Category Archive Home

UFUNUO Mlango wa 2: Sehemu ya kwanza.

(Sehemu ya kwanza)

Jina kuu la BWANA wetu YESU KRISTO litukuzwe milele yote. Karibu katika mwendelezo wa uchambuzi wa kitabu cha Ufunuo, Leo tutaitazama ile sura ya pili. Kama tulivyotangulia kusoma katika ile sura ya kwanza, Tuliona Yohana akionyeshwa Sura na umbo la YESU KRISTO , na wasifa wake ambao alionyeshwa kwa lugha ya picha,(Kumbuka Bwana Yesu kiuhalisia hana muonekano kama ule), jinsi alivyokuwa anaonekana na nywele nyeupe kama sufu, macho ya moto, miguu ya shaba, upanga unaotoka kinywani mwake, mwenye sauti kama maji mengi, aendaye katikati ya vile vinara saba vya dhahabu n.k. hizo zote zilisimama kama viashiria (Nembo) vya tabia yake, ambayo kila moja ina nafasi yake katika hichi kitabu cha Ufunuo na ndio maana zilitangulizwa kuelezwa mwanzoni kabisa mwa kitabu hichi.

Hivyo katika sura ile ya kwanza mwishoni tuliona jinsi Yohana anaambiwa ayaandike yale aliyoyaona na ayapeleke kwa yale makanisa saba. 

Ufunuo 1: 19 Basi, uyaandike mambo hayo uliyoyaona, nayo yaliyopo, na yale yatakayokuwa baada ya hayo.

20 Siri ya zile nyota saba ulizoziona katika mkono wangu wa kuume, na ya vile vinara saba vya dhahabu. Zile nyota saba ni malaika wa yale makanisa saba; na vile vinara saba ni makanisa saba.”

Ni muhimu kufahamu Barua hizi Yohana alizopewa hazikuyahusu tu yale makanisa 7 yaliyokuwa Asia ndogo kwa wakati ule, bali pia na kwa makanisa yatakayokuja huko mbeleni na ndio maana hapa anaambiwa ayaandike mambo hayo YALIYOPO na YATAKAYOKUJA baada ya hayo. Ikiwa na maana kuwa yale yaliyoko ndio yale makanisa 7 yaliyokuwa Asia katika wakati wa Yohana, na yale yatakayokuja ni Makanisa 7 tuliopo sisi baada ya Yohana kuondoka. Kwahiyo Tunaposoma leo hii kitabu cha ufunuo tunajua kuwa yale makanisa 7 yaliyokuwa katika kipindi cha Yohana yameshapita. Na tangu kipindi cha Bwana YESU kuondoka hadi sasa ni takribani miaka 2,000 na kanisa la Kristo limekuwa likipita katika vipindi tofauti tofauti saba ndani ya huo muda wa miaka 2000, vijulikanavyo kama NYAKATI SABA ZA KANISA.

Sasa tukirudi katika sura ya pili. Tunaona Bwana Yesu akianza kutoa ujumbe kwa kanisa moja baada ya lingine, Kuanzia kanisa la Efeso mpaka Laodikia ambalo ndio la mwisho. Tunasoma;

KANISA LA EFESO:

Ufunuo 2:1 “Kwa malaika wa kanisa lililoko Efeso andika; Haya ndiyo anenayo yeye azishikaye hizo nyota saba katika mkono wake wa kuume, yeye aendaye katikati ya vile vinara saba vya dhahabu”.

Awali ya yote tunaona Bwana Yesu anajitambulisha hapa kama “yeye aendaye katikati ya vile vinara saba vya dhahabu na aliyeshika zile nyota saba”. Kumbuka hapa hajajitambulisha yeye kama yeye mwenye macho ya moto au uso ung’aao kama jua. Lakini alisema yeye aendaye katikati ya vile vinara saba vya dhahabu ikiwa na maana kuwa uelekeo wake wote utakuwa katika kuchunguza kinara cha hilo kanisa na yale makanisa mengine. Kumbuka kinara ni taa iliyokuwa inawekwa katika nyumba ya Mungu (Hekaluni) Kwa ajili ya kutia Nuru kule ndani (Patakatifu) ili shughuli za kikuhani ziende sawasawa (Kutoka 27:20), na kilikuwa hakizimwi muda wote, sharti ni lazima kimulike daima usiku na mchana pasipo kuzimwa. Vivyo hivyo hapa Bwana alipoanza kwa kujitambulisha hivyo alikuwa anatazamia nuru isiyozimika ndani ya hilo kanisa husika (nyumba yake) ambalo analitolea habari zake hapo chini.

Siri ya zile nyota saba ulizoziona katika mkono wangu wa kuume, na ya vile vinara saba vya dhahabu. Zile nyota saba ni malaika wa yale makanisa saba; na vile vinara saba ni makanisa saba.

(katika nyumba ya Bwana kinara cha taa kilikuwa na mirija/matawi saba, na kilikuwa kinatia nuru nyumba ya Mungu daima)

Na NURU hii ni ipi Bwana aliyokuwa aliitazamia kuiona inaangaza?. Biblia inatuambia

1Yohana 2: 8 Tena nawaandikia amri mpya, neno lililo kweli ndani yake na ndani yenu; kwa kuwa giza linapita na ile nuru ya kweli imekwisha kung’aa.

9 Yeye asemaye kwamba yumo NURUNI, naye amchukia ndugu yake, yumo gizani hata sasa.

10 Yeye ampendaye ndugu yake, akaa katika nuru, wala ndani yake hamna kikwazo.

11 Bali yeye amchukiaye ndugu yake, yu katika giza, tena anakwenda katika giza, wala hajui aendako, kwa sababu giza imempofusha macho.

Na pia tukisoma 1Wakorintho 13 inasema Upendo huvumilia yote, huamini yote, hutumaini yote, hustahimili yote, Upendo haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli n;k. Hivyo kwa ujumla NURU ni UPENDO. Ambao huo unaanza kwanza kwa KUMPENDA BWANA MUNGU WAKO kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote na kwa akili zako zote,na kwa nguvu zako zote, (Kwa kuzishika na kuzifuata amri zake) na pia kumpenda jirani yako kama nafsi yako. Kwa kuzingatia hayo mawili KINARA CHAKO kitakuwa kinatoa Nuru ya kutosha.

Sasa tukirudi katika Kanisa lile la EFESO, tunaona Bwana aliendelea kulitolea habari zake na kusema:

Ufunuo 2:2-5 “Nayajua matendo yako, na taabu yako, na subira yako, na ya kuwa huwezi kuchukuliana na watu wabaya, tena umewajaribu wale wajiitao mitume, nao sio, ukawaona kuwa waongo;

3 tena ulikuwa na subira na kuvumilia kwa ajili ya jina langu, wala hukuchoka.

Lakini nina neno juu yako, ya kwamba umeuacha upendo wako wa kwanza.

Basi, kumbuka ni wapi ulikoanguka; ukatubu, ukayafanye matendo ya kwanza. Lakini, usipofanya hivyo, naja kwako, nami nitakiondoa kinara chako katika mahali pake, usipotubu.

6 Lakini unalo neno hili, kwamba wayachukia matendo ya Wanikolai, ambayo na mimi nayachukia.”

Kwanza kabisa maana ya neno EFESO ni “Kuacha mema yaondoke”. Hivyo hili kanisa kama jina lake lilivyo mwanzoni lilianza kuenenda katika Nuru ya Neno ambao ni UPENDO wa kiungu, lilikuwa japokuwa linapitia majaribu mengi liliendelea kumpenda Mungu, lilivumilia mabaya,Hii tunaona katika utawala wa Rumi chini ya kiongozi mkatili Nero, aliyewaua wakristo wengi wakati ule kwa kuwasingizia kuwa wameuchoma mji na hali sio wao. Kanisa hili pia mwanzoni lilijiweka katika utakatifu wa hali ya juu, liliwapima manabii wa uongo na kugundua kuwa sio, kwa muda mrefu sana. Walikuwa na uwezo pia wa kuyagundua matendo ya WANIKOLAI na kuyapinga katikati ya Kanisa. Kumbuka neno “Nikolai” tafsiri yake ni “Kuteka madhabahu” Hivyo kulikuwa na tabia zilizokuwa zimeanza kujitokeza katikati ya baadhi ya makanisa, watu(wasio wa Mungu) walianza kijipachikia vyeo vilivyoua uongozi wa Roho Mtakatifu. kwamfano watu badala ya kwenda kumuomba Mungu msamaha, walianza kuwafuata wanadamu wenzao wawaombee au wawaondolee dhambi zao kwa niaba ya Mungu, Badala karama za roho ziongoze kanisa, vyeo vya kibinadamu vikaanza kuongoza kanisa n.k. Huku ndiko kuteka madhabahu na hayo ndiyo yaliyokuwa matendo ya Wanikolai, ambayo kanisa la Kristo la kweli lilichukizwa nayo na Bwana vilevile.

Lakini Kanisa hili la Efeso lilifikia kipindi ule upendo waliokuwa nao hapo kwanza ukaanza kupoa (wakaanza kuacha mema yaondoke katikati yao kama vile Jina la kanisa lao lilivyo), uvumilifu kwa ajili Imani, utakatifu na subira vikaanza kupoa, zamani walikuwa wanawajaribu manabii wa uongo na kuwaondoa katikati yao lakini sasa hawafanyi hivyo tena.. Na ndio maana Bwana hapa anatokea na kuanza kukichunguza kinara chao na kuwaambia NURU yao imeanza kufifia na kukaribia kuzima Ukiendelea kusoma utaona Bwana anawaambia watubu 

” 5 Basi, kumbuka ni wapi ulikoanguka; ukatubu, ukayafanye MATENDO YA KWANZA. Lakini, usipofanya hivyo, naja kwako, nami nitakiondoa kinara chako katika mahali pake, usipotubu.”

Kama tulivyoona Pale mwanzoni katika ile sura ya kwanza juu ya ule mwonekano wake, jinsi alivyoonekana akipita katikati ya vile vinara vya taa, ikiwa na maana kuwa anapeleleza na kufanya masahihisho, kinara kilichofifia na kukaribia kuzima anakiondoa na kile kinachozidi kuwaka anakiongezea nuru, kwasababu biblia inasema “mwenye nacho ataongezewa asiye nacho hata kile kidogo alicho nacho atanyang’anywa” Hivyo kama wasingeimarisha matendo yao, hata ile nuru waliyokuwa nayo kidogo ingeondolewa kwao. Na ile taabu yao ya mwanzo waliyoisumbukia ingekuwa ni sawa na bure.

Sasa kanisa hili la Efeso lenye tabia hizi lilianza kati ya kipindi cha 53WK hadi mwaka 170WK. Na Malaika wa kanisa hilo alikuwa ni Mtume Paulo. Kumbuka Neno “malaika” tafsiri yake ni “mjumbe”  hivyo wapo wajumbe wa kimbinguni(ndio malaika wa rohoni) na wapo wajumbe wa duniani. Hawa wanaotajwa katikati ya haya makanisa saba ni wajumbe wa kiduniani (yaani wanadamu). Kwahiyo malaika wa Kanisa hili la Efeso alikuwa ni Mtume Paulo. Kwasababu yeye ndiye mtume aliyepewa neema ya kupeleka Injili kwa mataifa. Na mafunuo mengi aliyopewa yalikuwa ni msingi katika makanisa ya wakati ule, na hata sasa.

Kadhalika na sisi tuliopo katika Kanisa la mwisho (Laodikia) ambalo tutakuja kusoma habari zake hapo baadaye na sisi pia tunaonywa tusipotubu kinara chetu kitaondolewa.. Kumbuka BWANA pale anaonekana akipita katikati ya vile vinara saba na sio “Kinara kimoja“. Hivyo anavichunguza vyote kuanzia cha kwanza mpaka cha mwisho. Na kama asipoiona ile nuru aliyoikusudia iwepo katika kinara chetu vile vile kitaondolewa.. Na tunafahamu madhara ya Nuru kuondolewa, anamaanisha giza linaachiliwa liingie ndani yako.

Ndugu Mwanzoni ulipoanza kuamini ulikuwa mtakatifu lakini sasa hivi utakatifu wako umepoa, ulikuwa unasali, ulikuwa unavaa vizuri, ulikuwa na huruma kwa ndugu, ulikuwa na upendo, ulikuwa na uvumilivu juu ya imani yako hata kama watu wanaokuzunguka wanakudhihaki, ulikuwa huwezi kuabudu sanamu au kuchukuliana na mafundisho ya uongo lakini sasahivi unayapokea mafundisho ya uongo na kuyafurahia, Injili zisizokufanya utazama ufalme wa mbingu ndio unazozipenda, huwezi tena kusali, kujisitiri huwezi tena, hukutazamii tena kuja kwa Bwana umechoka na kuishiwa nguvu. Hizo ni dalili za Kinara chako kuzima..Jitahidi kabla hakijaondolewa. Maana siku kitakapoondolewa ndugu hali yako ya mwisho itakuwa mbaya kuliko ile ya kwanza. Ule upendo uliokuwa nao kwanza wa Mungu unaondoka kabisa ndani yako, unafanana tena na watu wasiomjua Mungu, au unakua kama vile mtu ambaye hajawahi kumjua Mungu kabisa.

Hivyo tujitahidi na sisi TAA zetu ziwe zinawaka katika hizi siku za kumalizia kwasababu Bwana hivi karibuni anarudi.. yeye mwenyewe alisema; katika Luka 12: 35 Viuno vyenu na viwe vimefungwa, na TAA ZENU ZIWE ZINAWAKA; 36 nanyi iweni kama watu wanaomngojea bwana wao, atakaporudi kutoka arusini, ili atakapokuja na kubisha, wamfungulie mara.”

Ubarikiwe sana.

Endelea hapo chini sehemu ya pili ya sura hii ya pili ya kitabu cha Ufunuo,.ambapo tutakuja kuona ujumbe wa kanisa la pili (SMIRNA).

Tafadhali “Share” kwa wengine ujumbe huu na Mungu atakubariki.

1.Ufunuo: Mlango wa 2: Sehemu ya 2

Nyumbani

Print this post

UFUNUO: Mlango wa 1

Jina la BWANA wetu YESU KRISTO lihimidiwe daima. Karibu katika uchambuzi wa kitabu cha Ufunuo leo tukianza na ile sura ya kwanza.; Tunasoma…

“1 Ufunuo wa Yesu Kristo, aliopewa na Mungu awaonyeshe watumwa wake mambo ambayo kwamba hayana budi kuwako upesi; naye akatuma kwa mkono wa malaika akamwonyesha mtumwa wake Yohana; 

2 aliyelishuhudia Neno la Mungu, na ushuhuda wa Yesu Kristo, yaani, mambo yote aliyoyaona.”

Awali ya yote tunaona hapa Yohana akiandika na kusema “Ufunuo wa Yesu Kristo” akimaanisha kuwa alichokipokea sio ufunuo wake bali ni wa Yesu mwenyewe. Kumbuka Yohana ndiye Mtume pekee aliyekuwa karibu sana na Bwana, na aliyependwa na Bwana kuliko mitume wote, Kiasi kwamba hata siri za karibu sana za Bwana alikuwa anazipokea kwanza yeye ndiye ndipo wengine wafuate, ni mtume pekee aliyekuwa akiegema kifuani mwa Bwana muda wote (Yohana 13:23, na Yohana 21:20), Na ndio maana tunaona wakati ule wa jioni wa kuumega mkate, Bwana aliposema mmoja wenu atanisaliti, Petro alimpungia mkono Yohana amuulize Bwana ni nani atakayemsaliti, na Bwana akamfunulia Yohana ni yule atakaye mmegea tonge na kumpa, kwasababu Petro alijua Yohana ndiye  kipenzi wa Bwana.

Kwasababu ya uhusiano wake wa kipekee na Bwana, ilimpelekea, mpaka kufikia hatua ya kupewa neema hii ya MAFUNUO na Bwana mwenyewe, mambo ambayo yatakuja kutokea katika siku zake na siku za mwisho. Yohana ni mfano wa Danieli ambaye naye alikuwa ni mtu aliyependwa sana na Mungu, Ikapelekea yeye naye kupewa mafunuo yanayofanana na ya Yohana. Kwahiyo kama ukichunguza utagundua watu wanaofunuliwa Mafunuo makuu kama haya sio tu kila mkristo, au mwamini yoyote bali ni mtu yule anayependezwa na Mungu, Vivyo hivyo na sisi tukimpendeza Bwana atatupa siri zake za ndani zaidi.

Mstari wa 3 unasema; “Heri asomaye na wao wayasikiao maneno ya unabii huu, na kuyashika yaliyoandikwa humo; kwa maana wakati u karibu”. Hapa Biblia inasema heri ikiwa na maana kuwa amebarikiwa mtu yule ASOMAYE, ASIKIAYE, na AYASHIKAYE ..Na kusikiwa kunakozungumziwa hapo ni kusikia kwa masikio ya ndani (yaani kupata Ufunuo ) na sio masikio ya nje, na kuyashika ikimaanisha kuyaishi uliyoyasikia. Hivyo Mtu yeyote afanye hivyo biblia inasema amebarikiwa. Kumbuka Si watu wote wanapata neema hii ya kikielewa kitabu hichi, kwasababu ni kitabu kilichofungwa hivyo kinahitaji kufunguliwa na Roho mwenyewe. Kwahiyo kama wewe umepata neema, jitahidi kuyaishi yaliyoandikwa humo ili na wewe uitwe HERI.

Tukiendelea mistari inayofuata;

“4 Yohana, kwa yale makanisa saba yaliyoko Asia; Neema na iwe kwenu na amani, zitokazo kwake yeye aliyeko na aliyekuwako na atakayekuja; na zitokazo kwa roho saba walioko mbele ya kiti chake cha enzi;

5 tena zitokazo kwa Yesu Kristo, shahidi aliye mwaminifu, mzaliwa wa kwanza wa waliokufa, na mkuu wa wafalme wa dunia. Yeye atupendaye na kutuosha dhambi zetu katika damu yake,

6 na kutufanya kuwa ufalme, na makuhani kwa Mungu, naye ni Baba yake; utukufu na ukuu una Yeye hata milele na milele. Amina”.

Tunasoma hapa Yohana anaanza na salamu kwa yale makanisa 7 aliyopewa kuyaandikia maneno hayo. Anasema neema iwe kwenu na amani zitokazo kwa yeye “aliyekuwako, aliyeko na atakayekuja”, Hii inafunua umilele wa Mungu Elohimu, Yeye pekee ndiye asiyekuwa na mwanzo wala mwisho. Tena zitokazo kwa Roho saba walioko mbele ya kiti cha enzi cha Mungu. Sasa kumbuka Mungu hana Roho 7, Tunajua wote Mungu mwenyewe ni Roho(1),na nafsi moja, hapo anaposema hapa roho 7 haina maana kuwa anazo roho 7, bali anaonyesha jinsi Roho ya Mungu ilivyokuwa inatenda kazi katika yale makanisa 7 ambayo tutasoma habari zake hapo baadaye. Na pia anasema Neema na Amani zitakazo kwa Yesu Kristo aliyeshahidi mwaminifu, mzaliwa wa kwanza wa waliokufa. Kama tunavyojua Mungu alitoka katika UMILELE akaingia katika MUDA ili kumkomboa mwanadamu. Hivyo akaundaa mwili ili akae ndani yake. Na huo mwili ukawa YESU.

Kwahiyo Mungu alikuwa ndani ya Yesu akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake (2Wakorintho 5:18-19). Kwahiyo hapa haizungumzii UTATU, hapana Mungu ni mmoja anayo nafsi moja, na Roho moja. Kwa mfano mimi ninaweza kuzungumza na wewe kwa kutumia account ya facebook, yenye jina, picha na utambulisho wangu. Ninazungumza, ninaongea na wewe ninajibu maswali, lakini haimaanishi sisi tupo wawili. kwamba wa kwanza ni mimi  na wapili yule wa mtandaoni hapana mimi ni yule yule mmoja isipokuwa nimeingia ndani ya facebook ili  nikutane na jamii ya watu fulani. vivyo hivyo na Mungu ambaye hana mwanzo wala mwisho aliingia ndani ya mwili wa kibinadamu (1Timotheo 3:16) ili tu kutupata sisi wanadamu..Na kama vile ile account yangu siku moja  ilikuwa na mwanzo wake vivyo hivyo Bwana Yesu alikuwa na mwanzo, na ndio maana utakuja kuona kuna mahali anasema yeye ni ALFA NA OMEGA. Lakini haimaanishi kuwa Mungu (ELOHIM) ana mwanzo na mwisho…hapana Yeye hana mwanzo wala mwisho, kwasababu yeye ndio mwanzo na ndio mwisho.

“7 Tazama, yuaja na mawingu; na kila jicho litamwona, na hao waliomchoma; na kabila zote za dunia wataomboleza kwa ajili yake. Naam. Amina.

8 Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, asema Bwana Mungu, aliyeko na aliyekuwako na atakayekuja, Mwenyezi”.

Sasa Biblia inasema upo wakati Bwana aliouweka wa yeye kurudi tena ambao kila jicho litamwona na hao waliomchoma mkuki pale Kalvari (yaani wayahudi na watu wa mataifa) watamwombolezea, kumbuka hapa sio ule wakati wa kulichukua kanisa lake, hapana bali utakuwa ni ujio wa Bwana Yesu kuja duniani na watakatifu wake waliokuwa wameshanyakuliwa muda wa miaka 7 iliyopita tangu tukio hilo litokee. Hapo ndipo kila jicho la watu waliosalia ambao majina yao hayakuandikwa katika kitabu cha uzima tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu watamwona na kumuombolezea..

Mathayo 24: 29 “

Lakini mara, baada ya dhiki ya siku zile, jua litatiwa giza, na mwezi hautatoa mwanga wake, na nyota zitaanguka mbinguni, na nguvu za mbinguni zitatikisika;
30 ndipo itakapoonekana ishara yake Mwana wa Adamu mbinguni; ndipo mataifa yote ya ulimwengu watakapoomboleza, nao watamwona Mwana wa Adamu akija juu ya mawingu ya mbinguni pamoja na nguvu na utukufu mwingi. (soma pia Yuda 1:14 na Ufunuo 19:11-21,)

Tukiendelea mistari inayofuata….

” 9 Mimi Yohana, ndugu yenu na mwenye kushiriki pamoja nanyi katika MATESO na UFALME na SUBIRA ya Yesu Kristo, nalikuwa katika kisiwa kiitwacho Patmo, kwa ajili ya Neno la Mungu, na ushuhuda wa Yesu.

10 Nalikuwa katika Roho, siku ya Bwana; nikasikia sauti kuu nyuma yangu, kama sauti ya baragumu,

11 ikisema, Haya uyaonayo uyaandike katika chuo, ukayapeleke kwa hayo makanisa saba: Efeso, na Smirna, na Pergamo, na Thiatira, na Sardi, na Filadelfia, na Laodikia.”

Yohana anasema “mimi ndugu yenu mwenye kushiriki pamoja nanyi”…Ikiwa na maana kuwa kile alichokuwa anakipitia, ndugu wengine walikuwa wanakipitia pia.mateso, dhiki,vifungo, na subira ya Yesu Kristo. Hii inaonyesha kabisa mojawapo ya utambulisho wa mkristo kwamba yupo katika safari ya Imani ni kupitia hayo kwa ajili ya Bwana.(Kumbuka ni kwa ajili ya Bwana, na si kwasababu nyingine zozote)

Lakini tunapokuwa wakristo lakini hatuna subira, kwa ajili ya Bwana, inaonyesha kabisa hatupo miongoni mwa hao ndugu waaminio.. Yohana anasema alikuwa katika kisiwa kiitwacho PATMO.Hichi  ni kisiwa kilichokuwa maeneo ambayo sio mbali sana na yale makanisa 7 yaliyokuwepo Asia ndogo (ambayo kwasasa ni maeneo ya UTURUKI) umbali wa takribani km 60-120.

Ni kisiwa ambacho wafungwa walikuwa wanaenda kuachwa huko wafe, ni kisiwa kilichokuwa na mawe mawe tu, mijusi nyoka na kenge, na nge. Hakuna mimea kumezungukwa na maji kote, hivyo ni mahali pasipokuwa na jinsi yoyote ya kuishi au kutoroka mtu utaishia kufa kwa njaa au kuuawa na wanyama wakali. Hivyo Yohana naye alitupwa kule kama mmojawapo wa wafungwa. Na ndipo huko huko Bwana akamfunulia mambo ya siri kama tunavyoyasoma. Nasi pia tunajifunza wakati mwingine tukitupwa katika majaribu mazito (maadamu ni wakristo) tujue ni Bwana anaruhusu mwenyewe ili kutupa mafunuo zaidi.

Hivyo maono hayo Yohana aliyoonyeshwa hayakuwa ndani ya siku moja yote..Bali ulikuwa ni mfululizo wa maono kwa kipindi cha muda fulani.Ndipo akapewa maagizo kwamba ayaandike mambo yote anayoyaona na ayapeleke kwa yale makanisa saba yaliyopo Asia, yaani  Efeso, na Smirna, na Pergamo, na Thiatira, na Sardi, na Filadelfia, na Laodikia.

 MTU MFANO WA MWANADAMU.

“12 Nikageuka niione ile sauti iliyosema nami. Na nilipogeuka, niliona vinara vya taa saba vya dhahabu;
13 na katikati ya vile vinara nikaona mtu mfano wa Mwanadamu, amevaa vazi lililofika miguuni, na kufungwa mshipi wa dhahabu matitini.
14 Kichwa chake na nywele zake zilikuwa nyeupe kama sufu nyeupe, kama theluji; na macho yake kama mwali wa moto;
15 na miguu yake kama shaba iliyosuguliwa sana, kana kwamba imesafishwa katika tanuru; na sauti yake kama sauti ya maji mengi”.

Tunaona Yohana alipogeuka aisikie ile sauti akaona mtu “MFANO” wa mwanadamu. aliyevaa vazi lililofika miguuni, na kufungwa mshipi wa dhahabu matitini. Kumbuka Yohana kuonyeshwa vile haikuwa na maana kuwa Bwana Yesu anataka kuonyesha mwili wake jinsi ulivyo na utukufu au unavyotisha mbele za wanadamu, hapana, bali kila kitu alichokuwa anakiona katika mwili wake kilikuwa kina maana fulani.. Kumbuka lile lilikuwa ni ONO sio kitu halisi.

Tukisoma tunaona Mtu yule alikuwa na nywele kama sufu nyeupe. Ikiashiria kuwa ni HAKIMU. (Kumbuka mahakimu huwa ni desturi yao kuvaa wigi nyeupe kichwani) Hivyo yule ni Muhukumu wa mambo yote, na weupe wake inaashiria usafi na haki ya hukumu yake. Atakapokuja kuketi katika kiti chake cha enzi cheupe, atawahukumu kwa haki watu wote. Tutakuja kuona vizuri katika sura 20.

Na pia mtu huyu alionekana ana macho kama mwali wa moto, na miguu iliyosuguliwa kama shaba. Ikifunua hukumu yake juu ya waovu katika kanisa na wasiomcha yeye ulimwenguni kote,.Kumbuka na macho kazi yake ni kuona, na miguu ni kukanyaga. Hivyo anapoonekana na macho ya moto inamaanisha kuwa anaona mambo yote yanayopaswa kuhukumiwa kwa moto. Tutakuja kuona pia katika kanisa la tatu la Thiatira (jinsi Bwana alivyojionyesha kwao kama miale ya moto na miguu ya shaba, kutokana na maovu yaliyojificha ndani ya kanisa hilo,).

Na kama miguu yake ilivyokuwa  ya SHABA atakanyaga mambo yote maovu ndani ya kanisa lake kwanza kisha baadaye atamalizia na kwa ulimwengu mzima tutakapofika  katika  sura ya 14 tutaona pia jinsi atakavyokuja kukanyaga shinikizo la mvinyo ya ghadhabu ya hasira ya Mungu mwenyezi (Ufunuo 19:15).

Tukizidi kuendelea kusoma mistari inayofuata..;

“16 Naye alikuwa na nyota saba katika mkono wake wa kuume; na upanga mkali, wenye makali kuwili, ukitoka katika kinywa chake; na uso wake kama jua liking’aa kwa nguvu zake. 

17 Nami nilipomwona, nalianguka miguuni pake kama mtu aliyekufa. Akaweka mkono wake wa kuume juu yangu, akisema, Usiogope, Mimi ni wa kwanza na wa mwisho,

18 na aliye hai; nami nalikuwa nimekufa, na tazama, ni hai hata milele na milele. Nami ninazo funguo za mauti, na za kuzimu. 19 Basi, uyaandike mambo hayo uliyoyaona, nayo yaliyopo, na yale yatakayokuwa baada ya hayo. 

20 Siri ya zile nyota saba ulizoziona katika mkono wangu wa kuume, na ya vile vinara saba vya dhahabu. Zile nyota saba ni malaika wa yale makanisa saba; na vile vinara saba ni makanisa saba”.

Tunaona pia mtu huyu anaonekana akiwa na nyota saba katika mkono wake wa kuume. Hizi nyota saba tafsiri yake kama inavyoelezwa ni malaika saba, mkono tunajua  kazi yake ni kubeba, na ukiwa wa kuume, inamaana unabeba kitu stahiki, hivyo wale malaika (wajumbe 7) watakuwa wamebeba ujumbe stahiki kwa kanisa husika. na pia alionekana akitembea katikati ya vile vinara 7 vya taa ambavyo ndiyo yale makanisa 7. Jiulize ni kwanini hakuonekana akiwa katikati ya madhabahu, au katika birika ya shaba Katika Hekalu la Mungu?, bali anaonekana katikati ya vile vinara 7 vya Taa akitembea katikati yake?. Inamaana kuwa makao yake ni katikati ya yale makanisa saba. Huko ndipo jicho lake lilipo na Roho yake ilipo.

Mtu huyu pia alionekana na Upanga mkali ukatao kuwili unaotoka kinywani mwake. Kwa  kawaida mtu hawezi kutoa upanga mdomoni, Tunafahamu Neno la Mungu ndio upanga wa Roho (soma waefeso 6:17) na pia waebrania  4: 12 inasema …“Maana Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo”.

Hivyo upanga huo ambao ni NENO lake ameuandaa tayari kwa ajili ya vita kwa watu wote wanaokwenda kinyume na mapenzi ya Mungu. Na kama anavyosema ni upanga ukatao kuwili anamaanisha kuwa ni upanga unaokata pande zote yaani watu walioko ndani ya kanisa na watu walioko nje ya Kanisa.

Jambo hili tutakuja kuliona jinsi Bwana alivyojifunua kwao(Kanisa la pili Pergamo) kwamba yeye ndiye mwenye ule upanga mkali ukatao kuwili…aliasema “anayajua matendo yao na kwamba watubu na wasipotubu  atakuja kufanya vita nao kwa huo upanga wa kinywa chake.(Ufunuo 2:16).

Kadhalika na kwa watu wa mataifa wasiomjua Mungu wao nao Bwana atakuja kufanya nao vita kwa huo upanga, jambo hili tutakuja kuliona katika ile sura ya 19:15 katika siku ile atakapokuja mara ya pili na watakatifu wake.

Utaona pia baada ya Yohana kuuona muonekana wa nje wa yule mtu alianguka chini kwa hofu na kutetemeka, Tunasoma ” 17 Nami nilipomwona, nalianguka miguuni pake kama mtu aliyekufa. Akaweka mkono wake wa kuume juu yangu, akisema, Usiogope, Mimi ni wa kwanza na wa mwisho,
18 na aliye hai; nami nalikuwa nimekufa, na tazama, ni hai hata milele na milele. Nami ninazo funguo za mauti, na za kuzimu. “

Ndipo baada ya hayo yule mtu akajitambulisha kwa tabia zake za ndani ambazo Yohana hakuziona kwa macho..nazo ni

1)yeye ni wa kwanza na wa mwisho,

2) aliye hai,aliyekuwa amekufa na sasa yu hai milele na milele na ambaye 

3) anazo funguo za Kuzimu.

Sasa kwa tabia hizo TATU Yohana ndipo alipojua kuwa yule MTU ni YESU KRISTO mwenyewe. Hivyo ule muonekano wa Nje ni msingi utakaotusaidi kuelezea  ujumbe na kuelewa utendaji kazi wa Yesu katika habari husika zinazofuata. Ni muhimu kuzingatia hivyo vipengele, mfano tunaweza kuona katika kila kanisa anaanza kwa kujitambulisha kwa kipengele kimoja wapo cha mwili wake au tabia zake.

Hivyo kwa ufupi Alichoonyeshwa Yohana ni mfano wa ile sanamu aliyoonyeshwa Nebukadreza juu ya zile Falme 4 zitakazokuja kutawala mpaka mwisho wa dunia. Na kwamba kila sehemu ya ile sanamu (Kichwa cha dhahabu, kifua cha fedha, kiuno cha shaba na miguu ya chuma) ilikuwa na maana, na ndio iliyounda msingi wa kuelewa undani wa kitabu cha Danieli katika sura za mbeleni.Kadhalika na hichi kitabu cha Ufunuo, sura hii ya kwanza (Ambayo Inayoonyesha muonekano na tabia za Yesu Kristo ) ni msingi wa sisi kuelewa ujumbe katika sura zinazofuata za kitabu cha Ufunuo.

Hivyo usikose mwendelezo wa sura zinazofuata..

Ubarikiwe sana.

Washirikishe na wengine habari hizi.

Kwa Mwendelezo >>Ufunuo: Mlango wa 2 Part 1.

Ikiwa utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara,  kwa njia ya whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255789001312. Na kama utapenda kwa njia ya E-mail basi tuandikie email yako katika boksi la maoni chini.


Mada Zinazoendana:

KWANINI YESU KRISTO ALIKUJA DUNIANI?

SIFA TATU ZA MUNGU

JE! HIZI ROHO SABA ZA MUNGU NI ZIPI?


Rudi Nyumbani

Print this post

CHUKIZO LA UHARIBIFU

Jina la Bwana wetu YESU KRISTO libarikiwe sana. Karibu tuongeze maarifa katika kulichambua Neno la Mungu leo tutajifunza juu ya chukizo la uharibifu, natumai ujumbe huu utakutoa sehemu moja ya kiroho hadi nyingine, sasa ili tuweze kwenda kwa uzuri ni vema uwe na biblia pembeni ili kukusaidia kufuatilia baadhi ya mistari tutakayokuwa tunaipitia katika somo hili.

Kwa kuanza ni vizuri tukifahamu nini maana ya “chukizo la uharibifu”: Kwa lugha nyepesi tunaposema chukizo la uharibifu ni sawasawa na kusema “chukizo linaloleta uharibifu” au “Chukizo linalopelekea uharibifu”..Kwahiyo hapo kuna mambo mawili, la kwanza ni CHUKIZO, na la pili ni UHARIBIFU. Sasa chukizo ni nini? Na uharibifu ni nini?.

CHUKIZO: Kwa tafsiri ya kibiblia hilo neno chukizo maana yake ni kuudhi/kuleta hasira, hususani pale panapohusishwa na uzinzi, Hivyo mambo yote yaliyokuwa yanafanywa na watu wa Mungu ambayo yalikuwa kinyume na sheria zake mfano kuabudu miungu mingine, kujichongea sanamu, kufanya uchawi, n.k. hayo yote mbele za Mungu yalijulikana kama MACHUKIZO (mambo ya kuudhi au kukasirisha).

Kwa mfano tunaweza kuona Bwana aliwaambia wana wa Israeli katika Kumbukumbu 18: 9-13 akisema:

“9 Utakapokwisha kuingia katika nchi akupayo Bwana, Mungu wako usijifunze kutenda kwa mfano wa MACHUKIZO ya mataifa yale.

10 Asionekane kwako mtu ampitishaye mwanawe au binti yake kati ya moto, wala asionekane mtu atazamaye bao, wala mtu atazamaye nyakati mbaya, wala mwenye kubashiri, wala msihiri,

11 wala mtu alogaye kwa kupiga mafundo, wala mtu apandishaye pepo, wala mchawi, wala mtu awaombaye wafu.

12 KWA MAANA MTU ATENDAYE HAYO NI CHUKIZO KWA BWANA; kisha ni kwa sababu ya hayo Bwana, Mungu wako, anawafukuza mbele yako.

13 Uwe mkamilifu kwa Bwana, Mungu wako”.

Unaona hapo mambo waliowafanya wafukuzwe (“mataifa yaliyokuwa Kaanani”) na kuondoshwa kabisa ni MACHUKIZO yao mbele za Mungu, hivyo Mungu akatangulia kuwaonya mapema watu wake kwamba watakapofika katika hiyo nchi ya Ahadi wasijaribu kutenda mfano wa mambo hayo. Kwani Watu wa mataifa walikuwa wana loga, wanaabudu miungu mingi, wanaabudu masanamu, wanapitisha watoto wao kwenye moto, wauaji, n.k. Kwasababu hiyo basi wana wa Israeli walionywa sana wakae mbali na hivyo vitu, kwani vitawasababisha wao nao yawapate yale yale yaliyowapata mataifa mengine.

UHARIBIFU: Kama tulivyoona hapo juu, sababu kubwa iliyowapelekea mataifa yale makubwa yafukuzwe na KUHARIBIWA kabisa haikuwa kwasababu ya kwamba Mungu anawachukia tu!au anawapenda Israeli kuliko wao hapana bali ni kwasababu ya machukizo yao na ndiyo ikawapelekea kuharibiwa na kutolewa katika ile nchi ya Kaanani na kupewa wana wa Israeli. Na kama tunavyojua siku zote kitu kikiwa kinachukiza mara kwa mara kinachofuata ni kuangamizwa au KUHARIBIWA kabisa.

Bwana aliwaaonya tena wana wa Israeli na kusema:

Mambo ya walawi 18: 24 “Msijitie unajisi katika mambo hayo hata mojawapo; kwa maana hizo taifa nitakazozitoa mbele zenu zimekuwa najisi kwa mambo hayo yote;

25 na hiyo nchi imekuwa najisi; kwa ajili ya hayo naipatiliza uovu wake juu yake, na hiyo nchi yatapika wenyeji wake na kuwatoa.

26 Kwa hiyo mtazishika amri zangu na hukumu zangu, wala msifanye MACHUKIZO hayo mojawapo; yeye aliye mzalia, wala mgeni aketiye kati yenu;

27 (kwa kuwa hao watu wa nchi wameyafanya MACHUKIZO HAYA YOTE, hao waliotangulia mbele zenu, na hiyo nchi imekuwa najisi;)

28 ili kwamba hiyo nchi isiwatapike na ninyi pia, hapo mtakapoitia unajisi, kama ilivyoitapika hiyo taifa iliyotangulia mbele yenu.

29 KWANI MTU AWAYE YOTE ATAKAYEFANYA MACHUKIZO HAYO MOJAWAPO, NAFSI HIZO ZITAKAZOFANYA ZITAKATILIWA MBALI NA WATU WAO.

30 Kwa ajili ya hayo yashikeni mausia yangu, ili kwamba msifanye kabisa desturi hizi ZICHUKIZAZO mojawapo, zilizotangulia kufanywa mbele zenu, wala msijitie unajisi katika mambo hayo; mimi ndimi Bwana, Mungu wenu.”

Unaona hapo, machukizo yote yaliyokuwa yanazungumiziwa mwisho wake yote yalipelekea UHARIBIFU kwa namna moja au nyingine kwa hilo taifa au mtu mmoja mmoja aliyeyafanya.. Sasa kumbuka vitu hivi kama uchawi, ulawiti, uuaji, uongo n.k. haya yote yalikuwa ni machukizo yanayoleta uharibifu lakini LIPO CHUKIZO MOJA, lililozungumziwa na BWANA YESU, na katika kitabu cha DANIELI, ambalo litakuja kusimama sehemu patakatifu na kuleta uharibifu mkubwa kwa watu wengi wa Mungu litakalosababisha kuwepo na dhiki kubwa ambayo haijawaki kutokea tangu ulimwengu kuwako, na ndilo litakalopelekea hata uharibifu wa dunia.

Kumbuka wakati wana wa Israeli walipokuwa wanaingia katika nchi ya Kaanani, Mungu hakuteua mahali popote katikati ya miji yao pa kuliweka jina lake, na kuwa sehemu takatifu, hivyo wakati huo wote waisraeli walipokuwa wanafanya machukizo Bwana aliwaharibu mara nyingine kwa kuwatia katika mikono ya maadui zao kama wafilisti na walipotubu Bwana aliwanyanyulia waamuzi ambao waliwaokoa na mikono ya maadui zao lakini hawakuwa wanaondolewa taifa lao. Lakini ulipofika wakati Bwana alipojiteulia mahali PATAKATIFU pake pa kuwekea Jina lake yaani YERUSALEMU, zamani za mfalme Daudi, mambo yalianza kubadilika, siku ile HEKALU LA MUNGU lilipokamilika kujengwa kwa mikono ya Sulemani mwana wa Daudi, Baraka na bila kusahau LAANA pia ziliongezwa makali, Na ndio maana Bwana alimwambia Sulemani baada ya kuijenga ile nyumba maneno haya..

1Wafalme 9: 6 “Bali mkighairi, mkaacha kunifuata, ninyi na watoto wenu, msizishike sheria zangu na amri zangu, nilizoziweka mbele yenu, TENA MKIENDA NA KUITUMIKA MIUNGU MINGINE NA KUIABUDU,

BASI NITAWAKATILIA ISRAELI MBALI NA NCHI HII NILIYOWAPA na nyumba hii niliyoitakasa kwa jina langu, nitaitupilia mbali na macho yangu, na Israeli watakuwa MITHALI NA NENO LA TUSI KATIKA MATAIFA YOTE.

8 Na ijapokuwa nyumba hii imetukuka namna hii, lakini kila apitaye atasituka na kuizomea; nao watasema, Kwa nini Bwana ameitenda nchi hii na nyumba hii mambo haya?

9 Na watu watajibu, Kwa sababu walimwacha Bwana, Mungu wao, aliyewatoa baba zao katika nchi ya Misri, wakashikamana na miungu mingine na kuiabudu na kuitumikia, basi ndiyo sababu Bwana ameleta mabaya haya yote juu yao”.

Unaona hapo?. Baada ya Mungu kuichagua YERUSALEMU, kama mahali pake patakatifu na HEKALU kama mahali atakapoweka Jina lake alitarajia muda wote Israeli wakae katika hali ya usafi wa hali ya juu kuliko hapo kwanza, kwamba wakifanya machukizo mbele za Patakatifu pa Mungu, wakatakatiliwa mbali, na kutawanywa katika mataifa yote, na watakuwa mithali kwa kila wawatazamao.

Lakini tukirudi katika kitabu cha Wafalme tunaona hawakuisikia hiyo sauti ya Mungu, badala ya kudumu katika usafi kwa Mungu wakaanza kidogo kidogo kuingiza ibada nyingine katika Israeli na katika nyumba ya Mungu iliyoko Yerusalemu, licha ya kwamba Mungu aliwatumia manabii wengi kuwaonya lakini hawakutaka kubadilika (Kuyaacha machukizo yao mbele za Mungu) ikapelekea Mungu kutamka UHARIBIFU WAO. Kama alivyoahidi katika NENO lake, pale Nebukadneza Mfalme wa Babeli Bwana alipomruhusu kwenda kuuteketeza mji wa Yerusalemu, na kuliharibu kabisa lile hekalu la Sulemani, wakauawa majemedari wengi wa Israeli kwa upanga, wengine njaa, na wengine magonjwa, Dhiki ilikuwa kubwa sana, wakachukuliwa utumwani na Israeli ikabaki kama ukiwa, Kutokana na MACHUKIZO waliyoyasimamisha wao wenyewe hivyo yakawapelekea UHARIBIFU MKUBWA namna hiyo.. Naamini kidogo kidogo utakua umeanza kuelewa nini maana ya chukizo la uharibifu.

2Mambo ya nyakati 36:14 “Na zaidi ya hayo wakuu wote wa makuhani, na watu, wakakosa mno sawasawa na MACHUKIZO YOTE YA MATAIFA; WAKAINAJISI NYUMBA YA BWANA ALIYOITAKASA KATIKA YERUSALEMU.

15 Naye Bwana, Mungu wa baba zao, akatuma kwao kwa mikono ya wajumbe wake, akiondoka mapema, na kutuma; kwa sababu aliwahurumia watu wake, na makao yake;

16 lakini waliwadhihaki wajumbe wa Mungu, na kuyadharau maneno yake, na kuwacheka manabii wake, HATA ILIPOZIDI GHADHABU YA BWANA JUU YA WATU WAKE, HATA KUSIWE NA KUPONYA.

17 Kwa hiyo akaleta juu yao mfalme wa Wakaldayo{Wa-babeli}, aliyewaua vijana wao kwa upanga nyumbani mwa patakatifu pao, asiwahurumie kijana wala mwanamwali, mzee wala mkongwe; akawatia wote mkononi mwake.

18 Na vyombo vyote vya nyumba ya Mungu, vikubwa kwa vidogo, na hazina za nyumba ya Bwana, na hazina za mfalme, na za wakuu wake; vyote pia akavileta Babeli.

19 WAKAITEKETEZA NYUMBA YA MUNGU, wakaubomoa ukuta wa Yerusalemu, wakayateketeza kwa moto majumba yake yote, WAKAVIHARIBU vyombo vyake vyote vya thamani.

20 Na wale waliookoka na upanga akawachukua mpaka Babeli; wakamtumikia yeye na wanawe hata kulipoingia milki ya Uajemi;

Tukio hili lililiathiri Taifa la Israeli kwa vizazi vingi, Kama ukifuatilia historia utaona kuwa Israeli halikuwahi kuwa tena taifa huru kwa muda wa miaka 2500, tangu ule wakati walipopelekwa Babeli mpaka juzi juzi tu mwaka 1948, ndio wamekuwa taifa huru tena, siku zote hizo walikuwa wanaishi kama wageni mahali popote walipopelekwa au kukaa. Na hata walipotoka Babeli walikuwa chini ya mataifa yaliyokuwa yanamiliki dunia kwa wakati huo. Unaweza ukaona ni MACHUKIZO MAKUBWA kiasi gani yaliyowasababishia kupitia uharibifu na adhabu kali kaisi hicho… Mungu ni Mungu mwenye WIVU hapendi mahali pake patakatifu panajisiwe kwa namna yoyote ile..

Na tunaona baada ya kutoka Babeli, Bwana aliwarehemu akawajalia kujenga tena hekalu la pili baada ya lile la kwanza lililotengenezwa na Sulemani kubomolewa na mfalme Nebukadneza wa Babeli. Kadhalika Mungu aliwaonya pia yale masalia ya wayahudi waliorudi wasifanye machukizo kama waliyoyafanya mababa zao. Mwanzo walitii lakini kilipopita kipindi Fulani walikengeuka, wakaanza kufanya mfano wa machukizo ya mataifa. (Kumbuka wakati huu Israeli ilikuwa haijiongozi yenyewe kama hapo kwanza) ilikuwa chini ya utawala wa wafalme wengine. Hivyo njia pekee shetani aliyoitumia kusimamisha machukizo katika nyumba ya Mungu kiurahisi sio kuwatumia wayahudi peke yake, bali alianza kuwatumia pia wafalme wa mataifa kwasababu wao ndio waliokuwa na nguvu juu ya taifa la Israeli,

Tukisoma katika kitabu cha Danieli tunaona Danieli akionyeshwa katika maono juu ya mfalme atakayenyanyuka katika utawala wa Umedi & Uajemi ambao ndio kwa wakati huo ulikuwa unatawala dunia, alionyeshwa kiongozi mkatili akilisimamisha chukizo la uharibifu tena katikati ya wayahudi na patakatifu na huyu hakuwa mwingine zaidi ya ANTIOKIA IV EPIFANE (Kumbuka mpaka Antiokia kuja kulitia unajisi hekalu ilikuwa ni matokeo ya kukengeuka kwa wana wa Israeli,mfano wasingeasi Bwana angewaepusha na hayo mambo) Tukisoma

Danieli 11: 31 Na wenye silaha watasimama upande wake, nao watapatia unajisi mahali patakatifu, ndiyo ngome, nao wataondoa sadaka ya kuteketezwa ya kila siku, NAO WATALISIMAMISHA CHUKIZO LA UHARIBIFU..

Kulingana na historia inavyoeleza, kiongozi huyu alinyanyuka na kuingia katika hekalu la Mungu na kufanya maasi yote ambayo hayapaswi kuwepo katika nyumba ya Mungu, aliweza kusitisha sadaka zote za kuteketezwa ambazo zilikuwa zinafanywa na makuhani katika nyumba ya Mungu, na kuiweka sanamu ya ZEU mungu ambayo ilikuwa inamwakilisha yeye, kadhalika akawa anatoa dhabihu ya viumbe najisi kwa wayahudi kama nguruwe katika madhabahu iliyokuwa ndani ya Hekalu la Mungu na kuwalazimisha wanywe damu zao hivyo viumbe, mambo ambayo yalikatazwa katika Torati ya Musa, hakuishia hapo tu, aliwaua wayahudi wengi sana na kuwakosesha kuabudu katika dini yao, hivyo ikawa ni machukizo makubwa sana mbele za Mungu…Lakini Mungu alikuja kumuua Antiokia, kwa mambo hayo lakini hekalu halikubomolowa,(Ni sadaka tu ya kuteketezwa ndio iliyokomeshwa) kwahiyo kile kitendo cha yeye kwenda pale pamoja na majeshi yake na kutia unajisi patakatifu pa Mungu, ni CHUKIZO LA UHARIBIFU,.kama Danieli alivyolinena.

Sasa huyu Antiokia alikuwa anatimiza sehemu ya kwanza ya chukizo la uharibifu juu ya Hekalu la pili..Sehemu ya pili ambayo ilipelekea tena Uharibifu mkubwa mpaka Hekalu la Mungu kubomolewa na wana wa Israeli kutawanya katika mataifa yote ilitokea mwaka wa 70WK. Wakati jeshi la Rumi chini ya jenerali TITO alipouzunguka mji wa Yerusalemu na kuuchoma moto, na kulibomoa hekalu na kuliteketeza kabisa, na kuwatawanya wana wa Israeli kutoka katika nchi yao, hii ikawa ni mara ya pili ya hekalu la Mungu kuteketezwa baada ya lile la kwanza lililobomolewa na mfalme Nebkadreza wa Babeli.

Na kama vile lile la kwanza lilivyoteketezwa kwasababu ya maovu na maasi ya wana wa-israeli kadhalika na hili la pili lilibomolewa kwasababu hiyo hiyo,? Tunasoma wana wa Israeli walianza kwa kumkataa Yohana mbatizaji kisha wakaja kumkataa BWANA YESU mwenyewe, na kibaya zaidi wakamsulibisha, Bwana aliwaambia katika Yohana 8: 24 “Kwa hiyo naliwaambieni ya kwamba mtakufa katika dhambi zenu; kwa sababu msiposadiki ya kuwa mimi ndiye, mtakufa katika dhambi zenu”..Na ni kweli hawakumsadiki Bwana, na ndio maana siku ile alipoukaribia mji wa Yerusaleu aliulilia na kusema.

Luka 19: 41 “Alipofika karibu aliuona mji, akaulilia,

42 akisema, Laiti ungalijua, hata wewe katika siku hii, yapasayo amani! Lakini sasa yamefichwa machoni pako.

43 Kwa kuwa siku zitakuja, adui zako watakapokujengea boma, likuzunguke; watakuzingira na kukuhusuru pande zote;

44 watakuangusha chini wewe na watoto wako ndani yako, wasikuachie jiwe juu ya jiwe, kwa sababu hukutambua majira ya kujiliwa kwako”.

Unaona hapo? Sababu ya kwanza iliyowapelekea wana wa Israeli mpaka kuharibiwa mji wao tena pamoja na Hekalu na jeshi la Rumi ni zile zile kwani waliwakataa manabii wa Mungu kwa kuwaua (soma Luka 13:34) na kuwasulibisha na zaidi ya yote walimkataa aliyemkuu wa uzima wakamkataa mfalme wao (ambaye ni Yesu) wakamkubali mfalme mwingine wa kidunia (KAISARI) na kumkiri hadharani kuwa huyo ndiye mfalme wao.

Yohana 19: 15 “Basi wale wakapiga kelele, Mwondoshe! Mwondoshe! Msulibishe! Pilato akawaambia, Je! Nimsulibishe mfalme wenu! Wakuu wa makuhani wakamjibu, Sisi hatuna mfalme ila Kaisari”.

Hivyo wakaendelea na maovu yao, pamoja na wafalme wao wa kipagani, Ndipo wakati wa mapatilizo ulipofika mji kuteketezwa na watu kuuawa na dhiki kubwa ikatokea. Lakini kabla ya huo wakati kufika Bwana alishawaonya wale waliokuwa tayari kumsikiliza kwamba watakapoona ishara Fulani (Yaani majeshi ya Rumi) kuuzunguka Yerusalemu waondoke katikati ya mipaka ya Yerusalemu. Hivyo wale waliomwamini Bwana Yesu na maneno yake (yaani Wakristo) waliepuka hiyo dhiki kwa kuondoka Yerusalemu lakini wale waliosalia waliangamia wote, Yerusalemu iligeuka kuwa ziwa la damu. Jeshi la Rumi liliwaua watu wote na kubomoa Hekalu la Mungu.

Na ndio maana Bwana alisema hivi.

Luka 21: 20 “Lakini, hapo mtakapoona mji wa Yerusalemu umezungukwa na majeshi, ndipo jueni ya kwamba UHARIBIFU wake umekaribia.

21 Ndipo walio katika Uyahudi na wakimbilie milimani, na walio katikati yake wakimbilie nje, na walio katika mashamba wasiuingie.

22 Kwa kuwa siku hizo ndizo za mapatilizo, ili yatimizwe yote yaliyoandikwa.

23 Ole wao wenye mimba na wanaonyonyesha katika siku hizo! Kwa kuwa kutakuwa na shida nyingi katika nchi, na hasira juu ya taifa hili.

24 Wataanguka kwa ukali wa upanga, nao watatekwa nyara na kuchukuliwa katika mataifa yote; na Yerusalemu utakanyagwa na Mataifa, hata majira ya Mataifa yatakapotimia”.

Kwahiyo yale maasi waliokuwa wanayafanya katika (nyumba ya Mungu) pamoja na kuwaua manabii wa Mungu kadhalika na kumkataa Masihi wao, ndio lililokuwa CHUKIZO lililopelekea UHARIBIFU wao.

Baada ya hapo wayahudi wote walitapanywa katika mataifa mengi duniani, pasipo kuwa na makao maalumu kama hapo mwanzo, lakini tunaona Bwana aliwakumbuka tena, akawahurumia mwaka 1948, pale Mungu alipowarudishia taifa lao tena. Na sasa wameshaanza kujitambua wao ni wakina nani mbele za Mungu ile neema imeshaanza kuwarudia kidogo kidogo Hivi karibuni wataenda kujenga HEKALU LA TATU, na hili litakuwa ni la mwisho. Maandalizi yote ya kulijenga yapo tayari, kinachongojewa ni kujengwa tu, na zile dhabihu walizokuwa wanatoa kama zamani, zitaanza kutolewa tena. Na mahali patakatifu pa Mungu patawekwa wakfu tena, Na Mungu ataikumbuka Israeli tena kama zamani.

 Lakini kumbuka shetani yupo katika kazi siku zote,..Alilokuwa analifanya nyuma ndilo atakalokuja kulifanya katika siku za mwisho, tena na zaidi ya pale. Kumbuka “machukizo ya uharibifu” yote ya nyuma yaliyotangulia yalikuwa ni kivuli tu cha CHUKIZO LA UHARIBIFU hasaa litakalokuja katika siku hizi za mwisho.

Bwana Yesu alisema katika Mathayo 24: 15 “Basi hapo mtakapoliona chukizo la uharibifu, lile lililonenwa na nabii Danieli, limesimama katika patakatifu (ASOMAYE NA AFAHAMU),

16 ndipo walio katika Uyahudi na wakimbilie milimani;

17 naye aliye juu ya dari asishuke kuvichukua vitu vilivyomo nyumbani mwake;

18 wala aliye shambani asirudi nyuma kuichukua nguo yake.

19 Ole wao wenye mimba na wanyonyeshao siku hizo!

20 Ombeni, ili kukimbia kwenu kusiwe wakati wa baridi, wala siku ya sabato.

21 KWA KUWA WAKATI HUO KUTAKUWAPO DHIKI KUBWA, AMBAYO HAIJATOKEA NAMNA YAKE TANGU MWANZO WA ULIMWENGU HATA SASA, WALA HAITAKAKUWAPO KAMWE.

22 Na kama siku hizo zisingalifupizwa, asingeokoka mtu ye yote; lakini kwa ajili ya wateule zitafupizwa siku hizo”.

Kumbuka kutakuwepo CHUKIZO LA UHARIBIFU la tatu na la mwisho litakalokuja kusimamishwa huko Yerusalemu katika Hekalu la TATU. Wakati ule wana wa Israeli kwasababu ya makosa yao Ikasababisha Nebukadneza kuja kuliteketeza hekalu la kwanza, na kwasababu ya makosa yao tena ya kumkataa Masihi ndipo Jeshi la Rumi likaja kuuteketeza mji na Hekalu la pili. Kadhalika na kwa makosa yao tena ndiyo yatakayokuja kupelekea Mpinga-kristo kunyanyuka na kupatia unajisi patakatifu na kuleta uharibifu, pamoja na dhiki kuu katika hekalu la tatu.

Sasa kosa lenyewe litakuwa ni lipi?

Danieli alionyeshwa kosa hilo, tunasoma katika 

Danieli 9:26 “27 NAYE {mpinga-kristo} ATAFANYA AGANO THABITI NA WATU WENGI KWA MUDA WA JUMA MOJA; na kwa nusu ya juma hiyo ataikomesha sadaka na dhabihu; na mahali pake litasimama CHUKIZO LA UHARIBIFU; na hivyo, hata ukomo, na ghadhabu iliyokusudiwa imemwagwa juu yake mwenye kuharibu”.

Kwahiyo unaona hapo kuna AGANO ambalo mpinga-kristo ataingia na watu wengi, na hawa watu si wengine zaidi ya wayahudi ambao wataingia agano hilo na huyu mpinga-kristo ambalo litakuwa kwa kipindi cha miaka 7, agano hili litahusisha kupewa nafasi mpinga-kristo katika Hekalu la Mungu, jambo ambalo Mungu alishalikataza kwamba kisionekane kitu chochote katika hekalu la Mungu isipokuwa wayahudi tu tena makuhani wa uzao wa Walawi, lakini hawa wayahudi baadhi watampa heshima mpinga kristo wakijua tu ni mtu anayeheshimika duniani, hivyo anastahili kuwa na sehemu katika hekalu la Mungu, kama tu wale wa wayahudi wa kipindi cha Bwana Yesu walivyompa Heshima Kaisari, lakini hawatajua kama Yule ndio mpinga-kristo mwenyewe (ambaye atakuwa ni PAPA wa wakati huo) , na hiyo itapelekea kuwa CHUKIZO KUU kuliko yote, na ndipo Mungu ataruhusu hili agano livunjwe, lakini Yule mpinga-kristo ataghadhibika na kuleta dhiki kuu, ambayo haijawahi kuwako tangu ulimwengu kuumbwa.

Na ndio maana biblia inamtaja..katika

 2Thesalonike 2: 3 “Mtu awaye yote asiwadanganye kwa njia yo yote; maana haiji, usipokuja kwanza ule ukengeufu; akafunuliwa yule mtu wa kuasi{MPINGA-KRISTO}, mwana wa uharibifu;

4 yule mpingamizi, ajiinuaye nafsi yake juu ya kila kiitwacho Mungu ama kuabudiwa; hata yeye mwenyewe KUKETI KATIKA HEKALU LA MUNGU, akijionyesha nafsi yake kana kwamba yeye ndiye Mungu.

5 Je! Hamkumbuki ya kuwa wakati nilipokuwapo pamoja nanyi naliwaambieni hayo?

6 Na sasa lizuialo mwalijua, yule apate kufunuliwa wakati wake.

7 Maana ile siri ya kuasi hivi sasa inatenda kazi; lakini yuko azuiaye sasa, hata atakapoondolewa.{kumbuka bibi-arusi wa Kristo ndiye azuiaye mpaka atakapoondolewa kwa kwenda kwenye unyakuo} 

8 Hapo ndipo atakapofunuliwa yule asi, ambaye Bwana Yesu atamwua kwa pumzi ya kinywa chake, na kumwangamiza kwa ufunuo wa kuwapo kwake;

9 yule ambaye kuja kwake ni kwa mfano wa kutenda kwake Shetani, kwa uwezo wote, na ishara na ajabu za uongo;

10 na katika madanganyo yote ya udhalimu kwa hao wanaopotea; kwa sababu hawakukubali kuipenda ile kweli, wapate kuokolewa”.

Hivyo huyu mpinga-kristo ataleta dhiki duniani kwa kuihimiza chapa ya mnyama kutenda kazi,ataua wayahudi wengi sana, japokuwa sio wote kwasababu wapo ambao wataiepuka ile dhiki kwa kupitia ile injili ya manabii wawili (Ufunuo 11),na kwenda kujificha hawa watakuwa ni wale wayahudi 144,000 wanaozungumziwa katika (Ufunuo 7), lakini waliosalia wote wataungana na wale wanawali wapumbavu (yaani watu wa mataifa ambao hawakwenda kwenye unyakuo) kwa pamoja watapitia dhiki kuu ambayo itakudumu kwa muda wa miaka mitatu na nusu. Kama inavyosema katika Danieli:

Danieli 12:11 “Na tangu wakati ule ambapo sadaka ya kuteketezwa ya daima itaondolewa, na hilo chukizo la uharibifu litakaposimamishwa, itapata siku elfu na mia mbili na tisini”.

Kwahiyo hilo chukizo ni pale wayahudi watakapokuja kuingia agano na mpinga-Kristo, ambaye atataka kuja kuabudiwa kama Mungu..Hayo ni Machukizo makubwa ambayo yatasababisha Uharibifu kwa Wayahudi na kwa Dunia nzima, na kwa mpinga-kristo mwenyewe kwa kupatia unajisi patakatifu pa Mungu.( kumbuka pia Msikiti wa OMAR(Al-aqsa) uliopo pale Yerusalemu sio chukizo la uharibifu kama inavyodhaniwa na wengi .)

Kwahiyo ndugu hili chukizo la uharibifu sio tu kwa Yerusalemu peke yake hapana hata kwa KANISA, maana Kanisa ni HEKALU la Mungu biblia inasema hivyo. Na hili chukizo pia limesimama patakatifu pa Mungu, mahali ambapo pangepaswa YESU KRISTO peke yake aabudiwe, pamekuwa sehemu ya kuabudiwa sanamu pamoja na wanadamu. Bwana anasema Ufunuo 18: 4 “……..Tokeni kwake, enyi watu wangu, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake. Kwa maana dhambi zake zimefika hata mbinguni, na Mungu amekumbuka maovu yake”.

Tukijua kuwa tunaishi katika siku za hatari ni wakati wa kujiweka sawa, je! Bwana akija leo utaenda nae kwenye unyakuo?. Umeamini na kubatizwa?, je! wewe Ni miongoni mwa watakatifu?. Kama sivyo fanya hima katika muda huu wa nyiongeza tuliopewa. Weka mambo yako sawa siku ile isije ikakujia kama mwivi.

Ubarikiwe sana.

Print this post

JE! UMEYABATILISHA MAMBO YA KITOTO?

1Wakoritho 13: 11 “Nilipokuwa mtoto mchanga, nalisema kama mtoto mchanga, nalifahamu kama mtoto mchanga, nalifikiri kama mtoto mchanga; tokea hapo nilipokuwa mtu mzima, nimeyabatilisha mambo ya kitoto”.
 
Katika maisha ya kawaida, mwanadamu ni lazima apitie katika hatua hizi mbili; UTOTO na UTU UZIMA. Na kila hatua ni lazima iwe na uongozi juu yake, Kwamfano mtoto mdogo hawezi kujiongoza mwenyewe kwasababu akili yake haijakomaa kuweza kutambua jema na baya au kupambanua kanuni za maisha hivyo ni lazima aandaliwe na mzazi wake au mlezi wake kanuni fulani za kufuata aidha apende au asipende kwake huyo zinakuwa ni sheria na amri, na ndio maana tunaweza kuona mtoto anapofikisha umri fulani labda miaka 6/7, anapelekewa shule sio kwa mapenzi yake, hapana, pia analazimishwa kuamshwa asubuhi kila siku ili aende shule na tunafahamu hakuna mtoto anayependa kuamshwa asubuhi apige mswaki na kwenda shule, yeye atatamani tu acheze cheze na kurukaruka,
 
Kadhalika akirudi baadaye nyumbani, atalazamishwa alale mchana, atalazimishwa aoge, atalazimishwa afanye homework,atachaguliwa nguo za kuvaa, na wakati mwingine atachaguliwa mpaka na marafiki wa kucheza naye, n.k. Hivi vyote atafanya tu hata kama hataki, na wakati mwingine akikosea mojawapo ya hizo kanuni alizowekewa itamgharimu adhabu. Hivyo ukichunguza kwa undani utaona kuwa sio kwamba Yule mtoto anatimiza zile sheria kwa kupenda la! Bali anafanya vile kwa kutimiza tu matakwa ya baba / mama yake basi, laiti angepewa uhuru kidogo tu! Asingedhubutu kufanya mojawapo ya hayo, angeenda kufanya mambo yake mengi kuzurura zurura tu.
 
TABIA YA MTU MZIMA.
 
Lakini Yule mtoto atakapokuwa mtu mzima kidogo kidogo mabadiliko yataanza kutokea ndani yake, ataanza kuona umuhimu wa yeye kuamka asubuhi na mapema na kupiga mswaki mwenyewe, na umuhimu wa kwenda shule , ataona umuhimu wa kuoga, ataona umuhimu wa kuwa na marafiki wazuri, n.k. Lakini ni kwasababu gani anafanya hivyo?. Ni kwasababu ameshakuwa mtu mzima na anajua kufanya hivyo ni kwa faida yake mwenyewe na sio kwa faida ya mzazi. Na hiyo ndiyo dalili kubwa ya kuonyesha kuwa mtu huyo amekuwa. Kwasababu ile sheria na maagizo aliyopewa na wazazi wake sasa anayatimiza mwenyewe ndani ya moyo wake pasipo kushurutishwa. Na ndipo mzazi anapoona sababu ya kumwamini na kumwacha huru kabisa kabisa ayaongoze maisha yake mwenyewe.
 
Mfano mwingine tunaweza tukajifunza kwa mwanafunzi: alipokuwa shule ya msingi ni tofauti na atakapokuwa chuo kikuu, kule nyuma alikuwa analazimishwa kuwepo shule kila siku alfajiri, ahudhurie kila kipindi cha darasani, alilazimshwa avae sare, alichapwa alipokosea, alikaguliwa notes alizoandika n.k.. Lakini alipofika chuo hakuna tena sheria ya kumwambia aamke alfajiri kila siku aende chuo, ni kwasababu gani? Ni kwasababu chuo kinatambua kwamba Yule mtu anajielewa, hivyo hata asipohudhuria leo atakuwa na sababu za msingi za kutokufanya hivyo tofauti na alipokuwa shule ya msingi, mfano angepewa uhuru tu! Angeutumia katika michezo na utoro, kadhalika pia akiwa chuo hapewi sare, hashikiwi kiboko kulazimishwa kusoma, hakaguliwi notes n.k. lakini japokuwa hakuna sheria zote hizo, mwisho wa siku utakuta Yule mwanafunzi anafaulu. Unaona hapo? hayo yote haimaanishi kuwa chuo hakikuwa na sheria hapana, kilikuwa nayo sana tu, bali kimemweka huru mbali na ile sheria kwasababu kilitambua aliyefika chuo ameshajitambua vya kutosha na anajua jukumu lake kama mwanafunzi.
 
Kadhalika na katika KANISA LA MUNGU nalo pia limepitia katika hatua zote mbili: UTOTO na UTU UZIMA. Hatua ya utoto ni pale Mungu alipolizaa kanisa kwa mara ya kwanza kule jangwani, hivyo kama lilikuwa ni changa ni dhahiri kuwa lingehitaji kupewa sheria ya kuliongoza kwasababu halijaweza bado kupambanua mema na mabaya. Na ndio tunaona sheria/ Torati ilikuja na zile amri zote kutolewa kwa mkono wa Musa na kupewa watu, kwamba waishi katika hizo. Na kama tunavyojua sheria kwa mtoto inakuwa ni AMRI na sio OMBI, kadhalika na hawa nao (kanisa-jangwani waisraeli) ilikuwa ni AMRI kuzitimiza sheria za Mungu zilizotolewa, ndio maana ilikuwa ni amri mtu asiibe, asizini, asiue, aishike sabato, asiabudu sanamu n.k.na kwa yeyote asiyefanya aliadhibiwa vikali. Na kwasababu walikuwa ni watoto walifanya vile kwaajili ya kumridhisha tu baba yao (MUNGU), Walitimiza zile sheria sio kwasababu wanapenda hapana, ni kwasababu baba yao hapendi dhambi, laiti wangeachiwa uhuru kidogo wasingezishika.
 
Lakini ulipofika wakati wa KANISA LA MUNGU KUKUA, Ilipasa zile sheria ziingizwe ndani ya moyo wa kanisa ili zitimizwe kwa mapenzi ya mtu mwenyewe na sio mapenzi ya Mungu na bila shuruti. Kama biblia ilivyotabiri zamani za manabii tukisoma.
 
Yeremia 31: 31 “Angalia, siku zinakuja, asema Bwana, nitakapofanya agano jipya na nyumba ya Israeli, na nyumba ya Yuda.
32 Si kwa mfano wa agano lile nililolifanya na baba zao, katika siku ile nilipowashika mkono, ili kuwatoa katika nchi ya Misri; ambalo agano langu hilo walilivunja, ingawa nalikuwa mume kwao, asema Bwana.
33 Bali agano hili ndilo nitakalofanya na nyumba ya Israeli, baada ya siku zile, asema Bwana; NITATIA SHERIA YANGU NDANI YAO, NA KATIKA MIOYO YAO NITAIANDIKA; nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.
34 Wala hawatamfundisha kila mtu jirani yake, na kila mtu ndugu yake, wakisema, Mjue Bwana; kwa maana watanijua wote, tangu mtu aliye mdogo miongoni mwao hata aliye mkubwa miongoni mwao, asema Bwana; maana nitausamehe uovu wao, wala dhambi yao sitaikumbuka tena”.
 
Jambo hili lilikuja kutimia siku ya PENTEKOSTE, pale ROHO wa Mungu alipomiminwa juu ya mioyo ya watu kwa mara ya kwanza na kuwafanya wavuke daraja la utoto na kuingia katika daraja la UTU UZIMA. Sasa kuanzia huo wakati Roho alipomshukia mtu, kitu cha kwanza alichokuwa anafanya ni kuiingiza ile sheria ndani ya moyo wake, kiasi kwamba Yule mtu ile sheria anakuwa anaitimiza kwa mapenzi yake mwenyewe na sio kwa mapenzi ya Mungu. Kama vile mwanafunzi aliyeko chuo anasoma kwa mapenzi yake na sio kwa mapenzi ya Baba yake au mama yake tofauti na alivyokuwa akifanya shule ya msingi. Hicho ndicho alichokifanya Roho Mtakatifu siku ya Pentekoste. Na ndio anachoendelea kukifanya mpaka sasa hivi.
 
Sasa kuanzia ule wakati wote walioshukiwa na Roho wa Mungu, wakawa hawazini, sio kwasababu Mungu kawakataza bali ni kwasababu waliona ni kwa faida yao wenyewe, wakawa hawaabudu sanamu sio kwasababu Mungu kawakataza hapana bali ni kwasababu wanajua Mungu pekee ndiye anayestahili kuabudiwa, wakawa wanaomba sio kwasababu Mungu kawaagiza lakini kwasababu waliona umuhimu wa kuomba kama Mkristo ili kuepukana na majaribu, hawakuishika sabato kama amri, kwamba tumwabudu Mungu tu katika siku fulani, hapana bali sabato yao ilikuwa kila siku, kwasababu walijua Mungu haabudiwi katika siku Fulani bali katika Roho na Kweli.Kadhalika na zile sheria zote walizopewa walipokuwa wachanga walikuwa wanazitimiza pasipo AMRI bali kwa moyo na kwa uelewa. Kwasababu hiyo basi Mungu akawacha huru kabisa mbali na SHERIA na TORATI. Na ndio maana biblia inasema:
 
Wagalitia 5: 18 “Lakini mkiongozwa na Roho, hampo chini ya sheria”. Na pia inasema…
Warumi 8: 2 “Kwa sababu sheria ya Roho wa uzima ule ulio katika Kristo Yesu imeniacha huru, mbali na sheria ya dhambi na mauti”.
Warumi 8: 4 “ili maagizo ya torati yatimizwe ndani yetu sisi, tusioenenda kwa kufuata mambo ya mwili, bali mambo ya roho”.
 
Kwahiyo unaona hapo? Umuhimu wa kuwa na Roho Mtakatifu?..Ni kukufanya wewe utoke katika hali ya utoto wa kiroho(utumwa) na uingie katika hali ya utu uzima(Uhuru) na hiyo ndiyo neema. Ukiona mtu pale unapomuuliza ni kwanini huzini, au huibi? Na anakwambia ni kwasababu Mungu kanikataza, moja kwa moja unajua huyo bado ni mtoto yupo chini ya Sheria hata kama atajifanya yupo chini ya neema. Ukiona mtu anakwambia mimi nashikilia siku moja ya kuabudia sabato, unajua huyo naye yupo chini ya sheria ya utoto, au mtu akikuambia mimi sivai vimini, sinywi pombe, sivuti sigara kwasababu Mungu kakataza, ujue huyo pia ni mtoto bado hajawekwa huru na sheria ya dhambi, Ukiona mtu anasema mimi siabudu sanamu kwasababu amri ya 2 inasema hivyo, unajua kabisa huyo bado ni mtoto Roho wa Mungu bado hajamfanya kuwa huru nk….
 
Lakini wale wote waliowekwa huru na ROHO, hawataona mzigo wowote kuishi maisha ya utakatifu wataona kutokuzini, kutokuvaa vimini, kutokuweka make-up, kutokuvaa suruali, kutokusengenya, kutoiba, kutokwenda disco, n.k. wataona kuwa hayo ni majukumu yao na ni kwa faida ya Roho zao na sio kwa faida ya Mungu, au sio kwasababu Mungu kawaambia. Watafanya yote yawapasayo kufanya iwe ni Mungu kawaagiza, au hajawaagiza.. Na hiyo ndio DALILI ya mtu kuwa amepokea kweli kweli Roho Mtakatifu…Utakatifu anautimizwa kwa kupenda na sio kwa maagizo Fulani.
 
Warumi 8: 9 “Lakini ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu, ninyi hamwufuati mwili; bali mwaifuata roho. Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wake”.
 

Hivyo ndugu, na wewe upo katika uchanga au utu uzima?. Umejazwa Roho Mtakatifu au bado unaongozwa na dini?. Tafuta Roho Mtakatifu kumbuka Roho Mtakatifu ndio muhuri wa Mungu (Waefeso 4:30) pasipo huyo hakuna UNYAKUO.

Ubarikiwe sana.


Mada Nyinginezo:

JIRANI YAKO NI NANI?

UMUHIMU WA KUISHI MAISHA YAMPENDEZAYO MUNGU SASA.

JIHADHARI NA ROHO ZIDANGANYAZO

JE! SISI NI WAFALME NA MAKUHANI KWA NAMNA GANI?

PETRO ALIAMBIWA NA BWANA YESU UKIONGOKA WAIMARISHE NA NDUGU ZAKO. JE! KUONGOKA MAANA YAKE NINI?


Rudi Nyumbani

Print this post

Nilipokuwa mtoto mchanga, nalisema kama mtoto mchanga

Licha ya kuwa na INJILI YA MSALABA,ambayo ndio kiini cha kila mwanadamu ipo injili nyingine pia ijulikanayo kama INJILI YA MILELE, hii ni tofauti na injili ya msalaba. Injili ya msalaba yenyewe inatangaza wokovu kwa mwanadamu tu, kwa kupitia mmoja naye ni YESU KRISTO BWANA wetu. Kwahiyo injili nyingine yeyote inayodai kumkomboa mwanadamu na haimweki Bwana Yesu kama kiini cha injili yenyewe, basi injili hiyo ni batili, kwasababu yeye pekee ndiye Njia, kweli na uzima, hakuna mtu yeyote atakayemwona Mungu, pasipo kupitia kwake yeye biblia inasema hivyo(Yohana 14:6).. Kwahiyo zipo injili nyingi zinazodai zinaweza kumkomboa mwanadamu lakini kati ya hizo ni moja tu itakayoweza kumkomboa mwananadau! Nayo ni Kwa kupitia Yesu Kristo, na ndio maana Mtume Paulo alisema|:
 
2Wakoritho 11: 4 “Maana yeye ajaye akihubiri Yesu mwingine ambaye sisi hatukumhubiri, au mkipokea roho nyingine msiyoipokea, au INJILI NYINGINE msiyoikubali, mnatenda vema kuvumiliana naye!”
 
Unaona hapo? Biblia inasema kuna Yesu mwingine, roho mwingine na injili nyingine tofauti na ile iliyohubiriwa na mitume. Kwahiyo injili yoyote inayohusishwa na ukombozi wa mwanadamu inapaswa imlenge YESU KRISTO ALIYESULIBIWA,akafa na kufufuka kama kiini cha Ukombozi wenyewe, kwa asilimia mia yeye peke yake na sio pamoja mtu mwingine.
 
Lakini leo kwa ufupi tutaitazama INJILI YA MILELE ambayo ipo na imezungumziwa katika biblia..kama tunavyosoma katika;
Ufunuo 14: 6 “Kisha nikaona malaika mwingine, akiruka katikati ya mbingu, mwenye INJILI YA MILELE, awahubiri hao wakaao juu ya nchi, na kila taifa na kabila na lugha na jamaa,
7 akasema kwa sauti kuu, Mcheni Mungu, na kumtukuza, kwa maana saa ya hukumu yake imekuja. Msujudieni yeye aliyezifanya mbingu na nchi na bahari na chemchemi za maji”.
 
Sasa hii injili ya milele ni ipi?
 
Kama jina lake lilivyo “Milele” inamaana kuwa ni injili ambayo Ipo milele yote, ilikuwepo kabla ya mwanadamu kuumbwa, ipo sasa, na itaendelea kuwepo milele na milele, Kumbuka INJILI YA MSALABA ilikuwa na mwanzo, na itakuwa na mwisho, mwanzo wake ilikuwa ni Kalvari, na mwisho wake itakuwa katika Unyakuo. Baada ya hapo hakutakuwa na nafasi tena ya ukombozi, kwasababu mlango wa neema utakuwa umefungwa. Kitakachokuwa kimebaki ni ile ile injili ambayo ilikuwepo milele na milele.
 
Na ndio maana ukisoma mstari huo hapo juu utaona kuwa yule malaika(mjumbe) anapita kuitangaza hiyo injili ambapo kwa wakati huo unyakuo wa kanisa utakuwa umeshapita na mlango wa neema ya kuokolewa utakuwa umefungwa kwa watu wa mataifa.
 
Kwahiyo injili hii ni tofauti na ya msalaba tuliyonayo sasa, hii ya msalaba tunaifahamu kwa “kuhubiriwa”. Hatuwezi kuifahamu pasipo kuhubiriwa ndio maana biblia inasema katika;
 
Warumi 10: 13 “kwa kuwa, Kila atakayeliitia Jina la Bwana{YESU KRISTO} ataokoka.
14 Basi wamwiteje yeye wasiyemwamini? Tena wamwaminije yeye wasiyemsikia? TENA WAMSIKIEJE PASIPO MHUBIRI?
15 Tena wahubirije, wasipopelekwa? Kama ilivyoandikwa, Ni mizuri kama nini miguu yao wahubirio habari ya mema!{INJILI YA MSALABA}”
 
Kwahiyo unaona hapo, ni lazima awepo mtu wa kuihubiri ndipo watu waokolewe.
 
Tofauti na ilivyo INJILI YA MILELE. Injili hii haisambazwi kwa kuhubiriwa na mtu yeyote, Ni Mungu mwenyewe anaiweka ndani ya mtu, katika eneo maalumu la moyo wa mwanadamu linaloitwa “DHAMIRA”..ambayo kila mtu anazaliwa nayo. Na inafanya kazi ya kuhukumu njia zote mbaya zinazokwenda kinyume na mapenzi ya Mungu ndani ya mtu..Na Injili hii haipo tu kwa wanadamu, ilikuwepo hata kwa malaika, kwasababu ni ya milele, ilikuwepo huko enzi na enzi, ipo na itakuwepo.
 
Kwahiyo sasa kitendo tu cha mtu kuwa mwanadamu, tayari moja kwa moja kuna kitu ndani yake kitakuwa kinamshuhudia mambo yanayofaa na yasiyofaa, bila hata kuhubiriwa au na mtu yeyote, au kukumbushwa na mtu yeyote, kwamfano, kila mtu anafahamu kuwa uuaji sio sawa, iwe anayo hofu ya Mungu au hana hofu ya Mungu, kila mtu anafahamu kuwa dhuluma ni mbaya, hata kama sheria isingesema hivyo, ndani ya moyo wake dhamira inamuhubiria kuwa kitendo hicho ni kibaya, Kadhalika haihitaji kuifahamu biblia kujua kuwa uonevu ni makosa, wizi ni makosa, utukanaji, ubakaji, rushwa ni makosa hayo yote hata kama mtu hajawahi kumsikia Mungu, au chochote kinachoitwa Mungu anajua kabisa hayo mambo hayafai kufanya, pia haihitaji kwenda katika vyuo vya biblia kutambua kuwa kulala na ndugu yako wa damu ni makosa, kadhalika na ushoga au usagaji ni makosa, utajikuta tu wewe mwenyewe unachukia kufanya hivyo au unalipinga hilo wazo ndani yako pale linapokuja kwasababu unajua kabisa kuwa hayo ni makosa. Sasa hiyo ndio inayoitwa INJILI YA MILELE, Mungu anayoihubiri ndani ya moyo wa mtu. Na ndiyo hiyo siku za mwisho itakuja kukumbushwa kwa watu, wamche Mungu.wakati huo unyakuo utakuwa umeshapita.
 
Kwahiyo usidhani kuwa wale watu ambao hajasikia habari za YESU(Injili ya msalaba) mahali popote, hawatahukumiwa. Hapana Watahukumiwa tu kama wale wengine kwa injili hiyo. Watu wa kipindi cha Nuhu hawakuwa na sheria waliyopewa na Mungu kama watu wa Musa na kuendelea,Na ndio maana Mtume Paulo alieleza habari za watu hawa kama tunavyosoma katika…
 
Warumi 1: 17 Kwa maana haki ya Mungu inadhihirishwa ndani yake, toka imani hata imani; kama ilivyoandikwa, Mwenye haki ataishi kwa imani.
18 Kwa maana GADHABU YA MUNGU imedhihirishwa kutoka mbinguni juu ya uasi wote na uovu wa wanadamu waipingao kweli kwa uovu.
19 Kwa kuwa MAMBO YA MUNGU YANAYOJULIKANA YAMEKUWA DHAHIRI NDANI YAO, KWA MAANA MUNGU.
20 Kwa sababu mambo yake yasiyoonekana tangu kuumbwa ulimwengu yanaonekana, na kufahamika kwa kazi zake; YAANI, UWEZA WAKE WA MILELE NA UUNGU WAKE; hata wasiwe na UDHURU;
21 kwa sababu, walipomjua Mungu hawakumtukuza kama ndiye Mungu wala kumshukuru; bali walipotea katika uzushi wao, na mioyo yao yenye ujinga ikatiwa giza.
22 Wakijinena kuwa wenye hekima walipumbazika;
23 wakaubadili utukufu wa Mungu asiye na uharibifu kwa mfano wa sura ya binadamu aliye na uharibifu, na ya ndege, na ya wanyama, na ya vitambaavyo.
24 Kwa ajili ya hayo Mungu aliwaacha katika tamaa za mioyo yao, waufuate uchafu, hata wakavunjiana heshima miili yao.
25 Kwa maana waliibadili kweli ya Mungu kuwa uongo, wakakisujudia kiumbe na kukiabudu badala ya Muumba anayehimidiwa milele. Amina.
26 Hivyo Mungu aliwaacha wafuate tamaa zao za aibu, hata wanawake wakabadili matumizi ya asili kwa matumizi yasiyo ya asili;
27 wanaume nao vivyo hivyo waliyaacha matumizi ya mke, ya asili, wakawakiana tamaa, wanaume wakiyatenda yasiyopasa, wakapata nafsini mwao malipo ya upotevu wao yaliyo haki yao.
28 Na kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wayafanye yasiyowapasa.
29 Wamejawa na UDHALIMU, UOVU na TAMAA na UBAYA; wamejawa na HUSUDA, na UUAJI, na FITINA, na HADAA; watu wa NIA MBAYA, wenye KUSENGENYA,
30 wenye KUSINGIZIA, wenye KUMCHUKIA MUNGU, wenye JEURI, wenye KUTAKABARI, wenye MAJIVUNO, wenye KUTUNGA MABAYA, WASIOTII WAZAZI WAO,
31 wasio na UFAHAMU, wenye KUVUNJA MAAGANO, WASIOPENDA JAMAA ZAO, WASIO NA REHEMA;
32 ambao wakijua sana hukumu ya haki ya Mungu, ya kwamba wayatendao hayo wamestahili mauti, wanatenda hayo, wala si hivyo tu, bali wanakubaliana nao wayatendao.
 
Umeona hapo ndugu, biblia inasema wakijua kabisa watendao mambo kama hayo wamestahili mauti lakini bado wanayatenda. Dhamira zao zikiwashuhudia ndani kuwa wanayoyafanya sio sahihi lakini wanaendelea kuyafanya, Na wewe je! Ambaye upo kwenye dhambi utahitaji mhubiri siku moja aje kukuthibitishia kwenye biblia kwamba, uvutaji sigara ni dhambi, au uasherati ni dhambi?? Angali ndani ya moyo wako dhamira inakushuhudia kabisa unachofanya ni makosa?..hakika unaweza usilione lakini fahamu kuwa hukumu inakungojea.!
 
Wewe unayevaa vimini, na kutembea nusu uchi barabarani unasema Mungu haangalii mavazi lakini moyo wako unakuambia kabisa hayo ni makosa unayoyafanya na bado unaweka moyo mgumu, wewe unayevaa suruali,unayepaka wanja, na kupaka lipstick, na kuvaa wig na hereni, Hukumu ipo mbeleni dada!, wewe unayesengenya, wewe ambaye ni shoga, wewe unayejisaga, wewe unayetoa mimba, wewe uliye mwasherati, wewe uliye mlevi, wewe unayetazama pornography, wewe unayefanya masturbation, wewe unayeabudu sanamu za watakatifu waliokufa zamani angalia biblia inavyokuambia hapo juu < wakaubadili utukufu wa Mungu asiye na uharibifu kwa mfano wa sura ya binadamu aliye na uharibifu(sanamu), na ya ndege, na ya wanyama, na ya vitambaavyo >..Unaona unajua kabisa Mungu hawezi kufananishwa na mfano wowote wa kinyago cha kuchonga lakini wewe bado unakwenda kuvipiga magoti na kuviabudu..
 
2Wakorintho 6: 16 inasema “Tena pana mapatano gani kati ya hekalu la Mungu na sanamu?”..
 
Lakini biblia inaendelea kusema kwa jinsi utakavyozidi kuweka moyo wako mgumu, kuna kipindi kitafika Mungu anakuacha uendelee hivyo hivyo kwasababu umekataa kuitii hiyo sauti inayosema ndani yako, mpaka ile siku ya hukumu ije na utaingia kuzimu!! Alisema “”28 Na kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wayafanye yasiyowapasa”.
Kwahiyo dada/kaka hukumu ya Mungu haikwepeki hata uwe nje ya kanisa, njia pekee ni kujisalimisha maisha yako kwa BWANA YESU ambaye yeye ndiye aliyetoa uhai wake ili akuokoe, Tubu geuka, ukapewe uwezo wa kushinda dhambi. Muda umekwenda kuliko unavyodhani, na Injili ya msalaba sio ya milele utafika wakati utatamani uingie utakosa, muda ndio huu, mpe Bwana maisha yako tangu sasa.
 
Ubarikiwe.
 
Tafadhali “Share” kwa wengine na Mungu atakubariki
https://wingulamashahidi.org/2019/10/17/nilimwona-shetani-akianguku-kutoka-mbinguni/
https://wingulamashahidi.org/2019/08/12/usitafute-faida-yako-mwenyewe-bali-ya-wengine/

Print this post

Je! ni kweli dunia iliumbwa takribani miaka 6000 iliyopita? na je! shetani alikuwepo duniani wakati dunia inaumbwa?

JIBU: Kulingana na hesabu ya vizazi na miaka yao waliyoishi katika biblia, inakadiriwa tangu Edeni mpaka wakati wa Gharika, ni miaka elfu 2, na tangu wakati wa gharika mpaka kuzaliwa kwa Bwana Yesu ilipita miaka elfu 2 hivi, na tangu kipindi cha Bwana wetu Yesu hata leo nacho pia ni kipindi cha miaka elfu 2 kimepita. Kwahiyo jumla yake tangu Edeni mpaka sasa ni miaka kama elfu 6 hivi, au imezidi kidogo au imepungua kidogo..Sasa kumbuka huo ulikuwa ni mwanzo wa Edeni, lakini haukuwa mwanzo wa Dunia..dunia ilikuwepo kabla ya Edeni..Tunasoma.
 
Mwanzo 1:1 “hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi”
 
…hapa hajasema huo mwanzo ulikuwa ni wa miaka mingapi iliyopita inaweza ikawa ni miaka elfu kumi,milioni kumi au vinginevyo…
 
lakini mstari wa pili unasema nayo nchi ilikuwa ukiwa na utupu inamaanisha kuwa kuna jambo lilitokea likaifanya hiyo nchi kuwa ukiwa baada ya Mungu kuziumba mbingu na nchi na hapa si mwingine zaidi ya shetani ndiye aliyeiharibu na kuifanya ukiwa (kama anavyoendelea kuiharibu sasa hivi) maana Mungu hakuiumba ukiwa yaani dunia iwe ukiwa bali ikaliwe na watu,
 
Isaya 48:18 inasema
 
18 Maana Bwana, aliyeziumba mbingu, asema hivi; Yeye ni Mungu; ndiye aliyeiumba dunia na kuifanya; ndiye aliyeifanya imara; hakuiumba ukiwa, aliiumba ili ikaliwe na watu; Mimi ni Bwana, wala hapana mwingine. “.
 
Lakini baada ya dunia kuharibiwa kwa viwango vya hali ya juu, ikapoteza umbo lake ikawa kama moja ya sayari nyingine, na ndio tunaona Mungu akaanza kufanya uumbaji upya baada ya nchi kukaa muda mrefu katika hali ya ukiwa, hapo mbingu na nchi zilikuwa tayari zimeshaumbwa muda mrefu nyuma.
 
Kwahiyo mwanadamu na viumbe vyote inakadiriwa viliumbwa takribani miaka  6000 iliyopita lakini dunia iliumbwa kabla ya hapo na shetani alikuwepo duniani kabla ya mwanadamu kuumbwa, kwasababu tunamuona alionekana katika bustani ya Edeni na biblia inamwita shetani kama yule nyoka wa zamani
 
Ufunuo 20:2 Akamshika yule joka, yule nyoka wa zamani, ambaye ni Ibilisi na Shetani, akamfunga miaka elfu;,
 
kwahiyo inamaanisha alikuwepo toka zamani kabla hata ya mwanadamu kuumbwa, ambapo tunaona alitupwa huku duniani baada ya kuasi mbinguni pamoja na malaika zake.
 
Ubarikiwe sana.

 


 

Mada zinazoendana:

JUMA LA 70 LA DANIELI

Kati ya Unyakuo wa kanisa, Dhiki kuu, Vita vya har-magedoni, Utawala wa miaka 1000, Vita ya Gogu na Magogu, hukumu ya kiti cha enzi cheupe. Je, ni kipi kinaanza na kingine kufuata?

SIKU YA BWANA INAYOTISHA YAJA!

AMIN! NAWAAMBIA KIZAZI HIKI HAKITAPITA!


Rudi Nyumbani:

Print this post

Nini maana ya kusali kwa kupayuka payuka?

Swali linaendelea…..Na Je, nisali kwa namna gani ili maombi yangu yasionekane kuwa ni ya kupayuka payuka mbele za Mungu?
 
JIBU: Mungu akubariki ndugu,Mathayo 6:7 Inasema:
 
Nanyi mkiwa katika kusali, msipayuke-payuke, kama watu wa mataifa; maana wao hudhani ya kuwa watasikiwa kwa sababu ya maneno yao kuwa mengi.
 
 Sasa mstari huo ukiangalia kwenye tafsiri nyingine hilo neno “kupayuka-payuka” halimaanishi kama “kupaza sauti kwa nguvu,” kama watu wengi wanavyodhani, hapana bali linamaanisha “KURUDIA-RUDIA” maneno yale yale, Hilo la kupaza sauti kwa nguvu mstari wake ni ule wa juu yake kabla ya huu unaosema:
 
“Mathayo 6: 5 Tena msalipo, msiwe kama wanafiki; kwa maana wao wapenda kusali hali wamesimama katika masinagogi na katika pembe za njia, ili waonekane na watu. Amin, nawaambia, Wamekwisha kupata thawabu yao.
 
6 Bali wewe usalipo, ingia katika chumba chako cha ndani, na ukiisha kufunga mlango wako, usali mbele za Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi.
 
 
Unaona, aina hii ya watu ndio wanaopenda kupaza sauti zao kwa nguvu kwa lengo la kuonekana na watu ndio hao wanaoonekana wamesimama katika masinagogi na katika pembe za njia. Watu wa namna hiyo Bwana anasema Wamekwisha kupata thawabu yao, Lakini pia kumbuka hilo halimaanishi watu wasiombe kwa kupaza sauti zao, hapana, biblia inasisitiza sana tupaze sauti zetu tumliliapo Mungu…Lakini sio kwa lengo la kujionyesha sisi tunajua kusali, au sisi ni wa kiroho sana. Vinginevyo tutakuwa tumeshapata thawabu zetu.
 
Lakini sasa kwa wale wanao payuka payuka mstari wao ndio huo unaofuata…
 
 
7 Nanyi mkiwa katika kusali, msipayuke-payuke, kama watu wa mataifa; maana wao hudhani ya kuwa watasikiwa kwa sababu ya maneno yao kuwa mengi.
8 Basi msifanane na hao; maana Baba yenu anajua mnayohitaji kabla ninyi hamjamwomba. “
 
Hivyo watu wanao rudia-rudia maneno, kwa mfano watu dini nyingine na watu wanaosali rozari na sala za bikira mariamu wanafahamu,huwa wanarudia rudia maneno yale yale kwa muda mrefu hata masaa na masaa wakidhani kuwa kwa kufanya vile Mungu atasikia dua zao. Hizo ni desturi za kipagani ndio maana tumeonywa tusifanane na hao. kwahiyo tunapoenda mbele za Mungu tuwe na malengo, tutoe hoja zetu zote, kisha zikishaisha, basi, tushukuru tuondoke Tukiamini kuwa Mungu kashatusikia na sio kuanza kurudia rudia tena kile tulichokiomba kana kwamba Mungu hasikii,. kwa ufupi usiweke mfumo fulani unaoonyesha mrudio rudio katika kusali, kuwa huru mbele za Mungu ndivyo Sala zako zitakavyokuwa na thamani mbele za Mungu.
 
Ubarikiwe sana.

 


 

Mada zinazoendana:

Biblia ituambia tusalimiane kwa busu takatifu. Hili busu ndio lipi?

JE! NI LAZIMA WATU WOTE WANENE KWA LUGHA?

Kunena kwa lugha kukoje?

“heri walio maskini wa roho maana ufalme wa mbinguni ni wao” je hatuna ruhusa ya kuwa matajiri katika roho?


Rudi Nyumbani:

 

Print this post

Je! wayahudi wote wataokolewa kulingana na Warumi 11:26?

 SWALI: Je! Wayahudi wote wataokolewa? maana biblia inasema katika;

Warumi 11:25 “Kwa maana, ndugu zangu, sipendi msiijue siri hii, ili msijione kuwa wenye akili; ya kwamba kwa sehemu ugumu umewapata Israeli, mpaka utimilifu wa Mataifa uwasili.
26 Hivyo Israeli wote wataokoka; kama ilivyoandikwa, Mwokozi atakuja kutoka Sayuni; Atamtenga Yakobo na maasia yake”.

Hapo anaposema Israeli wote wataokoka, je hata kama ni watenda dhambi wataokolewa siku ya mwisho?


JIBU: Watu wengi wanadhani hivyo, lakini ukweli ni kwamba Hapana! sio waisraeli wote atakaookolewa bali wale tu walioishi maisha yanayolingana na torati yao ila wengine wasioishi kulingana na maagizo ya dini yao(torati) watahukumiwa kama tu watu wasioamini…

Warumi 9:6-7 ” Si kana kwamba neno la Mungu limetanguka. Maana hawawi wote Waisraeli walio wa uzao wa Israeli.Wala hawawi wote wana kwa kuwa wazao wa Ibrahimu, bali, Katika Isaka wazao wako wataitwa; ”

 Unaona hapo! ni kama tu vile si “wakristo” wote walio “wa-kristo” kwelikweli isipokuwa wale waliozaliwa mara ya pili, na kuishi maisha matakatifu. Wapo wengi leo wanaojiita wakristo, kwasababu tu wamezaliwa kwenye familia za kikristo lakini ukiangalia mienendo yao, na matendo yao hayaendani na ukristo, sasa hao wanakuwa ni wakristo-jina vivyo hivyo na kwa wayahudi. Wapo wayahudi wengi leo hii japo ni wayahudi kweli kweli lakini hawaamini hata kama kuna Mungu ni kama wapagani, na hata hawamtazamii Masihi wao, wanapinga kila imani!.

Sasa mtu wa namna hiyo hawezi kuokeolewa isipokuwa labda atubu na kubadili mwenendo wake?.Hata katika biblia agano la kale wapo wengi ambao waliharibiwa na Mungu japo walikuwa ni wayahudi kweli kweli mfano tunao Kora na Dathani, na wale wana wawili wa Eli n.k. Wapo wengine pia biblia inarekodi ni wachawi, na wapinga-kristo mfano tunamwona yule aliyekutana na Paulo aliyeitwa Bar Yesu:

Matendo 13:6 “Walipokwisha kupita katikati ya kisiwa chote mpaka Pafo, wakaona mtu mmoja, MCHAWI, nabii wa uongo, MYAHUDI jina lake Bar-Yesu;

7 mtu huyu alikuwa pamoja na liwali Sergio Paulo, mtu mwenye akili. Yeye liwali akawaita Barnaba na Sauli waje kwake, akataka kulisikia neno la Mungu.

8 Lakini Elima, yule mchawi (maana ndiyo tafsiri ya jina lake), akashindana nao, akitaka kumtia yule liwali moyo wa kuiacha ile imani.

9 Lakini Sauli, ambaye ndiye Paulo, akijaa Roho Mtakatifu, akamkazia macho,

10 akasema, Ewe mwenye kujaa hila na uovu wote, mwana wa Ibilisi, adui wa haki yote, huachi kuzipotoa njia za Bwana zilizonyoka? “

Unaona Bar Yesu alikuwa mchawi, Kwahiyo siyo wayahudi wote walio waisraeli, na sio wayahudi wote watakaokolewa bali ni wale watakaozishika amri za Mungu ambao majina yao yameandikwa kwenye kitabu cha uzima kabla misingi ya ulimwengu kuwekwa.

Lakini ijapokuwa kwasasa hivi wayahudi wengi hawamkubali Yesu kama masihi wao(Lakini wanamwamini YEHOVA), Hiyo Mungu karuhusu ni kwa makusudi kabisa ya Mungu kafanya hivyo ili sisi mataifa tupate neema ya kuokolewa, lakini utafika wakati nao umeshakaribia ambapo neema itaondoka kwetu na kurejea tena israeli, wakati huo wayahudi wengi (walio wayahudi hasaa wenye hofu ya Mungu) watampokea Kristo kama Masihi wao,na kubatilisha desturi zao za sheria na kuipokea neema ya BWANA YESU KRISTO.

Warumi 11:24 “Kwa maana ikiwa wewe ulikatwa ukatolewa katika mzeituni, ulio mzeituni mwitu kwa asili yake, kisha ukapandikizwa, kinyume cha asili, katika mzeituni ulio mwema, si zaidi sana wale walio wa asili kuweza kupandikizwa katika mzeituni wao wenyewe?

25 Kwa maana, ndugu zangu, sipendi msiijue siri hii, ili msijione kuwa wenye akili; ya kwamba kwa sehemu ugumu umewapata Israeli, mpaka utimilifu wa Mataifa uwasili.

26 Hivyo Israeli wote wataokoka; kama ilivyoandikwa, Mwokozi atakuja kutoka Sayuni; Atamtenga Yakobo na maasia yake.

Na baada ya hayo kutokea hapo ndipo ule mwisho utakapokuja.(Mathayo 24:14), je! jiulize wakati sasa neema inakaribia kuondoka huku kwetu wewe imeipokea? kwasababu utafika wakati utatamani kuingia utashindwa pale mwenye nyumba(Bwana Yesu) atakaposimama na kufunga mlango Luka 13:25..biblia inasema mlango ni mwembamba na njia imesonga iendayo uzimani na wanaoiona ni wachache, je! na wewe umeiona njia? je! taa yako inawaka, maisha yako yanahakisi wokovu? muda umekwenda kushinda tunavyofikiri kama Mungu aliweza kuwakatilia mbali watu wake (wayahudi) ili sisi mataifa ambao tulikuwa makafiri tupate neema, unadhani atashindwa kutukatilia na sisi mbali ili awarejee watu wake wateule israeli?? Ambapo hivi karibuni atafanya hivyo?.

Waebrania 2:3″sisi je! Tutapataje kupona, tusipojali wokovu mkuu namna hii? Ambao kwanza ulinenwa na Bwana, kisha ukathibitika kwetu na wale waliosikia;”

Ubarikiwe sana.

Mada Nyinginezo:

MAJONZI YA MTUME PAULO KWA NDUGU ZAKE.

Amin, nawaambia, Kizazi hiki hakitapita.

FANYA KAMA UONAVYO VEMA.

NINI KINATOKEA BAADA YA KIFO?

AINA SABA (7) ZA UNAFIKI, AMBAZO UNAPASWA UJIEPUSHE NAZO.

Rudi Nyumbani

Print this post

6# SWALI : Dhambi ya kumkufuru Roho Mtakatifu ni ipi?

JIBU: Tukisoma;

Mathayo 12:25-32 ” Lakini Mafarisayo waliposikia, walisema, Huyu hatoi pepo, ila kwa Beelzebuli mkuu wa pepo.

25 Basi Yesu akijua mawazo yao, akawaambia, Kila ufalme ukifitinika juu ya nafsi yake, hufanyika ukiwa; tena mji au nyumba yo yote ikifitinika juu ya nafsi yake, haitasimama.

26 Na Shetani akimtoa Shetani, amefitinika juu ya nafsi yake; basi ufalme wake utasimamaje?

27 Na mimi nikitoa pepo kwa Beelzebuli, je! Wana wenu huwatoa kwa nani? Kwa sababu hiyo hao ndio watakaowahukumu.

28 Lakini mimi nikitoa pepo kwa Roho wa Mungu, basi ufalme wa Mungu umekwisha kuwajilia.

29 Ama awezaje mtu kuingia ndani ya nyumba ya mtu mwenye nguvu na kuviteka vyombo vyake, asipomfunga kwanza yule mwenye nguvu? Ndipo atakapoiteka nyumba yake.

30 Mtu asiye pamoja nami yu kinyume changu; na mtu asiyekusanya pamoja nami hutapanya.

31 Kwa sababu hiyo nawaambia, KILA DHAMBI, NA KILA NENO LA KUFURU, watasamehewa wanadamu, ILA KWA KUMKUFURU ROHO HAWATASAMEHEWA.

32 Naye mtu ye yote atakayenena neno juu ya Mwana wa Adamu atasamehewa, bali yeye atakayenena neno juu ya Roho Mtakatifu hatasamehewa katika ulimwengu wa sasa, wala katika ule ujao. “

Tunavyosoma mistari hiyo tunaona kabisa wale Mafarisayo walikuwa wanajua Bwana Yesu ni kweli alikuwa anatoa pepo, na kutenda mambo yote kwa uweza wa Roho wa Mungu, lakini wao kwa ajili ya wivu, na kwa tamaa zao wenyewe,ili tu wawavutie watu kwao, wakakusudia kwa makusudi kabisa, wawageuze watu mioyo ili watu wasimuamini Bwana Yesu,wawaamini wao, na ndipo wakaanza kutoa maneno ya makufuru wanawaambia watu kuwa BWANA anatoa pepo kwa uwezo wa belzebuli mkuu wa Pepo angali ndani ya mioyo yao walikuwa wanajua kabisa anachofanya ni kwa uweza wa Roho wa Mungu.

Ukweli wa jambo hilo unajidhihirisha kwa Nikodemo ambaye naye alikuwa ni mmoja wa wale mafarisayo alipomwendea Yesu usiku na kumwambia

Yohana 3:1-2″Basi palikuwa na mtu mmoja wa Mafarisayo, jina lake Nikodemo, mkuu wa Wayahudi.

2 Huyo alimjia usiku, akamwambia, RABI, “TWAJUA” YA KUWA U MWALIMU, UMETOKA KWA MUNGU; KWA MAANA HAKUNA MTU AWEZAYE KUZIFANYA ISHARA HIZI UZIFANYAZO WEWE, ISIPOKUWA MUNGU YU PAMOJA NAYE. “

kwahiyo unaona walikuwa wanajua kabisa lakini kwa ajili ya wivu wakaanza kuzusha maneno ya uongo juu ya kazi ya Roho wa Mungu, sasa huko ndiko kumkufuru Roho Mtakatifu. hivyo basi Bwana Yesu alitoa angalizo tunapozitazama kazi za Mungu, pale mtu mwenye Roho wa Mungu anatenda kazi za Mungu kweli huku tunajua ni Mungu ndiye anayefanya kazi ndani yake, na kuanza kusema yule ni mchawi, au anatumia uchawi, au mshirikina, au tapeli, au mwizi, ili tu watu wasiziamini kazi za Mungu au vinginevyo, au unaanza kuzusha propaganda za uongo juu yake, pengine kwa kusudi la kumkomoa! hapo ndugu utakuwa unajimaliza mwenyewe. (Ni kweli si watumishi wote ni wa Mungu,hao ni sawa kuufunua uovu wao). Lakini Hapa tunamzungumzia yule unayemfahamu kabisa ni mtumishi wa BWANA,..wewe hujui umewakosesha wangapi, ambao kwa kupitia yeye, watu wengi wangeokolewa? kufanya hivyo ni hatari sana tuwe makini.

Hivyo hii dhambi unawahusu wale wanaozipinga kazi za Mungu kwa makusudi kabisa (Mfano wa mafarisayo). Hao kwao hakuna msamaha, hawawezi tena kutubu hata iweje wanachongojea ni ziwa la moto.

Lakini shetani naye anapenda kulitumia hili neno kuwafunga watu wajione kuwa wamemkufuru Roho Mtakatifu na kwamba dhambi zao hazisameheki hata wafanyeje,
Hii inakuja sana sana kwa watu waliowachanga ki-imani, kuna shuhuda nyingi za watu waliofungwa na shetani kwa namna hiyo wakidhani kuwa dhambi zao hazisameheki, kuna watu wamekata tamaa wanajiona kwa wingi wa dhambi zao, Mungu hawezi kuwasemehe tena, pengine wameua, wametoa mimba sana, n.k, Sasa jambo la namna hii likija katika mawazo yako likatae linatoka kwa yule mwovu kukufanya wewe ujione kuwa Mungu hawezi kukusamehe umemkufuru, hivyo usijisumbue kutubu kwasababu Mungu hatakusikiliza.

Kumbuka kama tulivyosema Dhambi hii inakaa kwa wale watu ambao ndani yao mioyo ya toba imekufa, au hofu ya Mungu haipo tena kwao, watu waliojikinai, wanaompinga Mungu katika fikra zao japo kuwa walimjua Mungu na uweza wake wote, wanazipotosha kazi za Mungu kwa makusudi kwa faida zao wenyewe,ili wawavute watu kwao, au wawe washirika wao na sio kwa Mungu. Hivyo basi kitendo tu cha wewe kuwa na hii hofu ya kumwogopa Mungu ujue Roho wa Mungu anatenda kazi ndani yako na hayo mawazo ya kwamba umemkufuru Roho Mtakatifu yapinge huyo ni adui ndio moja ya njia zake hizo ili usiufikie wokovu na anapenda kuwatesa watu wengi katika andiko hili.

Ubarikiwe sana.


Mada zinazoendana:

DHAMBI YA MAUTI

DHAMBI ILIYOMKOSESHA SHETANI.

DHAMBI ZINAZOTANGULIA NA ZINAZOFUATA.

DHAMBI ISIYO NA MSAMAHA.


Rudi Nyumbani:

Print this post

Je! dhambi zote ni sawa Kuna dhambi kubwa na ndogo?

 

SWALI: Naomba kufahamu Je! Kuna dhambi kubwa na ndogo, na kama hakuna je! Mtu aliyeua na aliyetukana je watapata adhabu sawa?


JIBU: Dhambi ni dhambi iwe kubwa au ndogo, zote ni kosa, biblia inasema.

Yakobo 2:10 “Maana mtu awaye yote atakayeishika sheria yote, ila akajikwaa katika neno moja, amekosa juu ya yote.

11 Kwa maana yeye aliyesema, Usizini, pia alisema, Usiue. Basi ijapokuwa hukuzini, lakini umeua, umekuwa mvunja sheria. “

Unaona hapo? Kwahiyo mtu akitenda dhambi iwe kubwa au ndogo ataadhibiwa. lakini adhabu zitatofautiana huko waendako kulingana na wingi wa makosa, kwasababu Bwana Yesu pia alisema aliyeua kwa upanga atauawa kwa upanga, apandacho mtu ndicho atakachovuna. adhabu ya shetani haiwezi ikawa sawa na adhabu ya mwanadamu. Biblia inaeleza..

Luka 12:47 “Na mtumwa yule aliyejua mapenzi ya bwana wake, asijiweke tayari, wala kuyatenda mapenzi yake, ATAPIGWA SANA.

48 Na yule asiyejua, naye amefanya yastahiliyo mapigo, ATAPIGWA KIDOGO. Na kila aliyepewa vingi, kwake huyo vitatakwa vingi; naye waliyemwekea amana vitu vingi, kwake huyo watataka na zaidi. “

Kwahiyo mapigo yanatofautiana kulingana na matendo ya mtu aliyoyatenda akiwa hapa duniani, ni kama tu vile thawabu zitavyotofautiana kwa mtu na mtu mbinguni kwa jinsi alivyotaabika katika kumtumikia Bwana vivyo hivyo na jehanamu adhabu zitatofautiana kulingana na dhambi mtu alizotenda akiwa ulimwenguni. Na jinsi gani alivyoipuuzia neema ya wokovu.

Hivyo hatupaswi kuipima dhambi kwa namna yoyote, ni kukaa nayo mbali kwasababu iwe ni kubwa au ndogo mshahara wake ni MAUTI, Warumi 6:23.

Dhambi kubwa na ndoto zote zina adhabu ya mauti.

Je! Umempa Yesu maisha yako ndugu yangu? Unatambua kuwa hizi ni nyakati za mwisho?. Ukifa leo utakuwa mgeni wa nani, huko uendako?. Tubu sasa mgeukie yeye atakusamehe, na kukupa uzima wa milele.

Mungu akubariki.

 Jiunge na Magroup yetu ya Whatsapp kwa kubofya hapa>> Group-Whatsapp


Mada nyinginezo:

Dhambi ya kumkufuru Roho Mtakatifu ni ipi?

“Yodi” ni nini ?

Nini maana ya “Kandake” (Matendo 8:27)

Wote wanaokumbwa na mauti sasa ni kutokana na dhambi zao?

Je wale waliomsulubisha Bwana, wataenda mbinguni, kwakuwa walisamehewa?

UNYAKUO.

Rudi Nyumbani Print this post

UTAPENDA KUCHANGIA HUDUMA HII?

Tutamshukuru Mungu kwa ajili yako, kwa mchango wako, ili kuifanya injili hii isonge mbele Tuma sadaka yako kwa namba hizi:
Airtel:+255789001312 -Devis Magembe
Mpesa: +255767992434-Denis Magembe