Kuchagua mwenza wa Maisha si jambo la kulichukulia kiwepesi wepesi tu kama vile kuchagua Rafiki, ambaye hata mkigombana mnaweza mkaachana na kurudiana muda wowote.
Tena ikiwa wewe ni mtu uliyeokoka ndio unapaswa uwe makini mara dufu, kwasababu ukifanya maamuzi yasiyosahihi utajikuta sio tu kuupoteza wokovu wako bali pia kufanyika chombo cha kuwapoteza na wengine.
Ipo mifano mingi katika biblia ya watu ambao waliingia katika mikono ya wenza ambao sio sahihi. Kwamfano tunamwona mtu mmoja aliyeitwa Ahabu yeye alimwoa Yezebeli, hakuna asiyejua mke wake huyu jinsi alivyokuwa mwiba kwake na kwa Israeli nzima.. Na hiyo yote ni kwasababu alifanya uamuzi usiosahihi katika kuchagua mwenza wa maisha wa kuoa.
1Wafalme 21:25 “(Lakini hapakuwa na mtu kama Ahabu, aliyejiuza atende maovu machoni pa Bwana ambaye Yezebeli mkewe alimchochea. 26 Akachukiza mno, kwa kuzifuata sanamu sawasawa na yote waliyoyafanya Waamori, Bwana aliowafukuza mbele ya wana wa Israeli.)”
1Wafalme 21:25 “(Lakini hapakuwa na mtu kama Ahabu, aliyejiuza atende maovu machoni pa Bwana ambaye Yezebeli mkewe alimchochea.
26 Akachukiza mno, kwa kuzifuata sanamu sawasawa na yote waliyoyafanya Waamori, Bwana aliowafukuza mbele ya wana wa Israeli.)”
Tunamwona tena mtu mwingine aliyeitwa Samsoni, jinsi alivyoanguka katika mikono ya mwanamke Delila, binti wa kifilisti, Tunamwona tena Sulemani alivyoanguka kwa wanawake wa mataifa mengine jinsi walivyomgeuza moyo na kumfanya aabudu miungu mingine ikawa kikwazo kwake kwa Mungu hadi ikafikia hatua ya Mungu kumuundokeshea maadui ….
Vilevile tunaomwona mwanamke Abigaili jinsi alivyoanguka mikononi kwa mume mpumbavu mlevi aliyeitwa Nabali..Ambaye ilikuwa ni nusura tu amsababishie mauti yeye pamoja na familia yake yote na wafanyakazi wake wote (soma 1Samweli 25).
Tunaomwona Herode naye, ambaye alijiingiza katika uuaji wa damu isiyokuwa na hatia ya Yohana Mbatizaji kwa wivu tu wa mke wake, ambaye kiuhalisia hata hakuwa mke wake bali mke wa kaka yake alimuua Yohana kwa shinikizo la mke wake katili.
Matatizo kama hayo vilevile yanaweza kumpata mtu yeyote kama asipojua njia ipasayo ya kumpata mwenza wa maisha sahihi.
Leo hii tutajifunza kanuni chache za kibiblia ambazo ukizifuata utakuwa na uhakika wa kuwa huyu uliyempata asilimia mia ni mwenza Mungu aliyekupangia.
Sasa kabla hatujaenda mbali hapa natazamia kuwa naongea na mtu ambaye ameshaokoka. Kama hujaokoka basi mwisho wa somo hili fanya hivyo, ndio ujumbe huu utakuwa na manufaa kwako.
HATUA YA KWANZA:
Usiwe na haraka ya kuoa au kuolewa: Biblia inatuambia wazi kuwa mapenzi huwa yanachochewa na huwa yanaamshwa..na kama yanaamshwa inamaanisha kuwa kumbe huwa yanapoa pia soma:
Wimbo uliobora 2:7 “Nawasihi, enyi binti za Yerusalemu, Kwa paa na kwa ayala wa porini, Msiyachochee mapenzi, wala kuyaamsha, Hata yatakapoona vema yenyewe”.
Hizi ni hekima tunafundishwa.. mambo ya kuingia katika ndoa si ya kuyakurupukia. Kisa umemwona Fulani ameolewa au Fulani kaolewa, au umempenda binti yule au kijana yule hivyo na wewe ukaamu moja kwa moja ukaanze mahusiano naye ili mfunge ndoa..Biblia inatuasa tusiyachochee mapenzi kabla ya wakati wake..Mapenzi yana wakati wake..
Ikiwa wewe bado ni binti/kijana mdogo unatafuta mpenzi wa nini wakati unajua kabisa hamna mpango wa kuoana?. Hali kama hiyo ikikujia au vishawishi kama hivyo vikikujia vikatae, kwasababu wakati wake haujafika….Au wewe ni mwanafunzi hujamaliza masomo yako, unataka kuingia katika mahusiano ambayo lengo lake linapaswa liwe ni ndoa, Je utamwoa huyo au yule na huku ukiwa bado masomoni? Huoni kama huo sio wakati wake?..Hivyo ukijikuta unataka kufanya hivyo kataa hiyo hali, toa mawazo yako huko, fanya mambo yako kama vile mtoto mchanga, mpaka wakati wake huko mbeleni utakapofika..
Vilevile wewe bado upo chini ya wazazi wako, au unajijua bado hali yako kiuchumi bado haijaimarika vizuri, unakimbilia wapi kufikiria mambo kama hayo..Simaanishi kuwa mpaka uwe Tajiri ndio uoe, lakini unapaswa ujiandae kisaikolojia, je! Nikifanya hivi, huyo mke wangu nitaweza kumuhudumia hata kwa yale mahitaji ya msingi tu,? Mambo kama hayo unatakiwa uyafikirie kabla hujaanza kutafuta mwenza wa maisha.
Usiogope labda umri umeenda au vipi, Isaka na Yakobo walipata wake zao wakiwa katika umri mkubwa tu, lakini tunaona wake waliowapata walikuwa ni bora Zaidi ya wake wa watu wengine..Vivyo hivyo usikimbilie tu kuoa au kuoelewa kwasababu Fulani Fulani bali uvumilivu pia ni muhimu katika kupata mwenza sahihi na ndoa iliyo bora.
Lakini sasa ikiwe umeyazingatia hayo vizuri na sasa upo tayari kuwa na mwenza, basi zingatia mambo yafuatayo:
Nikisema ni lazima awe ni mkristo simaanishi awe amezaliwa katika dini ya ki-kristo, anaweza akawa amezaliwa lakini matendo yake yapo mbali na ukristo, bali namaanisha ni lazima awe ameokoka, na yupo katika mstari ulionyooka wa wokovu wake, Maisha yake yakimshuhudia kuwa ameokoka, kama wewe ulivyo.
Ukiangalia watu wote tulioona kwenye biblia kuanzia Ahabu mpaka Sulemani wote hao waliingia katika matatizo makubwa kwasababu waliyakaidi maagizo ya Mungu..Pale walipoambiwa wasioe wala wasioelewe na watu walio nje ya taifa la Israeli.
Soma
Kumbukumbu 7:3 “binti yako usimpe mwanawe mume, wala usimtwalie mwanao mume binti yake. 4 Kwa kuwa atamkengeusha mwanao mume asinifuate, ili wapate kuabudu miungu mingine; ndipo itakapowaka hasira ya Bwana juu yenu, naye atakuangamiza upesi”.
Kumbukumbu 7:3 “binti yako usimpe mwanawe mume, wala usimtwalie mwanao mume binti yake.
4 Kwa kuwa atamkengeusha mwanao mume asinifuate, ili wapate kuabudu miungu mingine; ndipo itakapowaka hasira ya Bwana juu yenu, naye atakuangamiza upesi”.
Mungu alikuwa na sababu kuwaambia vile, kwasababu alijua watawageuza moyo na kuandamana nao na miungu yao.
Nehemia 13:25 “Nikagombana nao, nikawalaani, nikawapiga baadhi yao, na kuwang’oa nywele zao; nikawaapisha kwa Mungu, nikasema, Msiwaoze wana wao binti zenu, wala msiwatwae binti zao ili waolewe na wana wenu, wala na ninyi wenyewe. 26 Je! Sulemani, mwana wa Daudi, hakufanya dhambi kwa kutenda hayo? Lakini katika mataifa mengi hapakuwa na mfalme mwingine mfano wake. Tena alipendwa na Mungu wake, naye Mungu akamfanya mfalme juu ya Israeli; walakini wanawake wageni walimkosesha hata yeye”.
Nehemia 13:25 “Nikagombana nao, nikawalaani, nikawapiga baadhi yao, na kuwang’oa nywele zao; nikawaapisha kwa Mungu, nikasema, Msiwaoze wana wao binti zenu, wala msiwatwae binti zao ili waolewe na wana wenu, wala na ninyi wenyewe.
26 Je! Sulemani, mwana wa Daudi, hakufanya dhambi kwa kutenda hayo? Lakini katika mataifa mengi hapakuwa na mfalme mwingine mfano wake. Tena alipendwa na Mungu wake, naye Mungu akamfanya mfalme juu ya Israeli; walakini wanawake wageni walimkosesha hata yeye”.
Hivyo jambo la kwanza kabisa la kumtambua kuwa huyu ni mwenza wa maisha sahihi au sio sahihi usikimbilie kumtazama sura, au maumbile yake, au upendo wake kwako..Hilo jambo liondoe akilini kabisa..Usiangalie elimu yake au fedha zake, au ukarimu wake..wala usikimbilie kusema nimeoteshwa kwenye ndoto au nimeonyeshwa kwenye maono kuwa huyu ndio mpenzi wangu…Nataka nikumbie Neno la Mungu ni Zaidi ya ndoto au maono yoyote..Ndoto yoyote au unabii unaokinzana na Neno la Mungu unapaswa uukatae hata kama utaonekana unao uhalisia kiasi gani, Neno ndio linatuambia hivyo soma Kumbukumbu 13 utalithibitisha hilo.
Hivyo mwanamke yeyote au mvulana yeyote, anayekujia anataka kukuoa au unataka kumuoa, mwangalie kwanza Je! yeye ni mkristo aliyesimama katika Imani?…Na kama sio mkristo Je! Yupo tayari kuamini na kumfuata YESU..Ikiwa yupo tayari aanze kwa kugeuka kwanza ndipo hatua nyingine za kumtathimini zifuate.
2.USIWE NA HARAKA KUFUNGA NAYE NDOA:
Jambo lingine watu wasilolijua ni hili, pindi imetokea tu amemwona kuwa huyu ni mzuri, au anafaa, au ni mtakatifu, anaenda kanisani, bila kutuliza akili zao, moja kwa moja wanakimbilia kwenda kuoa au kuolewa naye..Na baadaye akishagundua kumbe yupo hivi au vile anaishia kujuta..
Sikuzote tendo la haraka haraka mara nyingi huwa halitokani na Mungu. Ukiona mtu Fulani anakushurutisha haraka haraka ufanye kitu Fulani, au mfanye biashara Fulani bila hata kuwa na nafasi ya kuitafakari vizuri basi ikatae moja kwa moja, ukiona mtu anakulazimisha ununue hiki au kile harakaraka bila hata ya kukiangalia vizuri basi usikinunue kwanza hata kama kwa macho kinaonekana ni kizuri.. Shetani naye huwa ndio anawashurutisha watu hivyo kuingia katika dhambi, atakuambia fanya hichi chapchap hakina shida, lakini baadaye ndio utakuja kujutia milele kwanini ulifanya vile.
Hivyo ukishamthibitisha kuwa huyu au yule ni mkristo, mtakatifu anampenda Mungu, chukua nafasi kumtathimini, pata muda wa kutosha hata miezi kadhaa, ikiwezekana hata mwaka kumwangalia Maisha yake, ..hiyo itakusaidia kuondoa kule kukurupuka ndani yako, na utapata nafasi ya kujua vile ambavyo mwanzoni ulikuwa huvijui kuhusu yeye au vile ambavyo amevificha mbele yako. Yusufu hakuwa na haraka ya kumfanya Mariamu kuwa mke wake, bali alingoja kwa kipindi Fulani na ndio maana alipogundua kuwa ana mimba, kumbuka mpaka mimba ionekane labda ni kuanzia miezi 3 na kuendelea, hivyo wakati huo wote hakuwahi kumkaribia wala kumjua, isipokuwa alikuwa amemposa tu, na baadaye alipogundua kuwa ana mimba, akawa radhi kumuacha..Ndipo Mungu akasema usimuache.. Hivyo na wewe chukua nafasi ya kumtathimini huyo anayetaka kuwa mpenzi wako.
Kisha ukiwa katika hali hiyo ya kumtazama sasa ndipo umwombe Mungu..Hapo unajinyenyekeza mbele za Mungu unamwambia nimemwona dada huyu au kaka huyu, ikiwa ni sawasawa na mapenzi yako Ee Mungu naomba unifanikishe na ikiwa sio sawa na mapenzi yako uniepushe naye..
Ukishamaliza kuomba hivyo kwa muda wa kutosha, ikiwezekana kufunga kwa kipindi Fulani..Basi anza harakati za kwenda kutoa mahari kama wewe ni mume, na kama wewe ni mwanamke himiza tendo hilo kwa huyo mwanaume, kwasababu Mungu yupo pamoja na wewe katika kila hatua, kama huyo siye yeye Mungu mwenyewe atamwondoa kwako, au atakuepusha naye, hivyo uwe na amani kuanzia huo wakati kwasababu ulishazitanguliza kwanza kanuni zake, hivyo ni wajibu wa Mungu kukulinda baada ya hapo..
Hakikisha unakwenda kujitambulisha kwao, na yeye kwenu, unatoa mahari, mnafuata hatua zote za ndoa ya kikristo.Kisha baada ya hapo mnafungishwa ndoa kanisani…Hapo ndipo huyu anakuwa mwenza Mungu aliyemkusudia kwa ajili yako.
Ikiwa utazingatia kufuata hatua hizo zote, ondoa wasiwasi kuwa ndoa yako itakuwa na miiba ndani yake, kinyume chake ndio utaimarika hata katika Imani yako kwasababu mke atakuwa msaidizi kwa mume, na mume atakuwa ulinzi kwa mke..Wote wawili wakisimama katika imani mafanikio tele ya rohoni na mwilini yataambatana nao, na Watoto wao pia watabarikiwa.
IKIWA HAUJAOKOKA:
Lakini kama wewe hujaokoka. Fahamu kuwa upo katika hatari kubwa sana, kwanza kwa kuukosa uzima wa milele, Na pili kwa kutokuwa na ndoa yenye baraka za Mungu..Kwasababu unataka kuoa au kuolewa lakini hujui kuwa anayeifungisha ndoa yenye heri na baraka ni Mungu..Sasa ikiwa umekosana na Mungu wako unatazamia vipi uwe heri katika ndoa yako unayoitazamia..Au upate wapi mwenza wa maisha aliye sahihi..Kwasababu wewe hapo ulipo tayari sio sahihi..utaishia kuoa asiyesahihi mwenzako na mwisho wake ni mlipuko.
Ni vizuri ukafanya uamuzi sahihi leo. Hizi ni siku za mwisho. Yesu yupo mlangoni kurudi..Dalili zote zinaonyesha kuwa unyakuo ni wakati wowote, Parapanda itakapolia wewe utakuwa wapi, wakati wenzako wapo mbinguni wewe utakuwa hapa chini katika dhiki kuu ya mpinga-kristo. Na baada ya hapo unaishia katika ziwa lile la moto. Kama ulikuwa hujui hili ndio kanisa la mwisho, lijulikanalo kama Laodikia, soma Ufunuo 3, Na kwanza hakutakuwa na kanisa lingine Zaidi ya hili,.Na kanisa hili ndio lililokemewa sana na Bwana Yesu kuliko makanisa mengine yaliyotangulia nyuma,.kwamba lipo vuguvugu,..Ni heri tungekuwa baridi au moto, kwasababu hiyo tumeambiwa tutatapikwa.Na tunajua matapishi huwa hayarudiwi tena. Hivyo ikifikia hatua ya wewe ndugu yangu kutapikwa, basi ujue hutakaa urudiwe tena, sehemu yako itakuwa ni katika lile ziwa la moto.
Unasubiri nini kwanini usimpe Yesu Kristo Maisha yako leo ayaokoe, Kesho inaweza ikawa isiwe yako. Nazungumza na wewe unayejiita mkristo, lakini huishi kama KRISTO, ndio maana Bwana anasema wewe ni vuguvugu…
Kama upo tayari kufanya hivyo kumpa Bwana Maisha yako…
Basi uamuzi unaoufanya ni wa busara sana ambao hautakaa uujutie. Unachopaswa kufanya, hapo ulipo, chukua muda mchache ujitenge peke yako. Kisha piga magoti, kisha fuatisha sala hii kwa Imani, ukijua kuwa Mungu yupo hapo karibu na wewe pembeni yako kukusikia..Kisha ukiwa sasa katika utulivu Sema sala hii kwa sauti.
EE MUNGU BABA, NAJA MBELE ZAKO, NIKIWA NINAJITAMBUA KUWA MIMI NI MKOSAJI NA NIMEKUTENDA DHAMBI NYINGI, NA KWAMBA NIMESTAHILI HUKUMU. LAKINI WEWE MUNGU WANGU ULISEMA KATIKA NENO LAKO KUWA WEWE NI MUNGU WA REHEMA UNAYEWAREHEMU MAELFU ELFU YA WATU WANAOKUPENDA WEWE. NA LEO HII NINAKUJA MBELE ZAKO NAHITAJI MSAMAHA WAKO NA MSAADA WAKO MUNGU WANGU, NINATUBU DHAMBI ZANGU ZOTE KWA KUMAANISHA NA KWA MOYO WANGU WOTE, NINAKIRI KUWA YESU KRISTO NI BWANA, NA YEYE NDIYE MWOKOZI WA HUU ULIMWENGUNI. HIVYO NAOMBA DAMU YA MWANAO TAKATIFU INISAFISHE UOVU WANGU WOTE SASA NIFANYIKE KUWA KIUMBE KIPYA KUANZIA LEO NA HATA MILELE. ASANTE BWANA YESU KWA KUNIPOKEA NA KUNISAMEHE. AMEN.
EE MUNGU BABA, NAJA MBELE ZAKO, NIKIWA NINAJITAMBUA KUWA MIMI NI MKOSAJI NA NIMEKUTENDA DHAMBI NYINGI, NA KWAMBA NIMESTAHILI HUKUMU. LAKINI WEWE MUNGU WANGU ULISEMA KATIKA NENO LAKO KUWA WEWE NI MUNGU WA REHEMA UNAYEWAREHEMU MAELFU ELFU YA WATU WANAOKUPENDA WEWE. NA LEO HII NINAKUJA MBELE ZAKO NAHITAJI MSAMAHA WAKO NA MSAADA WAKO MUNGU WANGU, NINATUBU DHAMBI ZANGU ZOTE KWA KUMAANISHA NA KWA MOYO WANGU WOTE, NINAKIRI KUWA YESU KRISTO NI BWANA, NA YEYE NDIYE MWOKOZI WA HUU ULIMWENGUNI. HIVYO NAOMBA DAMU YA MWANAO TAKATIFU INISAFISHE UOVU WANGU WOTE SASA NIFANYIKE KUWA KIUMBE KIPYA KUANZIA LEO NA HATA MILELE.
ASANTE BWANA YESU KWA KUNIPOKEA NA KUNISAMEHE.
AMEN.
Sasa ikiwa umefuatisha sala hiyo kwa Imani ..Hatua iliyobakia kwako ni kuithitisha toba yako kwa Vitendo ikiwa ulikuwa unafanya mambo yote ambayo hayampendezi Mungu unayaacha na kujitenga nayo, Na Mungu akishaona umegeuka kwa vitendo basi toba yako anaipokea na atakuja ndani yako wakati huo huo na kufanya makao ya milele kwako. Vile vile unahitaji, kutafuta kanisa la kiroho ambalo utajumuika na wakristo wengine katika kumwambudu Mungu, na kujifunza biblia ili uukulie wokovu. Na vilevile ili upate ubatizo sahihi wa kuzamishwa katika maji mengi na kwa jina la YESU KRISTO kwa ajili ya ondoleo la dhambi zako.
Zingatia hayo na Bwana atakuwa pamoja nawe. Vilevile Usiacha kutembelea Website hii https://wingulamashahidi.org mara kwa mara ili ujifunze maneno ya uzima..
jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Ubarikiwe sana.
Mada Nyinginezo:
NDOA NA HARUSI TAKATIFU.
Je! ni halali kutoa cheti kwa wakristo wanaooa?
Je! Ni halali kuoa/kuolewa na mtu ambaye tayari anao watoto?
Je! Ni sahihi kuoa/kuolewa na mtu uliyemzidi umri?
JE NI HALALI KUOA WAKE WENGI AU KUTOA TALAKA?
ANTIPA SHAHIDI WANGU, MWAMINIFU WANGU.
JE ADAMU ALIKUWA NA KITOVU?
Roho, Nafsi, na Mwili vina utofauti gani?
Rudi Nyumbani:
Print this post
Jiunge na group la Whatsapp, ujifunze biblia na upate Neno la siku kila asubuhi. Pamoja na maswali mengi ya biblia yaliyojibiwa..kwa link hii >>>> https://chat.whatsapp.com/GRri9BATojl2FNGbOJpjC6
Imani ni nini? ..Je tunaweza kufikia imani ya kuhamisha milima?..Nini maaha ya mstari huu?..Warumi 10:17 “Basi imani chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo”.
Biblia imesema wazi nini maana ya Imani katika kitabu cha Waebrania..
Waebrania 11:1 “Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana”.
Unakuwa na uhakika kwamba jambo fulani litatokea ambalo halipo sasa..Hiyo ni Imani. Na imani sio tumaini wala ujasiri..Unaweza ukawa na matumaini ya kutokea jambo fulani lakini bado usiwe na uhakika. Imani maana yake ni kuwa na uhakika…Kwamba asilimia 100 unaamini jambo fulani litatokea…Na kwamba jambo hilo ni lazima litokee..
Na Imani mtu hujiamulii kuamini tu!..Bali lazima kiwepo kitu cha kuishikilia hiyo Imani.
Kwamfano mwanafunzi ambaye amesoma kwa bidii na ameshafanya mazoezi ya kutosha huko nyuma na kuufahamu uwezo wake hivyo ujapo mtihani wa mwisho mbele yake anaamini kwamba ni lazima afaulu!..Kwanini anaamini hivyo?..Ni kwasababu ameshajiandaa vya kutosha. Hawezi tu kusema nitafaulu mtihani huu wakati hata kushika kalamu hajawahi kuiona. (Sasa huo ni mfano tu).
Tukirudi katika Ukristo ni hivyo hivyo..Mtu ili awe na Imani..Ni sharti kiwepo kitu cha kuisupport au kuishikilia hiyo Imani yake..Vinginevyo hiyo haitakuwa Imani bali tumaini.
Kadhalika katika Ukristo Mtu ili awe na Imani labda ya kuponywa ugonjwa wake na Yesu Kristo, Ni lazima awe ameshawahi kusoma au kusikia mahali kwamba Yesu anaponya..au ameshawahi kushuhudia mtu mwingine akiponywa na Yesu..au ameshawahi kuthibitisha uponyaji wa Yesu kwa kusikia ushuhuda mahali fulani….Nguvu ya Ushuhuda ule ndio unaoelezea Nguvu ya Imani mtu aliyonayo…Haiwezekani mtu ambaye hajawahi kusikia kabisa habari za Yesu kwamba ni mponyaji akawa na Imani ya kuponywa..Hiyo haiwezekani ni lazima awe amesikia kwanza..
Ndio maana Biblia inasema..
Warumi 10:17 “Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo”.
Ndio maana ili kuikuza imani..Mtu anatakiwa alijue sana Neno la Mungu..Na Kulijua Neno la Mungu sio kukariri mistari ya Biblia…hapana bali kumwelewa Yesu Kristo kwa mapana na marefu na kuzifahamu shuhuda zake.
Unaposoma Neno na kukutana na Mstari ambao Yesu Kristo alimponya kipofu Batimayo katika Marko
Marko 10:46 “Wakafika Yeriko; hata alipokuwa akishika njia kutoka Yeriko, pamoja na wanafunzi wake, na mkutano mkubwa, mwana wa Timayo, Bartimayo, yule mwombaji kipofu, alikuwa ameketi kando ya njia. 47 Naye aliposikia ya kwamba ni Yesu Mnazareti, alianza kupaza sauti yake, na kusema, Mwana wa Daudi, Yesu, unirehemu. 48 Na wengi wakamkemea ili anyamaze, lakini alizidi kupaza sauti, Mwana wa Daudi, unirehemu. 49 Yesu akasimama akasema, Mwiteni. Wakamwita yule kipofu, wakamwambia, Jipe moyo; inuka, anakuita. 50 Akatupa vazi lake, akaruka, akamwendea Yesu. 51 Yesu akamjibu, akamwambia, Wataka nikufanyie nini? Yule kipofu akamwambia, Mwalimu wangu, nataka nipate kuona. 52 Yesu akamwambia, Enenda zako, imani yako imekuponya. Mara akapata kuona; akamfuata njiani”.
Marko 10:46 “Wakafika Yeriko; hata alipokuwa akishika njia kutoka Yeriko, pamoja na wanafunzi wake, na mkutano mkubwa, mwana wa Timayo, Bartimayo, yule mwombaji kipofu, alikuwa ameketi kando ya njia.
47 Naye aliposikia ya kwamba ni Yesu Mnazareti, alianza kupaza sauti yake, na kusema, Mwana wa Daudi, Yesu, unirehemu.
48 Na wengi wakamkemea ili anyamaze, lakini alizidi kupaza sauti, Mwana wa Daudi, unirehemu.
49 Yesu akasimama akasema, Mwiteni. Wakamwita yule kipofu, wakamwambia, Jipe moyo; inuka, anakuita.
50 Akatupa vazi lake, akaruka, akamwendea Yesu.
51 Yesu akamjibu, akamwambia, Wataka nikufanyie nini? Yule kipofu akamwambia, Mwalimu wangu, nataka nipate kuona.
52 Yesu akamwambia, Enenda zako, imani yako imekuponya. Mara akapata kuona; akamfuata njiani”.
Imani ni nini? Unaposoma habari hiyo na kulihifadhi tukio hilo moyoni mwako badala ya kuikariri mistari hiyo..Hapo tayari Neno la Mungu umeliweka moyoni…hata kama hujaikariri mistari hiyo…Sasa tukio hilo tayari ni Neno la Mungu na tayari ni chanzo cha Imani…Sasa unapopitia wakati wa majaribu labda umeugua kifua…Ukamwomba na ukawa hatiani kufa..Ukalikumbuka hilo tukio…na kusema moyoni kama Bwana alimponya kipofu Batimayo hata mimi nitapona tu!..Hiyo tayari ni Imani yenye chanzo sahihi cha Neno la Mungu..Hivyo italeta majibu tu! haijalishi itachukua muda gani.
Na wakati ukifika kifua hicho kikapona kulingana na Imani hiyo…Imani yako kwa Mungu itakuwa zaidi.. Hivyo hata Lijapo jaribu lingine kubwa kuliko hilo..Unatumia ushuhuda wa Bartimayo na ushuhuda wa kwako kupona kifua unazijumlisha shuhuda hizo kuangusha tatizo hilo kubwa lililokuja mbele zako hata kufikia imani ya kuhamisha milima….Lakini huwezi kuangusha tatizo lolote kubwa mbele yako au huwezi kuamini jambo kubwa kama litatoke kama huna ushuhuda wowote au Neno la Mungu kukushikilia nyuma.
Unaweza kujiuliza Daudi alitolea wapi Imani kubwa kama ile ya kumwangusha Goliathi…Hakikuwa ni kitu cha kuamka tu na kupata ujasiri! hapana..Ile Imani ilitengenezwa tangu siku nyingi…Ukisoma Biblia utaona Mungu alikuwa anamwokoa Daudi na makucha ya simba na dubu wakati anachunga…sasa mkusanyiko wa shuhuda zile ziliipandisha Imani yake na hata kufikia kusema kama Bwana ameniokoa mikononi mwa simba basi hakuna mwanadamu yoyote ambaye Bwana hawezi kuniokoa mikononi mwake. Na alipokutana na Goliathi alimwona ni mdogo kuliko simba na dubu aliokoka nao.
1Samweli 17:33 “Sauli akamwambia Daudi, Huwezi wewe kumwendea Mfilisti huyu upigane naye; maana wewe u kijana tu; na huyu ni mtu wa vita tangu ujana wake. 34 Daudi akamwambia Sauli, Mtumishi wako alikuwa akichunga kondoo za baba yake, na alipokuwa akija simba, au dubu, akamkamata mwana-kondoo wa lile kundi, 35 mimi hutoka nikamfuata, nikampiga, nikampokonya kinywani mwake; na akinirukia, humshika ndevu zake, nikampiga, nikamwua. 36 Mtumishi wako alimwua simba na dubu pia; na huyu Mfilisti asiyetahiriwa atakuwa kama mmoja wao, kwa sababu amewatukana majeshi ya Mungu aliye hai. 37 Daudi akasema, Bwana aliyeniokoa na makucha ya simba, na makucha ya dubu, ataniokoa na mkono wa Mfilisti huyu. Sauli akamwambia Daudi, Enenda, na Bwana atakuwa pamoja nawe”.
1Samweli 17:33 “Sauli akamwambia Daudi, Huwezi wewe kumwendea Mfilisti huyu upigane naye; maana wewe u kijana tu; na huyu ni mtu wa vita tangu ujana wake.
34 Daudi akamwambia Sauli, Mtumishi wako alikuwa akichunga kondoo za baba yake, na alipokuwa akija simba, au dubu, akamkamata mwana-kondoo wa lile kundi,
35 mimi hutoka nikamfuata, nikampiga, nikampokonya kinywani mwake; na akinirukia, humshika ndevu zake, nikampiga, nikamwua.
36 Mtumishi wako alimwua simba na dubu pia; na huyu Mfilisti asiyetahiriwa atakuwa kama mmoja wao, kwa sababu amewatukana majeshi ya Mungu aliye hai.
37 Daudi akasema, Bwana aliyeniokoa na makucha ya simba, na makucha ya dubu, ataniokoa na mkono wa Mfilisti huyu. Sauli akamwambia Daudi, Enenda, na Bwana atakuwa pamoja nawe”.
Lakini Huwezi kuwa na imani hii kabla ya kuliamini Neno la Mungu..Usipoamini kwamba Bwana Yesu ni kweli alimponya Bartimayo huwezi kuwa na Imani ya kuponywa…Usipoamini kwamba ni kweli Yesu Kristo alikuja duniani miaka 2000 iliyopita na alikuja kufa kwaajili ya dhambi zetu, na alifufuka huwezi kuwa na Imani ya kitu chochote.
Hivyo inatangulia kwanza imani ya kumwamini Yesu Kristo na maneno yake..Ukimwamini huyo ndipo Imani kwa vitu vingine itafuata na utaona mambo makubwa na ya ajabu katika maisha yako ambayo yanaonekana kama hayawezekaniki..lakini yatawezekanika kwa kumwamini Yesu Kristo.
Hivyo kama hujamwamini Yesu Kristo ni wakati wako leo… Tambua kwamba yupo, na hapo ulipo anakutazama na anakutamani uwe wake na anakuita hivyo usishupaze shingo yako..Mkubali kwa kutubu dhambi zako zote kwa kumaanisha kutozifanya tena…kama ulikuwa mwasherati unaacha uasherati wako kuanzia sasahivi..kama ulikuwa ni mshabiki wa mambo ya ulimwengu huu kama miziki leo hii unaiacha yote na kama ipo kwenye simu yako ya mkononi..ifute sasahivi yote usiache hata mmoja..kama ulikuwa ni mlevi acha leo, na kama unazo pombe kwenye friji yako kazimwage sasahivi..na mkubali huyu Yesu aingie moyoni mwako.
Na ukishamwamini kwa vitendo namna hiyo..tafuta mahali ambapo unaweza kujifunze Neno la Mungu kwa ufasaha zaidi..Roho Mtakatifu atakayeingia ndani yako atakuongoza katika kweli yote..Pia hakikisha unabatizwa katika ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa jina la Yesu Kristo sawasawa na Matendo 2:38. Na kwa kufuata hatua hizo utakuwa umeokoka kwa kuzaliwa mara ya pili.. Hivyo usitende dhambi tena, na Roho Mtakatifu atakupa uwezo wa ajabu wa kushinda dhambi…Na hapo utakavyozidi kudumu katika kuyasoma maneno ya Yesu Kristo Imani yako itakuwa mpaka kufikia Imani ya kuhamisha milima.
Hivyo kwa hitimisho Imani ni nini?..Ni kuwa na uhakika wa mambo yatarajiwayo..na chanzo chake ni kuyaamiini maneno ya Yesu Kristo. Na maneno ya Yesu Kristo ni Yesu mwenyewe (Yohana 1:1). Ukimpokea Yesu umeyaamini maneno yake, hivyo tayari una Imani.
Bwana akubariki sana.
Tafadhali share na wengine.
Mafundisho mengine:
+255693036618/ +255789001312
KIWANGO CHA TATU CHA IMANI.
IMANI “MAMA” NI IPI?
IMANI NI KAMA MOTO.
MAMBO (2) YATAKAYOKUTENGA NA IMANI SIKU HIZI ZA MWISHO.
MWANANCHI WA UFALME WA MBINGUNI
Nini maana ya huu mstari ” Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda;”?(2Timotheo 4:7)
Shalom mtu wa Mungu karibu tujifunze Biblia…Neno la Mungu linatuambia katika kitabu cha.. Mhubiri 7:16 “Usiwe na haki kupita kiasi; Wala usijiongezee hekima mno; Kwani kujiangamiza mwenyewe?”. Maana yake ni nini?
Hapo kuna maswali machache tunayoweza kujiuliza….Je ni kwanini inasema hivyo?..Kwani kuna ubaya gani kuwa mwenye haki kupita kiasi…Mbona ndio vizuri Zaidi kuwa mwenye haki kupita kiasi kuliko kuwa mwovu au kuwa mwenye haki kidogo?.
Ni kweli tukiusoma mstari huo kwa mantiki hiyo tunaweza kuchanganyikiwa na kuona kama biblia inajichanganya kuona sehemu moja inatuasa tuwe wenye haki na hapa inatuambia tusiwe wenye haki kupita kiasi….Lakini ukweli ni kwamba Biblia ni kitabu kilichohakikiwa na Roho wa Mungu aliye mmoja tu asiyeweza kukosea wala kufanya masahihisho..Na huyo sio mwingine zaidi ya Mungu aliyeziumba Mbingu na nchi, aliyefunuliwa ndani ya YESU KRISTO (Waebrania 1;1-2, 2Wakorintho 5:19).
Huyo hawezi kukosea embu jaribu kifiria tangu hii dunia iumbwe jua halijawahi kukosea majira yake, kwamba siku moja lichelewe lisionekane upande mmoja, au siku siku nyingine liwahi kupambazuka, miaka nenda rudi, majira yake hayabadiliki, hiyo ni kuthibitisha kuwa kazi ya Mungu haijawahi kuwa na mapungufu hata kidogo, siku zote sisi ndio tunaotazama mzunguko wa jua ili kurekebisha majira yetu, na sio jua kututegemea sisi…miungu mingine iliyotengenezwa kwa mchanga na ngano, na chokaa na vipande vya kuni hiyo ndiyo inaweza kukosea lakini si Mungu wetu Yehova tunayemwabudu kupitia Yesu Kristo kwake hakuna mapungufu..
Biblia iliposema tusiwe na haki kupita kiasi ilimaanisha…
“Tusiwe watu wa kujihesabia haki mno!”..Mtu anayejihesabia haki mno anakuwa na kiburi na kuishia kudharau wengine wote na kujiona yeye ni bora kuliko wengine..
Bwana Yesu aliwaona mafarisayo na masadukayo kwamba ni watu wenye kujihesabia haki mno.
Luka 18:9 “ Akawaambia mfano huu watu waliojikinai ya kuwa wao ni wenye haki, wakiwadharau wengine wote. 10 Watu wawili walipanda kwenda hekaluni kusali, mmoja Farisayo, wa pili mtoza ushuru. 11 Yule Farisayo akasimama akiomba hivi moyoni mwake; Ee Mungu, nakushukuru kwa kuwa mimi si kama watu wengine, wanyang’anyi, wadhalimu, wazinzi, wala kama huyu mtoza ushuru. 12 Mimi nafunga mara mbili kwa juma; hutoa zaka katika mapato yangu yote. 13 Lakini yule mtoza ushuru alisimama mbali, wala hakuthubutu hata kuinua macho yake mbinguni, bali alijipiga-piga kifua akisema, Ee Mungu, uniwie radhi mimi mwenye dhambi. 14 Nawaambia, huyu alishuka kwenda nyumbani kwake amehesabiwa haki kuliko yule; kwa maana kila ajikwezaye atadhiliwa, naye ajidhiliye atakwezwa”.
Luka 18:9 “ Akawaambia mfano huu watu waliojikinai ya kuwa wao ni wenye haki, wakiwadharau wengine wote.
10 Watu wawili walipanda kwenda hekaluni kusali, mmoja Farisayo, wa pili mtoza ushuru.
11 Yule Farisayo akasimama akiomba hivi moyoni mwake; Ee Mungu, nakushukuru kwa kuwa mimi si kama watu wengine, wanyang’anyi, wadhalimu, wazinzi, wala kama huyu mtoza ushuru.
12 Mimi nafunga mara mbili kwa juma; hutoa zaka katika mapato yangu yote.
13 Lakini yule mtoza ushuru alisimama mbali, wala hakuthubutu hata kuinua macho yake mbinguni, bali alijipiga-piga kifua akisema, Ee Mungu, uniwie radhi mimi mwenye dhambi.
14 Nawaambia, huyu alishuka kwenda nyumbani kwake amehesabiwa haki kuliko yule; kwa maana kila ajikwezaye atadhiliwa, naye ajidhiliye atakwezwa”.
Umeona?..Haki yetu haipaswi kuzidi mipaka hiyo hadi kufikia hatua ya kujikweza na kuwa na kiburi na kuwadharau wengine wote…Elimu yetu ya dini isitufanye tujione tu wenye haki kuliko wengine wote…karama zetu zisitufanye tujione sisi ni bora mbele za Mungu kuliko wengine wote…hata usafi na utakatifu tulio nao usizidi mipaka ya kujiona tu wenye haki saana!..tukifanya hivyo tutakuwa tu wenye haki kupita kiasi. Kadhalika kama tuna hekima ya ki-Mungu basi tusijione ni wenye hekima sana ya Neno la Mungu kiasi kwamba hakuna kama sisi, wala hakuna mtu yeyote anayeweza kutuongezea kitu…tukifanya hivyo tutakuwa tumejiongezea hekima kupita kiasi!..na hivyo tutajiangamiza wenyewe.
Mhubiri 7:16 “Usiwe na haki kupita kiasi; Wala usijiongezee hekima mno; Kwani kujiangamiza mwenyewe?”.
Mafarisayo na Masadukayo walijiangamiza wenyewe kwa haki yao iliyozidi na kujiona kwao wanajua maandiko kuliko wengine wote..Mwishowe wakajikuta badala ya kumwamini Mwokozi wa ulimwengu wakajikuta wanampinga na hata kwenda kumwua.
Kadhalika wewe ni Mchungaji, au Nabii au Mhubiri au Mwalimu au Una Neno la Hekima na Maarifa, au una karama ya uponyaji, au Imani au miujiza au ni Muumini ambaye kuna Neema ya kipekee ambayo Mungu kakukirimia ambayo inaweza kukutofautisha wewe na wengine kwa sehemu Fulani au popote pale ulipo…Neno hili usilisahau…“USIWE MWENYE HAKI KUPITA KIASI”. Kila siku jione wewe si kitu mbele za Mungu..ni kwa Neema tu za Mungu upo kama ulivyo na si kwa haki yako..wala kwa nguvu zako binafsi,. Haki yako isizidi mipaka na kujiona ni kwa jitihada zako umestahili kuwa hivyo ulivyo..Hakuna anayestahili hata mmoja wote ni makapi tu! tumechaguliwa na kuokolewa kwa Neema..hivyo hakuna cha kujisifia..
Waefeso 2:8 “Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; 9 wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu”
Bwana akubariki.
Kama bado hujaokoka!..Dunia hii inakwenda kuisha..Kipindi sio kirefu sana Dunia itakwenda kushuhudia mabadiliko makubwa ya ghafla!..Ghadhabu ya Mungu itamwagwa duniani kote na wale wote waliomkataa Mwana wa Mungu Yesu Kristo, wataangamizwa kwa maangamizo makubwa yasiyoelezeka kasome Ufunuo 16. Hivyo unyakuo upo karibuni sana kutokea ambapo watakatifu (Yaani wale wote waliompokea Yesu Kristo na kuishi maisha ya utakatifu) watanyakuliwa na kwenda mbinguni kwa Bwana kuipisha ghadhabu hiyo kupita. Je wewe utakuwa wapi?..kama leo hii bado unamkataa Kristo?..kama leo hii bado ni mlevi, ni mwasherati, mtazamaji wa picha chafu, mchatiji wa mambo machafu mitandaoni, mfanyaji masturbation, mtukanaji, mtoaji mimba, mvaaji nusu uchi, mpakaji malipstick, mvaaji mawigi, masuruali n.k?..Siku hiyo utakuwa wapi?
Leo isikupite kabla hujageuka, biblia inasema saa ya wokovu ni sasa..Unachopaswa kufanya hapo ulipo ni kujitenga peke yako, na kupiga magoti na kuomba toba mbele za Mungu..Mwombe Mungu akusamehe dhambi zako leo..na yeye ni mwaminifu atakusamehe..Baad a ya Toba hiyo anza leo kubeba msalaba wako na kumfuata Kristo..Futa leo miziki yote ya kidunia iliyopo kwenye simu yako na picha zote za uchafu pamoja na namba za wanaume/wanawake uliokuwa unachat nao..kadhalika kachome nguo zote fupi ulizonazo pamoja na vipodozi vyote na suruali..baki kama ulivyo katika uhalisia wako. Na mambo mengine yote yasiyompenda Mungu uliyokuwa unayafanya.
Ukishafanya hivyo..basi utakuwa umemwonyesha Kristo kwamba umeamua kweli kumfuata yeye kwa matendo yako..Na yeye akishaona hivyo..Neno lake linasema “Yoyote ajaye kwangu sitamtupa nje kamwe Yohana 6:37”. Hivyo atakuwa na wewe na utasikia Amani ya ajabu ambayo hujawahi kuisikia hapo kabla..
Na baada ya kumgeukia Yesu kwa vitendo namna hiyo..haraka sana katafute mahali ambapo unaweza kuukulia wokovu..na pia kubatizwa kama hukubatizwa..Kumbuka Ubatizo sahihi ni muhimu na ni ule wa maji mengi (Yohana 3:23) na wa Jina la Yesu Kristo (Matendo 2:38). Na Roho Mtakatifu ndani yako atakusaidia kupembua mema na mabaya baada ya hapo na kuendelea..atakuongoza mpaka kufikia utimilifu na Zaidi ya yote atakuwezesha kushinda dhambi na vishawishi vyote vya huu ulimwengu, na yale mambo maovu yaliyosalia ndani yako ambayo kwa nguvu zako ulishindwa kuyaondoa, yeye atayashughulikia yote..
Ukifanya hivyo kwa dhati kabisa utakuwa umezaliwa mara ya pili..na kuwa miongoni mwa wateule wapendwao na Bwana..Na hata unyakuo ukipita leo, nawe utakuwa miongoni mwa wale watakokwenda kuishuhudia karama ya mwana-kondoo ambayo Kristo alikuwa amekwenda kutuandalia kwa miaka elfu mbili sasa.
Maran atha.
Tafadhali share na kwa wengine
CHACHU YA MAFARISAYO NA CHACHU YA HERODE.
NGUVU ILIYOPO KATIKA MAAMUZI.
NYAKATI SABA ZA KANISA NA WAJUMBE WAKE.
DUNIANI MNAYO DHIKI.
kanisa la kwanza duniani ni lipi?
IELEWE SAUTI YA MUNGU.
WhatsApp
Njia za Mungu hazichunguziki, Mariamu akutana na Elisabeti..Elisabeti katika uzee wake aliambiwa atapata mimba, wakati ambao kizazi kimeshanyauka. Je! Ni nini tunaweza kujifunza hapo?.
Nakusalimu katika jina kuu la Emanueli, Bwana wetu YESU KRISTO.
Wakati tukiwa katika kipindi hichi cha Krisimasi na kufunga mwaka. Napenda tufunge kwa kuwatazama wanawake hawa wawili Mariamu na Elisabeti. Wanawake hawa wanawakilisha makundi mawili ya Watoto wa Mungu ambao wapo tayari kupokea baraka zao hivi karibuni.
Kama tunavyojua walikuwa ni wanawake waliokuwa wanamcha Mungu, mmoja alikuwa ni mzee sana, na mwingine alikuwa bado ni kijana mdogo. Lakini cha ajabu ni kuwa kila mmoja alipokea ripoti ambayo ilikuwa ni kinyume na matarajio yake.
Elisabeti katika uzee wake aliambiwa atapata mimba, wakati ambao kizazi kimeshanyauka, na mayai ya uzazi hayapo, wakati ambapo mawazo ya kuwa na mtoto kichwani yameshafutika, Anachosubiri ni kifo tu, lakini ghafla anapokea ripoti kutoka kwa malaika Gabrieli kuwa atazaa mtoto mwanamume, na sio tu mtoto ilimradi mtoto bali mtoto ambaye atakuwa mkuu sana Luka 1:15).
Tukirudi upande wa pili wa Mariamu, yeye naya akiwa bado binti mdogo tu, ndio kwanza amechumbiwa..Akiwa bado hata hajamkaribia mwanamume, hata mawazo ya kuwa na mtoto hayajaingia kichwani mwake. Lakini tunaona hapa yeye naye anapokea ripoti ya ghafla kutoka kwa malaika yule yule Gabrieli kuwa atapata mimba. Naye atazaa mtoto, naye si mtoto ilimradi mtoto tu, bali atakuwa mfalme mkuu, ambaye ufalme wake utakuwa hauna mwisho.
Mariamu apolisikia hivyo hakukawia, alifunga safari kwenda kwa Elisabeti kuusikiliza ushuhuda wake, huku naye pia akiwa na ushuhuda wa kumweleza wa kwake.. shauku ilimjaa sana..
Jaribu kufikiria walipokutana walianza kuzungumza maneno gani..Mmoja atasema, nilidhani mpaka nitakapokutana na mwanamume ndio nitapata ujauzito, mwingine atasema, nilidhani wakati nilipokuwa na mwanamume, wakati ambao mayai yangu yakiwa tumboni ndio ningepata ujauzito..Lakini sasa wakati ambapo hatukutegemea hapo ndipo Mungu alipotuonekania..
Hata wewe leo ambaye umeokoka, unaweza ukajiona bado ni mchanga, bado ni mdogo Mungu kukutimizia malengo yako, unaweza ukadhani mpaka Bwana anitumie katika kazi yake ni lazima ufikie umri wa makamo, Au mpaka ufanikiwe ni lazima uwe umemaliza shule kwanza, au umefanya kazi miaka kadhaa, au umefikisha umri fulani.. Nataka nikuambie ondoa mawazo hayo kichwani kwako ikiwa wewe ni mtoto wa Mungu…
Njia za Mungu hazichunguziki, Mariamu hakuwahi kufikiria kuwa angewahi kubeba ujauzito kabla ya kukutana na mwanamume..Lakini iliwezekana kwasababu Gabrieli alimwambia hakuna linaloshindikana kwa Mungu..(Luka 1:37)
Vivyo hivyo na wewe. Neema hiyo Bwana anaweza akaishusha juu yako, ni nani ajuaye itakuwa katika huu mwaka unaonza 2020, atakuwa tayari ameshakupigisha hatua kubwa katika utumishi wako?, katika huduma yako?..ukawa msaada kwa wengi.. Kama ulikuwa nawe ni Tasa, Bwana akakupatia mtoto kama Elizabeth…Na Katika Maisha yako pia?, ukawa na nyumba yako mwenyewe, ukawa na biashara zako mwenyewe? Angali bado ni mdogo, angali hujasoma, angali bado hujaoa au hujaolewa? ..Lakini hiyo yote ni kama utakuwa katika mstari wa kutembea katika mapenzi ya Mungu..
Vilevile mwingine unaweza ukajiona, muda umeshakwenda sana, umri umesogea, ukiangalia kile ulichokuwa unakiongojea kwa muda mrefu hakijakufikia kwa wakati, mpaka sasa hujapiga hatua inayoonekana kwa macho, bado huna kwako, bado kula ni kwa shida..Ukiangalia hata useme ukaanze kutafuta bado utakuwa umechelewa, ni kama vile umeshajikatia tamaa kila kitu..Nataka nikuambie hata Elisabeti alidhani hivyo katika uzee wake, lakini wakati ulipofika wa yeye kupata mimba ya shujaa wa Imani aliyeitwa Yohana Mbatizaji ambaye Bwana Yesu alimshuhudia kuwa katika uzao wa wanawake hakuwahi kutokea aliye mkuu kama yeye, yaani kwa namna nyingine hata akina Musa, na Eliya na manabii wote hakuna hata mmoja aliyemzidi kwa ukuu Yohana Mbatizaji kule mbinguni..
Vivyo hivyo na wewe uliyeokoka ambaye kwa muda mrefu unaona kuna utasa katika huduma yako au biashara yako, au kazi yako..Ni nani ajuaye kipindi hichi ndicho Mungu anatungisha mimba hiyo ya mafanikio yako. Na mpaka mwaka kesho unaisha unakuwa umeyafikia malengo na kuvuka hata Zaidi ya matarajio yako?
Wagalatia 4:27 “Kwa maana imeandikwa, Furahi, wewe uliye tasa, usiyezaa; Paza sauti, ulie, wewe usiye na utungu; Maana watoto wake aliyeachwa pekee ni wengi Kuliko wa huyo aliye na mume”.
Lakini hiyo yote inakuja ikiwa upo katika mstari ulionyooka wa kuyatenda mapenzi ya Mungu kama alivyokuwa Elisabeti biblia inavyosema alikuwa mtu wa Haki, akienenda katika amri zote za Mungu bila lawama (Luka 1:6).
Lakini kama upo nje ya Kristo. Usitegemee miujiza ya Mungu kama hii kuja katika Maisha yako..Ni vizuri ndugu uumalize mwaka wako na Bwana, Ili ukifungua mwaka mpya, Bwana naye aanze na wewe.. Na akishaanzana na wewe, anaanzana na wewe kweli kweli Kama vile tulivyoona hapo juu, njia za Mungu hazichunguzi, unaweza kusema bado sana, kumbe ni wakati wenyewe..Unaweza kusema nimechelewa kumbe ndio wakati wa kufarijiwa
Unachopaswa kufanya ni kuyasalimisha Maisha yako kwa Bwana..Na hiyo inakuja kwa kutubu kwa kumaanisha kabisa kuacha dhambi zako zote bila kubakisha hata moja, kama ulikuwa ni mlevi leo hii unasema basi, kama ulikuwa ni mzinzi leo hii unasema inatosha, kama ulikuwa unaishi na mke au mume ambaye si wako leo hii unaaacha, kama ulikuwa unatapeli watu unasema sitaki tena mambo hayo nataka nianze mwaka wangu upya na Bwana..Na hutubu kwasababu unataka uwe na gari au nyumba..unatubu kwasababu umeona maisha yako yanamhitaji Yesu Kristo, na hayatoshi bila yeye.
Sasa ikiwa utakuwa umefanya hivyo kwa moyo wako wote, na umemaanisha kumgeukia Kristo kikweli kweli fahamu kuwa Mungu atauona moyo wako, na akishauona umegeuka basi yeye mwenyewe atakuwa ameshakusamehe na atakuwa na jukumu la kukuvuta kwake Zaidi kwa nguvu ya ajabu sana..Atakuvika uwezo wa kipekee wa kufanyika mwana wa Mungu ,(Yohana 1:12) Na uwezo huo ndio utakaokufanya uweze kuyashinda yale yaliyosalia yaliyokuwa magumu kuyashinda na kudumu katika wokovu.
Vilevile ukishafanya hivyo ili kuukamilisha wokovu wako, tafuta kwenda kubatizwa katika ubatizo sahihi wa kuzamwishwa katika maji mengi (Yohana 3:23) na kwa jina la YESU KRISTO sawasawa na Matendo 2:38, Na baada ya hapo Roho Mtakatifu atakuwa na wewe daima, Mpaka siku ya kufa kwako, ikiwa unyakuo utakuwa bado haujapita. Na baraka zote hizo ambazo Mungu anazileta nje ya matarajio yetu kwa Watoto wake wote wampendao zitaachiliwa na juu yako wewe uliyeokoka.
Bwana akubariki sana. Tafadhali “Share” na wengine ujumbe huu.
Shalom.
MWAKA WA BWANA ULIOKUBALIWA.
YOHANA MBATIZAJI
Mungu anasema hatagharikisha dunia na maji tena,.Kwanini watu wanasema dunia itaangamizwa?
FREEMASONS NI NINI? NA MTU ATATOKAJE HUKO?
UMEFUNULIWA AKILI?
Sanduku la Agano lilikuwa linawakilisha nini katika Agano jipya?
Shalom…Jina la Bwana, libarikiwe..Karibu tuzidi kujifunza Neno la Mungu…Ambalo ni Taa iongozayo miguu yetu na mwanga wa njia zetu. (Zaburi 119:105).
Leo tutajikumbusha namna Mungu anavyotenda kazi ili tusijikute tunaingia kwenye manung’uniko pale tunapojikuta tunapitia hali fulani tofauti na vile tulivyoitegemea…Kama wengi wetu tujuavyo Maisha ya Yusufu kwenye Biblia yamebeba funzo kubwa sana ya jinsi gani Mungu anaweza kumtoa mtu aliyekata tamaa katika mateso na kumnyanyua juu tena.
Lakini pamoja na hayo kuna jambo la Muhimu la kujifunza juu ya Yusufu…Ukitazama katika hatua zote Yusufu alizopitia utagundua kuwa Mungu alikuwa naye hakumwacha…
Utaona wakati yupo nyumbani kwa Potifa..japokuwa alikuwa ni mtumwa ndani ya ile nyumba lakini Mungu alimfanikisha kila alilolifanya lilifanikiwa….Akiwa ndani ya nyumba ile pengine mifugo aliyopewa aisimamie na Bwana wake ilizaliana na kuwa na afya Zaidi kuliko ya wafanyakazi wengine…Pengine shamba alilopewa alisimamie lilikuwa linazaa Zaidi ya watumwa wengine…pengine kila alilotumwa na Bwana wake Potifa lilikuwa linafanikiwa..tofauti na wanapotumwa watumwa wengine n.k…Hivyo Potifa Bwana wake aliliona hilo ndipo akaamua kumweka juu ya kila kitu chake kwasababu aliona kijana ana Neema ya mafanikio.
Mwanzo 39:2 “Bwana akawa pamoja na Yusufu, naye akasitawi; naye alikuwa katika nyumba ya bwana wake, yule Mmisri. 3 Bwana wake akaona ya kwamba Bwana yu pamoja naye, na ya kuwa Bwana anafanikisha mambo yote mkononi mwake. 4 Yusufu akaona neema machoni pake, akamtumikia. Naye akamweka awe msimamizi juu ya nyumba yake, na yote yaliyomo akayaweka mkononi mwake. 5 Ikawa tokea wakati alipomweka awe msimamizi juu ya nyumba yake, na vyote vilivyomo, Bwana akabariki nyumba ya yule Mmisri kwa ajili ya Yusufu. Mbaraka wa Bwana ukawa juu ya vyote alivyokuwa navyo katika nyumba, na katika shamba. 6 Akayaacha yote aliyokuwa nayo mkononi mwa Yusufu; wala hakujua habari za kitu cho chote chake, ila hicho chakula alichokula tu”.
Mwanzo 39:2 “Bwana akawa pamoja na Yusufu, naye akasitawi; naye alikuwa katika nyumba ya bwana wake, yule Mmisri.
3 Bwana wake akaona ya kwamba Bwana yu pamoja naye, na ya kuwa Bwana anafanikisha mambo yote mkononi mwake.
4 Yusufu akaona neema machoni pake, akamtumikia. Naye akamweka awe msimamizi juu ya nyumba yake, na yote yaliyomo akayaweka mkononi mwake.
5 Ikawa tokea wakati alipomweka awe msimamizi juu ya nyumba yake, na vyote vilivyomo, Bwana akabariki nyumba ya yule Mmisri kwa ajili ya Yusufu. Mbaraka wa Bwana ukawa juu ya vyote alivyokuwa navyo katika nyumba, na katika shamba.
6 Akayaacha yote aliyokuwa nayo mkononi mwa Yusufu; wala hakujua habari za kitu cho chote chake, ila hicho chakula alichokula tu”.
Vivyo hivyo…hata baada ya Yusufu kupachikiwa kesi ya jaribio la ubakaji…alipokuwa mule gerezani Mungu aliendelea kuwa naye…Na yale yale aliyoyaona Potifa kwa Yusufu..Mkuu wa gereza naye akayaona kwa Yusufu..akaona mbona tangu huyu kijana amekuja humu gerezani utaratibu wa gereza umebadilika…mambo yanakwenda vizuri…Na alipojaribu kumweka kuwa kiongozi wa wafungwa ndio mambo yalivyozidi kunyooka Zaidi, usumbufu wa wafungwa ulipungua…pengine alitamani hata Yusufu angeendelea kuwa mfungwa siku zote jinsi mambo yanavyokuwa yanakwenda vizuri mule gerezani.
Lakini ni nini tunaweza kujifunza hapo?…Hata katika hali ya utumwa na vifungo Mungu yupo na watu wake… Wengi hawalijui hilo?..wanadhani kama ni mkristo ukishapitia kwenye matatizo basi huo ni uthibitisho tayari Mungu kashakuacha…. Kitendo tu cha wewe kuwa mtumwa wa mwingine basi Mungu hayupo na wewe hivyo unahitaji maombi ya kufunguliwa…kitendo tu cha kufanya kazi ya kusafisha barabara basi upo chini ya laana na vifungo…Kuuza genge basi wewe ndio huna roho ya mafanikio Huo ni uongo wa shetani.
Hufanyi kazi wizarani lakini unafanya kazi katika nyumba ya mtu kama kijakazi…Kazi hiyo siyo uthibitisho kwamba Mungu hayupo na wewe…yupo na wewe huko huko kama alivyokuwa na Yusufu katika nyumba ya Potifa maadamu unajua umeokoka na unaishi kulingana na Maneno ya Yesu Kristo basi uwe na amani uwepo wa Bwana upo na wewe…Yusufu hakuwa na laana ya ukoo yeye kuuzwa utumwani…Alikuwa ni mwana wa Ibrahimu aliyebarikiwa….
Hivyo Kuwa tu mnyenyekevu usinung’unike ni suala la muda tu…utafika wakati utapelekwa hatua nyingine…lakini wewe tazama tu..kama kiongozi wako anapenda kuwa na wewe…na anaona anapata raha kuwa na wewe..na anafanikiwa sana anapokuwa na wewe kuliko alivyokuwa na wengine huko nyuma na hataki uondoke huo ni uthibitisho kwamba Mungu anafanikisha mambo yake kwaajili yako wewe…kama ilivyokuwa kwa Yusufu…Hivyo kuwa mnyenyekevu bado uwepo wa Bwana upo na wewe ni suala la muda tu…Usianze kusema anakutesa au anakutumia wewe kupata faida zake mwenyewe, wewe kuwa mtulivu endelea kuwa mwaminifu kama Yusufu.
Mungu hakushindwa kumtoa Yusufu nyumbani kwa Potifa na kwenda kumpa kwake binafsi na ambariki lakini alimbakisha pale pale kwa Potifa kwa kusudi maalumu.…Na Mungu hakuvifanikisha vitu vya Yusufu bali alivifanikisha vitu vya Potifa kwaajili ya Yusufu…Alifanikisha mifugo ya potifa na si ya Yusufu..ingawa chanzo cha baraka hizo ilikuwa ni Yusufu…Kadhalika aliistawisha kazi ya mkuu wa Gereza na si Yusufu..
Lakini ulipofika wakati, siku, tarehe, mwezi na Mwaka katika kalenda za kimbinguni…Njaa ilikuwa imekusudiwa duniani kote…na kwamba kwa kupitia mtu mmoja Yusufu dunia yote ilipaswa ipate Neema…Ndipo wakati wa Yusufu ulifika….Sasa hebu jaribu kufikiri endapo Mungu angemfungua Yusufu awe huru wakati wa Potifa na Mungu na kwenda kukaa kwake na kujenga nyumba nzuri na kumstawisha na kumbariki…je! huo wakati wa njaa ungefika na Yusufu na utajiri wake wote angekuwa wapi?..si na yeye angekufa na njaa tu kama wengine au angeuza kila kitu chake anunue chakula kama wengine?…manyumba yake yangekuwa wapi saahiyo?..mifugo yake ingekuwa wapi saahiyo?..Baba yake huko alikokuwa amemwacha Mungu alimbarikia katika mifugo na mali nyingi lakini pamoja na baraka zote hizo kutoka kwa Mungu walifunga safari kwenda Misri kutafuta chakula…unadhani endapo na Yusufu asingepitia hatua hizo angesalimika vipi na hiyo njaa ambayo imeikumbwa dunia?.
Kwahiyo wakati wa Mungu ni bora kuliko wakati mwingine wowote!..Na huo si mwanadamu anauamua..bali ni Mungu mwenyewe anaupanga mbinguni…tunachopaswa sisi kufanya ni kujinyenyekeza kila siku chini ya kusudi lake na kuishi Maisha yasiyo ya manungu’uniko tukijua kuwa uwepo wa Bwana bado upo na sisi…Usiseme mimi sasa nauza hiki au kile ningepaswa niwe kule au kama yule…Usiseme hivyo, jiangalie je! Unakwenda sawa na Mungu katika unachokifanya kama Yusufu?.. huku ukifahamu kuwa hata katikati ya dhiki, au katikati ya shida, au katikati ya misiba, au katikati ya utumwa mgumu, au katika ya kukandamizwa…Mungu yupo pamoja na sisi na anatuwazia yaliyo mema…
Endao tukiwa waaminifu kuishi katika Neno lake Kila mahali Mkono wa Mungu upo na sisi kutuongoza..hakuna tutakapopitia yeye asiwe pamoja na sisi biblia inasema hivyo…
Zaburi 139:5 “Umenizingira nyuma na mbele, Ukaniwekea mkono wako.…….7 Niende wapi nijiepushe na roho yako? Niende wapi niukimbie uso wako? 8 Kama ningepanda mbinguni, Wewe uko; Ningefanya kuzimu kitanda changu, Wewe uko. 9 Ningezitwaa mbawa za asubuhi, Na kukaa pande za mwisho za bahari; 10 HUKO NAKO MKONO WAKO UTANIONGOZA, Na mkono wako wa kuume utanishika. 11 Kama nikisema, Hakika giza litanifunika, Na nuru inizungukayo ingekuwa usiku; 12 Giza nalo halikufichi kitu, Bali usiku huangaza kama mchana; Giza na mwanga kwako ni sawasawa.”.
Zaburi 139:5 “Umenizingira nyuma na mbele, Ukaniwekea mkono wako.…….7 Niende wapi nijiepushe na roho yako? Niende wapi niukimbie uso wako?
8 Kama ningepanda mbinguni, Wewe uko; Ningefanya kuzimu kitanda changu, Wewe uko.
9 Ningezitwaa mbawa za asubuhi, Na kukaa pande za mwisho za bahari;
10 HUKO NAKO MKONO WAKO UTANIONGOZA, Na mkono wako wa kuume utanishika.
11 Kama nikisema, Hakika giza litanifunika, Na nuru inizungukayo ingekuwa usiku;
12 Giza nalo halikufichi kitu, Bali usiku huangaza kama mchana; Giza na mwanga kwako ni sawasawa.”.
Hivyo nakutia moyo wewe uliyeamua kujikana nafsi na kuukataa ulimwengu na kumfuata Yesu Kristo kwa gharama zozote, amesema yupo na wewe ni kweli yupo na wewe Neno lake si uongo Uwepo wa Bwana utakuwa nawe siku zote….Zidi kumtegemea, zidi kumwamini, ishi Maisha ya furaha, usijifananishe na wengine..Bali mtazame Mungu katika mambo yako yote. Na mambo yote Mungu atayafanikisha mbele zako kwa wakati wake.
TWEKA MPAKA VILINDINI.
KAMA MUNGU ANABORESHA KAZI ZAKE, KWANINI WEWE USIBORESHE ZA KWAKO?.
UTHABITI WA AGANO LA MUNGU KWA MKRISTO.
UPAKO NI NINI?
Nini maana ya maneno haya ya Bwana? “Nami nikiinuliwa juu ya nchi,NITAWAVUTA WOTE KWANGU”(Yohana12:32).
Vitabu vilivyothibitika vya historia vinavyoeleza maisha na vifo vya watakaifu wengi wa kwanza vinaeleza kuwa Antipa alikuwa ni kasisi aliyeteuliwa na mtume Yohana, kuwa mwangalizi wa kanisa lililokuwa Pergamo. Kama vile Timotheo alivyowekwa na Mtume Paulo kuwa mwangalizi wa makanisa yote baada yake.
Ikumbukwe kuwa kipindi hicho ndio wakati ambao kanisa la kwanza la Kristo lilikuwa katika kilele cha dhiki ambacho kiliasisiwa na mtawala katili wa kirumi aliyeitwa Nero (54 W.W -68 W.W)..
Nero ndiye aliyehusika kwa kumwagika kwa damu ya mashahidi wengi wa Kristo katika kanisa la kwanza. Na hiyo ilisababishwa na tukio la moto usiojulikana chanzo chake ni nini kuzuka huko Rumi mjini, na kusingiziwa wakristo ndio waliousababisha moto huo..Hivyo marufuku ikapigwa kwa mtu yeyote kujihusisha na imani ya kikristo.
Kipindi hicho mtu yeyote ambaye alionekana anaishikilia imani ya kikristo adhabu yake ilikuwa ni kifo na kama hutakufa basi utafungwa na kupelekwa uamishoni. Mtume Yohana baada ya kukwepa majaribio mengi ya kifo kimiujiza walimshika na kwenda kumfunga katika kisiwa cha Patmo. Huko ndipo Mungu alipompa ufunuo wa kitabu cha Ufunuo.
Na katika moja ya barua alizopewa azirudishe kwa yale makanisa 7, ndani yake Kristo alimkumbusha juu ya mtu aliyemfahamu anayeitwa Antipa..
Tusome:
Ufunuo 2:12 “Na kwa malaika wa kanisa lililoko Pergamo andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye na huo upanga mkali, wenye makali kuwili. 13 Napajua ukaapo, ndipo penye kiti cha enzi cha Shetani; nawe walishika sana jina langu, wala hukuikana imani yangu, hata katika siku za Antipa shahidi wangu, mwaminifu wangu, aliyeuawa kati yenu, hapo akaapo Shetani”.
Ufunuo 2:12 “Na kwa malaika wa kanisa lililoko Pergamo andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye na huo upanga mkali, wenye makali kuwili.
13 Napajua ukaapo, ndipo penye kiti cha enzi cha Shetani; nawe walishika sana jina langu, wala hukuikana imani yangu, hata katika siku za Antipa shahidi wangu, mwaminifu wangu, aliyeuawa kati yenu, hapo akaapo Shetani”.
Unaona Antipa alikuwa ni mtu aliyethibitika katika imani, japo alikuwa katikati ya vita vikali vya imani kama vile vya kuuawa na kuteswa, lakini hakuacha kuihubiri injili kwa nguvu. Katika utumishi wake alifanikiwa kuwageuza watu wengi wa mji ule kuacha kutoa sadaka kwa miungu , na masanamu. Lakini makuhani wa kipagani wa Rumi, walipomwona anawavuna watu wao wengi, na kuiacha Imani yao. walimfuata na kumkataza asiwafundishe watu imani za miungu migeni katika jamii yao. Na asiingilie miungu yao. Kama tu ilivyokuwa kwa Mtume Paulo alipofika kule Efeso, na kuwahubiria watu habari ya Kristo, wale wachonga vinyago walipoona biashara yao inakaribia kufa, walizusha vurugu katika mji.(Matendo 19:24)
Lakini Antipa hakusita kuwaambia bila kuogopa.. Alisikika akiwaambia
…“mimi siyatumikii mapepo ambayo yanaweza kunikimbia, yasiyo na maisha ya milele, mimi ninamwabudu Mungu muweza yote, Na nitaendelea kumwabudu Mungu muumba wa vyote, katika Kristo Yesu na Roho Mtakatifu siku zote za maisha yangu”.
Wale makuhani wakamjibu, na kumwambia mungu wetu sisi alikuwepo tangu zamani, lakini nyie mnamuabudu Yesu ambaye aliuliwa na Pontio Pilato kama uhalifu.
Lakini Antipa naye hakuacha kuwajibu..
“miungu yenu ya kipagani ni kazi ya mikono ya watu ambayo ndani yake kinachozaliwa si kingine zaidi ya maovu na machafuko”.
Antipa aliendelea kwa ushujaa huo huo kuikiri imani yake katika YESU KRISTO bila woga mbele zao daima. Wale makuhani wa kipagani walipoona mtu huyu hana dalili ya kuacha kumuhubiri Kristo, na kuwafundisha watu wasiabudu sanamu, uzalendo ukawashinda wakamkamata na kumpeleka mbele Ya hekalu la mungu wao Artemi. Wakamtupa ndani ya tanuru la moto jekundu la shaba ambalo walikuwa wameliandaa kwa ajili ya kutengeneza ng’ombe wao kwa shaba ile.wakamtupa ndani mule.
Wakati akiwa ndani ya moto ule mkali alisikika akiomba, akisema Mungu ipokee roho yangu. Na pia ziimarishe imani za wakristo wote. Kisha akalala katika usingizi wa amani kama ule wa Stefano.
Usiku ulipofika, ndugu zake wa imani wakaja kumchukua na kwenda kumzika pembezoni mwa mji huo wa Pergamo.
Siku zikapita siku zinakaenda, pengine akasahaulika na wengi lakini siku moja baada ya miaka kadhaa mbele, Mtume Yohana akiwa katika kisiwa cha Patmo.. alimsikia Yesu Kristo akimtaja kwa maneno haya:..
“Antipa shahidi wangu, mwaminifu wangu”..
Hadi sisi leo hii tunazisoma na kuziandika habari zake.
Mtume Paulo aliandika hivi juu ya watu hawa:
Waebrania 11:36 “wengine walijaribiwa kwa dhihaka na mapigo, naam, kwa mafungo, na kwa kutiwa gerezani; 37 walipigwa kwa mawe, walikatwa kwa misumeno, walijaribiwa, waliuawa kwa upanga; walizunguka-zunguka wakivaa ngozi za kondoo na ngozi za mbuzi; walikuwa wahitaji, wakiteswa, wakitendwa mabaya; 38 (watu ambao ulimwengu haukustahili kuwa nao), walikuwa wakizunguka-zunguka katika nyika na katika milima na katika mapango na katika mashimo ya nchi. 39 Na watu hao wote wakiisha kushuhudiwa kwa sababu ya imani yao, hawakuipokea ahadi; 40 kwa kuwa Mungu alikuwa ametangulia kutuwekea sisi kitu kilicho bora, ili wao wasikamilishwe pasipo sisi”.
Waebrania 11:36 “wengine walijaribiwa kwa dhihaka na mapigo, naam, kwa mafungo, na kwa kutiwa gerezani;
37 walipigwa kwa mawe, walikatwa kwa misumeno, walijaribiwa, waliuawa kwa upanga; walizunguka-zunguka wakivaa ngozi za kondoo na ngozi za mbuzi; walikuwa wahitaji, wakiteswa, wakitendwa mabaya;
38 (watu ambao ulimwengu haukustahili kuwa nao), walikuwa wakizunguka-zunguka katika nyika na katika milima na katika mapango na katika mashimo ya nchi.
39 Na watu hao wote wakiisha kushuhudiwa kwa sababu ya imani yao, hawakuipokea ahadi;
40 kwa kuwa Mungu alikuwa ametangulia kutuwekea sisi kitu kilicho bora, ili wao wasikamilishwe pasipo sisi”.
Kisha akamalizia na kusema..
Waebrania 12:1 “Basi na sisi pia, kwa kuwa tunazungukwa na WINGU KUBWA LA MASHAHIDI namna hii, na tuweke kando kila mzigo mzito, na dhambi ile ituzingayo kwa upesi; na tupige mbio kwa saburi katika yale mashindano yaliyowekwa mbele yetu”.
Tunapokuwa wakristo halafu bado tunashikilia mizigo ya vimini, mizigo ya makeup, mizigo ya nguo za kikahaba, mizigo ya uchawi, ushirikina, uzinzi na hasira… tutawezaje kupiga mbio kwa spidi kama hawa watu waliojikana nafsi siku ile?. Ikiwa leo hii mizigo ya uzinzi bado tunaishikilia, mizigo ya mustabation, mizigo ya betting, mizigo ya usengenyaji, mizigo ya rushwa, mizigo ya shughuli za ulimwengu huu zisizotupa hata nafasi ya kumfanyia Mungu ibada..Tutaweza siku ile kufananishwa na kundi hili la watu?.
Bwana hana upendeleo, kile apandacho mtu ndicho atakachovuna.. Mungu atusaidie sana tupande kilichochema, ili siku ile tuvune kilichochema. Tuitumie mizigo yetu. Tumtazame Kristo.
Ikiwa hujampa Kristo Maisha yako!..Nataka nikuambie haijalishi utakufa kifo cha heshima kiasi gani na kuzikwa na watu wengi kiasi gani…Kumbukumbu lako litakuwa limeishia hapo hapo hakuna mtu atakukumbuka wala Mbingu haitakukumbuka…lakini Ukitubu na kumwishia Kristo leo, ukasema kuanzia leo mimi ni anasa basii,..mimi na ulevi basii mimi na uasherati basii..ukaonyesha kwa vitendo kabisa kwamba umeachana na hivyo vitu…
Basi Yesu Kristo atakusamehe kama alivyosema katika Neno lake..na hata ukifa leo hii kumbukumbu lako halitasahauliwa kama Antipa..na Bwana atakupa kipawa cha Roho wake mtakatifu atakayekusaidia kushinda dhambi ulizokuwa unashindwa kuzishinda..na atakuongoza na kuijua kweli yote ya maandiko..Ikiwa upo tayari kufanya hivyo..hapo ulipo tubu na Bwana atakusamehe.
Ubarikiwe sana..
VIFO VYA MITUME WA YESU/ JINSI MITUME WALIVYOKUFA.
TUMEPEWA, SI KUMWAMINI TU KRISTO, ILA NA KUTESWA KWA AJILI YAKE;
ALIYE MKUU KATIKA UFALME WA MBINGUNI.
SIKU ILE NA SAA ILE.
WAMNGOJEAO BWANA WATAPATA NGUVU MPYA.
Utangulizi:
Tusomapo, habari za mashujaa hawa wa Imani, lengo lake ni kututia hamasa ya kutua mizigo yote ya dhambi inayotusonga , na kupiga mwendo kwa saburi katika safari yetu ya wokovu tuliyo nayo hapa duniani kama vile biblia inavyotuambia katika Waebrania 12:1. Tukijua kuwa lipo wingu kubwa la Mashahidi linalotuzunguka sikuzote.
Karibu katika maelezo mafupi ya watu hawa. Ili kusoma bofya Jina husika kuingia.
Zifahamu namba katika biblia na maana zake.
Tafsiri ya namba kibiblia.
Shalom, Jina la Bwana Yesu libarikiwe.
Kabla hatujaenda moja kwa moja katika tafsiri ya namba kibiblia, awali ya yote tunapaswa tufahamu kuwa hatuishi kwa kuangalia namba, hatutumii kigezo cha namba kuamua hatma ya Maisha yetu, au kutumia hizo kuunda siku fulani maalumu ya kuabudu, au kuifanya namba Fulani kuwa takatifu Zaidi ya nyingine. Lengo la kutoa tafsiri hizi ni kukusaidia wewe msomaji wa biblia kupata uelewa mpana zaidi jinsi namba hizi zilivyotumika na zinavyomaanisha rohoni.
Wakati mwingine Mungu anaweza kusema nawe kupitia namba, pengine kwa ndoto au maono au kwa kusoma. Hivyo ukipata uelewa wa kutosha juu tafsiri ya namba hizo kibiblia itakuwa rahisi kwako wewe kuielewa sauti ya Mungu..
Hii ni namba ya Mungu, inayoeleza utoshelevu. Mungu yupo peke yake yeye ni mmoja tu, na anajitosheleza yeye kama yeye. Hakuna mwanadamu au kiumbe kingine chochote kinachoweza kujitosheleza chenyewe isipokuwa Mungu peke yake.. Ni hiyo inayotupa ujasiri wa kumwabudu Mungu kwa amani yote tukijua kuwa hakuna mwingine yoyote pembeni yake anayeweza kuchukua nafasi yake au kumpindua.
Kumbukumbu 6:4 “Sikiza, Ee Israeli; Bwana, Mungu wetu, Bwana ndiye mmoja. 5 Nawe mpende Bwana, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote.
Hii ni namba ya Ushahidi: Kristo alipowachagua wanafunzi wake wengine wale wasabini aliwatuma wawili wawili(Luka 10:1). Manabii wawili tunaowasoma katika kitabu cha Ufunuo sura ya 11, ambao biblia inasema watatoa unabii wao siku 1260 yaani miezi 42, pale Yerusalemu wakiwa wamevaa nguo za magunia siku za mwisho haiwataji tu kama manabii bali inawataja kama Mashahidi ni kwasababu gani? Ni kwasababu wapo wawili.. Angekuwa ni mmoja, wasingeitwa mashahidi.
Hivyo na sisi unabii wowote au ndoto yoyote inaposemwa kwetu, kabla ya kuipokea ni lazima tupate uthibitisho wa Ushahidi Zaidi ya mara moja, Hata Farao alipoota ndoto, ilijirudia mara mbili ndipo alipofahamu kuwa Ndoto ile inatoka kwa Mungu..(Mwanzo 41:32)
Vile vile namba 2 inasimama kama namba ya muunganiko. Ndoa ni muunganiko wa watu wawili (Mwanzo 2:23-24). Vilevile muunganiko katika ya Kristo na kanisa lake. (1Wakorintho 12). Biblia takatifu ni muunganiko wa maagano mawili, la kale na jipya.
Hivyo na sisi tunapotembea wawili katika Imani tunapata nguvu Zaidi kuliko tukiwa mmoja mmoja.
Mhubiri 4: 11 “Tena, wawili wakilala pamoja, hapo watapata moto; lakini mmoja aliye peke yake tu awezaje kuona moto? 12 Hata ikiwa mtu aweza kumshinda yule aliye peke yake, wawili watampinga…”
Usipende kupigana vita ya kiroho peke yako.
Ni namba ya uthibitisho na uhakiki, mashahidi wanapokuwa watatu kila Neno linathibitika. Mungu alijidhirisha kama Mungu wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo. Kristo aliuonyesha utukufu wake katika ule mlima mrefu akiwa na wanafunzi wake watatu yaani Petro, Yohana na Yakobo, kama mashahidi walioshuhudia na kuona.
Halikadhalika hata katika kutoa hukumu, biblia inasema.
Mathayo 18:15 Na ndugu yako akikukosa, enenda ukamwonye, wewe na yeye peke yenu; akikusikia, umempata nduguyo. 16 La, kama hasikii, chukua pamoja nawe tena mtu mmoja au wawili, ili kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu kila neno lithibitike.
Vilevile, Mungu naye amethitika kwetu kati ofisi zake kuu tatu: Yaani Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu. Hii ni namba timilifu ya Mungu kwetu sisi wanadamu. Kama Mungu asingejifunua kwetu kupitia ofisi zake hizi kuu tatu leo hii tusingekaa aidha tumwelewe au tuokolewe au tumkaribie kwa namna yoyote ile. Pale tunapookolewa ni sharti tupite hatua tatu, ya kwanza ni utakaso wa Damu ya Yesu, ya pili ni ubatizo wa maji, na ya tatu ni ubatizo wa Roho Mtakatifu.
Hivyo tunapopata Ushahidi wa tatu katika mambo yote Tunathibitika Zaidi, kuliko tunapopata mbili. Vilevile tunapozingatia hatua hizo tatu za utakaso bila kuacha hata moja,. Ndipo tunapothibitika ipasavyo kwa Mungu.
Hii ni namba ya kueneza kwa jambo fulani au tukio Fulani sehemu zote. Pale Edeni, Mungu aliutokeza mto kupita bustanini na baada ya pale akaugawanya katika vichwa vinne (Mwanzo 2:4).Kama vile biblia inavyosema pembe nne za nchi (Ufunuo 7:1, Isaya 11:12,). Vilevile Bwana akiiadhibu dunia au nchi huwa anatumia fimbo zake nne nazo ni, njaa, tauni, upanga, na hawayani wa mwituni,Soma.
Ezekieli 14:21 Maana Bwana MUNGU asema hivi; Je! U zaidi sana nitakapoleta hukumu zangu nne zilizo kali juu ya Yerusalemu, yaani, upanga, na njaa, na wanyama wabaya, na tauni, niwakatilie mbali nayo wanadamu na wanyama?
Sehemu nyingine anatumia parare, tunutu, nzige, na madumadu..(soma Yoeli 2:25-27).
Lakini shetani naye vilevile anatumia namba hii, kuleta mafuriko yake ya uovu duniani. Ukisoma Ufunuo kuanzia sura ya 5 utaona wale wapanda farasi 4 ambao wanafunua roho ya mpinga-kristo inayofanya kazi duniani kote, wa kwanza akiwa mweupe, wa pili mwekundu, wa tatu wa mweusi na wanne ni wa kijivu..
Lakini ashukuriwe Mungu naye aliachilia roho 4 za kudhibiti hizo roho 4 za ibilisi duniani katika kanisa la Mungu..ndio wale wenye uhai wanne tunaowasoma katika Ufunuo 4:6
Hivyo kwa kuhitimisha namba nne ni namba ya kutekeleza kusudi fulani au kueneza jambo, sehemu zote.
Hii ni namba ya mwanadamu. Mwanadamu aliumbwa siku ya sita. Na vilevile inasimama kama mwisho wa kazi..Mungu alisitisha kazi yake yote aliyoifanya katika siku ya 6. Mwisho wa kazi ya mtu inaonekana katika namba 6. Hata katika Maisha ya kawaida umri wa kustaafu ni miaka 60, ambayo ni sawa na 10×6, baada ya hapo unaingia katika pumziko lako.
Rohoni kila mmoja wetu amepewa siku sita za kutumika. Hivyo tumia muda wako vizuri. Bwana anasema Je! Siku za mchana si 12?, yaani 6×2..Imetupasa kuifanya kazi maadamu ni mchana, usiku waja mtu asiweze kuitenda kazi.(Yohana 9:4).
Hivyo wakati wako ulionao hapa duniani, kibiblia upo chini wa namba hii 6,
Hii ni namba ya utimilifu. Kwamfano wana wa Israeli walipokuwa wanaingia katika nchi yao ya ahadi waliagizwa wauzunguke ukuta wa Yeriko mara 7 kisha utaanguka. Nebukadneza alikaa maporini kwa muda wa miaka 7 kabla ya kurudishiwa ufahamu wake na kuwa mfalme tena wa Babeli. Makanisa ya Kristo yapo saba. Na wajumbe wake saba..Vilevile mapigo ya mwisho ambayo Mungu atayamwaga duniani kote kumaliza kazi zote mbovu za ulimwengu huu yatakuwa saba.
Lakini pamoja na hayo yote hii namba katika biblia inasimama kama namba ya pumziko. Mungu aliumba dunia kwa siku sita na siku ya saba akapumzika. Sabato ya Bwana.
Hivyo na sisi pia Watoto wa Mungu tumeundiwa sabato yetu na Mungu ambayo tutapumzika naye. Nayo itakuwa katika ule utawala wa miaka 1000
Waebrania 4: 8 “Maana kama Yoshua angaliwapa raha, asingaliinena siku nyingine baadaye. 9 Basi, imesalia raha ya sabato kwa watu wa Mungu”
Hivyo siku tutakapoanza kutawala na Kristo katika ule utawala wa miaka 1000 katika roho tutakuwa katika namba hii 7 ya Mungu.
Inawakilisha jumla, tunaona Amri kumi za Mungu, Jumla yake zilikuwa ni 10, wale wanawali ambao waliokuwa wanamsubiria Bwana wao aje kuwachukua waingie karamuni, walikuwa 10, ambao nusu yao walikuwa werevu na nusu yao wapumbavu. Soma tena Luka 19:13.
Hivyo hii namba katika biblia inawakilisha jumla kamili.
Hii ni namba ya msingi na ya malango. Taifa la Israeli limenyanyuka kutokana na Watoto 12 wa Israeli. Vilevile Kanisa la Mataifa limezaliwa kutoka katika injili ya mitume 12 wa Kristo. Wakristo tumejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, namba 12. Mji ule, Mtakatifu Yerusalemu mpya utakaoshuka kutoka mbinguni, utakuwa na misingi 12 na malango 12 ambao ni wale mitume 12 wa Bwana, na makabila 12 ya Israeli. (Ufunuo 21)
Hivyo, palipo na msingi wowote wa rohoni, au malango yoyote ya mbinguni basi fahamu yameundwa kwa namba hii 12
Namba ya maombolezo. Danieli alifunga siku 21,akiomboleza.
Danieli 10:2 “Katika siku zile mimi, Danielii, nalikuwa nikiomboleza muda wa majuma matatu kamili. 3 Sikula chakula kitamu, wala nyama wala divai haikuingia kinywani mwangu, wala sikujipaka mafuta kabisa, hata majuma matatu kamili yalipotimia. 4 Na siku ya ishirini na nne ya mwezi wa kwanza, nilipokuwa kando ya ule mto mkubwa, Hidekeli; 5 naliinua macho yangu, nikatazama, na kumbe, mtu aliyevikwa nguo za kitani, viuno vyake vimefungwa dhahabu safi ya Ufazi;
Danieli 10:2 “Katika siku zile mimi, Danielii, nalikuwa nikiomboleza muda wa majuma matatu kamili.
3 Sikula chakula kitamu, wala nyama wala divai haikuingia kinywani mwangu, wala sikujipaka mafuta kabisa, hata majuma matatu kamili yalipotimia.
4 Na siku ya ishirini na nne ya mwezi wa kwanza, nilipokuwa kando ya ule mto mkubwa, Hidekeli;
5 naliinua macho yangu, nikatazama, na kumbe, mtu aliyevikwa nguo za kitani, viuno vyake vimefungwa dhahabu safi ya Ufazi;
Siku za kuomboleza kwetu, rohoni zinatimizwa kwa namba hiyo 21. Mungu anaweza kukupitisha katika maombolezo mfano wa Yeremia akiiombolezea Yerusalemu. Ukiona hivyo ujue upo katika siku hizi 21 rohoni,..upo wakati utafika yatakoma na Mungu atakujibu dua zako.
Namba ya kumaliza jaribu. Wana wa Israeli walizunguka nyikani kwa miaka 39 na mwaka wa 40 waliingia nchi yao ya ahadi, Musa, alikaa nyikani miaka 40 baada ya kuikimbia Misri, na mwisho wa miaka hiyo akarudishwa tena kwa ajili ya utumishi wa kuwaokoa wana wa Israeli. Kristo alijaribiwa nyikani siku 40.
Hata wewe kama ni mtoto wa Mungu, jiandae na 40 zako, kupitishwa jangwani. Kabla ya kufanywa kuwa chombo kiteule cha Mungu. Mtoto yeyote wa Mungu ni lazima apitishwe katika 40 zake ili amtengenezee Mungu Njia.. Isaya 40.
Hii ni namba ya kutekeleza hukumu. Mpinga-Kristo siku mwisho atapewa mamlaka ya kufanya kazi miezi 42, ambayo ni sawa na miaka mitatu na nusu..Vilevile wale mashahidi wawili wa Bwana watapewa nao ruhusu ya kutoa unabii wao miezi 42, huduma yao itafuatana na mapigo yale kama Musa na Eliya waliyokuwa wanayatekeleza Misri na Israeli. Kwa kufahamu zaidi soma kitabu cha Ufunuo sura ya 11.
Maachilio, kufanywa huru au wa kuanza upya tena. Mwaka wa 50 kwa wana wa Israeli uliitwa mwaka wa YUBILEE. (Walawi 25:8-13)Ni mwaka wa kuachwa uhuru kwa watumwa wote,.Katika agano jipya Roho Mtakatifu aliachiliwa katika siku ya Pentekoste ambayo ilikuwa ni siku ya 50 baada ya kufufuka kwa Bwana wetu Yesu Kristo.
Hivyo na wewe siku unapompokea Roho Mtakatifu rohoni, unahesabika upo katika namba hii ya maachilio yaani namba ya 50.
Ni namba ya utumishi: Bwana Yesu awachagua tena wanafunzi wake 70 wengine, kwa lengo la kuwatuma waende kuitenda kazi ya Mungu. (Luka 10:1). Utaona pia Musa aliwachagua wazee wengine 70 kwa ajili ya kumsaidia kazi ya kuwahukumu watu.(Hesabu 11:16).
Vilevile hii namba katika biblia inasimama kama idadi kamili ya kumaliza jambo fulani…Kwamfano wana wa Israeli walipopelekwa Babeli Mungu alimwambia Yeremia kuwa watakaa kule Babeli kwa muda wa miaka 70..
Ukisoma tena Danieli 9 utaona Mungu akimwonyesha idadi ya majuma yaliyobakia kwa taifa la Israeli mpaka mwisho wa dunia utakapofika, akaambiwa yatakuwepo majuma 70.
Hivyo na wewe siku utakapoona hii dunia imeisha basi ujue namba hii imetimia, vilevile utakapoona Kazi ya Mungu inahubiriwa kwa kasi tena, yaani utumishi wa Mungu umeamka tena, basi ufahamu watumishi hao wapo katika idadi ya hii namba 70 katika ulimwengu wa roho.
Hii ni mamba ya mpinga-Kristo. Soma Ufunuo 13 inamueleza yule mnyama na hesabu ya jina lake ambayo ni 666. Kimsingi, yule mpinga Kristo atakaponyanyuka, na kazi zake kuonekana basi rohoni atakuwa katika namba hii, na uthibitisho kuwa atakuwa katika namba hii, ni kuwa hata jina lake litakuwa na hesabu ya namba hii 666.
Hadi sasa tumeshafahamu mpinga-Kristo atatokea wapi..Atatokea si pengine zaidi ya kanisa la Rumi, katika kile kiti cha juu kabisa cha kipapa.
Leo hii mtu yeyote anayekalia kiti cha kipapa anajulikana kama VICARIVS FILII DEI.. Yaani tafsiri yake kwa kiswahili ni BADALA YA MWANA WA MUNGU.
Hivyo ukihesabu hizo namba za kirumi, utaona idadi yake inakuja moja kwa moja katika namba 666.
Jina hili lipo katika kofia ile ya mapapa yenye ngazi tatu. Hivyo pamoja na ishara nyingine nyingi zilizonazo kanisa hili, ambazo zinamuhusu mpinga kristo katika kanisa hili. Tunaojasiri wa kimaandiko kusema kuwa mpinga-Kristo atatokea katika kanisa hili la Rumi.
Hivyo ndugu hizi ni nyakati za mwisho, Dunia imeisha, hizi ni saa za majeruhi, ikiwa unadhani hii dunia itakuwa na miaka mingi tena mbeleni jiangalie mara mbili.
Kama hujaokoka, Muda ndio huu, saa ya wokovu ndio sasa, usisubiri kesho. Hapo ulipo chukua muda mchache, jitenge binafsi piga magoti ukiwa peke yako, lia mbele za Mungu wako, mwambie nimekosa nisamehe Baba yangu. Maanisha kufanya hivyo kwasababu hapo ulipo yupo karibu na wewe kukusikia na kukusamehe.
Ukishatubu dhambi zako kwa kumaanisha kuziacha, basi ufahamu kuwa Damu ya Yesu imeshakusafisha moyo wako, uthihirisho kuwa utasikia amani au utulivu wa ajabu ndani ya moyo wako kuanzia huo wakati. unachopaswa kufanya bila kupoteza muda, ni kuacha kwa vitendo vile vitu viovu ulivyokuwa unavifanya kabla..kama ulikuwa na miziki ya kidunia kwenye siku yako ni unaifuta, kama ulikuwa na una picha za ngono kwenye siku yako unafuta zote, kama ulikuwa mzinifu, unazidi na mtu ambaye si mke wako, unaacha mara moja..
Sasa Kristo akishaona Imani yako iliyo katika matendo, ataingia ndani yako kufanya makao kwako na kukupa nguvu ya kushinda vile vilivyosalia. Pia baada ya kuokoka kwako, bila kupoteza muda nenda katafute mahali utakapobatizwa katika ubatizo sahihi wa kuzamwishwa katika maji mengi, na Kwa jina la YESU KRISTO sawasawa na Matendo 2:38. Ili kuukamilisha wokovu wako.
Na baada ya hapo Mungu mwenyewe atakupa kiwapa cha Roho wake mtakatifu.
Ubarikiwe sana.jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
ZIFAHAMU HUDUMA KUU (10) ZA SHETANI DUNIANI.
Tofuati kati ya Myahudi, Mwisraeli na Muebrania ni ipi?
NENO NI LILE LILE, LAKINI UJUMBE NI TOFAUTI.
MKUU WA ANGA.
SWALI: Je ulipwaji wa Mahari ina ulazima wowote?..je ni Agizo la kibiblia? Na kama ni hivyo Je! Adamu alitoa mahari kwa nani ili ampate Hawa?
JIBU: Ndoa ya kwanza ilifungishwa na Mungu mwenyewe…Na hakukuhusika mahari wala viapo…Hiyo yote ni kwasababu Hawa hakuwa na Baba wala Mama…
Lakini sasa wake zetu wanao wazazi wao..hatuwatoi ubavuni mwetu kama Adamu alivyompata Hawa..Hatuna budi kuwatoa kutoka kwa wazazi wao…Na wazazi wao waliwalea na kuwatunza kwa gharama zao.
Hivyo sio vyema kuwaiba kutoka kwa wazazi wao na kuwafanya wetu…Hatuna budi kufuata taratibu za kuwatoa kutoka kwao na kuwaleta kwetu…Na taratibu hizo zinahusisha ulipwaji wa mahari. Ulipwaji wa mahari hakumaanishi kumnunua huyo mwanamke…hapana! Bali kumthaminisha Yule binti kwamba hajaokotwa tu.
Laiti kama tungekuwa tunawapata wake zetu kama Adamu kwamba Mungu anatuletea usingizi na kuwatoa kutoka ubavuni mwetu..hapo kungekuwa hakuna haja ya mahari wala ndoa kanisani..hapo mahari ina ulazima wowote?..haina ulazima kwasababu wametoka kwetu(kwenye miili yetu kama Adamu)…lakini tulio nao hawajatoka kwetu wametoka kwa wengine… Hivyo ni lazima mtu upitie hatua za kuposa, na kuposa kuna taratibu zake ikiwemo mahari,
Luka 2:4 “Yusufu naye aliondoka Galilaya, toka mji wa Nazareti, akapanda kwenda Uyahudi mpaka mji wa Daudi, uitwao Bethlehemu, kwa kuwa yeye ni wa mbari na jamaa ya Daudi; 5 ili aandikwe pamoja na Mariamu mkewe, ambaye amemposa, naye ana mimba”.
Luka 2:4 “Yusufu naye aliondoka Galilaya, toka mji wa Nazareti, akapanda kwenda Uyahudi mpaka mji wa Daudi, uitwao Bethlehemu, kwa kuwa yeye ni wa mbari na jamaa ya Daudi;
5 ili aandikwe pamoja na Mariamu mkewe, ambaye amemposa, naye ana mimba”.
Hivyo hatua hiyo ikishavukwa kinachofuata sasa ni kwenda kanisani…Tulipowatoa! tumewatoa katika jamii..watu wote walikuwa wanajua binti Yule hajaolewa..hivyo binti kwa idhini yake sasa hana budi kwenda kukiri mbele ya umati wa jamii ya watu wake na mbele ya kanisa la Kristo na mbele ya Mungu kwamba amekubali kwa idhini yake mwenyewe kuolewa na kijana huyo..Na kijana naye vivyo hivyo anatamka kwa kukiri..kuwa ushuhuda..Na hapo ndipo Mungu anapoiridhia kuwa ni ndoa takatifu ya kikristo.
Hivyo ndoa na mahari ni mambo ya kimaandiko kabisa hata Bwana wetu Yesu Kristo aliingia gharama ili kututoa katika ulimwengu…Ilimgharimu uhai wake ili tu atupate sisi bibi-arusi wake..
Je umeithamini gharama Kristo aliyoingia ili akupate wewe?..Damu yake ilimwagika pale msalabani kwaajili yako na yangu..ili sisi tuwe mali yake yeye…tuondoke katika ulimwengu tukaishi naye..Kama hujaokoka unasubiri nini?..siku ile utakuwa mgeni wa nani kule au utakuwa mfano wa wale wanawali wapumbavu tunaowasoma katika kitabu cha Mathayo 25?..Uchaguzi ni wako, mlango wa rehema bado upo wazi.
Maran atha. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Je! Ni sahihi kwa mkristo kuoa/kuolewa na mtu wa imani nyingine?
WAZAZI WA YOHANA NA YAKOBO.
KILEMBA CHA NEEMA, JE! UMEMVIKA MWANAO?
SIKU YA UNYAKUO ITAKUKUTAJE?
Shalom, jina la mfalme mkuu Yesu Kristo libarikiwe daima.Kama ukisoma kitabu cha Waebrania sura ile ya 11 yote, Utaona Mtume Paulo, akiwaelezea kwa mapana wale mashujaa wa Imani (Wingu kubwa la mashahidi) kuanzia wakati wa Habili kuelekea kwa Nuhu, mpaka kwa Ibrahimu, na manabii , jinsi walivyoipagania na kuishindania imani kwa ujasiri wote,..
Waebrania 11:4 “Kwa imani Habili alimtolea Mungu dhabihu iliyo bora kuliko Kaini…Kwa imani Ibrahimu alipoitwa aliitika, atoke aende mahali pale atakapopapata kuwa urithi; akatoka asijue aendako…Maana alikuwa akiutazamia mji wenye misingi, ambao mwenye kuubuni na kuujenga ni Mungu…. 24 Kwa imani Musa alipokuwa mtu mzima, akakataa kuitwa mwana wa binti Farao; 25 akaona ni afadhali kupata mateso pamoja na watu wa Mungu kuliko kujifurahisha katika dhambi kwa kitambo; 26 akihesabu ya kuwa kushutumiwa kwake Kristo ni utajiri mkuu kuliko hazina za Misri; kwa kuwa aliyatazamia hayo malipo….. 36 wengine walijaribiwa kwa dhihaka na mapigo, naam, kwa mafungo, na kwa kutiwa gerezani; 37 walipigwa kwa mawe, walikatwa kwa misumeno, walijaribiwa, waliuawa kwa upanga; walizunguka-zunguka wakivaa ngozi za kondoo na ngozi za mbuzi; walikuwa wahitaji, wakiteswa, wakitendwa mabaya;”
Waebrania 11:4 “Kwa imani Habili alimtolea Mungu dhabihu iliyo bora kuliko Kaini…Kwa imani Ibrahimu alipoitwa aliitika, atoke aende mahali pale atakapopapata kuwa urithi; akatoka asijue aendako…Maana alikuwa akiutazamia mji wenye misingi, ambao mwenye kuubuni na kuujenga ni Mungu….
24 Kwa imani Musa alipokuwa mtu mzima, akakataa kuitwa mwana wa binti Farao;
25 akaona ni afadhali kupata mateso pamoja na watu wa Mungu kuliko kujifurahisha katika dhambi kwa kitambo;
26 akihesabu ya kuwa kushutumiwa kwake Kristo ni utajiri mkuu kuliko hazina za Misri; kwa kuwa aliyatazamia hayo malipo…..
36 wengine walijaribiwa kwa dhihaka na mapigo, naam, kwa mafungo, na kwa kutiwa gerezani;
37 walipigwa kwa mawe, walikatwa kwa misumeno, walijaribiwa, waliuawa kwa upanga; walizunguka-zunguka wakivaa ngozi za kondoo na ngozi za mbuzi; walikuwa wahitaji, wakiteswa, wakitendwa mabaya;”
Wote hawa ni mashujaa wa Imani na Mtume Pauloa alianzana na utangulizi huo wa mashujaa hao ili mwishoni aufikishe ujumbe aliokuwa anataka kuufikisha, na ujumbe wenyewe tunausoma katika sura inayofuata..
Waebrania 12:1 “Basi na sisi pia, kwa kuwa tunazungukwa na wingu kubwa la mashahidi namna hii, na tuweke kando kila mzigo mzito, na dhambi ile ituzingayo kwa upesi; na tupige mbio kwa saburi katika yale mashindano yaliyowekwa mbele yetu, 2 tukimtazama Yesu, mwenye kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu; ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake aliustahimili msalaba na kuidharau aibu, naye ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu”.
Waebrania 12:1 “Basi na sisi pia, kwa kuwa tunazungukwa na wingu kubwa la mashahidi namna hii, na tuweke kando kila mzigo mzito, na dhambi ile ituzingayo kwa upesi; na tupige mbio kwa saburi katika yale mashindano yaliyowekwa mbele yetu,
2 tukimtazama Yesu, mwenye kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu; ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake aliustahimili msalaba na kuidharau aibu, naye ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu”.
Unaweza ukaona hapo lengo kubwa la Paulo kuwataja wale, ni ili kuwatia watu hamasa, kwamba wapige mbio kwa bidii kama wale walivyopiga…Kama wale walivyoshinda nao wao pia washinde, wapate wivu, hivyo kama kuna mizigo yoyote ya dhambi inayowalemea waitupe chini wapige mbio kwa saburi katika mashindani ya imani yaliyowekwa mbele yao.
Hivyo na sisi pia tumeona, tuanze kuandika, shuhuda mbali mbali za mashujaa wa Imani ambao habari zao zimethitishwa katika historia kuwa ni kweli.. wale ambao habari zao hazipo kwenye biblia, lakini utumishi wao wa injili umethibitishwa na maisha yao kwa ujumla.
Tunaandika hivyo ili kusudi na sisi ambao tunalegalega, tujifunze kwa wale, na vilevile tukijua kuwa ipo siku tutasimamishwa pamoja na wao kwenye viti vya hukumu kutoa hesabu ya mambo yetu yote tunayoyafanya sasa hivi duniani..Hivyo basi na sisi kwa kuwatazama hao tupate nguvu ya kukaza mwendo katika safari yetu ya wokovu na kuweka kando kila mzigo wa dhambi.
Leo kwa Ufupi tutamwangalia mtu mmoja anayeitwa JOHN WESLEY.
Baadhi yetu tunamfahamu, kama muasisi wa makanisa ya ki-Methodist. Huyu alizaliwa huko Epworth, nchini Uingereza mwaka 1703. Akiwa ni mtoto wa 15 kati ya watoto 19 waliozaliwa katika familia yao. John Wesley alianza kuwa na kiu ya kumtafuta Mungu tangu akiwa mdogo. Lakini ndoto zake za kuifanya kazi ya Mungu zilikuja kutimia baada ya kuhitimu chuo Oxford,alipokuwa chuoni Oxford ndipo Bwana alipoanza kuyabadilisha maisha yake kwa kasi ya ajabu. Baada ya hapo yeye na kaka yake aliyeitwa Charles waliunda kikundi cha kikristo pamoja na wenzao wawili chenye kauli mbiu ya “Kuishi maisha kama Kristo aliyoishi”, kuliko kuishi maisha ya kidini, safari yao ilianza kidogo kidogo walianza kwenda kuwatembelea wagonjwa mahospitalini, na wafungwa, na kuwahurumia maskini, n.k na kujifanya wao wenyewe kuwa vielelezo(njia ya kufuata) hivyo wakajiundia utaratibu wa kiroho ambao waliuita “(METHOD yaani NJIA”)..na kuanzia huo wakati wakazoeleka kuitwa WAMETHODISTI. Methodist ilivyoanza na akina Wesley sivyo ilivyo leo…Leo hii imebakia kuwa ni dini tu kama zilivyo dini nyingine. Katika safari yao walikumbana na vipingamizi vikali vya wakuu wa dini..lakini walishinda safari yao..
Baada ya hapo Wesley na wenzake Bwana aliwagusa kwa namna ya kipekee, wakaona umuhimu wa kwenda kufanya kazi ya umishionari duniani kote. Hapo ndipo injili ikaanza kupelekwa duniani kote kwa nguvu, kasi na kwa bidii ya ajabu hata zile sehemu ambazo zilikuwa ngumu kufikiwa kama Afrika zilifikiwa na nuru ya neno la Mungu. Huo ndio ule wakati wamisionari wengi walisafiri mabara ya mbali kama vile Asia na Afrika na Amerika ya kusini kusambaza injili. Walilenga kufundisha UTAKATIFU, Kama ndio nyenzo muhimu ya mtu kuokolewa sawasawa na (Waebrania 12:14 inayosema.. “ Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, NA HUO UTAKATIFU, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao”).
John Wesley daima alikuwa anatumia farasi wake kwenda kuhubiri injili, inakadiriwa mwendo aliozunguka na farasi kuhubiri sikuzote za maisha yake ni zaidi ya Km laki 4 ambayo ni sawa na kuizunguka dunia mara 10 kwa farasi..Nyakati hizo magari na ndege hizi tulizonazo hayakuwepo.
Wesley alikuwa ni mtu aliyeimarika kiroho sana, anasema hakumbuki kama alishawahi kupungua nguvu rohoni hata kwa robo saa tangu siku aliyozaliwa. Alisema hakuwahi kulala zaidi ya masaa 6 siku zote za huduma yake, kila siku alikuwa akiamka saa 11 alfajiri, na kwenda kuhubiri zaidi ya mara nne kwa siku, ili kwamba kwa mwaka afikishe kwa wastani wa mafundisho 800.
Mtu kama huyu kama angekuwa na usafiri tulio nao leo hii wa haraka kama gari au ndege angeshaizunguka dunia mara ngapi kuhubiri? Lakini sisi tunaokila kitu hatuwezi, Bwana atusaidie sana..
Kama ulikuwa hufahamu huyu ndiye mjumbe wa kanisa la 6 lijulikanalo kama Filadelfia linalozungumziwa katika kitabu cha Ufunuo 3.. Na hili ndio kanisa pekee ambalo Kristo alilisifia kwa matendo yake mema,
Ufunuo 3:7 “Na kwa malaika wa kanisa lililoko Filadelfia andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye mtakatifu, aliye wa kweli, aliye na ufunguo wa Daudi, yeye mwenye kufungua wala hapana afungaye, naye afunga wala hapana afunguaye. 8 Nayajua matendo yako. Tazama, nimekupa mlango uliofunguliwa mbele yako, ambao hapana awezaye kuufunga, kwa kuwa unazo nguvu kidogo, nawe umelitunza neno langu, wala hukulikana jina langu. 9 Tazama, nakupa walio wa sinagogi la Shetani, wasemao kwamba ni Wayahudi, nao sio, bali wasema uongo. Tazama, nitawafanya waje kusujudu mbele ya miguu yako, na kujua ya kuwa nimekupenda. 10 Kwa kuwa umelishika neno la subira yangu, mimi nami nitakulinda, utoke katika saa ya kuharibiwa iliyo tayari kuujilia ulimwengu wote, kuwajaribu wakaao juu ya nchi. 11 Naja upesi. Shika sana ulicho nacho, asije mtu akaitwaa taji yako”.
Ufunuo 3:7 “Na kwa malaika wa kanisa lililoko Filadelfia andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye mtakatifu, aliye wa kweli, aliye na ufunguo wa Daudi, yeye mwenye kufungua wala hapana afungaye, naye afunga wala hapana afunguaye.
8 Nayajua matendo yako. Tazama, nimekupa mlango uliofunguliwa mbele yako, ambao hapana awezaye kuufunga, kwa kuwa unazo nguvu kidogo, nawe umelitunza neno langu, wala hukulikana jina langu.
9 Tazama, nakupa walio wa sinagogi la Shetani, wasemao kwamba ni Wayahudi, nao sio, bali wasema uongo. Tazama, nitawafanya waje kusujudu mbele ya miguu yako, na kujua ya kuwa nimekupenda.
10 Kwa kuwa umelishika neno la subira yangu, mimi nami nitakulinda, utoke katika saa ya kuharibiwa iliyo tayari kuujilia ulimwengu wote, kuwajaribu wakaao juu ya nchi.
11 Naja upesi. Shika sana ulicho nacho, asije mtu akaitwaa taji yako”.
Yeye ndiye aliyechochea moto wa injili ya Kristo kupelekwa ulimwenguni kote, na wale walioshirikiana naye walifanya kazi kama yeye aliyoifanya…Wakati sisi waafrika tunaabudu miungu na kufanya matambiko ya kichawi, watu kama hawa walijitoa kwa hali na mali kutoka katika bara la Ulaya kama wamisionari kuja kutuletea sisi mwanga wa Injili. Na sisi je! tunafanya kipi ili kuwapelekea wengine injili?.
Bwana akubariki.. Tutaendelea na mashujaa wengine wa Imani kwa jinsi Bwana atakavyotupa neema…
MAMBO YA KUJIFUNZA KATIKA WARAKA WA TATU WA YOHANA.
MAMBO YA KUJIFUNZA KATIKA WARAKA WA PILI WA YOHANA.
NUHU WA SASA.
MAMBO YA KUJIFUNZA KATIKA KITABU CHA RUTHU: