Isaka, alipofika mahali panaitwa Gerari alivikumbuka visima vilivyochimbwa na baba yake Ibrahimu zamani, lakini alipotazama na kuvikuta vimeharibiwa, alianza kazi ya kuvichimba tena, Alipokifukua cha kwanza na kutoa maji maandiko yanatuambia wachungaji wa mahali pale wakakigombania..
Akakiita Eseki, akasogea mbele kodogo akakichimbika Kingine tena nacho kikagombaniwa akikiita Sitna, akasogea tena Mbele akachimba kingine cha tatu..
Hicho hawakukigombania akakiita..Rehobothi
Kisha akasema..Kwa kuwa sasa BWANA ametufanyia nafasi, nasi tutazidi katika nchi.
Mwanzo 26:18-22
[18]Isaka akarudi akavichimbua vile visima vya maji walivyovichimba siku za Ibrahimu babaye; maana wale Wafilisti walikuwa wamevifukia baada ya kufa kwake Ibrahimu; naye akaviita majina kufuata majina alivyoviita babaye. [19]Watumwa wa Isaka wakachimba katika lile bonde, wakapata kisima cha maji yanayobubujika. [20]Wachungaji wa Gerari wakagombana na wachungaji wa Isaka wakisema, Maji haya ni yetu. Ndipo akakiita jina la kile kisima Eseki, kwa sababu waligombana naye. [21]Wakachimba kisima kingine, wakagombania na hicho tena. Akakiita jina lake Sitna. [22]Akaondoka huko akachimba kisima kingine, wala hicho hawakukigombania. Akakiita jina lake Rehobothi, akasema, Kwa kuwa sasa BWANA ametufanyia nafasi, nasi tutazidi katika nchi.
[18]Isaka akarudi akavichimbua vile visima vya maji walivyovichimba siku za Ibrahimu babaye; maana wale Wafilisti walikuwa wamevifukia baada ya kufa kwake Ibrahimu; naye akaviita majina kufuata majina alivyoviita babaye.
[19]Watumwa wa Isaka wakachimba katika lile bonde, wakapata kisima cha maji yanayobubujika.
[20]Wachungaji wa Gerari wakagombana na wachungaji wa Isaka wakisema, Maji haya ni yetu. Ndipo akakiita jina la kile kisima Eseki, kwa sababu waligombana naye.
[21]Wakachimba kisima kingine, wakagombania na hicho tena. Akakiita jina lake Sitna.
[22]Akaondoka huko akachimba kisima kingine, wala hicho hawakukigombania. Akakiita jina lake Rehobothi, akasema, Kwa kuwa sasa BWANA ametufanyia nafasi, nasi tutazidi katika nchi.
Sauti ya Mungu nyuma ya habari hii ni nini?
Fahamu ukishaokoka, kuna kisima cha maji ya uzima kinapandwa ndani yako na Yesu Kristo mwenyewe. Kisima hiki licha ya kukupa uzima wa milele..lakini kina kazi ya kukupa raha, kukustawisha na kukufanikisha, maisha yako hapa duniani na mbinguni.
Yohana 7:38
[38]Aniaminiye mimi, kama vile maandiko yalivyonena, mito ya maji yaliyo hai itatoka ndani yake.
Anasema tena..
Yohana 4:14
[14]walakini ye yote atakayekunywa maji yale nitakayompa mimi hataona kiu milele; bali yale maji nitakayompa yatakuwa ndani yake chemchemi ya maji, yakibubujikia uzima wa milele.
Lakini ni kazi ya adui kukifukia kisima hicho, na hatimaye uwe mkavu kabisa usione raha ya wokovu au matunda yoyote ya imani yako ndani ya Kristo.
Hapo mwanzo ulikuwa ni moto rohoni, ulikuwa unaweza kuomba, kusoma Neno, Bwana alijifunua kwako kwa viwango vya juu..Ukitembea uliuhisi uwepo wa Roho Mtakatifu karibu na wewe…lakini sasa huhisi chochote,huwezi tena kuomba, kushuhudia n.k ukiona hivyo fahamu kuwa kisima kimefukiwa…lakini tumaini ni kuwa maji yapo chini waweza kuanza tena kuchimba na kurudia viwango vyako vya juu hata na zaidi..
Ulirudi nyuma, mpaka ukafikia hatua ya kuyatenda yale machafu ya dunia uliyoyaacha, Ukahisi kama Mungu hawezi kukusamehe tena…ukweli ni kwamba tumaini lipo, anza tu kukichimba kisima chako, maji utayaona.
Ulikuwa na maono mazuri, Na shauku ya kufikia hatma yako, ulikuwa unaona mwendelezo mzuri wa kile ulichokuwa unakifanya hata katika magumu hukutukisika lakini yale maono yamekufa, huelewi ni nini kimetokea, ujue kisima kimefukiwa…anza Upya tena.
Ila ni lazima ukubali kuchukua hatua bila kukata tamaa..Ilimgharimu Isaka visima vitatu lakini hakukata tamaa, hata alipofukua cha kwanza alisumbuliwa, akaendelea tena na tena…alipofikia cha tatu..ambacho ni Rehobothi..basi ikawa ni pumziko lake la daima.
Sisi kama watoto wa Mungu ni Lazima tujue adui ana wivu na hapendi kuona chemchemi za uzima na mafanikio zinabubujika ndani yetu…atafanya juu chini kuhakikisha vinafukiwa na hatimaye kutoona matokeo yoyote ya wokovu kwenye maisha yetu, na wakati huo sio mpango wa Mungu ..ataleta majaribu, misuko-suko, tufani n.k. Lakini ukistahimili Mpaka mwisho utashinda..na hatimaye utakaa mahali pa kudumu pa raha yako kama Isaka..
Ufanye nini?
Anza sasa kujizoesha kwa nguvu kusoma Neno, hata kama mwili hautaki, omba, hudhuria Mikesha acha uvivu, jitenge na dhambi zote. Na hatimaye utaona mwanzo mpya tena wenye nguvu rohoni mpaka mwilini.
Chimba kisima chako
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >>
https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Mafundisho mengine:
Uzao wa Ibrahimu unamilikije mlango wa adui? (Mwanzo 22:17)
Je yale Makabila kumi na mawili ya Israeli, kila kabla lilikuwa na kazi gani maalumu?
Huyu “Yeye ashindaye” Ni mtu mmoja maalumu au wengi?
Print this post