Category Archive Uncategorized @sw-tz

UPENDO WA KRISTO WATUBIDISHA;

Mtu akikufanyia fadhila ya hali ya juu, ni wazi kuwa nafsi yako haitatulia mpaka na wewe utakapohakikisha umemrudishia naye pia fadhila..hiyo ni hali ya kawaida ya kibinadamu kabisa, hata kama hakitafikia kile alichokufanyia walau utaonyesha shukrani kwa kumwombea dua kwa Mungu.

Hata sisi tunapookoka, tunapogundua kuwa kumbe kuna mtu alitupenda upeo, kumbe kuna mtu alikufa kwa ajili ya dhambi zetu na kama asingekufa leo hii sisi tungekuwa ni wa kuzimu.

Ni dhahiri kuwa kama tumeithamini fadhila hiyo ya kipekee basi na sisi ni lazima tutaonyesha kurudisha kitu Fulani kwake, ni kweli hatuwezi kumrudishia fadhila za matendo yetu mema kama yeye aliyotufanyia, kwasababu mpaka hapa tulipo tulishamkosea Mungu mara nyingi sana. Lakini fadhili tunayoweza kumrudishia ni kuupeleka Upendo wake, uwafikie na wengine, ambao bado haujawafikia, ili nao pia waokolewe kama sisi. Na hiyo ndio inayotufanya tuwahubirie injili na wengine, na kuwaombea.

Mtume Paulo alisema maneno haya;

2Wakorintho 5:14 “MAANA, UPENDO WA KRISTO WATUBIDISHA; maana tumehukumu hivi, ya kwamba mmoja alikufa kwa ajili ya wote, basi walikufa wote”;

Unaona? Vivyo hivyo na sisi, huu upendo wa ajabu wa Yesu kutoa maisha yake kwa ajili yetu sisi bure, ugeuke na kuwa deni kwetu,..Huu ndio utupe sababu ya kuwapelekea watu wengine habari njema, tusiuchukulie bure tu..

2Wakorintho 6:1 “Nasi tukitenda kazi pamoja naye twawasihi msiipokee neema ya Mungu bure.
2 (Kwa maana asema, Wakati uliokubalika nalikusikia, Siku ya wokovu nalikusaidia;tazama,wakati uliokubalika ndiyo sasa; tazama siku ya wokovu ni sasa)”.

Kama wewe umeokolewa mshukuru Mungu sana kwa neema hiyo , lakini kumbuka wapo watu wengi wanaohitaji kuokolewa kama wewe, swali tujiulize tangu tumeokoka Je viungo vyetu vimeleta faida yoyote kwa Kristo? Je kilishamleta mmoja katika neema ya wokovu au la? Kama karama yako haijawahi kufanya hivyo, badala yake imetumika kuwaburudisha tu watu, basi ujue karama hiyo ni feki, haijatoka kwa Mungu.

Hivyo kwa pamoja sote, tuufanye upendo wa Kristo kama deni kwetu. Huo utubidiishe kumtumikia Mungu, kwa karama zetu na kwa tulivyonavyo, ili neema ya Mungu iwafikie na wengine kama sisi nao pia waufurahie wokovu wa Bwana wetu Yesu Kristo.

Kilichoawafanya mitume waupindue ulimwengu kwa wakati wao, ni kwasababu kwa pamoja waliutambua Upendo wa Kristo, hivyo ukageuka kuwa deni kwao, wakamtumikia Mungu kwa vyote walivyokuwanavyo, na ndio maana na hapo wanasema Upendo wa Kristo watubidiisha, vivyo hivyo na sisi, tuugeuze Upendo huu kuwa deni.

Na Bwana atatuonekania katika maisha yetu.

Shalom.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

UWEZA WA MUNGU UNAONEKANA WAPI?

Mungu aliposema Yesu ni mwanawe pekee, alimaanisha hakuwa na wengine?

LAKINI USIKU WA MANANE, PAKAWA NA KELELE.

MISTARI YA BIBLIA KUHUSU UPENDO.

Rudi Nyumbani:

Print this post

JE! KUNA UCHAWI KATIKA KUTENDA WEMA?

Ni wajibu wa kila mkristo kutambua kuwa kuna vita vikubwa sana katika kuyafanya mapenzi ya Mungu, na mapenzi ya Mungu ni Neno la Mungu..Mtu anapolisoma Neno la Mungu na kulielewa na kulifanya au kulitenda kama lilivyoandikwa, hapo anakuwa anafanya mapenzi ya Mungu.

Leo tutakwenda kutazama kipengele kimoja cha Neno la Mungu ambacho huwa shetani anakiua kwa watu wengi. shetani huwa hapendi watu walishike Neno la Mungu, kwasababu Neno la Mungu ndio ufunguo wa mafanikio yote.

Kwamfano Neno la Mungu linasema tuwe watu wa kuomba (Wakosai 4:2, Wafilipi 4:6, Yakobo 5:16, Yuda 1:20) na pia kuomba/kusali ndio ngao pekee ya kujilinda na majaribu ya yule Adui Marko 14:38. Hivyo mtu anayeomba, kamwe shetani hawezi kumshinda kwa majaribu..Na njia mojawapo shetani anayoitumia kuangusha watu ni kwa njia ya majaribu.

Utauliza majaribu kwa namna gani?

Unapopanga kwenda kanisani halafu linatokea jambo la kukukwamisha, hilo tayari ni jaribu, unapopanga kwenda kutenda wema lakini kinatokea kitu cha kuvuruga huo mpango hilo tayari ni jaribu..Sasa majaribu kama hayo yanaweza kuepukika kama ukiwa mtu wa kuomba.

Ukiwa mtu wa kuomba utaona kila unalolipanga linakwenda kama ulivyolipanga…Ulipanga jumapili uende kanisani, unaona siku hiyo inafika hakuna vikwazo vyovyote vinavyojitokeza kuanzia asubuhi mpaka jioni, umepanga uende ukahubiri unaona ratiba zinakwenda kama ulivyopanga n.k.

Sasa turudi kwenye somo letu, lenye kichwa kinachosema je! Kuna uchawi katika kutenda mema?

Ndugu hakuna uchawi wowote katika kutenda wema/mema. Shetani amekuwa akiwatishia watu wengi kuwa ukifanya kitu fulani kwa mtu fulani unaweza kujikuta unalogwa!. Hivyo ni vitisho vya shetani kuwazuia watu wasibarikiwe. Kwasababu anajua funguo mojawapo ya kubarikiwa ni kuwa mtoaji..Bwana wetu Yesu alitufundisha hiyo siri ambayo tulikuwa hatuijui alisema..

Luka 6:38  “Wapeni watu vitu, nanyi mtapewa; kipimo cha kujaa na kushindiliwa, na kusukwa-sukwa hata kumwagika, ndicho watu watakachowapa vifuani mwenu. Kwa kuwa kipimo kile kile mpimacho ndicho mtakachopimiwa”.

Sasa shetani hataki tufanikiwe! Anachotaka tuendelee kuwa jinsi tulivyo..Na ili kuhakikisha hilo linafanikiwa anakimbilia kuligeuza hili neno la Bwana wetu Yesu, linalosema wapeni watu vitu nanyi mtapewa…yeye (shetani) analigeuza na kusema (usimpe mtu usiyemjua kitu usimpe nguo zako, atazipeleka kwa mganga na mwisho wa siku utajikuta wewe ndio unakuwa maskini, atakwambia usisaidie watu barabarani wengine ni wachawi, chuma ulete, utajikuta nyota yako inahamishwa).

Hayo ndiyo mahubiri ya shetani, ya kuwazuia watu wasibarikiwe. Na kwasababu inakuja na vitisho vikali, watu wengi inawaogopesha na hivyo inawafanya wasidhubutu kusaidia saidia hovyo!!. Nimewahi kuona filamu fulani inaonyesha mtu kapita barabarani akakutana na mtu anaomba msaada, na katika kuomba kwake akamsaidia kwa kumpa fedha, ghafla yale matatizo ya yule mtu yakahamia kwake huyo aliyetoa msaada.

Ndugu usidanganyike na injili hiyo ya kuzimu!..(kumbuka kulishika Neno la Mungu ni vita!)..lazima upambane hiyo vita na uishinde..na huishindi kwa maneno tu! Bali kwa kulijua Neno la Mungu vizuri, vinginevyo ni rahisi kwenda na maji..kwasababu shetani anavitisho vya kutosha kuhakikisha hulitendi neno la Mungu. Kila jambo kwako atakuundia picha ya kulogwa tu.

Hivyo ni uongo kwamba ukifanya wema utalogwa, au utafungua mlango kwa shetani kuyadhuru maisha yako…Huo ni uongo

Sasa unaweza kuuliza hata kama “yule fulani namjua ni mchawi, au anaamini ushirikina, au ni mganga wa kienyeji” akija kuniomba fedha au chochote kile nimpe??..je hatanidhuru?..Jibu ni ndio mpe..hutapatikana na madhara yoyote badala yake ndio utabarikiwa…hata kama ni mchawi kaja kukuomba na umeona ni kweli anahitaji msaada mpe usifikiri mara mbili mbili…kwasababu hakuna uchawi katika kutenda mema!..

Mithali 25:21 “Adui yako akiwa ana njaa, mpe chakula; Tena akiwa ana kiu, mpe maji ya kunywa; 22 Maana utatia makaa ya moto kichwani pake; Na Bwana atakupa thawabu”..

Utasema hilo ni agano la kale, vipi katika agano jipya? Kasome Warumi 12:20.

Sasa hapo anasema “Adui yako” na si rafiki yako, maana yake ni kwamba “yule mtu ambaye unaona anaweza kukuletea madhara”.. Huyo ndiye msaidie kwa kumpa chakula au chochote kile, kwasababu hakuna chochote kitakachokupata wewe cha kukuletea madhara unapomsaidia, badala yake hicho ulichompa ndio kitakuwa chachu ya kumponya yeye, na Mungu atakubariki wewe kwa kufanya hivyo.

Ndugu kuna vita kali katika kulishika Neno, tena si ndogo…Hilo Neno la Bwana Yesu kulisoma ni rahisi, lakini ukilileta katika maisha halisi linavita vingi, limejaa vitisho vya shetani ndani yake, limewafanya hata watu wakiona mtu kalala barabarani, kaishiwa nguvu wampite tu! Bila kutoa msaada wowote..wakihofia kwamba endapo wakimsaidia ndio nyota zao zitakwenda hivyo..kumbe kwa kumpita yule ndio wanazipita baraka zao hivyo hivyo.(kasome Luka 10:32-36).

Na  kuna mahubiri siku hizi yanayofundisha kinyume cha hilo Neno zuri la Bwana wetu Yesu Kristo, “neno lililojaa upendo wa ajabu”…lakini wanahubiri na kulitukuza neno la Adui shetani lililojaa chuki na vitisho!. Tangu lini Mungu aliye na upendo akamkataza mwanadamu wake kuwa na upendo?. 

Unataka kupata fursa? Unataka kupata vitu? Unataka kubarikiwa?..Njia ni hiyo (wapeni watu vitu nanyi mtapewa), na sio tu fedha, au chakula.. bali hata faraja..wafariji wanaohitaji kufarijiwa nawe pia siku ya kupata mashaka na masononeko, Bwana atamtuma mtu wa kukufariji, watie moyo wanaohitaji kutiwa moyo ili itakapofika siku ambayo utakuwa umekaribia kukata tamaa, uwe na deni kwa Mungu wako la wewe kufarijiwa pia n.k n.K.

Mathayo 5:42  “Akuombaye, mpe; naye atakaye kukopa kwako, usimpe kisogo. 

43  Mmesikia kwamba imenenwa, Umpende jirani yako, na, Umchukie adui yako; 

44  lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi, 

45  ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni; maana yeye huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki. 

46  Maana mkiwapenda wanaowapenda ninyi mwapata thawabu gani? Hata watoza ushuru, je! Nao hawafanyi yayo hayo? 

47  Tena mkiwaamkia ndugu zenu tu, mnatenda tendo gani la ziada? Hata watu wa mataifa, je! Nao hawafanyi kama hayo? 

48  Basi ninyi mtakuwa wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu”

Bwana akubariki, na Bwana atubariki wote.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

JIEPUSHE NA UNAJISI.

NA ROHO NA BIBI-ARUSI WASEMA, NJOO!

KWA VILE ALIVYOKUWA MTU WA HAKI.

UPONYAJI WA ASILI

SIKU YA UNYAKUO ITAKUKUTAJE?

CHUKIZO LA UHARIBIFU

Rudi Nyumbani:

Print this post

Baradhuli/Mabaradhuli ni nini au ni nani kwenye biblia?

Baradhuli ni nani/ ni nini kama lilivyotumika kwenye biblia?


Kibiblia Baradhuli ni mtu asiyefaa, mpumbavu sana, aliyevuka mipaka

Ipo mistari kadha wa kadha inayoeleza tabia za watu wabaradhuli. Kwa mfano:

  1. Watu wanaoabudu miungu mingine kwa makusudi mbali na Mungu wa Israeli, muumba wa mbingu na nchi, hao ni mabaradhuli kibiblia.

Wanaokwenda kwa waganga wa kienyeji angali wanajua kabisa wanachokifanya ni kinyuma na mapenzi ya Mungu, wanaofanya uchawi, wanaofanya matambiko n.k. Hao ni mabaradhuli kibiblia.

Kumbukumbuku 13:12 Ukisikia yasemwa habari ya miji yako mmojawapo, akupayo Bwana, Mungu wako, ukae humo, ukiambiwa,

13 Kumetoka katikati yako MABARADHULI kadha wa kadha, wamewapotoa wenyeji wa mji wao, wakisema, Twendeni tukaabudu miungu mingine msiyoijua;

14 ndipo nawe uulize na kutafuta, ukiuliza kwa bidii; nawe angalia, ikiwa kweli, na jambo lile halina shaka, kwamba machukizo mfano wa haya yafanyika katikati yako;

15 hakika yako uwapige wenyeji wa mji ule kwa makali ya upanga, kwa kuwaangamiza kabisa, pamoja na vitu vyote vilivyomo, na wanyama walio humo, kwa makali ya upanga.

  1. Mabaradhuli pia ni watu wanaomwaga damu isiyo na hatia.

Ukisoma kitabu cha Waamuzi utaona Gideoni alikuwa na watoto sabini na wawili, lakini baada ya Gideoni kufa, mtoto wake mmoja aliingiwa na tamaa kutawala sehemu ya Gideoni hivyo akaamua kuwaua ndugu zake wote waliosalia ili yeye afanywe muamuzi badala yake, Ndipo biblia inatuambia alikwenda kuwaajiri watu Mabaradhuli ili kutekeleza adhma yake hiyo ya uuaji,..Hao watu wakashirikiana naye kuwaua ndugu zake wote siku moja juu ya jiwe. (Waamuzi 9:1-5).

  1. Mabaradhuli ni watu wanaofanya vitendo vya ubakaji na ulawiti.

Ukisoma tena kitabu cha Waamuzi 19  utamwona Yule mlawi ambaye alikuwa na suria wake, aliyekwenda kufanya ukahaba, kitendo ambacho kilimpelekea amrudishe nyumbani kwa baba yake, hivyo akakaa kule kwa muda wa miezi 4, ndipo baadaye akaghahiri akaamua amfuate surua wake amrudishe kwake, sasa alipokuwa njiani mji mmoja wa ugenini, alikaribishwa na mzee mmoja wa mji ule. Lakini usiku mambo yalibadilika kwani wale watu wa mji ule wa Benyamini, waliizingira nyumba wakataka wapewe hao wageni walale nao..Kama tunavyoijua habari Yule mlawi akaona ni heri amtoe suria wake wamfanye waliyotaka kumfanya..Wakafanya hivyo mpaka asubuhi baadaye Yule Suria akafa..

Waamuzi 19:22 “Hapo walipokuwa wakifurahisha mioyo yao, tazama, watu wa mji huo, watu MABARADHULI wakaizingira hiyo nyumba pande zote, wakagonga mlango; wakasema na huyo mwenye nyumba, huyo mzee, na kumwambia, Mlete nje mtu yule aliyefika nyumbani kwako, ili tupate kumjua”.

Soma sura yote ya 19,20 na 21, upate picha kamili, na nini kiliendelea baada ya pale..

  1. Mabaradhuli pia ni watu waasi.

Watu wanaoshikamana na viongozi waasi, au waliokosa heshima katika jamii.

2Nyakati 13:7, Waamuzi 11:3.

Je mpaka sasa mabaradhuli wapo?

Unapaswa ujiulize je! tabia mojawapo ya hizo unazo?

Kumbuka kuwa waovu wote, sehemu yao ni katika lile ziwa la moto. Ikiwa wewe ni muuaji, wewe ni baradhuli, ikiwa wewe ni mchawi(unakwenda kwa waganga) wewe ni baradhuli, n.k.

Ufunuo 21:8 “Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili”.

Lakini tumaini lipo kwa Yesu tu peke yake. Yeye peke yake ndiye anayeweza kuyageuza maisha yako na kukusaheme kabisa kabisa. Na kukufanya kuwa mwana wake.

Je! unahitaji kuokoka leo?

Unahitaji Yesu ayabadilishe maisha yako leo?

Unahitaji kupokea Roho Mtakatifu?

Biblia inasema..

Isaya 1:18 “Haya, njoni, tusemezane, asema Bwana. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu.

19 Kama mkikubali na kutii mtakula mema ya nchi”;

Kama ndivyo basi fungua hapa kwa ajili ya kuongozwa sala ya Toba>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312

Bwana akubariki.

Mada Nyinginezo:

MWEZI WA ABIBU/NISANI NI MWEZI GANI?

Arabuni maana yake ni nini?

LAKINI USIKU WA MANANE, PAKAWA NA KELELE.

MAPIGO YA VITASA SABA, NA SIKU YA BWANA.

SIKU YA UNYAKUO ITAKUKUTAJE?

MKUMBUKE MKE WA LUTU.

Rudi Nyumbani:

Print this post

Ibada ni nini,Na je ili ikamilike inapaswa iwe na nini na nini?

SWALI: Ibada ni nini, Na je ili ibada ikamilike inapaswa iwe na nini na nini? Na je ni siku gani maalumu ya kufanya ibada?


Ibada ni kitendo chochote kifanywacho kuonyesha unyenyekevu wa hali ya juu, utiifu, heshima, shukrani,  na utukufu, aidha  kwa Mungu au kitu kingine, na hiyo inaambata na mambo kadha wa kadha, ikiwemo kusifu, kuabudu, kusujudu, kuimba, kufunga, kutoa sadaka, na kushiriki maagano ya imani, Na vilevile kujitoa mwili wako kuvitumikia, hiyo nayo ni ibada kamili.

Kibiblia kuna ibada za aina tatu

  1. Ibada kwa Mungu.
  2. Ibada kwa shetani.
  3. Na ibada za wanadamu walizojitungia wenyewe kwa Mungu.
  1. Tukianzana na ibada kwa Mungu:

Hizi, ni zote tuzifanyazo aidha kanisani au manyumbani kwetu wenyewe, tunapokutana kumwimbia na kumwabudu Mungu, au kumshukuru, au kushiriki meza ya Bwana, hiyo tayari ni ibada kwa Mungu.

Matendo 13:2 “Basi hawa walipokuwa wakimfanyia Bwana ibada na kufunga, Roho Mtakatifu akasema, Nitengeeni Barnaba na Sauli kwa kazi ile niliyowaitia”.

Na kama tulivyosema awali hata kujitoa mwili wako kwa ajili ya kutenda matendo yote yampendezayo Mungu ni ibada kamili tayari..

Warumi 12:1 “Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana”.

  1. Ibada kwa Shetani.

Hizi kwa jina lingine ndio ibada za sanamu. Ambazo biblia imezikemea sehemu nyingi sana katika biblia. Unapokwenda kuisujudia sanamu yoyote ile, iwe na mfano wa mtakatifu Fulani mbinguni, tayari hiyo ni ibada kamili  ya sanamu.. Inayomtia Mungu wivu wa kukuangamiza haraka sana.

Kutoka 20:4 “Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia.

5 Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, Bwana, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao,

6 nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri zangu”.

1Wakorintho 10:14 “Kwa ajili ya hayo, wapenzi wangu, ikimbieni ibada ya sanamu”.

 Lakini kama hilo halitoshi, unaweza pengine ukawa husujudii masanamu, lakini mwili wako unafanya maasi, hiyo nayo ni ibada kamili ya sanamu sawasawa na kusujudia vinyago.

Wakolosai 3:5 “Basi, vifisheni viungo vyenu vilivyo katika nchi, uasherati, uchafu, tamaa mbaya, mawazo mabaya, na kutamani, ndiyo ibada ya sanamu”;

  1. Ibada watu walizojitungia wenyewe kwa Mungu:

Hizi ni ibada ambazo, hazitokani na Mungu wala shetani, bali zinatokana na watu wenyewe, wamejitungia wakidhani kuwa wanamfanyia Mungu, kumbe wanafanya kimakosa..

Wakolosai 2:20 Basi ikiwa mlikufa pamoja na Kristo mkayaacha yale mafundisho ya awali ya ulimwengu, kwa nini kujitia chini ya amri, kama wenye kuishi duniani,

21 Msishike, msionje, msiguse;

22 (mambo hayo yote huharibika wakati wa kutumiwa); hali mkifuata maagizo na mafundisho ya wanadamu?

23 Mambo hayo yanaonekana kana kwamba yana hekima, KATIKA NAMNA YA IBADA MLIYOJITUNGIA WENYEWE, na katika kunyenyekea, na katika kuutawala mwili kwa ukali; lakini hayafai kitu kwa kuzizuia tamaa za mwili.

Na zina madhara yake makubwa, kwasababu wakati mwingine zinasababisha hata watu waue watu wengine wakidhani kuwa ndio wanampendeza Mungu, kama tu walivyokuwa wanafanya Warumi na Wayahudi kwenye kanisa la kwanza, na jinsi zinavyofanywa na baadhi dini leo hii duniani kuchinja watu. Zote hizo ni ibada ambazo watu wamejitungua lakini hazitokani na Mungu.

Yohana 16:2 “Watawatenga na masinagogi; naam, saa yaja atakapodhania kila mtu awauaye ya kuwa ANAMTOLEA MUNGU IBADA.

Hivyo kwa kuhitimisha ni kuwa, ibada halisi ni moja tu, nayo ni kwa Mungu muumba wa mbingu na nchi (YEHOVA), na Kristo wake aliyesulibiwa kwa ajili ya dhambi zetu sisi wanadamu. Na maagizo pekee ya ibada hiyo halisi yanapatikana katika biblia tu.. Ibada nyingine yoyote tofauti na hiyo, ni machukizo makubwa kwake.

Na pia tunaikamilisha kwa miili yetu kama biblia inavyotufundisha, kwa kuishi maisha yampendezayo Bwana, ndio ibada yenye maana, ikiwa tutakuwa tunahudhuria kanisani kila siku, tunamwabudu Mungu usiku na mchana, tunamtolea matoleo mengi, tunashiriki meza ya Bwana kila wiki halafu matendo yetu, au miili yetu tumeiuza kwa shetani, ibada zetu bado ni batili..Zinakuwa ni ibada za sanamu, au ibada tulizojitungia tu sisi wenyewe.

Lakini kama utayakamilisha yote ya rohoni na mwilini, basi ibada hiyo  inafaa sana mbele za Mungu, na inathawabu nyingi sana. Wanaomfanyia Mungu ibada kamili wanakuwa marafiki wa karibu sana Mungu.

Na pia hakuna siku maalumu ya kumfanyia Mungu ibada, kwani ibada yetu halisi ipo rohoni, hivyo wakati wowote na muda wowote uwapo na nafasi inaingia uweponi mwa Mungu, kumsifu, kumshukuru, kumwabudu, kumtolea dhabihu za shukrani n.k.. Lakini pia ipo ibada ya watakatifu wote, ambayo inafanyika kila juma, hivyo ikiwa ni jumapili au Jumamosi, inapaswa ifuatwe. Kama tulivyoambiwa tusiache kukutanika pamoja..

Bwana wetu atusaidie sote, tuweze kuyakamilisha hayo.

Shalom.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

USILETE UJIRA WA KAHABA, NYUMBANI KWA MUNGU.

Nyama zilizosongolewa ni zipi?Je kunywa damu ni dhambi?

JE KUVAA PETE NI DHAMBI?

Amin, nawaambia, Kizazi hiki hakitapita, hata hayo yote yatakapotimia..!!

CHAPA YA MNYAMA

MKUMBUKE MKE WA LUTU.

LAKINI USIKU WA MANANE, PAKAWA NA KELELE.

Rudi Nyumbani:

Print this post

MUNGU HANA MBARAKA MMOJA TU!..MWAMINI.

Jina la Bwana wetu Yesu Kristo libarikiwe daima, karibu tujifunze biblia.

Imani ni kuwa na uhakika wa mambo yatarajiwayo.. Je! Una uhakika wa mambo yatakayokuja ambayo bado hujayaona wala kuyafikia?..Na kama ndio, je kwa kiwango gani?.

Ili Imani yako ionekane kuwa kubwa ni lazima uwe na uwezo wa  kuamini vitu visivyoweza kuaminika. Yaani uwe na kila sababu itakayokufanya kuwa na uhakika kwamba jambo Fulani lazima litokee.

Kwamfano ukizungumza na mtu kwenye simu, aliye umbali Fulani akakwambia panda gari (daladala) unifuate mahali nilipo baada ya lisaa limoja…bila shaka kama utakuwa na fedha ya kutosha mfukoni mwako, hutakuwa na wasiwasi wa kufika pale alipo…kwasababu unajua hata Ukikosa daladala utatafuta tax, na hata ukikosa hiyo  bado unaweza kupanda pikipiki ukafika pale alipo katika muda ule ule. Hivyo huo uwezo wa kuwa na kila sababu ya kufika pale kwa muda unaotakiwa ndio unaoitwa IMANI (una uhakika wa mambo yatarajiwayo yatafanikiwa asilimia 100). 

Lakini kama huna fedha kabisa au unafedha kidogo tu ya daladala, utakuwa na wasiwasi, utasema itakuwaje endapo nikikosa gari? itakuwaje endapo gari nitakalopanda likiharibikia njiani?..si nitachelewa n.k Hivyo unakuwa huna uhakika sana wa mambo yatarajiwayo..Hapo inahesabika kuwa Imani yako ya kufika unakotaka kwenda kwa muda unaotakiwa ni ndogo au huna kabisa.

Sasa tukirudi katika Biblia ni hivyo hivyo..Ili uweze kuhesabika kuwa na Imani kubwa ya kutosha ya kuweza kupata kile unachokihitaji kwa Asilimia zote, ni lazima uwe na Hazina ya kutosha ya UELEWA WA MAANDIKO, ili uweze kukipata kile kitu. Kumbuka hapo ninasema ni UELEWA WA MAANDIKO, na si IDADI YA MAANDIKO. Mtu mwenye idadi kubwa ya maandiko pasipo kuyaelewa huyo ni sawa redio yenye idadi kubwa ya sauti na nyimbo zinazotoka ndani yake, lakini yenyewe haielewi chochote.

Hivyo kinachojalisha kwetu ili tuhesabike kuwa na Imani ya kuweza kupokea jambo lolote lile ni HAZINA YA KUYAELEWA MAANDIKO NA KUYACHAMBUA. 

Hebu tujifunze mfano mmoja kwenye biblia ya Mtu aliyekuwa na hazina na uwezo wa kuyaelewa maandiko vyema na kuyagawanya..

Mathayo 15:22  “Na tazama, mwanamke Mkananayo wa mipaka ile akatokea, akampazia sauti akisema, Unirehemu, Bwana, Mwana wa Daudi; binti yangu amepagawa sana na pepo. 

23  Wala yeye hakumjibu neno. Nao wanafunzi wake wakamwendea, wakamwomba, wakisema, Mwache aende zake; kwa maana anapiga kelele nyuma yetu. 

24  Akajibu, akasema, Sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli

25  Naye akaja akamsujudia, akisema Bwana, unisaidie. 

26  Akajibu, akasema, Si vema kukitwaa chakula cha watoto na kuwatupia mbwa. 

27  Akasema, Ndiyo, Bwana, lakini hata mbwa hula makombo yaangukayo mezani pa bwana zao. 

28  Ndipo Yesu akajibu, akamwambia, Mama, imani yako ni kubwa; na iwe kwako kama utakavyo. Akapona binti yake tangu saa ile”.

Unaweza kuona hapo, anakatishwa tamaa kwa maneno ya YESU, na kama tunavyojua maneno ya Yesu ni Neno la Mungu. Lakini kwa maneno hayo hayo, mwanammke anayafafanua vizuri kwa Bwana, na hatimaye anapata haki yake.. “ni kweli si vyema kutwaa chakula cha watoto kuwatupia mbwa, lakini hata mbwa wanakula makombo yaangukayo chini ya meza za Bwana zao”…Maana yake ni kwamba sistahili kweli kupewa hichi ninachokitafuta, (ni kweli mimi ni kama mbwa).. Lakini kuna vile vidogo vichache vinavyobakigi..ipo neema kidogo inakuwepo kwa Mungu kwa wale wasiomcha yeye…Hiyo ndio ninayoihitaji mimi!..Ni kweli Mungu hasikii maombi ya waovu, lakini bado Mungu huyo huyo anawanyeshea mvua waovu na wema…anawaangazia jua lake wenye haki na wasio haki..

Ni kweli mimi sio mkamilifu mbele zake, lakini bado wale waovu kuliko mimi anahakikisha wanafikiwa na miale ya jua, anahakikisha upepo mwanana unawaburudisha, anahakikisha wanapata hewa safi ya oksijeni kila dakika..hivyo kwa rehema hizo, ni lazima na mimi na mimi lazima nipone, lazima nibarikiwe na kufanikiwa katika yote..Mungu hana mbaraka mmoja tu!.

Hebu tujifunze Zaidi kisa cha Esau na Yakobo.

Tusome..

Mwanzo 27: 33 “Isaka akatetemeka tetemeko kuu sana, akasema, Ni nani basi yule aliyetwaa mawindo akaniletea? Nami nimekwisha kula kabla hujaja wewe, nikambariki; naam, naye atabarikiwa.  

34 Esau aliposikia maneno ya babaye, akalia kilio kikubwa cha uchungu sana, akamwambia babaye, Nibariki na mimi, mimi nami, Ee babangu. 

 35 Akasema, Nduguyo amekuja kwa hila, akauchukua mbaraka wako.  

36 Akasema, Je! Hakuitwa Yakobo kwa haki, maana amejitia mahali pangu mara mbili hizi? Alichukua haki yangu ya mzaliwa wa kwanza, na sasa amechukua mbaraka wangu. Akasema, Je! Hukuniwekea na mimi mbaraka? 

 37 Isaka akajibu, akamwambia Esau, Tazama, nimemfanya awe bwana wako, na ndugu zake wote nimempa kuwa watumishi wake; kwa nafaka na mvinyo nimemtegemeza, nami nikufanyie nini sasa, mwanangu? 

 38 ESAU AKAMWAMBIA BABAYE, UNA MBARAKA MMOJA TU, BABANGU? Unibariki mimi, mimi nami, Ee babangu. Esau akapaza sauti yake, akalia.  

39 Isaka, baba yake, akajibu, akamwambia,Angalia,penye manono ya nchi patakuwa makao yako,Na penye umande wa mbingu unaotoka juu”.

Hebu tafakari Esau, angenyamaza asingelia kuomba na yeye abarikiwe, hebu tafakari angeishia kuondoka kwa majonzi leo hi angeishia kuwa kama Kaini, asingekuwa na baraka yoyote….Lakini japokuwa aliikosa ile Baraka kuu, lakini alilia kwa baba yake..akamwambia baba yake nibariki na mimi, kwani una mbaraka mmoja tu??? Na mwishowe akabarikiwa akaambiwa palipo na manono ya nchi patakuwa mahali pake, ingawa Mungu alimchukia Esau(Warumi 9:13)… lakini bado alimbariki alikuwa na mali nyingi hata Zaidi ya Yakobo kasome (kasome Mwanzo 33:9)

Na sisi ni hivyo hivyo, (simaanishi kuwa tuwe waovu, Mungu atusaidie), nachomaanisha ni kuwa ikiwa wewe ni mkristo hupaswi kukata tamaa hata kama inaonekana mambo yameshashindikana…Tujue tu! Mungu hana mbaraka mmoja tu!, usijiangalie ukamilifu wako!..Esau Mungu alimchukia lakini kwa kupambana akambariki hivyo hivyo…

Ukiona jambo Fulani katika Maisha kama haliwezekani, basi jua huo ndio uthibitisho kwamba linawezekana….kibiblia kutokuwezekana ndio uthibitisho wa kuwezekana kwa jambo. Amini tu! Amini tu.. usiache kumwamini Mungu kamwe.

Mwisho kabisa kama tulivyosema… “kubarikiwa wakati mwingine sio uthibitisho wa kumpendeza Mungu”..Esau hakumpendeza Mungu lakini alibarikiwa, na wengine wengi katika biblia…na hata leo Mungu ni yule yule…anawanyeshea mvua waovu na wema…Kwahiyo kuzimu watakuwepo matajiri sana, na mbingu pia watakuwepo maskini, hivyo lililo la Muhimu sana ni kutafuta kuyatenda mapenzi ya Mungu, ambayo hiyo inakuja kwa kutubu na kumpokea Yesu kama Bwana na mwokozi wa Maisha yako na kutafuta ubatizo sahihi wa kimaandiko (Matendo 2:38), na kupokea Roho Mtakatifu, hilo ndio jambo la muhimu na la kwanza, mengine yatafuata. Lakini kama unahitaji jambo lolote…Mwombe Mungu kwa bidii na kumwamini, utaona majibu…

Bwana anakupenda, Bwana anatupenda, na Bwana atubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312 Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > WHATSAPP-Group

Mada Nyinginezo:

LAKINI USIKU WA MANANE, PAKAWA NA KELELE.

HIZI NI NYAKATI ZA KUJIINGIZA KWA NGUVU.

JIFUNZE KULIGAWANYA VYEMA NENO LA MUNGU.

Atakapokuja Mwana wa Adamu, je! Ataiona imani duniani? Maana yake nini?

BWANA SI MWEPESI WA HASIRA, LAKINI BWANA NI MWINGI WA HASIRA.

Amin, nawaambia, Kizazi hiki hakitapita, hata hayo yote yatakapotimia..!!

Rudi Nyumbani:

Print this post

Neema ya Bwana Yesu Kristo

 2Wakorintho 13:14 “Neema ya Bwana Yesu Kristo, na pendo la Mungu, na ushirika wa Roho Mtakatifu ukae nanyi nyote”.


Hii ni salamu ya kumalizia ambayo mtume Paulo aliwaandikia wakorintho, na watu wote watakaousoma waraka huo (ikiwemo mimi na wewe).

Maneno haya, yamegusa Nyanja zote tatu za Kusudi la Mungu kwetu sisi wanadamu.

> Paulo anaanza kwa kusema, Neema ya Bwana Yesu Kristo, ikae nasi; Akiwa na maana kuwa mpaka sisi tukamilike, mpaka sisi tushinde, tunaihitaji hii neema ya Yesu Kristo wakati wote itembee na sisi, tukipungukiwa neema, basi ni ngumu kuweza kuushinda ulimwengu. Na neema hii inaanza kutembea juu ya mtu kwa mara ya kwanza pale anapookoka.

> Anasema tena, Pendo la Mungu likae nasi: Ni kwa njia ya upendo Mungu alitukuomboa (Yohana 3:16). Hivyo na sisi tukiukosa Upendo, haijalishi tutakuwa washirika wazuri kiasi gani, haijalishi tutafanya miujiza mingi kiasi gani, tutanena kwa lugha za malaika nyingi kiasi gani, bado sisi tutabakia kuwa si kitu. Hivyo Pendo la Mungu linapokaa ndani yetu basi Mungu anakuwa karibu na sisi. Na pendo la Mungu ndio lile linalozungumziwa katika 1Wakorintho 11:1-8

Na ndio huo Paulo alikuwa analiombea kanisa ukae ndani yao.

> Anamalizia na kusema pia Ushirika wa Roho Mtakatifu ukae nanyi nyote; Hii ikiwa na maana palipo na Roho Mtakatifu pana ushirika.. Sisi kama wakristo tuliookoka ni jukumu letu kuutunza ushirika wa Roho tukinia mamoja, tukiifanya kazi ya Mungu..

Waefeso 4:3 “na kujitahidi kuuhifadhi umoja wa Roho katika kifungo cha amani.

4 Mwili mmoja, na Roho mmoja, kama na mlivyoitwa katika tumaini moja la wito wenu.

5 Bwana mmoja, imani moja, ubatizo mmoja.

6 Mungu mmoja, naye ni Baba wa wote, aliye juu ya yote na katika yote na ndani ya yote”.

Mambo haya matatu yakienda pamoja na sisi, basi Mungu naye ataenda pamoja na sisi, lakini tukipungukiwa kimoja wapo, aidha neema, au Upendo, au Ushirika, ni ngumu kusimama kama Kanisa.

Hivyo mimi na wewe tujitathmini ni wapi, hatujakamilisha, kisha tukamilishe, Na Bwana atusaidie.

Shalom.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

UNYAKUO.

KWANINI MUNGU ALIMTUMIA MUSA KWA VIWANGO VILE?

UPONYAJI WA ASILI

JE UDHAIFU WANGU UNAWEZA KUZUIA INJILI?

ADAM NA EVA.

Amin, nawaambia, Kizazi hiki hakitapita, hata hayo yote yatakapotimia..!!

Rudi Nyumbani:

Print this post

MISTARI YA BIBLIA YA FARAJA (Mwongozo 2026).

Jiunge na channel yetu ya Whatsapp, ujifunze biblia na upate Neno la siku kila asubuhi. kwa link hii >>> https://chat.whatsapp.com/GWxBOH2GXncIc0pwVIhnch


Mistari ya Biblia ya Faraja

Unaweza ukawa unapitia wakati mgumu, mateso, majaribu, jangwa, au shida. Kama mkristo, imani yako inaweza kujaribiwa. Lakini Biblia peke yake ndiyo inayoweza kukupa faraja ya kweli. Haijalishi maneno elfu kumi ya faraja kutoka kwa wanadamu, Biblia peke yake inaweza kukupa utulivu wa kweli.

Mistari ya Faraja kutoka Biblia

Wafilipi 4:13

“Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu”.

Isaya 41:10

“Usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako; nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kuume wa haki yangu”.

Isaya 40:31

“Bali wao wamngojeao Bwana watapata nguvu mpya; watapanda juu kwa mbawa kama tai; watapiga mbio, wala hawatachoka; watakwenda kwa miguu, wala hawatazimia”.

Kumbukumbu 31:6

“Iweni hodari na moyo wa ushujaa, msiogope wala msiwahofu; kwa maana Bwana, Mungu wako, yeye ndiye anayekwenda pamoja nawe, hatakupungukia wala kukuacha”.

Isaya 40:29

“Huwapa nguvu wazimiao, humwongezea nguvu yeye asiyekuwa na uwezo”.

1 Wakorintho 10:13

“Jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo kawaida ya wanadamu; ila Mungu ni mwaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili mweze kustahimili”.

Kutoka 15:2

“Bwana ni nguvu zangu, na wimbo wangu; Naye amekuwa wokovu wangu. Yeye ni Mungu wangu, nami nitamsifu; Ni Mungu wa baba yangu, nami nitamtukuza”.

Kumbukumbu 20:4

“Kwa maana Bwana, Mungu wenu, ndiye awaandamaye kwenda kuwapigania juu ya adui zenu, ili kuwaokoa ninyi”.

Isaya 12:2

“Tazama, Mungu ndiye wokovu wangu; Nitatumaini wala sitaogopa; Maana Bwana YEHOVA ni nguvu zangu na wimbo wangu; Naye amekuwa wokovu wangu”.

Mathayo 6:34

“Basi msisumbukie ya kesho; kwa kuwa kesho itajisumbukia yenyewe. Yatosha kwa siku maovu yake”.

Zaburi 27:1

“Bwana ni nuru yangu na wokovu wangu, Nimwogope nani? Bwana ni ngome ya uzima wangu, Nimhofu nani”?

Zaburi 31:24

“Iweni hodari, mpige moyo konde, Ninyi nyote mnaomngoja Bwana”.

Zaburi 73:26

“Mwili wangu na moyo wangu hupunguka, Bali Mungu ni mwamba wa moyo wangu Na sehemu yangu milele”.

Zaburi 29:11

“Bwana atawapa watu wake nguvu; Bwana atawabariki watu wake kwa amani”.

Zaburi 23:4

“Naam, nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti, Sitaogopa mabaya; Kwa maana Wewe upo pamoja nami, Gongo lako na fimbo yako vyanifariji”.

Zaburi 118:14

“Bwana ni nguvu zangu na wimbo wangu, Naye amekuwa wokovu wangu”.

Habakuki 3:19

“YEHOVA, aliye Bwana, ni nguvu zangu, Yeye huifanya miguu yangu kuwa kama ya kulungu, Naye ataniendesha katika mahali pangu palipoinuka”.

Yohana 16:33

“Hayo nimewaambieni mpate kuwa na amani ndani yangu. Ulimwenguni mnayo dhiki; lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu”.

2 Wathesalonike 3:3

“Lakini Bwana ni mwaminifu, atakayewafanya imara na kuwalinda na yule mwovu”.

Luka 1:37

“Kwa kuwa hakuna neno lisilowezekana kwa Mungu”.

Yeremia 29:11

“Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema Bwana, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho”.

Wafilipi 1:6

“Nami niliaminilo ndilo hili, ya kwamba yeye aliyeanza kazi njema mioyoni mwenu ataimaliza hata siku ya Kristo Yesu”.

Zaburi 34:8

“Onjeni mwone ya kuwa Bwana yu mwema; Heri mtu yule anayemtumaini”.

Mathayo 11:28

“Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha”.


Jiunge na Forum ya Neno la Mungu

Mada zaidi zinazohusu Faraja:


Uko Tayari Kumfuata Yesu Leo?

Inawezekana hujaokoka, lakini leo hii unataka Yesu asikupite bila kuyaokoa maisha yako. Ikiwa umeamua kumgeukia Mungu kwa moyo wako wote, yeye mwenyewe anasema:

“Kila ajaye kwangu sitamtupa Nje kamwe”.

Leo hii Yesu ataingia ndani ya maisha yako kama umeamua kweli kumfuata. Fungua hapa kwa ajili ya kuongozwa Sala ya Toba: KUONGOZWA SALA YA TOBA


Bwana akubariki.


Ikiwa unataka, naweza pia kuunda meta description na SEO keywords zinazofaa ili chapisho hiki kionekane vizuri kwenye Google, bila kubadilisha maneno.

Je, nifanye hivyo pia?

 

Mada Nyinginezo:

NJONI, NUNUENI MLE NA MNYWE.

Rudi Nyumbani:

Print this post

Arabuni maana yake ni nini?

Tukiachilia mbali, Eneo linaloitwa Arabuni ambalo limetajwa sana katika biblia,  .

Kama tunavyosoma katika vifungu vifuatavyo..

2Nyakati 9:14 “mbali na ile waliyoileta wachuuzi na wafanya biashara; tena wafalme wote wa Arabuni, na maliwali wa nchi wakamletea Sulemani dhahabu na fedha”.

 

Isaya 21:13 “Ufunuo juu ya Arabuni. Ndani ya msitu wa Arabuni mtalala, Enyi misafara ya Wadedani”.

 

Yeremia 25: 13 “Ufunuo juu ya Arabuni. Ndani ya msitu wa Arabuni mtalala, Enyi misafara ya Wadedani”.

 

Wagalatia 1:17 “wala sikupanda kwenda Yerusalemu kwa hao waliokuwa mitume kabla yangu; bali nalikwenda zangu Arabuni, kisha nikarudi tena Dameski”.

 

Wagalatia 4:25 “Maana Hajiri ni kama mlima Sinai ulioko Arabuni, umelingana na Yerusalemu wa sasa; kwa kuwa anatumika pamoja na watoto”.

Eneo ambalo walikuwa wanaishi jamii ya watu wa kiarabu.. Au kwa jina lingine linaitwa Arabia.Tazama picha juu.


Lakini Neno hili limetajwa kwa namna nyingine, katika biblia kama tunavyosoma katika vifungu vifuatavyo

2Wakorintho 1:22 “naye ndiye aliyetutia muhuri akatupa arabuni ya Roho mioyoni mwetu”.

 

2Wakorintho 5:5 “Basi yeye aliyetufanya kwa ajili ya neno lilo hilo ni Mungu, aliyetupa arabuni ya Roho”.

 

Waefeso 1:3 “Nanyi pia katika huyo mmekwisha kulisikia neno la kweli, habari njema za wokovu wenu; tena mmekwisha kumwamini yeye, na kutiwa muhuri na Roho yule wa ahadi aliye Mtakatifu.

14 Ndiye aliye arabuni ya urithi wetu, ili kuleta ukombozi wa milki yake, kuwa sifa ya utukufu wake”.

Sasa Mungu alipotugawia ahadi zake za uzima wa milele na nyinginezo, hakutaka kutupa mikono mitupu tu hivi hivi bila uthibitisho wowote, Hivyo ili kututhibitishia kuwa ahadi zake ni kweli alitupa uhakika huo kwa kutugawia Roho Mtakatifu,  kama garantii au tunaweza kusema, kuponi, ya kuwa ahadi zake tutafikia, au atatutimizia.. Sasa hiyo garantii/kuponi  ndio inayoitwa arabuni.

Ukipokea Roho Mtakatifu basi unayo arabuni ya uzima wa milele, kama alivyowaahidia wale waliomwamini.

Ukipokea Roho Mtakatifu basi una uhakika kuwa wewe ni mbarikiwa wa Mungu, hakuna laana yoyote inayoweza kukaa juu yako.

Ukipokea Roho Mtakatifu basi maombi yako ni hakika kuwa yanasikiwa na kujibiwa mbinguni, sawasawa na ahadi za Yesu kwa wote waliomwamini.

Lakini ukiwa huna Roho Mtakatifu, na unasema umeokoka, bado mbinguni hutaenda..Kama vile maandiko yanavyosema..

Warumi 8:9 “…Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wake”.

Hivyo kama na wewe unataka upate hii arabuni(garantii) ya urithi wa ahadi za Mungu zote za mwilini na rohoni,, basi ni sharti umpokee Roho Mtakatifu. Na mtu anampokea Roho Mtakatifu kwa kuzaliwa mara ya pili.

Mtu anazaliwaje mara ya pili?

Pale unapotubu dhambi zako kwa kumaanisha kabisa kuziacha, , na baada ya kutubu  ukawa tayari kwenda kubatizwa katika ubatizo sahihi wa kuzamishwa katika maji mengi na kwa jina la Yesu Kristo, sawasawa na Mdo 2:38, hapo utakuwa tayari umeshazaliwa mara ya pili.

Na moja kuwa moja, kuanzia huo wakati na kuendelea Roho anashuka ndani yako..Na unakuwa tayari umeshapokea garantii hiyo(arabuni) ya kuwa wewe ni mwana wa ahadi… Hivyo kama hutarudi nyuma utaendelea tu kuishi katika maisha matakatifu ya wokovu ya kumpendeza Mungu na kudumu katika ushirika wa Mungu..Ni uhakika kuwa hata ukifa usiku huo huo, wewe ni wa mbinguni tu mrithi wa ahadi zote za Mungu..

Hivyo kama hujaokoka, basi anza sasa kufuata hatua hizo kwa moyo wako wote..Kama unahitaji leo kumpa Yesu maisha yako basi fungua hapa kwa ajili ya kuongozwa sala ya Toba.>>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA

Na ikiwa utahitaji kubatizwa usisite kuwasiliana nasi kwa namba hizi +255789001312: Ubatizo ni bure, na unafanyika pindi tu mtu anapotubu dhambi zake..Hakuna madarasa ya kupitia, wala hakuna kutoa fedha, kwasababu biblia haitufundishi kanuni hizo..

Bwana akubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

Yuko azuiaye sasa hata atakapoondolewa! ni nani huyo?

USIFIKIRI FIKIRI.

KILA MMOJA WENU AJUE KUUWEZA MWILI WAKE.

https://wingulamashahidi.org/ikabodi-maana-yake-ni-nini/

AMELAANIWA AANGIKWAYE MSALABANI.

UNYAKUO.

Rudi Nyumbani:

Print this post

Nini maana ya “Usimtokose mwana-mbuzi katika maziwa ya mama yake?”

SWALI: Biblia inamaanisha nini inaposema “Usimtokose mwana-mbuzi katika maziwa ya mama yake.”


JIBU: Huu ni msemo ambao umeonekana ukipachikwa katikati ya vifungu kadha wa kadha kwenye biblia..

Kwa mfano utaona.. pale kwenye Kutoka 23:18-19 inasema..

18 Usisongeze damu ya dhabihu zangu pamoja na mkate uliotiwa chachu, wala mafuta ya sikukuu yangu usiyaache kusalia hata asubuhi.

19 Ya kwanza ya malimbuko ya nchi yako utayaleta na kuyatia ndani ya nyumba ya Bwana, Mungu wako. Usimtokose mwana-mbuzi katika maziwa ya mama yake.

Ukisoma tena..Kutoka 34:25-26, utaona inasema hivi..

“25 Usisongeze damu ya sadaka yangu pamoja na mkate uliotiwa chachu; wala hiyo sadaka ya sikukuu ya pasaka haitasazwa hata asubuhi.

26 Vitu vya kwanza vya malimbuko ya nchi yako utavileta na kuvitia ndani ya nyumba ya Bwana Mungu wako. Usimtokose mwana-mbuzi katika maziwa ya mama yake”.

Ukirudi tena kwenye Kumbukumbu 14:21 nayo pia utaona ikisema.

“Msile nyamafu yo yote; waweza kumpa mgeni aliye ndani ya malango yako, ili apate kula; au kumliza mtu wa mataifa; kwa kuwa wewe u taifa takatifu kwa Bwana, Mungu wako. Usimtokose mwana-mbuzi katika maziwa ya mamaye”.

Sasa pale anaposema, usimtokose mwana-mbuzi, katika maziwa ya mama yake, anamaanisha kumchemsha mtoto wa mbuzi, kwa maziwa ya mama yake, yaani badala ya kumchemsha kwenye maji, wewe unachukua yale maziwa anayoyanyonya kutoka kwa mama yake na kumchemshia nayo..

Kwa namna ya kawaida ni kitendo kisicho cha kiungwana chenye ukakasi kidogo, hata kwako wewe unayesikia eti?..Utajiuliza ni kwanini ufanye hivyo? Kwani hakuna maji ya kumchemshia, au kitu kingine mpaka utumie maziwa, tena yale yale ya mama yake? Ni sawa na nguruwe aliyezaa mtoto, halafu unampa mtoto wake mwenyewe amle kama chakula chake..sasa hiyo ndio picha iliyopo hapo.

Ni kitendo kinachoonyesha unyama si unyama, ukosefu wa nidhamu..?

Ni utaratibu na mfumo wa kipagani ambao ulikuwa unafanyika na watu wa mataifa wasiomjua Mungu, walikuwa wanafanya hivyo kwa sababu za kishirikina, ni kama mila zinazoendelea siku hizi, hivyo Mungu aliwaonya wana wa Israeli wasifanye mambo kama hayo, kwasababu ni machukizo mbele zake, ni Utaratibu ambao hauna tofauti na ule wa kuwapitisha watoto kwenye moto, (soma 2Wafalme 21:6, 2Wafalme 16:3).

Hata sasa, wengi wetu tunafanya kafara kama hizo rohoni?.

Tunamtolea Mungu dhabihu zilizochanganyikana na mambo ambayo Mungu ameyakataza, tunafanya mambo kama watu wa mataifa. Tunamsifu Mungu na huku vinywa vyetu vimejaa matusi, na masengenyo, chuki na visasi, tunamtolea Mungu na huku biashara zetu ni haramu, tunahudhuria kanisani lakini tunaendelea kudumisha mila zetu za kishirikina, hali kadhalika tumeokoka lakini heshima kwa mzazi haipo, na heshima kwa Watoto wetu haipo (hiyo yote katika roho ni sawa na kumtokosa mwanambuzi katika maziwa yake) N.k.

Bwana atusaidie, tuzishike amri zake na tumpendeze yeye.

Bwana atuokoe na kutubariki..

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312


Mada Nyinginezo:

USITUMAINISHWE NA MANENO YA UONGO.

YESU KWETU NI RAFIKI

Bali wajane walio vijana ukatae kuwaandika hao.

ZIFAHAMU HUDUMA KUU (10) ZA SHETANI DUNIANI.

CHOCHOTE UMFANYIACHO KRISTO KINA THAMANI.

Rudi Nyumbani:

Print this post

AINA ZA MAJINI, MAJINA YAO, KAZI ZAO, NA TIBA ZAKE.

Ndugu Msomaji, nakukaribisha katika ukurasa huu kupata maarifa ya rohoni, Awali ya yote nakutahadharisha kuwa mitandaoni kuna elimu nyingi za uongo, Hivyo uisamini kila kitu mtu anachokuambia, kwasababu wengine, hawana nia njema wapo kwa ajili ya kutangazama biashara zao, na hawana lolote la kukusaidia kiroho.

 Sasa turudi katika kutazama majini, na kazi zao.

Nataka ufahamu kuwa ufalme wa Roho, upo katika pande kuu mbili tu!

  1. Upande wa Mungu.
  2. Upande wa Shetani.

Hakuna upande wa hapo katikati..

Upande wa Mungu yupo Mungu mwenyewe pamoja na malaika zake watakatifu. Na upande wa Shetani, Yupo shetani na malaika zake(Mapepo), Haya mapepo ndio wale malaika walioasi mbinguni, na kwa jina lingine wanaitwa MAJINI.

Usidanganywe na mwanadamu yeyote chini ya jua kukwambia kuwa kuna majini wazuri..Huo ni uongo mkubwa sana. Hakuna majini wazuri, majini wote ni roho za mashetani zinazofanya kazi duniani  kuangamiza roho wa watu, na lengo lao kubwa ni kuwapeleka  watu kuzimu..Na ndio maana nakuambia chukua tahadhari mpendwa. Mafundisho ya mashetani yalitabiriwa kutokea sana katika siku hizi za mwisho

1Timotheo 4:1 “Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani;

Pengine ulishawahi kukutana na watu wakikueleza juu ya majini wazuri, na wabaya akakutajia mmojawapo kati ya hawa..

  • Jini subiani,
  • Jini Maimuna,
  • Jini Makata,
  • Jini Ruhani,
  • Jini Kabula,
  • Jini Kajadu,
  • Jini Sharifu,
  • Jini Jabari,
  • Jini bahari,
  • Jini Bedui,
  • Jini Zuhura,
  • Jini Zohari,
  • Jini Zamda n.k. n.k.

Haya yote ni mapepo ya kuzimu, na mbali ya kuwapeleka watu kuzimu huwa yanafanya na kazi nyingine pia za kuiharibu dunia na jamii,

  • mengine yanawafanya watu wawe vichaa na kutembea uchi ..

Mathayo 8:28 “Naye alipofika ng’ambo, katika nchi ya Wagerasi, watu wawili wenye pepo walikutana naye, wanatoka makaburini, wakali mno, hata mtu asiweze kuipitia njia ile”.

  • Mengine yawanawafanya watu wawe na ulemavu wa kudumu.

Luka 13:11 “Na tazama, palikuwa na mwanamke aliyekuwa na pepo wa udhaifu muda wa miaka kumi na minane, naye amepindana, hawezi kujinyosha kabisa.

12 Yesu alipomwona alimwita, akamwambia, Mama, umefunguliwa katika udhaifu wako.

  • Wawe mabubu, na vipofu, na viziwi..

Luka 11:14 “Naye alikuwa akitoa pepo bubu; ikawa pepo alipotoka, yule bubu akanena, makutano wakastaajabu”.

  • Mengine yanawafanya watu wasimpende Mungu, pale wanapotakana kusoma biblia, au kusikia mahubiri wanachukia na kuleta vurugu na kutaka kuondoka maeneo hayo.

Luka 8:2 “na wanawake kadha wa kadha ambao walikuwa na pepo wabaya na magonjwa wakaponywa; nao ni Mariamu aitwaye Magdalene aliyetokwa na pepo saba”,

  • Mengine yanawafanya watu wasifanikiwe, katika mambo yao; Ndoa, biashara, elimu, n.k. n.k.k

Sasa, watu wanawadanganya watu na kuambiwa , jini(Pepo) ukitaka kulituma au  likikuingia, fauta taratibu Fulani za asili kulitoa, labda aidha chukua majivu changanya na hiki au na kile, au andika maneno kwenye karatasi jeupe fanya hivi au vile, au ukilala angalia juu, au chukua udongo wa makaburini uchanganye na maji ya bahari na hiki au kile…Mambo kibao, Na ukifanya hivyo basi utaweza kulitoa jini hilo, au kulituma kufanya kazi Fulani.

Ndugu kama ulishawahi kufanya hivyo, ujue kuwa hukulitoa wala hukulituma, bali ndio umelikaribisha ndani ya maisha yako kukuharibu.

Idadi ya mapepo ulimwenguni ni kubwa sana, na yapo yanazunguka zunguka duniani kila mahali (Ayubu 1:7), hivyo kwa namna moja au nyingine ikiwa hujafahamu njia ya kufanya yasikukurabie basi utateswa sana. Na wengi wanadhani mpaka yawepo ndani yako, ni mpaka yatakapojidhihirisha..Hilo jambo si kweli, Mapepo ni roho, na yanafanya kazi kwa njia nyingi, mtu anaweza kuwa ni jini ndani yake lakini lisijidhirishe hata kidogo, lakini utamjua tu huyo mtu kwa tabia ya kitofauti aliyonayo.

NIFANYE NINI ILI MAJINI YASINIFUATE?

Lakini habari njema ni kuwa, yupo mmoja tu, anayeweza kumtoa mtu Mapepo/Majini kabisa kabisa, Na NI mmoja TU anayeweza kumzuia mtu asisogelewa na hayo maroho ya mashetani ndani yake kabisa kabisa, na huyo mtu si mwingine zaidi ya YESU KRISTO.

Ikiwa wewe ni Mkristo/muislamu, huna haja ya kuzunguka kwa waganga, au kwa watu wanaojiita mataalamu wakuondolee,au wakufukuzie mapepo katika maisha yako, hao wanakudanganya tu..unamuhitaji YESU..

Yeye pekee yake ndiye aliyeweza kuyatoa majini kama aliweza kuyatoa majini (zaidi ya 82,000) kwa wakati mmoja, kwa mtu ambaye alishindikana katika mji mzima yeye akayatoa .Na saa ile ile Yule kichaa akawa mzima..

Mathayo 8:28 “Naye alipofika ng’ambo, katika nchi ya Wagerasi, watu wawili wenye pepo walikutana naye, wanatoka makaburini, wakali mno, hata mtu asiweze kuipitia njia ile.

29 Na tazama, wakapiga kelele, wakisema, Tuna nini nawe, Mwana wa Mungu? Je! Umekuja kututesa kabla ya muhula wetu?

30 Basi, kulikuwako mbali nao kundi la nguruwe wengi wakilisha.

31 Wale pepo wakamsihi, wakisema, Ukitutoa, tuache twende, tukaingie katika lile kundi la nguruwe.

32 Akawaambia, Nendeni. Wakatoka, wakaingia katika nguruwe; na kumbe! Kundi lote wakatelemka kwa kasi gengeni hata baharini, wakafa majini”.

Na wewe hivyo hivyo, ukimpokea Yesu leo katika maisha yako, atakufanya kuwa huru..Biblia inasema hivyo katika Yohana 8:36..

Je! Unataka leo Yesu akuokoe?..Kumbuka wokovu sio dini, wokovu sio fedha..Wokovu ni bure kwa watu wote watakaompokea Yesu, Hivyo, kama upo tayari leo akubadilishe, unachopaswa kwanza kufanya ni kukubali kuacha dhambi zako zote,  Kisha unatubu, na baada ya hapo Yesu atayabadilisha maisha yako.

Sasa kabla sijakwenda kukuombea neema ya Yesu, ikuponye hapo hapo ulipo..Fuatisha kwanza hii sala ya Toba, kwa kumaanisha kabisa..

Hapo ulipo, chukua muda mchache ujitenge peke yako. Kisha piga magoti, kisha sema maneno haya kwa Imani,

EE MUNGU BABA, NAJA MBELE ZAKO, NIKIWA NINAJITAMBUA KUWA MIMI NI MKOSAJI NA NIMEKUTENDA DHAMBI NYINGI, NA KWAMBA NIMESTAHILI HUKUMU. LAKINI WEWE MUNGU WANGU ULISEMA KATIKA NENO LAKO KUWA WEWE NI MUNGU WA REHEMA UNAYEWAREHEMU  MAELFU ELFU YA WATU WANAOKUPENDA WEWE. NA LEO HII NINAKUJA MBELE ZAKO NAHITAJI MSAMAHA WAKO NA MSAADA WAKO MUNGU WANGU, NINATUBU DHAMBI ZANGU ZOTE KWA KUMAANISHA NA KWA MOYO WANGU WOTE, NINAKIRI KUWA YESU KRISTO NI BWANA, NA YEYE NDIYE MWOKOZI WA HUU ULIMWENGUNI. HIVYO NAOMBA DAMU YA MWANAO TAKATIFU INISAFISHE UOVU WANGU WOTE SASA NIFANYIKE KUWA KIUMBE KIPYA KUANZIA LEO NA HATA MILELE.

ASANTE BWANA YESU KWA KUNIPOKEA NA KUNISAMEHE.

AMEN.

Sasa ikiwa umefuatisha sala hiyo kwa Imani ..Hatua iliyobakia kwako ni kuithitisha toba yako kwa Vitendo ikiwa ulikuwa unafanya mambo yote ambayo hayampendezi Mungu unayaacha na kujitenga nayo, Sasa Mungu akishaona umegeuka kwa vitendo basi toba yako anaipokea na atakuwa na uhalali kwa kuja ndani yako wakati huo huo na kufanya makao ya milele kwako.

Sasa upo tayari kuombewa..

Bwana Yesu, wewe ni yeye Yule jana na leo na hata milele, uliwaponya wale, ukaniponya mimi, utamponya na huyu ndugu aliyetubu leo hii.. Nakuomba Bwana Yesu unyooshe mkono wako umguse, roho yake, uyaguse maisha yako, uuguse mwili wako. Chunguza kiungo kimoja hadi kingine, uone ni wapi, pana kasoro umponye Bwana Yesu kama ulivyomponya Yule kichaa. Nguvu zote za giza zinazomsumbua mwili wake, au familia yake, au biashara yake, au ajira yake, leo hii nazitangazia mwisho wake kwa jina lako YESU KRISTO. Natuma moto wa Roho Mtakatifu ukayafunike maisha yake kama ulivyofunika Ayubu kuanzia leo na hata milele.

Asante Bwana Yesu kwa kumponya. Amen.

Sasa ikiwa umefuatisha maelekezo yote, kuanzia hichi kipindi utaanza kuona jinsi Yesu atakavyotembea na wewe maishani mwako. Hivyo usiache kujifunza Neno la Mungu lililo hai. Mwisho kabisa wa somo hili kuna masomo mengine ya kiroho, anza kuyapitia ujifunze ukue kimaarifa.

Pia kama utahitaji msaada zaidi, wa kupata mafundisho ya mara kwa mara kwa njia ya email. Au whatsapp yako, na ubatizo, basi wasiliana nasi kwa namba hizi : +255789001312

Bwana akubariki sana. Na hongera kwa wokovu.

Group la whatsapp Kwa mgawanyo bora wa masomo download App hapa>> App wingu la mashahidi

Mada Nyinginezo:

MAJINI WAZURI WAPO?

SI MAPEPO YOTE NI YA KULIPUKA.

NDIPO HUENDA AKACHUKUA PEPO WENGINE SABA.

Je! Wana wenu huwatoa kwa nani? maana yake ni nini?

MAPEPO YANATAFUTA HIFADHI NDANI YAKO KWA BIDII SANA.

Rudi Nyumbani:

Print this post