Ndoto za ajali zinaweza kuja katika maumbile mengi tofauti tofauti, wengine wanaota ajali za pikipiki, wengine za magari, wengi ndege, wengine meli, wengine treni, katika namna tofauti tofauti. Wengine wanaota mtu kagongwa na gari, au magari yanagonga gongana n.k… kwa vyovyote vile, ndoto hizo zinabeba maudhui moja nayo ni “AJALI”
Sasa ili kupata tafsiri sahihi ya ndoto hiyo ni vizuri ukajitambua wewe upo katika kundi gani.
1.) Kundi la kwanza ni waliookoka.
2) Kundi la pili ni wenye dhambi.
Tukianzana na kundi la kwanza: Ikiwa wewe, umeokoka (yaani unao uhakika umesimama ndani ya Kristo). Basi fahamu kuwa ni Mungu anakutahadharisha tukio lililopo mbele yako, aidha kuna ajali utakutana nayo, au itatokea kwa mtu mwingine, au mahali fulani. Hivyo unachopaswa kufanya, ni kuingia katika maomba ya kuvunja hiyo mipango ya adui. Ambayo pengine imepangwa kwako au kwa mtu mwingine..kemea kwa bidii kwa mamlaka uliyopewa katika jina la Yesu. Na Mungu ataisambaratisha hiyo mipango yote.
Ikiwa ndoto hiyo imekuja kwa uzito usiipuuzie, kwasababu Mungu kukuonyesha hivyo, ni ili usimame kama askari wa Mungu kushindana na hizo nyakati mbaya kabla hazijafika.( Soma Ayubu 33:14-15)
Kundi la Pili: Mwenye dhambi.
Ikiwa wewe ni mwenye dhambi(yaani hujaokoka, Kristo hayupo ndani yako). Ujue ndoto hiyo ni ishara ya tahadhari kubwa sana kwako. Kwamba kipindi si kirefu Mungu atakuadhibu, na kuadhibu kwake, kunaweza kukawa ni kifo cha ghafla, au kunaswa katika dhambi zako unazozifanya, na ukashindwa kutoka huko milele.
Soma hii Habari kwa makini;
Ezekieli 7: 6 “Mwisho umekuja, mwisho huu umekuja; unaamka ukupate; angalia, unakuja.7 AJALI YAKO IMEKUJIA, wewe ukaaye katika nchi hii; majira yamewadia, siku ile inakaribia; siku ya fujo, wala si ya shangwe milimani.8 BASI HIVI KARIBU NITAMWAGA GHADHABU YANGU JUU YAKO, nitazitimiza hasira zangu juu yako, nami nitakuhukumu sawasawa na njia zako; nami nitakupatiliza machukizo yako yote.9 Jicho langu halitaachilia, wala sitaona huruma; nitakupatiliza njia zako na machukizo yako yote yatakuwa katikati yako; nanyi mtajua ya kuwa mimi, Bwana, napiga.10 ANGALIA, SIKU HIYO; ANGALIA, INAKUJA; AJALI YAKO IMETOKEA; fimbo imechanua, kiburi kimechipuka”.
Ezekieli 7: 6 “Mwisho umekuja, mwisho huu umekuja; unaamka ukupate; angalia, unakuja.
7 AJALI YAKO IMEKUJIA, wewe ukaaye katika nchi hii; majira yamewadia, siku ile inakaribia; siku ya fujo, wala si ya shangwe milimani.
8 BASI HIVI KARIBU NITAMWAGA GHADHABU YANGU JUU YAKO, nitazitimiza hasira zangu juu yako, nami nitakuhukumu sawasawa na njia zako; nami nitakupatiliza machukizo yako yote.
9 Jicho langu halitaachilia, wala sitaona huruma; nitakupatiliza njia zako na machukizo yako yote yatakuwa katikati yako; nanyi mtajua ya kuwa mimi, Bwana, napiga.
10 ANGALIA, SIKU HIYO; ANGALIA, INAKUJA; AJALI YAKO IMETOKEA; fimbo imechanua, kiburi kimechipuka”.
Umeona? Hayo maandiko yenyewe yanajieleza, ikiwa wewe ni mzinzi, fahamu kubwa ajali ya Ukimwi ipo mbele yako, wewe ni fisadi ajali ya vifungo ipo mbele yako, wewe ni mwizi ajali ya kifo ipo mbele yako, wewe ni mshirikina ajali ya jehanum ipo mbele yako.
Kwa ujumla kama wewe ni mwenye dhambi ujue mwisho wako upo karibuni sana. Na ukifa ni motoni. Ndio tafsiri ya ndoto hiyo.
Unasubiri nini mpaka hayo yote yakukute, ikiwa upo tayari leo kutubu dhambi, basi, Bwana Yesu atakusamehe, na kukuepusha na madhara hayo yote aliyokuonyesha mbele yako. Angeweza kukaa kimya tu, hayo mambo yakukute kwa ghafla, lakini kwasababu hataki uangamie ndio maana amekutahadharisha mapema.. Hivyo leo hii fungua moyo wako, kubali kugeuka, na uache dhambi zako zote, ili Kristo ayatengeneze tena Maisha yako.
Ikiwa upo tayari kutubu leo, basi fungua hapa, kwa ajili ya mwongozo wa SALA YA TOBA. >>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Bwana akubariki.
Angalia pia Kuota Unajenga nyumba
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa mgawanyo bora wa masomo download App hapa>> App wingu la mashahidi
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali. Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
Mada Nyinginezo:
KUOTA UNAPEWA PESA.
KUOTA UNACHEZA MPIRA.
KUOTA UNAJIFUNGUA.
KUOTA MTU ALIYEKUFA.
KUOTA UNAFANYA TENDO LA NDOA.
Rudi nyumbani
Print this post
Nakusalimu katika jina kuu, la Bwana wetu Yesu Kristo karibu katika sehemu ya pili ya Makala hii inayohusu migogoro katika ndoa. Sehemu ya kwanza tuliona Upande wa mwanaume, Leo tutaangazia upande wa mwanamke. Kwa kurejea mgogoro uliozuka katika ndoa ya kwanza ya Adamu. Kama hukupata sehemu ya kwanza tutumie msg inbox tukutumie uchambuzi wake.
Wewe kama mke.
Unapaswa utambue kuwa mume ndio kichwa cha Familia, Ndoa ya kwanza ulitikiswa na mwanamke, kuonyesha kuwa vyanzo vya migororo ya ndoa nyingi hadi sasa ni WANAWAKE.
Na hiyo yote ni kwasababu wepesi kufungua milango kwa shetani kuwadanganya kirahisi. Kwamba wao pia wajione wanauwezo wa kujiamulia tu mambo yao bila hata ya waume zao au kumshirikisha Mungu ? Hiyo ni hatari kubwa sana.
Usijaribu kufanya hivyo mwanamke, utaiharibu ndoa yako kwa mikono yako mwenyewe. Kinyume chake, anza kuwa MTIIFU kwa mume wako kama biblia inavyosema katika..
Waefeso 5:22 “ENYI WAKE, WATIINI WAUME ZENU KAMA KUMTII BWANA WETU. 23 Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe, kama Kristo naye ni kichwa cha Kanisa; naye ni mwokozi wa mwili. 24 Lakini kama vile Kanisa limtiivyo Kristo vivyo hivyo wake nao wawatii waume zao katika kila jambo”.
Waefeso 5:22 “ENYI WAKE, WATIINI WAUME ZENU KAMA KUMTII BWANA WETU.
23 Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe, kama Kristo naye ni kichwa cha Kanisa; naye ni mwokozi wa mwili.
24 Lakini kama vile Kanisa limtiivyo Kristo vivyo hivyo wake nao wawatii waume zao katika kila jambo”.
Kuwa mtiifu, mume wako anapokutakana uwahi kurudi nyumbani, TII, anapokuambia nipikie chakula, Tii, anapokuambia nifulie nguo, usimwambie housegirl si yupo, anapokuambia fanya hivi, au fanya vile wewe tenda, anapokushauri usifanye shughuli Fulani, sio nzuri, tii pia, kwasababu yule ndio kichwa chao. Ondoa kiburi ndani yako, wewe sio kichwa, ukijaribu kufanya hivyo, ndipo hapo shetani atakupa mbinu mbadala, utafute marafiki/wanaume wengine nje ya ndoa yako wenye pesa, ili kumkomoa mume wako, kumbe hujui kuwa ndio unajiangamiza wewe mwenyewe. Ndicho alichokiwaza Hawa alipokwenda kutafuta mashauri kwa nyoka.
Kwahiyo, simama katika nafasi yako, ya utiifu. Mbinu aliyotumia shetani kumwangamiza Hawa, ndio hiyo hiyo ataitumia na kwako, isiposimama katika nafasi yako kama mwanandoa. Na majuto utayaona baadaye sio sasa wakati una kiburi.
Kumbuka, mwanamke hutakaa ufanikiwe kwa kujitenga na mume wako? Kamwe halitawezekana. Mwanaume anaweza kujaribu kuishi, japo itakuwa kwa shida sana, lakini wewe sahau kuishi kwasababu Ubavu hauna ubongo,wala mikono, wala miguu, wala pua, wala macho,. Ni kipande cha nyama tu. Ndivyo ilivyo kwako wewe, ujue kuwa huna Maisha nje ya mume wako wa ndoa. Ukimwacha leo, haijalishi, una kipato kikubwa kuliko yeye, au ni mjanja kuliko yeye, nataka nikuambie hauna Maisha wewe duniani.
Na mwisho kabisa, hayo yote unaweza kuyafikia, ikiwa tu upo ndani ya Kristo, Haiwezekani kuwa mtiifu, au mwombaji, au mtakatifu, au mtu wa kusamehe, kama hutakuwa ndani ya Kristo. Kwahiyo hatua ya kwanza ni kumpa Kristo Maisha yako.
Ikiwa upo tayari kufanya hivyo leo. Basi unaweza kufuatisha sala hii kwa Imani. Ukiifuatisha kwa kumaanisha kabisa ujue kabisa Bwana Yesu atakusamehe leo na kuja ndani yako….Tafuta sehemu ya utulivu kisha piga magoti, na useme sala hii kwa sauti.
“EE MUNGU BABA, NAJA MBELE ZAKO, NIKIWA NINAJITAMBUA KUWA MIMI NI MKOSAJI NA NIMEKUTENDA DHAMBI NYINGI, NA KWAMBA NIMESTAHILI HUKUMU, (KWA KUIJERUHI NDOA YANGU). LAKINI WEWE MUNGU WANGU ULISEMA KATIKA NENO LAKO KUWA WEWE NI MUNGU WA REHEMA UNAYEWAREHEMU MAELFU ELFU YA WATU WANAOKUPENDA WEWE. NA LEO HII NINAKUJA MBELE ZAKO NAHITAJI MSAMAHA WAKO NA MSAADA WAKO MUNGU WANGU, NINATUBU DHAMBI ZANGU ZOTE KWA KUMAANISHA NA KWA MOYO WANGU WOTE, NINAKIRI KUWA YESU KRISTO NI BWANA, NA YEYE NDIYE MWOKOZI WA HUU ULIMWENGUNI. HIVYO NAOMBA DAMU YA MWANAO TAKATIFU INISAFISHE UOVU WANGU WOTE SASA NIFANYIKE KUWA KIUMBE KIPYA KUANZIA LEO NA HATA MILELE.
ASANTE BWANA YESU KWA KUNIPOKEA NA KUNISAMEHE.
AMEN.”
Ikiwa umefuatisha sala hiyo kwa Imani, ujue kuwa Kristo ameshakusamehe na kuanzia sasa anza kuwajibika kwa ajili ya ndoa yako. Na kama hujabatizwa, na unahitaji kubatizwa katika ubatizo sahihi wa kuzamishwa katika maji mengi, na kwa jina la Yesu Kristo, basi wasiliana na sisi kwa namba hizi, +255693036618 au +255789001312 Tukusaidie.
Mungu akubariki sana.
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
KWANINI NDOA NYINGI ZINAVUNJIKA? (Sehemu ya 2: Upande wa wanawake)
Nini maana ya..“wakiwazuia watu wasioe” (1Timotheo 4:1)
Kwanini wajane vijana hawakupaswa kuandikwa?
NDOA NA TALAKA:
NINI TUNAJIFUNZA KWA THEOFILO MTUKUFU?
Katika siku hizi za mwisho, migogoro ya kindoa imekuwa ni mingi sana, kiasi kwamba ndoa kudumu hata mwaka mmoja, ni jambo la kushukuru sana. Kila kukicha mikwaruzano, hakuna amani, kila mmoja amemchoka mwenzake. Mpaka wengine kudhani huyo mwenzi aliyemuoa au aliyeolewa naye halikuwa chaguo sahihi kutoka kwa Mungu, hivyo suluhisho pekee ni kuachana.
Nataka nikuambie, kabla hujafikiria kuachana na huyo mwenzi wako, Tafuta kwanza kama kuna watu walishapitia tatizo kama hilo la kwako, na uone walilitatuaje tatuaje, au mwisho wao ulikuwaje..
Kumbuka kuvunjika kwa ndoa, ni kushindwa kwa pande zote mbili (au moja), kujua wajibu wake katika ndoa kama Neno la Mungu linavyoagiza..
Ndoa inafananishwa na safari ya Maisha/ ya wokovu, si wakati wote, itakuwa ni “HONEY MOON”, si wakati wote mtakuwa ni vijana, si wakati wote mtakuwa Pamoja, na si wakati wote mambo yataenda sawa.. Haijalishi ndoa hiyo, atakuwa ameifungishwa Mungu mwenyewe Kanisani au la. Kushuka na kupanda kutakuwa ni sehemu ya Maisha yenu.
Leo hii tutajifunza, mfano wa ndoa moja maarufu katika biblia, na jinsi ilivyokumbana na migogoro mikubwa sana, ambayo naamini ni Zaidi ya migogoro ya ndoa zote zilizowahi kutokea ulimwenguni, lakini Pamoja na hayo bado iliendelea kudumu hadi dakika ya mwisho, naamini kwa kupitia hiyo itakuponya na wewe pia ambaye kwenye ndoa yako zimeshaanza kuonekana dalili za nyufa.
Na ndoa hiyo si nyingine Zaidi ya ile ya ADAMU.
Adamu alichaguliwa mke na Mungu mwenyewe, tena aliyeumbwa kutoka katika ubavu wake kabisa,kuonyesha kuwa ni wake kweli kweli,. Lakini waliishi kwa kipindi Fulani kirefu kwa raha na furaha bila taabu wala shida yoyote, hadi siku mambo yalipoanza kubadilika,
Na yalibadilika, kwa kukengeuka kwa mwanamke kwanza, pale ambapo aliacha kusikiliza maagizo ya mume wake(aliyopewa na Mungu), ya kutokula matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya, lakini yeye akayala kwa tamaa ya kutaka kuwa kama Mungu, ya kutaka kuwa kichwa (yaani kumzidi hata mume wake),ya kutaka kumiliki, akayala bila kumshirikisha mume wake, lakini kinyume chake ni kuwa tamaa hiyo Mungu aliipindua na kuihamishia kwa mume wake badala yake, na ndio maana utaona leo hii kwanini wanaume wanauchu wa kutawala, kuwa vichwa, hiyo tamaa mwanzoni haikuwepo kwao bali ilikuwa kwa mwanamke, baada ya kuasi Mungu ndio akamuadhibu mwanamke kwa kosa hilo la kumuhamishia mwanaume.
Mwanzo 3:16 “Akamwambia mwanamke, Hakika nitakuzidishia uchungu wako, na kuzaa kwako; kwa utungu utazaa watoto; na tamaa yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala”.
Sasa na baadaye Adamu alipoona, mke wake kaharibu, ameasi, akakubali na yeye, kuingia katika matatizo ya mke wake kwa hiari yake yeye mwenyewe (kwasababu yeye hakudanganywa), na baada ya hapo, Mungu akamlaani naye pia.
Tangu huo wakati, Maisha yakawa magumu kweli, kwasababu dhambi imeshaingia, kulima kwa shida kukanza, magonjwa yakazuka, vifo vikaingia, kila aina ya shida ikazuka tangu huo wakati na kuendelea, kila kukicha hali ndio ilizidi kuwa mbaya, hadi kwa Watoto waliowazaa, hakuna amani katikati yao, wakawa wanauana.. Embu tengeneza picha ingekuwa wewe ni Adamu ungemfanyaje huyo mwanamke baada ya hapo?
Ni wazi kuwa ungempa talaka siku ile ile ya kwanza alipofanya kosa lile si ndio?. Tena baada ya hapo ungekuwa ni wa kulaumu Maisha yako yote, kwamba Mungu amekupa mkosi na balaa, ni heri ungebakia tu peke yako bila kuoa, lakini tangu ulipompata huyo mwanamke, mambo yako ndio yameenda kombo kabisa kabisa…
Lile kampuni amelifilisi, mali zote zimepukutika umerudia umaskini ambao ulikuwa umeshauaga zamani, amekuletea gonjwa la ukimwi kwa kutanga tanga kwake, amekufanya utengane sio tu na ndugu zako, bali hata na Mungu wako. Mwanzoni ulikuwa ukifanya ibada vizuri, lakini tangu umuoe yule mwanamke, muda kusali haupo! Kila kitu unakipata kwa shida, tofauti na ulivyokuwa ‘Single’.
Lawama kama hizo Adamu angestahili kuwa nazo kwa mke wake, Lakini hatuoni mahali popote Adamu alimwacha mke wake, na kutamani kuishi na wanyama kama hapo mwanzo, bali alimkumbatia, akakubaliana na hali, akamsamehe, akayapanga tena upya. Akijua kuwa ule tayari ni ubavu wake. Na Mungu hakukosea kumpa, lilikuwa ni chaguo sahihi.
Mwanaume,
Kumbuka kuwa, mpaka umefikia hatua ya kumwoa huyo binti/ mwanamke, ujue kuwa ndio UBAVU wako huo Mungu aliokupa, usidhani kumtambua mke mwema ni mpaka uishi naye bila migogoro, sikuzote za Maisha yako, si kweli. Huyo ambaye upo naye katika migogoro, ni wako, na atabakia kuwa wako mpaka kifo kitakapowatenganisha.
Unachopaswa kufanya ni wewe kusimama katika nafasi yako kama ADAMU.
Suluhisho sio kumwacha, kumbuka ukimwacha huyo maana yake, unataka kurudia kuishi na Wanyama, Mpende mke wako, kwasababu hakuna kitu kinachojenga Zaidi ya upendo, mkumbatie, msamehe, mjenge upya, mvumilie, pale anapokosa, hata kama alikuletea balaa kubwa namna gani, mkumbuke Adamu, alivyoweza kuwa mvumilivu, kwa kunyang’anywa kila kitu na Mungu lakini hakumwacha Hawa. Kwani biblia inasema aliishi miaka 930, na unajua mara nyingi wanawake huwa wanakuwa na umri mrefu kuliko wanaume, kwahiyo si ajabu kuona Adamu aliishi na mke wake kwa Zaidi ya miaka hata 800, lakini sisi miaka 3 tu tumeshachokana.
Biblia inasema..
Waefeso 5:25 “Enyi waume, WAPENDENI WAKE ZENU, kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake; 26 ili makusudi alitakase na kulisafisha kwa maji katika neno; 27 apate kujiletea Kanisa tukufu, lisilo na ila wala kunyanzi wala lo lote kama hayo; bali liwe takatifu lisilo na mawaa. 28 Vivyo hivyo imewapasa waume nao kuwapenda wake zao kama miili yao wenyewe. Ampendaye mkewe hujipenda mwenyewe. 29 Maana hakuna mtu anayeuchukia mwili wake po pote; bali huulisha na kuutunza, kama Kristo naye anavyolitendea Kanisa. 30 Kwa kuwa tu viungo vya mwili wake. 31 Kwa sababu hiyo mtu atamwacha baba yake na mama yake, ataambatana na mkewe na hao wawili watakuwa mwili mmoja”.
Waefeso 5:25 “Enyi waume, WAPENDENI WAKE ZENU, kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake;
26 ili makusudi alitakase na kulisafisha kwa maji katika neno;
27 apate kujiletea Kanisa tukufu, lisilo na ila wala kunyanzi wala lo lote kama hayo; bali liwe takatifu lisilo na mawaa.
28 Vivyo hivyo imewapasa waume nao kuwapenda wake zao kama miili yao wenyewe. Ampendaye mkewe hujipenda mwenyewe.
29 Maana hakuna mtu anayeuchukia mwili wake po pote; bali huulisha na kuutunza, kama Kristo naye anavyolitendea Kanisa.
30 Kwa kuwa tu viungo vya mwili wake.
31 Kwa sababu hiyo mtu atamwacha baba yake na mama yake, ataambatana na mkewe na hao wawili watakuwa mwili mmoja”.
UPENDO KWA MKE wako, ni agizo kutoka kwa Mungu, na sio ihari yako tu mwenyewe. Ukiwa mwanaume wa namna hii, nataka nikuambie utaiponya ndoa yako, na itadumu sana. Wanawake kukengeuka haraka, ni jambo la kawaida, lakini wakisharudi, wanakuwa ni lulu nzuri kwako. Jifunze kusamehe, na vilevile kumpenda.
Lakini hayo yote huwezi kuyafikia kama upo nje ya Kristo. Hivyo Okoka, mkaribishe Yesu katika Maisha yako, tubu dhambi zako, kwa kumaanisha kabisa, kisha ubatizwe, upokee Roho Mtakatifu, na Kristo atakupa uwezo huo, wa kumpenda mkeo kama alivyokuwa Adamu.
Usikose, sehemu ya pili ya Makala hii.. Ambayo inamlenga mwanamke, kama chanzo cha migogoro ndani ya ndoa, na afanye nini ili aweze kuiponya ndoa yake.
Je! “Mke wa ujana wako” ni yupi kibiblia?
Ndoa ya serikali ni halali?
NDOA NA HARUSI TAKATIFU.
MISTARI YA BIBLIA KUHUSU NDOA.
WhatsApp
Tukisoma 2Samweli 24:13, tunaona biblia imesema ni miaka 7 imewekwa mbele ya Dauidi, Lakini tukienda kusoma tena habari hiyo hiyo katika kitabu cha 1Nyakati 21:12, tunaona biblia inataja miaka 3 ya njaa na si 7 tena. Je! Ipi ni ipi?
Labda tuanze kusoma habari hiyo katika kitabu cha 2 Samweli..
2Samweli 24:11 “Na Daudi alipoondoka asubuhi, neno la Bwana likamjia nabii Gadi, mwonaji wake Daudi, kusema, 12 Nenda, ukanene na Daudi, Bwana asema hivi, Nakuwekea mambo matatu; katika haya uchague moja, nikutendee hilo. 13 Basi Gadi akamwendea Daudi, akamweleza, akamwambia, Basi, MIAKA SABA YA NJAA ikujie katika nchi yako? Au miezi mitatu ukimbie mbele ya adui zako, huku wakikufuatia? Au siku tatu iwe tauni katika nchi yako? Fanya shauri sasa, ufikiri, ni jawabu gani nimrudishie yeye aliyenituma”.
2Samweli 24:11 “Na Daudi alipoondoka asubuhi, neno la Bwana likamjia nabii Gadi, mwonaji wake Daudi, kusema,
12 Nenda, ukanene na Daudi, Bwana asema hivi, Nakuwekea mambo matatu; katika haya uchague moja, nikutendee hilo.
13 Basi Gadi akamwendea Daudi, akamweleza, akamwambia, Basi, MIAKA SABA YA NJAA ikujie katika nchi yako? Au miezi mitatu ukimbie mbele ya adui zako, huku wakikufuatia? Au siku tatu iwe tauni katika nchi yako? Fanya shauri sasa, ufikiri, ni jawabu gani nimrudishie yeye aliyenituma”.
Hapo tunaona kweli ni miaka 7, Lakini tusome tena habari hiyo katika Mambo ya Nyakati.
1Nyakati 21:11 “Basi Gadi akamwendea Daudi, akamwambia, Bwana asema hivi, Kubali upendavyo; 12 MIAKA MITATU YA NJAA; au miezi mitatu kuangamia mbele ya adui zako, ukipatwa na upanga wa watesi wako; au siku tatu upanga wa Bwana, yaani tauni katika nchi, na malaika wa Bwana akiharibu kati ya mipaka yote ya Israeli. Haya basi ufikiri ni jawabu gani nimrudishie yeye aliyenituma”.
1Nyakati 21:11 “Basi Gadi akamwendea Daudi, akamwambia, Bwana asema hivi, Kubali upendavyo;
12 MIAKA MITATU YA NJAA; au miezi mitatu kuangamia mbele ya adui zako, ukipatwa na upanga wa watesi wako; au siku tatu upanga wa Bwana, yaani tauni katika nchi, na malaika wa Bwana akiharibu kati ya mipaka yote ya Israeli. Haya basi ufikiri ni jawabu gani nimrudishie yeye aliyenituma”.
Kwa mistari hiyo ni rahisi kusema biblia inajichanganya.. Lakini kiuhalisia, biblia haijichanganyi mahali popote, wala haijakosewa mahali popote.
Katika habari hiyo, waandishi wote wawili wa vitabu hivyo, walikuwa wapo sahihi.. hakuna ambaye hakuwa sahihi, kwasababu wote walikuwa wanaongozwa na Roho Mtakatifu katika kuandika. Isipokuwa kila mmoja aliandika katika mazingira tofauti na mwenzake, na hawakunakiliana hivyo, ushuhuda wa mmoja hauwezi kufanana asilimia mia na wa mwingine.
Hebu chukua mfano, umefungua taarifa ya habari katika vyombo viwili tofauti, ni wazi kuwa unaweza kusikia habari moja lakini imefafanuliwa tofauti katika vyombo vyote viwili lakini habari ni ile ile moja.
Habari hizo haziwezi kufanana asilimia mia, vinginevyo kimoja kitakuwa kimenakili habari ya mwingine kama ilivyo.
Kadhalika kitabu cha Samweli sio nakala ya kitabu cha Mambo ya Nyakati, kadhalika kitabu cha Luka sio nakala ya kitabu cha Mathayo..ingawa vyote vinaweza kuwa vinaelezea matukio yanayofanana, lakini haviwezi kufanana asilimia mia, kwasababu ni mashahidi wawili tofauti. Ndio maana unaona Ushuhuda wa Luka haifananini asilimia mia na wa Mathayo au Marko.
Sasa labda turudi katika habari hiyo ya Daudi..
Tukianza na kitabu hicho cha 2Samweli 24, labda turudi sura mbili nyuma, tuone ni tukio gani lilitokea.. kisha tutaanza kuelewa ni kwasababu gani Mwandishi hapa kataja miaka 7 badala ya 3..
Tusome,
2Samweli 21:1 “Kulikuwa na njaa siku za Daudi MUDA WA MIAKA MITATU, MWAKA KWA MWAKA; naye Daudi akautafuta uso wa Bwana. Bwana akasema, Ni kwa ajili ya Sauli, na kwa nyumba yake yenye damu, kwa kuwa aliwaua hao Wagibeoni”.
Umeona hapo? Kabla Daudi kutaka kwenda kuwahesabu watu, kulitangulia njaa miaka 3, ambapo njaa hiyo ilisababishwa na Sauli kuwaua wagibeoni.
Sasa baada ya Daudi kutafuta utatuzi wa njaa hiyo, maandiko yanatuambia alifanya kosa lingine la kwenda kuwahesabu Israeli, jambo ambalo lingeiingiza tena Israeli katika baa la njaa kwa miaka mingine 3 mbele. Na kama ukisoma pale, Sensa ya kuwahesabu Israeli ilichukua miezi kama 9 na siku 20 (2Samweli 24:8).
Kwahiyo ukichukua Miaka 3 ya njaa iliyosababishwa na Sauli, ukijumlisha na hiyo miezi 9.. utaona ni kipindi cha takribani Miaka 4. Na maandiko yanasema baada ya Daudi kuwahesabu Israeli ndipo Neno la Bwana likamjia..kwahiyo inawezekana ikawa siku ile ile alipomaliza kuwahesabu au wiki moja baadaye au mwezi mmoja baadaye ndipo Neno la Bwana likamjia.. Lakini yote katika yote miaka 4 iliisha ambayo ilikuwa ya njaa..kabla ya kuja mingine 3 kwaajili ya kosa hilo la kwenda kuwahesabu.
Kwahiyo ukichukua hiyo miaka 3 ya Sauli, ukajumlisha KIPINDI CHA MWAKA MZIMA cha SENSA, Pamoja na Neno la Bwana kumjia Daudi, Ukajumlisha na MIAKA HIYO 3 Daudi aliyoambiwa achague, Jumla yake utapata ni miaka 7.
Kwahiyo Mwandishi wa katika kitabu hicho cha Samweli alichokuwa anakimaanisha ni kwamba Endapo Daudi atachagua janga la miaka 3 ya njaa.. atakuwa amefanya JUMLA ya miaka ya njaa katika Israeli kuwa SABA.
Lakini tukirudi kwa mwandishi wa kitabu cha Mambo ya Nyakati, yeye alikwenda moja kwa moja kwenye hiyo miaka 3 ya mwisho, pasipo kuhesabu ile 3 ya kwanza iliyotangulia, pamoja na ule mmoja wa Sensa. Na ndio maana utaona katika kitabu hicho cha Mambo ya Nyakati hajaeleza popote kuhusu Njaa hiyo ya kwanza iliyosababishwa na Sauli…kama alivyoeleza mwandishi wa kitabu cha Samweli.
Kwahiyo hakuna utata wowote katika hiyo mistari.
Sasa ilikuwepo sababu kwanini Mungu achukizwe na Daudi katika kwenda kuwahesabu Israeli..Sababu hiyo kwa urefu unaweza kuisoma hapa>> USIZITEGEMEE NGUVU ZAKO KUKUSAIDIA
Mwisho, tukumbuke kuwa Kristo yupo mlangoni kurudi kulinyakua kanisa lake.. na atakuja kama mwivi, Je! umejiandaa?. Kama bado mwamini Yesu leo, na kubatizwa, upate ondoleo la dhambi.
Bwana atubariki.
Maran atha!
NJAA ILIYOPO SASA.
HUYU MELKIZEDEKI NI NANI?
RUDIA, TENA NA TENA KUMWOMBA MUNGU USIKATE TAMAA.
KUJIPAMBA NI DHAMBI?
Hii ni sehemu ya tatu ya mfululizo wa masomo kwa wanawake, katika sehemu ya kwanza na ya pili tumeona, ni kwanini Bwana aliwatambua baadhi ya wanawake, kwa jinsia zao, na sio kwa majina yao, kwa kuwaita “wanawake”, na sehemu nyingine kuwatambua kwa mionekano yao kwa kuwaita “Binti” na sio labda kwa majina yao..ipo sababu, ikiwa hujapata bado, chambuzi zake, basi tutumie msg inbox tukutumie..
Lakini leo tutasonga mbele tena, kuona ni kwanini baadhi ya wanawake, aliwatambua kwa majina ya “MAMA”.
Mama ni cheo cha ukomavu, kwasababu mpaka uitwe mama ni wazi kuwa lazima utakuwa na watoto uliowazaa au unaowalea chini yako. Sasa tukirudi kwa Bwana Yesu, kuna wanawake aliwaona ni “Wamama rohoni”, sio mwilini, kwasababu kulikuwa na wanawake wengi, lakini si wote aliwaita “Mama” kama tu vile si wote aliwaita “Binti yangu”, bali baadhi tu.
Sasa embu twende tukasome baadhi ya Habari katika biblia kisha tuone, ni nini Bwana anatufundisha katika Habari husika. Mwanamke wa kwanza tutakayemtazama ni yule mkananayo. Tusome;
Mathayo 15:21 “Yesu akaondoka huko, akaenda kando pande za Tiro na Sidoni.22 Na tazama, mwanamke Mkananayo wa mipaka ile akatokea, akampazia sauti akisema, Unirehemu, Bwana, Mwana wa Daudi; binti yangu amepagawa sana na pepo.23 Wala yeye hakumjibu neno. Nao wanafunzi wake wakamwendea, wakamwomba, wakisema, Mwache aende zake; kwa maana anapiga kelele nyuma yetu.24 Akajibu, akasema, Sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli.25 Naye akaja akamsujudia, akisema Bwana, unisaidie.26 Akajibu, akasema, Si vema kukitwaa chakula cha watoto na kuwatupia mbwa.27 Akasema, Ndiyo, Bwana, lakini hata mbwa hula makombo yaangukayo mezani pa bwana zao.28 Ndipo Yesu akajibu, akamwambia, MAMA, IMANI YAKO NI KUBWA; na iwe kwako kama utakavyo. Akapona binti yake tangu saa ile”.
Mathayo 15:21 “Yesu akaondoka huko, akaenda kando pande za Tiro na Sidoni.
22 Na tazama, mwanamke Mkananayo wa mipaka ile akatokea, akampazia sauti akisema, Unirehemu, Bwana, Mwana wa Daudi; binti yangu amepagawa sana na pepo.
23 Wala yeye hakumjibu neno. Nao wanafunzi wake wakamwendea, wakamwomba, wakisema, Mwache aende zake; kwa maana anapiga kelele nyuma yetu.
24 Akajibu, akasema, Sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli.
25 Naye akaja akamsujudia, akisema Bwana, unisaidie.
26 Akajibu, akasema, Si vema kukitwaa chakula cha watoto na kuwatupia mbwa.
27 Akasema, Ndiyo, Bwana, lakini hata mbwa hula makombo yaangukayo mezani pa bwana zao.
28 Ndipo Yesu akajibu, akamwambia, MAMA, IMANI YAKO NI KUBWA; na iwe kwako kama utakavyo. Akapona binti yake tangu saa ile”.
Angalia asili ya huyu mwanamke, hakumtafuta Bwana kwa shida zake mwenyewe, au kwa matatizo yake mwenyewe, bali alimtafuta Bwana Yesu kwa shida za mwanawe.. Japokuwa mwanzoni hakujibiwa chochote, hata baada ya pale alipewa na maneno ya kukatishwa tamaa ya kuitwa mbwa, lakini bado hakuacha kuomba kwa shida ya mtu mwingine, kwasababu uzito wa mwanae ulikuwa kama wakwake.
Hiyo ni kuonyesha ni jinsi gani asivyojali vya kwake tu, bali hata vya wengine…
Mwanamke mwingine ni Mama yake Yesu mwenyewe, ambaye tunamsoma katika Yohana 2:1-4 siku ile alipoalikwa katika Harusi..
Yohana 2:1 “Na siku ya tatu palikuwa na arusi huko Kana, mji wa Galilaya; naye mama yake Yesu alikuwapo.2 Yesu naye alikuwa amealikwa arusini pamoja na wanafunzi wake.3 Hata divai ilipowatindikia, mamaye Yesu akamwambia, Hawana divai. 4 Yesu akamwambia, MAMA, TUNA NINI MIMI NAWE? Saa yangu haijawadia”.
Yohana 2:1 “Na siku ya tatu palikuwa na arusi huko Kana, mji wa Galilaya; naye mama yake Yesu alikuwapo.
2 Yesu naye alikuwa amealikwa arusini pamoja na wanafunzi wake.
3 Hata divai ilipowatindikia, mamaye Yesu akamwambia, Hawana divai. 4 Yesu akamwambia, MAMA, TUNA NINI MIMI NAWE? Saa yangu haijawadia”.
Angalia tabia yake alijali shida za wengine, aibu za wengine, akazifanya kama ni za kwake. Na kumpelekea Kristo, na muda huo huo akamwita “mama”
Mwingine ni Mariamu Magdalena, asubuhi ile ya kufufuka kwa Bwana, alikuwa akilia pale makaburini ndipo Yesu akamtokea na kumwambia “Mama unalilia nini?” Saa hiyo hiyo Yesu akamtuma kwa ndugu zake kwenda kuwatangazia injili. Akawa mtu wa kwanza kupewa neema ya kuwahubiria watu wengine Habari za kufufuka kwa Bwana Yesu. (Yohana 20:11-18)..
Neema hiyo si kila mwanamke atapewa, bali ni wale “wamama rohoni tu” Wanawake waliokomaa kiroho,ambao wanajua wajibu wao kwa Bwana, wanajua kuwaongoza wengine katika njia za Mungu, haijalishi umri wao Rohoni watu kama hawa, wanawekwa kundi moja na akina Sara, na Rebeka, na Mariamu, na Elizabeti na wengineo. Kwasababu wamevuka viwango cha utoto, hadi kufikia hatua ya utu uzima ya kuzaa na kulea.
Swali ni je! Wewe, dada upo katika kundi gani? Bwana anapokuona anakutambuaje? msichana? Au Mtu? Mtoto? Au Mama?. Kabla hujafikiria kuyatazama Maisha ya mitume wa Yesu mfano wakina Petro waliishije, embu tafakari kwanza, Maisha ya wanawake wacha Mungu katika biblia waliishije. Hiyo itakusaidia sana mwanamke.
Tamani sana, Kristo akutambue kama “Mama” Ni heshima ya juu sana, Kristo anaweza kumpa mwanamke, iliyosawa na ya “Kitume”. Kua kiroho timiza wajibu wako wa kuitangaza injili na pia kuwasaidia wengine kumjua Mungu rohoni.
Maran atha.
MWANAMKE, BINTI, MAMA. (Sehemu ya 2)
MWANAMKE, BINTI, MAMA. (Sehemu ya 3)
TUJIFUNZE JAMBO KWA WANAWAKE HAWA WAWILI:
MAMA, TAZAMA, MWANAO.
Sadaka ya unga na sadaka ya kinywaji zilikuwaje?
SWALI: Je! Siku ya unyakuo watoto wachanga watanyakuliwa? Na vipi kuhusu walio bado tumboni, na wenyewe watanyakuliwa au wataachwa?
JIBU: Hili ni moja ya swali gumu kwasababu biblia haijaeleza moja kwa moja ni nini kitawatokea watoto siku ile ya Unyakuo, Hivyo tutajaribu kueleza kwa kadiri ya tunavyoona katika baadhi ya vifungu kwenye maandiko.
Ukitazama katika biblia, utaona, wapo watoto walipata neema kutokana na haki za wazazi wao, mfano wa hawa ni watoto wa Nuhu, na Lutu, vilevile wapo watoto walioadhibiwa kutokana na makosa ya wazazi wao. Utaliona hilo pia katika vile vizazi vyote vya Sodoma na Gomora, pamoja na gharika vyote viliteketezwa, hadi watoto walipata adhabu kwa dhambi za wengine. Lakini hiyo haimaanishi kuwa wataadhibiwa tena baada ya kifo.
Pia tukumbuke kuwa hata katikati ya kipindi cha dhiki kuu, bado watu wataendelea kutungishwa mimba na kuzaliwa, hivyo litakuwepo kundi la vichanga ambavyo vitazaliwa katikati ya dhiki kuu na vitakufa katika maangamizi yao..Hilo tunalithibitisha katika andiko hili;
Mathayo 24:19 “Ole wao wenye mimba na wanyonyeshao siku hizo!20 Ombeni, ili kukimbia kwenu kusiwe wakati wa baridi, wala siku ya sabato.21 Kwa kuwa wakati huo kutakuwapo dhiki kubwa, ambayo haijatokea namna yake tangu mwanzo wa ulimwengu hata sasa, wala haitakuwapo kamwe.22 Na kama siku hizo zisingalifupizwa, asingeokoka mtu ye yote; lakini kwa ajili ya wateule zitafupizwa siku hizo”.
Mathayo 24:19 “Ole wao wenye mimba na wanyonyeshao siku hizo!
20 Ombeni, ili kukimbia kwenu kusiwe wakati wa baridi, wala siku ya sabato.
21 Kwa kuwa wakati huo kutakuwapo dhiki kubwa, ambayo haijatokea namna yake tangu mwanzo wa ulimwengu hata sasa, wala haitakuwapo kamwe.
22 Na kama siku hizo zisingalifupizwa, asingeokoka mtu ye yote; lakini kwa ajili ya wateule zitafupizwa siku hizo”.
Unaona? Kwahiyo siku ile ikifika, kuna uwezekano wa watoto wengine kunyakuliwa (hata wale walio tumboni), na vilevile wengine kubaki, japo hatuwezi kusema hivyo ndivyo ilivyo, Yote tunamwachia Mungu. Ikiwa ni wote watanyakuliwa, au ni baadhi, Tunachopaswa kufahamu ni kuwa Mungu ni wa haki, atayaleta yote katika mizani, na yote yatakuwa sawa tu mwisho wa siku, na tutaona kabisa hukumu zake ni za haki. Kama vile Malaika mbinguni wanavyokiri hivyo..
Ufunuo 16:7 “Nikaisikia hiyo madhabahu ikisema, Naam, Bwana Mungu Mwenyezi, ni za kweli, na za haki, hukumu zako”.
Cha muhimu tunachopaswa kujua ni kuwa sisi ambao tayari tumeshafikia kimo cha kuyajua mema na mabaya, Kama hatutayatengeneza mambo yetu sasa, kwa kumpokea Bwana Yesu Kristo kwa kumaanisha kabisa, na kujitwika misalaba yetu na kumfuata, tujue kuwa unyakuo ukipita tutaachwa. Na matokeo yake, yatakuwa ni kuingia katika mateso makali ya dhiki kuu pamoja na Jehanamu ya moto.
Je! Umeokoka? Je! Umebatizwa katika ubatizo sahihi wa kuzamishwa katika maji mengi na kwa jina la Yesu Kristo kwa ajili ya ondoleo la dhambi zako? Kumbuka Unyakuo ni wakati wowote, tubu umruidie muumba wako. Parapanda ni siku yoyote inalia, hakuna dalili iliyosalia..
Bwana Yesu akubariki.
Maran Atha.
JE! WATOTO WACHANGA WANAWEZA KUHUKUMIWA NA KUTUPWA MOTONI.
SIKU YA UNYAKUO ITAKUKUTAJE?
Na hekima imejulikana kuwa ina haki kwa watoto wake wote.
NI LIPI KATI YA MAKUNDI HAYA, WEWE UPO?
Ni kweli Paulo alipuuzia maonyo aliyopewa ya kwenda Yerusalemu?
Mwerezi ni aina ya mti uliokuwa unapatikana maeneno ya nchi ya Lebanoni, Ulikuwa unastawi pia sehemu mbalimbali za dunia, lakini ulistawi zaidi katika nchi ya Lebanoni, iliyopo kaskazini mwa nchi ya Israeli.
Aina hii ya mti ilitumika kwa matumizi mengi, kutokakana ubora wake na uimara wake ukulinganisha na aina nyingine ya miti. Mti huu wa Mwerezi ulikuwa ni mgumu na usiooza kirahisi.
Nchi ya Lebanoni, ilijipatia utajiri kutokana na biashara ya miti hii, ambapo Mataifa mengi duniani kama Misri, Ashuru, Babeli na Israeli ilinunua miti hii kutoka huko Lebanoni, kwaajili ya matumizi mbalimbali ikiwemo ya ujenzi.
Mfalme Daudi alitumia miti hii ya Mierezi kutoka Lebanoni kuijenga nyumba yake.
2Samweli 5:11 “Kisha Hiramu, mfalme wa Tiro, akatuma wajumbe kwa Daudi, AKAMPELEKEA NA MIEREZI, NA MASEREMALA, NA WAASHI; NAO WAKAMJENGEA DAUDI NYUMBA”.
2Samweli 7:2 “mfalme akamwambia Nathani, nabii, Angalia sasa, mimi ninakaa katika NYUMBA YA MIEREZI, bali sanduku la Mungu linakaa ndani ya mapazia.”
Lakini pia Nyumba ya Mungu ambayo ilikuja kujengwa na Sulemani, Mwana wa Daudi, ilitengenezwa pia kwa Mierezi mingi kutoka Lebanoni.
1Wafalme 5:5 “Nami, tazama, nakusudia kujenga nyumba kwa jina la Bwana, Mungu wangu, kama Bwana alivyomwambia Daudi baba yangu, akisema, Mwana wako, nitakayemweka katika kiti chake cha enzi mahali pako, ndiye atakayeijenga nyumba kwa jina langu. 6 BASI UAMURU WANIKATIE MIEREZI YA LEBANONI; na watumishi wangu watafuatana na watumishi wako; na ujira wa watumishi wako nitakupa kama utakavyosema; kwa kuwa wajua ya kwamba hakuna kwetu mtu ajuaye kukata miti kama Wasidoni”.
1Wafalme 5:5 “Nami, tazama, nakusudia kujenga nyumba kwa jina la Bwana, Mungu wangu, kama Bwana alivyomwambia Daudi baba yangu, akisema, Mwana wako, nitakayemweka katika kiti chake cha enzi mahali pako, ndiye atakayeijenga nyumba kwa jina langu.
6 BASI UAMURU WANIKATIE MIEREZI YA LEBANONI; na watumishi wangu watafuatana na watumishi wako; na ujira wa watumishi wako nitakupa kama utakavyosema; kwa kuwa wajua ya kwamba hakuna kwetu mtu ajuaye kukata miti kama Wasidoni”.
Na hata baada ya Mfalme Nebukadneza kuliharibu hekalu hilo la Sulemani, hekalu la pili lilipokuja kujengwa na wakina Zerubabeli, lilijengwa sehemu kwa miti hiyo ya Mierezi.
Ezra 3:6 “Tangu siku ya kwanza ya mwezi wa saba walianza kumtolea Bwana sadaka za kuteketezwa, lakini msingi wa hekalu la Bwana ulikuwa haujawekwa bado. 7 Tena waliwapa waashi na maseremala fedha; wakawapa watu wa Sidoni, na watu wa Tiro, chakula, na vinywaji, na mafuta, ili walete MIEREZI KUTOKA LEBANONI mpaka Yafa kwa njia ya bahari, kwa kadiri walivyopewa ruhusa na Koreshi, mfalme wa Uajemi”.
Ezra 3:6 “Tangu siku ya kwanza ya mwezi wa saba walianza kumtolea Bwana sadaka za kuteketezwa, lakini msingi wa hekalu la Bwana ulikuwa haujawekwa bado.
7 Tena waliwapa waashi na maseremala fedha; wakawapa watu wa Sidoni, na watu wa Tiro, chakula, na vinywaji, na mafuta, ili walete MIEREZI KUTOKA LEBANONI mpaka Yafa kwa njia ya bahari, kwa kadiri walivyopewa ruhusa na Koreshi, mfalme wa Uajemi”.
Hivyo Mwerezi katika biblia imetumika kama ishara ya UTAJIRI. Kama vile DHAHABU.
Tunaona vitu vikuu viwili vilivyotajwa sana katika ujenzi wa nyumba ya Mungu ni MWEREZI pamoja na DHAHABU. Kutokana na uthamani wa vitu hivyo.
Na kama Mti wa Mwerezi ulivyojipatia sifa hivyo, Bwana Mungu anasema walio Haki wote watasitawi kama Mwerezi.
Zaburi 92:12 “Mwenye haki atasitawi kama mtende, Atakua kama MWEREZI WA LEBANONI. 13 Waliopandwa katika nyumba ya Bwana Watasitawi katika nyua za Mungu wetu. 14 Watazaa matunda hadi wakati wa uzee, Watajaa utomvu, watakuwa na ubichi. 15 Watangaze ya kuwa Bwana ni mwenye adili, Mwamba wangu, ndani yake hamna udhalimu”.
Zaburi 92:12 “Mwenye haki atasitawi kama mtende, Atakua kama MWEREZI WA LEBANONI.
13 Waliopandwa katika nyumba ya Bwana Watasitawi katika nyua za Mungu wetu.
14 Watazaa matunda hadi wakati wa uzee, Watajaa utomvu, watakuwa na ubichi.
15 Watangaze ya kuwa Bwana ni mwenye adili, Mwamba wangu, ndani yake hamna udhalimu”.
Je! Wewe ni mwenye HAKI?
Kumbuka mwenye haki sio mtu anayesema anafanya mema huku yupo nje ya Kristo, hiyo sio tafsiri ya mwenye haki. Bali tafsiri ya mwenye haki ni mtu Yule, aliyempokea Yesu, na kubatizwa na kupokea kipawa cha Roho Mtakatifu, huyo ndiye anayehesabiwa haki kwa IMANI HIYO ya kumwamini Yesu. Mwingine yeyote ambaye hamwamini Bwana Yesu, na kujitumainia katika mambo yake anayoyafanya anayoamini kuwa ni mema, anakuwa bado si mwenye haki mbele za Mungu.
Lakini wote waliompokea Yesu, watasitawi na kuwa na heshima kama miti ya Mierezi.
WALA MSIUANGALIE MWILI, HATA KUWASHA TAMAA ZAKE.
Biblia inamaanisha nini inaposema “Mwenye haki huufikiri uhai wa mnyama wake”?
Kwanini Bwana alirejea Tiro na Sidoni kwa mfano wa Sodoma?
Shilo ni nini?
Katika biblia Shilo ulikuwa mji mtakatifu, ambapo Kabla ya Mungu kupachagua Yerusalemu kama mji atakaoweka jina lake milele, hapo kabla wana wa Israeli walikuwa wanakusanyiko huko Shilo, kama sehemu takatifu ya kufanyia ibada na kutolea dhabihu.
Na hata sanduku la agano mara tu baada ya wana wa Israeli kuingia nchi ya ahadi, mji uliotueuliwa kwaajili ya kuliweka sanduku hilo la agano la Mungu..ulikuwa ndio huo wa mji wa Shilo, ambapo sanduku hilo lilikaa mjini huko bila kutoka kwa miaka mingi mpaka Wafilisti walipokuja kulichukua kutoka huko sababu ya makosa ya wana wa Israeli (1Samweli 10-11).
Huko Shilo pia ndiko Nabii Samweli alikolelewa maisha yake yote (1Samweli 1:24 )
Mji huu wa Shilo ulikuwa unapatikana kaskazini mji mwa mji wa Betheli, karibu na Samaria.
Unaweza kusoma zaidi kuhusu mji huo kupitia mistari ifuatayo > Yoshua 18:8-10, Yoshua 19:51, Yoshua 21:2, Waamuzi 18:31, Waamuzi 21:19, 1Samweli 1:9, Zaburi 78:60.
Lakini swali ni je! Hii Shilo mpaka leo ni sehemu takatifu?.
Jibu ni la!
Shilo ya Leo sio tena huko Israeli, bali ni katika Neno la Mungu.
Katika Kweli ya Neno la Mungu na katika Roho Mtakatifu..tunamwabudu Baba..kama Bwana Yesu alivyosema..
Yohana 4:21 “Yesu akamwambia, Mama, unisadiki, saa inakuja ambayo hamtamwabudu Baba katika mlima huu, wala kule Yerusalemu. 22 Ninyi mnaabudu msichokijua; sisi tunaabudu tukijuacho; kwa kuwa wokovu watoka kwa Wayahudi. 23 Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu”
Yohana 4:21
“Yesu akamwambia, Mama, unisadiki, saa inakuja ambayo hamtamwabudu Baba katika mlima huu, wala kule Yerusalemu.
22 Ninyi mnaabudu msichokijua; sisi tunaabudu tukijuacho; kwa kuwa wokovu watoka kwa Wayahudi.
23 Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu”
Je umempokea Roho Mtakatifu, je unaliishi Neno?.
Nini maana ya Dirii, Chepeo na Utayari?
Raheli aliwalilia vipi watoto wake?
Nini maana ya “Ulipo mzoga, ndipo watakapokutanika tai?
Kisima cha joka na lango la jaa ni nini?(Nehemia 2:13)
Jibu: Tusome,
Matendo 12:20 “Naye Herode ALIKUWA AMEWAKASIRIKIA SANA WATU WA TIRO NA SIDONI; wakamwendea kwa nia moja, na wakiisha kufanya urafiki na Blasto, mwenye kukitunza chumba cha mfalme cha kulalia, wakataka amani; kwa maana nchi yao ilipata riziki kwa nchi ya mfalme. 21 Basi siku moja iliyoazimiwa, Herode akajivika mavazi ya kifalme, akaketi katika kiti cha enzi, akatoa hotuba mbele yao. 22 Watu wakapiga kelele, wakisema, Ni sauti ya Mungu, si sauti ya mwanadamu. 23 Mara malaika wa Bwana akampiga, kwa sababu hakumpa Mungu utukufu; akaliwa na chango, akatokwa na roho”.
Matendo 12:20 “Naye Herode ALIKUWA AMEWAKASIRIKIA SANA WATU WA TIRO NA SIDONI; wakamwendea kwa nia moja, na wakiisha kufanya urafiki na Blasto, mwenye kukitunza chumba cha mfalme cha kulalia, wakataka amani; kwa maana nchi yao ilipata riziki kwa nchi ya mfalme.
21 Basi siku moja iliyoazimiwa, Herode akajivika mavazi ya kifalme, akaketi katika kiti cha enzi, akatoa hotuba mbele yao.
22 Watu wakapiga kelele, wakisema, Ni sauti ya Mungu, si sauti ya mwanadamu.
23 Mara malaika wa Bwana akampiga, kwa sababu hakumpa Mungu utukufu; akaliwa na chango, akatokwa na roho”.
Tiro na Sidoni ni miji iliyokuwepo kaskazini mwa mji wa Galilaya, miji hiyo kwasasa ni sehemu za Lebanoni.
Zamani za biblia Herodi ndiye alikuwa anatawala Yudea, na watu wa miji ya Tiro na Sidoni, walikuwa wanaitegemea Yudea kwa chakula. Lakini ulifika wakati Herode alichukizwa nao (biblia haijataja sababu ni nini), lakini alichukizwa nao, na akakatisha kuwauzia chakula hao watu wa Sidoni na Tiro.
Watu wa Tiro na Sidoni, walipokaa muda mrefu bila chakula, ikawabidi wakatafute amani na Herode huko Yudea, lakini njia waliyoitumia ni kumtafuta mtu aliyeitwa Blasto, ili amshawishi Herode waweze kuwa na mdahalo wa wazi na Hao watu wa Sidoni, kwasababu haikuwa rahisi Herode, kumfikia.
Huyu Blasto ambaye alikuwa anafanya kazi katika nyumba ya Mfalme Herode, na ambaye ndiye aliyekuwa mtu wake karibu kuliko wengine wote, alifanikiwa kumshawishi Herode azungumze na watu wa Tiro na Sidoni kwa wazi.
Hivyo siku ilipofika Herode alijitokeza kuzungumza na watu hao. Lakini kama inavyojulikana Herode alikuwa ni mtu wa kupenda utukufu, alikuwa anajitukuza yeye kama Mungu hapo Yudea. Alikuwa anapenda kuabudiwa kama Mungu. Alimuua Yakobo ndugu yake Yohana kwa upanga, na mwisho alimfunga Petro ili amuue kama alivyomuua Yakobo, lakini Malaika wa Bwana alimwokoa na mauti yake. Na hapa anasimama ili ajitukuze, awaonyeshe watu wa Sidoni na Tiro kwamba yeye ndiye anayetoa chakula!, pasipo yeye wao hawawezi kuishi.
Na watu wa Sidoni kwasababu ni watu wa kipagani waliozoea kuabudu miungu, na kumtukuza mtu yeyote ambaye wanamwona ni wa tofauti, kama wale watu wa Athene waliotaka kumtukuza Paulo na Barnaba..
Matendo 14:11 “Na makutano walipoona aliyoyafanya Paulo wakapaza sauti zao, wakisema kwa Kilikaonia, Miungu wametushukia kwa mifano ya wanadamu. 12 Wakamwita Barnaba, Zeu, na Paulo, Herme, kwa sababu ndiye aliyekuwa mnenaji”.
Matendo 14:11 “Na makutano walipoona aliyoyafanya Paulo wakapaza sauti zao, wakisema kwa Kilikaonia, Miungu wametushukia kwa mifano ya wanadamu.
12 Wakamwita Barnaba, Zeu, na Paulo, Herme, kwa sababu ndiye aliyekuwa mnenaji”.
Kadhalika na hawa watu wa Tiro na Sidoni walipomwona tu Herode kasimama anahutubia kimajivuno na kimajigambo kiasi kile, wote kwa pamoja wakaanza kupaza sauti zao na kusema “Hii ni sauti ya Mungu na si mtu..hii ni sauti ya Mungu na si mtu”
Tofauti na akina Paulo na Barnaba ambao wao walipoona watu wanawageuza miungu-watu walizirarua nguo zao na kuwaeleza kuwa wao ni watu tu kama wao, na sio Mungu. Kinyume chake Herode yeye hakufanya hivyo, bali moja kwa moja alizidi kujitukuza na kutaka kuchukua utukufu zaidi.
Na kwasababu Mungu hashiriki utukufu wake na wanadamu, pale pale Malaika wa Bwana alishuka akampiga Herode kwa change, Chango ni ugonjwa mbaya wa kuliwa na minyoo.. kwa maelezo marefu juu ya ugonjwa huu fungua hapa >>>>>> CHANGO KIBIBLIA
Lakini ni nini tunajifunza katika habari hiyo?
Tunachoweza kujifunza kikubwa ni kuwa Mungu hashirikiani utukufu na mwanadamu yeyote…Na ni jambo la hatari sana kutafuta ufukufu, jambo lililombadilisha shetani kutoka kuwa Kerubi na kuwa Ibilisi ni hilo hilo, la kutafuta kuabudiwa.
Na jambo lingine pia linalomhuzunisha Mungu sio sisi tu kutafuta kuabudiwa bali hata sisi tunapotafuta kuabudu watu au kitu kingine chochote.
Tunapoabudu sanamu, au watu, au fedha au kingine chotechote kile kuna hatari kubwa sana ya kuadhibiwa na Mungu.
Bwana atusaidie na kutubariki.
HERODE NA PILATO, MAADUI WAWILI WAPATANA.
TABIA ZA WATAKAOMKARIBIA SANA MUNGU SIKU ILE.
CHACHU YA MAFARISAYO NA CHACHU YA HERODE.
Jibu: Labda tuanze kusoma kuanzia juu kidogo..
Waefeso 5:31 “Kwa sababu hiyo mtu atamwacha baba yake na mama yake, ataambatana na mkewe na hao wawili watakuwa mwili mmoja. 32 SIRI HIYO NI KUBWA; ILA MIMI NANENA HABARI YA KRISTO NA KANISA. 33 Lakini kila mtu ampende mke wake kama nafsi yake mwenyewe; wala mke asikose kumstahi mumewe”
Waefeso 5:31 “Kwa sababu hiyo mtu atamwacha baba yake na mama yake, ataambatana na mkewe na hao wawili watakuwa mwili mmoja.
32 SIRI HIYO NI KUBWA; ILA MIMI NANENA HABARI YA KRISTO NA KANISA.
33 Lakini kila mtu ampende mke wake kama nafsi yake mwenyewe; wala mke asikose kumstahi mumewe”
Siri Paulo aliyoimaanisha hapo, sio nyingine Zaidi ya hiyo aliyoitaja hapo kwamba “WAWILI WATAKUWA MWILI MMOJA”. Hiyo ndiyo SIRI yenyewe.. Na kwanini iwe siri?, ni kwasababu ni jambo gumu kueleweka au kufafanulika kwamba watu wawili tofauti wenye miili miwili tofauti wamekutana halafu wanakuwa mwili mmoja, na ilihali ni watu wawili tofauti wenye miili miwili tofauti.. afadhali angesema “watakuwa nafsi moja au watakuwa wamoja”.. kidogo ingeweza kuwa rahisi kueleweka, lakini kuwa mwili mmoja? Hapo ni lazima kuna siri katikati yake.
Tunaona pia Bwana Yesu alilisisitiza tena jambo hilo hilo katika injili ya Marko.
Marko 10:7 “Kwa sababu hiyo mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; 8 NA HAO WAWILI WATAKUWA MWILI MMOJA; HATA WAMEKUWA SI WAWILI TENA, BALI MWILI MMOJA”
Marko 10:7 “Kwa sababu hiyo mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe;
8 NA HAO WAWILI WATAKUWA MWILI MMOJA; HATA WAMEKUWA SI WAWILI TENA, BALI MWILI MMOJA”
Kwahiyo hiyo ni SIRI kubwa sana.
Lakini biblia imetupa uvumbuzi wa siri hiyo, ni kwa jinsi gani, wawili wanakuwa mwili mmoja na si roho moja.
Na uvumbuzi huo tunaupata pale Mwanzo, Mungu alipowaumba Adamu na Hawa.. Biblia inasema
Mwanzo 2:21 “Bwana Mungu akamletea Adamu usingizi mzito, naye akalala; kisha akatwaa ubavu wake mmoja, akafunika nyama mahali pake, 22 na ule ubavu alioutwaa katika Adamu Bwana Mungu akaufanya mwanamke, akamleta kwa Adamu. 23 Adamu akasema, SASA HUYU NI MFUPA KATIKA MIFUPA YANGU, na NYAMA KATIKA NYAMA YANGU, basi ataitwa mwanamke, kwa maana ametwaliwa katika mwanamume. 24 Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja”.
Mwanzo 2:21 “Bwana Mungu akamletea Adamu usingizi mzito, naye akalala; kisha akatwaa ubavu wake mmoja, akafunika nyama mahali pake,
22 na ule ubavu alioutwaa katika Adamu Bwana Mungu akaufanya mwanamke, akamleta kwa Adamu.
23 Adamu akasema, SASA HUYU NI MFUPA KATIKA MIFUPA YANGU, na NYAMA KATIKA NYAMA YANGU, basi ataitwa mwanamke, kwa maana ametwaliwa katika mwanamume.
24 Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja”.
Hapo katika mstari wa 23, tunaona Adamu hakusema huyu ni “roho katika roho yangu” wala “nafsi katika nafsi yangu”..bali alisema huyu “ni nyama katika nyama yake”.. akimaanisha mwili wa mwanamke yule ni mwili wake…kwasababu katwaliwa kutoka kwake.
Kwahiyo mtu yeyote anayekwenda kuoa au kuolewa, yule aliyejiungamanisha naye, tayari wanakuwa mwili mmoja, kwasababu wote asili yetu ni Adamu. Na kama wanakuwa mwili mmoja maana yake, Baraka zote wanashiriki pamoja, na vile vile laana zote wanashiriki pamoja na mambo yote mazuri au mabaya, ya mwilini au rohoni wanakuwa wanashiriki pamoja.
Ndio maana kuna hatari kubwa sana ya kutoka nje ya ndoa na kuzini, au kufanya uasherati.. kwasababu yule unayezini naye, au unayefanya naye uasherati, kiroho unajiunganisha naye na kuwa mwili mmoja bila wewe kujijua, maandiko yanasema hivyo..
1Wakorintho 6:13 “…………….Lakini mwili si kwa zinaa, bali ni kwa Bwana, naye Bwana ni kwa mwili…………………. 15 Je! Hamjui ya kuwa miili yenu ni viungo vya Kristo? Basi nivitwae viungo vya Kristo na kuvifanya viungo vya kahaba? Hasha! 16 Au hamjui ya kuwa YEYE ALIYEUNGWA NA KAHABA NI MWILI MMOJA NAYE? MAANA ASEMA, WALE WAWILI WATAKUWA MWILI MMOJA”
1Wakorintho 6:13 “…………….Lakini mwili si kwa zinaa, bali ni kwa Bwana, naye Bwana ni kwa mwili………………….
15 Je! Hamjui ya kuwa miili yenu ni viungo vya Kristo? Basi nivitwae viungo vya Kristo na kuvifanya viungo vya kahaba? Hasha!
16 Au hamjui ya kuwa YEYE ALIYEUNGWA NA KAHABA NI MWILI MMOJA NAYE? MAANA ASEMA, WALE WAWILI WATAKUWA MWILI MMOJA”
Hivyo kahaba au mtu yeyote unayefanya naye uasherati, kama kuna Laana amezibeba katika maisha yake, wewe unayeshiriki naye, nawe pia unazibeba, kama ana roho na mapepo unaposhiriki naye uzinzi huo, yale mapepo nawe pia yanapata hifadhi ndani yako, (mnayashiriki pamoja) kwasababu tayari mmekuwa mwili mmoja.
Ndio maana moja ya amri za Mungu ni USIZINI! Kwasababu uzinzi una madhara makubwa sana kiroho na kimwili.
Wagalatia 5:19 “ Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, UASHERATI, uchafu, ufisadi, 20 ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi 21 husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu”.
Wagalatia 5:19 “ Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, UASHERATI, uchafu, ufisadi,
20 ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi
21 husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu”.
Bwana azidi atubariki.
Marna tha!
WALIPO WAWILI AU WATATU KWA JINA LANGU
Noeli ni nini, na je! Neno hili linapatikana katika biblia?
JISHUSHE ILI MUNGU AKUHUDUMIE.
Tofauti kati ya uchafu wa mwilini na rohoni ni ipi?