NAFASI YAKO WEWE MAMA KWA MTOTO NA WAJUKUU WAKO NI IPI?.

NAFASI YAKO WEWE MAMA KWA MTOTO NA WAJUKUU WAKO NI IPI?.

Jina la Bwana na Mwokozi wetu Yesu, lihimidiwe.. karibu tujifunze biblia..

Neno la Mungu linasema..

Mithali 22:6 “Mlee mtoto katika njia impasayo, Naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee”

Faida ya kumlea mtoto wako katika njia inayompasa ni kwamba atakapokuwa mzee hataiacha, na maana yake zaidi ni kwamba hawezi kufikia uzee kabla na yeye kuwa na watoto wake.. hivyo na wajukuu wako pia watanufaika kwa malezi yako wewe kwa mwanao, kwasababu kile mwanao alichokipokea kutoka kwako, na yeye atawafundisha watoto wake, hivyo kizazi chako chote hata cha tatu na cha nne au zaidi ya hapo kitakuwa kitakatifu na cha baraka.

Ukiona kuna shida kwa mjukuu, basi ujue kuwa shida ilianzia kwa bibi au babu, ikaingia kwa mtoto na kisha ikamalizikia kwa mjukuu.. Lakini kama babu au bibi alimlea mwanae katika njia inayompasa, ya kumcha Mungu na kumpenda Mungu, huyo mtoto naye pia ni lazima atawafundisha watoto wake njia hiyo hiyo, na hivyo wajukuu watakaozaliwa basi watakuwa wenye mwenendo mwema wa kumpendeza Mungu.

Tuangalie mfano mmoja wa kwenye biblia wa mtu aliyemlea vyema mtoto wake, na hata mjukuu aliyezaliwa akawa na mwenendo mzuri.

Mtu huyo si mwingine zaidi ya BIBI LOISI, ambaye alikuwa na binti yake aliyeitwa EUNIKE, ambaye ndiye aliyemzaa Askofu Timotheo, mtumwa wa Bwana..

2Timotheo 1:4  “Nami natamani sana kukuona, nikiyakumbuka machozi yako, ili nijae furaha;

5  nikiikumbuka imani uliyo nayo isiyo na unafiki, ambayo ilikaa kwanza katika bibi yako Loisi, na katika mama yako Eunike, nami nasadiki wewe nawe unayo”.

Hapa tunaona Paulo anamwandikia waraka Timotheo, na kukiri chanzo cha imani yake Timotheo, kwamba ilianzia kwa bibi yake Loisi, na hatimaye kwa mama yake aliyeitwa Eunike, na ndipo ikaja kwake, ikimaanisha kuwa msingi wa Timotheo kumpenda Mungu haukuanzia kwake, bali ulianzia kwa bibi yake huko.. Ndio maana ikawa hata vyepesi Timotheo kuiamini injili ya Bwana Yesu na hata kuja kuwa Askofu wa makanisa mengi,  na ndiye aliyekuwa pamoja na Paulo mpaka hatua ya mwisho.

Timotheo hakuwa Mwisraeli moja kwa moja, bali mama yake ndiye aliyekuwa mwisraeli, lakini baba yake alikuwa myunani… pamoja na mchanganyiko huo lakini malezi ya bibi yake na mama yake yalimfanya awe mwenye mwenendo bora kuliko vijana wengi.

Matendo 16:1  “Basi akafika Derbe na Listra, na hapo palikuwa na mwanafunzi mmoja jina lake Timotheo, mwana wa mwanamke Myahudi aliyeamini; lakini babaye alikuwa Myunani.

2  Mtu huyo alishuhudiwa vema na ndugu waliokaa Listra na Ikonio.

3  Paulo akamtaka huyo afuatane naye, akamtwaa akamtahiri kwa ajili ya Wayahudi waliokuwako pande zile; kwa maana wote walijua ya kuwa babaye ni Myunani”.

Je na wewe kama mzazi un akitu gani cha kuwarithisha watoto wako na wajukuu wako?… je ni elimu tu ndio unayoona ni ya muhimu kwao???….

Nataka nikuambie kama watakuwa na elimu ya kidunia halafu hawana Mungu, basi jua kuwa umewapoteza wanao, haijalishi watakuwa mamilionea huko mbeleni!!.. Bibi Loisi, aliona utukufu wa mjukuu wake mbeleni, na kwamba atakuja kuwa mtumishi wa MUNGU hodari katika kuwavuta watu kwa Mungu, hivyo akaanza kuweka msingi bora kwa binti yake Eunike, na Eunike akamfundisha mwanae Timotheo malezi bora.

Walikuwepo vijana wengi wenye elimu nyakati za akina Timotheo, lakini wapo wapi leo??..walikuwepo vijana mamilionea kipindi cha akina Timotheo, lakini hakuna hata mmoja habari yake tunaisoma leo, lakini Timotheo habari zake tunazisoma na zinawaponya mamilioni ya watu duniani hata leo. Bwana amempa Timotheo kumbukumbu lisilofutika..

Walikuwepo wamama wengi na wabibi wengi nyakati za akina Timotheo, lakini hakuna hata mmoja tunayezisoma habari zake, ila hawa wawili Loisi pamoja na mwanae Eunike, habari zao tunazosoma hadi leo..

Na Mungu ni yeye Yule, hajabadilika..ikiwa na sisi tutatembea katika kanuni zake atatupa kumbukumbu ambalo halitafutika. Ikiwa na sisi tutawalea watoto wetu katika njia zitupasazo basi kumbukumbu letu pamoja na watoto wetu, na wajukuu wetu, na vitukuu vyetu, na vilembewe na vilembwekeze litadumu milele na milele.

Anza kuwafunza watoto wako biblia, wafundishe wamjue Yesu zaidi ya Hisabati, wafundishe wazijue amri za Mungu, na kuwa waombaji na watu wa ibada zaidi hata ya shule za ulimwengu. Ukimfanya Mungu wa kwanza katika maisha yao, na Mungu atawafanya wa kwanza katika mambo yao.

Bwana atubariki sote.

Maran atha.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

“Si watu wa kutumia mvinyo sana”, je tunaruhusiwa kutumia mvingo kidogo?(1Timotheo 3:8).

KWANINI UNAPASWA UWE BIBI ARUSI NYAKATI HIZI ZA MAJERUHI?

MWANAMKE, BINTI, MAMA.( Sehemu ya 1)

TUMEFANYIKA KUWA WANA WA MUNGU!

Je! Mfalme Abiya na Mfalme Asa walikuwa ni ndugu?

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
3 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
ISAACK MLEMWA
ISAACK MLEMWA
1 year ago

Bwana yesu asifiwe!

Daniel Jacob Shotoli
Daniel Jacob Shotoli
1 year ago

Soma…Isaya 65:20
Ufunuo 21:4
Mathayo 22:24-28 kipi sahihi kuhusu mbingu mpya na nchi mpya?

Lakini kuhusu kuoa na kuolewa ktk nchi mpya na jibu la yesu katika hiyo mathayo 22:24-28