Kwanini Bwana Yesu alitumia neno “wewe wasema”(Mathayo 27:11)

Kwanini Bwana Yesu alitumia neno “wewe wasema”(Mathayo 27:11)

SWALI: Kwanini Bwana Yesu alitumia neno “wewe wasema” alipoulizwa maswali na sio kujibu moja kwa moja?(Mathayo 27:11)


JIBU: Ni kweli tunaona mahali kadha wa kadha Bwana Yesu alipoulizwa maswali Na baadhi ya wayahudi na wapagani, majibu yake hayakuwa yamenyooka moja kwa moja alitumia kauli ya “wewe wasema”…kwa mfano tazama vifungu vifuatavyo;

Mathayo 27:11

[11]Naye Yesu akasimama mbele ya liwali; liwali akamwuliza, akasema, Wewe ndiwe mfalme wa Wayahudi? Yesu akamwambia, Wewe wasema.

Luka 22:68-71

[68]Tena, nikiwauliza, hamtajibu.

[69]Lakini tangu sasa Mwana wa Adamu atakuwa ameketi upande wa kuume wa Mungu Mwenyezi.

[70]Wakasema wote, Basi, wewe ndiwe Mwana wa Mungu? Akawaambia, Ninyi mwasema kwamba mimi ndiye.

[71]Wakasema, Basi, tuna haja gani tena ya ushuhuda? Maana, sisi wenyewe tumesikia maneno ya kinywa chake.

Soma pia…Luka 23:3

Maana rahisi ya neno hilo ni ipi?

Maana yake ni

 “ndio, wewe umesema hivyo, sio mimi”

Au “ndio, wewe umeona kuwa ni hivyo

Sasa kwanini Atumie kauli hiyo?

Kwasababu alijua waliokuwa wanamuuliza hawakuwa na nia ya kutaka kufahamu ukweli, bali kutafuta neno la kumshitaki, au kumdhihaki, ndio maana kujibu kwake hakukuwa kwa moja kwa moja, yaani upande mmoja anaonyesha kukubali, lakini upande mwingine anaacha hukumu watoe wao wenyewe…

Hiyo ilikuwa ni desturi yake sio tu kwenye maswali bali hata kwenye Mafundisho yake kadha wa kadha…Alizungumza na makutano kwa mifano..kisha wale waliokuwa tayari kupokea aliwafunulia yote baadaye.

Hii ni hekima ambayo tunaweza jifunza hata sisi..

Kwamfano wewe ni mchungaji, kisha ukajikuta watu wasiopenda wokovu, wamekushitaki na kukupeleka Mahakamani halafu hakimu anakuuliza je wewe ndio wale wachungaji ambao, mnaweka Makapu ya sadaka mbele, ili mle Sadaka za waumini.

Sasa unajua kabisa kauli kama hiyo ni ya mtego, kukudhihaki, au kutaka sababu ya kukushitaki, sasa Ili kuikata kauli yake..kukataa Kuwa wewe sio mchungaji watasema unadanganya, kukataa kuwa chombo cha sadaka hakiwekwi mbele watu kutoa, watakuona Pia mwongo, lakini kukusingizia unakula sadaka za waumini unajua ni uongo…

Hivyo kujibu vema hiyo kauli ni kukubali upande mmoja, na mwingmwingiwaachia wao aaamue..

“Wewe Wasema”

Yaani *ndio, wewe umesema hivyo*

“Ndio wewe Umeona kuwa ndivyo ilivyo”.

Hapo umekata maneno yote..atakachoamua, Ni kulingana na mawazo yake mwenyewe lakini sio yale yaliyothibitishwa kikamilifu na wewe..

Hivyo yatupasa tutumie busara. katika ujibuji wetu wa maswali hususani kwa wale wanaotushitaki na kutushambulia

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Yesu alifundisha kwa mifano. Je hiyo mifano maana yake nini?

KWA WALE WALIO NJE “YOTE” HUFANYWA KWA MIFANO.

“Vya Kaisari mpeni kaisari”  ni vipi hivyo tunavyopaswa tumpe?.

Print this post

About the author

Nuru ya Upendo administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments