Kwa lugha ya kiingereza unajulikana kama OAK tree, Kisayansi Kuna ziadi ya jamii 600 za mti huu.. Na unapatikana sehemu mbalimbali duniani sana sana zile za baridi, lakini katika ukanda wa mediterenia yaani Maeneo yote ya mashariki ya kati ikiwemo Israeli mti huu unaota kwa asili.
Mti wa mwaloni unatoa mbao zinazosifika kwa ugumu, katika ujenzi, na matumizi mbalimbali ikiwemo kutengenezea mapipa ya kuhifadhia divai, na mbao za mashua..Vile vile Mti huu unaweza kuishi miaka hata zaidi ya elfu moja..
Lakini Mti wa mwaloni unaonekana pia ukitajwa sehemu nyingi katika biblia na baadhi ya vifungu hivyo ni kama vifuatavyo..
Mwanzo 35: 8 Akafa Debora mlezi wa Rebeka, akazikwa chini ya Betheli, chini ya mwaloni; na jina lake likaitwa Alon-bakuthi.
Yoshua 2: 25 Basi Yoshua akafanya agano na wale watu siku ile, akawapa amri na agizo huko Shekemu.
26 Yoshua akayaandika maneno haya katika kitabu cha torati ya Mungu; kisha akatwaa jiwe kubwa, akalisimamisha huko, chini ya ule mwaloni uliokuwa karibu na patakatifu pa Bwana.
Waamuzi 6:11 Malaika wa Bwana akaenda akaketi chini ya mwaloni uliokuwa katika Ofra, uliokuwa mali yake Yoashi, Mwabiezeri; na mwanawe Gideoni alikuwa akipepeta ngano ndani ya shinikizo, ili kuificha machoni pa Wamidiani.
2Samweli 18: 9 Na kwa bahati Absalomu akakutana na watumishi wa Daudi. Naye Absalomu alikuwa amepanda nyumbu wake, na yule nyumbu akapita chini ya matawi manene ya mwaloni mkubwa, hata kichwa chake kikakwama katika mwaloni huo, akanyakuliwa juu kati ya mbingu na nchi; na yule nyumbu aliyekuwa chini yake akaenda mbele.
Nakadhalika, na kadhalika…
Lakini Swali ni, Je mti wa mwaloni unayo maana yoyote rohoni?
Mti yote tunayoiona ikitajwa kwenye maandiko, ilikuwa na kwa kazi maalumu katika jamii, vilevile ikifunua jambo Fulani katika roho kwa mfano ukisoma
Waamuzi 9;8-15.. utaona mwandishi akieleza jamii ya miti akifananisha na jamii za watu waliopo..
Sasa tukirudi kwenye maandiko kile kitabu cha Isaya 6:1-4 kinasema..
1 Roho ya Bwana MUNGU i juu yangu; kwa sababu Bwana amenitia mafuta niwahubiri wanyenyekevu habari njema; amenituma ili kuwaganga waliovunjika moyo, kuwatangazia mateka uhuru wao, na hao waliofungwa habari za kufunguliwa kwao. 2 Kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa, na siku ya kisasi cha Mungu wetu; kuwafariji wote waliao; 3 kuwaagizia hao waliao katika Sayuni, wapewe taji ya maua badala ya majivu, mafuta ya furaha badala ya maombolezo, vazi la sifa badala ya roho nzito; WAPATE KUITWA MITI YA HAKI, iliyopandwa na Bwana, ili atukuzwe. 4 Nao watajenga mahali pa kale palipoharibiwa, watapainua mahali palipokuwa ukiwa zamani, watatengeneza miji iliyoharibiwa, mahali palipoachwa kizazi baada ya kizazi.
1 Roho ya Bwana MUNGU i juu yangu; kwa sababu Bwana amenitia mafuta niwahubiri wanyenyekevu habari njema; amenituma ili kuwaganga waliovunjika moyo, kuwatangazia mateka uhuru wao, na hao waliofungwa habari za kufunguliwa kwao.
2 Kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa, na siku ya kisasi cha Mungu wetu; kuwafariji wote waliao;
3 kuwaagizia hao waliao katika Sayuni, wapewe taji ya maua badala ya majivu, mafuta ya furaha badala ya maombolezo, vazi la sifa badala ya roho nzito; WAPATE KUITWA MITI YA HAKI, iliyopandwa na Bwana, ili atukuzwe.
4 Nao watajenga mahali pa kale palipoharibiwa, watapainua mahali palipokuwa ukiwa zamani, watatengeneza miji iliyoharibiwa, mahali palipoachwa kizazi baada ya kizazi.
Ukisoma tafsiri nyingine nyingi za biblia, pale kwenye neno ‘miti ya haki’, limetumiwa neno mialoni ya haki..
Sasa kama tulivyokwisha kuona kule mwanzo mwaloni ni mti uliotumika hasahasa katika ujenzi, ni mti uliosifika kuwa na mbao ngumu, na zenye uwezo wa kuitunza divai vizuri.
Hivyo rohoni, ukiwa wewe ni mjenzi wa nyumba ya Mungu (Kanisa lake) unafananishwa na Mwaloni. Kama wewe ni mhubiri kwa Bwana ni mwaloni wake, kama wewe ni shujaa wa Bwana katika kuifanya kazi yake basi ni mwaloni kwa Bwana…Kama wewe unaifanya kazi kama ya Kristo ya kuhubiri injili basi ni mwaloni mzuri ufaaye kwa kazi ya ujezi wa nyumba ya Mungu inayodumu.. sawasawa na Isaya 61:4.
Ubarikiwe. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Nyinginezo:
Pakanga ni nini?
Je! habari ya Yusufu, inabeba ujumbe gani kwa agano jipya?
JE! Kaini alimpatia mke wake wapi?
NINI KINATOKEA BAADA YA KIFO?
NINI MAANA YA KUSAGA MENO?
Rudi Nyumbani:
Print this post
SWALI: Kwanini Mungu alimwambia Musa hakuna mtu awazaye kuuona uso wake akaishi,(Kutoka 33:20) Je! Kwa Mungu kuna mauti, tunapaswa tujihadhari naye?
JIBU: Tunajua biblia inatuambia kuwa kwa Mungu ndipo chemchemi za maji ya uzima zinapotoka, na ndipo chanzo cha uhai kwa kila kiumbe hai kinapozaliwa..
Zaburi 104:29 “Wewe wauficha uso wako, Wao wanafadhaika; Waiondoa pumzi yao, wanakufa, Na kuyarudia mavumbi yao, 30 Waipeleka roho yako, wanaumbwa, Nawe waufanya upya uso wa nchi.
Zaburi 104:29 “Wewe wauficha uso wako, Wao wanafadhaika; Waiondoa pumzi yao, wanakufa, Na kuyarudia mavumbi yao,
30 Waipeleka roho yako, wanaumbwa, Nawe waufanya upya uso wa nchi.
Hivyo kusema kwa Mungu kuna mauti, jibu ni La, badala yake ndio kuna uzima..
Lakini swali linakuja ni kwanini basi Mungu alimwambia Musa maneno yale, kuwa hakuna mtu atakayeuona uso wake na akaishi?? Je! Kila atakayemwona Mungu ni lazima afe?..Na ndio maana Mungu akamwonyesha tu Musa sehemu ya nyuma ya utukufu wake ili asife au?
Kauli hiyo ukiitafakari kwa haraka unaweza kudhani Mungu alimaanisha kifo, lakini si kweli, kwasababu Mungu sio Kifo, tukimwona Mungu katika utimilifu wote ndivyo tutakavyozidi kuishi, isipokuwa sasa hatutaishi tena katika hali hii ya Maisha ya kawaida tuliyonayo siku zote..
Yaani itatulizimu kuvuka viwango hivi, na kwenda viwango vingine kiasi kwamba hata haya Maisha ya hapa duniani yatakuwa hayana maana tena kwetu, kuyaishi hatutaweza kuendelea kuishi tena hapa duniani..tutahamishwa na kuingia katika Maisha ya ufalme wa Mungu wetu..
Chukulia mfano, mtoto mdogo labda wa miaka 5, halafu akiwa bado ni mdogo vilevile umwondolee akili yake ya kitoto, kisha umwekee ubongo wa mtu mzima wa miaka 40 ndani yake..halafu umpe toy, za kitoto au umnunulie midoli aichezee.. Wewe unadhani ataifurahia tena, au atacheza nayo tena?…Kinyume chake utamwona ananyanyuka, na kwenda kusikiliza BBC, akitoka hapo utaona anaanza kuzungumzia Habari za uwekezaji, na kupanga mipango ya kimaendeleo.., kamwe huwezi kumkuta anachezea tena matope, au anaruka ruka barabarani kama Watoto wengine..
Ni kwasababu gani? Ni kwasababu akili yake imevukishwa mipaka yake ya utoto, hivyo hawezi kuishi tena Maisha ya utoto aliyopaswa ayaishi kwa umri wake..
Vivyo hivyo tukimwona Mungu kwa utimilifu wote, Maisha ya hapa duniani ndivyo yatakavyokuwa hayana maana tena kwetu.kinachobakia ni Kuondoka tu..
Bwana wetu YESU KRISTO yeye peke yake ndiye aliyemwona Mungu katika utimilifu wote..
Yohana 1:18 “Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wo wote; Mungu Mwana pekee aliye katika kifua cha Baba, huyu ndiye aliyemfunua”.
Na ndio maana aliondoka na kupaa na mpaka sasa, hajawahi kutokea mtu kama yeye, wakati huu wa sasa yupo kifuani mwa Mungu, hata makerubi na maserafi hajafikia bado hatua hiyo. Maisha yake hapa duniani yalikuwa ni ya kimiujiza tu, mpaka wengine wanadhani biblia iliongeza chumvi pale iliposema, mambo yote aliyoyafanya Yesu kama yangeandikwa moja moja sijui kama vitabu vyote duniani vingetosha..(Yohana 21:25)
Yesu alikuwa na uwezo wa kuuondoa uhai wake, na kuurudisha akiwa bado hapa hapa duniani,(Yohana 10:18), lakini hakutaka kufanya hivyo ili tu kutimiza kusudi la kutuokoa sisi, Je! Mtu huyo ni wa kawaida?
Na sisi pia tuzidi kumwomba Mungu azidi kujifunua kwetu, Zaidi na Zaidi, ili nasi tukifikie hatua ya kumjua yeye, mpaka kuifikia hatua ya kuondolewa duniani kwa tukio lile kuu la (UNYAKUO) alilotuahidia. Kama Bwana wetu alivyochukuliwa juu.
Shalom.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312
jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
MWAKA WA BWANA ULIOKUBALIWA.
Nifanye nini ili niwe na uhakika nikifa naenda mbinguni?
JINSI NEEMA YA MUNGU ILIVYOKUWA KUBWA KWA MKE WA LUTU.
MAMBO YA KUJIFUNZA KATIKA KITABU CHA RUTHU:
MSHIKE SANA ELIMU.
JE VIBWENGO NI KWELI VIPO?
WhatsApp
SWALI: Zile Mbao za mawe Musa alizoambiwa achonge kwa ajili ya zile amri 10 zilikuwaje?..je ni mbao za miti zilichonganyikana na mawe au zilikuwa ni kitu gani?
JIBU: Neno mbao asili yake sio miti…bali ni kipande cha kitu chochote ambacho kipo bapa, ambacho kinaweza kufaa kwa matumizi mbali mbali kama uandishi au ujenzi. Umoja wa neno mbao ni UBAO. Hivyo ubao unaweza kuwa wa miti, chuma, mawe, glasi au chochote kile.
Hivyo Mbao mbili Musa alizoambiwa achonge hazikuwa za miti, bali za mawe. Na ndizo hizo Mungu alizozitumia kuandikia amri zake. Sasa Kwanini Mungu alitumia mawe na si miti? Ni kwasababu maandishi yaliyoandikwa kwenye mawe yanadumu kwa muda mrefu zaidi ya yale yanayoandikwa kwenye miti…kwasababu miti inaoza na kuharibika na kuliwa na mchwa lakini mawe yanadumu miaka mingi..Hivyo Mungu kuonyesha kwamba Amri zake ni za daima na milele na kwamba hazifutiki ndio maana alitumia mawe.
Lakini Pamoja na hayo mawe yanaweza kuharibika pia na maandishi yale yakapotea miaka inapozidi kuwa mingi…Hivyo Mungu aliruhusu pia amri zile zikae kwenye mawe kwa muda tu, kwasababu mbeleni alikuwa na mpango mwingine maalumu sana wa mahali pa kuziandikia ambapo zitadumu milele.
Hivyo wakati ulipofika, akaleta mpango mwingine wa kuandika amri zake si katika miti wala mawe ambayo yapo leo na kesho kupotea…Ndipo akaleta agano jipya kupitia mwana wake mpendwa ambapo ataziandika amri zake na sheria zake mioyoni mwa watu wake..Humo ndimo mahali pekee ambapo ahaziwezi kufutika kamwe kama maandiko yanavyosema..
Yeremia 31:31“Angalia, siku zinakuja, asema Bwana, nitakapofanya agano jipya na nyumba ya Israeli, na nyumba ya Yuda. 32 Si kwa mfano wa agano lile nililolifanya na baba zao, katika siku ile nilipowashika mkono, ili kuwatoa katika nchi ya Misri; ambalo agano langu hilo walilivunja, ingawa nalikuwa mume kwao, asema Bwana. 33 Bali agano hili ndilo nitakalofanya na nyumba ya Israeli, baada ya siku zile, asema Bwana; Nitatia SHERIA YANGU NDANI YAO, NA KATIKA MIOYO YAO NITAIANDIKA; nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu. 34 Wala hawatamfundisha kila mtu jirani yake, na kila mtu ndugu yake, wakisema, Mjue Bwana; kwa maana watanijua wote, tangu mtu aliye mdogo miongoni mwao hata aliye mkubwa miongoni mwao, asema Bwana; maana nitausamehe uovu wao, wala dhambi yao sitaikumbuka tena”
Yeremia 31:31“Angalia, siku zinakuja, asema Bwana, nitakapofanya agano jipya na nyumba ya Israeli, na nyumba ya Yuda.
32 Si kwa mfano wa agano lile nililolifanya na baba zao, katika siku ile nilipowashika mkono, ili kuwatoa katika nchi ya Misri; ambalo agano langu hilo walilivunja, ingawa nalikuwa mume kwao, asema Bwana. 33 Bali agano hili ndilo nitakalofanya na nyumba ya Israeli, baada ya siku zile, asema Bwana; Nitatia SHERIA YANGU NDANI YAO, NA KATIKA MIOYO YAO NITAIANDIKA; nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.
34 Wala hawatamfundisha kila mtu jirani yake, na kila mtu ndugu yake, wakisema, Mjue Bwana; kwa maana watanijua wote, tangu mtu aliye mdogo miongoni mwao hata aliye mkubwa miongoni mwao, asema Bwana; maana nitausamehe uovu wao, wala dhambi yao sitaikumbuka tena”
Hivyo ili tuzishike amri za Mungu hatuna budi ziandikwe ndani ya mioyo yetu….Na zinaandikwa tu pale tunamwamini Yesu Kristo na kupokea Roho Mtakatifu. Kumbuka Yesu ndiye mjumbe wa Agano jipya (Malaki 3:1) Hivyo yoyote aliyemwamini, na kupokea Roho wake Mtakatifu amri na sheria za Mungu zinaandikwa katika mbao za moyo wake…anakuwa anazitimiza sheria zile bila kujilazimisha wala kulazimishwa, wala hazimfanyi kuwa mtumwa, kiasi kwamba anapata tabu kuzishika sheria za Mungu…yeye mwenyewe tu anajikuta anazipenda sheria za Mungu na kuzitenda.
Bwana atubariki.
Sanduku la Agano lilikuwa linawakilisha nini katika Agano jipya?
HUDUMA YA (ELIFAZI, SOFARI, NA BILDADI).
Sabato halisi ni lini, Je! ni Jumapili au Jumamosi?, Ni siku gani itupasayo kuabudu?
MUUNGANIKO WA MADHEHEBU NI MPANGO WA MPINGA-KRISTO.
IFANYE KAZI YA MUNGU PASIPO HOFU!
Kutoka 20:17 “Usiitamani nyumba ya jirani yako, usimtamani mke wa jirani yako; wala mtumwa wake, wala mjakazi wake, wala ng’ombe wake, wala punda wake, wala cho chote alicho nacho jirani yako”.
Bwana ameweka msisitizo mkubwa sana, katika jambo hili ‘Usitamani’..Na utaona ni karibu nyanja ya vitu vyote alivyonavyo jirani yako.
Sasa Usitamani kunako zungumziwa hapo sio kutotamani kuwa na kitu kama cha jirani yako, hapana, bali ni kule kutamani kile kitu (chenyewe) jirani yako alichonacho, na hivyo unatafuta kila namna na kila mbinu ya kukipata..(yaani kukitwaa na kiwe cha kwako) Hiyo ndiyo Mungu anaichukia.
Dhambi hii inagharimu sana na ndio maana Mungu aliisisitiza….
Wapo watu wawili katika biblia tunaweza kuwachukulia kama mfano jinsi waliiatamia dhambi hii na ikawagharimu vibaya mno,
(1)Wa kwanza ni Mfalme Daudi na
(2)Wa pili Ni Mfalme Ahabu.
Daudi alimtamani mke wa Huria, na kama tunavyojua ikamfanya atafuta kila njia ya kumwangamiza ili amchukue mke wake, kuifanya habari iwe fupi, leo hii hakuna mtu asiyejua madhara yaliyompata Daudi..ambayo yalimfanya ajutie tendo lile kwa miaka mingi sana, licha ya kufukuzwa tu na kuachwa na Mungu kwa muda, lakini pia masuria wake 10 walifanyiwa kitendo kilekile na mtoto wake mwenyewe aliyemzaa (Absalomu)..Jaribu kufikiria ni aibu kiasi gani?..mtoto wako anawabaka wake zako mbele ya taifa zima (2Samweli 11-18)…
Vile vile mwingine ni Mfalme ahabu, yeye naye alitamani kiwanja cha Nabothi Myezreeli, baada ya kukiona ni kizuri na kipo karibu na ikulu yake, hivyo baada ya kunyimwa ikamfanya akose raha kwa muda mrefu mpaka mkewe Yezebeli, akaamua kwenda kumuulia Nabothi ili tu akichukue kiwanja kile..Na ahabu alipoona vile Nabothi ameshauliwa, hakuchukua hatua yoyote ya kutubu badala yake akaenda kukichukua kile kiwanja na kukifanya kiwe chake..Lakini tunaijua habari yake jinsi ilivyokuja kuishia mbeleni, jinsi mbwa walivyokuja kuilamba damu yake mbele ya kiwanja kile kile cha Nabothi alichomuulia..(1Wafalme 21)
Tunapaswa tujiepushe na roho hii ya tamaa, kwamfano mwanamke mmoja ataenda nyumba ya jirani yake, halafu kule akamwona mfanyakazi wa jirani yake jinsi alivyo mzuri, mchapa kazi, mpishi mzuri wala hana usumbufu wowote..akiangalia huku nyuma , wa kwake ni mvivu, hafanyi kazi, Sasa, badala ajitahidi akatafute mwingine, mwenye vigezo kama vya yule wa jirani yake, yeye anaingiwa na tamaa, na kutafuta kila mbinu ya kumpata yule wa jirani yake, anaanza kumwahidia mshahara mkubwa, ili aache kazi kwa boss wake wa kwanza ahamie kwake..
Na kweli anafanikiwa lakini hajui kuwa na yeye mwisho wake utakuwa kama wa Ahabu wa kuliwa na mbwa, au kama wa Daudi wa kuabishwa na kufukuzwa..pale unapowatamani wake wa wengine..
Mwingine ni katika mambo ya biashara, anaona tu, mwenzake, Mungu anamfanikisha sehemu Fulani wateja wanakuja..Yeye naye anaingiwa tamaa, na kwenda kumwahidia mwenye pango kuwa atamlipa kodi kubwa Zaidi ili yeye aingie pale mwenzake alipokuwepo afanye biashara hapo..Hiyo ni tamaa yenye adhabu..
Na nyingine nyingi za namna hiyo..Na ndio maana Bwana alihitimisha na kusema.. “wala cho chote alicho nacho jirani yako”
Biblia inatuambia..
1Timotheo 6:6 “Walakini utauwa pamoja na kuridhika ni faida kubwa”.
Tunapaswa tuwe watu wa kuridhika na vile tulivyonavyo..
Hivyo angalia je chochote, unachokitamani , Je, mwisho wa siku kitamuathiri jirani yako?. Kama ndivyo ni heri ukaacha..Uepukane na laana.. Na mapigo.
Ubarikiwe.
Ubatizo wa moto ni upi?
Kuota unafanya Mtihani.
“Ninyi ni chumvi ya dunia” Andiko hilo lina maana gani?
KWANINI MUNGU ALIMTUMIA MUSA KWA VIWANGO VILE?
Warumi 8:35 “Ni nani atakayetutenga na upendo wa Kristo? Je! Ni dhiki au shida, au adha, au njaa, au uchi, au hatari, au upanga?”
Mstari huu ukiusoma kwa haraka haraka ni rahisi kuutafsiri hivi… “Ni nini kitakachotufanya sisi tuache kumpenda Yesu, au tumwache Yesu..je ni dhiki au shida au njaa au adha au uchi?”…Lakini hiyo sio tafsiri yake, wala Mtume Paulo hakuuandika mstari huo kwa msaada wa Roho Mtakatifu kulenga hiyo tafsiri, wala hakumaanisha hivyo…Kwasababu hakuna mtu yeyote duniani ambaye kwa nguvu zake mwenyewe anaweza kupitia njaa, au dhiki, au shida na asijitenge na Kristo…hakuna!. Lakini je mstari huo una maana gani?
Tafsiri ya mstari huo ni hii… “Ni nani au ni kitu gani kitachachotufanya sisi tusipendwe na Kristo au tuchukiwe na Kristo?, je ni njaa, dhiki, shida, uchi, hatari au upanga?”..Hii ndio tafsiri yake.
Upendo uliozungumziwa hapo si upendo wetu kwa Kristo bali ni upendo wa Kristo kwetu. Maana yake ni kwamba tunapopitia njaa Kristo hawezi kujitenga na sisi, tunapopitia shida Kristo hawezi kutukimbia wala kutuchukia, tunapopitia taabu bado atakuwa Pamoja na sisi kutufariji na kujishughulisha na mambo yetu, tutakapopitia upanga bado atakuwa upande wetu kutushika mkono na kutuongoza safarini kama maandiko yanavyosema katika..
Zaburi 23:4 “Naam, nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti, Sitaogopa mabaya; Kwa maana Wewe upo pamoja nami, Gongo lako na fimbo yako vyanifariji. 5 Waandaa meza mbele yangu, Machoni pa watesi wangu. Umenipaka mafuta kichwani pangu, Na kikombe changu kinafurika. 6 Hakika wema na fadhili zitanifuata Siku zote za maisha yangu; Nami nitakaa nyumbani mwa Bwana milele”.
Zaburi 23:4 “Naam, nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti, Sitaogopa mabaya; Kwa maana Wewe upo pamoja nami, Gongo lako na fimbo yako vyanifariji.
5 Waandaa meza mbele yangu, Machoni pa watesi wangu. Umenipaka mafuta kichwani pangu, Na kikombe changu kinafurika.
6 Hakika wema na fadhili zitanifuata Siku zote za maisha yangu; Nami nitakaa nyumbani mwa Bwana milele”.
Hivyo kama tumemwamini Kristo basi tufahamu kuwa Pendo lake limemiminwa juu yetu…Hivyo kamwe hawezi kutuacha katika mapito yoyote tutakayopishana nayo…Kwasababu majaribu tumewekewa, ni lazima tuyapitie lakini yeye ameahidi kuwa na sisi na kutupa ushindi..Kwasababu hakuna chochote kile kitakachotutenga na Upendo wake.
Lakini kama hujampokea Yesu, bado hujaingizwa katika Pendo lake hili…upo nje ya Mlango…Kristo hawezi kuwa upande wako kwasababu wewe humwamini na humtaki..Lakini anakuita leo..usifanye moyo wako kuwa mgumu..Unachotakiwa kufanya bila kupoteza muda ni leo kukata shauri la kuokoka..Maana yake ni kwamba unamkiri yeye kwa kinywa chako kwamba ni Bwana na mwokozi wa Maisha yako, na kisha unatubu (Kutubu maana yake ni kugeuka/kughairi maovu na mabaya yote uliyokuwa unayafanya yasiyompendeza Mungu)..maana yake ni kwamba kama ulikuwa ni mwasherati unageuka na kuuacha uasherati wako..kama ulikuwa unakwenda kuiba, unaacha hiyo safari na wizi wote kwa ujumla, kama ulikuwa ni muuaji unaacha mauaji..na mambo mengine yote yasiyompendeza Mungu unayaacha…
Sasa ukishayaacha hayo yote kwa vitendo namna hiyo, hapo ndipo utakuwa umetubu..na kama umetubu Mungu atakuwa tayari kukurehemu na kukusamehe uzinzi wako wote uliokuwa unaufanya huko nyuma, na rushwa zako na matusi yako na kila kitu ulichokuwa unakifanya kilicho kinyume na mapenzi yake…Baada ya rehema hiyo kuingia ndani ya moyo wako..kuna AMANI fulani isiyokuwa ya kawaida ambayo Mungu anaiachia kwa mara ya kwanza kwa wale wote waliotubu kwa kumaanisha kabisa…Amani hiyo isiyoelezeka itaingia ndani yako…utaona kama kuna kifungo fulani kimeachia ndani yako…Hiyo amani ndiyo uthibitisho wa msamaha wako…
Sasa ili usiizimishe amani hiyo nenda katafute ubatizo haraka sana. Ubatizo sahihi na wa kimaandiko ni ule wa maji tele (Yohana 3:23) na kwa jina la Yesu Kristo (Matendo 2:38, Matendo 8:16, Matendo 10:48, na Matendo 19:5)..Ambalo ndio jina la Baba, Mwana na Roho Mtakatifu. Ukifanya hivyo amani hiyo itadumu ndani yako siku zote. Amani hiyo ndio pendo hilo la Kristo ambalo hata utakapopitia magumu, au shida au mateso au raha au mafanikio haitaondoka kamwe ndani yako. Itakulinda mpaka siku ya mwisho.
Bwana akubariki.
BASI TUENDELEE KUMJUA MUNGU,NAYE ATATUJILIA KAMA MVUA YA VULI.
UPENDO NI NINI NA JE! KUNA AINA NGAPI ZA UPENDO?
NINI KINAFUATA SIKU ILE ILE YA KUOKOKA!
ANGALIA UZURI WAKO, USIGEUKE KUWA KITANZI CHAKO.
MOJA YA HIZI SIKU TUTAONA MABADILIKO MAKUBWA SANA.
Pakanga ni mmea fulani mchungu uliokuwa unajulikana enzi za kale za biblia, ulikuwa ni mmea unaoota sehemu kame na ulikuwa ni mchungu sana..Hivyo kutokana na sifa ya mmea huo, chochote kile ambacho kingeleta uchungu mkali zamani kiliitwa jina la pakanga Kwa mfano kwenye biblia tunaona neno hilo likitumika sehemu mbali mbali…
Yeremia 23:15 “Basi Bwana wa majeshi asema hivi, katika habari ya manabii, Tazama, nitawalisha pakanga, nitawanywesha maji ya uchungu; kwa kuwa kutoka kwa manabii hao wa Yerusalemu kukufuru kumeingia katika nchi yote”.
Soma tena..
Mithali 5:3 “Maana midomo ya malaya hudondoza asali, Na kinywa chake ni laini kuliko mafuta; 4 Lakini mwisho wake ni mchungu kuliko pakanga; Ni mkali kama upanga wa makali kuwili”.
Yeremia 9:14 “bali wameenenda katika ushupavu wa mioyo yao wenyewe, na kuandamana na Mabaali, kama walivyofundishwa na baba zao. 15 Basi, Bwana wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Tazama, nitawalisha pakanga, naam, watu hawa, nami nitawapa maji ya uchungu wayanywe. 16 Nami nitawatawanya kati ya mataifa, ambao wao hawakuwajua; wala baba zao, nami nitatuma upanga nyuma yao, hata nitakapowaangamiza kabisa”
Yeremia 9:14 “bali wameenenda katika ushupavu wa mioyo yao wenyewe, na kuandamana na Mabaali, kama walivyofundishwa na baba zao.
15 Basi, Bwana wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Tazama, nitawalisha pakanga, naam, watu hawa, nami nitawapa maji ya uchungu wayanywe.
16 Nami nitawatawanya kati ya mataifa, ambao wao hawakuwajua; wala baba zao, nami nitatuma upanga nyuma yao, hata nitakapowaangamiza kabisa”
Ufunuo 8:10 “Malaika wa tatu akapiga baragumu, nyota kubwa ikaanguka kutoka mbinguni, iliyokuwa ikiwaka kama taa, ikaanguka juu ya theluthi ya mito, na juu ya chemchemi za maji. 11 Na jina lake ile nyota yaitwa Pakanga; theluthi ya maji ikawa pakanga, na wanadamu wengi wakafa kwa maji hayo, kwa kuwa yalitiwa uchungu”.
Soma pia (Maombolezo 3:15,19), (Amosi 6:12), utaliona Neno hilo..
Hivyo biblia inapotumia hili Neno pakanga, inamaanisha uchungu mkali usio wa kawaida utakaowapata watu wanaotenda dhambi.. kama vile uasherati, uabuduji sanamu, utoaji wa unabii wa uongo n.k..
Hata leo Maisha yetu Mungu anaweza kuyatia pakanga, ikiwa tutaendelea kuishi Maisha ya kutokujali..Tuombe Bwana atuepushe na hayo mambo, huku tukikaa mbali na dhambi..Magonjwa haya tuyaonayo leo hii ni sehemu tu ndogo ya Pakanga, Ukilishangaisha ni hiyo itakayokuja kuachiliwa siku za mwisho ambapo watu watasaga ndimi, wakitamani vifo viwafikie, lakini mauti itawakimbia.. mambo hayo yatakuja baada ya unyakuo kupita.
NI WAPI MAHALI SAHIHI PA KULIPA ZAKA?
KUTUBU SIO KUOMBA REHEMA.
Neno I.N.R.I kwenye msalaba wa Yesu maana yake ni nini?
Utii ni nini? na ni nani tunayepaswa kumtii au kutokumtii?
NDUGU,TUOMBEENI.
Bwana aliposema kuwa yeye ni “Mungu wa miungu” alikuwa na maana gani?..je! yeye ni Mungu wa sanamu?
TIMAZI NI NINI
Karibu tujifunze Biblia.
Tukio la Ibrahimu kukubali kumtoa mwanawe kuwa sadaka ya kuteketezwa lilikuwa ni jambo gumu na la kishujaa sana…Kiasi kwamba ilihitajika kuwa mtu mwingine ndipo moyo huo mtu uweze kuwa nao.
Hebu jiulize leo itokee ni wewe umeambiwa hivyo kwamba ukamtoe mwanao wa kwanza wa kiume kuwa sadaka ya kuteketezwa..Kumbuka kwa wakati ule sadaka ya kuteketezwa ilikuwa ni unamkamata mbuzi au kondoo unamchinja, kisha unamkata kata nyama zake vipande vipande, kisha unamweka juu ya madhabahu ambayo ilikuwa inatengenezwa kwa mawe na kuni..halafu unawasha moto na kuichoma ile nyama mpaka iteketee kabisa kuwa jivu…harufu inayotoka ni kama ya nyama choma..Sasa piga mahesabu ni mwanao ndio unamfanyia hivyo, unamshika unamchinja akiwa mzima, anakuuliza baba ni nini unataka kufanya…halafu ghafla unaona machozi yanaanza kumshuka mashavuni.. kisha unamkata vipande vipande bila huruma na kuweka vipande vile juu ya kuni..na kuwasha moto…na kuichoma nyama yake mpaka iteketee kabisa…huku unatazama huku unaisikia ile harufu ya nyama ya mwanao. Utakuwa katika hali gani?
Bila shaka ni jambo gumu…lakini kwa Ibrahimu lilikuwa ni rahisi…Kwanini lilikuwa ni rahisi? Leo tutajifunza siri iliyomfanya Ibrahimu iwe rahisi kwake kutaka kumchinja mwanawe..
Na siri hiyo tunaipata katika kitabu cha Waebrania..
Waebrania 11:17 “Kwa imani Ibrahimu alipojaribiwa, akamtoa Isaka awe dhabihu; na yeye aliyezipokea hizo ahadi alikuwa akimtoa mwanawe, mzaliwa pekee; 18 naam, yeye aliyeambiwa, Katika Isaka uzao wako utaitwa, 19 AKIHESABU YA KUWA MUNGU AWEZA KUMFUFUA HATA KUTOKA KUZIMU; akampata tena toka huko kwa mfano”.
Waebrania 11:17 “Kwa imani Ibrahimu alipojaribiwa, akamtoa Isaka awe dhabihu; na yeye aliyezipokea hizo ahadi alikuwa akimtoa mwanawe, mzaliwa pekee;
18 naam, yeye aliyeambiwa, Katika Isaka uzao wako utaitwa,
19 AKIHESABU YA KUWA MUNGU AWEZA KUMFUFUA HATA KUTOKA KUZIMU; akampata tena toka huko kwa mfano”.
Umeona hapo mstari wa 19?…Siri ndio ipo hapo…Kwamba Ibrahimu alihesabu kuwa hata baada ya kumchinja mwanawe na kuwa jivu…Mungu huyo huyo aliyempa mtoto kimiujiza jiza wakati umri wake ukiwa umeshakwenda sana…anaweza kufanya muujiza wa kumtoa mwanawe kule kuzimu alipokwenda, na kuligeuza lile jivu lililochomwa juu ya zile kuni kurudi kuwa vile vipande vya nyama, kisha akavirudisha vile vipande vya nyama vilivyokatwa katwa na kuwa mtu kamili na kuirudisha ile damu iliyomwagika kuwa mtu tena na hata anauwezo wa kulifuta lile wazo kwa mwanawe kwamba alikuwa anakwenda kutolewa sadaka..na Mungu kumpa tena mwanawe akiwa mzima bila dhara lolote kama alivyokuwa mwanzo…
Kwa Imani hiyo ya kumwamini Mungu kuwa anaweza kufanya hayo…ndiyo iliyomfanya Ibrahimu asipate shida kumtoa mwanawe kuwa sadaka ya kuteketezwa….alijua hata kama mwanawe atateketea, ndani ya dakika tano Mungu anaweza kumrudisha tena akawa wake…kwahiyo akahesabu kumtii Mungu ni bora kuliko kusikiliza hisia zake..
Na siri hiyo hiyo ndiyo itakayotufanya na sisi tuweze kumtolea Mungu wetu vilivyo bora pasipo kuangalia hasara tutakazozipata…Tutaweza kumtolea Mungu vilivyo vikubwa ambavyo vinatugharimu tukifahamu kuwa japokuwa tumevipoteza vyote kwa ajili ya Mungu…lakini Mungu bado ana uwezo kuturudishia vile vitu kufumba na kufumbua kama vilivyo…
Sio hilo peke yake…pia tunapomwamini Kristo na kujitwika misalaba yetu na kumfuata ni sawa na tumeyatoa maisha yetu kuwa sadaka kwake…Maana yake ni kwamba tunaishi Maisha ya kujitoa kwa Kristo na kuzipoteza nafsi zetu kwa ajili yake na hata kuifia imani tukiamini kuwa japokuwa tumezipoteza nafsi zetu katika ulimwengu huu kwa ajili yake, lakini bado Mungu wetu anao uwezo wa kutufufua na kutufanya upya tena na kuturudishia uhai wetu na kutupa Maisha marefu na mazuri kuliko haya tuliyonayo hapa duniani…Lakini tusipoamini kwa namna hiyo, kamwe hatuwezi kuyatoa Maisha yetu kwa Kristo kikamilifu. Tutaanza kusema aah..kuna faida gani kumtumikia Mungu…kuna faida gani kuyatoa Maisha yangu kwake na kuishi kuzishika amri zake..
Biblia inasema..
Mathayo 16:24 “Wakati huo Yesu aliwaambia wanafunzi wake, Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake, anifuate. 25 Kwa kuwa mtu atakaye kuiokoa nafsi yake, ataipoteza; na mtu atakayepoteza nafsi yake kwa ajili yangu, ataiona. 26 Kwani atafaidiwa nini mtu akiupata ulimwengu wote, na kupata hasara ya nafsi yake? Au mtu atatoa nini badala ya nafsi yake?”
Mathayo 16:24 “Wakati huo Yesu aliwaambia wanafunzi wake, Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake, anifuate.
25 Kwa kuwa mtu atakaye kuiokoa nafsi yake, ataipoteza; na mtu atakayepoteza nafsi yake kwa ajili yangu, ataiona.
26 Kwani atafaidiwa nini mtu akiupata ulimwengu wote, na kupata hasara ya nafsi yake? Au mtu atatoa nini badala ya nafsi yake?”
YA KALE YAMEPITA, TAZAMA YAMEKUWA MAPYA
NI NINI TUNAJIFUNZA JUU YA MT. DENIS WA UFARANSA?
ESTA: Mlango wa 5, 6 & 7
SIKU ILE NA SAA ILE.
SWALI: Habari mtumishi, naomba kujifunza habari hii ya kwamba, agano la kale ni kivuli cha agano jipya.., sasa ile habari ya Yusufu ilikua ina ufunuo gani kwa agano jipya?
JIBU: Ni kweli kabisa agano la kale ni kivuli cha mambo yanayoendelea katika agano jipya biblia inatuambia hivyo katika (Waebrania 10:1, Wakolosai 2:17)…
Kwa msingi huo basi ipo habari iliyojificha nyuma ya maisha ya Yusufu ambayo tukiijua tutafungua siri nyingi za Mungu zinazoendelea katika wakati huu wa sasa wa agano jipya.
Maisha ya Yusufu ni mfano wa Maisha ya Bwana wetu Yesu Kristo kabisa tangu alipozaliwa hadi anakufa na hadi atakapokuja tena kuwaokoa wayahudi..
Kama tunavyofahamu, Yusufu mara baada ya kuwaeleza ndugu zake, kuhusu zile ndoto kuwa atakuja kuwatawala, mambo yalikuwa tofauti badala ya kumpenda walimchukia, na mwishowe wakamuuza kwa watu wa mataifa..
Mfano hai wa Bwana wetu Yesu alipokuja duniani, alikuja kwa watu wake(wayahudi), lakini walio wake hawakumpokea (Yohana 1:11), kinyume chake ndipo walipozidi kumchukia pale alipowaambia kuwa yeye ni mfalme, hivyo walichokifanya wakamweka mikononi mwa mataifa ili auawe,..
Na kama vile, Yusufu, alivyokwenda kuuzwa, Misri, na matokeo yake baada ya kutoka gerezani akavikwa mavazi ya kifalme na kuketi mkono wa kuume wa Farao na kukubalika na wamisri wote, akawa mkubwa sana, kule Misri, akajulikana sana na kuwa mkuu,..Ndivyo ilivyokuwa kwa Bwana Yesu, alipokataliwa na ndugu zake, wayahudi, akauzwa, na kuuawa na kuzikwa na kuwekwa katika kifungo cha kaburi kwa siku tatu…alipotoka kaburini kama vile Yusufu alivyotoka gerezani, hakuwa dhaifu tena…Bwana wetu Yesu aliketi mkono wa kuume wa Mungu baba kama vile Yusufu alivyoketi mkono wa kuume wa Farao.
Na kama vile mataifa yote ulimwenguni yalivyokuja kumwangukia Yusufu, na Bwana Yesu baada ya kufufuka kwake mataifa yote ulimwenguni yanamwangukia yeye sasa..Nafaka yote inatoka kwake mkuu wa uzima Yesu Kristo.
Hivyo kitendo cha Wayahudi kumkataa Yesu kimekuwa neema kwetu. ambapo mpaka sasa sisi tunaifurahia neema hiyo.. (Matendo 13:46-52)
Lakini wakati ulipofika wa Njaa kuipiga dunia na ndugu zake Yusufu kuona umuhimu wa kwenda kutafuta chakula cha uzima, ikawabidi washuke Misri kununua huko, ndipo wakakutana na ndugu yao Yule Yule ambaye walimuuza zamani..
Ndivyo ilivyo sasa, wayahudi wengi bado hawamwamini Bwana Yesu Kristo kama ndiye Yule masihi wao aliyetabiriwa atakayewaokoa, Leo hii ukiwaeleza habari za Yesu, wanaweza hata wakakupiga na hiyo yote ni kwasababu Mungu aliwapiga upofu kwa makusudi kabisa ili sisi watu wa mataifa tupate wokovu biblia inasema hivyo katika (Warumi 11:11-27)..Lakini utafika wakati ambao sasa upo karibuni, njaa ya kiroho itakuwa kali sana kwao…kiasi kwamba watahitaji maji ya uzima..na siku hiyo watamrudia Kristo naye atajifunua kwao tena kwa namna isiyokuwa ya kawaida, nao watamwamini..
Lakini jambo moja la kujifunza katika habari ile ya Yusufu ni kuwa, ule wakati ambao anataka kujifunua mbele ya ndugu zake, aliwaondoa kwanza watu wote wa nyumbani kwake, akiwemo mke wake, walipelekwa mbali na pale,..ndipo akajifunua mbele za ndugu zake..
Tusome..
Mwanzo 45:1 “Hapo Yusufu hakuweza kujizuia mbele yao wote waliosimama karibu naye. Akapiga kelele, na kusema, Mwondoeni kila mtu mbele yangu. Wala hakusimama mtu pamoja naye, Yusufu alipojitambulisha kwa nduguze. 2 Akapaza sauti yake akalia, nao Wamisri wakasikia. Watu wa nyumba ya Farao nao wakasikia”.
Mwanzo 45:1 “Hapo Yusufu hakuweza kujizuia mbele yao wote waliosimama karibu naye. Akapiga kelele, na kusema, Mwondoeni kila mtu mbele yangu. Wala hakusimama mtu pamoja naye, Yusufu alipojitambulisha kwa nduguze.
2 Akapaza sauti yake akalia, nao Wamisri wakasikia. Watu wa nyumba ya Farao nao wakasikia”.
Vivyo hivyo kabla Kristo hajajifunua kwa watu wake wayahudi, litatangulia kwanza tukio la UNYAKUO, Kristo atamwondoa kwanza bibi-arusi wake kwanza, na ndipo atakapojidhihirisha kwa wayahudi..
Na ndio huo wakati wayahudi watalia sana,na kumwombolezea waliyemchoma kama tunavyosoma katika Zekaria 12:10-14..kutakuwa na maombolezo makubwa Yerusalemu, wayahudi watatubu dhambi zao kwa kumaanisha.., Na ndio huo wakati Mungu ataipigania Israeli kama ilivyokuwa zamani.. huo wakati hakutakuwa na neema tena kwa watu wa mataifa,..Kitakachobakia ni dhiki tu..
Hivyo tunaweza kuona, ni muda mfupi kiasi gani tumebakiwa nao..Hii neema hivi kwetu sisi watu wa mataifa ipo karibuni inaondoka kwetu na kurudi kwa waliokusudiwa kupewa tangu zamani, lakini sisi bado tunauchezea wokovu. Biblia inatufundisha wazi kabisa mambo yatakayoendelea huko mbeleni ni ya kutisha, hizi ni siku za mwisho.. Na leo hii tunayashuhudia, hivyo huu sio wakati wa mtu kubembelezewa wokovu, ni wakati wako sasa wewe uliyelala kuamka na kumgeukia Kristo katika hichi kipindi kifupi tulichonacho.
Maran Atha.
YONA: Mlango 1
UFANYE NINI KAMA MKRISTO WAKATI HUU WA JANGA LA CORONA?
SAUTI NI SAUTI YA YAKOBO, LAKINI MIKONO NI YA ESAU.
IVUMBUE INJILI YA KRISTO KUTOKA KATIKA KILA JAMBO.
HISTORIA YA ISRAELI.
SWALI: Shalom, naomba msaada wenu kuna sehemu zimenichanganya.. Kutoka 1:15-20 ..wale wazalishaji wa kimisri.. wanatumia uongo na Mungu anawabariki… swali langu .. Je busara ya uongo inaweza tumika na isiwe kikwazo mbele ya mtu wa Mungu…
JIBU: Kama ulivyosema busara ya uongo..maana yake kuna uongo wa busara na usio wa busara…Wenye busara ni ule wenye nia ya kujenga na usio wa busara ni ule wenye nia ya kuharibu ambao ni wa Adui shetani.
Tuchukue mfano…mtoto mdogo wa miaka 5 anakuuliza mama/Baba eti Watoto wachanga wanatokea wapi?…sasa si busara kumweleze hatua zote za mtoto kuzaliwa..kwamba kuna vitendo vya kama kukutana kimwili vinahusika…kwa umri wake ule hastahili kufahamu hayo mambo..kwahiyo utamwambia tu kama tulivyokuwa tunaambiwa sisi tulivyokuwa wadogo kwamba “wanapatikana kwenye maua mazuri tu”..Huo ni uongo wa busara…na si dhambi.
Hali kadhalika ndugu yako amekuja kuomba msaada kwako na akakueleza siri zake za ndani sana na amekuomba tafadhali sana usimwambie mtu…na baada ya kutoka hapo..baadhi ya watu wanakufuata na kukuambia uwaambie Habari za ndugu yako yule (yaani maana yake wanataka habari za kumzungumzia kutoka kwako)..Sasa hapo ili kuizuia dhambi ya umbea na usengenyaji..na dhambi ya kumwumiza mwingine kwa kutoa siri zake nje…utawaambia tu wale watu waliokuja kutafuta umbea kutoka kwamba “sifahamu mengi sana kuhusu huyo mtu labda mngeenda kumwuliza mwenyewe”…Sasa hapo umetumia Uongo kuwadanganya kwamba hujui mengi kuhusu yule mtu, ili hali unafahamu mengi..Lakini kwasababu umetumia busara kumfichia ndugu yako aibu yake..basi hujafanya dhambi na Mungu atakubariki.
Lakini ukasema kwamba mimi sio mwongo ni mkweli…na kuwaambia wale watu ndio nafahamu kila kitu wacha nianze kutiririka…japokuwa yote utakayoyasema yatakuwa ni ukweli kuhusu yule mtu lakini mbele za Mungu una dhambi.
Au umepishana na mtu mbaya anatafuta Albino, na anakuuliza hivi mtaa huu kuna mtu ambaye ni Albino nataka tufanye dili, na wewe hapo moyoni ukijua kuwa huyu ni mwalifu, na huku unaona kabisa hapo mtaani kwenu yupo mtu wa namna hiyo..na kwa busara ukamwambia yule mtu hakuna mtu wa namna hiyo mtaani kwetu..hapo utakuwa umetumia uongo lakini uongo wa busara wa kuokoa Maisha ya wengine wasio na hatia hivyo, Bwana atakubariki…lakini ukaanza kueleza kila jambo hapo umesema ukweli lakini ukweli wenye dhambi nyuma yake…Na wengi hawafahamu kuwa shetani japokuwa ni baba wa uongo lakini wakati mwingine pia anazungumza ukweli….lakini ukweli wake anaouzungumza ni ukweli unaopotosha…Kwahiyo upo uongo unaojenga na ukweli unaopotosha vile vile…(Kufahamu juu ya ukweli unaopotosha unaweza kututumia ujumbe tutakutumia somo hilo).
Kwahiyo ndio maana Mungu pia aliwabariki hawa wazalishaji wa ki-Misri kwa busara walizotumia…Ingawa walitumia uongo lakini ulikuwa ni kwa lengo la kuokoa Maisha ya Watoto wasio na hatia.
Na kuna mifano mingi katika biblia watu walitumia uongo unaojenga na Mungu akawabariki…kasome Habari za Yaeli katika Waamuzi 4:17-24, na jinsi alivyobarikiwa kuliko wanawake wote katika Waamuzi 5:24, Hali kadhalika kasome Habari za Elisha katika 2Wafalme 6:19-20, na kasome pia Habari za Rahabu yule kahaba katika Yoshua 2:3-7 n.k
Lakini hiyo haifungua fursa ya kuzungumza uongo kila mahali kwa kisingizio kwamba ni busara tunatumia…Sio unaulizwa wewe ni mkristo unajibu la! Kwa kuogopa kufa..kwa kisingizio kwamba unatumia uongo kwa busara kujiokoa Maisha yako!, hiyo siyo busara bali ni kumkana Kristo, na Biblia inasema tuwe tayari hata kuutoa uhai wetu kwa ajili yake na alisema pia anikanaye mimi nami nitamkana mbele ya Baba yangu na malaika zake siku ile. (Mathayo 10:33)…
Vivyo hivyo sio unaona mtu ni mwasherati kanisani unamfumbia macho na kusema unatumia busara kumhifadhi…watu wote wanaofanya uasherati kanisani kwa makusudi baada ya kuijua kweli na Neno la Mungu, biblia imesema waondolewe, wasifichwe..(kasome 1Wakorintho 5). Hali kadhalika na wauaji, watukanaji, waizi na walevi kanisani…
Hali kadhalika hatupaswi kuambiana uongo kwa sababu nyingine yoyote, Ndugu yako anakuuliza upo sehemu fulani wewe unamwambia sipo hapo, kwasababu tu hutaki aje..huo ni uongo wa yule adui, Unaulizwa leo umesali unasema ndio..na wakati hujasali huo ni uongo wa adui..
Bwana atusaidie tuwe na busara.
Maran atha.
UKWELI UNAOPOTOSHA.
NITAPOKEAJE NGUVU YA KUSHINDA DHAMBI?
Mahuru ndio nini?
KUMBUKA, VIVUKO VYA YORDANI VINAKUNGOJA MBELENI.
https://wingulamashahidi.org/2018/06/27/maswali-na-majibu/
Nilikuwa naomba kujua utofauti kati ya DHAMBI, UOVU na KOSA kibiblia.asante!!
Fukuza tai wote..
Shalom, Jina la mwokozi wetu Yesu Kristo libarikiwe daima,.
Karibu tujifunze Neno la Mungu..
Lipo jambo naamini utaongeza katika Habari hii nzuri ya Ibrahimu ambaye tunamwita baba wa Imani, nasi leo tuige hii Imani yake..Embu tusome sasa..
Mwanzo 15:7 “Kisha akamwambia, Mimi ni Bwana, niliyekuleta kutoka Uru wa Wakaldayo nikupe nchi hii ili uirithi. 8 Akasema, Ee Bwana MUNGU, nipateje kujua ya kwamba nitairithi? 9 Akamwambia, Unipatie ndama wa miaka mitatu, na mbuzi mke wa miaka mitatu, na kondoo mume wa miaka mitatu, na hua, na mwana njiwa. 10 Akampatia hao wote, akawapasua vipande viwili, akaweka kila kipande kuelekea mwenzake, ila ndege hakuwapasua. 11 Hata tai walipotua juu ya mizoga Abramu akawafukuza. 12 Na jua lilipokuwa likichwa usingizi mzito ulimshika Abramu, hofu ya giza kuu ikamwangukia”.
Mwanzo 15:7 “Kisha akamwambia, Mimi ni Bwana, niliyekuleta kutoka Uru wa Wakaldayo nikupe nchi hii ili uirithi.
8 Akasema, Ee Bwana MUNGU, nipateje kujua ya kwamba nitairithi?
9 Akamwambia, Unipatie ndama wa miaka mitatu, na mbuzi mke wa miaka mitatu, na kondoo mume wa miaka mitatu, na hua, na mwana njiwa.
10 Akampatia hao wote, akawapasua vipande viwili, akaweka kila kipande kuelekea mwenzake, ila ndege hakuwapasua.
11 Hata tai walipotua juu ya mizoga Abramu akawafukuza.
12 Na jua lilipokuwa likichwa usingizi mzito ulimshika Abramu, hofu ya giza kuu ikamwangukia”.
Kama tunavyosoma Habari hiyo, kuna wakati Ibrahimu alimwomba Mungu amthibitishie kuwa alichomwahidia ni kweli, kama Gideoni alivyofanya..hivyo Mungu akampa maagizo Ibrahimu juu ya sadaka atakayomwandalia ili aitoe, Hivyo Pengine Ibrahimu akaamka asubuhi na mapema sana, na kwenda mbali kabisa na maeneo ya watu porini, kisha akaindaa akaiweka juu ya kuni, labda kwenye saa moja moja hivi asubuhi alikuwa ameshamaliza shughuli yote ya kuindaa, kinachofuata kwake ni kusubiria sasa aone hatua Mungu anayoichukua..Lakini kilichotokea kwake kilikuwa ni nje ya matarajio yake, alitazamia Mungu angeshuka kwenye muda ule ule, au saa mbili mbili hivi, lakini hakuona chochote,
Akasubiria tena labda kwenye saa nne nne, au saa tano, hakuona chochote, anaingalia tu ile sadaka, aone ni kitu gani Mungu atakwenda kufanya lakini hakuna chochote kilichotokea muda wote huo, mpaka Jua la saa saba linaanza kuwa kali, anaona sasa asogee pembeni kidogo kwenye mti wenye kivuli aendelee kuikodolea macho ile sadaka yake aliyoitoa mapema asubuhi lakini hakuona chochote, mchana kutwa mpaka inafika alasiri, bado akiwa huko porini mwenyewe haoni chochote, akiingalia tu ile nyama, ikianza kukakamaa na mainzi kuongezeka, mpaka sasa wale tai wa angani ambao kazi yao ni kupita porini kutafuta mizoga, wanaiona ipo pale kwa muda mrefu wakidhani pengine ni simba aliila na kuiacha, wakaanza kushuka sasa waile..
Lakini Ibrahimu hakukata tamaa na kuwaachia Tai wale waile sadaka yake aliyoitaabikia tangu asubuhi, japokuwa hamwoni Mungu akimjibu kwa lolote, badala yake kila walipojaribu kutua aliondoka pale kichakani alipokuwa amekaa, na kwenda kuwafukuza..
Aliendelea kufanya hivyo mpaka jua linaanza kuchwa(yaani kuzama), biblia inatuambia, hofu ya giza kuu ikaanza kumwangukia, ni wazi kuwa eneo lile halikuwa eneo lenye makazi ya watu, ni pori nene, hata sadaka yake akawa haioni tena vizuri, ni kama vile Mungu kaitelekeza, au pengine hajairidhia, au pengine alimkosea, lakini katikati ya hofu ile na mashaka yale, muda huo huo alipitiwa na usingizi mzito,..Na ndani ya usingizi ule Mungu akaanza kuzungumza naye, na kumwambia mambo yanayokuja kutokea mbele yake yeye na uzao wake na kumpa ahadi na kumbariki na kumwonyesha nchi atakayompa..
Na alipoamka tu, akashangaa kuona moto umetokea katikati ya ile Sadaka yake, na tayari umeshakwisha kuiteketeza..Ni furaha kiasi gani.kuona unajibiwa maombi yako wazi wazi na Zaidi ya yote Mungu anazungumza na wewe.
Lakini ni nini Mungu anataka tujue ndani ya Habari hiyo?
Wengi wetu, tunakuwa na moyo wa kumtolea Mungu sana katika siku za mwanzoni, na tukishamaliza huwa tunatazama ni wapi Mungu atatubariki, Labda utakuta mtu zamani, alikuwa anatoa ZAKA kwa wakati mbele za Mungu, alikuwa ni mwaminifu kutoa kile alichomwahidia Bwana,..Lakini baadaye alipoona mwezi wa kwanza, na wa pili, na wa tatu, unapita na bado haoni badiliko lolote, au haoni faida yoyote aliyoipata tangu aanze kumtolea Mungu, Zaidi ndio hali inazidi kuyumba hapo ndipo anapokata tamaa na kuacha kuendelea kumtolea Mungu..
Wengine, wanaweza kuwa na nia ya kuendelea kweli kumtolea Mungu, lakini sadaka zao wanaziruhusu zidokolewe na TAI, tofauti na pale mwanzoni wanasema moyoni moyoni aah! Mwaka mzima huu ninatoa fungu la 10, na sioni baraka zozote wacha mwezi huu niiongezee kwenye karo ya shule ya Watoto, kisha mwenzi ujao nitatoa, wengine wanasema, aah, dharura hii imenipata Rafiki yangu anaomba nimtolee mchango wa harusi ngoja mwezi huu nisitoe zaka yangu kwa Mungu..
Ndugu Ibrahimu, hakuruhusu, sadaka yake idokolewe na TAI, japokuwa hakumwona Mungu kwa wakati alioutegemea, lakini aliilinda sadaka yake, kuhakikisha kuwa kile alichoagizwa ndicho atakachokitoa kikiwa kamili hadi dakika ya mwisho muda wote,haijalishi Mungu atawahi au atachelewa.
Lakini tunaona kabla ya Ibrahimu kuingia katika giza kuu, Mungu alimjia na kumtokea, na kuiteketeza sadaka yake..Na kumbariki..
Ndivyo hivyo hata sisi, hatupaswi kuangalia na kusema, tangu nilipoanza kumtolea Mungu, sikuwahi kuona baraka yoyote, wewe endelea kumtolea kwa uaminifu, tu, usiruhusu, sadaka yako imegwe megwe na mambo yasiyokuwa na maana..Haijalishi huoni mabadiliko yoyote kwa miezi au miaka sasa..Lakini endelea kuwa mwaminifu na Mungu aliyemwaminifu Zaidi ya waaminifu, upo wakati ameuweka wa kushusha moto juu ya sadaka yako.. Ukifika huo wakati wewe mwenyewe hutahitaji kusema huyu ni Mungu, kwani mambo yatakuwa wazi mbele ya macho yako.
Tunaona mfano wa Kornelio katika agano jipya, jinsi sadaka zake, zilivyogeuzwa na kuwa ukumbushombele za Mungu (Matendo 10), Jambo lililomfanya sio awe mkristo, lakini hadi sasa tunaisoma Habari yake, katika maandiko.
Vivyo hivyo na sisi, wakati mwingine Mungu anaujaribu uaminifu wetu..Hivyo unapoona huoni faida yoyote sasa katika kumtolea Mungu, usiwe mjinga ukaacha kumtolea au ukaruhusu sadaka zako kudonolewa donolewa, na sababu zisizokuwa na maana yoyote, nataka nikuambie mwisho wa siku hutaambulia chochote, kwasababu Mungu hapokei sadaka kilema.(Malaki 1:14)
TUMTOLEE MUNGU VILE VINAVYOTUGHARIMU ZAIDI.
KWANINI UBATIZO NI WA MUHIMU.
SI KWA FAIDA YA MWENYEZI, BALI KWA FAIDA YETU.
TOA SADAKA ISIYO NA KASORO KWA BWANA.