Hili ni moja ya swali lenye mtafaruku mkubwa sana miongoni mwa wakristo, na wengi hata wameishia mpaka kugombana kabisa!..Wapo wanaoamini kanisa litapitia dhiki kuu ndipo linyakuliwe na wapo wanaoamini kanisa halitapita dhiki kuu, yaani utaanza kwanza unyakuo ndipo dhiki kuu ifuate.
Kuna kitu kimoja cha kimaandiko ambacho hakijulikani na wengi..nacho ni Mgawanyiko wa ujio wa Kristo;
Ujio huu umegawanyika katika vipengele vikuu 3, mtu akishindwa kuvielewa vipengele hivi basi biblia itamchanganya. Na vipengele hivyo ni kama ifuatavyo.
Huu ni ule wakati Kristo alipozaliwa na Bikira Mariamu, na kuishi kwa miaka 33 na nusu na kisha kufa, na kufufuka na kupaa mbinguni alikotoka.
Huu utahusisha Kristo kuwapokea wateule wake mawinguni katika tendo maarufu lijulikanalo kama unyakuo. Wakati huo, wafu waliopo makaburini watafufuka wataungana na watakatifu walio hai na kwa pamoja watakwenda mawinguni kumlaki Bwana. Katika Ujio huu Kristo hatashuka duniani, atabaki mawinguni, watakaonyakuliwa ndio watakaokwenda mawinguni kumfuata na kwenda naye mbinguni kwenye makao waliyoandaliwa.
Katika hatua hii ndio litatimia lile neno.. la kwenye Luka 17:34
“Nawaambia, usiku huo watu wawili watakuwa katika kitanda kimoja; mmoja atatwaliwa, mmoja ataachwa. 35 Wanawake wawili watakuwa wakisaga pamoja; mmoja atatwaliwa, mmoja ataachwa. 36 Watu wawili watakuwa shambani, mmoja atatwaliwa, mmoja ataachwa”.
“Nawaambia, usiku huo watu wawili watakuwa katika kitanda kimoja; mmoja atatwaliwa, mmoja ataachwa.
35 Wanawake wawili watakuwa wakisaga pamoja; mmoja atatwaliwa, mmoja ataachwa.
36 Watu wawili watakuwa shambani, mmoja atatwaliwa, mmoja ataachwa”.
Vilevile lile Neno “atakuja kama mwivi usiku”, ndio litatimia katika hatua hii..Pengine utakuwa umelala na mume wako/mke wako aliyeokoka na ghafla! utapoamka asubuhi hutamkuta kitandani. n.k.
Huu hautakuwa ujio wa kila jicho kumwona Yesu, kwasababu hatakuja kwa hukumu bali kwa ajili ya kuwachukua wateule wake na kwenda nao mbinguni kwenye karamu aliyowaandalia, ili kuwaepusha na dhiki ambayo itakwenda kuanza duniani muda sio mrefu. Dhiki ambayo inajulikana kwa jina lingine kama saa ya kuharibiwa ulimwengu!.
Ufunuo 3:10 “Kwa kuwa umelishika neno la subira yangu, mimi nami nitakulinda, utoke katika saa ya kuharibiwa iliyo tayari kuujilia ulimwengu wote, kuwajaribu wakaao juu ya nchi”.
Sasa huo sio wakati wa kila jicho kumwona Yesu mawinguni, wakati wa kila jicho kumwona utakuwa ni wakati wa ujio wa tatu, ambao tutauona mbele kidogo.
Sasa kabla ya kwenda hatua ya mwisho ya Ujio wa tatu, hebu tujiulize maswali machache juu ya huu ujio wa pili.
Na wakati wa kila jicho kumwona Kristo, biblia inasema Mataifa yote wataomboleza..na milima itahama na visiwa, kutakuwa na tetemeko kubwa la nchi, na jua litazima na mwezi utakuwa mwekundu kama damu. Kwa ufupi mwisho wa dunia utakuwa umefika..Sasa kama mambo hayo yote yatatokea katika siku ile ya unyakuo, ni nani atakuwa amelala kitandani, au yupo shambani analima, katikati ya dhiki kubwa namna hiyo, huyo mpinga-Kristo atatokea wapi na atawapa watu chapa muda gani?..
Kwahiyo ni wazi kuwa siku ya unyakuo ni nyingine na siku ya Ujio wa Kristo ambao kila jicho litamwona nayo ni nyingine. Haiwezekani siku ya unyakuo ndio iwe siku hiyo hiyo ya kila jicho kumwona, na visiwa na milima kuhama.
Sasa twende hatua ya mwisho ya tatu.
UJIO WA TATU:
Baada ya unyakuo kupita katika ujio wa pili, baadhi ya watu watatoweka, na dunia haitaelewa chochote, wengi watahisi watu wamepotea tu, kama ilivyo kawaida ya watu kupotea potea na kupatikana, na wengine wengi watajua ni habari za kuzusha tu!..taarifa chache zitafika vituoni, lakini mwisho zitaishia kupuuziwa… Kama baadhi ya taarifa za watu kupotea zinavyopuuzwa leo. Pasipo kujua kuwa Kristo tayari kashalinyakua kanisa lake (kundi dogo). Na siku hiyo hakutakuwa na ishara yoyote angani, wala jua halitazima..kutakuwa na ukimya tu kama wa siku zote.
Sasa katikati ya hicho kipindi, ndio utakuwa wakati wa mpinga-kristo kunyanyuka…Ndani ya miaka mitatu na nusu ya kwanza (yaani miezi 42), utakuwa ni wakati wa mpinga-kristo kuwadanganya watu waipokee chapa yake..wengi wataipokea chapa pasipo kujua, wakidhani ni mfumo mpya tu! Wa kimaendeleo umezuka, ambao utasaidia watu kutambulika kirahisi..Utakubalika duniani kwa muda mfupi sana, kiasi kwamba mtu atakayeukataa atakuwa anaenda kinyume na serikali, hivyo atatafutwa na kusingiziwa mambo yasiyofaa.
Wachache sana wataipokea kwa kujua, kwa kujua kabisa kwamba hii ni chapa, lakini wengi hawatajua..kwasababu mpinga-kristo hatakuwa mtu mwenye mapembe kama watu wanavyofikiri, bali atakuwa ni mtu mwenye ushawishi mkubwa sana wa kisiasa, kidini, kiuchumi na kijeshi, na anatakua ni mtu anayeshika biblia!. Hivyo hatajulikana na wengi kuwa ndiye mpinga-kristo mwenyewe, kwasababu ataheshimika kama kiongozi wa dini, atakayeleta amani..hivyo atapewa nguvu na dunia nzima.
Baada ya miaka mitatu na nusu ya kwanza kuisha, wale wachache ambao wataikataa chapa yake hiyo ndio watakaoanza kuipitia DHIKI KUU, wengine hawataguswa!..wataendelea na shughuli zao za KUUZA NA KUNUNUA bila usumbufu!…Lakini walioikataa watajaribu kujificha lakini watakamatwa na kupewa shutuma za uongo na hivyo kukusanywa katika magereza maalumu ya mateso…wakiwa humo watateswa mateso ambayo hayajawahi kutokea tangu dunia kuumbwa…na watamani kufa lakini wale waliowafunga hawatawaua mapema!!…
Lakini mwisho wa siku watakufa wote….na karibia na mwisho ya hiyo miaka mitatu na nusu ya mwisho, wataisha wote…Ndipo Mungu ataanza kuwapiga wanadamu wote waliopokea hiyo chapa ya mnyama kwa yale mapigo ya VITASA SABA, tunayoyasoma katika ufunuo 16. Kwahiyo DHIKI KUU, itaongezewa juu yake vitasa saba..Na Mwisho kabisa, miaka hiyo ya dhiki na vitasa itakapoisha, biblia inasema Jua litatiwa giza, na mwezi utakuwa mwekundu kama damu, Ishara ya mwana wa Adamu itaanza kuonekana mbinguni..
Bwana Yesu mwenyewe Mfalme wa wafalme atatokea mawinguni pamoja na jeshi kubwa na watakatifu walionyakuliwa…Atashuka kwa ajili ya vita vya Harmagedoni, na kwaajili ya utawala wa miaka elfu duniani.
Sasa siku hii kwa wale wachache ambao watakuwa wamesalia duniani, ambao waliipokea chapa lakini hawakufa katika mapigo ya vitasa saba..Wataona umeme ukimulika kutoka mashariki hata magharibi!..na dunia yote itakuwa giza ghafla (jua litazimwa)!…Na watamwona Kristo mawinguni, uso wake uking’aa kuliko jua…Hofu kuu itawaangukia wataomboleza kwa hofu, biblia inasema watatamani milima iwaangukie..
Mathayo 24:29 “Lakini mara, baada ya dhiki ya siku zile, jua litatiwa giza, na mwezi hautatoa mwanga wake, na nyota zitaanguka mbinguni, na nguvu za mbinguni zitatikisika; 30 ndipo itakapoonekana ishara yake Mwana wa Adamu mbinguni; ndipo mataifa yote ya ulimwengu watakapoomboleza, nao watamwona Mwana wa Adamu akija juu ya mawingu ya mbinguni pamoja na nguvu na utukufu mwingi 31 Naye atawatuma malaika zake pamoja na sauti kuu ya parapanda, nao watawakusanya wateule wake toka pepo nne, toka mwisho huu wa mbingu mpaka mwisho huu.”.
Mathayo 24:29 “Lakini mara, baada ya dhiki ya siku zile, jua litatiwa giza, na mwezi hautatoa mwanga wake, na nyota zitaanguka mbinguni, na nguvu za mbinguni zitatikisika;
30 ndipo itakapoonekana ishara yake Mwana wa Adamu mbinguni; ndipo mataifa yote ya ulimwengu watakapoomboleza, nao watamwona Mwana wa Adamu akija juu ya mawingu ya mbinguni pamoja na nguvu na utukufu mwingi
31 Naye atawatuma malaika zake pamoja na sauti kuu ya parapanda, nao watawakusanya wateule wake toka pepo nne, toka mwisho huu wa mbingu mpaka mwisho huu.”.
Soma tena…
Ufunuo 6:12 “Nami nikaona, alipoifungua muhuri ya sita, palikuwa na tetemeko kuu la nchi; JUA LIKAWA JEUSI KAMA GUNIA LA SINGA, MWEZI WOTE UKAWA KAMA DAMU, 13 na nyota zikaanguka juu ya nchi kama vile mtini upukutishavyo mapooza yake, utikiswapo na upepo mwingi. 14 Mbingu zikaondolewa kama ukurasa ulivyokunjwa, na kila mlima na kisiwa kikahamishwa kutoka mahali pake. 15 Na wafalme wa dunia, na wakuu, na majemadari, na matajiri, na wenye nguvu, na kila mtumwa, na mwungwana, wakajificha katika pango na chini ya miamba ya milima, 16 WAKIIAMBIA MILIMA NA MIAMBA, TUANGUKIENI, TUSITIRINI, MBELE ZA USO WAKE YEYE AKETIYE JUU YA KITI CHA ENZI, NA HASIRA YA MWANA-KONDOO. 17 Kwa maana siku iliyo kuu, ya hasira yao, imekuja; naye ni nani awezaye kusimama?.
Ufunuo 6:12 “Nami nikaona, alipoifungua muhuri ya sita, palikuwa na tetemeko kuu la nchi; JUA LIKAWA JEUSI KAMA GUNIA LA SINGA, MWEZI WOTE UKAWA KAMA DAMU,
13 na nyota zikaanguka juu ya nchi kama vile mtini upukutishavyo mapooza yake, utikiswapo na upepo mwingi.
14 Mbingu zikaondolewa kama ukurasa ulivyokunjwa, na kila mlima na kisiwa kikahamishwa kutoka mahali pake.
15 Na wafalme wa dunia, na wakuu, na majemadari, na matajiri, na wenye nguvu, na kila mtumwa, na mwungwana, wakajificha katika pango na chini ya miamba ya milima,
16 WAKIIAMBIA MILIMA NA MIAMBA, TUANGUKIENI, TUSITIRINI, MBELE ZA USO WAKE YEYE AKETIYE JUU YA KITI CHA ENZI, NA HASIRA YA MWANA-KONDOO.
17 Kwa maana siku iliyo kuu, ya hasira yao, imekuja; naye ni nani awezaye kusimama?.
Sasa utauliza hao wateule ambao Bwana atawakusanya wakati wa kutokea mawinguni kwa utukufu mwingi ni wakina nani?
Hao watakuwa ni Wayahudi 144,000, waliotiwa muhuri wa Mungu baada ya kuisikia ile injili ya manabii wawili wa kwenye Ufunuo 11, hivyo walifichwa mbali na mpinga-kristo na dhiki ya vitasa (Ufunuo 12:14-15). Kundi hili la wayahudi 144,000 ambao walifichwa mbali na yule joka…Ndio wanaoitwa wateule..
Hawa wakati Kristo atakaokuja ndio watakaokusanywa kutoka pepo nne, na kuletwa juu ya mlima Sayuni uliopo pale Israeli..(Ufunuo 14:1 “ Kisha nikaona, na tazama, huyo Mwana-Kondoo amesimama juu ya mlima Sayuni, na watu mia na arobaini na nne elfu pamoja naye, wenye jina lake na jina la Baba yake limeandikwa katika vipaji vya nyuso zao”).
Kwahiyo sio kanisa ambalo litakusanywa kutoka pembe nne, bali ni wayahudi hao 144,000, ambao waliisikia ile injili iliyohubiriwa na wale manabii wawili katika Ufunuo 11, na kutiwa muhuri wa Mungu juu ya vipaji vya nyuso zao…Kanisa tayari lilikuwa utukufuni, na ndio linalorudi na Kristo hapa!.
Sasa upo utata mmoja maarufu katika Ufunuo 7:9-16..Tusome
“ 9 Baada ya hayo nikaona, na tazama, mkutano mkubwa sana ambao hapana mtu awezaye kuuhesabu, watu wa kila taifa, na kabila, na jamaa, na lugha, wamesimama mbele ya kile kiti cha enzi, na mbele za Mwana-Kondoo, wamevikwa mavazi meupe, wana matawi ya mitende mikononi mwao; 10 wakilia kwa sauti kuu wakisema, Wokovu una Mungu wetu aketiye katika kiti cha enzi, na Mwana-Kondoo………………………… 13 Akajibu mmoja wa wale wazee akiniambia, Je! Watu hawa waliovikwa mavazi meupe ni akina nani? Na wametoka wapi? . 14 Nikamwambia, Bwana wangu, wajua wewe. Akaniambia, Hao ndio wanatoka katika dhiki ile iliyo kuu, nao wamefua mavazi yao, na kuyafanya meupe katika damu ya Mwana-Kondoo. 15 Kwa hiyo wako mbele ya kiti cha enzi cha Mungu, nao wanamtumikia mchana na usiku katika hekalu lake, na yeye aketiye katika kiti cha enzi atatanda hema yake juu yao. 16 Hawataona njaa tena, wala hawataona kiu tena, wala jua halitawapiga, wala hari iliyo yote”
“ 9 Baada ya hayo nikaona, na tazama, mkutano mkubwa sana ambao hapana mtu awezaye kuuhesabu, watu wa kila taifa, na kabila, na jamaa, na lugha, wamesimama mbele ya kile kiti cha enzi, na mbele za Mwana-Kondoo, wamevikwa mavazi meupe, wana matawi ya mitende mikononi mwao;
10 wakilia kwa sauti kuu wakisema, Wokovu una Mungu wetu aketiye katika kiti cha enzi, na Mwana-Kondoo…………………………
13 Akajibu mmoja wa wale wazee akiniambia, Je! Watu hawa waliovikwa mavazi meupe ni akina nani? Na wametoka wapi? .
14 Nikamwambia, Bwana wangu, wajua wewe. Akaniambia, Hao ndio wanatoka katika dhiki ile iliyo kuu, nao wamefua mavazi yao, na kuyafanya meupe katika damu ya Mwana-Kondoo.
15 Kwa hiyo wako mbele ya kiti cha enzi cha Mungu, nao wanamtumikia mchana na usiku katika hekalu lake, na yeye aketiye katika kiti cha enzi atatanda hema yake juu yao.
16 Hawataona njaa tena, wala hawataona kiu tena, wala jua halitawapiga, wala hari iliyo yote”
Mstari huu ndio unaowafanya wengi wahitimishe kwamba dhiki kuu itaanza ndipo tuende mbinguni…Lakini hebu soma vizuri mstari huo wa 9 unasema “nikaona, na tazama, mkutano mkubwa sana ambao hapana mtu awezaye kuuhesabu, watu wa kila taifa, na kabila, na jamaa, na lugha, wamesimama mbele ya kile kiti cha enzi”.
Hapa ni mbinguni baada ya unyakuo…na sio kundi moja la watu Fulani tu! Bali ni la watu wote (sio tu walio hai) bali hata waliokufa katika Kristo katika vizazi vyote vya nyuma, wakina Petro waliokatwa vichwa, wakina Stephano waliopigwa mawe, wakina Perpetua waliopitia dhiki za kuwekwa kwenye maarena na kufunguliwa Wanyama wakali, wakina Polikapi waliochomwa moto, wakina Antipa na wengine wengi na hata wakristo wote wanaopitia dhiki za kiimani hata sasa ambao watakuwa hai mpaka ile siku ya kunyakuliwa….
Sasa wote hawa kwa pamoja ndio wanaolijenga hilo jeshi kubwa hapo juu la Ufunuo 7…Kwahiyo hilo sio kundi moja tu la watu Fulani tu wachache!..bali ni la watu wa vizazi vyote waliokufa katika Kristo(Na mbele za Mungu, ni washindi wa dhiki za ulimwengu, kama Bwana Yesu alivyosema “ulimwenguni mnayo dhiki”). Mbinguni hakutakuwa na makundi mawili; ya waliopitia dhiki na ambao hawajapitia dhiki, ndio maana unaona hapo hakuna makundi mawili, bali kundi moja tu!.
Huo ni ufupisho tu kwa yatakayotokea siku za mwisho…Hivyo kwa hitimisho ni kwamba kanisa halitapitia Dhiki kuu ya mpinga-kristo… “litaepushwa na saa ya kuharibiwa”..watakaopitia dhiki kuu ya mpinga-kristo ni wale watakaoachwa kwenye unyakuo..na watauawa na mpinga-kristo (na hawatakuwa miongoni mwa watakaokwenda mbinguni), wataikosa karamu ya Mungu mbinguni ingawa wakati wa Kristo kurudi na watakatifu, watafufuliwa na kuingia katika utawala wa miaka elfu hapa duniani.
Na siku ya unyakuo sio siku ya kila jicho kumwona Yesu mawinguni, sio siku ya mataifa yote kuomboleza.
Sasa ni kitu gani kinachowafanya watu wachanganyikiwe?
Ni kwasababu ya kutoelewa kalenda ya Neno la Mungu…Ni wachache sana wanalijua na kulielewa andiko la kwenye Warumi 11, linalozungumzia Upofu waliopigwa Wayahudi (yaani waisraeli). Upofu huo walipigwa wasimwamini Masihi, Yesu Kristo ili sisi watu wa mataifa tupate Neema (hebu tenga muda binafsi soma taratibu Warumi 11 yote).
Kutokana na upofu waliopigwa iliwafanya wasimwamini kabisa Yesu, na kujikuta wakimtazamia Masihi mwingine. Na sisi watu wa Mataifa ikawa ni nafasi kwetu kumwamini, kwani wale mitume ambao walipaswa watumwe kwa wayahudi walikuja kwetu na sisi tukamwamini Yesu, macho yetu yakafunguliwa..tukaipokea hiyo neema. Na tumekaa na hiyo neema sasa kwa Zaidi ya miaka 2,000, ndio maana huoni ugumu leo kuhubiri injili ya Yesu na watu wakamwamini kirahisi tu!..Neema hii haipo kwa Waisraeli unaowaona leo!..Ukienda Israeli ukiwaeleza Habari za Yesu, wanakuona ni mwendawazimu…wanakupinga kabisa!..ni wachache sana wanaomwamini, lakini Zaidi ya asilimia 90 ya waisraeli wanamkataa Yesu. Na hiyo ni kutokana na upofu waliopigwa..yaani neema waliyopokonywa ili tupewe sisi.
Lakini biblia inasema katika hiyo hiyo warumi 11…kwamba hawatakuwa katika hiyo hali ya kutomwamini Yesu milele. Itafika siku ambapo macho yao yatafumbuliwa..Siku hiyo itakuwa ni zamu ya watu wa mataifa kupitia ukame wa rohoni kama wanayoipitia sasa waisraeli.
Siku hiyo itakuwa ni siku ya Neema ya wokovu kuondoka kwa watu wa Mataifa milele na kuhamia Israeli. Sasa Neema hiyo itahitimishwa na tukio la unyakuo. Kristo atakapolinyakua tu kanisa lake, na Mlango wa Neema siku hiyo hiyo utakuwa umefungwa kwa watu wa Mataifa na kubakia kwa waisraeli peke yao. Huku hata mtu aombe vipi, hakuna rehema. Roho Mtakatifu atahamia kwa Waisraeli, watahuzunika sana na kujilaumu ilikuwaje kuwaje mpaka wakamkataa Masihi kwa miaka yote hiyo…
Kwa kupitia injili ya wale manabii wawili, ndio watapatikana idadi ile 144,000 (Haijulikani kama ndio namba kamili, au ni ya kuwakilishi tu, kwamba idadi inaweza kuwa kubwa Zaidi ya hiyo). Lakini hao tu ndio watakaosalimika, ndio wateule, na watakusanywa katika Mlima Sayuni.
Warumi 11:25 “Kwa maana, ndugu zangu, sipendi msiijue siri hii, ili msijione kuwa wenye akili; ya kwamba kwa sehemu ugumu umewapata Israeli, mpaka utimilifu wa Mataifa uwasili. 26 Hivyo Israeli wote wataokoka; kama ilivyoandikwa, Mwokozi atakuja kutoka Sayuni; Atamtenga Yakobo na maasia yake. 27 Na hili ndilo agano langu nao, Nitakapowaondolea dhambi zao”.
Warumi 11:25 “Kwa maana, ndugu zangu, sipendi msiijue siri hii, ili msijione kuwa wenye akili; ya kwamba kwa sehemu ugumu umewapata Israeli, mpaka utimilifu wa Mataifa uwasili.
26 Hivyo Israeli wote wataokoka; kama ilivyoandikwa, Mwokozi atakuja kutoka Sayuni; Atamtenga Yakobo na maasia yake.
27 Na hili ndilo agano langu nao, Nitakapowaondolea dhambi zao”.
Sasa hapa kwenye WAKATI WA MATAIFA na WAKATI WA WAYAHUDI, ndiko kunakowafanya watu washindwe kuuelewa ujio wa Bwana. Asilimia kubwa ya watu hawajui kuwa kuna wakati wa Wayahudi kurudiwa na kumwamini mwokozi…wengi wanajua tu! Kuna unyakuo basi!…kwamba baada ya unyakuo hakuna chochote kitakachoendelea, na wanaamini kuwa mbinguni tutakaa huko milele, wala hakuna wakati tutarudi tena huko..Hawajui kwamba kuna utawala wa miaka elfu wa kutawala na Kristo duniani unatungoja. N.k
Tukiyajua hayo..huu sio wakati wa kucheza na Neema tuliyopewa sisi watu wa mataifa hata kidogo…Sasahivi unaweza kusikia injili, ukaikataa kwa mdomo lakini moyoni mwako ukashuhudiwa kwamba ni kweli yanayozungumzwa…Hicho kinachokushuhudia ndani yako ni sauti ya wito wa Mungu (Ni neema ya Mungu bado inatuita)..Itafika kipindi itaondoka kabisa…itahamia Israeli.. na hiyo sauti ya Roho Mtakatifu itakapoondoka..Ndipo mpinga-kristo atafunuliwa.
2Wathesalonike 2:7 “Maana ile siri ya kuasi hivi sasa inatenda kazi; lakini yuko azuiaye sasa, hata atakapoondolewa. 8 Hapo ndipo atakapofunuliwa yule asi, ambaye Bwana Yesu atamwua kwa pumzi ya kinywa chake, na kumwangamiza kwa ufunuo wa kuwapo kwake”
2Wathesalonike 2:7 “Maana ile siri ya kuasi hivi sasa inatenda kazi; lakini yuko azuiaye sasa, hata atakapoondolewa.
8 Hapo ndipo atakapofunuliwa yule asi, ambaye Bwana Yesu atamwua kwa pumzi ya kinywa chake, na kumwangamiza kwa ufunuo wa kuwapo kwake”
Bwana atubariki.
Jiunge na kundi letu la mafundisho ya Biblia whatsapp kwa kubofya hapa > Group-whatsapp
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
MAJONZI YA MTUME PAULO KWA NDUGU ZAKE.
YONA: Mlango wa 3
NA YEYE ALIYEKETI JUU YA WINGU AKAUTUPA MUNDU WAKE JUU YA NCHI, NCHI IKAVUNWA.
Kile kinara cha Taa ndani ya Hekalu la Sulemani kilikuwa kinawakilisha nini?
YAKINI NA BOAZI.
NEEMA YA MZALIWA WA PILI.
MKUMBUKE MKE WA LUTU.
JINSI SODOMA NA GOMORA ILIVYOKUWA INAVUTIA SANA..
Rudi Nyumbani:
Print this post
Zaburi 91, Ni Zaburi iliyo ya kipekee sana yenye nguvu, Na shetani analijua hilo, ukitaka kuamini jiulize, ni kwanini Shetani aliitumia Zaburi hii kumjaribu Bwana,? Kiasi kwamba mtego wake ungekubali basi Zaburi hii ndio ingekuwa silaha ya kumwangushia Bwana.
Ni kwanini ainukuu Zaburi 91? Shetani aliijua nguvu na ulinzi Mungu aliouweka juu ya wampendao..Lakini wengi wetu hatuifahamu…Alimwambia hivi Bwana..
Mathayo 4:6 “akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu jitupe chini; kwa maana imeandikwa, Atakuagizia malaika zake; Na mikononi mwao watakuchukua; Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe. 7 Yesu akamwambia, Tena imeandikwa, Usimjaribu Bwana Mungu wako”.
Mathayo 4:6 “akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu jitupe chini; kwa maana imeandikwa, Atakuagizia malaika zake; Na mikononi mwao watakuchukua; Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe.
7 Yesu akamwambia, Tena imeandikwa, Usimjaribu Bwana Mungu wako”.
Unaona, alijua kuwa mtu yeyote aliyempendeza Mungu, huwa anaachiliwa ulinzi wa kipekee, Mungu anamuagizia mpaka malaika zake, wamlinde, asijikwae,..
Hivyo kama wewe umeokoka na umesimama vizuri basi fahamu Zaburi 91, Ni salaha yako madhubuti ya kummaliza shetani na vitisho vyake, na majeshi yake..Isipokuwa tu usiitumie hiyo kwa lengo la kumjaribu Mungu, vinginevyo utampa shetani nafasi ya kukuangusha kama alivyojaribu kufanya kwa Bwana Yesu.
Embu tuisome,
ZABURI 91 1 Aketiye mahali pa siri pake Aliye juu Atakaa katika uvuli wake Mwenyezi. 2 Nitasema, Bwana ndiye kimbilio langu na ngome yangu, Mungu wangu nitakayemtumaini. 3 Maana Yeye atakuokoa na mtego wa mwindaji, Na katika tauni iharibuyo.
ZABURI 91
1 Aketiye mahali pa siri pake Aliye juu Atakaa katika uvuli wake Mwenyezi.
2 Nitasema, Bwana ndiye kimbilio langu na ngome yangu, Mungu wangu nitakayemtumaini.
3 Maana Yeye atakuokoa na mtego wa mwindaji, Na katika tauni iharibuyo.
Bwana anasema, atakuepusha na mitego ya mwindaji(Shetani), na tauni iharibuyo..akiwa na maana atakulinda na magonjwa hatari mfano wa Tauni kama Corona..Unaona ikiwa wewe ni mtakatifu, huna haja ya kuwa na hofu.
Anaendelea kusema…
Zaburi 91:4 Kwa manyoya yake atakufunika, Chini ya mbawa zake utapata kimbilio; Uaminifu wake ni ngao na kigao. 5 Hutaogopa hofu ya usiku, Wala mshale urukao mchana, 6 Wala tauni ipitayo gizani, Wala uele uharibuo adhuhuri,
Zaburi 91:4 Kwa manyoya yake atakufunika, Chini ya mbawa zake utapata kimbilio; Uaminifu wake ni ngao na kigao.
5 Hutaogopa hofu ya usiku, Wala mshale urukao mchana,
6 Wala tauni ipitayo gizani, Wala uele uharibuo adhuhuri,
Ndugu uliyeokoka, Bwana atakulinda tu, huna haja ya kuogopa, iwe ni mchana au usiku atakuwa na wewe kukulinda na mikono ya magonjwa na maadui.
Zaburi 91:7 Ijapo watu elfu waanguka ubavuni pako. Naam, kumi elfu mkono wako wa kuume! Hata hivyo hautakukaribia wewe. 8 Ila kwa macho yako utatazama, Na kuyaona malipo ya wasio haki. 9 Kwa kuwa Wewe Bwana ndiwe kimbilio langu; Umemfanya Aliye juu kuwa makao yako. 10 Mabaya hayatakupata wewe, Wala tauni haitaikaribia hema yako.
Zaburi 91:7 Ijapo watu elfu waanguka ubavuni pako. Naam, kumi elfu mkono wako wa kuume! Hata hivyo hautakukaribia wewe.
8 Ila kwa macho yako utatazama, Na kuyaona malipo ya wasio haki.
9 Kwa kuwa Wewe Bwana ndiwe kimbilio langu; Umemfanya Aliye juu kuwa makao yako.
10 Mabaya hayatakupata wewe, Wala tauni haitaikaribia hema yako.
Haijalishi utaona ni wangapi, wanadondoka, au wanashindwa pembeni yako, wameanguka, lakini wewe Bwana atakuwa na wewe wakati wote kuhakikisha hushindwi wala hupatwi na mabaya hayo yote, hata kama utaonekana kama unashindwa,lakini mwisho wa siku ushindi utakuwa ni wako tu,
Zaburi 91:11 Kwa kuwa atakuagizia malaika zake Wakulinde katika njia zako zote. 12 Mikononi mwao watakuchukua, Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe. 13 Utawakanyaga simba na nyoka, Mwana-simba na joka utawaseta kwa miguu.
Zaburi 91:11 Kwa kuwa atakuagizia malaika zake Wakulinde katika njia zako zote.
12 Mikononi mwao watakuchukua, Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe.
13 Utawakanyaga simba na nyoka, Mwana-simba na joka utawaseta kwa miguu.
Unaona zaidi ya hiyo, Malaika wa Bwana watakuwa na wewe kukulinda kila wakati, usijikwae, na mabaya..Na hiyo yote ni kwasababu gani? Ni kwasababu, umempenda Mungu na umemtafuta kwa bidii, umemfanya yeye kuwa tegemeo lako, na ndio maaana anasema..
Chapisho hili limefadhiliwa na https://www.swisswatch.is/ washirika wetu.
Zaburi 91:14 Kwa kuwa amekaza kunipenda Nitamwokoa; na kumweka palipo juu, Kwa kuwa amenijua Jina langu. 15 Ataniita nami nitamwitikia; Nitakuwa pamoja naye taabuni, Nitamwokoa na kumtukuza; 16 Kwa siku nyingi nitamshibisha, Nami nitamwonyesha wokovu wangu.
Zaburi 91:14 Kwa kuwa amekaza kunipenda Nitamwokoa; na kumweka palipo juu, Kwa kuwa amenijua Jina langu.
15 Ataniita nami nitamwitikia; Nitakuwa pamoja naye taabuni, Nitamwokoa na kumtukuza;
16 Kwa siku nyingi nitamshibisha, Nami nitamwonyesha wokovu wangu.
Maneno ya faraja sana na yanayotia nguvu, lakini mpaka Mungu kukutamkia hivyo ujue ni lazima kwanza uwe ni mwana wake mpendwa, vinginevyo, hakuna ulinzi wowote, utaokao kwake utakufikia..
Ili Mungu akulinde na tauni (Corona) isikuue, au magonjwa mengine ya kutisha yaliyozuka duniani leo hii, ni lazima uwe mwana wake mpendwa, ili Mungu akulinde na maadui (mapepo na wachawi), Ili Mungu akuagizie malaika zake watembee na wewe kila wakati kama alivyofanya kwa Elisha..basi ni lazima kwanza ufanyike mwana wake.
Ndipo hapo nawe utakapoitamka Zaburi 91 kwa ujasiri wote, na iwe kweli na maana kwako. Kumbuka Zaburi hii ilimwingia sana shetani kichwani, na ndio maandiko pekee aliyoyatamka kwa kinywa katika biblia nzima, hiyo ni kuonyesha kuwa ni jinsi gani anaona wivu, kuona watoto wa Mungu wanapokea ulinzi wa kipekee kutoka kwa Mungu.
Maana yake ni kuwa ukimkosa leo Kristo, basi huwezi mshinda shetani, kwasababu ulinzi wa Mungu haupo juu yako.. Hivyo kama upo tayari leo kumpa Yesu maisha yako, basi uamuzi utakaofanya ni mzuri na wa busara sana..Kama ni hivyo fungua hapa kwa ajili ya maelekezo juu ya sala ya Toba.>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Tafadhali Share na wengine,
Whatsapp: +255789001312
TAZAMA, NASIMAMA MLANGONI.
AGANO LAKO LINABEBWA NA NANI?.
WEWE NI BWANA UNIPONYAYE.
KIAMA KINATISHA.
JIFUNZE KUJITOA KWA MUNGU NA KUWA MKARIBISHAJI.
UNYAKUO.
Shalom, jina la Bwana wetu libarikiwe daima.
Neno linatuambia..
“Ni huruma za Bwana kwamba hatuangamii, Kwa kuwa rehema zake hazikomi.
Ni mpya kila siku asubuhi..” (Maombolezo 3:22-23).
Na wewe usomaye ujumbe huu rehema za Bwana zisikome juu yako daima.
Leo tutajifunza kwa ufupi, mambo machache ya kuzingatia tunapokwenda nyumbani kwa Bwana aidha kuzungumza naye, au kumwabudu, inaweza ikawa ni kanisani, au kwenye semina, au popote pale unapoweza kumfanyia Mungu ibada.
Kama tunavyosoma katika agano la kale tunaona kuna wakati ulifika wa Sulemani kumjengea Mungu Nyumba (Hekalu) ambalo lingekuwa ni kitovu cha waisraeli wote, na mataifa yote ulimwenguni kumwabudia Mungu , na kufanyiwa upatanisho wa makosa yao kwa wakati ule.. Kama tunavyojua hekalu lile lilijengwa kwa kipindi cha Miaka 7, na katika ujenzi ule, kulikuwa na vigezo vingi sana vya kuzingatia, pamoja na vipimo. Na kila kitu kilichotengenezwa kule kilikuwa kilikuwa kinafunua jambo kubwa sana rohoni kwa kanisa la Sasa, wale makerudi waliowekwa kule walikuwa wanafunua jambo Fulani rohoni, vile vinara 7 vya taa, vilivyokuwa na maana yake pia, halikadhalika zile madhabahu za dhahabu na za shaba , zote zilikuwa na maana, na lile sanduku la agano, mpaka yale mapambo yaliyokuwa kule ndani.
Sasa, karibu na mwisho kabisa wa ujenzi ule, Sulemani aliongozwa kujenga vitu vingine viwili muhimu katika hekalu, navyo si vingine Zaidi ya nguzo kubwa mbili zilizosimama katika maingilio ya Hekalu. Nguzo hizo zilikuwa ni ndefu na pana..
Nguzo ya kwanza iliwekwa upande wa kulia mwa kuingilia hekaluni, Na nguzo pili iliwekwa upande wa kushoto.
Ile iliyokuwa upande wa Kulia iliitwa YAKINI.. Na ile iliyowekwa upande wa kushoto iliitwa BOAZI.
2Nyakati 3:17 “Akazisimamisha nguzo hizo mbele ya hekalu, moja upande wa kuume, na ya pili upande wa kushoto; akaliita jina la ile ya kuume Yakini, na jina la ile ya kushoto Boazi”
Sasa maana ya maneno hayo ni hii:
Yakini ni: IMEDHANIWA KUWA ATATHIBITISHA.
Na Boazi: IMEDHANIWA KUWA IMO NGUVU.
Kulikuwa hakuna namna yoyote kuhani aingie hekaluni, apitilize mpaka patakatifu pa patakatifu, kwenda kufanya mambo ya ibada asipite katikati ya hizo nguzo mbili. Zilikuwa kama mihimili ya hekalu.
Ikifunua kuwa yeyote atakayeingia kule avukapo nguzo hizo ni lazima jambo hilo liwe kichwani mwake, kuwa Mungu atathibitisha(Yakini), Na humo humo ndani pia ipo nguvu ya Mungu (Boazi).
Hivyo kuhani akiingia mule, kwa shughuli yoyote ile aidha ya upatanisho au ya kuwasilisha maombi ya watakatifu, kichwani mwake anauhakika kuwa ni lazima Mungu ajibu maombi yao yaani alithibitishe agano lake alioingia nao kwa kupitia Ibrahimu, Na vilevile anajua kuwa nguvu ya Mungu ipo mule, kwahiyo ni lazima awe makini kwa atayayafanya vinginevyo atakuwa anajitafutia kifo mwenyewe au hata matatizo kwa wana wa Israeli wote.
Nguzo hizo zilisimama kwa wakati wote hekalu lilipokuwepo.
Lakini Ni ujumbe gani tunapewa kwa agano jipya?
Biblia inafananisha kanisa la Kristo kama hekalu la Mungu, tunapotoka na kwenda nyumbani mwake au uweponi mwake, Sisi wote tunaenda kuwa kama makuhani wa Mungu, hivyo Bwana anataka kila mmoja wetu, ajue kuwa nguzo hizo mbili (yaani Yakini na Boazi) zimesimama mbele ya hekalu lake takatifu.
Anataka tujue kuwa tunapokwenda nyumbani mwake tufahamu kuwa Mungu yupo pale, ili kulithibitisha agano lake aliloingia na watakatifu kupitia Yesu Kristo.. Na kwamba unapokwenda kusali, au kumwabudu au kumwomba chochote, yupo pale kukusikia na kukujibu maombi yako, sawasawa na maneno ya Kristo (Yohana 14:13) Huo ni uhakika, Hivyo uingie ukijua jambo hilo kichwani kuwa Mungu ni Mungu mshika maagano.
Vilevile anataka ujue kuwa ipo nguvu yake kule ndani, Hivyo uwe makini pia usiende kidunia/kimazoea.. Wapo watu wanajiamulia tu kuingia kanisani wanavyotaka na mavazi yao kizinzi, wanaingia kanisani na vimini, na suruali, wakidhani kule wanaenda kukutana na miungu isivyoweza kufanya jambo lolote. Hawajua jengo likishaitwa kanisa, Au nyumba ya Mungu, tayari nguzo mojawapo itwayo Boazi imesimama pale nje!, yaani ndani imo nguvu kubwa sana ya Mungu, inayoua na kuhuisha.
Kwahiyo pale mtu anapoingia bila heshima, anakuwa anajitafutia mwenyewe laana..Hilo unapaswa ulijue hili binti wa Mungu, hilo unapaswa ujue kijana,.Unapokwenda kanisani, halafu unajua jana umetoka kuzini, na wakati huo huo unakwenda kushiriki meza ya Bwana,..Unajitafutia matatizo yako mwenyewe..(Soma hapa uone laana iliyowapata watu wa dizaini hiyo katika kanisa la Kristo IWakorintho 11:27-34)
Nyumba ya Mungu, si ya kuifanyia mzaha hata kidogo..
Marko 11:17 “Akafundisha, akasema, Je! Haikuandikwa, Nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala kwa mataifa yote? Bali ninyi mmeifanya kuwa pango la wanyang’anyi”.
Hivyo ndugu kama wewe ni mkristo, zingatia hayo mambo mawili, yaweke kichwani mwako daima Nyumbani mwake Mungu anathibitisha, na nyumbani mwake imo nguvu. (Yakini na Boazi)
Bwana akubariki.
Ikiwa hujaokoka, kumbuka leo tena tumepiga hatua nyingine ya kuukaribia ule mwisho, pengine itakuwa leo, au kesho asubuhi, au wiki hii au vyovyote vile, hatuhitaji kuishi maisha ya kubahatisha, hivyo tukiyajua hayo, ni wakati wa kuamka usingizini, na kuzisafisha taa zetu.. Mpe leo Kristo maisha yako ayaokoe. Ufanyike kuwa mwana wake.
MAWE YALIYOKWISHA KUCHONGWA MACHIMBONI.
KUOTA UMEFUNGA NDOA.
USIINGIE MKATABA NA DHAMBI.
IFANYE KAZI YA MUNGU PASIPO HOFU!
AHADI ZA MUNGU.
POPOBAWA NI KWELI YUPO?
WhatsApp
Je Kifo ni nini? Na kuna aina ngapi za vifo?
Kifo ni pale uhai unapoondoka ndani ya kiumbe hai chenyewe. Kwa ufupi kifo ni Mwisho wa Maisha ya mwilini.
Lakini katika Biblia vipo vifo vikuu vya aina tatu.
Kifo cha Mwilini:
Hichi ni pale mwili na roho vinapotengana. Kifo hichi kinamkuta kila mmoja wetu, pale anapomaliza safari yake ya Maisha ya duniani ikiwa unyakuo utakuwa haujakukuta basi utakufa na kuzikwa.
Mwanzo 3:19 “…. kwa maana u mavumbi wewe, nawe mavumbini utarudi”.
Kifo cha namna hii haikuhusishi roho ya mtu..Roho inakuwa bado inaendelea kuishi sehemu nyingine..Bwana Yesu alisema..
Mathayo 10:28 “Msiwaogope wauuao mwili, wasiweze kuiua na roho; afadhali mwogopeni yule awezaye kuangamiza mwili na roho pia katika jehanum.”
Kifo cha Rohoni:
Hichi ni kifo ambacho kinamkumba mtu kwa ndani, lakini kwa nje bado anakuwa anaendelea kuishi kana kwamba hakuna chochote kinachoendelea.. Na kifo cha namna hii, kila mmoja wetu anacho aidha kwa kujua au kwa kutokujua..Leo hii ikiwa Maisha yako yapo mbali na dhambi (yaani umeokoka), tayari wewe rohoni unaonekana kuna mauti imetokea ndani yako, yaani unaonekana tayari umeshakufa kwa Habari ya dhambi, biblia inasema hivyo..
Warumi 6:1 “Tuseme nini basi? Tudumu katika dhambi ili neema izidi kuwa nyingi? 2 Hasha! SISI TULIOIFIA DHAMBI tutaishije tena katika dhambi.. 6:11 “Vivyo hivyo ninyi nanyi jihesabuni kuwa wafu kwa dhambi na walio hai kwa Mungu katika Kristo Yesu”.
Warumi 6:1 “Tuseme nini basi? Tudumu katika dhambi ili neema izidi kuwa nyingi? 2 Hasha! SISI TULIOIFIA DHAMBI tutaishije tena katika dhambi..
6:11 “Vivyo hivyo ninyi nanyi jihesabuni kuwa wafu kwa dhambi na walio hai kwa Mungu katika Kristo Yesu”.
Vilevile ikiwa injili inahubiriwa kwako halafu hubadiliki, fahamu kuwa katika ulimwengu wa roho umekufa kwa Habari ya haki hata kama utakuwa unaishii..
1Timotheo 5:6 “Bali, yeye asiyejizuia nafsi yake amekufa ingawa yu hai”.
Kifo cha Roho:
Kifo hichi ndio kibaya Zaidi, Na ndio kifo cha mwisho kinachojulikana kama Mauti ya pili. Kifo hichi ni pale, unapotenganishwa moja kwa moja na uso wa Mungu milele, katika lile ziwa la moto.. Ambapo utatetezwa huko na roho yako itaangamia milele.
Ufunuo 20:13 “Bahari ikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake; na Mauti na Kuzimu zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake. Wakahukumiwa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake. 14 Mauti na Kuzimu zikatupwa katika lile ziwa la moto. Hii ndiyo mauti ya pili, yaani, hilo ziwa la moto. 15 Na iwapo mtu ye yote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto”.
Ufunuo 20:13 “Bahari ikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake; na Mauti na Kuzimu zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake. Wakahukumiwa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake.
14 Mauti na Kuzimu zikatupwa katika lile ziwa la moto. Hii ndiyo mauti ya pili, yaani, hilo ziwa la moto.
15 Na iwapo mtu ye yote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto”.
Lakini Pamoja na hayo sisi tulio ndani ya Kristo tunalo tumaini la uzima wa milele ikiwa tutakufa leo. Kwasababu Yesu Kristo ambaye alishinda mauti, atakuja kutufufua tena, katika hii hii miili yetu, kisha atatuvika miili mingine mipya ya utukufu ya kimbinguni isiyo kufa wala kuugua, wala isiyo na madhaifu, na hiyo ndiyo tutakayoishi nayo milele.
Lakini ikiwa wewe ni mwenye dhambi bado hujamkabidhi Kristo Maisha yako ayaokoe, ukifa leo hii, huna tumaini lingine lolote Zaidi ya kungojea ile mauti ya pili ambalo ni ziwa la moto..
Lakini kwanini hayo yote yatukute angali tunayo nafasi bado?..Ikiwa wewe ni mmojawapo ambaye yupo bado katika dhambi, Na leo hii unataka Bwana Yesu akuokoe, hutaki neema ya wokovu ikupitie, basi popote pale ulipo anaweza kukusamehe dhambi zako ikiwa tu utamaanisha kufanya hivyo.
Kama upo tayari kutubu sasa dhambi zako, basi fungua hapa kwa ajili ya maelekezo ya sala ya Toba. >>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Bwana akubariki sana.
Ikiwa umemfuata maelekezo hayo ya kuokoka, sasa, upo tayari kujifunza na masomo mengine ya rohoni.Tafadhali tazama chini vichwa vya masomo kisha bofya lolote upendalo uzidi kujifunza zaidi.
MAUTI YA PILI NI NINI?
NINI KINATOKEA BAADA YA KIFO?
MADHARA YA KUKOSA MAJI YA UZIMA BAADA YA KIFO.
RABI, UNAKAA WAPI?
KAMA MMOJA TU NDIO HIVI! SI ZAIDI 153?
Kwanini Mungu awachome watu kwenye ziwa la moto na hali yeye ndiye aliyewaumba?
KIFO CHA REINHARD BONKEY KINAACHA UJUMBE GANI KWETU?
PENGINE MUNGU ALISHASEMA NAWE KWA NJIA HII.
Ni watu gani hao ambao mahali pao hapakuonekana? (Ufunuo 20:11)
JIBU: Tusome..
Ufunuo 20:11 “Kisha nikaona kiti cha enzi, kikubwa, cheupe, na yeye aketiye juu yake; ambaye nchi na mbingu zikakimbia uso wake, na mahali pao hapakuonekana”.
Hao wanaozungumziwa hapo kwamba “mahali pao hapakuonekana” sio binadamu!..bali ni “MBINGU NA NCHI”. Tafsiri za lugha nyingine zinaelezea vizuri.
Na kwanini zikimbie uso wake?..ni kwasababu ya utukufu wake…kwasababu hakuna kitu chochote kinachoweza kusimama mbele ya uso wa Mungu kwa kuwa yeye mkuu sana na mtakatifu!. Maserafi tu waliopo mbinguni ambao ni watakatifu, bado wanafunika nyuso zao na miguu yao mbele yake..si Zaidi viumbe vilivyopo katika mbingu na nchi tulizopo sisi?.
Ayubu 41:10 “….BALI NI NANI AWEZAYE KUSIMAMA MBELE YANGU MIMI?
Hivyo hakuna kiumbe chochote ambacho kinaweza kumkaribia Mungu kwa ukamilifu wake. Lakini ashukuriwe Mungu kwa sababu yupo mmoja ALIYESTAHILI KUMKARIBIA YEYE, na huyo si mwingine Zaidi ya mwanawe wa pekee aliyemtoa ambaye yeye alishinda na kustahili kumkaribia Mungu, na kuketi Pamoja naye katika kiti chake..Huyo pekee ndiye aliyestahili kumkaribia Mungu…na kwa kupitia yeye sisi tuliompokea tumepata nafasi ya kumkaribia Mungu..
Ufunuo 3:21 “Yeye ashindaye, nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi”.
Ufunuo 5:11 “Nikaona nikasikia sauti ya malaika wengi pande zote za kile kiti cha enzi, na za wale wenye uhai, na za wale wazee, na hesabu yao ilikuwa elfu kumi mara elfu kumi na elfu mara elfu, 12 wakisema kwa sauti kuu, ASTAHILI MWANA-KONDOO ALIYECHINJWA, kuupokea uweza na utajiri na hekima na nguvu na heshima na utukufu na baraka. 13 Na kila kiumbe kilichoko mbinguni na juu ya nchi na chini ya nchi ya juu ya bahari, na vitu vyote vilivyomo ndani yake, nalivisikia, vikisema, Baraka na heshima na utukufu na uweza una yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na yeye Mwana-Kondoo, hata milele na milele”.
Ufunuo 5:11 “Nikaona nikasikia sauti ya malaika wengi pande zote za kile kiti cha enzi, na za wale wenye uhai, na za wale wazee, na hesabu yao ilikuwa elfu kumi mara elfu kumi na elfu mara elfu,
12 wakisema kwa sauti kuu, ASTAHILI MWANA-KONDOO ALIYECHINJWA, kuupokea uweza na utajiri na hekima na nguvu na heshima na utukufu na baraka.
13 Na kila kiumbe kilichoko mbinguni na juu ya nchi na chini ya nchi ya juu ya bahari, na vitu vyote vilivyomo ndani yake, nalivisikia, vikisema, Baraka na heshima na utukufu na uweza una yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na yeye Mwana-Kondoo, hata milele na milele”.
Hivyo tukimwamini na kuingia ndani yake tunapata ujasiri wa kumkaribia Mungu sana, jambo ambalo katika hali ya kawaida lisingekaa liwezekane kabisa, lakini limewezekana kwa kupitia Yesu, lakini tukimkataa huyu Yesu, basi hatuna ujasiri wowote na hatuwezi kumkaribia Mungu kamwe…Tutaukimbia uso wake na kutengwa naye milele katika ziwa la moto.
Waebrania 10:19 “Basi, ndugu, kwa kuwa tuna ujasiri wa kupaingia patakatifu kwa damu ya Yesu, 20 njia ile aliyotuanzia iliyo mpya, iliyo hai, ipitayo katika pazia, yaani, mwili wake; 21 na kuwa na kuhani mkuu juu ya nyumba ya Mungu; 22 na tukaribie wenye moyo wa kweli, kwa utimilifu wa imani, hali tumenyunyiziwa mioyo tuache dhamiri mbaya, tumeoshwa miili kwa maji safi”.
Waebrania 10:19 “Basi, ndugu, kwa kuwa tuna ujasiri wa kupaingia patakatifu kwa damu ya Yesu,
20 njia ile aliyotuanzia iliyo mpya, iliyo hai, ipitayo katika pazia, yaani, mwili wake;
21 na kuwa na kuhani mkuu juu ya nyumba ya Mungu;
22 na tukaribie wenye moyo wa kweli, kwa utimilifu wa imani, hali tumenyunyiziwa mioyo tuache dhamiri mbaya, tumeoshwa miili kwa maji safi”.
Shalom.
UFUNUO: Mlango wa 20
DANIELI: Mlango wa 1
HAPO NDIPO WATU WALIPOANZA KULIITIA JINA LA BWANA.
SIKU YA UNYAKUO ITAKUKUTAJE?
Kitabu cha YASHARI kinachozungumziwa katika 2Samweli 1:17-18, ni kitabu gani?
URIMU NA THUMIMU NI NINI KATIKA BIBLIA?
ALIYOKUTANA NAYO YESU, YERIKO.
ZIKIMBIE TAMAA ZA UJANANI! NA MTU YEYOTE ASIUDHARAU UJANA WAKO.
Usinipite mwokozi Lyrics| Swahili, – “Pass me not, O Gentle Savior”
Historia ya nyimbo Usinipite mwokozi.
Wimbo huu uliandikwa mwaka 1868, na mwanamke wa kimarekani aliyeitwa Fanny Crosby. Mwanamke huyu mkristo alizaliwa akiwa mzima lakini wiki 8 baada ya kuzaliwa kwake alipatwa na opofu, ambao ulidumu mpaka kufa kwake, lakini katika maisha yake yote aliyoishi hapa duniani (yaani miaka 94), haikuwa bure kwa Mungu wake, alifanikiwa kuandika nyimbo zaidi ya 8,000..Hivyo hiyo ikamfanya apate umaarufu na kumfanya ajulikane kwa jina la “mtunzi-kipofu-wa-nyimbo-za-tenzi”, na “Malkia wa nyimbo za Injili”.
Lakini siku moja alipokuwa amealikwa kwenda kuzungumza na wafungwa wa mji, na alipokuwa akitembea kule gerezani alimsikia mfungwa mmoja akisema “Bwana mwema usinipite, usinigeuzie mgongo wako,unikumbuke”,
Fanny anasema aliguswa sana na maneno yale, jambo ambalo halikuondoka kwenye kichwa chake mpaka alipofika nyumbani. Na huko ndipo alipoandika beti zote nne za wimbo ujulikanao kama USINIPITE MWOKOZI.
Alipomaliza kuuandika akampa muhusika wa kuweka midundo, na mwaka, 1870 wimbo huo, ulizinduliwa rasmi katika machapisho..
Na kwa kipindi kifupi` sana ukapata umaarufu mkubwa duniani kote.
*****
Jambo hili tunaliona kwa wale kipofu wawili waliomsikia Yesu anapita..
Mathayo 9:27 “Yesu alipokuwa akipita kutoka huko, vipofu wawili wakamfuata wakipaza sauti, wakisema, UTUREHEMU, MWANA WA DAUDI. 28 Naye alipofika nyumbani, wale vipofu walimwendea; Yesu akawaambia, Mnaamini kwamba naweza kufanya hili? Wakamwambia, Naam, Bwana. 29 Ndipo alipowagusa macho, akasema, Kwa kadiri ya imani yenu mpate”.
Mathayo 9:27 “Yesu alipokuwa akipita kutoka huko, vipofu wawili wakamfuata wakipaza sauti, wakisema, UTUREHEMU, MWANA WA DAUDI.
28 Naye alipofika nyumbani, wale vipofu walimwendea; Yesu akawaambia, Mnaamini kwamba naweza kufanya hili? Wakamwambia, Naam, Bwana. 29 Ndipo alipowagusa macho, akasema, Kwa kadiri ya imani yenu mpate”.
Na itakuwa hivyo na kwako:
Ikiwa wewe umeokoka, na unaona unapita katika hali ngumu, ambayo unaona kwa namna ya kawaida huwezi kutoka, basi wakumbuke watu kama hawa, wakutie nguvu,..Zidi kumwita Yesu, atakuonekania kwa wakati wake. Kwasababu yeye anatupenda na kutujali, na yote yanawezekana kwake.
Lakini kama hujaokoka, basi ni vizuri leo ukamwita kwanza mwokozi akuokoe maisha yako, usiruhusu akupite, anapokwenda kuwapa wengine uzima wa milele, sema na mimi leo nauhitaji huo uzima, hivyo kama upo tayari kufanya hivyo, basi fungua hapa, kwa ajili ya Sala ya Toba..>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Bwana akubariki..
Tazama historia ya nyimbo nyingine za Tenzi chini.
MWAMBA WENYE IMARA
CHA KUTUMAINI SINA lyrics
BWANA MUNGU NASHANGAA KABISA lyrics
NI SALAMA ROHONI MWANGU Lyrics
TENZI ZA ROHONI
Mungu aliposema Yesu ni mwanawe pekee, alimaanisha hakuwa na wengine?
MUONEKANO MPYA WA YESU BAADA YA KUFUFUKA.
Ni salama rohoni mwangu lyrics- It is well with my soul.
Nyimbo hii ilitungwa na mwanasheria mmoja mkristo aliyeitwa Horatio Spafford, alitunga wimbo huu kutokana na mambo mazito aliyoyapitia katika maisha yake, Matatizo yake yalianza kwa kufiwa na mtoto wake wa pekee wa kiume aliyekuwa na miaka minne, hiyo ilikuwa ni mwaka 1870
Muda mfupi baadaye (mwaka 1871) moto mkubwa uliozuka huko Chicago Marekani mjini kwake, ukaharibu mali zake nyingi ukizingatia alikuwa ni mwanasheria aliyekuwa amefanikiwa sana. Hilo likafuatana na biashara zake pia kuporomoka kutokana na anguko la uchumi lililotokea mwaka 1873, Hivyo ikambidi apange safari ya kwenda Ulaya pamoja na familia yake, Lakini aliahirisha safari kwa ajili ya kuweka mambo yake ya vibiashara vizuri yaliyokuwa yameathiriwa na moto, hivyo ikambidi msafirishe kwanz mkewe na mabinti zake wanne,akiahidi kuwa atawafuta baadaye.
Lakini Meli ilipokuwa inakatisha bahari ya atlantiki, ilizama ghafla kwa kugongana na meli nyingine na mabinti zake wote wanne wakafariki kwenye ajali hiyo akasalimika mke wake tu, akiwa kule Marekani alipokea ujumbe wa telegrafu kutoka kwa mke wake unaosema “Nimepona peke yangu” ndipo Spafford akaondoka kumfuata mkewe, na huko huko akauandika wimbo huu..
https://www.high-endrolex.com/15
Baadaye vina vingine vya mashairi viliongezwa ndipo ukazaliwa wimbo huu, Ni salama Rohoni Mwangu.
****
Nionapo amani kama shwari,
Ama nionapo shida;
Kwa mambo yote umenijulisha,
Ni salama rohoni mwangu.
Salama, Salama, Rohoni, Rohoni, Ni salama rohoni mwangu.
Salama, Salama,
Rohoni, Rohoni,
Ingawa Shetani atanitesa,
Nitajipa moyo kwani;
Kristo ameona unyonge wangu,
Amekufa kwa roho yangu.
Dhambi zangu zote, wala si nusu,
Zimewekwa Msalabani;
Wala sichukui laana yake,
Ee Bwana himiza siku ya kuja,
Panda itakapolia;
Utakaposhuka sitaogopa,
Hata sisi Je! Tunapopitia shida na magumu tunazo nguvu za kusema ni salama rohoni mwangu?, Tunapopitia njaa, tunapopitia misiba, tunapopitia matatizo mazito Je! Bado Tunaweza kumwambia shetani ni Salama rohoni mwangu? Kama ilivyokuwa kwa Ayubu?
Siku zote kumbuka hili Neno..
Mithali 24: 10 Ukizimia siku ya taabu, Nguvu zako ni chache.
Hivyo jipe moyo songa mbele ikiwa wewe ni mkristo, Kwasababu mwisho wa Mungu sikuzote ni mzuri, kama ilivyokuwa kwa Yusufu, kama ilivyokuwa kwa Ayubu, na ndivyo itakavyokuwa na kwako.
Yakobo 5:11 “Angalieni, twawaita heri wao waliosubiri. Mmesikia habari ya subira yake Ayubu, mmeuona mwisho wa Bwana ya kwamba Bwana ni mwingi wa rehema, mwenye huruma”.
Tazama chini historia ya nyimbo nyingine za Tenzi:
Jiunge na kundi letu la mafundisho ya Biblia whatsapp kwa kubofya hapa >> WHATSAPP-GROUP
Kwa maombezi/ubatizo/ Kumpokea Yesu. Wasiliana nasi kwa namba hizi; +255789001312/+255693036618
YATAMBUE MAJIRA YA KUJILIWA KWAKO.
YESU AKALIA KWA SAUTI KUU.
SWALI: Mungu aliposema Yesu ni mwanawe pekee, Je! Ina maana hakuwa na wana wengine au hana wana wengine zaidi yake?
Yohana 3:16 “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele”.
Hivyo ndivyo inavyotafsiriwa na watu wengi na madhehebu mengi ya dini..Lakini sivyo inavyomaanisha hapo, Mungu kumwita Yesu mwanawe pekee, haimaanishi, hajawahi kuwa na wana wengine,(ambao ndio sisi), bali alimaanisha Yesu ni mwana-wake-wa-kipekee tofauti na sisi wengine aliyebakiwa naye, mwenye mahusiano ya kitofauti na wengine, mwana wa maagano ndio maana akimwita Kristo mwanawe pekee.
Ili kulithibitisha jambo hilo embu tutazame baadhi ya vifungu vya maandiko vinavyoelezea habari inayofanana na hiyo, Na hiyo si nyingine zaidi ya ile ya Ibrahimu na mwanawe Isaka..tusome.
Mwanzo 22:2 “Akasema, Umchukue mwanao, mwana wako wa pekee, umpendaye, Isaka, ukaende zako mpaka nchi ya Moria, ukamtoe sadaka ya kuteketezwa huko juu ya mlima mmojawapo nitakaokuambia”.
Soma tena..
Mwanzo 22:12 “Akasema, Usimnyoshee kijana mkono wako, wala usimtendee neno; kwa maana sasa ninajua ya kuwa unamcha Mungu, iwapo hukunizuilia mwanao, mwanao wa pekee”.
Waebrania 11:17 “Kwa imani Ibrahimu alipojaribiwa, akamtoa Isaka awe dhabihu; na yeye aliyezipokea hizo ahadi alikuwa akimtoa mwanawe, mzaliwa pekee”;
Unaona ukisoma mistari hiyo yote, unaweza kudhani Isaka ndio aliyekuwa mwana tu wa Ibrahimu hakuwa na wengine, lakini tunajua kuwa kabla ya Isaka alikuwepo Ishmaeli. Na baada ya Isaka walikuja wengine wengi (Mwanzo 25:1-4).
Lakini ni kwanini Mungu amwite Isaka kama mwana pekee wa Ibrahimu, ni kwasababu alikuwa mwana wa maagano, mwana wa ahadi, tofauti na wale wengine,…Isaka alifananishwa na Kristo
Hivyo Kristo Bwana wetu ndio mwana pekee wa Mungu, ambaye ameshikilia maagano yetu yote, kwa kupitia yeye, Mungu ametupenda tena, kwa kupitia yeye sisi tumebarikiwa, na kwa kupitia yeye, tunapata uzima wa milele, na tumaini la ufufuo baada ya kifo. Hivyo tukimwamini na kumpokea tunaingia katika huo mnyororo wa Pendo la Mungu.
“Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye; msikieni yeye”. Kama hujampokea huu ni wakati wako sasa.
Au Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > Group-whatsapp
KUSUDI LA MIMI KUWEPO DUNIANI NI LIPI?
Neno la Mungu la leo.
UPENDO WA MUNGU.
KIFO CHA MTAKATIFU POLIKAPI (Policarp).
JE NI LAZIMA MKRISTO AOE/AOLEWE?
BWANA MUNGU NASHANGAA KABİSA lyrics ~Swahili (How Great Thou Art).
Toleo la kwanza kabisa la Wimbo huu liliandikwa na mtu mmoja raia wa Sweden, aliyeitwa Carl Boberg wimbo huu aliuandika mnamo mwaka 1885 baada ya kuvutiwa na mazingira aliyopishana nayo alipokuwa akitoka Kanisani yeye na marafiki zake. Anasema muda wa mchana walipokuwa njia hali ya hewa iliwabadilikia ghafla, wakaona wingu la tufani likitokea kwa mbali, na mara hiyo hiyo kukaanza kumulika mianga mingi kama ya radi angani, upepo mzuri ukaanza kuvuma juu ya mashamba yaliyokuwa pembeni, Na kisha manyunyu ya mvua matulivu yakaanza kudondoka juu yao, na baada ya muda kidogo, wingu lile la tufani likapotea, muda huo huo ukatokea upinde mzuri wa mvua angani..
Na alipofika nyumbani na kufungua madirisha atazame nje, aliona ufukwe ya mji wake kama vile kioo, akatazama upande wa pili akasikia ndege wazuri wakitoa milio yao na kwa mbali kegele za kanisa zikilia, Hapo ndipo wimbo huu ulipomjia kichwani kuutunga na kuuandika.
Bwana Mungu nashangaa kabisa,
Nikifikiri jinsi ulivyo,
Nyota, ngurumo, vitu vyote pia,
Viumbavyo kwa uwezo wako.
Roho yangu na ikuimbie, Jinsi wewe ulivyo mkuu, Roho yangu na ikuimbie, Jinsi wewe ulivyo mkuu.
Roho yangu na ikuimbie,
Jinsi wewe ulivyo mkuu,
Jinsi wewe ulivyo mkuu.
Nikitembea pote duniani,
Ndege huimba nawasikia,
Milima hupendeza macho sana,
Upepo nao nafurahia.
Nikikumbuka vile wewe Mungu,
Ulivyompeleka mwanao,
Afe azichukue dhambi zetu,
Kuyatambua ni vigumu mno.
Yesu Mwokozi atakaporudi,
Kunichukua kwenda mbinguni,
Nitaimba sifa zako milele,
Wote wajue jinsi ulivyo.
Tujiulize na sisi tunao utaratibu kwa kukaa chini na kuushangaa utukufu wa Mungu na kumtukuza?..Au kila kitu tunaona ni kawaida tu..Kumbuka Sifa kamili kama hizi mbele za Mungu ni bora kuliko dua na sala tunazompelekea kila siku.
Mungu anataka kuona, na sisi tukiufurahia uumbaji wake, kwa kumwimbia.
Ubarikiwe.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo ya biblia kwa email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312
ACHENI MJUE YA KUWA MIMI NI MUNGU.
USITUPE LULU ZAKO MBELE YA NGURUWE.
CHA KUTUMAINI SINA, Swahili Lyrics. (My hope is built on nothing less)
Tenzi hii iliandikwa na mchungaji wa kanisa la kipatisti, aliyeitwa Edward Mote, raia wa nchi ya uingereza, mnamo mwaka 1834, Edward Mote alifanikiwa pia kuandika tenzi nyingine nyingi Zaidi ya 100, lakini iliyopata umaarufu mkubwa ni hii ijulikanayo kama “Cha Kutumaini sina”.
Tenzi hii aliibuni akirejea ule mfano alioutoa Bwana Yesu wa mjenzi mwenye akili aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba imara, Na yule mpumbavu ambaye aliijenga nyumba yake https://www.high-endrolex.com/2juu ya mchanga (Mathayo 7:24-27), Na kuonyesha ni jinsi gani mtu anapaswa aishi kwa kwa kumtegemea Kristo aliye mwamba salama, na ulio imara.
1Wakorintho 10:4 “wote wakanywa kinywaji kile kile cha roho; kwa maana waliunywea mwamba wa roho uliowafuata; na mwamba ule ulikuwa ni Kristo”
Na ndio hapo akaundika wimbo huu;
Cha kutumaini sinaIla damu yake Bwana,Sina wema wa kutoshaDhambi zangu kuziosha;
Kwake Yesu nasimama,Ndiye mwamba; ni salamaNdiye mwamba ni salama
Njia yangu iwe ndefuYeye hunipa wokovu;Mawimbi yakinipigaNguvu zake ndiyo nanga.
Damu yake na sadakaNategemea daima,Yote chini yakiisha,Mwokozi atanitosha.
Nikiitwa hukumuni,Rohoni nina amani;Nikivikwa haki yakeSina hofu mbele zake.
Amen hata mimi na wewe, tukiwa ndani ya Kristo, tupo salama wakati wote, lakini tukimkosa yeye ndani yetu, basi hata kuimba kwetu ni bure, tutakuwa tu sawa na yule mpumbavu aliyejenga nyumba yake juu ya mchanga..
Hivyo ukiwa unahitaji kuokoka ili Yesu leo awe kweli Mwamba ulio salama, basi fungua hapa kwa sala ya toba >>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo ya biblia kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312
MWAMBA WETU.
TOBA IGUSAYO MOYO WA BWANA.
KIFO CHA MTAKATIFU PERPETUA NA FELISTA.
WINGU KUBWA LA MASHAHIDI.
https://wingulamashahidi.org/2018/06/27/2-swali-kwanini-mtu-atoe-pepo-aombee-wagonjwa-wapone-asikie-sauti-ya-mungu-ikimwambia-hiki-na-kile-kuhusu-watu-na-yeye-mwenyewe-kufunua-siri-za-mioyo-yao-aone-maono-na-kutembea-na-malaika-katika/