“Mtima” ni neno linalowakilisha aidha “nafsi ya mtu” au “roho ya mtu”
Hivyo mtu anayeugua rohoni, ni sawa na kusema “anaugua katika mtima wake”.. kadhalika mtu aliyeumizwa nafsini mwake ni sawa na kusema “kaumizwa katika mtima wake”..hivyo ni neno linalotumika kuwakilisha aidha Roho au Nafsi ya mtu.
Katika biblia neno hilo limeonekana mara kadhaa..
Ayubu 19:27 “Nami nitamwona mimi nafsi yangu, Na macho yangu yatamtazama, wala si mwingine. Mtima wangu unazimia ndani yangu”.
Maombolezo 1:20 “Angalia, Ee Bwana; maana mimi ni katika dhiki; Mtima wangu umetaabika; Moyo wangu umegeuka ndani yangu; Maana nimeasi vibaya sana; Huko nje upanga hufisha watu; Nyumbani mna kama mauti”.
Yeremia 4:19 “Mtima wangu, mtima wangu! Naumwa katika moyo wangu wa ndani; moyo wangu umefadhaika ndani yangu; siwezi kunyamaza; kwa sababu umesikia, Ee nafsi yangu, sauti ya tarumbeta, mshindo wa vita”.
Mistari mingine inayotaja neno hilo ni pamoja na Zaburi 26:2, Mithali 20:30, na Zaburi 139:13.
Kila mwanadamu anao “Mtima” kwasababu ndio utu wa ndani. Na mitima yetu (yaani nafsi zetu na Roho zetu) zinapaswa ziwe safi siku zote.. Na Mungu anazitakasa nafsi zetu kwa sisi kwanza kujitenga na kila ubaya kama maandiko yanavyosema..
1Wathesalonike 5:22 “Jitengeni na ubaya wa kila namna”. 23 Mungu wa amani mwenyewe awatakase kabisa; nanyi NAFSI ZENU na ROHO ZENU na MIILI YENU mhifadhiwe mwe kamili, bila lawama, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo”.
1Wathesalonike 5:22 “Jitengeni na ubaya wa kila namna”.
23 Mungu wa amani mwenyewe awatakase kabisa; nanyi NAFSI ZENU na ROHO ZENU na MIILI YENU mhifadhiwe mwe kamili, bila lawama, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo”.
Je! Umejitenga na kila ubaya?..umejitenga na Ulevi?, uzinzi? Ushirikina?, uvaaji mbaya? Utukanaji?, wizi, ushabiki wa mambo ya kidunia?.. Kama bado hujajitenga na hayo yote, na huku unaomba kwamba Mungu akusafishe roho yako, au akupe amani katika nafsi yako, au aponye majeraha yako ya ndani, au akulinde na nguvu za giza..tambua kuwa unapoteza muda wako. Sharti kwanza ni wewe kujitenge na kila ubaya ili umfungulie Mungu mlango wa kukusafisha.
Lakini kama hutaki kujitenga na ubaya wote huo, bado unaukumbatia hakuna utakaso wowote utakaoupata kutoka kwa Mungu, kama bado unaishi na huyu unayemwita boyfriend, au girlfriend, tambua kuwa roho yako bado imefungwa, kama bado unashiriki mazungumzo machafu na hizo kampani za rafiki ulio nao, unajifungia mlango wa utakaso, kama bado unayo miziki ya kidunia na filamu za kidunia katika simu yako unafunga milango ya utakaso wako.
Maandiko yanasema “Tujitenge na ubaya wa kila namna” na sio “tuuombee Ubaya”.. Utakuta mtu anakwenda kutafuta kuombewa aache uzinzi, na huku hajajitenga na vichocheo vyote vya uzinzi. Mtu wa namna hii ataomba na kuombewa, na hakuna chochote atakachopokea, kwasababu hajajua kanuni ya kupokea Utakaso.
Utakaso unaanza kwanza kwa sisi “kujitenga na ule uovu”..Ndipo Roho Mtakatifu anatuongezea nguvu za sisi kuushinda uovu.
Bwana akubariki.
Maran atha!
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali. Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
Mada Nyinginezo:
UTAKASO NI SEHEMU YA MAISHA YA MKRISTO YA KILA SIKU.
Roho, Nafsi, na Mwili vina utofauti gani?
Mungu alikuwa anaongea na nani aliposema na “Tumfanye mtu kwa mfano wetu”,(Mwanzo 1:26)?
Ngome ni nini? Kwanini Mungu anafananishwa na ngome?
NINI MAANA YA KUWA MKRISTO?
Rudi nyumbani
Print this post