Tusome,
Zaburi 89:48 “Ni mwanamume gani atakayeishi asione mauti, Atakayejiokoa nafsi yake na mkono wa kuzimu?”
Awali ya yote ni vizuri kufahamu kuwa Mwandishi aliyeandika maneno haya, alikuwa katika mazingira gani, Mwandishi alikuwa katika mazingira ya Sala (yaani kuomba) na si kuhubiri au kutoa mahusia kama Zaburi nyingine. Kuna maneno ya kuzungumza na Mungu na ya kuzungumza na Watu.
Tunapozungumza na Mungu katika sala, ni kawaida yetu kujishusha..huwezi kujiinua mbele za Mungu kwamba wewe unafaa, hata kama kweli unafaa, huwezi kusema wewe unastahili hata kama kweli unastahili, ni lazima uwe si kitu mbele za Mungu. (Soma Luka 18:11-14).
Vile vile Mwandishi alikuwa anamjua HENOKO mtu wa Saba, baada ya Adamu, ambaye hakuonja mauti, bali alitwaliwa na Mungu bila kufa!.
Hivyo kama angekuwa amemaanisha kuwa kila mtu ni lazima afe, basi atakuwa amesema uongo, maana anamjua Henoko kwamba hakufa. (Na biblia sio kitabu cha uongo!)
Kwahiyo maana yake ni kwamba, Mwandishi hakumaanisha kama watu leo wanavyoutafsiri huo mstari, kwamba kila mtu ni lazima afe, bali alisema vile akiwa na maana nyingine kabisa.
Zaburi hiyo ya 89, yote ni Zaburi ya sala ya unyenyekevu, ambapo mwandishi anasali huku akimwinua Mungu, na kujishusha yeye.. na si Zaburi ya mahubiri wala maonyo!, ndio maana ukianzia mstari wa juu kidogo utaona anasema..
“46 Ee Bwana, hata lini? Utajificha hata milele? Ghadhabu yako itawaka kama moto?
47 Ukumbuke jinsi mimi nisivyo wa kudumu; Kwa ubatili gani umeiumba jamii ya wanadamu!
48 Ni mwanamume gani atakayeishi asione mauti, Atakayejiokoa nafsi yake na mkono wa kuzimu?”
Sasa ili tuelewe vizuri, hebu chukua mfano umsikie mtu aliye mgonjwa sana anaomba hivi.. “Ebwani nisaidie mimi niliye mdhaifu, niliye karibia na kufa, ni mwanadamu gani leo hii anaweza kuishi bila kufa?”
Bila shaka kwa kuomba huko, atakuwa hajamaanisha kuwa hakuna mtu anaweza kuishi bila kufa!, bali amemaanisha kuwa yeye ni mdhaifu, na wanadamu wote ni wadhaifu na hakuna mtu anaweza kuishi bila kufa kwa nguvu zake na uwezo wake mwenyewe”.
Ndicho mwandishi alichokuwa anakimaanisha hapo?..
Alikuwa katika sala, kuzungumza na Mungu na hivyo kujionyesha kuwa yeye ni mavumbi tu, na wanadamu wote tu mavumbi tu, na ni dhaifu, ndio ikamfanya aombe sala ya namna hiyo ya unyenyekevu, lakini Hakuwa anatoa mahubiri au mafundisho, au mashauri kwa watu kuwa kila mtu ni lazima afe, bali alikuwa katika sala!, anamweleza Mungu na si mwanadamu!..kuonesha ishara ya kujishusha na unyenyekevu mbele za Mungu.
Kwahiyo kwa hitimisho Si kila mtu atakufa!, Henoko hakufa, Nabii Eliya hakufa, kadhalika kuna watu watanyakuliwa wakiwa hai wakati Bwana Yesu atakapokuja mara ya pili (kwenye tukio maarufu lijulikanalo kama unyakuo).
1Wakorintho 15:51 “Angalieni, nawaambia ninyi siri; HATUTALALA SOTE, lakini sote tutabadilika,
52 kwa dakika moja, kufumba na kufumbua, wakati wa parapanda ya mwisho; maana parapanda italia, na wafu watafufuliwa, wasiwe na uharibifu, nasi tutabadilika”.
Hapo anasema “hatutalala sote” maana yake “hatutakufa wote”..Unyakuo utawakuta wengine wakiwa hai, hivyo watakuwa hawajakionja kifo, na vile vile katika maandiko hakuna mahali popote panaposema kuwa kila nafsi itaonja mauti, msemo huo ni maarufu sana lakini kiuhalisia haupo katika biblia.
Lakini kufa si hoja, au kutokufa.. Hoja ni je! Tutakuwa wapi baada ya kifo, au siku ile ya unyakuo itatukutaje?, kama tukifa katika dhambi basi tutangamia milele katika lile ziwa la moto, lakini kama tukifa katika Kristo tutadumu milele Pamoja na Bwana. Vile vile kama tukiwa hai ndani ya Kristo mpaka unyakuo utakapofika basi tutanyakuliwa na kwenda naye mawinguni, lakini kama unyakuo ukitukuta huku tuko nje ya Kristo, basi tutabaki hapa katika dhiki kuu ya Mpinga Kristo.
Na Unyakuo wa kanisa ni siku yoyote! Na wakati wowote!.. Je umejiandaaje?, umempokea Kristo na kubatizwa na kumpokea Roho Mtakatifu ndani yako?
Bwana yu karibu!
Maran atha!
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Mada Nyinginezo:
Biblia inamaana gani inaposema “Wewe uchukiaye sanamu, wateka mahekalu?”
Katika maandiko tunasoma kwamba Mungu alimshuhudia Musa kuwa ndiye mtu mpole kuliko watu wote duniani, lakini tunaona huyo Musa mbeleni (katika Hesabu 31:15) anakuja kuonekana kama mkatili sana?, hapo sijaelewa!.
Tusome,
Hesabu 31:14 “Musa akawakasirikia majemadari wa jeshi, na hao maakida wa elfu elfu, na wakuu wa mia mia, hao waliorudi kutoka katika kupiga vita.
15 MUSA AKAWAULIZA, JE! MMEWAPONYA WANAWAKE WOTE HAI?
16 Tazama, hawa ndio waliowakosesha wana wa Israeli, kwa shauri la Balaamu, wamfanyie Bwana dhambi katika hilo jambo la Peori, na kwa hivyo pigo lilikuwa katika mkutano wa Bwana.
17 Basi KWA AJILI HIYO MWUENI KILA MUME KATIKA HAO WATOTO, na kila mwanamke aliyemjua mume kwa kulala pamoja naye”.
Tusome tena..
Hesabu 12:3 “Basi huyo mtu, huyo Musa, alikuwa mpole sana zaidi ya wanadamu wote waliokuwa juu ya uso wa nchi”.
Bwana Mungu hawezi kusema uongo, ni kweli Musa alikuwa mtu mpole kuliko watu wote duniani, lakini hakuzaliwa hivyo, maandiko yanatuambia pia Musa hapo kwanza alikuwa mtu Hodari wa maneno na matendo.(maana yake hakuwa mpole), ndio maana alikimbia Misri baada ya kugundulika kuwa kaua mtu.
Matendo 7:22 “Musa akafundishwa hekima yote ya Wamisri, akawa hodari wa maneno na matendo”.
Sasa unaweza kujiuliza upole alikuja kuutolewa wapi?
Baada ya Musa kumkimbia Farao, alikwenda nchi ya Midiani, akiwa huko Mungu alikishusha kiburi chake, akamnyenyekeza kutoka kuwa Mwana wa kifalme mpaka mchunga mbuzi na kondoo, alichunga mifugo ya Yethro mkwewe kwa miaka mingi sana (Takribani miaka 40), hivyo kile kiburi chake chote kikaisha, yale majivuno yake yote yakaisha, ule ujuzi wake wote wa kuzungumza ukaisha, akawa ni mtu mpole sana, asiyeweza kuongea sana. Na ndipo katika wakati huo Mungu akamtokea na kumwagiza ashuke Misri akawaokoe ndugu zake. (Kwahiyo ni Mungu ndiye aliyemfanya mpole).
Lakini swali ni je! Kama tayari Mungu kamfanya mpole kwanini mbeleni tunaona tena anatoa mashauri ya kuua watu?
Hesabu 31:17 “Basi KWA AJILI HIYO MWUENI KILA MUME KATIKA HAO WATOTO, na kila mwanamke aliyemjua mume kwa kulala pamoja naye”.
Jibu ni kwamba, Musa hakutoa amri ya kuua kwa matakwa yake yeye, au kwa agizo lake yeye, BALI KWA AGIZO LA MUNGU. Mungu ndiye aliyetoa maagizo ya kuua watu wote wa Midiani, bila kubakisha yeyote, kutokana na kosa la wamidiani kumtoa Balaamu, na kumtuma kwa Balaki mfalme wa Moabu, ili awalaani Israeli, hivyo Mungu akaikasirikia nchi ya Midiani na kumwagiza Musa akawaue watu wote.
Na Musa alipowatuma majemedari wa Israeli wakaue, kwa agizo hilo la Bwana, wale majemedari wakaua kweli wanaume na wafalme lakini wakawaacha hai wanawake!, jambo ambalo ni kinyume na maagizo Bwana aliyoyatoa.
Tusome tena,
Hesabu 31:7 “Nao wakapigana na Midiani kama Bwana alivyomwagiza Musa; nao wakamwua kila mume.
8 Nao wafalme wa Midiani wakawaua pamoja na watu wengine waliouawa; Evi, na Rekemu, na Suri, na Huri, na Reba, hao wafalme watano wa Midiani; Balaamu mwana wa Beori naye wakamwua kwa upanga.
9 Wana wa Israeli wakawachukua mateka wanawake wa Midiani na watoto wao; na ng’ombe zao wote, na kondoo zao wote, na mali zao zote, wakachukua nyara.
10 Na miji yao yote, kila mahali walipokuwa wakikaa, na marago yao yote wakayateketeza kwa moto.
11 Nao wakatwaa hizo nyara zote, na mateka yote, ya wanadamu na ya wanyama.
12 Nao wakawaleta mateka ya wanadamu, na mateka ya wanyama, na hizo nyara, na kuyaweka mbele ya Musa, na mbele ya Eleazari kuhani, na mbele ya mkutano wa wana wa Israeli, hapo maragoni katika nchi tambarare za Moabu, zilizo karibu na Yordani hapo Yeriko.
13 Basi Musa, na Eleazari kuhani, na wakuu wote wa huo mkutano, wakatoka nje kwenda kuwalaki nje ya marago.
14 MUSA AKAWAKASIRIKIA MAJEMADARI WA JESHI, NA HAO MAAKIDA WA ELFU ELFU, NA WAKUU WA MIA MIA, HAO WALIORUDI KUTOKA KATIKA KUPIGA VITA.
15 MUSA AKAWAULIZA, JE! MMEWAPONYA WANAWAKE WOTE HAI?
16 Tazama, hawa ndio waliowakosesha wana wa Israeli, kwa shauri la Balaamu, wamfanyie Bwana dhambi katika hilo jambo la Peori, na kwa hivyo pigo lilikuwa katika mkutano wa Bwana.
17 Basi kwa ajili hiyo mwueni kila mume katika hao watoto, na kila mwanamke aliyemjua mume kwa kulala pamoja naye”.
Hivyo Musa aliendelea kuwa mpole vile vile, kuliko watu wote, lakini alikuwa anayashika maagizo ya BWANA bila kupindisha, kile Bwana atakachokisema anakitekeleza kama kilivyo ili ampendeze Mungu, na aliwaamuru watu kuyafanya maagizo ya Bwana bila kuyapindisha.
Tunachoweza kujifunza na sisi ni kwamba, hatuna budi kuyatekeleza maagizo ya Bwana kama yalivyo, bila kuyapindisha, haijalishi tutaonekanaje!
Maran atha!
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Mada Nyinginezo:
KWANINI NDOA NYINGI ZINAVUNJIKA? (Sehemu ya 2: Upande wa wanawake)
SWALI: Je Wakati Mfalme Nebukadreza anawatupa Shadraka, Meshaki na Abednego kwenye tanuru la Moto, Danieli alikuwa wapi?
JIBU: Kwasababu biblia haiandiki kila habari, bali inachagua yale matukio muhimu tu, yatakayotusaidia, ndivyo ilivyo katika habari hii, haielezi habari za Danieli kwa wakati huo, alikuwepo wapi, lakini katika sintofahamu hiyo, tuna la kujifunza.
Hivyo hapo mambo matatu yanawezekana,
La kwanza ni aidha Danieli hakuwepo, wakati huo, ambapo Nebudreza, anatoa amri, kwasababu utakumbuka kuwa yeye aliyewekwa juu ya waganga wote, na wenye hekima (Danieli 5:11). Hivyo kuna uwezekano, alipewa jukumu lingine la kwenda kulifanya nje ya Babeli kwa wakati huo , na mbio ilipopigwa yeye hakuwepo.
La pili, ni aidha, watu waliokuwa pamoja na mfalme agizo hilo halikuwahusu, kwasababu ukichunguza utaona, Nebukadreza, aliwaita wakuu wake wote waliokuwa katika majimbo yake yote ulimwenguni. Na lengo la kuwaita, lilikuwa ni kuwapima utiifu wao kwa serikali yake moja ya ulimwengu. Ndio maana akawalazimisha wakuu wote ambao wapo mbali naye waje kuisujudia sanamu yake. Hivyo kwasababu Danieli alikuwa katika jumba la mfalme agizo hilo halikumuhusu.
Danieli 2:49 “Tena, Danielii akamwomba mfalme, naye akawaweka Shadraka, na Meshaki, na Abednego, wawe juu ya mambo yote ya uliwali wa Babeli; lakini huyo Danielii alikuwa akiketi katika lango la mfalme”.
Na mwisho, ni kwamba Danieli, tangu mwanzo alisimama katika misingi ya Imani yake, utakumbuka, walipoitwa na kutaka kulishwa Divai, pamoja na vyakula najisi, moja kwa moja walivikataa yeye pamoja na hao wenzake watatu. (Danieli 1:8-16) Hivyo uwezekano pia wa Danieli kumweleza mfalme misimamo wake, ulikuwepo, na mfalme akamwelewa, akamwacha peke yake asiisujudie miungu yake.
Lakini kusema kwamba alitii amri ya mfalme, hilo jambo halipo, wala lisingewezekana kwa Danieli, kwasababu utakumbuka, hata baadaye sana, jaribio kama hilo lilitaka kufanyika, la kumzuia asimwabudu Mungu wake, lakini alikaidi amri yao bila kujali nani kasema, au adhabu gani imetolewa.
Lakini habari hii ya kutokuwepo kwa Danieli inatufundisha nini?
Ni kwamba, upo wakati Mungu atakuepusha na majaribu ambayo nafasi ya kuyakwepa ni ndogo sana, lakini pia upo wakati Mungu atakupitisha katika majaribu ya adui. Mwanzoni kikombe kile hakikumuhusu Danieli, lakini mwishoni, alishiriki kikombe cha kutupwa katika tundu la Simba.
Nasi pia, kuna nyakati ngumu zitapita mbele yetu katika eneo la imani yetu, na Mungu atatuvusha salama bila hata ugumu wowote, lakini pia zipo nyakati ataziacha zipite juu yetu. Lakini yote katika yote, tunapaswa tuwe katika msimamo wetu kama vile Danieli.
Nyakati zote za mvua, na joto, misingi ya imani yetu isitikiswe.
Bwana akubariki.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Mada Nyinginezo:
Tusome,
2 Wakorintho 4:12 “Basi hapo mauti hufanya kazi ndani yetu, bali uzima ndani yenu”.
Ili tuelewe vizuri, tuchukue mfano wa kondoo anayepelekwa machinjoni, yeye ndani yake ipo MAUTI kwasababu dakika chache mbele anaenda kufa, lakini sisi kwetu ni UZIMA kwasababu, anageuka kuwa chakula kinachotupa uzima wa miili yetu.
Hivyo ni sawa na kusema, mauti inafanya kazi ndani ya huyo kondoo na Uzima ndani yetu sisi tunaomla.
Kadhalika maandiko yanawafananisha watumishi wa Mungu kama Kondoo, na wa kwanza kabisa kufananishwa na kondoo ni mkuu wa Uzima Yesu Kristo.
Isaya 53:7 “Alionewa, lakini alinyenyekea, Wala hakufunua kinywa chake; Kama mwana-kondoo apelekwaye machinjoni, Na kama vile kondoo anyamazavyo Mbele yao wakatao manyoya yake; Naam, hakufunua kinywa chake”.
Huyo ni Bwana Yesu ambaye kwa kupitia mateso ya Mauti aliyoyapitia pale Kalvari, sisi tumepata uzima, pasipo yeye kuchubuliwa sisi tusingepata wokovu, pasipo yeye kuudhiwa sisi tusingepata ukombozi n.k
Isaya 53:5 “Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona”.
Hivyo sisi wakristo tunapopitia mateso wakati wa kuipeleka injili, ili watu wengine waokoke, hapo Mauti inafanya kazi ndani yetu lakini UZIMA ndani ya wale tunaowahubiria. Sisi tunataabika ili wao waupokee wokovu, sisi tunatukanwa ili neno la UZIMA liwafikie wengine.
Warumi 8:36 “Kama ilivyoandikwa, ya kwamba, Kwa ajili yako tunauawa mchana kutwa, Tumehesabiwa kuwa kama kondoo wa kuchinjwa”.
Hivyo kwa hitimisho ni kwamba hatuna budi sisi wote tuliookoka kujitoa na kukubali dhiki, uzia, shida na hata kukubali kuutoa uhai ili wengine wapate uzima wa milele kama tulivyoupata sisi.
Jambo hilo lina baraka kubwa sana.
1 Yohana 3:16 “Katika hili tumelifahamu pendo, kwa kuwa yeye aliutoa uhai wake kwa ajili yetu; imetupasa na sisi kuutoa uhai wetu kwa ajili ya hao ndugu”.
Maran atha!
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Mada Nyinginezo:
Mwanzo 2:9
[9]BWANA Mungu akachipusha katika ardhi kila mti unaotamanika kwa macho na kufaa kwa kuliwa; na mti wa uzima katikati ya bustani, na mti wa ujuzi wa mema na mabaya.
Unaweza kujiuliza kulikuwa na sababu gani Mungu kuuweka mti wa ujuzi wa mema na mabaya pale bustanini wakati alikuwa anajua kabisa una kifo ndani yake?
Kwanini asingeuacha tu ule wa uzima na ile mingine ..ili mwanadamu aishi milele kwa furaha pale Edeni.
Je Ni kwamba Mungu hana mipango ya kueleweka kwa watu wake au?(tukizungumza kibinadamu)
Jibu la La! Nataka nikuambie mipango ya Mungu ni mikamilifu sikuzote na ni mizuri..tofauti na tunavyodhani kuwa ule mti wa ujuzi wa mema na mabaya ulikuwa ni mbaya, haukustahili kuwepo pale.
Ukweli ni kwamba ule mti ulikuwa ni mzuri na unafaa sana, tena twamshukuru Mungu kwa kuuweka pale bustanini….Unajua ni kwasababu gani?
Ni kwasababu sisi kamwe tusingeweza kuwa kama Mungu, na malaika zake kama tusingepata ujuzi ndani yetu.
Kumbuka ujuzi ni jambo ambalo mwanadamu hakuumbiwa tangu mwanzo, si asili yetu..sisi tuliumbwa kutokujua mambo kama aibu, ustaarabu, mipango, maamuzi, ibada n.k hayo yote yalikuja baada ya kula matunda yale,
Sasa, Mungu aliliona hilo tangu mwanzo, hivyo akaona njia pekee ya kumkamilisha mwanadamu ili afanane na yeye ni kumpa ujuzi huo ndani yake..lakini aliona pia hatari yake..kwamba siku zote ujuzi una nguvu kubwa ya kupoteza,(1Wakorintho 8:1) hivyo akamtaadharisha mapema.
Ujuzi wa kujua mtu anahitaji kuishi katika nyumba na sio porini, kwamba anahitaji kujenga nyumba, kufanya biashara, kugundua vitu, kuvaa nguo na sio kukaa uchi, kujijengea mfumo n.k Mungu aliona mwisho wake utampoteza mtu, japo ujuzi wenyewe sio mbaya.
Ndipo akabuni njia ya kuweza kudhibiti tatizo hilo. Akaweka mti mwingine bustanini unaoitwa mti wa Uzima. Ambao mwanadamu akiyala matunda yake ataurejesha ule uzima ambao angeupoteza kwa kupokea ujuzi.
Na hapo mwanadamu atakuwa amepata faida mara mbili, kwanza ni kufanana na Mungu, pili ni kurejesha uzima wa milele.
Nachotaka ujue ni kuwa kila mwanadamu anayeishi duniani..ujuzi huu upo ndani yake..Na ndio maana unaweza kujiamulia mambo yako mwenyewe, unaweza kusema hapana au ndio..unaweza kusema nataka au sitaki..huwi kama mnyama, Au kama roboti bali una ujuzi wote wa kufanya unachotaka mwenyewe bila hata kumtegemea Mungu, mwanadamu au shetani..
Lakini nakuambia hii ni hatari kubwa kwasababu uhuru huu wa kifikra umetufanya wanadamu ndio tuende mbali sana na Mungu wetu, tupotee kabisa, tuone Mungu ni nani, mbona tunaweza kufanya wenyewe bila yeye, rangi zetu pekee hazitoshi, tujichubue kidogo, tujichore tatoo kidogo tupendeze, tuvute sigara, tunywe pombe tuwe fresh, tuzini na Wanyama, kwani kuna shida gani? . Kwa kifupi ni kuwa tumepotea kama tutaishi katika hii hali pasipo kuifahamu kinga.
Tunauhitaji mti wa uzima. Na mti wenyewe ni YESU KRISTO. Hakuna namna utaweza kuishi kwa ujuzi wako, au akili zako bila Yesu Kristo kukusaidia. Mwisho wa siku utakufa tu na kupotelea motoni.
Yohana 14:6
[6]Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.
Watu wengi leo wanadhani elimu zao, ndio zitawapa maisha, wanadhani tafiti zao ndio zitawafikisha ng’ambo, wanadhani mawazo yao na imani zao na teknolojia zao na ustaarabu wao ndio zitakazowavusha..
Hawajui kuwa mioyo yetu sisi wanadamu huwa ni midanganyifu kuliko kitu chochote huku duniani.
Yeremia 17:9
[9]Moyo huwa mdanganyifu kuliko vitu vyote, una ugonjwa wa kufisha; nani awezaye kuujua?
Na ndio maana Bwana Yesu alisema “Mtakufa katika dhambi zenu, kama msiposadiki kuwa mimi ndiye.”(Yohana 8:24)..tusipookolewa..hakuna tumaini ndugu. Bwana Yesu ndiye mti wenyewe wa uzima. Shusha kiburi chako, yasalimishe maisha yako kwake..akusaidie.
Siku hizi ni za mwisho, wakati wowote parapanda inalia hakuna mtu asiyelijua hilo, ipo wazi kulingana na dalili tunazoziona sasa. Hii dunia inafikia mwisho, mtafute Yesu Kristo, akuokoke na udanganyifu wa ujuzi.
Kama hujaokoka basi mkaribishe leo Yesu katika maisha yako, kisha ukabatizwe katika ubatizo sahihi wa kuzamishwa katika maji mengi na kwa jina la Yesu Kristo, kisha utapokea ondoleo la dhambi.
Mungu akubariki.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Mada Nyinginezo:
Nini maana ya kilichotarajiwa kikikawia kuja moyo huugua (Mithali 13:12)?.
Kuna tatizo sugu ambalo linalowasumbua watu wengi , hususani vijana pindi wanapookoka, Na pengine linakusumbua hata na wewe.
Vijana kadha wa kadha waliookoka, wamekuwa wakinipigia simu, wengine wakinitumia meseji wakisema mtumishi, tangu nilipookoka, nimejitahidi kweli kuacha uasherati na kutazama picha chafu (za ngono) mitandaoni, Lakini naona kama ninamkosea Mungu kwasababu, zile taswira za yale niliyokuwa ninayafanya au ninayatazama, zinanijia mara kwa mara akilini mwangu, wakati mwingine hata wakati nikiwa naomba, au najifunza Neno.
Hivyo naona kama bado sijakamilika, Mungu hajanisamehe na kuniosha dhambi zangu, najisikia vibaya sana, imenipelekea kukosa nguvu ya kumtumikia Mungu.. Nifanye nini?
Kama na wewe umekuwa na tatizo kama hili nataka nikuambie, wewe sio wa kwanza, Biblia inasema mtaifahamu kweli nayo hiyo kweli itawaweka huru.(Yohana 8:32)
Jambo ambalo wengi hatufahamu ni kuwa, Utakaso wa Mungu umegawanyika katika sehemu mbili.
Tukianzana na huo wa kwanza, zipo hali ndani yako, ambazo Mungu anaziondoa, mara moja pindi tu unapookoka, kwamfano kiu ya kutenda yale maovu uliyokuwa unayatenda huko nyuma, kama vile wizi, matusi, uvaaji mbaya, pombe n.k.
Lakini upo utakaso ambapo itakupasa upitishwe mahali Fulani kwanza kwa muda, ndipo uwe safi kabisa. Na ndio maana utaona katika agano la kale kuna unajisi ambapo ulikuwa ukishatakasika, ilikupasa usubirie mpaka ifike jioni ndio uwe safi, mwingine siku tatu, mwingine wiki mbili, inategemeana na unajisi wenyewe. Utajiuliza ni kwanini usiwe na saa hiyo hiyo?
Kwamfano embu soma vifungu hivi;
Walawi 11:25” na mtu awaye yote atakayechukua cho chote cha mizoga yao atafua nguo zake, naye atakuwa najisi hata jioni”.
Walawi 15:27 “Na mtu ye yote atakayevigusa vitu vile atakuwa najisi, naye atazifua nguo zake, na kuoga majini, naye atakuwa najisi hata jioni.
28 Lakini huyo mwanamke kwamba ametakaswa na kule kutoka damu kwake, ndipo atakapojihesabia siku saba, na baadaye atakuwa safi”.
Sasa katika suala kama hilo, la picha chafu kuondoka ndani yako, hupaswi, kudhani kuwa Mungu hajakusamehe, Umeshasamehewa, dhambi zako, tangu siku ile ulipookoka na kuacha kufanya hayo mambo, lakini ule utakaso kamili haujakamilika ndani yako, hivyo itakuchukua muda kidogo, hivyo kwa jinsi unavyozidi kujitenga na hayo mambo, ndivyo Mungu anakusafisha mpaka utafika wakati hizo picha hazitakujia tena katika akili yako.
Utajiuliza ni kwanini Musa alipelekwa jangwani miaka 40, kabla ya kuitwa kwenda kuwaokoa wana wa Israeli. Ilikuwa ni kwa kusudi la kuondoa, kiburi na majivuno ndani yake ambayo pengine yasingeweza kuondoka kwa siku moja au wiki moja. Vilevile wana wa Israeli walizungushwa jangwani kwa miaka 40, ilikuwa ni ili kuindoa miungu iliyokuwa mioyo mwao, wajifunze kumtegemea Yehova tu.
Hata gari lililo spidi haliwezi kuchuna breki na kusimamia hapo hapo tu, ni lazima litaendelea mbele kidogo, kwasababu lilikuwa katika mwendo kasi. Halikadhalika, ikiwa umeokoka leo, au hivi karibuni, hizo picha chafu ulizokuwa unazitazama, zilishaiharibu nafsi yako kwa muda mrefu sana, hivyo zinaweza kuchukua muda Fulani mpaka ziondoke kabisa. Ndio ujue dhambi sio jambo la kulichukuliwa kirahisi rahisi tu.
1Wathesalonike 4:3 “Maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu, kutakaswa kwenu, mwepukane na uasherati;
4 kila mmoja wenu ajue kuuweza mwili wake katika utakatifu na heshima;
5 si katika hali ya tamaa mbaya, kama Mataifa wasiomjua Mungu”.
Lakini usihofu wewe endelea kukaa mbali na uchafu wote, na kidogo kidogo, Bwana atayasafisha mawazo yako, na kuna wakati utafika, hata hayo mawazo au hizo picha zitakuwa kama ni Habari za utotoni.
Dhambi inagharama. Hivyo, usirudi nyuma, wala usifadhaike, songa mbele, zidisha ukaribu wako na Mungu, kaa tu mbali na vyanzo vyote vya uzinzi, tamthilia za kidunia acha, movie zote zenye maudhui hayo acha, mazungumzo yenye uzinzi ndani yake, kampani za marafiki wahuni achana nazo, mitandao ya kijamii kama instagramu, ikiwa huna jambo la maana unafuata kule, ondoa, kwasababu vingi vilivyomo kule havikujengi,.. vyote hivyo jitenge navyo.. Kwasababu biblia inasema moto hufa kwa kukosa kuni.
Mithali 26:20a “Moto hufa kwa kukosa kuni;..”
Bwana akubariki.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Mada Nyinginezo:
ZIKIMBIE TAMAA ZA UJANANI! NA MTU YEYOTE ASIUDHARAU UJANA WAKO.
Ni kwanini Bwana Yesu amefanyika kuwa ishara itakayonenewa?..Nini maana ya kunenewa?.
Luka 2:34 “Simeoni akawabariki, akamwambia Mariamu mama yake, Tazama, huyu amewekwa kwa kuanguka na kuinuka wengi walio katika Israeli, na kuwa ishara itakayonenewa”.
Kunenewa kunakozungumziwa hapo sio “kenenewa vizuri” bali “kunenewa vibaya”.
Wana wa Israeli, walitegemea Masihi atazaliwa katika jumba la Kifalme, ataishi maisha ya kifahari, atakuwa mkuu na Mfalme ndani ya muda mfupi sana. Na atakuwa na fahari kuliko Sulemani, na zaidi ya yote atakuwa hafi, anadumu milele.
Ndicho walichokuwa wanategemea, kukiona kwa Masihi atakayekuja.
Lakini alipokuja Masihi mwenyewe (yaani Yesu) na kuona kwanza anazaliwa zizini na si kwenye jumba la kifalme kama walivyopanga, wakapata mashaka.
Walipomwona anakula na kunywa na watu maskini tena wenye dhambi mashaka yakaongezeka zaidi.
Lakini zaidi ya yote waliposikia kwamba eti atakufa na kufufuka, ndio kabisa wakasema huyu sie!.
Yohana 12:32 “Nami nikiinuliwa juu ya nchi, nitawavuta wote kwangu.
33 Aliyanena hayo akionyesha ni mauti gani atakayokufa.
34 Basi mkutano wakamjibu, Sisi tumesikia katika torati ya kwamba Kristo adumu hata milele; nawe wasemaje ya kwamba imempasa Mwana wa Adamu kuinuliwa? Huyu Mwana wa Adamu ni nani?”.
Hivyo walikuwa wanazitafuta ishara kuu…katika vichwa vyao walikuwa wameshajiaminisha kuwa Masihi atakuwa kama Malaika-Mtu hawezi kufa, na atakuwa ameshika fimbo ya chuma kuyatiisha mataifa na wakati anazaliwa tu atakuwa tajiri.
Hivyo Ishara hiyo ya Ukuu uliopitiliza hawakuiona kwa Masihi, na kinyume chake masihi akaja kwa nyingine tofauti kabisa na ishara yenyewe ni ISHARA YA YONA.
Kikawaida hakuna mtu angependwa kufananishwa na Yona. Hakuna mtu anayevutiwa na tabia ya Yona, wala hakuna mtu anayetamani kuwa kama Yona, kwasababu ishara ya Yona sio nzuri.
Lakini Masihi aliichagua ishara hiyo badala ya ishara ya Ukuu na ufalme, Na kwa ishara hiyo ikawafanya watu kumnenea vibaya kama walivyomnenea nabii Yona.
Mathayo 12:38 “Hapo baadhi ya waandishi na Mafarisayo wakamjibu, wakasema, Mwalimu, twataka kuona ishara kwako.
39 Akajibu, akawaambia, Kizazi kibaya na cha zinaa chatafuta ishara, wala hakitapewa ishara, ila ishara ya nabii Yona.
40 Kwani kama vile Yona alivyokuwa siku tatu mchana na usiku katika tumbo la nyangumi, hivyo ndivyo Mwana wa Adamu atakavyokuwa siku tatu mchana na usiku katika moyo wa nchi”.
Tukio la Yona kukaa tumboni kwa samaki siku tatu, leo hii linaonekana kama la kipumbavu, lakini pasipo ile ishara watu wa Ninawi wasingetubu!..wangedhani Yona kajizukia tu na kuanza kuhubiri habari zake, lakini waliposikia kuwa alikaa tumboni siku tatu bila kufa, wakatafakati alipataje pataje hewa akiwa kule tumboni muda wa siku tatu, alikaajekaaje bila kufa kule, wakaogopa, wakajua ule ni uweza wa Mungu.
Hivyo wakatubu kwa ishara hiyo, lakini endapo Yona angetoka moja kwa moja Israeli na kwenda Ninawi bila ishara yoyote, watu wa Ninawi wasingemsikiliza.
Na hata leo ni hivyo hivyo, Masihi alipenda kuchagua njia ya Mauti kama ishara kuu, ili sisi tuzidi kumwamini.
Hebu tafakari angekuja tu na kuishi na kisha kupaa bila kufa, tungeaminije kwamba mtu akifa anaweza kufufuka tena?.
Hivyo ilibidi na yeye afe, azikwe na kisha afufuke ili sisi tuuone uweza wa kiungu uliopo ndani yake, na kupitia huo Umetufanya kumwamini yeye mara nyingi zaidi na vile vile kuleta mazao mengi zaidi kwake.
Yohana 12:23 “Naye Yesu akawajibu, akasema, Saa imefika atukuzwe Mwana wa Adamu.
24 Amin, amin, nawaambia, Chembe ya ngano isipoanguka katika nchi, ikafa, hukaa hali iyo hiyo peke yake; bali ikifa, hutoa mazao mengi”.
Swali ni je! Na wewe leo umemwamini Bwana kupitia Ishara hiyo Ya kufa na kufufuka kwake? Je unaineneaje hiyo ishara..unainenea vyema au vibaya?, Unamtazama Kristo kwa jicho gani leo?.
Unamtazamia Kristo yule wa kukupa majumba na magari ya kifahari, au unamtazamia yule aliyekufa kwaajili ya dhambi zako, yule anayekwambia utubu!
Kristo wa kweli anasema hivi.
Marko 8:34 “Akawaita mkutano pamoja na wanafunzi wake, akawaambia, Mtu ye yote akitaka kunifuata na ajikane mwenyewe, ajitwike na msalaba wake, anifuate.
35 Kwa kuwa mtu atakaye kuiponya nafsi yake, ataiangamiza, na mtu atakayeiangamiza nafsi yake kwa ajili yangu na kwa ajili ya Injili, huyu ataisalimisha.
36 Kwa kuwa itamfaidia mtu nini kuupata ulimwengu wote, akipata hasara ya nafsi yake?
37 Ama mtu atoe nini badala ya nafsi yake?”
Utatoa nini ili ujitoe kuzimu siku ile?, kwa uasherati unaoufanya?, Kwa ulevi unaoufanya, kwa wizi unaoufanya?..fedha hazitakutoa kuzimu siku ile, vile vile mzazi hatakutoa kuzimu, wala mpenzi, wala Raisi.
Ayubu 7:9 “Kama vile wingu likomavyo na kutoweka, Ni vivyo huyo ashukaye kuzimuni hatazuka tena kabisa.
10 Hatarudi tena nyumbani kwake Wala mahali pake hapatamjua tena”.
Mpokee leo Yesu akufanye kiumbe kipya, na ya kale yote yatakuwa yamepita, na atakufanya kuwa mpya.
Maran atha!
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Mada Nyinginezo:
SWALI: Biblia inamaana gani inaposema “Watu hawa ni miamba yenye hatari”. Hii miamba yenye hatari ni ipi?
JIBU: Tusome..
Yuda 1:12 “Watu hawa ni miamba yenye hatari katika karamu zenu za upendo walapo karamu pamoja nanyi, wakijilisha pasipo hofu; ni mawingu yasiyo na maji, yachukuliwayo na upepo; ni miti iliyopukutika, isiyo na matunda, iliyokufa mara mbili, na kung’olewa kabisa;
13 ni mawimbi ya bahari yasiyozuilika, yakitoa aibu yao wenyewe kama povu; ni nyota zipoteazo, ambao weusi wa giza ndio akiba yao waliowekewa milele”.
Hapa ni mtu Yuda alikuwa anawalinganisha wachungaji na mitume wa uongo kama miamba yenye hatari.
Sasa miamba inayomaanishwa hapo, si hii miamba tuionayo nchi kavu, hapana, bali ni ile miamba ya habarini ambayo baadhi yao inatabia ya kuchomoza juu hadi karibu na usawa wa bahari. Miamba hii ni hatari sana kwa mabaharia, kwasababu huwa haionekani, lakini meli inapopita karibu nayo, inaichana, kama sio kuiharibu kabisa na matokeo yake, ni aidha meli kugotea palepale, au kuzama kabisa.
Kama mabaharia wasipokuwa waangalifu, kwa kupita njia zilezile walizozithibitisha ni rahisi sana kukutana na hii miamba na kuzipoteza meli zao moja kwa moja.
Sasa hapo anaposema “Watu hawa ni miamba yenye hatari katika karamu zenu za upendo walapo karamu pamoja nanyi, wakijilisha pasipo hofu”;
Anamaanisha, wachungaji hawa, au watumishi hawa wa uongo ni ngumu kuwatambua, kama tu vile miamba hii hatari ilivyo ngumu kuiona habarini, pale ambapo Habari inaonekana shwari na tulivu yafaa kwa kusafiria kumbe ndipo ilipojifichia, halikadhalika, watumishi hawa wa uongo, mahali ambapo mpo katika karamu zenu za Upendo, yaani wakati ambapo mnamfurahia Mungu wenu, mnatangaza Habari njema, mkidhani kuwa wapo na nyie, kumbe ni mbwa mwitu katika mavazi ya kondoo.
Mfano wa watu hawa alikuwa ni Yuda,alitembea na Bwana Pamoja na mitume wengine, lakini haikuwa rahisi kumgundua, hadi dakika ya mwisho, utaona alipokuwa katika mlo wa jioni, kama mpelelezi, hakuna aliyemtambua isipokuwa Bwana tu peke yake.
Mtume Paulo aliliona hilo hata wakati wa kuondoka kwake akasema..
Matendo 20:29 “Najua mimi ya kuwa baada ya kuondoka kwangu mbwa-mwitu wakali wataingia kwenu, wasilihurumie kundi;
30 tena katika ninyi wenyewe watainuka watu wakisema mapotovu, wawavute hao wanafunzi wawaandamie wao”.
Hadi sasa, inasikitisha kuona watumishi wa namna hii wapo wengi katika kanisa la Mungu, ,hawaoni shida kuwadanganya watu, wengine ni wachawi, wengine ni matapeli, wengine wapo kwa lengo la kuzivuruga tu kazi za Mungu, ili watu watusiishi Maisha matakatifu, hawawahurumii watu wanaotaka kumjua Mungu, lakini cha ajabu ukiwaangalia kwa nje, wanalitaja jina la Yesu, wanaongoza makanisa, wanashiriki katika kampeni zote za kidini.
Huu ni wakati wa kuwa makini sana, Ni wakati ambao wewe kama mkristo, kuondoa uvivu wa kusoma biblia, tunadanganywa kwasababu hatuna maarifa ya kutosha kuhusu Mungu wetu na utendaji kazi wake. Hatuwezi kumshinda shetani kwa maneno tu, au kwa kumkemea, tutamshinda shetani kwa lile Neno lililokaa ndani yetu kwa wingi, ndiyo silaha ambayo Bwana Yesu aliitumia kumshinda shetani pale alipokuwa anajaribiwa nay eye kule jangwani.
Vinginevyo tukiyaendesha Maisha yetu hivi hivi tu kwa jinsi tunavyotaka, tujiandae kukutana na hii miamba yenye hatari, isiyoonekana. Tukiwa wavivu kujifunza biblia, hakuna namna tutamkwepa shetani, hakuna namna.
Bwana atusaidie.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Mada Nyinginezo:
Tusome,
1 Petro 4:8 “Zaidi ya yote iweni na juhudi nyingi katika kupendana; kwa sababu upendano husitiri wingi wa dhambi”.
Awali ya yote ni muhimu kufahamu maana ya neno “kusitiri” na vile vile ni muhimu kufahamu ni nani ambaye anayesitiriwa dhambi zake, je! ni yule anayependa au anayependwa?.
Neno “kusitiri” maana yake “kufunika au kuficha”..mtu aliyevaa nguo za kuufunika mwili wake wote, maana yake “kavaa nguo za kujisitiri mwili wake, ili asibakie kuwa tupu”. (Kauficha mwili wake).
Sasa tukirudi kwenye huo mstari wa kwenye 1Petro 4:8, maandiko yanasema upendano husitiri wingi wa dhambi.
Sasa dhambi zinazositiriwa/kufichwa si za yule anayependa bali yule anayependwa.
Sasa zinasitiriwa kwa namna gani?
Neno la Mungu linasema katika kile kitabu cha 1Wakorintho 13:4-5.
1 Wakorintho 13:4 “Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni;
5 haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya; Mwisho kabisa anasema “UPENDO HAUHESABU MABAYA”.
Kutokuhesabu mabaya ndio “Kusitiri dhambi”.
Maana yake ni kwamba mtu mwenye upendo, maisha yake yote ni ya kusamehe tu na kutoweka kumbukumbu ya mambo mabaya anayofanyiwa.
Mathayo 18:21 “Kisha Petro akamwendea akamwambia, Bwana, ndugu yangu anikose mara ngapi nami nimsamehe? Hata mara saba?
22 Yesu akamwambia, Sikuambii hata mara saba, bali hata saba mara sabini”.
Mfano mzuri wa Mmoja aliyeweza kusitiri wingi wa dhambi nyingi, ni Bwana wetu Yesu Kristo mwenyewe.
Kwa Upendo wake mwingi alijitoa nafsi yake sadaka ili sisi tupate kusitiriwa dhambi zetu. Kwake yeye tumepata ondoleo la dhambi. Tukiwa dhani yake hatuhukumiwi.
Mtume Paulo anazidi kuliweka wazi hilo katika kitabu cha Warumi.
Warumi 4:7 “Heri waliosamehewa makosa yao, Na waliositiriwa dhambi zao.
8 Heri mtu yule ambaye Bwana hamhesabii dhambi”.
Je na wewe leo dhambi zako zimesitiriwa na kuondolewa kabisa?? Kumbuka dhambi zako haziwezi kuondolewa kama haupo ndani ya pendo la Kristo, kwasababu ni upendo tu ndio unaositiri wingi wa dhambi, maana yake kama haupo ndani upendo wa Kristo, basi hauna msamaha wa dhambi.
Sasa utauliza, unaingiaje katika pendo hilo na kupata msamaha?.
Unaingia katika pendo hilo kwa kutubu dhambi zako zote kwa kumaanisha kuziacha, na kubatizwa katika ubatizo sahihi wa jina la Yesu Kristo na kumpokea Roho Mtakatifu.
Baada ya hapo dhambi zako zote zitaondolewa na kuwa mrithi wa ahadi za Mungu.
Na vile vile unapowahubiria wengine habari za Pendo la Kristo, na hata wao wakaingia katika pendo hilo, (kwa kutubu na kuacha dhambi)basi utakuwa umewasaidia dhambi zao kufunikwa na pia kuwaokoka na adhabu ya ziwa la moto, sawasawa na maandiko yafuatayo.
Yakobo 5:19 “Ndugu zangu, ikiwa mtu wa kwenu amepotelea mbali na kweli, na mtu mwingine akamrejeza;
20 jueni ya kuwa yeye amrejezaye mwenye dhambi hata atoke katika njia ya upotevu, ataokoa roho na mauti, na kufunika wingi wa dhambi.
Bwana atubariki sote.
Maran atha!
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Mada Nyinginezo:
Katika biblia ukiona neno “mwandamo wa mwezi”, au “mwezi mpya”, ujue ni neno lile lile moja linalomaanisha “siku ya kwanza ya mwezi”.
Katika agano la kale siku hii iliheshimiwa na kufanywa kama mojawapo ya siku takatifu, kama tu vile ilivyokuwa siku ya sabato, ambayo ni siku ya saba. Vivyo hivyo kila siku ya kwanza ya mwezi mpya, tarehe moja (kwa kalenda ya kiyahudi), ilikuwa ni takatifu kwao, na ni lazima watu wakamtolee Mungu sadaka za kuteketezwa, Sadaka za unga na vinywaji, Pamoja na kupiga tarumbeta juu ya sadaka hizo, (Hesabu 28:11-15), .Vilevile hukuruhusiwa kufanya shughuli yoyote au biashara yoyote(Nehemia 10:31-33)
Hesabu 28:11 “Tena katika mianzo ya miezi yenu mtamsongezea Bwana sadaka ya kuteketezwa; nayo ni ng’ombe waume wadogo wawili, na kondoo mume mmoja, na wana-kondoo waume wa mwaka wa kwanza, wakamilifu, saba;
12 pamoja na sehemu ya kumi tatu za efa za unga mwembamba kuwa sadaka ya unga, uliochanganywa na mafuta, kwa kila ng’ombe; na sehemu ya kumi mbili za unga mwembamba kuwa sadaka ya unga, uliochanganywa na mafuta, kwa huyo kondoo mume mmoja;”
Hesabu 10:10 “Tena katika siku ya furaha yenu, na katika sikukuu zenu zilizoamriwa, na katika kuandama miezi kwenu, mtapiga hizo tarumbeta juu ya sadaka zenu za kuteketezwa, na juu ya dhabihu za sadaka zenu za amani; nazo zitakuwa kwenu ni ukumbusho mbele za Mungu wenu; mimi ndimi Bwana, Mungu wenu”.
Lakini kuna wakati wayahudi, walizifanya sikukuu hizo kama mazoea tu, wakawa hawazitoi katika utakatifu, bali kama agizo tu la kidini na huku nyuma mioyo yao ipo mbali na Mungu, hivyo hiyo ikamfanya Mungu akasirishwe nao na hatimaye kuzitaa sikukuu zao hizo za mwandamo wa mwezi.
Isaya 1:13 “Msilete tena matoleo ya ubatili; uvumba ni chukizo kwangu; mwezi mpya na sabato, kuita makutano; siyawezi maovu hayo na makutano ya ibada.
14 Sikukuu zenu za mwezi mpya na karamu zenu zilizoamriwa, nafsi yangu yazichukia; mambo hayo yanilemea; nimechoka kuyachukua”.
Neno hili utalisoma pia katika vifungu hivi;
Zaburi 81:3 “Pigeni panda mwandamo wa mwezi, Wakati wa mbalamwezi, sikukuu yetu”.
1Samweli 20:5 “Naye Daudi akamwambia Yonathani, Tazama, kesho ni mwandamo wa mwezi, nami hainipasi kukosa kuketi chakulani pamoja na mfalme; lakini niache nijifiche bondeni hata siku ya tatu jioni.
Soma pia, 2Nyakati 2:4, 8:13, Ezra 3:5, Hosea 2:11.
Jibu ni la! Kama tu vile hatujapewa takwa la kuitunza sabato kama sheria , vivyo hivyo, na katika mwandamo wa mwezi mpya.
Wakolosai 2:16 “Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au sabato;
17 mambo hayo ni kivuli cha mambo yajayo; bali mwili ni wa Kristo”.
Ni kwamba tuthaminishe nyakati zetu mpya kwake. Wiki yako inapoisha na kuanza nyingine bila kumfanyia Mungu wako ibada, ni hatari kubwa sana, kama kwako ni jumapili, au jumamosi, ndio unamfanyia Mungu ibada, hakikisha unakutanika na wengine, kumwabudu Mungu wako, usiruhusu wiki yako ipite hivi hivi tu.
Halikadhalika, mwezi wako mpya unapoanza, usianze hivi hivi tu, bali chukua muda kwenda kumshukuru Mungu nyumbani kwake, ni muhimu sana. Ukiona wiki yako inapita hivi hivi tu, mwezi wako unapita hivi hivi tu, mwaka wako unapita hivi hivi tu, huna Habari na Mungu. Angalia Maisha yako ni lazima yatakuwa na kasoro Fulani tu.
Hivyo tujitahidi sana, tusiwe na mapengo pengo kwa Mungu wetu.
Bwana akubariki.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Mada Nyinginezo:
SABATO ILIFANYIKA KWAAJILI YA MWANADAMU NA SI MWANADAMU KWAAJILI YA SABATO!