SWALI: Katika 2Wakorintho 6:7, Hizo Silaha za Mkono wa kuume na za mkono wa kushoto ni zipi?
JIBU: Tusome,
2Wakorintho 6:7 “katika neno la kweli, katika nguvu ya Mungu; kwa silaha za haki za mkono wa kuume na za mkono wa kushoto”
Mkono wa kuume ni mkono wa kulia, Hivyo kulingana na hilo andiko zipo silaha za mkono wa kulia na za mkono wa kushoto. Lakini kiuhalisia zipo silaha za miguuni pia, na za kifuani na za kichwani..Lakini hapa tutakwenda kuzizungumzia hizi za mikononi tu, maana ndizo zilizotajwa hapa.
Sasa swali hizo silaha ni zipi?
Jibu tunalipata katika kitabu cha Waefeso.
Waefeso 6:13 “Kwa sababu hiyo twaeni SİLAHA zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama. 14 Basi simameni, hali mmejifunga kweli viunoni, na kuvaa dirii ya haki kifuani, 15 na kufungiwa miguu utayari tupatao kwa Injili ya amani; 16 zaidi ya yote MKİİTWAA NGAO YA İMANİ, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu. 17 Tena ipokeeni chapeo ya wokovu, na UPANGA WA ROHO ambao ni neno la Mungu”
Waefeso 6:13 “Kwa sababu hiyo twaeni SİLAHA zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama.
14 Basi simameni, hali mmejifunga kweli viunoni, na kuvaa dirii ya haki kifuani,
15 na kufungiwa miguu utayari tupatao kwa Injili ya amani;
16 zaidi ya yote MKİİTWAA NGAO YA İMANİ, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu.
17 Tena ipokeeni chapeo ya wokovu, na UPANGA WA ROHO ambao ni neno la Mungu”
Ukimsoma vizuri huyu Askari utaona Kashika UPANGA mkono mmoja na Mkono wa pili kashikilia NGAO. Sasa hizo mbili “Ngao pamoja na Upanga” ndio silaha za mkono wa kuume na kushoto.
Biblia imeelezea hapo Ngano ni nini? Kwamba ni Imani,..Maana yake ni kwamba Imani ni silaha, na inafungiwa mkononi, maana yake haipaswi kuangushwa hata kidogo, tukiwa nayo hiyo, tuna uwezo wa kuizima mishale yote ya adui shetani, Vile vile kwa Imani tunaweza kufanya mambo yasiyowezekana Kulingana na Waebrania 11.
Na pia biblia imeelezea Upanga ni nini? Kwamba ni Neno la Mungu..Tukiwa na Neno la Mungu la kutosha ndani yetu, shetani na majeshi yake hawatatuweza kamwe. Tutamkata na majeshi yake vipande vipande, kwasababu tunalijua Neno.
Waebrania 4:12 “Maana Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo. 13 Wala hakuna kiumbe kisichokuwa wazi mbele zake, lakini vitu vyote vi utupu na kufunuliwa machoni pake yeye aliye na mambo yetu”
Waebrania 4:12 “Maana Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo.
13 Wala hakuna kiumbe kisichokuwa wazi mbele zake, lakini vitu vyote vi utupu na kufunuliwa machoni pake yeye aliye na mambo yetu”
Hivyo IMANI na NENO LA MUNGU, ni pacha, wanakwenda pamoja…na vyote vinashikiliwa mkononi na si miguuni, na vinategemeana…kama biblia inavyosema katika Warumi…
Warumi 10:17 “Basi İMANİ, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa NENO LA KRİSTO”.
Umeona hapo? Hizo ndio silaha mbili za Mkono wa kuume na kushoto.
Je! Na wewe unazo?..Kumbuka hizo huwezi kusema unazo kama hujawa askari, na lazima kuwe na vita mbele yako?. Kama hakuna vita vyovyote vya kiimani unavyopambana basi wewe bado sio askari, hauhitaji ngao wala upanga mikononi mwako. Kama unakwenda disko, au bar au kujiuza…Ngao ya nini hapo? Unakinga nini kutoka kwa yule adui? Katika roho mikono yako inaonekana imebeba matatizo tu.
Lakini unapokuwa mkristo kweli kweli na kuacha mambo yote ya dunia, hapo wewe ni askari tena unayeogopeka katika ulimwengu wa adui shetani, Na pia ndio unayewindwa zaidi, hivyo inakugharimu kukisha kila wakati ili usipatikane na madhara.
Bwana atujalie tuwe maaskari wa bora wa Kristo, huku tumevaa silaha zote za haki.
Maran atha!
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
MASOMO MBALIMBALI YA NENO LA MUNGU.
Je! Kusoma biblia kwenye simu ukiwa kanisani ni dhambi?
Je! habari ya Yusufu, inabeba ujumbe gani kwa agano jipya?
KUOTA UMECHOMWA KISU/KUOTA UMEPIGWA RISASI.
NENO LA MUNGU NI NINI?.
Rudi Nyumbani:
Print this post
Shalom, Karibu tuyatafakari maneno ya uzima ya Bwana wetu.
Ndugu, ukilikosa tumaini ambalo linapatikana kwa YESU tu peke yake, ni ngumu kuimaliza hii safari yako hapa duniani salama, haijalishi utajifanya una furaha kiasi gani, furaha hiyo ni feki ndugu yangu, huwezi kuushinda huu ulimwengu uliojaa vishawishi na shida na taabu, na mitego mingi ya adui, huwezi..Haijalishi utasema nina pesa nyingi kiasi gani, bado utafika mahali utachukuliwa na maji tu, hata ukimtegemea mwanadamu Fulani, bado uzima wa milele hutaweza kuupata.
Na ndio maana kuna wakati Bwana Yesu alisema ili nyumba iwe salama, ni lazima ijengwe kwanza juu ya msingi, vinginevyo ikijengwa bila msingi upo wakati hata upepo wa kasi ukivuma tu, nyumba hiyo itakuwa gofu.. Na msingi huo ni Yesu Kristo. Soma..
Mathayo 7:24 “Basi kila asikiaye hayo maneno yangu, na kuyafanya, atafananishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba; 25 mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, isianguke; kwa maana misingi yake imewekwa juu ya mwamba”.
Mathayo 7:24 “Basi kila asikiaye hayo maneno yangu, na kuyafanya, atafananishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba;
25 mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, isianguke; kwa maana misingi yake imewekwa juu ya mwamba”.
Lakini pia upo wakati utapitia mahali ambapo huwezi kuchimba msingi chini yako, kwasababu chini yapo maji mengi, ipo bahari, lipo ziwa, n.k. kwamfano wanaosafiri kwa meli, wanajua ili kujilinda na hatari ya upepo mkali au dhoruba, inawapasa watembee na kifaa kingine cha kipekee , kinachoitwa NANGA.
Nanga kazi yake ni kwenda chini sana, kuhakikisha inashuka mahali ambapo bahari au ziwa linaishia, na kukutana na mwamba chini, kisha inajikita pale,, sasa ikishanasa hapo hata dhoruba ya upepo mkali ikipita kule juu ni ngumu kikipindua chombo..
Sifa ya Nanga ni kuwa inakwenda mbali sana, kutafuta msingi.. Jambo ambalo kitu kingine chochote hakiwezi kufanya..msingi wa nyumba unashuka mita mbili tatu, lakini nanga inashuka hata mita 300 au 500, kutafuta mwamba.
Ndivyo ilivyo kwa mtu aliyempokea Yesu kwa moyo wake wote leo,..Mungu anachofanya kuanzia huo wakati ni kuwa anamshushia nanga ya roho , inayoitwa TUMAINI, ambayo hiyo inakwenda moja kwa moja mpaka kwenye moyo wa Kristo (Mwamba halisi), kukuanganisha wewe na yeye, kiasi kwamba hata mawimbi makali vipi yaje mbele yako, hayawezi kukugharikisha..japokuwa chini yako hakuonekani msingi wowote.
Utapitia misukosuko ya kila namna, utapitia dhiki, utapitia kuumizwa, utapitia kila aina ya taabu kwa ajili ya imani yako, lakini kung’olewa katika mstari wa wokovu ni jambo ambalo halitawezekana daima.. Watu wataangalia msingi wako mbona hatuooni, wataoni ni kikamba tu kidogo kimeshuka majini, lakini huko chini kuna chuma kizito kinene, kimejikita kwenye mwamba mgumu sana (Yesu Kristo) Kiasi kwamba huwezi kutikiswa, na wimbi lolote la ibilisi.
Waebrania 6:18 “….sisi tuliokimbilia kuyashika matumaini yale yawekwayo mbele yetu; 19 TULIYO NAYO KAMA NANGA YA ROHO, YENYE SALAMA, YENYE NGUVU, yaingiayo hata mle mlimo ndani ya pazia, 20 alimoingia Yesu kwa ajili yetu, mtangulizi wetu, amekuwa kuhani mkuu hata milele kwa mfano wa Melkizedeki”.
Waebrania 6:18 “….sisi tuliokimbilia kuyashika matumaini yale yawekwayo mbele yetu;
19 TULIYO NAYO KAMA NANGA YA ROHO, YENYE SALAMA, YENYE NGUVU, yaingiayo hata mle mlimo ndani ya pazia,
20 alimoingia Yesu kwa ajili yetu, mtangulizi wetu, amekuwa kuhani mkuu hata milele kwa mfano wa Melkizedeki”.
Lakini kama hujampa Kristo maisha yako, au upo vuguvugu tu, yaani mguu mmoja nje, mwingine ndani, haueleweki, basi Tumaini hili Mungu hawezi kuliweka ndani yako..Na ndio hapo utashangaa, mtu dhoruba kidogo tu imemjia kashaurudia ulimwengu, ni kwasababu hakuchagua kumfuata Yesu kwa moyo wake wote..Nanga ile haikushushwa kukutana na mwamba usiotikisa ulionana chini ya bahari.
Ndugu wokovu ni jambo halisi sana, na ni nguvu ya Mungu kwelikweli, mtu yeyote anayedhamiria kumfuata Yesu, nanga hii ni lazima atashushiwa asilimia mia. Usijitumainishe na dini, au dhehebu, au mtu yeyote anayejiita mtume au nabii, au chochote kile, vyote haviwezi kukuokoa hapa duniani ni Kristo tu peke yake.
Na wokovu unakuja kwa kuamini, na kubatizwa, unapooamini moja kwa moja unakuwa tayari na kwenda kubatizwa pia katika ubatizo sahihi wa kuzamishwa katika maji mengi na kwa jina la YESU KRISTO. Na baada ya hapo unaanza kuishi maisha ya mtu kama aliyeokolewa..
Hapo ndipo Mungu analeta tumaini hili ndani yako, ambalo wimbi lolote la adui halitaweza kukuondosha..
Hivyo kama wewe upo nje ya Kristo au ulikuwa vuguvugu na ndio maana ulimwengu ukakushinda, ni wakati wako sasa huu kufanya uamuzi sahihi, dhamiria wewe mwenyewe kwanza kutoka katika moyo wako, kisha piga magoti tubu kuonyesha kwamba unahitaji msaada kutoka kwa Mungu, na kukiri makosa yako, kisha anza hatua za kutafuta ubatizo sahihi wa kuzamishwa kwenye maji mengi (kama utahitaji wasiliana nasi),.Na baada ya hapo anza kuishi maisha yanayoendeana na toba yako..
Na kuanzia huo wakati na kuendelea utaona mabadiliko makubwa maishani mwako kwa Yule Roho Mtakatifu atakapokuwa ameletwa ndani yako.. Kwasababu wokovu una nguvu zaidi ya jambo lingine lolote hapa duniani.
Bwana akubariki.
Daawa ni nini kama tunavyosoma katika biblia?
Naomba kujua nini maana ya kuteguka uvungu wa paja?
JE! KUNA UCHAWI KATIKA KUTENDA WEMA?
JIEPUSHE NA UNAJISI.
WEWE NI BWANA UNIPONYAYE.
Marijani ni nini?
Ni madini ya thamani, yenye rangi iliyo katikati ya wa waridi/pinki na nyekundu iliyokolea (rangi ya damu). Yamezoeleka kuitwa kwa jina la kiingereza “Ruby”. Tazama picha juu.
Kwenye biblia madini haya yametajwa sehemu nyingi kufunua vitu mbalimbali;
Kwamfano, katika Ayubu, inasema thamani ya hekima, haiwezi kufananishwa na thamani ya kito chochote, sio dhahabu wala marijani wala chochote, thamani ya hekima ipo mbali sana.
Ayubu 28:17 “Dhahabu na vioo haviwezi kulinganishwa nayo; Wala kubadili kwake hakutakuwa kwa vyombo vya dhahabu safi. 18 Havitatajwa fedhaluka wala bilauri; Naam, kima cha hekima chapita marijani”.
Ayubu 28:17 “Dhahabu na vioo haviwezi kulinganishwa nayo; Wala kubadili kwake hakutakuwa kwa vyombo vya dhahabu safi.
18 Havitatajwa fedhaluka wala bilauri; Naam, kima cha hekima chapita marijani”.
Maombolezo 4:7 “Wakuu wake walikuwa safi kuliko theluji, Walikuwa weupe kuliko maziwa; Miili yao, walikuwa wekundu kuliko marijani, Na umbo lao kama yakuti samawi”.
Ezekieli 27:16 “Shamu alikuwa mfanya biashara kwako, kwa sababu ya wingi wa kazi za mkono wako walifanya biashara kwa zumaridi, na urujuani, na kazi ya taraza, na kitani safi, na marijani, na akiki, wapate vitu vyako vilivyouzwa”.
Mithali 3:13 “ Heri mtu yule aonaye hekima, Na mtu yule apataye ufahamu. 14 Maana biashara yake ni bora kuliko biashara ya fedha, Na faida yake ni nyingi kuliko dhahabu safi. 15 Yeye ana thamani kuliko marijani, Wala vyote uvitamanivyo havilingani naye”.
Mithali 3:13 “ Heri mtu yule aonaye hekima, Na mtu yule apataye ufahamu.
14 Maana biashara yake ni bora kuliko biashara ya fedha, Na faida yake ni nyingi kuliko dhahabu safi.
15 Yeye ana thamani kuliko marijani, Wala vyote uvitamanivyo havilingani naye”.
Mithali 8:11 “Maana hekima ni bora kuliko marijani; Wala vyote vinavyotamanika havilingani nayo”.
Mithali 20:15 “Dhahabu iko, na marijani tele; Lakini midomo ya maarifa ni kito cha thamani”.
Vilevile biblia inataja ukubwa wa thamani wa mwanamke aliye mwema, na kusema thamani yake ni zaidi ya dini la marijani.
Mithali 31:10 “Mke mwema, ni nani awezaye kumwona? Maana kima chake chapita kima cha marijani”.
Hivyo na sisi, tukijikita kuitafuta Hekima, basi ni zaidi ya tunavyoitafuta almasi, au dhahabu, au ruby, au dini lingine lolote, kwasababu thamani na utajiri wa hekima na maarifa, ni wa kudumu, lakini mali na vito ni vya kupita tu.
Na hekima ya Mungu ni YESU KRISTO biblia inatuambia hiyo katika 1Wakorintho 1:23-24
Hivyo ukimpata Yesu kweli kweli katika moyo wako, umepata vyote, vya mwilini na rohoni..
Faidi yako ni kuwa hata ukifa unaouhakika wa uzima wa milele.
Swali ni je! Mimi na wewe tumeshamkaribisha Yesu maishani mwetu? Kama sivyo basi huu ndio wakati. Hivyo ikiwa utapenda kufanya leo uamuzi huo, basi fungua hapa kwa ajili ya kuongozwa sala ya Toba >> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Tazama maana ya mawe mengine katika biblia, pamoja na masomo chini.
Bilauri ni nini kibiblia?(Ufunuo 21:11,22:1)
Zabarajadi ni nini katika biblia (Ufunuo 21:20)?
NI NANI ATAKAYETUTENGA NA UPENDO WA KRISTO?
NGUVU YA HEKIMA NA AKILI
UNYAKUO.
Bilauri ni glasi, Na kama tunavyojua glasi huwa zina mwonekano mzuri wa kung’ara na wakuvutia, usiositiri uchafu, zimetengenezwa kwa madini yanayoitwa Crystal, tazama picha juu,
Katika biblia sehemu nyingi Neno hili limetumikia, na hiyo ni kufunua uzuri wa kitu, au mtu au Mungu au mahali fulani..Kwa mfano utaona, mstari huu,
Wimbo 7:2 “Kitovu chako ni kama bilauri iliyoviringana, Na isikose divai iliyochanganyika; Tumbo lako ni mfano wa chungu ya ngano, Iliyozungukwa na ugo wa nyinyoro”;
Kuonyesha uzuri, aliokuwa nao mpenzi wake anayemzungumzia hapo.
Ukisoma tena;
Mithali 23:31 “Usiitazame mvinyo iwapo ni nyekundu; Iitiapo bilauri rangi yake, ishukapo taratibu”
Pia,
Ezekieli 1:22 “Tena juu ya vichwa vya viumbe hai palikuwa na kitu mfano wa anga, kama rangi ya bilauri, lenye kutisha, limetandwa juu ya vichwa vyao”.
Vilevile..
Ufunuo 4:6 “Na mbele ya kile kiti cha enzi kulikuwa na mfano wa bahari ya kioo, kama bilauri; na katikati ya kile kiti cha enzi, na pande zote za kile kiti, walikuwako wenye uhai wanne, wamejaa macho mbele na nyuma”.
Soma pia; Ufunuo 22:1 na,
Ufunuo 21:10 “Akanichukua katika Roho mpaka mlima mkubwa, mrefu, akanionyesha ule mji mtakatifu, Yerusalemu, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mwenyezi Mungu; 11 wenye utukufu wa Mungu, na mwangaza wake ulikuwa mfano wa kito chenye thamani nyingi kama kito cha yaspi, safi kama bilauri”;
Ufunuo 21:10 “Akanichukua katika Roho mpaka mlima mkubwa, mrefu, akanionyesha ule mji mtakatifu, Yerusalemu, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mwenyezi Mungu;
11 wenye utukufu wa Mungu, na mwangaza wake ulikuwa mfano wa kito chenye thamani nyingi kama kito cha yaspi, safi kama bilauri”;
Unaona?
Hivyo, kwa ufupi ni kuwa makao tuliyoandaliwa kule mbinguni, hayaelezeki kwa namna ya kibinadamu, na ndio maana utaona hapo biblia inatumia neno “KAMA”, kama Bilauri/glasi, lakini bado bilauri lenyewe halielezea ipasavyo uzuri uliopo kule, hivyo, cha kufanya ni mimi na wewe, tufanye bidii ili tuwe na uhakika kuwa yaliyopo kule hatuyakosi.
Na hiyo inakuja kwanza kwa kutubu dhambi zetu kwa kumaanisha kabisa kuziacha, kisha, tukishatubu tunakubali kwenda kubatizwa katika ubatizo sahihi wa kuzamishwa katika maji mengi, na kwa jina la Yesu Kristo, kwa ajili ya ondoleo la dhambi zetu, sawasawa na Matendo 2:38, na baada ya hapo Roho Mtakatifu ataletwa ndani yetu, ili kutufundisha na kututia katika kweli yote. Mpaka siku ile ya unyakuo itakapofikia.
Je! na wewe upo tayari kufanya hivyo leo? Kama upo tayari basi fungua hapa kwa ajili ya kuongozwa sala ya Toba na mambo mengine. >>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Na Bwana akubariki sana.
Pia angalia maana nyingine za maneno ya biblia chini.
Neno beramu lina maana gani katika biblia?
JE KANISA LITAPITIA DHIKI KUU?
MAJONZI YA MTUME PAULO KWA NDUGU ZAKE.
Kwanini Bwana aliongea na Abramu baada ya kutengeana na Lutu?
MPINGA-KRISTO
Zabarajadi ni nini?
Ni moja ya mawe ya thamani, ambayo yanaonekana yakitajwa sehemu nyingi katika biblia, mawe haya yapo katika rangi mbalimbali, mengine yana rangi kama ya kijani, mengine njano, mengine nyekundu, bluu n.k. tazama picha.
Katika biblia tunaona kile kifuko cha kifuani cha Haruni, kati ya yale mawe 12 yaliyowekwa pale mojawapo lilikuwa ni hili la zabarajadi(Kutoka 28:20),
hata rangi ya magurudumu katika maono aliyoonyeshwa Ezekieli yalikuwa ya rangi ya zabarajadi,
Ezekieli 1:16 “Kuonekana kwake magurudumu hayo na kazi yake kulikuwa kama rangi ya zabarajadi; nayo yote manne yalikuwa na mfano mmoja; na kuonekana kwake na kazi yake kulikuwa kana kwamba ni gurudumu ndani ya gurudumu lingine.
Ezekieli 10:9 Nami nikaangalia, na tazama, yalikuwako magurudumu manne karibu na makerubi, gurudumu moja karibu na kerubi mmoja, na gurudumu lingine karibu na kerubi mwingine; na kuonekana kwa magurudumu kulikuwa kana kwamba ni zabarajadi.
Vilevile biblia inaonyesha, msingi wa ukuta wa mji ule wa kimbinguni (Yaani Yerusalemu mpya), nao pia utakuwa umenakshiwa na mawe haya..Japo pia inaweza kuwa ni lugha ya picha kuonyesha uzuri wa makao hayo jinsi ulivyo na sio mawe halisi, lakini mawe haya ya thamani yametumika katika vifungu hivyo.
Ufunuo 21:18 “Na majenzi ya ule ukuta wake yalikuwa ya yaspi, na mji ule ulikuwa wa dhahabu safi, mfano wa kioo safi. 19 Na misingi ya ukuta wa mji ilikuwa imepambwa kwa vito vya thamani vya kila namna. Msingi wa kwanza ulikuwa yaspi; wa pili yakuti samawi; wa tatu kalkedoni; wa nne zumaridi; 20 wa tano sardoniki; wa sita akiki; wa saba krisolitho; wa nane zabarajadi; wa kenda yakuti ya manjano; wa kumi krisopraso; wa kumi na moja hiakintho; wa kumi na mbili amethisto”.
Ufunuo 21:18 “Na majenzi ya ule ukuta wake yalikuwa ya yaspi, na mji ule ulikuwa wa dhahabu safi, mfano wa kioo safi.
19 Na misingi ya ukuta wa mji ilikuwa imepambwa kwa vito vya thamani vya kila namna. Msingi wa kwanza ulikuwa yaspi; wa pili yakuti samawi; wa tatu kalkedoni; wa nne zumaridi;
20 wa tano sardoniki; wa sita akiki; wa saba krisolitho; wa nane zabarajadi; wa kenda yakuti ya manjano; wa kumi krisopraso; wa kumi na moja hiakintho; wa kumi na mbili amethisto”.
Soma pia Danieli 10:5-6,
Shalom.
Tazama tafsiri ya mawe mengine, na maneno mengine ya biblia chini;
Rangi ya kaharabu ni ipi kibiblia(Ezekieli 1:4,27,8:2)?
Rangi ya samawi ni ipi kibiblia(Kutoka 36:37)?
Pomboo ni nini katika biblia?(Kutoka 25:5, Ezekieli 16:10)
MKUMBUKE MKE WA LUTU.
JE! NINYI NANYI MWATAKA KUONDOKA?
MAONO YA NABII AMOSI.
BONDE LA KUKATA MANENO.
Rangi ya kaharabani ni ipi?
Rangi ya kaharabu ni rangi iliyo katikati ya Njano na machungwa, kwa lugha rahisi ya kueleweka wengi wanaiita Njano, japo si njano kabisa. Tazama picha.
Hivi ni vifungu katika biblia vinavyoizungumzia rangi hiyo;
Ezekieli 1:4 “Nikaona, na tazama, upepo wa dhoruba ulitoka upande wa kaskazini, wingu kubwa sana, pamoja na moto, ukifanya duara ya nuru, na mwangaza pande zote, na katikati yake kitu kama rangi ya kaharabu, katikati ya moto huo”.
Ezekieli 1:27 “Nikaona kana kwamba ni rangi ya kaharabu, kama kuonekana kwa moto ndani yake pande zote, tangu kuonekana kwa viuno vyake na juu; na tangu kuonekana kwa viuno vyake na chini, naliona kana kwamba ni kuonekana kwa moto; tena palikuwa na mwangaza pande zake zote”.
Ezekieli 8:2 “Ndipo nikaangalia, na tazama, kana kwamba ni mfano wa moto; tangu mfano wa viuno vyake na chini, moto; na tangu mfano wa viuno vyake na juu, kana kwamba ni mfano wa mwangaza, kama rangi ya kaharabu”.
Ukuu na uweza wa Mungu umeonekana kwa rangi hii, Na ndio maana utaona karibu vifungu vyote, ambapo Mungu anaanza kujidhirisha mbele ya watu rangi hii au moto unatajwa. Kuashiria kuwa yeye ni kama Moto, unaosafisha fedha, na kuteketeza makapi.
Waebrania 12:29 “maana Mungu wetu ni moto ulao”.
Hivyo ni jukumu letu sisi kufanyika mawe ya thamani mbele za Mungu kama fedha na dhahabu ili apitapo juu yetu atusafishe zaidi badala ya kututeketeza, lakini tukiwa kama nyasi tu mbele zake, (mapaki), yaani watu waovu wasiomcha Mungu, watenda mabaya, ni wazi kuwa akipita juu yetu tutateketea kwasababu sisi ni mapaki tu..Na ndicho kinachowakuta watu wengi siku ile ya mwisho.
Mathayo 3:12 “……bali makapi atayateketeza kwa moto usiozimika”.
Bwana atusaidie.
Tazama maana nyingine za maneno chini, na masomo yake.
Jabari ni nini, kama linavyotumika kwenye biblia?
MAANA YA RANGI KIBIBLIA.
DAKIKA MOJA TU, INAKUFANYA UMWAMINI SHETANI?
CHUKIZO LA UHARIBIFU
TAZAMA, NASIMAMA MLANGONI.
Amin, nawaambia, Kizazi hiki hakitapita, hata hayo yote yatakapotimia..!!
Rangi ya samawi ni ipi?
Rangi ya samawi ndio rangi ya bluu, Kama unavyoona katika picha, katika biblia rangi hii ilitumika kwa matumizi mbalimbali husasani yale ya madhabahuni pa Mungu (hema ya kukutania na hekaluni),
Kutoka 39:1 “Na zile nyuzi za rangi ya samawi, na nyuzi za rangi ya zambarau, na nyekundu, wakafanya mavazi yaliyofumwa kwa ustadi sana kwa ajili ya kutumika katika mahali patakatifu, na kuyafanya hayo mavazi matakatifu ya Haruni, vile vile kama Bwana alivyomwagiza Musa. 2 Naye akaifanya hiyo naivera, ya nyuzi za dhahabu, na za rangi ya samawi, na za rangi ya zambarau, na za rangi nyekundu, na kitani nzuri ya kusokotwa”.
Kutoka 39:1 “Na zile nyuzi za rangi ya samawi, na nyuzi za rangi ya zambarau, na nyekundu, wakafanya mavazi yaliyofumwa kwa ustadi sana kwa ajili ya kutumika katika mahali patakatifu, na kuyafanya hayo mavazi matakatifu ya Haruni, vile vile kama Bwana alivyomwagiza Musa.
2 Naye akaifanya hiyo naivera, ya nyuzi za dhahabu, na za rangi ya samawi, na za rangi ya zambarau, na za rangi nyekundu, na kitani nzuri ya kusokotwa”.
Hesabu 15:38 “Nena na wana wa Israeli, na kuwaagiza ya kwamba wajifanyie vishada katika ncha za nguo zao, katika vizazi vyao, tena ya kwamba watie katika kila kishada cha kila ncha nyuzi za rangi ya samawi; 39 nacho kitakuwa kwenu ni kishada, ili mpate kukiangalia, na kuyakumbuka maagizo yote ya Bwana, na kuyafanya; tena kwamba msiende kutanga-tanga kuandama mioyo yenu wenyewe, na macho yenu wenyewe, ambayo mlikuwa mkiyaandama kwa uasherati hapo kwanza”;
Hesabu 15:38 “Nena na wana wa Israeli, na kuwaagiza ya kwamba wajifanyie vishada katika ncha za nguo zao, katika vizazi vyao, tena ya kwamba watie katika kila kishada cha kila ncha nyuzi za rangi ya samawi;
39 nacho kitakuwa kwenu ni kishada, ili mpate kukiangalia, na kuyakumbuka maagizo yote ya Bwana, na kuyafanya; tena kwamba msiende kutanga-tanga kuandama mioyo yenu wenyewe, na macho yenu wenyewe, ambayo mlikuwa mkiyaandama kwa uasherati hapo kwanza”;
Esta 8:15 “Naye Mordekai akatoka usoni pa mfalme, amevaa mavazi ya kifalme, ya rangi ya samawi na nyeupe, mwenye taji kubwa ya dhahabu, na joho ya kitani safi na rangi ya zambarau. Mji wa Shushani wakapaza sauti, wakashangilia”.
Hivyo rangi hii ni rangi ya utukufu wa Mungu, hata katika maisha ya kawaida, utaona vitu vingi vya asili Mungu amevipamba kwa rangi hii, ukitazama anga, utaiona, ukitazama bahari utaiona, ukitazama milima, utaiona,..Hivyo uinapo rangi hii jua umeona utukufu wa Mungu.
Tazama maana za rangi kikiblia chini na tafsiri nyingi za maneno.
Bwana Yesu alimaanisha nini aliposema; Mafarisayo Hupanua HIRIZI zao, na kuongeza MATAMVUA yao?
JE KUPOKEA CHANJO NI DHAMBI?
SIKU YA UNYAKUO ITAKUKUTAJE?
SWALI: Je! Kusoma biblia kwenye simu ukiwa kanisani, au sehemu yoyote ile ni dhambi? au kutumia Tablet madhabahuni, pia hilo nalo ni dhambi?
JIBU: Ili tupate jibu sahihi la swali hili, hebu tulihamishe na kumwuliza Mwalimu wa shuleni, Je! Ni vizuri yeye kuwafundisha wanafunzi wake kwa kutumia kitabu au tablet au simu?…Au je ni vizuri wanafunzi wake kumfuatilia anachofundisha kwa kutumia simu zao au tablets zao na si vitabu?.
Kwa Mwalimu yoyote ambaye anajua wajibu wake kamwe hataweza kuruhusu mwanafunzi wake aingie na simu pindi anapofundisha, haijalishi hiyo simu itakuwa na material gani anayoyahitaji yeye..wala yeye mwenyewe hawezi kuwafundisha wanafunzi wake kwa kutumia simu. Ataruhusu wanafunzi wake watumie hizo tablet zao, au simu zao, au ipad au computer baada ya kutoka kwenye masomo au endapo somo analotaka kuwafundisha wanafunzi wake linahusiana sana na hizo simu, au computer, au tablets..Lakini katika hali ya kawaida hawezi kamwe kuruhusu simu darasani kwake. Na lengo la kufanya hivyo sio kwamba simu ni mbaya, hapana!..bali ni kwasababu simu zina vitu vingi ambavyo ni rahisi kumtoa mwanafunzi katika umakini wa darasani, kwasababu wakati mwalimu anafundisha mara meseji imeingia, mara simu imeita, mara imezima chaji ghafla, mara imeganda ghafla n.k..
Tofauti na kitabu, Kitabu hakina muingiliano wa vitu vingi ambavyo vinaweza kuhamisha usikivu na umakini wa mtu. Hawezi mtu kusoma kitabu ghafla kikazima chaji, au kikaleta jumbe nyingi nyingi n.k. Ndio maana mpaka leo kusoma kwa kutumia kitabu imebaki kuwa njia bora na ya umakini kwa wanafunzi.
Na kanisani ni hivyo hivyo, Kanisani ni zaidi ya mashule na madarasa ya kidunia. Mtu anayeingia pale anakwenda kujifunza au kufundisha Elimu ya Mbinguni, ambayo ni kubwa kuliko elimu zote, hivyo umakini mkubwa sana unahitajika kwa anayekwenda kufundisha na anayekwenda kujifunza. Hivyo biblia iliyoandikwa kwenye kitabu Ndio njia bora na itabakia kuwa hivyo mpaka mwisho. Mtu anayefundisha kwa kutumia simu au anayeingia kanisani na simu iliyowashwa, bado hajajua anakwenda kumtafuta nani, na wala hajajua thamani ya Neno la Mungu.
Sasa sio kwamba matumizi ya biblia ya kwenye simu na Tablet na Computer ni mabaya! La si mabaya ni mazuri katika eneo husika, lakini si kanisani..Unaweza kuwa kwenye gari unasafiri umbali mfupi kwenye basi na ukatamani kusoma biblia na huna, hapo unaweza kutumia biblia kwenye simu yako, hali kadhalika unaweza ukawa upo kazini au barabarani na ukakutana na mtu ukamshuhudia na mahali hapo huna biblia ya kuweza kunukuu maandiko, hapo unaweza kutumia biblia ya kwenye simu yako au Tablet yako au ipad yako, kushuhudia au kujikumbusha maandiko. Lakini kanisani ni darasani, na si darasa la kidunia bali la kimbinguni, hivyo panahitajika Kitabu cha uzima kinachoitwa BIBLIA TAKATIFU.
KAMA MMOJA TU NDIO HIVI! SI ZAIDI 153?
USIISHIE KUTAZAMA JUU, ENDELEA MBELE.
JE UDHAIFU WANGU UNAWEZA KUZUIA INJILI?
WAKINYAMAZA HAWA, MAWE YATAPIGA KELELE.
Je! Bwana Yesu alibatiza akiwa hapa duniani?
WhatsApp
Shalom, Jina kuu la Bwana wetu Yesu Kristo libarikiwe daima.
Kama wewe umeokoka, na kwa kitambo sasa upo katika wokovu, nataka nikuambie katika wakati unapaswa uwe nao makini sana basi ni huu, kwasababu neema uliyokuwa nayo kipindi cha mwanzoni ulichookoka, sio sawa na uliyonayo sasa..
Kulikuwa na wakati Bwana Yesu aliwaambia watu wote ikiwemo wanafunzi wake maneno haya….
Mathayo 11:28 “Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. 29 Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu; 30 kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi”.
Mathayo 11:28 “Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.
29 Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu;
30 kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi”.
Maneno ya kukaribisha, maneno ya kufariji, maneno ya kutia moyo. Huu ni wakati ambao chochote walichokitaka kwa Bwana walikipita..
Lakini mambo hayakuendelea hivyo hivyo milele..Kuna wakati alianza kuwafundisha wanafunzi wake na makutano kwa namna nyingine, na baadhi yao kukwazika kwa maneno yake, utaona hakuwaambia tena, njoni, nifuateni, nitawafanya kuwa wavuvi wa watu, hakuwaita tena Boarnege, hakuwaambia tena nyie ni waisraeli kweli kweli msio na waa, kana kwamba anataka kuwavuta..bali aliwaambia “Je! Ninyi nanyi mwataka kuondoka”?..
Unajua mpaka mtu anakuuliza hivyo ni kiashirio kuwa yupo tayari kwa uamuzi wowote utakaoutoa, ..Kama unataka kwenda ni sawa nenda tu,kama unataka kubaki baki, hakuna kupembelezwa, wala kupewa maneno ya faraja tena..kama unakwenda nenda wala sitakuulizia wala kukutafuta..Lakini Petro kuona hilo alijibu haraka sana..
Yohana 6:67 “Basi Yesu akawaambia wale Thenashara, Je! Ninyi nanyi mwataka kuondoka? 68 Basi Simoni Petro akamjibu, Bwana! Twende kwa nani? Wewe unayo maneno ya uzima wa milele”.
Yohana 6:67 “Basi Yesu akawaambia wale Thenashara, Je! Ninyi nanyi mwataka kuondoka?
68 Basi Simoni Petro akamjibu, Bwana! Twende kwa nani? Wewe unayo maneno ya uzima wa milele”.
Huo wakati hata wewe na mimi tutaupitia tu..Si muda wote katika ukristo wako Yesu atakuambia Tubu, au njoo kwangu, si kila wakati atakuonya juu ya madhara ya dhambi.. Kuna wakati ile neema uliyokuwa nayo mwanzo hutaisikia tena ndani yako..Kwasababu Kristo anakuhesabia kuwa umeshafahamu yakupasayo kutenda..
Hivyo, atakapokuona upo nusu nusu, mguu mmoja nje, mwingine ndani, upo ndani ya wokovu lakini mambo ya kidunia bado unayatamani, miezi inaenda, miezi inarudi upo vilevile.. Nataka nikuambie sauti ya Kristo utakayoisikia ndani yako ni hii NA WEWE UNATAKA KUONDOKA? Unataka kurudi nyuma?
Hatakwambia kwa mdomo, lakini atakuambia kwa vitendo. Kipindi hicho, Roho mtakatifu hatakuwepo pembeni yako tena kukushuhudia chochote, au kuugua ndani yako kukuvuta upande wake, kama ilivyokuwa kule mwanzo, ambapo ulipokuwa unaona dhambi unaogopa, hapo utakuwa ni wewe na maamuzi wako binafsi, kuchagua Mungu au dunia..Kristo atakuwa amesimama pembeni anasubiria uamue moja.
Ukichagua dunia, wala hutaona badiliko lolote ndani, unaweza ukafikiri kama vile Mungu hakuoni, utaendelea na hali hiyo hiyo, mpaka siku ile utakapojikuta kuzimu.
Hivyo mimi na wewe tusifikie hicho kipindi ndugu yangu, hata kama Mungu hakupi kile unachokitaka leo hii, hata kama unaona maneno yake ni magumu, hupaswi kufikiria kurudi nyuma au kufikiria mambo ya ulimwenguni, kumbuka walioitwa ni wengi, lakini wateule ni wachache, wanafunzi wa Yesu walikuwa ni wengi sana, lakini waliovumilia mpaka mwisho walikuwa ni 11 tu, na wengine wachache sana mfano wa Mathiya.
Jiulize ni nini kilichokuvuta kwa Yesu zamani, mpaka ukaamua kuokoka, na leo hii ni nini kinachokufanya utake kurudi nyuma? Neema ya kukuvuta haipo tena..Kwako Neno linalobakia kutoka kwa Yesu ni hili; Je! Na wewe unataka kuondoka?
Waebrania 6:4 “Kwa maana hao waliokwisha kupewa nuru, na kukionja kipawa cha mbinguni, na kufanywa washirika wa Roho Mtakatifu, 5 na kulionja neno zuri la Mungu, na nguvu za zamani zijazo, 6 wakaanguka baada ya hayo, haiwezekani kuwafanya upya tena hata wakatubu; kwa kuwa wamsulibisha Mwana wa Mungu mara ya pili kwa nafsi zao, na kumfedhehi kwa dhahiri”.
Waebrania 6:4 “Kwa maana hao waliokwisha kupewa nuru, na kukionja kipawa cha mbinguni, na kufanywa washirika wa Roho Mtakatifu,
5 na kulionja neno zuri la Mungu, na nguvu za zamani zijazo,
6 wakaanguka baada ya hayo, haiwezekani kuwafanya upya tena hata wakatubu; kwa kuwa wamsulibisha Mwana wa Mungu mara ya pili kwa nafsi zao, na kumfedhehi kwa dhahiri”.
Hivyo tusonge mbele katika Imani, mitume walivumilia mpaka mwisho, lakini sasa sote tunatamani kuwa kama hao, Lakini wale wengine hata mmoja husikii habari yake baada ya pale.. Hivyo na sisi tukivumilia mpaka mwisho kwa Kristo, tutazirithi Baraka tulizoahidiwa na Mungu tangu zamani.
Taji la uzima limewekwa mbele yetu. Na siku ile tutaketi naye katika kiti chake cha enzi kama alivyotuahidia sisi wakristo wa kanisa hili la Laodikia(Ufunuo 3:21).
Bwana atusaidie, Bwana atutie nguvu sote.
Kwanini Kristo hakuitwa Imanueli badala yake akaitwa Yesu?
YESU AKALIA KWA SAUTI KUU.
KWANINI LEO HII KUNA KUNDI KUBWA LA WAKRISTO WALIORUDI NYUMA?
NA ROHO NA BIBI-ARUSI WASEMA, NJOO!
Hakuna asiyejua kuwa Mzazi mwenye hekima anapokaribia kumaliza siku zake, huwa anawaita wanawe kuwapa wosia mfupi wa maisha pamoja na kuwabariki. Na Mzazi mwenye upendo ni yule anayewaambia wanawe au wajukuu wake ukweli wa maisha, na anayewapa tahadhari na anayewapa faraja na tumaini.. Na zaidi sana anapokaribia kumaliza siku zake huwa anawaambia wanawe siri ambazo walikuwa hawazijui.
Ndivyo alivyofanya pia Bwana wetu Yesu Kristo, kabla ya kuondoka kwake..Aliwaita wanafunzi wake na kuwapa wosia na kuwaonya mambo watakayokutana nayo baada ya yeye kuondoka. Alitumia masaa kadhaa kuzungumza nao mambo kadha wa kadha.
Na wosia wake huo umegawanyika katika vipengele vitano:
KİPENGELE CHA KWANZA: Ambacho ndiyo ile sura ya 13 yote, utaona Bwana anawaonya wanafunzi wake juu ya unyenyekevu, utaona anawafundisha kwa vitendo namna ya kunyenyekeana, (kwa kuonyesha kielelezo yeye mwenyewe, kwa kuchukua maji na kuosha miguu yao) na akawaambia atakayetaka kuwa mkubwa kuliko wote sharti awe mdogo kuliko wote. Na kama yeye wanayemwita Bwana ameshika miguu yao wao, inawapasaje wao?..Hawana budi kunyenyekeana sana na kujishusha baada ya Bwana kuondoka.
KİPENGELE CHA PİLİ: Ambacho ni sura ya 14 yote utaona Bwana anawapa faraja wanafunzi wake, kwamba wasiogope wala wasifadhaike atakapowaacha…kwani anakwenda kuwaandalia makao. Na anawaambia hatawaacha yatima, bali atawaletea msaidizi ambaye ndiye Roho Mtakatifu, na furaha yao itarudia tena. Nao watajiona kama vile hawajaachwa.
KİPENGELE CHA TATU: Ambacho ni ile sura ya 15 yote, Utaona Bwana anawaonya na kuwakumbusha kuwa wazae matunda baada ya kuondoka kwake, na kuwakumbusha kupendana..
KİPENGELE CHA NNE: Ambacho ndiyo ile sura ya 16 yote, Utaona Bwana anawaonya kuhusu mambo yatakayokwenda kuwatokea baada ya yeye kuondoka, akawaambia, dhiki watakazopitia na mateso, lakini wasiogope kwasababu yeye atakuwa pamoja nao.
Yohana 16: 1 “Maneno hayo nimewaambia, msije mkachukizwa. 2 Watawatenga na masinagogi; naam, saa yaja atakapodhania kila mtu awauaye ya kuwa anamtolea Mungu ibada. 3 Na hayo watawatenda kwa sababu hawakumjua Baba wala mimi. 4 Lakini nimewaambia hayo, ili makusudi saa ile itakapokuja myakumbuke ya kuwa mimi naliwaambia. Sikuwaambia hayo tangu mwanzo, kwa sababu nalikuwapo pamoja nanyi”.
Yohana 16: 1 “Maneno hayo nimewaambia, msije mkachukizwa.
2 Watawatenga na masinagogi; naam, saa yaja atakapodhania kila mtu awauaye ya kuwa anamtolea Mungu ibada.
3 Na hayo watawatenda kwa sababu hawakumjua Baba wala mimi.
4 Lakini nimewaambia hayo, ili makusudi saa ile itakapokuja myakumbuke ya kuwa mimi naliwaambia. Sikuwaambia hayo tangu mwanzo, kwa sababu nalikuwapo pamoja nanyi”.
KİPENGELE CHA TANO NA CHA MWİSHO: Ambacho ndiyo ile sura ya 17, ni kipengele cha Yesu mwenyewe kuhitimisha kwa kuwaombea wanafunzi wake.
Sasa hata baba anapotoa wosia kwa wanawe kabla ya kufariki kwake, Mwishoni huwa anapowaombea baraka na heri, hawezi kuwaombea watu wa mtaani, au watu wa kazini kwake, ni lazima atawaombea na kuwabariki wale aliowausia pamoja na watoto wao, kwasababu ndio urithi wake.
Ndicho Bwana alichokifanya hapa, katika kipengele hichi baada ya kuwaambia mambo yatakayowatokea na majukumu yao, baada ya kuondoka kwake ndipo anawaombea..
Na anawaombea nini?
Jibu tunalipata mbele kidogo..(Zingatia hivyo vipengele vilivyoanishwa kwa herufi kubwa)
Yohana 17: 9 “Mimi nawaombea hao; siuombei ulimwengu; bali hao ulionipa, kwa kuwa hao ni wako; 10 na wote walio wangu ni wako, na walio wako ni wangu; nami nimetukuzwa ndani yao. 11 Wala mimi simo tena ulimwenguni, lakini hawa wamo ulimwenguni, nami naja kwako. Baba mtakatifu, KWA JİNA LAKO ULİLONİPA UWALİNDE HAWA, ili wawe na umoja kama sisi tulivyo. 12 Nilipokuwapo pamoja nao, mimi naliwalinda kwa jina lako ulilonipa, nikawatunza; wala hapana mmojawapo wao aliyepotea, ila yule mwana wa upotevu, ili andiko litimie. 13 Na sasa naja kwako; na maneno haya nayasema ulimwenguni, ili wawe na furaha yangu imetimizwa ndani yao. 14 Mimi nimewapa neno lako; na ulimwengu umewachukia; kwa kuwa wao si wa ulimwengu, kama mimi nisivyo wa ulimwengu. 15 Mimi siombi kwamba uwatoe katika ulimwengu; BALİ UWALİNDE NA YULE MWOVU. 16 Wao si wa ulimwengu, kama mimi nisivyo wa ulimwengu. 17 UWATAKASE KWA İLE KWELİ; NENO LAKO NDİYO KWELİ. 18 Kama vile ulivyonituma mimi ulimwenguni, nami vivyo hivyo naliwatuma hao ulimwenguni. 19 Na kwa ajili yao najiweka wakfu mwenyewe, ili na hao watakaswe katika kweli. 20 WALA Sİ HAO TU NİNAOWAOMBEA; LAKİNİ NA WALE WATAKAONİAMİNİ KWA SABABU YA NENO LAO. 21 WOTE WAWE NA UMOJA; kama wewe, Baba, ulivyo ndani yangu, nami ndani yako; hao nao wawe ndani yetu; ili ulimwengu upate kusadiki ya kwamba wewe ndiwe uliyenituma. 22 Nami utukufu ule ulionipa nimewapa wao; ili wawe na umoja kama sisi tulivyo umoja. 23 Mimi ndani yao, nawe ndani yangu, ili wawe wamekamilika katika umoja; ili ulimwengu ujue ya kuwa ndiwe uliyenituma, ukawapenda wao kama ulivyonipenda mimi. 24 BABA, HAO ULİONİPA NATAKA WAWE PAMOJA NAMİ PO POTE NİLİPO, WAPATE NA KUUTAZAMA UTUKUFU WANGU ULİONİPA; kwa maana ulinipenda kabla ya kuwekwa msingi ulimwengu. 25 Baba mwenye haki, ulimwengu haukukujua; lakini mimi nalikujua, na hao wamejua ya kuwa ndiwe uliyenituma. 26 Nami naliwajulisha jina lako, tena nitawajulisha hilo; ili pendo lile ulilonipenda mimi liwe ndani yao, nami niwe ndani yao”
Yohana 17: 9 “Mimi nawaombea hao; siuombei ulimwengu; bali hao ulionipa, kwa kuwa hao ni wako;
10 na wote walio wangu ni wako, na walio wako ni wangu; nami nimetukuzwa ndani yao.
11 Wala mimi simo tena ulimwenguni, lakini hawa wamo ulimwenguni, nami naja kwako. Baba mtakatifu, KWA JİNA LAKO ULİLONİPA UWALİNDE HAWA, ili wawe na umoja kama sisi tulivyo.
12 Nilipokuwapo pamoja nao, mimi naliwalinda kwa jina lako ulilonipa, nikawatunza; wala hapana mmojawapo wao aliyepotea, ila yule mwana wa upotevu, ili andiko litimie.
13 Na sasa naja kwako; na maneno haya nayasema ulimwenguni, ili wawe na furaha yangu imetimizwa ndani yao.
14 Mimi nimewapa neno lako; na ulimwengu umewachukia; kwa kuwa wao si wa ulimwengu, kama mimi nisivyo wa ulimwengu.
15 Mimi siombi kwamba uwatoe katika ulimwengu; BALİ UWALİNDE NA YULE MWOVU.
16 Wao si wa ulimwengu, kama mimi nisivyo wa ulimwengu.
17 UWATAKASE KWA İLE KWELİ; NENO LAKO NDİYO KWELİ.
18 Kama vile ulivyonituma mimi ulimwenguni, nami vivyo hivyo naliwatuma hao ulimwenguni.
19 Na kwa ajili yao najiweka wakfu mwenyewe, ili na hao watakaswe katika kweli.
20 WALA Sİ HAO TU NİNAOWAOMBEA; LAKİNİ NA WALE WATAKAONİAMİNİ KWA SABABU YA NENO LAO.
21 WOTE WAWE NA UMOJA; kama wewe, Baba, ulivyo ndani yangu, nami ndani yako; hao nao wawe ndani yetu; ili ulimwengu upate kusadiki ya kwamba wewe ndiwe uliyenituma.
22 Nami utukufu ule ulionipa nimewapa wao; ili wawe na umoja kama sisi tulivyo umoja.
23 Mimi ndani yao, nawe ndani yangu, ili wawe wamekamilika katika umoja; ili ulimwengu ujue ya kuwa ndiwe uliyenituma, ukawapenda wao kama ulivyonipenda mimi.
24 BABA, HAO ULİONİPA NATAKA WAWE PAMOJA NAMİ PO POTE NİLİPO, WAPATE NA KUUTAZAMA UTUKUFU WANGU ULİONİPA; kwa maana ulinipenda kabla ya kuwekwa msingi ulimwengu.
25 Baba mwenye haki, ulimwengu haukukujua; lakini mimi nalikujua, na hao wamejua ya kuwa ndiwe uliyenituma.
26 Nami naliwajulisha jina lako, tena nitawajulisha hilo; ili pendo lile ulilonipenda mimi liwe ndani yao, nami niwe ndani yao”
Wosia huu unatuhusu sisi pia, kama tumefanyika kuwa wanafunzi wa Kristo hatuna budi kupendana, kunyenyekeana, kuwa na umoja na kuifanya kazi yake. Tukizingatia huo wosia basi tutafanikiwa sana katika huu ulimwengu.
Vile vile maombi hayo si ya mitume peke yao..bali ni ya kwetu pia.. kwasababu hapo kwenye mstari wa 20 anasema “WALA Sİ HAO TU NİNAOWAOMBEA; LAKİNİ NA WALE WATAKAONİAMİNİ KWA SABABU YA NENO LAO.”
Bwana alishatuombea miaka 2000 iliyopita na ameshatubariki na kutupa utukufu..Ni haki yetu kudai utukufu wetu na baraka zetu, na hatuzidai kwa maneno, bali kwa kuyafanya mapenzi yake, tunapofanya mapenzi yake katika ulimwengu wa roho ni haki yetu kupata baraka na heri na afya.
Bwana atubariki tuzidi kuwa na umoja na kupendana na kunyenyekeana…Na zaidi sana tuifanye kazi yake..Na mwisho tuzipokee baraka zake alizotubariki miaka 2,000 iliyopita.
Maran tha!
DANIELI: Mlango wa 10
MWAMUZI WA KWELI:
MTAIFAHAMU KWELI NAYO HIYO KWELI ITAWAWEKA HURU.
KWA KUPIGWA KWAKE SISI TUMEPONA.
UMUHIMU WA KUOMBA MSAMAHA.