Kwanini Bwana alisema Hakuna aliye mwema ila mmoja?

Kwanini Bwana alisema Hakuna aliye mwema ila mmoja?

SWALI: Samahani mtumishi naomba ufafanuzi wa kauli hii ya Bwana Yesu aliimanisha nini? “KWA NINI KUNIITA MWEMA? HAKUNA ALIYE MWEMA ILA MMOJA, NDIYE MUNGU.” Hapa nashindwa kuelewa alivyomjibu kwani alikosea wapi maana hata mimi leo hii najua Yesu ni mwema na alikuwa mwema!! Nisaidie kunifafanulia. Amina.


JIBU: Tusome habari yenyewe..

Marko 10:17 “Hata alipokuwa akitoka kwenda njiani, mtu mmoja akaja mbio, akampigia magoti, akamwuliza, MWALIMU MWEMA, nifanye nini nipate kuurithi uzima wa milele?

18 Yesu akamwambia, Kwa nini kuniita mwema? Hakuna aliye mwema ila mmoja, ndiye Mungu.

19 Wazijua amri, Usiue, Usizini, Usiibe, Usishuhudie uongo, Usidanganye, Waheshimu baba yako na mama yako.

20 Akamwambia, Mwalimu, haya yote nimeyashika tangu utoto wangu.

21 Yesu akamkazia macho, akampenda, akamwambia, Umepungukiwa na neno moja. Enenda, ukauze ulivyo navyo vyote, uwape maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni; kisha njoo unifuate.

22 Walakini yeye akakunja uso kwa neno hilo, akaenda zake kwa huzuni; kwa sababu alikuwa na mali nyingi.

23 Yesu akatazama kotekote, akawaambia wanafunzi wake, Jinsi itakavyokuwa shida wenye mali kuingia katika ufalme wa Mungu!.

Wengi wanatumia vipengele hivi (hususani wale wasio wakristo), Kuthibitisha kuwa Yesu hakuwa Mungu, kwasababu hapa alikana kabisa kuwa yeye hakuwa mwema ila Mungu peke yake,…Lakini ukisoma kwa utulivu na ukimwomba Roho Mtakatifu akufumbue macho, utagundua kuwa Bwana Yesu hakukana kuwa yeye sio Mwema..Hakusema umekosea badili kauli yako!..Lakini alimuuliza swali tu!..Kwanini unaniita mimi mwema?..Kuuliza swali sio kukana….alitaka kupata mawazo yake, ni nini aliona ndani yake mpaka yeye amwite vile mwema…

Ni sawa na leo hii ukutane na mtu Fulani mkubwa ukamkimbilia na kumpigia magoti na kumwambia muheshimiwa, maagizo yoyote utakayonipa mimi nitayafanya..Na yeye akakuuliza ni kwanini unaniita mimi muheshimiwa?..anayeheshimiwa ni lazima awe kiongozi na mwenye mamlaka, Na hivyo utakuwa radhi, kutii chochote atakaachokuambia kukifanya kulingana na kauli yako… Na ndivyo ilivyokuwa kwa Bwana Yesu alipomwambia yule kijana, hakuna aliye mwema ila mmoja, ndiye Mungu, yaani yeyote uliyemwona kuwa ni mwema basi ujue huyo ni Mungu..

Hivyo Unaongea na huyo aliye mwema ambaye ni Mungu.. Kama unadhani Kristo alikuwa anapinga yeye kuitwa mwema..Soma tena, (Yohana 10:11) utaona anajiita mimi ndimi mchungaji mwema…Sasa ikiwa alikuwa anajipinga vile basi asingejiita na hapa pia mchungaji mwema..Na pia kasome Yohana 14:8-10 utaona Uungu wa Bwana Yesu. Lakini utaona alimuuliza kijana yule vile, ili kumjengea mazingira ya kukishika kila ambacho atakachokwenda kumwambia mbele, kwa kigezo kile kile cha kumtambua kuwa yeye ni mwema kama Mungu…

 Ndipo pale alipomwambia, umezishika amri akasema, nimezishika zote, lakini Bwana Yesu akaona kuwa hajazishika zote, imesalia moja, tena ile ya kwanza ya kumpenda Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote,kwa roho yako yote, kwa nguvu zako zote, na kwa akili zako zote..Ndipo akamwambia umepungukiwa na moja, nenda akauze vyote ulivyo navyo, na kuwapa maskini, kisha njoo amfuate..

Lakini Yule kijana aliposikia habari za mali zake zinagusiwa akaondoka amekunja uso wake, kwasababu alipenda mali zake kuliko kumpenda Mungu.. Jaribu kufikiria kama angemtii Kristo, kama alivyomtambua kuwa yeye ni mwema kama Mungu na kuyafuata yote aliyoambiwa ..Leo hii yule angekuwa wapi?..

Bila shaka angekuwa ni mtume wa 13, Lakini alipenda mali zake kuliko kumpenda Mungu. Hata leo hii, tukimjua Kristo kama Mungu, pale anapotuambia tumpende yeye kwa nguvu zetu zote, pale anapotuambia tuache mambo Fulani ya kidunia, hatuna budi kuacha mara moja vinginevyo tutakuwa ni wanafki..

Bwana akubariki.

Mada Nyinginezo:

Kwanini yule mtu hakukutwa na vazi la arusi wakati alialikwa?

Kwanini Bwana Yesu, aliruhusu yale mapepo yawaingie nguruwe?

KIFO CHA MTAKATIFU PERPETUA NA FELISTA.

Ufisadi una maanisha nini katika biblia?

USILALE USINGIZI WAKATI WA KUMNGOJEA BWANA.

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments