika hiki;
[28]kwa maana hii ndiyo damu yangu ya agano, imwagikayo kwa ajili ya wengi kwa ondoleo la dhambi.
[29]Lakini nawaambieni, Sitakunywa kabisa tangu sasa uzao huu wa mzabibu, hata siku ile nitakapokunywa mpya pamoja nanyi katika ufalme wa Baba yangu.
Hapo ndipo tutakapoona wema wote wa Mungu maishani mwetu. Tutakinywea kikombe hicho, tutamiminiwa thawabu na Raha isiyo na kifani. Hapo ndipo tutakapojua ni jinsi gani Mungu anavyotujali. Usikose mbingu ndugu, kosa vyote lakini Unyakuo usikupite.
Ndugu ukiona unamtumikia Mungu Leo huoni faida yoyote, kama vile huoni malipo yoyote, ,tambua kuwa Bwana anaona..anaweka tu akiba, utaipokea Raha siku Ile itakapofika.
Unapojitesa kuishi maisha ya haki, halafu unaona kama vile Mungu hakujali..usijidanganye kikombe unakijazilisha tu. Wakati wa kukinywea utafika.
Soma haya maneno ya faraja Mungu aliyoyatamka Kwa watu wake..
Malaki 3:13-18
[13]Maneno yenu yamekuwa magumu juu yangu, asema BWANA. Lakini ninyi mwasema, Tumesema maneno juu yako kwa namna gani?
[14]Mmesema, Kumtumikia Mungu hakuna faida; na, Tumepata faida gani kwa kuyashika maagizo yake, na kwa kwenda kwa huzuni mbele za BWANA wa majeshi?
[15]Na sasa twasema ya kwamba wenye kiburi ndio walio heri; naam, watendao uovu ndio wajengwao; naam, wamjaribuo Mungu ndio waponywao.
[16]Ndipo wale waliomcha BWANA waliposemezana wao kwa wao. Naye BWANA akasikiliza, akasikia; na kitabu cha ukumbusho kikaandikwa mbele zake, kwa ajili ya hao waliomcha BWANA, na kulitafakari jina lake.
[17]Nao watakuwa wangu, asema BWANA wa majeshi, katika siku ile niifanyayo; naam, watakuwa hazina yangu hasa; nami nitawaachilia, kama vile mtu amwachiliavyo mwanawe mwenyewe amtumikiaye.
[18]Ndipo mtakaporudi, nanyi mtapambanua kati ya wenye haki na waovu, na kati ya yeye amtumikiaye Mungu na yeye asiyemtumikia.
Bwana atupe macho ya kumwelewa yeye. Kijazilishe kikombe Cha wokovu wako. Ili siku Ile ushiriki mema yote.
Ubarikiwe.
Je umeokoka? Kama bado unasubiri Nini Leo usifanye hivyo. Ikiwa upo tayari kumgeukia Yesu na kumfanya mwokozi wa maisha Yako, akusamehe dhambi zako. Basi ni wewe tu kufungua moyo wako na kuikubali msamaha huo.Ikiwa upo tayari kufanya.hivyo basi fungua hapa Kwa mwongozo huo.
Bwana akubariki..
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mada Nyinginezo:
SIKU YA MAONYESHO MAKUU YA BWANA YESU, IPO KARIBU.
NIMEAZIMIA KUWAKUSANYA MATAIFA. NIPATE KUWAMWAGIA GHADHABU YANGU
KIKOMBE CHA GHADHABU YA MUNGU KINAJAA.
Kwanini Mungu aliwaagiza wana wa Israeli wasikisaze chakula?
“Romans road to salvation”
Njia ya wokovu ndani ya kitabu Cha Warumi ni Nini?
Ni mpango wa wokovu wa mwanadamu, ambao umeainishwa vyema kutoka katika kitabu Cha Warumi.
Kitabu hichi kinaeleza jinsi mtu anavyoweza kuupokea wokovu kutoka Kwa Mungu.
Hivyo ikiwa wewe bado hujaufahamu mpango wa Mungu kwako, wa namna ya kuupokea wokovu basi kitabu hichi kimeanisha vifungu ambavyo vinakuonesha ni jinsi gani utaweza kuupokea.
Lakini pia ikiwa wewe hujui ni wapi pa kuanzia unapokwenda kuwashuhudia watu habari za wokovu, basi kitabu hichi kinakupa mwongozo wa namna ya kuwahubiria wengine habari njema. Na vifungu muhimu vya kusimamia..
Hivi ni vifungu “mama”
Warumi 3:23
[23]kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu;
Tuendapo Kwa Mungu, lazima tujue hakuna mwenye haki hata mmoja sote Tumepungukiwa na utukufu wa Mungu. Tumetenda dhambi, Vilevile ikiwa wewe ni mhubiri/mshuhudiaji, huna budi kumuhubiria mtu jambo hilo, kwamba hakujawahi kutokea mwema hapa duniani. Hivyo wote tunauhitaji mpango wa Mungu wa wokovu katika maisha yetu.
[23]Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.
Hapa, Mungu anatuonesha, matokeo ya kudumu katika dhambi zetu, ambazo wote tulikuwa nazo, kuwa ikiwa tutaendelea kubaki katika Hali hiyo hiyo basi tutakutana na mauti ya milele, lakini tukipokea zawadi ya Mungu basi tutapata uzima wa milele.
[8]Bali Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi.
Kwamba sasa hiyo zawadi ya Mungu ambayo itapelekea uzima wa milele ni Yesu Kristo, yeye ndiye aliyetolewa na Mungu kuzichukua dhambi zetu zote, kwa kifo cha pale msalabani. Pale tuliposhindwa sisi wenyewe basi Yesu alikuja kutusaidia kuchukua makosa yetu.
Hiki sasa kinaeleza Namna ya kuupokea wokovu;
Warumi 10:9-10
[9]Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka.
[10]Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu.
Kwa kuamini kwetu kuwa Yesu Yu hai, na kwamba anakomboa wanadamu, na vilevile kumkiri Kwa kinywa kuwa ndiye Bwana na mwokozi wetu. Basi tunaupokea msamaha huo wa dhambi Bure, bila gharama yoyote. Na deni letu la dhambi linakuwa limefutwa tangu huo wakati
Hivyo ni sharti ujue kuwa msamaha wa dhambi hauji Kwa matendo Yako mema, Bali unakuja Kwa kuikubali kazi ya Yesu msalabani iliyofanyika Kwa ajili ya ukombozi wako.
Halikadhalika Wewe kama mshuhudiaji vifungu hivi viwepo kichwani mwako.
[1]Basi tukiisha kuhesabiwa haki itokayo katika imani, na mwe na amani kwa Mungu, kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo,
Maana yake ni kuwa baada ya mtu kumkiri Kristo, na kumkubali kama Bwana na mwokozi wake. Basi anapaswa awe na AMANI na Mungu kwasababu hakuna mashtaka yoyote ya adhabu juu yako. Hakuna hukumu yoyote ya mauti ipo juu yake.
Huo ndipo mpango wa awali wa wokovu wa Mungu Kwa mwanadamu. Ambapo tunapaswa kufahamu kama ulivyoanishwa katika kitabu hichi Cha Warumi.
Kisha baada ya hapo tunawafundisha watu kuitimiza haki yote au kusudi lote la Mungu juu yetu, Ikiwemo ubatizo wa maji, na ule wa Roho Mtakatifu.
Ikiwa bado hujaokoka, na utapenda kuupokea msamaha wa Yesu Bure maishani mwako, basi Unaweza kuwasiliana na sisi Kwa namba uzionazo chini ya chapisho hili kwa ajili ya mwongozo huo Bure. Vilevile na Ule wa ubatizo.
Bwana akubariki.
Shalom
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mada Nyinginezo:
Je! sheria ilikuwaje dhaifu kwasababu ya mwili? (Warumi 8:3)
TOFAUTI KATI YA SHERIA YA ROHO WA UZIMA NA SHERIA YA DHAMBI NA MAUTI!
Je Kauli ya Mungu katika Warumi 11:4 na 1Wafalme 19:18 inajichanganya?.
Nini tofauti ya haya maneno. 1) KUOKOKA, 2) WOKOVU, 3) KUONGOKA.?
Je mwanamke Fibi, alikuwa ni askofu wa makanisa, kama mitume?
Je! Moyo wako upo kweli kwake?
Kuna kauli Bwana Yesu alisema kuhusiana na watu kumwelewa Mungu na uweza wake kwetu, alisema..
Mathayo 13:14 “Na neno la nabii Isaya linatimia kwao, likisema, Kusikia mtasikia, wala hamtaelewa; Kutazama mtatazama, wala hamtaona. 15 Maana mioyo ya watu hawa imekuwa mizito, Na kwa masikio yao hawasikii vema, Na macho yao wameyafumba; Wasije wakaona kwa macho yao, Wakasikia kwa masikio yao, WAKAELEWA KWA MIOYO YAO, WAKAONGOKA, NIKAWAPONYA”
Ametaja mambo makuu matatu,
Hatua ya mwisho ambayo Mungu anatarajia, pindi anapomfundisha mtu, au kusema naye ni KUELEWA. Hivyo ataanza kwanza kwa kumwonyesha mambo kadha wa kadha, yatapita mbele yake, ataanza kusema na yeye kwa njia nyingi, aidha kwa wahubiri wake, au ndoto, au maono, au vitu vya asili, au kwa Neno lake, au kwa maisha yake mwenyewe.. Lakini pamoja na njia zote hizo bado mtu huyo anaweza asimwelewe Mungu, kama Moyo wako haupo kwake.
Jambo ambalo watu wengi hatujui, ni kwamba Mungu anazungumza na kila mmoja, Na kila mmoja anaonyeshwa maono mengi na Mungu, kila mtu ameshakutana na Mungu, aidha uso kwa uso au katika roho, haijalishi ni mwema au mwenye dhambi, Lakini ni wachache sana walioweza kuielewa sauti yake iliposema nao.
Ni kwasababu gani hawaielewi? Ni kwasababu inahitaji MOYO ili kuielewa, Na sio macho au sikio. Kama moyo wako haupo kwake, sahau kumwelewa Mungu anaposema na wewe kwa njia yoyote ile. Hata kama itakuja kwa dhahiri, bado hutamwelewa. Sauti yake kwako itakuwa ni ngurumo tu, kama ilivyokuwa kipindi kile Bwana Yesu alipokuwa anazungumza na makutano kuhusiana na ufalme wa mbinguni.
Yohana 12:28 “Baba, ulitukuze jina lako. Basi ikaja sauti kutoka mbinguni, Nimelitukuza, nami nitalitukuza tena. 29 Basi mkutano uliosimama karibu wakasikia, walisema ya kwamba kumekuwa ngurumo; wengine walisema, Malaika amesema naye.30 Yesu akajibu, akasema, Sauti hiyo haikuwako kwa ajili yangu, bali kwa ajili yenu”
Ni kwanini iwe hivyo kwao? Ni kwasababu kilichowapeleka kwa Yesu sio wokovu wa Roho zao, au upendo wao kwa Mungu, kilichowapeleka kwake, ni miujiza, uponyaji, uzuri, mwonekano, mazingira, basi, hakuna jipya. Wakishapata walichokuwa wanakitafuta hao wanaondoka zao kuendelea na mambo yao ya dhambi ya sikuzote.
Ndio maana hakukuwa na hata mmoja ambaye aliyeelewa mifano yote Yesu aliyokuwa anaisema mbele ya umati. Isipokuwa wanafunzi wake tu, pamoja na wachache waliomfuata baada ya pale kutaka kufafanuliwa.
Ndugu ikiwa leo unakwenda kanisani kutimiza tu ratiba, kutazama kwaya, kuangalia watu wamevaaje, hata ukiwepo humo unasinzia, unaangalia muda utatoka saa ngapi, ni kweli utakutana na Mungu, atasema na wewe, utamwona, utahisi uwepo wake, utanena hata kwa lugha, utasisimka moyo. Lakini kumwelewa, haitakaa iwezekane. Kwasababu Mungu hajifunui kwa watu ambao mioyo yao haipo kwake.Hana utaratibu huo.
Na sio tu kanisani, hata mahali popote pale, iwe ni shuleni, kazini, nyumbani, barabarani, Mungu huwa anazungumza, anasema kwa njia mbalimbali tena kirahisi sana, Lakini hutaelewa ikiwa huna moyo wa dhati kwa Mungu wako.
Alisema hivi;;
2Nyakati 16:9 “Kwa maana macho ya Bwana hukimbia-kimbia duniani mwote, ili ajionyeshe mwenye nguvu kwa ajili ya hao, WALIOKAMILIKA MOYO KUELEKEA KWAKE…”
Alisema pia..
Mathayo 15:7 “Enyi wanafiki, ni vema alivyotabiri Isaya kwa habari zenu, akisema, 8 Watu hawa huniheshimu kwa midomo; Ila mioyo yao iko mbali nami”.
Yatupasa sasa tuondoe unafiki wa ndani, kwa kumaanisha kweli kweli kumpenda Mungu kwa moyo, ili sasa aanze kutufunulia sauti yake na kazi zake. Tukimfuata Kristo tujue kinachotupeleka kule ni Utakatifu na haki, na sio kwasababu tunashida tutimiziwe mahitaji yetu, hapo ndipo atapendezwa na sisi, na hatimaye, tutamwona kila inapoitwa leo.
Bwana akubariki.
Shalom.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312 Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > WHATSAPP-Group
Mada Nyinginezo:
YESU HAYUPO KATIKA MAZINGIRA YALEYALE TU SIKUZOTE, USIJISAHAU.
Biblia inaposema “Wote tumetenda dhambi” si inamaanisha hakuna mtakatifu duniani?
Amri zilizo ndogo alizozizungumzia Yesu ni zipi?
NIFANYE NINI ILI NIKUBALIWE NA YESU?
SWALI: Kwanini vitabu vya biblia vipo katika mtiririko ule, na sio kinyume chake?
Ni vema kufahamu kuwa mtiririko wa kibiblia wa agano la kale na agano jipya, haukuwekwa na Mungu, kwamba kianze kitabu hiki kifuate hiki, kianze cha Mwanzo kisha kifuate cha Kutoka. Hapana bali ni utaratibu uliowekwa na wanadamu, ambao kimsingi unamaudhui mazuri, na uligawanya hivyo ili kumsaidia msomaji kufahamu vizuri, kuliko vingeorodheshwa tu kila kimoja eneo lake, ingewia ngumu kwa msomaji anayependa kujifunza Biblia kuelewa kiwepesi.
Mtiririko ambao sisi tunaoutumia ni tofauti na mtiririko ambao Wayahudi wanautumia kwa vitabu vya agano la kale.
Kwa mfano mtiririko wetu (Ambao unajulikana kama mtiririko wa kiprotestanti), una vitabu 39 vya Agano la kale. Lakini mtitiriko wa Kiyahudi, una vitabu 24 kwa agano hilo hilo la kale,.
Vitabu vyetu ni kama vifuatavyo
Lakini utajiuliza kwanini biblia ya kiyahudi iwe na vitabu 24 na sio 39? Je vingine vimeondolewa? Jibu ni hapana, bali baadhi yao vilijumuishwa kama ni kitabu kimoja kwamfano.
> Vitabu viwili vya wafalme kwao ni kitabu kimoja.
> Vitabu viwili vya Mambo ya Nyakati kwao ni kitabu kimoja.
> Vitabu viwili vya Samweli kwao ni kitabu kimoja.
> Ezra na Nehemia vimeweka kama kitabu kimoja.
> Vitabu 12 vya Manabii wadogo kwao ni kitabu kimoja.
Jumla yake ni vitabu 24 Badala ya 39.
Hivyo tukirudi katika biblia yetu, yenye vitabu 39 kwa agano la kale, Orodha ile haijawekwa kulingana na vipindi vilipoandikwa, bali kulingana na ‘asili ya vitabu’. Ndio hapo utaona hiyo migawanyo mikuu mitano (Yaani vitabu vya Sheria, vya historia, vya mashairi, vya Manabii wakubwa na wale wadogo).
Kutaja manabii wakubwa haimaanishi kuwa walikuwa na vyeo vya juu au walikuwa na nguvu zaidi ya wale wengine hapana, bali ni kutokana na wingi wa uandishi wao, yaani waliokuwa na uandishi mwingi waliwekwa katika kundi hilo la manabii wakubwa.
Vipo vitabu 27, na vyenyewe pia havijaandikwa kulingana na wakati wa uandishi, japo havipishani sana na wakati wa uandishi.
Huu ndio mgawanyo wake.
Halikadhalika Nyaraka za Mtume Paulo ziliorodheshwa katika mpangilio ule kutoka na urefu wa uandishi na sio umuhimu wa nyaraka Fulani zaidi ya nyingine, kwamfano utaona kitabu cha kwanza kwa urefu cha Mtume Paulo ni Warumi na ndio kilichowekwa cha kwanza. Vilevile kirefu zaidi ya vyote alivyoviandika kwa Watu, ni cha Timotheo ndicho kilichopangiliwa cha kwanza.
Lakini pamoja na kwamba havikuweka katika mpangalio wa nyakati za uandishi bado zinamtiririko mzuri unaelekeana na historia, kuanzia kitabu cha Mwanzo mpaka ufunuo. Japo pia katika usomaji haimaanishi ufuate mtiririko huo, bali unaweza kuanza vyovyote upendavyo kwa jinsi Roho Mtakatifu atakavyokuongoza.Kwasababu hakuna sehemu yoyote katika maandiko tumewekewa mtiririko huo.
Pia zipo biblia nyingine mfano ile ya Kikatoliki yenye vitabu 73, ambayo kimsingi haijavuviwa na Roho wa Mungu kwani kuna baadhi ya vitabu vimeongezwa ambavyo hukinzana na mafundisho ya msingi ya imani, na hivyo hatupaswi kuifuata. Biblia yetu ina vitabu 66 tu. Kama vilivyoorodheshwa hapo juu. Zaidi ya hivyo hutoka kwa Yule mwovu.
Bwana akubariki sana.
Shalom.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
Tofauti kati ya maandiko na Neno ni ipi?
TABIA YA WAZI INAYOWATOFAUTISHA MANABII WA UONGO NA WALE WA UKWELI.
HISTORIA YA BIBLIA YA KING JAMES, INA FUNZO GANI KWETU?
Vitabu vya Deuterokanoni ni vya kiMungu?
VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 1
FAHAMU MAISHA YA YESU KABLA YA HUDUMA.
Mimbari ni nini? Je tofauti kati ya Mimbari na madhabahu ni ipi?
Karibu katika mafunzo ya biblia.
Kwanini tunasema kuwa hili ni kanisa la Mwisho la Laodikia?, Je ni viashiria gani vinavyotutambulisha kuwa hali ya kanisa la Laodikia lile la saba ambalo Mtume Yohana alionyeshwa kwenye Maono katika kitabu cha Ufunuo ndio hali halisi ya kanisa letu la siku za mwisho?.
Awali ya yote hebu tujikumbushe historia ya yale makanisa saba, tunayoyasoma katika kitabu cha Ufunuo Mlango wa 2 na wa 3.
Makanisa saba tunayoyasoma katika kitabu cha Ufunuo ni makanisa ambayo yalikuwa katika miji 7 tofauti tofauti. (Efeso, Smirna, Pergano, Thiatira, Sardi, Filadelfia na Laodikia, Ufunuo 1:11).
Hivyo na makanisa hayo yalijulikana kwa majina ya miji hiyo, na Yote ilikuwa inapatikana katika eneo lijulikanalo kama “Asia Ndogo” ambapo kwasasa ni nchi ya “Uturuki”.
Sasa kila kanisa lilikuwa na tabia yake, kulingana na huo mji (unaweza kusoma tabia hizo katika Ufunuo 2-3). Na kanisa la Mwisho kabisa kutajwa ambalo ndio la saba lililoitwa Laodikia lilikuwa na tabia nyingine ya kipekee ambayo kwa hiyo ndiyo tutajua kuwa kanisa letu la sasa linafanana na kanisa la huo mji au la!.
Sasa kabla ya kwenda kusoma tabia za kanisa hilo katika kitabu cha Ufunuo, hebu kwanza tuweke msingi mwingine wa kuelewa jambo lingine, ambalo litatusaidia kuelewa hili vizuri.
Katika biblia maandiko yanatabiri kuwa dalili za siku za mwisho ni Maasi kuongezeka katika kiwango cha miji ya Sodoma na Gomora, au miji ya Nyakati za Nuhu (Soma Luka 17:26-28).
Maana yake ni kuwa kama hali ya maovu haijafikia kile kiwango cha maasi ya Sodoma na Gomora, basi bado ule mwisho utakuwa upo mbali, lakini kama hali ya mji itafikia kile kiwango cha maasi ya Sodoma na Gomora basi ni wazi kuwa ule mwisho umefika.
Kwahiyo ni sahihi kusema kuwa Miji ya Sodoma na Gomora ni ishara au alama ya miji ya siku za mwisho, Hivyo tukitaka kujua kuwa tupo siku za mwisho basi tujilinganishe na miji ya Sodoma na Gomora. (2Petro 2:6 na Yuda 1:7).
Na sasa tunaona kabisa kuwa kizazi chetu ni kama kile cha Sodoma na Gomora na hata huenda kimepita, kwasababu katika miji ya Sodoma na Gomora kulikuwa na mwingiliano wa ndoa za jinsia moja..vile vile na sasa hali ni hiyo hiyo, ushoga upo kila mahali, mauaji, dhuluma n.k kwahiyo tupo siku za mwisho.
Vile vile na kanisa la Mji wa Laodikia, ambao ulikuwepo katika enzi za kanisa la Kwanza, lilikuwa ni Ishara ya kanisa la siku za mwisho. Maana yake ni kuwa tukitaka kujua kuwa tunaishi katika kanisa la mwisho, basi tunapaswa tujilinganishe kanisa letu na lile la Laodikia. Tukiona yanafanana kitabia basi tujue kuwa hili ndio kanisa la mwisho na unyakuo umekaribia.. lakini tukiona kuwa bado hatujafikia viwango vya kanisa lile basi tujue kuwa ule mwisho huenda bado sana.
Sasa hebu tusome tabia za kanisa la Laodikia katika biblia.
Ufunuo 3:14 “Na kwa malaika wa kanisa lililoko Laodikia andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye Amina, Shahidi aliye mwaminifu na wa kweli, mwanzo wa kuumba kwa Mungu.
15 NAYAJUA MATENDO YAKO, YA KUWA HU BARIDI WALA HU MOTO; INGEKUWA HERI KAMA UNGEKUWA BARIDI AU MOTO.
16 Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu.
17 Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi”.
Umeona tabia za kanisa la Laodikia?..Biblia inasema ni kanisa ambalo lilikuwa vuguvugu, si moto wala si bariki.. mfano kamili wa kanisa la wakati huu. (Kumbuka hapa tunazungumzia kanisa na si watu wa ulimwengu, watu wa ulimwengu ishara yao ni miji ya Sodoma na Gomora na sisi kanisa ishara yetu ni kanisa la mji wa Laodikia).
Kanisa la wakati huu utaona mtu mguu mmoja nje mguu mmoja ndani, leo yupo kanisani kesho disco, leo anamwabudu Bwana kesho anasikiliza miziki ya kidunia, simu yake nusu ina nyimbo za injili nusu nyimbo za kidunia, kabati lake nusu lina nguo za kujisitiri nusu lina nguo za nusu uchi, maneno yake nusu ya heshima nusu ya kihuni, biashara yake nusu ni halali nusu ni haramu, duka lake nusu lina bidhaa njema nusu lina bidhaa haramu (pombe, na sigara), leo atatoa sadaka kesho anaonga/ anaogwa.n.k
Hiyo ndiyo ilikuwa hali ya kanisa la Laodikia na ndio hali ya kanisa la Sasa tulilopo.
Hiyo ndiyo alama pekee inayotutambulisha siku si nyingi unyakuo wa kanisa utatokea. Kwasababu hakutakuwa na kanisa lingine litakalotokea lenye tabia nyingine, hili la Laodikia biblia imetabiri ndio kanisa la Mwisho baada ya hapo ni unyakuo ndio maana utaona pale, baada ya ujumbe wake kumalizika kilichofuata ni Yohana kuchukuliwa juu mbinguni.
Ufunuo 4:1 “Baada ya hayo naliona, na tazama, mlango ukafunguka mbinguni, na sauti ile ya kwanza niliyoisikia kama sauti ya baragumu ikinena nami, ikisema, Panda hata huku, nami nitakuonyesha mambo ambayo hayana budi kuwako baada ya hayo”.
Wakati kanisa hili la Laodikia limechafuka hivi, Bwana analiandaa kundi lake dogo, na kuliambia litoke huko, kama vile alivyowaokoa Nuhu na Luthu..Vile vile kanisa la Laodikia litaingia katika dhiki kuu kwasababu ni kanisa vuguvugu lakini kundi dogo ambalo litakuwa safi na litakuwa Moto na si Vuguvugu hilo litaenda na Bwana katika unyakuo.
Ndugu unyakuo umekaribia sana, Yesu yupo Mlangoni kurudi, ondoka katika uvuguvugu, wa kidunia, kuwa Moto.. Ukiamua kumfuata Kristo basi mfuate kwelikweli, usiige desturi za kidunia, ukiamua kuwa mtu wa kujisitiri fanya hivyo kikweli kweli usiwe nusu nusu, ukiamua kumfuata Yesu basi jikane kweli kweli.
Uvuguvu Kristo anauchukia kuliko hata Yule mtu aliye baridi kabisa.. kwasababu yeye mwenyewe anasema ni heri mtu awe moto au baridi kuliko vuguvugu..
Bwana atusaidie.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Jiunge na kundi letu la mafundisho ya Biblia whatsapp kwa kubofya hapa > Group-whatsapp
Mada Nyinginezo:
AGENDA KUBWA YA SHETANI KWA KANISA HILI LA LAODIKIA.
SAUTI NI SAUTI YA YAKOBO, LAKINI MIKONO NI YA ESAU.
Babewatoto ni nani katika biblia?(Isaya 34:14).
Jina la Bwana Yesu Kristo libarikiwe. Karibu tujifunze Neno la Mungu.
Kama wengi wetu tunavyojua kuwa hakuna wokovu nje ya Yesu Kristo, wala hakuna Maisha nje ya Yesu Kristo. Kama Mtume Paulo alivyoandika kwa uweza wa Roho kwamba ‘Mauti ilikuja kwa njia ya mtu mmoja(Adamu)…kadhalika uzima utaletwa kwa njia hiyo hiyo ya mtu mmoja (ambaye ni Kristo)’.
Kwahiyo yeye peke yake ndio njia iliyo sahihi na iliyothibitishwa ya kumfikia Mungu..njia nyingine zote tofauti na yeye ni za upotevu, haijalishi zina wafuasi wengi kiasi gani.
Bwana Yesu alipokuwa hapa duniani, alizungumza kwa mifano mingi, yote ni kwa lengo la kumfanya mwanadamu aelewe mpango wa Mungu juu ya Maisha yake…Alitumia mifano ya miti, mashamba, wafanyabiashara, wakulima,familia, wageni, wafalme na mingine mingi ambayo hata haijaandikwa kwenye biblia, kwasababu kama yangeandikwa mambo yote aliyoyafanya moja moja…biblia inasema hata dunia isingetosha kwa jinsi vitabu vingekuwa ni vingi (Yohana 21:25)..
Lakini tunaona baada ya kuondoka alikuja tena kuzungumza na Mtume Yohana katika maono , alipokuwa katika kisiwa kile cha Patmo na kumpa mfano namna ambayo huwa anavyowajilia watu wake alimwambia…
Ufunuo 3: 20 ‘’Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami’’.
Mfano huo Bwana Yesu aliutoa kuonyesha ujio wake kwa mtu ni kama wa mgeni…Ujio huu sio wa kulichukua kanisa…kwasababu ujio wa kuja kulichukua kanisa alisema utakuwa kama ujio wa mwizi…hata kuja kwa kugonga na kusihi, bali atakuja usiku watu wakiwa wamelala na atachukua walio wake na kuondoka….ndio maana unyakuo ukipita sio watu wote watajua…Kwahiyo kuna kipindi Bwana Yesu atakuja kama mgeni na kuna kipindi atakuja kama mwivi.
Sasa katika mfano huu..anasema tazama nasimama mlangoni nabisha! Kubisha maana yake ni kugonga mlango huku unatoa sauti Fulani kama hodii hodii!! Hiyo ndiyo maana ya kubisha!..Kwahiyo hapa Bwana anasema nasimama nabisha, halafu anasema mtu akiisikia sauti yake na kuufungua mlango ataingia…hii ikiwa na maana kuwa mtu anaweza akaisikia sauti yake na asifungue…au mtu anaweza asiisikie kabisa sauti yake…labda kutokana na kwamba amelala au kutokana na usumbufu uliopo ndani ya nyumba kuwa mkubwa (labda kelele za miziki au watu).
Na baada ya kuingia utaona anasema…’nitakula pamoja naye na yeye pamoja nami’…sasa tafakari hapo kwa makini, hasemi tutakula pamoja hapana!…bali anasema nitakula pamoja naye…na yeye pamoja nami…ikiwa na maana kuwa alipokuwa anangonga alikuja na chakula chake, hakuja mikono mitupu…kadhalika na yule mtu aliyemfungulia atamkuta na chakula chake…na hivyo kila mmoja atashiriki na mwenzake kile alichokiandaa.
Sasa ukiingia ndani Zaidi kuutafakari mfano huu utaona kuwa unahusu wakati wa jioni…lugha yetu ya Kiswahili haijajitosheleza katika maneno mengi…lakini kama ukisoma tafsiri nyingine kama zile za kiingereza au kigiriki utaelewa vizuri kuwa ni wakati wa jioni ndio Bwana alikwenda kugonga mlango.. ni wakati wa chakula cha jioni (evening supper).
Kwahiyo katika mfano huo Bwana anakuja kugonga mlango wakati wa jioni…akiwa na chakula chake, hajaja kudoea wala kula vya watu bure!…Inaashiria kuwa Kristo anapotaka kuja kuingia katika Maisha yetu sio kwa lengo la kutaka vya kwetu, au kutuharibia Maisha hapana! Bali ni kwa lengo la kutupa sisi faida. Na atakuja jioni, hizi ni nyakati za jioni, wakati wa kumalizia wa mwisho wa dunia ndugu.
Na kama tunavyojua tabia ya mgeni anapogonga, huwa hagongi mfululizo kama vile analazimisha mlango ufunguliwe…bali utaona anagonga kidogo kwa utaratibu kisha anatulia kidogo, akiona hasikiwi atarudia tena kwa sauti kidogo baada ya muda Fulani kupita..atafanya vile kwa kipindi Fulani, akiona hakuna kabisa majibu labda yule mtu amelala usingizi mzito hawezi kusikia hatavunja mlango ataondoka arudi tena baadaye au arudi wakati mwingine…Lakini akigundua yule mtu kule ndani anamsikia lakini hataki kumfungulia makusudi tu! Basi ataondoka asirudi tena…kwasababu anajua hahitajiki mahali pale.
Na Ndivyo hivyo Kristo anavyogonga mioyoni mwetu leo hii, atakutumia wahubiri pale mahali ulipo, kwa kukusihi umfungulie moyoni mwako aingie…akiona bado humsikii ataongeza watumishi kila mahali utakapokwenda hata kwenye mitandao utakutana na Neno lake, sauti yake utaisikia kila mahali ikikuita, utakapoitii ataingia, na vitu alivyokuja navyo kukuletea hutaamini macho yako kuvioona..Lakini endapo unajua kabisa huyu ni Kristo ananiita kupitia mahubiri, na kuwa hii ni sauti yake kabisa na unafanya makusudi kutokumfungulia…basi ataondoka na Neema hiyo itakwenda kwa wengine..
Ndugu usidanganyike kuwa utatubu uzeeni, Sauti ya Mungu itarudia kuita kwa wale watu ambao wakati Bwana amegonga wapo usingizini…wale watu ambao nguvu za giza zimewafunga kiasi kwamba hawawezi kuisikia injili…hao ndio Bwana ataendelea kuwaita kila wanapokwenda, mpaka watakapoamka usingizini, na kundi hili mara nyingi ni lile kundi ambalo halijawahi kabisa kupata nafasi ya kuujua msingi wa Imani ya kikristo, wale watu ambao wamezaliwa katika familia za kipagani, au familia za watu wasio wa dini, na hawamjui Kabisa Kristo…hawa ni sawa wapo usingizini au wapo kwenye makelele ya ulimwengu kiasi kwamba hawawezi kuisikia sauti ya Bwana Yesu..Hivyo Bwana ataiongeza sauti yake mpaka wasikie.Watapata Neema kubwa Zaidi.
Lakini kwa wengine ambao wamezaliwa katika Ukristo tangu udogoni, wamehubiriwa vya kutosha kuhusu msalaba, na wanaielewa kabisa sauti ya Yesu inapoita, na wengine mpaka wamemwona Bwana katika maono, na wamepewa ishara kadha wa kadha, Bwana akiwaita na hawataki kusikia…Kristo ataondoka kwao na asirudi tena kamwe. Wengi hawapendi kusikia hivi lakini huu ndio ukweli maandiko yanasema hivyo..Wana wa Israeli Taifa la Mungu yaliwatokea hayo, si Zaidi watu wa mataifa.. Bwana Yesu aliwaambia waisraeli maneno haya, baada ya kuwaonya mara nyingi na kushupaza shingo zao haya ndio aliyowaambia:
Mathayo 23:37 ‘’Ee Yerusalemu, Yerusalemu, uwauaye manabii, na kuwapiga kwa mawe wale waliotumwa kwako! Ni mara ngapi nimetaka kuwakusanya pamoja watoto wako, kama vile kuku avikusanyavyo pamoja vifaranga vyake chini ya mabawa yake, lakini hamkutaka!
38 Angalieni, nyumba yenu mmeachiwa hali ya ukiwa.
39 Kwa maana nawaambia, HAMTANIONA KAMWE TANGU SASA, hata mtakaposema, Amebarikiwa ajaye kwa jina la Bwana’’.
Aliwaambia ‘’hamtaniona kamwe tangu sasa’’..Hili Neno ni kali sana na linaumiza…’’kutengwa na Mungu milele’’..Si ni afadhali tutengwe na wanadamu kuliko Mungu…Ni heri wanadamu wote wanichukie na kunitenga lakini sio Mungu, ni heri nichokwe na wanadamu wote lakini sio Mungu.
Hebu tafakari leo hii Kristo anakwambia haya maneno ‘HUTANIONA TENA KAMWE TANGU SASA’!!!…Yaani wewe na Kristo ndio Basii!!…
Leo hii usikiapo maneno haya kwenye mtandao, na bado hutaki kuacha dhambi na ulimwengu, kumbuka haukuwa mpango wa Mungu usikie injili yake kwa njia hii ya mitandao..Mpango wake ulikuwa siku ile ile ulipoisikia injili kwa mara ya kwanza ulipohubiriwa na mtu aliyeshika biblia mkononi ungeamini, kulikuwa hakuna sababu ya wewe kuja kusikia tena injili hapa……lakini kwasababu Moyo wako ulikuwa mgumu, ndio maana amekufuata kwa njia nyingine hii ya mtandao..ili awe na uhakika kabisa unaisikia sauti yake. Lakini unaidharau..pengine hii ndio sauti yake ya mwisho kwako, isikie ufungue, asije akakwambia kama alivyowaambia wayahudi ‘HUTANIONA TENA KAMWE TANGU SASA’….Maneno haya yalizungumzwa na Kristo yule yule aliyesema ‘njooni kwangu nyinyi nyote’….hapa anasema ‘hamtaniona tena kamwe’…sehemu nyingine anasema ‘tokeni kwangu’.
Pale ulipo mwambie Bwana natubu dhambi zangu zote, na kukusudia kutokuzifanya tena, tubu kabisa kwa kudhamiria kabisa kuacha kuzifanya.Mfungulie mlango na yeye ataingia ndani yako haraka kukugeuza, hataanza kukulaumu kwanini nimegonga muda wote huo ukufungua, yeye si kama sisi, moja kwa moja atazungumza na wewe na muda wa kula ukifika atakufungulia hazina zake alizokuletea mshiriki pamoja, atakupa baraka zote za mwilini na rohoni, na kukufundisha maneno yake ya uzima. Utakuwa na tumaini la uzima wa sasa na ule wa baadaye.
Lakini usipotaka ataondoka, na siku moja atakuja kama mwivi, siku hiyo hatokuja kwako tu bali atakuja kwa ulimwengu mzima, atavunja atavunja mlango na kuwaiba waliowake ndani, na kwenda nao mbinguni, huku nyuma moto utawaka. Usitamani uwepo hicho kipindi cha dhiki kuu. FIKIA TOBA LEO!
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe au piga namba hii +255 789 001 312 Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > WHATSAPP-Group
Ni maombi yangu kuwa utakitendea kazi ulichokisikia. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Zinazoendana:
USIMFANYIE JEURI ROHO WA NEEMA.
UMEIZALIA MATUNDA MIAKA 4 YA NEEMA ULIYOPEWA?
JINSI YA KUITUMIA VYEMA NEEMA YA MUNGU ILIYO JUU YANGU.