Sasa tukirudi katika roho, Uzima wa milele ni nini?..biblia imetupa majibu mafupi na marahisi..
Yohana 17:3 “Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma”
Ukimjua MUNGU na YESU KRISTO unao uzima wa milele..
Sasa si kwamba MUNGU na YESU ni vitu viwili tofauti.. La! ni MUNGU mmoja katika madhihirisho mawili tofauti..
Mfano mtu anaweza kukuona wewe mubashara (live)…au akakuona kupitia picha yako. Sasa wewe kwenye picha na wewe wa mubashara sio watu wawili tofauti ni mtu mmoja katika madhihirisho mawili tofauti.
Wakati mwingine badala ya kuonekana wewe mubashara unaweza kutuma picha yako au kuibandika katika nyaraka zako muhimu kama vyeti, au vitambulisho au barua na ikawa ni wewe yule yule.
Na YESU ni picha kamili ya Mungu, aliyemwona YESU amemwona MUNGU BABA, kwahiyo hatuwezi tena kutafuta kujua Baba yupoje, tukimwona Yesu tumemwona Baba, ndivyo maandiko yasemavyo..
Yohana 14:8 “Filipo akamwambia, Bwana, utuonyeshe Baba, yatutosha. 9 Yesu akamwambia, Mimi nimekuwapo pamoja nanyi siku hizi zote, wewe usinijue, Filipo? Aliyeniona mimi amemwona Baba; basi wewe wasemaje, Utuonyeshe Baba?”
Yohana 14:8 “Filipo akamwambia, Bwana, utuonyeshe Baba, yatutosha.
9 Yesu akamwambia, Mimi nimekuwapo pamoja nanyi siku hizi zote, wewe usinijue, Filipo? Aliyeniona mimi amemwona Baba; basi wewe wasemaje, Utuonyeshe Baba?”
Yohana 14:7 “Kama mngalinijua mimi, mngalimjua na Baba; tangu sasa mnamjua, tena mmemwona”
Sasa turudi kwenye “UZIMA WA MILELE”...anasema…“Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma”.
Maana yake ukisema unamjua MUNGU halafu unamkataa YESU maana yake huna UZIMA WA MILELE, Kwasababu YESU ni ufunuo kamili wa Mungu katika mwili.
Utaona watu wanasema, mimi namwamini Mungu lakini simwamini YESU, sasa utaikanaje picha ya mtu na kumkiri mtu?..
Nimekuletea picha yangu, halafu unaikana, na bado unakiri kunijua?.. kama ukiikana picha yangu maana yake unanifanya mimi kuwa mwongo.
Vile vile ukimkana YESU na kukiri kumjua MUNGU unamfanya MUNGU kuwa mwongo. (Soma 1Yohana 5:10).
Kama humwamini YESU ni moja kwa moja umwamini MUNGU pia, hiyo haina kutafakari mara mbili..kama humjui Yesu ni moja kwa moja humjui Mungu Baba hiyo haina kutafakari mara mbili pia.
Yohana 8:19 “Basi wakamwambia, Yuko wapi Baba yako? Yesu akajibu, Mimi hamnijui, wala Baba yangu hammjui; kama mngalinijua mimi, mngalimjua na Baba yangu”.
Kwahiyo wakati huu Uzima wa milele unapatikana kwa YESU tu pekee yake, zingatia hilo: YESU TU PEKE YAKE!!.…usijaribu kumtafuta Mungu nje ya YESU, ni kupoteza muda.
Usijaribu kumtumikia Mungu nje ya Yesu, ni kupoteza muda, usitafute uzima wa milele nje ya Yesu, ni kupoteza muda na uzima wako wa milele, akitokea mtu, awe nabii, mtume au mchungaji amshuhudii Yesu kama ndie njia pekee ya kufika mbinguni, mkimbie!
Akitokea kuhani na kukufundisha kuna mwingine au wengine wanaoweza kufanya kazi kama ya YESU, mkimbie!.. Kristo YESU hana pacha, wala msaidizi kwamba pia kupitia mtakatifu fulani aliye hai au aliyekufa tunaweza kumwona Mungu, kwamba tukimwamini huyo tunaweza kumwona MUNGU, kimbia!
YESU si mtu wa pembeni aliyeletwa kutuokoa, ni Mungu mwenyewe aliyevaa mwili… yaani Mungu aliyetengeneza mwili na kuweka tabia zake zote ndani ya huo mwili, akaja ili atuonyeshe njia na kutukomboa, hivyo hana msaidizi, kajitosheleza kwasababu yeye ni MUNGU. (1Timotheo 3:16).
Kwahiyo tusipomwamini Yesu kwa namna hiyo hatuna uzima wa milele, haijalishi tutajitahidi kufanya mema kiasi gani, kama tumeshamsikia na hatutaki kumwamini, hatuna uzima wa milele.
Swali ni je?.. Unao uzima wa milele?..je umemwamini YESU na kuyafanya anayoyasema?.
Luka 6:46 “Na kwa nini mnaniita, Bwana, Bwana, walakini hamyatendi nisemayo? 47 Kila mtu ajaye kwangu, na kuyasikia maneno yangu na kuyatenda, nitawaonyesha mfano wake. 48 Mfano wake ni mtu ajengaye nyumba, na kuchimba chini sana, na kuweka msingi juu ya mwamba; na kulipokuja gharika, mto uliishukia nyumba ile kwa nguvu, usiweze kuitikisa; kwa kuwa imejengwa vizuri. 49 Lakini yule aliyesikia ila hakutenda, mfano wake ni mtu aliyejenga nyumba juu ya ardhi pasipokuwa na msingi, mto ukaishukia kwa nguvu, ikaanguka mara; na maangamizi yake nyumba ile yakawa makubwa”.
Luka 6:46 “Na kwa nini mnaniita, Bwana, Bwana, walakini hamyatendi nisemayo?
47 Kila mtu ajaye kwangu, na kuyasikia maneno yangu na kuyatenda, nitawaonyesha mfano wake.
48 Mfano wake ni mtu ajengaye nyumba, na kuchimba chini sana, na kuweka msingi juu ya mwamba; na kulipokuja gharika, mto uliishukia nyumba ile kwa nguvu, usiweze kuitikisa; kwa kuwa imejengwa vizuri.
49 Lakini yule aliyesikia ila hakutenda, mfano wake ni mtu aliyejenga nyumba juu ya ardhi pasipokuwa na msingi, mto ukaishukia kwa nguvu, ikaanguka mara; na maangamizi yake nyumba ile yakawa makubwa”.
Mwamini YESU na tenda ayasemayo.
Maran atha!
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
TENDA AGIZO LA YESU, HILO NDIO LITAKALOKULINDA.
UJIO WA BWANA YESU.
JITIE NGUVU KWA BWANA MUNGU WAKO.
MAASI KUONGEZEKA NI ISHARA YA NINI?.
Na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa?. Ni mwamba gani huo?(Mathayo 16:18)
Print this post