DHAMBI INAZAA KIFO.

DHAMBI INAZAA KIFO.

Dhambi inazaa kifo.

Jina la Yesu Kristo Mkuu wa Uzima.. libarikiwe!.

Bwana Yesu alisema..

Yohana 8:33 “Wakamjibu, Sisi tu uzao wake Ibrahimu, wala hatujawa watumwa wa mtu wakati wo wote; nawe wasemaje, Mtawekwa huru?

34 Yesu akawajibu, Amin, amin, nawaambia, Kila atendaye dhambi ni mtumwa wa dhambi.

35 Wala mtumwa hakai nyumbani sikuzote; mwana hukaa sikuzote”

Mtu anayetenda kazi anafananishwa na Mfanyakazi…Na mfanyakazi anaweza akawa na cheo cha juu, au cha chini…Mara nyingi wale wenye vyeo vya chini sana wanaitwa watumwa…Watumwa wengi huwa wanapitia mateso..Mshahara wanaoupata haulingani na kazi wanazozifanya…Wanalazimika kumtumikia tu Bwana wao kwasababu hawana namna nyingine ya kujikwamua kimaisha.

Kadhalika Mtu atendaye dhambi!..Biblia inasema ni mtumwa wa dhambi..Na utumwa huo unafananishwa na utumwa wa wanyama…Kwamfano mnyama kama ng’ombe anaweza kutumikishwa kulima hekari hata 1,000 katika maisha yake yote, na kuzalisha maziwa lita elfu 5,000 katika maisha yake yote..lakini mshahara wake mwisho wa siku ni KISU SHINGONI MWAKE!. Na wala hakuna mtu anayejali kufa kwake…Na nyama yake itatumika kama kitoweo, na ngozi yake kwa kutengenezea viatu, na pembe zake kutengenezea mbiu na vifungo.

Kadhalika na utumwa wa dhambi ni hivyo hivyo…Dhambi inaweza kukutumikisha miaka yote na mwisho wa siku ikakuzawadia au kukulipa KIFO. Tena wakati mwingine kifo cha kikatili.

Biblia inasema..

Warumi 6: 23 “Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu”.

Ndugu mshahara wa dhambi ni mauti biblia haidanganyi!, …Usidanganywe na Tamaa za ulimwengu huu, “wanazoziita ustaarabu mpya”… zinazokuambia kuwa na boyfriend/girlfriend ni kwenda na wakati..zinazokuambia kujipamba uso na kujichubua na kuvaa wigi na hereni ni kujipenda!..zinazokuambia mpende akupendaye asiyekupenda mwache, na hivyo hata ukiwa na mke/mume msiyeelewana kidogo tu ni ruksa kumwacha na kutafuta mwingine!…

usidanganyike na Tamaa za anasa za ujanani zinazokuambia kwenda disko sio vibaya, zinazokuambia kunywa pombe yenye kidogo sio vibaya, zinazokuambia kuvaa vimini sio vibaya ni ujana tu!..utakapofikisha umri fulani ndipo utaanza kuvaa vizuri.

Biblia inasema katika

2Timotheo 2:22 “Lakini zikimbie tamaa za ujanani; ukafuate haki, na imani, na upendo, na amani, pamoja na wale wamwitao Bwana kwa moyo safi”…

Yakobo 1:14 “ kila mmoja hujaribiwa na tamaa yake mwenyewe huku akivutwa na kudanganywa.

15 Halafu ile tamaa ikiisha kuchukua mimba huzaa dhambi, na ile dhambi ikiisha kukomaa huzaa mauti”.

Ukitenda dhambi unajitengenezea mazingira ya kukutwa na kifo cha ghafla!….Sasa sio kwamba wote wanaokufa kwa ghafla wana dhambi!.. Hapana sio wote…Lakini idadi kubwa, Zaidi ya robo tatu ya vifo vinavyotoke leo hii duniani kote.. ni matokeo ya dhambi juu ya maisha ya watu Biblia inasema hivyo..(Soma Ezekieli 18:31, Ezekieli 33:11, Ezekieli. 18:20)

Uzinzi ni kifo!. Na kifo cha uzinzi na uasherati hakitokani tu na HIV au ugonjwa Fulani wa zinaa..kama wengi wanavyodhani….Wakati mwingine vifo vya ghafla visivyokuwa na chanzo au visivyoeleweka.. vinaweza kuwa ni matokeo ya dhambi ya uasherati juu ya maisha ya mtu..Mtu aliye mwasherati anaweza akafa tu hata kwa ajali sio lazima tu HIV..

Mshahara wa kushi na mwanamke/mwanamume ambaye hamjaoana ni kujitengenezea kifo,..kumwacha mkeo/mumeo na kwenda kuoa/kuolewa na mwingine ni umejitengenezea kifo mwenyewe..(Kwasababu biblia inasema kifo ndicho kitakachowatenganisha sasa wewe umefanyika kifo katikati ya hiyo ndoa ndio maana umeitenganisha)… kutowaheshimu wazazi ni mauti!..mshahara wa rushwa, na wizi wa namna yoyote ile ni kifo,(na kifo sio tu cha kuchomwa moto! Kinaweza kuwa kingine hata ugonjwa Fulani tu! Ukakupata ghafla na kukuondoa)..mshahara wa kutoa mimba, kuua, kulawiti, kucheza kamari, kufanya uchawi, kuuabudu sanamu, usengenyaji,utukanaji n.k ni KIFO!..chaa kimwili na cha Kiroho..

Dhambi ni mauti:

Haijalishi hiyo dhambi ilikuwa inakunufaisha kiasi gani…Hata baadhi ya wanyama kama kuku wanaweza kunufaika kwa kulishwa vizuri na kupewa kila aina ya chakula ilikusudi kwamba wawe na nyama nyingi au watage sana…lakini pamoja na kunenepeshwa kwao kote..mshahara wao wa mwisho ni mauti!..Siku wasiyoitazamia na wasioitegemea msiba wao unawafika kwa ghafla..Ni idadi ndogo sana ya kuku wanaokufa kifo cha kawaida..

Unaweza ukawa unakula rushwa leo na ukafanikiwa, unaweza ukawa unaiba na unafanikiwa lakini fahamu kuwa kifo kinakuja mbele… Nataka nikuambie kifo ni kama usingizi ni kitu ambacho huwezi kukipangia wakati wa kukuvaa…kama vile unavyozama usingizini hujui dakika halisi uliyolala…utakapozinduka ndipo utakapojua kumbe muda ule ulipotelea usingizini..,Unaweza kujilaza kitandani na ukasema kabla ya kulala nitafanya hichi au kile..wakati unawaza hayo ghafla unajikuta umezinduka na hujafanya uliyokuwa unayasema..Na kifo ndio hivyo hivyo kinakuja kama usingizi, wakati unasema bado sitakufa nitatubu tu sasa kumbe tayari umeshaondoka na kujikuta tu umetokezea mahali pengine pa mateso yasiyoelezeka…

Mhubiri 8:8 “ Hakuna mwenye uwezo juu ya roho aizuie roho; WALA HANA MAMLAKA JUU YA SIKU YA KUFA; Wala hakuna kuruhusiwa katika vita vile; Wala uovu hautamwokoa yule aliyeuzoea”.

Bwana akubariki.

Ikiwa hujampa Yesu Kristo maisha yako..na dhambi zinakutesa Kristo yupo sasa kukusaidia…

Kumbuka pia kuzimu ipo!..Mahali ambapo wenye dhambi wote watatupwa kama takataka na kupata mateso yasiyoelezeka… Mlango wa Neema sasa upo wazi..Na mpatanishi wetu sisi na Mungu yupo hai leo,.. Yesu Kristo anakuita utubu dhambi zako zote na akuoshe kwa damu yake na kukupa uzima wa Milele..na kukuokoa na ghadhabu ya Mungu itakayoikumba dunia kipindi sio kirefu tokea sasa..Na yeye Mungu hapendi sisi tuangamie, ndio maana akamtuma mwanawe mpendwa Yesu Kristo..Aje atuokoe sisi bure. Usipuuzie Neema hiyo, ipokee ikufanye kiumbe kipya maadamu unaishi.

Kumbuka tena, mshahara wa dhambi ni mauti. Na matokeo ya mauti itokanayo na dhambi ni kutupwa katika lile ziwa la moto..na chanzo cha dhambi ni Tamaa..

Maran atha. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Mada Nyinginezo:

SAUTI NI SAUTI YA YAKOBO, LAKINI MIKONO NI YA ESAU.

UPAKO NI NINI?

KWA KUWA NGUVU ZA MBINGUNI ZITATIKISIKA.

UWE MWAMINIFU HATA KUFA.

Uasherati wa Kiroho maana yake nini?

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments