Title November 2020

Kikoto ni nini?(Yohana 2:15)

Kikoto ni nini?


Kikoto ni aina ya kiboko mfano wa mjeledi. Tazama picha juu.

Tunaweza kuona wakati ule Yesu alipokwenda Hekaluni na kukuta watu wameigeuza nyumba yake kuwa pango la wanyang’anyi, tendo alilolifanya ni kuunda aina hii ya mjeledi, kwa kuusokota kwa kamba mbeleni. Ili awaadhibu vizuri wale watu waliokuwa wanasitiri maovu yao kule, waliokuwa wanafanya biashara zao mule ndani , pamoja na mifugo yao.

Yohana 2:13 “Na Pasaka ya Wayahudi ilikuwa karibu; naye Yesu akakwea mpaka Yerusalemu.

14 Akaona pale hekaluni watu waliokuwa wakiuza ng’ombe na kondoo na njiwa, na wenye kuvunja fedha wameketi.

15 Akafanya kikoto cha kambaa, akawatoa wote katika hekalu, na kondoo na ng’ombe; akamwaga fedha za wenye kuvunja fedha, akazipindua meza zao;

16 akawaambia wale waliokuwa wakiuza njiwa, Yaondoeni haya; msiifanye nyumba ya Baba yangu kuwa nyumba ya biashara”.

Ili kujua Bwana Yesu alimaanisha nini kusema msiigeuze nyumba ya Baba yangu kuwa pango la wanyang’anyi fungua hapa>> USIIGEUZE NYUMBA YA MUNGU KUWA PANGO LA WANYANG’ANYI.

Hiyo ni kutuonyesha kuwa wivu wa Mungu sikuzote unaleta adhabu.

Na adhabu hii ipo kwenye makundi mawili;

Kundi la kwanza: Ni kwa wale watu wanaolinajisi hekalu lake leo hii (yaani Kanisa), kwa kufanya mambo ambayo hayana misingi ya kiimani. Mfano kuigeuza kazi ya Mungu kama biashara, kuabudu masanamu, kwenda nusu uchi kanisani, n.k.

Na kundi la pili: Ni lile la watu wanaolinajisi hekalu lake (yaani Miili yao) kwa kufanya mambo ambayo hayampendezi. Kama vile uzinzi, uuaji, ulevi, n.k. Kwani biblia inasema;

1Wakorintho 6:18 “Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe.

19 Au hamjui ya kuwa MWILI WENU NI HEKALU LA ROHO MTAKATIFU aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe;

20 maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu”.

Na inasema tena;

1Wakorintho 3:16 “Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu?

17 Kama mtu akiliharibu hekalu la Mungu, Mungu atamharibu mtu huyo. Kwa maana hekalu la Mungu ni takatifu, ambalo ndilo ninyi”.

Unaona? Na kikoto hichi tayari kipo mkononi mwa Bwana. Hivyo tujichunguze na sisi tumelitunzaje hekalu lake?  Kama tumekuwa tukiliharibu, ni heri tumgeukie kwa Bwana sasa, kabla ya wakati wa kuharibiwa haujafika. Kwasababu ukishafika na tukakutwa katika hali kama hizo, tujue kuwa hakuna neema tena.

Shalom.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

Nini maana ya uvuvio?.

Nini maana ya kuabudu?

MOJA YA HIZI SIKU TUTAONA MABADILIKO MAKUBWA SANA.

FANYIKA SIPORA WA KRISTO, UNYAKUO UPO KARIBU.

MADHARA YA KUPUUZIA MAAGIZO YA MSINGI MUNGU ANAYOKUPA.

Mataifa ni nini katika Biblia?

Rudi Nyumbani:

Print this post

Nini maana ya uvuvio?.

Uvuvio ni Nini?

Neno uvuvio maana yake ni “kupuliza hewa kwa nguvu”..unapopuliza makaa ya moto maana yake unayavuvia makaa. Unaweza kuuvuvia makaa ya moto kwa mdomo au pepeo.

Ayubu 20: 26 “…..Moto ambao HAUKUVUVİWA na mtu utamla; Utayateketeza yaliyosalia hemani mwake”.

Maana ya mstari huo ni kwamba, moto ambao umezuka tu wenyewe ambao haujapulizwa na mtu utaiteketeza nyumba yake.. Jambo ambalo ni kweli, kwani nyumba zote zinazoungua, ni kutokana na moto, uliojivuvia wenyewe wakati mtu huyo hayupo..kwasababu kama mwenye nyumba angekuwa ni yeye kauvuvia huo moto asingeruhusu, auvuvie mpaka uwe mwingi kiasi cha kuunguza hema yake, anguvuvia kiasi cha kutosha kupikia au kufanyia shughuli zake ndogo, na kuuzima atakapomaliza. Pia unaweza kusoma Isaya 57: 13, inazungumzia habari hiyo hiyo ya Uvuvio.

Sasa tukirudi katika Agano jipya, tunaona biblia imelifananisha tendo la kupokea Roho Mtakatifu, na uvuvio.

Yohana 20: 22  “Naye akiisha kusema hayo, AKAWAVUVİA, akawaambia, Pokeeni Roho Mtakatifu”.

Maneno hayo aliyazungumza Bwana, kama ahadi ya kitu kitakachokuja kuwatokea wanafunzi wake siku chache mbele…Na tarehe ilipofika, iliyopangwa na Mbingu ya wao kumpokea Roho Mtakatifu (yaani siku ile ya Pentekoste)..Roho aliwafikia kama UVUVİO WA UPEPO.

Maana yake ni kwamba Roho Mtakatifu alikuja juu yao kama UPEPO ULİOPULİZWA.. Na kama unajua kazi ya upepo ni kuchochea moto. Kikawaida upepo unavyozidi kuwa mkali ndipo moto na wenyewe unavyozidi kuwaka na kusambaa kwa kasi na kusababisha madhara makubwa..

Matendo 2: 1  “Hata ilipotimia siku ya Pentekoste walikuwako wote mahali pamoja.

2  Kukaja ghafula toka mbinguni UVUMİ KAMA UVUMİ WA UPEPO WA NGUVU UKİENDA KASİ, ukaijaza nyumba yote waliyokuwa wameketi.

3  Kukawatokea ndimi zilizogawanyikana, kama ndimi za moto uliowakalia kila mmoja wao.

4  Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia kutamka”.

Ule upepo ulianza kuchochea, cheche ndogo iliyokuwepo ndani yao, na kufanya Moto mkubwa kuwaka ndani yao, Moto ule ulianza kukaa kwanza kwenye ndimi zao, kila mmoja akaanza kuzungumza kwa lugha mpya, na maneno yenye moto, unaounguza kila kazi za ibilisi na unaoteka nyara kila fikra ipate kumtii Kristo, na baadaye ukasambaa katika mwili wao wote, na kuwafanya waweze kufanya miujiza na ishara zisizo za kawaida.

Hivyo Roho Mtakatifu hata sasa yupo, Ahadi ile hawakupewa mitume pekee yao..Biblia inasema hivi..

Matendo 2:37  “Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu?

38  Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.

39  KWA KUWA AHADİ Hİİ Nİ KWA AJİLİ YENU, NA KWA WATOTO WENU, NA KWA WATU WOTE WALİO MBALİ, NA KWA WOTE WATAKAOİTWA NA BWANA MUNGU WETU WAMJİE.

40  Akawashuhudia kwa maneno mengine mengi sana na kuwaonya, akisema, Jiokoeni na kizazi hiki chenye ukaidi”.

Biblia inasema hapo katika mstari wa 39, kwamba ahadi hiyo ya Roho Mtakatifu ni kwa watu wote, watakaomjia Bwana. Yaani mimi na wewe, na mtu mwingine yeyote, Sasa tunamiaje Bwana?..Biblia imetupa jibu katika huo mstari wa 38 kwamba….. “Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu”.

Ndugu, inawezekana kuna kipawa Mungu kaweka ndani yako na haujijui, inawezekana kuna huduma ameweka ndani yako kwaajili ya kuujenga ufalme wake, na haujui au nguvu yako ni ndogo (ipo kama cheche tu).. Hiyo ni kwasababu UVUVIO haujapita juu yako.. moto uliopo ndani yako bado haujachochewa, lakini siku utakapochochewa ndipo utakapoona tofauti yako ya siku hizo na siku za nyuma. Kama unatamani uvuvio huo, fomula ni hiyo hapo juu.. “tubu dhambi zako, kwa kumaanisha kuziacha kabisa, kisha katafute ubatizo sahihi wa maji tele na kwa jina la Yesu sawasawa na Matendo 2:38, na Bwana ataleta uvuvio wa Roho Juu yako.

Maran atha!

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312


Mada Nyinginezo:

Nini tofauti kati ya Roho Mtakatifu na Roho Takatifu?

TUNAMHITAJI SANA ROHO MTAKATIFU KATIKA KUYAELEWA MAANDIKO.

HATUA ZA ROHO MTAKATIFU KATIKA KUTUONGOZA.

MATUNDA 9 YA ROHO MTAKATIFU

6# SWALI : Dhambi ya kumkufuru Roho Mtakatifu ni ipi?

Rudi Nyumbani:

Print this post

USIIGEUZE NYUMBA YA MUNGU KUWA PANGO LA WANYANG’ANYI.

Jina la Bwana wetu Yesu libarikiwe, Kama umeamka salama ni jambo la kumshukuru Mungu sana, hivyo nakukaribisha katika kuyatafakari maneno ya Uzima ya Bwana wetu, ambayo ndio chakula cha roho zetu.

Neno la Mungu linasema..

Yeremia 7: 9 “Je! Mtaiba, na kuua, na kuzini, na kuapa kwa uongo, na kumfukizia Baali uvumba, na kuifuata miungu mingine ambayo hamkuijua;

10 KISHA MTAKUJA NA KUSIMAMA MBELE ZANGU KATIKA NYUMBA HII, iitwayo kwa jina langu, na kusema, Tumepona; ILI MPATE KUFANYA MACHUKIZO HAYO YOTE?

11 Je! Nyumba hii, iitwayo kwa jina langu, imekuwa PANGO LA WANYANG’ANYI MACHONI PENU? Angalieni, mimi, naam, mimi, nimeliona jambo hili, asema Bwana”.

Tusome tena…

Mathayo 21: 13  “akawaambia, Imeandikwa, Nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala; bali ninyi mmeifanya kuwa PANGO LA WANYANG’ANYI

Umewahi kujiuliza kwanini, kwanini Bwana alitumia huo usemi…. “bali ninyi mmeifanya kuwa PANGO LA WANYANG’ANYİ”. Umewahi kutafakari pango la wanyang’anyi ni kitu gani?.

Siku zote wezi/vibaka wanakuwaga na maskani yao wanayojifichia, ambayo kwao ndio sehemu salama, na inakuwa ni sehemu ya maficho kwa muda, mara  nyingi inaweza kuwa kwenye kipori fulani, au kwenye jengo fulani ambalo halijakamilika, au kwenye mapango ambayo ndani yana giza, Lengo ni kwamba wakishamwibia mtu, wanakimbilia huko, kujificha kwa muda, na baadaye kurudia tena kufanya uhalifu wao…hivyo inakuwa ni ngumu kuwakamata.. Na mara nyingi kwenye hayo maficho yao, ndio sehemu zao za kuchezea kamari, au kuvuta sigara, au kufanyia biashara zao haramu kama za kuuziana mihadarati n.k

Mfano kamili wa leo, mtu atatoka kufanya uasherati, lakini mtu huyo huyo jumapili atakwenda kanisani…jumatatu atarudia kufanya kile kile kitu na kurudi tena kanisani, jumapili inayofuata…Mtu huyo ameigeuza nyumba ya Mungu kuwa pango la wazinzi, kanisa ni sehemu yake ya kujisitiri kwa muda, ili aonekane kwamba na yeye ni mkristo, au ili ajifariji moyoni kwamba bado anampenda na kumjali Mungu, na ili ajifariji kwamba jamii inamwona msafi..Lakini kiuhalisia hana mpango wa kuacha uasherati wake, wala hana mpango wa kumwacha yule mtu anayeishi naye ambaye wanayefanya naye uasherati.

Mwingine ni fisadi, au tapeli lakini atahudhuria kanisani kama ilivyo ada, na wala haendi kwa lengo la kubadilika, bali anakwenda pale kama sehemu yake ya kusitiri maouvu yake..

Ndugu yakumbuke maneno ya Bwana.. “Nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala; bali ninyi mmeifanya kuwa PANGO LA WANYANG’ANYİ”.

Usiigeuze nyumba ya Mungu kuwa ni sehemu yako ya maficho ya dhambi zako…bali pageuze kuwa mahali pa sala, mahali patakatifu pa kukujenga roho yako. Kadhalika nyumbani kwa Mungu sio mahali pa kwenda umevaa nusu uchi, umevaa vimini, au umepaka wanja na lipstick, au umenyoa kiduku, kwa ufupi sio mahali pa kutangaza mwili wako au biashara yako…pale ni mahali pa kumheshimu Mungu.

Kama Bwana alizipindua zile meza za wafanya biashara kwenye nyumba yake, hatashindwa kuipindua biashara ya kuuza mwili wako huo usio na staha uliokuja kuuza pale kwenye nyumba yake. Kama umeamua kutangaza biashara ya mwili wako, yapo mapango mengi huko mitaani, lakini usijaribu kuiguza nyumba ya Mungu kuwa kama mojawapo ya mapango hayo.

Kama hujampa Kristo maisha yako, wakati ni sasa. Tubu leo naye atakusamehe bure kabisa. Kumbuka Kristo anarudi, siku moja hutasikia maneno kama haya ambayo unaona sasa ni upuuzi na kelele..wakati huo unyakuo utakuwa umepita, na hutasumbuliwa sumbuliwa na mahubiri tena. Lakini akiamua kutubu leo, Kristo atakupokea kama neno lake linavyosema..katika Yohana, na atakupa Roho Mtakatifu atakayekuongoza katika kuijua kweli yote.

Yohana 6:37 “Wote anipao Baba watakuja kwangu; wala ye yote ajaye kwangu sitamtupa nje kamwe”.

Maran atha

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312


Mada Nyinginezo:

LIVUNJENI HEKALU HILI, NAMI KATIKA SIKU TATU NITALISIMAMISHA.

TOFAUTI KATI YA HEKALU, SINAGOGI NA KANISA NI IPI?

WEWE NI HEKALU LA MUNGU.

Bawabu ni nani/nini?

KWANINI YESU KRISTO NI WA MUHIMU KWETU SASA?

Rudi Nyumbani:

Print this post

Nini maana ya kuabudu?

Kuabudu ni nini?

Kuabudu maana yake ni “kufanya Ibada”.. Kitendo cha kufanya Ibada ndio “kuabudu”. .

Hivyo Ibada yoyote ile ni lazima ijumuishe vitu hivi vitano vifuatavyo.

  1. Kujifunza Maneno yake na kuyatafakari

Hii ndio sehemu ya kwanza na ya muhimu katika Ibada.. Na kumbuka kujifunza sio kukariri, bali ni kukaa chini na kuyachambua maandiko kwa uwezo wa Roho kama vile Mwalimu na mwanafunzi wanavyofundishana wakiwa darasani.

  1. Kumwimbia

 Hichi ni kipengele cha pili cha muhimu katika ibada, ambacho kinaweza kuwa katika mfumo wa kumshukuru Mungu na kumsifu kwa (Aidha tenzi za rohoni, au kwa nyimbo za sifa na kuabudu au vyote kwa pamoja)

  1. Kushiriki Meza ya Bwana

Hichi ni kipengele cha Tatu, na cha muhimu pia katika ibada…1Wakorintho 11:25 “Na vivi hivi baada ya kula akakitwaa kikombe, akisema, Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu; fanyeni hivi kila mnywapo, kwa ukumbusho wangu”.

  1. Maombi

Maombi yanajumuisha pia dua na sala..na ili ibada iwe ibada ni lazima kuwepo na kipindi cha maombi, wakati huu ndio wakati wa fursa ya kupeleka haja zetu kwa Mungu wetu.

         5 . Matoleo

Hichi ni kipengele cha mwisho kabisa, ambacho kinakamilisha IBADA. Biblia inasema (katika Kumbukumbu 16:16), kwamba tusiende nyumbani kwake, mikono mitupu. Matoleo ndio yanayokamilisha ibada. Hivyo mtu hawezi kusema leo nimekwenda kumwabudu Mungu bila kumtolea.

Hivyo mtu akivifanya vipengele hivyo vitano, katika ROHO NA KWELI,  Basi anakuwa amemwabudu wa kweli wa mbingu na nchi.

Sasa utauliza, je tunamwabudu vipi Mungu katika Roho na kweli?. Inamaana tuingie katika ulimwengu wa roho?

Ni muhimu kufahamu kuwa kuishi katika Roho sio kuishi kwa kuona mambo yasiyoonekana kama mapepo, au malaika, au kuona mbingu au kuona maono, hapana hiyo siyo tafisiri ya kuishi kwa Roho au kuabudu kwa Roho.. Tafsiri ya kuishi kwa Roho ni kuishi kwa kulifuata Neno la Kristo… Mtu yeyote anayeishi kwa kuyafuata maneno ya Kristo, huyo ni mtu wa rohoni asilimia mia, hata kama maisha yake yote hajawahi kuona ono hata moja, au hajawahi kuona malaika, wala mapepo. Kwasababu biblia inasema Maneno ya Kristo ndio Roho.

Yohana 6: 63  “Roho ndiyo itiayo uzima, mwili haufai kitu; MANENO HAYO NİLİYOWAAMBİA Nİ ROHO, tena ni uzima”.

Hivyo tunapomwambudu Mungu katika roho na kweli, maana yake ni kwamba tunafanya ibada kulingana na jinsi NENO LAKE linavyosema katika ukweli wote na usafi wa moyo.

Je umempokea Kristo?.. kama bado hujampokea na unakwenda kanisani tu kutimiza wajibu fulani, basi jua hapo huendi kumwabudu Mungu katika Roho na Kweli, hivyo hakuna baraka zozote za rohoni ambazo ulikuwa unazipata. Lakini leo ukiamua kutubu, na kuacha dhambi..Kristo ataingia moyoni mwako na kukuponya..na atakusafisha kwa damu yake, na kukufanya uweze kumwabudu Mungu katika Roho na Kweli.

Kama leo hii upo tayari kumpokea, basi fuatilisha sala hii fupi ya toba kwa kufungua hapa >> SALA YA TOBA.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312


Mada Nyinginezo:

Je! Mwanamke anapaswa afunikwe kichwa anapokuwa ibadani?

JE KUVAA PETE NI DHAMBI?

KUABUDU SANAMU/IBADA ZA SANAMU.

USIMWABUDU SHETANI!

JIFUNZE KULIGAWANYA VYEMA NENO LA MUNGU.

Rudi Nyumbani:

Print this post

Kwanini Kuhani wa Mungu Eli alikufa kwa kuvunjika shingo?

 Kwanini Kuhani wa Mungu Eli alikufa kwa kuvunjika shingo, Na sio kwa njia nyingine yoyote salama?

Habari ya Eli ni funzo tosha kwa kanisa la Kristo leo hii. Mungu aliruhusu afe kifo cha aina hiyo, ili kutimiza mstari huu wa biblia;

Mithali 29:1 “Aonywaye mara nyingi akishupaza shingo, Atavunjika ghafula, wala hapati dawa”.

Kama tunavyoijua habari ya Eli,alikuwa kuhani wa Mungu kwa muda wa miaka 40, na katika ukuhani wake, alifanya kazi hiyo pamoja na wanawe wawili, lakini watoto wake hawa walikuwa waovu kupindukia, kwani waliwakosesha Israeli kwa tabia zao sizizoakisi ukuhani, na habari yao ikavuma kila mahali kuwa hawafai, kwani walikuwa wanaila dhabihu isivyostahili na zaidi ya yote, walikuwa wanalala na wanawake waliokuwa wanatumika mbele ya hema ya kukutania, mfano  tu baadhi ya wakristo katika kanisa la Mungu leo hii.

Sasa dhambi hii ilikuwa ni kubwa sana, na Mungu alikuwa amekusudia kuwauwa wale watoto wawili wa Eli, na sio Eli mwenyewe, lakini tabia ya Eli ya kupuuzia na kuwaheshimu watoto wake zaidi kuliko Mungu, hilo lilimfanya Mungu amuue na yeye kwa kifo hicho. Kwasababu alijua kabisa uovu unaofanywa na wanawe lakini hakulitilia mkazo.

Eli alionywa mara tatu, mara ya kwanza alionywa na waisraeli, kuwa watoto wake hawafai na kwamba anapaswa awaondoe katika kazi ya ukuhani lakini hakusikia..

Akaonywa tena mara pili na Mungu kupitia nabii wake, (1Samweli 2:29), lakini bado hakuwaondoa, akawaheshimu wanawe kuliko Mungu.

Akaja tena kuonywa mara ya tatu kupitia mtoto Samweli, akaelezwa mpaka na hukumu itakayowakuta watoto wake, lakini yeye bado akaendelea kuwaacha wafanye machafuko yote hemani pa Bwana.

1Samweli 3:13 “Kwa maana nimemwambia ya kwamba nitaihukumu nyumba yake milele, kwa ajili ya ule uovu alioujua; kwa kuwa wanawe walijiletea laana, wala yeye hakuwazuia”.

Ndipo siku ya siku ilipofika, Wafilisti waliwavamia Israeli, wakawapiga, wakaliiba na sanduku la Agano, Na yeye akiwa amebaki hemani mwake kusubiria taarifa ya vita, kama tunavyoijua Habari, kijana mmoja alitoka huko akamletea habari, na kumwambia Israeli imepigwa, wanawe wote wawili wamekufa na kibaya zaidi Sanduku la Mungu limechukuliwa na wafilisti. Aliposikia tu habari hiyo akadondoka kwa nyuma, shingo yake ikavunjika na pale pale akafa.

1Samweli 4:13 “Alipofika, tazama, Eli alikuwa ameketi kitini pake kando ya njia, akingojea; maana moyo wake ulitetemeka kwa ajili ya sanduku la Mungu. Na yule mtu alipoingia mjini, akatoa habari, mji wote ukalia.

14 Naye Eli aliposikia kelele za kile kilio, akasema, Maana yake nini kelele za kishindo hiki? Yule mtu akafanya haraka, akaenda, akamwambia Eli.

15 Basi Eli umri wake umepata miaka tisini na minane; na macho yake yamepofuka hata asiweze kuona.

16 Yule mtu akamwambia Eli, Mimi ndimi niliyetoka jeshini, nami leo hivi nimekimbia toka jeshini. Naye akasema, Yalikwendaje, mwanangu?

17 Yeye aliyeleta habari akajibu, akasema, Israeli wamekimbia mbele ya Wafilisti, tena watu wengi sana wameuawa, hata na wana wako wawili, Hofni na Finehasi, wamekufa pia, na sanduku la Mungu limetwaliwa.

18 Ikawa alipolitaja sanduku la Mungu, Eli akaanguka kitini pake kwa nyuma, kando ya mlango, shingo yake ikavunjika, akafa; maana alikuwa mzee, tena mzito. Naye alikuwa amewaamua Israeli miaka arobaini”.

Hivyo  kitendo cha Eli kufa kifo cha kuvunja shingo ni Mungu alikuwa anafundisha jinsi madhara yatakavyowakuta watu wale wanaopuuzia na kudharau maagizo yake.

Tengeneza picha Eli alikuwa ni kuhani lakini alikufa kifo cha ghafla tu kwa kosa la kudharau maneno ya Mungu. Vipi kuhusu sisi ambao kila siku Mungu anatuonya tuache hichi au kile lakini hatutaki kusikia, Mtu anazini na bado anasema ameokoka.  Kila siku tunasikia maneno ya Mungu lakini bado hatutaki kuyakabidhi maisha yetu kwake.. Je! Ni kitu gani tunakitazamia siku za usoni?

Hututakufa kifo cha kuvunjika shingo kimwili, lakini rohoni tutavunjika shingo zetu ghafla, na hutakuwa na nafasi tena ya kumrudia Mungu, kwasababu hukumu tayari itakuwa umeshatolewa juu yetu.

Mithali 29:1 “Aonywaye mara nyingi akishupaza shingo, Atavunjika ghafula, wala hapati dawa”.

Inawezekana na wewe umeshaonywa mara nyingi kwa kupitia mahubiri ya Neno la Mungu, lakini ulikuwa umeshupaza shingo…. Kwanini leo, usimrudie muumba wako? Kwanini usianze maisha mapya na Kristo, uondokane na laana ya dhambi? Maisha ya dhambi yamekupa faida gani mpaka sasa, Ukifa leo ghafla huko utakapokwenda utakuwa ni mgeni wa nani?. Au Kristo akirudi leo wewe utakuwa wapi?. Kwasababu tupo ukingoni kabisa mwa nyakati, Kristo anarudi.

 Ulimwengu huu umeshatamkiwa meme, mene, Tekeli na Peresi kitambo sana, Umeshatamkiwa IKABODI, Hakuna cha ziada zaidi ya kuharibiwa tu. Tubu dhambi zako kama bado hujatubu. Na pia tafuta kubatizwa ikiwa bado hujabatizwa. Na Mungu atakupa Roho wake Mtakatifu. Katika wakati huu wa kumalizia.

Maran Atha.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312


Mada Nyinginezo:

IKABODI MAANA YAKE NI NINI?

NA NENO LA BWANA LILIKUWA ADIMU SIKU ZILE.

Kwanini Samweli aliruhusuiwa kuhudumu hekaluni kama vile Walawi wakati yeye ni mu-Efraimu?

Kitabu cha YASHARI kinachozungumziwa katika 2Samweli 1:17-18, ni kitabu gani?

ROHO YA MPINGA KRISTO IKITENDA KAZI SIKU HIZI ZA MWISHO

Rudi Nyumbani:

Print this post

Nzio ni nini?(Yohana 2:6)

Nzio ni kipimo cha ujazo wa kimimika kilichotumiwa zamani na wagiriki,  Nzio moja ina  ujazo wa karibia lita 40,

Katika biblia utaona ile habari ya Yesu kualikwa katika arusi kule Kana mji wa Galilaya, Neno hili lilitumika tusome;

Yohana 2:6 Basi kulikuwako huko mabalasi sita ya mawe, nayo yamewekwa huko kwa desturi ya Wayahudi ya kutawadha, kila moja lapata KADIRI YA NZIO mbili tatu.

Hivyo hapo unaweza kupata picha hapo, hayo mabalasi yalikuwa na ujazo mwingi kiasi gani. Kama kila balasi moja linachukua nzio mbili au tatu, ukikadiria hapo, ni kuwa balasi moja lina ujazo wa lita  80 mpaka 120.

Na mabalasi yalikuwa ni 6, hivyo ujazo wa maji yaliyowekwa pale na kubadilika kuwa divai ni karibia lita 480-720. Hivyo ni kiwango kikubwa sana. Hivyo unaweza kuona jinsi divai hiyo ingewahudumia watu wengi kiasi gani. Kumbuka mtu mmoja tu hawezi kunywa lita nzima ya divai, akijitahidi sana atakunywa nusu au robo.

Lakini ni nini Mungu alikuwa analifundisha kanisa?

Ni kuwa pale tulipo na mapungufu, yeye anaweza kutujaza, jambo hilo utaona tena alipoigawa ile mikate mitano na samaki wawili na kulisha maelfu ya watu. Na alifanya hivyo mara mbili , Hiyo ni kutuonyesha kuwa palipo na vichache, au pale ambapo hamna kabisa Mungu anaweza kugeuza kitu kingine kisichokuwa na thamani  kikawa na thamani kwetu. Ipo mifano mingi sana katika biblia, utaiona ile habari ya Elisha na yule mwanamke ambaye mume wake alikuwa anadaiwa, mpaka akafa hajalipa deni, yule anayemdai akaja akataka kwenda kuwachukua watoto wake awafanye kuwa watumwa, lakini yule mama alipokwenda kwa Elisha amsaidie, Elisha akamwomba Mungu, ndipo akamwambia akachukue vyombo vitupu kisha amimine mafuta kwenye vyombo hivyo, kwa kadiri awezavyo kwasababu mafuta yale hataisha, kisha aende kuuza, na fedha itakayopatikana, alipe deni lake, na itakayobaki atumie yeye na familia yake(2Wafalme 4:1-7) .

 Hiyo yote ni kuonyesha kuwa Mungu anaweza kutoa pale pasipowezekana na ndio maana anaitwa YEHOVA- YIRE, (yaani Mungu mpaji wetu). Hivyo na wewe ukimtegemea yeye atakutendea miujiza kama hiyo.

Lakini ni sharti kwanza uwe mwana wake. Swali ni Je! Kristo yupo ndani yetu? Majibu yote tunayo, lakini tujue kuwa hakuna kimbilio la kweli nje ya Kristo. HUO NDIO UKWELI PEKEE ULIODUMU DUNIANI KWA MIAKA YOTE.

Shalom.

Kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

Je! mabalasi Bwana Yesu aliyoyatumia kugeuzia maji kuwa divai, yalitumika tu kwa kazi hiyo?

Kuwatema farasi, maana yake ni nini?

HAMJAFAHAMU BADO?

KIFO CHA MTAKATIFU PERPETUA NA FELISTA.

VIFO VYA MITUME WA YESU/ JINSI MITUME WALIVYOKUFA.

Rudi Nyumbani:

Print this post

Hozi ni nini? (1Nyakati 4:10, 7:28, 9:2)

Hozi ni nini?


Hozi ni neno linalomaanisha himaya, ikijumuisha eneo na vitu mtu anavyomiliki.

Kwa mfano unaweza kuona, Yabesi, alimwomba Mungu ambariki na kumzidishia Hozi yake (Himaya yake), Hiyo akiwa na maana kuwa azidishiwe mifugo, azidishiwe uzao, azidishiwe mali, azidishiwe watumwa na wajakazi, azidishiwe ardhi, azidishiwe ukuu n.k. Na kweli kama tunavyosoma Mungu aliridhia maombi yake kwasababu alikuwa ni mcha Mungu, japokuwa alitokea katika chumbuko la huzuni.

1Nyakati 4:10 “Huyo Yabesi akamlingana Mungu wa Israeli, akisema, Lau kwamba ungenibarikia kweli kweli, na kunizidishia HOZI YANGU, na mkono wako ungekuwa pamoja nami, nawe ungenilinda na uovu, ili usiwe kwa huzuni yangu! Naye Mungu akamjalia hayo aliyoyaomba”.

Neno hilo utalisoma pia  katika vifungu hivi;

1Nyakati 7:27 “na mwanawe huyo ni Nuni, na mwanawe huyo ni Yoshua.

28 Na HIZI NDIZO HOZI zao na makao yao; Betheli na vijiji vyake, na upande wa mashariki Naara, na upande wa magharibi Gezeri na vijiji vyake; na Shekemu pia na vijiji vyake, hata Aza na vijiji vyake;

1Nyakati 9:1 “Hivyo Israeli wote walihesabiwa kwa nasaba; na tazama, hizo zimeandikwa katika kitabu cha wafalme wa Israeli; na Yuda wakachukuliwa mateka mpaka Babeli, kwa sababu ya makosa yao.

2 Basi wenyeji wa kwanza waliokaa katika HOZI ZAO katika miji yao walikuwa Israeli, na makuhani, na Walawi, na Wanethini”.

Vivyo hivyo na sisi, tukimcha Mungu, mfano wa Yabesi Mungu anaweza kuzizidisha himaya zetu mfano wa Yabesi pale tutakapomwomba. Lakini vilevile tusipomcha yeye, anao uwezo wa kummilikisha mtu mwingine hiyama zetu na tukabakiwa hatuna kitu kama vile alivyofanya kwa wana wa Israeli, walipomuasi akawapeleka utumwani Babeli, na himaya zao zikamilikiwa na watu wengine.

Na himaya sio lazima tu iwe ile ya mwilini, Rohoni pia tunazo himaya, pale tunapomkataa Mungu maisha mwetu, hapo hapo adui yetu shetani ibilisi anapata nguvu ya  kuzitawala himaya zetu. Na ndio hapo anakuwa na uwezo asilimia mia wa kujiamulia jambo lolote baya  katika maisha yetu, hata kutuua ataweza, kwasababu tumekusoma Baraka na ulinzi wa ki-Mungu.

Hivyo sisi nasi pia tunawajibu wa kuzilinda HOZI zetu. Kwa kuupokea wokovu na kuulinda katika utakatifu. Ndipo Bwana atakapotuzidisha na kutuongeza kupita kiasi.

Swali ni Je! Upo ndani ya wokovu? Je! Hozi zako zipo mikononi nani? Jibu unalo, jibu ninalo. Lakini Yesu Kristo ndio mwokozi.

Shalom.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

Kuwatema farasi, maana yake ni nini?

Sikukuu ya kutabaruku ni ipi?

Kutakabari ni nini katika biblia?.

DHIKI KUU INAKUJA NA UNYAKUO UPO KARIBU.

MAPIGO YA VITASA SABA, NA SIKU YA BWANA.

Rudi Nyumbani:

Print this post

CHUKI ULIZO NAZO KWA MAADUI ZAKO, SIZO ALIZONAZO MUNGU JUU YAO.

Shalom, Karibu tujifunze biblia, ambayo ni Neno la Mungu.

Ni vizuri kumjua Mungu ili tuwe na Amani.. Biblia inasema hivyo katika..

Ayubu 22: 21 “Mjue sana Mungu, ili uwe na amani; Ndivyo mema yatakavyokujia”.

Maana yake ni kwamba tukiyajua mapenzi ya Mungu na tabia za Mungu basi tutakuwa na AMANI,  Na ndivyo mema yatakavyotujia.

Leo kwa neema za Bwana hebu tujifunze kidogo, juu ya tabia ya Mungu.

Wengi wetu katika Maisha tunayoishi, tunakumbana na majaribu mengi yanayoletwa na wanadamu wenzetu. Yaani wapo watu wanatumika na Adui shetani, kutuumiza sisi kihisia na kimwili, na mbaya Zaidi wanafanya hayo huku wanajua kabisa. Kwa lugha iliyozoeleka sasa watu hao wanaitwa MAADUI.

Leo hii ukimwuliza mtu yeyote je! Unao maadui?.. Ni ngumu kusikia mtu akisema kwamba sina maadui kabisa!..  Ni lazima utakuta mtu anao maadui, kwa vyovyote vile.

Wengine maadui zao ni watu wanaowanyanyasa, wengine maadui zao ni watu wanaowadharau kupita kiasi, wengine maadui zao ni watu wanaojisifu juu yao, wengine maadui zao ni watu wanaowaonea wivu n.k. Na katika nyakati hizi tunazoishi, asilimia kubwa ya watu wanaomlilia Mungu, ni kutokana na vita walizonazo dhidi ya wanaowaita maadui zao.

Utakuta mtu atakwenda kanisani kuomba Mungu amnyanyue kwenye kazi yake ili azikomeshe dharau za watu Fulani wanaomdharau, mwingine utakuta yupo kwenye mfungo wa maombi apate fursa Fulani, iwafunge midomo watu Fulani (ambao kwake yeye ndio kama maadui zake). Ni wachache sana ambao utakuta wanafunga kumwomba Mungu awape kazi nzuri, au fursa Fulani ili wamtumikie yeye kupitia hiyo.

Sasa hiyo hali ya kuingia kwenye vita dhidi ya maadui, haikuanzia hapa, ilianzia tangu kwenye biblia..Leo tutajifunza mifano kadhaa ya watu waliopambana na maadui zao, na kwa kupitia mifano hiyo, na sisi pia tutapata kujua hisia za Mungu, juu ya tunaowaita maadui zetu, Pamoja na namna ya kushughulika nao.

HANA na PENINA.

Hawa walikuwa ni wanawake wawili wa mwanaume mmoja aliyejulikana kama Elkana. Penina alikuwa na watoto lakini Hana hakujaliwa kupata Watoto, na kama tunavyojua kitu gani kilifuata, Biblia inasema Penina alianza kumchokoza sana Hana kwasababu ni tasa (1Samweli 1:6). Kwa ufupi ni kwamba alikuwa anamdhihaki na kumdharau sana..kisa tu yeye ana Watoto na mwenzie hana.

Kama wewe unayesoma ujumbe huu ni mwanamke, hebu jiweke kwenye hiyo nafasi, huna mtoto, halafu mwingine aliye naye anakukebehi kebehi, anakupa kupa vijimaneno vya kukumiza na kukudhalilisha. Bila shaka tayari huyo kashakuwa adui yako.

Ndicho kilichomtokea Hana, baada ya kuzungumzwa sana na mke mwenza, uvumilivu ukamshinda ikabidi aanze kumlilia Mungu. Na baadaye kama tunavyoijua Habari, Mungu akasikia kilio chake na yeye akampa Watoto.

Lakini hebu turudi kwa upande wa Elkana, ambaye ndiye mume wa wanawake wote wawili (Hana na Penina). Wakati Hana na Penina ni maadui, Elkana alikuwa anawapenda wote. Wakati Hana anajifungua mtoto wa kwanza, haikumfanya Elkana awachukie Watoto wa Penina, wala haikumfanya amchukie Penina. Ijapokuwa Penina na Hana walikuwa ni maadui.

Ndivyo hivyo hivyo kwa Mungu wetu, Yule ambaye ni adui wako wewe, yule unayemchukia…haimaanishi kwamba Mungu naye anamchukia kama unavyomchukia wewe…yule anayekuudhi sana, haimaanishi kwamba anamuudhi Mungu kama anavyokuudhi wewe. Hivyo usichukue hasira zako ukazifanya za Mungu.

Hebu tujifunze tena mfano mwingine.. wa SARA na HAJIRI. Hawa nao walikuwa ni wanawake wawili, ambao ilifika wakati wakashiriki mume mmoja aliyeitwa IBRAHIMU. Na ikafika kipindi pia wakawa ni maadui kwasababu Hajiri alipata mtoto na Sara hakupata. Na Hajiri ambaye ni kijakazi alianza kumdharau bibi yake, kwasababu hakuwa na mtoto. Hivyo kukawa na ugomvi mkubwa wa chini kwa chini..(maadui hao wawili wamekutana). Na ulipofika wakati wa Mungu kumfungua tumbo Sara, alimfukuza Hajiri Pamoja na mwanawe Ishmaeli.

Lakini je! Jiulize chuki aliyokuwa nayo Sara dhidi ya mtoto wa kijakazi wake Hajiri (yaani Ishamaeli), je! ndiyo hiyo hiyo iliyokuwa juu ya Ibrahimu kwa Ishamaeli?.. Au chuki Hajiri aliyokuwa nayo kwa Isaka mwana wa Sara, ndiyo hiyo hiyo aliyokuwa nayo Ibrahimu kwa Isaka?.. La!..sio hiyo hiyo, Badala yake utaona Ibrahimu aliwapenda wanawe wote na wala hakuna aliyekuwa anamchukia, ijapokuwa mama zao walikuwa hawapatani.

Vivyo hivyo, huyo unayemwona ni Adui yako leo, ambaye ni mtesi wako leo, ambaye anakufanya ulie na kuhuzunika usifikiri Mungu anamchukia kama unavyomchukia wewe. Atakachofanya Mungu ni kumweka mbali na wewe, lakini usifikiri atakuwa na kinyongo naye kama ulichonacho wewe juu yake..wala usifikiri Mungu atamwua kwasababu yako wewe.. Futa hayo mawazo!…Kuanzia leo “anza kumjua Mungu ili uwe na amani”..Wala usipoteze muda wako kumwombea maombi ya kufa..kwasababu hatakufa!!..Ni sawa na Sara kumtuma Ibrahimu akamwue Ishamaeli..atakuwa anapoteza muda wake tu!.

Hali kadhalika usiogope!..Adui yako atakapokuombea shari kwa Mungu..atakuwa anapoteza muda wake tu!..Kwasababu chuki alizonazo yeye juu yako, sizo alizonazo Mungu juu yako. Ni sawa na Hajiri kumtuma Ibrahimu akamwue Isaka. Ni kitu kisichowezekana, atakuwa anapoteza muda wake tu!! Usipoteze muda wako, kufanya hivyo.

Utajifunza tena jambo kama hilo hilo kwa wake wa Yakobo.

Hivyo kwa hitimisho..Bwana wetu Yesu Kristo aliyasema maneno haya…

Mathayo 5:43  “Mmesikia kwamba imenenwa, Umpende jirani yako, na, UMCHUKIE ADUI YAKO;

44  lakini mimi nawaambia, WAPENDENI ADUI ZENU, WAOMBEENI WANAOWAUDHI,

45  ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni; maana yeye huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki.

46  Maana mkiwapenda wanaowapenda ninyi mwapata thawabu gani? Hata watoza ushuru, je! Nao hawafanyi yayo hayo?”

Kama unanyanyaswa..usipoteze muda kumwombe shari ndugu yako..kwasababu hayo sio mapenzi ya Mungu, wala usifurahie kuanguka kwake…je! Unadhani Elkana alikuwa anafurahishwa na ugomvi uliokuwepo kati ya Hana na Penina?..vivyo hivyo Mungu hapendezwi na sisi tunapokuwa na ugomvi na watu wanaotuchukia..na wala maombi ya magomvi hayampendezi..

Mithali 24:17 “Usifurahi, adui yako aangukapo; Wala moyo wako usishangilie ajikwaapo;

18 Bwana asije akaliona hilo, likamkasirisha; Akageuzia mbali naye hasira yake”.

Na pia usiogope! Mtu anapokuchukia au anapokufanyia ubaya..au anapokushitaki mbele za Mungu…fahamu kuwa anapoteza muda tu!..kwasababu Mungu hakuchikii kama yeye anavyokuchukia.

Bwana atubariki

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

MPENDE JIRANI YAKO KAMA NAFSI YAKO.

KWANINI NI YESU KRISTO WA NAZARETI?

HEKIMA YA KIMUNGU, INAINGIAJE MIOYONI MWETU?

MALAIKA WAPELELEZI WA HUKUMU WANAPITA SASA.

CHAPA YA MNYAMA

Rudi Nyumbani:

Print this post

Kuwatema farasi, maana yake ni nini?

SWALI: Naomba kufahamu kuwatema farasi maana yake ni nini?. Kwanini Mungu aliwaagiza wana wa Israeli wakati mwingine wawateme farasi za maadui wao vitani?

Neno hilo tunalisoma katika kifungu hiki;

Yoshua 11:6  “Bwana akamwambia Yoshua, Usiche wewe kwa ajili ya hao; kwani kesho wakati kama huu nitawatoa hali wameuawa wote mbele ya Israeli; UTAWATEMA FARASI ZAO, na magari yao utayapiga moto.

7 Basi Yoshua akaenda, na watu wote wa vita pamoja naye, ili kupigana nao hapo penye maji ya Meromu ghafula; wakawaangukia.

8 Bwana akawatia mkononi mwa Israeli, nao wakawapiga, na kuwafukuza hata kufikilia Sidoni ulio mkuu, na hata kufikilia Misrefoth-maimu, tena hata kufikilia bonde la Mispa upande wa mashariki; wakawapiga hata wasiwasaze hata mtu mmoja aliyesalia.

9 Yoshua akawafanyia vile vile kama Bwana alivyomwamuru; AKAWATEMA FARASI ZAO, na magari yao akayapiga moto”.

Kama tunavyojua Yoshua na wana wa Israeli walipovuka Yordani walikutana na maadui zao wengi kule Kaanani, maadui ambao walikuwa na uzoefu mkubwa wa kivita, na wenye majeshi mengi. Na hapa tunaona wana wa Israeli walipofika sehemu moja walikutana na huyu adui yao mmoja “Yabini” mfalme wa Azori ambaye hakumwendea peke yake bali alikwenda kukusanya nguvu kutoka katika mataifa ya kando kando yake ili yamsaidie kummaliza Yoshua na wana wa Israeli wote kwa ujumla,na  biblia inasema lilikuwa ni jeshi kubwa kama mchanga wa bahari, wenye magari mengi ya vita na wafasi wengi sana.

Lakini utaona hapa Mungu anampa maagizo Yoshua na kumwambia kuwa watakapowapiga wasichukue chochote bali wayachome magari yao ya vita na wawateme farasi zao.

Kutema farasi maana yake nini?

Kutema ni kujeruhi tishu za misuli ya miguu, ambazo zinasababisha mtu au mnyama kuweza kutembea, au kukimbia au kuruka au kupanda.  Tishu hizo ngumu kwa mwanadamu au kwa mnyama zipo sehemu ya nyuma ya miguu kuanzia kwenye paja hadi kwenye goti, na kwa mnyama vivyo hivyo kwenye miguu yake ya nyuma.

Tishu hizo zikikatwa huwa haziponyeki, na mtu au mnyama unakuwa mlemavu wa kudumu. Hawezi kukimbia, au kuruka au kutembea.

Hivyo ilikuwa ni desturi za kivita zamani na hata sasa, farasi wa kivita, wasiohitajika, hawakuachwa hivi hivi bali walitemwa (walikatwa tishu hizo) ili kusudi kwamba wasije tumiwa kwa vita tena na maadui zao. Kwahiyo wanyama hao walibakia kuwa hawana kazi yoyote tena baada ya hapo.

Sasa ni kwanini Mungu hakuwaruhusu wana wa Israeli wawachukue farasi wale,  wawasaidie pengine kwa ajili ya vita vilivyokuwa mbele yao, lakini badala yake akawaamuru wawateme?

Ni kwasababu Mungu alitaka tegemeo lao liwe kwake na sio kwenye silaha au majeshi..Na kwamba wajue kuwa yeye huwa haikoi kwa silaha au kwa majeshi bali kwa Roho wake.

Daudi alisema..

Zaburi 20:7 “Hawa wanataja magari na hawa farasi, Bali sisi tutalitaja jina la Bwana, Mungu wetu”.

Na kama tunavyoona, wana wa Israeli hawakutumia magari wala farasi mahali popote walipovuka Yordani, lakini waliogopwa na maadui zao wote waliowazunguka, hiyo ni kwasababu walimtumaini Mungu peke yake ambaye angeweza kuwaokoa.

Vivyo hivyo na sisi, tukitaka tumshinde shetani kabisa kabisa au maadui zetu, hatupaswi kuweka tumaini letu kwa wanadamu au kwenye mali au chochote kile, bali tuweke tumaini letu kwa Yesu Kristo Bwana wetu, awezaye kutuokoa. Huku tukiwa tumezavaa silaha zote za haki (Waefeso 6) ili kusudi kwamba shetani akitaka kututema, sisi ndio tuwe wa kwanza kumtema yeye, Kwa jina la Yesu.

Bwana akubariki.

Je! Yesu akirudi leo unao uhakika wa kwenda naye? Je! Unahafahamu kwa hizi ndio zile nyakati ambazo biblia ilitabiri kutakuwa na makundi mawili ya wakristo? (yaani wanawali werevu na wanawali wapumbavu Math. 25) ambao wote wanadai wanamngojea Bwana? Lakini wale wapumbavu waliikosa karamu kwasababu hawakuwa na mafuta ya kutosha katika taa zao. Hivyo nyakati hizi kigezo cha kusema wewe ni mkristo pekee haitoshi, kusema wewe umeokoka haitoshi, unapaswa ujiulize ni nini kinachonipa uhakika ndani yangu kuwa Kristo akirudi leo nitakwenda naye?

Je! Mafuta ya Roho Mtakatifu yaliyo ndani yangu yaninitosha au yalishakwisha siku nyingi?

Maran Atha.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312


Mada Nyinginezo:

USIZITEGEMEE NGUVU ZAKO KUKUSAIDIA!

MTEGEMEE MUNGU, NA SI MWANADAMU.

DAKIKA MOJA TU, INAKUFANYA UMWAMINI SHETANI?

JIHADHARI NA UONGO WA SHETANI UNAOKARIBIANA NA UKWELI.

USITUMAINISHWE NA MANENO YA UONGO.

Rudi Nyumbani:

Print this post

Sikukuu ya kutabaruku ni ipi?

Jibu: Kuna tofauti ya Neno “kutakabari” na “kutabaruku”. Kutakabari ni “kuwa ni majivuno yanayotokana na kiburi” unaweza kusoma kusoma kwa urefu hapa >> KUTAKABARI

Lakini “kutabaruku” ambako ndiko tunakokwenda kukuzungumzia leo, maana yake ni “KUWEKA WAKFU”.

Sasa sikuku ya kutabaruku maana yake ni “Sikukuu ya kuweka wakfu”. Sikukuu hii ilianza kusheherekewa na Wayahudi (yaani waisraeli), miaka kadhaa baada ya Nabii wa mwisho katika biblia kutokea (yaani Nabii Malaki).

Sikukuu hii haikuwa miongoni mwa zile sikukuu 7 ambazo Musa aliagizwa na Mungu awape wana wa Israeli. Hivyo sherehe hii ilikuja kutengenezwa na baadhi ya wayahudi wachache kama ukumbusho wa kilichotokea katika Hekalu lao.

Sikukuu hii iliidhinishwa na Myahudi mmoja aliyeitwa Yuda Makabayo, pamoja na wazee wengine wa Israeli  wachache, kipindi ambacho Mtawala Antiokia IV Epifane, alipozuka na kushuka Yerusalemu na kulitia unajisi Hekalu la Mungu, kama unabii unavyosema katika Danieli 8:9 (Ile Pembe ndogo).

Mtawala huyu aliwalazimisha wayahudi wote wasiabudu katika Nyumba ya Mungu, na badala yake kuwalazimisha kufuata desturi za kipagani,

Sasa ndipo wakatokea wayahudi hao wachache (Yuda Makabayo pamoja na wenzake) wakaingia porini kupambana naye na kumwondosha, na hatimaye KULIWEKA TENA WAKFU HEKALU ambalo alilichafua, huyu Antiokia IV Epifane. Na tangu muda huo wakaifanya hiyo tarehe, kuwa ni tarehe ya kuadhimishwa kwa jinsi Mungu alivyowafungulia mlango wa kurejeshwa kwa Ibada takatifu za Nyumba ya Mungu. Kwa urefu kuhusu Mtawala huyu pamoja na Yuda Makabayo fungua hapa >> Danieli Mlango wa 8

Sikukuu hii haina tofauti na ile ya akina Mordekai (Sikukuu ya Purimu). Ambayo Mordekai na Esta waliitengeneza kama kumbukumbu ya mambo Mungu aliyowafanyia, baada ya kuwaokoa na mkono wa Hamani, adui yao.

Esta 9: 27 “Wayahudi wakaagiza na kutadariki juu yao wenyewe, na juu ya wazao wao, na juu ya wote watakaojiunga nao, isikome, ya kwamba watazishika siku hizo mbili sawasawa na andiko lile, na kwa majira yake kila mwaka;

28 siku hizo zikumbukwe na kushikwa kwa vizazi vyote na kila jamaa, katika kila jimbo na kila mji; wala siku hizo za Purimu zisikome katikati ya Wayahudi, wala kumbukumbu lake lisiishe kwa wazao wao”

Sikukuu hii ya kutabaruku na hiyo ya Akina Mordekai zote hazikuwepo miongoni mwa sikukuu Bwana alizowaagiza kwa mkono wa Musa..Ni sikukuu zilizotengenezwa baada ya Mungu kuwafanyia mema watu wake, hivyo na wao wakazingeneza kama kurudisha shukrani kwa Mungu wao.

Ni jambo gani tunajifunza katika sikukuu hii ya kutabaruku?

Chochote tunachomfanyia Mungu, anakiheshimu.. Daudi alifikiria kumjengea Mungu nyumba, ingawa alijua kabisa Mungu hakai kwenye nyumba zilizotengenezwa na mikono ya wanadamu, lakini Mungu alimheshimu kwa mawazo yake hayo, na wala hakuidharau ile nyumba, zaidi ya yote aliitukuza sana kwa mwanawe Sulemani.

Vivyo hivyo hawa wakina Yuda Makabayo na wenzake, ambao walipenda kuadhimisha siku ya Nyumba ya Mungu kuwekwa tena wakfu, huku wakimshukuru kwa kumfanyia Ibada, Mungu aliiheshimu sikukuu yao hiyo..Ndio maana ilidumu mpaka wakati wa Bwana Yesu.

Yohana 10:22  “Basi huko Yerusalemu ilikuwa SIKUKUU YA KUTABARUKU; ni wakati wa baridi.

23  Naye Yesu alikuwa akitembea hekaluni, katika ukumbi wa Sulemani”.

Je umeokoka?..Kama bado unangoja nini?..kipindi si kirefu parapanda ya mwisho italia, na watakatifu ambao unadhani hawapo leo duniani, wataondolewa duniani…Na utakuwa umepoteza nafsi yako milele.. Hujui dakika tano mbele nini kitatokea..ukifa leo au parapanda ikilia leo utakuwa wapi?..kumbuka kuzimu ipo, na biblia inasema haishibi watu.. Mpokee leo Kristo kama bado hujafanya hivyo…

Kama upo tayari kutubu leo na kuanza safari mpya ya wokovu basi fungua hapa >> SALA YA TOBA

Maran atha!

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312


Mada Nyinginezo:

SIKUKUU 7 ZA KIYAHUDI ZINAFUNUA NINI KWETU?

SIKUKUU YA VIBANDA.

PASAKA NI NINI? NA JE TUNARUHUSIWA KUSHEHEREKEA PASAKA?

JE WAKRISTO TUNARUHUSIWA KUSHEHEREKEA VALENTINE’S DAY?

JE NI LAZIMA MKRISTO AOE/AOLEWE?

Rudi Nyumbani:

Print this post