SWALI: Samahani mtumishi kuna andiko linatoka kitabu cha Mhubiri 7:29 sijalielewa vizuri linamaanisha nini
Mhubiri 7:29 “Tazama, hili tu nimeliona; Mungu amemfanya mwanadamu mnyofu, lakini wamebuni mavumbuzi mengi”.
JIBU: Mungu alipomuumba mwanadamu alimuumba katika ukamilifu wote, Adamu na Hawa walikuwa ni watu ambao hawakuwa na kasoro yoyote, si ya kimwili, si ya kiroho. Waliumbwa katika ukamilifu wa furaha,amani, upendo, maarifa na kumcha Mungu.
Lakini ilifika wakati, hawakuridhika, na vile ambavyo Mungu alivyowaumba na kuwaweka, wakataka kuwa sawa na Mungu, wakabuni namna yao wenyewe ya kuishi, ya kutaka uhuru wao wenyewe. Na ndio hapo utaona wakashawishika kwenda kula matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya, ambayo Mungu aliwaambia wasile, Ili wakipate wanachokitafuta. Lakini matokeo yake ni kuwa mpaka sasa mwanadamu hajakipata alichokitafuta tangu wakati ule, kinyume chake ndio matatizo yalizidi kuongezeka japokuwa anajibunia kila siku njia zake mwenyewe za kuishi.
Mpaka sasa mambo hayo yanaendelea, tunavyoona watu wakijibadilisha maumbile yao, kisa tu hayawavutii machoni pao. Na ndio hapo utaona, wanawake wanachubua ngozi zao, ili waonekane weupe, wengine wanapaka make-up ili waonekane wa kitofauti na wenye mvuto zaidi, wanaweka kucha za bandia, wanavaa wigi za wazungu.. Yote hayo ni mavumbuzi mengi watu wanaojibunia..na kibaya zaidi leo hii wameshafikia mpaka hatua ya kubadilisha maumbile yao kwa kufanyiwa upasuaji na kunyeshwa madawa makali.
Hawataki tena kuwa wao wa asili kama Mungu alivyowaumba ,wanataka wawe kama wanavyotaka wao. Sasa badala mavumbuzi yao yawasaidie, kinyume chake ndio yanawaletea madhara kama sio kuwapoteza kabisa.
Hivyo, tunapaswa tujue kuwa si mpango wa Mungu tujigeuze mionekano yetu, kwasababu Mungu alituumba kwa mfano wake na sura yake, alishatuumbia ukamilifu ndani yetu,.Jukumu letu sisi ni kumcha yeye, na kuisiliza sauti yake basi.
Shalom.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali. Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
Mada Nyinginezo:
Nini maana ya tumeumbwa kwa mfano na sura ya Mungu?
Nini maana ya “yasiyokuwapo hayahesabiki”(Mh 1:15)
KITABU CHA YUDA: SEHEMU YA 1
VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 1
Ufunuo 12 inaelezea vita vya wakati upi?
LAKINI NINYI, NDUGU, MSIKATE TAMAA KATIKA KUTENDA MEMA.
Rudi nyumbani
Print this post
Swali: Yale maelezo ya Ufunuo 12:7-12, yanaeleza vita vya wakati upi?, ile ya kwanza kabisa kabla ya sisi kuumbwa au kuna nyingine iliyotokea tena?
Zipo vita mbili kuu zinazowahusu shetani na Malaika watakatifu.
Vita ya kwanza: Ni ile iliyopiganwa mbinguni, zamani sana kabla ya wanadamu kuumbwa, pale ambapo ibilisi (yaani shetani), alipoasi kwa kutamani kuwa kama Mungu, na hivyo akashindwa vita ile na kutupwa chini, na baada ya kushindwa vita hiyo akawa hana uwezo tena wala mamlaka ya kurudi katika nafasi yake mbinguni. (akaondolewa mbinguni). Lakini hiyo haikumfanya asifike kwenye enzi ya haki ya Mungu iliyopo mbinguni.
Hata katika maisha ya kawaida, mtu anapoasi katika ngazi Fulani kuu ya serikalini mfano Uwaziri, na hata kufikia kufukuzwa, na kuipoteza ile nafasi, hiyo haimfanyi asiwasilishe mashtaka yake mahakamani. Maana yake kama ana haki zake za msingi, anazozidai kule alipoondolewa, au anajambo la kupashitaki kule alipotoka, mahakama ya haki lazima imsikilize na kumpa haki yake kama anastahili. Kwasababu Mahakama ni moja ya muhimili wa serikali ambayo, haina upandeo fulani wa kuegemea wala kupendelea, ina uwezo hata wa kuishtaki serikali nzima ilimradi tu impatie mtu mmoja haki yake, na mtu yeyote anauwezo wa kwenda mahamani kushitaki.
Na pia enzi ya Mungu (yaani mbinguni) pamegawanyika katika sehemu kuu mbili, ipo sehemu ambapo Malaika wapo, ambapo ndio kule shetani alipokuwepo kabla ya kuasi, na pia kuna mahali pa kiti cha Hukumu ya Mungu.
Sasa shetani aliondolewa katika nafasi yake huko mahali malaika walipo, huko hawezi kufika tena wala kurudi, lakini mahali pa hukumu ya Mungu, mbinguni bado ana uwezo wa kufika, na kupeleka hoja zake, na mashtaka yake. Na Mungu siku zote ni wa haki, huwa hana upendeleo, anayestahili kumpatia haki yake anampatia na asiyestahili hampatii.
Sasa vita ya kwanza ilimwondoa shetani katika nafasi yake ya ukuu kule mbinguni, lakini haikuishia hapo, ipo vita nyingine ya pili ambayo ilianza kuendelea tangu alipoondolewa mbinguni mpaka sasa, na hiyo si nyingine zaidi ya vita katika enzi ya hukumu ya Mungu, huko shetani anafika kila siku, kupeleka hoja zake na mashtaka yake dhidi yetu. Na siku zote inajulikana vita vya mtu aliyeshindwa huwa ni vikali mno na vinaumiza kichwa, kwasababu kila siku utasikia yupo mahakamani kushitaki hiki au kile, mara kakata rufaa n.k. Kwahiyo hata baada ya shetani kushindwa mbinguni, bado anaendeleza vita katika enzi ya hukumu ya Mungu, iliyopo mbinguni.
Ndio maana kuna umuhimu mkubwa sana wa kumpokea Yesu, na kuishi maisha ya ukamilifu na uangalifu, kwasababu adui yetu shetani yupo kila siku kuchukua habari zetu na kuzifikisha mbele za Mungu, na kutushitaki.
Lakini tunapookoka na kuishi maisha ya uangalifu katika hii dunia, shetani anakosa hoja za kupeleka mbele za Mungu, na badala yake, malaika watakatifu wanapeleka mambo mazuri tunayoyafanya mbele za Mungu, ili tupewe thawabu. Kwasababu kama vile wanavyotumwa na Mungu kutulinda, vile vile wanachukua mambo yetu mazuri tunayoyafanya na kuyapeleka mbele za haki ya Mungu..
Mathayo 18: 10 “Angalieni msidharau mmojawapo wadogo hawa; kwa maana nawaambia ya kwamba malaika wao mbinguni siku zote huutazama uso wa Baba yangu aliye mbinguni”.
Na kamwe malaika watakatifu hawapeleki mashitaka yetu mabaya mbele za Mungu wetu..ni shetani peke yake ndio anafanya hivyo…
2Petro 2: 11 “Wenye ushupavu, wenye kujikinai, hawatetemeki wakiyatukana matukufu; ijapokuwa malaika ambao ni wakuu zaidi kwa uwezo na nguvu, hawaleti mashitaka mabaya juu yao mbele za Bwana”
Kwahiyo kwasasa kinachoendelea mbinguni, mahali pa haki ya Mungu, wanasimama malaika watakatifu kututetea na wakati huo huo anapita shetani kila mara kutushitaki.. Hiyo ndio vita inayoendelea sasa katika roho, (mapambano kati ya Mikaeli na malaika zake wakishindana na Yule joka na malaika zake), kuhusu mambo yetu sisi tuliomwamini Yesu, Malaika wanatutetea, shetani anatushitaki..(Kwa urefu juu ya hoja hizo fungua hapa >> Huduma ya Malaika watakatifu)
Na vita hivyo vitahitimishwa na unyakuo, wakati watakatifu watakapoondolewa duniani, shetani hatakuwa tena na mtu wa kumshitaki, wala hoja ya kwenda kupeleka mbele za Mungu, kuwashitaki wateule, kwasababu watakuwa wameshashinda na wapo mbinguni wakati huo, na hivyo atatolewa moja kwa moja katika hiyo enzi ya haki ya Mungu, na baada ya kuondolewa na kutupwa chini atakasirika kwasababu hatafika tena kumshtaki mtu yeyote wa Mungu, hivyo atashuka kwa hasira na kuanza kufikiri jambo lingine la kufanya..
Na jambo la kwanza litakalomjia ni kutafuta kufanya vita na vita na Taifa la Israeli, pamoja na wale wakristo vuguvugu walioachwa kwenye unyakuo, ambao watakataa kuipokea chapa yake. Hivyo atashuka chini na kumwingia Yule mwana wa kuasi (Mpinga-Kristo) na kuonyesha rangi zake zote kwa ulimwengu mzima, atawatesa watu kwa miaka mitatu na nusu (Miezi 42). Huo ndio ule wakati wa dhiki kuu.
kama tunavyosoma katika Ufunuo 12..
Ufunuo 12:7 “Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake; 8 nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni. 9 Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye. 10 NIKASIKIA SAUTI KUU MBINGUNI, IKISEMA, SASA KUMEKUWA WOKOVU, NA NGUVU, NA UFALME WA MUNGU WETU, NA MAMLAKA YA KRISTO WAKE; KWA MAANA AMETUPWA CHINI MSHITAKI WA NDUGU ZETU, YEYE AWASHITAKIYE MBELE ZA MUNGU WETU, MCHANA NA USIKU. 11 Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-Kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; ambao hawakupenda maisha yao hata kufa. 12 Kwa hiyo shangilieni, enyi mbingu, nanyi mkaao humo. Ole wa nchi na bahari! Kwa maana yule Ibilisi ameshuka kwenu mwenye ghadhabu nyingi, akijua ya kuwa ana wakati mchache tu”
Ufunuo 12:7 “Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake;
8 nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni.
9 Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye.
10 NIKASIKIA SAUTI KUU MBINGUNI, IKISEMA, SASA KUMEKUWA WOKOVU, NA NGUVU, NA UFALME WA MUNGU WETU, NA MAMLAKA YA KRISTO WAKE; KWA MAANA AMETUPWA CHINI MSHITAKI WA NDUGU ZETU, YEYE AWASHITAKIYE MBELE ZA MUNGU WETU, MCHANA NA USIKU.
11 Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-Kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; ambao hawakupenda maisha yao hata kufa.
12 Kwa hiyo shangilieni, enyi mbingu, nanyi mkaao humo. Ole wa nchi na bahari! Kwa maana yule Ibilisi ameshuka kwenu mwenye ghadhabu nyingi, akijua ya kuwa ana wakati mchache tu”
Hapo katika mstari wa 10, utaona Malaika mmoja anatangaza kwamba…“Sasa kumekuwa wokovu, na nguvu, na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake; kwa maana ametupwa chini mshitaki wa ndugu zetu, yeye awashitakiye mbele za Mungu wetu, mchana na usiku”..Maana yake Yule anayewashitaki watakatifu hawezi tena kupanda kwenda kuwashitaki…kashashindwa, kwasababu wateule wameshamshinda kwa damu ya mwanakondoo, na wameenda kwenye unyakuo mbinguni..huko hawezi kuwashitaki tena awatoe huko..
Lakini “ole wa nchi na bahari”..maana yake ole wa waliobakia ambao hawakwenda mbinguni. Ibilisi anashuka kwao mwenye ghadhabu nyingi, na pia ole kwa Taifa la Israeli, ambalo ndio “Yule mwanamke mwenye mimba (Ufu.12:1)”.
Hivyo hiyo biblia inatutahadharisha, juu ya mambo yanayokuja. Ndugu sasa hivi unafahamika kama ni mkristo lakini unazini kwa siri, unaiba, unaua, unacheza kamari, unavaa vibaya, unatukana, n.k..kumbuka shetani anayefikisha hayo kila siku mbele za haki ya Mungu, na kukushitaki. Na lengo lake ni ufe katika hizo dhambi ili uwe wake milele, au kama unyakuo utapita leo wewe ubaki, uingie katika dhiki kuu.
Dhiki kuu sio sehemu ya kutamani kuwepo, kama umeshindwa leo kumkiri Yesu wakati neema ya Mungu bado ipo, hutaweza siku ile katika dhiki kuu. Kama umeshindwa kuvumilia njaa ya siku moja katika kufunga ili uutafute uso wa Mungu hutaweza kuvumilia njaa ya miaka mitatu na nusu ya dhiki kuu. Kama leo hii kipindi cha amani unashindwa kujikana nafsi na kuchukua msalaba wako umfuate Yesu, kamwe hutaweza kufanya hivyo wakati wa dhiki kuu.
Hapo Yule malaika anasema… “Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-Kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; AMBAO HAWAKUPENDA MAISHA YAO HATA KUFA”.
Je leo hii unayapenda maisha yako kiasi kwamba, wokovu kwako ni jambo lililopitwa na wakati?, fashion za dunia,umaarufu, kusifiwa, kutukuzwa, kupendwa na kila mtu ndio mambo ya heshima kwako?…Hapo biblia inasema “ambao hawakupenda maisha yao hata kufa!!!”, ndio waliomshinda shetani!!.
Bwana Yesu pia alisema.. Yohana 12:25 “Yeye aipendaye nafsi yake ataiangamiza; naye aichukiaye nafsi yake katika ulimwengu huu ataisalimisha hata uzima wa milele”.
Kama bado hujampokea Kristo maishani, ni vizuri ukampokea leo, kwa kumwamini kwamba alikuja duniani akafa kwaajili ya dhambi zako, na akafufuka na kupaa mbinguni, na pia atarudi tena. Na kwa kutubu dhambi zako kwa kumaanisha kutozifanya tena, Na pia kwa kubatizwa katika ubatizo sahihi wa maji tele (Yohana 3:23), na kwa jina la Yesu Kristo (Matendo 2:38, 8:16), naye atakupa kipawa cha Roho wake mtakatifu, atakayekuongoza na kukutia katika kweli yote ya kuyaelewa maandiko.
Bwana akubariki.
HUDUMU YA MALAIKA WATAKATIFU.
JE! UMEPOKEA KWELI ROHO MTAKATIFU?
BIBLIA INAITAJA NJIA KUU YA MFALME, NJIA HII NI IPI?
Chuo cha vita vya Bwana ni kipi?(Hesabu 21:14)
JE NI KWELI SAMAKI NGUVA YUPO?
2Wathesalonike 3:13 inasema..
“Lakini ninyi, ndugu, msikate tamaa katika kutenda mema”.
Unajua mpaka biblia inakuambia usikate tamaa, inamaanisha kuwa si kitu chepesi kukishikilia wakati wote. Si kitu ambacho unaweza ukaona faida yake moja kwa moja pale unapokifanya.. Lakini katika yote hayo bado inakuambia usikate tamaa.
Ili jambo lolote liwe wema, ni lazima malipo yake yasilingane na huduma iliyotolewa. Kwamfano mtu anapokwenda kuwasaidia yatima au maskini, huo ni wema, kwasababu hawana cha kumlipa hata baada ya kuwapa mahitaji yao, au pale anapowasomesha ndugu, huo nao ni wema, kwasababu pesa hizo ungeweza kuzitumia katika mambo yake mengine lakini ameona vema, ujinyime yeye uwape wengine maarifa.. Au unapowapa wengine chakula au mavazi bila kuwachaji pesa au kuwadai kitu chochote huo ni wema.. Au unapowapa wengine maarifa ya ufalme wa mbinguni bila malipo yoyote huo nao ni wema mkuu sana n.k.
Lakini katika hayo, kuna wakati akili inaweza kukujia, ukajisikia kuchoka na kusema nimeshasaidia watu sana mbona sioni faida yoyote ya kufanya hivyo? Au mbona sioni nikirudishiwa fadhila yoyote kutoka kwao? Wacha nipunguze wema wangu, nianze kujijali mimi mwenyewe. Au nitafute mambo yangu mwenyewe.
Katika mazingira kama hayo, biblia inasema.. usichoke kutenda wema..Kwasababu ni mbegu nzuri sana ambayo unaipanda leo, lakini siku moja utavuna matunda yake ukiwa mvumilivu.
Wagalatia 6:9 “Tena tusichoke katika kutenda mema; maana tutavuna kwa wakati wake, tusipozimia roho”.
Hata kama utaona wale uliowatendea mema wamekutangulia,wewe umekuwa daraja kwao la kufika juu, au wengine wamekudharau kwa ukarimu wako, bado usichoke katika kutenda kwako, kwasababu hicho unachokipanda thamani yake ni kubwa kuliko fedha au dhahabu. Utakuja kujua vizuri utakapovuka kule ng’ambo.
Katika biblia, tunamwona, mtu mmoja aliyeitwa Mordekai, yeye alikuwa ni mlinda mlango wa mfalme, lakini siku moja baadhi ya watumishi walipanga njama ili wamuue mfalme. Mordekai alipopata habari, kwasababu alikuwa ni mtu mwema, hakukaa kimya bali alikwenda kutoa taarifa ya njama hizo, na hatimaye mfalme akanusurika kifo, lakini biblia inatuonyesha akasahaulika, muda mrefu ukapita, wala hakuna aliyekumbuka wala kujali wema wake.
Siku moja akiwa katika hatihati ya kuuliwa na adui yake aliyeitwa Hamani, biblia inatuambia usiku huo huo mfalme alikosa uzingizi kabisa, ndipo akaanza kupitia vitabu vya kumbukumbu za taarifa za kifalme, ndipo akakutana na tukio la wema alilofanyiwa na Mordekai, mfalme akauliza je mtu huyu alitendewa fadhila gani?, wakasema, hakutendewa lolote. Ndipo akatoa maagizo kwamba avikwe mavazi yake ya kifalme anayoyavaa yeye, kisha apandishwe kwenye farasi ambaye yeye mwenyewe ndiye anayempanda, kisha wamzungushwe mji mzima, huku akipigiwa mbiu, ili atukuzwe mbele ya watu wote, kwasababu mfalme AMEMUHESHIMU biblia inasema hivyo;. Soma Esta 6
Sasa mambo hayo yanafunua na ya rohoni pia. Ukiwa ni mtenda wema, ipo Heshima ya kipekee sana, itokayo kwa Mungu mwenyewe, italetwa juu yako, siku ile ikifika. Atakugawia ule utukufu wake mwenyewe,.. Biblia inasema..
Warumi 2:6 “atakayemlipa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake; 7 wale ambao KWA SABURI KATIKA KUTENDA MEMA WANATAFUTA UTUKUFU NA HESHIMA NA KUTOKUHARIBIKA, watapewa uzima wa milele; 8 na wale wenye fitina, wasioitii kweli, bali wakubalio dhuluma, watapata hasira na ghadhabu; 9 dhiki na shida juu ya kila nafsi ya mwanadamu atendaye uovu, Myahudi kwanza na Myunani pia; 10 BALI UTUKUFU NA HESHIMA NA AMANI KWA KILA MTU ATENDAYE MEMA, Myahudi kwanza na Myunani pia”;
Unaona? hivyo, usichoke kutenda mema, kumbuka wema mkuu ni pamoja na kuwakumbuka walio katika dhambi na kuwavuta kwa Bwana. Pia kuwafariji na kuwaombea wale waliowadhaifu katika Imani. Swali ni je! Katika maisha yako, ni mema mangapi, ulishawahi kufanya kwa ajili ya Mungu?
Bwana atusaidie, tuyatimilize yote.
NGAZI 7 AMBAZO MKRISTO NI LAZIMA AZIPANDE KUUFIKIA UKAMILIFU.
TUSIWE WATU WA KUPUNGUKIWA AKILI.
INJILI YA MANENO LAINI ITAKUGHARIMU.
FAHAMU UWIANO MUNGU ANAOHITAJI KUUONA KWETU.
Nini maana ya mhubiri 9:11? si wenye mbio washindao katika michezo?
SWALI: a) Naomba kujua tofauti Kati ya Hekima , Ufahamu na Maarifa kwenye biblia
b) jinsi gani vitu hivyo vinavyohusiana?
Mithali 2:6 “Kwa kuwa BWANA huwapa watu hekima; Kinywani mwake hutoka maarifa na ufahamu”;
2 Mambo ya Nyakati 1:10 “Basi sasa nipe hekima na maarifa, nijue kutoka na kuingia mbele ya watu hawa; kwa kuwa ni nani awezaye kuwahukumu watu wako hawa walio wengi”?
JIBU:
Maarifa ni uwezo wa kujua mambo mengi, na hiyo inakuja kwa kusoma sana, au kujifunza Neno la Mungu kwa bidii, au kusikiliza, au kupitia mazingira Fulani ambayo yatakupa uzoefu husika.
Mungu anatutaka sana watu wake tuwe na maarifa ya kutosha kuhusu yeye ili tusiangamie. Kwani biblia inasema,
Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa; (Hosea 4 :6)
Na ndio maana moja ya zile ngazi 7 zinazozumngumziwa katika kitabu cha 2Petro ambazo kila mkristo anapaswa azipitie, ni maarifa.
2Petro 1:5 “Naam, na kwa sababu iyo hiyo mkijitahidi sana kwa upande wenu, katika imani yenu tieni na wema, na katika wema wenu maarifa”
Tukikosa maarifa hata kama sisi tutasema ni wakristo tutashindwa kuwa na ujasiri na Mungu kwasababu hatujui tabia zake, tutashindwa hata kumwamini Mungu ipasavyo kwasababu hatuujui uweza wake, vilevile tutaishi maisha ya uvuguvugu kwasababu tu,hatuna maarifa ya kutosha ya kujua nyakati na majira tunayoishi. Hivyo maarifa ni nyenzo muhimu sana kwa mkristo yeyote.
Na hayo yanakuja kwanza kwa kuonyesha bidii kusoma Neno lake ‘kwa kujifunza’ na sio kama gazeti. Pia kwa kuonyesha kiu ya kutafuta kuijua kweli yake kwa kusikiliza mafundisho sahihi yatakayokusaidia kumjua yeye kupitia watumishi wake.
Hekima. Ni uwezo wa kupambanua, kuhukumu, na kufanya maamuzi sahihi. Sulemani alimwomba Mungu hekima na Mungu akampa, na ndio maana utaona mwanzoni kabisa,mwa hekima yake kujidhihirisha ilikuwa ni siku ile wale wanawake wawili walipomfuata, awamue kwa habari ya watoto wao, sasa kwa tukio lile kama asingekuwa na hekima ya ki-Mungu ndani yake asingeweza kupambanua lolote..(Soma 1Wafalme 3:16-18 )
Utaona tena wakati ule yule malkia wa Sheba alipokuja kumjaribu kwa mafumbo yake ya ndani, aliweza kuyafichua yote, kwa usahihi, mpaka yule malkia akashangaa sana (1Wafalme 10)
Vivyo hivyo katika siku hizi za mwisho, Mungu anasema walio na hekima, ndio watakaoelewa siri za Mungu na mafumbo ya yule mnyama(mpinga-Kristo) na kazi zake, inahitaji hekima ya Mungu ya kutosha iwepo ndani yetu ili tuelewe, vinginevyo, zipo habari katika haya maandiko kamwe hatutakaa tuzielewe, hususani zile zinazozuhusu nyakati za mwisho. Soma
Danieli 12:10 “Wengi watajitakasa, na kujifanya weupe, na kusafika; bali wabaya watatenda mabaya; wala hataelewa mtu mbaya awaye yote; BALI WAO WALIO NA HEKIMA NDIO WATAKAOELEWA.
Ufunuo 3:17 “tena kwamba mtu awaye yote asiweze kununua wala kuuza, isipokuwa ana chapa ile, yaani, jina la mnyama yule, au hesabu ya jina lake. 18 HAPA NDIPO PENYE HEKIMA. Yeye aliye na akili, na aihesabu hesabu ya mnyama huyo; maana ni hesabu ya kibinadamu. Na hesabu yake ni mia sita, sitini na sita”.
Ufunuo 3:17 “tena kwamba mtu awaye yote asiweze kununua wala kuuza, isipokuwa ana chapa ile, yaani, jina la mnyama yule, au hesabu ya jina lake.
18 HAPA NDIPO PENYE HEKIMA. Yeye aliye na akili, na aihesabu hesabu ya mnyama huyo; maana ni hesabu ya kibinadamu. Na hesabu yake ni mia sita, sitini na sita”.
Ufahamu ni uelewa. Ukikosa uelewa huwezi kutafuta maarifa, wala kuomba hekima. Wanyama hawana ufahamu, na ndio maana hawajui kumtafuta Mungu, halikadhalika, wanadamu pia tumepishana viwango vya ufahamu, na ndio maana wengine hawamtafuti Mungu kwasababu wamekosa ufahamu wa kujua umuhimu wa Mungu maishani mwao ni upi.
Kwa mfano mtu anayepata ufahamu wa kujua madhara ya zinaa, kamwe hawezi kwenda kuzini ovyo, kwasababu anajua mwisho wake utakuwa ni ukimwi, au mimba zisizotarajiwa. Au kijana anayepata ufahamu wa kujua elimu ina umuhimu gani kwake ,kamwe hawezi kuchezea shule.
Vivyo hivyo kibiblia mtu anayeikimbia dhambi huyo amepata ufahamu.
Ayubu 28:27 “Ndipo alipoiona na kuitangaza; Aliithibitisha, naam, na kuichunguza. 28 Kisha akamwambia mwanadamu, Tazama, kumcha Bwana ndiyo hekima, NA KUJITENGA NA UOVU NDIO UFAHAMU”.
Ayubu 28:27 “Ndipo alipoiona na kuitangaza; Aliithibitisha, naam, na kuichunguza.
28 Kisha akamwambia mwanadamu, Tazama, kumcha Bwana ndiyo hekima, NA KUJITENGA NA UOVU NDIO UFAHAMU”.
b) Hivyo vyote hivi vitatu ni nguzo kwa mtu yeyote kuwa navyo katika maisha yake, Ufahamu, maarifa na Hekima. Na vyote hivi Mungu anataka kuviona ndani yetu.
Hivyo tumche Bwana, pia tuonyeshe kumpenda na kumtafuta ndipo atakapotugawia.
Jiunge na kundi letu la mafundisho ya Biblia whatsapp kwa kubofya hapa > Group-whatsapp
Nini maana ya “katika wingi wa hekima mna wingi wa huzuni”.
HEKIMA YA KIMUNGU, INAINGIAJE MIOYONI MWETU?
Nakusalimu katika jina kuu lipitalo majina yote la Bwana wetu Yesu Kristo. Karibu tuyatafakari maneno yake pamoja, Tukisoma kitabu cha Mathayo ile sura ya saba inatuambia..
Mathayo 7:28 “Ikawa, Yesu alipoyamaliza maneno hayo, makutano walishangaa mno kwa mafundisho yake; 29 kwa maana alikuwa akiwafundisha kama mtu mwenye amri, wala si kama waandishi wao”.
Mathayo 7:28 “Ikawa, Yesu alipoyamaliza maneno hayo, makutano walishangaa mno kwa mafundisho yake;
29 kwa maana alikuwa akiwafundisha kama mtu mwenye amri, wala si kama waandishi wao”.
Maandiko hayo yanatuonyesha, mafundisho ya Yesu yalikuwa ni ya tofauti sana na jinsi yalivyotegemewa na watu wengi wakati ule, na hata yanavyochukuliwa na watu wengi leo hii, hapo anasema alipoanza kufundisha makutano walishangaa “MNO”.. Ikiwa na maana maneno yake yalikuwa ni tofauti sana na walichokuwa wanakitarajia kwake, na sababu ya kushangaa kwao ni kwasababu alikuwa akifundisha kama mtu mwenye AMRI, na sio kama waandishi wao.
Mtu mwenye amri sikuzote huwa ni mtu mwenye mamlaka, na mtu wa namna hiyo maneno yake huwa sio ya kupinda pinda, au ya kupamba pamba, bali maneno yake yananyooka, na ya wazi sana, kwamfano raisi akisimama mbele ya watumishi wake, huwa hawambelezi bembelezi, bali anapotoa maagizo, labda akisema, nataka huu mradi uishe ndani ya wiki mbili, hapo ni hakuna cha majadiliano, yule mtumishi ni lazima afanye ili uishe, asipofanya hivyo ni kazi hana, kamwe haji kumwambia naomba unisaidie kama ikikupendeza huu mradi uishe ndani ya wiki 2, Huwezi kusikia mwenye mamlaka yoyote kuzungumza maneno ya kusihi sihi namna hiyo.
Ndivyo Bwana Yesu alivyokuja kuhubiri ulimwenguni, ukisoma mistari iliyotangulia ya juu na mengine iliyofuata utaona maneno yake yalikuwa yamenyooka sana, bila maficho ficho tofauti na ya waandishi, ambao wenyewe walikuwa ni kufundisha desturi za kiyahudi tu kwa watu, na kuwapembeleza, hawawaambii watu wajibu wao kwa Mungu, au madhara yatokanayo na dhambi, au kumpenda Mungu kwa mioyo yao yote.
Lakini Bwana Yesu aliwaambia, mmesikia imenenewa, ‘Lakini mimi nawaambia hivi’ kuonyesha kuwa anayo mamlaka “YEYE”..Unaona, kuna mahali akasema kiungo chako kimoja kikikukosea king’oe ukitupe mbali na wewe, kuliko mwili wako wote kutupwa jehanum, mahali ambapo funza wa kule hawafi wala moto wake hauzimiki..Maneno ambayo usingekaa uyasikie yakitoka kwenye vinywa vya waandishi hata siku moja, kumwambia mtu apoteze kiungo chake kimoja kwa ajili ya kunusuru maisha yake ya milele, hakuna jambo kama hilo. Kuipoteza biashara yakoe haramu, au kuwapoteza marafiki zake waovu, au kupoteza hata kiungo cha mwili wake mwenyewe kinachomkosesha, huwezi sikia wakifundisha hivyo.
Aliwaambia, mtu asiyeuchukua msalaba wake, na kumfuata hawezi kuwa mwanafunzi wake, ampendaye Baba au mama kuliko yeye hamstahili, aipataye nafsi yake ataipoteza, na aipotezaye kwa ajili yake ataipata…
Wengi watakuja wakati ule wakisema, Bwana hatukutoa pepo, na kufanya miujiza mingi kwa jina lako? Lakini mimi nitawaambia Dhahiri, siwajui ninyi ondokeni kwangu mtendao maovu.
Jitahidini kuingia kupitia mlango uliomwembamba, kwasababu njia ni pana iendayo upotevuni. .
Unaona maneno hayo ni maneno yaliyonyooka, yanakueleza madhara ya kitu Fulani,kama usipochukua tahadhari.
Hata sasa kinywa cha Bwana ni kilekile, kwasababu anasema yeye ni yule yule jana na leo na hata milele. Bado anazungumza kama mtu mwenye amri, lakini watu wa leo, wanayatafsiri maneno ya namna hiyo kama KUHUKUMU au KUTISHA WATU. Watu wanataka kusikia maneno kama ya waandishi. ‘Yesu anakupenda’, wewe kuwa tu mtu mwema inatosha, utabarikiwa, utafanikiwa, waandishi hawataki kukueleza uvuuaji wako mbovu, kuwa hautakupeleka mbinguni, hawawezi kukueleza hivyo, kwasababu wanaogopa wasimpoteze mshirika wao.
Waandishi hawawezi kukueleza habari za siku za mwisho, wanahisi watakuogopesha, na hivyo utawakimbia.
Ndugu Ukiona upo mahali unahubiriwa maneno laini laini tu, wakati wote ujue kuwa Yesu hayupo hapo, bali ni waandishi ndio wanaokufundisha. Yesu sikuzote anazungumza kwa amri, ndivyo alivyo anasema..
Ufunuo 3:19 “Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu”.
Usidanganywe na mtu anayesema kufundishwa maneno laini ndio ishara ya upendo. Bwana Yesu hakufanya hivyo, lakini ni mtu aliyetupenda kuliko mtu yeyote aliyewahi kuishi hapa duniani.
Hii ni moja ya njia ambayo utayatambua mafundisho ya kweli ya Bwana..
Maran atha.
IFAHAMU HUZUNI NA FURAHA YA MALAIKA.
Amri zilizo ndogo alizozizungumzia Yesu ni zipi?
TUMEPEWA AMRI YA KUKANYAGA NGE NA NYOKA.
WhatsApp
SWALI: Shalom wana wa Mungu Naomba msaada kuelewa andiko hili;
Mhubiri 9:11 “Nikarudi, na kuona chini ya jua, ya kwamba si wenye mbio washindao katika michezo, wala si walio hodari washindao vitani, wala si wenye hekima wapatao chakula, wala si watu wa ufahamu wapatao mali, wala wenye ustadi wapatao upendeleo; lakini wakati na bahati huwapata wote”.
JIBU: Ukisoma utaona Sulemani anasema, nikarudi na kuona chini ya jua, ikiwa na maana kuwa ni jambo ambalo amekuwa akiliona likitokea mara kwa mara duniani, hivyo akaona aandike, pengine na sisi tukilichunguza tunaweza kuliona, au pengine tulishawahi kuliona sehemu fulani.
Kwamba si wote wenye mbio, au ujuzi, au maarifa, au nguvu, ustadi au hekima mara zote zinawasaidia kupata mafanikio makubwa kuliko wale wengine wasiokuwa navyo. Na ndio maana hapo mwishoni mhubiri anamalizia kusema “lakini wakati na bahati huwapata wote”..Ikiwa na maana majira hubadilika, leo elimu yako inaweza ikawa na faida ikakuletea mfanikio mengin lakini kesho, isiwe na maana sana, lakini yule mwingine ambaye hakuwa na elimu mambo yakambadilikia pengine kwa ujuzi wake tu wa kuzaliwa aliokuwa nao ukamfanya apate fursa nyingi kuliko wewe, na matokeo yake akawa juu yako.
Na ndio maana tunapaswa tujue majira hayo yanayobadilika yapo mikononi mwa Mungu, Bahati hizo anazitoa Mungu mwenyewe na sio mwanadamu.. Paulo alisema..
Warumi 9:16 “Basi, kama ni hivyo, si katika uwezo wa yule atakaye, wala wa yule apigaye mbio; bali wa yule arehemuye, yaani, Mungu”.
Vivyo hivyo na sisi, kwa kuwa hatujui ni majira gani yapo mbele yetu, basi tujifunze kuwa wanyenyekevu chini ya Mungu atoaye mema yote, bila kuwadharau wengine, haijalishi tutakuwa na maarifa mengi kiasi gani kuwazidi wao, au elimu kubwa kiasi gani, au nguvu hatupaswi kujiona tumefika, vinginevyo, neno hili linaweza kutimia mbele ya macho yetu kwa wale tunaowadharau.
1Petro 5:6 “Basi nyenyekeeni chini ya mkono wa Mungu ulio hodari, ili awakweze kwa wakati wake”;
NI NINI KITAKACHOTUFANYA TUPIGE MBIO BILA KUPUNGUZA MWENDO?
TUMEKUWA TAMASHA KWA DUNIA; KWA MALAIKA NA WANADAMU.
NITAUPATAJE UPENDO WA KI-MUNGU NDANI YANGU?
Warumi 13:14 “Bali mvaeni Bwana Yesu Kristo, wala msiuangalie mwili, hata kuwasha tamaa zake”.
Shalom, Jina la Bwana wetu Yesu Kristo, mweza wa yote libarikiwe daima. Nakukaribisha tena tuyatafakari kwa pamoja maneno ya uzima ya Bwana wetu.
Kama hayo maandiko hapo juu yanavyotuambia tusiuangalie mwili, kuangalia mwili maana yake ni kuujali mwili kupitiliza, na matokeo ya kufanya hivyo, mwisho wa siku huwa ni kuziwasha tamaa zake.
Na ikishafikia hatua hiyo ya kuwasha tamaa za mwili, ndio hapo unafanyika mtumwa au teja wa mwili, kiasi kwamba mwili ukitaka hivi, ni lazima upatiwe haja yake vinginevyo utakusumbua sana, kama sio kukuletea shida..
Leo kwa ufupi tutakwenda kuzitazama baadhi ya hizi tamaa za mwili na jinsi gani tutaweza kuzidhibiti sisi kama wakristo. Zipo nyingi lakini tutazitazama hizi kuu tatu (3), kwa leo.
Lakini kabla ya kwenda kuziangalia jambo ambalo tunapaswa tujue ni kwamba tamaa za mwili ni Mungu mwenyewe katuumbia, wala si shetani. Lakini hakutuumbia zitushinde, bali tuzitawale ili zitumike pale zinapopasa au zinapostahili.
Sasa embu tuzitazame baadhi ya hizo;
Mwili huwa unatamani kupumzika, na ndio maana utashangaa muda mwingine usingizi wenyewe unaanza kuja bila hata wewe kuukaribisha, sasa hiyo ni tamaa ambayo Mungu kaiweka katika mwili. Lakini sote tunajua si kila wakati ni wa kulala. Kwasababu unajua kabisa ukifanya hivyo utapata hasara ya mambo mengi.
Mithali 20:13 “Usipende usingizi usije ukawa maskini; Fumbua macho yako nawe utashiba chakula”.
Ukiundekeza usingizi hutakwenda kazini kwako, hutakwenda shuleni, hutafanya jambo lolote lenye faida, wakati mwingine utashindwa hata kuamka usiku usali, kama ikiwa wewe utakuwa ni wa kulala kila wakati. Lakini kiuhalisia ni kwamba, tamaa hii watu wengi wameweza kuishinda, kwasababu moja au nyingine, wameshauzoeza mwili mpaka mwili wenyewe umeshazoea,
Kwamfano utakuta labda mtu amejipangia ratiba ya kuamka kila siku za 11 alfajiri awahi kazini, kwa kuwa ameshajijengea huo utaratibu kwenye kichwa chake, ukishafika huo muda tu usingizi wenyewe unakata. Hata kama angejijengea iwe ni saa 9 alfajiri bado mwili ungezoea vilevile, lakini wakati huo huo utaona mtu mwingine atashindwa!! Inakuwa kama ni mtihani mkubwa kwake, , lakini ukiangalia sio kwamba yule aliyeweza amepewa uwezo tofauti hapana, utagundua kwamba mmoja kauendekeza na ndio maana unamshinda, na mwingine kaudhibiti na ndio maana anaamka muda ule bila shida yoyote. Japo mwanzoni alianza kwa shida, Lakini aliweza kwasababu alijizoesha.
Tamaa nyingine ya mwili ni chakula. Kila mmoja ameumbiwa njaa na kiu. Hivyo utafika wakati, unajisikia tu mwenyewe hamu ya kuweka kitu tumboni, au kuburudisha koo lako, na kama tunavyojua katika kula na kunywa ipo burudani Fulani mtu anaipata.
Lakini pia kwenye chakula au kwenye vinywaji mtu asipokuwa na kiasi tunajua ni kitu gani kitampata, yaani kila wakati yeye ni kula tu, ataishia kuvimbiwa, au kupata uzito wa kupita kiasi na magonjwa,
Lakini ni heri angekuwa inaishia kwenye kuvimbiwa tu, lakini mtu kama mlevi ni kwasababu gani amekuwa mlevi? ni kwasababu ameitii KIU ya mwili wake. Ameona mwili wake unahitaji kuburudisho cha namna ile na yeye akautii, akaanza kunywa mpaka akawa mlevi, anasahau madhara yatakayotoka na unywaji ule. Halikadhalika wavutaji sigara, na watumiaji wa madawa ya kulevya, wote, hawa ni matokeo ya kutii kiu na miili yao, na ndio maana wanakuwa majeta wa mambo hayo..
Mithali 23:20 “Usiwe miongoni mwao wanywao mvinyo; Miongoni mwao walao nyama kwa pupa. 21 Kwa maana mlevi na mlafi huingia umaskini, Na utepetevu humvika mtu nguo mbovu”.
Mithali 23:20 “Usiwe miongoni mwao wanywao mvinyo; Miongoni mwao walao nyama kwa pupa.
21 Kwa maana mlevi na mlafi huingia umaskini, Na utepetevu humvika mtu nguo mbovu”.
Aliyeacha pombe sio kwamba hakuwa na kiu kama uliyo nayo wewe, lakini alipata ufahamu ni jinsi gani ya kudhibiti matamanio ya kiu yake na hivyo, akajizuia. Akawa anakunywa tu soda. Na mwisho wa siku mwili wake ukazoe, mpaka ile kiu ya pombe ikakatika ndani yake. Asione tena ni shida kuiacha, hali kadhalika na sigara na madawa ya kulevya waliaocha, wengi wao walifanya vivyo hivyo.
Hii ni moja ya tamaa ya mwili, ambayo nguvu yake hainatofauti sana na ile ya usingizi au chakula, kuishinda, isipokuwa watu wengi wameiendekeza kwa kutaka kwao wenyewe. Kiuhalisia ni kwamba Mungu kaiweka tamaa hii ndani ya kila mwanadamu, Lakini itumike kwa wakati maalumu.. Na kwa kiasi pia. Na ni rahisi kuithibiti kabisa.
Mungu aliruhusu itumike kwa wana-ndoa tu, lakini pale mtu anapoanza kuichochea kabla ya wakati wake, hapo ndipo inapoleta madhara ambayo ni heri tu yangekuwa ya mwilini, lakini zaidi sana ni yanakwenda mpaka rohoni. Tutakuwa wanafki kama tutaweza kuudhibiti usingizi hata kama pale unapotulemea, mpaka inakuwa ni desturi yetu hatuoni shida tena, lakini tutashindwa kudhitibi zinaa.
Ukijizoesha utazishinda na wala hazitakuendesha, lakini ukiziendekeza kwa kuutazama mwili zitakushinda na utakuwa teja wa hizo. Utakuwa mzinzi kila siku, utakuwa mtazamaji wa video chafu mitandano, utakuwa mfanyaji wa punyeto kila siku, na hutashindwa kuziacha kwasababu umeuendekeza mwili kwa mambo kama hayo..
Wimbo 3:5 “Nawasihi, enyi binti za Yerusalemu, Kwa paa na kwa ayala wa porini, Msiyachochee mapenzi, wala kuyaamsha, Hata yatakapoona vema yenyewe”.
Sasa utaacha kwa namna gani?
Ni kwa kuviweka mbali vichochezi vyote vya uzinzi vilivyo karibu na wewe, kama vile kuepuka mazungumzo ya kizinzi ukutanapo na rafiki zako.
Waefeso 5:3 “Lakini uasherati usitajwe kwenu kamwe, wala uchafu wo wote wa kutamani, kama iwastahilivyo watakatifu;”
Vilevile kufuta muvi zote, na kuacha kuangalia tamthilia zenye maudhui za kimapenzi kwenye tv, pia kuacha kuperuzi peruzi na kusoma Makala na vitabu vyenye taswira kama hizo mitandaoni. Hilo litakusaidia sana kuzizima tamaa hizi za mwili. Kwasababu Biblia inasema..
Mithali 26: 20 “Moto hufa kwa kukosa kuni;…
Vilevile Kuacha kuchat-chat na watu wa jinsia tofauti na wewe, kwenye mambo yasiyokuwa na msingi..Hilo nalo ni lango ambalo shetani analitumia sana kuwanasa watu wengi kwenye mitego hiyo.
Ukizingatia hayo tamaa hizo zitazimika ndani yako, na wewe mwenyewe utashangaa jinsi ilivyo rahisi kuvishinda, utaweza kukaa hata miaka 50, bila kufanya hayo mambo na usione ugumu wowote ule.
Na jambo hili, sio tu kwa wale ambao hawajaoa/ au kuolewa. Ni kwa watu wote, kwasababu kama pia usipokuwa na kiasi katika hili kwenye ndoa yako, shetani naye atakujaribu mpaka kwenye mambo mengine yasiyompendeza Mungu. Na ndio hapo utasikia wana-ndoa wanaingiliana kinyume na maumbile, au wengine wanatoka nje ya ndoa zao, hiyo yote ni kukosa kiasi.. Biblia inasema..
1Wakorintho 7:5 “Msinyimane isipokuwa mmepatana kwa muda, ili mpate faragha kwa kusali; mkajiane tena, Shetani asije akawajaribu kwa kutokuwa na kiasi kwenu”.
Hivyo kwa kuhitimisha ni kwamba, kila mmoja wetu aanze kuishi maisha ya kutoutazama mwili, (yaani kutoruhusu tamaa za mwili wake kumwendesha). Na hiyo itatupelekea kuyashinda mambo mengi sana. Kwasababu adui wetu wa pili, baada ya shetani ni miili yetu. Na sisi hatupaswi kuwa watu wa mwilini kama wanyama. Bali watu wa rohoni, ambao tunaweza kudhibiti vyote kwa yeye atutiaye nguvu. Ambaye ni Bwana wetu Yesu Kristo.
Bwana akubarikijiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Soma na hapa; >> MOTO HUFA KWA KUKOSA KUNI.HATA UASHERATI NAO
Choyo ni nini kibiblia? (Luka 12:15, Zaburi 10:3)
KITABU CHA YUDA: SEHEMU YA 3
Nini maana ya “mkilichukia hata vazi lililotiwa uchafu na mwili”?
KUJIFUNUA KWA YESU KWA PILI.
UFUNUO: Mlango wa 15
Kuokoka tu peke yake hakutoshi, zipo ngazi saba, za kupanda ili kuufikilia ukamilifu Mungu anaotaka kuuona kwako kabla hujaondoka hapa duniani. Tunapomwamini Bwana Yesu, kwa kumkiri na kubatizwa, hatupaswi kuishia hapo hapo tu, kwani biblia inatuonyesha tutakuwa watu wasiokuwa na ushuhuda wowote, kama sio kufa kabisa kiroho.
Sasa kulingana na ufunuo Mtume Petro aliopewa na Roho mtakatifu aliandika mambo saba, ambayo mara baada ya mtu kuwa mkristo anapaswa atie bidii yeye mwenyewe kufanya bila kukawia kawia
Na mambo hayo tunayasoma katika kitabu cha 2Petro 1-12. Tukianzana na jambo la kwanza;
2Petro 1:5 “Naam, na kwa sababu iyo hiyo mkijitahidi sana kwa upande wenu, katika imani yenu tieni na wema, …..,
Tukishaamini, ni wajibu wetu kuonyesha Imani yetu kwa matendo yetu mema katika jamii inayotuzunguka, na kwa watu wote. Wema ni kitendo cha kuonyesha kujali, kuthamini, nidhamu na uaminifu.
Sio kwasababu watu wa kidunia, hawasalimii wengine, na sisi tusiwasalimie watu, au hawawasaidii watu na sisi tusiwasaidie, hawawaelekezi watu na sisi tuwe hivyo hivyo, huo sio wema, Halikadhalika wewe kama boss kazini kwako, kwasababu umeona, watu wengine wote wanawalipa wafanyakazi wao mshahara fulani kidogo na wewe unawaiga, huwapandishii mishahara wa kwako au huwapi bonus kwa kazi wanazokufanyia labda kwasababu hazina elimu kubwa au vinginevyo, huo sio wema, wape tu.. Kumbuka ule mfano Bwana Yesu alioutoa, juu ya wale watu aliowapeleka shambani mwake saa 11 jioni wamfanyie kazi, lakini kulikuwa na wale wengine waliokuwepo tangu asubuhi, na ulipofika wakati wa malipo walitaka wale waliochelewa walipwe kidogo kuliko wao. Lakini Yesu akawaambia..
Mathayo 20:14 “Chukua iliyo yako, uende zako; napenda kumpa huyu wa mwisho sawa na wewe. 15 Si halali yangu kutumia vilivyo vyangu kama nipendavyo? Au jicho lako limekuwa ovu kwa sababu ya mimi kuwa MWEMA”?
Mathayo 20:14 “Chukua iliyo yako, uende zako; napenda kumpa huyu wa mwisho sawa na wewe.
15 Si halali yangu kutumia vilivyo vyangu kama nipendavyo? Au jicho lako limekuwa ovu kwa sababu ya mimi kuwa MWEMA”?
Unaona? Wema wema kama huu pia ni wa kuigwa, housegirl wako au mlinzi wako nyumbani.
Barnaba naye alitajwa kama mtu mwema aliyeshuhudiwa na watu wote, kwa vile alivyokuwa anawajali sana ndugu, (Matendo 11:-25), hususani wale waliokataliwa, mpaka akaitwa mwana wa faraja.
Na sisi tunapaswa pindi tunapookoka, tupige hatua moja zaidi, tuonyeshe wema wetu kwa watu, tulionyeshee bidii, Kumbuka hilo ni moja ya matunda 9 ya Roho Mtakatifu yanayozungumziwa katika Wagalatia 5:22. (Utu wema)
Warumi 12:21 “Usishindwe na ubaya, bali uushinde ubaya kwa wema”.
Petro anaendelea kusema..
“ 1:5..na katika wema wenu maarifa,”
Tukishakuwa na uhakika sasa wema upo ndani yetu, tupige hatua nyingine mbele ya kuongeza maarifa juu yake. Maarifa yanayozungumziwa hapa ni maarifa ya kumjua Mungu, sio ya kibinadamu.
Wakristo wengi sana tunakosa maarifa haya, na hivyo tunaangamia, hatujui utendaji kazi wa Mungu kulingana na wakati na majira tuliyopo ni upi, na ni nini tunapaswa tufanye. Kwamfano, kutokujua kuwa ipo nguvu ya upotevu iliyoachiwa na Mungu mwenyewe, leo hii duniani ili iwadanganye watu wasiotaka kuitafuta kweli, na kwamba nguvu hiyo inafanyakazi katikati ya manabii wa uongo, kwa kupitia miujiza ya kweli ya Mungu. Sasa kwa kukosa kujua maarifa hayo Kunatufanya tuangamie,.
Vilevile kuhusiana na neema ya wokovu, kwamba haitadumu milele kwetu sisi watu wa mataifa, upo wakati itaondolewa na kurejeshwa kule Israeli, na huku kwetu tutabakia kuwa kama mafarisayo na masadukayo. Hilo nalo halijulikani na wakristo wengi, na ndio maana ukristo unachukuliwa juu juu tu, na watu wengi, kwasababu wanadhani muda utaendelea kuwepo wakati wote.
Na mambo mengine mengi kama hayo, yaliyo katika maandiko. Hivyo Mungu anatutaka tuwe watu wa kujifunza Neno lake kila siku, na kuyachunguza maandiko na kwa kuwa tunaye Roho wake mtakatifu ndani yetu atatusaidia kuyaelewa yote, na siri zote na mpango wote wa Mungu unaoendelea nao katika wakati wetu huu tunaoishi.
Hivyo hiyo ni hatua ya pili ya ukomavu, kuhakikisha maarifa ya ki-Mungu yanajaa ndani yetu.
“1:6 na katika maarifa yenu kiasi”,
Sasa tukishakuwa na maarifa, tunapaswa tuongezee juu yake kitu kingine kinachoitwa kiasi. Wapo wakristo ambao wamekamilika katika maarifa na utu wema, lakini kiasi hawana, hawawezi kujizuia kwenye baadhi ya mambo, mpaka mwisho wa siku mambo hayo yanageuka kuwa kama dhambi kwao. Utakuta mtakatifu anawaza muda wote kazi za mikono yake, mpaka anakosa muda wa kuwa faragha na Mungu, Na wakati anapopaswa afanya hivyo anasema amechoka, atasali siku nyingine, ataendea ibadani wiki nyingine?
Au mwingine, anashikilia sana kufanya mambo yasiyomjenga, kama vile kutazama Tv, Au kuchati, au kuperuzi internet kuangalia vya kidunia tu..na atatumia muda wake mwingi huko, kufanya hayo mambo, lakini kwenye kusali atatumia muda mchache.
Biblia inatuambia sisi tulio wa mchana tuwe na kiasi (1Wathesalonike 5:8). Ili tupate muda wa kuwa karibu na Mungu wetu.
“1:6…Na katika kiasi chenu saburi”,
Anasema, tukishajifunza kuwa na kiasi, basi tuongezee na saburi pia. Saburi, ni uvumilivu/ustahimilivu katika Imani. Tukikosa utahimilivu hususani pale tunapopishana na majaribu, ni ngumu sana kusonga mbele. Ni rahisi mtu kuacha Imani kwasababu anapitia njaa, au kwasasa hana kazi, au yupo katika mazingira yasiyofaa ya kubanwa, au ananyanyaswa na watu.
Mtume walikuwa wanafungwa na kupigwa, lakini bado walikuwa wanaendelea kuhubiri injili, kule kule walipofukuzwa.
Kukosa saburi, kwa ajili ya shida za kiulimwengu ambazo huwa hazidumu, ni ngumu sana kufikia kiwango ambacho Mungu alikitarajia kwetu, Vilevile kutokuwa wavumilivu katika huduma, au Imani, ni jambo ambalo linawakwamisha wakristo wengi sana, pale wanapoona matarajio yao hayajatokea kwa wakati walioupanga basi wanakata tamaa. Tumeaswa tusifike huko, tujifunze kuwa na saburi, kwasababu saburi ni mpango wa Mungu kwetu.
Warumi 5:3 “Wala si hivyo tu, ila na mfurahi katika dhiki pia; mkijua ya kuwa dhiki, kazi yake ni kuleta saburi; 4 na kazi ya saburi ni uthabiti wa moyo; na kazi ya uthabiti wa moyo ni tumaini;
Warumi 5:3 “Wala si hivyo tu, ila na mfurahi katika dhiki pia; mkijua ya kuwa dhiki, kazi yake ni kuleta saburi;
4 na kazi ya saburi ni uthabiti wa moyo; na kazi ya uthabiti wa moyo ni tumaini;
Hivyo hili jambo pia tulihifadhi ndani ya mioyo yetu. Tuliruhusu liwe na nafasi yake. Kwasababu hizo ndio ngazi za kufikia ukamilifu wa Kristo.
“1:6…na katika saburi yenu utauwa”.
Utauwa ni tabia ya uungu. Mungu ni Mtakatifu, hivyo ili na sisi tuwe na uungu ndani yetu tunapaswa tuwe watakatifu, Lazima tujizoeshe kuishi maisha ya utakatifu ya kuikataa dhambi, na mambo yasiyofaa.
1Petro 1:16 “kwa maana imeandikwa, Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu”
Ili tuweze kuishi maisha hayo tunapaswa tuwe watu wa maombi, watu wa kufunga, watu wa kuwatangazia wengine habari njema. Huo ndio utauwa ambao hata Bwana wetu Yesu Kristo alikuwa nao. Lakini kama hatutakuwa waombaji, bado hatukifikia kiwango hichi cha utauwa Bwana anachokizungumzia hapa.
“1:7 na katika utauwa wenu upendano wa ndugu,”
Sasa ikiwa utauwa umeshakamilika ndani yetu, jambo lingine ambalo tunapaswa kulionyeshea bidii ni upendano wa ndugu. Kumbuka hatua hizi huwezi kuzifikia kama yale ya chini hayajakamilika kwanza.
Upendano wa ndugu unaozungumziwa hapa sio ule wa ndugu wa kimwilini, hapana, bali ndugu katika Kristo. Tunapaswa tufikie hatua hii ya kupendana sisi kwa sisi kama wakristo. Jambo ambalo limekuwa gumu sana kufikiwa na wengi wetu wa leo, kusengenyana, kurushiana maneno, kuumizana, kana kwamba hatujaokolewa na Bwana mmoja.
Hivyo tujitathimini sana, tugeuke, kwasababu mambo haya hayahitaji maombi bali bidii.
1Petro 1:22 “Mkiisha kujitakasa roho zenu kwa kuitii kweli, hata kuufikilia upendano wa ndugu usio na unafiki, basi jitahidini kupendana kwa moyo”.
Unaona, unahitaji bidii ili kuupata.
“1:7…na katika upendano wa ndugu, upendo”.
Upendano wa ndugu ni tofauti na huu upendo unaozungumziwa hapa. Upendo huu ni upendo wa Ki-Mungu, ambapo mtu akiufikia huo basi mtu anakuwa karibu sana na Mungu, au kwa namna nyingine anakuwa anamjua sana Mungu.
Upendo huu ni upendo usio na masharti, kwamba kisa fulani kanifanyia hivi ndio nimtendee hivi hapana. Mungu aliupenda ulimwengu kisha akamtoa mwanawe wa pekee, sio kwamba tulimfanyia jambo jema kwanza, ndio maana akamtoa hapana, bali alimtoa kwa Pendo lake tu kwetu.
Huu ni upendo usio wa asili ya kibidamu au wanyama, bali asili yake ni mbinguni..Ndio ule unaozungumziwa katika 1Wakorintho 13 unasema..
4 Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni; 5 haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya; 6 haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli; 7 huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; hustahimili yote. 8 Upendo haupungui neno wakati wo wote; bali ukiwapo unabii utabatilika; zikiwapo lugha, zitakoma; yakiwapo maarifa, yatabatilika.
4 Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni;
5 haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya;
6 haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli;
7 huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; hustahimili yote.
8 Upendo haupungui neno wakati wo wote; bali ukiwapo unabii utabatilika; zikiwapo lugha, zitakoma; yakiwapo maarifa, yatabatilika.
Hapa ndipo kilele cha kila kitu.
Sasa tukishaweza kuyafikia hayo yote.. basi Mtume Petro anasema kwanza tutakuwa si watu wavivu wasio na matunda, pili hatutakuwa watu wa kujikwaa kwaa ovyo katika imani na zaidi ya yote tutakuwa na uwezo wa kuyaona mambo ya mambo yanayokuja.
2Petro 1:8 “Maana mambo hayo yakiwa kwenu na kujaa tele, yawafanya ninyi kuwa si wavivu wala si watu wasio na matunda, kwa kumjua Bwana wetu Yesu Kristo. 9 Maana yeye asiyekuwa na hayo ni kipofu, hawezi kuona vitu vilivyo mbali, amesahau kule kutakaswa dhambi zake za zamani. 10 Kwa hiyo ndugu, jitahidini zaidi kufanya imara kuitwa kwenu na uteule wenu; maana mkitenda hayo hamtajikwaa kamwe. 11 Maana hivi mtaruzukiwa kwa ukarimu kuingia katika ufalme wa milele wa Bwana wetu, Mwokozi wetu Yesu Kristo”
2Petro 1:8 “Maana mambo hayo yakiwa kwenu na kujaa tele, yawafanya ninyi kuwa si wavivu wala si watu wasio na matunda, kwa kumjua Bwana wetu Yesu Kristo.
9 Maana yeye asiyekuwa na hayo ni kipofu, hawezi kuona vitu vilivyo mbali, amesahau kule kutakaswa dhambi zake za zamani.
10 Kwa hiyo ndugu, jitahidini zaidi kufanya imara kuitwa kwenu na uteule wenu; maana mkitenda hayo hamtajikwaa kamwe.
11 Maana hivi mtaruzukiwa kwa ukarimu kuingia katika ufalme wa milele wa Bwana wetu, Mwokozi wetu Yesu Kristo”
Sasa tukishayajua hayo ni wakati wetu sisi sote tujitathimini tupo, katika hatua ipi na kisha, pale tulipozembea au tulipokwama tuanze kupatendea kazi kwa bidii. Tusiwe tu wasomaji wa makala,.
LIFAHAMU SANA JAMBO HILI, ILI MUNGU AKUTUMIE.
Kitabu kifupi katika biblia ni kipi, na ujumbe wake ni upi?
NA BAADA YA LILE TONGE, SHETANI AKAMWINGIA.
Tunapaswa tujue daraja kubwa sana la Mungu kututumia sisi kwa ajili ya kazi zake maalumu, ni kuishi maisha ya uchaji wa Mungu ambao utashuhudiwa na watu wa nje. Kiasi kwamba hata Mungu akipitisha neno lake kinywani mwako, watu wengi wataamini moja kwa moja kwasababu maisha yako tayari yalishawashuhudia hata hapo kabla.
Tukiweza kufikia hapo, basi tujue Mungu atatufunulia mambo mengi sana, kwa ajili ya ufalme wake. Kwamfano katika biblia tunamsoma mtu mmoja anayeitwa Anania, Mtu huyu alitumwa na Mungu ili amfuate Paulo, amwombee, na ambatize. Unaweza ukajiuliza kwani hapakuwa na wakristo wengine pale karibu na ile nyumba ambayo Paulo alikuwepo, mpaka Mungu amtoe Anania mbali kidogo, aje pale?. Jibu ni kuwa walikuwepo, lakini Mungu alijua ili ushuhuda wa mtume Paulo baadaye uwe na nguvu katikati ya watu atakaowasimulia ilimuhitaji mtu, aliyejulikana kweli na watu wengi ni mcha Mungu na mwaminifu, na ndio maana akampelekea huyu Anania..
Tusome kidogo..
Matendo 9:10 “Basi palikuwapo Dameski mwanafunzi jina lake Anania. Bwana akamwambia katika maono, Anania. Akasema, Mimi hapa, Bwana. 11 Bwana akamwambia, Simama, enenda zako katika njia iitwayo Nyofu, ukaulize katika nyumba ya Yuda mtu aitwaye Sauli, wa Tarso; maana, angalia, anaomba; 12 naye amemwona mtu, jina lake Anania, akiingia, na kumwekea mikono juu yake, apate kuona tena. 13 Lakini Anania akajibu, Bwana, nimesikia habari za mtu huyu kwa watu wengi, mabaya mengi aliyowatenda watakatifu wako Yerusalemu; 14 hata hapa ana amri itokayo kwa wakuu wa makuhani awafunge wote wakuitiao Jina lako. 15 Lakini Bwana akamwambia, Nenda tu; kwa maana huyu ni chombo kiteule kwangu, alichukue Jina langu mbele ya Mataifa, na wafalme, na wana wa Israeli. 16 Maana nitamwonyesha yalivyo mengi yatakayompasa kuteswa kwa ajili ya Jina langu. 17 Anania akaenda zake, akaingia mle nyumbani; akamwekea mikono akisema, Ndugu Sauli, Bwana amenituma, Yesu, yeye aliyekutokea katika njia uliyoijia, upate kuona tena, ukajazwe Roho Mtakatifu.
Matendo 9:10 “Basi palikuwapo Dameski mwanafunzi jina lake Anania. Bwana akamwambia katika maono, Anania. Akasema, Mimi hapa, Bwana.
11 Bwana akamwambia, Simama, enenda zako katika njia iitwayo Nyofu, ukaulize katika nyumba ya Yuda mtu aitwaye Sauli, wa Tarso; maana, angalia, anaomba;
12 naye amemwona mtu, jina lake Anania, akiingia, na kumwekea mikono juu yake, apate kuona tena.
13 Lakini Anania akajibu, Bwana, nimesikia habari za mtu huyu kwa watu wengi, mabaya mengi aliyowatenda watakatifu wako Yerusalemu;
14 hata hapa ana amri itokayo kwa wakuu wa makuhani awafunge wote wakuitiao Jina lako.
15 Lakini Bwana akamwambia, Nenda tu; kwa maana huyu ni chombo kiteule kwangu, alichukue Jina langu mbele ya Mataifa, na wafalme, na wana wa Israeli.
16 Maana nitamwonyesha yalivyo mengi yatakayompasa kuteswa kwa ajili ya Jina langu.
17 Anania akaenda zake, akaingia mle nyumbani; akamwekea mikono akisema, Ndugu Sauli, Bwana amenituma, Yesu, yeye aliyekutokea katika njia uliyoijia, upate kuona tena, ukajazwe Roho Mtakatifu.
Sasa utajiuliza uaminifu wake, umeandikwa wapi kwenye maandiko? Tukisoma matendo sura ile ya 22, utaona mtume Paulo alipowekwa mbele ya baraza la wayahudi ili kutoa ushuhuda wake, utaona akimtaja mtu huyu kama ni mtu aliyejulikana na wayahudi wote kwa utauwa wake..Sasa pale mbele kidogo utaona alisema..
Matendo 22:12 “BASI MTU MMOJA, ANANIA, MTAUWA KWA KUIFUATA SHERIA, ALIYESHUHUDIWA WEMA NA WAYAHUDI WOTE WALIOKAA HUKO, 13 Akanijia, akasimama karibu nami, akaniambia, Ndugu yangu Sauli, uone. Nikamwinulia macho yangu saa ile ile. 14 Akasema, Mungu wa baba zetu amekuchagua wewe upate kujua mapenzi yake, na kumwona yule Mwenye haki, na kuisikia sauti itokayo katika kinywa chake. 15 Kwa maana utakuwa shahidi wake kwa watu wote, wa mambo hayo uliyoyaona na kuyasikia. 16 Basi sasa, unakawilia nini? Simama, ubatizwe, ukaoshe dhambi zako, ukiliitia jina lake”
Matendo 22:12 “BASI MTU MMOJA, ANANIA, MTAUWA KWA KUIFUATA SHERIA, ALIYESHUHUDIWA WEMA NA WAYAHUDI WOTE WALIOKAA HUKO,
13 Akanijia, akasimama karibu nami, akaniambia, Ndugu yangu Sauli, uone. Nikamwinulia macho yangu saa ile ile.
14 Akasema, Mungu wa baba zetu amekuchagua wewe upate kujua mapenzi yake, na kumwona yule Mwenye haki, na kuisikia sauti itokayo katika kinywa chake.
15 Kwa maana utakuwa shahidi wake kwa watu wote, wa mambo hayo uliyoyaona na kuyasikia.
16 Basi sasa, unakawilia nini? Simama, ubatizwe, ukaoshe dhambi zako, ukiliitia jina lake”
Unaona? Kumbe Sifa zetu nzuri kwa Mungu miongoni mwa watu wanaotuzunguka, ni daraja zuri la Mungu kututumia kwa shuhuda zake nzito, lakini kama tutaitwa watumishi, halafu mitaani tuna shuhuda za matukio ya kizinzi, au tutajiita wakristo tuliookoka lakini mitaani tunajulikana kama wasengenyaji, au watukanaji, tunategemea vipi Mungu atutumie? Kama tutakuwa wakristo halafu kazini kwetu tunaiba, Mungu atatutumiaje kama alivyomtumia Danieli?
Kumbuka Danieli alikuwa mwaminifu sana katika kazi yake ya uwaziri mkuu kule Babeli, pamoja na kwamba alikuwa katika shughuli za kidunia lakini Mungu alimtumia, kutufikishia sisi maono makubwa ambayo mpaka sasa hivi yanatusaidia. Hiyo yote ni kwasababu alishuhudiwa na watu wote, ni mtu anayemcha Mungu. Nasi pia Kama tutaitwa wakristo halafu mitaani tunaonakena tumevaa nguo zisizo na heshima, watu watatuheshimuje?
Kumbuka sisi ni barua tunayosomwa na watu wote, biblia ndio inatuambia hivyo 2Wakorintho 3:2. Kama watu hawatatuheshimu, basi tujue kuwa Mungu ndio Zaidi.
Hivyo ni wajibu wetu, tubadilike, tuanze kujenga shuhuda zilizo hai, kwa watu wanaotuzunguka, tuweke kando mambo yote yanayotukwamisha. Vikao vya usengenyaji tujiepushe navyo, tabia za kidunia pia tujitenge nazo, Na kwa kufanya hivyo, kidogo kidogo, ndivyo tutakavyomvutia Mungu atutumie kama alivyofanya kwa Anania.
Bwana atusaidie sote.
SIRI YA KUFANIKIWA KWA MTUME PAULO.
Tofauti kati ya lijamu na hatamu ni ipi kibiblia?
MAMBO YA KUJIFUNZA KATIKA WARAKA WA PILI WA YOHANA.
YONA: Mlango 1
JE! NI WAPI UTAPOKEA HISIA ZA KWELI ZA KI-MUNGU?
Kuna maneno haya ambayo mtume Paulo alisema..
Wagalatia 1:15 “Lakini Mungu, aliyenitenga tangu tumboni mwa mama yangu, akaniita kwa neema yake, 16 alipoona vema kumdhihirisha Mwanawe ndani yangu, ili niwahubiri Mataifa habari zake; mara sikufanya shauri na watu wenye mwili na damu; 17 WALA SIKUPANDA KWENDA YERUSALEMU KWA HAO WALIOKUWA MITUME KABLA YANGU; bali nalikwenda zangu Arabuni, kisha nikarudi tena Dameski”.
Wagalatia 1:15 “Lakini Mungu, aliyenitenga tangu tumboni mwa mama yangu, akaniita kwa neema yake,
16 alipoona vema kumdhihirisha Mwanawe ndani yangu, ili niwahubiri Mataifa habari zake; mara sikufanya shauri na watu wenye mwili na damu;
17 WALA SIKUPANDA KWENDA YERUSALEMU KWA HAO WALIOKUWA MITUME KABLA YANGU; bali nalikwenda zangu Arabuni, kisha nikarudi tena Dameski”.
Tukisoma maneno hayo tunaweza kuona kuwa kipindi kile kulikuwa na utamaduni Fulani, kwamba ikitokea mtu ana wito wa kumtumikia Mungu, ni lazima kwanza, apande kwenda Yerusalemu (kanisa lilipoanzia), akaonane kwanza na wale mitume wa Bwana ambao ni nguzo, kama vile Petro, na Yohana, ili atambuliwe au awekwe kwanza chini ya mafundisho yao ndipo akatumike,Tukisoma maneno hayo tunaweza kuona kuwa kipindi kile kulikuwa na utamaduni Fulani, kwamba ikitokea mtu ana wito wa kumtumikia Mungu, ni lazima kwanza, apande kwenda Yerusalemu (kanisa lilipoanzia), akaonane kwanza na wale mitume wa Bwana ambao ni nguzo, kama vile Petro, na Yohana, ili atambuliwe au awekwe kwanza chini ya mafundisho yao ndipo akatumike,
Lakini tunamwona mtu kama Paulo alikuwa wa tofauti sana, yeye baada ya kuamini, hakujisumbua kwenda kutafuta kukaa chini ya watu hao wakubwa wenye vyeo, bali, aliondoka na kwenda zake mbali mahali panapoitwa Arabuni, kwa muda wa miaka mitatu huko akiutafuta uso wa Mungu.
Na hata aliporudi, biblia inatuambia hakusubiri kwanza akatambulike kwenye makanisa ya wakristo ndipo akahubiri injili, bali, alianza kuhubiri injili hivyo hivyo, wao walichosikia tu ni kwamba yule aliyeliharibu kanisa zamani sasa hivi anamuhubiri Kristo. Sio kwamba alikuwa anajionyesha yeye anajua Zaidi hapana, bali hakuona umuhimu wa kufanya hivyo, kana kwamba ni kitu cha lazima sana.
Wagaliatia 1:21 “Baadaye nalikwenda pande za Shamu na Kilikia. 22 Lakini sikujulikana uso wangu na makanisa ya Uyahudi yaliyokuwa katika Kristo; 23 ila wamesikia tu ya kwamba huyo aliyetuudhi hapo kwanza, sasa anaihubiri imani ile aliyoiharibu zamani. 24 Wakamtukuza Mungu kwa ajili yangu”.
Wagaliatia 1:21 “Baadaye nalikwenda pande za Shamu na Kilikia.
22 Lakini sikujulikana uso wangu na makanisa ya Uyahudi yaliyokuwa katika Kristo;
23 ila wamesikia tu ya kwamba huyo aliyetuudhi hapo kwanza, sasa anaihubiri imani ile aliyoiharibu zamani.
24 Wakamtukuza Mungu kwa ajili yangu”.
Pengine walipomuona anafanya kazi kwa bidii wengine walianza kuulizana je, mnamtambua huyu kwenye makanisa yenu? Wengine wakasema hapana, hatumjui Je! Mitume kule Yerusalemu wanamtambua? Wanasema hapana hawamtambui? Sasa katokea wapi huyu na injili hii ya moto namna hii?
Lakini hilo halikumfanya Paulo asihubiri injili, kisa hatambuliwi na mitume ambao ndio nguzo, bali aliitenda kazi akimwangalia yeye aliyemwita yaani YESU KRISTO. Na baada ya miaka mingi sasa, kama 14 hivi ndipo tunamwona anapanda kwenda Yerusalemu kuonana na mitume, kusikiliza mausia kutoka kwao. Lakini anasema alipofika kule hawakumuongezea chochote badala yake alimkuta Mtume Petro amekwenda kinyume na Imani, na hivyo akamkemea mbele ya wote.
Wagalatia 2:6 Lakini wale wenye sifa ya kuwa wana cheo; (walivyokuwa vyo vyote ni mamoja kwangu; Mungu hapokei uso wa mwanadamu); nasema, hao wenye sifa hawakuniongezea kitu;……. 11 Lakini Kefa alipokuja Antiokia, nalishindana naye uso kwa uso, kwa sababu alistahili hukumu. 12 Kwa maana kabla hawajaja watu kadha wa kadha waliotoka kwa Yakobo, alikuwa akila pamoja na watu wa Mataifa; lakini walipokuja wao, akarudi nyuma akajitenga, huku akiwaogopa waliotahiriwa. 13 Na hao Wayahudi wengine wakajigeuza pamoja naye, hata na Barnaba pia akachukuliwa na unafiki wao. 14 Walakini, nilipoona ya kuwa njia yao haiendi sawasawa na ile kweli ya Injili, nalimwambia Kefa mbele ya wote, Ikiwa wewe uliye Myahudi wafuata desturi za Mataifa, wala si za Wayahudi, kwa nini unawashurutisha Mataifa kufuata desturi za Wayahudi?
Wagalatia 2:6 Lakini wale wenye sifa ya kuwa wana cheo; (walivyokuwa vyo vyote ni mamoja kwangu; Mungu hapokei uso wa mwanadamu); nasema, hao wenye sifa hawakuniongezea kitu;…….
11 Lakini Kefa alipokuja Antiokia, nalishindana naye uso kwa uso, kwa sababu alistahili hukumu.
12 Kwa maana kabla hawajaja watu kadha wa kadha waliotoka kwa Yakobo, alikuwa akila pamoja na watu wa Mataifa; lakini walipokuja wao, akarudi nyuma akajitenga, huku akiwaogopa waliotahiriwa.
13 Na hao Wayahudi wengine wakajigeuza pamoja naye, hata na Barnaba pia akachukuliwa na unafiki wao.
14 Walakini, nilipoona ya kuwa njia yao haiendi sawasawa na ile kweli ya Injili, nalimwambia Kefa mbele ya wote, Ikiwa wewe uliye Myahudi wafuata desturi za Mataifa, wala si za Wayahudi, kwa nini unawashurutisha Mataifa kufuata desturi za Wayahudi?
Mpaka mwishoni kabisa mwa huduma yake, Paulo anashuhudia kwa uvuvio wa Roho kuwa yeye ndiye aliyefanya kazi kuliko hata mitume wengine wote waliomtangulia. Na sisi tunalithibitisha hilo.
Sasa habari hiyo inatufundisha nini sisi wa kanisa la leo.
Kumbuka wenye vyeo na wenye sifa waliojulikana zamani ni 12 tu, ndio wale mitume wa Bwana Yesu, lakini leo hii wenye vyeo na wenye sifa katikati ya kanisa la Mungu, idadi yake haihesabiki. Kiasi kwamba watu wengi wameshindwa kumtumikia Mungu, kisa tu, kuna ngazi zimewekwa hapo juu yao, ambazo ni lazima wazipitie kutoka kwa viongozi wao waliowatangulia au wapate kibali kwanza cha kufanya hivyo.
Ndugu sio lazima upokee kila agizo chini ya kasisi wako, ndio ni vizuri kufanya hivyo, ikiwa huwekewi vikwazo, au hutumii nguvu nyingi kutumika, lakini mara nyingi zinakwamisha huduma za watu wengi sana Mungu alizoweka ndani ya mioyo yao. Wakati mwingine utaambiwa pitia shule ya biblia miaka 4, ndipo uhitimu utumike.
Si kila kitu ni cha kutafuta kujiweka chini ya mtu Fulani kwanza, wakati mwingine Mungu anataka aanze kutembea wewe peke yako, akufundishe wewe kama wewe. Maadamu nia yako ni njema kwake, na una lengo kweli la kuujenga ufalme wa Mungu hilo tu linatosha. Kumbuka hiyo haimaanishi kuwa usijifunze kutoka kwa wengine hapana, lakini ujijengee akilini kuwa, Mungu amekuita umtumikie yeye, na si wanadamu.
Alilolichagua mtume Paulo, ndio hilo na likamsaidia sana,. Nasi pia tujitahidi kupunguza mizigo ya kuwategemea wanadamu, zama hizi ambazo watu wa namna hiyo wapo wengi, unaweza ukajikuta unadumaza huduma Mungu aliyoiweka ndani yako.. Wewe fanya utakuja kuwafuata baadaye.
JINSI PAULO ALIVYOPAMBANA NA UJINGA WA ROHONI.
Makao ambayo Yesu alikwenda kutuandalia ni yapi?
Nini maana ya “Tumejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii”?
Kwanini Yesu aliwakataza mitume wake kumdhihirisha?
ANGALIENI MWITO WENU.