Shalom, karibu tujifunze maneno ya uzima.. Lipo swali ambalo linaulizwa na watu wengi, kwamba kama Mungu anajua kuna jambo litakwenda kutokea mbeleni ambalo litanisababishia mauti, kwanini basi asinizuie kwenda kulifanya badala yake ananiacha mpaka naingia, na mwisho wa siku napotea na kwenda kuzimu? Mbona kama vile atakuwa sio Mungu wa upendo?
Kama na wewe swali hili lipo ndani yako basi tuzidi kutafakari pamoja somo letu la leo,
Kitabu cha Mithali kinasema..
“Kwa kuwa mtego hutegwa BURE, Mbele ya macho ya ndege ye yote”.( Mithali 1:17).
Embu jiulize, mtu anayetega mtego wa kumshika ndege kwa ajili ya kitoweo chake, Je! Unadhani Mungu hampendi ndege yule? Au unadhani Mungu hajampa uwezo wa kuwakimbia maadui zake kiwepesi?
Au mtu anayetega mtego wa kunasa panya, unadhani Mungu anawachukia panya, na hivyo kawaondolea uwezo wa kuwakimbia adui zao?
Au mtu anayetega ndoano kuvua samaki, unadhani Mungu hawapendi samaki wake,?
Sikuzote mpaka umeona kitu fulani kinaundiwa mitego, basi ujue kuwa kitu hicho kilishashindikana kukamatika kwa njia rahisi, au ya kawaida, hivyo kimetafutiwa njia mbadala, kwamfano leo hii unaweza kumuona ndege katua hapo pembeni yako, hatua kadhaa tu pembeni, lakini embu kajaribu kwenda kumkamata kwa mikono yako kama utaweza,? Au umwone panya anakatiza kwenye kona ya nyumba, au store, halafu fanya mazoezi ya kwenda kumkata kwa mikono kama vile unavyokamata chura uone kama itakuwa ni kazi rahisi kwako.
Au umwone samaki anaelea juu ya maji, hivyo unatakwenda kwenda kumchota haraka kwa mikono yako, jaribu zoezi hilo kama litakuwa rahisi. Huwezi kuwapata kwasababu Mungu tayari kashawekea uwezo ndani yao wa kujiangua kutoka kwa maadui zao kivyepesi sana.. na wenyewe wanajua kabisa maadui zetu ni ngumu kutushika kwasababu hawana wepesi tulionao sisi, au hawana uhodari tulionao sisi wenyewe.. Na sisi tunaowawinda tunajua kuwa ili waendelee kuwa salama ni wajibu wao, kutotuamini sisi kwa kitu chochote siku zote za maisha yao hapa duniani, haijalishi tutawavutia kwa vitu vingi kiasi gani wanavyovipenda.
Vivyo hivyo na sisi wanadamu, Mungu ameshatupa uwezo mkubwa sana ndani yetu wa kumshinda adui yetu shetani, na yeye analijua hilo, hawezi kuja na kukukamata hivi hivi kama anavyotaka, hana uwezo huo, anajua kabisa hawezi kukupata, lakini anachokifanya ni kijiundia mitego yake mbalimbali, ambayo hiyo ikishakunasa, basi hapo ndipo anakuwa na uwezo wa kukufanya chochote anachotaka ikiwemo hata kukuua.
Kwamfano mtego mmojawapo maarufu , ni uasherati, shetani anaweza kukuletea kahaba, ili mkazini, lengo lake sio ukutane na kahaba au uzini tu halafu basi, hapana, bali ni ukosane na Mungu wako kwa kitendo hicho, ili apate nafasi ya kuyaachilia mapepo yake yaingie katika maisha yako kukuharibu kirahisi katika kila nyanja, ikiwemo upate na magonjwa ya zinaa kama vile ukimwi ili ufe kabla ya wakati wako.
Lakini hayo anajua hayawezi kuja hivi hivi, ni mpaka akuwekee mtego, ndipo hapo anakuletea kahaba mzuri, au mwanaume mwenye pesa, anakulaghai na wewe bila kufikiri kuwa ule ni mtego umewekwa mbele yako unakwenda kuuva, ukidhani kuwa Mungu atakuepusha nao.. Hilo Mungu hawezi kulifanya ndugu yangu.
Kwa nafasi yako soma kitabu cha Mithali sura ya 7 yote, uone jinsi, kijana mpumbavu aliyetegwa na mwanamke mzinzi, na hatma yake inavyokuwa; hatuwezi kusoma vyote lakini vile vifungu vya mwisho mwisho vinasema..
Mithali 7:21 “Kwa maneno yake mengi na ulaini akamshawishi, Kwa ubembelezi wa midomo yake akamshinda. 22 Huyo akafuatana naye mara hiyo, KAMA VILE NG’OMBE AENDAVYO MACHINJONI; Au mpumbavu kuadhibiwa katika pingu; 23 Hata mshale umchome maini; KAMA NDEGE AENDAYE HARAKA MTEGONI; Wala hajui ya kuwa ni hasara ya nafsi yake. 24 Basi, wanangu, nisikilizeni sasa, Mkayaangalie maneno ya kinywa changu. 25 Moyo wako usizielekee njia zake, Wala usipotee katika mapito yake. 26 Maana amewaangusha wengi waliojeruhi, Naam, JUMLA YA WALIOUAWA NAYE NI JESHI KUBWA. 27 Nyumba yake ni njia ya kwenda kuzimu, Hushuka mpaka vyumba vya mauti.
Mithali 7:21 “Kwa maneno yake mengi na ulaini akamshawishi, Kwa ubembelezi wa midomo yake akamshinda.
22 Huyo akafuatana naye mara hiyo, KAMA VILE NG’OMBE AENDAVYO MACHINJONI; Au mpumbavu kuadhibiwa katika pingu;
23 Hata mshale umchome maini; KAMA NDEGE AENDAYE HARAKA MTEGONI; Wala hajui ya kuwa ni hasara ya nafsi yake.
24 Basi, wanangu, nisikilizeni sasa, Mkayaangalie maneno ya kinywa changu.
25 Moyo wako usizielekee njia zake, Wala usipotee katika mapito yake.
26 Maana amewaangusha wengi waliojeruhi, Naam, JUMLA YA WALIOUAWA NAYE NI JESHI KUBWA.
27 Nyumba yake ni njia ya kwenda kuzimu, Hushuka mpaka vyumba vya mauti.
Ndege anayenaswa kwenye mtego ni kajitakia mwenyewe na sio kwamba alikuwa ni dhaifu, tamaa zake ndizo zilizompeleka pale,. Leo hii, unapojikuta kwenye matatizo mazito, ambayo unajua kabisa ni kwasababu ya dhambi Fulani uliyoifanya ndio yakakukuta, usianze kumlaumu Mungu ni kwanini hakukuepusha nayo hapo kabla. Mungu alishakupa uwezo huo tangu zamani, Na Mungu naye hawezi kumlaumu shetani, kwasababu shetani naye analo la kujitetea, anasema mimi sikumuita mtu aje kwenye mtego wangu, wala sikumlazimisha mtu, kufuata kile nilichokiweka kwenye mtego, ni yeye mwenyewe alinifuata, ni ndio hapo akanasikia akaangamia, ilikuwa ni wajibu wake kuchukua tahadhari anapoishi duniani.
Na ndio maana biblia inasema..
Hosea 4: 6 “Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa;..”
Tukikosa maarifa ya kuzijua njama za shetani, au kuyajua mafumbo ya shetani, tutajikuta tunaingia katika matatizo ambayo tutajiuliza ilikuwaje kuwaje tumejikuta hapa,
Ufunuo 2:24 “Lakini nawaambia ninyi wengine mlioko Thiatira, wo wote wasio na mafundisho hayo, WASIOZIJUA FUMBO ZA SHETANI, kama vile wasemavyo, Sitaweka juu yenu mzigo mwingine. 25 Ila mlicho nacho kishikeni sana, hata nitakapokuja”.
Ufunuo 2:24 “Lakini nawaambia ninyi wengine mlioko Thiatira, wo wote wasio na mafundisho hayo, WASIOZIJUA FUMBO ZA SHETANI, kama vile wasemavyo, Sitaweka juu yenu mzigo mwingine.
25 Ila mlicho nacho kishikeni sana, hata nitakapokuja”.
Hivyo kila mmoja anao wajibu wa kupata maarifa sahihi ya kuitambua mitego ya adui. Na maarifa hayo utayapata kutoka katika Neno la Mungu tu basi, biblia imejaa siri za kuepukana na hila za adui. Na ndio maana shetani hapendi watu waisome.
Kuwa msomaji wa biblia kila siku, tafakari , usiisome kama gazeti, hiyo tu ndio itakayokuwa nuru yako katika zama hizi za kumalizia, kumbuka mitego ni mingi, vishawishi ni vingi, na ipo ya aina tofauti toauti, uwezo umepewa, pengine umepungukiwa tu na maarifa. Hivyo ni wajibu wako kuyatafuta maarifa hayo, ambayo utayapata katika Neno la Mungu. Yaani BIBLIA.
Hakuna jaribu lolote linalotendeka leo hii, ambalo halijawahi kuandikwa katika biblia na njia ya kuepukana nalo., Hivyo jijengee desturi ya kusoma Neno la Mungu. Ili usiwe wa kumlaumu Mungu, kwanini hiki, kwanini kile, wakati ni wewe mwenyewe uliyakataa maarifa, hivyo ukanasika kirahisi.
Bwana akubariki.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
UFUNUO NI NINI, NA NITAPOKEAJE UFUNUO KUTOKA KWA MUNGU?
ZIFAHAMU HUDUMA KUU (10) ZA SHETANI DUNIANI.
Uga ni nini? Na kazi yake ni ipi kibiblia?
TAZAMA, NASIMAMA MLANGONI.
Kwanini Mungu awachome watu kwenye ziwa la moto na hali yeye ndiye aliyewaumba?
JINA LAKE KWA KIEBRANIA NI ABADONI, NA KWA KIYUNANI NI APOLIONI.
Rudi nyumbani
Print this post
Ufunuo ni kitu kilichofunuliwa.. Maana yake ni kwamba kilikuwa kimefichika/kimefichwa sasa kimefunuliwa.
Tunaposoma maandiko na kupata kitu kipya ambacho hatukuwa tunakijua hapo kwanza, hapo ni sawa na hicho kitu kimefunuliwa kwetu.
Kwamfano unaposoma biblia kuhusu damu ya Yesu, na ukagundua kitu kipya kuhusu damu hiyo, hicho ulichokipata ndio ufunuo. Sasa hicho ndicho kinachoelezea ukubwa wa Imani yako, Ukipata kujua/kugundua kitu kikubwa zaidi kuhusu damu ya Yesu, ndivyo Imani yako inavyozidi kuwa kubwa. Maana yake ni kwamba kwa ufunuo huo unaweza kutatua matatizo makubwa ya kiroho, au kufanya mambo makubwa, tofauti na yule mtu ambaye bado hajapata ufunuo wowote kuhusu damu ya Yesu.
Na maneno mengine yote ya Mungu ni hivyo hivyo, Ukipata kugundua kitu cha kipekee kumhusu Yesu, ambacho hapo kwanza ulikuwa hukijui.. Hicho ulichokigundua ndicho shetani kinachomwogopesha na ndicho hicho kinachoweza kukupa matokeo makubwa ya rohoni.Na kugundua huko kunaletwa na Roho Mtakatifu mwenyewe ndani ya mtu.
Sasa Ufunuo upo wa uongo, na Pia upo wa ukweli.
Unaweza kusoma neno ukapata kitu au ukagundua kitu ambacho ulikuwa hujakijua hapo kwanza.. Sasa hicho kitu ulichokigundua kama ni cha ukweli (maana yake kama kimetokana na Mungu kupitia Roho wake Mtakatifu) basi kitakubaliana na mistari mingine au habari nyingine za kwenye biblia.
Lakini kama si cha ukweli basi kitakinzana na mistari mingine ya biblia. Maana yake si cha kukipokea wala kukiamini.
Sasa ni kwa namna gani tutapokea Ufunuo?. Zipo njia kuu Mbili.
Wengi hawapendi kulisoma Neno la Mungu wao binafsi, na badala yake wanapenda kufundishwa, au kutazama filamu fulani tu za kikristo, Lakini pasipo kujua kuwa kuna hatari kubwa sana ya kudanganywa kama usipojijengea tabia ya kulisoma mwenyewe Neno.
Kwasababu wanaofundisha uongo ni wengi kuliko wanaofundisha ukweli. Bwana Yesu alisema Njia ni nyembamba, maana yake mimi na wewe hakuna namna tunaweza kuifanya iwe nene, na alisema Manabii wengi wa uongo watatokea watawadanganya hata yamkini walio wateule, hakuna namna tunaweza kuwafanya wawe wachache hawa manabii wa uongo. Kwahiyo Njia itakayobakia kuwa bora siku zote ni ile ya mtu binafsi kutafuta kulisoma Neno yeye binafsi maadamu anao uwezo wa kusoma na kuandika. Na hapo hapo Roho Mtakatifu anapata nafasi ya kumfunulia maandiko.
Na kumbuka tunapozungumzia kusoma Neno hatumaanishi kwenda kuchukua mstari mmoja hapa kwenye Mathayo na kisha kwenda kuruka kutafuta mstari mwingine wa faraja kwenye Isaya, Na kurudi kuunganisha mwingine kwenye Yeremia..na hivyo kujikuta kwa siku umesoma mistari mia, tofauti tofuati kwa masaa mawili na kujipongeza kuwa umelisoma Neno..Nataka nikuambia hapo utakuwa hujasoma biblia bali umeiperuzi biblia, wanaoiperuzi biblia ni wahubiri, na wanafanya hivyo kwa lengo la kufundisha, somo lipate kueleweka kwa muda mfupi. Hivyo wewe usiiperuzi biblia, hutaelewa chochote na wala hutapata kitu cha kudumu cha kukusaidia roho yako.
Kusoma Neno kunakofaa ni huku, kushika kitabu kimoja kimoja…kukisoma chote pasipo kuruka…sio lazima ukisome chote kwa siku moja hapana, Mfano unaweza kuanza kusoma kitabu cha Mwanzo, sura 10 za kwanza na kisha kupata muda mrefu wa kuzitafakari, na hata kuzirudia tena hizo mpaka utakapoona umeelewa vya kutosha kusonga mbele.. lakini ukisoma sura 4, 5 ukafika sehemu inazungumzia vizazi ukaboreka na kisha ukarukia kitabu cha kutoka hutakaa uielewe biblia..
Soma kitabu cha Mwanzo chote kimalize, haijalishi itakuchukua wiki au mwezi, kisha nenda kitabu kinachofuata… Ukifanya hivyo utaielewa biblia sana, na Ndio chanzo kikubwa cha KUPATA UFUNUO WA KWELI wa Neno . Na pia unaposoma biblia, hakikisha unafungua kule nyuma kwenye ramani, uielewe pia ramani kama biblia yako inayo ramani..fuatilia kwenye ramani zile hatua Ibrahimu alizopita, Wana wa Israeli walizopita, miji Bwana Yesu aliyokuwa anatembea n.k.
Sasa kama tulivyotangulia kusema, Kuna hatari kubwa sana katika kutegemea njia hii kupata ufunuo wa Neno la Mungu. Lakini njia hii ikitumika sahihi pia ni rahisi kupata mengi.
Sasa njia bora sio kufungulia redio au internet na kwenda kusoma au kusikiliza mahubiri yanayoendelea kila siku, na huku huna habari kabisa na biblia yako, hapo nakuambia utakwenda na maji, haijalishi mhubiri huyo umemwamini kiasi gani.
Njia bora ni ya kupata ufunuo wa Neno la Mungu kupitia watumishi wa Mungu, ni wewe kwenda kusoma Neno kwanza, labda mada fulani katika biblia.. Na kisha ukishaisoma hiyo mada na ukaielewa, isipokuwa kuna vipengele vichache ambavyo hukuvielewa na ungehitaji kuviongezea maarifa, ndipo unamtafuta Mtumishi na kumuuliza kulingana na ile mada uliyoisoma, au unakwenda katika internet na kukitafuta kitu kile, uone maoni ya watumishi mbali mbali kuhusu jambo hilo.
Hiyo ni njia bora ambayo itakusaidia kutokudanganywa kirahisi, kwasababu utakuwa unakwenda kutafuta kujua kitu ambacho tayari una ufahamu nacho angalau kidogo, hivyo ni ngumu kudanganyika…Kamwe usiende kutafuta kuuliza kitu ambacho hata wewe mwenyewe hujui kinapatikana wapi kwenye biblia.
Ni sawa umekwenda kwenye mji uliochanganyikana kama Kariakoo, na kuanza kuuliza uliza, bila ya wewe kuwa na angalau taarifa ndogo ya kile unachokitafuta au unakokwenda, kwasababu kama hujui kabisa ni rahisi kutapeliwa na kupoteza kila kitu ulichonacho..Unaweza kuomba kuelekezwa benki ukaelekezwa kichochoro cha vibaka, ukaibiwa kila kitu hata nauli uliyokuwa umebakiwa nayo.
Ndio maana Bwana Yesu alisema katika Luka..
Luka 8:8 “Jiangalieni basi jinsi msikiavyo; kwa kuwa mwenye kitu atapewa, na yule asiye na kitu atanyang’anywa hata kile ambacho anadhaniwa kuwa nacho.”
Bwana anatuonya tujiangalie jinsi TUNAVYOSIKIA. Maana yake ukienda kutafuta kusimuliwa vitu bila wewe mwenyewe kutafuta kusoma kile kitu kwanza, angalau kidogo, kuna hatari kubwa ya wewe kupoteza kila kitu hata kile kidogo kizuri ulichokuwa nacho moyoni mwako. Ni rahisi hata kama kulikuwa na kitu cha ukweli moyoni mwako, ni rahisi kukipoteza hicho, Kwasababu utakayekutana naye kama atakuwa ni mwalimu au nabii wa uongo, atakutoa kabisa kwenye mstari (huko ndio kunyang’anywa hata kile kidogo ulicho nacho).
Kwamfano unakwenda kumuuliza Mwalimu/Nabii (wa uongo) kuhusu habari fulani kwenye biblia ambayo ulisikia tu watu mtaani wakisimuliana, ili hali wewe hujawahi hata kwenda kuifuatilia kwenye biblia inasemaje, yule nabii atakudanganya, na wewe utamwamini..na zaidi ya hayo, kama pia kama ulikuwa unaamini kuwa si sahihi kuoa wake wengi, huyo nabii atakupa maandiko na maandiko pia ya kukuambia ni ruksa kuoa wake wengi, na wewe utamwamini. Pasipo kujua kuwa tayari umeshanyang’anywa hata kile kidogo ulicho nacho.
Roho Mtakatifu anataka kutufundisha mengi, lakini sisi ndio hatutaki kumpa nafasi ya yeye kutufundisha, kwasababu tunakuwa wavivu wa kusoma (Waebrania 5:11). Tujitahidi kumpa nafasi.
Bwana atubariki.
Kama hujampokea Yesu, Basi fahamu kuwa ANARUDI.
Waebrania 10:37 “Kwa kuwa bado kitambo kidogo sana, Yeye ajaye atakuja, wala hatakawia”.
Hivyo mkaribie leo naye atakukaribia.
JIFUNZE NENO LA MUNGU KWA BIDII ZOTE.
MWILI NA DAMU YA YESU KRISTO.
VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 10 (Kitabu cha Zaburi).
CHUKIZO LA UHARIBIFU
Uga ni sakafu ya kupuria/kupepetea nafaka iliyotumika zamani.
Ikumbukwe kuwa zamani, hawakuwa na mashine za kupuria kama tulizonazo sasahivi baadhi ya sehemu, ilikuwa nafaka ikishatolea shambani, na majani yake, ilipelekwa moja kwa moja kwenye sakafu hii maalumu iliyonyooka ambayo ilijengwa kwa mawe, au juu ya ardhi ngumu,..Karibu kila shamba lilikuwa ni lazima liwe na sakafu yake maalumu kama hii, na kama shamba ni dogo, basi waliungana wawili au watatu kushea Uga mmoja.
Tazama picha juu,
Sasa nafaka ilipokuwa ikipelekwa pale, hatua ya kwanza, ilimwagwa kwenye Uga huo, kisha wanyama, kama Ng’ombe, au Punda, au Farasi, walipitishwa juu ya nafaka hiyo kuikanyanga kanyaga..Na lengo la kufanya hivyo ni kuyalegeza magamba magumu yaliyoishikilia nafaka.
Sehemu nyingine walitumia fimbo badala ya wanyama, na kuzichapa kama vile wanavyochapa maharage au mbaazi, katika baadhi ya sehemu tunazoishi, vivyo hivyo katika enzi za biblia hususani kipindi kile cha Ruthu.
Sasa baada ya hatua hiyo, kilichofuata, ilikuwa ni kupepeta ili kuondoa hayo makapi yaliyochanganyikana na nafaka.. Hivyo walitumia kifaa maalumu kilichoitwa pepeto.. pepeto lililotumika wakati ule, halikuwa kama hili la kwetu, la chekecheke, hapana, bali lilikuwa ni beleshi fulani ambalo mbeleni lina mdomo kama wa uma, au rato.
Hivyo walichokifanya ni kupitisha pepeto hilo katikati ya mchanganyiko huo wa nafaka na makapi, na kurusha juu, waliporusha juu, yale makapi yalichukuliwa na upepo na nafaka kurudi chini, na hivyo, wanairudia hatua hiyo, tena na tena na tena..mpaka nafaka peke yake ibaki chini kwenye ile sakafu. (Uga)
Kisha inaichotwa na kwenda kusagwa ajali ya matumizi ya nyumbani.. Hayo ndiyo yalikuwa matumizi ya Uga.
Unaweza kulisoma neno hilo katika vifungu hivi baadhi;
Ruthu 3:1 “Kisha Naomi akamwambia mkwewe, Je! Mwanangu, si vizuri nikutafutie raha, ili upate mema? 2 Basi na huyu Boazi, je! Siye wa mbari yetu, ambaye ulikuwapo pamoja na wasichana wake? Tazama, usiku wa leo atakuwa akipepeta shayiri pale ugani. 3 Basi wewe oga, ujipake mafuta ujivike mavazi yako, kisha uende kwenye uga; walakini usijionyeshe kwake mtu yule, ila atakapokwisha kula na kunywa”.
Ruthu 3:1 “Kisha Naomi akamwambia mkwewe, Je! Mwanangu, si vizuri nikutafutie raha, ili upate mema?
2 Basi na huyu Boazi, je! Siye wa mbari yetu, ambaye ulikuwapo pamoja na wasichana wake? Tazama, usiku wa leo atakuwa akipepeta shayiri pale ugani.
3 Basi wewe oga, ujipake mafuta ujivike mavazi yako, kisha uende kwenye uga; walakini usijionyeshe kwake mtu yule, ila atakapokwisha kula na kunywa”.
Soma pia kwa wakati wako, Ruthu 3:6,14, 1Nyakati 13:9, Yoeli 2:24, 1Samweli 14: 2 , Hosea 13:3, Yeremia 51:33
Je kuna umuhimu wowote wa sisi kufahamu juu ya Uga?
Jibu ni ndio, kwa kujua hilo itatusaidia kufahamu, Yohana alimaanisha nini pale inaposema juu ya habari za Yesu kuwa pepeto lake lipo mkononi mwake, kuusafisha uwanda wake..
Tusome;
Mathayo 3:11 “Kweli mimi nawabatiza kwa maji kwa ajili ya toba; bali yeye ajaye nyuma yangu ana nguvu kuliko mimi, wala sistahili hata kuvichukua viatu vyake; yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto. 12 Ambaye pepeto lake li mkononi mwake, naye atausafisha sana uwanda wake; na kuikusanya ngano yake ghalani, bali makapi atayateketeza kwa moto usiozimika”.
Mathayo 3:11 “Kweli mimi nawabatiza kwa maji kwa ajili ya toba; bali yeye ajaye nyuma yangu ana nguvu kuliko mimi, wala sistahili hata kuvichukua viatu vyake; yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto.
12 Ambaye pepeto lake li mkononi mwake, naye atausafisha sana uwanda wake; na kuikusanya ngano yake ghalani, bali makapi atayateketeza kwa moto usiozimika”.
Anachofanya Kristo leo hii ulimwenguni, ni kuusafisha uwanda wake(sakafu yake ya kupepetea ambalo ndio kanisa lake), na anaisafisha kwa pepeto, (uma) ulio mkononi mwake, Hivyo sote ni kama tunarushwa rushwa juu, na kama wewe utakuwa ngano halisi utashuka chini, lakini ukiwa kapi jepesi, utapeperushwa na upepo. Na baadaye utakusanywa na kwenda kuchomwa moto usiozimika.
Zipo pepo za aina nyingi leo hii ndugu yangu, Upepo wa mafundisho ya uongo, upepo wa unasa, upepo wa uzinzi, upepo wa fedha n.k..vyote hivi vinawapeperusha watu, Hizi ni nyakati za mwisho. Injili tuliyonayo sasa hivi sio injili ya kupembelezwa tena, ni injili ya kujichunguza umesimama wapi. Na unakwenda wapi. Hakuna mtu ambaye hajawahi kusikia injili, hivyo ni wajibu wako wewe mwenyewe kuhakikisha Kristo yupo ndani yako. Ili uwe mahali salama.
Shalom.
Tazama maana ya maneno mengine ya biblia chini.
USIPIGE MATEKE MCHOKOO!
Hisopu/ Hisopo ni nini katika biblia?(Zaburi 51:7)
Bwana Yesu alikufa akiwa na umri gani?
Duara ya Ahazi ni ipi? Na je! Kivuli cha Hezekia kilirudije nyuma?
Mungu anaposema “nitaliweka jina langu” ana maana gani?
Biblia inatuonyesha Bwana Yesu alianza huduma yake akiwa na umri wa miaka kama 30. Luka 3:23.
Sasa ili tujue alikufa na umri gani, ni vizuri kwanza tukajua urefu wa huduma yake ulikuwa ni miaka mingapi, na hiyo ndio itakayotusaidia kujua alikufa na umri gani.
Tukisoma kitabu cha Yohana kinatuonyesha Bwana alihudhuria sikukuu za Pasaka zisizopungua tatu.
Ya kwanza tunaisoma katika Yohana 2:13, Ya pili katika 6:4, Na ya tatu tunaisoma katika 11:55-57
Kama tunavyojua pasaka hizi zilikuwa ni mwaka kwa mwaka, hivyo tukijumlisha hapo, tunaweza kupata hesabu ya miaka miwili (2).Ili kuelewa vizuri, chukulia mfano sikukuu ya kwanza ilikuwa ni mwezi april mwaka huu, sikukuu ya pili itakuwa ni mwezi April mwaka kesho, na sikukuu ya tatu itakuwa ni mwezi April mwaka kesho kutwa,. Hivyo ukianza kujumlisha tangu april mwaka huu, hadi April mwaka kesho kutwa utaona ni jumla ya miaka miwili mizima.
Lakini kutokana na kurekodiwa kwa matukio mengi ambayo aliyafanya Yesu, pamoja safari zake nyingi, wanazuoni walihitimisha kuwa kulikuwa na pasaka nyingine ambayo haijaandikwa katika biblia ilipita hapo katikati.
Na pasaka yenyewe iliangukia kati ya ile pasaka ya kwanza (Yohana 2:13) na ile ya pili (Yohana 6:4)..Kufanya muda wa huduma ya Yesu Kristo kuwa ni miaka 3.
Lakini, pia yapo matukio mengine ambayo yalitendekea kabla ya ile pasaka ya kwanza kufika, tunaona tangu Bwana Yesu abatizwe pale Yordani na Yohana, kulikuwa ni kipindi ambacho alifunga siku 40 kule jangwani, kulikuwa na wakati alisafiri kutoka Yordani, kwenda Kana, na baadaye kwenda Yerusalemu, kulikuwa na kipindi aliwaita wanafunzi wake na kuanza huduma ya kuhubiri, yote hayo yalichukua kipindi cha miezi kadhaa,kabla ya kuifikia ile pasaka ya kwanza. Na pia baada ya kufa na kufufuka kulikuwa na siku 40 ambazo aliwatokea watu wengi, kabla ya kupaa.
Hivyo tunaweza kusema, huduma ya Yesu Kristo, inakadiriwa kwenda kwa miaka mitatu na nusu.
Tukijumlisha na ile miaka 30 ya mwanzo, tunapata miaka thelathini na tatu na nusu. Hivyo Bwana Yesu alikufa akiwa na umri wa miaka hiyo (Thelathini na tatu na Nusu).
Lakini ni nini tunajifunza katika maisha ya Kristo?
Kristo Yesu Bwana wetu alikufa akiwa bado na umri mdogo sana, kwa dunia ya sasa watu watasema amekufa kabla ya wakati. Lakini tunaona katika umri huo mdogo aliimaliza kazi ile aliyoitwa duniani, na hivyo mbinguni akaonekana ndiye aliyefanya kubwa na yenye faida kuliko wanadamu wote waliowahi kuishi duniani, sio wale waliokufa wakiwa na miaka 900, wala wale waliokuwa na miaka 120, hakuna hata mmoja aliyefanya kazi kubwa yenye matunda mengi kama Kristo hapa duniani.
Siri ilikuwa ni nini?
Embu tafakari kwa maneno yake mwenyewe aliyoyasema katika vifungu hivi;
Yohana 9:4 “Imetupasa kuzifanya kazi zake yeye aliyenipeleka maadamu ni mchana, usiku waja asipoweza mtu kufanya kazi”.
Yohana 11:9 “Yesu akajibu, Je! Saa za mchana si kumi na mbili? Mtu akienda mchana hajikwai; kwa sababu aiona nuru ya ulimwengu huu”.
Yohana 4:33 “Basi wanafunzi wake wakasemezana, Je! Mtu amemletea chakula? 34 Yesu akawaambia, Chakula changu ndicho hiki, niyatende mapenzi yake aliyenipeleka, nikaimalize kazi yake”.
Yohana 4:33 “Basi wanafunzi wake wakasemezana, Je! Mtu amemletea chakula?
34 Yesu akawaambia, Chakula changu ndicho hiki, niyatende mapenzi yake aliyenipeleka, nikaimalize kazi yake”.
Mpaka hapo tunaweza kuona Bwana wetu alikuwa ni mtu wa namna gani.. Ni mtu ambaye aliuthamini muda wake akiwa hapa duniani, alijua kuwa muda hautakuwepo wakati wote, kuna siku giza litakuja na mtu asiweze kufanya kazi tena, aliichukulia kazi ya Mungu kama ndio chakula chake, kinachomfanya aishi hapa duniani, kwamba bila hicho atakufa, na kama tunavyojua mtu kula ni lazima kila siku.Hivyo yeye kuifanya kazi ya Mungu ilikuwa ni desturi yake kila siku na kila wakati..
Na ndio maana haikumchukua hata muda mrefu kumaliza huduma yake, hakusongwa na kitu chochote katika huu ulimwengu..
Je! Na sisi tunaweza kufanana naye?. Bwana atutie nguvu tuwe kama yeye.. Kwa nguvu zake tu peke yake ndio tutaweza.
MWANZO WA INJILI YA YESU KRISTO.
KWANINI NI YESU KRISTO WA NAZARETI?
MWINUE YESU KRISTO KATIKA MAISHA YAKO.
ALIPO NA ATAKAPOKUWEPO BIBI-ARUSI WA YESU KRISTO.
JINSI SHETANI ANAVYOZUIA MAJIBU YA MAOMBI YETU.
UTAWALA WA MIAKA 1000.
WhatsApp
Hisopo au Hisopu ni jamii ya mmea, ambao ulitumiwa zamani na wana wa Israeli kwa matumizi mbalimbali. Tazama picha ya mmea wenyewe juu.
Lakini mmea huu sana sana ulitumiwa kwa kwaajili ya shughuli za utakaso wa kimaagano, Kwamfano Hisopo ilitumika kuwatakasa watu waliokuwa na ukoma na nyumba zote zilizoathiriwa na ugonjwa huu,
Walawi 14:4 “ndipo huyo kuhani ataagiza kwamba watwae kwa ajili yake atakayetakaswa ndege wawili walio hai, ambao ni safi, na mti wa mwerezi, na sufu nyekundu, na hisopo; 5 kisha kuhani ataagiza ndege mmoja achinjwe katika chombo cha udongo kilicho juu ya maji ya mtoni; 6 kisha huyo ndege aliye hai atamshika, na huo mti wa mwerezi, na hiyo sufu nyekundu, na hisopo, naye atavichovya hivyo, pamoja na yule ndege aliye hai, katika damu ya huyo ndege aliyechinjwa juu ya maji ya mtoni; 7 kisha atamnyunyizia huyo atakayetakaswa na ukoma mara saba, naye atasema kwamba yu safi, kisha atamwacha yule ndege aliye hai aende zake nyikani”.
Walawi 14:4 “ndipo huyo kuhani ataagiza kwamba watwae kwa ajili yake atakayetakaswa ndege wawili walio hai, ambao ni safi, na mti wa mwerezi, na sufu nyekundu, na hisopo;
5 kisha kuhani ataagiza ndege mmoja achinjwe katika chombo cha udongo kilicho juu ya maji ya mtoni;
6 kisha huyo ndege aliye hai atamshika, na huo mti wa mwerezi, na hiyo sufu nyekundu, na hisopo, naye atavichovya hivyo, pamoja na yule ndege aliye hai, katika damu ya huyo ndege aliyechinjwa juu ya maji ya mtoni;
7 kisha atamnyunyizia huyo atakayetakaswa na ukoma mara saba, naye atasema kwamba yu safi, kisha atamwacha yule ndege aliye hai aende zake nyikani”.
Soma pia Walawi 14:51
Waebrania 9:19 “Maana kila amri ilipokwisha kunenwa na Musa kwa hao watu wote, kama ilivyoamuru sheria, aliitwaa damu ya ndama na ya mbuzi, pamoja na maji na sufu nyekundu na hisopo, akakinyunyizia kitabu chenyewe, na watu wote”,
Brashi la kupakia damu, wakati ule Mungu anawapiga wamisri kwa pigo la mwisho, la kuwaua wazaliwa wa kwanza wa kimisri aliwaambia wana wa Israeli, watwae damu ya kondoo, kisha watumie tawi la hisopo kama brash la kuipaka damu hiyo, kiashirio cha kutakaswa kwao.
Kutoka 12:22 “Nanyi twaeni tawi la hisopu, mkalichovye katika ile damu iliyo bakulini na kukipiga kizingiti cha juu, na miimo miwili ya mlango, kwa hiyo damu iliyo katika bakuli; tena mtu ye yote miongoni mwenu asitoke mlangoni mwa nyumba yake hata asubuhi”.
Zaburi 51:7 “Unisafishe kwa hisopo nami nitakuwa safi, Unioshe, nami nitakuwa mweupe kuliko theluji”
Wale askari walitumia ufito wa mmea huu, kushikilizia ile sifongo(sponji), ili kumnywesha Bwana Yesu siki,.
Yohana 19:29 “Kulikuwako huko chombo kimejaa siki; basi wakatia sifongo iliyojaa siki juu ya ufito wa hisopo, wakampelekea kinywani”.
Kama tunavyojua mmea huu ni mmea wa utakaso, ulitumika kusafishia, hatushangai, kuona kwanini Kristo alipelekewa siki kwa mmea huu. Ni kuonyesha kuwa tayari alikuwa ni dhabihu safi iliyotakaswa, iliyowekwa tayari kwa ajili ya kutundolea sisi dhambi zetu.
Hivyo, mimi na wewe, tutatakaswa kwa hisopo ya rohoni si kwa kitu kingine zaidi ya damu ya Yesu Kristo tu. Kama hatutaoshwa kwa damu hii, kamwe tusitazamie ukoma wetu wa rohoni utaondoka, kamwe tusitazamia unajisi wetu utaondoka, kamwe tusitazamie tutamshinda shetani, na kamwe tusitazamie tutampendeza Mungu.
Swali ni Je! Umesafishwa kwa damu ya Yesu? Kama bado unasubiri nini mpendwa. Mkaribishe moyoni mwako akuokoe hizi ni siku za mwisho. Kuwa serious na maisha yako ya rohoni. Tubu dhambi zako, ufanywe mwana wa Mungu.
Maran Atha.
Tazama maana ya maneno mengine ya biblia chini,
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 693036618 / +255789001312
SIFONGO NA SIKI NI NINI?
Bisi ni nini? (Walawi 23:14, Ruthu 2:14)
Nini maana ya kumlingana Mungu?
Sharoni ni nini au ni wapi kibiblia?(1Nyakati 5:16)
Jabari ni nini, kama linavyotumika kwenye biblia?
Baradhuli/Mabaradhuli ni nini au ni nani kwenye biblia?
Rudi Nyumbani:
Kumlingana Mungu ni Kiswahili cha zamani chenye maana ya “kumwita Mungu”. Pale mtu anapopitia jaribu, au tatizo, anapomwita au kumlilia Mungu wake kwaajili ya kupata msaada, maana yake mtu huyo “amemlingana” Mungu.
Tunaweza kuona mifano michache katika biblia ya watu waliomlingana Mungu.
Wana wa Israeli:
Hawa walimwacha Bwana, na Bwana akawatia chini ya utumwa mkali kwa maadui zao.
Waamuzi 3: 8 “Kwa hiyo hasira za Bwana ziliwaka juu ya Israeli, naye akawauza na kuwatia mikononi mwa Kushanrishathaimu mfalme wa Mesopotamia; na wana wa Israeli wakamtumikia huyo Kushan-rishathaimu muda wa miaka minane. 9 Kisha wana wa Israeli walipomlingana Bwana, Bwana akawainulia wana wa Israeli mwokozi, aliyewaokoa, yaani, Othnieli mwana wa Kenazi, ndugu mdogo wa Kalebu”.
Waamuzi 3: 8 “Kwa hiyo hasira za Bwana ziliwaka juu ya Israeli, naye akawauza na kuwatia mikononi mwa Kushanrishathaimu mfalme wa Mesopotamia; na wana wa Israeli wakamtumikia huyo Kushan-rishathaimu muda wa miaka minane.
9 Kisha wana wa Israeli walipomlingana Bwana, Bwana akawainulia wana wa Israeli mwokozi, aliyewaokoa, yaani, Othnieli mwana wa Kenazi, ndugu mdogo wa Kalebu”.
Yabesi:
1 Nyakati 4: 10 “Huyo Yabesi akamlingana Mungu wa Israeli, akisema, Lau kwamba ungenibarikia kweli kweli, na kunizidishia hozi yangu, na mkono wako ungekuwa pamoja nami, nawe ungenilinda na uovu, ili usiwe kwa huzuni yangu! Naye Mungu akamjalia hayo aliyoyaomba”.
Kwa Habari ndefu kuhusu huyu Yabesi na maisha yake unaweza kufungua hapa >> MAISHA YA YABESI.
Pia Neno hilo limetumika katika mistari mingine michache ifuatayo..1Nyakati 5:20, na 1Nyakati 21:26.
Jambo tunalojifunza ni kwamba hata sisi tunapoadhibiwa na Mungu, kutokana na makosa yetu tunapomgeukia Bwana na kumlilia (kumlingana), yeye ni mwenye rehema na huruma, anaghairi mabaya.
Na kama tupo kwenye dhambi, yaani hatumkabidhi Yesu Maisha yetu, basi ghadhabu ya Mungu ipo juu yetu, na kila tunapoisikia injili inayohubiriwa na watumishi wa Mungu, na kuidharau, Mabaya yanatuandama…
Yeremia 26:2 “Bwana asema hivi, Simama katika uwanja wa nyumba ya Bwana, useme na miji yote ya Yuda, wajao ili kuabudu katika nyumba ya Bwana; sema nao maneno yote ninayokuamuru kuwaambia, usizuie hata neno moja. 3 Labda watasikia, na kughairi na kuacha kila mtu njia yake mbaya; ili niyaghairi mabaya niliyokusudia kuwatenda, kwa sababu ya uovu wa matendo yao”.
Yeremia 26:2 “Bwana asema hivi, Simama katika uwanja wa nyumba ya Bwana, useme na miji yote ya Yuda, wajao ili kuabudu katika nyumba ya Bwana; sema nao maneno yote ninayokuamuru kuwaambia, usizuie hata neno moja.
3 Labda watasikia, na kughairi na kuacha kila mtu njia yake mbaya; ili niyaghairi mabaya niliyokusudia kuwatenda, kwa sababu ya uovu wa matendo yao”.
Bwana yupo tayari kughairi mabaya aliyokuwa ameyapanga kuyaleta juu yako kwasababu ya uzinzi wako, au kwasababa ya utoaji wako mimba, au ulevi wako, au yoyote yale mabaya unayoyafanya. Endapo ukiamua kutubu na kumgeukia yeye.
Kama upo tayari leo kutubu na kumwita yeye (kumlingana), kama alighairi mabaya kwa wana wa Israeli, na kwa watu wengine wengi, ikiwemo mimi hatashindwa na wewe basi kama upo tayari leo kuanza maisha mapya fungua hapa kwa msaada Zaidi >> SALA YA TOBA.
Na kama tayari umeshaokoka, basi usiache kumwita (kumlingana) Mungu wako kila wakati, kwasababu yeye anajishughulisha sana na mambo yako.
Maran atha!
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312
WAENDEE WANA WA ISAKARI, UWE SALAMA.
WAPE WATU WANGU RUHUSA ILI WAPATE KUNITUMIKIA.
Je! Wana wenu huwatoa kwa nani? maana yake ni nini?
Jina la Bwana wetu Yesu Kristo libarikiwe.
Silaha moja kubwa ya adui ni Hofu. Na biblia inatuambia Hofu ina adhabu (1Yohana 4:18).. Leo hii tutaona adhabu kuu ya hofu ni nini..
Tukisoma Mithali Mithali 10:24 Inatuambia..
“Aogopacho mtu asiye haki ndicho kitakachomjilia;..”
Leo hii kiini cha ukristo hakipo tena katika mafundisho ya wokovu na ufalme wa mbinguni, bali kipo katika elimu za uchawi na uganga. Kiasi kwamba mtu hajui ubatizo wa Roho Mtakatifu ni nini, lakini ukimuuliza kuhusu habari za wachawi anajua A-Z. Hilo jambo ni hatari sana, mimi sipingi uchawi, lakini tuangalie katika biblia, je! uchawi umepewa uzito gani katika maisha yetu ya wokovu ya kila siku?
Kwanini mitume au Bwana Yesu hakutufundisha au kutusisitiza sana juu ya siri za wachawi? .Unadhani hawakuwepo? Walikuwepo wengi, lakini waliijua nguvu nyingine iliyo kubwa zaidi ya wao, na ndio hiyo walijikita kuwahubiria watu waiamini, kwasababu walijua hiyo wakishaipata, ni ulinzi tosha, dhidi ya nguvu zote za Yule adui.
Hofu ya uchawi imewashika watu wengi, na kibaya zaidi imewakamata na wakristo waliookoka pia, wao ambao ndio wangepaswa kuwa wakwanza kuzidharau.
Sasa hizi ni baadhi ya hofu za hofu zinazowakamata wengi leo hii;
Kwamfano kama utaona mjusi ndani kwako, na kusema ile ni roho , ujue kuwa hofu hiyo imeshakuvaa.
Kama utaona panya ndani, au mende, au sisimizi, au konokono, au nzi vitu ambavyo vingehitaji usafi tu kuviondoa, na ukasema hizo ni roho, ujue kuwa hofu hiyo ipo ndani yako.
Kama utaona paka, na ukahisi ni wachawi wamekutembelea, basi ujue hofu hiyo ipo ndani yako.
Kama utaona, mtu fulani na ukahisi ni mchawi na atakudhuru kwa nguvu za giza, basi ujue hofu hiyo ipo ndani yako. N.k.
Sasa kama biblia inavyotuambia, hofu ina adhabu.. basi ujue adhabu yenyewe ndio hii “Aogopacho mtu asiye haki ndicho kitakachomjilia;..” hiyo ndio adhabu!!
Ukiona roho ndani ya konokono, ujue kuwa shetani anaumbika nyuma ya konokono huyo, na inakuwa roho hai kweli, na madhara yatakukuta kupitia konokono huyo, kwasababu pepo la hofu ya uchawi umeliruhusul ifanye kazi ndani ya konokono, na hivyo madhara yote yatokanayo na pepo hilo utayapata tu.
Ukiamini, kuwa miti fulani ni ya kichawi, ukweli ni kwamba hilo jambo litaaumbika kwako na madhara hayo utayapata ya kutosha, kama ni kifo utakipata, lakini wakati huo huo utaona jirani yako anao mti kama huo, na wala hakuna lolote baya linalompata.
Kwasababu hofu yoyote ina adhabu..
Ukiamini panya ndani kwako ndio wanaokusababishia umaskini na usisonge mbele, basi umaskini wako utakujia kwa njia ya hao hao panya, utafunga usiku kucha kuomba, na kukemea, bado hali itakuwa ngumu kwako, panya mwingine atakapokatiza ndani kwako,.. kwasababu umeshafungua mlango wa hofu kwa kupita viumbe hao, lakini jirani yako ataona panya, atakachofanya ni kukumbuka kuwa mazingira yake hayapo safi, hivyo atayaweka sawa kwa kufanya usafi na kutafuta namna ya kuwaua , akaendelea kuishi maisha yake ya furaha.
Hiyo ndio adhabu ya hofu ndugu.. Ukikutana na bundi ukaamini katumwa kukuletea msiba, basi msiba huo utakujia tu kwa mlango wowote,
Kwasababu Biblia inasema Imani ni kuwa na uhakika, wa mambo yatarajiwayo..Ukiwa na uhakika kwamba utapata msiba kutokana na bundi uliyemwona, basi ni kweli utakuja kwa njia hiyo hiyo uliyoamini.
kumbe bundi alikuwa anapita tu katika safari yake usiku na kwa bahati nzuri au mbaya akakutana na wewe, lakini kwasababu wewe umelipa nafasi pepo la hofu ya mauti na uchawi, nalo likapata nafasi kupitia ndege Yule huyo mrembo. Na siku si nyingi unasikia msiba,, na wewe unadhani unabii umetimia, kumbe ni hofu imekuzalia matunda yake, uliyokuwa unayatarajia.
Ndugu ukiwa ndani ya Kristo huhitaji kuishi maisha ya kuogopa ogopa kila kitu, hata kama kweli ni nguvu za giza, zipo ndani yao, lakini Bwana Yesu alituambia..
Luka 16.18 “watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa;..”
Utatumiwa uchawi, lakini hautakudhuru ikiwa upo ndani ya Kristo, utatengewa chakula cha kichawi, kilichotoka kuzimu kabisa, lakini hakitakuwa na madhara yoyote ndani yako, kwasababu nguvu iliyo ndani yako NI KUBWA kuliko yao. Lakini ukianza kuhangaika huko na huko, unafuta kila njia ya kujilinda mwenyewe dhidi ya kila kitu unachokiona, utapata shida nyingi sana hapa duniani, na wala hutaufurahia wokovu wako, hata kidogo.
Kwasababu maisha yako yatakuwa ni ya vita kila siku, visivyokuwa na sababu.
Hivyo Ikiwa wewe ni mmojawapo wa walioathirika na mafundisho hayo manyonge, ambayo yanahubiriwa kila mahali, nataka nikuambie leo hii anza upya na Kristo, toka kwenye hicho kifungo, kisha jibidiishe katika kusoma biblia, kuliko kusikiliza hadithi hizo za kimila, na za wachawi, na kidogo kidogo utaanza kupata amani moyoni mwako, kama vile biblia inavyosema;
Yohana 8:32 “tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru”.
Shalom!.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312/+255 693036618
JE! PAKA KULIA USIKU NI ISHARA YA UCHAWI?
Ni kosa gani Daudi alilolifanya katika kuwahesabu watu, mpaka kupelekea vifo vya waisraeli wengi?
USIWE NA HOFU, USHUKAPO CHINI.
USIKATE TAMAA UNAPOPITIA MAGONJWA.
Shalom, Biblia inasema;
Luka 12:58 “Maana, unapofuatana na mshitaki wako kwenda kwa mwamuzi, hapo njiani fanya bidii kupatanishwa naye, asije akakuburuta mpaka mbele ya kadhi; yule kadhi akakutia mikononi mwake mwenye kulipiza, na yule mwenye kulipiza akakutupa gerezani. 59 Nakuambia, Hutoki humo kamwe hata uishe kulipa senti ya mwisho”.
Luka 12:58 “Maana, unapofuatana na mshitaki wako kwenda kwa mwamuzi, hapo njiani fanya bidii kupatanishwa naye, asije akakuburuta mpaka mbele ya kadhi; yule kadhi akakutia mikononi mwake mwenye kulipiza, na yule mwenye kulipiza akakutupa gerezani.
59 Nakuambia, Hutoki humo kamwe hata uishe kulipa senti ya mwisho”.
Hapo mwanzoni nilidhani mshitaki wetu ni shetani tu peke yake kama tunavyosoma katika 1Petro 5:8, na Ufunuo 12:10, lakini biblia inatuonyesha kuwa wapo washitaki wengine ambao watatushitaki sisi huko tunapokwenda, ambao sisi hatuwajui..
Ukiuchunguza huo mstari kwa makini, unaposema patanishwa na mshitaki wako, kabla ya kufika kwa mwamuzi, utajiuliza shetani atapatanishwaje na sisi? sisi hatuwezi kupatanishwa na yeye kwa lolote kwasababu yeye sikuzote ni mpingamizi na ni adui.. Hivyo wapo washitaki wengine wanaozungumziwa, ambao Bwana Yesu aliwamaanisha hapo,.. Na hao si washitaki, wa kidunia labda wa mahakamani,hapana ni kweli ukisoma hapo alitumia mfano wa washitaki wa kidunia, lakini alikuwa anamaanisha washitaki wengine wa rohoni.
Je washitaki hao ni wakina nani?
Tukirudi nyuma katika mazingira ya Kristo aliyokuwepo, waisraeli wengi walikataa kumsikiliza kwa kisingizio kuwa wanaye Musa, (Wakiwa na maana wanaifuata torati yake, na sio maneno ya tu mwingine yeyote). Lakini kiuhalisia torati yenyewe walikuwa hawaishiki, na kwa mantiki hiyo Bwana Yesu kuna mahali akawaambia maneno haya;
Yohana 5:45 “Msidhani kwamba mimi nitawashitaki kwa Baba; yuko anayewashitaki, ndiye Musa, mnayemtumaini ninyi. 46 Kwa maana kama mngalimwamini Musa, mngeniamini mimi; kwa sababu yeye aliandika habari zangu”.
Yohana 5:45 “Msidhani kwamba mimi nitawashitaki kwa Baba; yuko anayewashitaki, ndiye Musa, mnayemtumaini ninyi.
46 Kwa maana kama mngalimwamini Musa, mngeniamini mimi; kwa sababu yeye aliandika habari zangu”.
Wana wa Israeli hawakujua kuwa Musa wanayemwamini ndiye atakayekuwa mshitaki wao siku ile ya mwisho kwanini hawakuyashika alichowaagiza.. Na ndio maana Bwana Yesu akatumia mfano huo, na kuwaambia patana kwanza na mshitaki wako, Patana kwanza na Musa, patana kwanza na torati, kabla hamjafika kwa kadhi, Kadhi hapo anamaanishi Mungu, katika siku ile ya Hukumu.
Kwasababu ukishajikuta mbele ya kadhi (yaani Mungu) siku ile , kitakachofuata si kingine zaidi ya Hukumu, na ukishahukumiwa utawekwa mikononi mwa mwenye kulipiza,(Askari), ambao ni malaika watakatifu, kisha hao watakukamata, na kwenda kukutupa kwenye ziwa la moto.
Anamalizia kwa kusema..
Ukishafikia hatua hiyo, hutoki huko mpaka utakapolipa senti ya mwisho, maana yake ni kwamba Ukishashushwa kuzimu, habari yako ndio imeisha hapo rafiki, hakuna cha msamaha, hakuna cha dhamana, hakuna cha kulipa kidogo kidogo ukiwa nje..Utaishia huko milele na milele.
JE! NA SISI PIA TUNAO WASHITAKI?
Waisraeli walijifanya kuwa ni watoto wa Musa, hivyo Musa akawa mshitaki wao, vivyo hivyo na sisi, washitaki wetu ni mitume na manabii.. Tunasema sisi ni wakristo, tunayoiamini biblia, tunasema tumejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii lakini walichokisema mitume baba zetu hatukifanyi katika maisha yetu.. Hao ndio watakaokuwa washitaki wetu. Hizo Injili zao ndizo zitakazotushitaki siku ile..
Na ndio maana biblia inatusisitiza sana, tuhakikishe tunapatanishwa nao, angali tukiwa hapa katikati njiani, Maana yake ni angali tukiwa angali hapa duniani,hatujafa bado, tunayo nafasi ndogo, kabla hatujamaliza mwendo, tuhakikishe, wokovu tunaupata, tuhakikishe tunalizingatia lile andiko linalosema, tafuteni kwa bidii, kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu ambao hakuna mtu atakayemwona Mungu asipokuwa nao (Waebrania 12:14). Tuhakikishe hayo tunayo, tuhakikishe tumebatizwa kweli kwa Roho Mtakatifu. Tumetiwa muhuri.
Kwasababu hawa ndio watakaosimama siku ile kutushitaki, kuwa walituambia lakini sisi tulikataa.
Paulo alisema..
Warumi 2:16 “katika siku ile Mungu atakapozihukumu siri za wanadamu, sawasawa na injili yangu, kwa Kristo Yesu”.
Bwana atusaidie tuitii injili.
Je umeokoka? Je, unaouhakika wa maisha yako ya milele kwamba hata ukifa leo utakwenda mbinguni? Kama sivyo, basi leo tubu, mkabidhi Yesu maisha yako ayasafishe, kwasababu hizi ni siku za mwisho, wote tunalijua hilo, tunaishi katika dakika za nyiongeza tu, dakika za majeruhi, Unyakuo ni wakati wowote, Hivyo sote kwa pamoja tuamke, tumgeukie Muumba wetu. Ni wakati wa kujitwika msalaba wako wewe kama wewe, na kumfuata Kristo, ni wakati wa kuchagua lililo la msingi kwanza, na hayo mengine ndio yafuate baadaye kama yanayoulazima. Hii mizigo ya duniani tuipe pumziko kidogo tufanya lililo la kwanza, ili tuwe mahali salama.
Tupatanishwe na washitaki wetu.
SI MAPEPO YOTE NI YA KULIPUKA.
NI NINI TUNAJIFUNZA JUU YA MT. DENIS WA UFARANSA?
NYAYO TUNAZOPASWA KUZIFUATA.
USITAFUTE KUKANWA NA BWANA SIKU ILE.
Nyuma kidogo nilikuwa nadhani mtu mwenye mapepo, ni lazima yalipuke, na ikiwa hayalipuka, basi hana mapepo ndani yake. Kumbe mtazamo huu sio sahihi. Tunapaswa tujue kuwa mtu yeyote ambaye hayupo ndani ya Kristo kwa namna moja au nyingine lipo pepo ambalo linaishi ndani yake, aidha kwa kujua au kwa kutokujua, haijalishi kuwa litamlipuka au halimtalipuka.
Biblia inatufundisha hivyo, Si wakati wote Mapepo yote yaliyokutana na Yesu yalilipuka, au yalitolewa kwa kukumewa kama tunavyodhani.. Embu tusome habari hii pengine ulishawahi kuisoma mara nyingine lakini jambo hili hukulijua..tusome.
Luka 13:10 “Siku ya sabato alikuwa akifundisha katika sinagogi mojawapo. 11 Na tazama, palikuwa na mwanamke aliyekuwa NA PEPO WA UDHAIFU muda wa miaka kumi na minane, naye amepindana, hawezi kujinyosha kabisa. 12 Yesu alipomwona alimwita, akamwambia, Mama, umefunguliwa katika udhaifu wako. 13 Akaweka mikono yake juu yake, naye akanyoka mara hiyo, akamtukuza Mungu”.
Luka 13:10 “Siku ya sabato alikuwa akifundisha katika sinagogi mojawapo.
11 Na tazama, palikuwa na mwanamke aliyekuwa NA PEPO WA UDHAIFU muda wa miaka kumi na minane, naye amepindana, hawezi kujinyosha kabisa.
12 Yesu alipomwona alimwita, akamwambia, Mama, umefunguliwa katika udhaifu wako.
13 Akaweka mikono yake juu yake, naye akanyoka mara hiyo, akamtukuza Mungu”.
Kwa mistari hiyo michache tunaweza kusema, Yesu alijua kabisa huyu mama kilichokaa nyuma yake si kingine zaidi ya Pepo, na hilo pepo nalo lilijua kabisa aliyesimama mbele yake ni Yesu mkuu wa uzima. Lakini pepo hili limekaa nyuma ya kivuli cha udhaifu, nyuma ugonjwa wa kibiongo, wala halipigi kilele, wala halijidhihirishi kama ilivyo desturi yao. Ndipo Yesu akamwita, akamwekea mikono yake, na hilo pepo likaondoka saa ile ile, na mama yule akawa mzima.
Lilipotoka Mama huyu hakujua chochote, kwasababu hakugarara chini, au hakupiga kelele, kilichomfanya ajue kuwa pepo limeondoka na mabadiliko ya ghafla aliyoanza kuyaona katika mwili wake baada ya pale.
Nachotaka kusema ni kuwa, nguvu za giza hazichagui wa kumwingia, maadamu upo nje ya “himaya ya Kristo Yesu” hayatakosa mahali popote tu pa kukaa, panaweza pasiwe katika ugonjwa, panaweza pasiwe katika mwili, utaenda kanisani kama kawaida, mtafanya maombi ya nguvu pengine, na wala lisilipuke pepo lolote. Lakini linaweza likakukaa katika ulevi, likakukaa katika uzinzi, likakukaa katika wizi, likakaa katika usengenyaji n.k. Au katika tabia fulani ambayo wewe mwenyewe inakushinda. Na hayo yote hutajua kama yalikuwa ndani yako mpaka utakapookolewa na Yesu.
Lakini kama upo ndani ya wokovu Pepo haliwezi kuwa na nafasi ndani yako.
Hivyo wewe unayeusoma ujumbe huu, na hujaokoka pengine ulikuwa hujui kuwa kuna maroho ya giza yamekuzunguka kwenye maisha yako. Na leo umejua, basi fahamu kuwa njia pekee ya kuzishinda roho hizo, ni kwa kujikabidhi kwa Bwana Yesu. Yeye pekee kwa damu yake iliyomwagika pale msalabani ndiyo yenye nguvu ya kuweza kuondoa na anayeweza Kufuta laana yote ya dhambi iliyokuwa juu yako, pamoja na kufukuza miungu yote migeni inayoishi humo nafsini mwako. Ikiwa tu utakubali leo hii kutubu, na kuyasalimisha maisha yako kwake kikamilifu, kwa kumaanisha kabisa kutoka katika moyo wako, kwamba hutorudi nyuma tena. Basi leo hii anaweza kukusamehe kabisa.
Hivyo Kama upo tayari kwa hilo hii, basi fuatisha sala hii fupi kwa imani, ukijua kuwa Mungu anakusikia, na kwa kufanya hivyo Bwana ataanza kuunda jambo jipya katika maisha yako, kuanzia leo. Fungua tu moyo wako.
Mahali ulipo jitenge kasha piga magoti sehemu ya utulivu kisha Sema maneno haya;
EE MUNGU BABA, NAJA MBELE ZAKO, NIKIWA NINAJITAMBUA KUWA MIMI NI MKOSAJI NA NIMEKUTENDA DHAMBI NYINGI, NA KWAMBA NIMESTAHILI HUKUMU. LAKINI WEWE MUNGU WANGU ULISEMA KATIKA NENO LAKO KUWA WEWE NI MUNGU WA REHEMA UNAYEWAREHEMU MAELFU ELFU YA WATU WANAOKUPENDA WEWE. NA LEO HII NINAKUJA MBELE ZAKO NAHITAJI MSAMAHA WAKO NA MSAADA WAKO MUNGU WANGU, NINATUBU DHAMBI ZANGU ZOTE KWA KUMAANISHA NA KWA MOYO WANGU WOTE, NINAKIRI KUWA YESU KRISTO NI BWANA, NA YEYE NDIYE MWOKOZI WA HUU ULIMWENGUNI. HIVYO NAOMBA DAMU YA MWANAO TAKATIFU INISAFISHE IONDOE UOVU WANGU WOTE SASA NDANI YANGU, NIFANYIKE KUWA KIUMBE KIPYA KUANZIA LEO NA HATA MILELE. ASANTE BWANA YESU KWA KUNIPOKEA NA KUNISAMEHE. AMEN.
EE MUNGU BABA, NAJA MBELE ZAKO, NIKIWA NINAJITAMBUA KUWA MIMI NI MKOSAJI NA NIMEKUTENDA DHAMBI NYINGI, NA KWAMBA NIMESTAHILI HUKUMU. LAKINI WEWE MUNGU WANGU ULISEMA KATIKA NENO LAKO KUWA WEWE NI MUNGU WA REHEMA UNAYEWAREHEMU MAELFU ELFU YA WATU WANAOKUPENDA WEWE. NA LEO HII NINAKUJA MBELE ZAKO NAHITAJI MSAMAHA WAKO NA MSAADA WAKO MUNGU WANGU, NINATUBU DHAMBI ZANGU ZOTE KWA KUMAANISHA NA KWA MOYO WANGU WOTE, NINAKIRI KUWA YESU KRISTO NI BWANA, NA YEYE NDIYE MWOKOZI WA HUU ULIMWENGUNI. HIVYO NAOMBA DAMU YA MWANAO TAKATIFU INISAFISHE IONDOE UOVU WANGU WOTE SASA NDANI YANGU, NIFANYIKE KUWA KIUMBE KIPYA KUANZIA LEO NA HATA MILELE.
ASANTE BWANA YESU KWA KUNIPOKEA NA KUNISAMEHE.
AMEN.
Sasa ikiwa sala hiyo imetoka moyoni mwako, ujue kuwa hiyo ni hatua ya kwanza, kuelekea kufanywa huru kweli kweli na Bwana Yesu. hatua inayofuata kwako ni kupokea Ubatizo sahihi, ambao ni ule wa kuzamishwa katika maji tele (Yohana 3:23) na uwe katika jina la BWANA YESU KRISTO sawasawa na Matendo 2:38,8:16,10:48,19:5. Na ukilikamilisha hilo kuanzia hapo Bwana mwenyewe atakupa kipawa cha Roho wake Mtakatifu.
Hivyo kama utakuwa tayari kwa ajili ya Tendo hili la ubatizo ambalo ni maagizo la msingi tuliyopewa na Bwana wetu Yesu Kristo kwamba kila aaminiye na kubatizwa ataokoka.(Luka 16:16), itakuwa ni vema sana. Hivyo wewe tayari umeshaamini, hatua iliyobaki kwako ni kubatizwa. Usipuuzie agizo hilo. Tafuta ubatizo sahihi kwa ajili ya kuukamilisha wokovu wako.
Kama utakuwa tayari kwa tendo hilo, basi wasiliana na sisi, inbox au kwa namba hizi hapa chini, tujue pa kukusaidia kwa mahali ulipo. +255693036618 / +255789001312,
Bwana akubariki sana.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hapo juu.
YESU MPONYAJI.
FAHAMU JINSI KRISTO ANAVYOPONYA WATU ROHO.
RABI, UNAKAA WAPI?
VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 6
TUMEPEWA AMRI YA KUKANYAGA NGE NA NYOKA.
Mlima wa Mizeituni ni moja ya milima saba ambayo inauzunguka mji wa Yerusalemu kule Israeli . Mlima huu upo upande wa Mshariki mwa mji huo, umbali usiozidi kilometa moja, mpaka kuuingia mjini Yerusalemu. Hivyo haupo mbali sana.
Umeitwa mlima wa Mizeituni, kutokana na kuwa na sifa ya kuzungukwa na miti mingi ya mizeituni pembezoni mwa mlima huo.
Mlima huu umetajwa mara mbili katika agano la kale, mara ya kwanza ni siku ile Daudi alipokuwa anafukuzwa na mwanawe Absalomu, biblia inatuambia aliupanda mlima huu akiwa analia peku, akiambatana na wale watu aliokuwa nao kwenye ufalme.(2Samweli 15:30).
Sehemu nyingine ni katika kitabu cha Zekaria ambacho kinaeleza unabii wa masihi siku atakaposhuka mara ya pili hapa duniani, kwamba atashukia kwanza juu ya mlima huu;
Zekaria 14:3 “Hapo ndipo atakapotokea Bwana, naye atapigana na mataifa hayo, kama vile alipopigana zamani siku ya vita. 4 Na siku hiyo miguu yake itasimama juu ya mlima wa Mizeituni, unaoelekea Yerusalemu upande wa mashariki, nao mlima wa Mizeituni utapasuka katikati yake, upande wa mashariki na upande wa magharibi; litakuwako huko bonde kubwa sana; na nusu ya mlima ule utaondoka kwenda upande wa kaskazini, na nusu yake itaondoka kwenda upande wa kusini”.
Zekaria 14:3 “Hapo ndipo atakapotokea Bwana, naye atapigana na mataifa hayo, kama vile alipopigana zamani siku ya vita.
4 Na siku hiyo miguu yake itasimama juu ya mlima wa Mizeituni, unaoelekea Yerusalemu upande wa mashariki, nao mlima wa Mizeituni utapasuka katikati yake, upande wa mashariki na upande wa magharibi; litakuwako huko bonde kubwa sana; na nusu ya mlima ule utaondoka kwenda upande wa kaskazini, na nusu yake itaondoka kwenda upande wa kusini”.
Lakini katika agano jipya mlima huu umetajwa mara nyingi kidogo;
Lakini cha kufahamu zaidi ni kuwa habari zote ambazo Yesu Kristo alizitaja kuhusiana na siku za mwisho na kurudi kwake mara ya pili duniani, alizizungumzia juu ya mlima huu wa mizeituni. Utasoma hayo katika (Mathayo 24, Marko 13, Luka 21)
Hata siku ile Yesu alipoulilia mji wa Yerusalemu, juu ya maangamizi yake yaliyo mbeleni, alikuwa amesimama juu ya mlima huu.(Luka 19:37-44)
Na juu ya mlima huu, ndio aliopaa kutoka ulimwenguni, mara ya mwisho alipokutana na wanafunzi wake baada ya siku zile 40 na kuwapa maagizo ya kuhubiri injili, na kuingojea ahadi ya Roho Mtakatifu..
Matendo 1:9 “Akiisha kusema hayo, walipokuwa wakitazama, akainuliwa, wingu likampokea kutoka machoni pao. 10 Walipokuwa wakikaza macho mbinguni, yeye alipokuwa akienda zake, tazama, watu wawili wakasimama karibu nao, wenye nguo nyeupe, 11 wakasema, Enyi watu wa Galilaya, mbona mmesimama mkitazama mbinguni? Huyu Yesu aliyechukuliwa kutoka kwenu kwenda juu mbinguni, atakuja jinsi iyo hiyo mlivyomwona akienda zake mbinguni”.
Matendo 1:9 “Akiisha kusema hayo, walipokuwa wakitazama, akainuliwa, wingu likampokea kutoka machoni pao.
10 Walipokuwa wakikaza macho mbinguni, yeye alipokuwa akienda zake, tazama, watu wawili wakasimama karibu nao, wenye nguo nyeupe,
11 wakasema, Enyi watu wa Galilaya, mbona mmesimama mkitazama mbinguni? Huyu Yesu aliyechukuliwa kutoka kwenu kwenda juu mbinguni, atakuja jinsi iyo hiyo mlivyomwona akienda zake mbinguni”.
JE! MLIMA HUU UNAO UMUHIMU WOWOTE KWETU? NA JE! NI SAHIHI KWENDA KUOMBA JUU YA MLIMA HUU?.
Ni wajibu wetu kujua kuwa huu ndio mlima ambao Kristo atashukia siku ile atakaporudi mara ya pili kuuhukumu ulimwengu na kutawala kama mfalme. Na kama tulivyosoma katika unabii wa Zekaria ni kwamba siku hiyo atakapokuja, mlima huu utagawanyika katikati, upande wa Mashariki, na Upande wa Magharibi, na hapo katikati kutakuwa na bonde kubwa sana. Siku hiyo atauwa waovu wote watakaokuwepo duniani kwa wakati huo.. Kipindi hichi ndio kile biblia inasema kila jicho litamwona, na mataifa yote watamwombolezea, watu watatamani milima iwaungukie kwasababu watauliwa na Kristo mwenyewe. (Mambo hayo watakutana nao wale watakaoukosa unyakuo)
Kwa urefu wa somo hilo fungua hapa >>WATAMTAZAMA YEYE AMBAYE WALIMCHOMA;
Na baadaye akishawamaliza waovu wote ataingia mji wa Yerusalemu, na kisha atatawala kama Mfalme wa Wafalme na Bwana wa Mabwana, juu ya dunia nzima kwa muda wa miaka 1000,
Ataitengeneza upya hii dunia, kutakuwa na amani ya milele isiyoelezeka. Dunia itakuwa kama paradiso. Na wakati huo upo karibuni sana. Hivyo ni wajibu wetu sisi sote kujua mambo yatakayoendelea Israeli katika siku za mwisho, ikiwemo juu ya mlima huu wa mizeituni, ili tujue leo hii tunasimama wapi. Tusiishi tu kama watu wengine wa ulimwengu, wasioona mambo ya mbeleni.
Lakini sasa tukirudi kwenye sehemu ya pili ya swali letu je! Ni Sahihi kwenda kuomba juu ya mlima huu?
Watu wengi wamekuwa wakienda Yerusalemu, kupeleka maombi yao, wakidhania kuwa mahali pale ndipo Mungu atawasikia vizuri zaidi kuliko huku walipo, wengine wamekuwa wakikesha kwenye ule ukuta wa maombolezo, wengine juu ya mlima huu wa Mizetuni, wengine kwenye mto Yordani n.k..
Lakini ukweli ni kwamba kufanya hivyo ni kukosa maarifa ya kutosha juu ya agano tulilo nalo leo hii. Bwana Yesu alimwambia Yule mwanamke;..
Yohana 4:21 “Yesu akamwambia, Mama, unisadiki, saa inakuja ambayo hamtamwabudu Baba katika mlima huu, wala kule Yerusalemu…. 4.23 Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu.
Yohana 4:21 “Yesu akamwambia, Mama, unisadiki, saa inakuja ambayo hamtamwabudu Baba katika mlima huu, wala kule Yerusalemu….
4.23 Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu.
Agano la Damu ya Yesu, ni agano la kimbinguni, kiasi kwamba mtu yeyote mahali popote atasikiwa na Mungu ikiwa tu ataingizwa katika agano hilo lililo bora. Na Mtu ataingia ndani ya agano hilo, kwanza kwa kumwamini Yesu Kristo, kisha kutubu dhambi zake, na baada ya hapo kuwa tayari kubatizwa na kupokea Roho Mtakatifu. Akikamilisha hatua hizo anakuwa ameshaokoka.
Na mtu kama huyo maombi yake yanasikiwa, ziadi hata mtu aliyekwenda kuomba juu ya mlima huu.
Je! Wewe umeingizwa kwenye agano hili?. Je! Una habari kuwa Yesu Kristo yupo mlangoni kurudi? Na unabii huo upo mlangoni kutimia? Unasubiri nini usimkaribishe Kristo moyoni mwako. Bado unatangatanga na ulimwengu ili siku ile ikujie ghafla?. Mambo yatakayoendelea huku duniani kwa watakaoukosa unyakuo hayaelezeki ndugu yangu, Ni heri leo ukayakabidhi maisha yako kwa Yesu. Kama moyo wako leo hii upo tayari kufanya hivyo. Basi uamuzi huo ni wa busara sana. Hivyo fungua hapa kwa ajili ya kupata maelekezo ya sala ya Toba. >>> SALA YA TOBA
Na Bwana akubariki sana.
MAPIGO YA VITASA SABA, NA SIKU YA BWANA.
UFUNUO: Mlango wa 20
Amin, nawaambia, Kizazi hiki hakitapita..