SWALI: Hujambo mpendwa,naomba nieleweshwe hili tafadhali katika mwanzo 22:14 utaona Ibrahimu alipaita mahali pale YEHOVA-YIRE ambapo alimtoa yule kondoo kuwa sadaka, badala ya Isaka, lakini ukisoma tena katika Kutoka 6:2-3 Mungu anamwambia Musa kwamba hakuwai kujidhihirisha kama YEHOVA kwa Ibrahimu ,Isaka, na Yakobo, bali Mungu mwenyezi. Je! Biblia inajipinga? Asante sana.
JIBU: Kumbuka vitabu vitano vya mwanzo vimeandika na mtu mmoja ambaye ni MUSA (Ambavyo ni Mwanzo, kutoka, Mambo ya Walawi, Hesabu na kumbukumbu la Torati ).. Na kama tunavyojua Musa aliviandika vitabu hivi alipokuwa jangwani (yaani akiwa njiani kuelekea nchi ya Ahadi).. Na katika kitabu cha Mwanzo ambacho ndicho tunapata huko habari za Ibrahimu…wakati anaziandika habari hizo akiwa jangwani tayari alikuwa ameshafunuliwa jina hilo jipya la Mungu yaana YEHOVA. Hivyo mahali popote ambapo alisoma habari za Ibrahimu, akimtaja Mungu kwa jina lolote lile yeye Musa ni lazima angeliandika kwa jina YEHOVA, kadhalika mahali popote ambapo Nuhu angemtaja Mungu kwa jina lolote lile yeye Musa angesahihisha katika maandishi yake na kuandika jina YEHOVA badala yake..na hivyo hivyo kwa Lutu, Yakobo, Isaka, Yusufu na wengineo.
Sasa utauliza mbona kila mahali katika vitabu hivyo vitano vya kwanza vya Musa kila mahali Mungu katajwa kama BWANA, na si hilo YEHOVA ??
Kumbuka Katika biblia yetu ya Kiswahili na ya kiingereza na ya lugha nyingine zote…kila mahali ambapo leo hii tunapasoma pameandikwa neno BWANA, Kwa asili hapakupaswa paandikwe hivyo…Sehemu nyingi katika agano la lake unapopaona pameandikwa neno BWANA, kwa asili pangepaswa paandikwe neno YEHOVA. Musa nyingi alizitafsiri kama Yehova..kwa mfano katika
Mwanzo 2:7 biblia inasema
“ Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai”…Mstari huu Musa aliuandika hivi “Yehova Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai ”
Lakini sasa watafsiri wa kwanza biblia waliona ili kuliheshimu zaidi hilo jina la Mungu si vyema kuandika jina hilo Tukufu na kuu kama lilivyo…Hivyo kwa hekima ya Roho ndipo likawekwa jina BWANA badala ya YEHOVA..Kitu ambacho ni kizuri!..kama tu vile isivyo hekima wala heshima kumwita mzazi wako jina lake halisi na badala yake unamwita jina lake la cheo “BABA”..huwezi kusema shikamoo Joseph badala yake utasema shikamoo Baba. Hivyo si dhambi kumwita Mungu BWANA kama inavyochukuliwa leo na ndugu zetu mashahidi wa Yehova wakidhani kuwa kumuita Mungu BWANA ni kumvunjia heshima..
Biblia zote, pale kwenye utangulizi, zimechapishwa na angalizo hilo pale mwanzoni kabisa.. Kuwa BWANA lilimaanisha YEHOVA.
Kwahiyo kitabu cha Mwanzo kimetaja Yehova na kitabu cha Kutoka kwasababu mwandishi ni huyo huyo mmoja, na aliviandika vitabu hivyo akiwa tayari ameshalijua jina la Mungu kamilifu yaani Yehova.
jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Nyinginezo:
Kwanini Bwana alisema Hakuna aliye mwema ila mmoja?
Kwanini wanawake wengi huwa wanalipuka mapepo?
Kwanini kila nikitaka kusali naingiwa na uvivu?
KWANINI BWANA YESU ALISULUBIWA NA WEZI WAWILI?
Kwanini Mungu aliikubali sadaka ya Yeftha ya kumtoa binti yake kafara?
Rudi Nyumbani:
Print this post
Ufunuo 12:12 “Kwa hiyo shangilieni, enyi mbingu, nanyi mkaao humo. Ole wa nchi na bahari! Kwa maana yule Ibilisi ameshuka kwenu mwenye ghadhabu nyingi, akijua ya kuwa ana wakati mchache tu. 13 Na joka yule alipoona ya kuwa ametupwa katika nchi, alimwudhi mwanamke yule aliyemzaa mtoto mwanamume. 14 Mwanamke yule akapewa mabawa mawili ya tai yule mkubwa, ili aruke, aende zake nyikani hata mahali pake, hapo alishwapo kwa wakati na nyakati na nusu ya wakati, mbali na nyoka huyo. 15 Nyoka akatoa katika kinywa chake, nyuma ya huyo mwanamke, maji kama mto, amfanye kuchukuliwa na mto ule. 16 Nchi ikamsaidia mwanamke; nchi ikafunua kinywa chake, ikaumeza mto ule alioutoa yule joka katika kinywa chake. 17 Joka akamkasirikia yule mwanamke, akaenda zake afanye vita juu ya wazao wake waliosalia, wazishikao amri za Mungu, na kuwa na ushuhuda wa Yesu; naye akasimama JUU YA MCHANGA WA BAHARI”.
Ufunuo 12:12 “Kwa hiyo shangilieni, enyi mbingu, nanyi mkaao humo. Ole wa nchi na bahari! Kwa maana yule Ibilisi ameshuka kwenu mwenye ghadhabu nyingi, akijua ya kuwa ana wakati mchache tu.
13 Na joka yule alipoona ya kuwa ametupwa katika nchi, alimwudhi mwanamke yule aliyemzaa mtoto mwanamume.
14 Mwanamke yule akapewa mabawa mawili ya tai yule mkubwa, ili aruke, aende zake nyikani hata mahali pake, hapo alishwapo kwa wakati na nyakati na nusu ya wakati, mbali na nyoka huyo.
15 Nyoka akatoa katika kinywa chake, nyuma ya huyo mwanamke, maji kama mto, amfanye kuchukuliwa na mto ule.
16 Nchi ikamsaidia mwanamke; nchi ikafunua kinywa chake, ikaumeza mto ule alioutoa yule joka katika kinywa chake.
17 Joka akamkasirikia yule mwanamke, akaenda zake afanye vita juu ya wazao wake waliosalia, wazishikao amri za Mungu, na kuwa na ushuhuda wa Yesu; naye akasimama JUU YA MCHANGA WA BAHARI”.
Shalom, Jina la Bwana wetu Yesu Kristo libarikiwe, kama ukisoma mistari iliyotangulia kabla ya hiyo, utaona kuwa shetani kuna majira alijaribu kufanya vita katika mbingu, lakini alishindwa kama biblia inavyotuambia akatupwa chini na mahali pake hapakuonekana tena mbinguni kuanzia huo wakati.
Lakini biblia inatuambia pia alipotupwa, hakukaa katika eneo la nchi peke yake, au hakwenda baharini moja kwa moja , hapana, bali alikwenda kusimama juu ya mchanga wa bahari….Kwa namna nyingine alikwenda kusimama ufukweni mahali ambapo nchi na bahari vinakutana.
Shetani alifahamu kuwa, hivyo ndivyo vitu viwili vinavyoikamilisha dunia, hakuegemea tu upande mmoja afanye makao yake huo hapana..badala yake alisimama pale ufukweni ili aweze kuyaona na kuyatawala yale yanayotoka katika nchi na yale yanayotoka katika bahari. Na ndio maana baada ya pale biblia inasema “Ole wa nchi na bahari”, Kwa maana yule Ibilisi ameshuka kwenu mwenye ghadhabu nyingi, akijua ya kuwa ana wakati mchache tu..
Unaona? haituambii nchi tu peke yake, au bahari peke yake, hapana bali vyote viwili, kwasababu ndipo alipopania kuwanasa wanadamu.
SASA NCHI NA BAHARI KIBIBLIA VINAWAKILISHA NINI?
BAHARI: au sehemu yenye maji mengi, biblia imeshatupa majibu yake,.Tusome.
Ufunuo 17:15 “Kisha akaniambia, Yale maji uliyoyaona, hapo aketipo yule kahaba, ni jamaa na makutano na mataifa na lugha”.
Kumbe maji yanawakilisha jamaa, na makutano na mataifa na lugha…Yaani kwa ufupi watu wengi.
Vilevile, tunaweza kuona jambo lingine, pale Bwana Yesu alipochagua mitume wake, wengi wao aliwachagua kutoka katikakati ya wavuvi, akifunua kuwa watakuja kufanya kazi ya uvuvi wa watu wengi, yaani jamaa, na mataifa la Lugha, kama alivyomwambia Petro na Andrea katika (Mathayo 4:19)..
Hivyo Bahari inawakalisha watu wengi, kwahiyo shetani tangu alipoona ameshindwa hawezi tena kupigana yeye kama yeye aliamua sasa kuelekeza macho yake katikati ya watu ili apate nguvu, na chombo kikubwa anachokitumia ili kupata ufuasi mkubwa wa watu ni kupitia kitu kinachoitwa DINI, penye dini ndipo palipo na watu wengi, sio katika siasa au makabila..
Hivyo mpaka sasa yupo katika kilele cha kuzikutanisha dini zote na madhehebu yake yote ambayo tangu zamani yalishautupilia mbali uongozo wa Roho Mtakatifu na kufuata mapokeo yao ya kibinadamu, ili zikubaliane katika kitu kimoja.
Na ndio maana ukisoma ile sura inayofuata ya 13, utaona Yule joka aliposimama tu pale kwenye mchanga wa bahari, wakati huo huo wanyama wawili walitokea, mmoja alitokea baharini, na mwingine akatokea nchi kavu (Soma ufunuo sura ya 13 yote utaona)..Sasa Yule aliyetokea habarini ndiyo huyu atakayepata nguvu ya kuwa na wafuasi wengi sana duniani kwa kupitia dini…
NCHI: NI Hifadhi ya kimwili, tangu mwanzo, Mungu alipomuumba Adamu alimpa ardhi ailime na kuitunza kwasababu huko ndipo alipomchipulia chakula chake kitakachomfanya aishi hapa duniani.
Ayubu 28:5 “Katika ardhi ndimo kitokeamo chakula;…”..
Hata sasa chakula na utajiri vipo katika ardhi..Hivyo kwa lugha ya sasa nchi tunaweza kusema inawakilisha Uchumi,..Fedha, biashara, hazina, vitu vinavyoweza kumpatia mwanadamu Rizki ili aishi hapa duniani n.k…
Kwahiyo shetani kuona hivyo, alisimama pia katika eneo hilo.. tangu huo wakati akajikita kudhibiti mihimili hiyo miwili mikuu, Watu, na uchumi.. nchi na bahari..
Kwanza Ili awapate Watu anatumia kivuli cha dini, ambapo hivi karibu anaenda kutimiza adhma yake ya kuzileta dini zote zilizopoteza uongozo wa Roho Mtakatifu pamoja, zikiongozwa na ile dini mama ya Rumi, na cha ajabu biblia inatuambia watu wote na mataifa yote ambao majina yao hayakuandikwa katika kitabu cha uzima cha mwanakondoo tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu wataufurahia huo utawala na mfumo mzima wa ibilisi ..
Na sasa ili kuwalazimisha watu wote waufuate huo mfumo wa mpinga-Kristo, shetani atamnyanyua mnyama mwingine ambaye atakuwa na nguvu ya kiuchumi sana,(taifa kubwa) ambalo hilo litayahimiza mataifa mengine yote yapokee maagizo kutoka kwa huo umoja wa dini duniani, na mtu yoyote atakayekataa kuupokea hataruhusiwa kununua wala kuuza, wala kufanya biashara yoyote, wala kuajiriwa mahali popote.. Unaona Jinsi hali itakavyokuwa mbaya.. Ni nani atapona hapo.
Haya ni mambo ambayo tunaweza kuyashuhudia siku za hivi karibuni wala tusidhani bado miaka mingi, jaribu kufikiria jinsi ugonjwa huu wa Corona ulivyozuka tu ghafla, na athari yake ndogo tu inawafanya watu wasiweze kutembea hata nje katika baadhi ya nchi, na imetokea tu ndani ya kipindi kifupi cha miezi mitatu tu, hakuna ambaye angeamini kuwa dunia ingeweza kuwa namna hii, dunia ambayo inashamra shamra za kila namna..Lakini mambo yamekuwa hivyo barabara zipo wazi..Hata matajiri na wana wa wafalme, na watu mashuhuri na fedha zao haziwasaidii wakati huu. Ndivyo mambo yatakavyobadilika ghafla tu wakati huo ukifika.
Shetani ameshajidhatiti vya kutosha, na ghafla tu, dini zote zitafikia muafaka mmoja zikiongozwa na dini ile mama ya Rumi, watafikia muafaka mmoja, watapata sapoti kutoka katika kila pembe ya dunia, watakuwa na kiongozi wao mmoja ambaye ndio atakuwa mpinga-Kristo..Huyo ataishawishi dunia iwe na ustaarabu mpya, Lakini lengo lake ni kuihimiza ile chapa ya mnyama ili awanase wanadamu wote.. Sasa kwa kuwa yeye amejikita katika masuala ya kiimani sana, kama tulivyosema atapata msaada mwingine kutoka katika taifa lenye nguvu ya kiuchumi duniani, ili kuyalazimisha mataifa mengine yote yamtii yeye kwa shuruti.
Mpaka wakati huo umefika ujue unyakuo tayari umeshapita ndugu yangu, sijui utakula nini wewe unayemkataa Yesu leo, wewe ambaye utakuwepo ulimwenguni wakati huo, pona yako itakuwa ni kufia njaa ndani, kama utakuwa hujakamatwa na kuuliwa kwa mateso yasiyokuwa ya kawaida.. Hakuna mtu yoyote atayevumiliwa na mtu au chombo chochote cha dola ambaye ataonekana hajapokea chapa hiyo ya mnyama.. usifikiri utapona..Ni ngumu sana ndugu, usidhani akaunti yako ya benki itakusaidia wakati huo, hilo jambo halitakuwepo, usidhani utakimbilia mafichoni, ondoa hayo mawazo, usidhani elimu yako itakusaidia kupata ajira wakati huo, acha kufikiria hivyo..Chapa utaipokea tu.
Hizi ni nyakati za hatari tunazoishi, ole wa nchi na bahari!…Kimbilio pekee ni Kristo tu saa hii..Ikiwa upo bado nje ya Kristo, basi fanya uamuzi wa Busara leo hii, tubu dhambi zako kwa kumaanisha kuziacha, omba toba kwa Mungu, nenda kabatizwe ikiwa bado hujafanya hivyo. huu ni wakati sasa wa kuamka usingizini.
Warumi 13:11 “Naam, tukiujua wakati, kwamba saa ya kuamka katika usingizi imekwisha kuwadia; kwa maana sasa wokovu wetu u karibu nasi kuliko tulipoanza kuamini”.
Bwana akubariki sana.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312
UFUNUO: Mlango wa 13
UCHAWI WA BALAAMU.
CHUKIZO LA UHARIBIFU
DANIELI: Mlango wa 7
MWISHO WA DUNIA UTAKUJAJE?
Nini maana ya “Siku moja nyuani mwa Bwana ni bora kuliko miaka elfu”?
Hesabu 23:23 “Hakika hapana uchawi juu ya Yakobo, Wala hapana uganga juu ya Israeli”
Wengi tunalifahamu hili andiko na tunalitumia, pale tunapohisi roho za kichawi zinatunyemelea…Na tunapolitumia kwa Imani linaleta majibu hakika kwasababu ni pumzi ya Mungu…Lakini hebu leo tuingie kwa undani kidogo kujifunza juu ya Neno hili ili tupate faida mara mbili Zaidi.
Siku zote tunashauriwa tujifunze biblia na sio tuisome tu…tukichukua tu kipengele cha mstari wa biblia na kukitumia hicho bila kutafuta maana ya mstari huo, kwanini mwandishi aliandika hivyo, na Mungu alikuwa anamaanisha nini juu ya mstari huo..hapo tutakuwa hatujajifunza bali tumesoma tu..ambapo matokeo yake ni madogo kuliko kama tungeketi chini na kujifunza kuanzia juu chanzo cha mstari huo na dhima, na maudhui ya huo mstari ukoje.
Sasa tukirudi katika mstari huo hapo juu, kama ukianza kusoma kitabu hicho cha Hesabu kuanzia sura zilizotangulia kabla ya hiyo ya 23, utaona inahusu safari ya wana wa Israeli (au wana wa Yakobo), walipokuwa wanatoka Misri kuelekea nchi yao ya Ahadi,
Wakiwa njiani jangwani walikutana na kikwazo, Ilikuwa kwamba ili waendelee na safari yao iliwapasa wakatize katika nchi ya watu fulani ambao walijulikana kama wamoabu.
Nchi hiyo ilikuwa na mfalme na huyo mfalme akawakatalia wasikatize katika nchi hiyo, na hakukuwa na njia nyingine ya karibu isipokuwa kukatiza katika nchi hiyo..Ijapokuwa waliwaomba sana na kuwaahidi kwamba watalipia gharama zote za uharibifu wowote kama ukijitokeza katika kukatiza kwao lakini wenyeji wa mji ule walikataa katakata wakiongozwa na mfalme wao..Na kwa hofu Mfalme wao hakuishia tu kuwazuia bali alipanga pia kwenda kupigana nao, hivyo akatafuta pia namna ya kuwalaani(au kwa lugha rahisi kuwaloga) ili atakapokwenda kupigana nao aweze kuwashinda kirahisi bila kutumia nguvu nyingi.
Katika harakati za kutafuta mtu mashuhuri wa kuloga, akampata mtu anayeitwa Balaamu mchawi (Hesabu 24:1), huyu alikuwa ni mchawi wa viwango vya juu sana na aliyejulikana kwa kuloga hata mataifa, ambaye alitumia nguvu za giza, na alikuwa anauwezo wa kuisikia pia sauti ya Mungu..na kabla ya kuloga alikuwa anauwezo wa kupima kiwango cha kiroho mtu alichopo kabla ya kumwangusha…na sio hilo tu, alikuwa anazo mpaka mbinu mbadala zisizo za kuweza kumwangusha mtu bila kutumia uchawi wowote…(na huo ndio mbaya Zaidi ambao ndio alioutumia kuwaangusha wana wa Israeli).
Sasa alipoitwa kama wengi wetu tunavyoijua habari…haraka sana aliwajua wana wa Israeli ni watu gani…alijua ni watu wa Mungu na wamezungukwa na ukingo wa Mungu pande zote…hakuna namna ya kuweza kuwaingia kwa njia ya uganga wala uchawi (hakuna namna yoyote vibuyu na dawa za miti shamba zinaweza kufanya kazi juu yao)..hata hivyo alinusurika kifo njiani wakati anajaribu kutaka kwenda kuwalaani…Ili litimie lile neno la kwanza (akulaaniye atalaaniwa, na akubarikiye atabarikiwa).
Hivyo Balaamu alilijua hilo na alipofika kwa mfalme wa MOABU akamwambia wazi kabisa kwamba “HAKIKA HAPANA UCHAWI JUU YA YAKOBO, WALA HAPANA UGANGA JUU YA ISRAELI”.
Hiyo ndiyo asili ya Neno hilo…Ni mchawi Balaamu ndiye aliyeyasema maneno hayo sio Mungu kama wengi wetu tunavyodhani. Balaamu alikiri kabisa..Hivyo akaacha kujaribu kuwaloga/kuwalaani Israeli ambaye ndiye Yakobo, kinyume chake akawabariki, kwasababu alijua endapo angetaka kuwaalaani ni kujitafutia laana na kifo..hivyo akaamua kuhamia kwenye Mbinu yake ya pili ambayo ndiyo KUBWA NA KUU.
Hesabu 24:1 “Basi Balaamu alipoona ya kuwa ilimpendeza Bwana kuwabariki Israeli, hakwenda, kama hapo kwanza, ili kutafuta uchawi, bali alielekeza uso wake jangwani”
Mbinu hiyo siyo ya kutumia vitunguli tena/wala vibuyu/ wala ya kuwatamkia maneno mabaya..Mbinu hii ya pili ambayo ndio UCHAWI HASAA ni ya kuwakosesha wana wa Israeli na Mungu wao..Ili Mungu awakasirikie na kuwaadhibu yeye mwenyewe…kwasababu kuwaangusha kwa njia ya uchawi imeshindikana sasa dawa ni kuwachonganisha na Mungu wao..Hivyo akamfundisha Mfalme wa Moabu namna ya kuwakosesha wana wa Israeli ili wapigwe na Mungu wao..
Akamfundisha na kumwambia wawaalike wana wa Israeli baadhi katika sadaka za miungu yao na kuwapa wanawake wao walio wazuri na warembo, hivyo Wana wa Israeli watakapoona hivyo wataingia tamaa na kuzini na wanawake hao katika karamu hizo za miungu na hasira ya Mungu itawaka juu ya wana wa Israeli..Tusome
Hesabu 25:1 “Basi Israeli akakaa Shitimu, kisha watu wakaanza kuzini pamoja na wanawake wa Moabu; 2 kwa kuwa waliwaalika hao watu waende sadakani, sadaka walizowachinjia miungu yao; watu wakala chakula, wakaisujudu hiyo miungu yao. 3 Ikawa Israeli kujiungamanisha na Baal-peori; hasira za Bwana zikawaka juu ya Israeli”.
Hesabu 25:1 “Basi Israeli akakaa Shitimu, kisha watu wakaanza kuzini pamoja na wanawake wa Moabu;
2 kwa kuwa waliwaalika hao watu waende sadakani, sadaka walizowachinjia miungu yao; watu wakala chakula, wakaisujudu hiyo miungu yao.
3 Ikawa Israeli kujiungamanisha na Baal-peori; hasira za Bwana zikawaka juu ya Israeli”.
Ukiendelea kusoma utaona Mungu aliwakasirikia na aliwaua kwa pigo watu elfu 24. Kama sio mtu mmoja kwenda kurekebisha Israeli wote wangeisha siku hiyo mbele ya ghadhabu ya Mungu..Hivyo japokuwa Yule mchawi balaamu hakuwaloga kwa uchawi wa uganga na vibuyu lakini aliwaloga kwa kuwakosesha na Mungu wao.
Jambo hilo hilo linaendelea hata sasa katika nyakati hizi za agano jipya. Ni kweli hakuna uganga wala uchawi juu yako, umelindwa na kuzungukwa na kingo za moto pande zote, katika afya yako, katika kazi zako, katika familia yako, mpaka una ujasiri wa kusema Bwana ndiye anisaidiaye sitaogopa mabaya, wala uchawi wala uganga..Ndio shetani analijua hilo na wala hawezi kukuloga kwa vitunguli, wanaokuendea kwa waganga ni kweli wanapoteza muda..nataka nikuambie shetani akishalijua hilo wala hapotezi muda wake kukutumia watu kutafuta kukuloga wewe…kwasababu hawezi kulaani kilichobarikiwa…hviyo acha kufikiri kwamba wachawi wanakuwinda wewe uliyeokoka kweli kweli, walishaacha siku nyingi wakati ule walipogundua tu unazungukwa na jeshi la mbinguni…
Shetani anachofanya sasa juu yako ni kutafuta njia ya kukukosesha wewe na Mungu wako, ili Mungu akuadhibu…na anatumia watu mfano wa Balaamu..wanaoonekana nje ni watu wa Mungu kumbe ndani ni mbwa-mwitu wa kali…Hao watakwambia kuoa mke wa pili si dhambi, watakwambia kuziangukia sanamu na kuzibusu na kuzipa heshima sio kuzisujudia.
Na biblia imeshatabiri nyakati hizi za mwisho watu wengi wataangukia katika kosa hili la Balaamu..
Yuda 1:11 “Ole wao! Kwa sababu walikwenda katika njia ya Kaini, na kulifuata kosa la Balaamu pasipo kujizuia, kwa ajili ya ujira, nao wameangamia katika maasi ya Kora”.
Watakwambia kufanya matambiko ya ukoo sio dhambi, watakuwambia kuishi na mwanamke/mwanamume ambaye hamjaoana hakuna tatizo, watakuwambia kuzini ni mapungufu ya kila mtu, watakuweka katika kila kishawishi cha wewe kufanya dhambi, , Zaidi sana watakufariji katika dhambi na watakukemea katika kuwa mtakatifu…lengo na madhumuni ni kukukosesha wewe na Mungu wako ili Mungu akukasirikie na kukuangamiza (Huo ndio uchawi mkubwa shetani anaowalogea watu wa Mungu kuliko hata ule wa vibuyu)..
Bwana Yesu alisema maneno hayo Dhahiri katika Ufunuo.
Ufunuo 2:14 “Lakini ninayo maneno machache juu yako, kwa kuwa unao huko watu washikao mafundisho ya Balaamu, yeye aliyemfundisha Balaki atie ukwazo mbele ya Waisraeli, kwamba wavile vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu, na kuzini”.
Je! Na wewe umedanganyika na uchawi huo wa Balaamu? Nabii wa uongo?..Unadhani shetani anahangaika na bati lako usiku na kundi lake la wachawi?..usidanganyike!..anahangaika sasa kukukosesha na Mungu wako. Hataki ulifahamu neno na anafanya juu chini ufe katika dhambi zako ili siku ile uingia katika adhabu ya hasira ya Mungu katika ziwa la moto. Hivyo mwache aende peke yake huko yeye na mabalaamu wake, sisi tujitenge na yeye kwa kutubu leo na kushika amri za Mungu na Neno lake, kwa kujitenga na uasherati wote, wizi, rushwa, anasa, tamaa mbaya, wivu, matusi, na mambo yote machafu na kuzidi kujitakasa kila siku, na kuishi katika utakatifu ndipo tutakapojiepusha na ghadhabu ya Mungu na kupata baraka zote alizozikusudia katika Maisha yetu. Hatuna haja ya kuogopa wachawi wa vibuyu kwasababu huko waliko wanakiri kwamba hakuna uchawi wala uganga kwa waliokoka..
Sisi tupambane kujilinda na dhambi ndilo jukumu tulilolonalo sasa.
KITABU CHA YUDA: SEHEMU YA 1
KIFO CHA MTAKATIFU PERPETUA NA FELISTA.
WAKAMTUKANA MUNGU, WALA HAWAKUTUBU.
NENO NI LILE LILE, LAKINI UJUMBE NI TOFAUTI.
VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 2
JINA LA MUNGU NI LIPI?
Nakusalimu katika jina kuu la mwokozi wetu Yesu Kristo. Karibu tujifunze maneno ya uzima..
Kwanini mara nyingine tunakuwa ni wepesi kufanya dhambi, ni wepesi kuwasengenya majirani zetu, ni wepesi kwenda kuzini, licha ya kwamba tunasema tumeokoka, au tupo karibu na Mungu, lakini bado ni wepesi kutazama picha chafu mitandaoni na kufanya masturbation….
Ni kwasababu tunamdhania Mungu yeye ni kama sisi, kwamba anaelewa tu! Ni madhaifu ya kawaida ya mwili..Na kibaya Zaidi pale tunapoona Mungu hachukui hatua yoyote ya adhabu katika ouvu tulioufanya, pengine pale tulipoenda kutazama picha chafu mitandaoni halafu Mungu akakaa kimya, halafu kesho yake tena tukarudia jambo hilo hilo na bado akawa yupo vilevile, hakuna lolote baya amelifanya katika Maisha yetu, kesho kutwa tena tukaenda kuzini, jambo likawa vilevile, kanisani tunahudhuria, kwaya tunaimba, maombi tunafanya, wala hakuna shida yoyote, wiki ijayo tukaanza kuwazungumizia vibaya majirani zetu, tulikuwa hatuli rushwa wala hututoi rushwa lakini tulipoanza kula rushwa na tukaona hakuna jambo lolote baya lililotukuta basi ndio ikawa desturi yetu kufanya hivyo, licha ya kuwa unasema ni mkristo.
Imekuwa hivyo hivyo miaka nenda miaka rudi, unawaza moyoni na kusema “hata Mungu anaelewa mambo haya”, ndio maana haniadhibu kwa lolote, Unadhani yeye ni kama wewe, Unadhani anavyowaza juu ya maovu ni kama wewe unavyowaza, unamchukulia kama mtu mwenzako asiyeweza kujali mambo madogo madogo kama hayo, unadhani kuwa hawezi kukuacha, wala kukuadhibu kwa vitu kama hivyo..
Lakini leo sikiliza Neno la Mungu linavyosema..
Zaburi 50:16 “Bali mtu asiye haki, Mungu amwambia, Una nini wewe kuitangaza sheria yangu, Na kuliweka agano langu kinywani mwako? 17 Maana wewe umechukia maonyo, Na kuyatupa maneno yangu nyuma yako. 18 Ulipomwona mwivi ulikuwa radhi naye, Ukashirikiana na wazinzi. 19 Umekiachia kinywa chako kinene mabaya, Na ulimi wako watunga hila. 20 Umekaa na kumsengenya ndugu yako, Na mwana wa mama yako umemsingizia. 21 NDIVYO ULIVYOFANYA, NAMI NIKANYAMAZA; UKADHANI YA KUWA MIMI NI KAMA WEWE. Walakini nitakukemea; Nitayapanga hayo mbele ya macho yako. 22 Yafahamuni hayo, Ninyi mnaomsahau Mungu, Nisije nikawararueni, Asipatikane mwenye kuwaponya”
Zaburi 50:16 “Bali mtu asiye haki, Mungu amwambia, Una nini wewe kuitangaza sheria yangu, Na kuliweka agano langu kinywani mwako?
17 Maana wewe umechukia maonyo, Na kuyatupa maneno yangu nyuma yako.
18 Ulipomwona mwivi ulikuwa radhi naye, Ukashirikiana na wazinzi.
19 Umekiachia kinywa chako kinene mabaya, Na ulimi wako watunga hila.
20 Umekaa na kumsengenya ndugu yako, Na mwana wa mama yako umemsingizia.
21 NDIVYO ULIVYOFANYA, NAMI NIKANYAMAZA; UKADHANI YA KUWA MIMI NI KAMA WEWE. Walakini nitakukemea; Nitayapanga hayo mbele ya macho yako.
22 Yafahamuni hayo, Ninyi mnaomsahau Mungu, Nisije nikawararueni, Asipatikane mwenye kuwaponya”
Angalia tena ule mstari wa 21 anasema.. “Ndivyo ulivyofanya, nami nikanyamaza; ukadhani ya kuwa mimi ni kama wewe”…Unaona, Mungu anapokaa kimya kutokana na dhambi zako unazozifanya kwa siri, usidhani yeye anakufurahia tu!.. Unasema umeokoka na huku unayo mambo yako ya siri ambayo unajua kabisa ni machukizo kwa Mungu, lakini Mungu hakusemeshi kwa lolote na wewe umestarehe tu, unadhani Mungu ni kama wewe, ataendelea na wewe hivyo siku zote..La! Anasema atakurarua na asipatikane mtu wa kukuponya..
Hasemi atakupiga tu, halafu basi au atakuadhibu, hapana anasema atakurarua..Na unajua anayerarua ni mnyama mkali kama vile simba, maana yake ni kuwa atakuharibu vibaya sana, kiasi cha kwamba hutaweza kusimama tena baada ya hapo, hata uombeweje, au uhubiriweje, hutaweza tena kusimama…Ndio maana anasema hapo “asipatikane mtu wa kukuponya”
Na ujumbe huo Mungu anausema kwa wale wote wanaomsahau..Inamaanisha kuwa hapo mwanzo walishawahi kuwa wake, lakini wakamzoelea wakamwona kama yeye ni kama wao, wakawa hawaogopi tena kufanya dhambi mbele zake..
Ndugu ikiwa wewe ni mmojawapo, Basi wakati wako wa kutubu kwa kumaanisha ndio huu, pengine umebakisha kipindi kifupi sana kukumbana na makucha hayo ya Mungu (Usitafute kuujua upande wa pili wa ghadhabu ya Mungu, kwasababu inatisha sana).. Ikiwa unafanya dhambi kisirisiri za kujirudia rudia ambazo hazimpendezi Mungu, na umekuwa ukizifanya kwa muda mrefu sasa na Mungu amekaa kimya tu, ni heri usiendelee kuzifanya, kwasababu kwa kukaa kwake kimya hivyo usidhani yeye ni kama wewe..
Hivyo chukua hatua sasa ya kuuimarisha wokovu wako, na Mungu atakusamehe na kuiahirisha ghadhabu yake kwako.
Kumbuka hizi ni nyakati za mwisho, hakuna haja ya kuthibitishiwa tena kuwa tunaishi katika majira ya kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo, hali halisi yenyewe inaonekana kwa mambo yanayoendelea sasa hivi duniani, hivyo huu si wakati wa kuweka mguu mmoja kwa Kristo na mwingine nje, huu ni wakati wa kuzama moja kwa moja kwa Bwana, kwasababu UNYAKUO sasa ni wakati wowote.
2Petro 1:10 “Kwa hiyo ndugu, jitahidini zaidi kufanya imara kuitwa kwenu na uteule wenu; maana mkitenda hayo hamtajikwaa kamwe”.
Bwana akubariki.
JINSI NEEMA YA MUNGU ILIVYOKUWA KUBWA KWA MKE WA LUTU.
MUNGU WETU, JINSI LILIVYO TUKUFU JINA LAKO DUNIANI MWOTE!
KWANINI UNAPASWA UJIWEKE TAYARI SASA, KABLA YA ULE WAKATI KUFIKA?.
KWA VILE ALIVYOKUWA MTU WA HAKI.
KRISIMASI (CHRISTMAS) NI NINI? JE IPO KATIKA BIBLIA?
Mitume wote waliopita walikuwa ni watu weupe hata manabii wote waliopita hadi Ma-papa ni ngozi nyeupe. ni kweli ngozi nyeusi ililaaniwa ?
Pasaka ni nini kibiblia?, na je tunaruhusiwa kusheherekea pasaka sisi wakristo kama wayahudi?
Pasaka ni neno la Kiswahili ambalo limetokana na neno la kigiriki “pascha” ambalo tafsiri yake kwa lugha ya kiingereza ni “passover” kwa Kiswahili ni “pita juu”. Hivyo pasaka kwa Kiswahili tunaweza kusema tafsiri yake ni “pita juu au vuka upite”.
Asili ya Neno hili ni siku ile wana wa Israeli walipokuwa wanatolewa kutoka Misri, usiku ule ambao ndio walikuwa wanatoka Misri, Bwana Mungu aliwaagiza wasitoke kwenye nyumba zao kwamba mpaka watakapomchinja yule Mwanakondoo na damu yake kuipaka katika miimo miwili ya Milango…ili wakati yule malaika ambaye alitumwa kuwaangamiza wazaliwa wa kwanza wote wa wanadamu na wanyama waliokuwepo katika Misri nzima..atakapopita katika kila nyumba na kuiona damu hiyo ya mwanakondoo kwenye miimo ya mlango basi hataingia katika nyumba hiyo kumharibu mzaliwa wa kwanza wa nyumba hiyo “ATAVUKA JUU, AU ATAPITA JUU” Kuendelea na nyumba nyingine…na atakapofika katika nyumba nyingine na kukuta damu juu ya miimo ya mlango kama nyumba ya kwanza vile vile ATAPITA JUU na kuendelea mpaka atakapokuta nyumba ambazo hazina damu hiyo, ndipo ataingia na kuangamiza.
Kutoka 12:12 “Maana nitapita kati ya nchi ya Misri usiku huo, nami nitawapiga wazaliwa wa kwanza wote katika nchi ya Misri, wa mwanadamu na wa mnyama; nami nitafanya hukumu juu ya miungu yote ya Misri; Mimi ndimi Bwana. 13 Na ile damu itakuwa ishara kwenu katika zile nyumba mtakazokuwamo; nami nitakapoiona ile damu, NITAPITA JUU YENU, lisiwapate pigo lo lote likawaharibu, nitakapoipiga nchi ya Misri”.
Kutoka 12:12 “Maana nitapita kati ya nchi ya Misri usiku huo, nami nitawapiga wazaliwa wa kwanza wote katika nchi ya Misri, wa mwanadamu na wa mnyama; nami nitafanya hukumu juu ya miungu yote ya Misri; Mimi ndimi Bwana.
13 Na ile damu itakuwa ishara kwenu katika zile nyumba mtakazokuwamo; nami nitakapoiona ile damu, NITAPITA JUU YENU, lisiwapate pigo lo lote likawaharibu, nitakapoipiga nchi ya Misri”.
Hivyo hicho kitendo cha kuvuka na KUPITA JUU ndicho kinachoitwa Passover, kwa kigiriki Pascha, kwa Kiswahili PASAKA.
Sasa katika Agano jipya damu ya mwanakondoo yule ndio inayofanananishwa na damu ya Bwana wetu Yesu Kristo, Sisi tuliokuwa dhambini tulipotolewa dhambini (yaani Misri yetu) na tunapoelekea nchi yetu ya ahadi mbinguni…Damu ya Yesu ndiyo iliyotuokoa na laana ya Mungu dhidi ya watu wote walio katika dhambi..Na damu ya Yesu ni ishara ya Agano kwamba kwa kupitia damu yake tunalindwa na hukumu ya Mungu..Hukumu ya Mungu inapoachiliwa au itakapoachiliwa tutakuwa tumefunikwa chini ya damu ya Yesu na Malaika yule wa hukumu ATAPITA JUU YETU, na tutanusurika na hukumu ya Mungu.
Swali ni Je tunaruhusiwa kusheherekea pasaka kama watu wengine?
Tafsiri ya kusheherekea kibiblia ni tofauti na tafsiri ya kusheherekea kama inavyotafsiriwa na ulimwengu. Tafsiri ya sherehe kwa ulimwengu ni kula, na kunywa na kulewa, na kwenda kujiburudisha, kujifurahisha, kufanya uasherati, kujisisimua na kufanya anasa na kufanya kila aina ya mambo ya kimwili.
Lakini kibiblia tafsiri ya kusheherekea sio hiyo…Hata wayahudi hawakusheherekea Pasaka kwa hivyo…Kibiblia, kusheherekea ni kujiweka katika ibada, na ibada sio kwenda kanisani tu..bali kujinyenyekeza na kujishusha chini ya uwepo wa Mungu, kwa kuomba, kusali, na kuzidi kujitakasa mbele zake huku tukikumbuka kuwa kwa tukio kama hili lililowahi kutokea miaka mingi iliyopita Bwana alitupa wokovu kwa kupitia damu yake pale Kalvari. Hivyo ni wakati wa kumwekea Bwana nadhiri, wakati wa kuishiriki meza ya Bwana katika vigezo vya kimaandiko, ni wakati wa kusamehe Zaidi (sio kwamba sasa hatupaswi kusamehe mpaka siku ya pasaka ifike, hapana! tunasamehe kila siku, siku hiyo ikifika ni kumalizia tu kuvisafisha vile vidogo ambavyo tulikuwa hatujavimalizia), kwasababu utakatifu sio tu siku ya pasaka hapana bali kila siku!, siku hiyo ni kumalizia tu kuvisafisha vile vichache ambavyo vilikuwa vimesalia. Hivyo hiyo ndiyo tafsiri ya sherehe. Tukisheherekea kwa namna hiyo kuna amani fulani na furaha ya ajabu ambayo Mungu anaimimina ndani yetu..
Lakini tukisheherekea kidunia kwamba ndio siku ya kutafuta kwenda disko, ndio siku ya kwenda kulewa, ndio siku ya kuvaa nguo za nusu-uchi na kutembea nazo barabarani, kwamba ndio siku ya kwenda kwenye dansi, n.k..Tutakuwa tumejitafutia laana badala ya Baraka..Tutakuwa tumeshirikiana na shetani asilimia mia kuudhihaki na kuuzalilisha msalaba wa Kristo, na damu yake ya thamani. Hivyo tutakuwa tumejiharibia wenyewe. Lakini tukisheherekea kibiblia tutapata baraka.
(Pasaka ni nini)
Jiunge na kundi letu la mafundisho ya Biblia whatsapp kwa kubofya hapa > Group-whatsapp
Mada Nyinginezo
Je! kuna sikukuu za pasaka mbili? (Hesabu 9:11)
Easter ni nini?..Na je tunaruhusiwa kuisheherekea?
Ijumaa kuu ni nini? Na kwanini iitwe kuu?
KWA MIOYO YAO WAKAREJEA MISRI.
Je! Karamu za ‘Idi’ ndio zipo hizo tunazozisoma katika Hosea (12:9)
Ni muda gani Bwana Yesu alisulibiwa. Je! Ni saa 3 au saa 6?
HAPANA MFUPA WAKE UTAKAOVUNJWA.
JE! UTATOA HESABU YA NINI KATIKA SIKU ILE?
SWALI: Nini maana ya “Tusitweze unabii”?
JIBU: Tusome..
1Wathesalonike 5:19 “Msimzimishe Roho; 20 msitweze unabii; 21 jaribuni mambo yote; lishikeni lililo jema; 22 jitengeni na ubaya wa kila namna”.
1Wathesalonike 5:19 “Msimzimishe Roho;
20 msitweze unabii;
21 jaribuni mambo yote; lishikeni lililo jema;
22 jitengeni na ubaya wa kila namna”.
Maana ya neno “kutweza” ni kudharau au kupuuzia jambo fulani…Hivyo biblia inaposema msitweze unabii maana yake ni “msiudharau/msiupuuzie unabii”..Na unabii unaozungumziwa hapo ambao haupaswi kutwezwa (maana yake haupaswi kudharauliwa/kupuuziwa)..ni unabii wa kurudi kwa Bwana mara ya pili.. ambao Mtume Paulo aliwaonya Wakristo hao waliopo Thesalonike mwanzoni kabisa mwa sura hiyo ya tano(5). Tusome..
1 Wathesalonike 5:1 “Lakini, ndugu, kwa habari ya nyakati na majira, hamna haja niwaandikie. 2 Maana ninyi wenyewe mnajua yakini ya kuwa siku ya Bwana yaja kama vile mwivi ajavyo usiku. 3 Wakati wasemapo, Kuna amani na salama, ndipo uharibifu uwajiapo kwa ghafula, kama vile utungu umjiavyo mwenye mimba, wala hakika hawataokolewa”.
1 Wathesalonike 5:1 “Lakini, ndugu, kwa habari ya nyakati na majira, hamna haja niwaandikie.
2 Maana ninyi wenyewe mnajua yakini ya kuwa siku ya Bwana yaja kama vile mwivi ajavyo usiku.
3 Wakati wasemapo, Kuna amani na salama, ndipo uharibifu uwajiapo kwa ghafula, kama vile utungu umjiavyo mwenye mimba, wala hakika hawataokolewa”.
Huu ndio unabii wa kwanza ambao haupaswi kupuuziwa hata kidogo, na haukuandikwa kwa Wathesalonike tu peke yao, bali hata kwetu sisi, kwasababu ndio tunaoishi ukingoni mwa nyakati kabisa kuliko vizazi vyote vilivyotangulia. Ukisoma sura yote ya 5 hiyo ambayo ndio ya mwisho kabisa ya kitabu hicho cha 1Wathesalonike utaona jinsi biblia inavyotuonya kwa msisitizo mkubwa kujiweka tayari na siku hiyo ya kurudi kwa pili kwa Kristo, Kwamba siku hiyo inakuja kama mwivi na tusilale usingizi kama wengine walalavyo, na TUSIUUPUUZIE WALA KUUDHARAU HUO UNABII…Kwasababu ni kweli siku hiyo yaja na Mungu hawezi kusema uongo…wote wanaoudharau huo unabii siku hiyo itawajia kama mwivi na kutakuwa na maombolezo makubwa na majuto makubwa, watatamani warudishwe dakika tano nyuma warekebishe mambo yao, lakini itashindikana.
Na hautwezwi kwa midomo tu bali matendo pia…Mtu ambaye hajajiweka tayari kwa kumwamini Yesu Kristo na kutubu dhambi zake kwa kumaanisha kuziacha, na kuishi kulingana na Neno la Mungu, ingawa kila siku anasikia injili lakini anapuuzia mtu huyo ANAUTWEZA UNABII, hali kadhalika mtu ambaye kila siku anasikia habari za kurudi kwa Kristo mara ya pili na anadhihaki na kudharau na kuwaona wanaomgoja Bwana ni watu waliorukwa na akili, na wanaopoteza muda wao, au wamepoteza dira ya Maisha, huyu naye anafanya dhambi hiyo hiyo ya kuutweza unabii ambapo siku moja atajuta majuto makuu na hatapata nafasi ya kurekebisha mambo yake, na mambo hayo yatakuwa hivi karibuni, moja ya hizi siku hii dunia itakuwa si dunia tena..
Vilevile Na unabii mwingine wowote wa kwenye biblia sio wa kuudharau kabisa, kwasababu kila alilolisema Bwana lazima litatimia.
Hivyo kama hujaokoka, saaa wokovu ni sasa, sio baadaye wala kesho..Tubu sasa na Kristo atakusamehe bure kama alivyoahidi.
SIKU YA UNYAKUO ITAKUKUTAJE?
KUSUDI LA MIMI KUWEPO DUNIANI NI LIPI?
IELEWE SAUTI YA MUNGU.
MAMBO MANNE,YANAYODHOOFISHA UOMBAJI WAKO.
Siku zote mwache Yesu, ndio awe wa kwanza kukuhurumia!.
Nakusalimu katika jina kuu la Bwana wetu Yesu Kristo.
Ni jambo la kawaida kila mmoja wetu kuijali kwanza hali yake binafsi, na si dhambi kufanya hivyo, japo hilo halitufanyi tuonekane kuwa wa maana sana mbele za Mungu.. Kuna wakati Bwana Yesu aliitisha mkutano mkubwa sana, pengine eneo la mjini lilikuwa ni dogo la kuuketisha umati mkubwa wa watu, au pengine palikuwa na usumbufu fulani ambao ungewafanya watu wasimsikilize vizuri, Hivyo akaamua kuwaitisha eneo la mbali kidogo na mji, mahali ambapo hapana makazi ya watu, eneo la nyika tupu,..mahali ambapo hakuwaandalia mahema ya kukutania wala hakuwachagulia penye miti mingi, ambapo walau wangekaa chini yake wapate uvuli, bali alichagua eneo la jangwa lenye nyika tupu.
Na mkutano huo ulikuwa ni Mkutano wa siku tatu..
Lakini biblia inatuambia wengi waliposikia habari ile wakatoka mbali sana, wakaenda eneo hilo la jangwa ili kwenda kuyasikiliza maneno ya uzima ya Bwana Yesu,..Watu wale walifikia pengine asubuhi sana na mapema, wakijua kuwa siku zote tatu zitakuwa ni siku za kufunga, za kumsikiliza tu Bwana Yesu si vinginevyo, hivyo walifika mahali pale wakilijua hilo asubuhi sana, wakakaa chini kwenye jua lile, kuanzia asubuhi mpaka jioni,..
Jaribu kutengeneza picha, masaa 12 ya mchana wanamsikiliza tu Bwana Yesu akiwafundisha, na usiku vivyo hivyo.. siku ya kwanza, siku ya pili, mpaka siku tatu zinakwisha, wamekaa tu pale, nyikani wakimsikiliza Bwana Yesu kwa makini bila kuondoa miguu yao, huku njaa zikiwauma, lakini waliona kile wanachokisikiliza ni Zaidi ya chakula cha mwilini.. Walijua mtu hawezi kuishi kwa mkate tu, bali kwa kila Neno linalotoka katika kinywa cha Bwana..
Embu tengeneza tena picha Bwana alikuwa anajua kabisa watu wale, walikuwa katika hali ngumu kweli kweli katika eneo lile la ukame na jua kali, alijua kabisa walikuwa hawajala kwa muda wa masaa mengi sana, alijua kabisa hali zao zinakaribia kuwa mbaya..lakini aliendelea kuwafundisha bila kuwahudumia kwa lolote, kwasababu aliona utayari wao wa kumsikiliza yeye bila kuchoka, mpaka siku tatu kamili zilipokwisha..
Lakini siku ile alipomaliza kuwafundisha, biblia inatuambia Bwana Yesu hakuwaacha hivi hivi waondoke waende zao katika hali zile za njaa bali aliona umaskini wao, aliona njaa zao, aliona mateso yako, aliona kiu yao, aliona mahitaji yao na pale pale maandiko yanatuambia AKAWAHURUMIA ..embu tusome:
Marko 8:1 “Katika siku zile, kwa vile ulivyokuwa mkuu tena ule mkutano, nao wamekosa kitu cha kula, akawaita wanafunzi wake, akawaambia, 2 NAWAHURUMIA MKUTANO kwa sababu yapata siku tatu wamekaa nami, wala hawana kitu cha kula; 3 nami nikiwaaga waende zao nyumbani kwao hali wanafunga, watazimia njiani; na baadhi yao wametoka mbali. 4 Wanafunzi wake wakamjibu, Je! Ataweza wapi mtu kuwashibisha hawa mikate hapa nyikani? 5 Akawauliza, Mnayo mikate mingapi? Wakasema, Saba, 6 Akawaagiza mkutano waketi chini; akaitwaa ile mikate saba, akashukuru, akaimega, akawapa wanafunzi wake wawaandikie; wakawaandikia mkutano. 7 Walikuwa na visamaki vichache; akavibarikia, akasema wawaandikie na hivyo pia. 8 Wakala, wakashiba, wakakusanya mabaki ya vipande vya mikate makanda saba. 9 Na watu waliokula wapata elfu nne. Akawaaga”.
Marko 8:1 “Katika siku zile, kwa vile ulivyokuwa mkuu tena ule mkutano, nao wamekosa kitu cha kula, akawaita wanafunzi wake, akawaambia,
2 NAWAHURUMIA MKUTANO kwa sababu yapata siku tatu wamekaa nami, wala hawana kitu cha kula;
3 nami nikiwaaga waende zao nyumbani kwao hali wanafunga, watazimia njiani; na baadhi yao wametoka mbali.
4 Wanafunzi wake wakamjibu, Je! Ataweza wapi mtu kuwashibisha hawa mikate hapa nyikani?
5 Akawauliza, Mnayo mikate mingapi? Wakasema, Saba,
6 Akawaagiza mkutano waketi chini; akaitwaa ile mikate saba, akashukuru, akaimega, akawapa wanafunzi wake wawaandikie; wakawaandikia mkutano.
7 Walikuwa na visamaki vichache; akavibarikia, akasema wawaandikie na hivyo pia.
8 Wakala, wakashiba, wakakusanya mabaki ya vipande vya mikate makanda saba.
9 Na watu waliokula wapata elfu nne. Akawaaga”.
Unaona hapo?..Walipaswa waondoke vile vile, lakini kwa jinsi alivyoona “WAMEKAA NAYE” siku zote tatu bila kuondoka uweponi mwake, bila kwenda kuhangaika hangaika kuyajali maisha yao, familia zao, biashara zao, miradi yao, ili wapate chakula wao na Watoto wao, badala yake wamedumu pamoja naye kwa siku kadhaa bila kuchoka..basi tukio hilo lilimfanya Bwana Yesu AWAHURUMIE hata kwa yale mengine waliyoyakosa..
Na kama tunavyosoma kitu gani kilifuata.. Wote walishibishwa mikate wakiwa pale nyikani, wakapata na ya kuondokea, mpaka ikabaki na wale samaki vivyo hivyo…Sasa unaweza ukafikiri Bwana Yesu aliwashibisha pale tu…La! Alikuwa anawadhihirishia kuwa baada ya pale na Maisha yao pia yatabarikiwa kwa mfano ule ule wa vikapu, na wala hawatapungukiwa kabisa…Lakini hiyo yote ilikuwa ni kwasababu ya yale maneno ya uzima waliokuwa wanayasikia bila kuchoka ndio yakazaa vikapu vile vya mikate na baraka walizoziendea baada ya pale.
Na sisi tujiulize Je tunaweza kufikia hatua kama hii ya hawa watu?…Je tunaweza kuwa tayari kufunga kutokula kwa ajili tu ya kuutafuta uso wa Bwana kwa kipindi kirefu?, Je tunaweza Kufunga mihangaiko yetu, na shughuli zetu tukatenga wakati wa kuhudhuria ibada na semina ndefu za Neno la Mungu?..kwa kutokujali eneo lenyewe, kutokujali mazingira yanaruhusu kiasi gani, kutokujali umbali, kutokujali hata uzima wako na afya yako?.. Ikiwa tu tutaalikwa mahali ambapo tumewekewa mahema, chini kuna vivuli, lakini bado hatutakwenda ikiwa tunayo makanisa mazuri tena mengine yana feni lakini hatuwezi kukaa hata masaa 2, Je tutawezaje ikiwa tutalikwa mahali penye njika tupu kama pa hawa watu?..Na wakati huo huo bado tunataka Bwana Yesu azihurumie hali zetu,?
Mungu anatuambia tumkaribie yeye na yeye atatukaribia sisi (Yakobo 4:8)..Hivyo tukiwa hatupo tayari kujinyima nafsi zetu na kujitesa katika kuutafuta uso wa Mungu kwa bidii, katika kuutafuta ufalme wake na haki yake, basi tujue itakuwa shida sana kuyaona matendo makuu ya Mungu maishani mwetu.
Usikazane kutafuta kujihurumia kwanza wewe unapoutafuta uso wa Mungu, subiri kwanza mwache Yesu akuhurumie yeye..jukumu letu ni kuutafuta uso wa Mungu kwa bidii mengine tumuachie yeye, kwasababu anajua shida zetu, na mahitaji kabla hata sisi hatujamwambia. (Mathayo 6:32).
Bwana atusaidie katika hilo. Na atujalie tuchukue hatua zinazostahili katika hilo.
Maran Atha.
MIILI YA UTUKUFU ITAKUWAJE?
USIWE NA HOFU, USHUKAPO CHINI.
MUNGU AKIKUPITA LEO, HAIMAANISHI KUWA HAJAKUCHAGUA.
Je! Ni kweli ubatizo wa maji hatuuhitaji tena?
SAKRAMENTI NI NINI, NA JE! IPO KATIKA MAANDIKO?
WhatsApp
Kipindi kifupi kabla ya ghadhabu ya Mungu kumwagwa juu ya dunia, biblia imetabiri kuzuka kwa mambo ya ajabu sana na ya kutisha ulimwengu…na mambo hayo yapo mengi ikiwemo kuzuka kwa manabii wa uongo na makristo wa uongo, lakini pamoja na hayo yapo mengine matatu ya muhimu, ambayo ni …1) VITA 2) TAUNI na 3) NJAA.
Luka 21:10 “Kisha aliwaambia, Taifa litaondoka kupigana na taifa, na ufalme kupigana na ufalme; 11 kutakuwa na MATETEMEKO MAKUBWA YA NCHI; NA NJAA NA TAUNI mahali mahali; na mambo ya kutisha na ishara kuu kutoka mbinguni”.
Kama tujuavyo mgonjwa kabla hajaanza kuumwa anakuwa anaanza kuonyesha dalili kwanza, labda ataanza kusikia kichefuchefu na baadaye akawa sawa, muda kidogo atasikia kichwa kinamuuma lakini si sana..na baadaye tena homa lakini si sana..kiasi kwamba anaweza akazivumilia dalili zile na kuendelea na shughuli zake kipindi cha mwanzoni..na wakati mwingine hata akajisikia nafuu kabisa kana kwamba haumwi tena….
Lakini siku ikifika yenyewe ambapo ugonjwa ule utanyanyuka..huo ndio wakati ambao kila siku kwake itakuwa ni afadhali na jana kuliko leo…zile dalili alizokuwa anazisikia mwanzo, kama kichwa kuumwa kidogo, homa kidogo, sasa vinazidi na kujizidisha na kuwa vikali mara nyingi zaidi..hapo atasikia kichwa kikiumwa hata mara kumi ya kile alichokuwa anakisikia hapo mwanzo..Homa inajizidisha mara nyingi kuliko mwanzo na mara nyingine anajikuta anaishia tu kalala kitandani. Mtu anapofikia hali ya kuumwa kiwango hiki huwa anatamani hata afe atokane na mateso hayo.
Sasa mambo hayo yanafananishwa na siku za maangamizi ya dunia zitakavyokuwa …Wengi wetu hatujui nini maana ya dalili ya siku za mwisho…Dalili maana yake ni mwanzo wa kitu…Hivyo biblia inavyosema kuwa dalili za siku za mwisho ni hizi au zile, inamaanisha kuwa mwisho wa siku mambo yatakuwa ni mabaya kuliko hata mwanzo.
Sasa Bwana Yesu alisema dalili mojawapo ya siku za mwisho ni kuwepo kwa matetemeko makubwa ya nchi(Luka 21:11)…maana yake ni kwamba siku yenyewe ya mwisho wa dunia ikifika kutakuwepo na tetemeko kubwa lisiloelezeka mara nyingi zaidi ya yale ya dalili..
Kadhalika Bwana Yesu alivyosema kwamba vita ni dalili mojawapo ya siku za mwisho, maana yake ni kwamba Siku yenyewe ya mwisho wa dunia ikifika kutakuwa na vita kubwa na kali na ya ajabu ambayo haijawahi kutokea, ambayo madhara yake hayajawahi kufananishwa na vita yoyote huko nyuma..na vita hiyo itakuwa si nyingine zaidi ya vita vya Har -magedoni.Kama hizi vita zilizopo sasa tumezoea kusikia watu elfu kadhaa wamekufa..vita hiyo ya mwisho ya Harmagedoni itamaliza mamilioni ya watu.
Pia alisema dalili nyingine ni NJAA, na njaa hiyo inasababishwa na kukosekana kwa mvua na kunyanyuka kwa wadudu wanaoharibu mazao kama nzige waliotokea wakati wa Farao, na waliopo sasa..Siku ya kuharibiwa dunia Itatokea Njaa ambayo haijawahi kuwa mfano wake…Baada ya watu kuifurahia chapa ya mnyama kwa kitambo..Mungu ataipiga dunia nzima kwa njaa..ambapo maji yote yatageuka kuwa damu na mifereji na mito..na mvua itaacha kunyesha(Ufunuo 16:4-6).
Kadhalika Bwana Yesu alisema dalili nyingine ya siku za mwisho ni KUZUKA KWA MAGONJWA MABAYA ambayo yanafanishwa na Tauni kibiblia(Luka 21:11)...magonjwa hayo yatakuwa hayana tiba na yanayoambukiza kwa kasi…Dalili za magonjwa hayo zimeanza kuonekana tangu mwanzo mwa karne ya 21, na mpaka kufikia sasa yameshaongezeka idadi..Kama ijulikanavyo kuna ugonjwa sasa unaoitwa Corona ulimwenguni.. Ugonjwa huu ni dalili tu (mwanzo wa utungu)..ambapo siku yenyewe ya mwisho ikifika ambayo inaweza kuwa hata leo..utazuka ugonjwa mpya ambao utakuwa ni mbaya kuliko huu uliopo sasa…utakuwa ni ugonjwa wa virusi mfano wa huu wa sasa…
Ugonjwa huu utashambulia ngozi na kusababisha majipu ya vidonda ambavyo vinaoza(Biblia inasema majipu yake yatakuwa ni mabovu, maana yake ni ya kuoza) na utakuwa unateseka kwa muda mrefu..Utakuwa ni tofauti na huu uliopo sasa ambao baada ya siku kadhaa mtu anaweza kupona…ugonjwa huo wa majipu utakuwa hauna tiba na wala hautakuwa unapona wenyewe, utampata kila mtu ambaye atakuwepo ulimwenguni wakati huo…
Ufunuo 16: 2 “Akaenda huyo wa kwanza, akakimimina kitasa chake juu ya nchi; pakawa na jipu baya, bovu, juu ya wale watu wenye chapa ya huyo mnyama, na wale wenye kuisujudia sanamu yake”.
Mambo haya sio hadithi bali ni mambo ambayo yatakuja kutokea dhahiri kabisa. Siku za ugonjwa huo jua litashushwa pia na kuwaunguza wanadamu wote wenye ugonjwa huo, duniani kutakuwa sio sehemu ya kuishi tena..kila mtu atakuwa kivyake akiugulia na kuteseka kivyake vyake kutakuwa hakuna hospitali itakayopokea wagonjwa kwasababu hata wauguzi wenyewe watakuwa na ugonjwa huo..(Hiyo itakuwa sio siku za dalili tena bali ya ugonjwa wenyewe, dalili ni wakati huu wa sasa).. Unyakuo upo karibu sana kutokea!..Kwasababu kabla ya siku hizo..watakatifu watanyakuliwa kwanza.
Ishara za magonjwa haya ni kutuonyesha kuwa Hukumu tayari imeshatamkwa juu ya ulimwengu..kama vile ambavyo ugonjwa unavyomwingia mtu..na hatua za kwanza ni dalili..na sasa tupo katika dalili ya ghadhabu ya Mungu. Hii hofu iliyopo sasa si hofu, hofu hasaa itakuja wakati huo wa mapigo hayo ya Mungu.
Ni nini kifanyike sasa? Katika hatua hii ya dalili?
Kinachopaswa kufanyika sasa ni kujiweka tayari tu…Tunajiwekaje tayari?..ni kwa kutubu, kujiosha mioyo yetu, kuacha dhambi na kuzidi kujitenga na ulimwengu kila siku… Kuacha kuziabudu sanamu na kuzisujudia , Kuacha ulevi, kuacha rushwa, kuacha wizi, kuacha matusi, kuacha kutazama picha za ngono, uasherati, kuacha kwenda ma disko, kuacha kuvaa nguo za kuonyesha maungo, na vimini na suruali kwa wanawake….mambo haya ndiyo yanayoisukuma ghadhabu ya Mungu imwagike haraka ulimwenguni na juu yako wewe..ni kama mgonjwa ambaye tayari kashaanza kuonyesha dalili, halafu bado hazingatii tiba..pasipo kujua kuwa ndio anazidi kujiharibu na kuuvuta ugonjwa zaidi..
Wakolosai 3: 5 “Basi, vifisheni viungo vyenu vilivyo katika nchi, uasherati, uchafu, tamaa mbaya, mawazo mabaya, na kutamani, ndiyo ibada ya sanamu; 6 kwa ajili ya mambo hayo huja ghadhabu ya Mungu”.
Umeona mstari wa 6, usemavyo?… “kwa ajili ya mambo hayo huja ghadhabu ya Mungu”..Soma tena..
Waefeso 5:5 “Maana neno hili mnalijua hakika, ya kwamba hakuna mwasherati wala mchafu wala mwenye tamaa, ndiye mwabudu sanamu, aliye na urithi katika ufalme wa Kristo na Mungu. 6 Mtu asiwadanganye kwa maneno yasiyo na maana; kwa kuwa kwa sababu ya hayo hasira ya Mungu huwajia wana wa uasi”.
Waefeso 5:5 “Maana neno hili mnalijua hakika, ya kwamba hakuna mwasherati wala mchafu wala mwenye tamaa, ndiye mwabudu sanamu, aliye na urithi katika ufalme wa Kristo na Mungu.
6 Mtu asiwadanganye kwa maneno yasiyo na maana; kwa kuwa kwa sababu ya hayo hasira ya Mungu huwajia wana wa uasi”.
Unaona tena? mstari wa mwisho huo wa 6.. “kwa kuwa kwa sababu ya hayo hasira ya Mungu huwajia wana wa uasi”
Hiyo pekee ndiyo njia ya kujikinga na kujiepusha na ghadhabu ya Mungu…
Utauliza kutokana na tatizo hili lililopo sasa…je ! ni sahihi kunawa mikono na kutosalimiana na mtu kwa kushikana mikono njiani?
Kama tunavyoambiwa ni wajibu wa kila mtu kusimama pindi wimbo wa Taifa unapoimbwa…na wakristo pia wanatii agizo hilo..Hivyo na agizo la kunawa mikono popote tufikapo, tuingiapo na tutokapo wakristo tunatii bila shuruti kwasababu hakutupunguzii chochote katika Imani yetu…Tukijua ya kwamba mioyo yetu tayari imeoshwa kwa sabuni ya kimbinguni (Damu ya Yesu)..Na tumaini letu halipo katika maji na sabuni za mwilini bali katika maji na damu ya Yesu Kristo. Hiyo ndiyo inayotutakasa na kutulinda na kutuepusha na ghadhabu ya Mungu. Hivyo hatuna hofu, na hatuogopi kwasababu tunamtegemea Bwana, wakati ulimwengu unaogopa magonjwa, na njaa na vita sasa…sisi tunaigopa dhambi tu!..
Zaburi 125:1 “Wamtumainio Bwana ni kama mlima Sayuni, Ambao hautatikisika, wakaa milele. 2 Kama milima inavyouzunguka Yerusalemu, Ndivyo Bwana anavyowazunguka watu wake, Tangu sasa na hata milele”.
Zaburi 125:1 “Wamtumainio Bwana ni kama mlima Sayuni, Ambao hautatikisika, wakaa milele.
2 Kama milima inavyouzunguka Yerusalemu, Ndivyo Bwana anavyowazunguka watu wake, Tangu sasa na hata milele”.
Lakini kama tukinawa mikono na mwili mzima mahali popote tuingiapo na tutokapo na huku mioyoni mwetu bado kuna uasherati, bado kuna wivu, hasira, wizi, ufisadi, ibada za sanamu, rushwa, na ulevi hakuna chochote tunachoweza kuepuka…Maji na sabuni na mlo kamili kamwe haviwezi kutuepusha na ghadhabu ya Mungu…Havijawahi katika agano la kale na hata katika agano jipya.
Hivyo kwa hitimisho kama hujampa Yesu Kristo maisha yako, Hizi ni siku za mwisho..huhitaji kuhadithiwa na mtu tena..leo hii ile mipira uliyokuwa unajitumainisha nayo kuwa itakupatia faraja iko wapi? Kule kubet ulikokuwa unajitumainisha nako kuko wapi?…Zile visa na zile biashara zako ambazo ulikuwa unajitumainisha nazo unazifanya ulimwenguni kote ziko wapo leo?, elimu unayojitumainia iko wapi?, disko unayojitumainishia nayo iko wapi? Katika mataifa makubwa zimeshafungwa labda na kwako inaweza kuwa hivyo siku sio nyingi, wale waliokuwa wanakuambia kwamba dunia haitafikia mwisho wako wapi leo?..Uliwahi kufikiri kwamba ingetokea siku moja miji mikubwa mikubwa ingekosa watu barabarani?, mashule mengi ulimwenguni yangefungwa?,
umewahi kutafakari kwamba siku moja ingefika mamilioni ya watu hawataruhusiwa kwenda kazini wala makanisani?..Naam Hali inaweza kurudi kama kawaida na maisha yakarudi kama mwanzo na hata zaidi ya pale..lakini je! Umejifunza nini?…bado upo tu nje ya safina?
Huu ni mwanzo tu kwamba tutubu kwasababu siku yenyewe… ikifika hata hii Neema ya kutubu na ya kusikia mahubiri haitakuwepo?….Siku yenyewe ikifika itakuwa haiwezekani kabisa hata kwenda kanisani, licha ya kutafuta mtu wa kukuhubiria, hata kwa njia ya mitandao halitapatikana…wanaohusika na mitandao watakuwa matatizoni, vituo vya satellite vyote vitafungwa…Chapa ya mnyama itakuwa inafanya kazi na kipindi kifupi baada ya kuipokea chapa hiyo magonjwa hayo yataanza..
Yeremia 28:7 “Lakini lisikilize sasa neno hili nilisemalo, masikioni mwako, na masikioni mwa watu wote, 8 Manabii waliokuwako kabla ya zamani zangu, na zamani zako, walitabiri juu ya nchi nyingi, na juu ya falme kubwa, habari ya vita, na ya mabaya, na ya tauni”.
Kabla ya dunia kufikia maharibifu hayo..waliokuwa ndani ya Kristo watakuwa wamenyakuliwa je utakuwa miongoni mwao?..
Kama hujatubu..Na upo tayari kufanya hivyo leo hii, Basi uamuzi unaoufanya ni wa busara sana ambao hautakaa uujutie maisha yako yote kama ilivyokuwa hata kwetu sisi. Unachopaswa kufanya, hapo ulipo, chukua muda mchache ujitenge peke yako. Kisha piga magoti, kisha fuatisha sala hii kwa Imani, ukijua kuwa Mungu yupo hapo karibu na wewe pembeni yako kukusikia..Kisha ukiwa sasa katika utulivu Sema sala hii kwa sauti.
EE MUNGU BABA, NAJA MBELE ZAKO, NIKIWA NINAJITAMBUA KUWA MIMI NI MKOSAJI NA NIMEKUTENDA DHAMBI NYINGI, NA KWAMBA NIMESTAHILI HUKUMU. LAKINI WEWE MUNGU WANGU ULISEMA KATIKA NENO LAKO KUWA WEWE NI MUNGU WA REHEMA UNAYEWAREHEMU MAELFU ELFU YA WATU WANAOKUPENDA WEWE. NA LEO HII NINAKUJA MBELE ZAKO NAHITAJI MSAMAHA WAKO NA MSAADA WAKO MUNGU WANGU, NINATUBU DHAMBI ZANGU ZOTE KWA KUMAANISHA NA KWA MOYO WANGU WOTE, . NINAKIRI KUWA YESU KRISTO NI BWANA, NA YEYE NDIYE MWOKOZI WA HUU ULIMWENGUNI. HIVYO NAOMBA DAMU YA MWANAO TAKATIFU INISAFISHE UOVU WANGU WOTE SASA NIFANYIKE KUWA KIUMBE KIPYA KUANZIA LEO NA HATA MILELE. ASANTE BWANA YESU KWA KUNIPOKEA NA KUNISAMEHE. AMEN.
EE MUNGU BABA, NAJA MBELE ZAKO, NIKIWA NINAJITAMBUA KUWA MIMI NI MKOSAJI NA NIMEKUTENDA DHAMBI NYINGI, NA KWAMBA NIMESTAHILI HUKUMU. LAKINI WEWE MUNGU WANGU ULISEMA KATIKA NENO LAKO KUWA WEWE NI MUNGU WA REHEMA UNAYEWAREHEMU MAELFU ELFU YA WATU WANAOKUPENDA WEWE. NA LEO HII NINAKUJA MBELE ZAKO NAHITAJI MSAMAHA WAKO NA MSAADA WAKO MUNGU WANGU, NINATUBU DHAMBI ZANGU ZOTE KWA KUMAANISHA NA KWA MOYO WANGU WOTE, . NINAKIRI KUWA YESU KRISTO NI BWANA, NA YEYE NDIYE MWOKOZI WA HUU ULIMWENGUNI. HIVYO NAOMBA DAMU YA MWANAO TAKATIFU INISAFISHE UOVU WANGU WOTE SASA NIFANYIKE KUWA KIUMBE KIPYA KUANZIA LEO NA HATA MILELE.
ASANTE BWANA YESU KWA KUNIPOKEA NA KUNISAMEHE.
AMEN.
Sasa ikiwa umefuatisha sala hiyo kwa Imani ..Hatua iliyobakia kwako ni kuithitisha toba yako kwa Vitendo ikiwa ulikuwa unafanya mambo yote ambayo hayampendezi Mungu unayaacha na kujitenga nayo, Sasa Mungu akishaona umegeuka kwa vitendo basi toba yako anaipokea na atakuja ndani yako wakati huo huo na kufanya makao ya milele kwako. Vile vile unahitaji, kutafuta kanisa la kiroho ambalo utajumuika na wakristo wengine katika kumwambudu Mungu, na kujifunza biblia ili uukulie wokovu. Na vilevile ili upate ubatizo sahihi wa kuzamishwa katika maji Mengi na kwa jina la YESU KRISTO kwa ajili ya ondoleo la dhambi zako.
MAPIGO YA VITASA SABA, NA SIKU YA BWANA.
UFUNUO: Mlango wa 16.
Rudi Nyumbaani:
Kwanini yesu kristo ni wa muhimu kwetu?
Moja ya majukumu tuliyonayo ni “Kumfahamu sana Yesu Kristo”..Hili ni moja ya jukumu kubwa sana tulilonalo kwasababu ndio msingi wa ukombozi wetu..Tusipomfahamu Yesu kwa mapana na marefu basi ni ngumu kujua nafasi zetu pamoja na Neema tuliyopewa…Na matokeo ya kutomwelewa Yesu ni kuishia kuidharau neema na kupotea.
Sasa jukumu la kumjua Yesu, sio kujua sura yake alikuwa ni mzuri kiasi gani, au alikuwa na rangi gani, au alikuwa na nywele za namna gani, au alikuwa anapenda kula nini?..Hapana hilo sio jukumu tulilopewa la kumfahamu kwa namna hiyo..Jukumu tulilopewa ni KUIFAHAMU VIZURI ILE NAFASI ALIYONAYO. Tukishaifahamu ile nafasi basi tutamjua Mungu sana. Na mpaka sasa hakuna aliyefikia kikomo cha kuijua hiyo nafasi yote..bali kwa siku zinavyozidi kwenda tunazidi kuilewa na ndivyo tunavyozidi kumpenda Mungu na kumheshimu.
Waefeso 4:13 “hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo”
Leo tujikumbushe ni kwa namna gani kifo cha Yesu kilivyokuwa na umuhimu kwetu sisi tuliokuwa tumepotea kwenye dhambi.
Katika Biblia tunasoma muda mfupi kabla ya Bwana Yesu kupandishwa msalabani..Pilato aliwafungulia mfungwa mmoja ambaye alikuwa ni mkatili katika mji ule..Na huyo si mwingine Zaidi ya BARABA.
Huyu Baraba alikuwa na Kesi ya mauaji ya watu kadhaa hapo mjini, na alikuwa ni mkatili..Biblia inamwita “mfungwa mashuhuri” (Mathayo 27:16). Watu wote walimshuhudia kuwa alikuwa ni mkatili, hivyo walikuwa hawamhitaji hata kidogo, hivyo alikamatwa na warumi na kutiwa gerezani akisubiria hukumu yake ipite..Na bila shaka angeuawa kifo cha kikatili kuliko mtu mwingine yoyote yule, kwasababu kila mtu alikuwa amemkinai. Na alivyokuwa kule gerezani kila mtu pamoja na yeye mwenyewe alikuwa anajua ndiye anayestahili adhabu kubwa kuliko wote. Kulikuwa hakuna uwezekano wa kupona hata kidogo…Lakini kama wasemavyo watu “hata mnyororo ulio imara sana, lazima utakuwa na sehemu yake dhaifu”..Hata kama sehemu inaonekana hakuna njia basi Mungu anaweza kufanya njia.
Baraba akiwa mule gerezani labda moyo wake ukaanza kumchoma na kujihisi alifanya makosa, aliua wale watu pasipo hatia, akitazama pembeni anajua kuna mtu aliua tu mtu mmoja na alihukumiwa kukatwa kichwa yeye akijiangalia kashaangusha watu kadhaa huko nyuma hukumu yake itakuwaje?…
Siku moja tu asubuhi alishangaa anaitwa nje, atoke gerezani..na alipotoka akijua anakwenda kuuawa na pengine wafungwa wote wakajua anakwenda kumalizwa kwa hasira nyingi..ghafla anatoka nje anaona watu wengi wanamshangilia nje, wanafurahi kufunguliwa kwake..anaona wanampigia mpaka vigelegele, Baraba afunguliwe! Baraba afunguliwe!… kwa pembeni anamwona Pilato anamwambia kuanzia leo upo huru kama watu wengine, rudi nyumbani kwako kafurahi na mke wako na Watoto wako, upo huru..Wakati anashangaa jambo hilo linawezekanaje labda walikosea wanamaanisha Baraba mwingine…. kwa pembeni kidogo anaona mtu amewekwa taji la miiba kichwani kakaa kimya sana, mpole kama mwanakondoo anayekaribia kuchinjwa….Pilato anamwambia Yule kabeba hukumu yako…Yule atakufa kwa niaba yako…Ni wazi bila shaka alishangaa kidogo..
Naamini Maisha yake yalianza kubadilika kuanzia pale na kuendelea…Kwasababu alijua chanzo cha uzima wake na uhuru wake ni nini?..kwamba kama si Yesu kuwa vile alivyokuwa, kufanyiwa yale aliyofanyiwa, kama sio Yesu kukataliwa yeye angekufa…kwasababu kama Yesu angekubaliwa basi yeye asingepona…Hivyo kwa kupingwa na kupigwa kbbwake Yesu yeye amepona!.
Je mtu wa namna hiyo atarudia tena kuua?, atamkebehi YESU?, Ataudharau msalaba? Atajisifu?…Na je mfano akiudharau msalaba na kutoka pale na kuendelea na mauaji yake unahisi ni nini kitampata mbele za Mungu na watu?
Hiyo ndiyo nafasi ya Yesu kwetu ilivyo… Baraba ni mfano wa mimi na wewe…Sasa ni kwa namna gani Bwana Yesu anachukua dhambi zetu?..Sio kwa kubeba kifurushi na kukiweka mabegani kwake…Hapana ilimgharimu Maisha yake…ilimgharimu kukataliwa, kupingwa, kutemewa mate, kutukanwa, kudhihakiwa..Kwajinsi alivyodhihakiwa sana na kutukanwa sana ndipo thamani ya Baraba kule gerezani ilivyokuwa inazidi kupanda. Hadhi ya Bwana Yesu ilishuka ili yetu ipande.
Wakati Baraba yupo kule gerezani alikuwa hajui kama Kristo anatukanwa huko nje kwaajili yake.
Ndugu yangu…Msalaba sio jambo la kupuuzia au kuchezea hata kidogo…Mambo yote mema unayoyapata leo hii ni kwasababu ya Yesu Kristo, kama sio yeye dunia ingeshaisha siku nyingi…Mungu angeshaimaliza dunia kwa laana kitambo sana…Maisha yangeshaisha miaka mingi sana iliyopita huko nyuma.
Watu wengi hawajui kuwa wanapiganiwa na Mungu pasipo hata wao kumwomba Mungu, wengi hawajui hata katika uasherati wao ni Mungu ndiye anayewapa riziki pasipo hata wao kumwomba, na hawajui ni hiyo neema, ni kwasababu ya YESU KRISTO. Kama sio Yesu kuteseka miaka 2020 iliyopita hakuna mwasherati ambaye mpaka leo angekuwa anaishi..Wote tulistahili kufa.
Lakini Neema hii unaichezea..unadhani ni haki yako kuishi na usherati wako, uwizi wako, ufisadi wako, ulevi wako, uuaji wako, utukanaji wako, usagaji wako, ulawiti wako, uchafu wako n.k Hii Neema ipo siku itaisha na siku hiyo ndipo utakapojua kuwa Hii neema ilikuwa ni ya thamani kiasi gani.
Hii Neema itakapoondolewa, itaondoka na kanisa..watakatifu wataondolewa ulimwenguni, dhiki kuu itaanza, mpingakristo atanyanyuka, ataua wengi na baadaye maji ya bahari na visima na mito yote itageuzwa kuwa damu, utatokea ugonjwa wa majipu ulio hatari kuliko huu uliozuka sasa unaoitwa CORONA. Utasambaa duniani kote hakuna mtu atakayesalimika kwa wale watakaoachwa kwenye unyakuo, wakati huo hakutakuwa na mtu wa kukwambia utubu dhambi zako.
Siku hizo hakutakuwa na masinema tena watu wanayokwenda kuangalia michezo , hakutakuwa na mipira watu wanayokwenda kuangalia, barabara zitakuwa wazi, kila mtu atakuwa peke yake peke yake akiugulia mapigo hayo..Unaona leo ugonjwa huu wa Corona leo ulivyosababisha mabarabara kufungwa, mashule kufungwa, hakuna mtu kwenda kazini kwenye mataifa yaliyoathirika, kila mtu kajifungia ndani..siku hizo itakuwa mara 100 ya hiyo, hata mnyama wako wa kufugwa hutamsogelea, kutakuwa hakuna kutembea mabarabarani..kila mtu anashiriki mapigo hayo kivyakevyake.
Katikati ya gonjwa hilo la ajabu litakalolipuka la majipu…mvua zitaacha kunyesha, jua litashushwa chini, kutakuwa hakuna kitu chochote kilicho kijani kitakachoonekana, mvua ya mawe itashuka, sio ya mawe ya barafu..mawe kama mawe, makubwa kama talanta, kutatokea matetemeko na milipuko ya volcano duniani kote, na baada ya siku za maunguzo ya jua kupita….jua litakuja kuondolewa kutakuwa na giza la ajabu kuliko lile lililotokea kipindi cha Farao, nyota hazitakuwepo, mwezi utaonekana kuwa mwekundu kama damu kwa kipindi kirefu, mambo hayo yote yanakuja ndani ya wakati mmoja..na mambo mengine mengi ya ajabu yatakuwepo, mambo haya sio hadithi za kutunga kasome Ufunuo 16 yote, utaona, na kama unyakuo utakupita basi utayashuhudia hayo yote.
Waebrania 10:25 “wala tusiache kukusanyika pamoja, kama ilivyo desturi ya wengine; bali tuonyane; na kuzidi kufanya hivyo, kwa kadiri mwonavyo siku ile kuwa inakaribia. 26 Maana, kama tukifanya dhambi kusudi baada ya kuupokea ujuzi wa ile kweli, haibaki tena dhabihu kwa ajili ya dhambi; 27 bali kuna kuitazamia hukumu yenye kutisha, na ukali wa moto ulio tayari kuwala wao wapingao. 28 Mtu aliyeidharau sheria ya Musa hufa pasipo huruma, kwa neno la mashahidi wawili au watatu. 29 MWAONAJE? HAIKUMPASA ADHABU ILIYO KUBWA ZAIDI MTU YULE ALIYEMKANYAGA MWANA WA MUNGU, NA KUIHESABU DAMU YA AGANO ALIYOTAKASWA KWAYO KUWA NI KITU OVYO, na kumfanyia jeuri Roho wa neema? 30 Maana twamjua yeye aliyesema, Kupatiliza kisasi ni juu yangu, mimi nitalipa. Na tena, Bwana atawahukumu watu wake. 31 Ni jambo la kutisha kuanguka katika mikono ya Mungu aliye hai.”
Waebrania 10:25 “wala tusiache kukusanyika pamoja, kama ilivyo desturi ya wengine; bali tuonyane; na kuzidi kufanya hivyo, kwa kadiri mwonavyo siku ile kuwa inakaribia.
26 Maana, kama tukifanya dhambi kusudi baada ya kuupokea ujuzi wa ile kweli, haibaki tena dhabihu kwa ajili ya dhambi;
27 bali kuna kuitazamia hukumu yenye kutisha, na ukali wa moto ulio tayari kuwala wao wapingao.
28 Mtu aliyeidharau sheria ya Musa hufa pasipo huruma, kwa neno la mashahidi wawili au watatu.
29 MWAONAJE? HAIKUMPASA ADHABU ILIYO KUBWA ZAIDI MTU YULE ALIYEMKANYAGA MWANA WA MUNGU, NA KUIHESABU DAMU YA AGANO ALIYOTAKASWA KWAYO KUWA NI KITU OVYO, na kumfanyia jeuri Roho wa neema?
30 Maana twamjua yeye aliyesema, Kupatiliza kisasi ni juu yangu, mimi nitalipa. Na tena, Bwana atawahukumu watu wake.
31 Ni jambo la kutisha kuanguka katika mikono ya Mungu aliye hai.”
Kama hujageuka na kutubu mlango wa Neema leo upo wazi…Ni heri usitumie muda ku-comment na ku-like badala yake ukatubu kama hujatubu. Usisome tu kama hadithi ya kukufurahisha, bali ujumbe huu ukawe sababu ya mageuzi kwako..
Na maana ya kutubu ni “kugeuka”..maana yake unadhamiria kuyaacha yale uliyokuwa unayafanya yasiyompendeza Mungu, na unakwenda kubatizwa katika ubatizo sahihi na kupokea Roho Mtakatifu. Mambo hayo unayafanya kwa moyo wako wote.
Bwana akubariki sana. Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako
jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa > WHATSAPP
RABI, UNAKAA WAPI?
USIPOWATAMBUA YANE NA YAMBRE, KATIKA KANISA LA KRISTO, UJUE UMEPOTEA.
YULE JOKA WA ZAMANI.
HAPANA HATA MMOJA ATAKAYEIONJA KARAMU YANGU.
UVUMILIVU WA MUNGU ULIPOKUWA UKINGOJA.
SWALI: Samahani mtumishi naomba ufafanuzi wa kauli hii ya Bwana Yesu aliimanisha nini? “KWA NINI KUNIITA MWEMA? HAKUNA ALIYE MWEMA ILA MMOJA, NDIYE MUNGU.” Hapa nashindwa kuelewa alivyomjibu kwani alikosea wapi maana hata mimi leo hii najua Yesu ni mwema na alikuwa mwema!! Nisaidie kunifafanulia. Amina.
JIBU: Tusome habari yenyewe..
Marko 10:17 “Hata alipokuwa akitoka kwenda njiani, mtu mmoja akaja mbio, akampigia magoti, akamwuliza, MWALIMU MWEMA, nifanye nini nipate kuurithi uzima wa milele? 18 Yesu akamwambia, Kwa nini kuniita mwema? Hakuna aliye mwema ila mmoja, ndiye Mungu. 19 Wazijua amri, Usiue, Usizini, Usiibe, Usishuhudie uongo, Usidanganye, Waheshimu baba yako na mama yako. 20 Akamwambia, Mwalimu, haya yote nimeyashika tangu utoto wangu. 21 Yesu akamkazia macho, akampenda, akamwambia, Umepungukiwa na neno moja. Enenda, ukauze ulivyo navyo vyote, uwape maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni; kisha njoo unifuate. 22 Walakini yeye akakunja uso kwa neno hilo, akaenda zake kwa huzuni; kwa sababu alikuwa na mali nyingi. 23 Yesu akatazama kotekote, akawaambia wanafunzi wake, Jinsi itakavyokuwa shida wenye mali kuingia katika ufalme wa Mungu!.
Marko 10:17 “Hata alipokuwa akitoka kwenda njiani, mtu mmoja akaja mbio, akampigia magoti, akamwuliza, MWALIMU MWEMA, nifanye nini nipate kuurithi uzima wa milele?
18 Yesu akamwambia, Kwa nini kuniita mwema? Hakuna aliye mwema ila mmoja, ndiye Mungu.
19 Wazijua amri, Usiue, Usizini, Usiibe, Usishuhudie uongo, Usidanganye, Waheshimu baba yako na mama yako.
20 Akamwambia, Mwalimu, haya yote nimeyashika tangu utoto wangu.
21 Yesu akamkazia macho, akampenda, akamwambia, Umepungukiwa na neno moja. Enenda, ukauze ulivyo navyo vyote, uwape maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni; kisha njoo unifuate.
22 Walakini yeye akakunja uso kwa neno hilo, akaenda zake kwa huzuni; kwa sababu alikuwa na mali nyingi.
23 Yesu akatazama kotekote, akawaambia wanafunzi wake, Jinsi itakavyokuwa shida wenye mali kuingia katika ufalme wa Mungu!.
Wengi wanatumia vipengele hivi (hususani wale wasio wakristo), Kuthibitisha kuwa Yesu hakuwa Mungu, kwasababu hapa alikana kabisa kuwa yeye hakuwa mwema ila Mungu peke yake,…Lakini ukisoma kwa utulivu na ukimwomba Roho Mtakatifu akufumbue macho, utagundua kuwa Bwana Yesu hakukana kuwa yeye sio Mwema..Hakusema umekosea badili kauli yako!..Lakini alimuuliza swali tu!..Kwanini unaniita mimi mwema?..Kuuliza swali sio kukana….alitaka kupata mawazo yake, ni nini aliona ndani yake mpaka yeye amwite vile mwema…
Ni sawa na leo hii ukutane na mtu Fulani mkubwa ukamkimbilia na kumpigia magoti na kumwambia muheshimiwa, maagizo yoyote utakayonipa mimi nitayafanya..Na yeye akakuuliza ni kwanini unaniita mimi muheshimiwa?..anayeheshimiwa ni lazima awe kiongozi na mwenye mamlaka, Na hivyo utakuwa radhi, kutii chochote atakaachokuambia kukifanya kulingana na kauli yako… Na ndivyo ilivyokuwa kwa Bwana Yesu alipomwambia yule kijana, hakuna aliye mwema ila mmoja, ndiye Mungu, yaani yeyote uliyemwona kuwa ni mwema basi ujue huyo ni Mungu..
Hivyo Unaongea na huyo aliye mwema ambaye ni Mungu.. Kama unadhani Kristo alikuwa anapinga yeye kuitwa mwema..Soma tena, (Yohana 10:11) utaona anajiita mimi ndimi mchungaji mwema…Sasa ikiwa alikuwa anajipinga vile basi asingejiita na hapa pia mchungaji mwema..Na pia kasome Yohana 14:8-10 utaona Uungu wa Bwana Yesu. Lakini utaona alimuuliza kijana yule vile, ili kumjengea mazingira ya kukishika kila ambacho atakachokwenda kumwambia mbele, kwa kigezo kile kile cha kumtambua kuwa yeye ni mwema kama Mungu…
Ndipo pale alipomwambia, umezishika amri akasema, nimezishika zote, lakini Bwana Yesu akaona kuwa hajazishika zote, imesalia moja, tena ile ya kwanza ya kumpenda Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote,kwa roho yako yote, kwa nguvu zako zote, na kwa akili zako zote..Ndipo akamwambia umepungukiwa na moja, nenda akauze vyote ulivyo navyo, na kuwapa maskini, kisha njoo amfuate..
Lakini Yule kijana aliposikia habari za mali zake zinagusiwa akaondoka amekunja uso wake, kwasababu alipenda mali zake kuliko kumpenda Mungu.. Jaribu kufikiria kama angemtii Kristo, kama alivyomtambua kuwa yeye ni mwema kama Mungu na kuyafuata yote aliyoambiwa ..Leo hii yule angekuwa wapi?..
Bila shaka angekuwa ni mtume wa 13, Lakini alipenda mali zake kuliko kumpenda Mungu. Hata leo hii, tukimjua Kristo kama Mungu, pale anapotuambia tumpende yeye kwa nguvu zetu zote, pale anapotuambia tuache mambo Fulani ya kidunia, hatuna budi kuacha mara moja vinginevyo tutakuwa ni wanafki..
Kwanini yule mtu hakukutwa na vazi la arusi wakati alialikwa?
Kwanini Bwana Yesu, aliruhusu yale mapepo yawaingie nguruwe?
Ufisadi una maanisha nini katika biblia?
USILALE USINGIZI WAKATI WA KUMNGOJEA BWANA.