SWALI: Nini maana “nitawabariki wakubarikio, naye akulaaniye nitamlaani;”..Je! Ni kwa namna gani tunapaswa tulibariki taifa la Israeli. Je! Ili tubarikiwe tunapaswa, tufunge na kuliombea Taifa la Israeli usiku na mchana, au tuwe na bendera za taifa lile makanisani kwetu au majumbani mwetu?.
Ni kwa namna gani tutapokea Baraka kwa kulibariki tu taifa hilo?
JIBU: Maneno hayo, kwa mara ya kwanza tunaona Mungu akiyatamka kwa Ibrahimu katika;
Mwanzo 12:1 “Bwana akamwambia Abramu, Toka wewe katika nchi yako, na jamaa zako, na nyumba ya baba yako, uende mpaka nchi nitakayokuonyesha; 2 nami nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, na kukubariki, na kulikuza jina lako; nawe uwe baraka; 3 nami nitawabariki wakubarikio, naye akulaaniye nitamlaani; na katika wewe jamaa zote za dunia watabarikiwa”.
Mwanzo 12:1 “Bwana akamwambia Abramu, Toka wewe katika nchi yako, na jamaa zako, na nyumba ya baba yako, uende mpaka nchi nitakayokuonyesha;
2 nami nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, na kukubariki, na kulikuza jina lako; nawe uwe baraka;
3 nami nitawabariki wakubarikio, naye akulaaniye nitamlaani; na katika wewe jamaa zote za dunia watabarikiwa”.
Maandiko hayo hayatupi tafsiri ya kwamba tukeshe kuliombea taifa la Israeli usiku na mchana ili tubarikiwe, hapana utaona maneno hayo, Mungu alisema akilenga wakati ambapo watu wanapanga kuliangusha, au kuliporomosha au kuliletea vitisho taifa hilo, aidha kwa kulivamia, au kuliloga, n.k. kwa namna yoyote ile, hapo ndipo anayejaribu kufanya hivyo anakumbushwa,kuwa aibarikiye Israeli, atabarikiwa, na ailaaniye Israeli atalaaniwa.
Jambo kama hilo tunalithibitisha kwa Yule Balaamu mchawi, ambaye aliajiriwa na Balaki, ili aende kuwalaani Israeli, (yaani kuwaloga) kwa ushirikina ili wasifanikiwe kuvuka katika nchi ya Balaki. Lakini Ilikuwa nusura Mungu amuue Yule Balaamu, kwa kitendo tu hicho cha kujaribu kuliloga taifa teule. Kinyume chake ikabidi alibariki ili tu awe salama..Mpaka yeye mwenyewe akakiri,na kusema hapana uchawi katika Israeli wala uganga..
Hesabu 23:21 “Hakutazama uovu katika Yakobo, Wala hakuona ukaidi katika Israeli. Bwana, Mungu wake, yu pamoja naye, Na sauti kuu ya mfalme i katikati yao. 22 Mungu amewaleta kutoka Misri, Naye ana nguvu kama nguvu za nyati”.
Hesabu 23:21 “Hakutazama uovu katika Yakobo, Wala hakuona ukaidi katika Israeli. Bwana, Mungu wake, yu pamoja naye, Na sauti kuu ya mfalme i katikati yao.
22 Mungu amewaleta kutoka Misri, Naye ana nguvu kama nguvu za nyati”.
Hiyo ni kuonyesha kuwa, hata sasa yapo mataifa mengi ambayo yameshatangaza uadui na Israeli, mojawapo ni Somalia, na Libya, embu yaangalie mataifa hayo leo hii yapoje., na hiyo yote ni kwasababu yamejaribu kuleta vita na vitisho kwa taifa teule la Mungu, na matokeo yake ni kuwa yamepigwa, kila kukicha ni vita. Na mengine yanalitamkia maneno ya laana kama vile Palestina,, na mengine kuliwekea vikwazo. Embu Yatazame ustawi wao hayo mataifa au hao watu leo hii walivyo.
Halikadhalika, taifa ambalo halitaki shari na Israeli, bali linalitakia mema amani na mafanikio daima, basi taifa hilo au Mtu huyo Mungu atambariki. Hivyo umeona hapo, inalenga katika habari ya amani na shari, yaani pale ambapo unalazimishwa utamke mabaya, uwalaani, uwatukane, au upigane vita kinyume chao, hapo unapaswa uende kinyume chake, uwabariki, na kuwatakia amani. Ndipo utakapobarikiwa.
Lakini sio kuacha kufuata kanuni za Mungu za kimaandiko na kukesha kuliombea taifa la Israeli ili tubarikiwe. Mpaka tunasafiri kwenda kule Yerusalemu, kupokea Baraka hizo, Mungu havutiwi sana na sisi tunapofanya hivyo, anavutiwa na sisi pale tunapoishi kulingana na Neno lake, hivyo tu. Kwahiyo, usipeleke fikra zako sana Israeli, bali zipeleke kwenye maisha yako, vilevile maombi yako, yaelekeze kwa watu wenye dhambi leo hii ulimwenguni. Kesha kuwaombea hao, na kuiombea Injili.
Bwana akubariki.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali. Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp yanayotumwa kila siku basi fungua bofya hapa ujiunge >>> WHATSAPP
Mada Nyinginezo:
ALAMA ZA BENDERA YA ISRAELI ZINAWAKILISHA NINI?
Israeli ipo bara gani?
Mataifa ni nini katika Biblia?
Bwana Yesu alimaanisha nini kusema “yamfaa afungiwe shingoni jiwe kubwa la kusagia, na kutoswa katika kilindi cha bahari?”
REKEBISHA YAFUATAYO ILI UCHUMI WAKO UKAE SAWA.
Je Mkristo kutembea na walinzi (Bodyguards),ni sawa?
Rudi nyumbani
Print this post
Wakati Mungu anawatoa Israeli kutoka Misri, Mungu hakuwapa bendera kuwa kama Ishara ya Taifa hilo, Hivyo bendera kwa Israeli ni kitu kilichokuja kuzalika miaka mingi baada ya Kristo kuja duniani katika harakati za kutafuta uhuru.
Sasa swali, ni je zile rangi katika bendera hiyo zinawakilisha nini?, Na ile nyota iliyopo katikati ya bendera inawakilisha nini?.
Bendera ya Israeli ina rangi mbili tu! Nyeupe na Blue (kwa kiswahili Samawi). Rangi nyeupe inawakilisha utakatifu wa Mungu. Na Blue inawakilisha utukufu wa Mungu.
Tukitazama juu mbinguni, anga linaonekana la rangi ya Blue(Samawi).
Kufunua utukufu wa Mungu.Hata vitu vingine vya asili kama milima, bahari utaona vina mwonekano wambwa wa rangi hii ya blue kufunua utukufu wa Mungu.
Lakini kitu cha mwisho katika bendera ya Israeli, ni ile alama kama ya Nyota, yenye pembe sita, iliyopo katikati ya bendera hiyo. Alama hiyo inajulikana kama Nyota ya Daudi au Ngao ya Daudi.
Imejulikana hivyo, kwasababu inaaminika Ngao ya Daudi ilikuwa na umbile hilo mfano wa hiyo nyota, na inaaminika ngao hiyo ilikuwa ina nguvu fulani ya kiungu. Vile vile zile pembe sita katika hiyo ngao zinawakilisha zile tabia sita za Roho wa Mungu katika Isaya 11.
Isaya 11:2 “Na roho ya BWANA atakaa juu yake, roho ya hekima na ufahamu, roho ya shauri na uweza, roho ya maarifa na ya kumcha BWANA”.
Na vile vile kama ilivyokuwa na pembe tatu mbili, moja inaangalia juu na nyingine chini, inawakilisha uhusiano wetu sisi na Mungu.
Ingawa hakuna mahali popote katika torati wala biblia nzima, nyota hiyo ilitajwa kwa sifa hizo, lakini wayahudi wa karne ya 17, walishawishika kuamini hivyo na kuitumia hiyo kama ishara ya Nembo ya Taifa lao, na hata kuitumia katika bendera yao.
Lakini katika jicho lingine, nyota hiyo inaaminika kama ishara ya Masihi, yaani Yesu Kristo, yeye ndiye Uzao wa Daudi, na ndiye ile nyota ing’aayo, ambaye Mataifa yote watamtumainia.
Ufunuo 22:16 “Mimi Yesu nimemtuma malaika wangu kuwashuhudia ninyi mambo hayo katika makanisa. Mimi ndimi niliye Shina na Mzao wa Daudi, ile nyota yenye kung’aa ya asubuhi”.
Lakini swali ni je! Bendera hiyo kwetu sisi wakristo, ina manufaa yoyote kiroho?, Kwamba tunapokuwa na bendera ya Israeli katika makanisa yetu, au katika vyombo vyetu vya usafiri, au katika nyumba zetu, tunakuwa tunajiongezea baraka??.
Jibu ni la!. Bendera ya Taifa la Israeli haituongezei chochote, zaidi sana mtu anapoiweka ndani kwake, na kuifanya kama mungu wake atakuwa anajizombea laana badala ya baraka. Kwasababu kwake yeye ni kama mungu.
Baraka pekee tunayoweza kuipata sisi ni kuishi kulingana na Neno lake na kanuni zake, utakatifu sawasawa na Waebrania 12:14, ndiyo bendera yetu, na alama ya kukubaliwa na Mungu..na sio bendera ya Israeli ndani kwetu.
Hivyo hakuna ulazima wowote wa Mkristo au mhubiri kutembea na bendera kana kwamba ndio kitovu chake cha baraka, labda atembee nayo kwa lengo lingine lakini sio hilo la kutafuta baraka kupitia hiyo.
Maandiko yaliposema “ambarikiye Israeli amebarikiwa” hiyo sio maana yake..Maana yake ni nyingine kabisa.
Maran atha!
Pia kama utapenda uwe unafikiwa na masomo ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP basi bofya hapa ujiunge moja kwa moja >>>> WHATSAPP
MAISHA ULIYOPITIA NYUMA NI USHUHUDA TOSHA WA WEWE KUMTUMIKIA MUNGU
WEKA KUMBUKUMBU YA MAMBO BWANA ANAYOKUFANYIA KWASABABU YATAKUFAA MBELENI.
Neno Kupatiliza maana yake nini katika biblia?
Babewatoto ni nani katika biblia?(Isaya 34:14).
Ni kosa gani Daudi alilolifanya katika kuwahesabu watu, mpaka kupelekea vifo vya waisraeli wengi?
Maana Ya Maneno Katika Biblia.
SWALI: Nini maana ya huu mstari..
Mithali 15:27
[27]Atamaniye faida huifadhaisha nyumba yake mwenyewe; Bali achukiaye zawadi ataishi.
[27]Atamaniye faida huifadhaisha nyumba yake mwenyewe;
Bali achukiaye zawadi ataishi.
JIBU: Mstari huo ni mgumu kueleweka kidogo kwasababu kiswahili kilichotumika hapo ni kile cha zamani..
Ukiangalia tafsiri nyingine..mstari huo unamaana hii.. Atamaniye kupata vingi kwa njia isiyohalali huifadhaisha nyumba yake mwenyewe bali achukiaye rushwa ataishi.
Jambo ambalo ni kweli..kwamfano Mtu anayejiingiza katika biashara ya madawa ya kulevya kwa tamaa tu ya kupata fedha nyingi..hajui kuwa mwisho wake ni kujibomoa yeye mwenyewe na pamoja nyumba yake yote.
Habakuki 2:9
[9]Ole wake yeye aipatiaye nyumba yake mapato mabaya, ili apate kukiweka kioto chake juu, apate kujiepusha na mkono wa uovu!
Mwingine utakuta anatoa rushwa ili bidhaa zake zisilipishwe kodi..lakini hajui mwisho wake utakuwa mbaya siku moja.
Lakini kinyume chake biblia inasema atakayeyakwepa hayo yote ataishi..
Sikuzote tamaa ya za haraka haraka mwisho wake huwa ni mitegoni..
Mhubiri 4:6
[6]Heri konzi moja pamoja na utulivu, Kuliko konzi mbili pamoja na taabu; na kujilisha upepo.
[6]Heri konzi moja pamoja na utulivu,
Kuliko konzi mbili pamoja na taabu;
na kujilisha upepo.
SABATO ILIFANYIKA KWAAJILI YA MWANADAMU NA SI MWANADAMU KWAAJILI YA SABATO!
Maana ya huu mstari ni ipi? Mithali 14:4 ‘Zizi ni safi ambapo hapana ngombe;bali nguvu za ngombe zaleta faida nyingi’.
UMEDI NA UAJEMI ZILITAWALAJE?
KUNA AINA NGAPI ZA MAOMBI?
HUANGUA MAYAI YA FIRA, NA KUSUKA WAVU WA BUIBUI;
Tusome,
2Wakorintho 1:15 “Nami nikiwa na tumaini hilo nalitaka kufika kwenu hapo kwanza, ili mpate karama ya pili”
Sio wakati wote neno “karama” linapotumika kwenye biblia linamaanisha “karama ya roho kama vile unabii, uchungaji, ualimu n.k”. Bali karama pia ni neno linalomaanisha “Zawadi au Baraka”.
Kwamfano kuna andiko linasema “karama ya Mungu ni uzima wa milele”.
Warumi 6:23 “Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu”.
Sasa hapo haimaanishi kwamba Mungu karama yake ni “Uzima wa milele” kama sisi karama zetu zilivyo kutoa unabii, au Kunena kwa lugha, au kutabiri nk.
Mungu yeye hana kipawa fulani maalumu, kwasababu vyote vinatoka kwake.
Bali hapo biblia imemaanisha kuwa “Zawadi ya Mungu ni uzima wa milele”..au “Baraka ya Mungu kwetu ni uzima wa milele”
Kadhalika Mtume Paulo aliposema kuwa “nalitaka kufika kwenu hapo kwanza, ili mpate karama ya pili” hakumaanisha kuwa kuna karama nyingine ya pili tofauti na hiyo ya kitume aliyokuwa nayo, au nyingine mpya hivyo anataka kwenda kuwapa, au kuwanufaisha katika hiyo, hapana!, bali alimaanisha “Baraka ya Pili”.
Ni sawa mhubiri aliyeko Dar es Salaam, aende kuhubiri Morogoro, kwa wiki moja na kisha arudi Dar, na ghafla apate tena safari ya kwenda Dodoma kuhubiri baada ya wiki moja wakati kasharudi Dar, bila shaka hawezi kufika Dodoma bila kupita Morogoro, hivyo Mhubiri huyu akawasiliana na wale aliokwenda kuwahubiria hapo kwanza (Watu wa Morogoro) kwamba atapita tena kuhubiri kwa siku moja na siku inayofuata atakwenda Dodoma.. Hivyo watu wa Morogoro wakawa wamepata Baraka mara mbili. Ndicho Mtume Paulo alichomaanisha hapo!.
Kwamba alishapita kwao (watu wa Korintho) na kuwabariki kwa Mafundisho akaondoka, lakini alitaka tena kupita kwao kwa mara nyingine ya pili wakati anaelekea Makedonia ili wapate Baraka mara mbili.
Maisha ya Paulo yanatufundisha kuwa na bidii na jitihada katika kuifanya kazi ya Mungu, ijapokuwa Paulo alikuwa anapitia vita vikali katika kuhubiri, lakini mara zote alitafuta kurudia kuhubiri mahali ambapo ameshapita kuhubiri.
Matendo 15:36 “Baada ya siku kadha wa kadha Paulo akamwambia Barnaba, Haya! Mrejee sasa tukawaangalie hao ndugu katika kila mji tulipolihubiri neno la Bwana, wa hali gani”.
Bwana atusaidie na sisi tuwe kama watakatifu hawa wa kanisa la kwanza.
KWANINI YESU NI ADAMU WA PILI?
Kuhubiri injili kwa husuda na fitina ndio kupi?
NA VIUNGO VYETU VISIVYO NA UZURI VINA UZURI ZAIDI SANA.
USIRUDI NYUMA KWA KUITUMAINIA HAKI YAKO.
Talanta ni nini katika biblia (Mathayo 25:14-30)
Nyakati zote kabla na hata baada ya Kristo miaka inahesabiwa kwa kwenda mbele, hakuna wakati wowote au kipindi chochote miaka ilihesabiwa kwa kurudi nyuma.
Litakuwa ni jambo lisilo la kiakili kama miaka itahesabiwa kwa kurudi nyuma..yaani kwa mfano leo ni mwaka 2021 halafu mwakani iwe mwaka 2020 badala ya 2022.
Sasa kama ni hivyo tunaweza kujiuliza ni kwanini, miaka ya nyuma inaonekana kama inahesabika kwa kurudi nyuma?.
Ili tuelewe vizuri hilo hebu tujifunze katika huu mfano mdogo.
Tuseme mwaka 2019 kulitokea janga kubwa la dunia la Korona lililobadilisha mfumo mzima wa maisha ya walimwengu.
Na kisha mtu mmoja akataka kurejea tukio fulani lililotokea mwaka2015 ambapo kulitokea janga la kimbunga,na akasema.. “miaka 4 kabla ya Korona kuzuka duniani, kulitokea kimbunga kikubwa kikaharibu miundo mbinu”.
Na mwingine labda akataka kurejea tukio lililotokea mwaka 1978, wakati Tanganyika inapigana na Idd Amini wa Uganda, badala ya kusema mwaka 1978 kulitokea vita, akasema miaka 41, kabla ya janga la korona (41Kk) kulitokea vita kati ya Tanganyika na Uganda, vilivyogharimu uhai wa watu wengi.
Vile vile mtu mwingine labda akataka kurejea vita vya pili vya dunia vilivyotokea mwaka 1945, hivyo badala ya kutaja huo mwaka 1945 akasema, miaka 74 kabla ya Korona,(74kk) ilitokea vita kubwa sana ya dunia iliyogharimu maisha ya watu wengi..
Tuseme na mwingine akataka kurejeatukio la ajali lililotokea mwaka 2021, hivyo badala ya kusema mwaka 2021 kulitokea ajali mbaya sana, akasema miaka miwili baada ya Korona kuzuka duniani(2Bk), kulitokea ajali mbaya sana. N.k hiyo ni mifano tu.
Sasa kwa kusema hivyo haimaanishi, kwamba kuanzia mwaka huo wa 2019 janga la Korona lilipotokea kushuka chini, miaka ilikuwa inahesabiwa kwa kurudi nyuma.
La! Miaka ilikuwa inahesabiwa kwa kupanda, lakini kwasababu kulitokea tukio kubwa na maarufu mwaka 2019 ikabidi kalenda ibadilike, matukio yote ya nyuma yatajwe kwa kurejea tukio fulani kubwa lililowahi kutokea.
Kadhalika Kuzaliwa kwa MKUU WA UZIMA, NA MWANZILISHI WA MAMBO YOTE, YESU KRISTO. Ni lazima dunia itetemeke, tarehe haziwezi kubaki vile vile, majira hayawezi kubaki vile vile, kadhalika na kuzimu haiwezi kubaki vile vile. Ni lazima mabadiliko makubwa yaambatane na kuzaliwa kwake, kwasababu kitu alichokileta ulimwenguni ni kikubwa, Damu yake iliyomwagika pale Kalvari, imeleta mageuzi makubwa katika ulimwengu wa mwili na roho.
Maandiko yanasema..Kristo alikuja kuutangaza MWAKA WA BWANA uliokubaliwa (Isaya 61:1-2). Hivyo haiwezekani “aje autangaze mwaka wa Bwana” halafu tarehe zibaki vile vile. Ni lazima tu matukio yote ya kabla au baada yarejee kuzaliwa kwake.
Isaya 61:1 “Roho ya Bwana MUNGU i juu yangu; kwa sababu BWANA amenitia mafuta niwahubiri wanyenyekevu habari njema…. 2 Kutangaza mwaka wa BWANA uliokubaliwa, na siku ya kisasi cha Mungu wetu; kuwafariji wote waliao”.
Isaya 61:1 “Roho ya Bwana MUNGU i juu yangu; kwa sababu BWANA amenitia mafuta niwahubiri wanyenyekevu habari njema….
2 Kutangaza mwaka wa BWANA uliokubaliwa, na siku ya kisasi cha Mungu wetu; kuwafariji wote waliao”.
Bwana Yesu amekuwa Jiwe kuu la pembeni, Jiwe la kurejea..Korona imetikisa dunia lakini bado haijaweza kubadilisha majira, wapo wanadamu waliokuwa maarufu lakini hawajabadili majira, wamekuja na kupita, ni mkuu wa Uzima (Yesu), pekee yake ndiye ambaye mpaka leo, alama yake ipo katika kila mwanzo wa barua, mwanzo wa siku, na miezi na Miaka. Kuonesha kwamba yupo hai mpaka sasa hivi, na hakuna aliyemzidi, leo hii hakuna mahali utakwenda usilisikie jina la Yesu likitajwa.
Na kama jinsi yeye alivyokuwa nguzo ya kurejewa, atabaki kuwa hivyo hivyo milele.
Je! Umemwamini leo?.. Umetubu dhambi zako kwa kumaanisha kuziacha?, umebatizwa katika ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa jina la Yesu upate ondoleo la dhambi zako?. Kama bado ni vyema ukafanya hivyo leo, maadamu mlango wa neema upo wazi, siku utakapofungwa kutakuwa hakuna nafasi tena ya kutubu.
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
TABIA YA WAZI INAYOWATOFAUTISHA MANABII WA UONGO NA WALE WA UKWELI.
BIBLIA INAITAJA NJIA KUU YA MFALME, NJIA HII NI IPI?
Jiepushe na tamaa ya Mali/kupenda fedha.
USITAZAME NYUMA!
SI MAPEPO YOTE NI YA KULIPUKA.
Mithali 25: 20 “Amwimbiaye nyimbo mtu mwenye moyo mzito, Ni kama yeye avuaye nguo wakati wa baridi; Ni kama siki juu ya magadi”.
Anaposema amwimbiaye nyimbo..anamaanisha nyimbo za furaha, au za shangwe kumwimbia mtu mwenye moyo mzito, kwa kudhania kuwa ndio zitatuliza uchungu wake, kumbe kinyume chake, ndio zinamwongezea masikitiko moyoni mwake.
Sulemani kwa hekima ya ki-Mungu aliliona hilo, kwamba, ni vema kuendana na hisia za mtu, kwamfano, kuna watu wapo katika uchungu mzito sana mioyoni mwao, pengine labda wa kufiwa na mume/mke wake, au mzazi wake, au ndugu yake wa karibu sana, na wewe kwa mawazo yako ukaona ili kuwatuliza ni kwenda kuwachekesha, chekesha, au kuwaburudisha kwa nyimbo za furaha,..Ujue kuwa hapo hautatui tatizo. Ni lazima ujue hali ya mtu wakati huo, yupo katika uchungu wa namna gani.
Biblia inasema..
Warumi 12:15 “Furahini pamoja nao wafurahio; lieni pamoja nao waliao”.
Lakini kama unaonyesha kufurahi pamoja na hao walioa, ukidhani ndio kiashiria cha kuwachangamsha..Ni rahisi kuwasha moto mwingine,
Kwasababu mtu Yule anaweza kudhani hujathamini hata kile anachokipitia, na matokeo yake atachukia badala ya kupona,..Ni ndio hapo anasema sawa na kumvua mtu nguo zake wakati wa baridi kali, ni nini kinatokea? Ni mateso zaidi kama sio kifo.
Kwahiyo tuwe na hekima ya kujua ni dawa ipi tunaitumia kumponya mtu aliyevunjika moyo. Ikiwa kweli anahitaji, furaja za nyimbo tutumie hizo, lakini kama yupo katika uchungu mwingi sana wa moyo, tuendane na hisia zake, hiyo ndio dawa pekee ya kuwaponya watu kama hao.
SIFONGO NA SIKI NI NINI?
Nini maana ya Mungu amemfanya mwanadamu mnyofu?
Kuwaogopa wanadamu huleta mtego,(Mithali 29:25)
Nini maana ya “Uchungu wa mauti ni dhambi, na nguvu za dhambi ni torati”
Zaburi maana yake nini, katika Biblia?
NGUVU ZA ZAMANI ZIJAZO:
WhatsApp
Lengo la Mungu kuwapa watu amri ya kuitunza sabato lilikuwa ni tofauti na lilivyochukuliwa au kutafsiriwa.Tuchukue mfano wa kawaida wa kimaisha…
Kikawaida, kila mtu ni lazima katika siku moja anao muda wa kulala (kupumzika), ili mwili wake uwe katika ustawi bora, hakuna mtu asiyelala kabisa.Hivyo ni sawa na kusema usingizi umeumbwa kwa ajili yetu sisi, ili tupate kuwa na afya bora na sio sisi tumeumbwa tuutumikie usingizi. Kwa mantiki hiyo basi, ingawa tuna sheria ya kulala kila siku, lakini hatuna sheria ya muda wa kulala au wakati wa kulala.
Wengine watalala kuanzia saa 3 usiku na kuamka saa 11 alfajiri ili kuwahi shughuli zao..hivyo wakawa wamelala masaa 8.
Wengine wataanza kulala kuanzia saa 6 usiku na kuamka saa 2 asubuhi na wakawa wamelala masaa yaleyale 8..wengine hawatalala kabisa usiku bali watalala mchana..
Hao wote wametimiza sheria ya kulala,ilitowekwa na Mungu, hakuna hata mmoja aliyeivunja..isipokuwa kila mtu kaitimiza kwa wakati wake aliouona unafaa.
Hivyo muda wa kulala haujalishi kinachojalisha ni masaa na matokeo baada ya kulala..kwamba wote mtalala na miili itakuwa imepumzika..Na usipolala mwili wenyewe utakutumia taarifa ya deni la usingizi, hivyo hilo deni utalilipa tu, na taarifa hiyo sio Mungu anayekutumia bali ni mwili ndio unaokutumia.
Lakini sasa inapotokea kwamba ni amri kwamba kila saa 3 usiku mpaka saa 11 asubuhi watu wote wawe vitandani wamelala, hapo tutakuwa tunauabudu usingizi, tutakuwa ni watumwa wa usingizi, na tutakuwa wajinga na maana ya kulala itakuwa imepotea kabisa.
Kwasababu kuna wakati itakubidi uwahi kulala ili uwahi kuamka, kuna kipindi utachelewa kulala kutokana na dharura za kimaisha na hivyo utajikuta unachelewa kuamka pia, kuna wakati utaugua utakuwa kitandani muda wote, au usiwe unapata usingizi kabisa..Hivyo usingizi upo lakini ni sisi ndio tunaouendesha na sio wenyewe unatuendesha sisi..Hatuwi watumwa wa usingizi!
Na Sabato ni hivyo hivyo..
Maandiko yanasema Sabato ilifanyika kwaajili yetu na sio sisi kwaajili ya sabato.
Marko 2:27 “Akawaambia, Sabato ilifanyika kwa ajili ya mwanadamu, si mwanadamu kwa ajili ya sabato”
Mungu aliiweka sabato ili tupumzike tupate muda wa kumtafakari yeye, na kutengeneza mambo yetu ya kiroho katika wiki inatofuata mbele yetu, kama vile usingizi ulivyowekwa kwamba tupumzike ili miili yetu istawi, ipate nafasi ya kujitengeneza upya kwaajili ya kuiendea siku inayofuata. Hivyo ni kweli tumepewa amri ya kuishika sabato, lakini hiyo hatuishiki kwa kanuni fulani maalumu, kwamba ni lazima iwe ni kila jumamosi, kiasi kwamba mtu ukiabudu siku tofauti na hiyo ni kosa!…au kwamba ni lazima iwe kila jumapili kiasi kwamba mtu akiabudi jumamosi ni kosa, hapo tutakuwa hatujaelewa maana ya Sabato!.
Hivyo siku ya Bwana ni chaguzi wetu, kwamba siku ipi ni bora kwetu, kama ni jumamosi, au jumapili, au jumatatu, au jumanne au siku nyingine yeyote maadamu, katika hiyo tutaifanya siku nzima iwe takatifu kwa Bwana.
Kulingana na mfumo wa kalenda ya nchi yetu, siku ambazo hazina masumbufu ni jumamosi na jumapili, hizo ni siku ambazo ni nzuri kuzifanya kuwa za Bwana, lakini pia sio amri, hata jumanne ni siku iliyokubalika, hata jumatano, lakini shida ya siku hizo ni kwamba zina masimbufu mengi ya kimaisha, hivyo ni ngumu kuzitakasa.
Mataifa ya kiarabu, siku ya ijumaa ndio siku isiyo na masumbufu kwao, kama vile ilivyo jumapili na jumamosi kwetu, kwao ni ijumaa…hivyo siku kama hiyo kulingana na kalenda za mataifa hayo ni vizuri kuifanya siku ya Bwana iwe Ijumaa kuliko jumapili au jumamosi kwasababu, siku ya jumapili ni sheria watu wao kwenda makazini kama kawaida tofauti na huku kwetu.
Ni jambo la aibu mkristo kushindania siku ya kuabudu. Utakuta mtu hafahamu kitu kingine chochote zaidi ya kushabikia jumamosi au jumapili. Mtu kama huyo anakuwa hana tofauti na mtu anayeshabikia muda wa kulala.
Bwana atupe macho ya kuyaona haya, na tutokane na upofu huo, ambao unaufanya ukristo usieleweke kwa watu waliopo nje.
1 Wakorintho 14:40 “Lakini mambo yote na yatendeke kwa uzuri na kwa utaratibu”
Neno Saumu lina maana gani katika biblia?
IMESALIA RAHA YA SABATO KWA WATU WA MUNGU.
TUSIRUHUSU MAMBO YA KUSUBIRISHA, YAVURUGE MUDA WETU NA MUNGU.
Sabato halisi ni lini, Je! ni Jumapili au Jumamosi?, Ni siku gani itupasayo kuabudu?
Ratili ni kipimo cha uzito kilichotumika enzi za kale..chenye uzito sawa na Gramu 500 hivi. Karibia na nusu kilo.
Neno hilo utalisoma katika vifungu hivi kwenye biblia..
Yohana 19:39
[39]Akaenda Nikodemo naye, (yule aliyemwendea usiku hapo kwanza), akaleta machanganyiko ya manemane na uudi, yapata ratli mia.
Pia..
Yohana 12:3
[3]Basi Mariamu akatwaa ratli ya marhamu ya nardo safi yenye thamani nyingi, akampaka Yesu miguu, akamfuta miguu kwa nywele zake. Nayo nyumba pia ikajaa harufu ya marhamu.
Unaweza kupata picha Mariamu alibeba manukato yaliyokuwa na uzito wa karibia nusu kilo..na yote akammwagia Bwana Yesu..manukato ambayo ingetosha tu kuchukua kidogo na kumpaka lakini yeye aliyamimina kwake kama maji.
Kwasasa mafuta hayo kwa wingi wake ni thamani isiyo pungua milioni 6 kwa fedha za kitanzania..kufunua ni jinsi gani Mariamu alimthaminisha Yesu kuliko mtu mwingine yeyote au mfalme yeyote duniani..
Si ajabu kwanini matendo ya watu kama hawa tunayasoma hadi leo katika maandiko..Ni kutufundisha kuwa na sisi pia tukitoa vitu vyetu vya thamani nyingi sana kwa ajili ya Mungu..
Mungu naye ni lazima arudishe fadhila kwetu kwa kutupa kumbukumbu la daima..ndivyo alivyofanya kwa yule mwanamke pale watu walipomng’unikia kwa upotevu wote ule..Bwana alisema..
Marko 14:8-9
[8]Ametenda alivyoweza; ametangulia kuupaka mwili wangu marhamu kwa ajili ya maziko. [9]Amin, nawaambia, Kila ihubiriwapo Injili katika ulimwengu wote, na hili alilotenda huyu litatajwa kwa kumbukumbu lake.
[8]Ametenda alivyoweza; ametangulia kuupaka mwili wangu marhamu kwa ajili ya maziko.
[9]Amin, nawaambia, Kila ihubiriwapo Injili katika ulimwengu wote, na hili alilotenda huyu litatajwa kwa kumbukumbu lake.
Swali ni je na sisi tunaweza kumthamini Bwana kwa namna hiyo? Bwana atupe macho hayo.
Shalom.
VIPIMO MBALIMBALI VYA KIBIBLIA.
Santuri ni nini? (Danieli 3:5,10)
Panda/ Sauti ya panda ni nini kibiblia?(Danieli 3:5)
Kinubi ni nini katika biblia? (1Samweli 16:16, 23)
“Mtima” ni neno linalowakilisha aidha “nafsi ya mtu” au “roho ya mtu”
Hivyo mtu anayeugua rohoni, ni sawa na kusema “anaugua katika mtima wake”.. kadhalika mtu aliyeumizwa nafsini mwake ni sawa na kusema “kaumizwa katika mtima wake”..hivyo ni neno linalotumika kuwakilisha aidha Roho au Nafsi ya mtu.
Katika biblia neno hilo limeonekana mara kadhaa..
Ayubu 19:27 “Nami nitamwona mimi nafsi yangu, Na macho yangu yatamtazama, wala si mwingine. Mtima wangu unazimia ndani yangu”.
Maombolezo 1:20 “Angalia, Ee Bwana; maana mimi ni katika dhiki; Mtima wangu umetaabika; Moyo wangu umegeuka ndani yangu; Maana nimeasi vibaya sana; Huko nje upanga hufisha watu; Nyumbani mna kama mauti”.
Yeremia 4:19 “Mtima wangu, mtima wangu! Naumwa katika moyo wangu wa ndani; moyo wangu umefadhaika ndani yangu; siwezi kunyamaza; kwa sababu umesikia, Ee nafsi yangu, sauti ya tarumbeta, mshindo wa vita”.
Mistari mingine inayotaja neno hilo ni pamoja na Zaburi 26:2, Mithali 20:30, na Zaburi 139:13.
Kila mwanadamu anao “Mtima” kwasababu ndio utu wa ndani. Na mitima yetu (yaani nafsi zetu na Roho zetu) zinapaswa ziwe safi siku zote.. Na Mungu anazitakasa nafsi zetu kwa sisi kwanza kujitenga na kila ubaya kama maandiko yanavyosema..
1Wathesalonike 5:22 “Jitengeni na ubaya wa kila namna”. 23 Mungu wa amani mwenyewe awatakase kabisa; nanyi NAFSI ZENU na ROHO ZENU na MIILI YENU mhifadhiwe mwe kamili, bila lawama, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo”.
1Wathesalonike 5:22 “Jitengeni na ubaya wa kila namna”.
23 Mungu wa amani mwenyewe awatakase kabisa; nanyi NAFSI ZENU na ROHO ZENU na MIILI YENU mhifadhiwe mwe kamili, bila lawama, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo”.
Je! Umejitenga na kila ubaya?..umejitenga na Ulevi?, uzinzi? Ushirikina?, uvaaji mbaya? Utukanaji?, wizi, ushabiki wa mambo ya kidunia?.. Kama bado hujajitenga na hayo yote, na huku unaomba kwamba Mungu akusafishe roho yako, au akupe amani katika nafsi yako, au aponye majeraha yako ya ndani, au akulinde na nguvu za giza..tambua kuwa unapoteza muda wako. Sharti kwanza ni wewe kujitenge na kila ubaya ili umfungulie Mungu mlango wa kukusafisha.
Lakini kama hutaki kujitenga na ubaya wote huo, bado unaukumbatia hakuna utakaso wowote utakaoupata kutoka kwa Mungu, kama bado unaishi na huyu unayemwita boyfriend, au girlfriend, tambua kuwa roho yako bado imefungwa, kama bado unashiriki mazungumzo machafu na hizo kampani za rafiki ulio nao, unajifungia mlango wa utakaso, kama bado unayo miziki ya kidunia na filamu za kidunia katika simu yako unafunga milango ya utakaso wako.
Maandiko yanasema “Tujitenge na ubaya wa kila namna” na sio “tuuombee Ubaya”.. Utakuta mtu anakwenda kutafuta kuombewa aache uzinzi, na huku hajajitenga na vichocheo vyote vya uzinzi. Mtu wa namna hii ataomba na kuombewa, na hakuna chochote atakachopokea, kwasababu hajajua kanuni ya kupokea Utakaso.
Utakaso unaanza kwanza kwa sisi “kujitenga na ule uovu”..Ndipo Roho Mtakatifu anatuongezea nguvu za sisi kuushinda uovu.
UTAKASO NI SEHEMU YA MAISHA YA MKRISTO YA KILA SIKU.
Roho, Nafsi, na Mwili vina utofauti gani?
Mungu alikuwa anaongea na nani aliposema na “Tumfanye mtu kwa mfano wetu”,(Mwanzo 1:26)?
Ngome ni nini? Kwanini Mungu anafananishwa na ngome?
NINI MAANA YA KUWA MKRISTO?
Katika biblia tunaona kama Umedi na Uajemi zikitajwa kwa pamoja, kana kwamba ni Taifa moja, ingawa ni falme mbili tofauti, sasa zilitawalaje?
Umedi na Uajemi Ni utawala mmoja ulioundwa na Falme mbili tofauti, Ili kuelewa vizuri tuchukue mfano wa Taifa la Tanzania, Taifa la Tanzania limeundwa na mataifa mawili, Zanzibar na Tanganyika, Na yalipoungana ndio ikawa Tanzania, Kwahiyo badala ya kusema Tanzania, tunaweza kusema ni Taifa la Tanganyika na Zanzibar. Na ukitazama utaona unapofika wakati uchaguzi wa uRaisi, Raisi anayechaguliwa kuiongoza nchi yote anaweza kutoka upande wowote ule kati ya pande hizo mbili. Utaona leo anaweza kutokea Tanganyika, awamu ijayo akatokea Zanzibar.
Ndivyo ilivyokuwa kwa Ufalme wa Umedi na Uajemi. Zilikuwa ni falme mbili zilizoungana na kuwa ufalme mmoja. Lakini wafalme waliokuwa wanatawala, walikuwa wanapokezana, awamu hii mfalme anaweza kutokea Umedi, awamu ijayo akatokea Uajemi. Kama vile Raisi wa Tanzania, leo anaweza kutokea Bara, awamu ijayo akatokea Zanzibar.
Ndio maana utaona baada tu ya Ufalme wa Babeli kuanguka, ufalme uliochukua hatamu ni Dario, wa Umedi, huyu ndiye aliyemwangusha Nebukadneza, lakini bado hakuwapa ruhusa Israeli warudi nchini kwao, Israeli waliendelea kukaa mateka. Ingawa huyu Dario, alimheshimu sana Danieli, hata kumweka Danieli kuwa mkuu wa Maliwali wa ufalme wake wote.
Danieli 6:30 “Usiku uo huo Belshaza, mfalme wa Wakaldayo, akauawa. 31 Na Dario, Mmedi, akaupokea ufalme, naye umri wake alikuwa na miaka sitini na miwili”.
Danieli 6:30 “Usiku uo huo Belshaza, mfalme wa Wakaldayo, akauawa.
31 Na Dario, Mmedi, akaupokea ufalme, naye umri wake alikuwa na miaka sitini na miwili”.
Danieli 6:1 “Ilimpendeza Dario kuweka juu ya ufalme maliwali mia na ishirini, wawe juu ya ufalme wote; 2 na juu yao akaweka wakubwa watatu, na Danielii alikuwa mmoja wao; ili maliwali hawa watoe hesabu kwao, mfalme asipate hasara. 3 Basi Danielii huyo alipata sifa kuliko wakubwa na maliwali, kwa kuwa roho bora ilikuwa ndani yake; naye mfalme akaazimu kumweka juu ya ufalme wote”.
Danieli 6:1 “Ilimpendeza Dario kuweka juu ya ufalme maliwali mia na ishirini, wawe juu ya ufalme wote;
2 na juu yao akaweka wakubwa watatu, na Danielii alikuwa mmoja wao; ili maliwali hawa watoe hesabu kwao, mfalme asipate hasara.
3 Basi Danielii huyo alipata sifa kuliko wakubwa na maliwali, kwa kuwa roho bora ilikuwa ndani yake; naye mfalme akaazimu kumweka juu ya ufalme wote”.
Lakini ulipofika utawala wa Koreshi miaka michache baadaye ambaye alikuwa ni Muajemi ndipo Israeli walipofunguliwa kutoka katika utumwa, na kupewa ruhusa kurudi nchini kwao, kuutengeneza mji wao na Hekalu la Mungu lililobomolewa na Mfalme Nebukadneza.
2Nyakati 36:22 “Ikawa katika mwaka wa kwanza wa Koreshi, mfalme wa Uajemi, ili kwamba neno la Bwana alilolisema kwa kinywa cha Yeremia lipate kutimizwa, Bwana akamwamsha roho yake Koreshi, mfalme wa Uajemi, hata akapiga mbiu katika ufalme wake wote, akaiandika pia, akisema, 23 Koreshi, mfalme wa Uajemi asema hivi; Bwana, Mungu wa mbinguni, amenipa falme zote za dunia; naye ameniagiza nimjengee nyumba katika Yerusalemu, ulioko Yuda. Basi kila mtu katika ninyi nyote mlio watu wake, Bwana, Mungu wake, na awe pamoja naye, na akwee”.
2Nyakati 36:22 “Ikawa katika mwaka wa kwanza wa Koreshi, mfalme wa Uajemi, ili kwamba neno la Bwana alilolisema kwa kinywa cha Yeremia lipate kutimizwa, Bwana akamwamsha roho yake Koreshi, mfalme wa Uajemi, hata akapiga mbiu katika ufalme wake wote, akaiandika pia, akisema,
23 Koreshi, mfalme wa Uajemi asema hivi; Bwana, Mungu wa mbinguni, amenipa falme zote za dunia; naye ameniagiza nimjengee nyumba katika Yerusalemu, ulioko Yuda. Basi kila mtu katika ninyi nyote mlio watu wake, Bwana, Mungu wake, na awe pamoja naye, na akwee”.
Hivyo utawala huu wa Umedi na Uajemi, ndio Mungu alioutumia kuwapa raha Israeli, kwani ndio uliowaweka Israeli huru, na kuwapa ruhusa ya kwenda kuijenga nchi yao, ingawa ni kwa vipindi vya tabu, lakini hatimaye kazi ya ujenzi ilikamilika katika utawala huu kabla ya kuingia utawala wa UYUNANI, ambao uliusumbua sana Israeli.
Pia katikati ya utawala huu wa Umedi na Uajemi, ndipo Malkia Esta alitokea.
Esta 1:1 “Zamani za Ahasuero; naye huyu Ahasuero alimiliki toka Bara Hindi mpaka Kushi, juu ya majimbo mia na ishirini na saba; 2 siku zile mfalme Ahasuero alipoketi katika kiti cha enzi cha ufalme wake, huko Shushani ngomeni; 3 mwaka wa tatu wa kumiliki kwake, ikawa aliwafanyia karamu maakida wake wote na majumbe wake; WAKUU WA UAJEMI NA UMEDI, watu wenye cheo na maakida wa majimbo, wakihudhuria mbele zake”.
Esta 1:1 “Zamani za Ahasuero; naye huyu Ahasuero alimiliki toka Bara Hindi mpaka Kushi, juu ya majimbo mia na ishirini na saba;
2 siku zile mfalme Ahasuero alipoketi katika kiti cha enzi cha ufalme wake, huko Shushani ngomeni;
3 mwaka wa tatu wa kumiliki kwake, ikawa aliwafanyia karamu maakida wake wote na majumbe wake; WAKUU WA UAJEMI NA UMEDI, watu wenye cheo na maakida wa majimbo, wakihudhuria mbele zake”.
Lakini pamoja na kwamba ulikuwa ni ufalme uliotawala dunia, na uliowanufaisha Israeli kwa sehemu kubwa, hata kufikia wakati binti wa kiisraeli, (yaani Esta) kuwa Malkia wa dunia, lakini bado ufalme huo ulikuja kuanguka, kuonyesha kuwa Falme zote zitaanguka haijalishi ni Nzuri au Mbaya. Lakini ufalme wa Mmoja tu Yesu Kristo ndio utakaodumu milele. Sawasawa na maono aliyoyaona Nebukadreza.
Nebukadreza aliona jiwe lililochongwa pasipo kazi ya mikono, ikizipiga zile falme tano zilizotawala, (yaani Babeli, Umeni na Uajemi, Uyunani, na Rumi), na kuziangusha zote, na kisha jiwe hilo kuwa milima mikubwa iliyoijaza dunia yote. Na ufunuo wa jiwe hilo ni utawala wa Yesu Kristo, ambao ndio utazivunja falme hizo zote na utasambaa duniani kote.
Siku si nyingi parapanda ya mwisho italia, na wafu watafufuliwa na kwenda mbinguni, na hukumu ya mataifa waliosalia duniani itaanza, mataifa yataanguka yote na dunia itatikiswa, kabla ya kuanza utawala wa Mfalme Yesu Kristo, wa miaka elfu, ambao utasambaa ulimwenguni kote. Utakuwa ni utawala wa Amani kabla ya kuingia katika umilele katika mbingu mpya na nchi mpya.
Je utakuwa wapi siku hiyo? Utawala wa Farao ulipita, utawala wa Nebukadneza ulipita, utawala wa Malkia Esta ulipita, na tawala nyingine zote zilipita!, unadhani ni nini ambacho hakitapita kilichosalia katika huu ulimwengu?.. Vyote vitapita lakini Maneno ya Yesu Kristo hayatapita kamwe, alisema atarudi! Atarudi tu!, haijalishi dunia itasemaje!.. na atakuja kama mwivi.
Mathayo 24:35 “Mbingu na nchi zitapita; lakini maneno yangu hayatapita kamwe”.
UTAWALA WA MIAKA 1000.
Tofauti kati ya ufalme wa mbinguni na ufalme wa Mungu ni ipi?
YEZEBELI ALIKUWA NANI
IFAHAMU HUZUNI NA FURAHA YA MALAIKA.
MISTARI YA BIBLIA KUHUSU WATOTO.