SWALI: Je Mungu anawapenda watu wote?..Kama ndivyo kwanini alisema mahali Fulani kwamba anamchukia Esau. (Warumi 9:13)
JIBU: Tusome,
Warumi 9:13 “Kama ilivyoandikwa, Nimempenda Yakobo, bali Esau nimemchukia”.
Chuki inayozungumziwa hapo sio chuki ya kinyongo, kama sisi wanadamu tulizonazo…Sisi wanadamu tukimchukia mtu “tunatamani hata Yule mtu afe au apate madhara Fulani mabaya”…Chuki ya namna hii ni mbaya sana na inatoka kwa Yule mwovu.
Lakini chuki inayozungumziwa hapo katika Warumi 9:23 ni chuki ya “kutopendezwa na mtu”…Mungu wetu anawapenda watu wote lakini hapendezwi na watu wote. Hivyo andiko hilo sio la kulitafsiri kibinadamu au kimitazamo yetu ya kibinadamu…Tukilitafsiri kwa njia hiyo basi tutashindwa kumwelewa Mungu vizuri.. “kila mahali utaona kama biblia inajichanganya”
Mstari mwingine tena ambao unazungumzia chuki ambayo usipotafsirika vizuri ni rahisi kupoteza maana kabisa ni huu..
Luka 14:25 “Makutano mengi walipokuwa wakifuatana naye, aligeuka, akawaambia, 26 Kama mtu akija kwangu naye HAMCHUKII baba yake, na mama yake, na mke wake, na wanawe, na ndugu zake waume na wake; naam, na hata nafsi yake mwenyewe, hawezi kuwa mwanafunzi wangu. 27 Mtu ye yote asiyeuchukua msalaba wake na kuja nyuma yangu, hawezi kuwa mwanafunzi wangu”.
Luka 14:25 “Makutano mengi walipokuwa wakifuatana naye, aligeuka, akawaambia,
26 Kama mtu akija kwangu naye HAMCHUKII baba yake, na mama yake, na mke wake, na wanawe, na ndugu zake waume na wake; naam, na hata nafsi yake mwenyewe, hawezi kuwa mwanafunzi wangu.
27 Mtu ye yote asiyeuchukua msalaba wake na kuja nyuma yangu, hawezi kuwa mwanafunzi wangu”.
Umeona hapo?…haimaanishi kwamba tuwachukie wazazi wetu na ndugu zetu, tusiwapende kabisa, kiasi kwamba hata tuwafanya kuwa maadui zetu ndio iwe tiketi ya sisi kumfuata Yesu na kukubaliwa na yeye…Hiyo sio tafsiri yake…bali tafsiri ya chuki inayozungumziwa hapo ni kitendo cha kuyakataa mapenzi ya ndugu zetu yanayokinzana na mapenzi ya Mungu, na kuchagua kufuata mapenzi ya Mungu zaidi ya mapenzi yao.
Kwamfano Baba/mama/ndugu anakwambia twende kwa mganga…ilihali wewe ni mkristo na unajua hayo sio mapenzi ya Mungu, hapo huna budi kuyakataa maamuzi yao na kufuata mapenzi ya Mungu…sasa kile kitendo cha wewe kuyakataa matakwa yao na kufuata matakwa ya Mungu…Mbingu inatafsiri kama “umemchukia Baba yako/Ndugu yako na umempenda Mungu”. Ingawa wewe upendo wa ndugu zako upo pale pale, unawaombea, unawahurumia, unawaheshimu na kuwajali na kuwatunza.
Ndivyo hivyo hivyo kwa Esau, Mungu hakumchukia kwa chuki za kibinadamu, kwamba hataki kumwona mbele zake, kwamba ni adui yake, na hata hataki kumweka akilini mwake…hapana! bali alimaanisha “hakupendezwa naye kwa matendo yake kama alivyopendezwa na Yakobo”.
Hivyo na sisi hatuna budi kumpendeza Mungu kila siku katika maisha yetu…ili yasitupate kama yaliyompata Esau.
Maran atha.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
Je! Hamna nyumba za kulia na KUNYWEA?.Mstari huu unahalalisha unywaji wa pombe?
WAKATI ULIOKUBALIKA NDIO SASA.
JE! PAKA KULIA USIKU NI ISHARA YA UCHAWI?
MWISHO WA DUNIA UTAKUJAJE?
Rudi Nyumbani:
Print this post
Kuna mambo ambayo Mungu anaweza kukuagiza ufanye, ukayaona kama hayana maana yoyote rohoni,ukayapuuzia tu na ukaendelea na shughuli zako kama kawaida, hata ukawa unaendelea kumtumikia Mungu, lakini hujui kuwa machoni pa Mungu ukaoekana kuwa si kitu.
Kwa mfano tukirudi kwenye maandiko, utaona kuna wakati mtume Paulo, alipokea kweli ufunuo wa Roho Mtakatifu kuwa tohara ya mwilini hamfikishi myahudi popote, awe ametahiriwa awe hajatahiriwa kama mtu huyo haishiki torati basi ni sawa na kazi bure tu.(Warumi 2:25-29)
Lakini utaona anasema tena, tohara ni muhimu kwao kwa kila njia, ikimaanisha kuwa sio jambo la wao kulipuuzia hata kidogo, Soma..
Warumi 3:1 “Basi Myahudi ana ziada gani? Na kutahiriwa kwafaa nini? 2 Kwafaa sana kwa kila njia. Kwanza kwa kuwa wamekabidhiwa mausia ya Mungu”.
Warumi 3:1 “Basi Myahudi ana ziada gani? Na kutahiriwa kwafaa nini?
2 Kwafaa sana kwa kila njia. Kwanza kwa kuwa wamekabidhiwa mausia ya Mungu”.
Unaona, japokuwa aliwahubiria wayahudi kuwa tohara ya mwilini haiwezi kuondoa dhambi zao, lakini aliwahimiza watahiriwe wote, kwasababu lilikuwa tayari ni agizo la Mungu.
Sasa hilo lilikuwa ni agizo kwa wayahudi..
Vipi kuhusu sisi wakristo, ambao sheria yetu ililetwa na Bwana wetu YESU KRISTO?.
Yeye alisema..
Marko 16:16 “Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa”.
Kama tunavyosoma hapo sio kuamini tu, bali na kubatizwa pia..Lakini cha kushangaza wapo wakristo wanaosema, ubatizo haumpeleki mtu mbinguni, unaweza ukawa umebatizwa na maji hata ya mto Yordani na mbinguni bado usiende, kwasababu maji hayaondoi dhambi za mtu isipokuwa damu ya Yesu …mtu huyo anaendelea kusema kinachojalisha ni kumwamini Yesu tu basi,ukishatubu ndio tayari umeupata wokovu wenyewe..hayo masuala ya kubatizwa, tena kwa kuzamishwa, sio lazima kwa mkristo.. Wewe amini tu inatosha, imani yako ndio itakayokupeleka mbinguni..
Lakini Kristo anataka ufahamu jambo hili, kwamba ubatizo wafaa sana kwa kila njia, na kwanza ni kwasababu yeye ametupa maagizo hayo..hata kama kwetu hayana maana lakini kwake yanayo maana kubwa..
Tukijiona sisi ni wa rohoni sana kuliko yeye mwenyewe aliyetupa maagizo hayo, na kwamba tunajua kumtumikia kuliko kuyafuata maagizo yake.. Basi siku zote tuyakumbuke maneno yake haya aliyoyasema:
Luka 6:46 “Na kwa nini mnaniita, Bwana, Bwana, walakini hamyatendi nisemayo? 47 Kila mtu ajaye kwangu, na kuyasikia maneno yangu na kuyatenda, nitawaonyesha mfano wake. 48 Mfano wake ni mtu ajengaye nyumba, na kuchimba chini sana, na kuweka msingi juu ya mwamba; na kulipokuja gharika, mto uliishukia nyumba ile kwa nguvu, usiweze kuitikisa; kwa kuwa imejengwa vizuri. 49 Lakini yule aliyesikia ila hakutenda, mfano wake ni mtu aliyejenga nyumba juu ya ardhi pasipokuwa na msingi, mto ukaishukia kwa nguvu, ikaanguka mara; na maangamizi yake nyumba ile yakawa makubwa”.
Luka 6:46 “Na kwa nini mnaniita, Bwana, Bwana, walakini hamyatendi nisemayo?
47 Kila mtu ajaye kwangu, na kuyasikia maneno yangu na kuyatenda, nitawaonyesha mfano wake.
48 Mfano wake ni mtu ajengaye nyumba, na kuchimba chini sana, na kuweka msingi juu ya mwamba; na kulipokuja gharika, mto uliishukia nyumba ile kwa nguvu, usiweze kuitikisa; kwa kuwa imejengwa vizuri.
49 Lakini yule aliyesikia ila hakutenda, mfano wake ni mtu aliyejenga nyumba juu ya ardhi pasipokuwa na msingi, mto ukaishukia kwa nguvu, ikaanguka mara; na maangamizi yake nyumba ile yakawa makubwa”.
Sisi tulio na masikio na tusikie maneno ya Bwana na tuyatii.Kumbuka Neno ubatizo tafsiri yake ni kuzamwishwa/kuzikwa, hivyo unapofikiria kwenda kubatizwa maana yake ni kuwa unakwenda kuzamishwa katika maji, mwili wote unapotelea majini, na sio kunyunyiziwa,.Na ndio hapo suala la maji mengi/ maji tele linakuja sawasawa na (Yohana 3:23). Na hiyo inaweza ikafanyika popote pale aidha mtoni, au bwawani, au baharini, au kwenye kisima kilichochimbwa, au popote pale maadamu tendo hilo liwe ni la kuzamwishwa mwili wote majini.
Vilevile ubatizwe uwe ni kwa jina lake yeye aliyekuagiza yaani YESU KRISTO anayeweza kuzifuta dhambi zetu sawasawa na (Matendo 3:38,8:16,10:48, 19:5)..Ukikamilisha hayo maagizo ipasavyo basi ujue kuwa wokovu wako ni thabiti, Na kama ingekuwa ni kupewa cheti cha kimwili basi mbingu ingekupa. Hivyo kama hujawahi kubatizwa kabisa au ulibatizwa isivyopaswa, basi wakati ndio huu kwako kwenda kufanya hivyo.
Na Bwana akubariki.
MITHALI AU METHALI ZA BIBLIA
UTASIMAMA PEKE YAKO SIKU ILE.
RAFIKI MWEMA.
Je! Ni halali kuoa/kuolewa na mtu ambaye tayari anao watoto?
Israeli ipo Bara la Asia, katika ukanda wa Asia Magharibi (au ukanda wa Mashariki ya kati). tofuati na inavyodhaniwa na baadhi ya watu kuwa Israeli ipo bara la Ulaya.
Ikumbukwe kuwa Bara la Asia ndio bara lililokubwa kuliko yote duniani, na limegawanyika katika maeneo makuu sita (6),
Kwa maelezo marefu juu ya mataifa hayo unaweza kuyasoma Wikipedia fungua link hii >> https://sw.wikipedia.org/wiki/Asia
Sasa katika huo ukanda wa Asia Magharibi /Asia ya kati ambao ndio unaundwa na nchi kama Jordan, Siria, Lebanoni, Palestina, Saudi Arabia, Oman, Yemen n.k Ndio huko sasa nchi ya Israeli nayo inapatikana.
Hivyo ni vema pia kujua juu ya historia ya muhimu zaidi ihusulo taifa hili,. Kwani huko ndiko alipotokea mkombozi wa huu ulimwenguni, ajulikanaye kama YESU KRISTO wa Nazareti. Ambaye kwa kupitia yeye mimi na wewe tumepokea uzima wa milele bure kama tukimwamini.
Hakuna mwadamu aliyewahi kutokea mwenye malengo, na mkamilifu kama Yesu Kristo..Huyu alitumwa na Mungu mwenyewe ili kuja kutuokosa sisi tulio katika shida na vifungo na mateso ya dhambi.
Na siku akirudi, miguu yake itatua tena kwa mara ya kwanza katika taifa hili hili la Israeli, juu ya milima ujulikanao kama mlima wa mizeituni (Zekaria 14:4), na taifa hili ndilo litakalokuwa makao yake makuu, ambapo atatawala kama BWANA WA MABWANA na MFALME WA WAFALME juu ya dunia nzima katika Yerusalemu yake mpya atakayoifanya.
Wakati huo dunia haitakuwa kama ilivyo sasa, kwani itakuwa imeshatengenezwa na kurudishwa katika katika hali ambayo haielezeki kwa jinsi ya kibinadamu. Tutatawala Pamoja naye kwa muda wa miaka 1000 ni kisha baada ya hapo tutaingia katika umilele.
Kwa maelezo marefu, fungua vichwa vya masomo mengi hapo chini ufahamu kalenda yote ya ki-Mungu kwetu sisi wanadamu duniani..
Shalom.
KWANINI YESU KRISTO ALIKUJA DUNIANI?
UTAWALA WA MIAKA 1000.
MAPIGO YA VITASA SABA, NA SIKU YA BWANA.
UNYAKUO.
CHUKIZO LA UHARIBIFU
Nabii Malaki alikuwa ni nabii kama walivyo manabii wengine katika biblia kama nabii Yeremia, nabii Isaya, nabii Samweli, Nabii Danieli..Biblia haijaeleza maisha yake kama ilivyoelezea kwa baadhi ya manabii wengine kama Samweli, Yeremia na Danieli. Nabii Malaki ni nabii ambaye maisha yake hayapatikani katika vitabu vingine vya biblia. Na ndiye nabii wa mwisho aliyeandika kitabu cha mwisho katika agano la kale. Kitabu cha Malaki kiliandikwa kati ya mwaka 441-400KB. Na kina Sura nne tu, lakini zilizoshiba Jumbe nzito.
Sasa tunaposema ni nabii wa mwisho haimaanishi kwamba hawakutokea manabii wengine baada yake..la!..walitokea wengine waliotumwa na Mungu, katikati ya hicho kipindi cha miaka 400 lakini Bwana Mungu hakuruhusu jumbe zao ziwe miongoni mwa orodha ya vitabu hivyo vya agano la kale. Na kama havijaruhusiwa kuwekwa kwenye orodha na Roho Mtakatifu mwenyewe hatupaswi sisi kuvitafuta na kuvipachika, wala hatupaswi kutafuta majina ya hao manabii ni wakina nani..Tukifanya hivyo tutafungua mlango wa roho ya Ibilisi kutupotosha…Roho Mtakatifu alikuwa na maana yake kubwa kuzuia visiwekwe kwenye orodha.
Hivyo kitabu cha Malaki ndio kitabu cha mwisho katika vitabu vya agano la kale, vingine vinavyochomekwa sasa ni batili.
kitabu cha malaki
Sasa tukirudi kwa huyu Nabii Malaki, ndiye Nabii pekee aliyepewa ufunuo wa kurudi kwa Roho ya Eliya duniani tena….hakuna Nabii mwingine yeyote aliyefunuliwa ufunuo huo zaidi yake yeye,
Malaki 4:5 “Angalieni, nitawapelekea Eliya nabii, kabla haijaja siku ile ya Bwana, iliyo kuu na kuogofya. 6 Naye ataigeuza mioyo ya baba iwaelekee watoto wao, na mioyo ya watoto iwaelekee baba zao, ili nisije nikaipiga dunia kwa laana”.
Malaki 4:5 “Angalieni, nitawapelekea Eliya nabii, kabla haijaja siku ile ya Bwana, iliyo kuu na kuogofya.
6 Naye ataigeuza mioyo ya baba iwaelekee watoto wao, na mioyo ya watoto iwaelekee baba zao, ili nisije nikaipiga dunia kwa laana”.
Na unabii huo wa Ujio wa Eliya, ulikuja kutimia kwa Yohana Mbatizaji .
Mathayo 17:10 “Wanafunzi wake wakamwuliza, wakisema, Basi kwa nini waandishi hunena ya kwamba imempasa Eliya kuja kwanza? 11 Naye akajibu, akawaambia, Kweli Eliya yuaja kwanza, naye atatengeneza yote, 12 ila nawaambia, ya kwamba Eliya amekwisha kuja, wasimtambue, lakini wakamtenda yote waliyotaka. Vivyo hivyo Mwana wa Adamu naye yuaenda kuteswa kwao. 13 Ndipo wale wanafunzi walipofahamu ya kuwa amesema nao habari za Yohana Mbatizaji”.
Mathayo 17:10 “Wanafunzi wake wakamwuliza, wakisema, Basi kwa nini waandishi hunena ya kwamba imempasa Eliya kuja kwanza?
11 Naye akajibu, akawaambia, Kweli Eliya yuaja kwanza, naye atatengeneza yote,
12 ila nawaambia, ya kwamba Eliya amekwisha kuja, wasimtambue, lakini wakamtenda yote waliyotaka. Vivyo hivyo Mwana wa Adamu naye yuaenda kuteswa kwao.
13 Ndipo wale wanafunzi walipofahamu ya kuwa amesema nao habari za Yohana Mbatizaji”.
Nabii Malaki pia kwa ufunuo wa Roho ndiye nabii aliyezungumzia ZAKA kwa kina, Bwana alimfunulia kuwa wote wanaokwepa kulipa zaka, ni kama wezi mbele zake.
Malaki 3:8 “Je! Mwanadamu atamwibia Mungu? Lakini ninyi mnaniibia mimi. Lakini ninyi mwasema, Tumekuibia kwa namna gani? Mmeniibia zaka na dhabihu. 9 Ninyi mmelaaniwa kwa laana; maana mnaniibia mimi, naam, taifa hili lote. 10 Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema Bwana wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la”.
Malaki 3:8 “Je! Mwanadamu atamwibia Mungu? Lakini ninyi mnaniibia mimi. Lakini ninyi mwasema, Tumekuibia kwa namna gani? Mmeniibia zaka na dhabihu.
9 Ninyi mmelaaniwa kwa laana; maana mnaniibia mimi, naam, taifa hili lote.
10 Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema Bwana wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la”.
Nabii Malaki ndiye nabii pekee ambaye alifunuliwa hisia za Mungu kipekee sana tofauti na manabii wengine…Mungu alimfunulia ni vitu gani vinavyomchosha yeye kutoka kwa wanadamu, na vitu vinavyomchukiza ambavyo wengi hawajui kama vinamchukiza Mungu. Kwamfano suala la kuachana, wengi hawajui kwamba linamchukiza Mungu kwa kiwango kikubwa sana…
Malaki 2:16 “Maana mimi nakuchukia kuachana, asema Bwana, Mungu wa Israeli; naye aifunikizaye nguo yake kwa udhalimu namchukia, asema Bwana wa majeshi; basi jihadharini roho zenu, msije mkatenda kwa hiana”.
Na pia kuna mambo tuyafanyayo yanayomchosha Mungu wetu pasipo sisi kujua..
Malaki 2:17 “Mmemchokesha Bwana kwa maneno yenu. Lakini ninyi mwasema, Tumemchokesha kwa maneno gani? Kwa kuwa mwasema, Kila atendaye mabaya ni mwema machoni pa Bwana, naye huwafurahia watu hao, au, Mungu mwenye kuhukumu yuko wapi?”
Na pia Nabii Malaki alionyeshwa kuwa kuna maneno tuyazungumzayo ambayo ni magumu kwa Mungu wetu, ambayo hatupaswi kuyasema…
Malaki 3:13 “Maneno yenu yamekuwa magumu juu yangu, asema Bwana. Lakini ninyi mwasema, Tumesema maneno juu yako kwa namna gani? 14 Mmesema, Kumtumikia Mungu hakuna faida; na, Tumepata faida gani kwa kuyashika maagizo yake, na kwa kwenda kwa huzuni mbele za Bwana wa majeshi? 15 Na sasa twasema ya kwamba wenye kiburi ndio walio heri; naam, watendao uovu ndio wajengwao; naam, wamjaribuo Mungu ndio waponywao. 16 Ndipo wale waliomcha Bwana waliposemezana wao kwa wao. Naye Bwana akasikiliza, akasikia; na kitabu cha ukumbusho kikaandikwa mbele zake, kwa ajili ya hao waliomcha Bwana, na kulitafakari jina lake. 17 Nao watakuwa wangu, asema Bwana wa majeshi, katika siku ile niifanyayo; naam, watakuwa hazina yangu hasa; nami nitawaachilia, kama vile mtu amwachiliavyo mwanawe mwenyewe amtumikiaye”.
Malaki 3:13 “Maneno yenu yamekuwa magumu juu yangu, asema Bwana. Lakini ninyi mwasema, Tumesema maneno juu yako kwa namna gani?
14 Mmesema, Kumtumikia Mungu hakuna faida; na, Tumepata faida gani kwa kuyashika maagizo yake, na kwa kwenda kwa huzuni mbele za Bwana wa majeshi?
15 Na sasa twasema ya kwamba wenye kiburi ndio walio heri; naam, watendao uovu ndio wajengwao; naam, wamjaribuo Mungu ndio waponywao.
16 Ndipo wale waliomcha Bwana waliposemezana wao kwa wao. Naye Bwana akasikiliza, akasikia; na kitabu cha ukumbusho kikaandikwa mbele zake, kwa ajili ya hao waliomcha Bwana, na kulitafakari jina lake.
17 Nao watakuwa wangu, asema Bwana wa majeshi, katika siku ile niifanyayo; naam, watakuwa hazina yangu hasa; nami nitawaachilia, kama vile mtu amwachiliavyo mwanawe mwenyewe amtumikiaye”.
Hivyo Neno la Mungu ni taa..kuna mambo mengi ya kujifunza katika kitabu cha Malaki, hayo ni baadhi tu machache…lakini kila mmoja wetu akitenga muda kukisoma, huku akimruhusu Roho Mtakatifu awe mwalimu wake, yapo makubwa ya kunufaika na ya kulinufaisha kanisa la Kristo, Bwana atusaidie katika kulisoma Neno lake na kulitendea kazi.
Malaki 1
Maran atha!
JE! ULEVI NI DHAMBI?.
VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 7 (Yeremia na Maombolezo)
Biblia ni nini?
WhatsApp
“Mithali” na “Methali” ni neno lenye maana moja.. ambalo maana yake ni kipande cha sentensi chenye kubeba ujumbe halisi wa kimaisha…Methali/Mithali zinaweza kuwa ni sentensi zenye ujumbe wa wazi au zenye ujumbe wa fumbo.
Kwa mfano methali inayosema “akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki wa kweli” hii ni methali iliyo wazi kabisa yenye ujumbe wa kwamba…mtu Yule ambaye wakati wa dhiki yupo na wewe huyo ndiye rafiki wa kweli tofauti na Yule ambaye wakati wa dhiki anakukimbia lakini wakati wa raha ndio anakukaribia.
Lakini pia kuna mithali kama “mtaka cha uvunguni sharti ainame” methali hii inahitaji kutafakari sana ndipo upate ujumbe… “Kwamba ili upate jambo Fulani huna budi kuingia gharama” Na nyingine zote ni hivyo hivyo.
Sasa katika biblia pia zipo methali/Mithali…Mithali hizi Roho Mtakatifu karuhusu ziandikwe na wenye hekima ili ziwape hekima watoto wa Mungu.
Katika biblia tunamsoma mtu mmoja anayeitwa Sulemani, ambaye alimwomba Mungu Hekima badala ya Mali, na hivyo Mungu alimpa hekima nyingi sana, mpaka wafalme na mamalkia wa dunia wakawa wanamwendea kusikiliza hekima zake. Na nyingi ya hekima alizojaliwa aliziandika kwa mfumo huo wa Methali na nyimbo.
1Wafalme4: 29 “Mungu akampa Sulemani hekima, na akili nyingi sana, na moyo mkuu, kama mchanga ulioko pwani. 30 Hekima ya Sulemani ikapita hekima ya wana wote wa mashariki, na hekima zote za Misri. 31 Kwa kuwa alikuwa na hekima kuliko watu wote; kuliko Ethani Mwezrahi, na Hemani, na Kalkoli, na Darda, wana wa Maholi; zikaenea sifa zake kati ya mataifa yote yaliyozunguka. 32 NAYE AKANENA MIFANO ELFU TATU, NA NYIMBO ZAKE ZILIKUWA ELFU MOJA NA TANO. 33 Akanena habari za miti tangu mwerezi ulioko Lebanoni hata hisopo umeao ukutani; pia akanena habari za wanyama, na za ndege, na vitambaavyo, na samaki. 34 Wakaja wa mataifa yote ili waisikie hekima ya Sulemani, toka wafalme wote wa ulimwengu, waliokuwa wamepata habari za hekima yake”.
1Wafalme4: 29 “Mungu akampa Sulemani hekima, na akili nyingi sana, na moyo mkuu, kama mchanga ulioko pwani.
30 Hekima ya Sulemani ikapita hekima ya wana wote wa mashariki, na hekima zote za Misri.
31 Kwa kuwa alikuwa na hekima kuliko watu wote; kuliko Ethani Mwezrahi, na Hemani, na Kalkoli, na Darda, wana wa Maholi; zikaenea sifa zake kati ya mataifa yote yaliyozunguka.
32 NAYE AKANENA MIFANO ELFU TATU, NA NYIMBO ZAKE ZILIKUWA ELFU MOJA NA TANO.
33 Akanena habari za miti tangu mwerezi ulioko Lebanoni hata hisopo umeao ukutani; pia akanena habari za wanyama, na za ndege, na vitambaavyo, na samaki.
34 Wakaja wa mataifa yote ili waisikie hekima ya Sulemani, toka wafalme wote wa ulimwengu, waliokuwa wamepata habari za hekima yake”.
Kwahiyo biblia ni kitabu kilichojitosheleza..asilimia 100, kina faraja, kina wasaa, kina elimu, kina Mithali, na hekima na maarifa. Kama mtu mmoja alivyowahi kusema “kama nikipatiwa biblia na mshumaa katika chumba chenye giza, basi nitaweza kukuelezea kila kitu kinachoendelea katika dunia”. Na hiyo ni kweli kabisa..
Sasa hebu tusikilize baadhi ya Mithali za biblia, kama methali tu methali ya kidunia inayosema “akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki wa kweli” inaweza kutusaidia kutambua marafiki wa kweli, basi biblia ni dhahiri kuwa ina mithali nyingi zinazofanana na hizo ambazo zimejaa hekima kuliko mithali hizi zetu za kidunia..
Mithali juu ya wanaokuchukia/kukuwazia mabaya:
Mithali 24: 17 “Usifurahi, adui yako aangukapo; Wala moyo wako usishangilie ajikwaapo; 18 Bwana asije akaliona hilo, likamkasirisha; Akageuzia mbali naye hasira yake. 19 Usikasirike kwa sababu ya watenda mabaya; Wala usiwahusudu wabaya; 20 Kwa maana mtu mbaya hapati thawabu; Taa ya mtu mbaya itazimika”.
Mithali 24: 17 “Usifurahi, adui yako aangukapo; Wala moyo wako usishangilie ajikwaapo;
18 Bwana asije akaliona hilo, likamkasirisha; Akageuzia mbali naye hasira yake.
19 Usikasirike kwa sababu ya watenda mabaya; Wala usiwahusudu wabaya;
20 Kwa maana mtu mbaya hapati thawabu; Taa ya mtu mbaya itazimika”.
Hiyo ni Methali ya maisha, kamwe usifurahi…adui yako anapopatwa na mabaya!..bali uhuzunike!, na kumhurumia na Bwana atakuongezea amani na furaha, na kukupenda!…
Na mithali nyingine ni hii..
Mithali 25: 21 “Adui yako akiwa ana njaa, mpe chakula; Tena akiwa ana kiu, mpe maji ya kunywa; 22 Maana utatia makaa ya moto kichwani pake; Na Bwana atakupa thawabu”.
Mithali 25: 21 “Adui yako akiwa ana njaa, mpe chakula; Tena akiwa ana kiu, mpe maji ya kunywa;
22 Maana utatia makaa ya moto kichwani pake; Na Bwana atakupa thawabu”.
Mithali ya Njia unayoiendea:
Mithali 14: 12 “Iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu, Lakini mwisho wake ni njia za mauti”.
Maana yake ni kwamba kuwa makini na ile njia ambayo unaweza kuiona ni sawa machoni pako…. “chunguza sana njia zako, hususani zile unazoziona zipo sawa, nyingi zinaishia upotevuni”. Njia zinazofuatwa na watu wengi zinaishia upotevuni.
Zipo methali nyingi sana katika kitabu cha Mithali, Mhubiri, Zaburi na Ayubu, hatuwezi kuziandika zote hapa, lakini hizi chache ni ili kukukumbusha wewe ndugu kwamba Biblia ni neno la Mungu lililojitosheleza… anza kutenga muda kusoma biblia, kuna mambo mengi ambayo ulikuwa huyajui utayajua, kuna hekima nyingi ambazo zitakufumbua macho katika hali unayopitia sasa…Mambo ambayo ulikuwa huna majibu nayo, basi utayapata ndani ya biblia.
Anza leo kusoma vitabu hivyo vya mithali na vingine vyote, na Bwana atakuwa na wewe, zipo ambazo zina ujumbe wa wazi na zipo zenye ujumbe wa mafumbo, zenye ujumbe wa kimafumbo, yupo Roho Mtakatifu kutusaidia kuyafumbua mafumbo hayo.
Ubarikiwe.
RAFIKI WA KWELI NI YUPI?
https://wingulamashahidi.org/2020/07/03/kutomzuia-kutombana-mtoto-wako-ni-dhambi/
IKIMBIE DHAMBI KWA GHARAMA ZOZOTE ZILE!
Je! Bwana Yesu alibatiza akiwa hapa duniani?
JIBU: Moja ya vitu vilivyokuwepo ndani ya hekalu la Mungu, ni kinara cha Taa, vingine vilivyokuwepo ni sanduku la agano, madhabahu ya dhahabu ya kuvukizia uvumba, na sanduku la agano.
Sasa kama tunavyojua nyumba ikijengwa na kisha haina chanzo cha Nuru ndani yake, nyumba hiyo bado haijakamilika…Hiyo ndio maana kila nyumba ikijengwa ni lazima iwekwe na mfumo wa taa ili kwamba wakati wa usiku ndani kusiwe giza shughuli zikakwama…
Na ndani ya Hema lililotengenezwa na Musa, Bwana aliagiza kuwepo na chanzo cha mwanga ndani ya lile hema, ili shughuli za kikuhani ziweze kufanyika, kama kuvukiza uvumba na kuhani mkuu kuweza kufanya upatanisho (Hivyo Bwana aliagiza pawepo kinara cha taa chenye matawi saba)….
Hali kadhalika mpaka wakati wa hekalu lilipokuja kujengwa na Sulemani jambo ni lile lile, nyumba ya Mungu haiwezi kuwa giza ndani ni lazima kuwepo na Nuru…na kwasababu nyumba ile Sulemani aliyoijenga ilikuwa ni kubwa kuliko hema la Musa, ilihitajika vinara vingi zaidi kule ndani ili pawe na mwanga wa kutosha…Hivyo vikaongezeka kutoka kinara kimoja na kuwa vinara 10…Na kila kinara kilikuwa na taa 7…Hivyo kwa ujumla ndani tu ya ile nyumba kulikuwa na taa 70..(Hivyo kulikuwa na mwanga wa kutosha).
Sasa biblia inasema sisi ni NURU ya Ulimwengu…Maana yake ni kwamba wakristo wa kweli au kanisa la Kristo linafananisha na Taa. Maana yake linamulika na kuangaza kote kote..
Mathayo 5: 14 “Ninyi ni nuru ya ulimwengu. Mji hauwezi kusitirika ukiwa juu ya mlima. 15 Wala watu hawawashi taa na kuiweka chini ya pishi, bali juu ya kiango; nayo yawaangaza wote waliomo nyumbani. 16 Vivyo hivyo nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni”.
Mathayo 5: 14 “Ninyi ni nuru ya ulimwengu. Mji hauwezi kusitirika ukiwa juu ya mlima.
15 Wala watu hawawashi taa na kuiweka chini ya pishi, bali juu ya kiango; nayo yawaangaza wote waliomo nyumbani.
16 Vivyo hivyo nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni”.
Hivyo basi kanisa la Kristo ndilo linalofananishwa na “kile kinara cha taa ndani ya Nyumba ya Mungu” Siri hiyo haikujulikana tangu zamani mpaka wakati Bwana Yesu alipokuja kuifichua siri hiyo tukisoma katika..
Ufunuo 1:20 “Siri ya zile nyota saba ulizoziona katika mkono wangu wa kuume, na ya vile vinara saba vya dhahabu. Zile nyota saba ni malaika wa yale makanisa saba; na vile VINARA SABA NI MAKANISA SABA”.
Unaona? Na kama ukifuatilia kwa makini maagizo Musa aliyopewa kuhusu kile kinara cha taa ni kwamba…kinapaswa kiwake daima!…(hakuna siku kinapaswa kiwe kimezima kwa kuishiwa mafuta), hivyo hilo lilikuwa ni agizo la Mungu kwahiyo wana wa Israeli walikuwa wanahakikisha kuwa hakizimi kwa gharama zozote zile…hivyo kwa mamia ya miaka viliendelea kuwaka tu hivyo hivyo…hakuna siku kilizima, wakati wa Mfalme Sulemani.
Na sisi hatupaswi Nuru yetu izime kama biblia inavyosema hapo katika Mathayo 5:16, Na nuru yetu ni matendo yetu..Yanapaswe yawe yanaangaza muda wote..Na tunapaswa tutoe mwanga mweupe na si mwekundu wala wa blue…tunapokuwa wauaji, wazinzi, watukanaji na bado tujajiita wakristo hapo ni tonatoa mianga ya rangi nyingine…
Bwana atubariki na atujalie Neema yake siku zote.
FAHAMU JINSI KRISTO ANAVYOPONYA WATU ROHO.
UUMBAJI BORA WA MUNGU, UPO NDANI YA MWANADAMU.
IMANI NI KUWA NA UHAKIKA WA MAMBO YATARAJIWAYO.
Je kupiga miayo ni ishara ya mapepo?
MJUMBE WA AGANO.
WANA JUHUDI KWA AJILI YA MUNGU, LAKINI SI KATIKA MAARIFA.
Ni kwanini wakati mwingine tunaona kama kuna mambo hayaendi sawa katika kanisa la Kristo, kwasababu tunafiri mambo yote yanatatuliwa na mchungaji, au mwalimu au mwinjilisti peke yake..
Kila kiungo katika mwili wa Kristo kinayo kazi yake, hivyo kimoja kisipowajibika ipasavyo ni lazima tu mapungufu yataonekana haijalishi vile vingine vitawajibika kiasi gani…
Leo hii utajiuliza ni kwanini wanawake wengi wanayo malezi mabaya ya watoto.. utakuta mwanamke anaye mtoto lakini hana heshima au maadili, au anaye mtoto lakini kichwani pamejaa miziki ya kidunia na wakati huo huo hajui hata mstari mmoja wa biblia..Unadhani hiyo inatokana na nini? Inatokana na mtu mmoja kushindwa kutimiza jukumu lake katika kanisa la Kristo.
Au utakuta mwanamke hamuheshimu mume wake, anajibizana naye kama mtoto, hajui kuwa ni agizo la Mungu kila mke amuheshimu mume wake, kama vile sisi tunavyomuheshimu Kristo na kila mume ampende mke wake, kama vile Kristo anavyotupenda sisi..Lakini yeye hilo si kitu kwake, anaona ni kawaida tu, na bado anafahamika kama mkristo, unadhani kilichomfanya awe na tabia hizo ni nini? ni kwasababu mtu Fulani hakutimiza jukumu lake katika kanisa, alimwachia mchungaji, au mtumishi Fulani afanye yeye kila kitu.
Au kwanini wanawake wengine, hawatulii katika shughuli zao, majumbani mwao, kinyume chake, ni kujizungusha mitaani, kutafuta habari za wengine, wanakosa staha, wanavaa mavazi yasiyo na heshima, nusu uchi wanakatiza barabarani, na bado ni waimba kwaya,…Unadhani hiyo inatokana na nini wakati mwingine? Ni kwasababu mtu Fulani hakutimiza jukumu lake katika mwili wa Kristo..
Paulo alimwandikia Timotheo maneno haya, akamwambia..
Tito 2:3 “Vivyo hivyo na wazee wa kike wawe na mwenendo wa utakatifu; wasiwe wasingiziaji, wasiwe wenye kutumia mvinyo nyingi, bali wafundishao mema;4 ILI WAWATIE WANAWAKE VIJANA AKILI, wawapende waume zao, na kuwapenda watoto wao;5 na kuwa wenye kiasi, kuwa safi, kufanya kazi nyumbani mwao, kuwa wema, kuwatii waume zao wenyewe; ili neno la Mungu lisitukanwe”.
Tito 2:3 “Vivyo hivyo na wazee wa kike wawe na mwenendo wa utakatifu; wasiwe wasingiziaji, wasiwe wenye kutumia mvinyo nyingi, bali wafundishao mema;
4 ILI WAWATIE WANAWAKE VIJANA AKILI, wawapende waume zao, na kuwapenda watoto wao;
5 na kuwa wenye kiasi, kuwa safi, kufanya kazi nyumbani mwao, kuwa wema, kuwatii waume zao wenyewe; ili neno la Mungu lisitukanwe”.
Unaona hapo biblia inaeleza wazi kabisa huduma ya mwanamke mzee ni ipi kanisani…Kumbuka mwanamke mzee sio lazima awe ni mzee kikongwe, lakini walau mwanamke ambaye ameshafikia umri wa makamo, ameshapitia mambo mengi hususani katika ndoa, anajua jinsi gani ya kuishi na mume katika Kristo..
Ikiwa wewe ni mmojawapo na upo katika kanisa, basi fahamu kuwa unalo jukumu zito la kuwasimamia ipasavyo wanawake vijana, ukijionyesha kwanza wewe mwenyewe kama kielelezo, kwa mwenendo wako wa utakatifu na tabia. Kisha ndio uwafundishe na kuwasimamia mabinti, na wanawake vijana jinsi ya kuishi kama mwanamke wa Kikristo..
Vinginevyo usipofanya hivyo, ujue kuwa jina la Mungu linatukanwa kwa ajili yako.
Hi ni huduma kubwa sana katika kanisa, lakini cha kushangaza ni kwamba mwanamke huyu huyu mzee na yeye anataka awe mchungaji kwasababu anaona huduma aliyopewa kama vile ni ndogo haijulikani.. Hafahamu kuwa hata katika kanisa wanawake huwa ndio wengi kuliko wanaume, hivyo kama huduma basi yeye ndio mwenye huduma kubwa ya kuwaangalia watu kuliko mwanaume, lakini hilo halitaki, anataka yeye naye asimame mimbarani, ahubiri kama askofu mkuu Fulani, au mwalimu Fulani au nabii fulani..Na matokeo yake ndio unakuta migogoro mingi ya kifamilia mara mwanaume huyu kagombana na mkewe kwasababu hamuheshimu mara Yule kapigwa na memewe n.k..mwisho wa siku jina la Mungu linatukanwa kwasababu tu kiungo Fulani kanisani kilishindwa kutimiza kusudi lake.
Ikiwa wewe ni mama, leo hii tambua jukumu lako. Na ufahamu kuwa Kristo anaiheshimu sana huduma yako kama tu anavyoliheshimu lile la mchungaji, na askofu…na kama utafanya vizuri ina thawabu kuliko hata hizo zinazoonekana ni kubwa kuliko nyingine.
Bwana akubariki.
Shalom
NAFASI YA MWANAMKE KATIKA KANISA
JE NI DHAMBI KUWA NA MAHUSIANO KABLA YA NDOA?
MAMBO YA KUJIFUNZA KATIKA WARAKA WA PILI WA YOHANA.
TUJIFUNZE JAMBO KWA WANAWAKE HAWA WAWILI.
USHAURI KWA MWANAMKE WA KIKRISTO.
Shalom, karibu tujifunze Biblia…
Nimewahi kukutana na watu kadha wa kadha ambao ukijaribu kuwaeleza tu habari za msalaba na wokovu ulioletwa na mwokozi wetu Yesu Kristo, wanasema Bwana Yesu alikuwa ni mzungu, hivyo hawawezi kumfuata mzungu, wala dini iliyoletwa na wazungu…Huko ni kutawaliwa na wazungu na wanahitimisha kwa kusema kwanini sisi waafrika tusidumishe Imani zetu, kwanini mpaka tuige vitu tulivyoletewa na wazungu? Kwanini tusifuate vya kwetu, huo ni ukoloni mamboleo?..kwanini hatujikubali?.
Hii ni hoja kubwa sana ambayo inawasumbua watu wengi….. na inatokana na kutojiamini na uchungu moyoni…Sasa kabla ya kwenda kwenye swali letu la msingi hapo juu linalouliza “Je Bwana Yesu alikuwa ni mzungu au la!” hebu tutafakari kwanza vipengele vifuatavyo.
Mtu unayehoji kwamba “hatupaswi kufuata kitu chochote cha mzungu” bali tudumishe vya kwetu…basi anapaswa akatae vyote vilivyoletwa na watu hao pia wa magharibi bila kuacha hata kimoja…ikiwemo simu anayoitumia, asiitumie tena, nguo anazovaa asizivae tena (kwasababu hata nguo anazovaa zimetengenezwa na viwanda vya hao hao anaowaita wazungu)..hivyo anapaswa aendelee kuvaa mavazi yake ya asili waliokuwa wanavaa waafrika wa zamani kama ni Kamba au makuti au nyuzinyuzi.
Hali kadhalika hapaswi kuishi kwenye nyumba za kisasa zenye umeme, kwasababu hata huo mfumo wa ujenzi ni kutoka kwa hao hao anaowaita wazungu na umeme pia, hapaswi kutumia dawa ya meno, pasi, hatakiwi kutumia hata trekta kulimia, hapaswi pia kuangalia wala kutumia TV, hapaswi pia kutumia jiko la gesi, wala sufuria,wala hapaswi kumiliki gari wala chombo chochote cha usafiri wa moto kwasababu vyote vimeletwa na hao hao anaowaita wazungu, akitaka kusafiri kutoka mji mmoja kwenda mwingine hana budi kutumia punda…na pia hapaswi kwenda hospitali yoyote wala kutumia aina yoyote ya matibabu ya kisasa na mwisho hapaswi kupeleka Watoto wake shule….Kama hivyo vyote atakuwa amefanikiwa kuacha kuvitumia basi atakuwa sio mnafiki kuikataa pia na Imani iliyoletwa na wazungu…lakini kama hawezi kuacha hivyo vyote na anavipenda basi atakuwa ni MNAFIKI kuchukia Imani ambayo imeletwa na hao anaowaita Wazungu, kwa kisingizio kwamba imeletwa na watu weupe!.
Sasa baada ya kutafakari hayo twende mbele Zaidi….
Ni ukweli usiopingika kwamba Imani ya Kikristo iliingia barani Afrika kupitia Wamisionari waliotoka nchi za Ulaya…Hao wamisionari hawakuwa waafrika bali walikuwa watu weupe (wazungu)….kwa njia yeyote ile waliyokuja nayo huku, lakini mwisho tunajua kuwa ilikuwa ni mpango wa Mungu wao kufika huku kuleta Habari za Mwokozi.
Sasa swali la msingi la kujiuliza ni kwamba hawa Wazungu/wamisionari je waliitolea wapi Imani ya Kikristo?…Kama unasoma biblia utakuwa unalo jibu tayari kwamba Imani ya kikristo chanzo chake ni Taifa la Israeli. Taifa la Israeli ndio taifa pekee ambalo Mungu alilichagua liwe mwanzo wa kupitisha kusudi lake hapa duniani… Hivyo hilo pekee ndio lilikuwa taifa teule la Mungu…na mataifa mengine yaliyosalia duniani yaliitwa “MATAIFA”….sasa hili neno “mataifa” ni neno la ki-ujumla ambalo lilikuwa linawakilisha makundi ya nchi zote ulimwenguni mbali na Israeli ambazo hazikuwa zinamwabudu Mungu mmoja wa mbingu na nchi (Yehova)…Ni Taifa moja tu pekee ambalo ndilo lililokuwa linamwabudu Mungu wa mbingu na nchi kulingana na jinsi yeye anataka!…na hilo si lingine Zaidi ya Taifa la Israeli.
Na waisraeli hawakuwa wazungu!…walikuwa ni watu wanaokaribia kufanana sana na “waarabu”.. Hivyo kama wewe unajua vyema jamii za watu unaweza kujua tofauti ya mzungu na mwarabu kimwonekano, hawafanani, na hata waarabu si weupe kama wazungu! Na hawana macho ya blue kama wazungu!, na nywele zao ni nyuesi na si za gold kama za wazungu!….
Sasa mwokozi wetu Yesu Kristo ndiko alikozaliwa (yaani huko Israeli) hivyo kwa mwonekano alikuwa anafanana na hawa wa Israeli…Na waisraeli hawakuwa watu hodari wa kimaendeleo wakati wa mwokozi kuishi ulimwenguni..ndio maana utaona wakati Kristo akiwa duniani, Warumi(ambao sasa ndio walikuwa wazungu) walikuwa waitawala Israeli. Na Mungu aliwafanya Israeli kuwa wadogo mpaka kufikia hatua ya kutawaliwa, kutoka na makosa yao waliomuasi. Hivyo hawakuwa na maendeleo yoyote ya kushangaza ukilinganisha na mataifa mengine ya kizungu kama Rumi na Ugiriki(Uyunani).
Sasa tukirudi kwenye swali letu.. “je Bwana Yesu alikuwa ni mzungu?”..Jibu utakuwa umelipata kulingana na maelezo hayo hapo juu….hakuwa mzungu bali mtu wa Taifa la Israeli..Waliokuwa wazungu ni wakina Pilato, Herode ambao ndio walikuwa Warumi.
Kwahiyo kimwonekano Kristo hakuonekana kama Mzungu bali kama Mwisraeli…..
Sasa hawa wazungu ilitokeaje wakamwamini Bwana Yesu ambaye hakuwa mzungu?…Habari hizo unaweza kuzipata katika historia, lakini kwaufupi ni kwamba nao pia walipelekewa habari za Yesu kama sisi tu tulivyoletewa . Wale waliozipokea ipasavyo walijua kabisa kwamba na wao ni watu wa Mataifa ambao hawakustahili kuitwa watu wa Mungu lakini kwa kupitia mkombozi mmoja Yesu Kristo waliingizwa katika neema hiyo..ambayo iliwastahili Waisraeli tu peke yao!.
Hivyo wao nao wakatuletea sisi Injili, kwasababu huku Afrika kulikuwa ni giza nene, watu walikuwa wanaabudu miungu na imani potofu….na katika zama hizi za siku za mwisho, mambo yamebadilika ni wakati wa Afrika sasa nao kuipeleka Injili kwa wazungu kwasababu huko kwao sasa kumeoza, kile kizazi kilichomtumaini Mungu kimeshaondoka kimezuka kizazi cha watu wasiomwogopa Mungu huko kwao ndio kitovu cha watu mashoga, watu wanaokufuru, watu wanaotembea uchi mabarabarani n.k. Hivyo injili inahitajika sana sasa kwa wazungu Zaidi ya kwa waafrika, kama wao walivyotuletea ni wakati sasa wa sisi kuwapelekea wao watubu, wamwamini mwokozi.
Kwahiyo ndugu, kamwe usikae uliingize suala la wokovu wa mwokozi wetu Yesu Kristo na “Rangi” Mungu wa Israeli hana ubaguzi wa rangi na anaabudiwa na watu wa rangi zote…ili awe Mungu wa mbingu na nchi ni lazima apatikane kwa watu wote…Ukiona unamwabudu Mungu anayepatikana Afrika tu, au anayepatikana Ulaya tu!…basi huo ni uthibitisho tosha kwamba huyo sio Mungu wa kweli wa mbingu na nchi..Kwasababu Mungu wa kweli wa dunia yote ni lazima aabudiwe na kutangazwa ulimwenguni kote na watu wa rangi zote!.
Na usisahau jambo hili mwokozi Yesu Kristo, alikufa, akafufuka na akapaa mbinguni na atarudi tena mara ya pili, hivyo kama umeisikia injili na bado hujamwamini, au ulikuwa unafikiri labda ukimwamini utakuwa umetimiza matakwa ya watu weupe, au ni ukoloni!..basi hilo wazo lifute kuanzia leo… hukumu inakuja, hivyo tubu leo kama hujatubu,vilevile ukabatizwe ili dhambi zako ziondolewe na Bwana atakupa kipawa cha Roho wake mtakatifu atakayekusadia kushinda dhambi na kukusaidia kuelewa mambo ambayo ulikuwa huyaelewi kuhusu yeye.
Bwana atubariki.
DHIKI KUU INAKUJA NA UNYAKUO UPO KARIBU.
Je! Ni kweli kuna samaki mtu (Nguva) Baharini.
Tofuati kati ya Myahudi, Mwisraeli na Muebrania ni ipi?
KWA VILE ALIVYOKUWA MTU WA HAKI.
KRISIMASI (CHRISTMAS) NI NINI? JE IPO KATIKA BIBLIA?
Makedonia ni mojawapo ya mataifa tunayoyasoma sana katika biblia, hususani katika ziara za mtume Paulo za kuhubiri injili katika mataifa. Makedonia ni taifa ambao mpaka sasa lipo, na linajulikana kwa jina hilo hilo makedonia (kwa kiingereza Macedonia), taifa hili lipo kusini mashariki mwa bara la Ulaya.
Tunaweza kusoma habari zake, katika biblia na kuona kuwa taifa hili lilikuwa ni miji mikuu mitatu, nayo ni Filipi, Beroya na Thesalonike, ambayo Mtume Paulo aliiendea kuhubiri injili. Kabla ya kupita na kwenda katika taifa lingine lijulinalo kama Akaya mji wa Athene.
Sifa mojawapo ya mji huu ni kwamba watu wake walikuwa na kiu sana ya kujua habari za Mungu tofauti na watu wa miji mingine, licha ya kwamba walikuwa ni maskini kuliko makanisa mengine,(soma 2Wakoritho 8:1-3) jambo ambalo lilipelekea mpaka Paulo kuzuiliwa kwanza na Roho Mtakatifu kuhubiri katika miji mingine iliyokuwa Asia ndogo wakati ule, kama vile Galatia na Frigia, Utasoma hilo katika..
Matendo 16:6 “Wakapita katika nchi ya Frigia na Galatia, wakikatazwa na Roho Mtakatifu, wasilihubiri lile neno katika Asia. 7 Walipofika kukabili Misia wakajaribu kuenda Bithinia, lakini Roho wa Yesu hakuwapa ruhusa, 8 wakapita Misia wakatelemkia Troa. 9 PAULO AKATOKEWA NA MAONO USIKU; ALIMWONA MTU WA MAKEDONIA AMESIMAMA, AKIMSIHI, NA KUMWAMBIA, VUKA, UJE MAKEDONIA UTUSAIDIE. 10 Basi alipokwisha kuyaona yale maono, mara tukataka kutoka kwenda Makedonia, kwa kuwa tuliona hakika ya kwamba Mungu ametuita tuwahubiri Habari Njema”.
Matendo 16:6 “Wakapita katika nchi ya Frigia na Galatia, wakikatazwa na Roho Mtakatifu, wasilihubiri lile neno katika Asia.
7 Walipofika kukabili Misia wakajaribu kuenda Bithinia, lakini Roho wa Yesu hakuwapa ruhusa,
8 wakapita Misia wakatelemkia Troa.
9 PAULO AKATOKEWA NA MAONO USIKU; ALIMWONA MTU WA MAKEDONIA AMESIMAMA, AKIMSIHI, NA KUMWAMBIA, VUKA, UJE MAKEDONIA UTUSAIDIE.
10 Basi alipokwisha kuyaona yale maono, mara tukataka kutoka kwenda Makedonia, kwa kuwa tuliona hakika ya kwamba Mungu ametuita tuwahubiri Habari Njema”.
Hivyo nasi pia tunalo la kujifunza juu ya watu hawa wa makedonia,. Kwamba tuwe na bidii katika kumtafututa Mungu, na pia tuwe watu wa kupenda kuyachunguza maandiko kwanza kabla ya kubisha pale tunapohubiriwa mfano wa watu wa Beroya walivyofanya (Maendo 17:10). Ndivyo Mungu atakavyotuona na sisi tunastahili kupokea neema ya wokovu.
VUKA UJE MAKEDONIA UTUSAIDIE.
WINGU KUBWA LA MASHAHIDI.
JE KUNA UISLAMU KATIKA BIBLIA?
JE! UMEPOKEA KWELI ROHO MTAKATIFU?
KUMBUKA, VIVUKO VYA YORDANI VINAKUNGOJA MBELENI.
UFALME WAKO UJE.
Kuna wakati Israeli ilikuwa inapitia majira tofauti tofauti, Si kila wakati Mungu alikuwa anazungumza nao, ana kwa ana au kwa kupitia manabii au waamuzi, hapana Kuna wakati Mungu alikuwa hasemi chochote kabisa kwa kipindi fulani, Lakini hiyo haikumaanisha kuwa Mungu amewaacha au hafuatilii mienendo yao kabisa, bali ni jinsi tu yeye, alivyopenda na anafanya hivyo wakati mwingine ili tu kupima uaminifu wa watu wake.
Kipindi kimojawapo kilikuwa ni kile cha Nabii Samweli, na kingine ni kipindi cha kati ya Nabii Malaki hadi wakati wa Yohana mbatizaji ambapo inakadiriwa ni Zaidi ya miaka 300. Sasa kwa mfano tukirudi katika kipindi cha Samweli, tunaona ulifika wakati biblia inasema Neno la Bwana lilikuwa ni adimu sana, na kulikuwa hakuna mafunuo Dhahiri, hii ikiwa na maana kuwa Mungu hakuwa anajifunua moja kwa moja kwa watu wake, aidha kwa kupitia manabii au makuhani, au kitu chochote tusome..
1Samweli 3:1 “Basi, mtoto Samweli akamtumikia Bwana mbele ya Eli. Na neno la Bwana lilikuwa adimu siku zile; hapakuwa na mafunuo dhahiri.”
Unaona, sasa matokeo yake ni kuwa watu wengi walipoona hivyo, kwanini Mungu hasemi chochote, hazungumzi chochote, hapigi popote, wakadhani kuwa hawatazamwi mienendo yao na matendo yao, hapo ndipo baadhi ya watumishi wake wakaanza kupoa na kukengeuka mpaka kufikia hatua ya kufanya mambo ya ajabu madhabahuni pake…Kama vile tu ilivyo leo..
Mfano ukisoma pale utaona kulikuwa na Watoto wawili wa Kuhani aliyeitwa Eli, ambaye wa kwanza aliitwa Hofni, na wa pili aliitwa Finehasi, hawa walifikia hatua ya kuidharau sadaka ya Bwana,kwa kuchukua kiwango ambacho hawajaamuriwa kwa nguvu na Zaidi ya yote walikuwa wanazini na wanawake ambao walikuwa wanatumika katika nyumba ya Bwana.. Hofu ya Mungu ilikuwa imeshaondoka ndani yao, kwasababu tu waliona Mungu hafanyi lolote, wala hachukui hatua yoyote kwao..
Lakini siku ya siku ilipofika ya Mungu kuanza kusema tena Dhahiri..Hapo ndipo walipojua Mungu tangu zamani alikuwa anawatazama, na kuwalipa mema wale waliostahili mema, na mabaya wale waliostahili mabaya..
Siku moja kijana Samweli alipokuwa amelala usiku Bwana alimtokea na kumwambia..
1Samweli 3:11 “Bwana akamwambia Samweli, Angalia, nitatenda tendo katika Israeli, ambalo kila atakayelisikia masikio yake yatamwasha. 12 Siku hiyo nitayatimiza maneno yale yote niliyoyasema juu ya Eli katika habari za nyumba yake, tangu mwanzo hata mwisho. 13 Kwa maana nimemwambia ya kwamba nitaihukumu nyumba yake milele, kwa ajili ya ule uovu alioujua; kwa kuwa wanawe walijiletea laana, wala yeye hakuwazuia. 14 Na kwa hiyo nimeapa juu ya nyumba ya Eli, ya kwamba uovu wa nyumba ya Eli hautasafika kwa dhabihu wala kwa sadaka hata milele”.
1Samweli 3:11 “Bwana akamwambia Samweli, Angalia, nitatenda tendo katika Israeli, ambalo kila atakayelisikia masikio yake yatamwasha.
12 Siku hiyo nitayatimiza maneno yale yote niliyoyasema juu ya Eli katika habari za nyumba yake, tangu mwanzo hata mwisho.
13 Kwa maana nimemwambia ya kwamba nitaihukumu nyumba yake milele, kwa ajili ya ule uovu alioujua; kwa kuwa wanawe walijiletea laana, wala yeye hakuwazuia.
14 Na kwa hiyo nimeapa juu ya nyumba ya Eli, ya kwamba uovu wa nyumba ya Eli hautasafika kwa dhabihu wala kwa sadaka hata milele”.
Ujumbe huo ulikuwa ni mzito sana hata kwa Samweli ambaye haumuhusu, itakuwaje kwa wale wahusika?, Ukifuatilia Habari ile utaona ndani kipindi kifupi sana, zaidi ya watu elfu 80 walikufa kwa kupigwa na Mungu.. ikiwemo wale wana wawili wa Eli.
Hata sasa, upo wakati utaonekana kama Bwana amekaa kimya (Nikimaanisha kwa mapigo, yanaonekana kama adimu), lakini hilo lisitufanye tudhani kuwa haoni yanayoendelea katika kanisa lake..Tujue kuwa lipo kusudi analitekeleza na mojawapo ndio hilo la kuwapima walio waaminifu ni wapi …
Lakini wakati utafika, ambao utakuja kwa ghafla, atazungumza hukumu zake, lakini atakapozungumza safari hii ujue kuwa sikio lako litawasha . Leo hii unapata ujasiri wa kuvaa nusu uchi kanisani, unadhani Mungu kuwa kimya, inainajisi madhabahu yake ni kwamba anapendezwa na wewe, unashiriki meza ya Bwana halafu ukitoka hapo unakwenda kuzini, unadhani Mungu hakuoni.
wewe ni mchungaji lakini kuzini na washirika wako mfano wa Hofni na Finehasi ni kitu cha kawaida kwako, kwa kuwa huoni kitu chochote kikitokea katika Maisha yako, sasa unadhani ndivyo itakavyokuwa hivyo siku zote.
Unafanya mambo ya ajabu madhabahuni pa Mungu, wala huogopi, unafanya comedy, na siasi, ili upendwe na watu ukijiona wewe ni mjanja, nataka nikuambie wakati utafika wa mwenye madhabahu kuzungumza..
Wengine wanasema tunaishi chini ya neema, Mungu hawezi kuwaadhibu watu aliowakomboa kwa damu ya mwanawe.. Ndugu, Kasome Habari za Hanania na Safira na mke wake, halafu useme lile ni agano la kale au jipya?..Watu wale walikufa kwa kutotimiza tu viapo vyao kwa Mungu vya kumtolea sadaka, jiulize wewe ambaye ni mzinzi, halafu unashiriki meza ya Bwana, utakuwaje?
Tufahamupo hukumu za Mungu, basi tuchukue tahadhari kabla mabaya hayajatukuta mimi na wewe. Nyakati hizi ni za nyakati za hatari.
Maran Atha!
KIFO CHA REINHARD BONKEY KINAACHA UJUMBE GANI KWETU?
Je! msalaba kaburini una umuhimu wowote?