Je Malaika wana viongozi?.

Je Malaika wana viongozi?.

Swali: Je Malaika watakatifu walioko mbinguni wanao uongozi, kama sisi wanadamu tulivyo na viongozi wanaotuongoza?.


Jibu: Kama vile sisi binadamu tulivyo na Uongozi duniani biblia inatuonyesha pia Malaika wanao uongozi mbinguni,  maana yake wapo walio viongozi na wasio viongozi.

Kwa mfano tukisoma kitabu cha Ufunuo 12, tunaona Mikaeli anatajwa akiwa pamoja na malaika zake, hiyo ni kuonyesha kuwa Mikaeli ni kiongozi.

Ufunuo 12:7 “Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake;

8 nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni”.

Soma pia Yuda 1:9, utaona Mikaeli anatajwa tena kama Malaika Mkuu..

Na pia wakati ule Yoshua anakutana na yule Malaika wa Bwana baada ya kuvuka Yordani, Malaika yule alijitambulisha kuwa ni AMIRI wa jeshi la Bwana…Sasa Amiri maana yake ni kiongozi wa jeshi.

Yoshua 5:13 “Ikawa hapo Yoshua alipokuwa karibu na mji wa Yeriko, akavua macho yake na kuangalia, na tazama, mtu mume akasimama kumkabili mbele yake, naye alikuwa na upanga wazi mkononi mwake; Yoshua akamwendea, na kumwambia, Je! Wewe u upande wetu, au upande wa adui zetu?

14 Akasema, La, lakini nimekuja sasa, nili amiri wa jeshi la BWANA. Yoshua akapomoka kiusouso hata nchi, naye akasujudu, akamwuliza, Bwana wangu aniambia nini mimi mtumishi wake?

15 Huyo amiri wa jeshi la BWANA akamwambia Yoshua, Vua viatu vyako miguuni mwako; kwa kuwa mahali hapo usimamapo ni patakatifu. Yoshua akafanya vivyo”

Hivyo huyu Malaika alikuwa ni kiongozi wa Malaka wengine wa vita mbinguni, ndio maana akajitambulisha kama “Amiri”.

Lakini pamoja na kwamba upo uongozi katikati ya Malaika, hiyo bado haiwafanyi waabudiwe au wasujudiwe au kusifiwa.

Anayestahili kusifiwa na kusujudiwa duniani na mbinguni ni MUNGU peke yake.

Wakolosai 2:18 “Mtu asiwanyang’anye thawabu yenu, kwa kunyenyekea kwa mapenzi yake mwenyewe tu, NA KUABUDU MALAIKA, akijitia katika maono yake na kujivuna bure, kwa akili zake za kimwili”.

YESU KRISTO anarudi mwamini na mtumikie.

Shalom.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments