Shalom.. Karibu tujifunze Biblia pamoja.
Zipo nyakati Ngumu ambazo kama mkristo utazipitia, ni nyakati za dhiki, na vilio wakati mwingine…na nyakati hizo haimaanishi kuwa Mungu kakuacha, hapana!, ni iko namna hiyo tu.… maana maandiko yanasema tumewekewa hizo, ingawa ni za kitambo tu.
1Wathesalonike 3:3 “mtu asifadhaishwe na dhiki hizi; maana ninyi wenyewe mnajua ya kuwa twawekewa hizo. 4 Kwa kuwa tulipokuwapo kwenu tulitangulia kuwaambia kwamba tutapata dhiki, kama ilivyotukia, nanyi mwajua”.
1Wathesalonike 3:3 “mtu asifadhaishwe na dhiki hizi; maana ninyi wenyewe mnajua ya kuwa twawekewa hizo.
4 Kwa kuwa tulipokuwapo kwenu tulitangulia kuwaambia kwamba tutapata dhiki, kama ilivyotukia, nanyi mwajua”.
Sasa inapotokea umekutana na dhiki, au majaribu na huku ukijitazama upo sawa kiimani, na wala hujarudi nyuma, ni nini cha kufanya?
Jambo ni moja tu, nalo ni kusimama na kuendelea mbele na si kuendelea kulia (USIKATE TAMAA)…… Machozi yapo kweli, lakini hayawezi kukusaidia sana wakati wa majaribu, bali ujasiri na kusimama ndio kuendelea mbele ndio Nguvu ya kuvuka huo wakati.
Tujifunze kwa habari ya Daudi kabla hajawa mfalme. Maandiko yatuambia, kuna siku alirudi mjini mwake akakuta mji umevamiwa na Waamaleki na wake zake wamechukuliwa mateka pamoja na mali zao, ilikuwa ni kilio kikubwa cha uchungu mkubwa, na Daudi pamoja na wenzake walilia sana..
1Wafalme 30:1 “Ikawa, Daudi na watu wake walipokuwa wamefika Siklagi siku ya tatu, hao Waamaleki walikuwa wameshambulia Negebu, na Siklagi, nao wameupiga Siklagi, na kuuchoma moto; 2 NAO WAMEWACHUKUA MATEKA WANAWAKE WALIOKUWAMO WAKUBWA KWA WADOGO; HAWAKUWAUA WO WOTE, ILA WAKAWACHUKUA, WAKAENDA ZAO. 3 Basi Daudi na watu wake walipoufikilia mji, tazama, ulikuwa umechomwa moto; na wake zao, na watoto wao, waume kwa wake, wamechukuliwa mateka. 4 Ndipo Daudi na watu waliokuwa pamoja naye WAKAINUA SAUTI ZAO NA KULIA, HATA WALIPOKUWA HAWANA NGUVU ZA KULIA TENA 5 Na hao wake wawili wa Daudi walikuwa wamechukuliwa mateka, Ahinoamu wa Yezreeli, na Abigaili, aliyekuwa mkewe Nabali, wa Karmeli ”.
1Wafalme 30:1 “Ikawa, Daudi na watu wake walipokuwa wamefika Siklagi siku ya tatu, hao Waamaleki walikuwa wameshambulia Negebu, na Siklagi, nao wameupiga Siklagi, na kuuchoma moto;
2 NAO WAMEWACHUKUA MATEKA WANAWAKE WALIOKUWAMO WAKUBWA KWA WADOGO; HAWAKUWAUA WO WOTE, ILA WAKAWACHUKUA, WAKAENDA ZAO.
3 Basi Daudi na watu wake walipoufikilia mji, tazama, ulikuwa umechomwa moto; na wake zao, na watoto wao, waume kwa wake, wamechukuliwa mateka.
4 Ndipo Daudi na watu waliokuwa pamoja naye WAKAINUA SAUTI ZAO NA KULIA, HATA WALIPOKUWA HAWANA NGUVU ZA KULIA TENA
5 Na hao wake wawili wa Daudi walikuwa wamechukuliwa mateka, Ahinoamu wa Yezreeli, na Abigaili, aliyekuwa mkewe Nabali, wa Karmeli ”.
Sasa baada ya Daudi na wenzake kulia mpaka machozi yalipoisha ni kitu gani kilitokea….tuendelee…
6 Naye Daudi akafadhaika sana; kwa sababu watu walikuwa wakisema kwamba apigwe kwa mawe, kwa maana nafsi za hao watu wote walisononeka, kila mtu kwa ajili ya wanawe na binti zake; lakini Daudi ALIJITIA NGUVU KATIKA BWANA, MUNGU WAKE. 7 Kisha Daudi akamwambia Abiathari, kuhani, mwana wa Ahimeleki, Tafadhali niletee hapa hiyo naivera. Naye Abiathari akamletea Daudi naivera huko. 8 Daudi akauliza kwa Bwana, akasema, Je! Nikiwafuata jeshi hili, nitawapata? Naye akamjibu, Fuata; kwa kuwa hakika utawapata, nawe hukosi utawapokonya wote…………….. 16 Na hapo alipokuwa amewaongoza chini, tazama, hao walikuwa wametawanyika juu ya nchi yote, wakila na kunywa, na kufanya karamu, kwa sababu ya hizo nyara kubwa walizochukua katika nchi ya Wafilisti, na katika nchi ya Yuda. 17 Naye Daudi akawapiga tangu ukungu wa jioni hata jioni ya siku ya pili; hakuna aliyeokoka, ila vijana mia nne waliopanda ngamia na kukimbia. 18 DAUDI AKAWAPOKONYA WOTE WALIOKUWA WAMECHUKULIWA NA WAAMALEKI; NAYE DAUDI AKAWAOKOA WAKEZE WAWILI. 19 Wala hawakupotewa na kitu, mdogo wala mkubwa, wana wala binti, nyara wala cho chote walichojitwalia hao; Daudi akavirudisha vyote”.
6 Naye Daudi akafadhaika sana; kwa sababu watu walikuwa wakisema kwamba apigwe kwa mawe, kwa maana nafsi za hao watu wote walisononeka, kila mtu kwa ajili ya wanawe na binti zake; lakini Daudi ALIJITIA NGUVU KATIKA BWANA, MUNGU WAKE.
7 Kisha Daudi akamwambia Abiathari, kuhani, mwana wa Ahimeleki, Tafadhali niletee hapa hiyo naivera. Naye Abiathari akamletea Daudi naivera huko.
8 Daudi akauliza kwa Bwana, akasema, Je! Nikiwafuata jeshi hili, nitawapata? Naye akamjibu, Fuata; kwa kuwa hakika utawapata, nawe hukosi utawapokonya wote……………..
16 Na hapo alipokuwa amewaongoza chini, tazama, hao walikuwa wametawanyika juu ya nchi yote, wakila na kunywa, na kufanya karamu, kwa sababu ya hizo nyara kubwa walizochukua katika nchi ya Wafilisti, na katika nchi ya Yuda.
17 Naye Daudi akawapiga tangu ukungu wa jioni hata jioni ya siku ya pili; hakuna aliyeokoka, ila vijana mia nne waliopanda ngamia na kukimbia.
18 DAUDI AKAWAPOKONYA WOTE WALIOKUWA WAMECHUKULIWA NA WAAMALEKI; NAYE DAUDI AKAWAOKOA WAKEZE WAWILI.
19 Wala hawakupotewa na kitu, mdogo wala mkubwa, wana wala binti, nyara wala cho chote walichojitwalia hao; Daudi akavirudisha vyote”.
Unapofika wakati umeishiwa nguvu, huo ndio wakati wa KUJITIA NGUVU!.. kwasababu maandiko yanatufundisha kuwa “tulipo dhaifu, ndipo tulipo na nguvu (2Wakorintho 12:10)”
Laiti Daudi angeendelea kulia pale bila kuchukua hatua yoyote, wale watu wangempiga mawe, au hata wasingempiga kwa mawe, bado asingewapata wake zake na mali zake, lakini ALIPOJITIA NGUVU KWA BWANA ndipo nguvu ikaongezeka kwake na Bwana akamsaidia.
Ukipitia majaribu ya afya jitie nguvu endelea mbele na maombi, pia ishi kwa ujasiri kana kwamba huumwi, na utaona maajabu makuwa….
Ukipitia majaribu ya familia jitie nguvu kwa Bwana endelea na maombi na kutafuta masuluhisho Bwana atakuwa nawe,
Ukipitia majaribu ya watoto au ndoa jitie nguvu kwa Bwana,
Ukipitia majaribu ya huduma jitie nguvu kwa Bwana songe mbele,
Ukipitia majaribu ya kipato vile vile jitie nguvu kwa Bwana songe mbele, zidi kumwomba Bwana wala usikate tamaa, njia itaonekana tu na milango itafunguka, haijalishi umeshapita muda gani… na magumu mengine yote fahamu kuwa ni ya kitambo, lakini ujasiri wako kwa Bwana unahusika sana huo wakati.
Bwana atusaidie.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
JIPE MOYO MKUU.
USIKATE TAMAA UNAPOPITIA MAGONJWA.
NI JAMBO GANI LINALOMTAMANISHA SANA BWANA TUMWOMBE BILA KUKATA TAMAA?
Kwanini kuna mrudio wa uumbaji kwenye Mwanzo sura ya pili?
LAKINI NINYI, NDUGU, MSIKATE TAMAA KATIKA KUTENDA MEMA.
Print this post