Mtume Paulo alikuwa na maana gani kusema katika 1Wakorintho 15:31″…NIKAKUFA KILA SIKU?

Mtume Paulo alikuwa na maana gani kusema katika 1Wakorintho 15:31″…NIKAKUFA KILA SIKU?

JIBU: Katika ukristo KUFA kupo kwa namna mbili:  

>Aina ya kwanza ni kufa kwa habari ya dhambi.  

>Aina ya pili ni kufa kwa ajili ya Ndugu: Yaana kuwa tayari kuiponza roho yako, mpaka kufikia hatua ya kuweza kuitoa roho yako kwa ajili ya injili na kwa ajili ya Kristo.  

Ukristo sio wa leo na kesho halafu basi, Tunapokuwa wakristo inamaanisha tunajikana nafsi zetu kila siku, na kumwishia Mungu siku zetu zote zilizobakia na ndio maana Bwana YESU alisema:

Luka 9:23 “ Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake KILA SIKU, anifuate.

24 Kwa kuwa mtu atakaye kuiponya nafsi yake ataiangamiza, na mtu atakayeiangamiza nafsi yake kwa ajili yangu ndiye atakayeisalimisha.”  

Unaona hapo, ni kuchukua msalaba wako na kumfuata KILA SIKU na sio siku moja au mbili kisha basi. Kwa lugha iliyo rahisi ni kwamba kila siku unapaswa UFE kwa habari ya ulimwengu na uwe hai kwa habari ya Kristo.

Unakufa kila siku kwa habari ya fashion za ulimwengu huu, unakufa kila siku kwa kampani za marafiki wabovu, unakufa kila siku kwa habari ya matusi, kila siku unakufa kwa habari ya uasherati na tama zake kwa kujiweka mbali nazo, unakufa kwa habari ya rushwa, unakufa kwa habari ya usengenyaji, na anasa n.k.  

Kadhalika pia tunapoona ndugu zetu walio wachanga na wanahitaji msaada wa kiroho wa injili kutoka kwetu nasi tunajua kabisa tusipofanya hivyo wataangamia, hapo pia tunagharimika kuwaendea kwa gharama zozote zile bila kujali ni hatari gani tutakumbana nayo huko mbeleni kama vile mtume Paulo alivyokuwa anasema..Bila kujali jamii itakutenga vipi, bila kujali serikali itapingana nawe vipi, bila kujali watu wenye chuki watakuvizia muda wowote kukuua, bila kujali watu wa dini wanakuchuliaje n.k.   Sasa huko ndio KUFA KILA SIKU WA AJILI YA KRISTO.

Lakini ikiwa maisha yetu kila siku yatakuwa hivyo hayana mabadiliko yoyote, kila siku tunaonakena hatuna tofuati na watu wa ulimwengu. Hiyo ni dalili tosha kutuonyesha kuwa bado hatujamfauta Kristo..

  Ubarikiwe.


Mada zinazoendana:

JIKANE NAFSI MTEULE WA MUNGU.

JE! NI KWELI UMEMFUATA YESU?

NJIA YA MSALABA

AGIZO LA UTUME.

KITABU CHA YUDA: SEHEMU YA 1

NGURUMO SABA

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments