Jibu: Tusome..
Warumi 12:11 “kwa BIDII, si walegevu; mkiwa na JUHUDI katika roho zenu; mkimtumikia Bwana”
“Bidii” ni hamasa/msukumo wa ndani wa kufanya jambo fulani… na mtu anaweza kuwa na bidii lakini asiwe na juhudi.
Kwamfano mtu anaweza kwa na bidii kubwa katika kupanga mambo, lakini katika utekelezaji akashindwa.
Lakini “Juhudi” yenyewe inakwenda mbali zaidi katika utekelezaji kwa vitendo, kwamfano mtu anaweza kuwa na bidii ya kuweka mikakati ya kilimo na mipango, na baadaye akafanya juhudi katika kilimo kwa kuingia shambani na kulima.
Mtu anaweza kuwa na bidii ya kununua vitabu vingi vya imani vya kumsaidia kukua kiroho na akaonyesha “juhudi” ya kuvisoma vile vitabu na akazalisha kitu katika maisha yake ya kiroho… au mtu anaweza kuwa na bidii nyingi kujua mafundisho ya upendo, imani, maombi au wokovu lakini kama hatakuwa na “juhudi” ya kuishi au kukitenda kile anachojifunza au kikosoma “bidii” yake ni bure..
Biblia inatufundisha kuwa na bidii na juhudi pia katika mambo yote..
Usiwe na bidii na kukosa Juhudi kwani Juhudi ni ngazi ya msingi sana kufikia lengo la kiroho..
Tito 2:14 “ambaye alijitoa nafsi yake kwa ajili yetu, ili atukomboe na maasi yote, na kujisafishia watu wawe milki yake mwenyewe, wale WALIO NA JUHUDI KATIKA MATENDO MEMA”.
Kwahiyo sio tu BIDII katika kusoma, bali pia na JUHUDI katika kutenda, ndivyo Biblia inavyotufundisha..
1Petro 3:13 “Naye ni nani atakayewadhuru, mkiwa wenye juhudi katika mema?”
1Petro 4:8 “Zaidi ya yote iweni na juhudi nyingi katika kupendana; kwa sababu upendano husitiri wingi wa dhambi”.
Bwana atusaidie.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Ipi tofauti ya Kukemea na kukaripia? (2Timotheo 4:2)
Ipi Tofauti ya Agano jipya na Agano la Kale?.
Ipi tofauti ya utakatifu na utukufu?
Ipi tofauti ya Falme, Mamlaka na Wakuu wa giza (Waefeso 6:12)
Ipi tofauti ya Hasira na Ghadhabu ya MUNGU?.
Print this post