SWALI: Yakobo 5:14 inasema, wazee wa kanisa wakitaka kumwombea mgonjwa wampake mafuta, je! yale ni mafuta ya upako au?. Na kama sio, ni mafuta gani yanayozungumziwa pale?.
Yakobo 5:14 “Mtu wa kwenu amekuwa hawezi? Na awaite wazee wa kanisa; nao wamwombee, na kumpaka mafuta kwa jina la Bwana”.
JIBU: Kabla hutujaona ni mafuta gani yanayozungumziwa pale..Tuutazame kwanza kwa ukaribu mstari huo, ukiungalia vizuri utaona umegawanyika katika vipengele viwili.. utaona baada ya hao wazee wa kanisa kuitwa, hatua ya kwanza ni wanamuombea, (hicho ni kipengele cha kwanza kilichotenganishwa na alama ya mkato), na hatua ya pili inayofuata sasa baada ya hapo ni kumpaka mafuta kwa jina la Bwana.
Watu wengi hawalioni hilo, wanayaunganisha hayo maneno mawili pamoja, na ndio hapo wanadhani, mafuta Fulani ya chupa ndio maombezi yenyewe, .. Jambo ambalo si sahihi?. Kilichomaanishwa pale ni kuwa maombi yakishakwisha, kinachofuata ni kupakwa mafuta…Ukisoma biblia kwa haraka haraka ni rahisi kupoteza shabaha ya maandiko mengi.
Sasa tukirudi kwenye swali ni mafuta gani yale yaliyomaanishwa?..
Biblia inasema..
1Yohana 2:20 “Nanyi mmepakwa mafuta na Yeye aliye Mtakatifu nanyi mnajua nyote”.
Roho Mtakatifu ndiye anayepaka watu mafuta, na mafuta yenyewe ni Neno lake (Yohana 16:13). Hivyo mtu aliye na Neno la Mungu kwa wingi ndani yake, mtu huyo ana mafuta mengi sana ya kumsaidia.
2Wakorintho 1:21 “Basi Yeye atufanyaye imara pamoja nanyi katika Kristo, na kututia mafuta, ni Mungu. 22 naye ndiye aliyetutia muhuri akatupa arabuni ya Roho mioyoni mwetu.”
2Wakorintho 1:21 “Basi Yeye atufanyaye imara pamoja nanyi katika Kristo, na kututia mafuta, ni Mungu.
22 naye ndiye aliyetutia muhuri akatupa arabuni ya Roho mioyoni mwetu.”
Sasa mitume na wazee wa kanisa kwa kujua mafuta hasaa na halisi ni yapi, ilikuwa ni desturi yao mara baada ya kuwaombea wagonjwa, jambo linalofuata na kuwaimarisha kwa Neno, ,Kwasababu walijua hicho ndicho kinachoweza kumfanya mtu asimame na kuweza kufanya mambo yote mwenyewe, hata baada ya kutoka pale.
1Yohana 2:27 “Nanyi, mafuta yale mliyoyapata kwake yanakaa ndani yenu, wala hamna haja ya mtu kuwafundisha; lakini kama mafuta yake yanavyowafundisha habari za mambo yote, tena ni kweli wala si uongo, na kama yalivyowafundisha, kaeni ndani yake”.
Vivyo hivyo, na sasa, tunapaswa tuendeleze desturi hiyo, si kuwaombea tu wagonjwa matatizo yao, sio kufanyia tu kuwafanyia maombi ya ukombozi peke yake halafu hakuna cha ziada baada ya hapo, bali pia, tuwapake mafuta ya Roho wa Bwana..Tuwape chakula cha uzima..ambacho hata wakitoka pale, wanaweza kusimama wao wenyewe, pindi wanapokumbana na matatizo kama hayo na hata kumshinda shetani.
Huo ndio uponyaji hasaa, Lakini kama mtu atatolewa mapepo kwa kuombewa, halafu hatiwi mafuta,(Yaani hufundishwi au ajifunzi maneno ya uzima), akitoka pale, ataendelea na dhambi zake, na yale mapepo yatamrudia baada ya kipindi kifupi, tena yenye nguvu mara saba zaidi, na hali yake ya mwisho itakuwa mbaya kuliko ile ya kwanza kama biblia inavyosema. Na kazi inakuwa ni bure, Hivyo jitathmini na wewe kama mhubiri je unafanya hivyo?.
Kwahiyo mafuta yanayozungumziwa pale, sio mafuta ya chupa, bali ni Neno la Mungu, linalomiminwa na Roho Mtakatifu mwenyewe ndani ya mtu..
Shalom.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
JINSI YA KUSOMA BIBLIA.
Kwanini Mungu alisema hakuna mtu awazaye kuuona uso wake akaishi?
PASAKA NI NINI? NA JE TUNARUHUSIWA KUSHEHEREKEA PASAKA?
Roho Mtakatifu ni nani?.
Rudi Nyumbani:
Print this post
Mistari ya biblia kuhusu kifo.
Kifo ni jambo lisilozoeleka kwa mtu yeyote, Lakini pamoja na hayo lipo tumaini la uzima tena, kwa wale waliomwamini Bwana Yesu Kristo. Na ndio maana mtume Petro aliwatia moyo waaminio wote wa wakati ule, akiwaambia wasistaajabie sana, msiba huo utakapowapata kwa ghafla kama jaribu la moto, kinyume chake wafurahie kwasababu lipo tumaini tena la uzima siku ile ya ufufuo..Kwasababu watafufuliwa tena, na kuwaona wapendwa wao.
1Petro 4:12 “Wapenzi, msione kuwa ni ajabu ule msiba ulio kati yenu, unaowapata kama moto ili kuwajaribu, kana kwamba ni kitu kigeni kiwapatacho. 13 Lakini kama mnavyoyashiriki mateso ya Kristo, furahini; ili na katika ufunuo wa utukufu wake mfurahi kwa shangwe”.
1Petro 4:12 “Wapenzi, msione kuwa ni ajabu ule msiba ulio kati yenu, unaowapata kama moto ili kuwajaribu, kana kwamba ni kitu kigeni kiwapatacho.
13 Lakini kama mnavyoyashiriki mateso ya Kristo, furahini; ili na katika ufunuo wa utukufu wake mfurahi kwa shangwe”.
Hivyo na wewe unapoipitia mistari hii naomba uitafakari kwa utulivu, itakuponya sehemu Fulani.
Kwababu biblia inasema tena..
Mhubiri 7:2 “Heri kuiendea nyumba ya matanga, Kuliko kuiendea nyumba ya karamu. Kwa maana huo ndio mwisho wa wanadamu wote, naye aliye hai atautia moyoni mwake. 3 Huzuni ni afadhali kuliko kicheko, Maana simanzi ya uso ni faida ya moyo”.
Mhubiri 7:2 “Heri kuiendea nyumba ya matanga, Kuliko kuiendea nyumba ya karamu. Kwa maana huo ndio mwisho wa wanadamu wote, naye aliye hai atautia moyoni mwake.
3 Huzuni ni afadhali kuliko kicheko, Maana simanzi ya uso ni faida ya moyo”.
Na pia Bwana Yesu alisema…
Mathayo 5:4 “Heri wenye huzuni; Maana hao watafarijika”.
Na bado biblia inaendelea kusisitiza na kusema..
Mhubiri 7: 1 “Heri sifa njema kuliko marhamu nzuri; Na siku ya kufa kuliko siku ya kuzaliwa”.
1Wathesalonike 4:13 “Lakini, ndugu, hatutaki msijue habari zao waliolala mauti, msije mkahuzunika kama na wengine wasio na matumaini.14 Maana, ikiwa twaamini ya kwamba Yesu alikufa akafufuka, vivyo hivyo na hao waliolala katika Yesu, Mungu atawaleta pamoja naye.15 Kwa kuwa twawaambieni haya kwa neno la Bwana, kwamba sisi tulio hai, tutakaosalia hata wakati wa kuja kwake Bwana, hakika hatutawatangulia wao waliokwisha kulala mauti.16 Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza.17 Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele.18 Basi, farijianeni kwa maneno hayo.”.
Zaburi 23:4 “Naam, nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti, Sitaogopa mabaya; Kwa maana Wewe upo pamoja nami, Gongo lako na fimbo yako vyanifariji”.
Warumi 14:8 “Kwa maana kama tukiishi, twaishi kwa Bwana, au kama tukifa, twafa kwa Bwana. Basi kama tukiishi au kama tukifa, tu mali ya Bwana”.
Luka 23:43 “Yesu akamwambia, Amin, nakuambia, leo hivi utakuwa pamoja nami peponi”.
Yohana 11:26 “naye kila aishiye na kuniamini hatakufa kabisa hata milele. Je! Unayasadiki hayo”?
Yohana 14:1 “Msifadhaike mioyoni mwenu; mnamwamini Mungu, niaminini na mimi. 2 Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali. 3 Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo. 4 Nami niendako mwaijua njia”.
Yohana 14:1 “Msifadhaike mioyoni mwenu; mnamwamini Mungu, niaminini na mimi.
2 Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali.
3 Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo.
4 Nami niendako mwaijua njia”.
Zaburi 116:15 “Ina thamani machoni pa Bwana Mauti ya wacha Mungu wake”.
Ufunuo 14:13 “Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Andika, Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana nao”.
Mhubiri 3:1 “Kwa kila jambo kuna majira yake, Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu. 2 Wakati wa kuzaliwa, na wakati wa kufa; Wakati wa kupanda, na wakati wa kung’oa yaliyopandwa; 3 Wakati wa kuua, na wakati wa kupoza; Wakati wa kubomoa, na wakati wa kujenga; 4 Wakati wa kulia, na wakati wa kucheka; Wakati wa kuomboleza, na wakati wa kucheza”;
Mhubiri 3:1 “Kwa kila jambo kuna majira yake, Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu.
2 Wakati wa kuzaliwa, na wakati wa kufa; Wakati wa kupanda, na wakati wa kung’oa yaliyopandwa;
3 Wakati wa kuua, na wakati wa kupoza; Wakati wa kubomoa, na wakati wa kujenga;
4 Wakati wa kulia, na wakati wa kucheka; Wakati wa kuomboleza, na wakati wa kucheza”;
1Wakorintho 15:26 “Adui wa mwisho atakayebatilishwa ni mauti”.
Ufunuo 21:4 “Naye atafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita”.
2Wakorintho 5:1 “Kwa maana twajua ya kuwa nyumba ya maskani yetu iliyo ya dunia hii ikiharibiwa, tunalo jengo litokalo kwa Mungu, nyumba isiyofanywa kwa mikono, iliyo ya milele mbinguni”.
Wafilipi 3:20 “Kwa maana sisi, wenyeji wetu uko mbinguni; kutoka huko tena tunamtazamia Mwokozi, Bwana Yesu Kristo; 21 atakayeubadili mwili wetu wa unyonge, upate kufanana na mwili wake wa utukufu, kwa uweza ule ambao kwa huo aweza hata kuvitiisha vitu vyote viwe chini yake.
Wafilipi 3:20 “Kwa maana sisi, wenyeji wetu uko mbinguni; kutoka huko tena tunamtazamia Mwokozi, Bwana Yesu Kristo;
21 atakayeubadili mwili wetu wa unyonge, upate kufanana na mwili wake wa utukufu, kwa uweza ule ambao kwa huo aweza hata kuvitiisha vitu vyote viwe chini yake.
2Wakorintho 12:9 “Naye akaniambia, Neema yangu yakutosha; maana uweza wangu hutimilika katika udhaifu. Basi nitajisifia udhaifu wangu kwa furaha nyingi, ili uweza wa Kristo ukae juu yangu. 10 Kwa hiyo napendezwa na udhaifu, na ufidhuli, na misiba, na adha, na shida, kwa ajili ya Kristo. Maana niwapo dhaifu ndipo nilipo na nguvu”.
2Wakorintho 12:9 “Naye akaniambia, Neema yangu yakutosha; maana uweza wangu hutimilika katika udhaifu. Basi nitajisifia udhaifu wangu kwa furaha nyingi, ili uweza wa Kristo ukae juu yangu.
10 Kwa hiyo napendezwa na udhaifu, na ufidhuli, na misiba, na adha, na shida, kwa ajili ya Kristo. Maana niwapo dhaifu ndipo nilipo na nguvu”.
Warumi 5:12 “Kwa hiyo, kama kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo mauti; na hivyo mauti ikawafikia watu wote kwa sababu wote wamefanya dhambi”
Lakini tukishafahamu hayo, tukishafahamu kuwa haya maisha ni ya kitambo tu, yanayeyuka kama mvuke, swali linakuja je! Wewe umejiwekaje kipindi hichi kifupi ulichobakiwa nacho duniani?
Yakobo 4:14 “walakini hamjui yatakayokuwako kesho. Uzima wenu ni nini? Maana ninyi ni mvuke uonekanao kwa kitambo, kisha hutoweka”.
Jiulize ukifa na wewe leo ghafla, utakuwa upande gani?.Ukiona moyoni mwako huna jibu la uhakika ni wazi kuwa ukifa huwezi kwenda mbinguni..Kwasababu wanaokwenda mbinguni Yesu Kristo anauweka uhakika huo moyoni mwao. Lakini kama wewe ni mwenye dhambi, biblia inasema, mauti ya pili inakuongojea huko mbeleni, hata baada ya kifo hichi cha kawaida.
Warumi 6:23 “Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu”
Embu yatafakari vizuri maisha yako, hata ukipata kila kitu, na pesa zote duniani ujue ipo siku isiyokuwa na jina utakuwa ni vumbi tu..
Mhubiri 12:7 “Nayo mavumbi kuirudia nchi kama yalivyokuwa, Nayo roho kumrudia Mungu aliyeitoa”.
Mhubiri 9: 5 “kwa sababu walio hai wanajua ya kwamba watakufa; lakini wafu hawajui neno lo lote, wala hawana ijara tena; maana kumbukumbu lao limesahauliwa”.
Zaburi 146: 4 “Pumzi yake hutoka, huurudia udongo wake, Siku hiyo mawazo yake yapotea”.
Ndio kifo kitakukuta, lakini Bwana hapendi ufe katika hali ya dhambi, kwasababu hutakuwa na tumaini tena la maisha baada ya hapo.
Ezekieli 18:32 “Maana mimi sikufurahii kufa kwake afaye, asema Bwana MUNGU; basi ghairini, mkaishi”.
Inawezekana upo katika msiba wa mtu wako wa karabu, fahamu kuwa wakati mwingine Bwana anaruhusu uyapitie hayo, au uyaone hayo ili kukumbusha jambo la muhimu unalotakiwa kulifikiria kwanza.
Mhubiri 7: 14 “Siku ya kufanikiwa ufurahi, Na siku ya mabaya ufikiri. Mungu ameifanya hiyo moja kwenda sambamba na hiyo ya pili, ili mwanadamu asipate kulijua neno lo lote litakalofuata baada yake”.
Unaona?
Lakini ukimpa leo Yesu maisha yako, atakupa tumaini la kweli, atakuondolea hofu la mauti, atakuponya roho yako na wewe utakuwa na amani wakati wote, hata ikitokea umekufa leo, unaouhakika wa kwenda mbinguni.. anasema..
Mathayo 11:28 “Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha”.
Wokovu ni bure, kwa wakati wote, na unapatikana wakati wowote mtu anapoufungua moyo wake. Kwanini usimkaribishe Yesu mwokozi maishani mwako?
Yohana 3:16 “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele”.
Hivyo ikiwa leo umeguswa ndani yako na unasema sitaki tena kuishi maisha ya kubahatisha, sitaki kuishi maisha ya mguu mmoja ndani mwingine nje, nataka kuwa upande wa Yesu moja kwa moja. Basi uamuzi huo ni wa busara sana kwako, Kwasababu yeye anasema wote wajao kwangu sitawatupa nje kamwe.. Hivyo fungua hapa kwa ajili ya kuongozwa sala ya Toba na Bwana akubariki. >>>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Maran Atha.
NINI KINATOKEA BAADA YA KIFO?
USIUZE URITHI WAKO.
VIFUNGO VYA GIZA VYA MILELE.
UNYAKUO.
Amin, nawaambia, Kizazi hiki hakitapita, hata hayo yote yatakapotimia..!!
MIHURI SABA
Naomba kufahamu Nyama zilizosongolewa ni zipi?Je kunywa damu ni dhambi kwa Mkristo?
Nyama zilizosongolewa ni nyama za wanyama ambao hawajachinjwa, na damu yao kumwagika chini.
Kipindi kabla hata ya agano la kwanza(Kale) , Mungu tayari alikuwa ameshampa Nuhu maagizo kuwa asile nyama ya mnyama yoyote pamoja na damu yake ndani yake.
Mwanzo 9:4 “Bali nyama pamoja na uhai, yaani, damu yake, msile”.
Tunaona miaka mingi baadaye Mungu anakuja kumwambia tena Musa jangwani maneno hayo hayo:
Kumbukumbu 12:23 “Ila ujihadhari kwamba usile damu, kwani ile damu ndiyo uhai; na uhai usile pamoja na nyama. 24 Usiile; imwage juu ya nchi kama maji”.
Walawi 17:10 “Kisha mtu awaye yote wa nyumba ya Israeli, au miongoni mwa hao wageni wakaao kati yao, atakayekula damu, ya aina yo yote, nitakunja uso wangu juu ya mtu huyo alaye damu, nami nitamkatilia mbali na watu wake. 11 Kwa kuwa uhai wa mwili u katika hiyo damu; nami nimewapa ninyi hiyo damu juu ya madhabahu, ili kufanya upatanisho kwa ajili ya nafsi zenu; kwani ni hiyo damu ifanyayo upatanisho kwa sababu ya nafsi. 12 Kwa hiyo naliwaambia wana wa Israeli, Hapana mtu miongoni mwenu aliye na ruhusa kula damu, wala mgeni aketiye kati yenu asile damu”.
Walawi 17:10 “Kisha mtu awaye yote wa nyumba ya Israeli, au miongoni mwa hao wageni wakaao kati yao, atakayekula damu, ya aina yo yote, nitakunja uso wangu juu ya mtu huyo alaye damu, nami nitamkatilia mbali na watu wake.
11 Kwa kuwa uhai wa mwili u katika hiyo damu; nami nimewapa ninyi hiyo damu juu ya madhabahu, ili kufanya upatanisho kwa ajili ya nafsi zenu; kwani ni hiyo damu ifanyayo upatanisho kwa sababu ya nafsi.
12 Kwa hiyo naliwaambia wana wa Israeli, Hapana mtu miongoni mwenu aliye na ruhusa kula damu, wala mgeni aketiye kati yenu asile damu”.
Lakini tukirudi tena katika agano letu jipya, tunaona moja ya maagizo ambayo mitume wanalipa kanisa la mataifa(yaani sisi) Ni kutokula nyama zilizongolewa( yaani nyama ambazo hazijachinjwa na damu kumwagika)..
Matendo 15:19 “Kwa sababu hiyo mimi naamua hivi; Tusiwataabishe wale waliomgeukia Mungu katika Mataifa; 20 bali tuwaandikie kwamba wajiepushe na unajisi wa sanamu, na uasherati, na nyama zilizosongolewa, na damu. 21 Kwa maana tangu zamani za kale Musa anao watu wahubirio mambo yake; katika kila mji husomwa kila sabato katika masinagogi”.
Matendo 15:19 “Kwa sababu hiyo mimi naamua hivi; Tusiwataabishe wale waliomgeukia Mungu katika Mataifa;
20 bali tuwaandikie kwamba wajiepushe na unajisi wa sanamu, na uasherati, na nyama zilizosongolewa, na damu.
21 Kwa maana tangu zamani za kale Musa anao watu wahubirio mambo yake; katika kila mji husomwa kila sabato katika masinagogi”.
Sasa swali linakuja Je kwa mantiki hiyo wakristo haturuhusiwi kabisa kula nyama zilizongolewa au kunywa damu?
Ukweli ni kwamba kulingana na mazingira ya wakati ule kwa watu wa mataifa, na ya sasa, ni ngumu kuishi bila kukutana na nyama za namna hiyo.. Kwasababu nyama nyingi siku hizi, hazichinjiwi nyumbani, unazikuta mabuchani, au supermarket, na kule hujui zimechinjwaje chinjwaje.. Hivyo huwezi kuuliza hii nyama iliandiliwaje, vinginevyo hutakaa ule nyama kabisa…Sasa Bwana Yesu kwa kulijua hilo akawaagiza mitume wake, kuwa watakachokutana nacho mbele yao kila mahali mnapokaribishwa wale (Luka 10:8),
Mtume Paulo naye aliliweka wazi hilo kwa wakorintho na kuwaambia..
1Wakorintho 10:25 “Kila kitu kiuzwacho sokoni kuleni, bila kuuliza-uliza, kwa ajili ya dhamiri; 26 maana, Dunia ni mali ya Bwana na vyote viijazavyo”.
1Wakorintho 10:25 “Kila kitu kiuzwacho sokoni kuleni, bila kuuliza-uliza, kwa ajili ya dhamiri;
26 maana, Dunia ni mali ya Bwana na vyote viijazavyo”.
Kwamfano Soseji nyingine zinatengenezwa na damu ndani yake, na nyingine hazitengenezwi na damu, Hivyo ukipewa kula bila kuuliza uliza, ukikuta zinauzwa dukani nunua ule bila kuuliza uliza.
Kwasababu sisi agano letu halipo katika vyakula, bali lipo rohoni..vyakula havitubadilishi kitu. Lakini pale inapotokea unachinja mbuzi wako, au kuku wako, au ng’ombe wako nyumbani ni vema ukaimwaga damu ya mnyama huyo chini, usinywe kisusio..Si vema kufanya hivyo, kwasababu tumeshapewa maagizo hayo.
Zaidi ya yote amani ya Kristo iamue ndani yako.
Bwana akubariki.
DAMU YA YESU INANENAJE MEMA KULIKO YA HABILI?
MUNGU AKIKUPITA LEO, HAIMAANISHI KUWA HAJAKUCHAGUA.
USITAFUTE FAIDA YAKO MWENYEWE BALI YA WENGINE.
MAJONZI YA MTUME PAULO KWA NDUGU ZAKE.
HUDUMA YA WALE MASHAHIDI WAWILI.
SWALI: Je tunaruhusiwa kujipaka mafuta au kujipulizia marashi/manukato (perfumes)?
JIBU: Sio vibaya kujipaka mafuta usoni au mwilini, ili kuondoa ule mpauko wa asili, mafuta hususani yale ya asili ni mazuri kwa ngozi, lakini pia sio amri kwamba lazima tujipake mafuta, hata hivyo ngozi zetu huwa zinatoa zenyewe mafuta yake ya asili.
Lakini yapo mafuta ya kuchubua ngozi, na yenye marashi makali, hayo ni kinyume na maandiko kuyatumia kwasababu lengo lake ni kubadilisha maumbile, ambayo maudhui yake ni Udunia!..Biblia inasema miili yetu ni hekalu la Roho Mtakatifu na pia miili yetu sio mali yetu wenyewe, ni mali ya Mungu, hivyo hatupaswi kuibadilisha kutoka katika hali yake ya asili na kuifanya tutakavyo sisi (1Wakorintho 6:19).
Sasa unaweza kuuliza ni wapi katika agano jipya tumepewa ruhusa ya kutumia mafuta?
Mathayo 6: 16 “Tena mfungapo, msiwe kama wanafiki wenye uso wa kukunjamana; maana hujiumbua nyuso zao, ili waonekane na watu kuwa wanafunga. Amin, nawaambia, wamekwisha kupata thawabu yao.17 Bali wewe ufungapo, JİPAKE MAFUTA KİCHWANİ, UNAWE USO;18 ili usionekane na watu kuwa unafunga, ila na Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi”
Mathayo 6: 16 “Tena mfungapo, msiwe kama wanafiki wenye uso wa kukunjamana; maana hujiumbua nyuso zao, ili waonekane na watu kuwa wanafunga. Amin, nawaambia, wamekwisha kupata thawabu yao.
17 Bali wewe ufungapo, JİPAKE MAFUTA KİCHWANİ, UNAWE USO;
18 ili usionekane na watu kuwa unafunga, ila na Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi”
Hayo ni maneno yaliyozungumzwa na Bwana Yesu mwenyewe.
Swali lingine ni je! Ni mafuta gani yanayofaa?..Hakuna orodha maalum ya mafuta yanayofaa, kikubwa mafuta yoyote yale yawe ya kiwandani au ya asili ambayo hayana kemikali nyingi na hayana marashi makali yanafaa kutumika.
Na Marashi ni hivyo hivyo, yapo marashi ya nguo..ambayo lengo lake ni kudhibiti nguo isitoe harufu mbaya aidha ya jasho au ya kitu kingine kisichofaa. (Katika mazingira fulani)
Nayo pia sio vibaya kuyatumia, ilimradi tu yasiwe na maudhui ya kishetani. Marashi yanayotumika mengi siku hizi yana maudhui ya kidunia, marashi mtu anayotumia ambapo mtu aliyesimama mita 2 mbele yake au nyuma yake anasikia harufu yake, tayari lengo la marashi hayo sio kudhibiti harufu bali kuvuta hisia kutoka kwa mwingine…jambo ambalo sio sawa.
Kiwango cha marashi kinapaswa kiwe kidogo sana)..kiasi kwamba mpaka pua ifike karibu na nguo ndipo isikike..(na hiyo ni kama kuna ulazima wa kuyatumia kutokana na mazingira, lakini kama hakuna ulazim hayapaswi kutumika kabisa).
Na zaidi sana, mafuta mengi tunayotumia au sabuni zina kiwango tosha cha marashi ambayo hatuhitaji kuongeza mengine juu yake.
Katika biblia marashi yametafsiriwa sehemu kadha wa kadha kama “Marhamu” au “Manukato”. Unaweza kupitia mistari ifuatayo binafsi (Mathayo 26:7-13, Marko 14:3, Marko 16:1).
Lakini zaidi sana Marashi yetu yanayompendeza Mungu ni Maombi yetu kwake, na utakatifu wetu.
Ufunuo 5:8 “Hata alipokitwaa kile kitabu, hao wenye uhai wanne na wale wazee ishirini na wanne wakaanguka mbele za Mwana-Kondoo, kila mmoja wao ana kinubi, na vitasa vya dhahabu vilivyojaa MANUKATO, AMBAYO Nİ MAOMBİ YA WATAKATİFU”.2Wakorintho 2:14 “Ila Mungu ashukuriwe, anayetushangiliza daima katika Kristo, na kuidhihirisha harufu ya kumjua yeye kila mahali kwa kazi yetu.15 Kwa maana sisi tu manukato ya Kristo, mbele za Mungu, katika wao wanaookolewa, na katika wao wanaopotea;16 katika hao wa pili harufu ya mauti iletayo mauti; katika hao wa kwanza harufu ya uzima iletayo uzima. Naye ni nani atoshaye kwa mambo hayo”
Ufunuo 5:8 “Hata alipokitwaa kile kitabu, hao wenye uhai wanne na wale wazee ishirini na wanne wakaanguka mbele za Mwana-Kondoo, kila mmoja wao ana kinubi, na vitasa vya dhahabu vilivyojaa MANUKATO, AMBAYO Nİ MAOMBİ YA WATAKATİFU”.
2Wakorintho 2:14 “Ila Mungu ashukuriwe, anayetushangiliza daima katika Kristo, na kuidhihirisha harufu ya kumjua yeye kila mahali kwa kazi yetu.
15 Kwa maana sisi tu manukato ya Kristo, mbele za Mungu, katika wao wanaookolewa, na katika wao wanaopotea;
16 katika hao wa pili harufu ya mauti iletayo mauti; katika hao wa kwanza harufu ya uzima iletayo uzima. Naye ni nani atoshaye kwa mambo hayo”
Hivyo tukiwa maridadi wa mwilini, tukanukia vizuri na huku rohoni tunatoa harufu mbaya, hatusali, hatufungi, hatuombi, hatuishi maisha ya kumpendeza yeye..basi mbele za Mungu tunapeleka harufu mbaya.
Lakini tukiwa waombaji, tukimwomba Mungu rehema, na neema..pamoja na tukiwaombea na wengine na kuliombea kanisa, na tukiishi maisha masafi, basi tutakuwa ni lulu mbele za Mungu.
Mungu atasaidie katika hilo.
Maran atha!
KUJIPAMBA NI DHAMBI?
MSAMARIA MWEMA.
ROHO HUTUOMBEA KWA KUUGUA KUSIKOWEZA KUTAMKWA!
MIGUU ILIYO MYEPESI KUKIMBILIA MAOVU, NI CHUKIO KWA BWANA.
UWEZO WA KIPEKEE.
SWALI: Ni jeshi gani la Mbinguni ambalo Mungu aliwaacha wana wa Israeli waliabudu katika Matendo 7:42? Je ni Malaika au?
JIBU: Matendo 7: 41 “Wakafanya ndama siku zile, wakaleta dhabihu kwa sanamu ile, wakafurahia kazi za mikono yao. 42 Basi Mungu akaghairi, akawaacha ili waliabudu jeshi la mbinguni, kama ilivyoandikwa katika chuo cha manabii, Je! Mlinitolea mimi dhabihu na sadaka Miaka arobaini katika jangwa, enyi nyumba ya Israeli?”
JIBU: Matendo 7: 41 “Wakafanya ndama siku zile, wakaleta dhabihu kwa sanamu ile, wakafurahia kazi za mikono yao.
42 Basi Mungu akaghairi, akawaacha ili waliabudu jeshi la mbinguni, kama ilivyoandikwa katika chuo cha manabii, Je! Mlinitolea mimi dhabihu na sadaka Miaka arobaini katika jangwa, enyi nyumba ya Israeli?”
Habari hii inawazungumzia wana wa Israeli wakati wanatoka Misri. Wakiwa jangwani biblia inasema walikuwa wakikengeuka mara kadhaa, walikuwa wakimwacha Mungu na kugeukia kuchonga sanamu, na wakati mwingine kumjaribu Mungu (Kutoka 17:2).
Lakini kuna jambo lingine tunaliona walilokuwa wanalifanya ambalo lilikuwa ni machukizo kwa Mungu, na hilo si lingine zaidi ya KULIABUDU JESHI LA MBINGUNI.
Sasa swali la msingi hapo ni je! Hilo jeshi ni lipi?, ni malaika au ni nini?.
Jibu ni kwamba si Malaika, bali ni miungu ya kipagani.
Si kila mahali kwenye biblia palipoandikwa neno “mungu” panamaanisha “Mungu wa mbingu na nchi”, vivyo hivyo sio kila mahali katika biblia palipoandikwa neno “bwana” panamaanisha “Bwana Mungu wa mbingu na nchi”…hali kadhalika sio kila mahali katika biblia palipoandikwa neno “mbingu” au “mbinguni”, panamaanisha “Mbinguni malaika watakatifu walipo”..
Dini karibia zote zinaamini kwamba kuna mbingu..kwamba kuna mahali huko juu ambapo kuna viumbe watakatifu wanaishi,..Na nyingine zinaamini huko mbinguni kuna miungu mingi, kuna jeshi kubwa la miungu, ambayo yote inastahili kuabudiwa. Kwamfano dini ya kihindu tu peke yake ina zaidi ya miungu milioni 330.
Sasa ikatokea kwa mtu ambaye ni mkristo, ambaye ameshajua ukweli wote kwamba Mungu ni mmoja tu aliyeko mbinguni ambaye anaabudiwa katika roho na kweli.. akaiacha hiyo imani na kisha akaenda kujiunga na imani nyingine(kama hiyo ya kihundu) inayoamini kwamba mbinguni kuna miungu mingi, na akaenda kuiabudu hiyo miungu yao. Hapo ni sawa na kusema “AMEKWENDA KULİSUJUDİA JESHİ LA MBİNGUNİ”..na si mbingu ile ambayo malaika watakatifu wapo bali ni mbingu ya kihindu, ambayo kiuhalisia haipo! ni uongo uliotengenezwa na shetani tu kuwadanganya watu kuwa kuna mbingu yenye miungu mingi!,
Ni agenda ya shetani na mapepo yake Kutafuta kuabudiwa na kuwapotosha watu wa Mungu. Hiyo idadi yote ya miungu wanayoiabudu ni mapepo yanayojiguza na kuchukua sura ya hivyo wanavyoviabudu. (zingatia: wengi wanaoabudu hiyo miungu, sio watu wabaya na wala si maadui zetu, wengi wao ni watu wazuri, wanafanya hayo kwasababu bado hawajaujua ukweli, au macho ya mioyo yao bado hayajafumbuliwa, kwahiyo wanaabudu vitu wasivyovijua, hivyo ni jukumu letu wewe na mimi kuwapelekea injili na kuwaombea!, ili macho yao yafumbuliwe wapate kuona na kuokolewa Matendo 17:29-31).
Kwahiyo Jeshi la mbinguni linalozungumziwa hapo sio Malaika waliopo mbinguni, bali ni miungu iliyopo mbinguni huko angani, ambayo kiuhalisia ni shetani na mapepo yake.
Na malkia wa mbinguni aliyezungumziwa pia katika Yeremia 7:18, 44:17-25 sio Bikira Mariamu wala sio Malaika fulani wa kike aliyeko mbinguni bali ni mungu fulani wa kipagani, wanayedai kwamba yupo mbinguni (kwa maelezo marefu utatutumia ujumbe inbox), ambaye ni Pepo!.
Mwisho ni muhimu kuchukua tahadhari!.. pale tunapoonywa mara nyingi!…Hapo kwenye matendo 7:42, biblia inasema “ Basi MUNGU AKAGHAİRİ, AKAWAACHA ili waliabudu jeshi la mbinguni,”.
Litazame hilo neno kwa makini!..Mungu akaghairi!, akawaacha!! İli waliabudu jeshi la mbinguni…Ni jambo la kuogopesha sana pale Mungu anapoghairi juu yako, na kukuacha uendelee kufanya unayoyafanya!…hilo ni jambo la kuogopesha sana!..Anaabudu masanamu unayodhani ni watakatifu Fulani wa mbinguni, na umeonywa mara nyingi husikii, hapo unamfanya Mungu aghairi juu yako.
Warumi 1:28 “Na kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wayafanye yasiyowapasa”
2Wathesalonike 2:10 “na katika madanganyo yote ya udhalimu kwa hao wanaopotea; kwa sababu hawakukubali kuipenda ile kweli, wapate kuokolewa. Kwa hiyo Mungu awaletea nguvu ya upotevu, wauamini uongo”.
Jiupeshe na ibada za sanamu ni dhambi, jiepushe na mambo yote maovu na mwisho soma neno kwa bidii..
Bwana atubariki.
AINA YA MAADUI UTAKAOKUTANA NAO KATIKA SAFARI YAKO YA WOKOVU.
CHUKIZO LA UHARIBIFU
MUNGU WANGU,MBONA UMENIACHA?.
Kibanzi Na Boriti, kwenye biblia vinamaanisha nini?
Boriti ni kipande kikubwa sana cha mbao, kinaweza kikawa ni ki-gogo, au nguzo, au mbao yoyote pana..
Lakini kibanzi, ni kichembe kidogo sana cha mbao, kama mchanga, hata wakati mwingine kufikia kuwa kama vumbi la mbao ambalo ni ngumu sana kuliona. Hicho ndicho kibanzi.
Sasa Bwana Yesu alitoa mfano huo, wa picha ili kuweka msisitizo kile alichotaka kukisema, yaani katika hali ya kawaida, kama wewe huwezi kuona nguzo iliyosimama mbele ya macho yako inayokuzuia usione kabisa, utaona vipi vumbi la mbao lililo katika jicho la mwenzako?..Umeona moja kwa moja huo ni unafki..
Vivyo hivyo na sisi kabla hatujawahukumu watu, tuyachunguze maisha yetu Je! hayo wanayoyafanya Je, hayapo ndani yetu na sisi? Kabla hujamwambia Fulani acha usengenyaji, Je! na wewe si msengenyaji? Kama sivyo basi ni heri ukae tu kimya, kwasababu mistari ya juu yake inasema, kipimo kile kile tuhukumucho ndicho tutakachokuhumiwa na sisi.
Mathayo 7:1 “Msihukumu, msije mkahukumiwa ninyi. 2 Kwa kuwa hukumu ile mhukumuyo, ndiyo mtakayohukumiwa; na kipimo kile mpimiacho, ndicho mtakachopimiwa. 3 Basi, mbona wakitazama kibanzi kilicho ndani ya jicho la ndugu yako, na boriti iliyo ndani ya jicho lako mwenyewe huiangalii? 4 Au utamwambiaje nduguyo, Niache nikitoe kibanzi katika jicho lako; na kumbe! Mna boriti ndani ya jicho lako mwenyewe? 5 Mnafiki wewe, itoe kwanza ile boriti katika jicho lako mwenyewe; ndipo utakapoona vema kukitoa kile kibanzi katika jicho la ndugu yako.
Mathayo 7:1 “Msihukumu, msije mkahukumiwa ninyi.
2 Kwa kuwa hukumu ile mhukumuyo, ndiyo mtakayohukumiwa; na kipimo kile mpimiacho, ndicho mtakachopimiwa.
3 Basi, mbona wakitazama kibanzi kilicho ndani ya jicho la ndugu yako, na boriti iliyo ndani ya jicho lako mwenyewe huiangalii?
4 Au utamwambiaje nduguyo, Niache nikitoe kibanzi katika jicho lako; na kumbe! Mna boriti ndani ya jicho lako mwenyewe?
5 Mnafiki wewe, itoe kwanza ile boriti katika jicho lako mwenyewe; ndipo utakapoona vema kukitoa kile kibanzi katika jicho la ndugu yako.
Bwana atusaidie sote tuyashinde hayo.
https://wingulamashahidi.org/ikabodi-maana-yake-ni-nini/
KAMA MMOJA TU NDIO HIVI! SI ZAIDI 153?
MKUMBUKE MKE WA LUTU.
Israeli ipo bara gani?
SWALI: Biblia inamaanisha nini inaposema “Usimtokose mwana-mbuzi katika maziwa ya mama yake.”
JIBU: Huu ni msemo ambao umeonekana ukipachikwa katikati ya vifungu kadha wa kadha kwenye biblia..
Kwa mfano utaona.. pale kwenye Kutoka 23:18-19 inasema..
18 Usisongeze damu ya dhabihu zangu pamoja na mkate uliotiwa chachu, wala mafuta ya sikukuu yangu usiyaache kusalia hata asubuhi. 19 Ya kwanza ya malimbuko ya nchi yako utayaleta na kuyatia ndani ya nyumba ya Bwana, Mungu wako. Usimtokose mwana-mbuzi katika maziwa ya mama yake.
18 Usisongeze damu ya dhabihu zangu pamoja na mkate uliotiwa chachu, wala mafuta ya sikukuu yangu usiyaache kusalia hata asubuhi.
19 Ya kwanza ya malimbuko ya nchi yako utayaleta na kuyatia ndani ya nyumba ya Bwana, Mungu wako. Usimtokose mwana-mbuzi katika maziwa ya mama yake.
Ukisoma tena..Kutoka 34:25-26, utaona inasema hivi..
“25 Usisongeze damu ya sadaka yangu pamoja na mkate uliotiwa chachu; wala hiyo sadaka ya sikukuu ya pasaka haitasazwa hata asubuhi. 26 Vitu vya kwanza vya malimbuko ya nchi yako utavileta na kuvitia ndani ya nyumba ya Bwana Mungu wako. Usimtokose mwana-mbuzi katika maziwa ya mama yake”.
“25 Usisongeze damu ya sadaka yangu pamoja na mkate uliotiwa chachu; wala hiyo sadaka ya sikukuu ya pasaka haitasazwa hata asubuhi.
26 Vitu vya kwanza vya malimbuko ya nchi yako utavileta na kuvitia ndani ya nyumba ya Bwana Mungu wako. Usimtokose mwana-mbuzi katika maziwa ya mama yake”.
Ukirudi tena kwenye Kumbukumbu 14:21 nayo pia utaona ikisema.
“Msile nyamafu yo yote; waweza kumpa mgeni aliye ndani ya malango yako, ili apate kula; au kumliza mtu wa mataifa; kwa kuwa wewe u taifa takatifu kwa Bwana, Mungu wako. Usimtokose mwana-mbuzi katika maziwa ya mamaye”.
Sasa pale anaposema, usimtokose mwana-mbuzi, katika maziwa ya mama yake, anamaanisha kumchemsha mtoto wa mbuzi, kwa maziwa ya mama yake, yaani badala ya kumchemsha kwenye maji, wewe unachukua yale maziwa anayoyanyonya kutoka kwa mama yake na kumchemshia nayo..
Kwa namna ya kawaida ni kitendo kisicho cha kiungwana chenye ukakasi kidogo, hata kwako wewe unayesikia eti?..Utajiuliza ni kwanini ufanye hivyo? Kwani hakuna maji ya kumchemshia, au kitu kingine mpaka utumie maziwa, tena yale yale ya mama yake? Ni sawa na nguruwe aliyezaa mtoto, halafu unampa mtoto wake mwenyewe amle kama chakula chake..sasa hiyo ndio picha iliyopo hapo.
Ni kitendo kinachoonyesha unyama si unyama, ukosefu wa nidhamu..?
Ni utaratibu na mfumo wa kipagani ambao ulikuwa unafanyika na watu wa mataifa wasiomjua Mungu, walikuwa wanafanya hivyo kwa sababu za kishirikina, ni kama mila zinazoendelea siku hizi, hivyo Mungu aliwaonya wana wa Israeli wasifanye mambo kama hayo, kwasababu ni machukizo mbele zake, ni Utaratibu ambao hauna tofauti na ule wa kuwapitisha watoto kwenye moto, (soma 2Wafalme 21:6, 2Wafalme 16:3).
Hata sasa, wengi wetu tunafanya kafara kama hizo rohoni?.
Tunamtolea Mungu dhabihu zilizochanganyikana na mambo ambayo Mungu ameyakataza, tunafanya mambo kama watu wa mataifa. Tunamsifu Mungu na huku vinywa vyetu vimejaa matusi, na masengenyo, chuki na visasi, tunamtolea Mungu na huku biashara zetu ni haramu, tunahudhuria kanisani lakini tunaendelea kudumisha mila zetu za kishirikina, hali kadhalika tumeokoka lakini heshima kwa mzazi haipo, na heshima kwa Watoto wetu haipo (hiyo yote katika roho ni sawa na kumtokosa mwanambuzi katika maziwa yake) N.k.
Bwana atusaidie, tuzishike amri zake na tumpendeze yeye.
Bwana atuokoe na kutubariki..
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312
USITUMAINISHWE NA MANENO YA UONGO.
YESU KWETU NI RAFIKI
Bali wajane walio vijana ukatae kuwaandika hao.
ZIFAHAMU HUDUMA KUU (10) ZA SHETANI DUNIANI.
CHOCHOTE UMFANYIACHO KRISTO KINA THAMANI.
WhatsApp
Imani ya mitume (Apostle’s creed), inapatikana wapi kwenye biblia?
Imani ya mitume ambayo unaisikia mara kwa mara ikikiriwa katika baadhi ya madhehebu hususani Katoliki, Lutherani, na Anglikana, haipo mahali popote katika maandiko, na wala haikuwahi kukikiriwa na mitume wa Kristo sehemu yoyote.
Imani hii, ilikuja kuaandikwa miaka mingi mbeleni(zaidi ya miaka 300),baada ya mitume kuondoka, waliiandika wakizingatia kiini cha wazo kuu la mitume walichokuwa wanaamini katika maandiko.
Na kimsingi imani hii ipo kimaandiko. Hivyo mtu kuikiri hakuna shida, kwasababu haimpotezi katika misingi ya imani ya biblia.
Inasema hivi.
Namwamini Mungu Baba mwenyezi, muumba wa mbingu na nchi, na Yesu Kristo, mwana wake wa pekee, Bwana wetu.Aliyechukuliwa mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu. Akazaliwa na bikira Mariamu. Akateswa zamani za Pontio Pilato. Akasulubiwa. Akafa. Akazikwa.Akashuka mahali pa wafu. Siku ya tatu akafufuka. Akapaa mbinguni. Ameketi mkono wa kuume wa Mungu Baba mwenyezi. Kutoka huko atakuja kuwahukumu walio hai na wafu.Namwamini Roho Mtakatifu, kanisa takatifu lililo moja, ushirika wa watakatifu, ondoleo la dhambi, ufufuo wa wafu na uzima wa milele.Amina.
Jambo la kuzingatia ni kuwa, ukiikiri/usipoikiri sio tiketi ya wewe ni mkristo, au utakwenda mbinguni, huu ni utaratibu tu au mapokeo tu ya baadhi ya wakristo. kitachokufa wewe uwe mkristo, ni kuamini, kutubu na kuoshwa dhambi zako kwa damu ya YESU Kristo, kwa njia ya ubatizo( sawasawa na Matendo 2:38).
Na ubatizo sahihi wa kimaandiko ni ule wa kuzamwishwa katika maji mengi,(Yohana 3:23) na kwa jina la Yesu Kristo.
Hivyo kama utahitaji upate ubatizo huu sahihi. Na Kama utapenda tuwe tunakutumia masomo ya biblia kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312
Je! Ni sahihi kutumia maji ya upako,katika kufanya maombezi?
Je mtu akifa anakuwa hana dhambi tena?
KWA KUWA NGUVU ZA MBINGUNI ZITATIKISIKA.
FANYIKA SIPORA WA KRISTO, UNYAKUO UPO KARIBU.
MAPIGO YA VITASA SABA, NA SIKU YA BWANA.
Je! Adamu alikuwa na mwanamke mwingine anayeitwa Lilith?
JIBU: Biblia imetupa majibu kama ifuatavyo..
Mwanzo 1:27 “Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa MUNGU ALIMWUMBA, MWANAMUME NA MWANAMKE ALIWAUMBA. 28 Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi”.
Mwanzo 1:27 “Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa MUNGU ALIMWUMBA, MWANAMUME NA MWANAMKE ALIWAUMBA.
28 Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi”.
Huo ni mstari wa kwanza kabisa unaozungumzia uumbaji wa mwanadamu katika biblia, hakuna mstari mwingine kabla ya huu.. Na unasema Mungu aliwaumba mwanaume na mwanamke. (maneno hayo mawili yapo katika umoja.). Na haijasema Mungu alimwumba Mwanaume na wanawake.. wala haijasema Mungu alimuumba mwanamke na wanaume.
Kwahiyo hakukuwa na mwanaume Zaidi ya Adamu, na wala hakukuwa na mwanamke mwingine Zaidi ya Hawa katika uumbaji.
Jambo linalowachanganya wengi ambalo ndilo limezua swali hili, ni kuhusu mke wa Kaini, kwamba Kaini alitolea wapi mke?
Kwanza kabisa Ni muhimu kufahamu kuwa Adamu na Hawa, walizaa Watoto wengine wengi wakike na wa kiume baada ya Habili na Kaini. Watoto wa Adamu hawakuwa wawili tu, bali wengi.
Mwanzo 5:4 “Siku za Adamu baada ya kumzaa Sethi zilikuwa miaka mia nane, akazaa wana, waume na wake. Siku zote za Adamu alizoishi ni miaka mia kenda na thelathini, naye akafa”.
Kwahiyo miongoni mwa hao Watoto wa kike aliowazaa Adamu, mmojawao ndio alikuwa mke wa Kaini, na Kaini na mkewe walizaa Watoto, na watoto wao walizaa Watoto, na wajukuu zao pia walizaa..Na wakati huo watu walikuwa na uwezo wa kuishi mamia ya miaka.
Kwahiyo ni uongo kusema kuwa Adamu alikuwa na mke mwingine tofauti na Hawa.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312
BUSTANI YA NEEMA.
NA NENO LA BWANA LILIKUWA ADIMU SIKU ZILE.
KIFO CHA REINHARD BONKEY KINAACHA UJUMBE GANI KWETU?
SIKU YA UNYAKUO ITAKUKUTAJE?
Jina la Bwana wetu Yesu Kristo, libarikiwe. Nakukaribisha katika kuyatafakari maandiko.
Tunajua kuja kwa Yesu mara ya kwanza, kulibeba siri nyingi za kuja kwake mara ya pili, kwa mfano wakati ule kabla ya Herode, kutaka kumuua Yesu pindi alipozaliwa, kulitangulia kwanza sensa kubwa kwa watu wote wa ulimwengu, ambayo ilimlazimu kila mmoja aende kwenye mji wake aliozaliwa ili ahesabiwe huko..Na ndivyo itakavyokuja kuwa kipindi kifupi kabla ya Yesu kurudi mara ya pili duniani, mpinga-Kristo ataleta utaratibu mpya wa watu wote kuhakikiwa, mfumo huu mpya ndio ile inayojulikana kama chapa ya Mnyama ambao utamlazimu kila mmoja awe nayo, kama mtu hana basi hataweza kuuza au kununua au kufanya biashara, au kuajiriwa mahali popote..kwa urefu wa somo hilo tutumie ujumbe inbox tukutumie ..
Lakini pia kulikuwa na jambo lingine, ambalo lilichochea kwa haraka sana dhiki kutokea pale Yerusalemu pindi tu Yesu alipozaliwa. Na jambo lenyewe, lilikuwa kwa wale Mamajusi kutoka Mashariki.
Sasa ukiangalia pale, utagundua habari ya kuzaliwa kwa Yesu ilikuwa imeshajulikana hata kabla ya baadha ya watu pale Israeli kujua, utaona kulikuwa na wale wachungaji kule makondeni waliotokewa na malaika na kuambiwa wamfuate mtoto..Ni kweli walienda na kushuhudia waliyoambiwa, na pengine baaada ya pale walisambaza taarifa za kuzaliwa kwa watu wengi vijijini na mijini, lakini habari zao hazikuwa na nguvu sana, wala hazikuleta mabadiliko yoyote kwa Israeli au kwa Herode, Vivyo hivyo, walikuwepo wakina Simoni na Hana, ambao Mungu aliwashuhudia kuwa huyu ndiye mwokozi na mfalme, pengine nao walitangaza, lakini taarifa zao pia hazikufika mbali sana.
Walikuwepo wakina Zekaria kuhani na mke wake Elisabeti, ambao walitangaza habari za Yesu na Yohana, ambazo kwa habari ya Yohana biblia inasema zilijulikana katika mji wote ule lakini bado hazikuwa na mashiko sana..Lakini tunaona kulikuwa na kundi lingine la watu, toka mbali sana, lililoleta habari,..Hilo halikuwa la watu wa pale Israeli, bali lilitoka mbali sana, ndio wale mamajusi wa Mashariki, walioina nyota yake na kufunga safari mpaka Israeli, na walipofika moja kwa moja wakamuuliza mfalme Herode, yupo wapi mfalme wa Wayahudi aliyezaliwa..Sasa kwa taarifa hizo Biblia inatuambia sio tu Herode zilimfadhaisha, bali na Israeli nzima. Hapo ndipo pakawa mwanzo wa sura nyingine kwa taifa la Israeli.
Mathayo 2:1 “Yesu alipozaliwa katika Bethlehemu ya Uyahudi zamani za mfalme Herode, tazama, mamajusi wa mashariki walifika Yerusalemu, wakisema, 2 Yuko wapi yeye aliyezaliwa mfalme wa Wayahudi? Kwa maana tuliiona nyota yake mashariki, nasi tumekuja kumsujudia. 3 Basi mfalme Herode aliposikia hayo, alifadhaika, na Yerusalemu pia pamoja naye. 4 Akakusanya wakuu wa makuhani wote na waandishi wa watu, akatafuta habari kwao, Kristo azaliwa wapi”?
Mathayo 2:1 “Yesu alipozaliwa katika Bethlehemu ya Uyahudi zamani za mfalme Herode, tazama, mamajusi wa mashariki walifika Yerusalemu, wakisema,
2 Yuko wapi yeye aliyezaliwa mfalme wa Wayahudi? Kwa maana tuliiona nyota yake mashariki, nasi tumekuja kumsujudia.
3 Basi mfalme Herode aliposikia hayo, alifadhaika, na Yerusalemu pia pamoja naye.
4 Akakusanya wakuu wa makuhani wote na waandishi wa watu, akatafuta habari kwao, Kristo azaliwa wapi”?
Sasa kama tunavyoijua habari kilichofuata pale ni Herode kwenda kuwaua watoto wote waliokuwa Bethlehemu wakati ule (kukawa na kilio kikuu Bethlehemu).
Mathayo 2:18 “Sauti ilisikiwa Rama, Kilio, na maombolezo mengi, Raheli akiwalilia watoto wake, Asikubali kufarijiwa, kwa kuwa hawako”.
Lakini kabla ya kuwaua, Mama na mtoto walihamishwa, na kupelekwa Misri kuikwepa dhiki.
Sasa, katika siku za mwisho, mambo kama hayo hayo yataenda kujirudia,. Baada ya Unyakuo kupita, dunia itakuwa imebakiwa na miaka 7 tu mpaka iishe kabisa, katika kipindi hicho, Mungu atawanyanyua watu watu wawili ambao watawatenga kwa lengo moja tu, la kwenda kuwatolea Unabii Israeli, juu ya kurudi kwa Kristo ulimwenguni kutawala kama mfalme wa wafalme…ndio mfano wa wale mamajusi wa Mashariki. (Na Huo ndio utakuwa wakati wa neema kuhamia Israeli)
Watu hawa ndio wale mashahidi wawili tunaowasoma katika Ufunuo 11, Watahubiri pale Israeli, kwa kipindi cha miaka mitatu na nusu kama biblia inavyotuambia,..Na wakati huo mpinga-Kristo, atawasikia, na hiyo ndio itakuwa kama alert yake, kuwa mwisho umefika.Atakachofanya ni kufanya vita na hawa watu, na kuleta dhiki Israeli, na duniani kote, hiyo ndio ile dhiki kuu,
Ufunuo 11:3 “Nami nitawaruhusu mashahidi wangu wawili, nao watatoa unabii siku elfu na mia mbili na sitini, hali wamevikwa magunia. 4 Hao ndio ile mizeituni miwili na vile vinara viwili visimamavyo mbele za Bwana wa nchi. 5 Na mtu akitaka kuwadhuru, moto hutoka katika vinywa vyao na kuwala adui zao. Na mtu akitaka kuwadhuru, hivyo ndivyo impasavyo kuuawa. 6 Hao wana amri ya kuzifunga mbingu, ili mvua isinyeshe katika siku za unabii wao. Nao wana amri juu ya maji kuyageuza kuwa damu, na kuipiga nchi kwa kila pigo, kila watakapo. 7 Hata watakapoumaliza ushuhuda wao, yule mnyama atokaye katika kuzimu atafanya vita nao, naye atawashinda na kuwaua”.
Ufunuo 11:3 “Nami nitawaruhusu mashahidi wangu wawili, nao watatoa unabii siku elfu na mia mbili na sitini, hali wamevikwa magunia.
4 Hao ndio ile mizeituni miwili na vile vinara viwili visimamavyo mbele za Bwana wa nchi.
5 Na mtu akitaka kuwadhuru, moto hutoka katika vinywa vyao na kuwala adui zao. Na mtu akitaka kuwadhuru, hivyo ndivyo impasavyo kuuawa.
6 Hao wana amri ya kuzifunga mbingu, ili mvua isinyeshe katika siku za unabii wao. Nao wana amri juu ya maji kuyageuza kuwa damu, na kuipiga nchi kwa kila pigo, kila watakapo.
7 Hata watakapoumaliza ushuhuda wao, yule mnyama atokaye katika kuzimu atafanya vita nao, naye atawashinda na kuwaua”.
Lakini kabla hajafanikiwa, lipo kundi dogo ambalo litasikia injili ya wale mashahidi wawili, na kuondoshwa na kwenda kufichwa, ndio wale wayahudi 144,000, hao watafichwa na dhiki kuu haitawapata (Ufunuo 7&11).
Ufunuo 12:13 “Na joka yule alipoona ya kuwa ametupwa katika nchi, alimwudhi mwanamke yule aliyemzaa mtoto mwanamume. 14 Mwanamke yule akapewa mabawa mawili ya tai yule mkubwa, ili aruke, aende zake nyikani hata mahali pake, hapo alishwapo kwa wakati na nyakati na nusu ya wakati, mbali na nyoka huyo. 15 Nyoka akatoa katika kinywa chake, nyuma ya huyo mwanamke, maji kama mto, amfanye kuchukuliwa na mto ule. 16 Nchi ikamsaidia mwanamke; nchi ikafunua kinywa chake, ikaumeza mto ule alioutoa yule joka katika kinywa chake. 17 Joka akamkasirikia yule mwanamke, akaenda zake afanye vita juu ya wazao wake waliosalia, wazishikao amri za Mungu, na kuwa na ushuhuda wa Yesu; naye akasimama juu ya mchanga wa bahari”.
Ufunuo 12:13 “Na joka yule alipoona ya kuwa ametupwa katika nchi, alimwudhi mwanamke yule aliyemzaa mtoto mwanamume.
14 Mwanamke yule akapewa mabawa mawili ya tai yule mkubwa, ili aruke, aende zake nyikani hata mahali pake, hapo alishwapo kwa wakati na nyakati na nusu ya wakati, mbali na nyoka huyo.
15 Nyoka akatoa katika kinywa chake, nyuma ya huyo mwanamke, maji kama mto, amfanye kuchukuliwa na mto ule.
16 Nchi ikamsaidia mwanamke; nchi ikafunua kinywa chake, ikaumeza mto ule alioutoa yule joka katika kinywa chake.
17 Joka akamkasirikia yule mwanamke, akaenda zake afanye vita juu ya wazao wake waliosalia, wazishikao amri za Mungu, na kuwa na ushuhuda wa Yesu; naye akasimama juu ya mchanga wa bahari”.
Unaona, Lakini wayahudi wengine wote, waliosalia duniani, pamoja na wale watu ambao hawakuipokea chapa ya mnyama, Watapitia dhiki kubwa isiyokuwa na mfano tangu dunia kuumbwa.
Injili inayohubiriwa sasa hivi haiwezi kutikisa au kuleta matatizo duniani, ila kipindi cha injili za hawa manabii wawili watakaposimama, na kutoa unabii pale Israeli, na kwa yale mapigo yaliyoorodheshwa pale ndipo ulimwengu utakapojua rangi halisi ya mpinga-Kristo.
Hawa watu pengine tayari wapo duniani, kwasababu dalili zote zinaonyesha.. Lakini mpaka hayo yote yatokee sisi tuliookoka ambao tumejiweka tayari, tutakuwa siku nyingi tumeshakwenda utukufuni (kanisa halitashuhudia mambo hayo ya manabii wawili). Jiulize na wewe ndugu ikiwa unyakuo utapita leo, wewe utakuwa wapi? Utajisikiaje kuona wenzako wapo mbinguni, wanaona vitu ambavyo jicho halijawahi kuona, na wewe bado upo hapa duniani, kwenye dhiki za mpinga-Kristo, ukizingatia ulihubiriwa injili mara nyingi na hukutaka kusikia?..
Je! bado unadanganywa na manabii wa uongo? Je bado, unapumbazwa na ulimwengu huu unaopita, Je! bado unasita sita kwenye mawazo mawili. Tubu kama bado hujafanya hivyo, ukabatizwe, dunia hii ipo ukingoni. Hatuna muda mrefu sana.?.
Neno I.N.R.I kwenye msalaba wa Yesu maana yake ni nini?
VITA VYA KIFIKRA BAADA YA KUZALIWA MARA YA PILI
USHIRIKINA NA MADHARA YAKE.
AMEFANYIKA BORA KUPITA MALAIKA!
Biblia inamaana gani kusema;aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi?