1Wakorintho 12:3 “Kwa hiyo nawaarifu, ya kwamba hakuna mtu anenaye katika Roho wa Mungu, kusema, Yesu amelaaniwa; wala hawezi mtu kusema, Yesu ni Bwana, isipokuwa katika Roho Mtakatifu.”
Katika hali ya kawaida kila mtu anaweza kusema “Yesu ni Bwana”, hata watu wa kidunia, wanaweza kulitamka hilo neno, lakini wasiwe wamemaanisha, au wamejua uzito wake, wakawa wamelitaja tu.. Lakini kwa mtu ambaye amempokea Roho Mtakatifu, na kufunuliwa kwa Roho kuwa Yesu ni nani, kwanini amekuja duniani, kwanini amwage damu yake, afe na kufufuka, na yupo wapi sasahivi?..Mtu wa namna hiyo kama akitamka “Yesu ni Bwana”,… kutamka kwake kunakuwa na maana sana na nguvu kubwa. Kwasababu amekutamka katika Roho.
Hivyo Mtu anayetaja “Yesu ni Bwana” katika Roho Mtakatifu ni lazima atakuwa ni mtakatifu, kwasababu amemjua Mungu, kadhalika atakuwa anamheshimu Mungu na kumwogopa, kutokana na ufunuo mzito alioupata kumhusu Yeye (Yesu).
Lakini Yule anayesema tu “Yesu ni Bwana” bila Roho, maana yake hamjui Yesu, hana mpango na maneno yake, hana ufunuo wowote alioupata unaomfanya yeye aseme hivyo, mtu wa namna hiyo kutamka kwake hakuna manufaa yoyote, ndio maana hapo biblia inasema.. “mtu hawezi kusema Yesu ni Bwana isipokuwa katika Roho Mtakatifu”..maana yake atakuwa anasema tu kimdomo, na si kwa kuelewa na kumaanisha.
Bwana Yesu alisema maneno haya…
Mathayo 7:21 “SI KILA MTU ANIAMBIAYE, BWANA, BWANA, ATAKAYEINGIA KATIKA UFALME WA MBINGUNI; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.
22 Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi?
23 Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu”
Umeona?.. Kusema tu “Yesu ni Bwana” bila ya kuwa na badiliko halisi la ndani, ambalo hilo linaletwa na Roho Mtakatifu mwenyewe, ni kazi bure!.. Vile vile huwezi kuwa na Roho Mtakatifu halafu useme Bwana Yesu kalaaniwa.. hilo haliwezekani.
Hivyo ili tuyafanye mapenzi ya Mungu, na maneno ya midomo yetu pamoja na sala zetu zikubalike mbele za Mungu, hatuna budi kuzaliwa mara ya pili, na kuzaliwa mara ya pili kunakuja kwa kutubu dhambi, kwa kumaanisha kuziacha, na kubatizwa katika ubatizo sahihi wa maji mengi pamoja na kupokea Roho Mtakatifu.
Baada ya hapo, lolote tunalolitamka la kumwadhimisha Mungu, kumsifu, kumwomba, na kumkiri linakuwa katika Roho, na hivyo linaleta matokeo makubwa sana. Lakini kama hatutatubu kwa kumaanisha kuacha dhambi, hata sala zetu zinakuwa ni bure, hata sifa zetu kwake zinakuwa ni bure…
2Timotheo 2: 19 “Lakini msingi wa Mungu ulio imara umesimama, wenye muhuri hii, Bwana awajua walio wake. Na tena, Kila alitajaye jina la Bwana na auache uovu”
Maran atha!
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mafundisho mengi
Mada Nyinginezo:
Kwanini Bwana Yesu aliwaambia wanafunzi wake wasichukue chochote isipokuwa fimbo tu?
Bwana Yesu alitupa dalili za kurudi kwake, akatuambia mkiona dalili Fulani Fulani kama vile matetemeko, mlipuko wa magonjwa, manabii wa uongo, vita n.k. Basi tujue yupo mlangoni kurudi. Lakini kamwe hakutupa dalili ya SIKU yenyewe atakayorudi itakuwaje.. Na hiyo ndio hatari Zaidi kwasababu watu wengi leo hii japokuwa wanajua Yesu atarudi siku yoyote kutokana na kuwa dalili hizo zimeshatimia zote, Lakini bado wanachunguza chunguza siku yenyewe, wakidhani labda watashtukia lolote.
Bwana Yesu alisema siku ya kuja kwake, inafanana na siku zile za Nuhu, Siku zile mpaka Nuhu anaingia kwenye Safina hakuna mtu yeyote alitambua kuwa tayari Mungu ameshaihukumu dunia.. mpaka zikapita siku saba, nyingine ndipo mvua ya gharika ikashuka kwenye dunia.
Mathayo 24:38 “Kwa kuwa kama vile siku zile zilizokuwa kabla ya Gharika watu walivyokuwa wakila, na kunywa, wakioa na kuolewa, hata siku ile aliyoingia Nuhu katika safina,
39 WASITAMBUE, HATA GHARIKA IKAJA, IKAWACHUKUA WOTE, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu.
40 Wakati ule watu wawili watakuwako kondeni; mmoja atwaliwa, mmoja aachwa;
41 wanawake wawili watakuwa wakisaga; mmoja atwaliwa, mmoja aachwa.
42 Kesheni basi; kwa maana hamjui ni siku ipi atakayokuja Bwana wenu”.
Unaona? Leo hii, kama wewe sio “bibi-arusi” wa kweli wa Kristo, nikimaanisha, kama sio mkisto aliyesimama katika wokovu kweli kweli, usitazamie utatambua lolote siku Kristo anarudi kuwanyakua watakatifu wake. Kwasababu hata Bibi-arusi wake mwenyewe hatojua siku hiyo itakavyokuwa sembuse wewe?..
Na ndio maana aliwaambia mpaka na wateule wake, kwamba wajiweke tayari, waifanye kazi yake, watimize wajibu wao walioitwa hapa duniani wa kuitangaza injili yake, kwasababu saa wasiodhani ndio atakayokuja..
Mathayo 24:43 “Lakini fahamuni neno hili; kama mwenye nyumba angaliijua ile zamu mwivi atakayokuja, angalikesha, wala asingaliiacha nyumba yake kuvunjwa.
44 Kwa sababu hiyo ninyi nanyi jiwekeni tayari; kwa kuwa katika SAA MSIYODHANI MWANA WA ADAMU YUAJA.
45 Ni nani basi yule mtumwa mwaminifu mwenye akili, ambaye bwana wake alimweka juu ya nyumba yake, awape watu chakula kwa wakati wake?
46 Heri mtumwa yule, ambaye bwana wake ajapo atamkuta akifanya hivyo.
47 Amin, nawaambieni, atamweka juu ya vitu vyake vyote.”
Hakuna mtu atakayeitambua siku hiyo, itakuja ghafla tu bila hodi, hakuna dalili yoyote itakayotutambulisha, itakuwa kama tu ilivyo leo, au jana, wakati ambapo watu wanapanga mipango yao ya kimaisha, wanalijenga taifa lao, wanauza pombe, na kufanya biashara hapo hapo, Unyakuo unapita , mmoja anatwaliwa mmoja anaachwa..
Watu wengi sana wataingiwa na butwaa, wakisema mbona Bwana hakutupa taarifa au kiashirio fulani, mbona, angani hakukuonekana chochote, mbona tulitazamia jambo Fulani kwanza tulione, ndio unyakuo upite, imekuwaje, amesharudi, wakati watu wengine hawajahubiriwa bado injili. Lakini ndio hivyo tayari watakatifu wameshaondolewa.
Wakati huo upo karibu sana ndugu yangu, ridhika na dalili tunazoziona, kwasababu hakutakuwa na nyingine Zaidi ya hizo zilizoandikwa kwenye biblia. Usidhani malaika atatokea hapo mawinguni kutuhubiria injili kwamba kesho Yesu ndio anarudi.
Kama utakosa unyakuo, basi ujue, utakuwa katika majuto na vilio na kusaga meno kusikokuwa kwa kawaida. Majuto hayo, unaweza ukayaona sio kitu leo kwasababu bado hayajakukuta, lakini subiri siku hiyo ikufikie, hutatamani uishi. Hicho kiburi cha uzima ulichonacho leo, siku hiyo kitayeyuka chote, utamtafuta Mungu hutamwona. Utalia hakuna atakayekusikia, makanisa yatakuwa hayana faida yoyote kwako. Hakuna chochote kitakuwa na maana kwao, kwasababu hata pesa hazitafanya kazi wakati huo.
Ndugu, ndani ya hichi kipindi kifupi tulichobakiwa nacho bado unayo nafasi ndogo sana ya kutubu, Tubu leo kwa kumaanisha kabisa kuacha dhambi zako, na Kristo atakupokea.
Shalom.
Kumbuka katika saa usiyodhani Kristo anakuja!
Maran Atha.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mafundisho mengi
Mada Nyinginezo:
Shalom!
Ni vizuri kulisoma Neno la Mungu kwa makini, huku tukimshirikisha Roho Mtakatifu, vinginevyo kwa kupitia biblia hii hii, tunaweza hata kumhalalisha shetani kuwa ni Mungu. Wako watu wanaotumia biblia hii kuhalalisha pombe, kadhalika wapo watu wanaotumia biblia hii hii kuhalalisha ndoa za jinsia moja, na wapo wanaotumia biblia hii kuhalalisha ndoa za mitara. Hivyo ni muhimu sana kumtumia Roho Mtakatifu katika kuyatafsiri maandiko..
2Wakoritho 3:6 “Naye ndiye aliyetutosheleza kuwa wahudumu wa agano jipya; si wa andiko, bali wa roho; kwa MAANA ANDIKO HUUA, BALI ROHO HUHUISHA”.
Sasa tukirudi katika habari ya Malkia Esta.
Malkia Esta hakwenda kupambwa kabla yakuingia kwa mfalme Ahasuero. Mfalme Ahasuero hakuwa anataka kuona uso uliopakwa make-up. Hapana!. Alichokuwa anafanyiwa Esta kwa miezi 12, sio kubadilishiwa lipstick kila siku, au hereni, au mavazi mazuri, mpaka awe mzuri.. Hapana!..Hata kwa akili za kawaida tu haileti maana. Mtu awekwe miezi 12 anapodolewa tu!..haina maana!.
Alichokuwa anafanyiwa Esta katika miezi 12, ni KUTIBIWA!.
Kumbuka wanawake waliojitokeza kutafuta nafasi ya umalkia walikuwa ni wengi, na wa madaraja yote, ndio maana hata Esta aliyekuwa daraja la chini kabisa alipata nafasi ya kuingia katika shindano lile. Sasa katika hali ya kawaida, mwanamke hata kama ni mzuri, lakini kama kaishi maisha fulani ya chini (duni) ni lazima ngozi yake itafifia kwa sehemu Fulani, au itakuwa na mabaka kadhaa, au makovu au michubuko, na makunyanzi, haiwezi kuwa sawa na ngozi ya mtu yule ambaye hapigwi na jua yupo ndani tu siku zote.
Sasa ili kuyaondoa hizo kasoro chache katika uso, na mabaka katika ngozi na kumrudisha mtu katika hali yake ya ASILI, yapo matibabu maalumu ambayo mtu anaweza kuwekwa chini ya hayo kwa miezi kadhaa, huku akizuiliwa pia na hari za kimaisha na baada ya kumaliza hayo, mtu Yule ngozi yake inaweza kurudi na kuwa kama ya mtoto mdogo. Na mtu akawa ni mzuri bila make-up yoyote.(Uso wake unakuwa ni mzuri lakini hauna make-up yoyote). Anakuwa anatakata, Ndicho Malkia Esta alichofanyiwa.
Esta 2:8 “Basi ikawa, wakati iliposikiwa amri ya mfalme na mbiu yake, wasichana wengi wakakusanyika huko Shushani ngomeni mikononi mwa Hegai; Esta naye aliingizwa katika nyumba ya mfalme, mikononi mwa Hegai mwenye kuwalinda wanawake.
9 Yule mwanamwali akampendeza, akapokea fadhili kwake; NAYE AKAMPA UPESI VIFAA VYA UTAKASO, pamoja na posho zake, na vijakazi saba walio haki yake, wa nyumbani mwa mfalme. Pia akamhamisha yeye na vijakazi wake akawaweka mahali pazuri katika nyumba ya wanawake..…….
12 Basi ilipowadia zamu yake mwanamwali mmojawapo aingie kwa mfalme Ahasuero, hali akiisha KUFANYIWA SAWASAWA NA SHERIA YA WANAWAKE MIEZI KUMI NA MIWILI; YAANI, NDIVYO ZILIVYOTIMIA SIKU ZAO ZA UTAKASO, MIEZI SITA KWA MAFUTA YA MANEMANE, NA MIEZI SITA KWA MANUKATO NA VIFAA VYA UTAKASO WA WANAWAKE”
Kwahiyo alichokuwa anafanyiwa Esta tunaweza kusema hakikuwa tofauti sana na walichokuwa wanafanyiwa wakina Danieli, Shedraka, Meshaki na Abedinego, kabla ya kuingia kwa mfalme..
Hivyo Esta hakuwa anajipaka wanja kwa miezi 12, wala kubadilisha badilisha wigi kichwani mwake mpaka apate litakalomkaa vizuri, wala hakuwa anajibangua bangua ngozi kwa miezi hiyo yote, wala kubadili hereni mpaka itakayomfaa, wala kuvaa vinguo vya kubana, wala kushona rasta kichwani, wala kupaka rangi uso wake, wala kuweka nyusi za plastiki, au kuzichonga, wala hakuwa anaweka kucha za bandia kwa miezi 12, ndipo aingie kwa mfalme. Hata kwa akili za kawaida ni mfalme gani anataka kuona mtu mithili ya kinyago, kimeingia ndani kwake, na tena kinyago hicho akiandae kwa miezi 12. Kama ni kujipodoa tu, siku moja tu! Ingetosha kumkamilisha Malkia Esta.
Hivyo ni muhimu kusoma maandiko kwa msaada wa Roho Mtakatifu.
Dada unayesoma ujumbe huu, kama unaweka wigi, fahamu kuwa unafanya jambo lisilo sahihi, kama unapaka wanja, au unajichubua ili uwe mweupe, Esta hakuwa anajichubua, kama angekuwa anafanya hivyo, ingemtosha siku mbili tu kukamilisha hilo zoezi, hivyo usidanganyike na injili za jehanamu, zinazokuambia kujichubua sio dhambi, kadhalika kama unapaka kucha rangi, au unavaa nguo za kubana, na zisizokupasa kama suruali, napenda nikushauri viache vyote hivyo kavichome moto, na wala hata usimpe mtu mwingine, kwasababu vitakupeleka jehanamu. (Mwili wako ni hekalu la Roho Mtakatifu na si roho yako). www wingulamashahidi org.
Kama unajipenda mwili wako hujakatazwa kuutunza, utunze, ioshe ngozi yako, paka mafuta yako ya asili, kama hutaki iwe na mabaka, hujakatazwa usitembee juani, kuwa mtu wa kukaa kivulini. Lakini hakikisha unakuwa wa asili siku zote.
Wengi wa wanawake wanaosumbuliwa na roho sugu leo, wengi ni kutokana na kutoithamini miili yao. Asilimia kubwa lazima utakuta hawataki kuacha kuichafua miili yao. Wapo radhi waache kila kitu, lakini si kuacha kujipaka wanja, au kuvaa suruali na mengineyo hawataki, hivyo miili yao inakuwa ni lango la maroho kuingia na kutoka.
1Wakorintho 3:17 “Kama mtu akiliharibu hekalu la Mungu, Mungu atamharibu mtu huyo. Kwa maana hekalu la Mungu ni takatifu, ambalo ndilo ninyi”.
1Timotheo 2:9 “Vivyo hivyo wanawake na wajipambe kwa mavazi ya kujisitiri, pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi; si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani;
10 bali kwa matendo mema, kama iwapasavyo wanawake wanaoukiri uchaji wa Mungu”.
Maran atha!
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mafundisho
Mada Nyinginezo:
Wewe kama mtumishi wa Mungu, je! unayafanya mapenzi ya Bwana Yesu?.
Ni muhimu kuyafahamu mapenzi ya Bwana Yesu na kuyatenda hayo ili umpendeze Mungu.
Sasa Mapenzi ya Bwana Yesu ni yapi?.
Tusome,
Yohana 6:37 “Wote anipao Baba watakuja kwangu; wala ye yote ajaye kwangu sitamtupa nje kamwe.
38 Kwa kuwa mimi sikushuka kutoka mbinguni ili niyafanye mapenzi yangu, bali mapenzi yake aliyenipeleka.
39 Na mapenzi yake aliyenipeleka ni haya, YA KWAMBA KATIKA WOTE ALIONIPA NISIMPOTEZE HATA MMOJA, BALI NIMFUFUE SIKU YA MWISHO.
40 Kwa kuwa mapenzi yake Baba yangu ni haya, ya kwamba KILA AMTAZAMAYE MWANA NA KUMWAMINI YEYE, AWE NA UZIMA WA MILELE; NAMI NITAMFUFUA SIKU YA MWISHO”
Hayo ndio mapenzi ya Mungu, kwamba “wote waliokuja kwa Yesu wasipotee hata mmoja” na pia “kila atakayemtazama Yesu na kumwamini apate uzima wa milele”..
Maana yake ni kwamba, mtumishi yeyote wa Mungu ili kuyatenda mapenzi kamili ya Mungu, hana budi KUISHI KATIKA HAYO MAONO MAWILI ;
1) kuhakikisha kwamba “anawafanya watu wamtazame Yesu, na kumwamini ili wapate uzima wa milele” na
2) kuhakikisha kwamba “wote waliomfuata Yesu, hapotei hata mmoja”.
Hayo ndio maono makuu mawili Bwana Yesu aliyotembea nayo, hata akashuhudiwa na Baba kuwa amempendeza yeye.
Ukitaka kumpendeza Yesu kikamilifu, hakikisha unawafanya watu wamtazame Yesu na kumwamini. Biblia inasema kuna furaha mbinguni, mtu mmoja atubupo, malaika wanashangilia na kuruka ruka. Hivyo ili tuifurahishe mbingu hatuna budi kuwafanya wengi wamwamini Yesu, kwa kadri tuwezavyo.
Na haishii hapo tu!, kuwageuza wamwache Yesu na kisha kuwaacha!.. Ili kuyakamilisha mapenzi ya Mungu, hatuna budi kuhakikisha kwamba Wote waliomfuata Yesu (yaani waliomwamini), hapotei hata mmoja. Maana yake kuwachunga! Na kuwalea na kuhakikisha sisi hatuwi sababu ya wao kurudi nyuma au kuanguka..(Kwa ufupi, tunakuwa tunawafanya wazidi kudumu katika wokovu).
Yohana 15:16 “Si ninyi mlionichagua mimi, bali ni mimi niliyewachagua ninyi; nami nikawaweka mwende mkazae matunda; NA MATUNDA YENU YAPATE KUKAA; ili kwamba lo lote mmwombalo Baba kwa jina langu awapeni”.
Hapo anasema “amesema ametuweka tukazae matunda” na “matunda hayo yapate kukaa”…Umeona hajaishia kusema tu!, mkazae matunda halafu basi!…hapana!..bali pia matunda hayo tutakayoyazaa yapate kukaa! Yaani yadumu kwa muda mrefu. Sio la leo na kesho, bali lidumu muda mrefu.
Bwana Yesu kuna wakati alimwuliza Petro kama anampenda..akamwambia..
Yohana 21:15 “Basi walipokwisha kula, Yesu akamwambia Simoni Petro, Je! Simoni wa Yohana, wewe wanipenda kuliko hawa? Akamwambia , Naam ,Bwana, wewe wajua kuwa nakupenda. Akamwambia, LISHA WANA-KONDOO WANGU.
16 Akamwambia tena mara ya pili, Simoni wa Yohana, wanipenda? Akamwambia, Ndiyo, Bwana, wewe wajua kuwa nakupenda. Akamwambia, CHUNGA KONDOO ZANGU.
17 Akamwambia mara ya tatu, Simoni wa Yohana, wanipenda? Petro alihuzunika kwa vile alivyomwambia mara ya tatu, Wanipenda? Akamwambia, Bwana, wewe wajua yote; wewe umetambua ya kuwa nakupenda. Yesu akamwambia, LISHA KONDOO ZANGU”.
Umeona hapo Bwana anamwambia vitu viwili LISHA, na CHUNGA. Hajamwambia tu alishe, bali pia achunge.. Na sisi tuna wajibu sio tu wa kulisha, bali pia kuchunga!. Tunachunga watu wasirudi nyuma, (hapo tutayafanya matunda yetu yakae), na ndio tutayafanya mapenzi ya Mungu.
Matendo 15:36 “Baada ya siku kadha wa kadha Paulo akamwambia Barnaba, Haya! Mrejee sasa tukawaangalie hao ndugu katika kila mji tulipolihubiri neno la Bwana, wa hali gani………………..
40 Lakini Paulo akamchagua Sila, akaondoka, akiombewa na wale ndugu apewe neema ya Bwana.
41 AKAPITA KATIKA SHAMU NA KILIKIA AKIYATHIBITISHA MAKANISA”.
Je na wewe unayatenda mapenzi ya Mungu?..Unawavuta watu kwa Yesu?, je unawafanya wadumu katika Imani?. Kama unafanya hayo, basi jua unafanya jambo jema sana na kuu.
Yohana 4:34 “Yesu akawaambia, Chakula changu ndicho hiki, niyatende mapenzi yake aliyenipeleka, nikaimalize kazi yake.
35 Hamsemi ninyi, Bado miezi minne, ndipo yaja mavuno? Tazama, mimi nawaambieni, Inueni macho yenu myatazame mashamba, ya kuwa yamekwisha kuwa meupe, tayari kwa mavuno”.
Bwana atusaidie tuyafanye mapenzi yake.
Maran atha!
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi:+255693036618/ +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
[07/11, 09:47] Justina Raphael: https://wingulamashahidi.org/2024/03/14/usiwe-mkristo-wa-kukaa-tu-ghalani/
*USIWE MKRISTO WA KUKAA TU GHALANI,*
Nakusalimu katika jina la Bwana wetu Yesu Kristo. Karibu tujifunze maneno ya uzima ya mwokozi.
Watu waliomwamini Yesu Kristo, yaani waliopokea ondoleo la dhambi zao. Hutambulika kama NGANO, lakini watu ambao bado wapo kwenye dhambi, hujulikana kama MAKAPI.
Sasa kazi ya kwanza ambayo Yesu anaifanya kwa mwamini, ni kumtenganisha yeye na makapi, kisha humweka katika ghala lake.
Mathayo 3:12 Ambaye pepeto lake li mkononi mwake, naye atausafisha sana uwanda wake; na kuikusanya ngano yake ghalani, bali makapi atayateketeza kwa moto usiozimika.
Ghalani ni uweponi mwa Mungu, yaani kutengwa na udunia.
Soma pia..Mathayo 13:29-30.
Sasa kama wewe unafahamu ukulima, unajua kabisa si mbegu zote zinawekwa ghalani kwa matumizi ya chakula, zipo nyingine, zinachukuliwa na kurudishwa shambani ili kwenda kuzalisha nyingine. Na baadaye huongeza ghala la mkulima.
Tofauti kabisa na ile inayobakia pale ghalani, itaendelea kubakia vilevile hata miaka 10, lakini ile inayokwenda shambani, ndani ya hicho kipindi cha miaka 10, yaweza kuongeza magunia mengi sana ya ngano nyingine.
Ndio maana Bwana Yesu alisema maneno haya;
Yohana 12:24 Amin, amin, nawaambia, CHEMBE YA NGANO ISIPOANGUKA KATIKA NCHI, IKAFA, HUKAA HALI IYO HIYO PEKE YAKE; BALI IKIFA, HUTOA MAZAO MENGI. 25 Yeye aipendaye nafsi yake ataiangamiza; naye aichukiaye nafsi yake katika ulimwengu huu ataisalimisha hata uzima wa milele. 26 Mtu akinitumikia, na anifuate; nami nilipo, ndipo na mtumishi wangu atakapokuwapo. Tena mtu akinitumikia, Baba atamheshimu.
Umeona hapo? Kumbe isipoanguka na kuoza basi itaendelea kubakia katika hali ile ile. Lakini ikikubali kuanguka na kuoza, ardhini, basi itachipuka kama shina, na mwisho wa siku itazaa sana.
Na hapa ndipo waamini wengi, hawataki kuingia gharama. Wanatamani wamzalie Mungu matunda, lakini hawawezi, kwasababu hawajakubali “kufa na kuoza” kwa habari ya huu ulimwengu.
Hawajakubali kuziangamiza nafsi zao kwa ajili ya Kristo. Sasa hiyo ndio inayopelekea wabakie tu kama wakristo wa ghalani,wasioweza kuzalisha chochote.
Yesu alitoa sifa za mbegu yenye kuzaa katika ule mfano wa mpanzi, akasema nyingine ziliangukia njiani, nyingine kwenye miamba, nyingine kwenye miiba, na nyingine kwenye udongo mzuri. Akasema vilizoangukia kwenye udongo mzuri ziliweza kuzaa kwa tendo moja tu la “kuvumilia”
Kuvumilia nini?
Kuvumilia dhiki, na udhia kwasababu ya Kristo, kuvumilia vishawishi vya anasa, udanganyifu wa mali, na shughuli za ulimwengu huu zilizopitiliza, lakini pia kwa unyofu wa moyo walikuwa wanalitendea kazi Neno ili walilolisikia lisiwe bure adui akaliiba ndani yao. (Luka 8:11-15). Hao ndio wakristo wasio wa ghalani, ni wakristo waliokubali kutoka nje, kumletea Bwana matunda.
Je! Na sisi tunaweza kupiga hatua nyingine? Umeokoka ndio, lakini ni lazima wokovu wako uwe na matokeo kwa wengine, uwavute na wengine kwa Kristo, kama wewe ulivyovutwa. Hivyo kubali kumaanisha kumfuata Yesu na kukaa mbali na udunia kwa kadiri uwezavyo.
Jitoe pia kwa Bwana, mali zako, zitumike kuhubiri injili, tenga fungu lako kwa Bwana, penda kusapoti kazi za Mungu, usiwe msomaji tu na kusema Amen!. Onyesha kuwa na wewe ni mtendaji kazi ili thawabu yenu iwe ni moja, na yule mtendaji kazi mwingine.
Bwana atusaidie, tutoke ghalani.
Shalom.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mafundisho
Mada Nyinginezo:
SI KWA UWEZA WALA KWA NGUVU BALI KWA ROHO YANGU, ASEMA BWANA.
Ni kipi kinakupa ujasiri wa kuishi ukristo ya juu juu tu ndugu ?
Bwana atusaidie tujue majira tunayoishi..
Ulishawahi kutafakari kwa makini kwanini Bwana alifananisha kuja kwake na umeme? Kama tunavyosoma katika kitabu cha Mathayo 24:27-28
“Kwa maana kama vile umeme utokavyo mashariki ukaonekana hata magharibi, hivyo ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu.
28 Kwa kuwa po pote ulipo mzoga, ndipo watakapokusanyika tai”.
Umeme unaozungumziwa hapo sio huu wa transforma unaowaka majumbani, hapana, ni ule wa radi tunaouona sana sana wakati wa mvua, ule mwanga, unaomulika kwa ghafla sana bila hodi, ambapo kwa kawaida ukimulika mara moja usiku, mahali hapo panabadilika unaweza ukadhani ni mchana, kwa jinsi unavyoangaza sana ..
Ndivyo Bwana Yesu alivyoifananisha na siku ya kurudi kwake kuja kulichukua kanisa, Nuru yake itamulika ulimwenguni kote kwa muda mfupi sana, ambao hakuna mwanadamu yoyote anaweza kuutazamia, na Nuru hiyo itamulika, kwa wakati mmoja ulimwenguni kote, kama vile mwanga wa radi unavyoonekana mashariki mpaka magharibi kwa wakati mmoja.
Kipindi hicho, ambacho kipo karibuni kutokea, Yesu atafunua siri ambazo, zitatuandaa moja kwa moja kwa ajili ya kwenda katika unyakuo. Na siri zenyewe hazijaandikwa hata kwenye biblia, kwasababu hakukuwa na umuhimu wa kuandikwa kwasababu, si za wakati wote, bali za wakati maalumu. Ambao ndio huo wa kurudi kwake kulinyakua kanisa lake.
Utauliza maneno hayo tumeyajulia wapi.?
Kumbuka, sikuzote, mwanga wa radi unapowaka angani, kinachofuata huwa ni Ngurumo. Hivi vitu viwili huwa vinakwenda pamoja. Sasa wakati huo ambao Kristo atakapoangaza Nuru yake ulimwenguni kote kwa kipindi kifupi sana.. Kutaambata na NGURUMO za rohoni,. Ndio zile ngurumo SABA zinazozungumziwa katika kitabu cha Ufunuo sura ya 10.
Ngurumo hizo Yohana alizisikia zikitoa sauti zao, lakini alipotaka kuziandika kwa ajili yetu sisi, alisikia sauti ikimwambia asiziandike bali azitie muhuri..Tusome.
Ufunuo 10:3 “Naye akalia kwa sauti kuu, kama simba angurumavyo. Na alipolia, zile ngurumo saba zikatoa sauti zao.
4 Hata ngurumo saba zilipotoa sauti zao, nalikuwa tayari kuandika. Nami nalisikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Yatie muhuri maneno hayo yaliyonenwa na hizo ngurumo saba, usiyaandike”.
Umeona? Hizo ni jumbe, maalumu ambazo Kristo atazifunua kwa kanisa lake safi, kwa watu maalumu siku hizi za mwisho, wakati huo ambao MWANGA huo utamulika duniani kote. Hatujui ni nini Yesu kakiandaa kwa watu wake, lakini mpaka hakijafunuliwa sasa, ni kuonyesha kuwa ni mambo ya ndani sana ya siri, ambayo hayo ndio yatampa bibi-arusi wa Kristo Imani ya kwenda katika unyakuo.
Sasa mwanga huo wa rohoni ukishamulika ulimwenguni kote, kama upo nje ya Kristo, basi ujue unyakuo utakupita tu, kwasababu hutaweza kuelewa hata Sauti ya hizo ngurumo saba zitakazonenwa ulimwenguni baada ya hapo.
Utauliza tena hilo tumelijuaje?
Ni kama tu kipindi kile cha Bwana Yesu sauti ilitoka juu mbinguni kuzungumza na makutano yaliyokuwa yanamfuata, lakini kwasababu NURU ilikuwa imeshawapita walichobakia kusikia tu ni ngurumo badala ya Sauti , ndivyo itakavyokuwa siku hiyo..
Yohana 12:28 “Baba, ulitukuze jina lako. Basi ikaja sauti kutoka mbinguni, Nimelitukuza, nami nitalitukuza tena.
29 Basi mkutano uliosimama karibu wakasikia, walisema ya kwamba kumekuwa ngurumo; wengine walisema, Malaika amesema naye.
30 Yesu akajibu, akasema, Sauti hiyo haikuwako kwa ajili yangu, bali kwa ajili yenu”.
Na ndio maana leo hii unaposisitizwa umtafute Kristo, maadamu muda mchache umebakia, wewe unachukulia mambo rahisi rahisi tu unadhani siku hiyo utaweza kuelewa kitu. Yesu alilijua hilo na ndio maana akatuambia, tujitahidi sasa kwa sababu upo wakati watu wengi watatamani waingie lakini wasiweze..wakati wenyewe ndio huo wakati wa NURU ya mwisho. Kwasababu itamulika kwa haraka sana kama vile radi, hatujui matukio hayo yatachukua muda gani pengine siku kadhaa tu, au wiki kadhaa tu, na kila kimekwisha.
Luka 13:24 “Jitahidini kuingia katika mlango ulio mwembamba, kwa maana nawaambia ya kwamba wengi watataka kuingia, wasiweze.
25 Wakati mwenye nyumba atakaposimama na kuufunga mlango, nanyi mkaanza kusimama nje na kuubisha mlango, mkisema, Ee Bwana, tufungulie; yeye atajibu na kuwaambia, Siwajui mtokako”;
Mimi sijui unasubiria nini, usiokoke, Wewe unadhani mambo yataendelea kuwa hivi milele? Hujui kuwa hii injili hadi sasa ingepaswa iwe imesharudi Israeli, maandalizi yao yapo tayari, usiku na mchana wanamlilia YEHOVA pale Yerusalemu kwenye ukuta ule wa maombolezo, kuomba warudishiwe ufalme, lakini sisi tumekaa tu tukidhani, neema hii tutakuwa nayo milele.
Ni vizuri tukajua agenda ya Mungu kwetu ni ipi sisi watu wa mataifa, inashangaza kuona mkristo anachojua ni kutabiriwa tu, na injili za kupokea, na mafanikio ya mwilini basi hana habari na mambo ya ufalme wa mbinguni. Inahuzunisha sana.
Biblia inatuambia “utimizeni wokovu wenu wenyewe kwa kuogopa na kutetemeka.
Kwa maana ndiye Mungu atendaye kazi ndani yenu”, (Wafilipi 2:12-13)
Kumbuka: UMEME na NGURUMO vipo mbioni.
Maran Atha.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
[07/11, 09:47] Justina Raphael: https://wingulamashahidi.org/2024/03/14/usiwe-mkristo-wa-kukaa-tu-ghalani/
*USIWE MKRISTO WA KUKAA TU GHALANI,*
Nakusalimu katika jina la Bwana wetu Yesu Kristo. Karibu tujifunze maneno ya uzima ya mwokozi.
Watu waliomwamini Yesu Kristo, yaani waliopokea ondoleo la dhambi zao. Hutambulika kama NGANO, lakini watu ambao bado wapo kwenye dhambi, hujulikana kama MAKAPI.
Sasa kazi ya kwanza ambayo Yesu anaifanya kwa mwamini, ni kumtenganisha yeye na makapi, kisha humweka katika ghala lake.
Mathayo 3:12 Ambaye pepeto lake li mkononi mwake, naye atausafisha sana uwanda wake; na kuikusanya ngano yake ghalani, bali makapi atayateketeza kwa moto usiozimika.
Ghalani ni uweponi mwa Mungu, yaani kutengwa na udunia.
Soma pia..Mathayo 13:29-30.
Sasa kama wewe unafahamu ukulima, unajua kabisa si mbegu zote zinawekwa ghalani kwa matumizi ya chakula, zipo nyingine, zinachukuliwa na kurudishwa shambani ili kwenda kuzalisha nyingine. Na baadaye huongeza ghala la mkulima.
Tofauti kabisa na ile inayobakia pale ghalani, itaendelea kubakia vilevile hata miaka 10, lakini ile inayokwenda shambani, ndani ya hicho kipindi cha miaka 10, yaweza kuongeza magunia mengi sana ya ngano nyingine.
Ndio maana Bwana Yesu alisema maneno haya;
Yohana 12:24 Amin, amin, nawaambia, CHEMBE YA NGANO ISIPOANGUKA KATIKA NCHI, IKAFA, HUKAA HALI IYO HIYO PEKE YAKE; BALI IKIFA, HUTOA MAZAO MENGI. 25 Yeye aipendaye nafsi yake ataiangamiza; naye aichukiaye nafsi yake katika ulimwengu huu ataisalimisha hata uzima wa milele. 26 Mtu akinitumikia, na anifuate; nami nilipo, ndipo na mtumishi wangu atakapokuwapo. Tena mtu akinitumikia, Baba atamheshimu.
Umeona hapo? Kumbe isipoanguka na kuoza basi itaendelea kubakia katika hali ile ile. Lakini ikikubali kuanguka na kuoza, ardhini, basi itachipuka kama shina, na mwisho wa siku itazaa sana.
Na hapa ndipo waamini wengi, hawataki kuingia gharama. Wanatamani wamzalie Mungu matunda, lakini hawawezi, kwasababu hawajakubali “kufa na kuoza” kwa habari ya huu ulimwengu.
Hawajakubali kuziangamiza nafsi zao kwa ajili ya Kristo. Sasa hiyo ndio inayopelekea wabakie tu kama wakristo wa ghalani,wasioweza kuzalisha chochote.
Yesu alitoa sifa za mbegu yenye kuzaa katika ule mfano wa mpanzi, akasema nyingine ziliangukia njiani, nyingine kwenye miamba, nyingine kwenye miiba, na nyingine kwenye udongo mzuri. Akasema vilizoangukia kwenye udongo mzuri ziliweza kuzaa kwa tendo moja tu la “kuvumilia”
Kuvumilia nini?
Kuvumilia dhiki, na udhia kwasababu ya Kristo, kuvumilia vishawishi vya anasa, udanganyifu wa mali, na shughuli za ulimwengu huu zilizopitiliza, lakini pia kwa unyofu wa moyo walikuwa wanalitendea kazi Neno ili walilolisikia lisiwe bure adui akaliiba ndani yao. (Luka 8:11-15). Hao ndio wakristo wasio wa ghalani, ni wakristo waliokubali kutoka nje, kumletea Bwana matunda.
Je! Na sisi tunaweza kupiga hatua nyingine? Umeokoka ndio, lakini ni lazima wokovu wako uwe na matokeo kwa wengine, uwavute na wengine kwa Kristo, kama wewe ulivyovutwa. Hivyo kubali kumaanisha kumfuata Yesu na kukaa mbali na udunia kwa kadiri uwezavyo.
Jitoe pia kwa Bwana, mali zako, zitumike kuhubiri injili, tenga fungu lako kwa Bwana, penda kusapoti kazi za Mungu, usiwe msomaji tu na kusema Amen!. Onyesha kuwa na wewe ni mtendaji kazi ili thawabu yenu iwe ni moja, na yule mtendaji kazi mwingine.
Bwana atusaidie, tutoke ghalani.
Shalom.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mafundisho
Mada Nyinginezo:
Zekaria 4:6 “Akajibu akaniambia, akisema, Hili ndilo neno la Bwana kwa Zerubabeli, kusema, Si kwa uwezo, wala si kwa nguvu, bali ni kwa roho yangu, asema Bwana wa majeshi”.
Shalom.
Yapo mambo utatumia nguvu kuyatimiza/kuyafanikisha lakini hayatatimia, vile vile yapo mambo ambayo utatumia uwezo ulionao au alionao mtu mwingine kuyatimiza lakini vile vile hayatatimia wala kufanikiwa, yatabaki kuwa changamoto kubwa sana kwako. Ukishafikia hicho kipindi/au huo wakati ni vizuri kujifunza njia nyingine sahihi na iliyo bora ya wewe kutatua matatizo yako. Na hiyo si nyingine Zaidi ya kumtumia Roho Mtakatifu.
Sasa kumtumia Roho Mtakatifu, hatumtumii kama vile tunavyotumia jina la Yesu. Hapana! Tutakuja kuona ni kwa namna gani tunamtumia Roho Mtakatifu mbele kidogo mwa somo hili, lakini sasa hebu tukisome hichi kisa ambacho kitatusaidia kuelewa vizuri kiini cha somo letu.
1Wafalme 19: 11 “Akasema, Toka, usimame mlimani mbele za Bwana. Na tazama, Bwana akapita; upepo mwingi wa nguvu ukaipasua milima, ukaivunja-vunja miamba mbele za Bwana; LAKINI BWANA HAKUWAMO KATIKA UPEPO ULE; na baada ya upepo, tetemeko la nchi; LAKINI BWANA HAKUWAMO KATIKA LILE TETEMEKO LA NCHI;
12 na baada ya tetemeko la nchi kukawa na moto; LAKINI BWANA HAKUWAMO KATIKA MOTO ULE; na BAADA YA MOTO SAUTI NDOGO, YA UTULIVU.
13 Ikawa, Eliya alipoisikia, alijifunika uso wake katika mavazi yake, akatoka, akasimama mlangoni mwa pango. Na tazama, sauti ikamjia, kusema, Unafanya nini hapa, Eliya?.
Katika hatua hizo Nne ambazo Eliya alidhani atapata suluhisho la majibu yake, tunaona ni njia moja tu ya mwisho ndio uliyompatia jibu, nyingine zote hazikuwa na msaada, ingawa zilikuwa na udhihirisho mkubwa. Tunaona katika upepo mkali Bwana hakuwepo, katika tetemeko kubwa Bwana hakuwepo, katika Moto Bwana pia hakuwepo…lakini katika Sauti Ndogo ya Utulivu ya Roho Mtakatifu ndipo Mungu alipokuwepo na akazungumza na Eliya, na kumpa suluhisho la mambo yake.
Tunaloweza kujifunza hapo ni kwamba, Sauti ya Roho Mtakatifu ndani yetu ndio suluhisho la mambo yote. Na wala si misisimko na mitikisiko na matetemeko.
Roho Mtakatifu anapokuwa ndani yako.. Ndio jibu la mafumbo yote, kwa sauti yake ya utulivu ndio inayotatua matatizo yote. Ndio maana Wakati Zerubabeli anaona ni jambo zito na gumu, kumjengea Mungu nyumba katikati ya maadui, tena jambo hilo aliliona kama Mlima Mkubwa sana mbele yake…Lakini Bwana alimwambia maneno yale…
Zekaria 4:6 “ Akajibu akaniambia, akisema, Hili ndilo neno la Bwana kwa Zerubabeli, kusema, Si kwa uwezo, wala si kwa nguvu, bali ni kwa roho yangu, asema Bwana wa majeshi.
7 Nani wewe, Ee mlima mkubwa? Mbele ya Zerubabeli utakuwa nchi tambarare; naye atalileta lile jiwe la kuwekwa juu kabisa pamoja na vigelegele vya, Neema, neema, ilikalie.”
Mlima huo Mkubwa Zerubabeli aliouona mbele yake, Bwana anasema utakuwa nchi tambarare..Lakini si kwa uwezo wala kwa nguvu, bali kwa Roho yake.
Je na wewe una mlima mkubwa mbele yako?, kiasi kwamba hujui utafanya nini?.. Suluhisho ni rahisi sana, Mpokee Roho Mtakatifu ndani yako?, huyo atakupa maelekezo sahihi ya maisha na utaona huo mlima mkubwa unageuka na kuwa nchi tambarare mbele ya macho yako. Hutahitaji kutumia nguvu nyingi kuusambaratisha huo mlima mkubwa uliopo mbele yako,bali ni vizuri utumie jitihada kumpata Roho Mtakatifu, atakayekuwezesha kulitoa tatizo lililoko mbele yako kiwepesi.
Sasa unampokeaje Roho Mtakatifu?.
Biblia imetupa jibu…
Matendo 2:37 “Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu?
38 Petro akawaambia, TUBUNI MKABATIZWE KILA MMOJA KWA JINA LAKE YESU KRISTO, MPATE ONDOLEO LA DHAMBI ZENU, NANYI MTAPOKEA KIPAWA CHA ROHO MTAKATIFU.
39 Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie”
Unapotii maagizo yake kwa kutubu, na kwenda kubatizwa katika ubatizo sahihi, hapo Roho Mtakatifu anaingia ndani yako kukutia muhumi (Waefeso 4:30)
Na Unapompokea Roho Mtakatifu na kumtii maagizo yake ndani yako, hapo ndipo umemtumia Roho Mtakatifu. Na hivyo hakuna mlima wowote utakaoweza kusimama mbele yako.
Maran atha!
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
[07/11, 09:47] Justina Raphael: https://wingulamashahidi.org/2024/03/14/usiwe-mkristo-wa-kukaa-tu-ghalani/
*USIWE MKRISTO WA KUKAA TU GHALANI,*
Nakusalimu katika jina la Bwana wetu Yesu Kristo. Karibu tujifunze maneno ya uzima ya mwokozi.
Watu waliomwamini Yesu Kristo, yaani waliopokea ondoleo la dhambi zao. Hutambulika kama NGANO, lakini watu ambao bado wapo kwenye dhambi, hujulikana kama MAKAPI.
Sasa kazi ya kwanza ambayo Yesu anaifanya kwa mwamini, ni kumtenganisha yeye na makapi, kisha humweka katika ghala lake.
Mathayo 3:12 Ambaye pepeto lake li mkononi mwake, naye atausafisha sana uwanda wake; na kuikusanya ngano yake ghalani, bali makapi atayateketeza kwa moto usiozimika.
Ghalani ni uweponi mwa Mungu, yaani kutengwa na udunia.
Soma pia..Mathayo 13:29-30.
Sasa kama wewe unafahamu ukulima, unajua kabisa si mbegu zote zinawekwa ghalani kwa matumizi ya chakula, zipo nyingine, zinachukuliwa na kurudishwa shambani ili kwenda kuzalisha nyingine. Na baadaye huongeza ghala la mkulima.
Tofauti kabisa na ile inayobakia pale ghalani, itaendelea kubakia vilevile hata miaka 10, lakini ile inayokwenda shambani, ndani ya hicho kipindi cha miaka 10, yaweza kuongeza magunia mengi sana ya ngano nyingine.
Ndio maana Bwana Yesu alisema maneno haya;
Yohana 12:24 Amin, amin, nawaambia, CHEMBE YA NGANO ISIPOANGUKA KATIKA NCHI, IKAFA, HUKAA HALI IYO HIYO PEKE YAKE; BALI IKIFA, HUTOA MAZAO MENGI. 25 Yeye aipendaye nafsi yake ataiangamiza; naye aichukiaye nafsi yake katika ulimwengu huu ataisalimisha hata uzima wa milele. 26 Mtu akinitumikia, na anifuate; nami nilipo, ndipo na mtumishi wangu atakapokuwapo. Tena mtu akinitumikia, Baba atamheshimu.
Umeona hapo? Kumbe isipoanguka na kuoza basi itaendelea kubakia katika hali ile ile. Lakini ikikubali kuanguka na kuoza, ardhini, basi itachipuka kama shina, na mwisho wa siku itazaa sana.
Na hapa ndipo waamini wengi, hawataki kuingia gharama. Wanatamani wamzalie Mungu matunda, lakini hawawezi, kwasababu hawajakubali “kufa na kuoza” kwa habari ya huu ulimwengu.
Hawajakubali kuziangamiza nafsi zao kwa ajili ya Kristo. Sasa hiyo ndio inayopelekea wabakie tu kama wakristo wa ghalani,wasioweza kuzalisha chochote.
Yesu alitoa sifa za mbegu yenye kuzaa katika ule mfano wa mpanzi, akasema nyingine ziliangukia njiani, nyingine kwenye miamba, nyingine kwenye miiba, na nyingine kwenye udongo mzuri. Akasema vilizoangukia kwenye udongo mzuri ziliweza kuzaa kwa tendo moja tu la “kuvumilia”
Kuvumilia nini?
Kuvumilia dhiki, na udhia kwasababu ya Kristo, kuvumilia vishawishi vya anasa, udanganyifu wa mali, na shughuli za ulimwengu huu zilizopitiliza, lakini pia kwa unyofu wa moyo walikuwa wanalitendea kazi Neno ili walilolisikia lisiwe bure adui akaliiba ndani yao. (Luka 8:11-15). Hao ndio wakristo wasio wa ghalani, ni wakristo waliokubali kutoka nje, kumletea Bwana matunda.
Je! Na sisi tunaweza kupiga hatua nyingine? Umeokoka ndio, lakini ni lazima wokovu wako uwe na matokeo kwa wengine, uwavute na wengine kwa Kristo, kama wewe ulivyovutwa. Hivyo kubali kumaanisha kumfuata Yesu na kukaa mbali na udunia kwa kadiri uwezavyo.
Jitoe pia kwa Bwana, mali zako, zitumike kuhubiri injili, tenga fungu lako kwa Bwana, penda kusapoti kazi za Mungu, usiwe msomaji tu na kusema Amen!. Onyesha kuwa na wewe ni mtendaji kazi ili thawabu yenu iwe ni moja, na yule mtendaji kazi mwingine.
Bwana atusaidie, tutoke ghalani.
Shalom.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mafundisho
Mada Nyinginezo:
Mlima Gerizimu na Ebali ni ipi, na umuhimu wao rohoni ni upi?
Kama wakitenda mambo haya katika mti mbichi, itakuwaje katika mkavu?
Kama wakitenda mambo haya katika mti mbichi, itakuwaje katika mkavu?
Jina la Bwana wetu Yesu Kristo libarikiwe.
Umewahi kujiuliza kwanini Yesu anajulikana kama Adamu wa Pili au Adamu wa mwisho?
Leo tutajifunza ni kwanini yeye anajulikana hivyo, na kwa kujua huko kutatupa msingi wa kumwelewa Mwana wa Mungu kwa viwango vingine..kama maandiko yanavyosema katika Waefeso 4:13
Waefeso 4:13 “hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani na KUMFAHAMU SANA MWANA WA MUNGU, HATA KUWA MTU MKAMILIFU, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo”
Sasa siri ya Yesu kufananishwa na Adamu ya mwisho, mtu wa kwanza kufunuliwa alikuwa ni Mtume Paulo, hebu tusome kidogo…
1Wakorintho 15:45 “Ndivyo ilivyoandikwa, Mtu wa kwanza, Adamu, akawa nafsi iliyo hai; ADAMU WA MWISHO NI ROHO YENYE KUHUISHA.
46 Lakini hautangulii ule wa roho, bali ule wa asili; baadaye huja ule wa roho.
47 Mtu wa kwanza atoka katika nchi, ni wa udongo. Mtu wa pili atoka mbinguni”
Huyo ni Bwana Yesu, mtume Paulo anayemzungumzia hapo.
Sasa ili tumwelewe Adamu wa Mwisho, tabia zake zitakavyokuwa, hebu tumsome kwanza huyu Adamu wa kwanza, alivyokuwa.
Kama wengi wetu tujuavyo Adamu ndiye mtu wa kwanza kuumbwa, na akapewa mamlaka juu ya vitu vyote vya ulimwengu, kwamba akatawale na kuvitiisha chini yake. Na ahadi hiyo hakupewa Adamu peke yake, bali na uzao wake wote, kwasababu sisi wote tulikuwa tumeshaumbwa katika viuno vya Adamu. (tulikuwa kama mbegu tu ambazo bado hazijapandwa). Hivyo Adamu na uzao wake wote ndio walioahidiwa kumiliki na kutawala kila kitu kilichopo chini ya mbingu. (Mwanzo 1:26).
Lakini kama tunavyojua, Adamu alianguka na kupoteza mamlaka yale, akaiuza haki yake ya Umamlaka na kumpa shetani, (ndio maana shetani kuanzia huo wakati akaitwa mkuu wa ulimwengu), hapo kwanza hakuwa hivyo, Adamu ndiye aliyekuwa mkuu wa ulimwengu. Na anguko la Adamu lilisababisha na sisi wote kuanguka kwasababu tulikuwa tupo katika viuno vya Adamu. Hivyo na sisi wote tutakaozaliwa baadaye tutakuwa hatuna mamlaka yoyote, kwasababu Baba yetu Adamu, alishayapoteza.
Hivyo kama si rehema za Mungu na huruma zake, tungekuwa tumeshafutwa kitambo na pengine Mungu angeshaanza uumbaji mwingine. Lakini kwasababu alituhurumia..Ikambidi amlete Adamu mwingine wa pili, kwasababu Adamu wa kwanza kashaharibu….huyu Adamu mwingine hatakuja kwa lengo la kuzaliana. Maana kama angekuja kwa lengo la kuzaliana, ingempasa na yeye awe na Hawa wake na kuzaa vizazi vipya duniani, visivyo na dhambi ambavyo ndivyo vitapewa urithi. Lakini huyu Adamu wa pili hakuletwa duniani kwa kusudi hilo, bali kwa kusudi la kukomboa, Maana yake ni kwamba, hatazaa watu wengine bali vile vile vizazi vya Adamu anavikomboa na kuvifanya uzao wake!.
Sasa anavikomboaje?. Ndio hapo alisema maneno yafuatayo…
Yohana 3:3 “Yesu akajibu, akamwambia, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu.
4 Nikodemo akamwambia, Awezaje mtu kuzaliwa, akiwa mzee? Aweza kuingia tumboni mwa mamaye mara ya pili akazaliwa?
5 Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu.
6 Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni roho.
7 Usistaajabu kwa kuwa nilikuambia, Hamna budi kuzaliwa mara ya pili”.
Hapo katika mstari wa 6 anasema, kilichozaliwa kwa Mwili ni mwili, maana yake Adamu wa kwanza ndiye aliyetuzaa sisi kimwili, lakini kuzaliwa kwa roho hatuna budi kuzaliwa na huyu Adamu wa pili (Yesu Kristo), kwasababu yeye ndiye anayetuzaa katika roho na si katika mwili kama Adamu baba yetu wa kwanza.
1Wakorintho 15:45 “Ndivyo ilivyoandikwa, Mtu wa kwanza, Adamu, akawa nafsi iliyo hai; ADAMU WA MWISHO NI ROHO YENYE KUHUISHA”.
Kwahiyo kama yule Adamu wa kwanza alivyokabidhiwa mamlaka yote ya duniani na Mungu, kadhalika na huyu Adamu wa pili alikabidhiwa mamlaka yote ya duniani, na si tu ya duniani, bali hata mbinguni.
Mathayo 11:27 “Akasema, Nimekabidhiwa vyote na baba yangu;……..”
Mathayo 28:18 “Yesu akaja kwao, akasema nao, akawaambia, NIMEPEWA MAMLAKA YOTE MBINGUNI NA DUNIANI”
Umeona? Hapo…Nguvu alizonazo Yesu. Si kama watu wanavyomdhania!
Na kama vile Adamu wa kwanza alivyopewa mamlaka hayo pamoja na uzao wake wa kimwili, kadhalika Adamu wa pili Yesu Kristo, mamlaka hayo alikabidhiwa pamoja na uzao wake wote katika roho, maana yake wote watakaozaliwa mara ya pili katika roho, wanakuwa uzao wake na wanakuwa wanarithi Baraka zote alizokabidhiwa Bwana Yesu na Baba.
Warumi 8:16 “Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu
17 na kama tu watoto, BASI, TU WARITHI; WARITHI WA MUNGU, WARITHIO PAMOJA NA KRISTO; naam, tukiteswa pamoja naye ili tupate na kutukuzwa pamoja naye”
Haiishii hapo!!..Kama vile Adamu wa kwanza alivyowasababishia wazao wake wote kuingia kwenye matatizo baada ya kuasi kwake, na hata wale wasio na hatia wakajikuta wanazaliwa katika laana. Kadhalika Adamu wa pili (Yesu Kristo), atauingiza uzao wake wote aliouzaa katika roho, katika hali ya kubarikiwa daima, kwa maana hatatenda dhambi. Umeona umuhimu wa kuzaliwa mara ya pili katika roho???..
Warumi 5:17 “Kwa maana ikiwa kwa kukosa mtu mmoja mauti ilitawala kwa sababu ya yule mmoja, zaidi sana wao wapokeao wingi wa neema, na kile kipawa cha haki, watatawala katika uzima kwa yule mmoja, YESU KRISTO.
18 Basi tena, kama kwa kosa moja watu wote walihukumiwa adhabu, kadhalika kwa tendo moja la haki watu wote walihesabiwa haki yenye uzima.
19 Kwa sababu kama kwa kuasi kwake mtu mmoja watu wengi waliingizwa katika hali ya wenye dhambi, kadhalika kwa kutii kwake mmoja watu wengi wameingizwa katika hali ya wenye haki”
Umeona ni jinsi gani, Mkuu wa Uzima Yesu Kristo, biblia inavyomfunua kama Adamu wa pili?.
Kumbuka wote waliozaliwa mara ya pili katika roho hao ndio wa uzao wa Yesu Kristo, na ni lazima kila mtu azaliwe mara ya pili kwa mbegu isiyoharibika ya Yesu Kristo ili aweze kuuona ufalme wa mbinguni kama yeye mwenyewe alivyosema. Mbegu ya Adamu imeshaharibika, ndio maana tunaumwa, tunakufa, tunateseka, tunarithi mauti n.k.
Lakini tunapozaliwa katika mbegu isiyoharibika ya Yesu Kristo, mauti, shida, dhiki, magonjwa yote yanakuwa yamekwisha… Na yatakwisha kikabisa kabisa wakati wa ukombozi wa miili yetu, utakaokuja siku ile ya unyakuo, tutakapovikwa miili ya utukufu. (Waefeso 4:30).
1Petro 1:23 “Kwa kuwa mmezaliwa mara ya pili; si kwa mbegu iharibikayo, bali kwa ile isiyoharibika; kwa neno la Mungu lenye uzima, lidumulo hata milele”.
Je umezaliwa mara ya pili?..
Kama bado unasubiri nini?..Hakuna tumaini lolote katika Uzao wa Adamu wa kwanza… yeye kashaharibu mambo yote, hana mamlaka tena…Mamlaka yote kwasasa yapo kwa huyu Adamu wa Pili Yesu Kristo. Na unaingia katika uzao wake kwa kuzaliwa mara ya pili…maana yake kwa kutubu dhambi zako zote na kubatizwa katika ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa jina la Yesu Kristo na kupokea Roho Mtakatifu (Matendo 2:38),. Hapo utakuwa umezaliwa kwa maji na kwa Roho,.
Na utakuwa umeingizwa katika uzao wa Yesu Kristo.
Bwana Mkuu, anayemiliki mbinguni na duniani, Adamu wa mwisho, aliyeshinda mauti na shida akubariki.
+255693036618/ +255789001312
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > WHATSAPP-Group
Mada Nyinginezo:
Nakusalimu katika jina lipitalo majina yote la Bwana wetu Yesu Kristo, karibu tuyatafakari maneno ya uzima maadamu bado tupo hai. Maandiko yanatuambia ;
Yohana 19:25 “Na penye msalaba wake Yesu walikuwa wamesimama mamaye, na umbu la mamaye, Mariamu wa Klopa, na Mariamu Magdalene.
26 Basi Yesu alipomwona mama yake, na yule mwanafunzi aliyempenda amesimama karibu, alimwambia mama yake, Mama, tazama, mwanao.
27 Kisha akamwambia yule mwanafunzi, Tazama, mama yako. Na tangu saa ile mwanafunzi yule akamchukua nyumbani kwake.”.
Unaweza ukajiuliza ni kwanini Bwana Yesu atengeneze mahusiano ya namna ile pale msalabani na sehemu nyingine yoyote. Bila shaka kulikuwa na watu wengi pale msalabani wakimtazama, walikuwepo wanawake wengi, vilevile walikuwepo wanafunzi wake wengine hata kama hawajaorodheshwa lakini utaona macho ya Bwana yaliwaelekea hao watu wawili tu. Mmoja ni mama yake, na mwingine ni yule mwanafunzi aliyempenda, ambaye ni mtume Yohana.
Jaribu kufikiria Bwana Yesu alikuwa na wadogo zake wengine wengi lakini hakuna hata mmoja aliyemkabidhisha mama yake, halikadhalika alikuwa na mitume wengi lakini hakuna hata mmojawao aliyemkabidhi mama yake. Vilevile Yohana alikuwa na mama yake mzazi, lakini Yesu hakumwambia amtazame mama yake, kinyume chake alimwambia amtazame Mariamu mama wa Bwana wake. Na wakati huo huo biblia inatuambia Yohana aliposikia maagizo hayo akamchukua na kumpeleka kwake kuishi naye.
Mahusiano ya namna hiyo, ya mtu kumtunza mama asiye mama yake, na mwingine kumwita mwanangu, asiye mwana wake, hayaji hivi hivi bali yanatoka kwa Kristo tu, kwa kumwangalia yeye peke yake. Sisi kama kanisa la Kristo hatuwezi kupendana, wala kuchukuliana kama ndugu, kama macho yetu hayatamwelekea Kristo aliyesulibiwa.
Tukiwa ni watu wa kumtazama yule Kristo wa mikate tu, kamwe mahusiano kama haya tusahau kuyaona katikati yetu, kama tutakuwa tunakwenda kumtafuta Kristo kanisani kwasababu ya biashara zetu tu, ili mambo yaende vizuri na wala si kingine, basi tutakuwa tunakusanyika bure, na baada ya hapo kila mmoja ataendelea na mambo yake mwenyewe, kama walivyofanya wale makutano waliokuwa yanamfuata Yesu kila mahali, kwa ajili ya uponyaji tu na vitu vya mwilini utagundua hakuna hata mmoja aliyemjua mwenzake, anakarama gani, japokuwa walikuwa maelfu kwa maelfu wamekutanika pamoja.
Vilevile leo tunaweza tukawa na idadi kama hiyo makanisani, lakini kama tutakosa umoja na upendo, na mshikamano, kamwe hatutaweza kuwa na nguvu ya kumwona Mungu. Kama tusipomwangalia Kristo katika ule msalaba wake, kamwe hatutakaa tupendane.
Bwana Yesu alisema..
Yohana 13:34 “Amri mpya nawapa, Mpendane. Kama vile nilivyowapenda ninyi, nanyi mpendane vivyo hivyo.
35 Hivyo watu wote watatambua ya kuwa ninyi mmekuwa wanafunzi wangu, mkiwa na upendo ninyi kwa ninyi”.
Bwana Yesu hafurahii, kuona tunasema sisi ni wakristo na huku, hatupendani sisi kwa sisi, kila mmoja anavita na mwenzake, anakinyongo na mwenzake, anajijali yeye tu, na huku wote mpo katika kanisa moja. Hiyo ni ishara kuwa hatujafika Goligotha na kumsikia Kristo anasema nini kwa ndugu zake.
Na mahusiano yale, ambayo Kristo aliyatengeneza kwa Mariamu na Yohana, hayakuwa ya bure bure tu, yalikuwa na faida nyingi sana kwa wote wawili. Kwanza Mariamu hakujiona tena mpweke , baada ya kuondokewa na mtoto wake, kwani alimpata mtu aliyemjali kama Yesu mwenyewe, pili, Yohana, alifahamu mambo mengine yamuhusuyo Yesu kupitia Mariamu ambayo pengine alikuwa hayajui kabla, ikumbukwe kuwa mitume walimjua Yesu kwa miaka mitatu na nusu tu, lakini nyuma ya hapo miaka yote 30 walikuwa hawajui chochote, siri ya Maisha yake zilikuwa kwa Mariamu mama yake.
Mariamu ni mwanamke ambaye aliyaweka mambo mengi sana ya Yesu moyoni, alikuwa si mtu wa kuchukulia mambo kawaida kawaida, au juu juu tu soma Luka 2:19
Hivyo ni wazi kuwa Yohana kwa kupitia Mariamu alipata kujua na mambo mengine ya ndani kumuhusu Kristo sikuzote alizokuwa anamtunza, tofauti na mitume wengine, na ndio maana utamwona Yohana, akitokewa tena na Kristo akionyeshwa maono yale makubwa sana na siri nyingine kati ya hizo aliambiwa asiziandike, alipokuwa kule Patmo, akiandika kitabu cha Ufunuo.
Vivyo hivyo na sisi, tunaweza vunjika mioyo kwa mambo mengi humu ulimwenguni, tunaweza kosa tumaini, lakini Kristo akatupa ndugu ambao watakuwa faraja yetu, Zaidi hata ya ndugu wengi tulionao, tunaweza tukawa hatujamjua Kristo vizuri, lakini yeye mwenyewe akatupa watu watakaotusaidia kumwelewa yeye kwa vizuri zaidi, kuliko hata waliotutangulia . Lakini hiyo yote haiji hivi hivi, bali inakuja kwa kumtazama Kristo aliyemsalabani.
Maana yake ni kuwa kwa kuyatafakari yale mateso pale msalabani, kwa jinsi alivyokufa kwa ajili yetu sisi tusiostahili, itatufanya na sisi kila siku, tujitoe kwa ndugu zetu wengine.
Hivyo na wewe pia fahamu kuwa katika kanisa lako, Kristo anavutiwa na Umoja wako, na Upendo wako kwa wakristo wenzako.
Bwana akubariki.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mafundisho
Mada Nyinginezo:
JIBU: Kwanza ni muhimu kufahamu nini maana ya neno “kuabudu”. Leo hii ukizungumzia neno kuabudu, haraka haraka katika vichwa vya wengi, italenga katika “kuimba nyimbo za kuabudu”. Lakini kiuhalisia kumuabudu Mungu sio kuimba nyimbo za kuabudu. Bali neno “kuabudu”, limetokana na neno “Ibada”. Kwahiyo “kufanya ibada” ndio “kuabudu”. Kwa urefu juu ya kuabudu unaweza kufungua hapa >> Kuabudu ni nini?
Mtu anayefanya ibada za mashetani, hapo anaabudu mashetani, kadhalika mtu anayefanya ibada kwa Mungu wa mbingu na nchi, hapo anamwabudu Mungu wa mbingu na nchi. Hizo nyimbo zinazokuja za kumsifu Mungu na kumwimbia wakati wa ibada, ndio zinazoitwa Nyimbo za kuabudu.
Kwamsingi huo basi, Neno la Mungu linasema katika..
Yohana 4:23 “Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika ROHO NA KWELI. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu.
24 Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.”
Maana yake ni kwamba, saa inakuja ambayo watu watakaomfanyia Mungu ibada, na ibada hiyo wataifanya katika roho na kweli.
Sasa nini maana ya… “katika roho na kweli” ?
Tusome.
Yohana 16:12 “ Hata bado nikali ninayo mengi ya kuwaambia, lakini hamwezi kuyastahimili hivi sasa.
13 Lakini yeye atakapokuja, HUYO ROHO WA KWELI, atawaongoza AWATIE KWENYE KWELI YOTE; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake”
Hapo anasema Roho Mtakatifu atakapokuja atatuongoza atutie katika kweli yote. Hivyo tukishampokea Roho Mtakatifu ndani yetu, na huyo Roho akatuongoza na kututia kweli yote, na baada ya kuipata hiyo kweli, tukaenda tukafanya ibada katika hiyo kweli, tuliyoipata kutoka kwa Roho Mtakifu aliye ndani yetu, basi hapo tutakuwa tumemwabudu Mungu katika “Roho na kweli”.
Kwahiyo kumwambudu Baba katika Roho na Kweli ni kufanya ibadaa huku tukiwa tumempokea Roho Mtakatifu na kweli ipo ndani yatu.
Sasa kweli ni nini?
Biblia imetupa jibu katika kitabu cha Yohana..
Yohana 17:16 “Wao si wa ulimwengu, kama mimi nisivyo wa ulimwengu.
17 Uwatakase kwa ile kweli; NENO LAKO NDIYO KWELI.”
Umeona hapo?. Neno la Mungu ndio “kweli”. Kwahiyo kumwabudu Baba katika roho na kweli, ni “kumfanyia Mungu ibada katika Roho Mtakatifu na katika Neno lake”.
Je wewe leo unamwabudu Mungu katika Roho na Kweli?. Fahamu huwezi kuijua kweli kama hauna Roho Mtakatifu ndani yako, na biblia inasema wote wasio na Roho Mtakatifu hao sio wake (Warumi 8:9).
Hivyo ni lazima kumpokea Roho Mtakatifu kwanza ndipo, aweze kukuongoza katika kweli yote. Si ajabu leo watu hawawezi kulielewa Neno kwasababu Hawana Roho ndani yao, ndio maana utaona mtu anakwenda kumfanyia Mungu ibada kanisani, huku yupo nusu tupu, kava kimini, au suruali, au kavaa hereni, au kanyoa kama jogoo na wala hasikii kuhukumiwa ndani yake. Ni kwanini?. Ni kwasababu hana Roho Mtakatifu ndani yake ambaye angeugua ndani yake kumshuhudia hicho anachofanya sio sahihi, na kumwongoza katika Kweli yote.
Hivyo Roho Mtakatifu ni muhimu na ni ahadi kwa kila mwamini aliyempokea Yesu (Matendo 2:38), Na kumpokea Roho Mtakatifu sio kunena kwa lugha!.. Lugha sio ishara pekee ya Mtu aliyempokea Roho Mtakatifu, Mtu anaweza asinene kwa lugha na bado akawa amempokea Roho Mtakatifu, na pia mtu anaweza kunena kwa lugha na asiwe na Roho Mtakatifu bali ni roho nyingine. (Kama utahitaji kufahamu zaidi juu ya Roho Mtakatifu na uthibitisho wake basi unaweza kutujuza inbox, au kwa namba hizi 0789001312/0693036618).
Kumbuka hizi ni siku za mwisho, Kristo yupo mlangoni anabisha mioyoni mwa wengi, wakati wowote parapanda ya mwisho italia, na wafu watafufuka, wale waliokufa katika Bwana, wataungana na wale walio hai, walio na Roho Mtakatifu, na kwa pamoja watakwenda mawinguni katika karamu ya mwanakondoo..
Je utakuwa wapi siku hiyo?
Bwana akubariki.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mafundisho
Mada Nyinginezo:
Kibiblia Naivera imemaanisha vitu viwili, cha kwanza, ni aina ya vazi maalumu lililotengenezwa kwa mfano wa Aproni(yale mavazi ya wapishi) kwa ajili ya ibada za kikuhani, au kwa ajili ya kujisogeza mbele za Mungu.
Kwamfano, Mungu alimuagiza Musa, atengeneza mavazi ya kikuhani, kwa ajili ya Haruni, na watoto wake, na mojawapo ya vazi hilo ilikuwa ni hiyo Naivera, Unaweza kutazama picha juu
Kutoka 28:4 “Na mavazi watakayoyafanya ni haya; kifuko cha kifuani, na naivera, na joho, na kanzu ya kazi ya urembo; na kilemba, na mshipi; nao watawafanyia Haruni nduguyo, na wanawe, mavazi matakatifu ili anitumikie katika kazi ya ukuhani”.
Ukisoma pia Kutoka 28:6-14, utaona inatoa maelezo hayo kwa urefu jinsi vazi hilo linavyopaswa kuundwa.
Nabii Samweli pia aliivaa Naivera, alipokuwa akitumika hemani pa Bwana.
1Samweli 2:18 “Lakini Samweli alikuwa akitumika mbele za Bwana, naye alikuwa kijana, mwenye kuvaa naivera ya kitani”.
Lakini utaona pia baadaye Naivera, ilikuja kuvaliwa na watu ambao hawakuwa makuhani, kama vile Daudi, sehemu mowajawapo ni wakati ule analitoa sanduku la agano kutoka katika nyumba ya Obed-edomu, mpaka mjini pake, siku ambayo alimchezea Mungu, mpaka nguo zikamtoka, alikuwa amevaa Naivera.
2Samweli 6:13 “Hata ikawa, watu waliolichukua sanduku la Bwana walipokwisha kwenda hatua sita, akachinja ng’ombe na kinono.
14 Daudi akacheza mbele za Bwana kwa nguvu zake zote; na Daudi alikuwa amevaa naivera ya kitani.
15 Basi Daudi na nyumba yote ya Israeli wakalileta sanduku la Bwana kwa shangwe, na kwa sauti ya tarumbeta”.
Jambo hilo hilo utalisoma pia katika 1Nyakati 15:26-28
“26 hata ikawa, Mungu alipowajalia Walawi waliolichukua sanduku la agano la Bwana, wakachinja ng’ombe saba, na kondoo waume saba.
27 Naye Daudi alikuwa amevaa joho ya kitani safi, na Walawi wote waliolichukua sanduku, na waimbaji, na Kenania msimamizi wa uchukuzi, na waimbaji; naye Daudi alikuwa amevaa naivera ya kitani.
28 Ndivyo Israeli wote walivyolipandisha sanduku la agano la Bwana kwa shangwe na kwa sauti ya tarumbeta, na kwa baragumu, na kwa matoazi, wakipiga sauti kuu kwa vinanda na vinubi.
Na si hapo tu utaona wakati mwingine, Daudi alipokuwa akikimbizwa na adui yake Sauli, alipofika kwa yule kuhani aliyeitwa Abiathari aliichukua ile Naivera iliyokuwa mkononi mwake akaivaa ndipo akamuuliza Mungu juu ya hatma yake,
Soma 1Samweli 23:6-12, utaipata habari hiyo.
Pia wakati mwingine ni pale alipokuwa anawafukizia maadui zake waliochukua mateka vitu vyao na wake zao utaona Daudi alifanya jambo hilo hilo kumuuliza Mungu, kwa njia hiyo hiyo ya kuivaa Naivera. (Soma 1Samweli 20:7-8)
Hivyo Naivera lilikuwa ni vazi maalumu lililotumika kwa ajili ya kumkaribia Mungu, au kuuliza kwa Mungu.
Pili Naivera, katika biblia inatajawa kama vitu cha kuabudiwa, mfano wa kinyago Fulani,.
Katika maandiko utaona kuna wakati Gideoni, aliwaagiza wana wa Israeli watoe vitu vyao vya thamani, ili kuiunda, jambo ambalo lilikuwa kikwazo kwake na kwa Israeli nzima.
Waamuzi 8:25 “Wakajibu, Tutakupa kwa mioyo. Basi wakatandika nguo chini, wakatia humo kila mtu pete za masikio ya mateka yake.
26 Na uzani wa hizo pete za dhahabu alizozitaka ulipata shekeli za dhahabu elfu moja na mia saba; mbali na makoja na vidani, na mavazi ya rangi ya zambarau waliyokuwa wameyavaa hao wafalme wa Midiani, tena mbali na mikufu iliyokuwa katika shingo za ngamia zao.
27 BASI GIDEONI AKAFANYA NAIVERA KWA VITU VILE, AKAIWEKA KATIKA MJI WAKE, mji huo wa Ofra; nao Israeli wote wakaenda na kuiandama kwa ukahaba huko; nayo ilikuwa ni tanzi kwa Gideoni na kwa nyumba yake”.
Je! Na sisi leo hii tunapaswa tuvae Naivera kila tunapomkaribia Mungu, kama walivyofanya watu wa agano la kale?.
Jibu ni hapana, Naivera yetu kwasasa ni Kristo tu, ukiwa na Kristo moyoni mwako, tayari ni vazi tosha la kukusogeza mbele za Mungu kuliko vazi lingine lolote unaloweza kulivaa katika mwili. Lakini Kristo hawezi kuwa vazi lako, ikiwa hujatubu kwa kumaanisha kabisa kuacha dhambi zako na kubatizwa, na kuishi Maisha ya utakatifu yanayompendeza hapa duniani.
Hivyo tubu dhambi zako mgeukie Bwana Yesu naye atakuokoa, kumbuka yeye mwenyewe alisema maneno haya;
Ufunuo 16:15 “(Tazama, naja kama mwivi. Heri akeshaye, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake.)