Sakafu ya mawe/ Gabatha ni nini?

Sakafu ya mawe/ Gabatha ni nini?

Neno hilo utalisoma katika andiko hili;

Yohana 19:13  Basi Pilato, aliposikia maneno hayo, akamleta Yesu nje, akaketi juu ya kiti cha hukumu, mahali paitwapo Sakafu ya Mawe, au kwa Kiebrania, Gabatha

Maana ya Gabatha ni “eneo lililoinuka”. Ni sehemu iliyojengwa mbele ya jumba la kifalme la Pilato ambapo hukumu zake alizitolea hapo. Kama biblia inavyosema paliitwa sakafu ya mawe. Maana yake palikuwa ni eneo la sakafu iliyojengwa kwa mawe.  (Tazama picha juu).

Hapo ndipo hukumu ya Bwana wetu Yesu Kristo ilipotolewa ya yeye kusulibiwa.

Lakini jambo ambalo unapaswa utafakari kuhusiana na tukio hilo, ni kuwa Mungu, ambaye ndiye muhukumu wa wanadamu wote, anasimama mbele ya kiti cha hukumu cha wanadamu kuhukumiwa. Mungu kukubali kuhukumiwa  Ni ishara ya unyenyekevu usiokuwa wa kawaida. Na hapo tunathibitisha kuwa hukumu za wanadamu hazitendi haki. Lakini utafika wakati na yeye mhukumu mkuu ataketi katika kiti chake cha enzi kuwahukumu wanadamu wote. Ambapo kwa haki kila mtu atalipwa sawasawa na matendo yake.

Jiulize wakati huo utakuwa upande upi?. Kwake hakuna upendeleo wa kibinadamu kama alivyofanya Pilato kwa wayahudi, kwake hakuna rushwa, kwake hakuna siri, yote yatamulikwa na kuwekwa wazi, na kama jina lako halipo katika kitabu cha uzima, utatupwa katika lile ziwa la moto, ambapo utateketea huko usiku na mchana.

Ufunuo 20:11  Kisha nikaona kiti cha enzi, kikubwa, cheupe, na yeye aketiye juu yake; ambaye nchi na mbingu zikakimbia uso wake, na mahali pao hapakuonekana. 12  Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi; na vitabu vikafunguliwa; na kitabu kingine kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima; na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu, sawasawa na matendo yao. 13  Bahari ikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake; na Mauti na Kuzimu zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake. Wakahukumiwa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake. 14  Mauti na Kuzimu zikatupwa katika lile ziwa la moto. Hii ndiyo mauti ya pili, yaani, hilo ziwa la moto. 15  Na iwapo mtu ye yote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto.

Je!  Umejiandaaje kukutana na mhukumu wa haki? Kumbuka huwezi kuokoka, ikiwa bado upo nje ya Kristo Yesu. Unachopaswa kufanya ni kutubu leo,  ili upate ondoleo la dhambi zako. Ndipo kuanzia huo wakati na kuendelea uwe na amani na Mungu wako,. Hakuna ukombozi kwa yoyote Yule zaidi ya Yesu Kristo.Huwezi kuokoka kwa nguvu zako mwenyewe. Yesu alikufa tayari kwa dhambi zako, ili aziondoe, akuhesabie sio mkosaji.

Ikiwa upo tayari leo kumkabidhi Bwana maisha yako ayaokoe na kuyaongoza, Basi fungua hapa kwa mwongozo wa sala ya Toba >>> KUONGOZWA SALA YA TOBA

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618. Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > WHATSAPP-Group

Mafundisho mengine:

Kiti cha Rehema kilikuwaje? (Kutoka 40:20)

Uga ni nini? Na kazi yake ni ipi kibiblia?

MAUTI NA KUZIMU ZIKAWATOA WAFU WALIOKUWAMO NDANI YAKE.

Wote wanaokumbwa na mauti sasa ni kutokana na dhambi zao?

Chetezo ni nini katika biblia? (Walawi 10:1)

“Shinikizo” ni nini kibiblia, Na maana yake rohoni ni ipi?

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments