SWALI: Maandiko yanasema “Nimekukimbilia Wewe, Bwana, Nisiaibike milele”, Je! ni aibu gani anaomba aepushwe nayo?. Mbona tunapitia kuabishwa, ijapokuwa tumemkimbilia Mungu?
JIBU: Vifungu kadha wa kadha kwenye zaburi vinaeleza, habari hiyo,
Zaburi 31:1 Nimekukimbilia Wewe, Bwana, Nisiaibike milele. Kwa haki yako uniponye
Zaburi 25:20 Unilinde nafsi yangu na kuniponya, Nisiaibike, maana nakukimbilia Wewe
Soma pia Zaburi 22:5, 71:1
Daudi ni mtu ambaye alizungukwa na maadui pande zote, na hivyo alijua nguvu zake zipo kwa Mungu tu, hivyo akishindwa nao basi itakuwa ni fedheha na aibu kwake, Vilevile ni mtu ambaye aliahidiwa mambo makubwa na Mungu, ikiwemo kudumishiwa kiti chake cha enzi milele, lakini kutokana na mapito na masumbufu mengi aliyokuwa anapitia na kukawia katika ufalme, ilionekana kama jambo hilo haliwezekani..Lakini hakuacha kumwomba Mungu, azitazame ahadi zake asiabike, kwa kumtumaini yeye.
Zaburi 89:49 Bwana, zi wapi fadhili zako za kwanza, Ulizomwapia Daudi kwa uaminifu wako? 50 Ee Bwana, ukumbuke, Wanavyosimangwa watumishi wako; Jinsi ninavyostahimili kifuani mwangu Masimango ya watu wengi. 51 Ambayo adui zako wamesimanga, Ee Bwana, Naam, wamezisimanga hatua za masihi wako. 52 Na ahimidiwe Bwana milele. Amina na Amina.
Hapo ndio utaona sasa kwanini sehemu nyingi, kwenye Zaburi Daudi anamwambia Bwana, akumbuke asiabike milele, kwa kuzitumainia fadhili zake..
Lakini katika agano jipya pia,
Nasi pia tunamtumaini Mungu ili tusiabike milele.Na Aibu kuu ni ile ya kutengwa na uso wa Mungu milele, ambayo watakutana nayo wenye dhambi, ile aibu ya kufukuzwa mbele ya uso wa Mungu.
2 Petro 3:13 Lakini, kama ilivyo ahadi yake, mnatazamia mbingu mpya na nchi mpya, ambayo haki yakaa ndani yake. 14 Kwa hiyo, wapenzi, kwa kuwa mnatazamia mambo hayo, fanyeni bidii ili mwonekane katika amani kuwa hamna mawaa WALA AIBU mbele yake.
Hiyo ndiyo Bwana atatuepusha nayo sisi tuliomtumainia.
Ni vema kufahamu kuwa tukiwa kama watoto wa Mungu, haimaanishi kuwa hatutaaibishwa au kudhalilishwa kwa ajili ya jina lake, vipindi hivyo tutapitia, lakini mwisho wetu utakuwa ni kutukuzwa katika utukufu mkuu milele..
Ni heri leo ukubali aibu ya kidunia, kuliko kukutana na ile ya Kristo wakati ule..
Mathayo 7:23 Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu.
Mathayo 25:31-34, 41
31 Hapo atakapokuja Mwana wa Adamu katika utukufu wake, na malaika watakatifu wote pamoja naye, ndipo atakapoketi katika kiti cha utukufu wake; 32 na mataifa yote watakusanyika mbele zake; naye atawabagua kama vile mchungaji abaguavyo kondoo na mbuzi; 33 atawaweka kondoo mkono wake wa kuume, na mbuzi mkono wake wa kushoto. 34 Kisha Mfalme atawaambia wale walioko mkono wake wa kuume, Njoni, mliobarikiwa na Baba yangu, urithini ufalme mliowekewa tayari tangu kuumbwa ulimwengu… 41 Kisha atawaambia na wale walioko mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake;
Bwana atusaidie.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Yuaabisha kichwa chake! Je ni aibu ya namna gani? (1Wakorintho 11:5)
Aibusu midomo atoaye jawabu la haki (Mithali 24:26)
Kwa aibu yako mwenyewe, na kwa aibu ya uchi wa mama yako.
Print this post