Mstari huu unamaana gani? ″Walakini hautapotea hata Unywele mmoja wa Vichwa vyenu? (Luka21:18)

Mstari huu unamaana gani? ″Walakini hautapotea hata Unywele mmoja wa Vichwa vyenu? (Luka21:18)

JIBU: Hii ni kuonyesha kuwa Bwana hakuja kukomboa roho zetu tu basi, bali hata miili yetu pia..Na aliposema hata unywele mmoja wa vichwa vyenu hautapotea, alikuwa anaamanisha kuwa hata kile kinachoonekana kuwa hakina thamani katika mwili wetu hakitapotea..vyote vitarejeshwa tena, ..Ikiwa ni mwamini alikufa hana mguu, basi siku ile ya ufufuo mguu wake utarejeshwa ikiwa alikufa na upara juu ya kichwa chake, basi nywele zake zote zitarejea katika siku ile na kuwa kama kijana. Na baada ya kurejeshwa ndipo miili mipya ya utukufu kutoka mbinguni ambayo asili yake ni mbinguni na sio ardhini itakuja kuivaa hii miili yetu ya ardhini. Kuonyesha kuwa hakuna kilichopotea hata kimoja…

1Wakoritho 15:51 “Angalieni, nawaambia ninyi siri; hatutalala sote, lakini sote tutabadilika,

52 kwa dakika moja, kufumba na kufumbua, wakati wa parapanda ya mwisho; maana parapanda italia, na wafu watafufuliwa, wasiwe na uharibifu, nasi tutabadilika.

53 MAANA SHARTI HUU UHARIBIKAO UVAE KUTOKUHARIBIKA, NAO HUU WA KUFA UVAE KUTOKUFA.

54 Basi huu uharibikao utakapovaa kutokuharibika, na huu wa kufa utakapovaa kutokufa, hapo ndipo litakapokuwa lile neno lililoandikwa, Mauti imemezwa kwa kushinda.

55 Ku wapi, Ewe mauti, kushinda kwako? U wapi, Ewe mauti, uchungu wako?”

Lakini pia ikiwa Bwana anasema “Walakini HAUTAPOTEA hata Unywele” alimaanisha kuwa wapo ambao UTAPOTEA..Na hao ndio wale wanampinga YESU mfalme wa uzima sasa hivi wakijua kabisa yeye pekee ndiye mwenye uwezo wa kuokoa roho zao na miili yao. Siku ile wakifa katika dhambi basi miili yao na roho zao vyote kwa pamoja zitateketea katika lile ziwa la Moto milele. Watapotea milele wala hakutakuwa na kumbukumbu kama hata hao watu walishawahi kuishi duniani. 

Ubarikiwe


Mada zinazoendana:

UTALIPWA KATIKA UFUFUO WA WENYE HAKI.

TUZO UTAPEWA KULINGANA NA NAFASI YAKO.

JINSI MWISHO ULIVYOKARIBIA.

MANA ILIYOSHUSHWA KUTOKA MBINGUNI.

NI MAONO YAPI HAYO UNAYOSUBIRIA?

TABIA YAKO NI YA MNYAMA GANI?


 

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
2 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Jackson joachim
Jackson joachim
1 year ago

Nashukuru kwa mafundisho yenu na siku izi za mwisho Mwenyezi Mungu wa Mbinguni azidi kuwabariki. AMEN