SWALI: Je Mungu alipomwumba Adamu kwa sura yake na mfano wake alikuwa na kitovu?..Kwasababu kazi ya kitovu ni kumlisha mtoto tumboni chakula kutoka kwa mama yake…..Sasa Adamu na Hawa hawakupitia hiyo hatua ya kukaa tumboni kwa mama zao je!..ingewezekanikaje wao kuwa na vitovu?…
JIBU: Mungu alipomwumba Adamu alimwumba akiwa kamili..Hakuna chochote kilichokuwepo kwa Adamu ambacho hakikuwepo kwa watoto wake. Umbile lake lote kuanzia kichwani mpaka miguuni lilikuwa ndio hilo hilo kwa uzao wake wote.
Sasa tukirudi kwenye swali linalouliza…je Adamu alikuwa na kitovu?..Jibu ni ndio alikuwa nacho!…Mungu alimuumba akiwa na kitovu..Sasa Mungu alipokiweka kitovu kwa Adamu na Hawa visingekuwa na kazi kwao lakini vingekuja kuwa na kazi kubwa kwa wanao ambao watawazaa hapo baadaye..kwani wanao watavitumia kupata chakula wakiwa tumboni.
Ni sawa na Adamu Mungu alipomwumba na chuchu mbili ndogo kifuani mwake…Mungu aliziweka vile kwa utukufu wake, ambapo Adamu pengine zisingekuwa na kazi yoyote kubwa kwake….kama leo tunavyoziona sizivyo na kazi kwa wanaume…Lakini umuhimu wa kuwepo zile chuchu mbili kifuani kwa Adamu tunakuja kuziona pale Hawa alipotoka ubavuni mwake….Kwani Hawa alizirithi zile chuchu kutoka kwa Adamu na zilikuja baadaye kutumika kama chanzo cha chakula kwa watoto wao.
Kadhalika na kitovu. Adamu alikuwa nacho lakini hakikuwa na kazi yoyote kwenye mwili wake…lakini kazi kubwa ilikuja kuonekana kwa wanawe aliokuja kuwazaa…kwani kitovu hicho walichokirithi kutoka kwa Adamu kimekuja kutumika kama njia ya kupitishia chakula kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto wakati wa ujauzito.
Hivyo Adamu alikuwa na kitovu pale alipoumbwa na Mungu. Na wanawe aliowazaa walikuwa kama yeye wote wana vitovu..Biblia inasema Adamu alizaa mwana kwa sura yake na mfano wake….Ikimaanisha kuwa kama Adamu angekuwa hana kitovu halafu mtoto aliyemzaa awe nacho basi biblia ingekuwa inasema uongo pale iliposema Adamu alizaa mwana wenye sura yake na mfano wake.
Mwanzo 5:1 “Hiki ndicho kitabu cha vizazi vya Adamu. Siku ile Mungu alipoumba mtu, kwa sura ya Mungu alimfanya; 2 mwanamume na mwanamke aliwaumba, akawabariki akawaita jina lao Adamu, siku ile walipoumbwa. 3 Adamu akaishi miaka mia na thelathini, akazaa mwana kwa sura yake, kwa mfano wake, akamwita jina lake Sethi”. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mwanzo 5:1 “Hiki ndicho kitabu cha vizazi vya Adamu. Siku ile Mungu alipoumba mtu, kwa sura ya Mungu alimfanya;
2 mwanamume na mwanamke aliwaumba, akawabariki akawaita jina lao Adamu, siku ile walipoumbwa.
3 Adamu akaishi miaka mia na thelathini, akazaa mwana kwa sura yake, kwa mfano wake, akamwita jina lake Sethi”. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Nyinginezo:
Adamu alikuwa na watoto wangapi?
BUSTANI YA NEEMA.
Je! Adamu aliwasaliana na Mungu kwa lugha ipi pale bustanini?
Je! mwanadamu wa kwanza kuumbwa ni yupi Mzungu mwafrika au Mchina na kama ni mmojawapo kati ya hao je hao wengine wametoka wapi?
Je! taratibu za kufunga ndoa [yaani harusi] ni agizo la Mungu au ni mapokeo tu ya kibinadamu?
Uzao wa Mwanamke ni upi? Unaozungumziwa katika Mwanzo 3:15?
Mungu alikuwa anaongea na nani aliposema na “Tumfanye mtu kwa mfano wetu”,(Mwanzo 1:26)?
JE! Kaini alimpatia mke wake wapi?
Rudi Nyumbani:
Print this post
JIBU: Kama yatakuwepo maombi ya kumtoa mtu aliyekufa katika dhambi kuzimu …basi yatakuwepo pia maombi..au itakuwepo namna ya kumtoa mtu aliyekufa katika haki paradiso.
Lakini kama hakuna maombi yoyote au namna yoyote ya kumtoa mtu paradiso na kumpeleka kuzimu..kadhalika hakutakuwepo na maombi yoyote ya kumtoa mtu jehanum na kumpeleka paradiso.
Biblia inasema katika…
Luka 16: 22 “ Ikawa yule maskini alikufa, akachukuliwa na malaika mpaka kifuani kwa Ibrahimu. Yule tajiri naye akafa, akazikwa. 23 Basi, kule kuzimu aliyainua macho yake, alipokuwa katika mateso, akamwona Ibrahimu kwa mbali, na Lazaro kifuani mwake. 24 Akalia, akasema, Ee baba Ibrahimu, nihurumie, umtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake majini, auburudishe ulimi wangu; kwa sababu ninateswa katika moto huu. 25 Ibrahimu akasema, Mwanangu, kumbuka ya kwamba wewe uliyapokea mambo mema yako katika maisha yako, na Lazaro vivyo alipata mabaya; na sasa yeye yupo hapa anafarijiwa, na wewe unaumizwa. 26 Na zaidi ya hayo, KATI YETU SISI NA NINYI KUMEWEKWA SHIMO KUBWA, ili wale watakao kutoka huku kwenda kwenu wasiweze; wala watu wa kwenu wasivuke kuja kwetu”.
Luka 16: 22 “ Ikawa yule maskini alikufa, akachukuliwa na malaika mpaka kifuani kwa Ibrahimu. Yule tajiri naye akafa, akazikwa.
23 Basi, kule kuzimu aliyainua macho yake, alipokuwa katika mateso, akamwona Ibrahimu kwa mbali, na Lazaro kifuani mwake.
24 Akalia, akasema, Ee baba Ibrahimu, nihurumie, umtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake majini, auburudishe ulimi wangu; kwa sababu ninateswa katika moto huu.
25 Ibrahimu akasema, Mwanangu, kumbuka ya kwamba wewe uliyapokea mambo mema yako katika maisha yako, na Lazaro vivyo alipata mabaya; na sasa yeye yupo hapa anafarijiwa, na wewe unaumizwa.
26 Na zaidi ya hayo, KATI YETU SISI NA NINYI KUMEWEKWA SHIMO KUBWA, ili wale watakao kutoka huku kwenda kwenu wasiweze; wala watu wa kwenu wasivuke kuja kwetu”.
Hapo inasema kumewekwa shimo kubwa…SHIMO Ni lugha ya kuonyesha kwamba haiwezekani kwa namna yoyote mtu aliyeko jehanamu kuvuka kuingia paradiso…wala aliyeko paradiso kwenda kuzimu..Ikifunua kwamba hata maombi hayawezi kumvusha mtu katika shimo hilo…
Nafasi ya kuvuka kutoka mautini kuingia uzimani tunayo tukiwa hapa hapa duniani. Tukishindwa kutengeneza mambo yetu tukiwa hapa duniani tukifika kule hakuna hiyo nafasi…Ibrahimu ambaye sisi sote tunamwita Baba wa Imani, ambaye ni mtakatifu na aliyekubaliwa na Mungu pengine kuliko mimi na wewe ameshindwa kumtoa huyo Tajiri kuzimu na kumwingiza paradiso…Je wewe au mimi ambaye tuna dhambi tutawezea wapi?…Ibrahimu ambaye sasa yupo utukufuni ambaye kashashinda vita vya ulimwengu huu, kashindwa kumtoa tajiri kuzimu… sisi ambao hata hatujui kinachoendelea ng’ambo..maombi yatu yatamtoaje mtu aliyekufa kutoka kuzimu kumpeleka peponi?.
Hivyo hiyo inatutahadharisha kuyaangalia Maisha yetu..Tujihakiki kila siku je tunampendeza Mungu?..Je tunastahili kuingia mbinguni?..Kama bado basi tutengeneze mambo yetu kabla siku zetu za kuishi hazijakwisha. Tusidanganywe na uongo wa shetani, ambao unakuja kwa kivuli cha faraja kwa ndugu zetu waliotangulia lakini kumbe nyuma yake kumejaa roho ya uongo na upotevu..Tuishi maisha masafi na ya kuwahubiria ndugu zetu kabla hawajaondoka duniani..Kwasababu hakuna nafasi ya pili baada ya kifo.
Hakuna kupitia kwanza ‘Toharani’ kisha ndio tuende mbinguni kama baadhi ya madhehebu yanavyoamini mfano wa Katoliki..Tukishakufa habari yetu ndio inakuwa imeisha hapo. kama tumeangukia upande wa uzima, basi tutabakia huko uzimani daima, kama tuliangukia upande wa mauti basi tutaishi mautini milele.
Tubu ikiwa bado hujatubu, angali nafasi ipo.
Bwana akubariki. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Wenye kubatizwa kwa ajili ya wafu ni wakina nani?
DUNIANI MNAYO DHIKI.
USIFE NA DHAMBI ZAKO!
ALIJARIBIWA SAWASAWA NA SISI KATIKA MAMBO YOTE.
Je! Ni sahihi kuoa/kuolewa na mtu uliyemzidi umri?
Alijaribiwa sawasawa na sisi katika mambo yote!!
Waebrania 4:14 “Basi, iwapo tunaye kuhani mkuu aliyeingia katika mbingu, Yesu, Mwana wa Mungu, na tuyashike sana maungamo yetu. 15 Kwa kuwa hamna kuhani mkuu asiyeweza kuchukuana nasi katika mambo yetu ya udhaifu; bali yeye alijaribiwa sawasawa na sisi katika mambo yote, bila kufanya dhambi”.
Waebrania 4:14 “Basi, iwapo tunaye kuhani mkuu aliyeingia katika mbingu, Yesu, Mwana wa Mungu, na tuyashike sana maungamo yetu.
15 Kwa kuwa hamna kuhani mkuu asiyeweza kuchukuana nasi katika mambo yetu ya udhaifu; bali yeye alijaribiwa sawasawa na sisi katika mambo yote, bila kufanya dhambi”.
Neno la Mungu linaposema, alijaribiwa sawasawa na sisi katika mambo yote..Linamaanisha kweli ni katika mambo yote, Kama ni njaa, Bwana Yesu anaielewa vizuri na alishawahi kuionja, kama ni kuumwa Bwana Yesu anaelewa vizuri nini maana ya kuumwa, Yeye alipoishi hapa duniani hakuwa kama kiumbe cha kipekee ambacho hakijawahi hata siku moja kujua shida tangu kuumbwa kwake, kwamba hajawahi kuisikia hata maumivu ya kichwa tangu kuzaliwa kwake hadi kufa kwake hapana, pale msalabani maumivu makali aliyokuwa anayasikia ni zaidi ya ugonjwa wowote duniani..
Kama ni kuwa na maadui yeye naye alikuwa nao wengi..Kama ni kuonekana si kitu alionekana sana mbele ya macho ya watu wengi (Soma Isaya 53), kama ni misiba yeye naye alipitia ya kufiwa na ndugu zake, ni vile tu biblia haiwezi kuandika habari zake zote..Hivyo hakuna jambo lolote au shida yoyote unayoipitia leo hii Bwana wetu YESU KRISTO asiielewe.
Na ndio maana tunamshukuru Mungu kwa ajili yake, kwasababu, pale tunapomwomba au kumlilia shida zetu tunajua kuwa ni mtu anayeelewa vizuri tunachokiomba kwake..Tofauti yake na sisi ni kwamba yeye katika majaribu hayo yote aliyoyapitia hakuwahi kutenda dhambi hata moja. Kwahiyo nataka nikutie moyo ndugu uliyemwamini Kristo, ujue kuwa umepata mwokozi kweli kweli anayoijua hali yako, Ni sawa na mtu ambaye alikuwa ni yatima akapitia maisha ya kuishi mtaani, chakula chake kilikuwa ni majalalani, kulala kwake ni kwenye mabaraza ya watu, lakini ikatokea siku moja kwa bahati tu akaokota almasi yenye thamani ya bilioni 5, akatajirika akawa maarufu sana katikati ya matajiri,(huo ni mfano tu!). wewe unadhani ni rahisi mtu huyo kuwasahau wale mayatima wenzake aliokuwa anahangaika nao mitaani? Kama ingekuwa hayajui hayo maisha isingekuwa rahisi kwake kuwajali, lakini kwasababu ameyapitia ni ngumu kuwasahau ndugu zake..
Hivyo Na wewe usiogope jaribu unalopitia sasa hivi kwasababu Kristo yupo pembeni yako kukusaidia anaelewa vizuri hali yako huhitaji hata kumweleza.. Yupo amesimama mbele za Mungu kama kuhani mkuu, kukuombea wewe.. Hivyo kaa ukijua tu, hata kama liwe bonde zito namna gani la mauti unalolipitia, ujue kuwa hatakuacha daima, yupo hapo kuhakikisha anakupigania, litadumu kwa kitambo tu, lakini nalo litapita.
Lakini kama wewe upo nje ya Kristo, fahamu kuwa kwa nguvu zako hutaweza kuyashinda mawimbi ya ibilisi katika huu ulimwengu.. Kristo hawezi kuwa mwombezi wako pale unapokwama, kwasababu hujataka awe rafiki yako.
Ukimkaribisha ndani ya moyo atakugeuza, na kuyaumba maisha yako upya tena. Atatembea na wewe, vilevile atakupa tumaini la uzima wa milele. Kwamba hata ukifa leo unaouhakika wa kwenda mbinguni. Lakini kama utautumikia ulimwenguni, ukifa leo huo ulimwengu umekuahidia nini baada ya hapa?. Yesu ni upendo anatupenda sote sawasawa wala hana ubaguzi, ukija kwake atakupokea haijalishi ni dhambi nyingi kiasi gani ulizowahi kufanya huko nyuma.
Anachotaka kwako ni moyo wa toba. Na ni kwanini utubu, kwasababu anataka kuanza na wewe ukiwa na dhamiri safi moyoni mwako. Unatubu kwa kumwomba msamaha, pili kwa kuacha yale mambo ambayo ulikuwa unayafanya huko nyuma.. Ukishafanya hivyo kwa moyo wako wote, kwasababu Mungu anaangalia moyo.. Basi Kristo saa hiyo hiyo atakuja na kufanya makao ndani yako.
Uthibitisho kuwa Yesu amekuja ndani yako na kufanya makao, ni kuwa utaona badiliko kubwa ndani yako, utaona shauku Fulani ndani yako, utaona amani Fulani ndani yako. Basi ujue kuwa Kristo ameshakuokoa na ameshakuja kufanya makao na wewe.
Lakini hiyo peke yake haitoshi..Unapaswa ukaukamalishe wokovu wako kwa kubatizwa ili kumpa Ruhusa Roho Mtakatifu kuja kufanya makao halali ndani yako. Hivyo nenda kabatizwe katika ubatizo sahihi, ambao ni ule wa kuzamishwa katika maji mengi(Yohana 3:23) na kwa jina la YESU KRISTO sawasawa na (Matendo 2:38,8:16,10:48, 19:5).
Ukifanya hivyo kwa moyo wako wote basi wewe ni mwana wa Mungu, Hivyo Kristo atakuwa na wewe kukulinda dhidi ya Yule adui na yeye mwenyewe atakupa dawa ya misukosuko mingi ya huu ulimwenguni inayowatesa wanadamu wengi,.
Bwana akubariki sana. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
HERI NINYI MLIAO SASA, KWA SABABU MTACHEKA.
NGUVU ILIYOPO KATIKA MAAMUZI.
YESU MPONYAJI.
NI KWA NAMNA GANI TUTASHINDA MAJARIBU?
Je Utoaji mimba/ kutoa mimba ni dhambi?..Je kama mtoto aliye tumboni anahatarisha uhai wa mama na madakatari wakamwambia anapaswa atoe hiyo mimba ili aishi vinginevyo atakufa..je endapo akiitoa ili kunusuru uhai wake kwa sababu za kiafya atakuwa amefanya dhambi ni muuaji?
JIBU: Kwanza ni muhimu kufahamu maana ya utoaji mimba..Utoaji mimba ni kitendo cha mzazi wa kike..kuondoa kiumbe ambacho tayari kimeshaanza kuishi katika tumbo lake..Hicho kinaweza kuwa katika wiki ya kwanza au katika mwezi wa mwisho wa 9. Hatua yoyote inayohusisha kukiondoa hicho kiumbe tumboni kwa mwanamke katika kipindi hicho cha muda ni kitendo cha UTOAJI MIMBA.
Utoaji mimba umegawanyika katika sehemu mbili..1) Utoaji mimba kwa sababu za kiafya 2) Utoaji kwa sababu nyingine zisizo za kiafya.
Tukianza na sababu za kiafya
Hii inahusisha pale mama mjamzito..labda kaugua ghafla na ile mimba ndani ya tumbo lake ikaharibika au mtoto akafa tumboni…Ili kuokoa maisha ya mama analazimika kwenda kuiondoa hiyo mimba hospitalini..Katika hali kama hiyo mama huyo hafanyi dhambi kwasababu tayari mtoto kashakufa..hivyo anapaswa atolewe huko aliko na kuzikwa.
Pia Inaweza kutokea mimba ya mama mjamzito ikatoka yenyewe kabla ya wakati wake…Hali kama hiyo pia hakuna dhambi iliyotendeka..Ingawa sio kawaida mimba kutoka yenyewe…
Lakini pia inaweza kutokea Mama mjamzito kapata tatizo au ugonjwa ambao utamlazimisha aondoe ile mimba iliyopo tumboni mwake ili kunusuru uhai wake. Na asipofanya hivyo kuna hatari ya kufa. Katika hali kama hiyo ambayo imethibitishwa..endapo mimba hiyo akiitoa hafanyi dhambi. Kwasababu amefanya hivyo ili kunusuru uhai wake…na asipofanya yeye pamoja na hicho kiumbe tumboni watakufa.
Lakini pia ni muhimu kufahamu kuwa..Hata katika hali hiyo ambayo madaktari wamesema kwamba ni ngumu kunusuru uhai wa mama akiwa na kiumbe tumboni..YESU KRISTO wa Nazareti hashindwi jambo..Mimba inaweza isitolewe na mwanamke huyo akazaa vizuri kabisa bila kufa wala kupata tatizo lolote..wanadamu wanashindwa mambo lakini Yesu Kristo hana rekodi ya kushindwa…Na wapo wanawake wengi wametendewa na Yesu miujiza kama hiyo…wamepewa ripoti na madaktari kwamba aidha waiondoe mimba waishi au waendelee kukaa na hiyo mimba wafe…lakini Bwana amewapigania na wameshinda vitisho vya vifo na wamejifungua salama kabisa bila tatizo lolote…Na waliotendewa hivyo na Yesu wapo wengi sana.
Lakini hiyo inahitaji imani thabiti isiyo na mashaka kwa Yesu Kristo…Lakini kama mtu ataingiwa na mashaka basi ni heri akaenda kuiondoa hospitalini…Kwasababu biblia imesema mtu asiye na imani asitegemee kupokea kitu kutoka kwa Mungu…
Yakobo 1.6 “… Ila na aombe kwa imani, pasipo shaka yo yote; maana mwenye shaka ni kama wimbi la bahari lililochukuliwa na upepo, na kupeperushwa huku na huku. 7 Maana mtu kama yule asidhani ya kuwa atapokea kitu kwa Bwana. 8 Mtu wa nia mbili husita-sita katika njia zake zote.”
Yakobo 1.6 “… Ila na aombe kwa imani, pasipo shaka yo yote; maana mwenye shaka ni kama wimbi la bahari lililochukuliwa na upepo, na kupeperushwa huku na huku.
7 Maana mtu kama yule asidhani ya kuwa atapokea kitu kwa Bwana.
8 Mtu wa nia mbili husita-sita katika njia zake zote.”
Sababu za PILI za kutoa mimba ni sababu zisizo za kiafya
Sababu hizi zinahusisha…Pale mwanamke anapopata mimba na wakati hana mpango wa kuwa na mtoto kwa wakati huo…Mwanamke wa namna hiyo akiitoa mimba ambayo tayari kashaipata anafanya dhambi..ni Muuaji.
Mwanamke ambaye amepata mimba kwa kubakwa au kwa mtu asiyempenda na akaenda kuitoa anafanya dhambi tayari, ni muuaji.
Mwanamke ambaye kapata mimba na kalazimishwa na mtu aliyempa mimba kwamba aitoe na yeye akaitoa anafanya dhambi huyo ni muuaji kabisa.
Mwanamke ambaye kapata ujauzito na Baba aliyehusika na ujauzito huo kaikataa hiyo mimba na mwanamke akaenda kuitoa hiyo mimba anafanya dhambi ni muuaji.
Mwanamke anayetoa mimba kwasababu ya umasikini au hali ngumu ya kimaisha kwa kuhofia malezi ya mtoto yatakuwaje anafanya dhambi ni muuaji.
Na sababu nyingine zote zilizosalia zisizo za kiafya..Ni dhambi kutoa mimba kwa kutumia hizo sababu.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe au piga namba hii 0789001812. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
KUOTA UNA MIMBA.
Je mama mjamzito anaruhusiwa kufunga?
KIELELEZO CHA MWANAMKE KATIKA NYUMBA.
Kwanini Mungu awachome watu kwenye ziwa la moto na hali yeye ndiye aliyewaumba?
WhatsApp
Nini tofauti kati ya Amri, sheria na Hukumu?
JIBU: Tukisoma kitabu cha Kumbukumbu 7:11 biblia inasema…
“Basi zishike AMRI, NA SHERIA, NA HUKUMU ninazokuamuru leo, uzitende. 12 Na itakuwa, kwa sababu mwazisikiliza hukumu hizi, na kuzishika na kuzitenda, basi Bwana, Mungu wako, atakutimilizia agano na rehema aliyowaapia baba zako”
“Basi zishike AMRI, NA SHERIA, NA HUKUMU ninazokuamuru leo, uzitende.
12 Na itakuwa, kwa sababu mwazisikiliza hukumu hizi, na kuzishika na kuzitenda, basi Bwana, Mungu wako, atakutimilizia agano na rehema aliyowaapia baba zako”
Ukisoma kwa makini utaona kweli kuna vitu vitatu hapo..Amri, Sheria na Hukumu..Hivi vi vitu vitatu tofauti lakini vinategemeana sana.
Amri maana yake ni Agizo lililotolewa na mamlaka iliyo kuu ambalo linapaswa litekelezwe bila shuruti..Amri huwa haina uchaguzi kwamba mtu anapaswa aitekeleze au asiitekeleze..Amri ikitolewa ni sharti wote waitekeleze na asiyefanya hivyo atakuwa hatihani. Katika Agano la kale..Mungu alitoa Amri kuu kumi kama tunavyozisoma katika kitabu cha Kutoka Mlango wa 20, na Kumbukumbu 5:3-21. (Unaweza ukazisoma binafsi).
Lakini pamoja na hizo Amri 10 kuwepo…bado zilikuwa hazijakamilika…Kwamfano kuna Amri moja inayosema USIZINI…Hiyo ni amri kweli..Mtu hatazini na mke wa jirani yake…lakini je! Ikitokea kazini na mnyama itakuaje?..atachukuliwa hatua gani? Atahukumiwaje?, au ikatokea mtu kazini na mzazi wake je atahukumiwaje? Hukumu yake itakuwaje, ikitokea mtu hajazini na mke wa jirani yake lakini kalala na mtu wa jinsia moja na yeye itakuwaje? N.k…Sasa maswali kama hayo unaona kabisa amri peke yake haijajitosheleza inahitajika ziwepo sheria pamoja na hukumu juu ya hizo amri…
Ndio maana unaona kwenye biblia zimeongezeka sheria nyingi nyingi ambazo zote zinasapoti Amri ya USIZINI. Na baadhi ya sheria hizo ni kama zifuatazo.
Walawi 18: 23 “Wala usilale na mnyama ye yote, ili kujitia unajisi kwake; wala mwanamke asisimame mbele ya mnyama ili kulala naye; ni uchafuko”…Hii ni sheria inayosapoti amri ya USIZINI.
Walawi 18: 6 “Mtu ye yote aliye wa kwenu asimkaribie mwenziwe aliye wa jamaa yake ya karibu ili kumfunua utupu; mimi ndimi Bwana. 7 Utupu wa baba yako, wala utupu wa mama yako, usifunue, maana ndiye mama yako; usifunue utupu wake. 8 Utupu wa mke wa baba yako, usifunue; maana, ni utupu wa baba yako. 9 Utupu wa umbu lako, binti ya baba yako, au binti ya mama yako, kwamba alizaliwa nyumbani mwenu au kwamba alizaliwa kwengine, utupu wa hao usifunue. 10 Utupu wa binti ya mwanao mume, au wa binti ya binti yako, utupu wao hao usifunue; kwa kuwa ndio utupu wako mwenyewe. 11 Utupu wa binti ya mkewe baba yako, aliyezaliwa na baba yako, yeye ni umbu lako, usifunue utupu wake”. Kufunua Utupu wa mtu maana yake kulala na huyo mtu (hiyo ni lugha ya kibiblia).
Walawi 18: 6 “Mtu ye yote aliye wa kwenu asimkaribie mwenziwe aliye wa jamaa yake ya karibu ili kumfunua utupu; mimi ndimi Bwana.
7 Utupu wa baba yako, wala utupu wa mama yako, usifunue, maana ndiye mama yako; usifunue utupu wake.
8 Utupu wa mke wa baba yako, usifunue; maana, ni utupu wa baba yako.
9 Utupu wa umbu lako, binti ya baba yako, au binti ya mama yako, kwamba alizaliwa nyumbani mwenu au kwamba alizaliwa kwengine, utupu wa hao usifunue.
10 Utupu wa binti ya mwanao mume, au wa binti ya binti yako, utupu wao hao usifunue; kwa kuwa ndio utupu wako mwenyewe.
11 Utupu wa binti ya mkewe baba yako, aliyezaliwa na baba yako, yeye ni umbu lako, usifunue utupu wake”. Kufunua Utupu wa mtu maana yake kulala na huyo mtu (hiyo ni lugha ya kibiblia).
Sasa hizo ni sheria zinazogongelea msumari Amri ya USIZINI..Lakini pamoja na hizo sheria ikitokea mtu kazikiuka atahukumiwaje?..Ndio hapo zijahitajika pia HUKUMU juu ya sheria na Amri.
Mfano wa hukumu hizo ni kama ifuatavyo..
Kutoka 22: 19 “Mtu awaye yote alalaye na mnyama sharti atauawa”. Walawi 20: 10 “Na mtu aziniye na mke wa mtu mwingine, naam, yeye aziniye na mke wa jirani yake, mtu mume aziniye, na mwanamke aziniye, hakika watauawa. 11 Na mtu mume atakayelala pamoja na mke wa baba yake amefunua utupu wa baba yake; wote wawili hakika watauawa; damu yao itakuwa juu yao. 12 Na mtu mume akilala na mkwewe mwanamke wote wawili hakika watauawa; wamefanya yaliyo uchafuko; damu yao itakuwa juu yao. 13 Tena mtu mume akilala pamoja na mtu mume, kama alalavyo na mtu mke, wote wawili wamefanya machukizo; hakika watauawa; damu yao itakuwa juu yao”.
Kutoka 22: 19 “Mtu awaye yote alalaye na mnyama sharti atauawa”.
Walawi 20: 10 “Na mtu aziniye na mke wa mtu mwingine, naam, yeye aziniye na mke wa jirani yake, mtu mume aziniye, na mwanamke aziniye, hakika watauawa.
11 Na mtu mume atakayelala pamoja na mke wa baba yake amefunua utupu wa baba yake; wote wawili hakika watauawa; damu yao itakuwa juu yao.
12 Na mtu mume akilala na mkwewe mwanamke wote wawili hakika watauawa; wamefanya yaliyo uchafuko; damu yao itakuwa juu yao.
13 Tena mtu mume akilala pamoja na mtu mume, kama alalavyo na mtu mke, wote wawili wamefanya machukizo; hakika watauawa; damu yao itakuwa juu yao”.
Umeona na Amri nyingine zote 9 zilizosalia zina sheria zake na hukumu zake…Kwahiyo Amri hazijakamilika bila sheria na hukumu. Hiyo ndiyo tofauti ya Amri, sheria na Hukumu.
Hivyo Mungu alipowaambia wana wa Israeli wazishike hukumu zake, alikuwa anamaanisha pia wazitelekeze hukumu za amri zote bila kuacha hata moja, aliyestahili kutozwa kitu atozwe, aliyestahili kutengwa atengwe, aliyestahili kifo, afe n.k.
Lakini Katika Agano jipya tulilopo sasa Amri za Mungu zinaandikwa ndani ya mioyo yetu, na kadhalika sheria na hukumu (Soma Yeremia 31:31-34)...Roho Mtakatifu anapoingia ndani yetu, hatuhitaji sheria kuzishika amri za Mungu..Sisi hatuhitaji kuambiwa kuzini na mnyama ni dhambi..tayari Roho aliyeko ndani yetu anatushuhudia kwamba jambo hilo si sawa..
Sheria anakuwa zinakuwa zimeandikwa ndani kabisa ya mioyo yetu..hatuhitaji kuambiwa kulala na mtu wa jinsia moja nasi ni dhambi..tayari sheria hiyo imeandikwa ndani ya mioyo yetu ipo..Hatuhitaji kuambiwa kuvaa vimini au nguo za nusu uchi ni dhambi..tayari ndani ya moiyo yetu Roho Mtakatifu anashuhudia kuwa jambo hilo si sawa kabla hata ya kuambiwa…hatuhitaji kupewa sheria ya kwamba tuwaheshimu wazazi wetu..tayari sheria hiyo ipo ndani ya mioyo yetu tunaitimiza bila shuruti…Hiyo ndio maana biblia inasema hatuishi kwa sheria bali kwa Imani..
Watu wa agano la kale hawakuwa na upendeleo tuliopewa sisi wa kipawa cha Roho Mtakatifu ambaye angewasaidia kuziishi sheria pasipo nyaraka…lakini sisi tumepewa zawadi hiyo ya Roho..Ni Neema ya ajabu sana..Ndio maana kuna umuhimu sana wa kuwa na Roho Mtakatifu. Ukiwa na Roho Mtakatifu hutakuwa kuwa ngumu kwako kuyatekeleza maagizo yote yaliyopo katika maandiko.
kumbuka biblia inasema wote wasiokuwa na Roho Mtakatifu hao sio wake (Soma Warumi 8:9). Hivyo kama unaona bado ni ngumu wewe kuishi maisha matakatifu basi hauna Roho Mtakatifu, unamhitaji..Na huyo ataingia ndani yako ikiwa utaamua kabisa kwa moyo wako kuukana ulimwengu na kumgeukia yeye..kwa kutubu dhambi zako leo, na kujinyenyekeza mbele zake..Na baada ya kutubu kwa dhati kabisa..bila kuchelewa nenda katafute ubatizo sahihi ukabatizwe kama hujabatizwa…Kumbuka ubatizo sahihi ni ule wa maji mengi(Yohana 3:23) na kwa jina la Yesu Kristo (Matendo 2:38)..Na kisha Roho Mtakatifu atakutia muhuri uwe wake milele. Hapo na kuendelea sheria za Mungu kwako hazitakuwa ni utumwa..bali zitabubujika zenyewe moyoni mwako pasipo hata kusukumwa sukumwa wala kuhubiriwa hubiriwa…
Tofuati kati ya Myahudi, Mwisraeli na Muebrania ni ipi?
TOFAUTI KATI YA SHERIA YA ROHO WA UZIMA NA SHERIA YA DHAMBI NA MAUTI!
Je! hizi roho saba za Mungu ni zipi? na je zinatofautiana na Roho Mtakatifu?
ROHO HUTUOMBEA KWA KUUGUA KUSIKOWEZA KUTAMKWA!
Neno ni lile lile, lakini ujumbe ni tofauti.
Shalom.
Wakati wana wa Israeli wanatoka Misri kuelekea Nchi yao ya ahadi walipokuwa wanapitia jangwani, walifikia mahali panapoitwa Kadesh-Barnea, eneo hilo lilikuwa ni kame sana, na ni eneo lililokuwa limezungukwa na milima mikubwa na mabonde mengi. Katika jangwa hilo ndilo eneo lililokuwa gumu kuliko yote kulivuka..Wana wa Israeli walipoona nyuma walipotoka ni mbali na mbele wanapoelekea ni mbali, Waakanza kumnung’unikia Mungu na Musa..
Ndipo Mungu akamwambia Musa autazame mwamba uliokuwa mbele yao, kiisha aende akaupige kwa ile fimbo aliyokuwa nayo na utatoa maji (Kutoka 17:6)..Musa akafanya kama alivyoagizwa, akaupiga mwamba ule, na maji yakatoka wana wa Israeli wakanywa wakashiba..Safari ikaendelea..
Lakini kikapita tena kipindi kirefu cha miaka mingi, Wakiwa wanazunguka tu huko huko jangwani kwa miaka 40, Mungu akawaleta tena wana wa Israeli eneo lile lile..Kama ilivyo kawaida eneo lile ni baya kushinda maeneo yote yaliyokuwa jangwani wakati ule, hali inazidi kuwa mbaya wakiutazama ule mwamba uliokuwa unachuruzika maji zamani sasa hautoi maji tena. Wakiangalia watoto wao na mifugo yao inaangamia kwa kiu..Kilichobakia kwao ni nini kama si kurudia yale yale waliyoyafanya mwanzoni, ya kumng’unikia Mungu na Musa..
Ndipo Musa akaenda kwa Bwana kumuuliza afanye nini, Ndipo Mungu akamwambia nenda ukasimame mbele ya mwamba ule, UUTAMKIE maji yatoke, nayo yatatoka..Lakini Musa hakuzingatia maagizo Mungu aliyompa..Akaenda kwa desturi na mazoea, akidhani Mungu naye yupo hivyo hivyo kama yeye.. Aliona kwasababu eneo ni lile lile la Kadesh-Barnea, mazingira ni yale yale, mwamba ni ule ule na wala si mwingine..Basi akahitimisha kuwa hata maagizo ni yale yale, ya kwenda kuupiga mwamba..
Hivyo akaenda kuupiga mwamba badala ya kuzungumza nao..Kilichotokea ni kweli maji yalitoka katika mwamba ule, watu wakanywa wakashiba, akadhani tayari kashatimiza kusudi la Mungu..Lakini Mungu alimwambia…
Hesabu 20:12 “Bwana akamwambia Musa na Haruni, Kwa kuwa hamkuniamini mimi, ili kunistahi mbele ya macho ya wana wa Israeli, basi kwa sababu hiyo, hamtawaingiza kusanyiko hili katika ile nchi niliyowapa”.
Ni kawaida ya Mungu kurudia mazingira yale yale kuzungumza na wewe, Lakini hiyo hauufanyi ujumbe kuwa ni ule ule..Kwamfano hii biblia tunayoisoma, ni ndogo tu yenye vitabu 66. Ukisoma unaweza ukaimaliza yote ndani ya wiki moja tu. Na wapo watu wameshaisoma na kurudi hata zaidi ya mara 500 siku zote za maisha yao. Lakini kama utaisoma tu kwa lengo kupata habari nyingine mpya, hutaambulia chochote, kwasababu kwako itakuwa ni kurudia rudia, na mwisho wa siku itakuboa.
Lakini kama utaisoma kwa lengo la kuisikia sauti ya Mungu, kila siku mstari mmoja utauona ni mpya kwako, kana kwamba hukuwahi kuusoma huko nyuma kabisa. Ni kwasababu gani, ni kwasababu uliweka ufahamu wako wote, kuisikia sauti ya Mungu, zaidi ya kuangalia uzoefu wako katika ulichokisoma au kukisikia.
Mfano mwingine katika maandiko ni huu, Kama ukisoma Kitabu cha Ufunuo, sura ile ya pili na ya tatu, utaona Bwana Yesu akimpa Yohana zile barua azipeleke katika yale makanisa 7 ya Asia ndogo..
Na ni kweli Yohana alipotoka katika kisiwa cha Patmo, alizitawanya zile barua kwa watakatifu wote waliokuwa katika miji yote saba ya Asia ndogo, na kila kanisa lilikuwa na ujumbe wake maalumu uliokuwa unalihusu kanisa hilo husika..Lakini kumbe ujumbe ule haukuwa tu kwa kipindi kile..Lakini Sisi tunaoishi katika wakati huu wa mwisho ndio tunaoelewa vizuri kuwa makanisa 7 pia yanamaanisha makanisa ya nyakati… Tangu kipindi cha mitume hadi sasa zimepita Nyakati saba za kanisa, na sisi ndio tunaoishi katika lile kanisa la mwisho na la saba linalojulikana kama Kanisa la Laodikia ambalo lilianza mwanzoni mwa karne ya 20 yaani miaka ya 1900, na litaisha na unyakuo.
Hivyo tunapaswa tuwe makini sana, katika kuisikia sauti ya Mungu, na kutokulizoelea Neno lake kwa kigezo cha mazingira yale yale yanayojirudia…kwa kigezo cha mistari ni ile ile tuliyowahi kuisoma… Laiti kama Musa angeisikia sauti ya Mungu ni nani ajuaye kuwa Mungu alikuwa amepanga mwamba ule utitirishe maji yake daima, utoe mto ndani yake ambao utafuatana nao mpaka watakapoingia katika nchi ya ahadi, tofauti na ile mara ya kwanza umbapo ulitoa tu maji kwa muda na ukakata?.
Kwasababu biblia inasema mwamba ule ulikuwa unamfunua Kristo, na Kristo huwa hatoi maji ya muda tu, bali chemichemi za maji ya uzima zinazotiririka daima. (1Wakorintho 10:4)
Hivyo, Mungu anafundisha tusilizoelee Neno lake, yapo mengi anataka kutufundisha kila siku, zipo hatua nyingi anataka kutupigisha kila siku, lakini kama tukishasema, Aah! Hichi tayari nilishahubiriwa, au hichi tayari nilishakisikia.. tujue kuwa bado tu wachanga katika kuielewa sauti ya Mungu.
Biblia inasema katika 1 Wakorintho 8:2
“Mtu akidhani ya kuwa anajua neno, hajui neno lo lote bado, kama impasavyo kujua”.
Ni matumaini yangu na maombi yangu, sisi sote kwa ujumla, tutaanza kuitafuta sauti ya Mungu, bila kujali ni tumeshahubiriwa Neno lile lile mara ngapi, tumeshalisoma Neno lile lile mara ngapi..
Zaburi 12: 6 “Maneno ya Bwana ni maneno safi, Ni fedha iliyojaribiwa kalibuni juu ya nchi; Iliyosafishwa mara saba”.
Ubarikiwe sana. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
IELEWE SAUTI YA MUNGU.
PENGINE MUNGU ALISHASEMA NAWE KWA NJIA HII.
KAMA MUNGU ANABORESHA KAZI ZAKE, KWANINI WEWE USIBORESHE ZA KWAKO?.
VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 1
KITABU CHA YUDA: SEHEMU YA 1
Siku ya unyakuo itakukutaje?
Shalom.Jina la Bwana wetu Yesu Krito libarikiwe.
Karibu tujifunze Biblia..Je unajua kuwa kuna siku Kristo atakuja kuwachukua wateule wake? Na kwenda nao mbinguni?..Je unajua watakaokwenda mbinguni ni wachache sana?…Biblia inasema njia ile imesonga na mlango ni mwembamba?..
Mathayo 7:14 “ Bali mlango ni mwembamba, na njia imesonga iendayo uzimani, nao waionao ni wachache”.
Je unajua…baada ya unyakuo kupita…watu watakaoachwa watajuta sana?..Wengi watatamani muda urudishwe dakika 5 tu nyuma angalau watubu…lakini watakuwa wameshachelewa…Je unajua karibia kila mtu duniani tayari kashaonyeshwa aidha kwa ndoto au kwa maono siku ya unyakuo? awe mwenye dhambi au asiye mwenye dhambi…tayari kashaota ndoto angalau moja inayohusiana na kurudi kwa Kristo mara ya pili?. Na wengi wao wanaoonyeshwa hayo wanakuwa wameachwa?..Na wanapata hisia kali sana baada ya kuamka na wanashukuru Mungu imekuwa ni ndoto na wala si kitu cha kweli?.
Binafsi nilishawahi kuota ndoto kama hizo mara kadhaa zamani sana…na zote nilikuwa najiona nimeachwa ni chache sana nilijiona nimekwenda na Bwana lakini nyingi nimeachwa.…na nikiwa ndani ya ndoto nilikuwa nalia na kuomboleza na kumwomba Mungu anirudishe muda angalau dakika 5 nyuma kabla ya unyakuo nirekebishe mambo yangu!…na nikishtuka kutoka usingizini nashukuru Mungu kwamba ni ndoto na si kitu halisi..Hivyo nakwenda kutubu na kumuahidi Mungu kuzidi kujitakasa ili nisije nikaachwa kwenye unyakuo halisi utakapofika…
Lakini yote hayo ni tisa..kumi ni siku tutakayokutana na tukio lenyewe la kuachwa kwenye unyakuo!!…
Siku moja, muda mrefu kidogo umepita, tulikuwa ndani ya nyumba nyakati za jioni kama saa moja na nusu hivi usiku…Umeme ulikatika mtaa mzima..Kukawa na giza lile tororo kabisa..tukaamua kutoka ndani kukaa nje…Na Mahali tulipokuwa tunaishi sio mahali penye watu wengi wanaojichanganya na wengine ni mahali ambapo ikifika jioni tu ni kimyaa na kila mtu kajifungia kwake..Sasa wakati tumekaa nje kidogo tulikuwa wawili mimi na ndugu yangu…tukasema hebu tutazame juu kidogo tuangalie nyota utukufu wa Mungu mbinguni…
Siku hiyo haikuwa na mawingu hivyo nyota zilikuwa zinaonekana vizuri hata zile zinazotembea….….Sasa wakati tunatazama juu ulitokea mwanga fulani wa ajabu wenye rangi unaokaribiana na blue hivi unaong’aa sana, kama mita 5 hivi juu yetu..ukimulika kutokea upande wa magharibi kuelekea upande wa mashariki..na ulikuwa kama unasogea hivi…. Haukuwa na sauti hata kidogo lakini ulikuwa na mwangaza mkali na ulidumu kwa muda kama wa sekunde 3 hivi au Zaidi kidogo..halafu ukatoweka!..ulimulika pale tulipokuwepo kote kukawa kama mchana hivi…
Haukuwa mwanga wa radi kwasababu kipindi hicho kilikuwa ni kipindi cha kiangazi, na wala haikuwa ile mianga inayotokea inamulika bila sauti yoyote wakati wa vipindi vya mvua. Siku hiyo juu hakukuwa na wingu hata moja ni nyota tuu zilikuwa zimetanda anga zima..tokea kaskazini, kusini mashariki mpaka magharibi..hakukuwa na dalili ya wingu…Na mwanga huo hakuja na sauti yoyote…Nakumbuka siku chache tu nyuma tulikuwa tunazungumzia masuala ya unyakuo..Na tulikuwa tunaufahamu ule mstari unaosema…
Luka 17:24 “kwa kuwa, kama vile umeme umulikavyo toka upande huu chini ya mbingu hata upande huu chini ya mbingu, ndivyo atakavyokuwa Mwana wa Adamu katika siku yake.”
Kwahiyo baada ya tukio hilo..Mstari huo ukaja kichwani haraka sana!…tukajua kwamba kuna uwezekanano tayari unyakuo umeshapita na tumeachwa…Baada ya hapo ilikuja hisia moja ambayo siwezi kuilezea, ambayo tangu huo wakati ndio ikanifanya nisichukulie tena kiwepesi suala la kubaki kwenye unyakuo…
Nilihisi kuvunjika moyo na kujuta majuto ambayo sijawahi kuyajuta…Nilianza siku zote nilikuwa nafanya nini mpaka siku hii imenikuta kama mjinga…Nikaanza kuwaza siku chache tu mbeleni nakwenda kumshuhudia mpinga-Kristo kwa macho yangu..siku chache mbeleni nakwenda kupokea chapa…siku chache mbeleni nakwenda kukutana na dhiki kuu, kama sitakufa basi nitashuhudia mapigo yote yale yaliyoandikwa kwenye kitabu cha Ufunuo sura ya 16, maji kuwa damu, jua kutiwa giza, mvua ya mawe n.k..Nikawaza siku chache tu mbeleni hakutakuwa tena na ndugu, wala mama, wala marafiki…wala hakutakuwa tena na kitu kinachoitwa nyumbani…wala hakutakuwa tena na kufanya kazi..Mwisho wa mambo yote umeshafika!.
Nikawaza tena wakati huu sasa hivi watakatifu, waliojitakasa na kuyachukia Maisha yao kwaajili ya Kristo wanafarijiwa mbinguni..sasa hivi Paulo, anafutwa machozi na tabu zake zote zinageuzwa kuwa furaha…Nikarudi kuwaza tena..Nikifa katika dhiki kuu ninakwenda kusimama mbele ya kiti cha hukumu..kuonana uso kwa uso na Yesu Kristo… na mwishowe kuhukumiwa nakwenda kutupwa kwenye ziwa la moto.. Nikakumbuka tena hakuna kutubu katika hii hali tuliyopo sasa..Wakati tunatafakari hayo wote wawili tulijua unyakuo umepita na tumeachwa….Tukawaza tutajibu nini mbele ya kiti cha hukumu.
Usiku ulizidi kuingia nikitamani hata mvua inyeshe ili tujifariji kwamba angalau ulikuwa ni mwanga wa radi ya mvua lakini wapi hakuna chochote…Nikatazama tena ujirudie juu ili pengine tuseme ni kawaida mianga mianga kupiga wakati wa mvua lakini wapi…..hakuna kilichotokea!…palikuwa pakame na juu kulikuwa kweupe vile vile, nyota zimetanda kote na hakuna hata dalili ya wingu …Zile hisia kali za kutazamia mambo yatakayoikumba dunia zilikuwa tayari zimeshafunika hisia za wakati tuliopo…nilitamani siku hiyo iwe ndoto..nizinduke usingizini nitubu kwa kumaanisha kubadilika kabisa..lakini wapi! Ilikuwa ni hali halisi kabisa..
Ndipo asubuhi Bwana akaanza kutufundisha…kwamba haukuwa unyakuo, bali Bwana alikuwa anataka kutufundisha hali itakayotukuta endapo tukiukosa unyakuo..(Na pia kuhusu jambo lingine ambalo halihusiani na hii mada ya leo alituambia kuhusu tukio hilo). Lakini kikubwa ni kuhusu siku ile itakavyokuwa. Na hisia zitakazowapata watu siki hiyo.
Hisia hizo ndizo zitakazowakuta wengi watakaoukosa unyakuo..na siku hiyo watakaoumia sana ni wale ambao tayari kwa namna moja au nyingine walishawahi kuisikia injili huko nyuma lakini hawakutubu au walipuuzia…ambao jana tu walitoka kuhubiriwa lakini wakaikataa injili au wakaipuuzia, ambao juzi tu wametoka kusikia au kusoma habari za kuja kwa Yesu mara ya pili lakini walipuuzia…Hao ndio watakaoomboleza sana na kulia..wengine wote wataona kawaida.
Hiyo kwetu ilikuwa ni ishara kubwa sana ambayo Mungu alizungumza na sisi..Kwa kweli ilitubadilisha Maisha yetu tangu huo wakati…Mpaka leo hii siwezi kuisahau hiyo hisia…nasema nikose chochote lakini sio UNYAKUO..Na namshukuru Mungu kwa kuzungumza na mimi kwa ishara ya nje kabisa kwani angesema nami kwa ndoto tu kama siku zote pengine nisingechukulia kwa uzito kwa kiwango hicho na mpaka leo ningebaki kuchukulia kuachwa ni jambo la kawaida.
Ndugu Kuna uchungu wa ajabu na hisia mbaya sana kwa watu watakaoukosa unyakuo…Hebu jiweke kwenye mazingira leo hii ndio unyakuo umepita na umeachwa?..utajisikiaje! labda unaweza usielewe sasa mpaka siku hali hiyo itakapokukuta…Lakini usitamani uwepo..Siku hiyo utasikia unyakuo umepita masaa machache tu umepishana na mahubiri ya kukuonya utubu.
Je! Umejiweka tayari?..Biblia inasema katika Waebrani 10:37 “Kwa kuwa bado kitambo kidogo sana, Yeye ajaye atakuja, wala hatakawia”.
Leo hii unasema unyakuo bado sana..siku hiyo ikifika utatamani urudishwe dakika 5 nyuma urekebishe mambo yako lakini utakuwa umeshachelewa.
Kama hujaokoka leo mlango wa Neema upo wazi..Hivyo pale ulipo jinyenyekeze kwa Mungu..Mwombe akusamehe dhambi zako zote ulizokuwa unazifanya za makusudi na ambazo sio za makusudi..Kisha baada ya kutubu fanya kama ulivyotubu..acha kufanya dhambi ulizokuwa unazifanya…kama ulikuwa mwasherati..acha uasherati, ulikuwa mwizi vivyo hivyo unaacha, ulikuwa unavaa nusu uchi..unaacha..ulikuwa mtazamaji wa picha chafu mitandaoni unazifuta na kuanza maisha mapya..
Ukishafanya hivyo Kristo atakupa amani ya ajabu moyoni mwako.Amani hiyo utakayoipata ndio itakuwa uthibitisho wa msamaha wako..Baada ya kufanya hivyo nenda kabatizwe kama hujabatizwa, ubatizo sahihi ni ule wa kuzamishwa katika maji mengi na kwa jina la Yesu Kristo. Na Roho Mtakatifu ndani yako atakuongoza katika mambo mengine yaliyosalia ikiwemo kukupa uwezo wa kushinda dhambi na ufahamu wa kuyaelewa maandiko. Ukiishi katika hali hiyo biblia imetupa uhakika wa kunyakuliwa Kristo atakaporudi..Hakuna namna yoyote ambayo unaweza usinyakuliwe.
Bwana azidi kutupa Neema yake tushinde ulimwengu huu kama yeye alivyoshinda. Ili siku ile tuifarahie karamu aliyotuandalia mbinguni milele.
Maran atha!
jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
UNYAKUO.
Ule mfano wa wanawali 10 (Mathayo 25), wale watano hawakuwa na mafuta ya ziada katika chupa zao je yale mafuta ya ziada yanawakilisha nini?
SIKU YA TAABU YA YAKOBO.
MAPIGO YA VITASA SABA, NA SIKU YA BWANA.
DHAMBI ILIYOMKOSESHA SHETANI:
Haya ni maneno matatu tofauti lakini kiuhalisia yanangumzia kitu kimoja..Ni sawa na useme, mtanzania, mtanganyika, na mswahili..Ni yule yule isipokuwa inategemea unamzungumzia katika nyanja ipi.
Ndivyo ilivyo kwa taifa la Israeli. Waebrania chimbuko lake ni Ibrahimu na kwa mara ya kwanza jina hilo linaonekana katika kitabu cha (Mwanzo 14:13) likimtambulisha Ibrahimu,ambapo kwa wakati huo akiitwa Abramu. Na baadaye tena tunaona Yusufu naye akitajwa kwa jina hilo (Mwanzo 39:14, 17)…Hivyo ni jina lililokuwa linawatambulisha wazao wote wa Ibrahimu, Japo biblia haitoi tafsiri yoyote halisi ya jina hilo, wengine wanasema jina hilo lina maana ya aliyevuka kutoka ng’ambo.
Lakini Israeli, ni jina jipya la Yakobo mwana wa Isaka, mjukuu wa Ibrahimu. aliitwa vile kutokana na kwamba alishindana na malaika wa Bwana usiku kucha katika mueleka na kumshinda, hivyo jina lake likabadilishwa na kuitwa Israeli, hivyo Watoto wake wote, waliozaliwa baada yake waliitwa wana wa Israeli, hadi walipoingia utumwani Misri walijulikana kwa majina yote mawili yaani wana wa waisraeli au waebrania. Lakini jina Israeli lilipata nguvu Zaidi hadi wakiwa wanarudi na kukaa katika nchi yao ya Ahadi..walifahamika kama waisraeli.
Lakini miaka mingi ilipopita na Taifa la Israeli kugawanyika katika pande kuu mbili, kaskazini na kusini. Wale waliokuwa upande wa kaskazini walibakia na jina hilo la Israeli, lakini waliokuwa katika upande wa kusini waliitwa Wayudea..Kutoka katika Neno Yuda, kwasababu taifa la Yuda ndilo lililokuwa linatawala upande wa kusini.
Lakini sasa mataifa yote yalipochukuliwa utumwani, yaani wale wa kaskazini kupelekwa Ashuru, na wale wa kusini kupelekwa Babeli, kama tunavyosoma waliorudi kwa asilimia kubwa katika nchi yao ni wale wa kusini waliopelekwa Babeli mara baada ya ile miaka 70 kuisha iliyotabiriwa na Danieli.. Hivyo walivyorudi jina lao waliendelea nao , wakijulikana kama wayudea, na ndio huko huko jina WAYAHUDI wayahudi lilipozaliwa..Maana ya wahayudi ni watu wa ardhi ya Uyahudi,au Yudea au Yuda. Hivyo watu wote wa taifa zima wakaitwa Wayahudi ikijumlisha hata na wale wachache waliorudi kutoka Ashuru walijulikana wote kama Wayahudi.
Lakini hiyo haikubadilisha asili yao kuitwa Waisraeli au Waebrania.
Kutokana na kuwa watu wa Yuda ndio Mungu aliwachagua kusimamia ujenzi wa hekalu na mji mtakatifu wa Mungu.Vilevile ndilo Kabila lililokuwa linatazamiwa kumleta Masihi wa ulimwengu duniani, Hivyo hiyo ililifanya kabila hilo liwe lenye misingi ya kiimani Zaidi ya mengine. Hivyo mwisraeli yoyote aliyejiita myahudi kwa wakati ule alikuwa ni sharti awe anazingatia dini na desturi zote za kiyahudi.
Hata leo hii, Taifa la Israeli ni kubwa lenye watu wengi waliozaliwa kule, ambao kiuraia wanajulikana kama waisraeli wengine waislamu, wengine wakristo, wengine hawana dini, lakini pamoja na wingi wao, na utaifa wao, si wote walio wayahudi. Wayahudi ni wale ambao wanashikilia misingi ya torati na tamaduni zao za kidini.. wanashika sikukuu zote zilizoamuriwa kwenye torati, vilevile wanafanya ibada kama vile za agano la kale.
Hivyo kwa ufupi, Myahudi yeyote anaweza kuitwa mwisraeli, au mwebrania lakini Mwisraeli yeyote hawezi kuitwa myahudi. Kama vile mtu yeyote aliyezaliwa Tanzania hata kama ni mzungu anaweza kuitwa mtanzania..Lakini sio kila mtu aliyezaliwa Tanzania anaweza akawa mswahili.. Mswahili ni jambo linaloendana na chimbuko la watanzania na lugha zao na desturi zao za asili.
Hiyo ndio Tofuati kati ya Myahudi, Mwisraeli na Muebrania
Ubarikiwe. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Je! wayahudi wote wataokolewa hata kama ni watenda dhambi, Kwasababu wote ni uzao wa Ibrahimu?
MZEITUNI HALISI UTAKAPOPACHIKWA.
NG’OMBE MWEKUNDU ALIYEZALIWA ISRAELI, ANAFUNUA NINI?
CHUKIZO LA UHARIBIFU
Je kuchoma maiti ni dhambi? mpaka iteketee kabisa na kuwa jivu?..Kwamfano maiti ya mtu aliyeokoka kuichoma kama wanavyofanya wahindu ni dhambi?..je hizo ni ibada za wafu?..mtu akifa roho yake inakwenda wapi?
JIBU: Kila kitu kinachofanywa na wanadamu kina sababu…hakuna kitu kinachofanyika bila sababu..katika Maziko, watu wanaoosha maiti kuna sababu kwanini wanafanya vile..kadhalika watu wanaoosha maiti na yale maji kupikia pia ipo sababu ya wao kufanya hivyo..Wanaokata kipande cha nyama ya maiti na kula kabla ya kumzika ipo sababu ya wao kufanya hivyo..
Kwahiyo hata wanaochoma maiti ipo sababu ya wao kufanya hivyo.. hawachomi basi tu kufanya mazingira yawe masafi..hapana! bali wanasababu kubwa kufanya hivyo..Na sababu hiyo ni ya kiroho…
Wahindu wanaamini kwamba mtu akifa roho yake inakuwa inaelea hapa hewani…lakini roho ya mtu yule bado inakuwa ina uwezo wa kuona na kuhisi mazingira iliyokuwepo..Na hiyo ni kutokana na ule mwili ulioacha hapo chini. Mwili ule unaizuia ile roho kuendelea na safari yake ya kwenda mbinguni..Kwahiyo ili kuifanya ile roho isibakie hapo juu muda mrefu..wahindu wanauchoma ule mwili kwa moto wote uteketee..ili roho isibaki kuutazama mwili na kuendelea kuishi katikati ya mazingira iliyokuwa inaishi.
Na baada ya mwili ule kuchomwa basi ile roho itakwenda mbinguni kwa haraka.
Je Mtazamo huo ni sahihi?
Jibu ni la!..Mtu akishakufa kama ni mwenye haki roho yake inakwenda moja kwa moja mahali panapojulikana kama paradiso au peponi…na anakuwa hana mawasiliano tena na mwili wake. Kadhalika aliyekufa katika dhambi anakwenda mahali pajulikanapo kama kuzimu/jehanamu. Naye pia anakuwa hana mawasiliano na mwili wake uliokufa.
Kwahiyo ni uongo wa shetani kusema kwamba mwili unazuia roho kwenda mbinguni..hivyo unapaswa uchomwe moto!..Hizo ni IBADA ZA WAFU. Kama zinavyofanywa na kanisa katoliki za kuwaombea wafu!.
Hivyo shetani amewadanganya watu wafanye hivyo (wachome maiti)..Kwasababu anajua kitendo hicho ni kama sadaka…Kumbuka sadaka zote katika agano la kale zilikuwa zinafanyika kwa kuchomwa…Sadaka ya kuteketezwa ilikuwa inafanyika kwa kumchukua aidha mwanakondoo au mbuzi na kumchinja na hatimaye kumkatakata na kuuweka mwili wake juu ya madhabahu na kuuchoma kwa moto mpaka uteketee kabisa..Na kitendo hicho kilikuwa kinaleta matokeo makubwa sana katika ulimwengu wa roho. Na madhabahu ilikuwa inatengenezwa kwa mawe kadhaa na juu ya mawe hayo zinapangwa kuna na kondoo anawekwa juu yake…kama tu wahindu wanavyoteketeza maiti zao.
Katika agano la kale Ili dhambi ifunikwe ni lazima sadaka ya kuteketezwa ifanyanyike..Na mambo mengine yote ili yafanikiwe ni lazima sadaka ya kuteketezwa itumike.
Sasa baada ya Agano jipya kuja..sadaka hizo Mungu alizifuta!…Yesu Kristo kwa kupigwa kwake na kufa kwake pale msalabani yeye ndiye akafanyika kuwa sadaka kwa ajili yetu.(Soma Waebrania 10:1-10)..Hatuhitaji tena maiti ya kondoo kuteketezwa kwa moto juu ya madhababu ndipo tupate msamaha wa dhambi…Damu ya Yesu Kristo inatosha.
Lakini shetani kazi yake ni kucopy vitu na kuvigeuza na kuvitumia kwa faida zake..Naye pia akaiga mfano huo wa sadaka za kwanza za kuteketezwa kufanya shughuli zake…leo mtu akienda kwa waganga ataambiwa apeleke mbuzi, au kuku achinjwe na damu ipatikane..sehemu nyingine ataambiwa amchinje na kumchoma moto…majivu akatupe baharini n.k
Sasa shetani kwa kuimarisha uchawi wake akaona maiti za mbuzi na kuku hazitoshi…sasa akahamia kwa maiti za watu…Na hizo atazipataje kirahisi?..kwa kuanzisha mafundisho hayo potofu ya roho kuelea hewani… ili watu wachome maiti na kafara iwe imeshafanyika… Na matokeo ya kafara hizo ni kuingiza mapepo ndani ya watu hususani wafiwa na washiriki wa kafara hiyo.
Baada ya kumaliza kafara hiyo mtu yule aliyeshiriki..hali yake ya kiroho inakuwa mbaya zaidi kuliko alivyokuwa hapo kwanza.
Sasa sisi wakristo hatupaswi kabisa kufanya hayo mambo…kwasababu yanahusiana na ibada za wafu..Na biblia imetuonya tusifanye hivyo au mambo yanayokaribiana kufanana na hayo..
Ezekieli 20:31 “Tena mtoapo matoleo yenu, na kuwapitisha watoto wenu motoni, je! Mnajitia unajisi kwa vinyago vyenu vyote hata leo? Na mimi je! Niulizwe neno nanyi, Enyi nyumba ya Israeli? Kama mimi niishivyo, asema Bwana MUNGU, sitaulizwa neno na ninyi”.
Soma tena..
2 Wafalme 17:16 “Wakaziacha amri zote za Bwana, Mungu wao, wakajifanyizia sanamu za kusubu, yaani, ndama mbili, wakafanya na Ashera, wakaliabudu jeshi lote la mbinguni, wakamtumikia Baali. 17 Wakawapitisha watoto wao, waume na wake, motoni, wakapiga ramli, wakafanya uchawi, wakajiuza nafsi zao wapate kufanya yaliyo maovu machoni pa Bwana, hata kumkasirisha. 18 Kwa hiyo Bwana akawaghadhibikia Israeli sana, akawahamisha mbali na uso wake; wala hapana aliyesalia ila kabila ya Yuda peke yake”
2 Wafalme 17:16 “Wakaziacha amri zote za Bwana, Mungu wao, wakajifanyizia sanamu za kusubu, yaani, ndama mbili, wakafanya na Ashera, wakaliabudu jeshi lote la mbinguni, wakamtumikia Baali.
17 Wakawapitisha watoto wao, waume na wake, motoni, wakapiga ramli, wakafanya uchawi, wakajiuza nafsi zao wapate kufanya yaliyo maovu machoni pa Bwana, hata kumkasirisha.
18 Kwa hiyo Bwana akawaghadhibikia Israeli sana, akawahamisha mbali na uso wake; wala hapana aliyesalia ila kabila ya Yuda peke yake”
Hivyo si sahihi kuchoma maiti..(kuchoma maiti ni dhambi!).. Maiti ikiungua yenyewe labda kwa ajali ya moto mpaka kufikia jivu..hapo hakuna ibada yoyote iliyohusika..majivu yake yatakwenda kuzikwa na hakuna ibada yoyote ya kiroho hapo… lakini kama ikihusisha masuala ya imani au ibada tayari ni dhambi kubwa mbele za Mungu.
Bwana akubariki.
Je umeokoka?..Au bado unaupenda ulimwengu?..kumbuka shetani yupo kasambaza kila kona upotofu wake..Na tunaishi katika siku za mwisho za kurudi Yesu Kristo. Unyakuo upo karibu sana kutokea na watakatifu watakwenda na Bwana. Je utakuwa miongoni mwao?..Hivyo tubu leo kama hujatubu na Bwana atakupokea, na kukupa Roho wake Mtakatifu.
Maran atha! jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
NINI KINATOKEA BAADA YA KIFO?
https://wingulamashahidi.org/2018/06/27/maswali-na-majibu/
Bwana alimaanisha nini kusema “waache wafu wazike wafu wao.(Mathayo 8:21)?
HERI WAFU WAFAO KATIKA BWANA
KUZIMU ni mahali pa namna gani, Je! huko wanaishi watu wakifa na kwenda kupata mateso au ni vinginevyo?
Roho za Wanyama zinakwenda wapi baada ya kifo? Je! Watafufuliwa?
Wokovu wa milele/ Ulinzi wa daima (eternal security) Je! ni neno la kimaandiko?
MKUU WA ANGA.
Yohana 7:45 ‘’Basi wale watumishi wakawaendea wakuu wa makuhani na Mafarisayo. Nao wakawaambia, Mbona hamkumleta? 46 Wale watumishi wakajibu. Hajanena kamwe mtu ye yote kama huyu anavyonena. 47 Basi Mafarisayo wakawajibu, Je! Ninyi nanyi mmedanganyika? 48 Ni nani katika wakuu amwaminiye, au katika Mafarisayo?
Yohana 7:45 ‘’Basi wale watumishi wakawaendea wakuu wa makuhani na Mafarisayo. Nao wakawaambia, Mbona hamkumleta?
46 Wale watumishi wakajibu. Hajanena kamwe mtu ye yote kama huyu anavyonena.
47 Basi Mafarisayo wakawajibu, Je! Ninyi nanyi mmedanganyika?
48 Ni nani katika wakuu amwaminiye, au katika Mafarisayo?
Amen. Leo hii tujiulize ni kwanini mtu aliye maarufu kuliko wote duniani kwa wakati wote na vizazi vyote ni YESU KRISTO?.
Ukiona hivyo ujue si bure kuna kitu alichokuwa nacho ambacho hakuna mtu mwingine duniani anacho,. Leo hii kitabu kinachosomwa kuliko vitabu vyote duniani ni biblia, kinachofuata chini yake hakikaribii hata chembe, na katika hiyo hiyo biblia ni miongoni mwa vitabu vinavyosomwa zaidi ni vitabu vya injili vinavyozungumzia maisha ya YESU, na maneno ya Yesu Kristo kwa ujumla. Ukiona hivyo ujue si bure bure tu, lipo jambo watu wameona ndani yake.
Wale watu waliotaka kwenda kumkamata Yesu na kumfunga, wakidhani yule alikuwa ni mtu wa kawaida tu labda pengine ni mwana mapinduzi ametokea anataka kuipundua nchi, au mwanasiasa Fulani kama wengine, au mwanaharakati huru, au jasusi, lakini walipokutana na maneno yaliyotoka kwenye kinywa chake..Matarajio yao yaligeuzwa, Nia zao zilibadilishwa, fahamu zao zikafunguliwa..Na wakakiri kwa vinywa vyao.
Hajanena kamwe mtu ye yote kama huyu anavyonena…, Kauli hiyo inathitisha kuwa walizunguka sehemu nyingi kushughulika na watu wa namna yake, wamekutana na wengi, wamewasikia wengi, na kufanikiwa kuwakamata, lakini walipofika kwa huyu, na kusikia maneno yale.. walikiri kwa vinywa vyao, hawajawahi kuona mtu aliyenena kama yeye..Maneno yaliyojaa neema, na uweza, na nguvu, na matumaini, na faraja, na elimu, na maarifa, na uzima, na roho.
Sasa ni miaka 2000 imepita, lakini kila kizazi, kinashuhudia hajatokea mtu yeyote mfano wa Yesu Kristo mwenye maneno ya kipekee kama yeye. Walikuwepo wengi wameondoka…Lakini kwa Kristo maneno yake yaliposikiwa yalipenya mpaka kwenye vilindi vya mioyo ya watu.
Embu fikiria mtu anayekuambia maneno haya;
Mathayo 11:28 “ Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. 29 Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu; 30 kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi..”
Mathayo 11:28 “ Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.
29 Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu;
30 kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi..”
Anakuambia tena.
Yohana 4:13 ‘’Yesu akajibu, akamwambia, Kila anywaye maji haya ataona kiu tena; 14 walakini ye yote atakayekunywa maji yale nitakayompa mimi hataona kiu milele; bali yale maji nitakayompa yatakuwa ndani yake chemchemi ya maji, yakibubujikia uzima wa milele.
Yohana 4:13 ‘’Yesu akajibu, akamwambia, Kila anywaye maji haya ataona kiu tena;
14 walakini ye yote atakayekunywa maji yale nitakayompa mimi hataona kiu milele; bali yale maji nitakayompa yatakuwa ndani yake chemchemi ya maji, yakibubujikia uzima wa milele.
Maneno hayo ni matamu sana…”
Sikia na haya..
Yohana 11:25 “Yesu akamwambia, Mimi ndimi huo ufufuo, na uzima. Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa anaishi; 26 naye kila aishiye na kuniamini hatakufa kabisa hata milele. Je! Unayasadiki hayo?”
Yohana 11:25 “Yesu akamwambia, Mimi ndimi huo ufufuo, na uzima. Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa anaishi;
26 naye kila aishiye na kuniamini hatakufa kabisa hata milele. Je! Unayasadiki hayo?”
N.k N.k. Yapo mengi..Hakuna kiongozi yeyote wa dini alishawahi kuahidi maneno kama haya na akayatelekeza, hata sasa hakuna..Na ndivyo inavyojulikana kwa watu wote, na dini zote, hakuna kama YESU KRISTO, Na kamwe hatakuwepo mtu anayenena maneno yaliyojaa neema kama yeye.
Maneno yake yamewabadilisha maelfu kwa maelfu, mamilioni kwa mamilioni, yamehakikishwa, yamethibitishwa ni kweli..Hakuwa mwanasiasa yule, kuahidi mambo ambayo hawezi kuyatimiza, Hata wewe leo hii ukiamua kumwamini na kumfuata kweli kweli, zile chemchemi za maji ya uzima alizozisema miaka 2000 iliyopita zitaanza kutiririka ndani yako leo..
Kama umelemewa na mizigo ya dhambi, na masumbufu ya maisha haya mpaka umekata tamaa ya kuishi, ukimfuata, atakupumzisha kweli kweli, kama alivyoahidi,..Utapata tumaini jipya, na mwanzo mpya wa maisha, hakuna aliyekwenda kwake akajuta..utafutaji wa mali hautakupa faraja!..Umezitafuta miaka yote je zimekufariji?..zaidi sana zinakutia presha kuliko kukufariji..
Na ndio maana maandiko yanasema..
Zaburi 34:8 “Onjeni mwone ya kuwa Bwana yu mwema; Heri mtu yule anayemtumaini”.
Onja na wewe, Yesu anayehubiriwa ulimwenguni kote, anaokoa kweli maisha ya watu, usimwache akupite.
Ikiwa bado unatanga tanga na ulimwengu..unasubiri nini? .Ikiwa bado unatazamia mtu mwingine atakayekutamkia maneno mazuri na ya faraja Zaidi ya Kristo, nataka nikuambie hautampata na hatakuwepo,. Tubu dhambi zako leo anza mwanzo mpya na Kristo. Hapo ulipo Bwana anaweza kukuokoa ikiwa utamaaanisha kweli kutubu. Unachopaswa kufanya ni kupiga magoti na kumweleza Kristo kuwa unahitaji msamaha wake na msaada wake. Na kwamba umemaanisha kuwa kuanzia leo na kuendelea utakuwa mwanafunzi wake, na utamfuata kwa gharama zote..Sasa Ukishatubu kuwa kumaanisha kabisa, ujue kuwa Kristo ameshakusamehe, kwasababu yupo hapo pembeni mwako kukusikia..
Unachopaswa kufanya, hatua inayofuata ni kuonyesha toba yako kwa vitendo, na tendo la kwanza ni kuacha yale mambo maovu uliyokuwa unayafanya nyuma, kukaa mbali nayo,..yote pamoja na vichochezi vyake.. pili unatafuta ubatizo sahihi wa kuzamishwa katika maji mengi na kwa jina la YESU KRISTO, kama hujabatizwa hivyo… na tatu ni kutafuta ushirika wakristo wa kweli walio karibu nawe na kujumuika nao..ili uweze kujifunza Neno la Mungu, kumega mkate na kusali kwa pamoja.
Na Kwa kufanya hivyo utakuwa umemdhihirishia Mungu toba yako kuwa ni kweli kwa Matendo yake..Na yeye akishaona hivyo atakuhakikishia ulinzi wa daima ikiwa hutatia nia ya kugeuka nyuma..atahakikisha anakupa uwezo wa kufanyika mwana wa Mungu. Hiyo ikiwa na maana kuwa atakuvika uwezo wa kufanana na Yesu Kristo, kwa neema zake. Na kuanzia hapo utaweza kuishinda dhambi kirahisi kwasababu Roho wa Mungu atakuwa ameshaachiliwa juu yako.
Bwana akubariki.jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
MTETEZI WAKO NI NANI?
BASI MUNGU AKAMUADHIMISHA SANA..
UFUNUO: Mlango wa 1
SAUTI NI SAUTI YA YAKOBO, LAKINI MIKONO NI YA ESAU.
Sanduku la Agano lilikuwa linawakilisha nini katika Agano jipya?