Ni udhaifu gani ulikuwa katika macho ya Lea mke wa Yakobo?

Ni udhaifu gani ulikuwa katika macho ya Lea mke wa Yakobo?

SWALI: Mwanzo 29:16 “Labani alikuwa na binti wawili, jina la mkubwa ni Lea, na jina la mdogo ni Raheli. 17 Naye Lea macho yake yalikuwa DHAIFU, lakini Raheli alikuwa mzuri wa umbo, na mzuri uso. 18 Yakobo akampenda Raheli akasema, Nitakutumikia miaka saba kwa kumpata Raheli, binti yako mdogo.”

Hapo Anaposema macho ya Lea yalikuwa dhaifu:Ni Udhaifu wakutokuona mbali au ni udhaifu wa namna gani huo??


JIBU: Biblia haituambii macho yake yalikuwa ni dhaifu kwa namna gani, kwamba ni makengeza, au yaliyolegea, au yenye kasoro ya kimaumbile kwamba ni makubwa sana au madogo sana au yanayoona karibu au mbali, hatujui lakini tunachojua ni kuwa alipofananishwa na mwenzake, Raheli alionekana ni mzuri kuliko yeye,…

Lakini Mungu hakuangalia hilo kama kigezo cha kuliunda taifa la Israeli, kwamba ampendelee Raheli zaidi ya Lea katika wana, kisa tu yeye ni mzuri wa sura na kwamba Yakobo kampenda zaidi…hapana kwanza utaona Lea ndiye aliyepewa uzao mkubwa zaidi, karibu nusu ya makabila yote ya Israeli yalitoka kwake isitoshe lile kabila la Bwana wetu Yesu Kristo kabila la YUDA lililoshinda makabila yote lilitoka kwa Lea…

Hivyo hiyo inatufundisha pia kutokukubaliwa na watu haimaanishi kuwa hatujakubaliwa na Mungu, Yabesi alikuwa ni mtu aliyezaliwa katika huzuni mpaka mama yake akamwita jina hilo ambalo lilimaanisha huzuni, Lakini Yabesi alijitahidi kuishi katika amani kwa heshima, kuliko ndugu zake wote, mpaka ikafikia wakati akamuomba Mungu dua amfanikishe katika mambo yake na Mungu akaisikia dua yake, mpaka habari yake leo hii tunaisoma katika biblia (1Nyakati 4:9-10,) …Hivyo ulemavu wowote mtu alionao haimaanishi kuwa hawezi kuwa jemadari katika ufalme wa mbinguni.

Ubarikiwe.


 

Mada Nyinginezo:

MAOMBI YA YABESI.

YESU MPONYAJI.

RUDIA, TENA NA TENA KUMWOMBA MUNGU USIKATE TAMAA.

JIPE MOYO.

TAZAMA, NASIMAMA MLANGONI.

UNYAKUO.

NYAKATI SABA ZA KANISA NA WAJUMBE WAKE.


Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments