Title March 2020

UKADHANI YA KUWA MIMI NI KAMA WEWE.

Nakusalimu katika jina kuu la mwokozi wetu Yesu Kristo. Karibu tujifunze maneno ya uzima..

Kwanini mara nyingine tunakuwa ni wepesi kufanya dhambi, ni wepesi kuwasengenya majirani zetu, ni wepesi kwenda kuzini, licha ya kwamba tunasema tumeokoka, au tupo karibu na Mungu, lakini bado ni wepesi kutazama picha chafu mitandaoni na kufanya masturbationโ€ฆ.

Ni kwasababu tunamdhania Mungu yeye ni kama sisi, kwamba anaelewa tu! Ni madhaifu ya kawaida ya mwili..Na kibaya Zaidi pale tunapoona Mungu hachukui hatua yoyote ya adhabu katika ouvu tulioufanya, pengine pale tulipoenda kutazama picha chafu mitandaoni halafu Mungu akakaa kimya, halafu kesho yake tena tukarudia jambo hilo hilo na bado akawa yupo vilevile, hakuna lolote baya amelifanya katika Maisha yetu, kesho kutwa tena tukaenda kuzini, jambo likawa vilevile, kanisani tunahudhuria, kwaya tunaimba, maombi tunafanya, wala hakuna shida yoyote, wiki ijayo tukaanza kuwazungumizia vibaya majirani zetu, tulikuwa hatuli rushwa wala hututoi rushwa lakini tulipoanza kula rushwa na tukaona hakuna jambo lolote baya lililotukuta basi ndio ikawa desturi yetu kufanya hivyo, licha ya kuwa unasema ni mkristo.

Imekuwa hivyo hivyo miaka nenda miaka rudi, unawaza moyoni na kusema โ€œhata Mungu anaelewa mambo hayaโ€, ndio maana haniadhibu kwa lolote, Unadhani yeye ni kama wewe, Unadhani anavyowaza juu ya maovu ni kama wewe unavyowaza, unamchukulia kama mtu mwenzako asiyeweza kujali mambo madogo madogo kama hayo, unadhani kuwa hawezi kukuacha, wala kukuadhibu kwa vitu kama hivyo..

Lakini leo sikiliza Neno la Mungu linavyosema..

Zaburi 50:16 โ€œBali mtu asiye haki, Mungu amwambia, Una nini wewe kuitangaza sheria yangu, Na kuliweka agano langu kinywani mwako?

17 Maana wewe umechukia maonyo, Na kuyatupa maneno yangu nyuma yako.

18 Ulipomwona mwivi ulikuwa radhi naye, Ukashirikiana na wazinzi.

19 Umekiachia kinywa chako kinene mabaya, Na ulimi wako watunga hila.

20 Umekaa na kumsengenya ndugu yako, Na mwana wa mama yako umemsingizia.

21 NDIVYO ULIVYOFANYA, NAMI NIKANYAMAZA; UKADHANI YA KUWA MIMI NI KAMA WEWE. Walakini nitakukemea; Nitayapanga hayo mbele ya macho yako.

22 Yafahamuni hayo, Ninyi mnaomsahau Mungu, Nisije nikawararueni, Asipatikane mwenye kuwaponyaโ€

Angalia tena ule mstari wa 21 anasema.. โ€œNdivyo ulivyofanya, nami nikanyamaza; ukadhani ya kuwa mimi ni kama weweโ€โ€ฆUnaona, Mungu anapokaa kimya kutokana na dhambi zako unazozifanya kwa siri, usidhani yeye anakufurahia tu!.. Unasema umeokoka na huku unayo mambo yako ya siri ambayo unajua kabisa ni machukizo kwa Mungu, lakini Mungu hakusemeshi kwa lolote na wewe umestarehe tu, unadhani Mungu ni kama wewe, ataendelea na wewe hivyo siku zote..La! Anasema atakurarua na asipatikane mtu wa kukuponya..

Hasemi atakupiga tu, halafu basi au atakuadhibu, hapana anasema atakurarua..Na unajua anayerarua ni mnyama mkali kama vile simba, maana yake ni kuwa atakuharibu vibaya sana, kiasi cha kwamba hutaweza kusimama tena baada ya hapo, hata uombeweje, au uhubiriweje, hutaweza tena kusimamaโ€ฆNdio maana anasema hapo โ€œasipatikane mtu wa kukuponyaโ€

Na ujumbe huo Mungu anausema kwa wale wote wanaomsahau..Inamaanisha kuwa hapo mwanzo walishawahi kuwa wake, lakini wakamzoelea wakamwona kama yeye ni kama wao, wakawa hawaogopi tena kufanya dhambi mbele zake..

Ndugu ikiwa wewe ni mmojawapo, Basi wakati wako wa kutubu kwa kumaanisha ndio huu, pengine umebakisha kipindi kifupi sana kukumbana na makucha hayo ya Mungu (Usitafute kuujua upande wa pili wa ghadhabu ya Mungu, kwasababu inatisha sana).. Ikiwa unafanya dhambi kisirisiri za kujirudia rudia ambazo hazimpendezi Mungu, na umekuwa ukizifanya kwa muda mrefu sasa na Mungu amekaa kimya tu, ni heri usiendelee kuzifanya, kwasababu kwa kukaa kwake kimya hivyo usidhani yeye ni kama wewe..

Hivyo chukua hatua sasa ya kuuimarisha wokovu wako, na Mungu atakusamehe na kuiahirisha ghadhabu yake kwako.

Kumbuka hizi ni nyakati za mwisho, hakuna haja ya kuthibitishiwa tena kuwa tunaishi katika majira ya kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo, hali halisi yenyewe inaonekana kwa mambo yanayoendelea sasa hivi duniani, hivyo huu si wakati wa kuweka mguu mmoja kwa Kristo na mwingine nje, huu ni wakati wa kuzama moja kwa moja kwa Bwana, kwasababu UNYAKUO sasa ni wakati wowote.

2Petro 1:10 โ€œKwa hiyo ndugu, jitahidini zaidi kufanya imara kuitwa kwenu na uteule wenu; maana mkitenda hayo hamtajikwaa kamweโ€.

Bwana akubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312

jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >>ย WHATSAPP

Mada Nyinginezo:

JINSI NEEMA YA MUNGU ILIVYOKUWA KUBWA KWA MKE WA LUTU.

MUNGU WETU, JINSI LILIVYO TUKUFU JINA LAKO DUNIANI MWOTE!

ย 

KWANINI UNAPASWA UJIWEKE TAYARI SASA, KABLA YA ULE WAKATI KUFIKA?.

KWA VILE ALIVYOKUWA MTU WA HAKI.

KRISIMASI (CHRISTMAS) NI NINI? JE IPO KATIKA BIBLIA?

Mitume wote waliopita walikuwa ni watu weupe hata manabii wote waliopita hadi Ma-papa ni ngozi nyeupe. ni kweli ngozi nyeusi ililaaniwa ?

Rudi Nyumbani:

Print this post

PASAKA NI NINI? NA JE TUNARUHUSIWA KUSHEHEREKEA?

Pasaka ni nini kibiblia?, na je tunaruhusiwa kusheherekea pasaka sisi wakristo kama wayahudi?

Pasaka ni neno la Kiswahili ambalo limetokana na neno la kigiriki โ€œpaschaโ€ ambalo tafsiri yake kwa lugha ya kiingereza ni โ€œpassoverโ€ kwa Kiswahili  ni โ€œpita juuโ€. Hivyo pasaka kwa Kiswahili tunaweza kusema tafsiri yake ni โ€œpita juu au vuka upiteโ€.

Asili ya Neno hili ni siku ile wana wa Israeli walipokuwa wanatolewa kutoka Misri, usiku ule ambao ndio walikuwa wanatoka Misri, Bwana Mungu aliwaagiza wasitoke nyumba zao kwamba mpaka watakapomchinja yule Mwanakondoo na damu yake kuipaka katika miimo miwili ya Milangoโ€ฆili wakati yule malaika ambaye alitumwa kuwaangamiza wazaliwa wa kwanza wote wa wanadamu na wanyama waliokuwepo katika Misri nzima..atakapopita katika kila nyuma na kuiona damu hiyo ya mwanakondoo kwenye miimo ya mlango basi hataingia katika nyumba hiyo kumharibu mzaliwa wa kwanza wa nyumba hiyo โ€œATAVUKA JUU, AU ATAPITA JUUโ€ Kuendelea na nyumba nyingineโ€ฆna atakapofika katika nyumba nyingine na kukuta damu juu ya miimo ya mlango kama nyumba ya kwanza vile vile ATAPITA JUU na kuendelea mpaka atakapokuta nyumba ambazo hazina damu hiyo, ndipo ataingia na kuangamiza.

Kutoka 12:12 โ€œMaana nitapita kati ya nchi ya Misri usiku huo, nami nitawapiga wazaliwa wa kwanza wote katika nchi ya Misri, wa mwanadamu na wa mnyama; nami nitafanya hukumu juu ya miungu yote ya Misri; Mimi ndimi Bwana.

13 Na ile damu itakuwa ishara kwenu katika zile nyumba mtakazokuwamo; nami nitakapoiona ile damu, NITAPITA JUU YENU, lisiwapate pigo lo lote likawaharibu, nitakapoipiga nchi ya Misriโ€.

Hivyo hicho kitendo cha kuvuka na KUPITA JUU ndicho kinachoitwa Passover, kwa kigiriki Pascha, kwa Kiswahili PASAKA.

jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >>ย WHATSAPP

pasaka ni nini

Sasa katika Agano jipya damu ya mwanakondoo yule ndio inayofanananishwa na damu ya Bwana wetu Yesu Kristo, Sisi tuliokuwa dhambini tulipotolewa dhambini(yaani Misri yetu) na tunapoelekea nchi yetu ya ahadi mbinguniโ€ฆDamu ya Yesu ndiyo iliyotuokoa la laana ya Mungu dhidi ya watu wote walio katika dhambi..Na damu ya Yesu ni ishara ya Agano kwamba kwa kupitia damu yake tunalindwa na hukumu ya Mungu..Hukumu ya Mungu inapoachiliwa au itakapoachiliwa tutakuwa tumefunikwa chini ya damu ya Yesu na Malaika yule wa hukumu ATAPITA JUU YETU, na tutanusurika na hukumu ya Mungu.

Swali ni Je tunaruhusiwa kusheherekea pasaka kama watu wengine?

Tafsiri ya kusheherekea kibiblia ni tofauti na tafsiri ya kusheherekea kama inavyotafsiriwa na ulimwengu. Tafsiri ya sherehe kwa ulimwengu ni kula, na kunywa na kulewa, na kwenda kujiburudisha, kujifurahisha, kufanya uasherati, kujisisimua na kufanya anasa na kufanya kila aina ya mambo ya kimwili.

Lakini kibiblia tafsiri ya kusheherekea sio hiyoโ€ฆHata wayahudi wahakushehereka Pasaka kwa hivyoโ€ฆKibiblia, kusheherekea ni kujiweka katika ibada, na ibada sio kwenda kanisani tu..bali kujinyenyekeza na kujishusha chini ya uwepo wa Mungu, kwa kuomba, kusali, na kuzidi kujitakasa mbele zake huku tukikumbuka kuwa kwa tukio kama hili lililowahi kutokea miaka mingi iliyopita Bwana alitupa wokovu kwa kupitia damu yake pale Kalvari. Hivyo ni wakati wa kumwekea Bwana nadhiri,  wakati wa kuishiriki meza ya Bwana katika vigezo vya kimaandiko, ni wakati wa kusamehe Zaidi (sio kwamba sasa hatupaswi kusamehe mpaka siku ya pasaka ifike, hapana! tunasamehe kila siku, siku hiyo ikifika ni kumalizia tu kuvisafisha vile vidogo ambavyo tulikuwa hatujavimalizia), kwasababu utakatifu sio tu siku ya pasaka hapana bali kila siku!, siku hiyo ni kumalizia tu kuvisafisha vile vichache ambavyo vilikuwa vimesalia. Hivyo hiyo ndiyo tafsiri ya sherehe. Tukisheherekea kwa namna hiyo kuna amani fulani na furaha ya ajabu ambayo Mungu anaimimina ndani yetu..

Lakini tukishehereka kidunia kwamba ndio siku ya kutafuta kwenda disko, ndio siku ya kwenda kulewa, ndio siku ya kuvaa nguo za nusu-uchi na kutembea nazo barabarani, kwamba ndio siku ya kwenda kwenye dansi,  n.k..Tutakuwa tumejitafutia laana badala ya Baraka..Tutakuwa tumeshirikiana na shetani asilimia mia kuudhihaki na kuuzalilisha msalaba wa Kristo, na damu yake ya thamani. Hivyo tutakuwa tumejiharibia wenyewe. Lakini tukishehereka kibiblia tutapata baraka.

Bwana akubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312

(Pasaka ni nini)

Jiunge na kundi letu la mafundisho ya Biblia whatsapp kwa kubofya hapa > Group-whatsapp

Mada Nyinginezo

Je! kuna sikukuu za pasaka mbili? (Hesabu 9:11)

Easter ni nini?..Na je tunaruhusiwa kuisheherekea?

Ijumaa kuu ni nini? Na kwanini iitwe kuu?

KWA MIOYO YAO WAKAREJEA MISRI.

Je! Karamu za โ€˜Idiโ€™ ndio zipo hizo tunazozisoma katika Hosea (12:9)

Ni muda gani Bwana Yesu alisulibiwa. Je! Ni saa 3 au saa 6?

HAPANA MFUPA WAKE UTAKAOVUNJWA.

JE! UTATOA HESABU YA NINI KATIKA SIKU ILE?

Rudi Nyumbani:

Print this post

Biblia inamaanisha nini inaposema “Tusitweze unabii”?

SWALI: Nini maana yaย  โ€œTusitweze unabiiโ€?


JIBU: Tusome..

1Wathesalonike 5:19 โ€œMsimzimishe Roho;

20 msitweze unabii;

21 jaribuni mambo yote; lishikeni lililo jema;

22 jitengeni na ubaya wa kila namnaโ€.

Maana ya neno โ€œkutwezaโ€ ni kudharau au kupuuzia jambo fulaniโ€ฆHivyo biblia inaposema msitweze unabii maana yake ni โ€œmsiudharau/msiupuuzie unabiiโ€..Na unabii unaozungumziwa hapo ambao haupaswi kutwezwa (maana yake haupaswi kudharauliwa/kupuuziwa)..ni unabii wa kurudi kwa Bwana mara ya pili.. ambao Mtume Paulo aliwaonya Wakristo hao waliopo Thesalonike mwanzoni kabisa mwa sura hiyo ya tano(5). Tusome..

1 Wathesalonike 5:1 โ€œLakini, ndugu, kwa habari ya nyakati na majira, hamna haja niwaandikie.

2 Maana ninyi wenyewe mnajua yakini ya kuwa siku ya Bwana yaja kama vile mwivi ajavyo usiku.

3 Wakati wasemapo, Kuna amani na salama, ndipo uharibifu uwajiapo kwa ghafula, kama vile utungu umjiavyo mwenye mimba, wala hakika hawataokolewaโ€.

Huu ndio unabii wa kwanza ambao haupaswi kupuuziwa hata kidogo, na haukuandikwa kwa Wathesalonike tu peke yao, bali hata kwetu sisi, kwasababu ndio tunaoishi ukingoni mwa nyakati kabisa kuliko vizazi vyote vilivyotangulia. Ukisoma sura yote ya 5 hiyo ambayo ndio ya mwisho kabisa ya kitabu hicho cha 1Wathesalonike utaona jinsi biblia inavyotuonya kwa msisitizo mkubwa kujiweka tayari na siku hiyo ya kurudi kwa pili kwa Kristo, Kwamba siku hiyo inakuja kama mwivi na tusilale usingizi kama wengine walalavyo, na TUSIUUPUUZIE WALA KUUDHARAU HUO UNABIIโ€ฆKwasababu ni kweli siku hiyo yaja na Mungu hawezi kusema uongoโ€ฆwote wanaoudharau huo unabii siku hiyo itawajia kama mwivi na kutakuwa na maombolezo makubwa na majuto makubwa, watatamani warudishwe dakika tano nyuma warekebishe mambo yao, lakini itashindikana.

Na hautwezwi kwa midomo tu bali matendo piaโ€ฆMtu ambaye hajajiweka tayari kwa kumwamini Yesu Kristo na kutubu dhambi zake kwa kumaanisha kuziacha, na kuishi kulingana na Neno la Mungu, ingawa kila siku anasikia injili lakini anapuuzia mtu huyo ANAUTWEZA UNABII, hali kadhalika mtu ambaye kila siku anasikia habari za kurudi kwa Kristo mara ya pili na anadhihaki na kudharau na kuwaona wanaomgoja Bwana ni watu waliorukwa na akili, na wanaopoteza muda wao, au wamepoteza dira ya Maisha, huyu naye anafanya dhambi hiyo hiyo ya kuutweza unabii ambapo siku moja atajuta majuto makuu na hatapata nafasi ya kurekebisha mambo yake, na mambo hayo yatakuwa hivi karibuni, moja ya hizi siku hii dunia itakuwa si dunia tena..

Vilevile Na unabii mwingine wowote wa kwenye biblia sio wa kuudharau kabisa, kwasababu kila alilolisema Bwana lazima litatimia.

Hivyo kama hujaokoka, saaa wokovu ni sasa, sio baadaye wala kesho..Tubu sasa na Kristo atakusamehe bure kama alivyoahidi.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312

jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >>ย WHATSAPP

Mada Nyinginezo:

SIKU YA UNYAKUO ITAKUKUTAJE?

KUSUDI LA MIMI KUWEPO DUNIANI NI LIPI?

IELEWE SAUTI YA MUNGU.

MUNGU WETU, JINSI LILIVYO TUKUFU JINA LAKO DUNIANI MWOTE!

MAMBO MANNE,YANAYODHOOFISHA UOMBAJI WAKO.

Rudi Nyumbani:

Print this post

MWACHE YESU, NDIO AWE WA ย KWANZA KUKUHURUMIA.

Siku zote mwache Yesu, ndio awe waย  kwanza kukuhurumia!.

Nakusalimu katika jina kuu la Bwana wetu Yesu Kristo.

Ni jambo la kawaida kila mmoja wetu kuijali kwanza hali yake binafsi, na si dhambi kufanya hivyo, japo hilo halitufanyi tuonekane kuwa wa maana sana mbele za Mungu.. Kuna wakati Bwana Yesu aliitisha mkutano mkubwa sana, pengine eneo la mjini lilikuwa ni dogo la kuuketisha umati mkubwa wa watu, au pengine palikuwa na usumbufu fulani ambao ungewafanya watu wasimsikilize vizuri, Hivyo akaamua kuwaitisha eneo la mbali kidogo na mji, mahali ambapo hapana makazi ya watu, eneo la nyika tupu,..mahali ambapo hakuwaandalia mahema ya kukutania wala hakuwachagulia penye miti mingi, ambapo walau wangekaa chini yake wapate uvuli, bali alichagua eneo la jangwa lenye nyika tupu.

Na mkutano huo ulikuwa ni Mkutano wa siku tatu..

Lakini biblia inatuambia wengi waliposikia habari ile wakatoka mbali sana, wakaenda eneo hilo la jangwa ili kwenda kuyasikiliza maneno ya uzima ya Bwana Yesu,..Watu wale walifikia pengine asubuhi sana na mapema, wakijua kuwa siku zote tatu zitakuwa ni siku za kufunga, za kumsikiliza tu Bwana Yesu si vinginevyo, hivyo walifika mahali pale wakilijua hilo asubuhi sana, wakakaa chini kwenye jua lile, kuanzia asubuhi mpaka jioni,..

Jaribu kutengeneza picha, masaa 12 ya mchana wanamsikiliza tu Bwana Yesu akiwafundisha, na usiku vivyo hivyo.. siku ya kwanza, siku ya pili, mpaka sikuย  tatu zinakwisha, wamekaa tu pale, nyikani wakimsikiliza Bwana Yesu kwa makini bila kuondoa miguu yao, huku njaa zikiwauma, lakini waliona kile wanachokisikiliza ni Zaidi ya chakula cha mwilini.. Walijua mtu hawezi kuishi kwa mkate tu, bali kwa kila Neno linalotoka katika kinywa cha Bwana..

Embu tengeneza tena picha Bwana alikuwa anajua kabisa watu wale, walikuwa katika hali ngumu kweli kweli katika eneo lile la ukame na jua kali, alijua kabisa walikuwa hawajala kwa muda wa masaa mengi sana, alijua kabisa hali zao zinakaribia kuwa mbaya..lakini aliendelea kuwafundisha bila kuwahudumia kwa lolote, kwasababu aliona utayari wao wa kumsikiliza yeye bila kuchoka, mpaka siku tatu kamili zilipokwisha..

Lakini siku ile alipomaliza kuwafundisha, biblia inatuambia Bwana Yesu hakuwaacha hivi hivi waondoke waende zao katika hali zile za njaa bali aliona umaskini wao, aliona njaa zao, aliona mateso yako, aliona kiu yao, aliona mahitaji yao na pale pale ย maandiko yanatuambia AKAWAHURUMIA ..embu tusome:

Marko 8:1 โ€œKatika siku zile, kwa vile ulivyokuwa mkuu tena ule mkutano, nao wamekosa kitu cha kula, akawaita wanafunzi wake, akawaambia,

2ย  NAWAHURUMIA MKUTANO kwa sababu yapata siku tatu wamekaa nami, wala hawana kitu cha kula;

3ย  nami nikiwaaga waende zao nyumbani kwao hali wanafunga, watazimia njiani; na baadhi yao wametoka mbali.

4ย  Wanafunzi wake wakamjibu, Je! Ataweza wapi mtu kuwashibisha hawa mikate hapa nyikani?

5ย  Akawauliza, Mnayo mikate mingapi? Wakasema, Saba,

6ย  Akawaagiza mkutano waketi chini; akaitwaa ile mikate saba, akashukuru, akaimega, akawapa wanafunzi wake wawaandikie; wakawaandikia mkutano.

7ย  Walikuwa na visamaki vichache; akavibarikia, akasema wawaandikie na hivyo pia.

8 Wakala, wakashiba, wakakusanya mabaki ya vipande vya mikate makanda saba.

9ย  Na watu waliokula wapata elfu nne. Akawaagaโ€.

Unaona hapo?..Walipaswa waondoke vile vile, lakini kwa jinsi alivyoona โ€œWAMEKAA NAYEโ€ siku zote tatu bila kuondoka uweponi mwake, bila kwenda kuhangaika hangaika kuyajali maisha yao, familia zao, biashara zao, miradi yao, ili wapate chakula wao na Watoto wao, badala yake wamedumu pamoja naye kwa siku kadhaa bila kuchoka..basi tukio hilo lilimfanya Bwana Yesu AWAHURUMIE hata kwa yale mengine waliyoyakosa..

Na kama tunavyosoma kitu gani kilifuata.. Wote walishibishwa mikate wakiwa pale nyikani, wakapata na ya kuondokea, mpaka ikabaki na wale samaki vivyo hivyoโ€ฆSasa unaweza ukafikiri Bwana Yesu aliwashibisha pale tuโ€ฆLa! Alikuwa anawadhihirishia kuwa baada ya pale na Maisha yao pia yatabarikiwa kwa mfano ule ule wa vikapu, na wala hawatapungukiwa kabisaโ€ฆLakini hiyo yote ilikuwa ni kwasababu ya yale maneno ya uzima waliokuwa wanayasikia bila kuchoka ndio yakazaa vikapu vile vya mikate na baraka walizoziendea baada ya pale.

Na sisi tujiulize Je tunaweza kufikia hatua kama hii ya hawa watu?…Je tunaweza kuwa tayari kufunga kutokula kwa ajili tu ya kuutafuta uso wa Bwana kwa kipindi kirefu?, Je tunaweza Kufunga mihangaiko yetu, na shughuli zetu tukatenga wakati wa kuhudhuria ibada na semina ndefu za Neno la Mungu?..kwa kutokujali eneo lenyewe, kutokujali mazingira yanaruhusu kiasi gani, kutokujali umbali, kutokujali hata uzima wako na afya yako?.. Ikiwa tu tutaalikwa mahali ambapo tumewekewa mahema, chini kuna vivuli, lakini bado hatutakwenda ikiwa tunayo makanisa mazuri tena mengine yana feni lakini hatuwezi kukaa hata masaa 2, Je tutawezaje ikiwa tutalikwa mahali penye njika tupu kama pa hawa watu?..Na wakati huo huo bado tunataka Bwana Yesu azihurumie hali zetu,?

Mungu anatuambia tumkaribie yeye na yeye atatukaribia sisi (Yakoboย  4:8)..Hivyo tukiwa hatupo tayari kujinyima nafsi zetu na kujitesa katika kuutafuta uso wa Mungu kwa bidii, katika kuutafuta ufalme wake na haki yake, basi tujue itakuwa shida sana kuyaona matendo makuu ya Mungu maishani mwetu.

Usikazane kutafuta kujihurumia kwanza wewe unapoutafuta uso wa Mungu, subiri kwanza mwache Yesu akuhurumie yeye..jukumu letu ni kuutafuta uso wa Mungu kwa bidii mengine tumuachie yeye, kwasababu anajua shida zetu, na mahitaji kabla hata sisi hatujamwambia. (Mathayo 6:32).

Bwana atusaidie katika hilo. Na atujalie tuchukue hatua zinazostahili katika hilo.

Maran Atha.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312

jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >>ย WHATSAPP


Mada Nyinginezo:

MIILI YA UTUKUFU ITAKUWAJE?

USIWE NA HOFU, USHUKAPO CHINI.

MUNGU AKIKUPITA LEO, HAIMAANISHI KUWA HAJAKUCHAGUA.

MAMBO MANNE,YANAYODHOOFISHA UOMBAJI WAKO.

Je! Ni kweli ubatizo wa maji hatuuhitaji tena?

SAKRAMENTI NI NINI,ย NA JE! IPO KATIKA MAANDIKO?

Rudi Nyumbani:

Print this post

KUTAKUWA NA MATETEMEKO YA NCHI, NJAA NA TAUNI.

Kipindi kifupi kabla ya ghadhabu ya Mungu kumwagwa juu ya dunia, biblia imetabiri kuzuka kwa mambo ya ajabu sana na ya kutisha ulimwenguโ€ฆna mambo hayo yapo mengi ikiwemo kuzuka kwa manabii wa uongo na makristo wa uongo, lakini pamoja na hayo yapo mengine matatu ya muhimu, ambayo ni โ€ฆ1) VITA 2) TAUNI na 3) NJAA.

Luka 21:10 โ€œKisha aliwaambia, Taifa litaondoka kupigana na taifa, na ufalme kupigana na ufalme; 11 kutakuwa na MATETEMEKO MAKUBWA YA NCHI; NA NJAA NA TAUNI mahali mahali; na mambo ya kutisha na ishara kuu kutoka mbinguniโ€.

Kama tujuavyo mgonjwa kabla hajaanza kuumwa anakuwa anaanza kuonyesha dalili kwanza, labda ataanza kusikia kichefuchefu na baadaye akawa sawa, muda kidogo atasikia kichwa kinamuuma lakini si sana..na baadaye tena homa lakini si sana..kiasi kwamba anaweza akazivumilia dalili zile na kuendelea na shughuli zake kipindi cha mwanzoni..na wakati mwingine hata akajisikia nafuu kabisa kana kwamba haumwi tenaโ€ฆ.

Lakini siku ikifika yenyewe ambapo ugonjwa ule utanyanyuka..huo ndio wakati ambao kila siku kwake itakuwa ni afadhali na jana kuliko leoโ€ฆzile dalili alizokuwa anazisikia mwanzo, kama kichwa kuumwa kidogo, homa kidogo, sasa vinazidi na kujizidisha na kuwa vikali mara nyingi zaidi..hapo atasikia kichwa kikiumwa hata mara kumi ya kile alichokuwa anakisikia hapo mwanzo..Homa inajizidisha mara nyingi kuliko mwanzo na mara nyingine anajikuta anaishia tu kalala kitandani. Mtu anapofikia hali ya kuumwa kiwango hiki huwa anatamani hata afe atokane na mateso hayo.

Sasa mambo hayo yanafananishwa na siku za maangamizi ya dunia zitakavyokuwa โ€ฆWengi wetu hatujui nini maana ya dalili ya siku za mwishoโ€ฆDalili maana yake ni mwanzo wa kituโ€ฆHivyo biblia inavyosema kuwa dalili za siku za mwisho ni hizi au zile, inamaanisha kuwa mwisho wa siku mambo yatakuwa ni mabaya kuliko hata mwanzo.

Sasa Bwana Yesu alisema dalili mojawapo ya siku za mwisho ni kuwepo kwa matetemeko makubwa ya nchi(Luka 21:11)โ€ฆmaana yake ni kwamba siku yenyewe ya mwisho wa dunia ikifika kutakuwepo na tetemeko kubwa lisiloelezeka mara nyingi zaidi ya yale ya dalili..

Kadhalika Bwana Yesu alivyosema kwamba vita ni dalili mojawapo ya siku za mwisho, maana yake ni kwamba Siku yenyewe ya mwisho wa dunia ikifika kutakuwa na vita kubwa na kali na ya ajabu ambayo haijawahi kutokea, ambayo madhara yake hayajawahi kufananishwa na vita yoyote huko nyuma..na vita hiyo itakuwa si nyingine zaidi ya vita vya Har -magedoni.Kama hizi vita zilizopo sasa tumezoea kusikia watu elfu kadhaa wamekufa..vita hiyo ya mwisho ya Harmagedoni itamaliza mamilioni ya watu.

Pia alisema dalili nyingine ni NJAA, na njaa hiyo inasababishwa na kukosekana kwa mvua na kunyanyuka kwa wadudu wanaoharibu mazao kama nzige waliotokea wakati wa Farao, na waliopo sasa..Siku ya kuharibiwa dunia Itatokea Njaa ambayo haijawahi kuwa mfano wakeโ€ฆBaada ya watu kuifurahia chapa ya mnyama kwa kitambo..Mungu ataipiga dunia nzima kwa njaa..ambapo maji yote yatageuka kuwa damu na mifereji na mito..na mvua itaacha kunyesha(Ufunuo 16:4-6).

Kadhalika Bwana Yesu alisema dalili nyingine ya siku za mwisho ni KUZUKA KWA MAGONJWA MABAYA ambayo yanafanishwa na Tauni kibiblia(Luka 21:11)...magonjwa hayo yatakuwa hayana tiba na yanayoambukiza kwa kasiโ€ฆDalili za magonjwa hayo zimeanza kuonekana tangu mwanzo mwa karne ya 21, na mpaka kufikia sasa yameshaongezeka idadi..Kama ijulikanavyo kuna ugonjwa sasa unaoitwa Corona ulimwenguni.. Ugonjwa huu ni dalili tu (mwanzo wa utungu)..ambapo siku yenyewe ya mwisho ikifika ambayo inaweza kuwa hata leo..utazuka ugonjwa mpya ambao utakuwa ni mbaya kuliko huu uliopo sasaโ€ฆutakuwa ni ugonjwa wa virusi mfano wa huu wa sasaโ€ฆ

Ugonjwa huu utashambulia ngozi na kusababisha majipu ya vidonda ambavyo vinaoza(Biblia inasema majipu yake yatakuwa ni mabovu, maana yake ni ya kuoza) na utakuwa unateseka kwa muda mrefu..Utakuwa ni tofauti na huu uliopo sasa ambao baada ya siku kadhaa mtu anaweza kuponaโ€ฆugonjwa huo wa majipu utakuwa hauna tiba na wala hautakuwa unapona wenyewe, utampata kila mtu ambaye atakuwepo ulimwenguni wakati huoโ€ฆ

Ufunuo 16: 2 โ€œAkaenda huyo wa kwanza, akakimimina kitasa chake juu ya nchi; pakawa na jipu baya, bovu, juu ya wale watu wenye chapa ya huyo mnyama, na wale wenye kuisujudia sanamu yakeโ€.

Mambo haya sio hadithi bali ni mambo ambayo yatakuja kutokea dhahiri kabisa. Siku za ugonjwa huo jua litashushwa pia na kuwaunguza wanadamu wote wenye ugonjwa huo, duniani kutakuwa sio sehemu ya kuishi tena..kila mtu atakuwa kivyake akiugulia na kuteseka kivyake vyake kutakuwa hakuna hospitali itakayopokea wagonjwa kwasababu hata wauguzi wenyewe watakuwa na ugonjwa huo..(Hiyo itakuwa sio siku za dalili tena bali ya ugonjwa wenyewe, dalili ni wakati huu wa sasa).. Unyakuo upo karibu sana kutokea!..Kwasababu kabla ya siku hizo..watakatifu watanyakuliwa kwanza.

Ishara za magonjwa haya ni kutuonyesha kuwa Hukumu tayari imeshatamkwa juu ya ulimwengu..kama vile ambavyo ugonjwa unavyomwingia mtu..na hatua za kwanza ni dalili..na sasa tupo katika dalili ya ghadhabu ya Mungu. Hii hofu iliyopo sasa si hofu, hofu hasaa itakuja wakati huo wa mapigo hayo ya Mungu.

Ni nini kifanyike sasa? Katika hatua hii ya dalili?

Kinachopaswa kufanyika sasa ni kujiweka tayari tuโ€ฆTunajiwekaje tayari?..ni kwa kutubu, kujiosha mioyo yetu, kuacha dhambi na kuzidi kujitenga na ulimwengu kila sikuโ€ฆ Kuacha kuziabudu sanamu na kuzisujudia , Kuacha ulevi, kuacha rushwa, kuacha wizi, kuacha matusi, kuacha kutazama picha za ngono, uasherati, kuacha kwenda ma disko, kuacha kuvaa nguo za kuonyesha maungo, na vimini na suruali kwa wanawakeโ€ฆ.mambo haya ndiyo yanayoisukuma ghadhabu ya Mungu imwagike haraka ulimwenguni na juu yako wewe..ni kama mgonjwa ambaye tayari kashaanza kuonyesha dalili, halafu bado hazingatii tiba..pasipo kujua kuwa ndio anazidi kujiharibu na kuuvuta ugonjwa zaidi..

Wakolosai 3: 5 โ€œBasi, vifisheni viungo vyenu vilivyo katika nchi, uasherati, uchafu, tamaa mbaya, mawazo mabaya, na kutamani, ndiyo ibada ya sanamu; 6 kwa ajili ya mambo hayo huja ghadhabu ya Munguโ€.

Umeona mstari wa 6, usemavyo?… โ€œkwa ajili ya mambo hayo huja ghadhabu ya Munguโ€..Soma tena..

Waefeso 5:5 โ€œMaana neno hili mnalijua hakika, ya kwamba hakuna mwasherati wala mchafu wala mwenye tamaa, ndiye mwabudu sanamu, aliye na urithi katika ufalme wa Kristo na Mungu.

6 Mtu asiwadanganye kwa maneno yasiyo na maana; kwa kuwa kwa sababu ya hayo hasira ya Mungu huwajia wana wa uasiโ€.

Unaona tena? mstari wa mwisho huo wa 6.. โ€œkwa kuwa kwa sababu ya hayo hasira ya Mungu huwajia wana wa uasiโ€

Hiyo pekee ndiyo njia ya kujikinga na kujiepusha na ghadhabu ya Munguโ€ฆ

Utauliza kutokana na tatizo hili lililopo sasaโ€ฆje ! ni sahihi kunawa mikono na kutosalimiana na mtu kwa kushikana mikono njiani?

Kama tunavyoambiwa ni wajibu wa kila mtu kusimama pindi wimbo wa Taifa unapoimbwaโ€ฆna wakristo pia wanatii agizo hilo..Hivyo na agizo la kunawa mikono popote tufikapo, tuingiapo na tutokapo wakristo tunatii bila shuruti kwasababu hakutupunguzii chochote katika Imani yetuโ€ฆTukijua ya kwamba mioyo yetu tayari imeoshwa kwa sabuni ya kimbinguni (Damu ya Yesu)..Na tumaini letu halipo katika maji na sabuni za mwilini bali katika maji na damu ya Yesu Kristo. Hiyo ndiyo inayotutakasa na kutulinda na kutuepusha na ghadhabu ya Mungu. Hivyo hatuna hofu, na hatuogopi kwasababu tunamtegemea Bwana, wakati ulimwengu unaogopa magonjwa, na njaa na vita sasaโ€ฆsisi tunaigopa dhambi tu!..

Zaburi 125:1 โ€œWamtumainio Bwana ni kama mlima Sayuni, Ambao hautatikisika, wakaa milele.

2 Kama milima inavyouzunguka Yerusalemu, Ndivyo Bwana anavyowazunguka watu wake, Tangu sasa na hata mileleโ€.

Lakini kama tukinawa mikono na mwili mzima mahali popote tuingiapo na tutokapo na huku mioyoni mwetu bado kuna uasherati, bado kuna wivu, hasira, wizi, ufisadi, ibada za sanamu, rushwa, na ulevi hakuna chochote tunachoweza kuepukaโ€ฆMaji na sabuni na mlo kamili kamwe haviwezi kutuepusha na ghadhabu ya Munguโ€ฆHavijawahi katika agano la kale na hata katika agano jipya.

Hivyo kwa hitimisho kama hujampa Yesu Kristo maisha yako, Hizi ni siku za mwisho..huhitaji kuhadithiwa na mtu tena..leo hii ile mipira uliyokuwa unajitumainisha nayo kuwa itakupatia faraja iko wapi? Kule kubet ulikokuwa unajitumainisha nako kuko wapi?…Zile visa na zile biashara zako ambazo ulikuwa unajitumainisha nazo unazifanya ulimwenguni kote ziko wapo leo?, elimu unayojitumainia iko wapi?, disko unayojitumainishia nayo iko wapi? Katika mataifa makubwa zimeshafungwa labda na kwako inaweza kuwa hivyo siku sio nyingi, wale waliokuwa wanakuambia kwamba dunia haitafikia mwisho wako wapi leo?..Uliwahi kufikiri kwamba ingetokea siku moja miji mikubwa mikubwa ingekosa watu barabarani?, mashule mengi ulimwenguni yangefungwa?,

umewahi kutafakari kwamba siku moja ingefika mamilioni ya watu hawataruhusiwa kwenda kazini wala makanisani?..Naam Hali inaweza kurudi kama kawaida na maisha yakarudi kama mwanzo na hata zaidi ya pale..lakini je! Umejifunza nini?…bado upo tu nje ya safina?

Huu ni mwanzo tu kwamba tutubu kwasababu siku yenyeweโ€ฆ ikifika hata hii Neema ya kutubu na ya kusikia mahubiri haitakuwepo?….Siku yenyewe ikifika itakuwa haiwezekani kabisa hata kwenda kanisani, licha ya kutafuta mtu wa kukuhubiria, hata kwa njia ya mitandao halitapatikanaโ€ฆwanaohusika na mitandao watakuwa matatizoni, vituo vya satellite vyote vitafungwaโ€ฆChapa ya mnyama itakuwa inafanya kazi na kipindi kifupi baada ya kuipokea chapa hiyo magonjwa hayo yataanza..

Yeremia 28:7 โ€œLakini lisikilize sasa neno hili nilisemalo, masikioni mwako, na masikioni mwa watu wote, 8 Manabii waliokuwako kabla ya zamani zangu, na zamani zako, walitabiri juu ya nchi nyingi, na juu ya falme kubwa, habari ya vita, na ya mabaya, na ya tauniโ€.

Kabla ya dunia kufikia maharibifu hayo..waliokuwa ndani ya Kristo watakuwa wamenyakuliwa je utakuwa miongoni mwao?..

Kama hujatubu..Na upo tayari kufanya hivyo leo hii, Basi uamuzi unaoufanya ni wa busara sana ambao hautakaa uujutie maisha yako yote kama ilivyokuwa hata kwetu sisi. Unachopaswa kufanya, hapo ulipo, chukua muda mchache ujitenge peke yako. Kisha piga magoti, kisha fuatisha sala hii kwa Imani, ukijua kuwa Mungu yupo hapo karibu na wewe pembeni yako kukusikia..Kisha ukiwa sasa katika utulivu Sema sala hii kwa sauti.

EE MUNGU BABA, NAJA MBELE ZAKO, NIKIWA NINAJITAMBUA KUWA MIMI NI MKOSAJI NA NIMEKUTENDA DHAMBI NYINGI, NA KWAMBA NIMESTAHILI HUKUMU. LAKINI WEWE MUNGU WANGU ULISEMA KATIKA NENO LAKO KUWA WEWE NI MUNGU WA REHEMA UNAYEWAREHEMU MAELFU ELFU YA WATU WANAOKUPENDA WEWE. NA LEO HII NINAKUJA MBELE ZAKO NAHITAJI MSAMAHA WAKO NA MSAADA WAKO MUNGU WANGU, NINATUBU DHAMBI ZANGU ZOTE KWA KUMAANISHA NA KWA MOYO WANGU WOTE, . NINAKIRI KUWA YESU KRISTO NI BWANA, NA YEYE NDIYE MWOKOZI WA HUU ULIMWENGUNI. HIVYO NAOMBA DAMU YA MWANAO TAKATIFU INISAFISHE UOVU WANGU WOTE SASA NIFANYIKE KUWA KIUMBE KIPYA KUANZIA LEO NA HATA MILELE.

ASANTE BWANA YESU KWA KUNIPOKEA NA KUNISAMEHE.

AMEN.

Sasa ikiwa umefuatisha sala hiyo kwa Imani ..Hatua iliyobakia kwako ni kuithitisha toba yako kwa Vitendo ikiwa ulikuwa unafanya mambo yote ambayo hayampendezi Mungu unayaacha na kujitenga nayo, Sasa Mungu akishaona umegeuka kwa vitendo basi toba yako anaipokea na atakuja ndani yako wakati huo huo na kufanya makao ya milele kwako. Vile vile unahitaji, kutafuta kanisa la kiroho ambalo utajumuika na wakristo wengine katika kumwambudu Mungu, na kujifunza biblia ili uukulie wokovu. Na vilevile ili upate ubatizo sahihi wa kuzamishwa katika maji Mengi na kwa jina la YESU KRISTO kwa ajili ya ondoleo la dhambi zako.

jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >>ย WHATSAPP

Mada Nyinginezo:

MAPIGO YA VITASA SABA, NA SIKU YA BWANA.

UFUNUO: Mlango wa 16.

NENO NI LILE LILE, LAKINI UJUMBE NI TOFAUTI.

MWISHO WA DUNIA UTAKUJAJE?

KWANINI UNAPASWA UJIWEKE TAYARI SASA, KABLA YA ULE WAKATI KUFIKA?.

Rudi Nyumbaani:

Print this post

MUNGU WETU, JINSI LILIVYO TUKUFU JINA LAKO DUNIANI MWOTE!

Jambo mojawapo ambalo lilikuwa linamfanya Daudi asichoke kumsifu Mungu, ni vile alivyokuwa anajijengea mazoea ya kuutafakari ukuu wake kila mahali alipokuwepo.. Daudi alikuwa akizitazama mbingu sana, akiangalia jinsi nyota na mwezi vilivyowekwa angani na Mungu kwa namna ya ajabu na ya kushangaza..

Nakuambia kuna raha na changamko fulani la kipekee linaingia ndani yako, pale unapotenga muda wako mrefu kutafakari kazi za Mungu hususani vitu vya asili kama vile mbingu, na milima, na mabonde na mito na bahariโ€ฆ.

Zaburi 8:1 โ€œWewe, MUNGU, Bwana wetu Jinsi lilivyo tukufu jina lako duniani mwote! Wewe umeuweka utukufu wako mbinguni; โ€ฆ.

3 Nikiziangalia mbingu zako, kazi ya vidole vyako, Mwezi na nyota ulizoziratibisha;โ€

Wakati mwingine tunajiuliza watu kama hao ambao hawakuwa na Darubini (Telescope) ya kuangalia magimba yaliyo mbali sana na dunia, lakini walimsifu Mungu kwa namna ile na kumfurahia, Je! Wangekuwepo katika wakati wetu huu, wangemsifu Mungu kwa jinsi gani?..Kwasababu ule wakati wao macho yao yaliishia kuona nyota tu za hapo angali, lakini sisi tunaishi katika kipindi cha teknolojia ya hali ya juu ndio tunaojua kuwa hata hizi nyota na hili jua, na huu mwezi, ni vitu vidogo sana ukilinganishaย  na matrilioni na magimba mengine Mungu aliyoyaumba huko angani.. kwa ufupi ni kwamba kila kitu unachokiona angani, ikiwemo na hizo nyota zote, ni sawa na chembe moja ya mchanga katika michanga yote iliyopo baharini..Sasa embu jiulizeย  huyu ni Mungu wa namna gani, kaumba vitu vingapi tusivyovijua sisi kwa akili zetu?

Na sisi pia, ila sifa zetu ziwe na nguvu, tutoke nje tuutazame ukuu wa Mungu, tuutafakari sana, tutenge hata muda tuziangalie mbingu sana. Sio kila siku usiku na mchana tu tunakuwa bize tu na shughuli zetu, halafu jumapili ndio tunakwenda kumsifu Mungu kanisani..Ni lipi litakalotufanya tumsifu yeye kwa kumaanisha kabisa?..Wakati mwingine si tutakuwa tunafanya hivyo kinafki?…

Vile vile tutafakari jinsi alivyoviumba viumbe vyake mbali mbali, ili tujue kuwa haja bahatisha kutuumba na sisi jinsi tulivyo, Tutafakariย  kwanini amuumbe mnyama mmoja na shingo ndefu, lakini mwingine amnyime lakini wote wakawa wanaishi bila shida yoyote, kwanini mwingine ampe miguu mingi (kama jongoo) lakini mwingine asimpe kabisa miguu (mfano nyoka), lakiniย  Yule asiye na miguu akawa na mbio, tena sana kuliko Yule mwenye miguu mingiโ€ฆKwanini mwingine amempa mbawa akawa anaruka na kupaa juu sana (Tai), na mwingine akampaย  mbawa kama hizo hizo lakini hawezi kuruka(kuku) akionyesha kuwa kupewa mbawa sio kigezo cha wewe kuruka,

Tujiulize kwanini mwingine amepewaย  meno lakini hawezi kula mifupa (ngโ€™ombe) lakini mwingine hana meno na mwororo lakini chakula chake ni mifupa (konokono) kwanini mwingine hana mdomo unaofanana na binadama kama vile nyani, lakini mwingine mwenye mdomo wa ndege lakini hata haukaribiani na mtu, lakini anao uwezo wa kuiga lugha ya mwanadamu ukadhani ni mtu anazungumza kumbe ni ndege (kasuku)..Kuonyesha kuwa sio wepesi wa ulimi ndio unamfanya mtu azungumze, bali ni kujaliwa tu, bubu hana matatizo yoyote katika ulimi wake, lakini ni Mungu ndiye alimfanya awe vile. N.k n.k

Tukiyatafakari hayo na mengine mengi tutaona mambo ya Mungu jinsi yalivyo mengi..Na tutakuwa na amani na kumshukuru Mungu kwa jinsi alivyotuumba.. Vile vile hapo ndipo tutakapojua kuwa kumbe Mungu hategemei bidii zetu kutunyanyua au kutushusha, hategemei mpaka tupate elimu ndio atufikishe mahali Fulani, hatagemei mpaka tuwe na miguu miwili, au mikono miwili ndio atupigishe hatua nyingineโ€ฆBali ni kwa neemaย  zake tu..

Hivyo ni jukumu letu sote kumsifu Mungu wetu, daima, kwa mambo yake ya ajabu, na uumbaji wake. Na huko ndipo tutakapomwona katika maisha yetu.

ZABURI 150

1 Haleluya. Msifuni Mungu katika patakatifu pake; Msifuni katika anga la uweza wake.

2 Msifuni kwa matendo yake makuu; Msifuni kwa kadiri ya wingi wa ukuu wake.

3 Msifuni kwa mvumo wa baragumu; Msifuni kwa kinanda na kinubi;

4 Msifuni kwa matari na kucheza; Msifuni kwa zeze na filimbi;

5 Msifuni kwa matoazi yaliayo; Msifuni kwa matoazi yavumayo sana.

6 Kila mwenye pumzi na amsifu Bwana. Haleluya.

Bwana akubariki.

Tafadhali โ€œShareโ€ na kwa wengine.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312

jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >>ย WHATSAPP


Mada Nyinginezo:

JINSI MUNGU ANAVYOIPIGA NA KUIPONYA AFRIKA.

Je! Ni halali kuoa/kuolewa na mtu ambaye tayari anao watoto?

KAMA MHUBIRI NI WOKOVU UPI UNAUPELEKA KWA WATU?

JE! MUNGU NI NANI?

LOLOTE ATAKALOWAAMBIA FANYENI.

Rudi Nyumbani:

Print this post

KWANINI YESU KRISTO NI WA MUHIMU KWETU SASA?

Kwanini yesu kristo ni wa muhimu kwetu?

Moja ya majukumu tuliyonayo ni โ€œKumfahamu sana Yesu Kristoโ€..Hili ni moja ya jukumu kubwa sana tulilonalo kwasababu ndio msingi wa ukombozi wetu..Tusipomfahamu Yesu kwa mapana na marefu basi ni ngumu kujua nafasi zetu pamoja na Neema tuliyopewaโ€ฆNa matokeo ya kutomwelewa Yesu ni kuishia kuidharau neema na kupotea.

Sasa jukumu la kumjua Yesu, sio kujua sura yake alikuwa ni mzuri  kiasi gani, au alikuwa na rangi gani, au alikuwa na nywele za namna gani, au alikuwa anapenda kula nini?..Hapana hilo sio jukumu tulilopewa la kumfahamu kwa namna hiyo..Jukumu tulilopewa ni KUIFAHAMU VIZURI ILE NAFASI ALIYONAYO. Tukishaifahamu ile nafasi basi tutamjua Mungu sana. Na mpaka sasa hakuna aliyefikia kikomo cha kuijua hiyo nafasi yote..bali kwa siku zinavyozidi kwenda tunazidi kuilewa na ndivyo tunavyozidi kumpenda Mungu na kumheshimu.

Waefeso 4:13 โ€œhata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristoโ€

Leo tujikumbushe ni kwa namna gani kifo cha Yesu kilivyokuwa na umuhimu kwetu sisi tuliokuwa tumepotea kwenye dhambi.

Katika Biblia tunasoma muda mfupi kabla ya Bwana Yesu kupandishwa msalabani..Pilato aliwafungulia mfungwa mmoja ambaye alikuwa ni mkatili katika mji ule..Na huyo si mwingine Zaidi ya BARABA.

Huyu Baraba alikuwa na Kesi ya mauaji ya watu kadhaa hapo mjini, na alikuwa ni mkatili..Biblia inamwita โ€œmfungwa mashuhuriโ€ (Mathayo 27:16). Watu wote walimshuhudia kuwa alikuwa ni mkatili, hivyo walikuwa hawamhitaji hata kidogo, hivyo alikamatwa na warumi na kutiwa gerezani akisubiria hukumu yake ipite..Na bila shaka angeuawa kifo cha kikatili kuliko mtu mwingine yoyote yule, kwasababu kila mtu alikuwa amemkinai. Na alivyokuwa kule gerezani kila mtu pamoja na yeye mwenyewe alikuwa anajua ndiye anayestahili adhabu kubwa kuliko wote. Kulikuwa hakuna uwezekano wa kupona hata kidogoโ€ฆLakini kama wasemavyo watu โ€œhata mnyororo ulio imara sana, lazima utakuwa na sehemu yake dhaifuโ€..Hata kama sehemu inaonekana hakuna njia basi Mungu anaweza kufanya njia.

Baraba akiwa mule gerezani labda moyo wake ukaanza kumchoma na kujihisi alifanya makosa, aliua wale watu pasipo hatia, akitazama pembeni anajua kuna mtu aliua tu mtu mmoja na alihukumiwa kukatwa kichwa yeye akijiangalia kashaangusha watu kadhaa huko nyuma hukumu yake itakuwaje?โ€ฆ

Siku moja tu asubuhi alishangaa anaitwa nje, atoke gerezani..na alipotoka akijua anakwenda kuuawa na pengine wafungwa wote wakajua anakwenda kumalizwa kwa hasira nyingi..ghafla anatoka nje anaona watu wengi wanamshangilia nje, wanafurahi kufunguliwa kwake..anaona wanampigia mpaka vigelegele, Baraba afunguliwe! Baraba afunguliwe!… kwa pembeni anamwona Pilato anamwambia kuanzia leo upo huru kama watu wengine, rudi nyumbani kwako kafurahi na mke wako na Watoto wako, upo huru..Wakati anashangaa jambo hilo linawezekanaje labda walikosea wanamaanisha Baraba mwingineโ€ฆ. kwa pembeni kidogo anaona mtu amewekwa taji la miiba kichwani kakaa kimya sana, mpole kama mwanakondoo anayekaribia kuchinjwaโ€ฆ.Pilato anamwambia Yule kabeba hukumu yakoโ€ฆYule atakufa kwa niaba yakoโ€ฆNi wazi bila shaka alishangaa kidogo..

Naamini Maisha yake yalianza kubadilika kuanzia pale na kuendeleaโ€ฆKwasababu alijua chanzo cha uzima wake na uhuru wake ni nini?..kwamba kama si Yesu kuwa vile alivyokuwa, kufanyiwa yale aliyofanyiwa, kama sio Yesu kukataliwa yeye angekufaโ€ฆkwasababu kama Yesu angekubaliwa basi yeye asingeponaโ€ฆHivyo kwa kupingwa na kupigwa kbbwake Yesu yeye amepona!.

Je mtu wa namna hiyo atarudia tena kuua?, atamkebehi YESU?, Ataudharau msalaba? Atajisifu?…Na je mfano akiudharau msalaba na kutoka pale na kuendelea na mauaji yake unahisi ni nini kitampata mbele za Mungu na watu?

Hiyo ndiyo nafasi ya Yesu kwetu ilivyoโ€ฆ Baraba ni mfano wa mimi na weweโ€ฆSasa ni kwa namna gani Bwana Yesu anachukua dhambi zetu?..Sio kwa kubeba kifurushi na kukiweka mabegani kwakeโ€ฆHapana ilimgharimu Maisha yakeโ€ฆilimgharimu kukataliwa, kupingwa, kutemewa mate, kutukanwa, kudhihakiwa..Kwajinsi alivyodhihakiwa sana na kutukanwa sana ndipo thamani ya Baraba kule gerezani ilivyokuwa inazidi kupanda. Hadhi ya Bwana Yesu ilishuka ili yetu ipande.

Wakati Baraba yupo kule gerezani alikuwa hajui kama Kristo anatukanwa huko nje kwaajili yake.

Ndugu yanguโ€ฆMsalaba sio jambo la kupuuzia au kuchezea hata kidogoโ€ฆMambo yote mema unayoyapata leo hii ni kwasababu ya Yesu Kristo, kama sio yeye dunia ingeshaisha siku nyingiโ€ฆMungu angeshaimaliza dunia kwa laana kitambo sanaโ€ฆMaisha yangeshaisha miaka mingi sana iliyopita huko nyuma.

Watu wengi hawajui kuwa wanapiganiwa na Mungu pasipo hata wao kumwomba Mungu, wengi hawajui hata katika uasherati wao ni Mungu ndiye anayewapa riziki pasipo hata wao kumwomba, na hawajui ni hiyo neema, ni kwasababu ya YESU KRISTO. Kama sio Yesu kuteseka miaka 2020 iliyopita hakuna mwasherati ambaye mpaka leo angekuwa anaishi..Wote tulistahili kufa.

Lakini Neema hii unaichezea..unadhani ni haki yako kuishi na usherati wako, uwizi wako, ufisadi wako, ulevi wako, uuaji wako, utukanaji wako, usagaji wako, ulawiti wako, uchafu wako n.k Hii Neema ipo siku itaisha na siku hiyo ndipo utakapojua kuwa Hii neema ilikuwa ni ya thamani kiasi gani.

Hii Neema itakapoondolewa, itaondoka na kanisa..watakatifu wataondolewa ulimwenguni, dhiki kuu itaanza, mpingakristo atanyanyuka, ataua wengi na baadaye maji ya bahari na visima na mito yote itageuzwa kuwa damu, utatokea ugonjwa wa majipu ulio hatari kuliko huu uliozuka sasa unaoitwa CORONA. Utasambaa duniani kote hakuna mtu atakayesalimika kwa wale watakaoachwa kwenye unyakuo, wakati huo hakutakuwa na mtu wa kukwambia utubu dhambi zako.

Siku hizo hakutakuwa na masinema tena watu wanayokwenda kuangalia michezo , hakutakuwa na mipira watu wanayokwenda kuangalia, barabara zitakuwa wazi, kila mtu atakuwa peke yake peke yake akiugulia mapigo hayo..Unaona leo ugonjwa huu wa Corona leo ulivyosababisha mabarabara kufungwa, mashule kufungwa, hakuna mtu kwenda kazini kwenye mataifa yaliyoathirika, kila mtu kajifungia ndani..siku hizo itakuwa mara 100 ya hiyo, hata mnyama wako wa kufugwa hutamsogelea, kutakuwa hakuna kutembea mabarabarani..kila mtu anashiriki mapigo hayo kivyakevyake.

Katikati ya gonjwa hilo la ajabu litakalolipuka la majipuโ€ฆmvua zitaacha kunyesha, jua litashushwa chini, kutakuwa hakuna kitu chochote kilicho kijani kitakachoonekana, mvua ya mawe itashuka, sio ya mawe ya barafu..mawe kama mawe, makubwa kama talanta, kutatokea matetemeko na milipuko ya volcano duniani kote, na baada ya siku za maunguzo ya jua kupitaโ€ฆ.jua litakuja kuondolewa kutakuwa na giza la ajabu kuliko lile lililotokea kipindi cha Farao, nyota hazitakuwepo, mwezi utaonekana kuwa mwekundu kama damu kwa kipindi kirefu, mambo hayo yote yanakuja ndani ya wakati mmoja..na mambo mengine mengi ya ajabu yatakuwepo, mambo haya sio hadithi za kutunga kasome Ufunuo 16 yote, utaona, na kama unyakuo utakupita basi utayashuhudia hayo yote.

Waebrania 10:25 โ€œwala tusiache kukusanyika pamoja, kama ilivyo desturi ya wengine; bali tuonyane; na kuzidi kufanya hivyo, kwa kadiri mwonavyo siku ile kuwa inakaribia.

26  Maana, kama tukifanya dhambi kusudi baada ya kuupokea ujuzi wa ile kweli, haibaki tena dhabihu kwa ajili ya dhambi;

27  bali kuna kuitazamia hukumu yenye kutisha, na ukali wa moto ulio tayari kuwala wao wapingao.

28  Mtu aliyeidharau sheria ya Musa hufa pasipo huruma, kwa neno la mashahidi wawili au watatu.

29  MWAONAJE? HAIKUMPASA ADHABU ILIYO KUBWA ZAIDI MTU YULE ALIYEMKANYAGA MWANA WA MUNGU, NA KUIHESABU DAMU YA AGANO ALIYOTAKASWA KWAYO KUWA NI KITU OVYO, na kumfanyia jeuri Roho wa neema?

30  Maana twamjua yeye aliyesema, Kupatiliza kisasi ni juu yangu, mimi nitalipa. Na tena, Bwana atawahukumu watu wake.

31  Ni jambo la kutisha kuanguka katika mikono ya Mungu aliye hai.โ€

Kama hujageuka na kutubu mlango wa Neema leo upo waziโ€ฆNi heri usitumie muda ku-comment na ku-like badala yake ukatubu kama hujatubu. Usisome tu kama hadithi ya kukufurahisha, bali ujumbe huu ukawe sababu ya mageuzi kwako..

Na maana ya kutubu ni โ€œkugeukaโ€..maana yake unadhamiria kuyaacha yale uliyokuwa unayafanya yasiyompendeza Mungu, na unakwenda kubatizwa katika ubatizo sahihi na kupokea Roho Mtakatifu. Mambo hayo unayafanya kwa moyo wako wote.

Bwana akubariki sana. Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako

jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >ย WHATSAPP


Mada Nyinginezo:

Rudi Nyumbani:

Print this post

Kwanini Bwana alisema Hakuna aliye mwema ila mmoja?

SWALI: Samahani mtumishi naomba ufafanuzi wa kauli hii ya Bwana Yesu aliimanisha nini? “KWA NINI KUNIITA MWEMA? HAKUNA ALIYE MWEMA ILA MMOJA, NDIYE MUNGU.” Hapa nashindwa kuelewa alivyomjibu kwani alikosea wapi maana hata mimi leo hii najua Yesu ni mwema na alikuwa mwema!! Nisaidie kunifafanulia. Amina.


JIBU: Tusome habari yenyewe..

Marko 10:17 โ€œHata alipokuwa akitoka kwenda njiani, mtu mmoja akaja mbio, akampigia magoti, akamwuliza, MWALIMU MWEMA, nifanye nini nipate kuurithi uzima wa milele?

18 Yesu akamwambia, Kwa nini kuniita mwema? Hakuna aliye mwema ila mmoja, ndiye Mungu.

19 Wazijua amri, Usiue, Usizini, Usiibe, Usishuhudie uongo, Usidanganye, Waheshimu baba yako na mama yako.

20 Akamwambia, Mwalimu, haya yote nimeyashika tangu utoto wangu.

21 Yesu akamkazia macho, akampenda, akamwambia, Umepungukiwa na neno moja. Enenda, ukauze ulivyo navyo vyote, uwape maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni; kisha njoo unifuate.

22 Walakini yeye akakunja uso kwa neno hilo, akaenda zake kwa huzuni; kwa sababu alikuwa na mali nyingi.

23 Yesu akatazama kotekote, akawaambia wanafunzi wake, Jinsi itakavyokuwa shida wenye mali kuingia katika ufalme wa Mungu!.

Wengi wanatumia vipengele hivi (hususani wale wasio wakristo), Kuthibitisha kuwa Yesu hakuwa Mungu, kwasababu hapa alikana kabisa kuwa yeye hakuwa mwema ila Mungu peke yake,โ€ฆLakini ukisoma kwa utulivu na ukimwomba Roho Mtakatifu akufumbue macho, utagundua kuwa Bwana Yesu hakukana kuwa yeye sio Mwema..Hakusema umekosea badili kauli yako!..Lakini alimuuliza swali tu!..Kwanini unaniita mimi mwema?..Kuuliza swali sio kukanaโ€ฆ.alitaka kupata mawazo yake, ni nini aliona ndani yake mpaka yeye amwite vile mwemaโ€ฆ

Ni sawa na leo hii ukutane na mtu Fulani mkubwa ukamkimbilia na kumpigia magoti na kumwambia muheshimiwa, maagizo yoyote utakayonipa mimi nitayafanya..Na yeye akakuuliza ni kwanini unaniita mimi muheshimiwa?..anayeheshimiwa ni lazima awe kiongozi na mwenye mamlaka, Na hivyo utakuwa radhi, kutii chochote atakaachokuambia kukifanya kulingana na kauli yakoโ€ฆ Na ndivyo ilivyokuwa kwa Bwana Yesu alipomwambia yule kijana, hakuna aliye mwema ila mmoja, ndiye Mungu, yaani yeyote uliyemwona kuwa ni mwema basi ujue huyo ni Mungu..

Hivyo Unaongea na huyo aliye mwema ambaye ni Mungu.. Kama unadhani Kristo alikuwa anapinga yeye kuitwa mwema..Soma tena, (Yohana 10:11) utaona anajiita mimi ndimi mchungaji mwemaโ€ฆSasa ikiwa alikuwa anajipinga vile basi asingejiita na hapa pia mchungaji mwema..Na pia kasome Yohana 14:8-10 utaona Uungu wa Bwana Yesu. Lakini utaona alimuuliza kijana yule vile, ili kumjengea mazingira ya kukishika kila ambacho atakachokwenda kumwambia mbele, kwa kigezo kile kile cha kumtambua kuwa yeye ni mwema kama Munguโ€ฆ

ย Ndipo pale alipomwambia, umezishika amri akasema, nimezishika zote, lakini Bwana Yesu akaona kuwa hajazishika zote, imesalia moja, tena ile ya kwanza ya kumpenda Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote,kwa roho yako yote, kwa nguvu zako zote, na kwa akili zako zote..Ndipo akamwambia umepungukiwa na moja, nenda akauze vyote ulivyo navyo, na kuwapa maskini, kisha njoo amfuate..

Lakini Yule kijana aliposikia habari za mali zake zinagusiwa akaondoka amekunja uso wake, kwasababu alipenda mali zake kuliko kumpenda Mungu.. Jaribu kufikiria kama angemtii Kristo, kama alivyomtambua kuwa yeye ni mwema kama Mungu na kuyafuata yote aliyoambiwa ..Leo hii yule angekuwa wapi?..

Bila shaka angekuwa ni mtume wa 13, Lakini alipenda mali zake kuliko kumpenda Mungu. Hata leo hii, tukimjua Kristo kama Mungu, pale anapotuambia tumpende yeye kwa nguvu zetu zote, pale anapotuambia tuache mambo Fulani ya kidunia, hatuna budi kuacha mara moja vinginevyo tutakuwa ni wanafki..

Bwana akubariki.

jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >>ย WHATSAPP

Mada Nyinginezo:

Kwanini yule mtu hakukutwa na vazi la arusi wakati alialikwa?

Kwanini Bwana Yesu, aliruhusu yale mapepo yawaingie nguruwe?

KIFO CHA MTAKATIFU PERPETUA NA FELISTA.

Ufisadi una maanisha nini katika biblia?

USILALE USINGIZI WAKATI WA KUMNGOJEA BWANA.

Rudi Nyumbani:

Print this post

USIMZIMISHE ROHO.

1Wathesalonike 5:18 โ€œShukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu. 19 MSIMZIMISHE ROHO;โ€

Roho Mtakatifu anafananishwa na motoโ€ฆWakati ule wa Pentekoste Roho aliposhuka juu ya wale watu..alishuka mfano wa ndimi za motoโ€ฆHakushuka kama ndimi tu, bali kama ndimi za moto.. Maana yake ni kwamba Roho Mtakatifu anafananishwa na moto kwa tabia zake.

Sasa maana ya ndimi za moto ni nini?…Maana yake ni katika vinywa vyao zilitoka lugha zenye kuchoma kazi zote za Aduiโ€ฆNdio maana muda mfupi tu baada ya tukio lile, wale mitume waliposimama na kuwashuhudia watu, walichomwa mioyo yao kwa namna isiyokuwa ya kawaida, na siku hiyo hiyo wakatubu watu elfu tatu na kubatizwa.

Matendo 2:1 โ€œHata ilipotimia siku ya Pentekoste walikuwako wote mahali pamoja.

2 Kukaja ghafula toka mbinguni uvumi kama uvumi wa upepo wa nguvu ukienda kasi, ukaijaza nyumba yote waliyokuwa wameketi.

3 Kukawatokea ndimi zilizogawanyikana, kama ndimi za moto uliowakalia kila mmoja wao.

4 Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia kutamka.

Na walikuwako Yerusalemu Wayahudi wakikaa, watu watauwa, watu wa kila taifa chini ya mbingu.

6 Basi sauti hii iliposikiwa makutano walikutanika, wakashikwa na fadhaa, kwa kuwa kila mmoja aliwasikia wakisema kwa lugha yake mwenyewe.

7 Wakashangaa wote, wakastaajabu wakiambiana, Tazama, hawa wote wasemao si Wagalilaya?

8 Imekuwaje basi sisi kusikia kila mtu lugha yetu tuliyozaliwa nayo?โ€

Tukienda mpaka mstari wa 37 unasema..

โ€œ37 Walipoyasikia haya WAKACHOMWA MIOYO YAO, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu?

38 Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.

39 Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie.

40 Akawashuhudia kwa maneno mengine mengi sana na kuwaonya, akisema, Jiokoeni na kizazi hiki chenye ukaidi.

41 Nao waliolipokea neno lake wakabatizwa; na siku ile wakaongezeka WATU WAPATA ELFU TATU.โ€.

Unaona? Hapo walichomwa mioyo yao?..sasa kilichowachoma ni niniโ€ฆni maneno ya moto yaliyokuwa yanatoka katika vinywa vya wale mitume walipokuwa wanawahubiria, siku zote walikuwa wanaishi na wakina Petro lakini maneno yao yalikuwa hayawachomi, lakini siku hii ya Pentekoste baada ya kupokea ndimi za moto..Maneno yao yakawa na uwezo wa kuchoma nia za Adui shetani ndani ya mioyo ya watu na kuwafanya waitii Injili. Hiyo yote ni kutokana na Roho waliyempokea na si kingine.

Hali kadhalika ndimi hizi hizi za moto walizozipokea Mitume ambazo kwa maneno yale machache tu siku ile waliweza kuwavuta watu wengi kwa Kristo takribani elfu 3โ€ฆNdio moto huo huo ambao wakiomba kitu kwa Mungu wa mbingu na nchi Mungu anawasikia na kuwajibu haraka zaidi kuliko wangekuwa hawana roho..Kwasababu ndimi hizo hizo zinaingia mpaka kwenye moyo wa Mungu na kwenda kumshawishi Mungu kwa kuugua kusikoweza kutamkwa na hivyo kupokea majibu kwa haraka sana..(Kumbuka neno ndimi ni wingi wa neno ULIMI, na ulimi ni neno linalowakilisha Lugha/usemi)..

Hivyo Usemi uliovuviwa Roho Mtakatifu unakuwa ni usemi wa moto. Kwahiyo mtu yeyote mwenye Roho Mtakatifu anapoomba iwe kwa kunena kwa lugha au isiwe kwa kunena kwa lugha, ule usemi wake mbele za Mungu unakuwa kama ni moto..unapenya mpaka kwenye vilindi vya moyo wa Mungu na kumshawishi kwa namna isiyoelezeka..hiyo ndiyo maana ya lile neno linalosema โ€œRoho hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa (Warumi 8:26)โ€.

Maana yake ni kwamba tunapoomba tukiwa na Roho Mtakatifu lugha zetu hizi mbele za Mungu haziendi kama za watu wengine wa kawaida bali zinakwenda zikiwa zimejazwa nguvu mara nyingi zaidi za kuushawishi moyo wa Mungu kuliko tunavyoweza kuelezea..Kama tu vile mtu mwenye Roho Mtakatifu anavyohubiri, hatatumia nguvu nyingi kumshawishi Yule mtu aokoke..bali yale maneno yake yatakwenda kama moto wa Roho kuugua ndani ya Yule mtu kwa namna isiyoweza kutamka, na hatimaye Yule mtu kukata shauri kuokoka.

Lakini sasa huyu Roho Mtakatifu anaweza kuzimishwa..na ndio biblia inatuambia hapo.. โ€œMsimzimishe Rohoโ€..Maana yake ule moto wa Roho ndani ya mtu unazima. Maneno yake yanakuwa hayana nguvu tena ya kumbadilisha mtu, wala yanakuwa hayana nguvu tena kuushawishi moyo wa Mungu kwa kuugua kusikoweza kutamkwa.

Mtu anapofikia hali kama hii ambapo โ€œRoho kashazima ndani yakeโ€โ€ฆatalazimisha kutumia nguvu zake za kimwili na hekima yake ya kibinadamu na kila mbinu kumshawishi mtu amgeukie Mungu na atashindwa..

1Wakorintho 2:4 โ€œNa neno langu na kuhubiri kwangu hakukuwa kwa maneno ya hekima yenye kushawishi akili za watu, bali kwa dalili za Roho na za nguvu,

5 ili imani yenu isiwe katika hekima ya wanadamu, bali katika nguvu za Munguโ€.

Hali kadhalika maombi yake siku zote yatakuwa sio ya kuushawishi moyo wa Mungu..

Sasa ni mambo gani yanayomzimisha Roho ndani ya Mtu?

Jambo la kwanza ni kuudharau msalaba na kumfanyia Jeuri Roho Mtakatifu kwa kulidharau Neno lakeโ€ฆNeno lake linaposema hivi, na ndani ya moyo wako Roho Mtakatifu anakushuhudia kabisa kwamba jambo hili kulifanya sio sawa,..lakini wewe unalipuuzia, unadharau au unaonyesha jeuri mbele yake unafanya yale yasiyompendeza..hapo ule moto ambao pengine ulikuwa umeshaanza kuwaka ndani yako unazima ghafla.

Waebrania 10:29 โ€œMwaonaje? Haikumpasa adhabu iliyo kubwa zaidi mtu yule aliyemkanyaga Mwana wa Mungu, na kuihesabu damu ya agano aliyotakaswa kwayo kuwa ni kitu ovyo, NA KUMFANYIA JEURI ROHO WA NEEMA?โ€

ย 2.Pili unapompinga Roho Mtakatifu kwa matendo yako..Kumpinga maana yake hukubaliani na kile anachokisema..Kwamfano biblia inasema.. โ€œWaefeso 5.18 Tena msilewe kwa mvinyo, ambamo mna ufisadi; bali mjazwe Roho;โ€..Na wewe unasema maana yake sio hiyo bali ni nyingine, na huku unaendelea kujihalalishia ulevi..hapo unampinga Roho Mtakatifu..Au biblia inaposema..

โ€œ1Timotheo 2:9 Vivyo hivyo wanawake na wajipambe kwa mavazi ya kujisitiri, pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi; si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani;

10 bali kwa matendo mema, kama iwapasavyo wanawake wanaoukiri uchaji wa Mungu.โ€โ€ฆ

Na wewe unasema maana yake sio hiyo bali ni nyingine..hapo unapingana na Roho Mtakatifu na hivyo upo hatarini kumzimisha Roho.

Matendo 7:51 โ€œEnyi wenye shingo gumu, msiotahiriwa mioyo wala masikio, siku zote mnampinga Roho Mtakatifu; kama baba zenu walivyofanya, na ninyi ni vivyo hivyoโ€.

Ili tufanikiwe katika kila kitu hapa duniani, tunamhitaji Roho Mtakatifu..Huyo ni kama moto, akizimika ndani yetu hakuna chochote tutakachoweza kufanya..hata maombi yetu yatakuwa ni bure mbele za Mungu..Na kama tayari kashazima ndani yetu suluhisho la kuurudisha ule moto wake ni kutubu na kuanza kumtii Roho Mtakatifu, na kutompinga wala kulidharau Neno lake.

Kama hujampa Yesu Kristo maisha yako basi mpe leo, ulitii Neno lake wala usiudharau msalaba kwani ni kwa faida yako, tubu leo kwa kumaanisha kuziacha dhambi zote ulizokuwa unazifanya, na nenda kabatizwe katika ubatizo sahihi wa kuzamishwa na kwa jina la YESU, na Roho Mtakatifu atashuka juu yako kama moto.

Bwana akubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312

jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >>ย WHATSAPP

Mada Nyinginezo:

Je! hizi roho saba za Mungu ni zipi? na je zinatofautiana na Roho Mtakatifu?

MAFUNDISHO YA MASHETANI

KWANINI AWE PUNDA NA SI MNYAMA MWINGINE?

SIKUJA KULETA AMANI DUNIANI, BALI MAFARAKANO.

JINSI ROHO MTAKATIFU ANAVYOWAFUNULIA WATU MAANDIKO.

Rudi Nyumbani:

Print this post

ู…ุง ู‡ูˆ ูƒุชุงุจ ุงู„ุญูŠุงุฉุŸ

๏ปณ๏ปฎ๏บฃ๏ปจ๏บŽ ๏บญ๏บ…๏ปณ๏บŽ 20:11-15

11ย ุซูู…ู‘ูŽ ุฑูŽุฃูŠุชู ุนูŽุฑุดุงู‹ ูƒูŽุจููŠุฑุงู‹ ุฃุจูŠูŽุถูŽุŒ ูˆูŽุฑูŽุฃูŠุชู ุงู„ุฌุงู„ูุณูŽ ุนูŽู„ูŽูŠู‡ู. ุงู„ุณู‘ูŽู…ุงุกู ูˆูŽุงู„ุฃุฑู’ุถู ู‡ูŽุฑูŽุจูŽุชุง ู…ูู†ู’ ุฃู…ุงู…ูู‡ูุŒ ููŽู„ูŽู…ู’ ูŠููˆุฌูŽุฏู’ ู„ูŽู‡ูู…ุง ุฃุซูŽุฑูŒ! 12ย ุซูู…ู‘ูŽ ุฑูŽุฃูŠุชู ุงู„ู…ูŽูˆุชูŽู‰ ุตูุบุงุฑุงู‹ ูˆูŽูƒูุจุงุฑุงู‹ ูŠูŽู‚ููููˆู†ูŽ ุฃู…ุงู…ูŽ ุงู„ุนูŽุฑุดู. ูˆูŽูƒุงู†ูŽุชู’ ู‡ูู†ุงูƒูŽ ูƒูุชูุจูŒ ู…ูŽูุชููˆุญูŽุฉูŒุŒ ุซูู…ู‘ูŽ ููุชูุญูŽ ูƒูุชุงุจูŒ ุขุฎูŽุฑู ู‡ููˆูŽ ูƒูุชุงุจู ุงู„ุญูŽูŠุงุฉู. ูˆูŽุญููƒูู…ูŽ ุนูŽู„ูŽู‰ ุงู„ู…ูŽูˆุชูŽู‰ ุจูุญูŽุณูŽุจู ุฃุนู…ุงู„ูู‡ูู…ู ุงู„ู…ูŽูƒุชููˆุจูŽุฉู ูููŠ ุงู„ูƒูุชูุจู. 13ย ูˆูŽุณูŽู„ู‘ูŽู…ูŽ ุงู„ุจูŽุญุฑู ุงู„ู…ูŽูˆุชูŽู‰ ุงู„ู‘ูŽุฐููŠู†ูŽ ูƒุงู†ููˆุง ูููŠู‡ูุŒ ูˆูŽุณูŽู„ู‘ูŽู…ูŽ ยซุงู„ู…ูŽูˆุชูยป ูˆูŽ ยซุงู„ู‡ุงูˆููŠูŽุฉูยป ุงู„ู…ูŽูˆุชูŽู‰ ุงู„ู‘ูŽุฐููŠู†ูŽ ูƒุงู†ููˆุง ู…ูŽุนูŽู‡ูู…ุง. ูˆูŽุญููƒูู…ูŽ ุนูŽู„ูŽู‰ ูƒูู„ู‘ู ูˆุงุญูุฏู ุญูŽุณูŽุจูŽ ุฃุนู…ุงู„ูู‡ู. 14ย ุซูู…ู‘ูŽ ุฃูู„ู‚ููŠูŽ ยซุงู„ู…ูŽูˆุชูยป ูˆูŽ ยซุงู„ู‡ุงูˆููŠูŽุฉูยป ุฅู„ูŽู‰ ุงู„ุจูุญูŽูŠุฑูŽุฉู ุงู„ู…ูุชู‘ูŽู‚ูุฏูŽุฉู. ุงู„ู‘ูŽุชููŠ ู‡ููŠูŽ ุงู„ู…ูŽูˆุชู ุงู„ุซู‘ุงู†ููŠ. 15ย ูˆูŽู…ูŽู†ู’ ู„ูŽู…ู’ ูŠูŽูƒูู†ู ุงุณู’ู…ูู‡ู ู…ูŽูƒุชููˆุจุงู‹ ูููŠ ูƒูุชุงุจู ุงู„ุญูŽูŠุงุฉูุŒ ุทูุฑูุญูŽ ูููŠ ุงู„ุจูุญูŽูŠุฑูŽุฉู ุงู„ู…ูุชู‘ูŽู‚ูุฏูŽุฉู.

ุขู…ูŠู†! ุจุงุชุจุงุน ุงู„ุขูŠุงุช ุฃุนู„ุงู‡ ุŒ ู†ุฑู‰ ููŠ ุงู„ูŠูˆู… ุงู„ุฃุฎูŠุฑ ู…ู† ุงู„ุฏูŠู†ูˆู†ุฉ ุนู†ุฏู…ุง ูŠุฌู„ุณ ุงู„ุฑุจ ูŠุณูˆุน ู„ูŠุญูƒู… ุนู„ู‰ ุดุนูˆุจ ุงู„ุนุงู„ู… ููŠ ุนุฑุดู‡ ุงู„ุฃุจูŠุถ ุŒ ุณูŠูƒูˆู† ู‡ู†ุงูƒ ู†ูˆุนุงู† ุฑุฆูŠุณูŠุงู† ู…ู† ุงู„ูƒุชุจ: ูƒุชุงุจ ุงู„ุญูŠุงุฉ ูˆุงู„ูƒุชุจ ุงู„ุฃุฎุฑู‰. ู‡ู†ุงูƒ ุชุฑู‰ ูƒุชุงุจ ุงู„ุญูŠุงุฉ ูŠุดุจู‡ู‡! ูˆู„ูƒู† ู‡ู†ุงูƒ ุฃูŠุถู‹ุง ูƒุชุจ ุฃุฎุฑู‰ ุŒ ุชู‚ุชุฑุญ ุงู„ูƒุซูŠุฑ ุŒ ูู„ู†ุณุชูƒุดู ุจุงุฎุชุตุงุฑ ู…ุง ู‡ูŠ ู‡ุฐู‡ ุงู„ูƒุชุจ ุญู‚ู‹ุง ุ›

1) ูƒุชุงุจ ุงู„ุญูŠุงุฉ

ูƒู…ุง ุชุตู ู†ูุณู‡ุง ูƒุชุงุจู‹ุง ูŠุตู ุงู„ุญูŠุงุฉ ุŒ ุชู…ุงู…ู‹ุง ูƒู…ุง ูŠุตู ูƒุชุงุจ ุงู„ุฑูŠุงุถูŠุงุช ุงู„ุฃุณุงู„ูŠุจ ุงู„ุฑูŠุงุถูŠุฉ ุŒ ูŠุดุฑุญ ูƒุชุงุจ ุงู„ุฌุบุฑุงููŠุง ุงู„ู‚ุถุงูŠุง ุงู„ุฌุบุฑุงููŠุฉ ุจุงู„ุฅุถุงูุฉ ุฅู„ู‰ ุฌู…ูŠุน ุงู„ูƒุชุจ ุงู„ุฃุฎุฑู‰. ูˆู†ุญู† ู†ุนู„ู… ุฃู† ุงู„ูƒุชุจ ุชู†ู‚ุณู… ุฅู„ู‰ ุตูุญุงุช ู…ุฎุชู„ูุฉ. ู„ูƒู†ู†ุง ู†ุฑู‰ ูƒู„ ู‡ุฐู‡ ุงู„ูƒุชุจ ุงู„ุชูŠ ู„ุฏูŠู†ุง ููŠ ุงู„ุนุงู„ู… ุชุฎุจุฑู†ุง ูู‚ุท ุจู…ุจุงุฏุฆ ูˆุชู‚ู†ูŠุงุช ุฃุดูŠุงุก ูƒุซูŠุฑุฉ ุนู† ู‡ุฐุง ุงู„ุนุงู„ู… ุŒ ูˆู†ุฑู‰ ุฃู†ู‡ ู„ุง ูŠูˆุฌุฏ ุฃูŠ ูƒุชุงุจ ููŠ ุงู„ุนุงู„ู… ูŠู…ูƒู† ุฃู† ูŠูุณุฑ ุญูŠุงุฉ ุงู„ุฅู†ุณุงู† ุจุงุณุชุซู†ุงุก ุงู„ูƒุชุงุจ ุงู„ู…ู‚ุฏุณ ูู‚ุท! ู„ุฐุง ุŒ ูุฅู† ูƒุชุงุจ ุงู„ุญูŠุงุฉ ุงู„ู…ุดุงุฑ ุฅู„ูŠู‡ ู‡ู†ุง ู‡ูˆ ุงู„ูƒุชุงุจ ุงู„ู…ู‚ุฏุณ ุงู„ุฐูŠ ู‡ูˆ ูƒู„ู…ุฉ ุงู„ู„ู‡.

2) ูƒุชุจ ุฃุฎุฑู‰

ู†ุฌุฏ ุฃู† ุงู„ูƒุชุงุจ ุงู„ู…ู‚ุฏุณ ู‚ุฏ ุฃุดุงุฑ ุฅู„ูŠู‡ู… ูƒุซูŠุฑู‹ุง ุŒ ูˆุงู„ุฐูŠ ุจุฏูˆุฑู‡ ูŠุฎุจุฑ ุจุนุถ ุงู„ู…ุนู„ูˆู…ุงุช ูˆู„ูŠุณ ุฃูƒุซุฑ ู…ู† ุงู„ุจุดุฑ ูˆูู‚ู‹ุง ู„ู„ูƒุชุงุจ ุงู„ู…ู‚ุฏุณ. ู‡ุฐู‡ ู‡ูŠ ูƒุชุจ ุงู„ุฑุฌุงู„ ูˆู„ูƒู„ ุฑุฌู„ ุญูŠุงุชู‡ ุงู„ุฎุงุตุฉ ุŒ ูˆุงุตูุง ุญูŠุงุชู‡ ูƒู…ุง ุนุงุด ุนู„ู‰ ู‡ุฐู‡ ุงู„ุฃุฑุถ ู…ู†ุฐ ูˆู„ุงุฏุชู‡ ุญุชู‰ ูˆูุงุชู‡. ูˆู‡ุฐู‡ ุงู„ูƒุชุจ ุชุญุชูˆูŠ ุฃูŠุถู‹ุง ุนู„ู‰ ุตูุญุงุช ุŒ ูˆู‡ูŠ ุงู„ุฎุทูˆุงุช ุงู„ุชูŠ ุชู…ุฑ ุจู‡ุง ู‡ู†ุง ุนู„ู‰ ุงู„ุฃุฑุถ ุŒ ูˆู„ูƒู† ูƒู„ ู‡ุฐู‡ ุงู„ูƒุชุจ ู„ูŠุณ ู„ู‡ุง ุญูŠุงุฉ ููŠู‡ุง ุŒ ูƒุชุงุจ ุงู„ุญูŠุงุฉ ู…ูˆุฌูˆุฏ ุŒ ูˆู„ูƒู† ูˆุงุญุฏ ุŒ ูˆู„ู‡ุฐุง ูŠุนุชู…ุฏูˆู† ุฌู…ูŠุนู‹ุง ุนู„ู‰ ู‡ุฐุง ุงู„ูƒุชุงุจ ู„ุฅุนุทุงุก ู…ุตูŠุฑ ุงู„ุฅู†ุณุงู†.

ุฅุฐุงู‹ ู…ุง ูŠุตูู‡ ูƒุชุงุจ ุงู„ุญูŠุงุฉ ู‡ูˆ ุงู„ู‚ูˆุงุนุฏ ูˆุงู„ู„ูˆุงุฆุญ ุงู„ุฎุงุตุฉ ุจูƒูŠููŠุฉ ุนูŠุด ุงู„ุฅู†ุณุงู† ุนู„ู‰ ู‡ุฐู‡ ุงู„ุฃุฑุถ ู…ู† ุฃุฌู„ ุฌุนู„ ู‡ุฐู‡ ุงู„ุญูŠุงุฉ ุฌุฒุกู‹ุง ู„ุง ูŠุชุฌุฒุฃ ู…ู†ู‡ุง ุŒ ู„ุฐุง ูŠุฌุจ ุนู„ู‰ ุงู„ุจุดุฑ ุงู„ุฐูŠู† ูŠูƒุชุจูˆู† ูƒุชุจ ุญูŠุงุชู†ุง ุฃู† ู†ูƒุชุจู‡ุง ู„ุชุดุจู‡ ูƒุชุงุจ ุงู„ุญูŠุงุฉ (ุงู„ูƒุชุงุจ ุงู„ู…ู‚ุฏุณ) ู…ู† ุทููˆู„ุชู†ุง ุฅู„ู‰ ุฑุญูŠู„ู†ุง ุนู† ุงู„ุนุงู„ู…. ู…ู† ุงู„ู…ูุชุฑุถ ุฃู† ุชุดุจู‡ ูƒุชุจู†ุง ู‡ุฐุง ุงู„ูƒุชุงุจ ุŒ ูˆู‡ุฐุง ู‡ูˆ ู…ุธู‡ุฑ ุฃุณู…ุงุฆู†ุง ููŠ ูƒุชุงุจ ุงู„ุญูŠุงุฉ.

ุฅุฐู† ูŠุง ุฃุฎูŠ ุŒ ูƒูŠู ุชูƒุชุจ ูƒุชุงุจูƒุŸ ุดุงู‡ุฏ ุงู„ูˆู‚ุช ูŠู†ูุฏ! ู„ุง ุชู‚ู„ ุฃู†ู†ูŠ ุณุฃุณุชู‚ุจู„ ุงู„ู…ุณูŠุญ ุฃูˆ ุฃู†ู†ูŠ ุณุฃุนูŠุด ุญูŠุงุฉ ู…ู‚ุฏุณุฉ ุญุชู‰ ุฃุตู„ ุฅู„ู‰ ุณู† ู…ุนูŠู† ุฃูˆ ุญุชู‰ ุฃุฎุชุจุฑ ุดูŠุฆู‹ุง ุชุนุฑู ุญุชู‰ ุงู„ุขู† ุนู„ู‰ ุฃู† ูƒุชุงุจูƒ ูŠูƒุชุจ ูˆูŠูˆู…ู‹ุง ุจุนุฏ ูŠูˆู… ุชูุชุญ ุตูุญุงุช ูˆูุตูˆู„ ุฌุฏูŠุฏุฉ ุŒ ูˆุณุฑุนุงู† ู…ุง ุณูŠู†ุชู‡ูŠ ูƒุชุงุจูƒ ูˆูŠุบู„ู‚ ุŒ ูˆุณูŠุจู‚ู‰ ุฌุงู‡ุฒู‹ุง ู„ู„ู†ุดุฑ ููŠ ูŠูˆู… ุงู„ู‚ูŠุงู…ุฉ

ูˆููŠ ูŠูˆู… ุงู„ู‚ูŠุงู…ุฉ ุณูŠูุชุญ ูƒุชุงุจ ุงู„ุญูŠุงุฉ ูˆูŠูุชุญ ู„ูƒ ูƒุชุงุจูƒ ุŒ ุณูˆุงุก ูƒุงู†ุง ู…ุชุดุงุจู‡ูŠู† ุฃู… ู„ุง !. ุฅุฐุง ูƒุงู†ุช ุญูŠุงุชูƒ ููŠ ูƒุชุงุจูƒ ู„ุง ุชุชุทุงุจู‚ ู…ุน ุชู„ูƒ ุงู„ุชูŠ ููŠ ุงู„ุญูŠุงุฉ (ุฃูŠ ุงู„ูƒุชุงุจ ุงู„ู…ู‚ุฏุณ ุŒ ูƒู„ู…ุฉ ุงู„ู„ู‡) ู…ู…ุง ูŠุนู†ูŠ ุนุฏู… ูˆุฌูˆุฏ ุญูŠุงุฉ ููŠูƒ ุŒ ูุฅู† ุงู„ุฌุฒุก ุงู„ุฎุงุต ุจูƒ ุณูŠูƒูˆู† ููŠ ุจุญูŠุฑุฉ ุงู„ู†ุงุฑ.

ูŠุฌุจ ุนู„ูŠู†ุง ูƒู…ุณูŠุญูŠูŠู† ูƒู„ ูŠูˆู… ู…ู‚ุงุฑู†ุฉ ุญูŠุงุชู†ุง ุจุงู„ูƒุชุงุจ ุงู„ู…ู‚ุฏุณ. ุชุฃูƒุฏ ู…ู† ุฃู† ู…ุง ู†ู‚ูˆู… ุจู‡ ูŠุชูˆุงูู‚ ู…ุน ูƒุชุงุจ ุงู„ุญูŠุงุฉ. ุฃู†ุช ุนู„ู‰ ุฏุฑุงูŠุฉ ุชุงู…ุฉ ุจุฃู† ุงู„ู…ูˆู…ุณุงุช ุŒ ูˆุงู„ุฒู†ุงุฉ ุŒ ูˆุงู„ุณูƒุฑ ุŒ ูˆุงู„ู…ุฐู†ุจูˆู† ุŒ ูˆุงู„ุฃูˆุซุงู† ุŒ ูˆุงู„ูƒุฐุงุจูˆู† ุŒ ูˆุงู„ุซุฑุซุฑุฉ ุŒ ูˆุงู„ู…ุซู„ูŠูˆู† ุŒ ูˆุงู„ู…ุซู„ูŠุงุช ุŒ ูˆุงู„ู…ุฏุฎู†ูˆู† ุŒ ูˆู…ู…ุงุฑุณูŠ ุงู„ุนุงุฏุฉ ุงู„ุณุฑูŠุฉ ุŒ ูˆุงู„ู…ุตูˆุฑูˆู† ุงู„ุฅุจุงุญูŠูˆู† ุŒ ูˆุงู„ู„ุตูˆุต ุŒ ูˆุงู„ู…ูุณุฏูˆู† ุŒ ูˆุงู„ุณุญุฑุฉ ุŒ ูˆุงู„ุฑุดุงูˆู‰ ุŒ ูˆุงู„ู‚ุชู„ุฉ ุŒ ูˆู…ุง ุฅู„ู‰ ุฐู„ูƒ ุŒ ุฃุดุฎุงุต ู…ุซู„ ู‡ุคู„ุงุก ุจุนูŠุฏูˆู† ุนู† ูƒุชุงุจ ุงู„ุญูŠุงุฉ ุŒ ูƒูŠู ุชุชูˆู‚ุน ุฃู† ุชุธู‡ุฑ ููŠ ุงู„ูƒุชุงุจ ุฅุฐุง ูุนู„ุช ู‡ุฐู‡ ุงู„ุฃุดูŠุงุก ุŸุŒ ุชุฐูƒุฑ ุงู„ุฃุณู…ุงุก ุงู„ู…ุฐูƒูˆุฑุฉ ู„ูŠุณ ู‡ู†ุงูƒ ุฌูˆู† ุฃูˆ ุฌูˆู† ุฃูˆ ู…ุงุฑูŠ ู„ูƒู†ู‡ุง ุญูŠุงุชูƒ. ุงู‚ุฑุฃ.
ย 

๏ปณ๏ปฎ๏บฃ๏ปจ๏บŽ ๏บญ๏บ…๏ปณ๏บŽ 21:27ย 

27ย ู„ูŽูƒูู† ู„ูŽู†ู’ ูŠูŽุฏุฎูู„ูŽู‡ุง ุดูŽูŠุกูŒ ู†ูŽุฌูุณูŒุŒ ูˆูŽู„ุง ุฅู†ุณุงู†ูŒ ูŠูู…ุงุฑูุณู ุงู„ู†ู‘ูŽุฌุงุณูŽุฉูŽ ุฃูˆู ุงู„ูƒูŽุฐูุจูŽ. ู„ูŽู†ู’ ูŠูŽุฏุฎูู„ูŽู‡ุง ุฅู„ู‘ุง ู…ูŽู†ู’ ูƒุงู†ูŽ ุงุณู’ู…ูู‡ู ู…ูŽูƒุชููˆุจุงู‹ ูููŠ ูƒูุชุงุจู ุงู„ุญูŽูŠุงุฉูุŒ ูƒูุชุงุจู ุงู„ุญูŽู…ูŽู„ู.

ู„ูƒุชุงุจุฉ ูƒุชุงุจูƒ ุจุดูƒู„ ุตุญูŠุญ ูˆูู‚ู‹ุง ู„ูƒุชุงุจ ุงู„ุญูŠุงุฉ ุŒ ุชุฐูƒุฑ ุฃู†ู‡ ู„ูŠุณ ุนู…ู„ูŠุฉ ุชุณุชุบุฑู‚ ูŠูˆู…ู‹ุง ูˆุงุญุฏู‹ุง. ูƒู„ ูŠูˆู… ูŠุฌุจ ุนู„ู‰ ุงู„ู…ุฑุก ุฃู† ูŠูุญุต ุญูŠุงุชู‡ ุŒ ู„ุง ูŠุญุชู‚ุฑ ุงู„ุฅู†ุฌูŠู„ ุŒ ุฅุฐุง ุณู…ุนุช ูƒู„ู…ุฉ ุงู„ู„ู‡ ุงู„ู„ูŠู„ุฉ ุŒ ู„ุง ุชุดุฏุฏ ู‚ู„ุจูƒ ุชููƒุฑ ู‡ู†ุงูƒ ุณูŠุฃุชูŠ ูˆู‚ุช ุชุชูˆุจ ููŠู‡. ุฅุฐุง ูƒู†ุช ุชุนูŠุด ุชู„ูƒ ุงู„ุญูŠุงุฉ ูู„ุง ุชุชูˆู‚ุน ุฃุจุฏู‹ุง ุชุทุงุจู‚ู‡ุง ููŠ ูŠูˆู… ูˆุงุญุฏ ุŒ ูุฅู†ู‡ุง ุชุชุทู„ุจ ุฃู† ุชุนูŠุด ุงู„ุญูŠุงุฉ ุญุชู‰ ุชูƒุชุจ ูƒุชุงุจู‹ุง ุฃูุถู„ ูŠุดุจู‡ ูƒุชุงุจ ุงู„ุญูŠุงุฉ. ู‚ุงู„ ุงู„ุฑุจ.
ย 

๏ปŸ๏ปฎ๏ป—๏บŽ 9:23ย 

23ย ุซูู…ู‘ูŽ ู‚ุงู„ูŽ ู„ูŽู‡ูู…ู’ ุฌูŽู…ููŠุนุงู‹: ยซุฅุฐุง ุฃุฑุงุฏูŽ ุฃุญูŽุฏูŒ ุฃู†ู’ ูŠูŽุฃุชููŠูŽ ู…ูŽุนููŠุŒ ููŽู„ุง ุจูุฏู‘ูŽ ุฃู†ู’ ูŠูู†ูƒูุฑูŽ ู†ูŽูุณูŽู‡ูุŒ ูˆูŽุฃู†ู’ ูŠูŽุฑููŽุนูŽ ุงู„ุตู‘ูŽู„ููŠุจูŽ ุงู„ู…ูุนุทูŽู‰ ู„ูŽู‡ู ูƒูู„ู‘ูŽ ูŠูŽูˆู…ู ูˆูŽูŠูŽุชุจูŽุนูŽู†ููŠ.

ุฑุจู†ุง ูŠุญู…ูŠูƒ!

ย 

ุชุนุงู„ูŠู… ุฃุฎุฑู‰:

ู…ู† ุฃูŠู† ุญุตู„ ู‚ุงูŠูŠู† ุนู„ู‰ ุฒูˆุฌุชู‡ุŸ

ู…ู† ุฃูŠู† ุญุตู„ ู‚ุงูŠูŠู† ุนู„ู‰ ุฒูˆุฌุชู‡ุŸ

ูˆุฏุนุง ูƒุซูŠุฑูŠู†ุŒ ูˆู„ูƒู† ู‚ู„ุฉ ู…ุฎุชุงุฑุฉ

ุงู„ุตูุญุฉ ุงู„ุฑุฆูŠุณูŠุฉ:

ย 

Print this post