Kukaramkia ni kufanya nini? (2Wakorintho 7:2)

Kukaramkia ni kufanya nini? (2Wakorintho 7:2)

Swali: Kukaramkia ni nini?

Jibu: Tusome,

2Wakorintho 7:2  “Tupeni nafasi mioyoni mwenu. Hatukumdhulumu mtu ye yote, wala kumharibu mtu, wala kumkaramkia mtu.

3  Sisemi neno hilo ili niwahukumu ninyi kuwa na hatia; kwa maana nimetangulia kusema, ya kwamba ninyi mmo mioyoni mwetu hata kwa kufa pamoja, na kuishi pamoja”

“Kukaramkia” ni Kiswahili kingine cha neno “Utapeli” (ambao unahusisha kuchukua fedha kutoka kwa mtu kwa njia ya ulaghai wa maneno). Mfano wa watu wanaokaramkia watu ni manabii wa uongo, na makristo wa uongo!, ambao wanaweza kutumia chochote kile kudanganya nacho watu, ili lengo lao wapate fedha kutoka kwao. ( Na fedha hizo ndizo zijulikanazo Kama mapato ya aibu, ambayo yanatajwa katika kitabu Cha Tito 1:7)

Katika siku hizi za mwisho manabii wa uongo wanatumia maji, mafuta, udongo na vyote vijulikanavyo kama visaidizi vya upako kulaghai watu, hivyo wanawakaramkia watu na kuchukua fedha zao na mali zao, huku wakiwaaminisha kuwa matatizo yao yameondoka.

Watumishi hawa wa uongo, maandiko yanasema kuwa mungu wao ni tumbo!!..

Wafilipi 3:17 “Ndugu zangu, mnifuate mimi, mkawatazame wao waendao kwa kuufuata mfano tuliowapa ninyi.

18  Maana wengi huenenda, ambao nimewaambieni mara nyingi habari zao, na sasa nawaambia hata kwa machozi, kuwa ni adui za msalaba wa Kristo;

19  mwisho wao ni uharibifu, mungu wao ni tumbo, utukufu wao u katika fedheha yao, waniao mambo ya duniani.

20  Kwa maana sisi, wenyeji wetu uko mbinguni; kutoka huko tena tunamtazamia Mwokozi, Bwana Yesu Kristo”

Mitume wa kanisa la kwanza hawakumkaramkia mtu yeyote, ili kupata faida.. Zaidi walihubiri injili kamili yenye kumgeuza mtu kutoka katika dhambi kuingia katika haki kupitia Yesu Kristo.

Na sisi hatuna budi kuwa kama hao, tuifanye kazi ya Mungu bila kumkaramkia mtu yeyote.

Maran atha!

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

Nini maana ya ELOHIMU?

Kwa namna gani mauti hufanya kazi ndani yetu na uzima kwa wengine? (2Wakorintho 4:12).

Je jina Eva na Hawa ni sawa?

USHIRIKA WA ROHO MTAKATIFU UKAE NANYI NYOTE.

JIHADHARI NA DHAMBI YA WIVU/HUSUDA.

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments