Category Archive home1

Yesu aitwaye Yusto alikuwa ni nani? (Wakolosai 4:11).

Swali: Je huyu Yesu anayetwaja katika Wakolosia 4:11 alikuwa ni nani, na je ni kwanini aitwe hilo jina tukufu?


Jibu: Turejee..

Wakolosai 4:11 “Na YESU AITWAYE YUSTO; hao ni watu wa tohara. Tena hao peke yao ni watendaji wa kazi pamoja nami kwa ajili ya ufalme wa Mungu; nao walikuwa faraja kwangu”.

Katika Biblia Kristo mwokozi wetu hakuwa wa kwanza kuitwa jina YESU, bali walikuwepo watu wengine kadhaa kabla yake walioitwa kwa hilo jina, kwani lilikuwa ni jina linalojulikana Israeli yote,

Na tafsiri ya jina YESU ni  (YEHOVA-MWOKOZI), kama vile ilivyokuwepo YEHOVA-YIRE ambayo tafsiri yake ni YEHOVA mpaji n.k

Kwahiyo YESU ni jina lililokuwepo hapo kabla, kama tu Simeoni aliyeitwa Petro, hakuwa wa kwanza kuitwa Simeoni, au Yuda aliyemsaliti Bwana YESU hakuwa wa kwanza kuitwa Yuda, kwani hata mtoto wa Yakobo,  aliitwa Yuda, na ndio ukoo Bwana YESU aliotokea.

Sasa ni kitu gani kilichomtofuatisha YESU mwokozi wetu na maYesu wengine?.. si kitu kingine bali ni kiunganishi cha mwisho cha jina hilo,.. Aliyetufia anajulikana kama YESU KRISTO,  maana yake YESU MTIWA MAFUTA na MUNGU…

Wengine wanaitwa “Yesu wa Yusto”, wengine “Bar-YESU” (soma Matendo 13:6) lakini ni mmoja tu anaitwa “YESU KRISTO”.. Huyu kwa jina lake hili ndio tunapata ondoleo la dhambi na wokovu (Matendo 4:12).

Na kwa jina la YESU KRISTO, Tunafunguliwa na kuponywa magonjwa yetu, na ziadi sana ndio kwa jina hili tunapaswa tuhubiri na kuhubiriwa ili tupate ukombozi.

Lakini katika hizi siku za mwisho shetani amewanyanyua maYesu wengi wa uongo, ambao na si Yule wa uzima.

2Wakorintho 11:3 “Lakini nachelea; kama yule nyoka alivyomdanganya Hawa kwa hila yake, asije akawaharibu fikira zenu, mkauacha unyofu na usafi kwa Kristo.

4 MAANA YEYE AJAYE AKIHUBIRI YESU MWINGINE AMBAYE SISI HATUKUMHUBIRI, au mkipokea roho nyingine msiyoipokea, au injili nyingine msiyoikubali, mnatenda vema kuvumiliana naye!”

Yesu mwingine, (asiye KRISTO) anahubiriwa sasa na manabii na watumishi wa uongo, ambaye yeye hahitaji utakatifu.. ukiona unahubiriwa kwa jina la YESU lakini injili hiyo haikupeleki kuwa msafi mwilini na rohoni, badala yake unazidi kuwa wa kidunia, fikiri mara mbili ni Yesu gani uliyempokea, kwahiyo hatuna budi kujipima.

Lakini tukirudi kwenye swali!, Je huyu Yesu aitwaye Yusto alikuwa ni nani?..

Huyu Yesu aitwaye Yusto, alikuwa ni mmoja wa wafuasi wa Bwana wetu YESU KRISTO, ambaye alishirikiana na akina Paulo (watumishi wa MUNGU) kuhubiri injili, na alikuwa ni Myahudi (ndio maana Biblia inasema hapo alikuwa ni mtu wa tohara, maana yake aliyetahiriwa).

Maana ya jina Yusto ni “mwenye haki”.. na aliitwa “Yesu aitwaye Yusto”, kumtofautisha na YESU KRISTO. Huyu hakusimama kutaka aabudiwe, bali kinyume chake alikuwa anamhubiri YESU KRISTO.

Je umempokea Bwana YESU KRISTO?. Kama bado unasubiri nini?

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

JE BWANA YESU ALIMTOKEA YUDA BAADA YA KUFUFUKA KWAKE?.

MANENO SABA YA YESU MSALABANI.

YESU MNAZARETI,  ANWANI YA MSALABA.

Je shetani ana uwezo wa kujua mawazo ya mtu?

Uchambuzi na mwandishi wa kitabu cha Waefeso.

Print this post