Ni kwa namna gani Neno la Mungu ni upanga?
Biblia haisemi Neno la Mungu ni upanga tu, hapana bali inasema ni zaidi ya upanga wowote mkali ukatao kuwili..
Waebrania 4:12 “Maana Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo.
13 Wala hakuna kiumbe kisichokuwa wazi mbele zake, lakini vitu vyote vi utupu na kufunuliwa machoni pake yeye aliye na mambo yetu.”.
Unaona? Ni zaidi ya upanga. Na kama tunavyojua upanga unaokata kuwili ni upanga ambao unatumika sana sana katika vita, yaani ukiupeleka upande wa kulia unakata na vilevile ukiurudisha upande wa kushoto bado unakata(Ufunuo 1:16, 2:12, 19:12).. Ni mfano wa msimeno unakata mbele na nyuma.
Sasa Mungu anakuambia Neno lake ni zaidi ya huo upanga. Akiwa na maana kuwa linakata pande zote, kwa wale wote watakaokwenda kinyume nalo, linakata matajiri, linakata maskini, linakata wenye vyeo linakata wasio na vyeo, linakata weupe, linakata weusi, linakata wenye dhambi vilevile linakata na waliookoka ikiwa hawatadumu katika maagizo yake.
Na kukata kwake sio butu, bali kwa ukali sana, likipita linatenganisha kabisa kabisa, yaani mfano Mungu akipitisha upanga katika taifa basi ujue taifa hilo ndio mwisho wake umefika, akipitisha upanga katika familia basi ujue ni upanga kweli kweli unaotenganisha, haijalishi ndugu hao watakuwa wanapendana au wameshikamana kiasi gani.Soma.
Mathayo 10:34 “Msidhani ya kuwa nimekuja kuleta amani duniani; la! Sikuja kuleta amani, bali upanga.
35 Kwa maana nalikuja kumfitini mtu na babaye, na binti na mamaye, na mkwe na mkwe mtu;
36 na adui za mtu ni wale wa nyumbani mwake”.
Vilevile alisema, katika wakati wa Mwisho atayaangamiza mataifa kwa Neno lake, ambao ndio huo upanga utokao katika kinywa chake..
Ufunuo 19:14 “Na majeshi yaliyo mbinguni wakamfuata, wamepanda farasi weupe na kuvikwa kitani nzuri, nyeupe, safi.
15 Na upanga mkali hutoka kinywani mwake ili awapige mataifa kwa huo. Naye atawachunga kwa fimbo ya chuma, naye anakanyaga shinikizo la mvinyo ya ghadhabu ya hasira ya Mungu Mwenyezi.
16 Naye ana jina limeandikwa katika vazi lake na paja lake, MFALME WA WAFALME, NA Bwana WA MABwana”.
Hivyo, Mungu anatuasa tutubu, tumgeukie yeye, ili kusudi kwamba Neno lake, liwe chakula na uzima kweli badala ya upanga, Kwasababu kwa kupitia hilo hilo Mungu alifanya mbingu na nchi, kwa kupitia hilo hilo, alituumba sisi, kwa kupitia hilo hilo alinatuponya na kutuokoa, na kutubariki. Lakini kwa kupita hilo hilo atatuhukumu kama tusipotaka kuitii injili. Na ndio anatuhimiza mpaka sasa tutubu kwa kurudi kwake kumekaribia.
Ufunuo 2.16 Basi tubu; na usipotubu, naja kwako upesi, nami nitafanya vita juu yao kwa huo upanga wa kinywa changu.
Neno la Mungu ni upanga.
Shalom.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
USIPOLITENDEA KAZI NENO LA MUNGU.
UTASIMAMA PEKE YAKO SIKU ILE.
MAPAMBANO DHIDI YA SHETANI.
KWANINI TUNAPASWA TUJIZUIE?
MAPIGO YA VITASA SABA, NA SIKU YA BWANA.
UTAWALA WA MIAKA 1000.
ROHO ZILIZO CHINI YA MADHABAHU:
Neno la Mungu la leo ni lipi?
Kwanza nakupongeza kwa kupenda kutafuta kujua Neno la Mungu la leo..
Bwana Yesu alisema kila atafutaye huona (Mathayo 7:8), Hivyo kwa kuwa na wewe umetafuta kujua Neno la Mungu la leo kwako, basi ni hakika kuwa lipo jambo jipya Mungu atakufundisha.
Sio kwa bahati mbaya umefika mahali hapa.,
Paulo alimwambia Timotheo.
1Timotheo 4:13 “Hata nitakapokuja, ufanye bidii katika kusoma…..”
Unaona ni jukumu la kila mmoja wetu kuonyesha bidii katika kusoma(kujifunza) Neno la Mungu.
Wewe unaonyesha bidii hiyo hivyo, usiache kupitia somo hili mpaka mwisho, lipo ambalo Mungu amekuandalia leo..
Lakini kabla hatujaendelea unaweza kufungua hapa uingie katika horodha ya masomo ya kujifunza yaliyotangulia zaidi ya 1000, pamoja na maswali na majibu ..
Leo tutajifunza nini maana ya Upendo na je! kuna aina ngapi za upendo?
Upendo ni kitendo cha kuonyesha hisia za tofauti za ndani kwa mtu mwingine, Ni hisia zinazoonyesha matokeo chanya, aidha umeridhishwa na mtu huyo, au umemkubali, au umemuhurumia, au unataka kumkaribia uwe karibu naye.
Kuna aina kuu tatu za upendo.
Upendo huu ndio ule ambao Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa mwanawe wa pekee ili kila mtu amwaminiye asipotee bali awe na uzima wa milele (Yohana 3:16).
Na Upendo aliokuwa nao Yesu, ukamfanya mpaka auote uhai wake kwa ajili yetu sisi wenye dhambi. Upendo wa namna hii ukiwa nao basi ujue kuwa Upo karibu na Mungu sana kuliko mwanadamu mwingine yeyote duniani.
Na unamjua Mungu, zaidi mwanadamu mwingine yoyote duniani haijalishi atasema anaona maono, au ana mafunuo mengi kiasi gani..
1Yohana 4:7 “Wapenzi, na mpendane; kwa kuwa pendo latoka kwa Mungu, na kila apendaye amezaliwa na Mungu, naye anamjua Mungu.
8 Yeye asiyependa, hakumjua Mungu, kwa maana Mungu ni upendo”.
Tabia za upendo huu unaweza kuzisoma katika kitabu cha 1Wakorintho 13:4-8
Kwa urefu wa maelezo haya juu ya aina hizi za upendo fungua hapa usome..>> UPENDO
Hivyo hiyo yote ni kuonyesha jinsi gani Mungu anatupenda na kutujali, Hivyo kama wewe ni mwenye dhambi ujue kuwa Mungu anakupenda bado na hivyo hataki upotee, uende kuzimu, mgeukie leo akuoshe dhambi zako. Ili ukaurithi uzima wa milele aliotuandalia. Hilo ndilo Neno la Mungu la leo.
Shalom.
Tazama vichwa vingine vya masomo chini, kwa maarifa zaidi ya kiroho.
Mada Nyinginezo:
RABI, UNAKAA WAPI?
KWANINI YESU ALIMUITA BABA YAKE “ABA”?
MANENO ALIYOWEZA KUTAMKA YESU TU PEKE YAKE.
SAMEHE KUTOKA NDANI YA MOYO WAKO.
WAFALME WATOKAO MAWIO YA JUA.
UNYAKUO.
Neno la Mungu ni nini?
Neno la Mungu ni ujumbe kutoka kwa Mungu, au mkusanyiko wa jumbe kutoka kwake. Ukisoma katika maandiko utaona mara nyingi manabii walikuwa wanasema maneno haya “Neno la Bwana linakanijia kusema”..Soma (Yeremia 1:11, Yeremia 13:3, 1Nyakati 22:8)
Wakiwa na maana ujumbe wa Mungu umenifikia kuwaambia. Hivyo biblia kwa ujumla inajulikana kama Neno la Mungu.
Lakini pia Neno la Mungu ni jina la YESU KRISTO.
Ukisoma..
Yohana 1:1 “Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu.
2 Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu.
3 Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika.
4 Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu….
14 Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli”.
Neno la Mungu ni nini?
Kwanini YESU aitwe Neno?
Anaitwa Neno Kwasababu yeye ndiye kinywa chote cha Mungu,(Yohana 8:38), Yeye ndio wazo lote la Mungu, yeye ndiye utimilifu wote wa Mungu kwa jinsi ya mwili (Wakolosai 2:9)..Yeye ndiye aliyepewa hukumu yote na Mungu, na yeye ndiye aliyepewa milki ya vitu vyote..
Hivyo chochote afanyacho, chochote asemacho, ni sauti ya Mungu kweli, na ujumbe wa Mungu kweli kweli kwetu..
Na ndio maana utamsoma katika Ufunuo akijitambulisha kwa jina hilo.
Ufunuo 19:12 “Na macho yake yalikuwa kama mwali wa moto, na juu ya kichwa chake vilemba vingi; naye ana jina lililoandikwa, asilolijua mtu ila yeye mwenyewe.
13 Naye amevikwa vazi lililochovywa katika damu, na jina lake aitwa, Neno la Mungu.
14 Na majeshi yaliyo mbinguni wakamfuata, wamepanda farasi weupe na kuvikwa kitani nzuri, nyeupe, safi”.
Hivyo ukiyashika maneno ya Yesu, basi umelishika Neno la Mungu, ukiyashika maagizo ya Yesu basi umeyashika maagizo yake…Naamini umeshafahamu sasa Neno la Mungu ni nini!
Bwana akubariki.
Je! Unatambua kuwa tunaishi katika siku za mwisho? Je! Una habari kuwa hili ndio kanisa la mwisho lijulikanalo kama Laodikia, na kwamba hatutakuwa na kanisa lingine zaidi ya hili,.Pengine kizazi chetu zitashuhudia tukio la ujio wa pili wa Kristo? Dalili zote zinaonyesha, Kama ni hivyo Je! Umejiwekaje tayari?..Bado upo kwenye dhambi?
Ikiwa utahitaji kumpa Yesu maisha yako leo basi uamuzi utakaoufanya ni wa busara sana, hivyo fungua hapa kwa ajili ya sala ya toba..>>>
Maran Atha.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
KWANINI YESU KRISTO ALIKUJA DUNIANI?
JINA LA MUNGU NI LIPI?
NITAFUNGUAJE MILANGO ILIYOFUNGWA MBELE YANGU?
USITOKE NJE YA HIFADHI YA MUNGU.
HUYU SI YULE SEREMALA, MWANA WA MARIAMU?
DHIKI KUU INAKUJA NA UNYAKUO UPO KARIBU.
Siku ile Bwana Yesu alipokufa biblia inatuambia makaburi yalipasuka na miili ya watakatifu wengi iliinuka, lakini katika ufufuo huo hawakuondoka pale makaburini mpaka siku Yesu alipofufuka, Ndipo wakaanza safari ya kuuelekea mji mtakatifu (Yerusalemu), Na walipofika kule biblia inatuambia wakawatokea watu wengi sana…
Lakini lipo swali tunaweza kujiuliza kulikuwa na umuhimu gani wale wafu watoke makaburini kwa kipindi kama kile, pili na ni kwanini walielekea mji mtakatifu Yerusalemu na sio mahali pengine..
Tusome.
Mathayo 27:50 “Naye Yesu akiisha kupaza sauti tena kwa nguvu, akaitoa roho yake.
51 Na tazama, pazia la hekalu likapasuka vipande viwili toka juu hata chini; nchi ikatetemeka; miamba ikapasuka;
52 makaburi yakafunuka; ikainuka miili mingi ya watakatifu waliolala;
53 nao wakiisha kutoka makaburini mwao, baada ya kufufuka kwake, wakauingia mji mtakatifu, wakawatokea wengi”.
Maswali kama hayo, tukiweza kuyatafakari vizuri naamini yatatupa mwanga wa jinsi siku ile kuu ya ufufuo wa wafu(katika unyakuo) itakavyokuwa.
Sasa ni kwanini, wakati ule makaburi yapasuke na watakatifu wafufuke,..Ni kwasababu Mungu alikuwa anataka kuwathibitishia baadhi ya wale watu wake, kuwa tendo la ufufuo lipo kweli, na mwanawe Yesu Kristo amefufuka kweli kweli.. Na alifanya hivyo ili baada ya hapo wakawe mashahidi wa ufufuo wa wafu kwa watu wengine..Kwasababu wakati huo yalikuwepo makundi mengi ya watu waliokuwa hawaamini suala la ufufuo wa wafu (Masadukayo), Na wengine walikuwa wanapinga na kuwatangazia watu kuwa ameibiwa..Hivyo ili Mungu kuwathibitishia kuwa suala la Ufufuo lipo ndipo akaruhusu makaburi yapasuke, wafu wafufuke waonekane na watu wengi.
Lakini Je! Hilo lilionekana na kila mtu tu?
Jibu ni Hapana, bali lilionekana na wale watu (watakatifu) waliokuwa Yerusalemu wakati ule. Kama tu vile Bwana alivyofufuka hakumtokea tu kila mtu isipokuwa wale waliokuwa wanamwamini. Na hao wafu ni hivyo hivyo hawakuwatokea watu wote isipokuwa tu wale watakatifu..
Kwasababu biblia inatuambia wafu wale walielekea Yerusalemu. Ni kwa vile tu biblia haiwezi kueleza kila kitu, lakini tukio lile liliwaacha katika butwaa kubwa sana wale watu waliokuwa Yerusalemu..Jaribu kufikiria, unatembea kila kona unawaona ndugu zako wa kale waliokufa katika Bwana, wengi sana, unawaona waliokuwa majirani zako kitambo, na wengine wanazungumza na wewe kabisa wanakuambia mimi ni Yusufu, mimi ni Sulemani, mimi ni Yeremia n.k…
Wewe unadhani watu hao walioshuhudia utaanzaje kuwaaninisha kuwa hakuna ufufuo wa wafu? kuwa Kristo hakufufuka bali aliibiwa?
Ufufuo huo uliwapa uthibitisho mkubwa sana, Ili kwamba wakawe mashahidi wa kufufuka kwake ulimwenguni kote, hilo ndio lilikuwa lengo lake..
Lakini upo ufufuo mwingine tunaoungojea sasa, ambapo upo karibu sana kutokea kuliko tunavyofikiria..Wakati huo PARAPARANDA kuu ya Mungu italia kutoka mbinguni..Na tukio kama lile lile la kwanza litatokea kwa mara nyingine, la makaburi kupasuka..Lakini safari hii watanyanyuka watakatifu wengi sana, wa vizazi vyote vilivyotangalia duniani..watu wengi sana..
Wakati huo watakatifu walio hai hawatajua chochote kwanza, wala ulimwengu pia..Ili lile Neno la kwamba hatutawatangulia wafu waliolala litimie..
1Wathesalonike 4:15 “Kwa kuwa twawaambieni haya kwa neno la Bwana, kwamba sisi tulio hai, tutakaosalia hata wakati wa kuja kwake Bwana, hakika HATUTAWATANGULIA wao waliokwisha kulala mauti.
16 Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; NAO WALIOKUFA KATIKA KRISTO WATAFUFULIWA KWANZA.
17 Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele.
18 Basi, farijianeni kwa maneno hayo”
Vivyo hivyo na wao hawataonekana na kila mtu tu aliye duniani…
wataonekana na watakatifu watakaonyakuliwa, (Yaani wale watu tu waliozaliwa mara ya pili ndio watakaowaona)..…na wenyewe wataenda katika mji mtakatifu (Yerusalemu ya rohoni, soma Wagalatia 4:24-31)…
Siku hiyo sisi tuliokuwa hai siku tutakapowaona, ndio tutakapojua kuwa Ufufuo wenyewe umefika, na kitendo cha kufumba na kufumbua tutatoweka, hatutaonekana tena ulimwenguni..
1Wakorintho 15:51 “ Angalieni, nawaambia ninyi siri; hatutalala sote, lakini sote tutabadilika,
52 kwa dakika moja, kufumba na kufumbua, wakati wa parapanda ya mwisho; maana parapanda italia, na wafu watafufuliwa, wasiwe na uharibifu, nasi tutabadilika”.
Wakati huo dunia haitaelewa chochote!. Wengi watasema wameibiwa, kama ilivyokuwa kipindi cha Bwana Yesu, wengine watasema tumepotea tu! Watapatikana n.k. Lakini suala la kwamba kanisa limenyakuliwa hilo halitaaminika na wengi hata kidogo. Kwasababu tutakuwa ni kundi dogo sana kama vile Bwana Yesu alivyosema.
Hivyo ndugu, mimi na wewe tujue kuwa tunaishi katika hayo majira ya Kunyakuliwa kwa kanisa, Dalili zote zinathibitisha hilo, hakuna asiyejua.. Lakini Swali ni Je! tumejiwekaje tayari? Je! Parapanda ikilia leo, unao uhakika wa kunyakuliwa? Kumbuka baada ya wakati huo mlango wa rehema hautakuwa tena wazi kwa ajili yetu, Bali kitakachokuwa kinaendelea duniani ni kumiminwa kwa ghadhabu ya Mungu. Na hukumu.
Muda bado tulio bakiwa nao mfupi sana. Hivyo ikiwa wewe ni mmojawapo ambaye Kristo yupo mbali na wewe, basi chukua uamuzi wa leo hii kumgeukia na atakupokea na kukufanya mwana wake.
Bwana akubariki sana.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
Kati ya Unyakuo,dhiki kuu, utawala wa miaka 1000 kipi kinaanza
Yesu akalia kwa sauti kuu..
Wengi tunajiuliza ni maneno gani aliyatoa Bwana Yesu pale msalabani alipolia kwa sauti ya juu namna hiyo?
Embu tusome vifungu vyenyewe;
Marko 15:34 “Na saa tisa Yesu akapaza sauti yake kwa nguvu, Eloi, Eloi, lama sabakthani? Maana yake, Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?
35 Na baadhi yao waliosimama pale, walisema, Tazama, anamwita Eliya.
36 Na mmoja akaenda mbio, akajaza sifongo siki, akaitia juu ya mwanzi, akamnywesha, akisema, Acheni, na tuone kwamba Eliya anakuja kumtelemsha.
37 NAYE YESU AKATOA SAUTI KUU, AKAKATA ROHO.
38 Pazia la hekalu likapasuka vipande viwili toka juu hata chini.
39 Basi yule akida, aliyesimama hapo akimwelekea, alipoona ya kuwa alikata roho jinsi hii, akasema, Hakika mtu huyu alikuwa Mwana wa Mungu”.
Ili kujua ni maneno gani aliyasema, ni vizuri tukaangalia katika vitabu vingine vya injili vinasema katika wakati huo huo alipokuwa anakaribia kukata roho Tusome..
Yohana 19:28 “Baada ya hayo Yesu, hali akijua ya kuwa yote yamekwisha kumalizika ili andiko litimizwe, akasema, Naona kiu.
29 Kulikuwako huko chombo kimejaa siki; basi wakatia sifongo iliyojaa siki juu ya ufito wa hisopo, wakampelekea kinywani.
30 Basi Yesu alipokwisha kuipokea ile siki, alisema, IMEKWISHA. Akainama kichwa, akaisalimu roho yake.”.
Unaona hapo mstari wa 30 unaonyesha dakika ile ya mwisho kabla ya kuikata roho yake alisema haya maneno “IMEKWISHA”..
Maneno haya hakuyasema kwa unyonge, au kwa utaratibu, au kwa sauti ya kawaida kama yale mengine..Hapana, bali alipofika hapo biblia inasema AKATOA SAUTI KUU.. IMEKWISHA.
Sauti ambayo kila mmoja aliyekuwa maeneo yale aliyasikia maneno haya..kiasi kwamba Yule akida wa askari alipoona jinsi alivyokata roho kwa Tamko zito kama lile..Akakiri kuwa Yule alikuwa kweli ni mwana wa Mungu.
Yesu akalia kwa sauti kuu,
Lakini kwanini Bwana Yesu aamue kufanya vile?,
Ilikuwa ni kutuambia mimi na wewe kuwa Ile hati ya mashitaka imekwisha. Na ndio maana saa ile ile pazia la hekalu likapasuka, na kiti cha rehema kikaonekana, ikiwa na maana kuwa tangu wakati wa Kristo kufa, rehema inapatikana bure, na kwa uwazi, sio tena nyuma ya pazia ambapo ilihitaji kuwepo na mtu wa kuwapatanisha na Mungu(Kuhani mkuu)..Lakini sasa hilo halipo tena, kwasababu hati ya mashitaka imeondolewa.
Mtu yeyote anaweza kumkaribia Mungu na kusamehewa kupitia YESU KRISTO.
Hivyo hata na wewe leo, kama ni mwenye dhambi unaweza kuupokea msamaha kutoka kwake hapo hapo ulipo. Yesu anaweza kuja ndani ya moyo wako siku hii hii ya leo, bila hata ya kuhani kuwepo karibu yako, au mchungaji, au mtu yeyote..Ni wewe tu kufungua moyo wako, na kukubali kumpokea Yesu.
Ikidhamiria kufanya hivyo alisema mwenyewe..
Yohana 6:37 “Wote anipao Baba watakuja kwangu; wala ye yote ajaye kwangu sitamtupa nje kamwe.”
Hivyo leo hii ukimpa maisha yako utaanza kuona badiliko la ajabu sana ndani yako. Kama upo tayari sasa kutubu dhambi zako..Basi fungua hapa kwa ajili ya sala ya toba. >>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Mada Nyinginezo:
Kwanini Bwana Yesu alisema pale msalabani naona kiu?
USO WAKE ULIKUWA UMEHARIBIWA SANA ZAIDI YA MTU YE YOTE.
KWANINI YESU KRISTO NI WA MUHIMU KWETU SASA?
WINGU KUBWA LA MASHAHIDI.
MKUU WA UZIMA AKUWEKE HURU.
Kuzimu kuna nini?
Kuzimu sio mahali pa kupatamani hata kidogo, wala sio mahali ambapo utatamani hata adui yako aingie..
Na ndio maana Bwana Yesu alisema maneno haya..
Marko 9:43 “Na mkono wako ukikukosesha, ukate; ni afadhali kuingia katika uzima u kigutu, kuliko kuwa na mikono miwili, na kwenda zako jehanum, kwenye moto usiozimika;
44 ambamo humo funza wao hafi, wala moto hauzimiki.]
45 Na mguu wako ukikukosesha, ukate; ni afadhali kuingia katika uzima, u kiwete, kuliko kuwa na miguu miwili, na kutupwa katika jehanum;
[ 46 ambamo humo funza wao hafi, wala moto hauzimiki.]
47 Na jicho lako likikukosesha, ling’oe, ulitupe; ni afadhali kuingia katika ufalme wa Mungu, una chongo, kuliko kuwa na macho mawili, na kutupwa katika jehanum;
48 ambamo humo funza wao hafi, wala moto hauzimiki”.
Unaona, akiwa na maana kuwa kama itabidi kiungo chako kimoja tu cha thamani, kiondoke ni heri ukafanya hivyo kuliko uende kuishia huko milele.
Ikiwa unataka kujua kwa Urefu Jehanum ni nini? Unataka kujua hao funza wanamaanisha nini?, kuzimu kuna nini ,fungua hapa usome Habari yao.. >>>> Jehanamu ni nini?
Haya Maisha tuliyopewa ni ya kitambo kifupi sana, tunapaswa tujitathimini tukifa leo tutakwenda wapi ikiwa tupo nje ya Kristo? Biblia inatuambia Kuzimu haishibi watu, wala uharibifu hauna kifuniko, ikiwa na maana kuwa kila dakika, kila sekunde watu wanashuka huko wengi sana..
Lakini kwanini hayo yote yatukute angali bado tunao muda wa kutubu? Tutubu dhambi zetu, na kuyasalimisha Maisha yetu kwake, tuseme ulimwengu sasa basi, leo hii tunamgeukia Kristo.
Hivyo Ikiwa wewe ni mmojawapo ambaye unasema leo nipo tayari kumpa Yesu Maisha yangu, basi uamuzi unaoufanya ni wa busara sana.
Basi, hapo ulipo, chukua muda mchache ujitenge peke yako. Kisha piga magoti, kisha fuatisha sala hii kwa Imani, ukijua kuwa Mungu yupo hapo karibu na wewe pembeni yako kukusikia..Kisha ukiwa sasa katika utulivu Sema sala hii kwa sauti.
EE MUNGU BABA, NAJA MBELE ZAKO, NIKIWA NINAJITAMBUA KUWA MIMI NI MKOSAJI NA NIMEKUTENDA DHAMBI NYINGI, NA KWAMBA NIMESTAHILI HUKUMU. LAKINI WEWE MUNGU WANGU ULISEMA KATIKA NENO LAKO KUWA WEWE NI MUNGU WA REHEMA UNAYEWAREHEMU MAELFU ELFU YA WATU WANAOKUPENDA WEWE. NA LEO HII NINAKUJA MBELE ZAKO NAHITAJI MSAMAHA WAKO NA MSAADA WAKO MUNGU WANGU, NINATUBU DHAMBI ZANGU ZOTE KWA KUMAANISHA NA KWA MOYO WANGU WOTE, NINAKIRI KUWA YESU KRISTO NI BWANA, NA YEYE NDIYE MWOKOZI WA HUU ULIMWENGUNI. HIVYO NAOMBA DAMU YA MWANAO TAKATIFU INISAFISHE UOVU WANGU WOTE SASA NIFANYIKE KUWA KIUMBE KIPYA KUANZIA LEO NA HATA MILELE.
ASANTE BWANA YESU KWA KUNIPOKEA NA KUNISAMEHE.
AMEN.
Sasa ikiwa umefuatisha sala hiyo kwa Imani ..Hatua iliyobakia kwako ni kuithitisha toba yako kwa Vitendo ikiwa ulikuwa unafanya mambo yote ambayo hayampendezi Mungu unayaacha na kujitenga nayo, Sasa Mungu akishaona umegeuka kwa vitendo basi toba yako anaipokea na atakuwa na uhalali kwa kuja ndani yako wakati huo huo na kufanya makao ya milele kwako.
Vile vile unahitaji, kutafuta kanisa la kiroho ambalo utajumuika na wakristo wengine katika kumwabudu Mungu, na kujifunza biblia ili uukulie wokovu. Na vilevile ili upate ubatizo sahihi wa kuzamishwa katika maji mengi na kwa jina la YESU KRISTO kwa ajili ya ondoleo la dhambi zako.
Hongera kwa kuokoka.
Pia nakualika kutembelea tovuti hii mara kwa mara, yapo mafundisho mengi zaidi ya 1000, na maswali mengi sana yaliyojibiwa ya kwenye biblia..
Au kama utakuwa unapenda utumiwe kwa njia ya whatsapp basi utatumia ujumbe katika namba hii +255789001312 .. Bwana akubariki sana.
Mada Nyinginezo:
MADHARA YA KUKOSA MAJI YA UZIMA BAADA YA KIFO.
DHIKI KUU INAKUJA NA UNYAKUO UPO KARIBU.
CHUKIZO LA UHARIBIFU
MAPIGO YA VITASA SABA, NA SIKU YA BWANA.
UTAWALA WA MIAKA 1000.
HAPO NDIPO WATU WALIPOANZA KULIITIA JINA LA BWANA.
Kuota upo mtu na maarufu/kuota unaongea na mtu maarufu kuna maana gani?
Ndoto zipo katika makundi makuu matatu, zipo ndoto zinazotokana na Mungu, pia zipo ndoto zinazotokana na shetani, halikadhalika zipo ndoto zinazotokana na mtu mwenyewe.
Ili kufahamu vizuri juu ya makundi haya. Bofya hapa usome. >>> Nitajuaje kama ndoto ni ya Mungu au ya Shetani?
Wengi wetu tunakosa shabaha pale tunapotaka kila ndoto ipatiwe tayari yake ya rohoni, lakini ukweli ni kwamba si kila ndoto inayotafsiri ya maana, husususani hizo zinazotokana na sisi wenyewe.
Sasa tukirudi kwenye swali Kuota upo na mtu maarufu/kuota unaongea na mtu maarufu kuna maana gani?
Jibu ni kwamba, ndoto nyingi za namna hii zinatokana na shughuli zetu za kila siku
Mhubiri 5:3 “Kwa maana ndoto huja kwa sababu ya shughuli nyingi; na sauti ya mpumbavu kwa njia ya wingi wa maneno”
Unaona Shughuli za kila siku ni Pamoja na yale mambo ambayo tunayoana mara kwa mara kila siku, au tunayasikia, kwamfano mtu kama raisi wa nchi, huyu ni mtu ambaye karibu kila siku tunamwona katika vyombo vya Habari, au tunamsikia katika radio, au tunamsoma katika magazeti, au tunamsikia akizungumziwa na watu wengine..
Ni mtu ambaye kila mmoja wetu amemkaa kichwani, kama vile tu ndugu zetu wa nyumbani. Hivyo mtu kuota raisi wa nchi, au kuota unaongea na raisi,au kuota uko na raisi si jambo la kushangaza.
Naamini ni maelfu ya watu kila siku yanamuota raisi wa nchi yao.
Na sio raisi tu, unaweza kumwota mtu mwingine yoyote maarufu, ambaye tayari anajulikana sana katika jamii, inaweza ikawa ni msanii, au mbunge, au mchungaji, au mchezaji n.k.
Hivyo ndoto ya namna hii, ikikujia usiitilie maanani sana.
Lakini ikija katika uzito wa hali ya juu, na ndoto yenyewe umeiota imeonekana kama ilikuwa ni kweli. Na ukaona kama ni bahati umekutana na mtu huyo,
Basi ujue ni Mungu anataka kukupa hisia Fulani ya kipekee uionje pale unapokutana na mtu Fulani maarufu. Anataka uone, jinsi inavyokuwa, ikiwa watu maarufu wa dunia hii ukikutana nao unajihisi wewe ni mtu Fulani spesheli uliyepata bahati, vipi kuhusu kukutana na yeye ambaye ni Maarufu na Mkuu kuliko watu wote na vitu vyote duniani siku ile? Utakuwa katika hali gani?
Anataka uone siku ile maelfu kwa maelfu wa watu watakapo kusanyika mbele zake , kupokea heshima zao kutoka kwake wewe utakuwa wapi?
Je! atakuita, uwe karibu naye, au atakukataa na kukufukuza?
Bwana Yesu mwenyewe alisema..
Luka 9:26 “Kwa sababu kila atakayenionea haya mimi na maneno yangu, Mwana wa Adamu atamwonea haya mtu huyo, atakapokuja katika utukufu wake na wa Baba na wa malaika watakatifu”.
Hivyo usimwonee haya Kristo mpe leo Maisha yako. Ili siku ile, atakapopokea heshima kutoka kwa watu wote na malaika zake, basi na wewe pia akuite.
Hiyo ndio maana ya Kuota upo na mtu maarufu/kuota unaongea na mtu maarufu.
Hivyo Kama upo tayari kumpa Yesu Maisha yako leo, utataka kuongozwa sala ya toba basi fungua hapa >>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Ubarikiwe sana..
Kwa mgawanyo bora wa masomo download App hapa>> App wingu la mashahidi
Mada Nyinginezo:
KARAMU YA MWANA-KONDOO.
BASI MUNGU ALIMWADHIMISHA MNO.
MFALME ANAKUJA.
KWANINI YESU KRISTO NI WA MUHIMU KWETU SASA?
MTINI, WENYE MAJANI.
Uasherati wa Kiroho maana yake nini?
Kuota unakojoa kitandani kuna maanisha nini?
Ndio ni kweli zipo ndoto zinazotokana na Mungu, na ni vizuri kuzifahamu hizo, na pia zipo ndoto zinazotokana na shetani pia hizo ni vizuri ukazifahamu.. Kama utahitaji kuzijua kwa undani bofya hapa >> Nitajuaje kama ndoto ni ya Mungu au ya Shetani?
Lakini kuna ndoto pia ambazo hazitokani na Mungu wala shetani bali zinatokana na sisi wenyewe.. Na hizo ndizo tunazoziota katika Maisha yetu kwa sehemu kubwa, naweza kusema hata Zaidi ya asilimia 90.
Tatizo linakuja ni pale watu wanapotaka ndoto zinazotokana na sisi wenyewe basi wapate tafsiri yake ya kiroho. Hilo ndio linalowafanya wengi waangukie katika tafsiri za uongo.
Lakini leo ni vizuri ukaujua ukweli juu ya ndoto za kuota unakojoa kitandani.
Biblia inasema.
Isaya 29:8 “Tena itakuwa kama mtu mwenye njaa aotapo, kumbe, anakula; lakini aamkapo, nafsi yake haina kitu; na kama mtu mwenye kiu aotapo, kumbe, anakunywa; lakini aamkapo, kumbe, anazimia, na nafsi yake inatamani; hivyo ndivyo utakavyokuwa huo wingi wa mataifa waletao vita juu ya mlima Sayuni”.
Umeuelewa mstari huo?
Ndoto kama hizi za ukota unakojoa kitandani ni ndoto zinazotokana na mwili wenyewe. Na hiyo inakuja pale kibofu chako kinapojaa sana mkojo, Na hapo ndipo ubongo wako unatengeneza matukio ambayo yatakufanya ujione kama unajiokojolea ili tu aumke, uende ukakoje.. Na kama mwili utakuwa umezidiwa sana, na ndio hapo unakuta mtu anajikojolea kweli, aidha sana au kidogo.
Mwingine utakuta anaota anakojoa mkojo ambao hauishi, au kila saa anakojoa kojoa, unaona yote hiyo mifumo tu ya mwili.
Kama vile unapolala na njaa, usiku utajiona unatafuta chakula, au unakula haushibi, huo ni mfumo wa ubongo, kukuarifu kuwa mwili unahitaji chakula. Vivyo hivyo unapojikuta katika ndoto ya kuota unakojoa kitandani, hupaswi kuwa na hofu au wasiwasi.
Ipuuzie tu, na kama inakuja mara kwa mara, hakikisha ulalapo hunywi maji mengi, au vitu vyenye maji maji, na kwa kufanya hivyo hutakaa uone tena ikikurudia.
Hivyo kuota unakojoa kitandani ni ndoto ya ubongo wetu wenyewe. Ipuuzie
Shalom.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Mada Nyinginezo:
HAPO NDIPO WATU WALIPOANZA KULIITIA JINA LA BWANA.
KIFO CHA REINHARD BONKEY KINAACHA UJUMBE GANI KWETU?
JISHUSHE ILI MUNGU AKUHUDUMIE.
WACHUNGAJI WA BWANA MAKONDENI.
KILA MMOJA WENU AJUE KUUWEZA MWILI WAKE.
Kwanini Mungu anasema “Afanyaye malaika zake kuwa pepo”?
ZIKIMBIE TAMAA ZA UJANANI! NA MTU YEYOTE ASIUDHARAU UJANA WAKO.
Kuota umefunga ndoa kuna maanisha nini?
Ndoto ya namna hii mara nyingi inaangukia katika kundi la ndoto zinazozotokana na shughuli nyingi..
Mhubiri 5:3 “Kwa maana ndoto huja kwa sababu ya shughuli nyingi; na sauti ya mpumbavu kwa njia ya wingi wa maneno”.
Na hii inatokana na kwamba pengine umekuwa ukiwaza kuoa au kuolewa hivi karibuni, au umekuwa ukitamani sana kuoa au kuolewa kwa muda mrefu lakini bado malengo yako ya ndoa hujayafikia, au umehudhuria ndoa nyingi, au umezitazama, n.k.
Hivyo siku zote zile unachokifanya sana, au unachokiwaza sana, ni lazima kitajirudia tu katika ndoto zako, kama sio mara moja basi ni mara kwa mara, hilo ni jambo la kawaida.
Kwa mfano utakuta mwingine amekuwa akitafuta sana ajira kwa muda mrefu, au amekuwa akiwaza sana ajira kwa muda mwingi, hivyo mtu kama huyu kuota yupo kwenye interview litakuwa ni jambo la kawaida kwake..
Na ndivyo vivyo hivyo katika kuota umefunga ndoa..mara nyingi ni ndoto itokanayo na shughuli za kila siku.
Lakini pia lipo jambo lingine la rohoni unapaswa ujue. Kumbuka kuwa Mungu huwa anazungumza pia na watu katika ndoto kwa kupitia Maisha ya kawaida kabisa ya siku zote. Hivyo Ikiwa ndoto hii ya kuota umefunga ndoa imekujia kwa uzito wa kitofauti..
Na ukaifarahia hiyo ndoa na ukatamani ingekuwa hivyo kweli, Fahamu kuwa Mungu anakuonyesha kuwa ipo HARUSI ILIYO BORA NA KUU kuliko hiyo, inayokuja huko mbele. Na hiyo si nyingine Zaidi ya mwanakondoo (Yesu Kristo na kanisa lake)
Hilo usilisahau hata kidogo, katika Maisha yako. Kwasababu biblia inatuambia itakuwa ni Harusi ya pekee sana, ambayo karamu yake itafanyika mbinguni. Wakati huo wapo watu watatamani kuingia lakini waseweze, kitakachobakia kwao ni kilio na kusaga, kwa kuikosa tu.
Harusi hiyo ya Bwana Yesu na kanisa lake sio kama hii ya kimwilini, hapana, bali itakuwa ni ya rohoni, ambapo ndoa inaanzia hapa hapa duniani, na karamu itakuwa ni mbinguni.
Huko ndipo tutakapokutana na mambo ambayo jicho halijawahi kuona wala sikio kusikia..ili kufahamu vizuri jinsi karamu hiyo itakavyokuwa..Fungua hapa >>>>> KARAMU YA MWANAKONDOO
Fahmu kuwa Hizi ni nyakati za mwisho, Unyakuo upo karibu, Yesu yupo mlangoni kurudi, kulinyakua kanisa lake Je! Umeokoka? Umemkabidhi Maisha yako? Kama bado ni vizuri ukafanya uamuzi huo sasa, kukutana na ujumbe huu sio bure.Bali Mungu anayo malengo makubwa na wewe maishani mwako… Fanya hima nawe pia usionekane umeikosa siku ile ya Harusi kuu ya mwana-kondoo.
Ufunuo 19:7 “Na tufurahi, tukashangilie, tukampe utukufu wake; kwa kuwa arusi ya Mwana-Kondoo imekuja, na mkewe amejiweka tayari.
8 Naye amepewa kuvikwa kitani nzuri, ing’arayo, safi; kwa maana kitani nzuri hiyo ni matendo ya haki ya watakatifu.
9 Naye akaniambia, Andika, Heri walioalikwa karamu ya arusi ya Mwana-Kondoo. Akaniambia, Maneno haya ni maneno ya kweli ya Mungu”
Shalom.
Kwa mgawanyo bora wa masomo download App hapa>> App wingu la mashahidi
Mada Nyinginezo:
Maombi ni nini?
Neno maombi limetokana na neno kuomba, Kwamfano mtu unapokuwa na hitaji ya kitu Fulani, labda tuseme kazi, basi huwa unatuma maombi yako kwanza kwenye ofisi husika au shirika, kisha wanapitia wasifu wako na kule wakisharidhiwa na maombi yako ndio wanakurudishia majibu ya kile ulichokiomba.
Kamwe huwezi ukapeleka maombi ya kazi, halafu yakarudi majibu ya mkopo, ya ufadhili, au ya kupewa bima badala yake..Hilo jambo halipo, kwa namna ya kawaida chochote kile unachokiomba ndicho utakachopewa, ukiomba ajira utarudishiwa majibu ya ajira, ukiomba mkopo utarudishiwa majibu ya mkopo, ukomba zabuni utarudishwa majibu ya zabuni, kamwe haiwezi ikavuka hapo.
Maombi ni nini katika ukristo?
Lakini katika Ukristo Maombi, yanavuka hiyo mipaka, hayalengi tu kupeleka hitaji na kujibiwa, halafu basi.. Bali yanakwenda mbele Zaidi na kufanya kazi nyingine nyingi kuliko hizo, na ndio maana maombi ni nyenzo muhimu sana kwa mtu yeyote anayejiita mkristo. Bila maombi umekwisha.
Watu wengi wanadhani, Mungu anakitazama tu kile tunachokwenda kumwomba kwa wakati huo halafu atujibu iwe imeisha..ni vizuri tukafahamu kuwa kabla hata hatujamwomba Mungu chochote, tayari alishajua ni nini tunachokwenda kumwomba..
Mathayo 6:7 “Nanyi mkiwa katika kusali, msipayuke-payuke, kama watu wa mataifa; maana wao hudhani ya kuwa watasikiwa kwa sababu ya maneno yao kuwa mengi. 8 Basi msifanane na hao; maana Baba yenu anajua mnayohitaji kabla ninyi hamjamwomba”.
Hivyo mbele za Mungu, maombi ni ziadi ya kile tunachokifikiria. Ikiwa anajua tayari tunachokwenda kumwomba, unaweza ukajiuliza ni kwanini sasa atusumbue tuende tukamwombe?..Hapo ndipo utakapojua kuwa maombi kwa Mungu ni Zaidi ya kupeleka mahitaji.
Maombi ni nini..
Pale unapopiga magoti na kumwambia Mungu hiki na kile, hafamfikii tu kama mahitaji peke yake, bali yanajitafsiri kama kitu kingine pia..yanafika kwake kama harusi nzuri ya manukato, kama sauti ya upole ya kumwita aje ndani yako, kuku rehema, kukupa neema zake, kukuponya n.k. Na hiyo inamfanya Mungu ashuke, na kuanza kuifanya kazi yake ndani ya maisha yako, ambayo hata wewe usiyoyajua..zaidi ya yale aliyokuwa anayaomba.
Na kwa jinsi unavyodumu zaidi katika maombi, ndivyo Mungu anavyotenda kazi zaidi ndani yako.
Mtu ambaye ni mwombaji mzuri, kamwe hawezi kushindwa na majaribu ya shetani, Bwana Yesu alishasema hivyo. Mtu ambaye ni mwombaji mzuri, huwa nyingi maishani mwake zza mambo ya ajabu ambayo Mungu amemtendea..Vilevile mtu ambaye ni mwombaji mzuri huwa unakutana na Mungu sana katika njia zake.
Tofauti na Yule ambaye haombi kabisa.. Huyo ni sawa na gari linalotembelewa miaka 20 halipelekwi gereji.
Biblia inasema..
1Wathesalonike 5:16 “Furahini siku zote; 17 ombeni bila kukoma;”
Maombi ni nini? Maombi ni kama karakana ya Mungu ndani ya moyo wa mwanadamu, pale tunapokwenda kuomba, anashuka kuyakarabati Maisha yetu..Hivyo suala la maombi ni jambo linalotakiwa liwe sehemu ya Maisha yetu na sio pale tu tunapojisikia.
Bwana wetu Yesu japo alikuwa ni Mungu katika mwili mkamilifu lakini alikuwa ni mwombaji mkubwa sana..
Luka 6:12 “Ikawa siku zile aliondoka akaenda mlimani ili kuomba, akakesha usiku kucha katika kumwomba Mungu. 13 Hata kulipokuwa mchana aliwaita wanafunzi wake; akachagua kumi na wawili miongoni mwao, ambao aliwaita Mitume”;
Na ndio huyo huyo alituambia..
Marko 14:38 “Kesheni mwombe, msije mkaingia majaribuni, roho i radhi ila mwili ni dhaifu”
Hivyo kama wewe umeokoka na sio mwombaji ni vizuri ukaanza sasa. Na Bwana alitupa kiwango cha kuomba cha siku ambacho walau kila mwaminio anapaswa akifanye..Nacho ni SAA MOJA kwa siku. Luka 14:37..Unaweza ukaona ni kirefu lakini ukijua kuwa yapo mambo mengi ya kuombea hutaona ni kirefu.
Maombi ni nini
Lakini ikiwa bado upo nje ya Kristo, Mungu hawezi kuyaumba Maisha yako vile anavyotaka, Lakini kama leo upo tayari kumkaribisha katika Maisha yako, basi uamuzi unaoufanya ni sahihi..
Bofya hapa kwa ajili ya sala ya toba..>> SALA YA TOBA
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
FAIDA ZA MAOMBI YA USIKU
MAOMBI YA VITA
ZIFAHAMU HOJA SABA ZENYE NGUVU MBELE ZA MUNGU.
DHIKI KUU INAKUJA NA UNYAKUO UPO KARIBU.
UTAWALA WA MIAKA 1000.
NYAKATI SABA ZA KANISA NA WAJUMBE WAKE.
UTOE MWILI WAKO KWA BWANA KWASABABU SI MALI YAKO.