Nini maana ya “mwondokeeni mtu mwenye mvi? (Walawi 19:32)”

Nini maana ya “mwondokeeni mtu mwenye mvi? (Walawi 19:32)”

Jibu: Turejee,

Walawi 19:32 “Mwondokeeni mtu mwenye mvi; heshimuni uso wa mtu mzee; nawe mche Mungu wako, Mimi ndimi Bwana”.

Maana ya kumwondokea ni “kumsogelea au kumkaribia ili kumsikiliza”. Hivyo biblia iliposema mwondokeeni mtu mwenye mvi, maana yake “tumsogeleeni mtu mwenye mvi na kumsikiliza”..

Na kwanini tumsogelee mtu/watu wenye mvi?..Ni kwasababu “kuna hekima katika wazee, kwani wameishi muda mrefu na kukutana na mengi na kujifunza mengi”. (wazee walio ndani ya KRISTO).

Ayubu 12:12 “Wazee ndio walio na hekima, Na katika kuishi siku nyingi iko fahamu”.

Soma pia Ayubu 32:6-7 na Mithali 23:22.

Hivyo ukitaka mashauri sahihi kuhusu maisha basi watafute walio na mvi, (yaani wazee) walio ndani ya Kristo, watakuambia au ukutahadharisha na mengi…

> Vile vile ukitaka maarifa na ushauri sahihi kuhusu ndoa, kazi au elimu watafute wenye mvi walio ndani ya KRISTO watakushauri na kukutahadharisha mambo yaliyo sahihi na yale yasio sahihi.

> Vile vile ukitaka mashauri sahihi ya kiroho watafute wenye mvi za kiroho watakushauri mambo sahihi.

Na mambo mengine yote ni hivyo hivyo, wenye mvi wanafahamu Zaidi kuliko vijana.

Lakini hasemi tu! Kumwondokea mwenye mvi… bali pia anasema “heshimuni uso wa mzee”. Maana yake mzee/wazee wanapaswa kuheshimiwa sana…. ni kosa kumvunjia mzee heshima, hata kama kafanya jambo lisilo sahihi mbele ya macho yako. Si ruhusa kumkemea mzee kama wanavyokemewa vijana au watoto.

 1Timotheo 5:1 “Mzee usimkemee, bali umwonye kama baba; na vijana kama ndugu;

2  wanawake wazee kama mama; wanawake vijana kama ndugu wa kike; katika usafi wote”.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

TUTAMKARIBIA MUNGU KWA IDADI YA MVI ZETU ROHONI.

HATA WAKATI WENU WA MVI NITAWACHUKUENI. (Isaya 46:3)

UTAKAPOKUWA MZEE, UTAINYOSHA MIKONO YAKO. NA MWINGINE ATAKUFUNGA

WALE WAZEE ISHIRINI NA WANNE (24), WANA KAZI GANI?

MWANAMKE ULIYEKOMAA KI-UMRI, ITAMBUE HUDUMA YAKO.

Rudi Nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments