Hozi ni nini? (1Nyakati 4:10, 7:28, 9:2)

Hozi ni nini? (1Nyakati 4:10, 7:28, 9:2)

Hozi ni nini?


Hozi ni neno linalomaanisha himaya, ikijumuisha eneo na vitu mtu anavyomiliki.

Kwa mfano unaweza kuona, Yabesi, alimwomba Mungu ambariki na kumzidishia Hozi yake (Himaya yake), Hiyo akiwa na maana kuwa azidishiwe mifugo, azidishiwe uzao, azidishiwe mali, azidishiwe watumwa na wajakazi, azidishiwe ardhi, azidishiwe ukuu n.k. Na kweli kama tunavyosoma Mungu aliridhia maombi yake kwasababu alikuwa ni mcha Mungu, japokuwa alitokea katika chumbuko la huzuni.

1Nyakati 4:10 “Huyo Yabesi akamlingana Mungu wa Israeli, akisema, Lau kwamba ungenibarikia kweli kweli, na kunizidishia HOZI YANGU, na mkono wako ungekuwa pamoja nami, nawe ungenilinda na uovu, ili usiwe kwa huzuni yangu! Naye Mungu akamjalia hayo aliyoyaomba”.

Neno hilo utalisoma pia  katika vifungu hivi;

1Nyakati 7:27 “na mwanawe huyo ni Nuni, na mwanawe huyo ni Yoshua.

28 Na HIZI NDIZO HOZI zao na makao yao; Betheli na vijiji vyake, na upande wa mashariki Naara, na upande wa magharibi Gezeri na vijiji vyake; na Shekemu pia na vijiji vyake, hata Aza na vijiji vyake;

1Nyakati 9:1 “Hivyo Israeli wote walihesabiwa kwa nasaba; na tazama, hizo zimeandikwa katika kitabu cha wafalme wa Israeli; na Yuda wakachukuliwa mateka mpaka Babeli, kwa sababu ya makosa yao.

2 Basi wenyeji wa kwanza waliokaa katika HOZI ZAO katika miji yao walikuwa Israeli, na makuhani, na Walawi, na Wanethini”.

Vivyo hivyo na sisi, tukimcha Mungu, mfano wa Yabesi Mungu anaweza kuzizidisha himaya zetu mfano wa Yabesi pale tutakapomwomba. Lakini vilevile tusipomcha yeye, anao uwezo wa kummilikisha mtu mwingine hiyama zetu na tukabakiwa hatuna kitu kama vile alivyofanya kwa wana wa Israeli, walipomuasi akawapeleka utumwani Babeli, na himaya zao zikamilikiwa na watu wengine.

Na himaya sio lazima tu iwe ile ya mwilini, Rohoni pia tunazo himaya, pale tunapomkataa Mungu maisha mwetu, hapo hapo adui yetu shetani ibilisi anapata nguvu ya  kuzitawala himaya zetu. Na ndio hapo anakuwa na uwezo asilimia mia wa kujiamulia jambo lolote baya  katika maisha yetu, hata kutuua ataweza, kwasababu tumekusoma Baraka na ulinzi wa ki-Mungu.

Hivyo sisi nasi pia tunawajibu wa kuzilinda HOZI zetu. Kwa kuupokea wokovu na kuulinda katika utakatifu. Ndipo Bwana atakapotuzidisha na kutuongeza kupita kiasi.

Swali ni Je! Upo ndani ya wokovu? Je! Hozi zako zipo mikononi nani? Jibu unalo, jibu ninalo. Lakini Yesu Kristo ndio mwokozi.

Shalom.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

Kuwatema farasi, maana yake ni nini?

Sikukuu ya kutabaruku ni ipi?

Kutakabari ni nini katika biblia?.

DHIKI KUU INAKUJA NA UNYAKUO UPO KARIBU.

MAPIGO YA VITASA SABA, NA SIKU YA BWANA.

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments