Je ni dhambi kuangalia movie?

Je ni dhambi kuangalia movie?

Kama mkristo ili uweze kuenenda  kikamilifu katika safari yako ya wokovu hapa duniani bila dosari zozote zisizokuwa na sababu, ipo mistari miwili ya kuzingatia..

Wa kwanza ni huu:

Wakolosai 3:17 “Na kila mfanyalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba kwa yeye”.

Na wa pili ni huu

Tito 2:11 Maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa;

12 nayo yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia; tupate KUISHI KWA KIASI, na haki, na utauwa, katika ulimwengu huu wa sasa;

Tukiweza kutembea na kanuni hizo mbili yaani kuishi kwa Kiasi na kufanya jambo lolote kwa kumshirikisha Mungu, basi tuwe na uhakika kuwa njema zetu zitanyooka, Sasa tukirudi kwenye swali lililoulizwa kuhusu picha za video (movies), hatuwezi kusema moja kwa moja usiangalie kabisa, ni kweli hakuna asiyejua movie nyingi hazina maudhui yoyote ya kumfaa au kumjenga mkristo lakini bado hatuwezi kusema ni zote, ni kama tu vipindi vya TV vipo vilivyo vizuri na vipo vilivyo vibaya, hivyo hatuwezi kumwambia mtu asiangalie TV kabisa kwasababu kuna vipindi vibaya vingi, hapo tutakuwa tumepoteza shabaha ya kulitibu tatizo..kwasababu kwenye TV pia kuna vipindi vya mahubiri na taarifa ya habari ambavyo kwa namna moja au nyingine vinaweza kumjenga mtu kiroho au kumfunza au kumjuza.

Lakini tukiwa na kiasi, inamaana kuwa hata tukitazama movie tutazama kwa kiasi tena zile tu ambazo zinaonekana kuwa na manufaa kwa mkristo, lakini leo hii utaona mtu anatazama series, kuanzia asubuhi mpaka jioni, hana muda wa kusali, hana muda wa kujisoma biblia, hana muda wa kwenda kanisani, hana muda wa kwenda fellowship, sasa hapo hata kama movie hiyo inayo maadili kiasi gani, lakini kwa kukosa tu kile kitu kinachoitwa kiasi tayari imekuwa ni kikwazo kwake na dhambi..

Vilevile utamwona mwingine anatazama tamthilia za mapenzi, au movie zilizojaa mambo maovu maovu tu, hajui kuwa moyo wa mwanadamu unatabia ya kujazwa na kile kinachofanywa, au kinachozungumzwa au kinachowazwa muda mrefu, kwa mfano ukiwa mtu wa kutafakari Neno la Mungu kila saa na kila wakati basi lile Neno linakuwa sehemu ya maisha yako..Vivyo hivyo ukiwa ni mtazamaji wa movie ambazo hazina vimelea vyovyote vya ki-Mungu ndani yake basi utakuwa mtu wa kufuatana na hivyo unavyovitazama,..Huko huko ndipo roho za uzinzi zinapozaliwa, na uuaji, na ulevi na matusi n.k…Na hiyo yote ni kwasababu hujazingatia lile Neno linalosema lolote mfanyalo kwa Neno au Kwa tendo fanyeni yote kwa jina la Yesu Kristo…Yaani kwa lugha nyepesi kufanya kwa jina la Yesu Kristo ni kabla hujafanya unaangalia je! Hichi ninachokitazama kina umuhimu gani katika maisha yangu ya rohoni…kama hakina  unakiacha, kama kinayo unakitazama, huko ndio kufanya kwa jina la YESU.

Ukiweza kutembea na mistari hiyo miwili basi hakuna jambo lolote litakalokuwa dhambi kwako, sio movie, sio radio, sio tv, sio simu, sio computa n.k.

Bwana akubariki.


 

Mada Nyinginezo:

JE! KUBET NI DHAMBI?

KUCHEZA KARATA NI SAHIHI KWA MTU ALIYE MKRITO?

JE! KUCHORA TATTOO NI DHAMBI?

JE NI SAWA KWA MKRISTO KUUZA MAZAO YA KUTENGENEZEA POMBE KAMA VILE MTAMA?

NI UTHIBITISHO UPI UNAOONYESHA KUWA KUNA MBINGUNI NA KUZIMU?

BWANA ALIMAANISHA NINI KUSEMA “WAACHE WAFU WAZIKE WAFU WAO.(MATHAYO 8:21)?


Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments