Tuwaonapo nzige wa jangwani ni nini tunajifunza?
Shalom.. Karibu tuongeze jambo lingine kuhusu ufalme wa mbinguni..
Bwana Yesu alipotuambia utafuteni kwanza ufalme wake na haki yake…Alimaanisha kweli ufalme huo ili kuupata inahitaji kuutafuta…Lakini jambo ambalo hatujui pia ni kuwa ufalme huo haujafichwa katika mambo magumu sana, kiasi kwamba itatuhitaji tuwe na shahada kubwa za elimu, au maarifa makubwa kuzijua, badala yake siri hizo zimefichwa katika mambo madogo sana, na hayo ndiyo yanayofanya ufalme huo usionekane kirahisi..Mambo mepesi sana ambayo huwezi kutazamia kama kweli hapo ndipo siri za Mungu zilipo.
Kwa mfano embu tafakari Bwana Yesu alivyosema..Watafakarini Kunguru (Luka 12:24),..hawapandi, wala hawavuni, wala hawana maghala lakini baba yenu wa mbinguni anawalisha hao wote, je ninyi si Zaidi kuliko hao wote?. Ikiwa wewe unaishi Dar es alaam au sehemu za pwani utakuwa umeshakutana na kunguru wengi sana, lakini kama Bwana Yesu asingelizunguza hili neno, ungekuwa unaona kama ni viumbe vyenye kero Fulani, vinaishi mjini tu kuuchafua mji, lakini kumbe siri moja ya ufalme wa mbinguni ipo hapo, kiasi kwamba mtoto wa Mungu akiitumia basi, atafanikiwa sana,
Kama hujui ni mmoja wa ndege wachache sana wanaoishi miaka mingi, kunguru anaishi mpaka miaka 80, anaishi mjini mahali wanaposema Maisha magumu(vyuma vimekaza), na kila siku anakula, anakunywa! Sasa ni rahisi kusema kunguru ndivyo walivyoumbwa staili hiyo ya maisha..Lakini Bwana Yesu anasema..Je! wale wanachokipi cha kuwapita nyie mpaka waishi Maisha ya kutokujisumbukia kama yale?..
Ndugu kama wewe umekosa Imani ya maneno kama hayo ya Kristo, nataka nikuambie wapo wenzako wanaishi kwa Neno hilo na Bwana anawahudumia kwa kila kitu Zaidi hata ya kunguru, mmojawapo ni mimi, hakuna siku inayopita bila kuwa na ushuhuda mpya maishani mwangu…mpaka nimeshazizolea naziona ni kawaida tu..Lakini zamani nalipoanza tu kuliamini hili Neno, nilijaribu kumweleza mchungaji mmoja kulitokea utata mkubwa.. Haijalishi Tutajaribu kuleta tafsiri nyingine tuzijuazo lakini Maneno ya Yesu ni imara, yatathibitika milele na milele..Hayo ndio mambo marahisi ambayo Mungu anajifunua ndani yake, lakini yanadharauliwa na wengi.
Leo hii tunasikia tena kuna jambo limezuka la wadudu wanaojulikana kama NZIGE WA JANGWANI, sana sana katika ukanda wa Afrika Mashariki. Tupaswa pia tujiulize maswali Je! Tupowatazama hawa wadudu tunaona tu maafa na majanga au tunaona pia kitu kingine ndani yake?..
Lakini biblia inawataja nzige kama moja ya kiumbe vinne vyenye AKILI nyingi sana..
Soma..
Mithali 30:24 “Kuna viumbe vinne duniani vilivyo vidogo; Lakini vina akili nyingi sana. 25 Chungu ni watu wasio na nguvu; Lakini hujiwekea chakula wakati wa hari. 26 Wibari ni watu dhaifu; Lakini hujifanyia nyumba katika miamba. 27 NZIGE HAWANA MFALME; LAKINI HUENDA WOTE PAMOJA VIKOSI VIKOSI. 28 Mjusi hushika kwa mikono yake; Lakini yumo majumbani mwa wafalme”.
Mithali 30:24 “Kuna viumbe vinne duniani vilivyo vidogo; Lakini vina akili nyingi sana.
25 Chungu ni watu wasio na nguvu; Lakini hujiwekea chakula wakati wa hari.
26 Wibari ni watu dhaifu; Lakini hujifanyia nyumba katika miamba.
27 NZIGE HAWANA MFALME; LAKINI HUENDA WOTE PAMOJA VIKOSI VIKOSI.
28 Mjusi hushika kwa mikono yake; Lakini yumo majumbani mwa wafalme”.
Kama hujawahi kufuatilia tabia ya nzige hawa, basi fahamu kuwa hawana tofuati sana na nzige hawa wa kawaida tunaowaona ambao kila mmoja anajitegemea kivyake, tofauti ipo tu pale ambapo wameshakuwa wengi huwa wote wanabadilika tabia, wanajikusanya pamoja..kisha wakishajikusanya wanaanza kuruka katika wingi wao, kama kimbunga, ukitazama kwa mbali unaweza ukaona kama ni vumbi tu linakuja jinsi walivyo wengi, unaambiwa katika kilometa moja ya mraba, wapo nzige Zaidi ya milioni 150, na katika kimbunga hicho wapo Zaidi ya nzige bilioni 100, na wote hawa wanaruka pamoja.
kwa siku wanaweza kusafiri zaidi ya kilimeta 150, sasa licha ya wao kuwa wengi hivyo unaambiwa katika kuruka kwao na kupishana kwao wakiwa bado hivyo mabilioni kwa mabilioni huko juu, hawagongani wakiwa angani, wala hawagusani, japokuwa wanaruka karibu karibu sana..Hawana kiongozi wa kuwaweza katika mstari, na kuwasimamia na kuwaambia wewe pita hapa, au wewe pita kule, lakini wanayo akili ya hali ya juu, ya kuwafanya waruke kwa ustaarabu, wakiwa na anza moja, ya kuelekea upande mmoja..
Na ndio hiyo inayowafanya wafanikiwe kufika mbali wote wakiwa pamoja, wahame kutoka taifa moja hadi lingine wakiwa na idadi hiyo hiyo ya majeshi..Na kusababisha maafa makubwa sana ya mazao isiyoelezeka..
Embu fikiria kikundi kimoja kinachojaza eneo la kilometa moja ya mraba, kwa siku moja kinauwezo wa kutafuna mazao, yanayoweza kuliwa na watu elfu thelathini na tano (35,000) ..Na wenyewe wakivamia basi wanamaliza mamilioni ya Hektari za mraba.. Na ndio maana wanakuwa tishio sana kwa mataifa..Hawa ndio mfano wa wale walitumwa kuitafuna nchi yote ya Misri.
Sasa, kwanini Biblia inatuambia wanaakili nyingi..Ni kwasababu Mungu anataka ni sisi tupate hekima ndani yake ili tufanikiwe katika kumshinda adui..
Si mpango wa Mungu tangu zamani tuwe na viongozi juu yetu sisi wa kutuongoza..Wana wa Israeli walimwomba Mungu awape mfalme juu yao..Mungu alikasirishwa sana na mawazo yao, kwasababu Mungu alitamani wamtumikie yeye wakiwa na nia moja kila mmoja bila kushurutishwa na mtu Fulani wa pembeni..(Soma 1Samweli 8:1-22)
Leo hii na sisi, tukitaka ulimwengu huu, tumshinde Shetani, hatuhitaji mpaka tuambiwe na watu Fulani majukumu ya kufanya..Bali sote kwa pamoja kila mmoja kwa nafasi yake, na kwa karama Mungu aliyopewa anyanyuke kwa nguvu zake aishambulie kambi ya Adui shetani kwa kuihubiri injili, tusisibirie mpaka Mchungaji wetu atuambie hivi au vile, tusisubiri mpaka viongozi watushurutishe tutoke tukaifanye kazi ya Mungu…Kwa jinsi shetani anavyoaharibu hakuna mtu asiyejua kuwa huu ni wakati wa mapambano..
Sisi ikiwa kila mmoja atasimama kwa nafasi yake, kama vile HAWA NZIGE WA JANGWANI.. Tukatoka tukiwa na lengo moja la kumuharibu ibilisi na kazi zake zote..Basi tujie kuwa kuzimu itabakia kuwa gofu..shetani atapata hasara isiyokuwa ya kawaida..Watu watamkimbilia Kristo kwa namna isiyoelezeka…Na tukitoka wote kama Jeshi kiongozi wetu akiwa ni Roho Mtakatifu na si mtu, kamwe hatutapishana kauli, kamwe hatutagongana katika njia zetu kama jinsi hawa nzige kwa wingi wao wasivyogongana wakiwa angani..
Lakini hiyo yote ni mpaka mimi na wewe, kutokuongejea mpaka tupangiwe majukumu ya kufanya na mtu Fulani, au mhubiri Fulani, au mpaka kanisa litupangie majukumu..
Naamini katika wakati huu wa kumalizia, tutalitafakari na hilo, katika kazi ya ujenzi wa ufalme wa mbinguni..Bwana azidi kutupa neema yake.
Maran atha!
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe au piga namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
UHURU WA ROHO.
KWA VILE ALIVYOKUWA MTU WA HAKI.
KIFO CHA MTAKATIFU POLIKAPI (Policarp).
KUSUDI LA MIMI KUWEPO DUNIANI NI LIPI?
SAA YA KUHARIBIWA IIJIAYO ULIMWENGU WOTE.
SIKU ILE NA SAA ILE.
Amin, nawaambia, Kizazi hiki hakitapita, hata hayo yote yatakapotimia..!!
KAMA ZILIVYOKUWA SIKU ZA NUHU NA ZA LUTU.
Rudi Nyumbani:
Print this post
Mwanamke wa Kikristo unapaswa ujue nini?
Karibu tujifunze Biblia, ambayo ndiyo mwanga wa njia zetu na Taa iongozayo miguu yetu.
Ujumbe huu unakuhusu wewe binti wa Mungu ambaye pengine una bidii ya kumtafuta Mungu, karibu leo tujifunze baadhi ya mambo ambayo yatakusaidia katika safari yako ya imani, na yatakayokuongezea maarifa ya kutosha ya namna ya kutembea na Mungu kwa jinsi anavyotaka wewe utembee naye.
Jambo la kwanza la kuzingatia binti wa Mungu usomapo biblia…usikimbilie kusoma habari za wanaume kama wakina Musa, Daudi, Ezekieli, Yohana au Paulo…Ni vizuri kusoma hayo yote!..lakini nataka nikuambie kwamba ukikimbilia kusoma habari za hao bila kusoma kwanza habari za wanawake wenzako kama wewe katika maandiko hakika nakuambia utakuwa umeukwepa msingi mkubwa sana na wa muhimu katika maisha yako.
Kabla ya kutaka kujifunza habari za Daudi na Ushujaa wake…Hebu ingia ndani kwanza kajifunze habari za bibi yake Daudi aliyeitwa RUTHU, ni jinsi gani alimpendeza Mungu..kayasome maisha yake na kajifunze habari zake kwa mapana na marefu jinsi alivyoishi na wakwe zake na jinsi alivyompendeza mumewe Boazi..Ikiwezekana kamata kalamu na karatasi zinakili zile points zote, zishike hizo na kuziishi ndizo zitakazokusaidia sana kuwa mwanamke unayeishi kwa kumpendeza Mungu kuliko kujifunza habari za ushujaa wa Daudi. Ushujaa wa Daudi kwako wewe mwanamke hauna manufaa sana kwako zaidi ya ushujaa wa Ruthu bibi yake Daudi, au ushujaa wa Abigaeli mkewe Daudi.
Kabla ya kujifunza kwa kina habari za Daudi jinsi alivyomwangusha Goliathi..hebu kajifunze kwanza habari za Abigaili mke wa Daudi jinsi alivyomzuia Daudi kwenda kumwaga damu, kajifunze kwanza jinsi Abigaili alivyomnyenyekea Daudi…ziige hizo tabia kwanza za mke wa Daudi, kabla ya kwenda kuziiga za Daudi.(1Samweli 25:2)
Hali kadhalika kabla ya kwenda kujifunza juu ya Imani ya Ibrahimu..Hebu kwanza jikite kumsoma kwa undani SARA!..Zitafute siri za mafanikio za Sara kabla ya kutamani kuzitafuta za Ibrahimu..za Ibrahimu hazitakusaidia sana wewe mwanamke zaidi ya za Sara..Ibrahimu aliambiwa akatahiriwe na asingefanya hivyo alikuwa anakwenda kinyume na maagizo ya Mungu sasa wewe Tohara inakusaidia nini, hayo maagizo yanakufundisha nini wewe?…Lakini ukijiingia ndani kujifunza Jinsi gani Sara alimpendeza Mungu..ukazijua siri zote za maisha ya Sara hakika hutabaki kama ulivyo, na shetani hatakaa akuweze kamwe kama alivyowashindwa wakina Sara.
Sara alifikia hatua ya kumweshimu mumewe mpaka akafikia hatua ya kumuita mumewe “Bwana” (kasome 1Petro 3:6)..Hebu na wewe iga kwanza hayo mazuri ya Sara kabla ya kukimbilia kutamani mazuri ya Ibrahimu.
Vivyo hivyo kabla ya kukimbilia kujifunza juu ya Petro, Yohana au Mathayo wanafunzi wa Bwana Yesu..hebu tenga muda kwanza kujifunza juu la kundi lingine la waliomfuata Yesu kwa bidii mfano wakina (Mariamu Magdalene, Susana, wakina Martha na Miriamu)…Ingia ndani kujifunza maisha ya hawa wanawake watakatifu ni jinsi gani walivyompendeza Mungu…usikimbilie kujifunza juu ya Mitume jinsi walivyokuwa hodari wa kwenda vijiji na vijiji kuhubiri…hayo hayatakusaidia sana zaidi ya kujifunza juu ya wanawake wakina Susana walivyomhudumia Bwana kwa mali zao..Hawakuwa miongoni mwa waliotumwa na Bwana kuzunguka huko na huko…. lakini sehemu kubwa ya Huduma ya Bwana michango ilitoka kwa hawa wanawake watakatifu.. Hilo ndio Jeshi kubwa linalomtumika Bwana!!
Luka 8:1 “Ikawa baada ya hayo alikuwa akizunguka-zunguka katika miji na vijiji akihubiri na kuitangaza habari njema ya ufalme wa Mungu; na wale Thenashara walikuwa pamoja naye, 2 na wanawake kadha wa kadha ambao walikuwa na pepo wabaya na magonjwa wakaponywa; nao ni Mariamu aitwaye Magdalene aliyetokwa na pepo saba, 3 na Yoana mkewe Kuza, wakili wake Herode, na Susana, NA WENGINE WENGI, WALIOKUWA WAKIMHUDUMIA KWA MALI ZAO”.
Luka 8:1 “Ikawa baada ya hayo alikuwa akizunguka-zunguka katika miji na vijiji akihubiri na kuitangaza habari njema ya ufalme wa Mungu; na wale Thenashara walikuwa pamoja naye,
2 na wanawake kadha wa kadha ambao walikuwa na pepo wabaya na magonjwa wakaponywa; nao ni Mariamu aitwaye Magdalene aliyetokwa na pepo saba,
3 na Yoana mkewe Kuza, wakili wake Herode, na Susana, NA WENGINE WENGI, WALIOKUWA WAKIMHUDUMIA KWA MALI ZAO”.
Kabla ya kujifunza mazuri ya Tajiri Zakayo jinsi alivyomkaribisha Bwana nyumbani kwake na kutoa zaidi ya Nusu ya mali zake na kuwapa masikini(Luka 19:1-8)…Hebu kajifunze kwanza juu ya Martha jinsi alivyomkaribisha Bwana nyumbani kwake na akatoa Marhamu ya Nardo safi yenye thamani nyingi akampaka Yesu miguuni..na wala hakwenda kuiuza na kuwapa maskini kama ambavyo angefanya Zakayo…Na hiyo ikamsababisha kumpendeza Yesu zaidi ya alivyofanya Zakayo.(Yohana 12:1-7). Kajifunze ni kwanini alifanya vile Martha na wewe ukafanye vilevile…
Usitangulie kujifunza juu ya mazingira Bwana Yesu aliyowatokea Mitume wake 12..shughulika sana kujifunza juu ya mazingira aliyowatokea wale wanawake walio mashujaa wa Imani..Hata hivyo Pamoja na Utume waliokuwa nao wakina Petro lakini hawakuwa wa kwanza kujua kwamba Bwana amefufuka..badala yake ni wale wanawake watakatifu ndio walioifunua siri hiyo wa kwanza ya kufufuka kwa Bwana.. Mariamu ni mwanamke wa kikristo aliyekaa katika nafasi yake na ndiye aliyekuwa wa kwanza kujua kwamba mwokozi anazaliwa ulimwenguni na Zaidi ya yote yeye ndiye aliyempokea..ni wanawake hao hao ndio waliokuwa wa kwanza kujua Mwokozi hayupo kaburini yu hai!….Huoni kama kuna siri kubwa sana hapo?…hata kuja kwa pili kwa Kristo si ajabu baadhi ya wanawake watakatifu ndio watakaokuwa wakwaza kujua…sasa kwanini leo unaikimbia nafasi yako wewe mwanamke wa kikristo??…Unataka kuwa PETRO?
Na wanawake wengine wote katika biblia ambao walikuwa ni mashujaa wa Imani.. kajifunze kwao kabla ya kwenda kujifunza juu ya mashujaa wa Imani wa kiume..kajifunze jinsi walivyovaa, kajifunze jinsi walivyojisitiri…kajifunze juu ya akina Debora jinsi alivyokuwa mnyenyekevu kwa Baraka na Israeli yote, kajifunze juu ya akina Hana, Rahabu, Dorkasi, Esta na wengineo wengi.
Nenda pia kasome, Waraka ule wa pili wa Yohana ambao uliandikwa kwa mama yule mteule jinsi alivyowalea Watoto wake na kuwatunza, mpaka wakakaa katika hiyo kweli, na sifa zake zikavuma katikati ya mitume wa Kristo, na kuaswa kuwa asiyaache matendo yake, bali aipokee thawabu tilimlifu..
Halidhalika, kasome maandiko yanayowazungumzia wanawake wengi, tabia zao mbaya ujiepushe nazo..Na moja ya tabia ambayo imendikwa ni ile ya Udadisi (Au kwa lugha ya kisasa umbea/usengenyaji) soma 1Timotheo 5:13. Itakufaa Zaidi kuliko mambo mengi unayoyasoma katika biblia..
Vivyo hivyo katika makosa usikimbilie kujifunza makosa ya wanaume wa kwenye biblia…kwamfano kosa la Daudi kulala na mke wa Uria sehemu yako ipo wewe kama mwanamke?..au linakufundisha nini?…zaidi somo lile linawafaa wanaume…Wewe kajifunze jinsi wanawake kama YEZEBELI walivyomchukiza Mungu..kajifunze ni tabia gani alizokuwa nazo mwanamke Yezebeli zilizomfanya Mungu amchukue…Yezebeli alikuwa ni mchawi, muuaji na mwanamke anayejipamba uso….Ni mwanamke pekee aliyekuwa anapaka uwanja machoni ndani ya Biblia nzima hakuna aliyekuwa kama yeye..(kasome 2Wafalme 9:30), vivyo hivyo kajifunze kwa wanawake waliofanya makosa kama Mke wa Luthu, makosa yale na wewe usiyafanye, Mke wa Ayubu…kajifunze wanawake wengine waliofanya makosa kama Yule mke wa Ahasuero aliyeitwa Vashti, ambaye alikuwa na kiburi hamweshimu mume wake, kisa tu yeye ni mzuri mpaka kusababisha nafasi yake kuchukuliwa na mwanamke mwenye adabu kama Esta. Jifunze juu ya viburi vya hao vilipowafikisha kabla ya kujifunza juu ya kiburi cha mwanamume Kora aliyemdharau Musa mtumishi wa Mungu.
Bwana akubariki sana…Naamini kwa hayo machache pamoja na mengine mengi Bwana atakayokufunulia utapiga hatua moja katika kuyatenda mapenzi ya Mungu, Ewe mwanamke wa kikristo.
Maran atha.
NAFASI YA MWANAMKE KATIKA KANISA
MAMBO YA KUJIFUNZA KATIKA WARAKA WA PILI WA YOHANA.
EWE MKE! HESHIMA YAKO IPO KWA WAKWE ZAKO.
RABONI!
MARIAMU AKUTANA NA ELISABETI.
TUJIFUNZE JAMBO KWA WANAWAKE HAWA WAWILI:
Je! Mungu anaupendeleo kwa wanaume zaidi ya wanawake?
CHAPA YA MNYAMA
Heshima na Baraka za mwanamke uliyeolewa zipo kwa wakwe zako (hususani mama mkwe wako).
Vitabu viwili vikuu vilivyoitwa kwa majina ya wanawake ni Esta, na Ruthu. Vimeitwa hivyo sio kwasababu tu Mungu anataka kupitisha ujumbe wake wa wokovu kwa kanisa, lakini pia upo ujumbe mahususi unaowahusu wanawake.
Leo tutamtazama Ruthu kwa maneno machache sana. Wanawake wengi wanapitia mikwaruzo katika ndoa zao, na kikubwa ni saikolojia wanayojijengea kabla na baada ya kuolewa kwao, kuhusu wakwe zao, hususani mama-mkwe..Na hapo ndipo panapokuwa chanzo cha matatizo yote…Wanawake wengi wanaoniuliza juu ya matatizo ya ndoa zao, nimegundua kuwa asilimia kubwa hawana mahusiano mazuri na wakwe zao.
Nataka nikuambie ulipokuwa hujaolewa Baraka zako zilikuwa kwa wazazi wako waliokuzaa, lakini unapoolewa ujue kuwa Baraka za ndoa na za uzao wako zinahamia kwa wakwe zako haijalishi ni wabaya kiasi gani..
Kama tunavyofahamu habari ya Ruthu, na Orpa, wote hawa wawili waliolewa na watoto wa Naomi mkwe wao, lakini kwa bahati mbaya, Naomi akafiwa na mume wake na watoto wake wote wawili akabakia kuwa mjane, hivyo akawa hana mume wala mtoto wala mjukuu,..Lakini Naomi kwa ukarimu wake akawatangazia uhuru wakwe zake, warudi makwao kila mmoja akaolewe tena kwasababu bado walikuwa ni vijana na pia bado hawajazaa..Orpa akakubali kuondoa kurudi kwao, lakini Ruthu hakukubali kwasababu alijua Baraka zake zipo wapi…
Hivyo akaamua kurudi na mkwe wake nchi ya Israeli, akajitoa tu kama wakfu kuwa kama mjakazi wake, walipofika wakaishi pamoja,Na Ruthu akawa anamtumika mkwe wake kama mtoto wake kwa amani tu..Ruthu aliipoteza nafsi yake, ili tu amrudhishe mama mkwe wake, lakini alijua ndani yake haitakuwa bure kuwa vile.
Lakini kama tunavyojua, ni nini kilifuata baadaye..Licha tu ya Ruthu kuolewa na Yule tajiri Boazi ndugu yake Naomi, lakini watu wote walimwona kuwa anastahili kuliko watoto 7 wa Naomi..
Ruthu 4: 13 “Basi Boazi akamtwaa Ruthu, naye akawa mke wake; naye akaingia kwake, na Bwana akamjalia kuchukua mimba, naye akazaa mtoto wa kiume.14 Nao wale wanawake wakamwambia Naomi, Na ahimidiwe Bwana, asiyekuacha leo hali huna wa jamaa aliye karibu; jina lake huyu na liwe kuu katika Israeli.15 Naye atakurejezea uhai wako, na kukuangalia katika uzee wako; kwa maana mkweo, ambaye akupenda, NAYE ANAKUFAA KULIKO WATOTO SABA, ndiye aliyemzaa.16 Basi Naomi akamtwaa yule mtoto, akamweka kifuani pake, akawa mlezi wake”.
Ruthu 4: 13 “Basi Boazi akamtwaa Ruthu, naye akawa mke wake; naye akaingia kwake, na Bwana akamjalia kuchukua mimba, naye akazaa mtoto wa kiume.
14 Nao wale wanawake wakamwambia Naomi, Na ahimidiwe Bwana, asiyekuacha leo hali huna wa jamaa aliye karibu; jina lake huyu na liwe kuu katika Israeli.
15 Naye atakurejezea uhai wako, na kukuangalia katika uzee wako; kwa maana mkweo, ambaye akupenda, NAYE ANAKUFAA KULIKO WATOTO SABA, ndiye aliyemzaa.
16 Basi Naomi akamtwaa yule mtoto, akamweka kifuani pake, akawa mlezi wake”.
Embu jiulize wewe mwanamke uliyeolewa, Je, mkwe wako alishawahi kukuona unastahili kuliko watoto wake wote alionao?.. Alishawahi kujivunia kwako kwa namna hiyo? Kama hakuna chochote alichowahi kujivunia kwako, lipo tatizo.
Na kama hiyo haitoshi, Ruthu ambaye alikuwa ni mwanamke wa kimataifa, akahesabiwa katika uzao wa Kiyahudi kama vile Rahabu alivyohesabiwa kwa tendo lake tu hilo , na huko huko baadaye ndipo alipokuja kutokea Mfalme Daudi.. Uzao wa kifalme na uzao wa Bwana wetu Yesu Kristo.
Jaribu kufikiria tena jinsi uzao wake ulivyobarikiwa zaidi hata ya wanawake wengi wa kiebrania waliozaliwa na Ibrahimu…Na hiyo yote siri ilikuwa kwa MAMA MKWE WAKE na si penginepo. Ni yeye tu na Esta ndio waliopata nafasi ya vitabu vyao kuandikwa majina yao.
Hata wewe mwanamke uliyeolewa au unayekwenda kuolewa.. Timiza jukumu lako la kuwapenda wakwe zako kwasababu huko ndipo uzao wako utakapobarikiwa na ndipo ndoa yako itakapokuwa na amani..
Wewe kama siku zote huna habari na wakwe zako, unawasengenya, huwahudumii, huwaheshimu, unagombana nao, unawapenda kinafki tu, unafanya ili kutimiza wajibu tu, lakini hujitoi kwao, unaifikiria familia yako tu na ndugu zako…usitazamie kuwa Utabarikiwa uzao wako.
Biblia inakupa fundisho, litii ulifuate , watu wengi wenye matatizo ya ndoa huwa chimbuko ni hapo, pasipo hata wao kujua. Ikiwa humpendi mama wa mume wako, na usimpende na mume wako pia, lakini kama unampenda mume wako basi mpende na mama yake na ndugu zake ndipo utakapoishi kwa rah ana amani katika familia yako. Unaweza ukasema mimi ninaishi kwa raha, hao wakwe wananihusu nini..ni kweli utaishi leo kwa raha, lakini uzao wako unaweza usiishi kwa raha huko mbeleni..Na vile vile Maisha yako pia yanaweza yasiwe ya baraka.
Hiyo ni sheria ya Mungu ambayo ipo katika maandiko, ikiwa utataka kuwazaa akina YESE na Mfalme Daudi basi ambata na wakwe zako bega kwa bega, na kanuni hiyo itakulipa..Epuka mafundisho na injili za kwenda kupiga maadui zako, na kuwalenga wakwe zako..hapo utakuwa unazipiga baraka zako mwenyewe, utakuwa unajimaliza mwenyewe, ukidhani unajihami kumbe unajimaliza…Ukiona kuna kasoro Fulani ipeleke kwenye sala ukimwomba Mungu azidi kukupatanisha na wakwe zako sana, maana milango ya baraka zako ndio ipo huko.. siku zote zingatia hilo
Bwana akubariki.
MATUNDA YAPATANAYO NA TOBA!
USIKIMBILIE TARSHISHI.
UZAO WA NYOKA.
KIELELEZO CHA MWANAMKE KATIKA NYUMBA.
JE! NI LAZIMA WATU WOTE WANENE KWA LUGHA?
JE TATIZO LA KULA KUCHA NI ISHARA YA KUWA NA MAPEPO?
USIMPE NGUVU SHETANI.
Usikimbilie tarshishi hakuna uzima
Jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo libarikiwe daima. Karibu tujifunze Neno la Mungu ambalo ndio mwanga wa njia yetu na Taa iongozayo miguu yetu.
Kama ni msomaji wa biblia utakumbuka habari za Nabii Yona jinsi alivyoukimbia uso wa Bwana na kuelekea Tarshishi. Lakini umewahi kujiuliza TARSHISHI ulikuwa ni mji wa namna gani?…Ninawi tunaujua ndio uliokuwa mji mkuu wa Ashuru..lakini Tarshishi je!
Hebu kwa ufupi tujifunze juu ya huu mji na kisha tutapata jambo jipya ambalo linaweza kutusaidia katika nyakati hizi za hatari tunazoishi.
Mji wa Tarshishi ni mji ambao ulikuwa mahali panapoitwa Tiro..ambapo kwa sasa ni nchi ya Lebanoni…Nchi ya Lebanoni ni nchi iliyopo kaskazini mwa Israeli, kama vile Kenya ilivyo kaskazini mwa Tanzania (Na mpaka leo hiyo nchi inaitwa hivyo hivyo Lebanoni haijabadilika, inakaliwa na Waarabu sasahivi, lakini haina tena utajiri/ushupavu uliokuwa nao wakati ule)..
Sasa wakati wa vipindi vya wafalme wa Israeli nchi hii ya Tiro (Lebanoni) ambao mji wake mkuu ni Tarshishi ndio ulikuwa ni mji wa kibiashara mkubwa kuliko miji mingine yote. Ulikuwa unasifika kwa kuwa na MERIKEBU NYINGI ZA KIBIASHARA kuliko miji mingine yote. Na ulikuwa ni mji wenye uzoefu wa ki-biashara
Biblia inasema katika kitabu cha Ezekieli…
Ezekieli 27:12 “Tarshishi alikuwa mfanya biashara kwako, kwa sababu ya wingi wa utajiri wa kila aina; kwa fedha, na chuma, na bati, na risasi, walifanya biashara, wapate vitu vyako vilivyouzwa”
Yeremia 10: 9 “Iko fedha iliyofuliwa ikawa mabamba, iliyoletwa kutoka Tarshishi, na dhahabu kutoka Ufazi,….”.
Unaona? Vilevile Miti ya Mierezi ambayo ilitumika katika ujenzi wa hekalu la kwanza la Sulemani, ilitoka huko Lebanoni, kulikuwa hakuna mahali pengine ambapo miti hiyo ilikuwa inapatikana, na njia ya usafirishaji iliyokuwa inatumika kusafirishia miti hiyo ni bahari (Njia ya Maji). Kwa ufupi sehemu kubwa ya malighafi za ujenzi wa hekalu la kwanza la Sulemani zilitoka huko Tiro, ambao mji wake mkuu ni Tarshishi. Hata Dhahabu Sulemani alizozitumia kutengenezea vyombo vyake zilitoka huko Lebanoni..Sulemani alinunua dhahabu nyingi kutoka huko Lebanoni mpaka kufikia kiwango cha kuwa tajiri sana hata kuona kutumia madini ya fedha(silver) kutengenezea vito vyake ni kama kujishushia heshima..
1Wafalme 10: 21 “Na vyombo vyote vya kunywea vya mfalme Sulemani vilikuwa vya dhahabu, na vyombo vyote vya nyumba ya mwitu wa Lebanoni vilikuwa vya dhahabu iliyosafika; hakuna vya fedha, fedha haikuhesabiwa kuwa kitu siku za Sulemani. 22 Kwa kuwa mfalme alikuwa na merikebu za Tarshishi baharini pamoja na merikebu za Hiramu; mara moja katika miaka mitatu huja merikebu za Tarshishi, zikileta dhahabu, na fedha, na pembe, na nyani, na tausi. 23 Basi mfalme Sulemani akawapita wafalme wote wa duniani kwa mali, na kwa hekima.”
1Wafalme 10: 21 “Na vyombo vyote vya kunywea vya mfalme Sulemani vilikuwa vya dhahabu, na vyombo vyote vya nyumba ya mwitu wa Lebanoni vilikuwa vya dhahabu iliyosafika; hakuna vya fedha, fedha haikuhesabiwa kuwa kitu siku za Sulemani.
22 Kwa kuwa mfalme alikuwa na merikebu za Tarshishi baharini pamoja na merikebu za Hiramu; mara moja katika miaka mitatu huja merikebu za Tarshishi, zikileta dhahabu, na fedha, na pembe, na nyani, na tausi.
23 Basi mfalme Sulemani akawapita wafalme wote wa duniani kwa mali, na kwa hekima.”
Huko Tarshishi walikuwepo pia manahodha waliobobea sana, na pia kulikuwa na watu wenye elimu ya ujenzi kubwa sana..baadhi ya wajenzi wa hekalu lile la mfalme Sulemani aliwatolea huko huko Lebanoni.
Hivyo ipo mistari mingi sana katika biblia inayoelezea ushupavu wa Tarshishi…ipo mingi sana unaweza kuipitia kwa muda wako upatapo nafasi…Kasome (Ezekieli 27: 25-27, Ezekieli 38:13, 1Wafalme 22: 48, ).
Sasa kwa kuielewa sifa ya Huu mji wa wa Tarshishi tunaweza kujua ni kwanini Yona alikimbilia huko…Na kwanini alipanda merikebu…Kumbuka kutoka Israeli mpaka Tarshishi(huko Lebanoni) kulikuwepo na njia ya nchi kavu nzuri tu..lakini yeye alikwenda kupanda merikebu. Ni sawa leo mtu atake kwenda Tanga..aache kupanda basi achague kutumia ferry/meli pale bandarini Dar es salaam aende Tanga. Ni lazima anayo sababu ya kufanya hivyo..
Na ni wazi kuwa sababu yenyewe si nyingine Zaidi ya biashara…Yona pengine alikuwa na mizigo yake anakwenda kufanya biashara.. Tarshishi haukuwa mji wa kitalii..ulikuwa ni mji wa kibiashara..hivyo alipoisikia sauti ya Mungu ikimwambia aende Ninawi kuhubiri yeye akaona njia pekee ya kuipotezea hiyo sauti ni kuzama kwenye biashara zake…wala hakuchagua kukimbilia miji mingine kama Misri, au Moabu ambayo angepata pumziko..yeye alikuwa na sababu ya kwenda Tarshishi.. Angalau apate riziki kidogo.
Lakini kama tunavyojua ni nini kilimtokea njiani. Biashara iliishia pale pale, wakapata hasara merikebuni kwa kutupa bidhaa zao majini kupunguza uzito.. na mtaji wote ukaishia palepale.
Sasa kitu cha muhimu cha kujifunza hapo ni nini?..Usiikimbie sauti ya Mungu leo inayokuambia fanya jambo fulani au tii jambo fulani, usiidharau sauti hiyo na kukimbilia kufanya biashara zako. Ni kama bahati tu Yona alipata neema mipango yake ilikatishwa katikati haikukamilika…..angeweza kuachwa aende huko anakokwenda na Mungu akamtafuta mtu mwingine wa kwenda Ninawi kuhubiri na watu wa Ninawi wakaokoka lakini Yona huko alikokimbilia akafanikiwa na utajiri wake lakini akafa na huku hajalitimiza kusudi la Mungu aliloletewa duniani, na mwisho wa siku kupotea katika ziwa la moto milele.
Hivyo leo isikie sauti ya Mungu lipo kusudi la wewe kuwepo hapa duniani la kufanya mapenzi ya Mungu.. usilikimbie kusudi hilo kwa kisingizio cha kufanya biashara, Hizo biashara ni za muhimu sawa..lakini kulitimiza kusudi la Mungu ni muhimu Zaidi..Una safari 5-6 za kwenda China kila mwezi lakini huna siku ya kukaa kufunga na kusali na kulitafakari Neno. Mwaka unapita hujawahi kufunga useme angalau nautafuta uso wa Mungu. Hujawahi kusema angalau mwezi huu wote sitasafiri nitajikita katika kutafuta kujua mapenzi ya Mungu kwangu…Unatengeneza pesa lakini hutengenezi hazina yako mbinguni..Nchi zinakujua, Benki zinakujua, lakini mbinguni hujulikani.
Watu wengi wananiambia, mtumishi ninatamani kujifunza Neno, wengine wanasema ninatamani kwenda kanisani lakini kazi zinanisonga, shughuli zinanifanya kuwa buzy,..Nataka nikuambie unayo hatari kubwa sana ya kuiokosa mbingu.
Unakimbilia Tarshishi unaiacha Ninawi?..Unakimbilia kufanya uwekezaji unasahau kutangaza habari za ufalme wa mbinguni..Kumbuka Neema aliyoipata Yona sio atakayoipata kila mtu. Simama katika nafasi yako muda ni mchache, usiruhusu mbegu yako kusongwa na kitu chochote.
Bwana atusaidie.
Ikiwa hujampa Kristo Maisha yako..na unakazana kuifuata njia ya Ninawi!..nakushauri geuka leo..Bwana Yesu alisema “Baba yetu wa mbinguni anajua kuwa tuna haja na hayo yote, bali tuutafute kwanza ufalme wake na haki yake, na hayo mengine yote tutazidishiwa”..Hivyo tubu leo kwa kukusudia kuacha dhambi, na kupunguza masumbufu ya Maisha haya ambayo yanakuvuta na kukusonga ukae mbali na Mungu wako.
Luka 21:34 “ Basi, jiangalieni, mioyo yenu isije ikalemewa na ulafi, na ulevi, NA MASUMBUFU YA MAISHA HAYA; siku ile ikawajia ghafula, kama mtego unasavyo; 35 kwa kuwa ndivyo itakavyowajilia watu wote wakaao juu ya uso wa dunia nzima. 36 Basi, kesheni ninyi kila wakati, mkiomba, ili mpate kuokoka katika haya yote yatakayotokea, na kusimama mbele za Mwana wa Adamu”.
Luka 21:34 “ Basi, jiangalieni, mioyo yenu isije ikalemewa na ulafi, na ulevi, NA MASUMBUFU YA MAISHA HAYA; siku ile ikawajia ghafula, kama mtego unasavyo;
35 kwa kuwa ndivyo itakavyowajilia watu wote wakaao juu ya uso wa dunia nzima.
36 Basi, kesheni ninyi kila wakati, mkiomba, ili mpate kuokoka katika haya yote yatakayotokea, na kusimama mbele za Mwana wa Adamu”.
Chukua hatua leo, na Bwana akubariki.
UVUMILIVU WA MUNGU ULIPOKUWA UKINGOJA.
Biblia ni nini?
ANGALIA USIJE UKANG’OA NGANO KATIKATI YA MAGUGU.
UTHABITI WA AGANO LA MUNGU KWA MKRISTO.
Nifanye nini ili niondokane na Hofu maishani mwangu?
WhatsApp
Saa ya kuharibiwa iliyo tayari kuujilia ulimwengu wote Inakuja..
Ufunuo 3:10 “Kwa kuwa umelishika neno la subira yangu, mimi nami nitakulinda, utoke katika saa ya kuharibiwa iliyo tayari kuujilia ulimwengu wote, kuwajaribu wakaao juu ya nchi”.
Kuna saa ya kuharibiwa inakuja huko mbeleni, ni wakati ambapo kila mtu kwa macho yake atakuwa anaona jinsi dunia inavyokwenda kuisha ndani ya kipindi kifupi sana, kutokana na dhiki, na mapigo, pamoja na mambo ya kutisha yatakayokuwa yanaendelea duniani wakati huo.. Kipindi hicho kitakuwa ni kifupi sana, kisichozidi miaka 7 tu. Na kitaanza muda mfupi tu baada ya unyakuo kupita.
Unyakuo ndio utakaokuwa kalenda ya kututambulisha kuwa dunia imebakisha umri wa miaka 7 tu. Na ndio maana itamgharimu Mungu awaondoe kwanza wale wateule wake watakatifu ambao walikuwa wanalishika Neno la Subira yake.. Watu ambao maisha yao yote, mawazo yao yote yalikuwa yanaelekea mbinguni tu, waliojikana nafsi, waliotengwa na ulimwengu, hao tu ndio Mungu atakaowanyakua ..Ili kupisha uharibifu huo kuchukua nafasi yake.
Kama tu vile alivyomwondoa Henoko, kwa kumnyakua asikutwe na gharika, …ndivyo itakavyokuwa kwa watu hao wachache sana, watanyakuliwa wasionekane duniani, kama vile alivyomtenga Ibrahamu akawa mbali na Sodoma na Gomora ndivyo itakavyokuwa kwa wale ambao wanaishi Maisha ya uaminifu sasa, wataondoshwa katika ulimwengu huu kabla ya siku ile ya uharibifu, na watakwenda kumlaki Bwana Yesu mawinguni na moja kwa moja safari ya kwenda kumwona Baba itaanzia hapo.
Lakini wale wengine ambao ni wakristo-vuguvugu, hawatakwenda popote, watakuwa mfano wa Nuhu wataishuhudia dhiki, wataingia katika misukosuko ya dhiki kuu na mateso makali ambayo biblia inasema haijawahi kuwepo tangu kuwekwa kwa misingi ya ulimwengu, kama vile Nuhu alivyokuwa katika dhiki ndani ya Safina..Kama vile Lutu alivyokuwa anapitia dhiki ile ya misukosuko sodoma ya Gomora ilivyokuwa inachomwa, siku zake zote alikuwa ni mbioni tu,..ndivyo itakavyokuwa kundi hilo kubwa la wakristo wanaosema wameokoka lakini Maisha yao hayana ushuhuda wowote hawaishi kama watu wanaomngojea Bwana wao. Dhiki hiyo itakuwa ni sehemu ya Maisha yao. Mpinga-kristo atawawinda huku na huko kama kuku..
Ndugu biblia inavyosema DHIKI basi ujue ni dhiki kweli kweli ,licha tu ile ya mpinga-kristo yatakuwepo pia mapigo mengine ya Mungu kwa wale watakaoipokea chapa, kasome Ufunuo 16, hadi mwisho kabisa , wanadamu wataadimika kama Dhahabu biblia inasema hivyo katika (Isaya 13),kama leo hii usivyoweza kuikota dhahabu kama mawe barabarani ndivyo itakavyokuwa kwa watu wakati huo, Kama alivyotoka tu Nuhu na wenzake 7 katika ya mabilioni ya watu ndivyo itakavyokuwa siku hiyo, kama walivyotoka watatu tu yaani Lutu na Watoto wake wawili ndivyo itakavyokuwa kwa mabilioni ya watu waliopo leo hii duniani.. kikundi kidogo sana, na tena watakuwa ni wale watakaowahifadhi wayahudi katika ule wakati wa dhiki za mpinga-kristo, Lakini wewe uliyepo leo hii unaipinga injili sasa , siku hiyo utakuwa ni jivu limelala hapo chini au mzoga, na ndege watakuwa wanakula nyama yako.
Tukiachilia mbali ile vita ya Harmagedoni, siku yenyewe ambayo Bwana atashuka na mawingu ambapo kila jicho litamwona, na watu watamwombolezea, misingi ya dunia hii unayoiona itatikisika, na kutakuwepo na tetemeko kubwa la ardhi ambalo halijawahi kuwepo, kumbuka wakati huo hayo yanaendelea tayari dunia imeshakuwa giza, hakuna jua wala mwezi, wala nyota yoyote angani, tetemeko hilo litaitikisa milima, mpaka hivi visiwa vyote unavyoviona leo hii vitahama, wewe wakati huo utakuwepo wapi Siku ya kuharibiwa? Wafalme, watakuwa wakilia wakiomba milima iwaungukie wafe, lakini wasikumbane na hiyo hasira ya mwana-kondoo.
Ufunuo 6:12 “Nami nikaona, alipoifungua muhuri ya sita, palikuwa na tetemeko kuu la nchi; jua likawa jeusi kama gunia la singa, mwezi wote ukawa kama damu, 13 na nyota zikaanguka juu ya nchi kama vile mtini upukutishavyo mapooza yake, utikiswapo na upepo mwingi. 14 Mbingu zikaondolewa kama ukurasa ulivyokunjwa, na kila mlima na kisiwa kikahamishwa kutoka mahali pake. 15 Na wafalme wa dunia, na wakuu, na majemadari, na matajiri, na wenye nguvu, na kila mtumwa, na mwungwana, wakajificha katika pango na chini ya miamba ya milima, 16 wakiiambia milima na miamba, Tuangukieni, tusitirini, mbele za uso wake yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na hasira ya Mwana-Kondoo. 17 Kwa maana siku iliyo kuu, ya hasira yao, imekuja; naye ni nani awezaye kusimama”?
Ufunuo 6:12 “Nami nikaona, alipoifungua muhuri ya sita, palikuwa na tetemeko kuu la nchi; jua likawa jeusi kama gunia la singa, mwezi wote ukawa kama damu,
13 na nyota zikaanguka juu ya nchi kama vile mtini upukutishavyo mapooza yake, utikiswapo na upepo mwingi.
14 Mbingu zikaondolewa kama ukurasa ulivyokunjwa, na kila mlima na kisiwa kikahamishwa kutoka mahali pake.
15 Na wafalme wa dunia, na wakuu, na majemadari, na matajiri, na wenye nguvu, na kila mtumwa, na mwungwana, wakajificha katika pango na chini ya miamba ya milima,
16 wakiiambia milima na miamba, Tuangukieni, tusitirini, mbele za uso wake yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na hasira ya Mwana-Kondoo.
17 Kwa maana siku iliyo kuu, ya hasira yao, imekuja; naye ni nani awezaye kusimama”?
Unaona?
Mambo haya utayashuhudia wewe ambaye bado upo nje ya Kristo, na wewe ambaye unaishi Maisha ya uvuguvugu sasahivi. Dalili zote zinathibitisha kuwa sisi watu wa kizazi hichi, haya mambo yatatupata, na dalili kubwa ni kuwa huu ni wakati ambao watu wanamejisahau, na pale watu walipojisahau na wanaona kuna Amani biblia inasema Hapo ndipo uharibifu unapokuja kwa ghafla (1Thesalonike 5:2)….Swali ni Je! Tumejiwekaje tayari..
Je! Bado unaishi Maisha ya kubahatisha? Utasema tena ni kwanini mnahubiri hivyo kana kwamba mnao uhakika kuwa Yesu atarudi wakati wetu..Ndio tunahubiri hivyo kwa nguvu zote kwasababu anayejua siku na saa ya kiama, ametuambia tuhubiri hivyo kwa nguvu sana…
Luka 14:33 “ Angalieni, kesheni, [ombeni], kwa kuwa hamjui wakati ule utakapokuwapo. 34 Mfano wake ni kama mtu mwenye kusafiri, ameiacha nyumba yake, amewapa watumwa wake amri, na kila mtu kazi yake, naye amemwamuru bawabu akeshe. 35 Kesheni basi, kwa maana hamjui ajapo bwana wa nyumba, kwamba ni jioni, au kwamba ni usiku wa manane, au awikapo jimbi, au asubuhi; 36 asije akawasili ghafula akawakuta mmelala. 37 Na hilo niwaambialo ninyi, nawaambia wote, Kesheni.
Luka 14:33 “ Angalieni, kesheni, [ombeni], kwa kuwa hamjui wakati ule utakapokuwapo.
34 Mfano wake ni kama mtu mwenye kusafiri, ameiacha nyumba yake, amewapa watumwa wake amri, na kila mtu kazi yake, naye amemwamuru bawabu akeshe.
35 Kesheni basi, kwa maana hamjui ajapo bwana wa nyumba, kwamba ni jioni, au kwamba ni usiku wa manane, au awikapo jimbi, au asubuhi;
36 asije akawasili ghafula akawakuta mmelala.
37 Na hilo niwaambialo ninyi, nawaambia wote, Kesheni.
Sasa ikiwa wewe, unasikiliza injili ya mapepo inayokuhubiria kuwa dunia haitaangamizwa, ujue kuwa upo hatarini sana,. Kama hujamaanisha kumfuata Bwana Yesu, basi ni heri ukafanya hivyo sasa kabla mlango wa neema haujafungwa..Chaguo ni lako, uamuzi ni wako..Lakini fahamu tu wale wanaolishika Neno la Subira yake leo hii, hao ndio watakaoepushwa na saa ile ya kuharibiwa..
Bwana, Mkuu wa uzima wetu akubariki.
Maran Atha!
SAKRAMENTI NI NINI, NA JE! IPO KATIKA MAANDIKO?
TOFAUTI KATI YA HEKALU, SINAGOGI NA KANISA NI IPI?
Kwanini Bwana Yesu, aliruhusu yale mapepo yawaingie nguruwe?
Ikiwa sisi tuliumbwa na Mungu,Je! Mungu aliumbwa na nani?
Nini maana ya huu mstari ” Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda;”?(2Timotheo 4:7)
SALA YA ASUBUHI
NINI MAANA YA SISI KUWA WATOTO WA MUNGU?
Ni kura ya aina gani waliipiga wale watu waliosafiri na Yona..hata ikamwangukia Yona? Na je! Mungu anatumia kura kuchagua watu?
JIBU: Biblia haijasema ni kura gani ilipigwa pale, kama ni ya kurusha kete au kwamba kila mmoja aliandika maoni yake binafsi na walipoyaleta yote yakaonekana yanamlenga Yona…Hakuna ajuye, na wala biblia haijaandika..Lakini yote katika yote ni kwamba kura ilipigwa pale na ikamwangukia Yona.
Kikubwa tunachoweza kujifunza ni kwamba..Mungu anaweza kutumia njia yoyote kukamilisha kusudi lake..anaweza kutumia njia iliyo rasmi au isiyo rasmi…Kwamfano kama wewe ni mwanafunzi mzuri wa Biblia utagundua kuwa Mungu alimpa Daudi ufalme wote wa Israeli kwa njia ya fitina..Mungu Alimwahidia atakuwa Mfalme juu ya Israeli yote na akampaka mafuta kwa mikono ya Nabii Samweli…lakini siku ilipofika ya unabii huo wa kuwa Mfalme wa Israeli kutimia..hakupata ufalme kwa njia ya uchaguzi bali kwa njia ya fitina. Yaani mfalme aliyekuwa madarakani (mtoto wa Sauli )alifanyiwa fitina ndipo Daudi akaingia madarakani….
Kwani siku hiyo walitokea tu watu Fulani waliokuwa wanaishi kwenye nyumba ya Mfalme na hao watu wakamvizia mfalme aliyekuwa madarakani wakampiga na kumuua na kumkata kichwa,..na kumpelekea kile kichwa Daudi na kumwambia leo Mungu amewalipiza kisasi maadui zako. Ingawa Daudi hakukubaliana na uovu wao…lakini kukawa hakuna namna ni lazima kiti cha ufalme kikaliwe na mtu mwingine na huyo hakuwa mwingine zaidi ya Daudi (kasome 2Samweli 4:5-12).
Kwani Israeli walipoona mfalme wao kauawa kukawa hakuna namna zaidi ya kumweka Daudi Madarakani awe mfalme.. Na unabii wa yeye kuwa Mfalme juu ya Israeli yote ukatimia pale.
Hali kadhalika Mungu anaweza kumchagua mtu kwa njia yoyote ile iwe rasmi au isiyo rasmi..Na anaweza kumtumia mtu yoyote Yule kukamilisha kusudi lake, anaweza kumtumia mwovu au mwenye haki…kwa jinsi apendavyo yeye. Akitaka kumweka mtu mahali anaweza kutumia kura au asitumie kura. Mathiya alichaguliwa kwa kura kuwa miongoni mwa Mitume 12 wa Bwana Yesu kuchukua nafasi ya Yuda. Lakini Petro na Mitume wengine hawakuchaguliwa kwa kura…Na hiyo haikumfanya Mathiya asiwe miongoni mwa wale mitume 12.
Kadhalika Yona alichaguliwa kwa kura ili kuadhibiwa na Mungu. Mungu angeweza kuwaonyesha maono wale watu kuwa Yona ndio chanzo cha matatizo, lakini pale hakuitumia hiyo njia…angeweza kumtuma malaika akawatokea na kuwaambia Yona ndie chanzo cha lile tatizo lakini haikumpendeza..
Hata katika chaguzi za viongozi wa shule, kijiji, mtaa, au nchi…wote wanaochaguliwa na kushika nafasi hizo ni Mungu ndio kawaweka pale…Iwe wamewekwa kwa njia iliyo halali au isiyo halali kama ya uwizi wa kura au la!,..hiyo haijalishi..Ni Mungu ndio kawaweka pale..(Siku ya mwisho ndio watakwenda kujibu kwanini waliiba kura au kwanini hawakuwa waaminifu katika nafasi hizo)..Lakini maadamu tayari wapo katika hizo nafasi ni Mungu ndiye kawaweka…
Maraisi wote waliopo madarakani ni Mungu ndiye kawaweka katika nafasi hizo haijalishi waliiba kura au hawakuiba..haijalishi ni madiktekta au sio madiktekta, haijalishi wanamjua Mungu au hawamjui..Ni Mungu ndiye kawaweka kwa kusudi lake maalumu…wengine kwa kusudi kama la Farao, wengine kama la Yeroboamu, wengine kama la Nebukadneza, wengine kama la Mfalme wa Ashuru, wengine kama Manase, wengine kama Hezekia… Kila mmoja kawekwa pale na Mungu kwa kusudi maalumu…
ROHO YA MPINGA KRISTO IKITENDA KAZI SIKU HIZI ZA MWISHO
KWANINI MUNGU ALIMTUMIA MUSA KWA VIWANGO VILE?
JE! MUNGU NI NANI?
Ni sahihi kumuita Mariamu mama wa Mungu?
KUOTA UMETUMBUKIA SHIMONI.
SI KILA KIPENDEZACHO KINATOKA KWA BWANA.
Sala ya Asubuhi inapaswa iweje?..Na je kuna sala ya jioni pia?
Hakuna sala rasmi ya Asubuhi iliyotungwa kwamba watu wafuate mfumo wake lakini ni wajibu wa kila mtu anayeitwa mkristo kusali..Katika kusali au kuomba kuna vitu vikuu vitatu vya kuzingatia katika sala yoyote ile.. Cha kwanza ni Shukrani, cha pili ni kupeleka mahitaji na cha tatu ni kutangaza.
Katika sala ya Asubuni pia ni muhimu kuzingatia hivyo vipengele vitatu. Mwishoni somo hili kuna somo lingine lenye kichwa kinachosema “FAIDA ZA MAOMBI”. Nakushauri ulisome ili uweze kuelewa uchambuzi wa vipengele hivyo vitatu vya maombi.
Lakini kama ndio kwanza umempa Kristo maisha, basi sala hii hapa chini kwa Asubuhi inaweza kukufaa.
Unapoamka kabla ya kufanya kitu chochote kile, hata kabla ya kwenda kupiga mswaki.. Sali sala hii kwa kumaanisha na kwa muda mrefu kwa jinsi uwezavyo ukitaja hata mambo ambao hayajaandikwa katika sala hii.
Sema…
‘Ee Baba yangu, Mungu muumba wa mbingu na nchi, nakushukuru kwa kuniamsha nikiwa mzima wa afya,(hata kama umeamka na udhaifu fulani mdogo huna buni kumshukuru Mungu pia)
Nasema ahsante sana ni kwa Neema zako tu, wapo ambao hawajaweza kuamka leo lakini mimi nimeamka.
Nakuomba unipe Neema yako katika siku ya leo inayoanza nikatembee katika mapenzi yako, nisikutende dhambi wala nisikuhuzunishe kwa jambo lolote, naomba ukaniepushe na majaribu yote, na mipango yote mibaya ya yule Adui aliyoipanga juu yangu na juu ya watu wangu na vitu vyangu na afya yangu na shughuli zangu katika hii siku ya leo.
Nijalie pia siku hii ya leo angalau niongeze kitu kimoja katika ufalme wako, hata itakapofika tena jioni nikapate kushuhudia matendo yako makuu na kukushukuru. Naomba haya machache katika Jina la Yesu Kristo.
Amen’.
Kumbuka pia tuna wajibu wa kusali muda wote na mahali popote sio tu asubuhi, au jioni…hapana bali hata tukiwa tunatembea, tunafanya kazi..tuna wajibu wa kuomba…sala ya jioni pia ni ya muhimu sana kama tu ilivyo sala ya Asubuhi.
FAIDA ZA MAOMBI.
FAIDA ZA MAOMBI YA USIKU
UNATAKA KUBARIKIWA? BASI USIKWEPE GHARAMA ZAKE.
HERI NINYI MLIAO SASA, KWA SABABU MTACHEKA.
JE NI KWELI MTU ANAWEZA KUTOKA NJE YA MWILI WAKE?.
MTAIFAHAMU KWELI NAYO HIYO KWELI ITAWAWEKA HURU.
SWALI: Biblia inamaana gani kusema “Bali wajane walio vijana ukatae kuwaandika hao, maana, wakizidiwa na tamaa kinyume cha Kristo, wataka kuolewa;nao wana hukumu kwa kuwa wameiacha imani yao ya kwanza”.(1Timotheo 5:11-12).
Ni kwanini wahukumiwe kwa kuolewa kwao tena, wakati biblia inaruhusu wajane kuolewa?
JIBU: Kama ukisoma kuanzia mistari ya juu utaona zamani za mitume kulikuwa na utaratibu wa kuwakumbuka wajane katika posho la kanisa..Na kulikuwa na masharti yake ili uweze kuandikwa,
1Timotheo 5:1 “Mjane asiandikwe isipokuwa umri wake amepata miaka sitini; naye amekuwa mke wa mume mmoja”;
1Timotheo 5.10 “naye ameshuhudiwa kwa matendo mema; ikiwa amelea watoto, ikiwa amekaribisha wageni, ikiwa amewaosha watakatifu miguu, ikiwa amewasaidia wateswao, ikiwa amefuata kwa bidii kila tendo jema”.
5.4 Lakini mjane akiwa ana watoto au wajukuu, na wajifunze kwanza kuyatenda yaliyo wajibu wao kwa jamaa zao wenyewe, na kuwalipa wazazi wao. Kwa kuwa hili lakubalika mbele za Mungu.
5.5 Basi yeye aliye mjane kweli kweli, ameachwa peke yake, huyo amemwekea Mungu tumaini lake, naye hudumu katika maombi na sala mchana na usiku.
Hivyo mjane yeyote ambaye alikuwa amekidhi hivyo vigezo basi alikuwa anaruhusiwa kuandikwa katika kanisa, na kanisa lilikuwa linawatambua watu kama hao, na walikuwa wanatengewa fungu lao maalumu.
Lakini sasa kama tayari alishajitoa kikamilifu kwa Bwana namna hiyo, ameshaingia katika nadhiri kama hizo kwamba tumaini lao lote sasa ni kwa Bwana tu, mpaka anafikia hatua ya kuchukua uamuzi wa kwenda kuandikwa katika kitabu cha kanisa kwamba ni yeye ni mjane kweli kweli aliyemwekea Mungu tumaini lake lote, halafu inatokea ghafla tu anageuka na kutaka kuja kuolewa tena….Sasa katika mazingira kama hayo watu wa namna hiyo maandiko haya ndio yanayowahusu.
5.12 wana hukumu kwa kuwa wameiacha imani yao ya kwanza..
Na ndio maana mtume Paulo akatoa angalizo kabisa, wajane wazee ni heri wasiandikwe waolewe, kwa namna nyingine ni kwamba kama wanajijua siku moja watakuja kuolewa basi wasijiingize katikati ya wajane kweli kweli waliodhamiria kumuishia Mungu maisha yao yote vinginevyo watakuwa wanajitafutia hukumu ya bure..wakizidiwa na tamaa.
Ubarikiwe.
Je! Ni halali kuoa/kuolewa na mtu ambaye tayari anao watoto?
Je! Ni sahihi kwa mkristo kuoa/kuolewa na mtu wa imani nyingine?
NDOA NA TALAKA:
JE! UNAYATUNZA MAVAZI YAKO?
SIKU YA UNYAKUO ITAKUKUTAJE?
Kwanini kila nikitaka kusali naingiwa na uvivu?
USILALE USINGIZI WAKATI WA KUMNGOJEA BWANA.
CHUKIZO LA UHARIBIFU
Jinsi sodoma na gomora ilivyokuwa inavutia sana.
Mwanzo 13:10 “Lutu akainua macho yake, akaliona Bonde lote la Yordani, ya kwamba lote pia lina maji, kabla Bwana hajaharibu Sodoma na Gomora, lilikuwa kama bustani ya Bwana, kama nchi ya Misri hapo unapokwenda Soari. 11 Basi Lutu akajichagulia Bonde lote la Yordani; Lutu akasafiri kwenda upande wa mashariki; wakatengana wao kwa wao”.
Mwanzo 13:10 “Lutu akainua macho yake, akaliona Bonde lote la Yordani, ya kwamba lote pia lina maji, kabla Bwana hajaharibu Sodoma na Gomora, lilikuwa kama bustani ya Bwana, kama nchi ya Misri hapo unapokwenda Soari.
11 Basi Lutu akajichagulia Bonde lote la Yordani; Lutu akasafiri kwenda upande wa mashariki; wakatengana wao kwa wao”.
Ndugu kama ulikuwa hujui, basi leo ujue, kuwa dhambi ni kitu kinachovutia sana! Kama dhambi ingekuwa haivutii hakuna mtu leo hii angenaswa na mtego wowote wa dhambi..Wengi wetu tunajua habari ya Lutu na mjomba wake Ibrahimu jinsi walivyopishana kauli kutokana na wingi wa mali walizokuwa nazo, mpaka ikafikia hatua sasa wajitenge kila mmoja achague upande wake wa kukaa.
Lutu akapewa kipaumbele cha kwanza cha kuchagua, akafanya utafiti wake wa mji bora wa kukaa, ndipo akaitazama miji yote iliyokuwa kando kando na pale walipokuwepo yeye na Ibrahimu, mwishowe akafanikiwa kuona miji mizuri sana, ambayo hakukuwa na mfano wake katika kaanani yote na miji yenyewe ni Sodoma na Gomora. Biblia inasema miji hiyo ilikuwa mfano wa BUSTANI YA MUNGU (Edeni). Ilikuwa nzuri karibia ifanane na Edeni..Hivyo sio kila mahali panapoonekana pazuri Mungu yupo…Uzuri wa sodoma na Gomora ulifananishwa na Edeni, lakini ilikuwa ni bustani ya shetani…Shetani naye anayo Edeni yake ambayo kwa uzuri inakaribia Ilikuwa ni miji yenye kijani kibichi, yenye chemchemi za maji, na mwonekano wa kuvutia.
Vivyo hivyo ilikuwa ni miji yenye ustaarabu uliomakini, yenye uchumi mkubwa, yenye fursa nyingi za biashara, isiyo na njaa wala kiu, miji ambayo mtu ukiishi unajua nini maana ya maisha,.mbali sana na hiyo Kaanani ambayo alikuwa anaishi yeye na Ibrahimu, ambayo ni jangwa tupu, hakuna hata chakula cha kutosha maji yenyewe ni ya shida, kama nusu-kijiji tu..
Na hiyo ndiyo sababu mojawapo iliyowafanya watu wa miji ile wasimwogope Mungu, wamuone kuwa si kitu cha maana sana kwao, wakaanza kujiamulia kuishi tu kama wapendavyo kama wanyama, wanazini wao kwa wao jinsia moja, wanazini na wanyama. N.k.
Sasa Lutu yeye hakuangalia nyuma ya pazia kuna nini..Yeye maadamu anaona fursa, na maisha mazuri akaamua kuingia moja kwa moja, kumbe kama sio neema ya Mungu ndio ulikuwa mwisho wake..
Biblia inatuambia wazi kabisa kama ilivyokuwa katika siku za Lutu ndivyo itakavyokuja kuwa katika siku za kuja kwake mwana wa Adamu.. Wote tunajua jinsi dunia ya leo ilivyo tofauti sana ile ya zamani, ustaarabu uliopo leo hii ni mkubwa sana, utajiri uliopo duniani leo hauwezi kulinganishwa na ule uliokuwepo wakati ule, teknolojia, elimu, uchumi, miundombinu ni ya ajabu sana, kiasi kwamba ukimleta mtu wa karne ya 18 ukamuonyesha miji ya kisasa iliyopo duniani pamoja na teknolojia tulizonazo anaweza kusema huu sio ulimwengu wa wanadamu, bali ni kitu kingine…
Lakini mambo hayo mawili yanakwenda sambamba, “mafanikio pamoja na uovu vinashadiiana”.. Leo hii huoni jinsi ndoa za jinsia moja zinavyohalalishwa kila mahali mambo ambayo huko zamani hayakuwepo?, ndoa za wanyama na wanadamu, uzinzi sasahivi kila mahali mtu akiwa na simu ya mkononi tu, tayari anaufahamu uzinzi wote wa ulimwenguni..jambo ambalo hata sodoma halikuwepo, Mungu leo hii anatukanwa hadharani, ukipeleka habari za Mungu tu unaonekana kama mpinga-uhuru wa haki za kibinadamu, unaonekana kama mtu wa kale mwenye itikadi za kizamani.
Na wana wa Mungu wanapoona, mbona Mungu hachukui hatua yoyote dhidi yao, nao pia wanakwenda kujichanganya na maovu yao, ..Hawajui kuwa wanajiangamiza wao wenyewe bila kujua.
Kule Sodoma..Siku ya maangamizo ilipofika haikumaliza hata siku moja, mji ile ilikuwa imeshakuwa jivu yote..Vivyo hivyo na siku ya maangamizi ya huu ulimwengu ambayo ipo mbioni kutokea ambayo biblia ilishasema itakuja kwa ghafla sana, tena na cha kuogopesha zaidi itakuja katika kipindi cha amani,..soma.
1Wathesalonike 5:2 “Maana ninyi wenyewe mnajua yakini ya kuwa siku ya Bwana yaja kama vile mwivi ajavyo usiku. 3 Wakati wasemapo, Kuna amani na salama, ndipo uharibifu uwajiapo kwa ghafula, kama vile utungu umjiavyo mwenye mimba, wala hakika hawataokolewa”.
1Wathesalonike 5:2 “Maana ninyi wenyewe mnajua yakini ya kuwa siku ya Bwana yaja kama vile mwivi ajavyo usiku.
3 Wakati wasemapo, Kuna amani na salama, ndipo uharibifu uwajiapo kwa ghafula, kama vile utungu umjiavyo mwenye mimba, wala hakika hawataokolewa”.
Sasa kama na wewe upo katikati ya sodoma, usidhani itakuwa ni rahisi, kupona wakati huo ..
Mungu alishatuasa watoto wake tutoke huko, tujitenge nao mambo ya ulimwengu.. (Ufunuo 18:4)..Tusiyakaribia hata kidogo…Tutoke Sodoma wala tusiikaribie hata kidogo…Tukae nayo mbali sana maelfu ya Maili…Kumbuka sio tu Sodoma na Gomora pekee yake ndio ziliteketezwa wakati wa Nuhu..Biblia inasema hata ile miji iliyokuwa kando kando ya Sodoma na Gomora iliteketezwa pia (kasome Yuda 1:7)..Haikuwa na maasi kama Sodoma na Gomora..lakini kitendo tu cha kuwa karibu na miji hiyo tayari ilikuwa imeshanajisika nayo pia..Kadhalika leo..tunaaswa tukae mbali na uchafu wa dunia hii, wala tusifungwe nira na wasio amini kwa jinsi isivyo sawasawa. (2Wakorintho 6:14) ili nasi tusije tukachanganywa huko huko katika hasira ya Mungu.
1Yohana 2:15 “Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake. 16 Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na Baba, bali vyatokana na dunia. 17 Na dunia inapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu hata milele”.
1Yohana 2:15 “Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake.
16 Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na Baba, bali vyatokana na dunia.
17 Na dunia inapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu hata milele”.
Unaona? Ikiwa umeokoka halafu bado unapenda kwenda disko basi ujue upo Sodoma, umeokoka na bado unasikiliza miziki ya kidunia, unavaa nguo za kikahaba, vimini na masuruali, ujue unaishi sodoma bado..Na siku ile ya Unyakuo hutakwenda popote.. utabaki hapa chini ukingojea hukumu ya Mungu kulingana na Biblia.
Ni maombi yangu, hutachukuliwa na tamaa kama za Lutu, kwa kupenda mambo haya ya kitambo ya ulimwenguni, bali sote tutajitahidi tumtazame Kristo na mambo ya ufalme wa mbinguni, hadi siku ile ya ukombozi wetu utakapofika.
MTU ASIYE PAMOJA NAMI YU KINYUME CHANGU.
Kwanini wanawake wengi huwa wanalipuka mapepo?
JE ADAMU ALIKUWA NA KITOVU?
MAJINI WAZURI WAPO?
NI NINI KINAKUPATA UNAPOIPUUZIA INJILI?
INJILI YA MILELE NI IPI KATIKA BIBLIA?
MIILI YA UTUKUFU ITAKUWAJE?
SADAKA YA MALIMBUKO.
Ufisadi una maanisha nini katika biblia? (Ufisadi ni nini? Ni uwizi wa fedha nyingi au?)
JIBU: Neno ufisadi tofauti na linavyotafsiriwa siku hizi kwamba ni mtu anahujumu uchumi wa Taifa Fulani au shirika Fulani. Lakini katika biblia tafsiri yake ni tofauti.
Katika biblia neno fisadi limetumika kumtambulisha mtu mwenye tabia ya uzinzi na uasherati uliopindukia ambao hata haujali jinsia, umri wala maadili (unahusisha chochote kile ilimradi tu ni zinaa inafanyika)..Kwa lugha nyingine (ni ukahaba/umalaya mchafu). Hivyo popote pale katika biblia linapoonekana neno hili fahamu kuwa linamaanisha “ukahaba/ umalaya wa namna hiyo”.. Kwamfano tunaweza kusoma baadhi ya mistari michache inayozungumzia tendo hilo…
Waefeso 4:19 “ambao wakiisha kufa ganzi wanajitia katika mambo ya ufisadi wapate kufanyiza kila namna ya uchafu kwa kutamani”….. Waefeso 5:18 “Tena msilewe kwa mvinyo, ambamo mna ufisadi; bali mjazwe Roho;”…
Waefeso 4:19 “ambao wakiisha kufa ganzi wanajitia katika mambo ya ufisadi wapate kufanyiza kila namna ya uchafu kwa kutamani”…..
Waefeso 5:18 “Tena msilewe kwa mvinyo, ambamo mna ufisadi; bali mjazwe Roho;”…
Maana yake ni kuwa ulevi na ukahaba/Umalaya ni pacha, vinakwenda sambamba…
Mstari mwingine ni kama huu..
Tito 1:6“ ikiwa mtu hakushitakiwa neno, naye ni mume wa mke mmoja, ana watoto waaminio, wasioshitakiwa kuwa ni WAFISADI wala wasiotii. 7 Maana imempasa askofu awe mtu asiyeshitakiwa neno ,kwa kuwa ni wakili wa MUNGU;asiwe mtu wa kujipendeza nafsi yake,asiwe mwepesi wa hasira,asiwe mlevi wala mgomvi,asiwe mpenda mapato ya aibu”.
Tito 1:6“ ikiwa mtu hakushitakiwa neno, naye ni mume wa mke mmoja, ana watoto waaminio, wasioshitakiwa kuwa ni WAFISADI wala wasiotii.
7 Maana imempasa askofu awe mtu asiyeshitakiwa neno ,kwa kuwa ni wakili wa MUNGU;asiwe mtu wa kujipendeza nafsi yake,asiwe mwepesi wa hasira,asiwe mlevi wala mgomvi,asiwe mpenda mapato ya aibu”.
Maana yake ni kwamba Watoto wa Maaskofu pia hawapaswi kuwa Malaya wala makahaba wala kujihusisha na vitendo vyovyote vya zinaa. Wanapaswa wawe watakatifu katika mwenendo wao ili wawe kielelezo kwa kanisa la Mungu. Mtu yoyote anayetaka kazi ya uaskofu kama Watoto wake ni wachafu kwa viwango hivyo biblia inasema hastahili kuwa Askofu..anapaswa awageuze kwanza Watoto wake ndipo aweze kulichunga kundi la Mungu.
Pia Wagalatia 5:19 inasema… “Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, UFISADI.”.. Na 2Wakorintho 12:21 pia inasema…“Nami nitakapokuja tena, Mungu wangu asije akanidhili kwenu, nami nikawasikitikia wengi waliokosa tangu hapo, wasiutubie uchafu, na uasherati, na ufisadi walioufanya”…
1Petro 4:3 “ Maana wakati wa maisha yetu uliopita watosha kwa kutenda mapenzi ya Mataifa; kuenenda katika ufisadi, na tamaa, na ulevi, na karamu za ulafi, na vileo, na ibada ya sanamu isiyo halali; 4 mambo ambayo wao huona kuwa ni ajabu ya ninyi kutokwenda mbio pamoja nao katika UFISADI ule ule usio na kiasi, wakiwatukana”
1Petro 4:3 “ Maana wakati wa maisha yetu uliopita watosha kwa kutenda mapenzi ya Mataifa; kuenenda katika ufisadi, na tamaa, na ulevi, na karamu za ulafi, na vileo, na ibada ya sanamu isiyo halali;
4 mambo ambayo wao huona kuwa ni ajabu ya ninyi kutokwenda mbio pamoja nao katika UFISADI ule ule usio na kiasi, wakiwatukana”
Mistari mingine pia ni katika kitabu cha Petro…
2 Petro 2:6 “ tena akaihukumu miji ya Sodoma na Gomora, akiipindua na kuifanya majivu, akaifanya iwe ishara kwa watu watakaokuwa hawamchi Mungu baada ya haya; 7 akamwokoa Lutu, yule mwenye haki aliyehuzunishwa sana na mwenendo wa UFISADI WA HAO wahalifu”. Kama tunavyojua miji ya Sodoma na Gomora kiwango cha uasherati walichofikia..hata kuwatamani Malaika.
2 Petro 2:6 “ tena akaihukumu miji ya Sodoma na Gomora, akiipindua na kuifanya majivu, akaifanya iwe ishara kwa watu watakaokuwa hawamchi Mungu baada ya haya;
7 akamwokoa Lutu, yule mwenye haki aliyehuzunishwa sana na mwenendo wa UFISADI WA HAO wahalifu”. Kama tunavyojua miji ya Sodoma na Gomora kiwango cha uasherati walichofikia..hata kuwatamani Malaika.
Na mistari mingine mingi inazungumzia tendo hilo…Unaweza kupitia binafsi mistari ifuatayo..(Marko 7:22, Warumi 13:13, 2Petro 2:18, na Yuda 1:4).
Je! Swali linakuja….Mafisadi watakwenda mbinguni?..Jibu ni la! Kama biblia ilivyosema hapo juu…
Wagalatia 5:19 “Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, UFISADI, 20 ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, 21 husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, KATIKA HAYO NAWAAMBIA MAPEMA, KAMA NILIVYOKWISHA KUWAAMBIA, YA KWAMBA WATU WATENDAO MAMBO YA JINSI HIYO HAWATAURITHI UFALME WA MUNGU”.
Wagalatia 5:19 “Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, UFISADI,
20 ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi,
21 husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, KATIKA HAYO NAWAAMBIA MAPEMA, KAMA NILIVYOKWISHA KUWAAMBIA, YA KWAMBA WATU WATENDAO MAMBO YA JINSI HIYO HAWATAURITHI UFALME WA MUNGU”.
Unaona biblia imetuonya mapema kabisa kwamba watu wafanyayo hayo hawataurithi uzima wa milele?..Je ulevi ni suluhisho la kupunguza uzinzi na uasherati?..Jibu ni la! Kinyume chake Ndio kichochoe kikubwa cha ukahaba na umalaya huo(Ufisadi). Lakini Roho Mtakatifu ndiye jawabu la kuondoa tamaa ya uasherati na uzinzi.. kama Waefeso 5:18 inavyosema.. “Tena msilewe kwa mvinyo, ambamo mna ufisadi; bali mjazwe Roho;”…
Je umempokea Roho Mtakatifu?..ambaye ndiye msaada wetu wa kushinda dhambi? Kama bado unangoja nini?
Matendo 2:37 “Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu? 38 Petro akawaambia, TUBUNI MKABATIZWE KILA MMOJA KWA JINA LAKE YESU KRISTO, MPATE ONDOLEO LA DHAMBI ZENU, NANYI MTAPOKEA KIPAWA CHA ROHO MTAKATIFU. 39 Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie. 40 Akawashuhudia kwa maneno mengine mengi sana na kuwaonya, akisema, Jiokoeni na kizazi hiki chenye ukaidi. 41 Nao waliolipokea neno lake wakabatizwa; na siku ile wakaongezeka watu wapata elfu tatu”.
Matendo 2:37 “Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu?
38 Petro akawaambia, TUBUNI MKABATIZWE KILA MMOJA KWA JINA LAKE YESU KRISTO, MPATE ONDOLEO LA DHAMBI ZENU, NANYI MTAPOKEA KIPAWA CHA ROHO MTAKATIFU.
39 Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie.
40 Akawashuhudia kwa maneno mengine mengi sana na kuwaonya, akisema, Jiokoeni na kizazi hiki chenye ukaidi.
41 Nao waliolipokea neno lake wakabatizwa; na siku ile wakaongezeka watu wapata elfu tatu”.
Njia ya kumpokea huyo Roho Mtakatifu ndiyo hiyo hapo juu..Kutubu kwa kudhamiria kuacha dhambi na kwenda kubatizwa….Na wewe Tubu leo, ukabatizwe katika Jina la YESU na utapokea kipawa hicho cha Roho Mtakatifu, kwasababu Mungu sio mwongo, Naye atakupwa uwezo huo wa kuzishinda hizo tamaa mbaya.
Bwana akubariki sana.
JUMA LA SABINI (70) LA DANIELI
JE WAKRISTO TUNARUHUSIWA KUSHEHEREKEA VALENTINE’S DAY?
WINGU KUBWA LA MASHAHIDI.
NJIA SAHIHI YA KUFUNGA.
NJIA YA ‘UTAJIRI MKUU’ KWA KIJANA.
TUMAINI NI NINI?
TENZI ZA ROHONI