“Msijisumbue kwa neno lolote;….(Wafilipi 4:6)
Vita nyingine kubwa ambayo inapiganwa katika akili ya mkristo, ni vita ya hofu ya maisha,.. kwamba kesho yangu itakuwaje, nitakula nini, nitavaa nini, nitakuwa wapi miaka 5 mbeleni,.. nikiendelea katika hali hii hii uzee wangu utakuwaje, kodi ya nyumba mwezi ujao ikiisha nitapata wapi nyingine, watoto wangu wakiugua kwa ghafla fedha ya matibabu makubwa nitaitolea wapi? n.k.n.k… hayo ni mawazo ambayo yanapenya katikati ya mawazo yetu, wakati mwingine aidha tunataka au hatutaki,, na madhara yake ni kuwa jambo hii likishakita mizizi ndani yetu, sasa Neno KUSUMBUKIA ndipo linapozaliwa..
Tunaanza Kujisumbua kwa mawazo mengi usiku na mchana, kwa nguvu nyingi, kwa gharama zozote ili tu ufikie malengo hayo..Sasa sio vibaya kufikiria mambo yajayo na kuyawekea mipango..lakini kupo kufikira kuliko sahihi na kupo kufikiria kusiko sahihi… Kufikiri kusiko sahihi kunaleta HOFU!!
Bwana alilifahamu hilo, na anajua kabisa kwa jinsi tulivyo hapa duniani tumezungukwa na mambo mengi ya kidunia, hofu ya maisha ni lazima ituvamie,…. lakini yeye alitupa suluhisho sahihi la sisi kuweza kuishinda hali hiyo akasema..
Wafilipi 4:6 “Msijisumbue kwa neno lolote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu”.
Unaona, anasema, msijisumbue kwa Neno lolote, sio moja, au mawili, au matatu, bali lolote.., anajua yapo mengi hayawezi kuisha, makubwa kwa madogo,hivyo lolote lile tusijisumbue nalo, yatatufanya tutoke katika mstari wa wokovu na fikra zetu za kutazama mambo ya mbinguni,.. bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu,”…
Tunapokutana na changamoto za ki-maisha, au shida Fulani, tusianze kupaniki kwa haraka na kuanza kuzichosha fahamu zetu,… kuwaza sana hadi kukosa usingizi, hapana bali tunapaswa tuchukue haja zetu hizo katika maombi, tumpelekee yeye haja zetu hizo, kwasababu anasema pia..
1Petro 5:6 “Basi nyenyekeeni chini ya mkono wa Mungu ulio hodari, ili awakweze kwa wakati wake; 7 huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu”.
1Petro 5:6 “Basi nyenyekeeni chini ya mkono wa Mungu ulio hodari, ili awakweze kwa wakati wake;
7 huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu”.
Unaona Mungu anajishughulisha sana na mambo yetu, pale tunapojinyenyekeza mbele zako na kumtwika yeye kila shida yetu.. ukitaka kufahamu hilo kama Mungu anajishughulisha kweli na mambo yetu, angalia huo moyo wako unaodunda miaka na miaka hatujawahi kuununulia betri ili uendelee kudunda kila saa,.. wala hujawahi kuuhudumia au kuufanyia service yoyote ili ufanye kazi vizuri, lakini fahamu yeye ndiye Mungu anayeudundisha kila wakati..hata chakula tunachokila tumboni baada ya hapo hatushughulikii mmengenyo wake..mwili ndio unaofanya hiyo kazi wenyewe…wewe huhusiki hata kidogo…Sasa ikiwa hatujajisumbukia kwa hilo kwanini kuumiza vichwa kwa hayo yaliyosalia..?
Angalia, kucha zako, zinavyokuwa, na nywele zako ambazo kila siku unazikata.., haijawahi kutokea hata sikumoja ukawa na hofu kwamba ahaa, pengine hizi nywele zinaweza zisiote tena, embu ngoja nikazitafutie mbolea nzuri za kuziwekea ili ziote vilevile kwa rangi ile ile,.. sasa ikiwa hayo hatuwezi kuyasumbukia ambayo yanayo umuhimu mkubwa zaidi kuliko kazi zetu, na nyumba zetu, na nguo zetu kwanini tuiruhusu hofu?…Huwezi kumtumikia Mungu ukiwa na hofu, huwezi kusonga mbele ukiwa na hofu, kazi ya Mungu huwezi kuifaya ukiwa na stress..Ukishaona unahofu kali kuhusu kesho fahamu kuwa Mungu hayupo hapo..kwasababu Roho wa Mungu kamwe hamletei Mtu hofu bali Amani na kabla ya kuanza kuzungumza na wewe na kukupa ufunuo fulani,..ataanza kushughulika kwanza na hofu iliyopo ndani yako..hiyo ikishaondoka ndipo azungumze na wewe..
Hivyo tukiwa waombaji, kudumu katika sala itatusaidia kuuvuta uwepo wa Mungu karibu zaidi na sisi Mungu muweza wa yote asiyeshindwa na lolote,.. Mungu aliyeumba milima, na bahari, nyangumi wa kubwa, na mabara, Mungu aliyeumba dhahabu zote na almasi zote za ulimwengu mzima,… aliyeumba matajiri na maskini, aliyeumbwa wafalme na viongozi wote, huyo ndiye anayekuambia Usijisumbue kwa Neno lolote, bali nitwike mimi fadhaa zako,niachie mimi wewe endelea kuwaza mambo ya ufalme wa mbinguni..
Ukiendelea sasa kusoma mstari ule ule mbele kidogo utaona unasema hivi..
Wafilipi 4:6 “Msijisumbue kwa neno lolote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu. 7 Na amani ya Mungu, ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu”.
Wafilipi 4:6 “Msijisumbue kwa neno lolote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu.
7 Na amani ya Mungu, ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu”.
Umeona hapo chini? Anasema “NA AMANI YA MUNGU, ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu”… Ukishamtwika yeye fadhaa zako zote, na shida zako zote, ukaondoa ufahamu wako wote katika matatizo yanayokuzunguka… ukijua kabisa yeye mwenyewe atayashughulikia..Basi ile AMANI yake itashuka juu yako wakati huo huo…hiyo ni amani ipitayo fahamu zote, amani ya ki-Mungu si ya kibinadamu, ambayo hiyo huwa ikishushwa juu ya mwanadamu, anakuwa mtu mwingine kabisa,
Watu wanaweza kumshangaa inakuwaje mtu huyu yupo katika hali hii au hali ile, amefiwa na ndugu zake wote, hana hiki au hana kile, kodi inakaribia kuisha.. lakini anayofuraha na amani kuliko hata sisi wenye kila kitu, yeye ndiye anayekuja kutufariji sisi? ..Hawajui kuwa hiyo ndiyo Amani ipitayo fahamu zote…Sio kwamba matatizo hayapo! Yapo lakini…Amani ya Kristo imeyafunika na hivyo huna hofu.
Zaburi 127:2b……. Yeye humpa mpenzi wake usingizi’.
Amani hiyo ikimwingia mtu vizuri, hofu yote inaondoka, anaishi kama ndege ambaye anaamka asubuhi akimwimbia Mungu nyimbo za furaha, na kabla ya kwenda kulala anamwimbia Mungu nyimbo za furaha, hajali kesho yake itakuwaje, kwamba kitakuwepo au hakitakuwepo..Lakini hata siku moja Mungu hutasikia kuwa Mungu amemnyima rizki..
Lakini amani hiyo ni ngumu kuifikia kwa namna ya kawaida kama hatutakuwa watu wa kuomba, na watu wa kushukuru, pamoja na kujijengea utaratibu wa kulitafakari Neno lake kwa wakati mwingi kwa kadri tuwezavyo mpaka. Ipo Mifano mingi ya kujifunza ndani ya Neno la Mungu..Tusiposoma Neno hatutaijua na hivyo kupungukiwa nguvu za rohoni.
Bwana akubariki.
jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mafundisho mengine:
Mada Nyinginezo:
FAIDA ZA MAOMBI.
MAJARIBU MATATU YA YESU KRISTO
KISIMA CHA MAJI YA UZIMA NI KILE KILE CHA ZAMANI.
SIKU ILE NA SAA ILE.
Rudi Nyumbani:
Print this post
Kwanini Bwana Yesu alisema sikuja kuleta amani duniani, bali mafarakano.
Luka 12: 51 “Je! Mwadhani ya kwamba nimekuja kuleta amani duniani? Nawaambia, La, sivyo, bali mafarakano. 52 Kwa kuwa tokea sasa katika nyumba moja watakuwamo watu watano wamefarakana, watatu kwa wawili, wawili kwa watatu. 53 Watafarakana baba na mwanawe, na mwana na babaye; mama na binti yake, na binti na mamaye; mkwe mtu na mkwewe, mkwe na mkwe mtu”.
Luka 12: 51 “Je! Mwadhani ya kwamba nimekuja kuleta amani duniani? Nawaambia, La, sivyo, bali mafarakano.
52 Kwa kuwa tokea sasa katika nyumba moja watakuwamo watu watano wamefarakana, watatu kwa wawili, wawili kwa watatu.
53 Watafarakana baba na mwanawe, na mwana na babaye; mama na binti yake, na binti na mamaye; mkwe mtu na mkwewe, mkwe na mkwe mtu”.
Yohana 14:27 “ Amani nawaachieni; amani yangu nawapa; niwapavyo mimi sivyo kama ulimwengu utoavyo. Msifadhaike mioyoni mwenu, wala msiwe na woga”.
Swali ni Je! maneno haya ya Bwana Yesu yanajichanganya yenyewe?..Maana sehemu moja anasema sikuja kuleta amani duniani..Na sehemu nyingine anasema Amani nawaachieni.
Tukiisoma Biblia pasipo msaada wa Roho Mtakatifu hatutaambulia chochote..zaidi ya kuona Biblia ina kasoro nyingi. Lakini tukiisoma kwa Msaada wa Roho Mtakatifu tutanufaika pakubwa na kuelewa mengi.
Ni vizuri kufahamu kuwa Mtu aliye katika dhambi, akiamua kukata shauri la kumpokea Yesu moyoni mwake..Kuna mambo mawili yatatokea maishani mwake… kwanza atapata amani Fulani ya moyo isiyoelezeka…Hiyo amani inaletwa na Roho Mtakatifu mwenyewe…ataanza kuhisi kuna wepesi Fulani na tumaini la ajabu limeingia ndani yake, ambalo limemsababishia amani isiyokuwa ya kawaida…Alikuwa anahofu na huzuni anaanza kuhisi faraja, alikuwa hana tumaini lakini anaanza kuona matumaini n.k
Lakini pia pamoja na amani hiyo ya kiMungu kuingia ndani yake..Kuna amani nyingine mtu huyo ataipoteza…Na hiyo ni AMANI YA NJE…Ndio hapo kutokana na kuokoka kwake wale marafiki zake waliokuwa wanakwenda naye kufanya mambo mabaya wanaanza kumchukia, wengine wanaanza kukwaruzana na wazazi wao, wengine wanaanza kugombana na ndugu zao wa kike na wakiume n.k..Sasa amani hiyo ya nje ambayo Inapotea ndiyo Bwana Yesu aliyokuwa anaizungumzia katika Mstari hapo juu unaosema kwamba amekuja kuleta mafarakano.
Lakini kumbuka amani ile ya ndani ya wokovu inakuwa ipo pale pale (Hiyo haiondoki)…yaani mtu pamoja na kwamba kakorofishana na ndugu, au jamaa na marafiki kutokana na imani yake kwa Kristo, lakini bado mtu huyo huyo kila siku moyoni mwake anakuwa anapata amani na faraja na furaha isiyo na kifani kwa kumjua Yesu Kristo.
Tunapomfuata Kristo kumbuka siku zote, Huwezi kuepuka kupoteza amani yako ya nje na watu wanaokuzunguka…ulikuwa mshirikina sasa umeacha, washirikina wenzako wataendeleaje kukupenda?..Ulikuwa msengenyaji sasa umeacha, wasengenyaji wenzako wataachaje kukuchukia na kuanza kukusengenya wewe? Na mambo mengine yote ni hivyo.
Gharama ya kuingiza amani ndani ya moyo wako ni kuiopoteza amani ya nje.
Bwana atusaidie tusikwepe gharama hizo, na zaidi ya yote tushinde na zaidi ya kushinda katika Jina la Yesu Kristo.
Ubarikiwe.
JE! NI KWELI UMEMFUATA YESU?
TUMEPEWA, SI KUMWAMINI TU KRISTO, ILA NA KUTESWA KWA AJILI YAKE;
TUUTAZAME PIA MWISHO WA UJENZI WETU.
INGIENI KWA KUPITIA MLANGO ULIO MWEMBAMBA.
UMEPATANISHWA NA MAADUI ZAKO?
SWALI: Krisimasi ni nini, Je! ni kweli Yesu alizaliwa tarehe 25 disemba, Je ni sahihi kwa mkristo kusheherekea Krisimasi?
Krisimasi au kwa lugha ya kigeni Christmas, Ni neno lenye muunganiko wa maneno mawili: Kristo na masi/misa na hivyo kuunda neno Kristo-masi, au misa ya Kristo, inayomaanisha pia ibada ya Kristo.
Ni siku ambayo mabilioni ya wakristo duniani kote wanaisheherekea kama siku ya kuzaliwa kwa mwokozi wetu Yesu Kristo, ambayo inadhaniwa kuwa ilikuwa ni tarehe 25 ya mwezi Disemba. Hivyo kila mwaka siku kama hii na tarehe kama hii wakristo wengi sana wanaienzi kama siku ya kuzaliwa kwa shujaa wa wokovu wetu YESU KRISTO.
Hakuna mahali popote katika biblia inatoa tarehe au mwezi wa kuzaliwa kwa Bwana wetu Yesu Kristo. Ni kwa kutathimini tu majira na mazingira yaliyokuwa yanaendelea siku ya kuzaliwa kwake ndiyo iliyopelekea kuzaliwa siku na miezi tofauti tofauti kama hiyo.
Sasa kutokana na kuwa na mitazamo mingi tofauti tofauti, makundi mengi yamezaliwa na kila moja linadai mwezi wake na tarehe yake. Mengine yanaamini Kristo alizaliwa mwezi Aprili, mengine yanaamini Kristo alizaliwa mwezi Agosti… na mengi septemba na mengine octoba na mengine Disemba n.k.. Lakini lililopata umaarufu mkubwa ni hilo la mwezi Disemba..Lakini Je! Kristo alizaliwa kweli mwezi huo?
kama tukisoma kitabu cha Luka tunaweza kupata kiashirio kimojawapo… tunaona kuwa malaika Gabrieli alimtokea Zakaria kuhani (babaye Yohana mbatizaji) siku fulani maalumu ambayo tayari ilikuwa imeshapangwa na mbingu, nayo tunasoma ilikuwa ni siku ya zamu za ukuhani wa ABIYA.
Luka 1: 5 “Zamani za Herode, mfalme wa Uyahudi, palikuwa na kuhani mmoja, jina lake Zakaria, wa ZAMU YA ABIYA, na mkewe alikuwa mmojawapo wa uzao wa Haruni, jina lake Elisabeti. 6 Na wote wawili walikuwa wenye haki mbele za Mungu, wakiendelea katika amri zote za Bwana na maagizo yake bila lawama. 7 Nao walikuwa hawana mtoto, maana Elisabeti alikuwa tasa, na wote wawili ni wazee sana. 8 Basi ikawa, alipokuwa akifanya kazi ya ukuhani katika taratibu ya zamu yake mbele za Mungu, 9 KAMA ILIVYOKUWA DESTURI YA UKUHANI, kura ilimwangukia kuingia katika hekalu la Bwana ili kufukiza uvumba”.
Luka 1: 5 “Zamani za Herode, mfalme wa Uyahudi, palikuwa na kuhani mmoja, jina lake Zakaria, wa ZAMU YA ABIYA, na mkewe alikuwa mmojawapo wa uzao wa Haruni, jina lake Elisabeti.
6 Na wote wawili walikuwa wenye haki mbele za Mungu, wakiendelea katika amri zote za Bwana na maagizo yake bila lawama.
7 Nao walikuwa hawana mtoto, maana Elisabeti alikuwa tasa, na wote wawili ni wazee sana.
8 Basi ikawa, alipokuwa akifanya kazi ya ukuhani katika taratibu ya zamu yake mbele za Mungu,
9 KAMA ILIVYOKUWA DESTURI YA UKUHANI, kura ilimwangukia kuingia katika hekalu la Bwana ili kufukiza uvumba”.
Ahaa! Tusoma Kumbe katika siku za zamu za Abiya.. ambazo alikuwa anafanya kazi za kikuhani ndizo Zekaria alizotokewa na malaika Gabrieli. Sasa ili kufahamu zamu ya Abiya ilikuwa inaangukia katika miezi ipi turudi katika agano la kale tusome ndipo tutakapopata majibu ya majira ya ambayo Zekaria alitokewa na Malaika Gabrieli.
1Nyakati 24: 7 “Kura ya kwanza ikamtokea Yehoiaribu, na ya pili Yedaya; 8 ya tatu Harimu, ya nne Seorimu; 9 ya tano Malkia, ya sita Miyamini; 10 YA SABA HAKOSI, YA NANE ABIA; 11 ya kenda Yeshua, ya kumi Shekania; 12 ya kumi na moja Eliashibu, ya kumi na mbili Yakimu; 13 ya kumi na tatu Hupa, ya kumi na nne Yeshebeabu; 14 ya kumi na tano Bilga, ya kumi na sita Imeri; 15 ya kumi na saba Heziri, ya kumi na nane Hapisesi; 16 ya kumi na kenda Pethahia, ya ishirini Ezekieli; 17 ya ishirini na moja Yakini, ya ishirini na mbili Gamuli; 18 ya ishirini na tatu Delaya, ya ishirini na nne Maazia”.
1Nyakati 24: 7 “Kura ya kwanza ikamtokea Yehoiaribu, na ya pili Yedaya;
8 ya tatu Harimu, ya nne Seorimu;
9 ya tano Malkia, ya sita Miyamini;
10 YA SABA HAKOSI, YA NANE ABIA;
11 ya kenda Yeshua, ya kumi Shekania;
12 ya kumi na moja Eliashibu, ya kumi na mbili Yakimu;
13 ya kumi na tatu Hupa, ya kumi na nne Yeshebeabu;
14 ya kumi na tano Bilga, ya kumi na sita Imeri;
15 ya kumi na saba Heziri, ya kumi na nane Hapisesi;
16 ya kumi na kenda Pethahia, ya ishirini Ezekieli;
17 ya ishirini na moja Yakini, ya ishirini na mbili Gamuli;
18 ya ishirini na tatu Delaya, ya ishirini na nne Maazia”.
Kwahiyo hapo tunaweza kuona zamu ya Abiya ilikuwa ni ya NANE katika ufanyaji wa kazi za kikuhani. Na kazi hizo zilikuwa zinafanyika sabato mpaka sabato yaani wiki mpaka wiki,.. hivyo zama ya Abiya iliangukia wiki ya 8 katika utendaji kazi wa kikuhani. Na tunajua kuwa mwaka wa kiyahudi hauanzi kama huu wa kwetu huku, januari hapana bali huwa unaanza mwanzoni mwa mwezi april,.. na hivyo ukihesabu hapo majuma mawili utaona zamu hiyo inadondokea katikati ya mwezi wa 6.
Kwahiyo mpaka hapo tunaweza kusema sasa Zekaria kumbe alitokewa majira ya mwezi wa 6 na muda mfupi baada ya hapo pengine mwezi wa 6 mwishoni au wa 7 mwanzoni mkewe Elizabethi alipata mimba, na biblia inatuambia pia miezi 6 baada ya kupata mimba kwake Elizabethi Malaika Gabrieli alimwendea Bikiria Mariamu na kumpasha habari za yeye kupata mimba ya Bwana Yesu (Luka 1:26).
Hivyo mpaka hapo tunaona itakuwa imeshafika mwezi wa 12 katikati, au mwezi wa kwanza mwanzoni, ndipo mimba ya Bwana wetu YESU ilipotungishwa. Na tunajua kuwa baada ya miezi 9 mtoto huwa ndio anazaliwa, sasa ukipiga hesabu utaona kuwa uwezekano mkubwa wa kuzaliwa kwa Bwana wetu YESU KRISTO unaweza angukia katikati ya mwezi wa 9 au mwanzoni mwa mwezi wa 10, kwa kalenda yetu sisi. Na ndio maana utaona pia Bwana Yesu alianza kuhubiri akiwa na miaka 30 na akamaliza kuhubiri akiwa na miaka 33 na nusu, na siku aliposulibiwa wote tunajua ilikuwa ni Mwezi wa nne (April). Kwahiyo ukihesabu vizuri hapo utagundua alianza kuhubiri kati ya mwezi wa 9 hadi wa 10, ambao ndio mwezi aliozaliwa, ili kutumizia jumla ya miaka mitatu na nusu ya huduma yake.
Zipo pia thibitisho nyingine zinaonyesha kuwa Kristo alizaliwa majira hayo lakini hatuwezi kuziandika zote hapa. Kwahiyo Yesu hakuzaliwa tarehe 25 Disemba..
Kwa kufuata na kuzaliwa kwa mungu ya kirumi TAMUZ ndipo tarehe hii ikageuzwa na kuwa ndio siku ya kuzaliwa kwa Bwana wetu YESU KRISTO.
Biblia haijatoa amri juu ya kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwa Yesu (krisimasi) mahali popote, kwamba ifanyike au isifanyike, zaidi tunajua Bwana alitupa amri ya kushiriki meza yake kama ishara ya kumbukumbu ya kifo chake (Luka 22:19)
Hivyo kama utaifanya hiyo kuwa ni siku yako ya kutafakari yaliyowahi kutokea miaka zaidi ya elfu 2 iliyopita (Kuzaliwa kwa YESU).
Lakini kama itaadhimishwa kwa kuabudu sanamu au kwenda kufanya uzinzi, au kunywa pombe, au kwenda disko, au kwenda kwenye anasa ni heri usingeihadhamisha kabisa kwasababu jambo unalolifanya ni machukizo makubwa..Unamsulibisha Kristo mara ya pili.
Je! Umeokoka? Unafahamu kuwa hizi ni siku za mwisho na KRISTO yupo mlangoni sana kurudi?.. Dalili zote zinaonyesha kuwa hichi kizazi tunachoishi mimi na wewe kinaweza kushuhudia tukio la kurudi kwa pili kwa Kristo..Unaongojea nini?
Tubu dhambi zako leo, ukabatizwe kwa JINA LA YESU KRISTO upate ondoleo la dhambi zako, Kisha Bwana atakupa kipawa cha Roho wake mtakatifu kukulinda mpaka siku ile ya UNYAKUO.
Nikutakie Krisimasi Njema, Na heri ya mwaka mpya ujao!
Kwa mafundisho zaidi ya Neno la Mungu/maombezi/wokovu/ushauri wasiliana nasi kwa namba hizi +255693036618/ +255789001312
Je! ni sahihi kwa Mkristo kusherekea siku yake ya kuzaliwa.[Birth day]?
Sabato halisi ni lini, Je! ni Jumapili au Jumamosi?, Ni siku gani itupasayo kuabudu?
MAPIGO YA VITASA SABA, NA SIKU YA BWANA.
CHUKIZO LA UHARIBIFU
Ni nani huyo “alikuwako naye hayuko, naye yu tayari kupanda kutoka kuzimu.?”
Shalom, Jina la Yesu Kristo Bwana wetu lizidi kubarikiwa daima Tunapaswa tukumbuke kuwa Kila tunapoiona siku mpya, basi ndivyo tunavyopiga hatua nyingine kuufikia ule mwisho..Zile dalili kuu za mwisho wa dunia zimeshatimia, hivyo wakati wowote tunaweza kulishuhudia tukio la unyakuo wa kanisa..Na kwa wale watakaobaki nao pia watazishuhudia kazi za mpinga-Kristo pamoja na mapigo yote ya Mungu aliyoyazungumzia katika Ufunuo 16
Hivyo tunapaswa tuwe macho vilevile tuwe na maarifa ya kutosha kuzijua njama za shetani,..Inasikitisha kuona kuwa watu wengi bado wanadhani mpinga-Kristo ni mtu ambaye atatoka sehemu isiyojulikana, na kwamba atakuwa ni mtu wa ajabu sana.. vilevile kazi zake zitaonekana ikishafika kipindi cha dhiki kuu, hatujui kuwa roho hii ilishaanza kutenda kazi tangu zamani, ikaleta uharibifu wake kwa sehemu, na ndiyo hiyo hiyo itakayoleta dhiki kuu wakati wa mwisho… kwa kutumia ufalme wake ule ule uliotumia mwanzoni.
Mhubiri 1:9 “Yaliyokuwako ndiyo yatakayokuwako; na yaliyotendeka ndiyo yatakayotendeka; wala jambo jipya hakuna chini ya jua”
Ni kweli kuwa hata kazi za mpinga-Kristo hazitakuwa mpya, zilishakwisha kuanza tangu zamani, na alishawahi kuzifanya huko nyuma na ni kitu kile kile ambacho atakuja kukifanya tena huko mbeleni,.. Kama Bwana wetu Yesu Kristo tunavyomtazamia kuja kwake… Na tunafahamu kuwa atatoka mbinguni, yeye mpinga-Kristo ana kitu gani hasa cha ziada tusijue atokako?..Hivyo usitazamie mambo makubwa sana, wala usitazamie mambo mapya sana, ..wala usitazamie atotokea nje ya ufalme tofauti na ule ule aliotokea nao mwanzo kuleta uharibifu..
Sasa tukirudi katika kitabu cha Ufunuo sura ya 17, tunaona Yohana akionyeshwa yule mwanamke kahaba, aliyeketi juu ya mnyama mwekundu sana.
Ufunuo 7:1 Akaja mmoja wa wale malaika saba, wenye vile vitasa saba, akanena nami, akisema, Njoo huku, nitakuonyesha hukumu ya yule kahaba mkuu aketiye juu ya maji mengi; 2 ambaye wafalme wa nchi wamezini naye, nao wakaao katika nchi wamelevywa kwa mvinyo ya uasherati wake. 3 Akanichukua katika Roho hata jangwani, nikaona mwanamke, ameketi juu ya mnyama mwekundu sana, mwenye kujaa majina ya makufuru, mwenye vichwa saba na pembe kumi. 4 Na mwanamke yule alikuwa amevikwa nguo ya rangi ya zambarau, na nyekundu, amepambwa kwa dhahabu, na kito cha thamani, na lulu, naye alikuwa na kikombe cha dhahabu mkononi mwake, kilichojawa na machukizo, na machafu ya uasherati wake. 5 Na katika kipaji cha uso wake alikuwa na jina limeandikwa, la siri, BABELI MKUU, MAMA WA MAKAHABA NA MACHUKIZO YA NCHI. 6 Nikamwona yule mwanamke amelewa kwa damu ya watakatifu, na kwa damu ya mashahidi wa Yesu. Nami nilipomwona nikastaajabu ajabu kuu. 7 Na yule malaika akaniambia, Kwani kustaajabu? Nitakuambia siri ya mwanamke huyu, na ya mnyama huyu amchukuaye, mwenye vile vichwa saba na zile pembe kumi. 8 Yule mnyama uliyemwona alikuwako, naye hayuko, naye yu tayari kupanda kutoka kuzimu na kwenda kwenye uharibifu. Na hao wakaao juu ya nchi, wasioandikwa majina yao katika kitabu cha uzima tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu, watastaajabu wamwonapo yule mnyama, ya kwamba alikuwako, naye hayuko, naye atakuwako. 9 Hapo ndipo penye akili zenye hekima. Vile vichwa saba ni milima saba anayokalia mwanamke huyo. 10 Navyo ni wafalme saba. Watano wamekwisha kuanguka, na mmoja yupo, na mwingine hajaja bado. Naye atakapokuja imempasa kukaa muda mchache. 11 Na yule mnyama aliyekuwako naye hayuko, yeye ndiye wa nane, naye ni mmoja wa wale saba, naye aenenda kwenye uharibifu. 12 Na zile pembe kumi ulizoziona ni wafalme kumi, ambao hawajapokea ufalme bado, lakini wapokea mamlaka kama wafalme muda wa saa moja pamoja na yule mnyama. 13 Hawa wana shauri moja, nao wampa yule mnyama nguvu zao na mamlaka yao. 14 Hawa watafanya vita na Mwana-Kondoo, na Mwana Kondoo atawashinda, kwa maana Yeye ni Bwana wa Mabwana, na Mfalme wa Wafalme, na hao walio pamoja naye ndio walioitwa, na wateule, na waaminifu.
Ufunuo 7:1 Akaja mmoja wa wale malaika saba, wenye vile vitasa saba, akanena nami, akisema, Njoo huku, nitakuonyesha hukumu ya yule kahaba mkuu aketiye juu ya maji mengi;
2 ambaye wafalme wa nchi wamezini naye, nao wakaao katika nchi wamelevywa kwa mvinyo ya uasherati wake.
3 Akanichukua katika Roho hata jangwani, nikaona mwanamke, ameketi juu ya mnyama mwekundu sana, mwenye kujaa majina ya makufuru, mwenye vichwa saba na pembe kumi.
4 Na mwanamke yule alikuwa amevikwa nguo ya rangi ya zambarau, na nyekundu, amepambwa kwa dhahabu, na kito cha thamani, na lulu, naye alikuwa na kikombe cha dhahabu mkononi mwake, kilichojawa na machukizo, na machafu ya uasherati wake.
5 Na katika kipaji cha uso wake alikuwa na jina limeandikwa, la siri, BABELI MKUU, MAMA WA MAKAHABA NA MACHUKIZO YA NCHI.
6 Nikamwona yule mwanamke amelewa kwa damu ya watakatifu, na kwa damu ya mashahidi wa Yesu. Nami nilipomwona nikastaajabu ajabu kuu.
7 Na yule malaika akaniambia, Kwani kustaajabu? Nitakuambia siri ya mwanamke huyu, na ya mnyama huyu amchukuaye, mwenye vile vichwa saba na zile pembe kumi.
8 Yule mnyama uliyemwona alikuwako, naye hayuko, naye yu tayari kupanda kutoka kuzimu na kwenda kwenye uharibifu. Na hao wakaao juu ya nchi, wasioandikwa majina yao katika kitabu cha uzima tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu, watastaajabu wamwonapo yule mnyama, ya kwamba alikuwako, naye hayuko, naye atakuwako.
9 Hapo ndipo penye akili zenye hekima. Vile vichwa saba ni milima saba anayokalia mwanamke huyo.
10 Navyo ni wafalme saba. Watano wamekwisha kuanguka, na mmoja yupo, na mwingine hajaja bado. Naye atakapokuja imempasa kukaa muda mchache.
11 Na yule mnyama aliyekuwako naye hayuko, yeye ndiye wa nane, naye ni mmoja wa wale saba, naye aenenda kwenye uharibifu.
12 Na zile pembe kumi ulizoziona ni wafalme kumi, ambao hawajapokea ufalme bado, lakini wapokea mamlaka kama wafalme muda wa saa moja pamoja na yule mnyama.
13 Hawa wana shauri moja, nao wampa yule mnyama nguvu zao na mamlaka yao.
14 Hawa watafanya vita na Mwana-Kondoo, na Mwana Kondoo atawashinda, kwa maana Yeye ni Bwana wa Mabwana, na Mfalme wa Wafalme, na hao walio pamoja naye ndio walioitwa, na wateule, na waaminifu.
Kumbuka mwanamke huyu anaonekana amelewa kwa damu za watakatifu na damu ya mashahidi wa Yesu,..Unaweza kujiuliza amelewaje lewaje, amewezaje kuwachinja hao watu wote na kunywa damu yake, angali yeye ni mwanamke tu?… Utagundua kuwa ni kwasababu hakuwa peke yake,bali ni yule mnyama anayemwendesha chini yake ndiye anayemsaidia kufanya hizo kazi…
Na mnyama huyo biblia inasema alikuwepo naye hayupo naye yupo tayari kupanda katika uharibifu..Ili kufahamu kama alikuwepo lini,.. tunapaswa turudi kwenye historia kidogo, wakati Yohana anaonyeshwa maono hayo tayari utawala wa Rumi ulikuwa umeshawaua wayahudi wengi sana,.. na watakatifu wengi sana..Kuanzana na Kristo mwenyewe Bwana wetu, Ni warumi ndio waliomsulubishwa..baadaye tena AD 70 uliuwa wayahudi wengi, na kuliteketeza hekalu,.. jambo ambalo Bwana Yesu alishalitabiri katika Mathayo 24, juu ya kuhusuriwa kwa Yerusalemu, baadaye tena katika majira ya kanisa la Pili hadi wakati wa matengenezo ya Kanisa, Rumi hii ambayo baadaye ilikuja kuwa ya kidini chini ya Kanisa Katoliki ilihusika na mauaji ya watakatifu Zaidi ya milioni 68, wasiokuwa na hatia yoyote, waliuliwa kwasababu tu waliishika Imani yao, na kukataa mafundisho mengine ambayo hayakuwa mafundisho ya mitume..Kama Yohana 16:2 inavyosema “naam, saa yaja atakapodhania kila mtu awauaye ya kuwa anamtolea Mungu ibada.”
Historia inaonyesha hakuna ufalme wowote, au dini yoyote, wala utawala wowote uliowahi kuuwa wakristo kwa idadi kubwa ya watu namna hiyo,..zaidi ya utawala wa KiRumi.. sio tu kuifikia idadi hiyo , bali hata kukaribia idadi hiyo haijawahi kutokea..
Dini ya kikatoliki iliyokuwepo wakati ule si sawa na iliyopo sasahivi, wakati ule ilikuwa mtu yeyote ambaye anaonekana tu kwenda kinyume na Imani ile adhabu yake ilikuwa ni kifo,.. na ilikuwa imeenea kila mahali, ilikuwa ni dini ya kitaifa, unaaishi chini ya uongozi wa kidini (Ilikuwa ni serikali ya kidini), hakukuwa na mtu wa kawaida aliyeruhusiwa kusoma biblia kama ilivyo sasahivi, isipokuwa viongozi wa juu sana wa kanisa hilo..,
Tunapozungumza hivi sio kwamba tunatangaza chuki,.. au tunahukumu..au tunashambulia imani za wengine.. au tunaonyesha kwamba upande mmoja unajua zaidi ya mwingine.. au tunawachukia wakatoliki, au tunatangaza Imani mpya au dhehebu jipya. Hilo sio lengo hata kidogo,… lakini tunazungumza ukweli wa kimaandiko, ili kwamba anayetaka kuelewa aelewe na kila mtu asikie ukweli… UTAWALA WA RUMI, NA DINI YA RUMI NDIYO MAKAO MAKUU YA SHETANI NA MPINGA-KRISTO ATAKAYEKUJA!…Kwasababu huko nyuma alikuwepo alishatenda kazi hizo, naye yupo sasa hivi, isipokuwa amepoa kwa muda na ndiye atakayepanda na kwenda katika uharibifu siku za usoni.
Tukilifahamu hilo tunaweza kuona ni wakati gani huu tunaishi, kwamba ule mwisho umekaribia sana, na moja ya hizi siku utawala huu utapata nguvu tena, na safari hii hautaleta dhiki peke yake bali utatumia mataifa kusababisha dhiki, hizo ndio zile pembe 10 za Yule mnyama.
Mpinga-Kristo atakayetokea huko kwa kupitia kiti cha UPAPA.. atazitumia serikali zote za dunia nzima kuhimiza chapa..Na mtu yeyote atayeonekana hana chapa hiyo basi adhabu yake itakuwa ni mateso na kifo, kama wakati ule ule wa makanisa ya mwanzo..
Unaweza kuona tunaishi katika kipindi cha hatari kiasi gani?,..kumbuka “Alikuwako, naye hayuko, naye yu tayari kupanda kutoka kuzimu.“
Kama wewe hujaokoka unasubiri nini?. Kila kiumbe kinafahamu wakati tuliobakiwa nao ni mchache hadi shetani mwenyewe anajua hilo na ndio maana anafanya kazi zake kwa kasi mno,.. kama tunavyoona wimbi zito la manabii wa uongo waliopo sasahivi..Tendo lililobaki ni kuTubu dhambi zako haraka kama hujatubu…kisha ukabatizwe kwa jina la YESU KRISTO kwa ajili ya ondoleo la dhambi zako (Matendo 2:3), na Bwana mwenyewe atakupa kipawa cha Roho wake Mtakatifu kukulinda na kukuongoza katika kuijua kweli yote. Mpaka ile siku ya Unyakuo.
Maran atha!
CHAPA YA MNYAMA
MPINGA-KRISTO
KWANINI DAUDI ALIKUWA NI MTU ALIYEUPENDEZA MOYO WA MUNGU?
NI KIPI MUNGU ANACHOKITAZAMA ZAIDI, MOYO AU MWILI?
Jina la Yesu Kristo libarikiwe. Karibu katika mwendelezo wa mafunzo ya vitabu vya Biblia.
Tulishapitia vitabu 15 vya kwanza, kama hujavipitia nakushauri uvipitie kwanza ili tuende pamoja katika vitabu hivi vya mbele….Kitabu cha Mwisho kilikuwa ni kitabu cha Ezra..Ambaye tuliona Biblia inamtaja kama Mwandishi mwepesi…Ezra alitokea baada ya Wana wa Israeli kuingia Babeli.. kama tulivyojifunza huko nyuma kimtitiriko basi vile vitabu vya manabii kama vile Isaya, Yeremia,Ezekieli Danieli, na vinginevyo vingepaswa vitangulie kuorodheshwa kwenye kabla ya kitabu cha Ezra, lakini ameruhusu viwe katika mtiririko huo kwa mapenzi yake mwenyewe.
Na leo kwa Neema za Bwana tutaviangalia vitabu viwili vya Nabii mmoja, ambavyo matukio yake yalitangulia kabla ya wakati wa Ezra..Navyo ni vitabu vya YEREMIA pamoja na MAOMBOLEZO. Vitabu hivi viwili viwili vimeandikwa na mtu mmoja (Yeremia)…Tumeviruka vitabu vya hapo katikati vinavyofuata baada ya kitabu cha Ezra kama vile Nehemia, Esta, Ayubu, Zaburi, Mithali, na Ayubu, tutakuja kuvipitia hapo baadaye. Hivyo nakushauri baada ya kusoma somo hili, wewe mwenyewe chukua nafasi ya kuvipitia vitabu hivyo viwili, Na Bwana atakufunulia na mengi Zaidi ya haya, kwani hapa tunaandika kama summary tu.
Kama wengi wetu tunavyojua kuwa Yeremia Mungu alimwita tangu akiwa mdogo sana..na aliambiwa atakuwa Nabii wa Mataifa. Sasa kama ni mwanafunzi wa Biblia utagundua kuwa Huduma kubwa ya Yeremia ilikuwa ni kuwatabiria mataifa juu ya hukumu Mungu atakayoileta juu ya Mataifa yote ulimwenguni kutokana na maasi ya dunia. Ikiwemo na Taifa la Mungu (Israeli) humo humo.
Mungu alitaka kuiadhibu dunia kwa kupitia Babeli. Aliupa Ufalme wa Babeli nguvu, ambao aliutumia huo kuwa kama fimbo kwa mataifa yote duniani ikiwemo Israeli ndani yake. Babeli iliyalazimisha mataifa yote yalitumikie taifa hilo. Na Mungu aliruhusu hilo ili kuyakomesha mataifa ya dunia yanayofanya maasi..Sasa kumbuka sio kwamba Babeli lilikuwa ni Taifa takatifu hapana!.Ni Mungu tu alilichagua kama chombo chake kutimiza kusudi fulani tu!..Baada ya kumaliza kutimiza kusudi hilo, nalo pia Mungu aliliadhibu kwa maasi yake.
Hivyo Mungu akamtuma Yeremia kuyaambia mataifa hayo hatari iliyopo mbele yao..Wengi walimdharau Yeremia na kumwona Nabii wa uongo,..wengine walimwona ni kibaraka wa mfalme Nebkadneza wa Babeli…wengine walimwona kama ni kimtu tu kimejizukia kutabiri tabiri ujinga..n.k Lakini Yeremia alikuwa ni Nabii kweli wa Mungu.
Alizunguka kwenye mataifa yote mpaka Misri kwa Farao (Soma Yeremia 25:5-29)..kumwonya lakini hawakumsikia.. Na mwisho akamalizia kwa Taifa lake Teule kulionya kuwa litakwenda Utumwani miaka 70 lisipotaka kujinyenyekeza lakini nalo pia halikusikia..Ukisoma kitabu cha Yeremia na 2Wafalme wa pili utaona ni jinsi gani Yeremia alivyosumbuliwa na Sedekia Mfalme wa Israeli.
Kutokana na wana wa Israeli kutokutii, Unabii wa Yeremia ukatimia juu yao..Wakauawa na Nebukadneza mfalme wa Babeli na wengine wakachukuliwa mateka na kwenda kukaa huko kwa miaka 70.
Siku hiyo ya maangamizi ilipofika wana wa Israeli walichukuliwa mateka mpaka Babeli…Na Nabii Yeremia ndiye alikuwa ni nabii pekee aliyeyashuhudia maangamizi hayo na uteka huo.. siku hiyo ilikuwa ni siku ya uchungu sana, maana theluthi ya watu walikufa kwa Tauni na wengine kwa njaa kutokana na kukosekana chakula wakati huo, kwani mji huo ulikuwa umehusuriwa kwa muda mrefu sana, na majeshi ya Babeli hivyo, hata chakula ndani ya mji kilikuwa ni shida, kwasababu hakukuwa na kinachoingia wala kutoka, theluthi nyingine walikufa kwa kuuawa kikatili na jeshi la Nebkadneza, wanawake na Watoto walichinjwa chinjwa kama kuku na theluthi nyingine walichukuliwa Mateka huku wamefungwa mpaka Babeli Utumwani. Mapigo hayo manne ndiyo yaliyoipata Israeli yaani NJAA, TAUNI,UPANGA na KUCHUKULIWA MATEKA.
Ezekieli 5: 11 “Kwa sababu hiyo, kama mimi niishivyo, asema Bwana MUNGU, hakika kwa kuwa umepatia unajisi patakatifu pangu, kwa matendo yako yote niyachukiayo, na kwa machukizo yako yote, kwa sababu hiyo mimi nami nitakupunguza; wala jicho langu halitaachilia, wala sitaona huruma. 12 Theluthi yenu mtakufa kwa tauni, na kwa njaa watakomeshwa ndani yako; na theluthi yenu wataanguka kwa upanga pande zako zote; na theluthi yenu nitawatawanya kwa pepo zote, kisha nitafuta upanga nyuma yao. 13 Hivyo ndivyo ghadhabu yangu itakavyotimia, nami nitatosheleza hasira yangu juu yao, nami nitafarijika; nao watajua ya kuwa mimi, Bwana, nimenena kwa wivu wangu, nitakapokuwa nimeitimiza ghadhabu yangu juu yao”.
Ezekieli 5: 11 “Kwa sababu hiyo, kama mimi niishivyo, asema Bwana MUNGU, hakika kwa kuwa umepatia unajisi patakatifu pangu, kwa matendo yako yote niyachukiayo, na kwa machukizo yako yote, kwa sababu hiyo mimi nami nitakupunguza; wala jicho langu halitaachilia, wala sitaona huruma.
12 Theluthi yenu mtakufa kwa tauni, na kwa njaa watakomeshwa ndani yako; na theluthi yenu wataanguka kwa upanga pande zako zote; na theluthi yenu nitawatawanya kwa pepo zote, kisha nitafuta upanga nyuma yao.
13 Hivyo ndivyo ghadhabu yangu itakavyotimia, nami nitatosheleza hasira yangu juu yao, nami nitafarijika; nao watajua ya kuwa mimi, Bwana, nimenena kwa wivu wangu, nitakapokuwa nimeitimiza ghadhabu yangu juu yao”.
Na maneno hayo yalitimia kama yalivyo. Theluthi walikufa kwa njaa na tauni, theluthi nyingine kwa kuuawa kwa upanga, na theluthi nyingine kwenda Babeli. Israeli pakabakia kuwa tupu!..Na nabii Yeremia alikuwa anayashuhudia hayo.. Jambo hilo likamhuzunisha sana, maana aliwaonya sana waIsraeli wamgeukie Mungu lakini wakakataa, hivyo maangamizi hayo yalimchoma moyo sana kwani aliyashuhudia kwa macho yake yaliyokuwa yanatendeka…Ndipo kwa msukumo wa Roho akaandika kitabu cha MAOMBOLEZO. (Kitabu hichi killiandikwa na Yeremia mwenyewe)..Kuombolezea kilicholikumba Taifa teule la Mungu..
Taifa ambalo hapo kwanza lilikuwa linaogopwa!..lenye utisho wa ki-Mungu..Taifa ambalo Mfalme mkuu wa dunia Sulemani alitokea, taifa ambalo Mungu wake alisifika kwa kutokushindwa na lolote,..leo hii linakwenda utumwani!!…Taifa ambalo Mungu alilitoa Misri kwa mkono Hodari na kumwaibisha Farao leo hii linarudi tena utumwani kwa aibu kuu kama hiyo!!?..Hayo kweli ni maombolezo na uchungu mkali. Ndio maana ukisoma kitabu cha Maombolezo utaona jinsi Nabii Yeremia anavyoitaja Israeli kwa kulifananisha na “binti Sayuni au mwanamke mjane”
Maombolezo 1:1 “Jinsi mji huu ukaavyo ukiwa, Huo uliokuwa umejaa watu! Jinsi alivyokuwa kama mjane, Yeye aliyekuwa mkuu kati ya mataifa! Binti mfalme kati ya majimbo, Jinsi alivyoshikwa shokoa! (shokoa maana yake ni kibarua wa ngazi ya chini kabisa!) 2 Hulia sana wakati wa usiku, Na machozi yake yapo mashavuni; Miongoni mwa wote waliompenda Hakuna hata mmoja amfarijiye; Rafiki zake wote wamemtenda hila, Wamekuwa adui zake”…. 5 Watesi wake wamekuwa kichwa, Adui zake hufanikiwa; Kwa kuwa Bwana amemtesa Kwa sababu ya wingi wa makosa yake; Watoto wake wadogo wamechukuliwa mateka Mbele yake huyo mtesi. 6 Naye huyo binti Sayuni Enzi yake yote imemwacha; Wakuu wake wamekuwa kama ayala Wasioona malisho; Nao wamekwenda zao hawana nguvu Mbele yake anayewafuatia.”
Maombolezo 1:1 “Jinsi mji huu ukaavyo ukiwa, Huo uliokuwa umejaa watu! Jinsi alivyokuwa kama mjane, Yeye aliyekuwa mkuu kati ya mataifa! Binti mfalme kati ya majimbo, Jinsi alivyoshikwa shokoa! (shokoa maana yake ni kibarua wa ngazi ya chini kabisa!)
2 Hulia sana wakati wa usiku, Na machozi yake yapo mashavuni; Miongoni mwa wote waliompenda Hakuna hata mmoja amfarijiye; Rafiki zake wote wamemtenda hila, Wamekuwa adui zake”…. 5 Watesi wake wamekuwa kichwa, Adui zake hufanikiwa; Kwa kuwa Bwana amemtesa Kwa sababu ya wingi wa makosa yake; Watoto wake wadogo wamechukuliwa mateka Mbele yake huyo mtesi.
6 Naye huyo binti Sayuni Enzi yake yote imemwacha; Wakuu wake wamekuwa kama ayala Wasioona malisho; Nao wamekwenda zao hawana nguvu Mbele yake anayewafuatia.”
Maombolezo 1:16 “Mimi ninayalilia mambo hayo; Jicho langu, jicho langu linachuruzika maji; Kwa kuwa mfariji yu mbali nami, Ambaye ilimpasa kunihuisha nafsi; Watoto wangu wameachwa peke yao, Kwa sababu huyo adui ameshinda. 17 Sayuni huinyosha mikono yake; Hakuna hata mmoja wa kumfariji; Bwana ametoa amri juu ya Yakobo, Kwamba wamzungukao wawe watesi wake; Yerusalemu amekuwa kati yao Kama kitu kichafu. 18 Bwana ndiye mwenye haki; Maana nimeiasi amri yake; Sikieni, nawasihi, enyi watu wote, Mkayatazame majonzi yangu; Wasichana wangu na wavulana wangu Wamechukuliwa mateka”.
Maombolezo 1:16 “Mimi ninayalilia mambo hayo; Jicho langu, jicho langu linachuruzika maji; Kwa kuwa mfariji yu mbali nami, Ambaye ilimpasa kunihuisha nafsi; Watoto wangu wameachwa peke yao, Kwa sababu huyo adui ameshinda.
17 Sayuni huinyosha mikono yake; Hakuna hata mmoja wa kumfariji; Bwana ametoa amri juu ya Yakobo, Kwamba wamzungukao wawe watesi wake; Yerusalemu amekuwa kati yao Kama kitu kichafu.
18 Bwana ndiye mwenye haki; Maana nimeiasi amri yake; Sikieni, nawasihi, enyi watu wote, Mkayatazame majonzi yangu; Wasichana wangu na wavulana wangu Wamechukuliwa mateka”.
Maombolezo 2: 1 “Jinsi Bwana alivyomfunika binti Sayuni Kwa wingu katika hasira yake! Ameutupa toka mbinguni hata nchi Huo uzuri wa Israeli; Wala hakukikumbuka kiti cha miguu yake Katika siku ya hasira yake. 2 Bwana ameyameza makao yote ya Yakobo, Wala hakuona huruma; Ameziangusha ngome za binti Yuda Katika ghadhabu yake; Amezibomoa hata nchi Ameunajisi ufalme na wakuu wake. 3 Ameikata pembe yote ya Israeli Katika hasira yake kali; Ameurudisha nyuma mkono wake wa kuume Mbele ya hao adui, Naye amemteketeza Yakobo kama moto uwakao, Ulao pande zote”.
Maombolezo 2: 1 “Jinsi Bwana alivyomfunika binti Sayuni Kwa wingu katika hasira yake! Ameutupa toka mbinguni hata nchi Huo uzuri wa Israeli; Wala hakukikumbuka kiti cha miguu yake Katika siku ya hasira yake.
2 Bwana ameyameza makao yote ya Yakobo, Wala hakuona huruma; Ameziangusha ngome za binti Yuda Katika ghadhabu yake; Amezibomoa hata nchi Ameunajisi ufalme na wakuu wake.
3 Ameikata pembe yote ya Israeli Katika hasira yake kali; Ameurudisha nyuma mkono wake wa kuume Mbele ya hao adui, Naye amemteketeza Yakobo kama moto uwakao, Ulao pande zote”.
Ukiendelea kusoma mlango wa tatu pia ni maombolezo tu kwa kilichotokea juu ya Taifa la Mungu..
Maombolezo 3: 42 “Sisi tumekosa na kuasi; Wewe hukusamehe. 43 Umetufunika kwa hasira na kutufuatia; Umeua, wala hukuona huruma. 44 Umejifunika nafsi yako kwa wingu, Maombi yetu yasipite. 45 Umetufanya kuwa takataka, na vifusi Katikati ya mataifa. 46 Juu yetu adui zetu wote Wametupanulia vinywa vyao. 47 Hofu imetujilia na shimo, Ukiwa na uharibifu”.
Maombolezo 3: 42 “Sisi tumekosa na kuasi; Wewe hukusamehe.
43 Umetufunika kwa hasira na kutufuatia; Umeua, wala hukuona huruma.
44 Umejifunika nafsi yako kwa wingu, Maombi yetu yasipite.
45 Umetufanya kuwa takataka, na vifusi Katikati ya mataifa.
46 Juu yetu adui zetu wote Wametupanulia vinywa vyao.
47 Hofu imetujilia na shimo, Ukiwa na uharibifu”.
Na Baada ya maombolezo hayo, Yeremia kwakuwa ni nabii wa Mungu na Anamjua Mungu sana. Alijua kuwa mateso hayo ni ya muda tu!. Hayatadumu milele, ni ya kitambo tu!. Ni kweli wamemwasi Mungu na Mungu kawakasirikia hata kuwauza kwa maadui zao…lakini ni kwa muda tu. Kwasababu Mungu hawezi kumtupa mtu milele. Kwa kulijua hilo akaandika maneno yafuatayo..
Maombolezo 3: 31 “Kwa kuwa BWANA HATAMTUPA MTU HATA MILELE. 32 MAANA AJAPOMHUZUNISHA ATAMREHEMU, Kwa kadiri ya wingi wa huruma zake. 33 Maana moyo wake hapendi kuwatesa wanadamu. Wala kuwahuzunisha. 34 Kuwaseta chini kwa miguu Wafungwa wote wa duniani, 35 Kuipotosha hukumu ya mtu Mbele zake Aliye juu, 36 Na kumnyima mtu haki yake, Hayo Bwana hayaridhii kabisa”.
Maombolezo 3: 31 “Kwa kuwa BWANA HATAMTUPA MTU HATA MILELE.
32 MAANA AJAPOMHUZUNISHA ATAMREHEMU, Kwa kadiri ya wingi wa huruma zake.
33 Maana moyo wake hapendi kuwatesa wanadamu. Wala kuwahuzunisha.
34 Kuwaseta chini kwa miguu Wafungwa wote wa duniani,
35 Kuipotosha hukumu ya mtu Mbele zake Aliye juu,
36 Na kumnyima mtu haki yake, Hayo Bwana hayaridhii kabisa”.
Unaona ijapokuwa wameuzwa lakini Mungu anatoa maneno ya matumaini kuwa hatawatupa milele,.. ipo siku inakuja watafunguliwa kutoka katika utumwa wao..Na watarudi tena kuwa Taifa teule la Mungu endapo wakitubu huko walipo…
Kuudharau unabii ni kubaya sana. Hususani unabii unaokutabiria mwisho wa mambo yote. Wengi wanapenda kutabiriwa mambo mazuri tu! Lakini hawapendi kuambiwa kuwa mshahara wa dhambi ni mauti. Nabii Yeremia yeye mwenyewe hakupenda kuwatabiria watu kila siku habari za hukumu ijayo..Lakini ilimbidi afanye vile ili watu angalau wasalimike kwa maana ni kweli hukumu ilikuwa ipo karibu sana..sasa itamfaidia nini awafiche halafu aje kuona ndugu zake wanachinjika mbele ya macho yake. Ni heri awaambie wakatae wenyewe kama alivyofanya kuliko asingewaambia halafu awaone wanachinjika vile, ni heri aonekane anahukumu kuliko kutowajuza watu kinachokuja mbeleni…Nafikiri haya maombolezo aliyoyaandika hapo juu yangekuwa yenye uchungu mara elfu kama wakingekufa pasipo kujua chochote.
Huyo ni Nabii wa kweli ambaye anawaambia ukweli juu ya mwisho wao huku yeye mwenyewe akiomboleza..sio kwamba alikuwa anafurahia. Kadhalika Bwana Yesu anatuonya.. “kuna hukumu inakuja”..Hatuambii hivyo huku anafurahia..bali huku anatuombolezea kwa yatakayotukuta tusipotubu. Mshahara wa nguo fupi uvaazo na make-up uwekazo usoni ni jehanamu!! huo ndio ukweli usisikilize watu wanaokudanganya huko na huko wanaojiita ni watu wa Mungu..mshahara wa uzinzi na uasherati ni jehanamu, mshahara wa ufisadi, na kutokusamehe ni jehanamu. Mshahara wa kuishi nje ya Kristo vile vile ni jehanamu.
Kama hujampa Kristo Maisha yako. Haijalishi unatenda haki kiasi gani upo hatarini sana. Hivyo nakushauri ufanye uamuzi sahihi leo, kwasababu huijui Kesho.
Bwana akubariki sana.
Ikiwa utapenda kupitia uchambuzi wa vitabu vilivyotangulia bofya hapa >>> VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 6
Na kwa mwendelezo bofya hapa >> VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 8 (Kitabu cha Ezekieli)
Kwa maombezi/ Ushauri/ Ratiba za Ibada/Maswali/ Whatsapp/ Piga namba hizi: +255693036618/ +255789001312
VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 1
Yeshuruni ni nani katika biblia?
KANUNI RAHISI YA KUFANIKIWA.
JINSI YA KUJIWEKA KARIBU NA MUNGU.
kisima cha maji ya uzima ni kile kile cha zamani. Hakitachimbwa kingine.
Shalom, Jina la Bwana wetu YESU KRISTO libarikiwe daima. Leo tutajifunza tena habari ya Isaka,.. kisha tuone ni nini Bwana anataka tujifunze kwa Mababa zetu hawa wa Imani,.. Mungu kujiita, yeye ni Mungu wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo, halafu akagotea hapo hakuendelea mbele, alikuwa anayo maana kubwa, Hivyo tunapaswa tujifunze sana juu ya watu hao watatu kwasababu zipo siri nyingi za ufalme zimelala hapo…
Tukisoma Mwanzo 26 tunaona kuna wakati njaa kali ilipita katika nchi yake,..Hivyo Isaka akalazimika kuhamisha makao yake kwa muda na kwenda kukaa kwa wafilisti,. lakini huko alipofika Mungu akamfanikisha kupita kiasi akawa Tajiri kiasi cha kuogopesha mpaka wenyeji kumwonea wivu na kumfukuza mpikani mwao,.. lakini alipokuwa huko ilimpasa pia awe na visima vya maji vya kulisha mifugo yake pamoja na watumwa wake, na watu wa nyumbani mwake wote..Lakini tunasoma Isaka hakuchimba kisima chochote kipya katika nchi ile bali alivifukua vile vile vilivyokuwa vimechimbwa na baba yake Ibrahimu tangu zamani sana ambavyo wafilisti walikuwa wamevifukia, na hapo ndipo somo letu la leo lilipo…
Mwanzo 26:15 “Na vile visima vyote walivyochimba watumwa wa baba yake, siku za Ibrahimu babaye, Wafilisti walikuwa wamevifukia, wakavijaza kifusi. 16 Abimeleki akamwambia Isaka, Utoke kwetu, maana wewe una nguvu sana kuliko sisi. 17 Basi Isaka akatoka huko akapiga kambi katika bonde la Gerari, akakaa huko. 18 Isaka akarudi akavichimbua vile visima vya maji walivyovichimba siku za Ibrahimu babaye; maana wale Wafilisti walikuwa wamevifukia baada ya kufa kwake Ibrahimu; naye akaviita majina kufuata majina alivyoviita babaye. 19 Watumwa wa Isaka wakachimba katika lile bonde, wakapata kisima cha maji yanayobubujika. 20 Wachungaji wa Gerari wakagombana na wachungaji wa Isaka wakisema, Maji haya ni yetu. Ndipo akakiita jina la kile kisima Eseki, kwa sababu waligombana naye. 21 Wakachimba kisima kingine, wakagombania na hicho tena. Akakiita jina lake Sitna. 22 Akaondoka huko akachimba kisima kingine, wala hicho hawakukigombania. Akakiita jina lake Rehobothi, akasema, Kwa kuwa sasa Bwana ametufanyia nafasi, nasi tutazidi katika nchi. 23 Akapanda kutoka hapo mpaka Beer-sheba”.
Mwanzo 26:15 “Na vile visima vyote walivyochimba watumwa wa baba yake, siku za Ibrahimu babaye, Wafilisti walikuwa wamevifukia, wakavijaza kifusi.
16 Abimeleki akamwambia Isaka, Utoke kwetu, maana wewe una nguvu sana kuliko sisi.
17 Basi Isaka akatoka huko akapiga kambi katika bonde la Gerari, akakaa huko.
18 Isaka akarudi akavichimbua vile visima vya maji walivyovichimba siku za Ibrahimu babaye; maana wale Wafilisti walikuwa wamevifukia baada ya kufa kwake Ibrahimu; naye akaviita majina kufuata majina alivyoviita babaye.
19 Watumwa wa Isaka wakachimba katika lile bonde, wakapata kisima cha maji yanayobubujika.
20 Wachungaji wa Gerari wakagombana na wachungaji wa Isaka wakisema, Maji haya ni yetu. Ndipo akakiita jina la kile kisima Eseki, kwa sababu waligombana naye.
21 Wakachimba kisima kingine, wakagombania na hicho tena. Akakiita jina lake Sitna.
22 Akaondoka huko akachimba kisima kingine, wala hicho hawakukigombania. Akakiita jina lake Rehobothi, akasema, Kwa kuwa sasa Bwana ametufanyia nafasi, nasi tutazidi katika nchi.
23 Akapanda kutoka hapo mpaka Beer-sheba”.
Isaka japokuwa alikuwa ni Tajiri, mwenye uwezo wa kuchimba visima vingine vingi vipya,.. lakini yeye hakufanya hivyo bali alivifukua visima vilevile vilivyochimbwa na Baba yake zamani…japo vilikuwa vimeshafukiwa na wafilisti havifai tena, lakini yeye alivifukua hivyo hivyo..kwasababu alijua anachokitafuta
Alitambua kuwa si kila Kisima kilicho mbele yake ni cha kunywa maji yake..
Hata leo hii vipo visima vingi, vinavyodai kutoa maji, wengine kwao elimu ndio Kisima pekee,.. wengine biashara, wengine uongozi, wengine kipaji..wengine umaarufu n.k…lakini kipo Kisima kimoja tu chenye uwezo wa kutoa maji yaliyo hai yenye uzima, ambacho mtu akinywa kwa kupitia hicho, hataona kiu milele..
Watu wengi wamejaribu kukifukia Kisima hiki tangu siku ile ya Pentekoste,..na kikaonekana kweli kama kimeshafukiwa na kupotea kabisa,.. wakati ule kanisa lilipopitia kipindi kirefu cha giza, kwa miaka Zaidi ya elfu moja..lakini kuanzia karne ya 15 kilianza kuchimbuliwa tena na wajenzi ambao Mungu alishaweka tayari kwa kazi kama hiyo, kama vile Calvin,Martin Luther, John Wesley, na wengineo, na mpaka kufikia karne ya 20 yaani kuanzia mwaka 1906 na kuendelea kikaonekana kikitoa maji tena, yale yale yaliyokuwa yanabubuja wakati wa Pentekoste ya kwanza ya mitume…yaani Mambo yale yale yaliyokuwa yanafanyika katika kanisa la Kwanza, yalianza kuonekana tena yakifanyika katika kanisa hili la mwisho…Ndiyo tuliyaona yakianza na wakina William Seymour, William Branham na wengineo…Na hata sasa yule yule anaendelea kufanya kazi…HALELUYA!!
Roho yule yule aliyeachiliwa kipindi cha Pentekoste ambaye Kristo alisema kuwa yeye ndiye atakayeleta chemi chemi ya maji uzima, ndiye aliyemwagwa tena katika kanisa letu hili la mwisho la Laodikia..
Yohana 7:37 “Hata siku ya mwisho, siku ile kubwa ya sikukuu, Yesu akasimama, akapaza sauti yake akisema, Mtu akiona kiu, na aje kwangu anywe. 38 Aniaminiye mimi, kama vile maandiko yalivyonena, mito ya maji yaliyo hai itatoka ndani yake. 39 Na neno hilo alilisema katika habari ya Roho, ambaye wale wamwaminio watampokea.”
Yohana 7:37 “Hata siku ya mwisho, siku ile kubwa ya sikukuu, Yesu akasimama, akapaza sauti yake akisema, Mtu akiona kiu, na aje kwangu anywe.
38 Aniaminiye mimi, kama vile maandiko yalivyonena, mito ya maji yaliyo hai itatoka ndani yake.
39 Na neno hilo alilisema katika habari ya Roho, ambaye wale wamwaminio watampokea.”
Lakini cha kusikitisha ni kuwa bado watu wanatafuta maji katika visima vingine,.. japokuwa hichi tayari kinaonekana kutoa maji mengi ya uzima tena bure, sio kwa kulipiwa kama vingine..Kaka/Dada ikiwa bado unaichezea hii neema, ipo siku utaitamani, na kuililia lakini utaikosa…Upo wakati utayatamani haya maji hata tone moja tu yakupe uzima lakini utayakosa…
Yule Tajiri aliyekuwa kule kuzimu aliye mwomba Lazaro achovye ncha ya kidole chake katika maji amnyweshe alikuwa hazungumzii maji ya bombani..hapana bali maji ya uzima, walau kidogo tu,.. yaani arudishwe duniani kuhubiriwa injili kwa dakika moja tu atubu aokoke kisha afe tena..Lakini ilishindikana na ndio maana akaomba basi ndugu zake wahubiriwe injili ili wasifike pale alipo..hakuomba ndugu zake wapewe maji mengi sana na washibe vizuri, ili wakifa wasisikie kiu huko aliko, au hakuomba wabebe maji ya kunywa kusudi huko wanakokwenda wawe naye mengi.. hapana aliomba wahubiriwe injili…kwasababu alijua hayo ndio maji ya uzima..
Leo hii itakufaidia nini upate, utajiri wote, upate elimu yote, upate umaarufu wote,.. na ujuzi wote, halafu unakufa ghafla, au kwa uzee mwema na kujikuta upo kuzimu.?..Ni kwanini leo hii usitafute jambo ambalo litakulinda sio tu ukiwa hapa duniani, bali pia hata huko unapokwenda….
Usipuuzie maji ya uzima, maji yaleyale yaliyochimbwa na mababa zetu mitume…Hayo ndio tunayoyaamini, na kumethibitishwa maji mengine, ni batili.
Ufunuo 21:6 “Akaniambia, Imekwisha kuwa. Mimi ni Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho. Mimi nitampa yeye mwenye kiu, ya chemchemi ya maji ya uzima, bure” Amen.jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
MADHARA YA KUKOSA MAJI YA UZIMA BAADA YA KIFO.
KAZI YA UZURURAJI WA SHETANI.
SEHEMU ISIYO NA MAJI.
Kwanini usitumainishwe na maneno ya uongo?
Kipindi kifupi sana kabla ya Hukumu ya Mungu kuja juu ya mtu, au juu ya nchi , au juu ya ulimwengu. Shetani huwa ananyanyua wimbi kubwa la manabii wa uongo, ambao kazi yao inakuwa ni kupunguza makali ya hukumu inayokuja. Shetani anajua kabisa watu wakiitafakari sana hukumu ijayo watatubu na hivyo atawapoteza na yeye hataki hata mmoja akose kwenda jehanamu pamoja na yeye, ndio lengo lake kubwa.
Tuutazama mfano mmoja katika biblia ambao utatupa mwanga kamili juu ya jambo hili. Mfano huu tunaoutoa kwenye Biblia kwasababu kila neno ili liwe kweli ni lazima lilinganishwe na biblia. Neno lolote linalotoka au kuhubiriwa kama halilingani au halipo kwenye biblia basi Neno hilo ni uongo. Hivyo tutamua biblia kuthibitisha mambo yote.
Tukisoma kitabu cha Wafalme wa pili, tunaona kuna wakati Maovu ya Wana wa Israeli yalifikia kiwango kikubwa sana mpaka Mungu akawatabiria kwamba watachukuliwa tena utumwani kama walivyochukuliwa wakati wa Farao wa Misri. Hivyo aliwaonya kwa kutumia watumishi wake wengi(manabii) watubu lakini hawakutaka (Soma 2Nyakati 36:15-17). Na hivyo kufikia kiwango ghadhabu ya Mungu kuachiliwa juu yao, kwa kuchukuliwa kwenda utumwani Babeli, na wengi wao kuuawa.
Ni kwasababu waliwasikiliza manabii wa Uongo badala ya kuwasikiliza manabii wa kweli wa Mungu. Kipindi hicho kulikuwa na manabii wa kweli wa Mungu kama vile Nabii Isaya ambaye alikuwa anawaonya juu ya maangamizi yanayokuja mbele yao, na kwamba wasipotubu watachukuliwa utumwani, lakini walimdharau. Bwana akamtuma na Nabii Yeremia ambaye aliwaonya na kuwaambia katika hali waliyofikia, kwenda utumwani watakwenda tu.
Hivyo wasitafute hata kupigana bali wajinyenyekeze kwa Nebukadneza, lakini badala yake wakamfunga na kumwona kama mtu asiye na Uzalendo na nchi yake na ni nabii wa uongo na kibaraka wa Nebkadneza. Hivyo wakawasikiliza manabii wengine ambao waliwatabiria mema. Kwamba hawatakufa, hawatapatikana na madhara, watastawi katika nchi ya Ahadi waliyopewa. Waliowatabiria kwamba watajenga na kupanda na kustawi. Manabii hao hawakugusia habari za maasi yao na kwamba wasipotubu watauawa, wao wakawahubiria habari za raha tu na amani..
Tunamsoma Nabii mmoja wa uongo anayeitwa HANANIA. Huyu ni mmoja wa walioibuka kipindi hicho cha Nabii Yeremia ambaye alikuwa anawatabiria watu amani kwamba kutakuwa shwari. Watu wasiogope Mungu bado yupo na wao, hajawaacha. Kamwe Nabii huyu hakuwahi kuwagusia habari za dhambi zao wanazozitenda zinazowafanya Mungu akae mbali nao, yeye aliwahubiria tu amani na mafanikio.
Yeremia 28:1 “Ikawa, katika mwaka ule ule, mwanzo wa kutawala kwake Sedekia, mfalme wa Yuda, mwaka wa nne, mwezi wa tano, HANANIA, mwana wa Azuri, nabii, wa Gibeoni, akasema nami ndani ya nyumba ya Bwana, mbele ya makuhani na watu wote, akisema, 2 Bwana wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Nimeivunja nira ya mfalme wa Babeli. 3 Kabla haujatimia muda wa miaka miwili mizima, nitavirudisha mahali hapa vyombo vyote vya nyumba ya Bwana, ambavyo Nebukadreza, mfalme wa Babeli, aliviondoa katika mahali hapa, akavichukua mpaka Babeli. 4 Nami nitamrudisha hapa Yekonia, mwana wa Yehoyakimu, mfalme wa Yuda, pamoja na mateka wote wa Yuda, waliokwenda Babeli, asema Bwana; maana nitaivunja nira ya mfalme wa Babeli. 5 Ndipo nabii Yeremia akamwambia nabii Hanania, mbele ya makuhani, na mbele ya watu wote waliosimama ndani ya nyumba ya Bwana, 6 naam, nabii Yeremia akasema, Amina, Bwana na atende hivi; Bwana ayatimize maneno yako uliyotabiri, kuvirudisha hapa vyombo vya nyumba ya Bwana na watu wote waliofungwa, toka Babeli, hata mahali hapa. 7 Lakini lisikilize sasa neno hili nilisemalo, masikioni mwako, na masikioni mwa watu wote, 8 Manabii waliokuwako kabla ya zamani zangu, na zamani zako, walitabiri juu ya nchi nyingi, na juu ya falme kubwa, habari ya vita, na ya mabaya, na ya tauni. 9 Nabii atabiriye habari za amani, neno la nabii yule litakapotokea, ndipo nabii yule atakapojulikana, kuwa Bwana amemtuma kweli kweli. 10 Ndipo nabii Hanania akaitwaa hiyo nira iliyokuwa juu ya shingo ya Yeremia, akaivunja. 11 Naye Hanania akanena mbele ya watu wote, akisema, Bwana asema hivi, Hivyo ndivyo nitakavyoivunja nira ya Nebukadreza, mfalme wa Babeli, kabla haujatimia muda wa miaka miwili mizima, na kuiondoa shingoni mwa mataifa yote. Basi nabii Yeremia akaenda zake”.
Yeremia 28:1 “Ikawa, katika mwaka ule ule, mwanzo wa kutawala kwake Sedekia, mfalme wa Yuda, mwaka wa nne, mwezi wa tano, HANANIA, mwana wa Azuri, nabii, wa Gibeoni, akasema nami ndani ya nyumba ya Bwana, mbele ya makuhani na watu wote, akisema,
2 Bwana wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Nimeivunja nira ya mfalme wa Babeli.
3 Kabla haujatimia muda wa miaka miwili mizima, nitavirudisha mahali hapa vyombo vyote vya nyumba ya Bwana, ambavyo Nebukadreza, mfalme wa Babeli, aliviondoa katika mahali hapa, akavichukua mpaka Babeli.
4 Nami nitamrudisha hapa Yekonia, mwana wa Yehoyakimu, mfalme wa Yuda, pamoja na mateka wote wa Yuda, waliokwenda Babeli, asema Bwana; maana nitaivunja nira ya mfalme wa Babeli.
5 Ndipo nabii Yeremia akamwambia nabii Hanania, mbele ya makuhani, na mbele ya watu wote waliosimama ndani ya nyumba ya Bwana,
6 naam, nabii Yeremia akasema, Amina, Bwana na atende hivi; Bwana ayatimize maneno yako uliyotabiri, kuvirudisha hapa vyombo vya nyumba ya Bwana na watu wote waliofungwa, toka Babeli, hata mahali hapa.
7 Lakini lisikilize sasa neno hili nilisemalo, masikioni mwako, na masikioni mwa watu wote, 8 Manabii waliokuwako kabla ya zamani zangu, na zamani zako, walitabiri juu ya nchi nyingi, na juu ya falme kubwa, habari ya vita, na ya mabaya, na ya tauni.
9 Nabii atabiriye habari za amani, neno la nabii yule litakapotokea, ndipo nabii yule atakapojulikana, kuwa Bwana amemtuma kweli kweli.
10 Ndipo nabii Hanania akaitwaa hiyo nira iliyokuwa juu ya shingo ya Yeremia, akaivunja.
11 Naye Hanania akanena mbele ya watu wote, akisema, Bwana asema hivi, Hivyo ndivyo nitakavyoivunja nira ya Nebukadreza, mfalme wa Babeli, kabla haujatimia muda wa miaka miwili mizima, na kuiondoa shingoni mwa mataifa yote. Basi nabii Yeremia akaenda zake”.
Huyu (HANANIA), Nabii wa uongo… Kawadanganywa wana wa Israeli kwasababu wanapenda faraja, hawapendi kushutumiwa, hawakupenda kukemewa maisha yao ya dhambi, ya uasherati wanaoufanya, ya ulevi, ya anasa, ya wizi na ushoga na chuki, na uabuduji sanamu..moja kwa moja wakamwamini Hanania na hivyo wakapumbazika, kuamini kwamba katumwa na Mungu. Sasa sikia Bwana kipindi kifupi tu baadaye Bwana alichomwambia Nabii Yeremia.
Yeremia 28: 15 “Kisha nabii Yeremia akamwambia nabii Hanania, Sikia sasa, Ee Hanania; Bwana hakukutuma; lakini UNAWATUMAINISHA WATU HAWA MANENO YA UONGO. 16 Basi Bwana asema hivi, Tazama, nakutuma uende zako toka juu ya uso wa nchi; mwaka huu utakufa, kwa sababu umenena maneno ya uasi juu ya Bwana. 17 Basi nabii Hanania akafa, mwaka uo huo, mwezi wa saba”.
Yeremia 28: 15 “Kisha nabii Yeremia akamwambia nabii Hanania, Sikia sasa, Ee Hanania; Bwana hakukutuma; lakini UNAWATUMAINISHA WATU HAWA MANENO YA UONGO.
16 Basi Bwana asema hivi, Tazama, nakutuma uende zako toka juu ya uso wa nchi; mwaka huu utakufa, kwa sababu umenena maneno ya uasi juu ya Bwana.
17 Basi nabii Hanania akafa, mwaka uo huo, mwezi wa saba”.
Umeona hapo?. Mambo yaliyotokea kipindi hicho ndiyo yanayotokea sasa kipindi hichi tunachoishi sasa. Shetani ameshajua tumeukaribia mwisho sana hivyo watu wote wanaanza kufikiri juu ya hukumu ijayo, ya moto wa umilele.
Na hataki mtu hata mmoja akose kuingia jehanamu, kwahiyo ili kuwapumbaza watu ananyanyua JOPO KUBWA LA MANABII WA UONGO!, Ambao kazi yao kubwa ni KUWATUMAINISHA WATU KWA MANENO YA UONGO..Kwamba hakuna hukumu!..Kwamba Dunia bado sana iishe, kwamba Mungu hawezi kuwatesa watu kwenye moto, kwamba usifikirie sana kuhusu mambo yajayo baada ya maisha haya…Watakazana kufundisha na kuhubiri namna ya kupata pesa!. Namna yakufunguliwa kiuchumi, namna ya kutoka kimaisha..Lakini kamwe hawatafundisha namna ya kutoka kwenye dhambi!!. Wana macho ya kuona kesho utaolewa, lakini hawana macho ya kuona kesho utakwenda jehanamu kama usipotubu. Wanaona maono ya wewe Kesho yako itakuwa ni ya kicheko, lakini hawaona maono kuwa Kesho yako itakuwa ni kilio na kusaga meno kama utaendelea kuishi na huyo mke ambaye si wa kwako, na huyo mume ambaye si wa kwako, na huo ulevi ambao unaufanya sasa, na hizo biashara haramu ambazo unazifanya sasa.
Ni wangapi leo hii wana maswali mengi yahusuyo maisha baada ya kifo na hawapati msaada wowote. Zaidi sana kila wanapokwenda wanaambiwa habari za kutabiriwa ndoa zao na biashara zao?. Huyo mtu akiwa tajiri namba moja duniani na akifa katika ulevi wake, au uasherati wake, au kutokusamehe kwake? au visasi vyake alivyonavyo moyoni. Huo utajiri vitakwenda kumsaidia nini huko?.
Biblia inasema katika 1 Wathesalonike 5:3 “Wakati wasemapo, Kuna amani na salama, ndipo uharibifu uwajiapo kwa ghafula, kama vile utungu umjiavyo mwenye mimba, wala hakika hawataokolewa”.
Kama hujasamehewa dhambi zako fahamu kuwa ni maelfu wamesamehewa dhambi zilizo nyingi kuliko za kwako bure na Bwana Yesu na anaendelea kutusamehe kila siku. Hivyo nafasi hiyo ya kipekee isikupite, kabla mlango wa Rehema kufungwa. Wakati ambao watu watatubu lakini hatawasikia. Hivyo unachopaswa kufanya ni kujitenga mahali ulipo kwa dakika chache. Na kutubu kwa kukiri makosa yako yote na kuahidi kutokutenda tena, na unaacha kwa vitendo. Hiyo ni hatua ya kwanza. Hatua ya pili kama hujabatizwa katafute ubatizo sahihi kwa maji mengi (Yohana 3:23) na kwa jina la Yesu kwaajili ya ondoleo la dhambi zako kulingana na (Matendo 2:38). Na baada ya hapo Roho Mtakatifu atakusaidia kufanya yaliyosalia ikiwemo kukupa uwezo wa ajabu kushinda dhambi, na kukupa uwezo mkubwa wa kuyaelewa maandiko.
Bwana akubariki.jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
JIEPUSHE NA MANENO YA MANABII WA UONGO.
EPUKA MUHURI WA SHETANI
Amin, nawaambia, Kizazi hiki hakitapita, hata hayo yote yatakapotimia..!!
JINSI WATU WANAVYOZAMA KATIKA USHIRIKINA NA UCHAWI.
Sauti ni sauti ya Yakobo, lakini mikono ni ya Esau maana yake ni nini?
Shalom! Kama vile Zaburi 68:19 inavyosema… “Na ahimidiwe Bwana, ambaye Siku kwa siku hutuchukulia mzigo wetu;”
..Hivyo kila inapoitwa leo hatuachi kumshukuru Mungu kwa msaada wake anaotupa maishani.
Tukisoma kitabu cha Mwanzo, tunaona maisha ya Isaka na wanawe wawili (Esau na Yakobo) jinsi yalivyokuwa,.. wengi wetu tunaifamu habari Esau kuwa alikuwa ni mtu aliyependwa sana na baba yake, na Yakobo alipendwa na mama yake, ..Isaka alimpenda Esau kwasababu alikuwa anamjali sana, ni mtu ambaye alikuwa radhi kupoteza muda wake mwingi ili tu kuhakikisha kuwa baba yake yupo katika hali nzuri, na nafsi yake inafurahi,.. alikuwa anamjali baba yake kiasi kwamba hakuruhusu hata mtu yeyote wa kawaida tu awe anamlisha baba yake, bali yeye mwenyewe alikuwa anatoka na kwenda kumtafutia mnyama mzuri,.. kisha anakuja kumwandaa mwenyewe, na kumtengea baba yake mezani, huo upendo sio wa kawaida..
Hivyo baba yake akampenda sana kwasababu alikuwa anatoa kilicho bora kwa ajili yake,..Esau hakuwa mtu wa kuingia tu zizini na kuchukua mbuzi au kondoo, na kuandaa kwa ajili ya baba yake..Kwake hicho aliona kama sio kitendo cha heshima, badala yake alijiota na kuingia porini mwenyewe kwenda kumtafutia baba yake chakula chenye ladha tofuati na vile ambavyo vinaliwa sikuzote nyumbani..Hata kama ingekuwa wewe ni mzazi ungeachaje kumpenda mtoto kama huyo….hakununulii tu suti zinazotoka labda Kariakoo, bali anafunga safari yeye mwenyewe kwenda kukutafutia suti nzuri nje ya nchi labda Ujerumani au Canada, ili tu nafsi yako ifurahi..
Hiyo ikamfanya baba yake amthamini sana Esau kuliko Yakobo, na ilipokaribia sasa wakati wa kufa kwake, akamwita Esau kisirisiri ili ambariki..hakumwambia hata Yakobo siri hiyo, lakini alimwita akamwambia amwandalie mawindo mazuri kama ilivyo desturi yake ya siku zote na mwisho aje kumbariki.. Esau akaondoka haraka pasipo kujua kuwa mama yake yupo karibu sana na Isaka kuliko yeye anavyodhani.. Ndipo mama yake akafanya haraka haraka kwenda kumweleza Yakobo mambo yote, na akampa siri ya kumfanya auchukue ule mbaraka wa Esau ..
Mwanzo 27:11 “Yakobo akamwambia Rebeka mamaye, Esau ndugu yangu ni mtu mwenye malaika, na mimi ni mtu laini. 12 Labda baba yangu atanipapasa, nami nitakuwa machoni pake kama mdanganyifu; nami nitaleta juu yangu laana wala si mbaraka. 13 Mamaye akamwambia, Laana yako na iwe juu yangu, mwanangu, usikie sauti yangu tu, enenda ukaniletee wana-mbuzi”.
Mwanzo 27:11 “Yakobo akamwambia Rebeka mamaye, Esau ndugu yangu ni mtu mwenye malaika, na mimi ni mtu laini.
12 Labda baba yangu atanipapasa, nami nitakuwa machoni pake kama mdanganyifu; nami nitaleta juu yangu laana wala si mbaraka.
13 Mamaye akamwambia, Laana yako na iwe juu yangu, mwanangu, usikie sauti yangu tu, enenda ukaniletee wana-mbuzi”.
Ukiendelea kusoma utaona, Rebeka alimwandalia Yakobo, mambo mawili makuu, moja ni vazi la mnyama, ili kuvaa shingoni na mikononi mwake, na pili ni vazi la Esau lenye harufu ya mawindo ili Isaka akimkaribia asikie harufu nzuri aliyozoea kumsikia nayo Esau kila alipokuwa akimletea mawindo mezani..
Mwanzo 27:21 “Isaka akamwambia Yakobo, Karibu, tafadhali, ili nikupapase, mwanangu, nione kwamba wewe ndiwe mwanangu Esau, ama siyo. 22 Basi Yakobo akamkaribia Isaka, babaye, naye akampapasa, akasema, Sauti ni sauti ya Yakobo, lakini mikono ni mikono ya Esau”.
Mwanzo 27:21 “Isaka akamwambia Yakobo, Karibu, tafadhali, ili nikupapase, mwanangu, nione kwamba wewe ndiwe mwanangu Esau, ama siyo.
22 Basi Yakobo akamkaribia Isaka, babaye, naye akampapasa, akasema, Sauti ni sauti ya Yakobo, lakini mikono ni mikono ya Esau”.
Pamoja na mengi yasiyofaa juu ya Esau ambayo tusingepaswa kuyaiga lakini pia upo ufunuo mwingine wa kipekee juu ya maisha ya Esau na Yakobo. Kama vile yasivyokuwa mengi ya kujifunza juu ya maisha ya yona (kwa tabia yake ya kutokutii), lakini pia kutokutii kwake kulibeba ufunuo wa Yesu kukaa kaburini siku tatu.(Soma Luka 11:30-31). Kadhalika na Esau ni hivyo hivyo, maisha yake yamebeba ufunuo juu ya Yesu.
Kumbuka Yakobo kama Yakobo ambaye tunamwona leo hii anayeitwa Israeli asingekuwa vile, wala asingekuwa na Baraka zile kama Sio Esau aliyemwandalia..Hivyo Esau ni mfano kamili wa Bwana wetu YESU KRISTO…Sisi tunaoitwa wakristo, tusingekuwa hivi tulivyo leo hii kama kusingekuwa na mtu ambaye tumemwibia Baraka zake..Na huyo si mwingine zaidi ya Bwana wetu YESU KRISTO…Yeye ndiye aliyempendeza Baba yetu (Mungu) kuliko mwanadamu yoyote hapa duniani, mpaka siku moja sauti ikasikika kutoka mbinguni ikisema huyu ni mwanangu mpendwa wangu niliyependezwa naye…Yeye ndiye mwana peke yake alistahili kupokea Baraka zote peke yake ndiye aliyestahili kubarikiwa na Mungu…Amefanyika kuwa laana kwa ajili yetu sisi, ili sisi tuzishiriki Baraka zake,..kama asingejitwika fedheha zetu, na dhambi zetu sisi leo hii sijui tungekuwa wapi..
Kumbuka halikuwa jambo la Yakobo kwenda tu kichwa kichwa kunyakuwa Baraka zile, kulikuwa na taratibu za kufuata. Kwanza ilimbidi avae mavazi ya Esau pili avae ngozi ya mnyama inayofanana na Esau vinginevyo angekumbana na laana ya baba yake badala ya baraka…Hata leo hii wapo watu wanamwendea Mungu bila kufuata kanuni Mungu aliyoiweka..na mwisho wa siku wanaangukia laana badala ya Baraka..Yaani kwa ufupi kama wewe upo nje ya Kristo, ni heri uendelee katika hali yako ya dhambi kuliko kumkaribia Mungu na kumfanyia ibada ukidhani kuwa ndio utampendeza….
Mungu hakuwahi kupendezwa na mwanadamu yoyote ni Yesu Kristo tu peke yake..Na hivyo ili na wewe uonekane unampendeza yeye ni sharti uvae vazi la YESU KRISTO..Kama sio Yesu Kristo sisi ni kama mbolea tu, hatustahili hata kulitaja jina la Mungu.
Tulishapotea siku nyingi kwenye dira za kiungu.
Hilo tu ndilo litakalo tufanya sisi tubarikiwe na Mungu..Na tunaweza kufanya hivyo kwa kutubu dhambi zetu zote kwa kudhamiria kuziacha kabisa kisha kwenda kubatizwa katika ubatizo sahihi wa kuzamishwa katika maji mengi (Yohana 3:23) na kwa jina la YESU KRISTO (Matendo 2:38), na baada ya hapo Roho Mtakatifu kuja juu yetu…Tukikamiliza hatua zote hizo tutakuwa na uhakika wote kuwa dhambi zetu zimeondolewa na sisi nasi tutazishiriki Baraka zile zile za Bwana wetu Yesu Kristo.
UTUKUFU UNA KRISTO YESU, BWANA WETU..MKUU WA WAFALME WA DUNIA (Ufunuo 1:5), Aliyetuosha dhambi zetu kwa Damu yake. Ubarikiwe sana.jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
YONA: Mlango 1
TUMAINI NI NINI?
UWE MWAMINIFU HATA KUFA.
BUSTANI YA NEEMA.
Maana ya Neno “Tenzi” ni Tungo zilizokaa katika mfumo wa “Mashairi”..Kwahiyo Mashairi yote ni Tenzi…Na Tenzi zipo za aina mbili. Kuna Tenzi za Mwilini na TENZI ZA ROHONI.
Haya ni mashahiri yote ambayo yametungwa na watu kwa kufikisha ujumbe wa mambo yahusuyo ulimwengu huu…Nyimbo zote zinazoimbwa na wasanii wa kidunia ni tenzi za mwilini…Mashairi yote yanatungwa na Wanafalsafa wa ulimwengu huu ni tenzi za mwilini…
Pamoja na kuwepo kwa tenzi za Mwilini,..zipo pia Tenzi za rohoni. Tenzi hizi ni nyimbo za mashahiri ambazo zinatungwa kwa uongozo wa Roho Mtakatifu kwa lengo la kuzinufaisha roho za watu.
Madhara ya Tenzi za rohoni yapo katika roho. Nyimbo hizi hazijatungwa kwa lengo la kuinufaisha dunia, wala kisisimua dunia.Ni nyimbo zilizobeba maonyo na mahubiri ya rohoni. Kiasi kwamba mtu akisikia kama alikuwa hajampa Kristo Yesu maisha yake anaguswa moyo na kumgeukia Kristo.
Kadhalika kama alikuwa amevunjika moyo, au amejeruhiwa rohoni basi anajengeka upya na kufarijika na kupata amani mpya tena na nguvu mpya ya kuendelea mbele.
Kadhalika kama kulikuwa na mtu ambaye amerudi nyuma kiimani basi kwa kupitia nyimbo hizo zinamrejesha upya kwenye mstari..Na kumwonya kuhusu hatari za kupotea njia. n.k
Kama Biblia inavyosema katika..
Wakolosai 3:16 “Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu”.
Hivyo tunaonyana kwa Zaburi, kwa Nyimbo (Ambazo hizi ni nyimbo za kawaida kama mapambio, sifa nk)..Na pia kwa Tenzi za Rohoni (Yaani Nyimbo za rohoni ambazo ni tofauti na sifa).
Kitabu hichi kimebeba mkusanyiko wa baadhi ya Nyimbo hizo za rohoni (yaani tenzi za rohoni)..Wengi wa watunzi wa nyimbo hizo ndani ya kitabu hicho hawakuzitunga kwa lengo la kupata fedha au kwa lengo la kusisimua watu..Au hawakuamka asubuhi na kuamua kuzitunga tu..
Wengi waliziimba hizo nyimbo kwa ufunuo wa Roho kutokana na mambo fulani ya kiroho waliyopitia katika maisha yao…Wengine walipokuwa matatizoni na Bwana akawaokoa au akaonyesha mkono wake Ndipo wakasukumwa kuziimba…
Kwamfano mwandishi wa wimbo wa tenzi unaoitwa “Yesu kwetu ni Rafiki”…aliyeitwa Joseph Scriven huyu baada ya mpenzi wake kufa kwa kuzama bahati mbaya kwenye maji..siku moja kabla ya harusi yao..alihamia Canada na huko akapata taarifa mama yake kuwa ni mgonjwa sana..Hivyo katika hali ile ya matatizo anayoyapitia akamwandikia shairi la kumfariji mama yake linalosema “omba bila kukata tamaa”..shahiri hilo likaja kubadilishwa jina na kuwa “Yesu Kwetu ni Rafiki”..ambalo ndilo tunaloliimba leo katika vitabu vyetu vya tenzi..
Wimbo huu ulitungwa na mtu anayeitwa Horatio Spafford.. Huyu alikuwa ni Mwanasheria aliyefanikiwa sana..Mambo yalimbadilikia ghafla baada ya moto mkubwa kuzuka katika mji aliokuwa anafanyia kazi wa Chicago mwaka 1871..ukasababisha kuchoma nyaraka zake zote za kazi na hivyo kubaki bila nyaraka yoyote ya kazi…Baada ya tukio hilo akaanza kuporomoka kiuchumi kwani kibarua chake kiliota nyasi… na hivyo kuazimia kuhamia Ulaya.
Wakati anawatanguliza mkewe na wanawe wakike wanne Ulaya yeye alibaki Chicago kumalizia kuweka mambo yake sawa ndipo awafuate wanawe na mkewe huyo Ulaya..Wakati wanawe na mkewe wapo safarini kwenye meli,.. Meli yao ilipata ajali na kuzama na kusababisha kifo cha wanawe wote wanne…Kwa bahati nzuri mkewe aliwahiwa kuokolewa lakini alikuwa katika hali ya mahutihuti.. Horatio alipozipata hizo habari alihuzunika sana, ikambidi afunge safari akamwangalie mkewe hali yake katika hali ya huzuni sana…Wakati yupo kwenye meli akapita lile eneo ambalo ajali ilitokea…Msukumo fulani ndani ukamjia kuimba huu wimbo “
1.Nionapo amani kama shwari, Ama nionapo shida; Kwa mambo yote umenijulisha, Ni salama rohoni mwangu. Salama rohoni, Ni salama rohoni mwangu. 2.Ingawa shetani atanitesa, Nitajipa moyo kwani Kristo ameona unyonge wangu, Amekufa kwa roho yangu.
1.Nionapo amani kama shwari, Ama nionapo shida; Kwa mambo yote umenijulisha, Ni salama rohoni mwangu.
Salama rohoni, Ni salama rohoni mwangu.
2.Ingawa shetani atanitesa, Nitajipa moyo kwani Kristo ameona unyonge wangu, Amekufa kwa roho yangu.
Umeona?..Ni wimbo wa kuganga roho…na sio kuburudisha..Ni wimbo wa kutia nguvu roho zetu katika tabu tunazopitia au tutakazopitia, shetani anapotutesa tunajipa moyo na kusema, ijapokuwa nimepoteza vyote lakini ni salama rohoni mwangu, Ninaye Kristo, ingawa nje hakuna usalama lakini Rohoni mwangu kuna usalama n.k…Huo ndio mfano wa Tenzi za rohoni.
Na watunzi wengine wote waliosalia wa tenzi za rohoni…walisukumwa na nguvu fulani ya kiMungu kuziandika.(Tazama historia ya nyimbo nyingine chini mwisho wa somo hili)
Hivyo Ni nyimbo njema ambazo Neno linatuagiza tuwe tunaziimba..sio tuziimba kwa kutimiza wajibu fulani..hapana bali kwa kuzifaidisha roho zetu…Kwasababu lengo la nyimbo hizo siokuijenga Roho ya Mungu bali roho zetu. Na pia zipo nyimbo nyingi za rohoni (yaani tenzi za rohoni)…Tofauti na hizo tunazozijua za kwenye kitabu cha Tenzi..Hivyo zozote zile Roho atakazokuongoza kuzitumia zina matokeo yale yale katika roho.
Bwana akubariki sana.jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Tafadhali share na wengine.
CHA KUTUMAINI SINA lyrics
USINIPITE MWOKOZI Lyrics
MWAMBA WENYE IMARA
MATESO YA MWENYE HAKI
TULICHUNGUZE UMBO LA YESU NA MWENENDO WAKE.
WhatsApp
Tuna wajibu wa kuombea mahali tulipo. hata kama ni pabaya kiasi gani.
Jina la Bwana wetu Yesu Kristo libarikiwe. Karibu tujifunze Biblia, leo tutajifunza kwa ufupi umuhimu wa kuombea nchi tuliyopo, sehemu za kazi tulizopo, nyumba tunazoishi, mitaa tunayoishi hata kama ndani yake inatupa shida na mateso kiasi gani. Maadamu tunaishi ndani yake hatuna budi kuiombea.
Tunajifunza kwa wana wa Israeli kipindi kile walichomwudhi sana Mungu kwa dhambi zao. Mpaka kufikia hatua ya Mungu kuwaadhibu kwa kuwatoa katika nchi yao na kuwapeleka utumwani Babeli. Na tunaona tarehe za kwanza kwanza kabisa za wao kufika Babeli wakiwa na minyororo mikononi na miguuni, Mungu alimwambia Nabii Yeremia ambaye alibaki Israeli, kwamba awaandikie waraka waisraeli wote waliofungwa huko Babeli kwamba, hiyo nchi waliyoifikia waitakie mema.
Yeremia 29: 4 “Bwana wa majeshi, Mungu wa Israeli, awaambia hivi watu wote waliochukuliwa mateka, niliowafanya wachukuliwe toka Yerusalemu mpaka Babeli; 5 Jengeni nyumba, mkakae ndani yake, kapandeni bustani, mkale matunda yake; 6 oeni wake, mkazae wana na binti; kawaozeni wake wana wenu, mkawaoze waume binti zenu, wazae wana na binti; mkaongezeke huko wala msipungue. 7 Kautakieni amani mji ule, ambao nimewafanya mchukuliwe mateka, MKAUOMBEE KWA BWANA; KWA MAANA KATIKA AMANI YAKE MJI HUO NINYI MTAPATA AMANI”.
Yeremia 29: 4 “Bwana wa majeshi, Mungu wa Israeli, awaambia hivi watu wote waliochukuliwa mateka, niliowafanya wachukuliwe toka Yerusalemu mpaka Babeli;
5 Jengeni nyumba, mkakae ndani yake, kapandeni bustani, mkale matunda yake;
6 oeni wake, mkazae wana na binti; kawaozeni wake wana wenu, mkawaoze waume binti zenu, wazae wana na binti; mkaongezeke huko wala msipungue.
7 Kautakieni amani mji ule, ambao nimewafanya mchukuliwe mateka, MKAUOMBEE KWA BWANA; KWA MAANA KATIKA AMANI YAKE MJI HUO NINYI MTAPATA AMANI”.
Unaona hapo?. Ni mji wa shida ni mji wa mateso na mji wa Ugenini, Ni mji wa wapagani, waabudu mizimu, ni mji ambao uliuteketeza mji wao na kuuwa ndugu zao. Lakini Bwana anawaambia wauombee amani mji huo, wasiulaani.
Ni kwasababu Mji huo ukiwa na Amani na wao watapata amani, na kinyume chake mji huo ukichafuka na wao watapata tabu. Hilo ni funzo tosha la hali tunazopitia sasa, kuna umuhimu mkubwa sana kuombea mahali tulipo, Nchi unayoishi, hata kama sio nchi yako lakini maadamu unaishi ndani ya hiyo nchi ni lazima uiombee. Kwasababu madhara yakija hata kama unamcha Mungu kiasi gani na wewe pia yatakuathiri tu.
Hebu fikiria vita vitokee ghafla katika nchi uliyopo, mabomu yakapigwa huku na kule. Barabara zikaharibika, miundombinu ya maji na umeme ikaharibika kiasi kwamba maji yakakosekana na umeme vilevile. Unadhani wewe unayemcha Mungu jambo hilo halitakuathiri?..Litakuathiri tu kwa namna moja au nyingine. Kwasababu unahitaji barabara kupitisha gari lako,..unahitaji umeme kuendesha shughuli zako..Unahitaji maji kwa matumizi yako binafsi na mifugo yako..Watoto wako wanahitaji kwenda shule, na sasa hawawezi kwenda tena kwasababu mji umechafuka n.k
Kwahiyo ni muhimu kuombea sehemu tulipo. Kadhalika unaishi kwenye nyumba ambayo si yako, wewe ni mgeni au mpangaji, au si mwanafamilia . Lakini umekaribishwa tu katika hiyo nyumba, Ni wajibu wako kuiombea hata kama hupati hisani wanazozipata wanafamilia. Ni wajibu wako kuiombea kwasababu Nyumba hiyo ikipata Amani nawe pia utanufaika kwahiyo amani…lakini usipoiombea ikipata shida na wewe hutasalimika utateseka mara mbili.
Vivyo hivyo katika sehemu ya kazi uliyopo. Una wajibu wa kuiombea hata kama wewe ndiye mfanyakazi unayelipwa mshahara kidogo kuliko wote..Kwasababu ukipaombea pakistawi na wewe pia utastawi..Lakini pakididimia na wewe utaathirika tu. Ndio maana Mungu akawaambia wana wa Israeli hapo juu “MKAUOMBEE KWA BWANA; KWA MAANA KATIKA AMANI YAKE MJI HUO NINYI MTAPATA AMANI”.
Ukiwa shuleni ni hivyo hivyo. Unaiombea shule uliyopo, au chuo. Kwasababu shule ikistawi na wewe utastawi ndani yake. Lakini usipoiombea na kuacha tu bila kujali, waalimu wakiwa wabaya itakuathiri na wewe… Miundo mbinu ikiwa mibovu itakuathiri na wewe… Wanafunzi wenzako wanaokuzunguka wakiwa wabaya utapata usumbufu usio wa lazima..Haijalishi wewe utakuwa mkamilifu kiasi gani, hizo tabu hutazikwepa. Na mambo mengine yote ni hivyo hivyo..Ni lazima kuyaombea. Ni lazima kuombea mahali tulipo Mpaka hapo Naamini utakuwa umeongeza kitu juu ya vile unavyovijua.
Kama hujampa Yesu Kristo Maisha yako. Mlango upo wazi ila hautakuwa hivyo siku zote. Wakati dunia inafurahia anasa…Ujio wa Kristo unazidi kukaribia kila sekunde inayosogea, ujio wake upo karibu kunashinda tunavyofikiri. Watu wa ulimwengu wataomboleza siku ile watakapokuja kugundua kwamba walikuwa wanapoteza muda kujifurahisha na anasa za ulimwengu. Bwana atusaidie tusiwe mimi na wewe. Hivyo Tubu kama hujatubu, na pia tafuta ubatizo kama hujabatizwa, na Upokee Roho Mtakatifu. Kwa hatua hizo tatu utakuwa umekamilisha wokovu wako.
Maran atha!jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Maandiko yanasema Eliya aliomba kwa bidii hadi akasimamisha mvua kunyesha kwa MUDA wa miaka 3 na nusu.(Yakobo5:17) Je! kuomba kwa bidii ni kuomba kwa namna gani?