Nzio ni nini?(Yohana 2:6)

Nzio ni nini?(Yohana 2:6)

Nzio ni kipimo cha ujazo wa kimimika kilichotumiwa zamani na wagiriki,  Nzio moja ina  ujazo wa karibia lita 40,

Katika biblia utaona ile habari ya Yesu kualikwa katika arusi kule Kana mji wa Galilaya, Neno hili lilitumika tusome;

Yohana 2:6 Basi kulikuwako huko mabalasi sita ya mawe, nayo yamewekwa huko kwa desturi ya Wayahudi ya kutawadha, kila moja lapata KADIRI YA NZIO mbili tatu.

Hivyo hapo unaweza kupata picha hapo, hayo mabalasi yalikuwa na ujazo mwingi kiasi gani. Kama kila balasi moja linachukua nzio mbili au tatu, ukikadiria hapo, ni kuwa balasi moja lina ujazo wa lita  80 mpaka 120.

Na mabalasi yalikuwa ni 6, hivyo ujazo wa maji yaliyowekwa pale na kubadilika kuwa divai ni karibia lita 480-720. Hivyo ni kiwango kikubwa sana. Hivyo unaweza kuona jinsi divai hiyo ingewahudumia watu wengi kiasi gani. Kumbuka mtu mmoja tu hawezi kunywa lita nzima ya divai, akijitahidi sana atakunywa nusu au robo.

Lakini ni nini Mungu alikuwa analifundisha kanisa?

Ni kuwa pale tulipo na mapungufu, yeye anaweza kutujaza, jambo hilo utaona tena alipoigawa ile mikate mitano na samaki wawili na kulisha maelfu ya watu. Na alifanya hivyo mara mbili , Hiyo ni kutuonyesha kuwa palipo na vichache, au pale ambapo hamna kabisa Mungu anaweza kugeuza kitu kingine kisichokuwa na thamani  kikawa na thamani kwetu. Ipo mifano mingi sana katika biblia, utaiona ile habari ya Elisha na yule mwanamke ambaye mume wake alikuwa anadaiwa, mpaka akafa hajalipa deni, yule anayemdai akaja akataka kwenda kuwachukua watoto wake awafanye kuwa watumwa, lakini yule mama alipokwenda kwa Elisha amsaidie, Elisha akamwomba Mungu, ndipo akamwambia akachukue vyombo vitupu kisha amimine mafuta kwenye vyombo hivyo, kwa kadiri awezavyo kwasababu mafuta yale hataisha, kisha aende kuuza, na fedha itakayopatikana, alipe deni lake, na itakayobaki atumie yeye na familia yake(2Wafalme 4:1-7) .

 Hiyo yote ni kuonyesha kuwa Mungu anaweza kutoa pale pasipowezekana na ndio maana anaitwa YEHOVA- YIRE, (yaani Mungu mpaji wetu). Hivyo na wewe ukimtegemea yeye atakutendea miujiza kama hiyo.

Lakini ni sharti kwanza uwe mwana wake. Swali ni Je! Kristo yupo ndani yetu? Majibu yote tunayo, lakini tujue kuwa hakuna kimbilio la kweli nje ya Kristo. HUO NDIO UKWELI PEKEE ULIODUMU DUNIANI KWA MIAKA YOTE.

Shalom.

Kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

Je! mabalasi Bwana Yesu aliyoyatumia kugeuzia maji kuwa divai, yalitumika tu kwa kazi hiyo?

Kuwatema farasi, maana yake ni nini?

HAMJAFAHAMU BADO?

KIFO CHA MTAKATIFU PERPETUA NA FELISTA.

VIFO VYA MITUME WA YESU/ JINSI MITUME WALIVYOKUFA.

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments